16
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 81 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Agosti 20 - 26, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Kamati ya Pamoja TanzaniteOne (JOC) Yazinduliwa Eneo La Muhintiri latengwa kwa wachimbaji wadogo Soma habari Uk. 3 SIMBACHAWENE AITAKA SKY ASSOCIATES KUTOBAGUA WATANZANIA UK 2 Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (aliyevaa miwani) akipata maelezo kuhusu uchimbaji, ndani ya shimo la mgodi wa chini (underground mine) wa TanzaniteOne wakati alipotembelea mgodi, kabla ya kuzindua Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji mgodi huo (JOC). Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene (aliyekaa katikati) katika picha na Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji “Joint Operating Committee – (JOC) ” ya mgodi wa TanzaniteOne, baada ya kuzindua Kamati hiyo mgodini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa JOC Bwana Faisal Juma Shahbhai na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Duesdedith Magala. Wajumbe wengine waliokaa wa kwanza kulia ni Bi. Asha Jumanne Ngoma, Prof. Peter Antony Kopoka (wa kwanza kushoto), Bwana Hussein Omary Gong’a (aliyesimama kushoto) na Bwana Halfan Mpenziye Hayeshi (aliyesimama kulia).

MEM 81 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MEM 81 Online.pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 81 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Agosti 20 - 26, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Kamati ya Pamoja TanzaniteOne (JOC) Yazinduliwa

Eneo La Muhintiri latengwa kwa wachimbaji wadogo Soma

habari Uk. 3

SIMBACHAWENE AITAKA SKY ASSOCIATES KUTOBAGUA WATANZANIA

UK2

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (aliyevaa miwani) akipata maelezo kuhusu uchimbaji, ndani ya shimo la mgodi wa chini (underground mine) wa TanzaniteOne wakati alipotembelea mgodi, kabla ya kuzindua Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji mgodi huo (JOC).

Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene (aliyekaa katikati) katika picha na Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji “Joint Operating Committee – (JOC) ” ya mgodi wa TanzaniteOne, baada ya kuzindua Kamati hiyo mgodini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa JOC Bwana Faisal Juma Shahbhai na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Duesdedith Magala. Wajumbe wengine waliokaa wa kwanza kulia ni Bi. Asha Jumanne Ngoma, Prof. Peter Antony Kopoka (wa kwanza kushoto), Bwana Hussein Omary Gong’a (aliyesimama kushoto) na Bwana Halfan Mpenziye Hayeshi (aliyesimama kulia).

Page 2: MEM 81 Online.pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Koleta Njelekela, STAMICO

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameiasa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji wa Mgodi

wa TanzaniteOne, “Joint Operating Committee”-JOC kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ili kuwanufaisha wadau wa Tanzanite katika uvunaji wa madini hayo, huku wakilinda maslahi ya mgodi huo kwa Taifa.

Simbachawene alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizindua Kamati ya hiyo ya JOC, katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mirerani, katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

“Suala la kulinda maslahi mapana ya mgodi huu kwa Wabia na Taifa linawezekana, iwapo Wanakamati ya JOC mtafanya kazi kama timu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake ipasavyo. Hivyo basi ipokeeni kazi hii na kuitekeleza kwa ari, kasi na nguvu kubwa” Alisisitiza Mh. Simbachawene.

aliagiza Kamati hiyo ya JOC kukamilisha majadiliano ya kuboresha

Mkataba wa ubia uliokuwepo baina ya STAMICO na TML kwani mabadiliko ya Mkataba huo yataleta matokeo chanya katika udhibiti na uendelezaji wa mgodi na biashara nzima ya Tanzanite kwa manufaa ya wabia wote na Taifa pia.

“Baadhi ya vipengele vinavyohitaji kuboreshwa ni pamoja na suala la kutangaza chimbuko la Tanzanite duniani kuwa ni Tanzania; kuimarisha mazingira ya mgodi kuwa kivutio cha utalii na mafunzo; kuchangia huduma za jamii zinazozunguka mgodi na kupanda

miti katika maeneo ya mgodi ili kutunza mazingira” alifafanua Mh. Simbachawene.

Kamati hiyo ya JOC ina wajumbe 6 ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Asha Jumanne Ngoma, Prof. Peter Antony Kopoka kwa upande wa STAMICO na Faisal Juma Shahbhai, Hussein Omary Gong’a na Halfan Mpenziye Hayeshi kwa upande wa Sky Associates Ltd. Kamati hii inaongozwa na Faisal Juma Shahbhai.

Katika uzinduzi wa Kamati hiyo, Simbachawene pia aliwakumbusha wajumbe wa Kamati ya JOC kumsimamia kikamilifu mwendeshaji wa mgodi huo yaani TML ili aweze kutekeleza masharti ya mkataba wa ubia katika uzalishaji wa Tanzanite, kwa manufaa ya pande zote.

Aidha aliwasisitiza wajumbe wa JOC kufanya maamuzi yenye tija katika uidhinishaji wa bajeti, kubuni mipango ya maendeleo ya mgodi; kuandaa sera za uendeshaji; kuunda kamati za ushauri kulingana na mahitaji na kuingia makubaliano ya pamoja na Kitengo cha Uangalizi na Usimamizi (Monitoring and Evaluation Unit), kuhusu mfumo wa uendeshaji mgodi, ili kuongeza uzalishaji wa tanzanite na kukuza soko la ndani.

Ameitaka Sky Associates kutoa nafasi

za ajira kwa Watanzania bila ubaguzi na kuzingatia misingi ya utawala bora katika uendeshaji wa mgodi huo huku wakitoa maslahi bora kwa wafanyakazi wake.

Simbachawene alisema STAMICO kwa upande wake, haina budi kuwapatia Wafanyakazi wake waliopo Mirerani vitendea kazi stahili ili wasiwe na kisingizio cha kushindwa kutekeleza majukumu yao, na ameitaka Menejimenti ya Shirika hilo ipime utendaji kazi wa wafanyakazi wake mara kwa mara ili kukuza ufanisi.

Kuhusu suala la kuboresha mahusiano mazuri na Wachimbaji wadogo, Simbachawene amesema mahusiano kati ya TanzaniteOne na Wachimbaji Wadogo yaendelee kuimarishwa, na amekiri kuitambua Kamati Maalum iliyoundwa na Kamishna wa Madini, ili kuisaidia Serikali kuweka mfumo mzuri wa uchimbaji katika mgodi huo, jambo ambalo litaepusha ajali na kupunguza migogoro baina ya wadau.

“Nazitambua changamoto za wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite ambazo ni matokeo ya wadau wasio waaminifu; nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Kifungu cha 6(4) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kifungu hicho sasa kinampa Kamishna wa Madini mamlaka kamili ya kutaifisha na kupiga mnada madini yanayokamatwa yakimilikiwa kinyume cha Sheria. Hivyo, wote wenye tabia ya kufanya biashara ya madini kinyume cha Sheria wajiandae kupoteza madini yao” Aliongeza kwa msisitizo Mh. Simbachawene.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Deusdedith Magala amemshukuru Simbachawene kwa kuunda Kamati hiyo ya JOC na kuizindua rasmi, kwani itasaidia kulinda hisa za STAMICO, za Serikali na mali za mgodi, na pia kuuwezesha mgodi kufanya maamuzi makubwa na yenye tija.

Magala alisema tangu Juni 2013 STAMICO ilipoingia ubia wa umiliki wa mgodi wa TanzaniteOne na kampuni ya TML kwa uwiano wa 50:50 wa leseni ya uchimbaji wa Tanzanite, Bodi za Wakurugenzi za wabia hao wawili ndio zimekuwa zikifanya kazi kama Kamati ya JOC, jambo ambalo lilileta mzigo mkubwa wa kazi kwa bodi hizo.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kamati ya Ushirikiano ya Mgodi wa TanzaniteOne, Simbachawene na ujumbe wake pia walikagua shughuli za uchimbaji wa Tanzanite katika mgodi wa CT, zikiwemo uchorongaji, uchotaji na utoaji wa udongo na kujionea athari za kimazingira zilizosababishwa na wachimbaji wadogo kwenye kitalu C.

Hafla hiyo ya uzinduzi wa JOC ilihudhuriwa na mwakilishi wa Kamishna wa Madini Tanzania, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Wakurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Ltd na TML, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Kamishna Msaidizi wa Madini - Kanda ya Kaskazini, Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji (JOC) na Waandishi wa Habari.

Kamati ya Pamoja TanzaniteOne (JOC) Yazinduliwa

Waziri wa Nishati na Madini , George Simbachawene (mwenye ovaroli ya bluu) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya JOC Bwana Faisal Juma Shahbhai (aliyevaa kofia ngumu ya Bluu) kuhusu uzalishaji wa Tanzanite katika mgodi wa TanzaniteOne. Anayemsikiliza (mwenye overall ya Kijani) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Duesdedith Magala.

Baadhi ya vipengele vinavyohitaji kuboreshwa ni pamoja na suala la kutangaza chimbuko la Tanzanite duniani kuwa ni Tanzania; kuimarisha mazingira ya mgodi kuwa kivutio cha utalii na mafunzo; kuchangia huduma za jamii zinazozunguka mgodi na kupanda miti katika maeneo ya mgodi ili kutunza mazingira”.

Page 3: MEM 81 Online.pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

Mhariri MkUU: Badra MasoudMSaNifU: Essy Ogunde

WaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji mgodi wa TanzaniteOne ichochee uvunaji wa

Tanzanite kwa manufaa ya Wadau wote

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Eneo La Muhintiri latengwa kwa wachimbaji wadogo

Na Mohamed Saif

Hatimaye eneo la Muhintiri wilayani Ikungi lililokuwa chini ya kampuni ya uchimbaji

dhahabu ya Shanta limetengwa maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.

Hayo yalisemwa na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia leseni za madini, John Nayopa katika kijiji cha Muhintiri, wilayani Ikungi, mkoa wa Singida kwenye mkutano wa hadhara uliohusisha wachimbaji wadogo wa madini wa eneo hilo. Kamishna Msaidizi alimwakilisha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Nayopa alisema lengo la mkutano huo ni kuhitimisha mchakato uliodumu kwa muda

mrefu ambao ulihusu kampuni hiyo ya Shanta kutoa eneo la uchimbaji madini la Muhintiri kwa wachimbaji wadogo.

“Wachimbaji wadogo wa madini waliomba kupatiwa walau eneo kidogo ili nao wafanye shughuli za uchimbaji kwenye eneo la Muhintiri. Hatimaye mmiliki wa eneo hilo, ambaye ni kampuni ya Shanta, ameridhia kuachia eneo lote na sio sehemu kama wachimbaji wadogo walivyokuwa wameomba hapo awali,” alieleza Nayopa.

Alieleza kuwa mnamo mwezi Machi, 2015, kwa nyakati tofauti, kikundi cha wachimbaji Wadogo wa Madini Kijiji cha Muhintiri, Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Singida (SIREMA) na Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) waliomba kampuni

ya Shanta na Wizara ya Nishati na Madini kumegewa sehemu ya leseni ya utafutaji mkubwa wa madini PL 6028/2009 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Nayopa alisema kwamba kwa mujibu wa Kifungu Na. 7(2) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, mtu hawezi kupewa leseni ya uchimbaji madini ndani ya leseni nyingine ya utafutaji madini bila idhini ya mwenye leseni husika.

“Vikao kadhaa vilifanyika chini ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Mb.) vikihusisha FEMATA, SIREMA na kampuni ya Shanta ambapo kampuni hiyo iliafiki kuliachia eneo hilo kwa ajili ya wachimbaji wadogo,” alieleza Nayopa.

Alisema taratibu za kisheria za kampuni ya Shanta kuliachia eneo hilo tayari zimefanyika na zimekamilika kama ambavyo wachimbaji hao walivyokuwa wameomba.

Nayopa alisisitiza kwamba kipaumbele kwa ugawaji wa maeneo hayo kitapewa kwa wachimbaji wadogo wa madini waliojiunga kwenye vikundi.

“Wizara imedhamiria kuhakikisha haki inatendeka katika ugawaji wa maeneo. Kipaumbele ni kwa wale ambao tayari wamo kwenye vikundi ambavyo vinatambuliwa na Serikali ya Kijiji na si vinginevyo,” alisema.

Aliwataka Maafisa madini pamoja na Maafisa wengine wa Serikali mkoani humo kuepuka maslahi binafsi kwa kugawa maeneo hayo kwa wasiokuwa walengwa.

Aidha, alimuagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati kuhakikisha taratibu za ugawaji wa madini zinakamilika ndani ya wiki moja ili kuepuka kuchelewesha shughuli za

Wiki hii tumeshuhudia Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ikizindua Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji “Joint Operating Committee” (JOC) ya mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mirerani na kuitaka Kamati hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuufanya uvunaji wa tanzanite uwe wa manufaa kwa wadau wote.

Tumeshuhudia jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali ili kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuongeza miradi ya uwekezaji katika mfumo wa ubia katika sekta ya madini hususani tanzanite ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Tumejionea mwaka 2013, Serikali kupitia STAMICO iliingia ubia wa umiliki wa mgodi wa TanzaniteOne na Kampuni ya Tanzania Mining Company Ltd (TML) kwa uwiano wa 50:50 wa leseni ya uchimbaji wa tanzanite huko Mirerani, ambapo Mwaka 2014 Richland Resources Ltd aliyekuwa mmiliki wa TanzaniteOne SA Ltd iliamua kuuza kampuni yake kwaSKY Associate Ltd, ambayo ndiye mmiliki mpya wa TML na mbia wa sasa na Serikali kupitia STAMICO.

Katika uzinduzi wa Kamati ya JOC, Serikali kupitia Wizara yake ya Nishati na Madini pia iliwakumbusha wajumbe kumsimamia kikamilifu mwendeshaji wa mgodi (TML) ili atekeleze masharti ya mkataba wa ubia katika uzalishaji wa tanzanite kwa manufaa ya pande zote.

Wakati umefika sasa kwa SKY Associates Ltd na STAMICO kuboresha vipengele vya mkataba wa ubia ili kuimarisha uendeshaji na uzalishaji. Hii ni pamoja na kuitangaza tanzanite duniani na kuonesha kuwa madini haya ambayo ni hazina ya nchi, chimbuko lake ni Tanzania; kuimarisha mazingira ya mgodi kuwa kivutio cha utalii na mafunzo; kuchangia huduma za jamii zinazozunguka mgodi; kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti;kuongeza thamani ya tanzanite kabla ya kuuza ili kumudu ushindani wa soko, kuongeza ajira kwa Watanzania na kuongeza uwazi katika mauzo kwa kuhusisha pande zote (STAMICO na Sky Associates) kwa 100% kuanzia hatua za uchambuzi (sorting) mpaka kuuza.

Hivi karibuni, Serikali imefanya marekebisho ya Kifungu cha 6(4) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kifungu hicho sasa kinampa Kamishna wa Madini mamlaka kamili ya kutaifisha na kupiga mnada madini yanayokamatwa yakimilikiwa kinyume cha Sheria. Hivyo, wote wenye tabia ya kufanya biashara ya madini kinyume cha Sheria wajiandae kupoteza madini yao.

Kamati ya JOC kwa upande mmoja na Kamati maalum ya Maridhiano kati ya mgodi na wachimbaji wadogo wa Mirerani wakiwemo Viongozi wa Wachimbaji wadogo (MAREMA na TAMIDA) iliyoundwa hivi karibuni na Kamishna wa Madini, shirikianeni kuweka mfumo mzuri wa uchimbaji wa madini ya tanzanite hapo ili kuepusha ajali, kupunguza migogoro baina ya wadau, kudhibiti mitobozano inayosababishwa na wachimbaji wadogo kutoka vitalu B na D, wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite unaosababishwa na wadau wasio waaminifu.

Kampuni ijipange vyema na matumizi ya teknolojia mpya ya sensors na CCTV cameras chini ya mgodi ili kudhibiti wizi na pia kwenda sambamba na mapinduzi ya sayansi na teknolojia yanayoendelea kutokea duniani ili kuzuia wizi wa madini ya tanzanite maeneo ya uchimbaji.

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), endeleeni kuimarisha usimamizi kwa wachimbaji wote wa tanzanite ambao wanakwepa kulipa kodi ili kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na rasilimali ya madini nchini yanachangia kwa kiwango stahili katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Sasa ni Kamati ya JOC wakati wa kufanya maamuzi yenye tija katika uidhinishaji wa bajeti, kubuni ya maendeleo ya mgodi; kuandaa sera za uendeshaji; kuunda kamati za ushauri kulingana na mahitaji ya mgodi, na kuingia makubaliano ya pamoja na Kitengo mipango cha Uangalizi na Utathiminishaji (Monitoring and Evaluation Unit), kuhusu mfumo wa uendeshaji mgodi, ili kuongeza uzalishaji wa tanzanite na kukuza soko la ndani ni sasa.

Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, John Nayopa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) kijijini Muhintiri wilayani Ikungi.

>>INAENDELEA UK. 4

Page 4: MEM 81 Online.pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Asteria Muhozya na Clinton Ndyetabula, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, amewakabidhi Nyaraka za Ufadhili na kuwaaga wanafunzi 22 wa

Kitanzania wanaokwenda masomoni nchini China, kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada za Uzamili (Masters) na Uzamivu (Phd).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Nyaraka hizo, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Simbachawene alisema kuwa, kutokana na ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia , Serikali imeweka mkazo kuendeleza wataalamu wazawa kutokana na mahitaji makubwa ya wataalamu katika sekta ndogo za mafuta na gesi.

Alisema kuwa, tayari Serikali imejenga miundombinu ya gesi asilia ikiwemo Bomba la gesi na mitambo wa Kuchakata gesi asilia, hivyo, uwepo wa wataalamu hao ni muhimu ili waweze kusimamia shughuli hizo vizuri jambo ambalo litawezesha watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi mkubwa wa gesi.

“Tayari tuna bomba la gesi, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni Tanzu ya Kusambaza Gesi (GASCO). Lakini pia yapo makampuni ya mafuta na gesi, hawa wote wanahitaji wataalamu wa kitanzania, kama Serikali, lazima tuwekeze kwa watu wetu”, alisema Simbachawene.

Aidha, Waziri Simbachawene alieleza kuwa, kupitia TPDC watanzania watashiriki katika uchumi huo kwa kuwa TPDC imeshiriki katika kila nyanja katika tasnia hizo na kuongeza kuwa hakuna mdau yoyote atakayefanya kazi pasipo kushirikiana kikamilifu na shirika hilo.

“TPDC imeshiriki na itaendelea kushiriki kikamilifu katika sekta hii. Wadau wengine wote wanaotaka kufanya kazi na sisi lazima washirikiane na TPDC. Taasisi hii ndiyo inatuwakilisha watanzania katika uchumi huu wa gesi. Faida zote ni kwa ajili ya taifa letu, kwa hivyo, TPDC ndio tafsiri ya ushiriki wa watanzania katika uchumi wa gesi,”alisisitiza Simbachawene.

Vilevile, alisema kuwa, Wizara ya Nishati na Madini ni miongoni mwa wizara zilizo katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika sekta ya nishati na kueleza kuwa, ili kutekeleza ipasavyo mpango huo, wanahitajika wataalamu

zaidi wazalendo waliobobea katika fani za mafuta na gesi .

Simbachawene pia alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili hatimaye waweze kusaidia Taifa katika kuanzisha vyanzo mbadala vya nishati ya umeme , kuongeza usimamizi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo, hivyo kusaidia katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

“Ni matumaini yangu kuwa mtatumia vizuri fursa mliyoipata, mtajifunza kwa bidii na kuiwakilisha nchi yetu vizuri na kuleta teknolojia zitakazosaidia kupata ufumbuzi au mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta hii,”alieleza Simbachawene.

Aidha, Waziri alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuwawezesha Watanzania kusoma masuala ya mafuta na gesi katika Vyuo Vikuu vilivyobobea katika taaluma hizo nchini humo.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mrimia Mchovu alisema kuwa, Serikali ya Watu wa China ilianza kuwafadhili Watanzania kusoma nchini humo tangu mwaka 2013 na kuongeza kuwa, Serikali hiyo imeahidi kuendelea kuifadhili Tanzania hadi ifikapo mwaka

2019.“ Serikali ya China ilianza kutoa ufadhili

mwaka 2013,ambapo walifadhiliwa watanzania 8 katika ngazi ya Uzamili, mwaka 2014 Uzamivu 1, uzamili 9, na mwaka huu 2015 uzamivu 3 na uzamili 19,” alisema Mrimia

Aliongeza kuwa, awali wizara ilitoa matangazo kuhusu uwepo wa ufadhili huo lakini idadi ya maombi ilikuwa ndogo sana, na hivyo kuongezwa siku kadhaa kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kuomba ufadhili huo ambapo jumla ya maombi 187 yalipokelewa. “Kimsingi ushindani ulikuwa mkubwa sana na waombaji 22 waliokidhi vigezo vilivyowekwa na Serikali ya China walifaulu,” alisema Mrimia.

Majina ya waliochaguliwa ni pamoja na Maagi Mtaki Thomas, Mkemai Rashid Mohamed, Mabeyo Petro Ezekiel, Hemed Kijakazi, Msafiri Kattiba Saada, Msongela Anna, Magambo Christina, Sanga Modekai, Sebe Mgeta Faustine, Kikulu Mukhusin Rajab, Lyimo Rosemary, Lyaka Japhet, Nziku Eliezery, Kessy Emmanuel Goodluck, Hechei Felician David, Mohamed Ad-Ham Said, Kironde Birungi Joseph, John Hillonga Emiliana, Hassa Khalfan Hamisi, Ryoba Catherine Robi, Mwijage Edith na Robert Faustine Edwin.

Watanzania 22 wapata Ufadhili kusoma Mafuta, Gesi China

uchimbaji madini kwenye eneo hilo.“Lengo la Serikali ni kuhakikisha

kunakuwa na uchimbaji madini wenye tija. Hatupo tayari kusikia zoezi hili linachelewa, lifanyike kuanzia hivi sasa na wenye sifa wapatiwe maeneo na kuyaendeleza,” alisema.

Alibainisha kwamba maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uchimbaji mdogo wa madini mkoani humo bado yapo mengi na Serikali inaendeleza juhudi zake za kutafuta maeneo mengine kwa ajili yao.

Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Zane Swanepoel alisema kampuni yake imeridhia kwa moyo mkunjufu kuachia eneo hilo kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kampuni yake inaelewa kuwa wachimbaji wadogo wa madini nchini wanauhitaji wa maeneo ya uchimbaji na hivyo kuamua kuliachia eneo hilo la Muhintiri kwa Serikali ili ligawiwe kwa wachimbaji wadogo.

“Tuna mahusiano mazuri na Serikali na kufuatia mazungumzo yetu na Serikali pamoja na wachimbaji wadogo, kwa ridhaa yetu tumeona ni vizuri pia wachimbaji wadogo wakawa na maeneo,” alisema Swanepoel.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Amanzi alipongeza hatua hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano mwema baina ya Serikali, wawekezaji na wachimbaji wadogo.

Aidha, Amanzi aliiomba Wizara hiyo kuendeleza juhudi zake za kusaidia wachimbaji wadogo wa madini nchini

kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo na uchimbaji wenye tija kwa mchimbaji na kwa Taifa kwa ujumla.

Amanzi alitumia fursa hiyo pia kuwaasa wachimbaji wadogo kuepuka anasa na badala yake kuhakikisha wanafungua akaunti za benki ili kuweka akiba faida inayopatikana kwa maendeleo ya baadaye.

“Punguzeni anasa ikiwa ni pamoja na matumizi yasiyo ya lazima, jibaneni muweke akiba kwa maisha ya baadae,” alisema.

Aliongeza kwamba ni vyema wakatambua kuwa shughuli za uchimbaji madini zina mwisho wake na hivyo kuwataka wajipange vizuri.

“Msisahau kuwekeza ili uwekezaji huo uwasaidie hapo baadaye. Leo mna nguvu wekezeni ili kesho mtakapokuwa hamna nguvu muwe tayari mna sehemu nyingine ya kuwapatia riziki,” alisema Amanzi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Kamishna Msaidizi Kanda ya Kati-Singida, Sosthenes Massola alisema utoaji wa leseni za kumiliki maeneo zitatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Madini na kanuni zake za Mwaka, 2010.

Aliwataka wachimbaji wote watakaopewa leseni kuzingatia utunzaji wa mazingira, usalama na afya maeneo watakayotumia kwa shughuli za uchimbaji madini.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa uuzaji madini kwa kufuata sheria. “Madini yatakayopatikana yauzwe kwa wenye leseni za biashara yaani ‘brokers na dealers’ na siyo nje ya hapo,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo, Katibu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida (SIREMA), John Metia aliishukuru Wizara hiyo kwa juhudi zake katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapatiwa maeneo.

Vilevile, aliipongeza kampuni ya Shanta kwa kuridhia kuachia eneo hilo la Muhintiri na kuwa eneo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo na pia kuahidi kuhakikisha wanalipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

“Serikali yetu ni sikivu nasi tunaahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali kwa kufanya shughuli zetu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kufikia malengo tulilojiwekea,” alisema Metia.

Leseni ya utafiti (PL 6028/2009) ilitolewa kwa kampuni ya Shanta Mining Ltd mnamo tarehe 20/08/2009 kwa muda wa miaka mitatu hadi tarehe 19/08/2015. Baada ya muda wake wa awali kumalizika, leseni hiyo ilihuishwa kwa muda wa miaka mitatu hadi tarehe 19/08/2015.

Eneo La Muhintiri latengwa kwa wachimbaji wadogo

Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kati-Singida, Sosthenes Massola akizungumza na wachimbaji wadogo wa Muhintiri (hawapo pichani).

>>INATOKA UK. 3

Page 5: MEM 81 Online.pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Mwijage atoa maagizo TPDC, TANESCONa Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amewataka wataalam wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

kupitia kampuni Tanzu ya Usambazaji Gesi (GASCO) pamoja na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha kuwa wanashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati ili kuwezesha miradi hiyo kufanyika kwa ufanisi.

Mwijage aliyasema hayo mkoani Mtwara wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi kuchakata gesi asilia katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara na miradi ya umeme vijijini awamu ya Pili inayotekelezwa pembezoni mwa bomba la Gesi linalotoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam.

Agizo la Naibu Waziri limekuja baada ya kufika katika kijiji cha Mnaweni mkoani Mtwara ambapo wananchi walimweleza changamoto ya mawasiliano iliyopo kati ya wataalam na wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini uliopangwa kutekelezwa katika kijiji hicho.

“Watu lazima washirikishwe na wataalam wa Tanesco muangalie namna ambavyo miradi hii ya umeme vijijini haitaathiri mali za wananchi kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tumeshakubaliana

kuwa hakutakuwa na fidia katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili pesa inayopatikana katika tozo ya mafuta

itumike kusambaza umeme zaidi badala ya kulipana fidia,” alisema Mwijage.

Aidha, aliiagiza TPDC kuongeza

ushirikiano kati yake na wadau wake kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji na kufanya mikutano ya mara kwa mara na wananchi wanaozunguka miradi ya gesi asilia ili kuwaeleza hatua mbalimbali za utekelezaji zinazoendelea katika miradi hiyo suala ambalo litapelekea wananchi hao kuwa ni sehemu ya ulinzi wa miundombinu hiyo.

Katika hatua nyingine Mwijage aliiagiza Tanesco kuwafungia wananchi kifaa mbadala ambacho tayari nyaya zimesukwa ndani yake kijulikanacho kwa jina la Readboard (Umeta) kinachotoa unafuu wa gharama ya kutandaza nyaya kwenye nyumba kwa kuwa mwananchi atapata umeme kwenye nyumba bila kutandaza nyaya za umeme.

“ Hata nyumba za gharama nafuu ambazo zimeezekwa na makuti zinapaswa kuwekewa umeme kupitia kifaa hiki, nawashauri wananchi mtumie kifaa hiki ambacho gharama yake ni shilingi elfu 60 na endapo mtu utapata uwezo zaidi wa kifedha, utafanya wiring ambayo ni gharama zaidi kuliko Umeta,” alisema Mwijage.

Kuhusu suala la utoaji wa huduma kwa jamii inayozunguka miradi ya gesi asilia, Mwijage alieleza kuwa suala hilo sasa litatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015 na kwamba miradi hiyo itatekelezwa baada ya kuwepo kwa majadiliano kati ya wawekezaji na wazawa wa eneo husika.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tano kushoto mstari wa mbele ) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walioko katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally na kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco, mkoa wa Mtwara, Daniel Kyando na (aliyevaa kizibao cha rangi ya machungwa) ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba .

Wachimbaji madini wadogo waipongeza SerikaliNa Veronica Simba – aliyekuwa Mwanza

Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), limetoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, hususani Kitengo cha

Uthaminishaji Madini ya Vito na Almasi (TANSORT), kwa jitihada inazofanya kuwainua wachimbaji wadogo nchini.

Pongezi hizo zilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa FEMATA, Gregory Kibusi wakati akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathaminishaji Madini ya Vito na Almasi iliyofanyika Agosti 12 na 13, jijini Mwanza.

“Kwa niaba ya uongozi wa FEMATA, naipongeza Serikali hasa Kitengo cha TANSORT kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa jitihada za makusudi kabisa za kuwainua wachimbaji wadogo nchini.”

Akifafanua zaidi, Kibusi alisema kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi lakini kutokana na ushirikiano ambao Serikali inautoa, hakuna shaka malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yatatimia.

Kibusi alisema, kupitia jitihada zinazofanywa na Serikali, wachimbaji wadogo wamekuwa na mwamko wa

kupata taarifa za mipango na mikakati ya Serikali juu ya maendeleo yao.

Pia, alisema jitihada za Serikali zimewezesha wachimbaji wadogo kushiriki maonesho ya madini ya vito na usonara ya ndani na nje ya nchi ambayo yanawawezesha kuuza madini hayo na kupata uzoefu kutoka nchi nyingine duniani.

“Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo sambamba na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa mlezi wa wachimbaji wao,” alisema Kibusi.

Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo wa kifedha katika kuendesha shughuli zao za uchimbaji na ukosefu wa elimu ya juu ya madini hasa ya vito.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini kutotambuliwa na baadhi ya Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kama wadau wakubwa wa maendeleo hasa kiuchumi na kijamii.

Akiwasilisha maombi ya FEMATA kwa Serikali, Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanahitaji wataalamu wa madini ya vito ili wawasaidie katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua, kuthamini, kusaidia kutafuta masoko pamoja na kutoa ushauri juu ya uongezaji thamani madini na namna bora ya kufanya biashara ya madini.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (Wa pili kushoto – waliokaa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi. Wengine kutoka Kulia (waliokaa) ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria - Magharibi, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Mrimia Mchomvu, pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo.

Page 6: MEM 81 Online.pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Zuena Msuya na Clinton Ndyetabula

Ujumbe kutoka nchini Uganda pamoja na Zanzibar wametembelea miradi ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(

BRN) inayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini ili kujifunza namna ambavyo miradi hiyo ilivyoanzishwa, inavyotekelezwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo katika eneo la Mtambo wa Kufua Umeme wa Kinyerezi 1 jijini Dar es salam, Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juma Mkobya alisema wataalam hao wamekuja kujifunza na kuona changamoto ambazo wanatakiwa kukukabiliana nazo mapema kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi kama hiyo katika nchini mwao.

Mkobya alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza kwa nchi za Afrika ambazo zimefanikiwa kuanzisha na kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa sasa katika sekta mbalimbali za maendeleo na hivyo kutumia fursa hiyo kuwataka watanzania kufanya kazi kwa kutumia mfumo wa BRN ambao unaondoa tabia kufanya kazi kwa mazoea ili kupata maendeleo ya haraka.

Mpango huo wa miaka mitatu kwa Awamu ya Kwanza ulianza Mwezi Julai 2013 na unaishia Juni 2016; kufuatia ubunifu huo, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikija nchini kujifunza ili kuwawezesha kutekeleza mpango huo katika nchi zao.

“Nchi nyingi ambazo ziko katika harakati za kuanzisha mpango wa matokeo makubwa sasa zimekuwa zikija hapa nchini kujifunza baada ya kuona mafanikio yaliyofikiwa na nchi yetu, hivyo watanzania tufanye kazi kwa kutumia mfumo wa BRN ili tuweze kujiharakishia maendeleo yetu,” alisema Mkobya.

Hata hivyo Mhandisi Mkobya

aliwaleza wajumbe hao kuwa katika miradi ya nishati inayohusisha ujenzi wa bomba la gesi, mitambo ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme ilikuwa na changamoto kadhaa zilizojitokeza kama vile mtaji, wataalam pamoja na muda wa kumaliza ujenzi huo tofauti na ilivyokuwa awali katika hatua za upembuzi yakinifu.

Pia aliwasisitiza wajumbe hao kuwa kabla ya kuanza kutekeleza mpango huo lazima waandae mpango kazi unaoweka wazi upembuzi yakinifu na ikiwezekana tayari wawe wametenga fungu maalum kwa ajili hiyo pamoja na wataalam.

Mkuu wa Msafara wa Wataalam kutoka nchini Uganda, Prof Ezra Suruma alisema ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyofikiwa na kwamba, watatumia fursa hiyo kujifunza zaidi ili na wao waweze kutekeleza mpango huo katika nchi yao kulingana na dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia na kuwataka watanzania kupiga hatua zaidi kupitia mpango huo.

“Sisi Waganda na tunajifunza kutoka Tanzania namna ya kuharakisha maendeleo kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa ambayo tayari Tanzania imepiga hatua, hapa tunajifunza mambo mengi sana hivyo watanzania mtumie fursa ya kujiletea maendeleo yatakayochangia kupiga hatua,” alisema Prof.Suruma.

Kwa upande wake Mkuu wa ujumbe kutoka Zanzibar, Kamishna Jamila Basefu aliwataka watanzania kufanya kazi kwa kutumia mfumo wa matokeo makubwa sasa ili kupata maendeleo ya haraka kwani kwa tangu mfumo huo uanzishwe kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali hasa zile zilizopo katika mpango huo.

Basefu alifafanua kuwa tayari Zanzibar imeanzisha mpango huo lakini inahitaji ujuzi zaidi kutoka Tanzania Bara ambao tayari wamefanikiwa na kutekeleza baadhi ya miradi ikiwemo ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara kwenda Dar es salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizi mengine itakayorahisisha upatikanaji wa umeme na kupunguza gharama za matumizi na uendeshaji.

Uganda, Z’bar wapata uzoefu BRN Sekta ya Nishati

Wajumbe kutoka nchini Uganda pamoja na Zanzibar wakipewa maelezo ya namna ambavyo miradi ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) inayotekelezwa na Wizara katika ukumbi wa mikutano Wizara ya Nishati na Madini.

Mkuu wa kitengo cha Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juma Mkobya akiwaeleza wajumbe hao masuala yaliyotekelezwa katika miradi hiyo.

Wajumbe kutoka nchini Uganda na Zanzibar wakitembelea mtambo wa kupokea gesi Kinyerezi Dar es Salaam.

Mkuu wa msafara wa wataalamu kutoka nchini Uganda, Professa Ezra Suruma akiwaaongoza wajumbe wengine kwenye mitambo ya kufua umeme Kinyerezi 1 jijini Dar es salaam.

Wajumbe kutoka nchini Uganda na Zanzibar katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha BRN Muhandisi Juma Mkobya wa tatu kutoka kulia.

Page 7: MEM 81 Online.pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

1. Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Gregory Kibusi akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

2. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Wizara ya Nishati na Madini, Mrimia Mchomvu, akitoa hotuba ya kufunga Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

3&4. Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

5. Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Kitengo hicho katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

6. Afisa kutoka Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Salome Tilumanywa, akiwasilisha mada kuhusu uchimbaji na biashara ya tanzanite katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

1

4

2

5

63

Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi

Page 8: MEM 81 Online.pdf

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza Mtaalamu (hayupo pichani)

Afisa Madini Mkazi- Kigoma, Adam Juma akifungua mafunzo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji madini wa Mkoani Kigoma (hawapo pichani). Kushoto kwake ni wataalamu kutoka Wizarani-Kitengo cha Leseni Idd Mganga akifuatiwa na Mhandisi Edward Mumba. Kulia kwake ni Viongozi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Kigoma (KIGOREMA), Karoli Ndimaso na Augustino Ruronona.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Mafunzo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao (OMCTP) yaliyofanyikia Mkoani humo na kuhudhuriwa na wachimbaji madini zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Baadhi ya wachimbaji madini mkoani Kigoma waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuelewa namna ambavyo mfumo huo unavyofanya kazi.

MFUMO WA HUDUMA YA UTOAJI LESENI KWA NJIA YA MTANDAO KIGOMA, CHUNYA

Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza Mtaalamu (hayupo pichani)

Maafisa kutoka Ofisi ya Madini ya Afisa Mkazi- Chunya wakifuatilia mafunzo. Wa kwanza kushoto ni Samwel Gombekile, Mzee Mussa (katikati) na Severine Haule.

Page 9: MEM 81 Online.pdf

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

ZIARA YA MWIJAGE MTWARA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu) akiangalia mafundi wa kampuni ya Namis wakisimika nguzo za umeme katika kijiji cha Sinde B mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kushoto ) akiwa katika chumba cha kuendeshea mitambo ya gesi kilichopo katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara mara alipowasili kituoni hapo kukagua mitambo ya kuchakata gesi (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu) akipata maelezo kuhusu hatua iliyofikia kwenye ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara.Anayetoa maelezo ni Karoli Blaz (kushoto) , Msimamizi wa Uendeshaji na Matengenezo ya Mitambo katika kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO).

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu) akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali kukagua kisima cha gesi (MB3) katika eneo la Msimbati mkoani Mtwara. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na aliyevaa kitenge ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kushoto mstari wa mbele ) akikagua mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally na kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba .

Baadhi ya mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara. Gesi asilia itasafishwa katika kituo hicho kabla ya kusafirisha kwa bomba la Gesi.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu ) akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walio katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara mara alipowasili kituoni hapo kukagua mitambo ya kuchakata gesi.Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba .

Naibu waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara.Kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Mtwara, ALfred Luanda.

Page 10: MEM 81 Online.pdf

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

KONGAMANO LA DIASPORA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Msanga Mkuu mkoani Mtwara, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio (kushoto) akizungumza na Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Michael Serek (wa pili kushoto) alipotembelea Banda la TPDC, pamoja na mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akimzawadia Cheti cha kutambua mchango wa Kongamano la Diaspora, Afisa kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ally Mluge (kulia).

Mhandisi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Felix Nanguka (kulia) akitoa maelezo kuhusu sehemu za uzalishaji wa gesi asilia kwa baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio (kulia) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) alipotembelea banda la TPDC katika Kongamano la Diaspora jijini Dar es Salaam.

Page 11: MEM 81 Online.pdf

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI KUHUSU MATUMIZI YAHUDUMA ZA LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO – KANDA YA ZIWA NYASA - SONGEA NA TUNDURU

Afisa Madini Mkazi Tunduru, Mhandisi Frederick Mwanjisi akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji madini yaliyofanyikia katika ukumbi wa Clasta wilayani Tunduru.

Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwaelekeza wachimbaji wadogo wa wilayani Tunduru namna Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa njia ya Mtandao unavyofanya kazi. Wa Kwanza kushoto ni Idd Mganga na anayemfuatia ni Mhandisi Edward Mumba.

Mchimbaji mdogo wa Wilayani Tunduru, Mwajuma Omari akitoa shukrani kwa niaba ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo hayo kwa Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini hawapo pichani.

Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mgangaakiongea jambo wakati wa mafunzo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ufundi (VETA), mjini Songea.

Baadhi ya wachimbaji Madini wa Songea wakimsikiliza Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo ya mjini Songea

Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini- Kitengo cha Leseni, Idd Mganga (kushoto aliyesimama) akielezea Historia ya utoaji Leseni za Madini nchini wakati wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Songea. Wa kwanza kulia ni Mtaalamu kutoka Kitengo hicho, Mhandisi Edward Mumba na anayemfuatia ni Mhandisi George Wandibha wa Ofisi ya Kanda ya Madini Songea.

Page 12: MEM 81 Online.pdf

12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Waziri akiwakabidhi nyaraka za kusafiria na zenye maelezo baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masoma katika masuala ya mafuta na gesi nchini China. Katikakati ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile.

Mmoja wa Wanafunzi waliopata ufadhili wa Masomo ya Shahada ya Uzamivu (Phd), Mabeyo Ezekiel akipokea Nyaraka za Ufadhili kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene , Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mrimia Mchomvu.

Baadhi ya Wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma masuala ya mafuta na gesi nchini China wakisoma baadhi ya nyaraka baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya Watumishi wa Wizara na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo katika ngazi za Shahada za Uzamivu (Phd) na Uzamili (Masters), katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akisisitiza jambo kwa wanafunzi kabla ya kuwakabidhi nyaraka za Ufadhili kwa ajili ya masomo yao nchini China.

Watanzania 22 wapata Ufadhili kusoma Mafuta, Gesi China

Page 13: MEM 81 Online.pdf

13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Mwandishi Wetu, Mongolia

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imedhamiria kuboresha mazingira ya uchimbaji mdogo wa madini nchini ili kuboresha vipato vya wachimbaji na hatimaye

kuchangia ukuaji uchumi wa taifa.Hatua hiyo imefikiwa na Wizara ya

Nishati kupitia Idara ya Madini baada ya kupeleka timu ya wataalam wa Madini inayoongozwa na Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja nchini Mongolia, kujifunza namna nchi hiyo ilivyofanikiwa kuboresha mazingira ya uchimbaji wa madini unaofanywa na wachimbaji wadogo na hatimaye kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa.

Miongoni mwa mafanikio ambayo Mongolia imepata kutoka kwa wachimbaji wadogo ni pamoja na kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Aidha, wachimbaji hufuata sheria na taratibu kwa kuhakikisha kwamba hakuna mchimbaji wa madini anayechimba bila ya kuwa na leseni pamoja na kuhakikisha hawasababishi uharibifu wa mazingira.

Pia, kila mchimbaji na wafanyakazi

wanaojishughulisha na uchimbaji mdogo lazima wazingatie masuala yote yanayohusu afya na usalama kazini kwa kuhakikisha wanatumia vifaa vya kujikinga na ajali.

Vilevile, wachimbaji wadogo wa Mongolia ni wanachama wa mifuko ya kijamii ambapo hupatiwa bima za afya, usalama kazini pamoja na bima baada ya kuacha shughuli za uchimbaji wa madini ambayo kwa namna moja ama nyingine huwasaidia kwa kiasi kikubwa wachimbaji wadogo.

Wachimbaji wadogo kwa kiasi kikubwa nchini Mongolia wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na Serikali ya nchi hiyo ambapo wakati wote maofisa mbalimbali wa madini wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kwa ajili ya kuwapatia elimu na taarifa ya namna bora ya uchimbaji madini pamoja na kuwakumbusha namna ya kujishughulisha na shughuli hizo kwa njia salama zaidi.

Mongolia ni miongoni mwa nchi chache zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mazingira mazuri ya wachimbaji wadogo ambapo kwa kiasi kikubwa huchangia uchumi wa nchi yao kutokana na shughuli za uchimbaji madini.

Shughuli za wachimbaji wadogo zilianza miaka kumi iliyopita baada ya nchi hiyo kupata changamoto ya dhoruba ya baridi kali zaidi ya nyuzi joto ‘negative 40’ na kusababisha mifugo mingi kufa ambayo ilikuwa tegemeo kubwa kwa nchi hiyo kiuchumi kutokana na wananchi wengi kujishughulisha na ufugaji.

Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeamua kupeleka maofisa wake wa madini kujifunza namna bora ya kuboresha uchimbaji mdogo ili kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini waweze kunufaika na kazi hiyo na kulinufaisha taifa kwa ujumla.

Dalili njema ugunduzi gesi asilia Morogoro, Pangani

Serikali kuboresha mazingira ya wachimbaji wadogo

Asteria Muhozya na Clinton Ndyetabula, Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameeleza kuwa, zipo dalili njema za kugundua gesi

katika maeneo mengine nchini baada ya kugundulika kwa kiasi kikubwa cha gesi asilia chenye futi za ujazo trilioni 55.08 (tcf) katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani.

Simbachawene aliyataja maeneo ambayo yameonesha dalili ya kuwepo gesi asilia mbali na mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa ni Morogoro na Pangani na kusema kuwa, maeneo hayo yameonyesha dalili njema ya uwepo wa gesi asilia.

Waziri Simbachawene aliyasema hayo hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, wakati akitoa nyaraka za ufadhili wa masomo kwa watanzania 22 waliopata ufadhili kusomea masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada za Uzamivu (Phd) na Uzamili (Masters), nchini China.

Alisema kuwa, uwepo wa gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na dalili ambazo zimeonekana katika maeneo mengine ni kiashiria kuwa, Tanzania inaingia katika uchumi wa gesi na hivyo

taifa linatarajiwa kunufaika na rasilimali hiyo kwa kuwa kiwango kilichopatikana ni kikubwa cha kuifanya nchi kupiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia rasilimali hiyo.

“Kuna nchi zina gesi futi za ujazo 10 (tcf) tu lakini wamepiga hatua kubwa ya maendeleo kupitia gesi asilia. Kwa kiasi tulichonacho na ambacho tunaendelea kugundua ni wazi kuwa tunaingia katika uchumi wa gesi na ndio sababu tumeanza kutayarisha wataalamu wetu wenyewe,” aliongeza Simbachawene.

Akizungumzia Sheria zilizosainiwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. Jakaya Kikwete, zikiwemo Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia, Uwazi na Uwajibikaji na Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi Asilia, alisema kuwa, Sheria hizo zinaondoa wasiwasi wa namna taifa litakavyonufaika na rasilimali hiyo.

“Lazima mwende mkijua hali halisi ya nyumbani ikoje kuhusu sekta hii. Tayari sheria zipo lakini hakuna mkataba wowote uliosainiwa zaidi ya Mikataba ya Songosongo, hivyo msidanganywe katika

hili. Mpaka sasa tuko salama kwa asilimia 99. Tutawapa sheria hizi mzisome ili mtushauri mahali tulipokosea,” alisisitiza Simbachwene.

Jumla ya wanafunzi waliopata ufadhili huo kutoka Serikali ya Watu wa China baada ya kukidhi vigezo ni 22, kati ya maombi 187 yaliyotumwa. Aidha, Serikali ya China imeahidi kuendelea kutoa ufadhili wa masomo ya mafuta na gesi kwa watanzania watakaokidhi vigezo vya kujiunga na Vyuo vilivyobobea katika masuala hayo nchini humo hadi mwaka 2019.

Majina ya waliochaguliwa ni pamoja na Maagi Mtaki Thomas, Mkemai Rashid Mohamed, Mabeyo Petro Ezekiel, Hemed Kijakazi, Msafiri Kattiba Saada, Msongela Anna, Magambo Christina, Sanga Modekai, Sebe Mgeta Faustine, Kikulu Mukhusin Rajab, Lyimo Rosemary, Lyaka Japhet, Nziku Eliezery, Kessy Emmanuel Goodluck, Hechei Felician David, Mohamed Ad-Ham Said, Kironde Birungi Joseph, John Hillonga Emiliana, Hassa Khalfan Hamisi, Ryoba Catherine Robi, Mwijage Edith na Robert Faustine Edwin.

Kuna nchi zina gesi futi za ujazo 10 (tcf) tu lakini wamepiga hatua kubwa ya maendeleo kupitia gesi asilia. Kwa kiasi tulichonacho na ambacho tunaendelea kugundua ni wazi kuwa tunaingia katika uchumi wa gesi na ndio sababu tumeanza kutayarisha wataalamu wetu wenyewe ”.

Mongolia ni miongoni mwa nchi chache zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mazingira mazuri ya wachimbaji wadogo”.

Na Mwandishi wetu, Mongolia

Serikali ya Mongolia imefanikiwa kudhibiti madini yote ya nchi hiyo kuuzwa kwa kupelekwa nje ya nchi na badala yake huuzwa Benki Kuu ambayo ndiyo yenye

mamlaka ya kuuza madini kwa wanunuzi wanaotoka nje ya nchi hiyo.

Hayo yameelezwa wakati wa ziara ya mafunzo ya Ujumbe kutoka Tanzania unaojifunza mafanikio iliyopata nchi ya Mongolia katika sekta ya Madini, ambapo ulielezwa kwamba, utaratibu huo mzuri unazuia kwa kiasi kikubwa utoroshaji wa madini pamoja na biashara haramu ya madini kwa nchi yoyote.

Maofisa waandamizi wa Benki Kuu ya Mongolia waliueleza ujumbe huo, kuwa njia hiyo ni bora katika kudhibiti biashara haramu na utoroshaji wa madini ambapo

kwa kiasi kikubwa umesaidia kuongeza mapato ya taifa hilo yanatokana na shughuli za madini katika nchi hiyo.

Walisema kuwa, wachimbaji wa madini wakubwa na wadogo pamoja na wauzaji wa madini wanapopeleka madini yao Benki Kuu, madini hayo hukaguliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Madini ijulikanayo kwa jina la Assay Inspection Department (AID) ili kuhakiki thamani yake na baada ya hapo madini hayo huchenjuliwa na Benki Kuu ya Mongolia na kuyaweka katika viwango vya kimataifa.

Imeelezwa kuwa, hatua hiyo imeisaidia kwa kiasi kikubwa Mongolia kuinua pato la taifa.

Kwa upande wa Tanzania utaratibu kama huo ulikuwapo awali mwaka 1990 ilipofika mwaka 1995 serikali iliusitisha utaratibu huo wa kuuza madini katika Benki Kuu ya Tanzania baada ya kutokea changamoto kadhaa.

Sekta ya Madini Tanzania yapata uzoefu Mongolia

Page 14: MEM 81 Online.pdf

14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Samwel Mtuwa, GST

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP),

imepata vifaa vya kisasa vya Jiofizikia kwa ajili ya utafiti wa madini pamoja na uanishaji wa maeneo mapya ya utafiti wa madini kutokana na taarifa za kiuchunguzi zitakazotolewa na vifaa hivyo.

Akizungumza na MEM Bulletin, Mkuu wa kitengo cha Jiofikia (GST) Octavian Minja, alisema kuwa, mradi wa SMMRP umeipatia GST vifaa vya kisasa vitakavyofanya kazi kwa ubora pamoja na kuongeza thamani ya taarifa za kiutafiti.

Alisema kuwa, uwepo wa vifaa hivyo vya kisasa unatokana na baadhi vifaa vya awali kuchakaa na kuvitaja kuwa ni pamoja na GSM – 19 GW v7.0Gradiometer , GSM-19W v7.0 Magnetometer , GSMP – 35 v 8.0 Signal Processing Console yenye RS-2323 na Strap , PROMIS –FDEM System , Kapameter , Portable Gamma –Ray Spectrometer , Gaussmeter Model GM-2 na Geovista Digital Logger.

Aidha aliongeza kuwa, kuwepo kwa vifaa hivyo kutasaidia kuongezeka kwa idadi ya watafiti ikiwemo kuongeza ufanisi na ubora wa kazi kutokana na vifaa hivyo

kutumia mfumo mzuri wa digitali katika upimaji na uchukuaji wa taarifa za kiutafiti wa miamba na madini.

“Kuwepo kwa vifaa hivi kutasaidia kuongezeka kwa idadi ya watu yaani watafiti na kuongeza ufanisi na ubora wa kazi ,kutokana na vifaa vipya kutumia mfumo mzuri wa digitali wa upimaji na uchukuaji wa taarifa za kiutafiti wa miamba na madini,” alisema Minja.

Minja aliongeza kuwa, vifaa hivyo vinafanya kazi mbalimbali ikiwemo kupima miamba yenye asili ya madini ya chuma ambayo yanaweza kuambatana na miamba yenye madini ya dhahabu, ikiwemo kusaidia kutambua miamba yenye mipasuko ya nyufa katika eneo linalofanyiwa utafiti (Magnetic Survey), kupima miamba yenye asili ya kupitisha umeme pamoja na kupima uwepo wa madini yenye asili ya mionzi kama vile Uranium, potassium na thorium.

Vilevile, alieleza kuwa, katika matumizi ya vifaa hivyo, GST na taifa kwa ujumla zitafaidika kwa kuwawezesha wawekezaji kupata maeneo sahii ya madini , kuongeza taarifa za Jiofikia katika Kanzi Data ya GST .

Minja alizitaja faida nyingine kuwa ni kufanya utafiti wa Jiofikia katika maeneo mapya yanayotarajiwa kupimwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu au

makazi ya watu na hivyo kuwapunguzia gharama wawekezaji katika utafiti wa madini kwa kutumia vifaa hivyo. “Hii ni kutokana kuwa hapo awali vifaa kama hivi vilipatikana kutoka nchi za jirani kama vile Botswana, Zimbambwe na Afrika ya kusini,” alisema Minja.

Pia, Minja aliwataka watanzania pamoja na wadau waliopo katika sekta ya madini kufika katika Ofisi za GST ili kupata huduma na taarifa za utafiti wa madini kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya sasa.

GST YAPATA VIFAA VYA JIOFIZIKIA

Mkuu wa kitengo cha Jiofizikia kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Octaviani Minja akionesha vifaa vya kisasa vya Jiofizikia vilivyopo katika kitengo cha Jiofizikia GST, pembeni yake alievaa shati la vyumba ni Priscuss Benard Afisa Biashara wa GST.

Mufindi waomba mafunzo ya OMCTP yatolewe migodiniNa Mohamed Saif, Mufindi

Wachimbaji wadogo wa madini wameiomba Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha mafunzo ya huduma

ya leseni kwa njia ya mtandao yanawafikia wachimbaji madini walioko migodini.

Ombi hilo lilitolewa hivi karibuni wilayani Mufindi na wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo hayo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Kitengo cha Leseni za Madini cha Wizara hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji madini waliohudhuria mafunzo hayo, Grace Mgina, mchimbaji mdogo wa madini kutoka kijiji cha Ihanzutwa wilayani humo aliiomba Wizara hiyo kutoa mafunzo ya namna hiyo kwenye maeneo ya migodini ili kuleta tija zaidi.

Alisema si wachimbaji wote wameweza kuhudhuria kutokana na sababu mbalimbali na hivyo haitakuwa vyema kama wizara haikutembelea migodini ili kuwafikia wale ambao hawakupata fursa hiyo.

“Tunaomba hii semina itolewe pia kijijini kule kwenye migodi ili kuepusha taarifa ambazo si sahihi kusambaa kwasababu si wachimbaji wote wameweza kuhudhuria,” alisema Mgina.

Aidha, aliipongeza wizara hiyo kwa kuandaa mafunzo na kueleza namna ambavyo huduma hiyo ya leseni kwa njia ya mtandao itakavyowanufaisha wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Al isema

kumekuwepo na changamoto nyingi katika

shughuli za uchimbaji madini hususan

miongoni mwa wachimbaji wadogo. “Mfumo huu ni mzuri sana maana tulikuwa na changamoto nyingi kwenye shughuli zetu lakini kwa namna tulivyoelezwa na wataalamu naona ufumbuzi sasa umepatikana,” alisema Mgina.

Mgina aliiomba wizara hiyo kulifanyia utafiti eneo la Ihanzutwa au isaidie kupeleka wataalam ili kuwahakikishia wachimbaji wadogo kama eneo hilo lina tija badala ya kuchimba mashimo kwa kubahatisha kama ilivyo hivi sasa.

“Kumekuwa na watu wanaojiita wataalam ambao wanadai wanavyo vifaa vya kutambua uwepo wa dhahabu ‘detector’. Wanaelekeza mahali pa kuchimba ila mwisho wake mchimbaji anajikuta ametumia gharama kubwa bila kupata madini hayo,” alisema Mgina.

Naye mtaalam kutoka wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga aliwaasa wachimbaji hao kuhakikisha wanafika katika Ofisi za Madini zilizo karibu yao ili waweze kusajiliwa na kuanza kutumia huduma hiyo.

“Mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mnafika katika Ofisi zetu ili tuwasijili. Kwa wenye leseni hai hakikisheni mnakuja na leseni halisi na sio nakala,”

alisisitiza Mganga.Alisema mafunzo kuhusu huduma ya

leseni kwa njia ya mtandao yataendelea kutolewa kwenye Ofisi za Madini nchi nzima na hivyo aliwataka wachimbaji hao kuhakikisha hawaachi kutembelea ofisi za madini zilizo karibu yao ili kuendelea kujifunza.

“Wataalamu kwenye kila ofisi za madini nchini wataendelea kuwaelekeza hadi hapo kila mmoja atakapoweza kuutumia mfumo huu yeye mwenyewe. Ukiona kuna sehemu inakutatiza usisite, fika kwenye ofisi iliyo karibu yako ili uelekezwe,” alisema.

Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mbeya, Mhandisi Ramadhan Lwamo aliwataka wachimbaji waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa wachimbaji wengine kwa kuhakikisha wanafikisha yale ambayo wao wamejifunza.

Alisema Ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya kuwasajili na pia kwa ajili ya kuwaelekeza zaidi kuhusu mfumo huo na pia kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za uchimbaji madini.

Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao tarehe 8 Juni, 2015. Pamoja na malengo mengine, inaelezwa kwamba mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.

Mhandisi Ramadhan Lwamo akifungua Mafunzo ya Huduma ya Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji wadogo wilayani Mufindi (hawapo pichani) kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mbeya.

Page 15: MEM 81 Online.pdf

15BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Teresia Mhagama, Mtwara

Imeelezwa kuwa Mpango Kabambe wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili katika mikoa ya Lindi na Mtwara umekamilika kwa asilimia 98.

Hayo yalisemwa na Mhandisi Christopher Bitesigirwe wa Wizara ya Nishati na Madini, katika ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage kukagua utekelezaji wa mradi wa kuchakata gesi asilia katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara na miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayotekelezwa pembezoni mwa bomba la Gesi linalotoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam.

Bitesigirwe alieleza kuwa, katika mkoa wa Lindi, ujenzi wa njia ya msongo wa kilovoti 33 wenye umbali wa kilomita 327 umekamilika kwa asilimia 100.

Vilevile ujenzi wa njia ya msongo mdogo yenye umbali wa kilomita 99 kati ya kilomita 108, imekamilika kwa asilimia 92.

Alifafanua kuwa, miradi hiyo katika mkoa wa Lindi inatekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya OK ambaye pia alipewa nyongeza ya vijiji katika

maeneo ambapo bomba la gesi linapita ambapo hivi sasa nguzo za umeme ambazo ni vifaa vya mwisho katika maandalizi zinatarajiwa kuwasili katika

eneo la mradi mwezi huu.Bitesigirwe aliongeza kuwa katika

mkoa wa Mtwara mkandarasi ambaye ni kampuni ya Namis amekamilisha kazi

yake ya usambazaji umeme kwa asilimia 98.6.

“Mkoani Mtwara ujenzi wa njia ya msongo wa kati wa kilovoti 33 yenye umbali wa kilomita 213 imekamilika kwa asilimia 100, pia katika ujenzi wa njia ya msongo mdogo, kilomita 81 kati ya kilomita 82.5 sawa na asilimia 98 zimekamilika na transfoma 34 kati ya 39 zimefungwa,” alisema Bitesigirwe.

Alibainisha kuwa, katika kutekeleza kazi ya nyongeza ya mkataba wa kupeleka umeme kwenye wilaya za Newala na Masasi yenye umbali wa kilomita 7.5 katika msongo wa kilovoti 33 na umbali wa kilomita 11.16 katika msongo mdogo, tayari usimikaji wa nguzo wa kati umekamilika kwa asilimia 100.

Vilevile alieleza kuwa kazi ya nyongeza ya mkataba inayohusisha upelekaji umeme kwenye wilaya za Mtwara Vijijini na Tandahimba na ambayo bomba la gesi linapita, mkandarasi Namis anaendelea kusambaza nguzo kwenye eneo la mradi. Kazi hiyo itahusisha ujenzi wa msongo wa kati wa umbali wa kiliomita 304.92, msongo mdogo kwa umbali wa kilomita 265.15 na kuunganisha kwa wateja wa awali wapatao 9,217.

Akifanya majumuisho ya ziara hiyo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya umeme vinafika kwa wakati katika maeneo husika ili kazi hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.

Miradi kabambe ya umeme Lindi, Mtwara yakamilika kwa asilimia 98

Naibu waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili) kushoto akijadiliana jambo na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini alioambatana nao katika ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa wa Mtwara.Kutoka kushoto ni Mjiolojia Mkuu, Sebastian Shana, Mhandisi Robert Dulle na Mhandisi Christopher Bitesigirwe.

OMCTP Mfumo rafiki kwa Wachimbaji wadogo wa madiniNa Mohamed Saif, Chunya

Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kutohofia Mfumo wa Huduma ya Utoaji Leseni kwa

njia ya Mtandao ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).

Wito huo ulitolewa hivi karibuni wilayani Chunya na Afisa Madini Mkazi- Chunya, Mhandisi Donald Mremi wakati wa akifungua Mafunzo ya Huduma ya Leseni kwa wachimbaji Madini wa wilayani hapo.

Mhandisi Mremi alisema Mfumo huo wa kielektroniki ni rafiki kwa mtumiaji na hivyo, kuwataka wachimbaji madini nchini wasiogope na badala yake wasikilize kwa umakini mafunzo yanayoendelea kutolewa na wataalamu wa Wizara.

“Nawaomba msikilize kwa makini yale ambayo wataalamu watawaeleza, na baada ya mafunzo mfike Ofisini ili tuwasajili. Vilevile, tutaendelea kuwa tunawapatia mafunzo kuhusu huduma hii,” alisema Mremi.

Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao tarehe 8 Juni, 2015. Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.

PICHA KUBWAAfisa Madini Mkazi- Chunya, Mhandisi Donald Mremi akifungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji wadogo wilayani Chunya.

PICHA NDOGOBaadhi ya wachimbaji wadogo wa Madini wa Wilayani Chunya wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Page 16: MEM 81 Online.pdf

16BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Na Godfrey Francis, Stamigold

Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella a m e u m w a g i a pongezi nyingi

mgodi wa dhahabu wa Stamigold Biharamulo ambao ni Kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), baada ya kuvutiwa na idadi kubwa ya wataalamu wazawa na menejimenti shiriki.

Mongella alitoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi katika mgodi huo unaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu, iliyolenga kufahamu shughuli nzima za uzalishaji zinazofanywa na mgodi wa Stamigold na kukutana na uongozi wa mgodi. Aidha, Mkuu huyo alipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali mgodini hapo na kupata maelezo ya kina kutoka kwa watalaamu ambao wote ni Watanzania hatua ambayo aliipongeza.

Mkuu huyo wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea eneo la uchimbaji (Mining/Pit) ambapo alipata ufafanuzi wa kitaalamu na eneo la Uchenjuaji Dhahabu (Process Plant) ambako pia alifahamishwa namna dhahabu inavyochenjuliwa.

Akizungumza katika ziara hiyo Mongella alipongeza uwepo wa wataalamu wazawa katika mgodi huo na kueleza kuwa, “nimejifunza kuwa Watanzania tunaweza, tujiamini. Katika ziara yangu hii mwanzo hadi mwisho nimekutana wataalam wazawa na wote wamenieleza masuala mbalimbali kwa weledi,” alisema Mongella.

Aidha, alipongeza kuhusu uongozi shirikishi uliopo mgodini hapo na kusema kuwa “wafanyakazi wote wana taarifa kuhusu mgodi huu na hili linadhihirisha ushirikishwaji mkubwa uliopo baina ya uongozi, wafanyakazi, wakandarasi na wadau wa kampuni hii,” aliongeza Mongella.

Vilevile, Mongella alipongeza kuhusu ulinzi na usalama uliopo mgodini hapo ikiwemo ushirikiano baina ya wafanyakazi wote na kusema “pongezi nyingi kwa uongozi na wafanyakazi wote, naahidi ushirikiano na nitatumia nafasi yangu kuwasemea ili kuhakikisha Stamigold inayafikia malengo yake iliyojiwekea”, aliongeza Mongella.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alishauri Kitengo cha Mawasiliano mgodini hapo kuandaa Mkakati wa Mawasiliano ili kuhakikisha taarifa sahihi kuhusu mgodi huo

zinawafikia Watanzania.Naye, Kaimu Meneja Mkuu

wa Stamigold, Enea Minga akizingumza wakati wa ziara hiyo, alizitaja changamoto kadhaa ikiwemo mgodini hapo kuwa, ni pamoja na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, Uvamizi unaofanywa na wachimbaji wadogo bila ya kusahau Mifugo na kuongeza kuwa, pamoja na changamoto hizo, uongozi wa mgodi kwa kukishirikiana na wataalamu wake umeendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kupunguza kama sio kumaliza kabisa changamoto hizo.

Akieleza kuhusu mafanikio yaliyopatikana mgodini hapo, Minga alisema kuwa, mgodi huo umefanikiwa kulipa kodi zote bila kupata msamaha, ajira zaidi ya 600 kwa watanzania, utafiti wakijiolojia ili kuongeza umri wa mgodi kutoka miaka 2 hadi 5, kujenga barabara ya

kilometa 4 ikianzia eneo la Uchimbaji hadi eneo la Uhifadhi Udongo wa Dhahabu (ROM PAD),

Aliyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja kutengeneza Madawati 1500 na kuyagawa kwa shule 30 zilizo mkoani Kagera, kuunda vikundi vidogo vidogo vya ujasiliamali ndani ya vijiji vya jirani vya mgodi ambavyo pia vimekuwa vikiuuzia mgodi huo vyakula mbalimbali kama mboga mboga ili kuinua uchumi wao.

“Kampuni ya Stamigold itaendelea kujivunia kuwepo kwa kiasi kikubwa cha hifadhi ya dhahabu iliyo katika maeneo yake, weledi wa wataalamu wake ambao ni watanzania waliojitolea kwa hali na mali, Ushirikiano na Mahusiano mema baina ya Mgodi na vijiji vilivyo jirani na mgodi,”alisema Minga.

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Mkuu huyo kutembelea mgodini hapo tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera mapema mwaka jana. Pamoja naye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo , Darry Ibrahim Rwegasira, Katibu wa Mkuu wa Mkoa, Thomas Salala na Afisa Misitu wilaya ya Biharamulo, Selemani.

MKUU WA MKOA KAGERA AIPONGEZA STAMIGOLD

Mkuu wa Mkoa Kagera John Mongella (Wa pili kulia - mbele) katika picha ya pamoja na Kaimu Meneja Mkuu Stamigold Enea Minga (katikati), Mkuu wa Wilaya –Biharamulo Darry Ibrahimu Rwegasira( wa pili kushoto), Mrakibu Rasilimali watu David Nyagiro (wa kwanza Kulia-mbele), Kaimu Meneja Uchimbaji Ayoub Nyenzi ( wa kwanza kushoto) na baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Stamigold Biharamulo hivi karibuni mara baada ya kuhitimisha ziara yake mgodini hapo.