Upload
others
View
266
Download
19
Embed Size (px)
Citation preview
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 1
MASWALI NA MAJIBU
Kidato cha 1 – 6
Tumia muongozo huu kupata umahiri wa jinsi ya kujibu maswali kwa usahihi, aidha usiishie hapo
kwani maswali ni mengi na si rahisi kuyachambua yote lakini kwa muongozo huu utaweza kupata
msingi bora wa kujibia maswali mbalimbali.
Iwapo una maoni, mapendekezo au ushauri wowote tafadhali wasiliana name kwa njia zilizopo
hapa chini.
Kwa mawasiliano zaidi:
Simu: 0717104507
0766104507
0735104507
0684104507
Baruapepe: [email protected]
Tovuti: www.mwalimuwakiswahili.co.tz
MAENEO YALIYOGUSWA:
1. FASIHI KWA UJUMLA
2. SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
3. UFAHAMU NA UTUNGAJI
4. MAENDELEO YA KISWAHILI
5. JINSI YA KUJIBU MASWALI YA VITABU
mailto:[email protected]
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 2
Fasihi kwa Ujumla
1. Eleza maana ya Fasihi.
Au: Ni nini maana ya Fashi?
Majibu:
Fasihi ni Sanaa itumiayo lugha kufiksha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia ya masimulizi yam
domo au maandishi. Fasihi husemwa kuwa ni Sanaa kwa sababu kwanza yenyewe ni mojawapo ya
matawi ya Sanaa (yaani ni sawa na kusema mtoto wa nyoka ni nyoka) lakini pili ni kuwepo kwa
vipengele vya kisanaa (kifani) katika kazi ya fasihi. Nyenzo kuu ya fasihi ni maneno teule ya lugha.
2. Taja dhima za fasihi katika jamii
Au: Taja faida za fasihi katika jamii
Au: Fafanua kazi za fasihi katika maisha ya mwanadamu
Au: Fasihi ina umuhimu gani katika jamii?
Majibu:
Fasihi ni Sanaa itumiayo lugha kufiksha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia ya masimulizi yam
domo au maandishi. Fasihi ina umuhimu mkubwa kwa jamii kama ifuatavyo:
Hukuza lugha ya jamii husika kupitia mawasiliano na kupashana habari za kifasihi miongoni
mwa wanajamii.
Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii husika
Huchochea maendeleo ya jamii kupitia kuhimiza kazi mfano nyimbo za kazi na majigambo.
Hudumisha umoja na mshikamano baina ya wanajamii kupitia tanzu kama ngoma
Hutoa malezi kwa jamii kupitia tanzu kama hadithi, michezo ya watoto na jando na unyago
Huchochea mabadiliko ya kijamii kifikra, kisiasa na kiuchumi na hivyo fasihi ni sawa na silaha
ya ukombozi wa jamii
Huhifadhi na kurithisha amali mbalimbali za jamii kwa vizazi mbalimbali.
3. Je, kuna tanzu ngapi za fasihi? Fafanua tofauti zinazojitokeza katika tanzu hizo.
Majibu:
Kuna tanzu mbili za fasihi ambazo ni fasihi simulizi na fasihi andishi. Fasihi simulizi ni ile
inayowasilishwa kwa njia ya masimulizi yam domo na kupokezwa kizazi kimoja na kingine. Usanii
wake humtegemea fanani ambaye huwasiliana ana kwa ana na hadhira yake.
Fasihi andishi ni ile ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Usanii wake humtegemea mwandishi
ambaye hukaa peke yake akaibuni, akaitunga na kuiandika kazi yote ya fasihi.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 3
Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi
Fasihi Simulizi Fasihi andishi
Huwasilishwa na fanani kwa njia ya masimulizi
yam domo
Huwasilishwa na mwandishi kwa njia ya
maandishi
Huhifadhiiwa kichwani na kusambazwa kwa njia
ya masimulizi
Huhifadhiwa kwa maandishi na kusambazwa kwa
maandishi
Ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi (hadithi,
semi, ushairi, Sanaa za maonesho)
Ina tanzu chache kuliko fasihi simulizi (ushairi,
riwaya, tamthiliya)
Ina uhuru wa kutumia wahusika wa aina
mbalimbali kama vile binadamu na viumbe
vinginevyo
Haina uhuru huo. Mara nyingi wahusika wake ni
binadamu wa kawaida tu
Ni mali ya jamii nzima inayohusika Ni mali ya mwandishi/mtunzi
Hadhira yake ni watu wote katika jamii – watoto,
wazee, wanaojua kusoma na wasiojua kusoma
Hadhira yake ni wale wanaojua kusoma na
kuandika tu
Ina hali ya utendaji – inapowasilishwa
huambatana na utendaji wa viungo vya mwili mf.
Kupiga makofi, vigelegele, kutingisha kichwa.
Haina utendaji wala ushiriki wa hadhira
Ni kongwe kuliko fasihi andishi. Ilianza baada ya kugunduliwa kwa maandishi
hivyo si kongwe
Hubadilika kulingana na wakati na mazingira Haibadiliki baada ya kuandikwa
4. Fafanua kwa mifano dhana zifuatazo:
(a) Nahau (b) Tashihisi (c) Tarihi (d) Mubalagha (e) Methali
Majibu:
(a) Nahau: ni semi fupifupi zenye kutoa maana iliyokinyume kwa kutumia lugha ya picha.
Mfano:
Amevaa miwani (amelewa)
Amepata jiko (ameoa)
Kumkalia kitako (kumsema)
Kumlamba kisogo (kumsengenya)
(b) Tashihisi: ni tamathali ya semi inayovipa uwezo wa kibinadamu vitu au viumbe visivyo na sifa ya
utendaji wa kibinadamu.
Mfano:
Kaburi lilimsitiri na aibu
Mawimbi yalipiga makofi
Misitu ikatabasamu
Mawingu yakafunga kumuondolea udhia
(c) Tarihi: ni kipera cha hadithi kinachosimuliwa kuhusu matukio ya kihistoria yaliyowahi kuikumba
jamii. Tarihi aghalabu huambatana na wakati wa utokeaji wa tukio lenyewe.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 4
(d) Mubalagha: ni tamathali ya semi inayotia chumvi mazungumzo kwa lengo la kuleta uhalisia wa
tukio lenyewe.
Mfano:
Tulimlilia Nyerere tukajaza bahari ya machozi
Watu walikuwa wengi kama sisimizi
Chakula kilikuwa kingi kama mchanga
(e) Methali: ni semi zenye hekima na busara zitumikazo kuonya, kuadibu na kuadilisha jamii.
Mfano:
Aisifuye mvua, karowa mwilini mwake
Asiyejua maana haambiwi maana, akiambiwa maana hiyo si maana.
Mwana wa muhunzi asiposana, hufukuta
Ada yam ja hunena, muungwana vitendo
5. Fafanua sifa mbalimbali za fasihi simulizi
Majibu:
Fasihi simulizi ni kazi ya Sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya masimulizi
yam domo.
Sifa za fasihi simulizi:
Inahusisha utendaji wa viungo vya mwili
Fanani na hadhira huonana ana kwa ana
Haina gharama za maandalizi
Haibagui watu kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika
Hadhira yake hushiriki katika uwasilishaji
Hubadilika kulingana na wakati na mazingira
Huwa ni mali ya jamii nzima
Huhifadhiwa kichwani
Huwa na uwanja maalumu wa kutendea mf. Matambiko (chini ya miti mikubwa, milimani au
mapangoni)
6. Fasihi simulizi ina dhima gani katika jamii?
Majibu:
Fasihi ni Sanaa itumiayo lugha kufiksha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia ya masimulizi yam
domo au maandishi.
Fasihi Simulizi ina dhima zifuatazo katika jamii:
Kuelimisha na kufundisha jamii ili ifuate mkondo mwema wa maisha mf. Jando na Unyago
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 5
Kuburudisha na kuliwaza jamii baada ya kazi ngumu mf. Ngoma
Kutoa maadili mema katika jamii mf. Vigano
Huhimiza umuhimu wa kazi katika jamii mf. Majigambo
Hutunza historia ya jamii mf simulizi kama tarihi
Huchangia katika uandishi wa fasihi andishi kutokana na kutumiwa kwa vipengele vya fasihi
simulizi kama ngoma, nyimbo, matambiko na hadithi katika fasihi andishi.
Husaidia kukuza lugha kutokana na watunzi wa fasihi simulizi kutumia lugha kisanaa
7. Fafanua aina tano za wahusika wa fasihi simulizi
Majibu:
Wahusika katika fasihi simulizi ni watu, wanyama, vitu na mahali. Wahusika hao kimsingi hujengwa na
fanani ili waweze kukidhi uwakilishaji wa sifa na tabia za binadamu katika fasihi.
Aina tano za wahusika wa fasihi simulizi ni:
Msimuliaji (fanani) – ndiye anayewasilisha na kutamba kazi husika ya fasihi simulizi.
Wasikilizaji (hadhira) – hawa hushirikiana na fanani katika uwasilishaji wa kazi ya
fasihi. Ushiriki wa hadhira husaidia kumpa fanani tathmini juu ya uwasilishaji wake.
Wanyama – hupewa sifa za kutenda kama binadamu. Huwakilisha tabia na sifa za watu
katika jamii.
Simba – huwakilisha watu wababe
Fisi – huwakilisha watu waoga/walafi/wenye tamaa
Nyoka – huwakilisha watu wenye tabia ya unafiki/uchonganishi/uongo
Pono (ndege/samaki)- huwakilisha watu wenye usingizi mwingi
Mkizi – huwakilisha watu wenye hasira za hovyo
Sungura – huwakilisha watu wenye kutumia akili nyingi sana
Kobe – huwakilisha watu wenye hekima na busara
Binadamu – wahusika wa aina hii huwa na sifa za kibinadamu kufuatana na hulka zao,
sifa na matendo yao. Mfano mzee mmoja, malkia wan chi, n.k
Vitu na mahali – hadithi inapohusisha sehemu kama vile vichakani, kaburini, bwawani,
porini au msituni, vitu hivyo na sehemu hizo hutumika kama aina fulani ya wahusik.
8. Elezea maana na kazi ya methali katika jamii.
Au: Methali kama utanzu wa fasihi simulizi una dhima gani kwa jamii?
Majibu:
Methali ni semi zenye hekima na busara zitumiwazo kuonya, kuadilisha na kuadimu jamii. Ni semi
ambazo hutolewa ili kufikisha ukweli fulani katika maisha.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 6
Kazi/dhima za methali:
Kuelimisha jamii – mfano: asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
Kuburudisha jamii – methali huburudisha, hufurahisha na kuliwaza jamii
Methali huhimiza ushujaa – mfano: kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake
Methali huadibu – mfano: kiburi si maungwana
Methali huhimiza ushirikiano – mfano: umoja ni nguvu, utengani ni udhaifu
Methali hukuza lugha – matumizi ya lugha kisanii katika methali huchangia kukuza lugha
9. Eleza maana na kazi ya vitendawili katika jamii
Majibu:
Vitendawili ni semi zenye kuchochea fikra na udadisi wa mambo. Ni mafumbo yenye kufikirisha
kulingana na mazingira halisi ya jamii husika.
Kazi za vitendawili ni:
Hutumika kuelimisha jamii
Huchochea utafiti kwa watoto, husaidia watoto kuwa wachunguzi wa mambo mbalimbali
Hutumika kukuza lugha, watoto hupata ujuzi wa kujieleza kwa lugha fasaha kwa kutumia
vitendawili
Hutumika kuonya na kukosoa jamii
Hutumika kufurahisha na kuburudisha jamii
Huchochea udadisi wa mambo na uwezo wa kufikiri haraka
Wakati mwingine vitendawili vina dhima ya kukejeli mfano: Wazungu wawili wanachungulia
dirisha = kamasi
10. Fafanua maana na sifa za hadithi za fasihi simulizi
Majibu:
Hadithi ni masimulizi yenye mtiririko wa matukio (visa) na wakati. Matukio hayo yaweza kuwa ya
kubuni au ya kweli kulingana na harakati mbalimbali za maisha ya binadamu. Hadithi za fasihi simulizi
ni kama vile ngano, tarihi, visasili na soga.
Hadithi za fasihi simulizi huwa na sifa zifuatazo:
Fanani na hadhira ni hai – yaani si wa kubuni na hukutana uso kwa uso wakati wa masimulizi
Huwa na mahali maalumu pa kutendea
Huelezea tukio maalumu
Huwa na mianzo maalumu mfano:
Hadithi hadithi………hadithi njoo
Paukwa……………..Pakawa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 7
Atokeani……………twaibu
Lengo la mianzo hiyo ni:
Kuonesha mwanzo wa hadithi
Kuitayarisha hadhira ili ifuatilie hadithi
Kumhakiki msikilizaji
Sifa nyingine ni kuwa msimuliaji wa hadithi wakati wa kusimulia hutumia sauti
kuwabainisha wahusika wote waliomo na pia hutumia vitendo au kushangaa ili mradi kufikia
lengo lake.
Sifa ingine ni kuwa msimuliaji anaweza kutumia mhusika hai au mfu, wa kidhanifu au
kiyakinifu ili mradi amechorwa vema na kufikisha ujumbe kwa jamii husika.
Hadithi za fasihi simulizi zina kazi (dhima) zifuatazo katika maisha (Taz. Swali la 10 hapa
chini):
11. Je, hadithi za fasihi simulizi zina dhima gani katika maisha?
Majibu:
Hadithi ni simulizi ya kweli au ya kubuni yenye mtiririko wa visa na wakati. Ni masimulizi ya mfululizo
wa nathari juu ya mambo yaliyotokea au juu ya mambo ya kubuni katika maisha ya jamii.
Hadithi za fasihi simulizi zina kazi (dhima) zifuatazo katika maisha:
Kujenga jamii na kuipa mielekeo mizuri ya maisha
Kuelimisha, kuadibu na kuonya jamii
Ni chombo cha kurithisha elimu na amali za jamii kutoka kizazi hadi kizazi
Husisitiza ushirikiano katika jamii – (ushirikiano huo ni katika shughuli mbalimbali za kijamii
mfano: kilimo, harusi, mzishi, n.k)
Huhifadhi kumbukumbu za watu katika jamii
Huhifadhi historia ya jamii husika mfano: ngano
12. Fafanua maana, aina na sifa za ushairi wa fasihi simulizi
Majibu:
Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa katika beti lugha ya mkato yenye kunata na kuvuta akili na mawazo
ya msikilizaji. Ushairi hujumuisha vipera kama vile mashairi, nyimbo, ngonjera, maghani, tenzi na
ngonjera.
Sifa za ushairi wa fasihi simulizi ni kama vile:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 8
Huwa na mpangilio maalumu wa maneno
Huwa na mapigo ya kimuziki
Huwa na uchaguzi na matumizi ya maneno
Huendana na mabadiliko/tukio maalumu katika jamii
Huwa na mwimbaji au waimbaji wanaoimba kwa sauti
Kuwepo kwa hadhira inayoimbiwa
Huelezea tukio maalumu katika jamii.
13. Ushairi (kama utanzu mmojawapo wa fasihi simulizi) una faida gani kwa jamii ya sasa?
Majibu:
Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa katika beti lugha ya mkato yenye kunata na kuvuta akili na mawazo
ya msikilizaji. Ushairi hujumuisha vipera kama vile mashairi, nyimbo, ngonjera, maghani, tenzi na
ngonjera.
Kazi/faida za ushairi katika jamii ni kama vile:
Hufundisha jamii mambo mbalimbali ya maisha – mfano nyimbo za jando na unyago
Huhimiza umuhimu wa kazi – mfano nyimbo za jando na unyago
Hufurahisha, huburudisha na kuliwaza jamii hasa baada ya kazi au wakati wa matatizo kama vile
misiba mfano nyimbo za msiba.
Huelimisha, huonya, huasa na kuadilisha jamii – mfano nyimbo za kanisani
Husifu mafanikio yanaypatikana kutokana na juhudi za wanajamii – mfano nyimbo za siasa
Hutunza historia ya jamii na utamaduni wa jamii – mfano nyimbo za jando na unyago
Hutatua migogoro katika jamii – mfano nyimbo za kanisani
Hukuza lugha ya jamii inayohusika.
14. Fafanua maana ya hadithi za ngano za fasihi simulizi ukizingatia sifa na wahusika wake.
Majibu:
Ngano ni hadithi za mwanzo kabisa. Ni hadithi za kimapokeo ambazo husimuliwa juu ya matukio katika
maisha ya binadamu (historia) pamoja na kuingiza mambo yanayosadikiwa na jamii fulani ya watu
(itikadi).
Hadithi za ngano zina sifa zifuatazo:
- Ni hadithi fupi fupi ili kuweza kukaririwa
- Hadithi za ngano huingia moja kwa moja katika kulitoa wazo kuu – mfano:- ridhika na kipato
chako, uzembe haufai, n.k
- Hadithi za ngano haziingilii mambo kwa undani sana
- Hadithi za ngano huwa na mwisho wenye matumaini na furaha. Mfano: Wakaishi raha
mustarehe.
- Hadithi za ngano zina sentensi fupi fupi ili kutoa nafasi kwa waitikiaji
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 9
- Hadithi za ngano huwa na mianzo mahususi
Mfano:
Paukwa - Pakawa
Hadithi, hadithi - Hadithi njoo, ubunifu njoo utamu kolea
Atokeani - Naam twaibu
Umuhimu wa mianzo ya kihadithi ni:
- Kumtayarisha msikilizaji
- Kumhakiki msikilizaji
- Kuonesha mwanzo wa hadithi
Wahusika wa hadithi za ngano huwa na sifa zifuatazo:
- Hawaumbwi sana – hawapambanuliwi kwa undani sana
- Huwa viwakilishi/vielelezo vya tabia na mienendo fulani
- Aghalabu wahusika hawa hawana majina halisi ila mtu mmoja, mfalme mmoja, Bi. Kizee
mmoja, n.k
- Mhusika mkuu hupewa jina maalumu au hapewi jina maalumu
- Wahusika wa hadithi za ngano huwa wachache sana ama hutajwa kwa makundi
- Wahusika wa hadithi za ngano hulazimika/hawalazimiki kuainishwa kama viumbe halisi;
wanaweza kuwa wanyama, wadudu, mashetani, n.k
15. Fasihi simulizi inajipambanua katika tanzu zipi?
Majibu:
Fasihi simulizi ni Sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia ya
masimulizi yam domo. Fasihi simulizi inaundwa na tanzu nne ambazo ni : Hadithi, Semi, Ushairi na
Sanaa za maonesho. Tanzu hizo na vipera vyake huweza kuoneshwa kwa kielelezo kifuatacho:
FASIHI SIMULIZI
Hadithi Semi Ushairi Sanaa za maonesho
Ngano Misemo Mashairi Maigizo
Tarihi Methali Nyimbo Matambiko
Visasili Vitendawili Ngonjera Utani
Vigano Mafumbo Maghani Michezo ya watoto
Soga Mizungu Tenzi Majigambo
Nahau Ngonjera
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 10
Lakabu Miviga
Ngoma
16. Eleza maana, kazi na matatizo yanayokwamisha maendeleo ya Sanaa za maonesho hapa nchini.
Majibu:
Sanaa za maonesho ni utanzu wowote wenye jumla ya mambo yafuatayo: dhana inayotendeka (tendo),
mtendaji (fanani), hadhira (wasikilizaji) na uwanja wa kutendea (mandhari).
Vijitanzu vya Sanaa za maonesho ni kama vile: majigambo, tambiko, miviga, michezo ya watoto, utani
na ngoma.
Kwa ujumla katika Sanaa za maonesho maneno huambatana na vitendo ili kukamilisha mawasiliano.
Lengo (kazi) kuu la Sanaa za maonesho ni: kujifurahisha au kuwafurahisha watazamaji, kujikumbusha
yaliyotokea zamani, kufufua utamaduni wa jamii, kuelezea/kuendeleza upendo katika jamii, kudumisha
ujasiri katika maisha.
Matatizo yanayokwamisha maendeleo ya Sanaa za maonesho hapa nchini ni:
Uhaba wa fedha za kuendeleza Sanaa hizo
Elimu duni kwa wananchi kuhusiana na Sanaa hizo na hivyo huzidharau
Kukosekana kwa uongozi imara na mipango thabiti
Ukosefu wa wataalamu wa kutosha
Uhaba wa kumbukumbu za awali zilizohusu Sanaa za maonesho
Kasumba ya baadhi ya watu kupenda Sanaa za nje zaidi na kudharau zile za ndani kwa kuziona
za kishamba
Changamoto ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo imebadili kabisa misingi ya Sanaa
za asili katika uwasilishaji na kibaya zaidi baadhi ya Sanaa haziwezi kuwekwa katika njia za
uhifazi kutokana na usiri wake mf. Matambiko.
17. Fafanua maana, aina, na hasara za utani katika jamii.
Majibu:
Utani ni maneno ya mzaha ambayo pengine huambatana na vitendo ambayo husaidia kukuza mahusiano
miongoni mwa wanajamii. Asili ya utani ilitokana na vita, koo kuoana, hama hama ya watu na biashara.
Aina za utani ni kati ya mtu na mtu, ukoo na ukoo, kabila na kabila – mfano:- Wahaya kwa Wakurya,
Wapare kwa Wachaga, au taifa na taifa n.k.
Faida za utani ni :
Kutoa maadili na mafunzo fulani
Kuimarisha umoja na mshikamano (udugu)
Kuhimiza ujasiri na juhudi katika maisha
Kuhimiza upendo katika maisha
Watu huambiana ukweli, hivyo hukosoana na kurekebishana
Hukuza mila na desturi
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 11
Hufariji, hustarehesha na kuburudisha
Hasara za utani ni:
Husababisha ugomvi katika jamii hasa utani unapozidi
Huleta hasara ya kuchukuliana vitu bila malipo, mfano mifugo
Huvunja au kuvunjiana heshima miongoni mwa wahusika
18. Eleza maana, aina, sehemu, faida na hasara za matambiko.
Majibu:
Matambiko ni ibada inayoambatana na sadaka itolewayo kwa miungu kupitia wahenga, mahoka au
mizimu. Sadaka itolewayo katika matambiko hujulikana pia kama kafara. Kafara huweza kuwa
mnyama, mazao kama nafaka au vinywaji kama maziwa au pombe ya asili kutegemeana na jamii husika.
Shabaha ya matambiko ni:
Kutoa shukrani juu ya jambo lililofanikiwa
Kuomba msaada fulani mfano mvua
Kuondoa balaa mfano ukame, mafuriko, njaa au vifo.
Kupatanisha wahusika na wahenga au miungu yao
Kuzuia matatizo fulani katika jamii
Kutambua au kukiri ukuu wa nguvu ya miungu au wahenga
Kukuza na kuendeleza mila na desturi za jamii husika
Aina za matambiko ni: aina za matambiko hutofautiana kati ya jamii moja na nyingine ingawa aina
zilizo kuu ni :
Matambiko ya wanyama – mifugo au mawindo
Matambiko ya vinywaji au vyakula maalumu
Matambiko ya mazao maalumu ya shambani
Matambiko ya ngoma/michezo maalumu
Matambiko ya watu maalumu
Sehemu za matambiko ni: sehemu za kufanyia matambiko ni kama vile: mapangoni, makaburini,
milimani au chini ya miti mikubwa.
Faida / umuhimu wa matambiko ni kama vile:
Kujenga Imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya jamii
Kuendeleza mila na desturi za jamii husika
Kujenga na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanajamii
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 12
Kuleta jamii pamoja na kuepusha mwingiliano usiokubalika
Kuhimiza uwajibikaji na kujituma katika uzalishaji mali
Kudumisha uadilifu ndani ya jamii
Huchochea uhifadhi wa mazingira kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matambiko
Hasara za matambiko ni:
Hujenga dhana potofu katika jamii – watu huamini nguvu fulani bila kuwa na uhakika
Huleta utengano miongoni mwa wanajamii – mfano waumini wa dini na wasiowaumini
(wapagani)
Husababisha matumizi makubwa ya mali bila sababu za msingi na kuleta uharibifu wa mali kama
mazao na vyakula
Ni chanzo kikubwa cha kushamiri kwa imani za kishirikina
Husababisha uhaba wa maeneo ya kufanyia shughuli kama za kilimo kutokana na maeneo
kutengwa kwa shughuli za matambiko
19. Fafanua maana ya miviga (sherehe) ukionesha faida na hasara zake kwa jamii.
Majibu:
Miviga ni sherehe zinazofanywa katika kipindi maalumu cha mwaka hasa baada ya mavuno. Mara
nyingi sherehe hizi huwa na lengo la kumtoa mtu kutoka kundi moja na kumuingiza kundi jingine, mfano
vijana kuingia utu uzima, harusi, kufuzu masomo, n.k
Umuhimu wa miviga/sherehe za jadi ni:
Hufundisha umuhimu wa kazi mfano ukulima, uwindaji, n.k
Huhimiza ujasiri katika maisha
Hufundisha masuala ya unyumba na malezi kwa ujumla
Husisitiza ushirikiano miongoni mwa wanajamii
Huleta ushindani, hivyo huchochea maendeleo
Hasara za miviga katika jamii
Ni ghali kuiendesha – huhitaji pesa na mali nyingi
Huleta mashindano na matokeo yake husababisha baadhi ya watu wasio na uwezo kujiingiza
katika wizi, utapeli, ujambazi, n.k
Sherehe hujenga ufahari ambao huwaacha wenye sherehe kwenye matatizo mbalimbali mfano
kulipa madeni
Sherehe huweza kusababisha ugomvi, chuki, tamaa, n.k
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 13
20. Majigambo kama utanzu wa Sanaa za maonesho una faida na hasara gani?
Majibu:
Majigambo ni vitendo vinavyoambatana na maneno ya kujisifu kwa ujasiri wa mtu binafsi au jamii
nzima. Katika majigambo fanani huweza kutamba kwa ushairi wa kimapokeo au wa kisasa. Mtambaji
hujiona ni bora kuliko watu wengine kwa kujiona, kujisifu na kujivuna.
Katika majigambo lazima pawepo mtendaji, hadhira, mandhari na hali ya utendaji. Utendaji huendana
na umri/rika mfano vijana kwa vijana au wazee kwa wazee.
Faida za majigambo
Hukuza ushujaa katika jamii kwa kukemea uoga, ulegevu na uzembe
Hukuza na kuendeleza mila na desturi za jamii
Huburudisha jamii maana fanani atambapo huonesha vichekesho vya kila aina
Huimarisha utendaji kazi katika jamii
Hukuza, huimarisha na kuchochea fani ya utambaji, lugha na kujieleza
Hujenga uaminifu katika jamii
Hasara za majigambo
Hukuza na kuendeleza ubinafsi kwani fanani huonekana ni bora kuliko watu wengine
Mkusanyiko wa hadhira hutumia fedha au vyakula kwa wingi hivyo husababisha hasara
Huleta chuki, uhasama, fitina katika jamii
Husababisha unafiki katika jamii
Fanani hutamba upande wa mafanikio tu wakati wote kitu ambacho si kweli katika maisha.
21. Ngoma ni aina ya mchezo unaochezwa kulingana na jamii inayohusika. Fafanua faida na hasara
za mchezo huu.
Majibu:
Ngoma huchezwa kutegemea jamii inayohusika. Hushirikisha watu wa rika moja mfano wazee, vijana
au watoto. Ngoma huchezwa katika eneo maalumu lililotengwa na jamii husika.
Faida za ngoma katika jamii ni:
Huhimiza ushujaa na ujasiri katika jamii
Hufurahisha, huburudisha na kuliwaza jamii
Hufafanua na kuendeleza mila na desturi za jamii
Hutunza historia ya jamii
Ngoma kwa kupitia maneno ya wimbo hutoa mafunzo fulani, hutoa taarifa fulani au sifa fulani
na kukosoa makossa ya watu
Hudumisha ari ya kufanya kazi kwa bidi
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 14
Hasara za ngoma katika jamii ni:
Ngoma huweza kugharimu pesa, vyakula na vinywaji na hivyo hutia hasara
Ngoma huchezwa katika mazingira yanayoweza kuchochea vitendo vya zinaa na kusababisha
kuenea kwa magonja hata UKIMWI
Ngoma huweza pia kusababishamigogoro katika familia mathalani mke anapokwenda kwenye
ngoma na kuchelewa kurudi nyumbani kumuandalia mumewe
Ngoma hufanya watu wasifanye kazi kwa muda wote wa uchezaji ngoma na hivyo kushusha
uzalishaji mali
Huchochea ushindani ndani ya jamii na pengine kuzalisha chuki na kusemana
22. Michezo ya watoto ina faida na hasara katika jamii. Eleza.
Majibu:
Michezo ya watoto ni maigizo yanayofanywa na watoto kutokana nay ale wanayoyaona katika jamii
wanamoishi. Watoto huiga tabia na matendo ya wazazi wao. Washiriki wa michezo hii ni watoto
wenyewe. Sehemu ya mchezo ni mahali popote pale kulingana na aina ya michezo.
Faida za michezo ya watoto:
Kuwajenga watoto kimawazo, busara, utii na hekima
Kuimarisha viungo vya watoto kiafya
Husaidia watoto kusadifu mazingira wanamoishi
Watoto huanza kujifunza umuhimu wa kazi na ujasiri kupitia michezo hii
Watoto hujifunza mbinu mbalimbali za kupambana na maadui
Watoto hujifunza utamaduni wa jamii yao
Watoto hujifurahisha kupitia michezo hii
Watoto hujijengea uhusiano mzuri miongoni mwao.
Husaidia kuibua, kuchochea na kuendeleza vipaji vya watoto
Hasara za michezo ya watoto:
Watoto huweza kuharibika kitabia iwapo watachangamana na watoto wenye tabia chafu
Watoto huweza kuumizana iwapo watacheza michezo ya hatari bila uangalizi
Huweza kuleta mifarakano baina ya wazazi kutokana na michezo mibaya
Michezo ya watoto huweza kuathiri maendeleo ya kitaaluma iwapo mtoto atavutwa kwenye
michezo na kukosa usimamizi katika masomo yake
Huweza kuleta hasara ya uharibifu wa mali mfano mchezo wa kupika huweza kusababisha
majanga ya moto
Michezo hii pia hushawishi tabia ya udokozi kutokana na watoto kulazimishana kuleta vitu vya
kuchezea
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 15
23. Fafanua matatizo yanayoipata fasihi simulizi ikihifadhiwa katika maandishi, kichwa na kwenye
vinasa sauti.
Majibu:
Uhifadhi wa fasihi simulizi katika maandishi, kichwa na vinasa sauti husababisha matatizo kama
yafuatayo:
Uhifadhi wa maandishi:
Hukuna utendaji wa viungo vya mwili
Huwezi kusikia sauti ya fanani
Hakuna ushiriki wa hadhira
Uhalisia wake hupungua
Ni gharama
Huwa mali ya mwandishi
Haibadili kwa urahisi
Uhifadhi wa kichwa:
Ni rahisi kusahau
Huweza kuongeza au kupunguza mambo muhimu
Huweza kupotea au kusahaulika kutokana na hali ya aliyehifadhi
Huifanya ishindwe kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
Uhifadhi wa vinasa sauti:
Hakuna ushiriki wa hadhira
Hupoteza utendaji
Hukosa uhalisia
Ni gharama
Haibadiliki
Huwa mali ya mtunzi
Hubagua wasio na uwezo kiuchumi
24. Ni kwa sababu gani vitendo vya wahusika katika fasihi simulizi ni vya muhimu sana?
Majibu:
Vitendo vya wahusika katika fasihi simulizi huimarisha hali ya utendaji katika fasihi simulizi. Fasihi hii
hutegemea utendaji ili kukamilisha mawasiliano. Hivyo vitendo vya wahusika katika fasihi simulizi ni
vya muhimu sana kwa sababu:
(a) Huamsha msisimko wa kutamba na kusikiliza
(b) Huleta ushiriki kati ya fanani na hadhira
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 16
(c) Huvuta umakini wa fanani na hadhira
(d) Huvuta usikivu wa hadhira
(e) Husaidia kueleweka kwa ujumbe kwa urahisi
(f) Husaidia kumpa fanani tathmini ya uwasilishaji wake
(g) Humpa fanani kujiamini na kuchochea ubunifu wake wa kisanii
25. Eleza maana ya maudhui katika kazi ya fasihi.
Majibu:
Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mambo ambayo mtunzi wa kazi ya fasihi anakusudia
kuyaeleza kwa hadhira yake. Maudhui hujengwa na vipengele kama vile: dhamira, ujumbe, migogoro,
falsafa, msimamo na mtazamo. Kwa ujumla maudhui ni sawa na chakula kilichomo ndani ya chungu na
chungu ndiyo fani yenyewe.
26. Fafanua vipengele vinavyounda fani katika kazi ya fasihi.
Majibu:
Fani katika kazi ya fasihi ni mbinu za kisanaa anazozitumia mtunzi ili kufikisha ujumbe wake kwa
hadhira aliyoikusudia. Vipengele vya fani ni kama vile: muundo, mtindo, wahusika, mandhari, matumizi
ya lugha.
27. Eleza maana ya (a) Ngano (b) Tarihi (c) Visasili (d) Vigano (e) Soga
Majibu:
Ngano – ni hadithi za kimapokeo zenye kusimulia matukio yenye kushabihiana na maisha halisi
ya mwanadamu. Ngano huanza kwa maneno ya kuvutia wasikilizaji kama
Paukwa……Pakawa……ngano hutumia wahusika wanyama, binadamu, vitu na mahali.
Tarihi – ni hadithi fupi zinazohusu matukio ya kihistoria yaliyowahi kutokea katika jamii fulani.
Tarihi husimuliwa ili kuikumbusha jamii ilipotoka, ilipo na ifanye nini kupiga hatua zaidi. Tarihi
huweza kuwa na mwisho wa furaha au huzuni.
Visasili – ni hadithi fupi zinazoeleza jinsi maumbile au tabia fulani zilivyoanza katika maisha ya
jamii fulani. Hutumiwa sana kutoa majibu ya maswali ya kisayansi au kiasili ambayo kimsingi
upeo wa maarifa yake hauwezi kufafanuliwa kwa wototo wadogo wakaelewa. Mfano: asili ya
jogoo kuwika, asili ya kiboko kuishi majini, n.k
Vigano – ni hadithi fupi za kimaadili ambazo husimuliwa kwa lengo la kukemea tabia na
mienendo isiyokubalika katika jamii kama vile ulafi, uchoyo, udokozi na tamaa. Wahusika hasa
huwa ni wanyama ambao hubebeshwa sifa na tabia za binadamu. Mfano: kigano cha mtoto
mchoyo aliyeficha kitumbua katika sanduku la nguo na kukisahau. Siku alipokumbuka kitumbua
chake akakuta panya wamekila na kisha kutafuna na nguo zake mpya za sikukuu. Vigano huishia
na methali inayotumiwa kuacha funzo.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 17
Soga – ni hadithi fupi za kuchekesha na kupoteza muda. Soga hutumia wahusika binadamu na
hasa watu wa kubuni. Wahusika hawa husadifu hali halisi ya mazingira fulani. Kupitia soga watu
hukosoana, hutupiana kejeli na dhihaka kwa njia ya utani kwa lengo la kurekebishana tabia.
28. Taja aina za nyimbo unazozifahamu hapa Tanzania.
Majibu:
Nyimbo ni tungo zenye mahadhi ya sauti inayopanda na kushuka. Huundwa kwa lugha ya mkato,
matumizi ya lugha ya picha na mapigo ya kisilabi. Aina za nyimbo zinazofahamika hapa Tanzania ni
kama vile:
Nyimbo za siasa
Nyimbo za ngoma (jando na unyago)
Nyimbo za watoto
Nyimbo za vita
Nyimbo za kazi
Nyimbo za kidini
Nyimbo za misiba
Nyimbo za tumbuizo
Nyimbo za kuaga mwaka
Nyimbo za mawaidha
Nyimbo za uvuvi.
29. Taja matatizo yanayojitokeza katika ukusanyaji wa kazi za fasihi simulizi.
Majibu:
Ukusanyaji wa fasihi simulizi ni hali ya kukusanya tanzu mbalimbali za fasihi hii. Tanzu hizo ni kama
vile: semi, Sanaa za maonesho, hadithi na ushairi. Matatizo yanayojitokeza katika kipengele hiki cha
ukusanyaji ni pamoja na:
Vyombo duni vya ukusanyaji
Changamoto za usafiri
Tatizo la tafsiri kwa kazi zilizo katika lugha za asili
Uhaba wa wataalamu
Kasumba ya kutothamini kazi za fasihi za asili kwa kuona zimepitwa na wakati
Ukosefu wa fedha
Mila na desturi kutoruhusu baadhi ya tanzu kukusanywa na kuhifadhiwa katika njia nyingine.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 18
30. (a) Taja sehemu tano za kitendawili
Majibu:
Muundo wa kitendawili hugawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:
(i) Kiingizi – mfano: Kitendawili –tega
(ii) Kitendawili chenyewe
(iii) Swali la msaada – mfano: Ni nini hicho?
(iv) Kichocheo – mfano: Naomba jibu
(v) Jibu lenyewe.
(b) Tegua vitendawili vifuatavyo:
(i) Chiriku alimwambia mwanawe, “Nikiinama nikiinuka ni mauti yetu”
(ii) Chukua ungo, wewe na mimi tupepete kisichopepeteka
(iii) Kuku wangu hutagia miibani
(iv) Mwenye kuitwa amefika lakini mjumbe bado hajarudi
(v) Babaangu amenipa visu viwili: kimoja nakitumia lakini cha pili siwezi kukitumia
(vi) Pana ng’ombe miongoni mwa kundi la ndama
(vii) Chini chakula, kati kuni, juu mboga
(viii) Hulala tulalapo, huamka tuamkapo
(ix) Nilianika unga wangu, asubuhi sikuukuta
(x) Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana miguu
Majibu:
(i) Mtego (ii) Maji (iii) Nanasi (iv) Nazi na mkwezi (v) Ardhi na anga (vi) Mwezi na nyota (vii)
Muhogo (viii) Jua (ix) Umande au nyota za angani (x) Kuku na yai
31. Eleza maana ya misemo ifuatayo.
(i) Akina baba kabwela
(ii) Jikaza kisabuni
(iii) Alikaa eda
(iv) Elimu ni bahari
(v) Toka nitoke
(vi) Mtu mwenye utu
(vii) Usingizi umepaa
(viii) Kula chumvi nyingi
(ix) Hawapikiki chungu kimoja
(x) Kuzunguka mbuyu
(xi) Kuvaa miwani
(xii) Piga vijembe
(xiii) Jipalia mkaa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 19
(xiv) Kazi ya kijungu jiko
(xv) Ndege mbaya
Majibu:
(i) Akina baba kabwela = Watu wenye kipato kidogo (wanyonge)
(ii) Jikaza kisabuni = Jitahidi hadi mwisho
(iii) Alikaa eda = Alitimiza muda wa kumlilia mumewe
(iv) Elimu ni bahari = Elimu haina mwisho
(v) Toka nitoke = Fuatana katika uzazi
(vi) Mtu mwenye utu = Muungwana
(vii) Usingizi umepaa = Usingizi umehama
(viii) Kula chumvi nyingi = Kuishi miaka mingi
(ix) Hawapikiki chungu kimoja = Hawaelewani/Hawapatani
(x) Kuzunguka mbuyu = Kula rushwa
(xi) Kuvaa miwani = Kulewa pombe
(xii) Piga vijembe = Sema mtu kwa mafumbo
(xiii) Jipalia mkaa = Jiingiza katika matatizo
(xiv) Kazi ya kijungu jiko = Kazi ya kumpatia mtu posho tu
(xv) Ndege mbaya = Bahati mbaya (mkosi)
32. Kwa kila methali hapa chini, andika methali yenye kufanana nayo.
Mfano: Akili nyingi huondoa maarifa >>> Werevu mwingi mbele kiza/giza
(i) Baada ya kisa mkasa
(ii) Baada ya dhiki faraja
(iii) Bandubandu humaliza gogo
(iv) Bendera hufuata upepo
(v) Dalili ya mvua mwaingu
(vi) Dawa ya moto ni moto
(vii) Jembe halimtupi mkulima
(viii) Kamba hukatikia pabovu/pembamba
(ix) Mbio za panya sakafuni huishia ukingoni
(x) Mgema akisifia tembo hulitia maji
(xi) Mpanda ngazi hushuka
(xii) Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
(xiii) Ngozi ivute i maji
(xiv) Ukuukuu wa Kamba si upya wa ukambaa
(xv) Penye nia pana njia
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 20
Majibu:
(i) Baada ya chanzo kitendo
(ii) Mtaka cha uvunguni sharti ainame Au: Mvumilivu hula mbivu Au: Mchumia juani hulia kivulini
(iii) Haba nah aba hujaza kibaba
(iv) Maji hufuata mkondo AU: Wengi wape
(v) Mwanzo wa ngoma ni lele
(vi) Sumu ya neno ni neno
(vii) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
(viii) Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu
(ix) Njia ya mwongo ni fupi Au: Siku za mwizi ni arobaini
(x) Ngoma ikilia sana hupasuka
(xi) Aliyejuu mngoje chini Au: Cheo ni dhamana
(xii) Fadhili ya punda mateke
(xiii) Samaki mkunje angali mbichi Au: Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
(xiv) Usidhani yote yang’aayo ni dhahabu
(xv) Abadi abadi Kamba hukata jiwe.
33. Kwa kila methali kati ya zifuatazo andika maana, busara (faida) na hasara yake kwa jamii.
(a) La kuvunda halika ubani
Maana: kitu kikiharibika kimeharibika, hakiwezi kurekebishwa.
Busara: hatuna budi kutupilia mbali vitu vilivyoharibika
Hasara: kuna vitu ambavyo vikiharibika huweza kurekebishwa na vikarudia hali yake ya
kawaida
(b) Yote yang’aayo usidhani dhahabu
Maana: si kila kitu katika dunia hii kina maana/thamani
Busara: inatulazimu tuwe makini katika uchaguzi au uteuzi wa vitu vionekanavyo machoni petu.
Hasara: tunaweza kuacha vitu vyenye manufaa katika maisha kwa kuzingatia kuwa si kila
king’aacho ni dhahabu.
(c) Kikulacho ki nguoni mwako
Maana: anayekufanyia unyama au uadui ni mtu uliyenaye karibu.
Busara: ni lazima tuwe macho na marafiki zetu wa karibu
Hasara: unaweza kupoteza uhusiano mzuri kwa marafiki au ndugu zako au jirani kwa ajili ya
kudhania tu.
(d) Mvumilivu hula mbivu
Maana: mtu anayevumilia mwisho wake hufanikiwa
Busara: tuwe na subira katika mipango yetu ili hatimaye tupate mafanikio hapo baadaye
Hasara: tunaweza kuvumilia lakini mwishowe tusifanikiwe.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 21
(e) Haraka haraka haina barak:
Maana: kufanya kitu kwa utaratibu au mipangilio mizuri huleta mafanikio mbeleni.
Busara: tusiwe na pupa na papara katika mambo tuyatendayo
Hasara: methali hii inaweza kuleta hasara kwa jamii kwani kuna mambo yanatakiwa kufanywa
haraka kama vile kumkimbiza mgonjwa hospitalini
34. Eleza maana ya:
(a) Fanani
(b) Hadhira
(c) Sanaa
(d) Lugha ya picha
(e) Wahusika katika fasihi
Majibu:
(a) Fanani katika kazi ya fasihi simulizi ni yule anayewasilisha kazi ya fasihi simulizi kwa hadhira yake.
Fanani ndiye anasimulia, kuimba na kutamba kazi ya fasihi simulizi.
(b) Hadhira ni wale wapokeaji, watazamaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi simulizi inayowasilishwa
na fanani.
(c) Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa. Kuna aina nyingi za Sanaa
(d) Lugha ya picha ni taswira inayotumiwa na fanani/mwandishi kuwakilisha dhana maalumu. Ni lugha
inayomfanya msikilizaji/msomaji atafakari zaidi na ndipo anagundua taswira hiyo inawakilisha nini.
(e) Wahusika katika kazi ya fasihi simulizi/fasihi andishi ni watu, wanyama, vitu au mahali. Wahusika
hao hujengwa na fanani ili waweze kukidhi na kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii.
35. Eleza maana ya semi na taja vipera vinavyounda semi.
Majibu:
Semi ni tungo fupi zinazoundwa kwa lugha ya picha, ishara na tamathali. Semi huwa inabeba busara,
hekima na ushauri mahususi kwa jamii. Semi za fasihi simulizi zina vipera kama vile: misemo,
mafumbo, vitendawili, mizungu, lakabu, methali, nahau.
36. Taja mambo matano yanayoifanya fasihi iwe Sanaa.
Majibu:
Fasihi ni Sanaa kwa sababu ya mambo yafuatayo:
Ufundi wa kutumia lugha kueleza jambo (matumizi ya lugha)
Mpangilio maalumu wa matukio (muundo)
Namna nzuri ya uwasilishaji (mtindo)
Uumbaji wa wahusika (wahusika)
Kuwepo kwa mandhari (sehemu ya matukio)
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 22
37. Eleza tofauti baina ya kazi ya fasihi na isiyo ya fasihi.
Majibu:
Fasihi ni kielelezo cha kisanaa kitumiacho maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Vipengele vinavyotofautisha kazi ya fasihi na ile isiyo ya kifasihi ni kama vile:
(a) Lugha – fasihi hutumia lugha kiufundi lakini kazi zingine zisizo fasihi hazitumii lugha kiufundi
(b) Wahusika – fasihi hutumia wahusika kubeba ujumbe tofauti na kazi zisizo za kifasihi
(c) Mandhari – kazi za kifasihi hasa simulizi huwa na uwanja maalumu wa kutendekea k.v. mapangoni,
milimani, kwenye miti mikubwa tofauti na matukio yasiyo ya kifasihi
(d) Fani na maudhui – kazi ya fasihi lazima iwe na umbo la nje (fani) na umbo la ndani (maudhui) kitu
ambacho huwezi kukikuta katika kazi isiyo ya kifasihi
(e) Muundo – kazi ya kifasihi huwa na msuko maalumu unahusu mpangilio wa visa na matukio tofauti
na kazi isiyo ya kifasihi
(f) Mtindo – huu ni upekee wa uwasilishaji wa kazi ya kifasihi ambao huweza kuwa masimulizi,
majibizano au kinudhumu lakini huwezi kukuta mtindo kama huu katika kazi isiyo ya kifasihi.
38. Kwa kutumia mifano, taja sifa nne za fasihi.
Majibu:
Fasihi ni kazi ya Sanaa inayotumia lugha ili kufikisha ujumbe wake kwa jamii iliyokusudiwa.
Zifuatazo ni sifa nne za fasihi:
(i) Fasihi ni Sanaa, maana yake ni matokeo ya kiufundi. Kitu chochote kilichotengenezwa kwa
ufundi hupendeza, huvutia na huamsha hisia ndani ya mhusika
(ii) Fasihi ni Sanaa itumiayo lugha. Fasihi ni ufundi wa kutumia lugha ili kuleta mchomo au hisia
fulani. Katika fasihi kuna aina mbalimbali ya matumizi ya lugha: kuna misemo, nahau, tamathali
za semi, na matumizi ya lugha ya picha.
(iii) Fasihi ni kielelezo, haina budi ieleze hali halisi ya maisha ya jamii inayohusika. Kueleza huku
hutumia na huzingatia ufundi wa kutumia lugha. Vilevile hubeba ujumbe maalumu ambao
unapelekwa kwa jamii inayohusika. Jamii hii huwakilishwa na watazamaji, wasomaji na
wasikilizaji. Hawa kifasihi huitwa hadhira.
(iv) Fasihi ni maelezo yenye fani na maudhui. Fani inaundwa na vipengele kama: muundo, mtindo,
wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Maudhui huundwa na: dhamira, ujumbe, migogoro,
falsafa, msimamo na mtazamo.
39. Taja mambo matano muhimu yanayotambulisha wimbo.
Majibu:
Wimbo ni kile kinachoimbwa. Hivyo hii ni dhana inayojumuisha tanzu nyingi. Hata baadhi ya tanzu za
kinathari kama vile hadithi huweza kuingia katika kundi la nyimbo pindi zinapoimbwa.
Mambo muhimu matano yanayotambulisha wimbo ni:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 23
(a) Muziki wa sauti ya mwimbaji au waimbaji
(b) Muziki wa ala (kama upo)
(c) Matini au maneno yanayoimbwa
(d) Hadhira inayoimbiwa
(e) Muktadha unaofungamana na wimbo husika mfano: msiba, sherehe, ibada, n.k
40. Eleza kazi ya makofi katika nyimbo za fasihi simulizi.
Majibu:
Kazi ya makofi katika nyimbo za fasihi simulizi ni kukata shauri juu ya mwendo wa wimbo (polepole
au haraka haraka). Katika makabila mengi, makofi huchukua nafasi kubwa katika nyimbo ambazo watu
huimba wamekaa au wamesimama bila kucheza.
Vilevile hutumika sana kumpa hamasa mchezaji aliyekatikakati na kadiri makofi yanavyoongezeka
ndivyo mchezaji anavyozidisha madoido na mbwembwe.
Makofi pia hutumiwa sana na wanawake katika nyimbo za harusi kutoa alama ya mwendo wa kasi na
hamasa ya waimbaji, wachezaji na namna ya kuishirikisha hadhira.
Vilevile makofi husaidia kuondoa usingizi na kumpa mwimbaji nafasi ya kupumzika na kumeza mate.
41. Andika maana ya tanzu zifuatazo za fasihi andishi.
(a) Riwaya (b) Ushairi (c) Tamthiliya
Majibu:
(i) Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana, lugha ya kinathari, mchanganyiko
wa visa na dhamira, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa kimantiki yenye kufungamana
na wakati ikishabihiana na maisha halisi.
(ii) Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye
mvuto, kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara, katika usemi, maandishi au ,ahadhi ya
wimbo ili kueleza wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au
mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.
(iii) Tamthiliya ni utungo wa kidrama ambao ni aina moja ya maandishi ya Sanaa za maonesho. Ni
Sanaa inayooneshwa kwa vitendo vya wahusika waliotumiwa na msanii na kuvitafakari kwa
makini.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 24
SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
42. Taja aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili. Kwa kila aina tunga sentensi moja na
pigia mstari aina ya neno ulilotumia katika sentensi.
Majibu:
Aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili ni:
(a) Jina/Nomino – (J/N): sentensi: Baba yangu ni mkulima hodari.
(b) Kivumishi – (V): sentensi: Baba yangu amesafiri.
(c) Kiwakilishi – (W): sentensi: Yule amefaulu.
(d) Kiunganishi – (U): sentensi: Baba na mama wanalima.
(e) Kihusishi – (KH): sentensi: John amepigwa kwa fimbo kubwa.
(f) Kitenzi – (T): sentensi: baba analima shambani.
(g) Kielezi – (E): sentensi: Nguo zimo kabatini.
(h) Kihisishi/Kiingizi – (H/I): sentensi: Lo! Baba amefariki.
43. (a) Eleza maana ya tungo.
(b) Taja aina nne za tungo katika lugha ya Kiswahili.
Majibu:
Tungo ni matokeo ya kuweka pamoja vipashio vidogo zaidi na sahili ili kuunda kipashio
kikubwa zaidi ya vyenyewe. Kwa mfano mofu hushikamanishwa pamoja na kuunda
tungo neno.
Kuna aina nne za tungo katika lugha ya Kiswahili ambazo ni:
(a) Tungo neno – ni tungo inayoundwa kwa kushikamanisha pamoja mofu/mofimu
(b) Tungo kirai/kikundi – ni tungo inayoundwa na neno moja au zaidi
(c) Tungo kishazi – ni tungo inayotawaliwa na kitenzi kinachotoa taarifa kamili au isiyokamili
kutokana na kushushwa hadhi kwa kupachikwa kiambishi rejeshi.
(d) Tungo sentensi – ni tungo yenye muundo wa kiima na kiarifu na inayotoa taarifa iliyokamili.
44. (a) Mofimu ni nini?
(b) Kuna aina ngapi za mofimu?
Majibu:
Mofimu ni neno au sehemu ya neno isiyogawanyika zaidi na yenye maana ya kisarufi au
kileksika.
Kuna aina mbili za mofimu ambazo ni:
(a) Mofimu huru: ni maumbo ya maneno yasiyogawanyika zaidi na yanayojitosheleza kimuundo na
kimaana. Mfano: baba, mama, maji, hewa.
(b) Mofimu tegemezi: hivi ni viambishi ambavyo hujiegemeza kwenye mzizi wa neno na kukamilisha
muundo na maana ya neno. Mfano:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 25
Analima = A-na-lim-a
Mofimu tegemezi hapo ni: A, na, a
45. Lugha yoyote ina vipashio vitano. Vitaje kwa mifano.
Majibu:
Vipashio ni vipande vitumikavyo kuunda lugha katika darajia mbalimbali kuanzia na darajia ndogo
kabisa ambayo ni mofu/mofimu hadi sentensi.
Vipashio hivyo vya lugha ni:
(a) Mofimu/mofu – ni kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu wa kisarufi au kileksika. Mfano:
baba, maji, hewa,
a-na-som-a, tu-me-lim-iw-a
(b) Neno – ni kipashio kinachoundwa kwa mofimu moja au zaidi. Neno linaloundwa kwa mofimu moja
huwa ni neno huru na lile linaloundwa kwa mofimu zaidi ya moja huwa ni neno changamano lenye
mzizi na viambishi. Mfano: paka, mtoto, chama, kikosi.
(c) Kirai/kikundi – ni kipashio kinachoundwa kwa neno moja au zaidi. Kirai huundwa kwa neno kuu na
kijalizo kimoja au zaidi. Mfano: mtoto, kijana mvivu, anasoma, amelima shamba.
(d) Kishazi – ni kipashio kinachotawaliwa na kitenzi kichojitosheleza au kisichojitosheleza, kishazi huru
huwa kina hadhi ya sentensi sahili na kishazi tegemezi hupewa hadhi ya kirai. Mfano:
Baba aliyekuja amesafiri leo asubuhi.
Baba aliyekuja……. (kitenzi hakijitoshelezi)
Baba amesafiri …… (kitenzi kinajitosheleza)
(e) Sentensi – ni tungo yenye muundo wa kiima na kiarifu na inayotoa taarifa iliyokamili.
Mfano: Baba yangu / amesafiri leo
K A
Baba na mama / wanalima shamba
K A
46. (a) Viwakilishi ni nini?
(b) Taja aina za viwakilishi unavyovifahamu.
Majibu:
(i) Viwakilishi (W) ni maneno yanayosimama badala ya nomino pindi nomino inapokosekana
kwenye nafasi yake katika tungo. Mfano: Wewe unaishi wapi?
(ii) Kuna aina tisa za viwakilishi kama ifuatavyo:
- Kiwakilishi kimilikishi – mfano: kwetu ni mbali
- Kiwakilishi cha idadi – mfano: Watano wamefika
- Kiwakilishi cha sifa – mfano: Wafupi waje mbele
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 26
- Kiwakilishi cha a-unganifu – mfano: ya moto imeisha
- Kiwakilishi kioneshi – mfano: Huyu ni mweusi
- Kiwakilishi kiulizi – mfano: Yupi ni mrembo?
- Kiwakilishi nafsi – mfano: Mimi nitalima
- Kiwakilishi cha amba – mfano: ambaye hakuniona apite mbele
- Kiwakilishi cha pekee – mfano: yeyote ajitolee kuandika
47. Fafanua dhima ya mofimu katika lugha.
Majibu:
Mofimu ni kipashio kidogo cha lugha ambacho huwakilisha maana maalumu kisarufi au kileksika.
Mofimu tegemezi ndizo hasa hubeba maana ya kisarufi na hivyo huwa na dhima mbalimbali kama
ifuatavyo:
(i) Kudokeza nafsi – mfano: a- katika anacheza (nafsi ya tatu umoja)
(ii) Kudokeza njeo/wakati – mfano: na- katika analima (njeo iliyopo)
(iii)Kudokeza idadi – mfano: ki- katika viatu (wingi)
(iv) Kudokeza urejeshi – mfano: ye- katika aliyetuita
(v) Kudokeza ukanushi – mfano: ha- katika hakufika
(vi) Kudokeza kauli ya utendeshi – mfano: ish-katika anaimbisha
*Kimsingi mofimu zina dhima nyingi sana katika lugha hizo ni kwa uchache tu.
48. (a) Eleza maana ya sentensi.
(b) sentensi inaundwa na sehemu kuu ngapi?
(c) Kuna aina ngapi za sentensi? Zitaje.
(d) Taja aina ya sentensi zifuatazo.
a. Baba yangu ni mkulima hodari.
b. Kijana aliyekuja jana ameondoka.
c. John angefika leo tungeondoka.
d. Baba na mama wanalima shambani.
e. Ng’ombe aliyezaa amekufa na ndama aliyezaliwa amepotea
Majibu:
i. Sentensi ni kifungu cha maneno, kuanzia neno moja na kuendelea chenye kiima na kiarifu na
kinachotoa maana kamili.
ii. Sentensi inaundwa na sehemu kuu mbili ambazo ni: Kiima (K) na Kiarifu (A)
Mfano: Baba / analima shamba
K A
iii. Kuna aina nne za sentensi ambazo ni:
Sentensi sahihi/huru
Sentensi changamano
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 27
Sentensi ambatano
Sentensi shurutia
iv. Sentensi zilizotajwa kwenye (47d) ni :
Sentensi sahili
Sentensi changamano
Sentensi shurutia
Sentensi sahili
Sentensi ambatano
49. (a) Eleza maana ya nomino.
(b) Taja na fafanua aina za nomino.
Majibu:
(i) Nomino (N) ni neno linalotaja vitu, viumbe, hali, matendo au mahali ili kuviainisha na
kuvitofautisha vitajwa miongoni mwa vingine.
(ii) Kuna aina zifuatazo za nomino:
Nomino za kawaida – ni majina ambayo si maalumu kwa vitajwa. Majina haya yatokeapo katika
maandishi huanza kwa herufi za kawaida isipokuwa mwanzoni mwa sentensi huanza kwa herufi
kubwa. Mfano:
Baba analima shamba
Mimi na baba tutaondoka kesho
Nomino za pekee – ni majina maalumu kwa vitajwa. Nomino hizi huanza kwa herufi kubwa
popote katika maandishi. Mfano:
Juma amenunua gari
Mimi na Juma tumenunua gari
Nomino dhahania – ni majina ya viumbe au hali zisizoonekana wala kushikika. Mfano:
Majina ya hali kama vile: afya, kiu, njaa, hasira
Majina ya tabia kama vile: upole, ukatili, ujasiri
Majina ya viumbe kama vile: malaika, zimwi, shetani, Mungu
Majina ya jamii – ni majina yanayotaja watu au vitu katika makundi. Mfano: jeshi, bunge, chama,
kikosi.
Majina ya wingi – haya hutaja vitu katika wingi ingawa vinavyotajwa havina umoja wala wingi.
Mfano: maziwa, maji, mafuta, mawasiliano, mazungumzo.
50. (a) Nini maana ya sentensi tata?
(b) Sentensi zifuatazo ni tata. Toa maana mbili au zaidi ili kuthibitisha utata wake.
(i) Wizi wa silaha umeongezeka
(ii) Majaliwa ameijia fedha yake
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 28
(iii)Mwalimu wa Kiingereza ni mkali
(iv) Mwanangu amelalia uji
(v) Mama yangu anaota
Majibu:
(a) Sentensi tata ni ile inayowezesha wasikilizaji au wasomaji wake kuibua maana zaidi ya moja.
(b) Majibu ya (49c i-v) hapo juu ni kama ifuatavyo:
(i) Wizi wa silaha umeongezeka
Maana: 1. Wizi wa kutumia silaha umeongezeka
2. Kuibiwa kwa silaha kumeongezeka
(ii) Majaliwa ameijia fedha yake
Maana: 1. Ametumia fedha yake kama nauli
2. Amekuja kuchukua fedha yake
(i) Mwalimu wa Kiingereza ni mkali
Maana: 1. Mwalimu wa somo la Kiingereza ni mkali
2. Mwalimu mwenye asili ya Uingereza ni mkali
(iv) Mwanangu amelalia uji
Maana: 1. Amekunywa uji tu akalala
2. Amelala juu ya uji uliomwagika
(v) Mama yangu anaota
Maana: 1. Anaota ndoto usingizini
2. Anaota moto kujipa joto
3. Anamea
51. (a) Ni nini maana ya kivumishi?
(b) Taja aina nane za vivumishi.
Majibu:
(a) Kivumishi (V) ni neno au kikundi cha maneno kinachotoa maelezo zaidi juu ya jina au kiwakilishi
kingine.
Mfano: Mtoto mzuri anakimbia
V
(b) Aina nane za vivumishi ni kama ifuatavyo:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 29
Vivumishi vya sifa – mfano: Mtoto mzuri, mrefu, mfupi, mtulivu, hodari, n.k
Vivumishi vya idadi – mfano: chakula kingi, haba, chote, mbuzi wanne, watano
Vivumishi vya vimilikishi – mfano: chumba chetu, chao, changu
Vivumishi vioneshi – mfano: kijiji hiki, kile, mtoto yule,
Vivumishi vya pekee – mfano: mtoto mwenyewe, yeyote,
Vivumishi vya a-unganifu – mfano: nguo za shule, za kijana, wavulana
Vivumishi vya jina kwa jina – mfano: mtoto kiziwi, kipofu,
Vivumishi viulizi – mfano: shule gani, ipi,
52. (a) Eleza maana ya Kiarifu katika sentensi.
(b) Taja vipashio vyote vinavyounda kiarifu.
Majibu:
(a) Kiarifu ni sehemu ya sentensi inayojazwa na maneno yanayoarifu tendo lililofanywa, linalofanywa
au litakalofanywa. Hutokea baada ya kiima.
Mfano: Baba yangu | analima shambani
A
(b) Vipashio vinavyounda kiarifu ni:
Aina zote za vitenzi
Mfano: Juma analima, Juma alikuwa analima, Juma ni mtoto
Shamirisho/kikundi jina
Mfano: Juma anafundisha mtoto Kiswahili
Chagizo/kikundi kielezi
Mfano: mama anasoma kitabu polepole
Juma anakimbia vibaya sana
53. (a) Eleza maana ya kielezi.
(b) Taja aina zote za vielezi
(c) Eleza matumizi ya kielezi
Majibu:
(a) Kielezi ni neno au maneno yanayotoa taarifa zaidi kuhusu kitenzi, kivumishi au kielezi kingine.
Mfano: Tulicheza vizuri, tulicheza vizuri sana, anasoma kitabu kizuri sana
(b) Kuna aina nane za vielezi kama ifuatavyo:
Vielezi vya namna/jinsi – mfano: John aliondoka kwa haraka
Vielezi vya mahali – mfano: anaishi porini
Vielezi vya idadi/kiasi – mfano: alimpiga mara nne
Vielezi vya wakati – mfano: mvua imenyesha asubuhi
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 30
(c) Matumizi ya vielezi ni:
Kuonesha namna au jinsi tendo lilivyofanyika
Kuonesha mahali tendo lilipotendekea
Kuonesha wakati tendo lilipotendeka
Kuonesha kiasi au idadi ya kutendeka kwa jambo
Kuonesha sababu ya kutendeka kwa tendo
54. Fafanua maana na dhima ya uambishaji katika lugha.
Majibu:
Uambishaji ni kitendo cha kupachika viambishi kwenye mzizi wa neno pasipokubadili kategoria ya
neno husika. Viambishi vya uambishaji huitwa viambishi ambatishi na hutokea kwa wingi kabla ya
mzizi wa neno.
Mfano: Neno cheza = anacheza, walivyocheza, wachezavyo
Dhima ya uambishaji katika lugha ni kama vile:
Kupanua maana ya neno mfano: lima-analima-walilima-wanaolima-walimavyo
Kudokeza nafsi mfano: amempiga
Kutaja njeo mfano: atampiga
Kutaja mtendwa mfano: aliyenisomea
Kudokeza mtendewa mfano: tuliowaita
Kudokeza urejeshi mfano: tulivuomkimbiza
* Zipo dhima nyingi sana za uambishaji hizo ni chache tu.
55. (a) Eleza maana ya viambishi.
(b) Taja aina za viambishi katika lugha ya Kiswahili.
Majibu:
(a) Viambishi ni mofimu zinazopachikwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo na maana
ya neno. Viambishi huweza kupachikwa kabla na baada ya mzizi wa neno.
(b) Viambishi katika Kiswahili ni vya aina kuu mbili ambazo ni:
Viambishi awali/tangulizi: hivi ni vile ambavyo hutokea kabla ya mzizi. Huitwa viambishi
awali kwa sababu huutangulia mzizi wa neno.
Mfano: a-na-ye-soma
Wa-li-vyo-ni-piga
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 31
Viambishi tamati/fuatishi: ni vile vinavyotokea baada ya mzizi wa neno. Hufuata mzizi wa
neno.
Mfano: anawalim-ish-a
Walivyoimb-ian-a
56. Tenga viambishi vya maneno yafuatayo kisha eleza kazi ya kila kiambishi.
(a) Anacheza
(b) Umependa
(c) Tuliongozana
(d) Analimisha
(e) Tutamwendeshea
(f) Atapika
(g) Amefika
(h) Tumecheka
(i) Waliompiga
Majibu:
(a) Anacheza = A-na-chez-a
A = kiambishi awali cha nafsi ya tatu umoja, uyakinishi, kipatanishi cha kisarufi.
na = kiambishi awali cha wakati uliopo hali ya kuendelea
chez = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana.
(b) Umependa = U-me-pend-a
U = kiambishi awali nafsi ya pili umoja
me = kiambishi awali wakati uliopita hali timilifu
pend = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana
(c) Tuliongozana = Tu-li-ongoz-an-a
Tu = kiambishi awali nafsi ya kwanza wingi
li = kiambishi cha wakati uliopita
ongoz = mzizi wa neno
an = kiambishi cha kauli ya kutendana
a = kiambishi tamati maana
(d) Analimisha = A-na-lim-ish-a
A = kiambishi cha nafsi ya tatu umoja
na = kiambishi cha wakati uliopo hali ya kuendelea
lim = mzizi wa neno
ish = kauli ya kutendesha
a = kiambishi tamati maana
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 32
(e) Tutamwendeshea = Tu-ta-mw-ende-sh-e-a
Tu = nafsi ya kwanza wingi
ta = wakati ujao
mw = mtendewa/yambiwa
ende = mzizi wa neno
sh = kauli ya kutendesha
e = kauli ya kutendea
a = kiambishi tamati maana
(f) Atapika = A-ta-pik-a
A = nafsi ya tatu umoja
ta = wakati ujao
pik = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana
(g) Amefika = A-me-fik-a
A = nafsi ya tatu umoja
me = wakati uliopita hali timilifu
fik = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana
(h) Tumecheka = Tu-me-chek-a
Tu = nafsi ya kwanza wingi
me = wakati uliopita hali timilifu
chek = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana
(i) Waliompiga = Wa-li-o-m-pig-a
Wa = nafsi ya tatu wingi
li = wakati uliopita
o = kirejeshi cha watenda
m = kiambishi cha mtendwa
pig = mzizi wa neno
a = kiambishi tamati maana
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 33
57. Eleza maana na dhima ya mnyambuliko katika lugha.
Majibu:
Mnyambuliko ni kitendo cha kupachika viambishi kwenye mzizi wa neno na kubadili kategoria ya
neno. Mnyambuliko huweza kutokea kabla au baada ya mzizi wa neno. Viambishi vya mnyambuliko
huitwa viambishi nyambuaji.
Mfano: cheza = chezeana, walichezesha, wanamchezea, mchezo, wachezaji
Dhima ya mnyambuliko katika lugha ni:
Kuzalisha maneno mapya kutokana na mzizi mmoja
Kupanua maana ya neno kwa kubadili viambishi
Kutambulisha kauili mbalimbali za vitenzi
Kuwezesha vitenzi kubeba nomino moja au zaidi
58. (a) Fafanua maana ya kiima katika sentensi.
(b) Fafanua vipashio vinavyounda kiima.
Majibu:
(a) Kiima ni sehemu katika sentensi ambayo hujaza nafasi ya mtenda wa jambo linaloelezwa na
hutokea kushoto mwa kitenzi katika sentensi.
Mfano: Juma / alikuwa anakimbia
K
(b) Vipashio vya kiima ni kama ifuatavyo:
Nomino peke yake mfano: Mtoto anacheza
Nomino + kivumishi mfano: Mzee mrefu amefika
Kiwakilishi peke yake mfano: Mimi ninaandika
Kiwakilishi + kivumishi mfano: Yule mweusi amekamatwa
Kitenzi jina + kivumishi mfano: Kucheza kwao kunavutia sana
Nomino + kishazi tegemezi vumishi mfano: Mzee aliyeumia ametibiwa
Nomino + kishazi tegemezi vumishi na nomino mfano: Mzee aliyeumia mguu ametibiwa
59. (a) Nini maana ya kitenzi.
(b) Kuna aina ngapi za vitenzi? Fafanua kwa mifano.
Majibu:
(a) Kitenzi ni neno linaloarifu jambo linalofanywa na mtu, kitu au kiumbe chochote chenye uwezo
wa kutenda jambo.
Mfano: Farida analima shamba, Maeda anafundisha Kiswahili.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 34
(b) Kuna aina kuu mbili za vitenzi ambazo ni:
Vitenzi halisi: aina hii inahusisha vitenzi vikuu (T), vitenzi visaidizi (Ts)
Vitenzi vishirikishi/husishi => t
Vitenzi halisi hueleza matendo yanayofanyika.
Mfano: kusema, kulima, kucheza, kuimba, n.k
Kitenzi kikuu hubeba wazo kuu katika tungo.
Mfano:
Nyumba hii imeezekwa vizuri sana.
Wanafunzi wamefuzu mtihani wao.
Vitenzi visaidizi (Ts) husaidia kitenzi kikuu kukamilisha ujumbe fulani. Vitenzi visaidizi
huweza kutokea zaidi ya kimoja katika tungo.
Mfano:
Baba alikuwa anataka kwenda kuoga
Upepo ulikwisha ezua mapaa ya nyumba.
Vitenzi vishirikishi (t) huonesha kuwepo au kutokuwepo kwa sifa au tabia fulani katika
nomino au kiwakilishi kinachohusishwa.
Mfano:
Ibrahim ni mpole sana
Gift si mkorofi
Huyu ndiye mgeni rasmi
60. (a) Eleza maana ya kiunganishi.
(b) Taja aina za viunganishi.
(c) Eleza matumizi ya kiunganishi.
Majibu:
(a) Kiunganishi ni neno au kikundi cha maneno chenye kuunganisha maneno, kikundi cha maneno,
kishazi au sentensi.
Mfano: Baba na mama wanalima
Kuruka na kuimba ni kazi nzuri
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 35
(b) Kuna aina mbili za viunganishi ambazo ni:
Viunganishi huru (vinavyojitegemea) – mfano: kaka na dada wanacheza
Viunganishi tegemezi (visivyojitegemea) – mfano: Ali-po-fika
(c) Matumizi ya viunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Mfano:
Jina na jina = shangazi na mjomba wanalima
Kishazi na kishazi = alichelewa kwa sababu alichelewa kuamka
Sentensi na sentensi = Baba analima lakini mama anapika jikoni
61. Eleza tofauti kati ya:
(a) Kihisishi (H) na Kihusishi (KH)
(b) Kitenzi kisaidizi na kitenzi kishirikishi
(c) Shamirisho na chagizo
Majibu:
(a) Kihisishi (H) ni maneno yanayodokeza miguso ya moyo au ya akili. Vionjo vya moyo huweza
kuwa vya furaha au huzuni, lakini vihusishi (KH) ni maneno yanayoonesha uhusiano baina ya
neno moja na jingine au baina ya kikundi kimoja na kingine.
Mfano wa kihisishi (H) ni: Kha! Ebo! Na mfano wa kihusishi ni (KH) ni chini ya, kwa ajili ya,
wa.
(b) Kitenzi kisaidizi (Ts) ni maneno yanayosaidia kitenzi kikuu (T) kukamilisha ujumbe lakini
kitenzi kishirikishi (t) ni maneno yanayoonesha kuwepo au kutokuwepo kwa hali fulani.
Mfano wa Ts ni: Juma alikuwa analima. Mfano wa kitenzi kishirikishi ni: ni, si, ndi, n.k.
(c) Shamirisho (Sh) ni jina au kikundi cha jina kinachojaza nafasi ya mtenda katika tungo na
hutokea baada ya kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi katika tungo hiyo lakini chagizo (Ch) ni
neno au kikundi cha maneno ambacho hujaza nafasi ya kielezi katika mpangilio wa sentensi.
Mfano wa (Sh) ni: Baba yangu analima shamba kubwa.
Mfano wa Ch ni: Baba yangu amekwenda shambani
62. Fafanua kauli mbalimbali zitumikazo katika vitenzi.
Majibu:
Kauli ya kutenda mfano: Lima, cheza, kimbia
Kauli ya kutendwa mfano: pigwa, somwa, limwa
Kauli ya kutendea mfano: imbia, somea, chezea
Kauli ya kutendewa mfano: somewa, imbiwa, chezewa, limiwa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 36
Kauli ya kutendeana mfano: someana, chezeana, limiana, imbiana
Kauli ya kutendeka mfano: imbika, pikika, chezeka, someka,
Kauli ya kutendesha mfano: imbisha, somesha, kalisha, zolesha, washa, ogopesha, ogofya,
lewesha, levya
Kauli ya kutendana mfano: imbana, somana, chekana, pigana
Kauli ya kutendua mfano: pindua, umbua, chomoa, tegua
63. Kwa kawaida sentensi yoyote ile ya Kiswahili inajieleza katika hali kuu tano. Fafanua hali hizo.
Majibu:
Hali ya maelezo (taarifa) mfano: Mwanaisha anakimbia vizuri sana
Hali ya kuuliza (swali) mfano: Baba amerudi?
Hali ya kushangaa mfano: Mwaka umeisha!
Hali ya ombi mfano: chukua kitabu hiki
Hali ya amri mfano: kimbia
64. Bainisha kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo:
(a) Mwimbaji yule maarufu aliyepewa zawadi amefariki dunia
(b) Kuimba kwake kunanifurahisha sana
(c) Baada ya hotuba hatukufanya kazi tena
(d) Mtoto aliyeumia mguu amelazwa hospitali
(e) Kijana yule mwembamba sana amefeli mtihani
Majibu:
(a) Mwimbaji yule maarufu aliyepewa zawadi / amefariki dunia
K A
(b) Kuimba kwake / kunanifurahisha sana
K A
(c) Baada ya hotuba / hatukufanya kazi tena
K A
(d) Mtoto aliyeumia mguu / amelazwa hospitali
K A
(e) Kijana yule mwembamba sana / amefeli mtihani
K A
65. Sarufi imegawanyika katika sehemu kuu nne (4). Taja sehemu hizo na fafanua kazi ya kila moja.
Majibu:
Sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya lugha. Sarufi hugawanyika
katika sehemu zifuatazo:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 37
(a) Sarufi matamshi/fonolojia – hushughulika na jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kuchunguza
mahali zinapotamkiwa na jinsi zinavyotamkwa. Sarufi matamshi ndiyo ghala la malighafi ya
kuundia maneno ambazo ni fonimu. Hivyo bila sarufi matamshi hatuwezi kuunda maneno ya
lugha. Mfano: neno baba linaundwa na fonimu = /b/, /a/, /b/, /a/
(b) Sarufi maumbo/mofolojia – ni tawi la sarufi linaloshughulika na maumbo ya maneno jinsi
yanavyoundwa na kazi za maneno hayo katika lugha. Sarufi matamshi ndiye mmiliki wa maumbo
ya maneno. Hivyo bila mofolojia hatuwezi kuunda tungo kama sentensi. Mfano kutokana na
maneno baba, shamba, analima, kubwa tunaweza kupata tungo kama:
Baba analima shamba kubwa
Baba analima shamba
Baba analima
(c) Sarufi miundo/sintaksia – ni tawi linaloshughulika na mpangilio na mfuatano wa vipashio ili
kuleta tungo yenye maana inayokubaliwa au iliyokusudiwa. Sintaksia ni kama fundi wa ujenzi
mwenye ujuzi wa kupangilia tofali (fonimu/maneno) ili kujenga ukuta ulionyoka. Ili kupata
maumbo ya maneno yanayokubalika ni lazima mpangilio wa fonimu uwe sahihi na pia ili kupata
sentnesi inayokubalika ni lazima mpangilio wa maneno uwe sawa na hiyo ni kazi ya sarufi miundo.
Mfano:
Neno abab halikubaliki lakini neno baba linakubalika kwa sababu ya mpangilio wa fonimu.
Tungo mdogo baba shamba analima kubwa haikubaliki lakini baba mdogo analima
shamba kubwa inakubalika kwa sababu ya mpangilio wake sahihi kwa sarufi ya Kiswahili.
(d) Sarufi maana/semantiki – hushughulika na maana zinazobebwa na maneno au sentensi katika
lugha. Maana huweza kuwa ya msingi au ya ziada hivyo ni kazi ya semantiki kupambanua maana
zote zilizosetiriwa na tungo husika. Mfano: Mzee amewachezea wanangu tungo hiyo ina maana
zaidi ya moja kama vile:
Mzee amecheza ili kuwafurahisha
Mzee amewaroga
Mzee amewadhalilisha kwa kuwaingilia
Mzee amecheza kwa niaba yao
66. Onesha aina za maneno yanayounda sentensi zifuatazo:
(a) Baba yake ni mfanyabiashara maarufu sana
(b) Mji huu ni mchafu
(c) Watoto hawakujua alimojificha kanga
(d) Maeda alikuwa anataka kwenda kununua sukari dukani
(e) Kiswahili kinaweza kufundishia masomo yote shuleni
(f) Baba na mama tunawaheshimu sana
(g) Nilikwenda kukopa kwa matajiri wangu
(h) Karoli alikunywa maji machafu sana
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 38
Majibu:
(a) Baba yake ni mfanyabiashara maarufu sana
N V t N V E
(b) Mji huu ni mchafu
N V t V
(c) Watoto hawakujua alimojificha kanga
N Ts T N
(d) Maeda alikuwa anataka kwenda kununua sukari dukani
N Ts Ts Ts T N E
(e) Kiswahili kinaweza kufundishia masomo yote shuleni
N Ts T N V E
(f) Baba na mama tunawaheshimu sana
N U N T E
(g) Nilikwenda kukopa kwa matajiri wangu
Ts T H N V
(h) Karoli alikunywa maji machafu sana
N T N V E
67. Kwa kila sentensi zifuatazo ainisha vivumishi vilivyopigiwa mstari.
(a) Watoto wazuri wanapanda ngazi.
(b) Mzee yule mrefu mwembamba ni baba yangu mkubwa
(c) Kwetu kuna bwana mmoja mchoma nyama
(d) Ng’ombe wa maziwa amepotea
(e) Watoto watano wamefuzu mtihani wa Kiswahili
(f) Vijana wametunza nguo zao kabatini
(g) Mwanafunzi hodari husoma kwa bidii
Majibu:
(a) wazuri = kivumishi cha sifa
(b) yule = kivumishi kioneshi
(c) mmoja = kivumishi cha idadi
(d) wa maziwa = kivumishi cha A-unganifu
(e) watano = kivumishi cha idadi
(f) zao = kivumishi cha kumiliki
(g) hodari = kivumishi cha sifa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 39
68. onesha aina za vielezi katika sentensi zifuatazo:
(a) Aliahidi kumpenda Hidari daima dumu
(b) Jumba lile limepasuka mara tano
(c) Mtoto yule alinijibu kihuni
(d) Huko Shinyanga kuna imani ya uchawi
(e) Simfahamu vizuri yule mtu tuliyempita
(f) Niwekee kikombe changu kabatini
(g) Leo ni sikukuu ya mashujaa
(h) Bunge hukutana mara kwa mara
Majibu:
(a) daima dumu = kielezi cha wakati
(b) mara tano = kielezi cha idadi
(c) kihuni = kielezi cha namna/jinsi
(d) huko Shinyanga = kielezi cha mahali
(e) vizuri = kielezi cha namna/jinsi
(f) kabatini = kielezi cha mahali
(g) leo = kielezi cha wakati
(h) mara kwa mara = kielezi cha idadi/kiasi
69. bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:
(a) Kucheza kunafurahisha watazamaji
(b) Anakusubiri kwa hamu sana
(c) Hapa ndipo mahali mtakapokutania
(d) Ng’ombe huyu ana matata sana
(e) La haula! kijana yule ameuawa
(f) Wewe ndiye kijana unipendezaye
(g) Anatembea kwa maringo sana
(h) Baba analima lakini mama anaimba nyimbo
Majibu:
(a) Kucheza = nomino (inatokana na kitenzi)
(b) kwa hamu sana = kielezi
(c) ndipo = kitenzi kishirikishi
(d) huyu = kivumishi
(e) La haula! = kihisishi
(f) Wewe = kiwakilishi
(g) lakini = kiunganishi
70. Andika “E” kwa kielezi au “V” kwa kivumishi katika maneno yaliyopigiwa mstari katika
sentensi zifuatazo.
(a) Hata ndege hukaa wawili wawili
(b) Viti hivi vizuri
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 40
(c) Mariam anaimba vizuri
(d) Macho yake malegevu
(e) Kitanda cha cha kwanza kushoto ndicho amelalia
(f) Mrembo yule asiye na kiuno amepewa zawadi
Majibu:
(a) E (b) V (c) E (d) V (e) V (f) V
71. Bainisha viwakilishi vilivyomo katika sentensi zifuatazo:
(a) Lile limetiwa rangi nyeupe
(b) Nyinyi mlifanya uchaguzi vizuri
(c) Ambao wamefika hapa ni wanasayansi
(d) Wangu hawatafika mapema
(e) Upi umepatikana?
Majibu:
(a) Lile = W-kioneshi
(b) Nyinyi = W-nafsi
(c) Ambao = W-cha urejeshi
(d) Wangu = W-kimilikishi
(e) Upi = W-kiulizi
72. Tunga sentensi zenye vipashio vifuatavyo:
(a) W + Ts + T + E
(b) N + V + V + T + N + E
(c) N + V + E + T + N + V + E
(d) N + V + T + N + V + E
(e) N + V + V + E + T + N + V
Majibu:
(a) Mimi nilikuwa naenda shuleni
(b) Watoto wawili warefu wanasoma kitabu polepole
(c) Mtoto aliyekuja jana ameweka kitabu kikubwa kabatini
(d) Mwanafunzi hodari anasoma kitabu kizuri sana
(e) Mwalimu mzuri aliyefika jana anafundisha somo zuri
73. Eleza maana ya:
(a) Kifungu tenzi
(b) Njeo
(c) Mzizi
(d) Sentensi shurutia
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 41
Majibu:
(a) Kifungu tenzi (fT) ni kitenzi kinachoambatana na viambishi awali na viambishi tamati.
Mfano: analima = a-na-lim-a
Anayekuja = A-na-ye-kuj-a
(b) Njeo katika kitenzi huwakilisha hali na wakati katika mpangilio wa vitenzi. Njeo hudokeza
wakati wa utendekaji wa jambo.
Mfano:
Anapika = a-na-pika (na- ni njeo iliyopo hali ya kuendelea)
Amelima = a-me-lima (me- inadokeza hali timilifu)
(c) Mzizi ni sehemu ye neno isiyobadilika baada ya neno kufanyiwa mnyambuliko au sehemu ya
neno inayobakia baada ya kuondolewa viambishi vyote awali na tamati.
Mfano:
Anasoma (mzizi = -som-)
Tumemuona (mzizi = -on-)
(d) Sentensi shurutia – ni sentensi inayotoa masharti kutokana na kubeba viambishi vya masharti
ambavyo ni (ki, nge, ngeli na ngali).
Mfano:
Ukisoma kwa bidi utafaulu
Angesoma kwa bidi angefaulu mtihani
Mngeliwahi mapema mngelimkuta nyumbani
Angalinisalimia ningalimuonesha
74. Pigia mstari vitenzi vishirikishi katika sentensi zifuatazo:
(a) Kiria ni mwanafunzi hodari sana
(b) Msichana huyu si mkorofi
(c) Joseph alikuwa mpole
(d) Huyu ndiye kiongozi wetu
(e) Wazee wa wakorofi
(f) Embe li kabatini
(g) Wewe u mlafi
Majibu:
(a) ni (b) si (c) alikuwa (d) ndiye (e) wa (f) li (g) u
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 42
75. Eleza tofauti iliyopo baina ya mzizi wa kitenzi na shina la kitenzi.
Majibu:
Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa viambishi vyote awali na tamati
lakini shina la kitenzi ni mzizi wowote uliofungiliwa kiambishi tamati maana.
Mfano:
Mzizi Shina
Lim- Lima
Chez- Cheza
Imb- Imba
Pig- Piga
Som- soma
76. Taja na fafanua tabia mbalimbali za vitenzi vya Kiswahili.
Majibu:
Kitenzi cha Kiswahili kina tabia tofautitofauti. Tabia hizo huonekana pale kitenzi kinapotoa taarifa
mbalimbali. Tabia hizo ni:
(a) Kutambulisha tendo linalotendeka mfano: cheza, imba, ruka, soma
(b) Kutambulisha wakati kama vile: wakati uliopita, wakati uliopo, wakati ujao
Mfano:
Aliniona (li- wakati uliopita)
Wanasoma (na- wakati uliopo)
Tutamuona (ta-wakati ujao)
(c) Kutambulisha nafsi
Mfano:
Ninasoma (ni-nafsi ya kwanza umoja)
Tumefika (tu-nafsi ya kwanza wingi)
Umeniona (u-nafsi ya pili umoja)
Mmewahi (nafsi ya pili wingi)
Analima (a-nafsi ya tatu umoja)
Wanalima (wa-nafsi ya tatu wingi)
(d) Kutambulisha hali ya tendo.
Mfano:
Anasoma (na- hali ya kuendelea)
Amefundisha (me- hali timilifu)
Husoma (hu- hali ya mazoea)
Akiwahi tutaondoka (ki- hali ya masharti)
(e) Kutambulisha kauli mbalimbali
Mfano:
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 43
Alinipigia (i – kauli ya kutendea)
Anamsomesha (esh – kauli ya kutendesha)
Watapigana (an- kauli ya kutendana)
(f) Kuonesha urejeshi
Aliyeimba (ye – urejeshi wa mtenda)
Walivyoimba (vyo – kirejeshi cha watenda/namna)
Kilicholetwa (cho – kirejeshi cha kitendwa)
77. Kirai ni nini? Kwa kutumia mifano orodhesha aina tano (5) za virai unazozifahamu.
Majibu:
Kirai ni neno au kifungu cha maneno chenye neno kuu moja. Aina ya kirai hutambulishwa na neno
kuu katika kirai husika. Kirai huwa ni kikubwa kuliko neno kihadhi na kidogo kuliko kishazi.
Aina tano za virai ni kama zifuatazo:
(a) Kirai nomino (KN) – mfano: watu wawili, baba mkubwa
(b) Kirai kivumishi (KV) – mfano: mtu mzuri kabisa, kijana mweupe mrefu amefika
(c) Kirai kitenzi (KT) – mfano: analima, anapika, tutamuona
(d) Kirai kielezi (KE) – mfano: sana sana, jana jioni, polepole mno
(e) Kirai kihusishi (KH) – mfano: kwa miguu, na mjomba, katika duka
78. Fafanua sifa tatu za sentensi sahili.
Majibu:
Sentensi sahili ni ile yenye kishazi huru kimoja tu. Sifa za sentensi sahili ni kama vile:
(a) Ina kiima ambacho kimetajwa wazi. Kiima hicho huweza kuwa jina, jina na jina au jina na
kivumishi.
(b) Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kishirikishi au kitenzi kisaidizi
na kitenzi kikuu pamoja na shamirisho na chagizo.
(c) Haifungamani na sentensi nyingine, na hivyo inajitosheleza kimuundo na kimaana.
Mifano ya sentensi sahili ni:
Paakwai analima shamba
Haidari ni mzembe sana
Hadija alikuwa anapika chakula
Kamenge alikuwa anataka kwenda kumpiga mke wake
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 44
79. Vifupisho vifuatavyo huwakilisha nini katika sarufi ya Kiswahili?
(a) KH (b) Ch (c) Sh (d) K (e) A (f) KN (g) KE (h) t (i) Ts (j) fT
Majibu:
(a) KH = kirai kihusishi
(b) Ch = chagizo
(c) Sh = shamirisho
(d) K = Kiima
(e) A = kiarifu
(f) KN = kikundi nomino/kirai nomino
(g) KE = kikundi/kirai kielezi
(h) t = kitenzi kishirikishi
(i) Ts = kitenzi kisaidizi
(j) fT = fungu tenzi
80. (a) Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ”Fafanua.
(b) Je, wanyama wana lugha? Toasababu.
Majibu:
(a) Lugha husemwa ni nasibu kwa sababu kuu zifuatazo:
Mwanadamu huwa hazaliwi na lugha bali hukutana nayo katika mazingira yake kwa bahati tu na kujifunza.
Hakuna kikao kilichowahi kukaa na kuamua juu ya kutumiwa lugha, lugha ilizuka tu.
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maneno ya lugha na maumbo ya vitu halisi. Mfano: neno “maji” halina uhusiano na kile kinachoitwa kwa neno hilo bali ni mazoea tu ya
watumiaji lugha.
(b) Wanyama hawana lugha kwa sababu hawana sifa za kumudu lugha kama mfumo wa mawasiliano. Lugha ni mali ya mwanadamu pekee na hutawaliwa na sifa zifuatazo.
Sauti: Lugha huambatana na sauti za binaadamu kutoka kinywani mwake. Binaadamu lazima atamke
jambo kwa kutoa sauti, zinazotamkwa kwa utaratibu maalumu kutoka kwenye maumbile yaliyo
ndani ya mwili wa mwanaadamu hususan kinywa, ambayo kiisimu huitwa ala za sauti.
Lugha ni lazima imhusu MwanadamuKimsingi hakuna kiumbe kisichokuwa mwanaadamu
(mtu) kinachoweza kuzungumza Lugha. Lugha ni chombo maalumu wanachokitumia binaadamu
kwa lengo la mawasiliano.
Lugha huzingatia utaratibu maalum;Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwa kwa kufuata
utaratibu fulani unaokubaliwa
na jamii ya watu wanaotumia lugha inayohusika. Kwa maneno mengine, si kila sauti
itokayo kinywani mwa mwanaadamu kuwa ni lugha. Sauti za vilio vya watoto, hoi
hoi na vigelegele vya waliofurahi, vikohozi vya wagonjwa wa pumu na vifua,
vicheko na kelele nyenginezo haziwezi kuitwa lugha.
Utaratibu huo maalumu unaofuatwa na lugha za wanaadamu huitwa sarufi.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 45
Lugha hufuata misingi ya fonimu Wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba fonimu ni
sauti yenye uwezo wa
kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno la lugha husika. Dhana ya
fonimu inatarajiwa kuzungumziwa kwa kirefu sana katika muhadhara wa sabaa. Kwa
mfano baadhi ya fonimu za Kiswahili ni .
/a/, /e/, /i/, /o/, /u/, kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno
yafuatayo:-/tata/~ /teta/~/tita/~/tota/~ /tuta/.
/p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /k/, /g/, /s/, /z/. kama zinavyoweza kubadilisha maana
katika maneno yafuatayo:-pawa~ bawa~ tawa~ dawa~ chawa~ jawa~ kawa~ sawa~ zawa, n.k
Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana Muundo wa Lugha huwa unafuata
mpangilio wa vipashio vyake maalumu na
lazima vipashio hivyo vifahamike. Mpangilio wa vipashio huo huanza na
fonimu, neno ambalo huundwa kwa mkusanyiko wa silabi au muunganiko wa
mofimu mbalimbali, kirai, kishazi na sentensi
Lugha inajizalishaVipashio vinavyoiunda lugha husika huwa na sifa ya kuweza
kunyumbulishwa ili
kupata maneno mapya. Kwa mfano vitenzi hunyambulishwa kwa kuongezwa
viambishi nz kwa hivyo, lugha hujiongezea maneno mapya. Kwa mfano tuangalie
mifano ifuatayo.
i) chez-a-------ku-chez-a-------ku-m-chez-a-------tu-li-m-chez-a.
ii) chez-e-a-------chez-ek-a----------chez-e-an-a-------chez-esh-a-------chez-w-a
iii) chez-esh-a- chez-esh-an-a- chez-esh-e-an-a
Lugha husharabu
Lugha husharabu kwa maana ya kwamba huchukuwa maneno kutoka lugha
nyengine ili kujiongezea msamiati wake.Tabia hii inazisaidia sana Lugha
zinazokua.
81. Kwa kutumia mifano miwili kwa kila muundo, taja miundo mine ya silabi. Majibu
a) Muundo wa kwanza ni ule unaojengwa na irabu peke yake.(I)
Hebu chunguza mifano ifuatayo:
silabi “a” katika neno “angalia” $a$ $nga$ $li$ $a$
silabi “u” katika neno “ugua” $u$ $gu$ $a$
silabi “I” katika neno “niite” $ni$ $i$ $te$
b) Muundo wa silabi wa Konsonanti na Irabu. (KI)
Mifano :
Zungumza =$zu$ $ngu$ $m$ $za$
Tapatapa =$ta$ $pa$ $ta$ $pa$
Maliza = $ma$ $li$ $za$
c) Muundo wa silabi wa Konsonanti, kiyeyusho na irabu (KkI)
Mifano:
Bwana =$bwa$
Fyata =$fya$
Mpya =$pya$
Upwa =$pwa$
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 46
Ukwezi =$kwe$
d) Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)
Mifano:
Mwandani =$nda$
Chongo =$cho$ $ngo$
Nguru =$ngu$
Daftari =$fta$
Boksi =$ksi$
Sekta = $kta$
82. Chunguza kwa makini nomino zifuatazo. Kisha kwa kuzingatia aina za nomino, tenganisha
nomio hizo katika makundi yake: mbuzi, Ashura, usingizi, kijiko, Januari, jeshi, matatizo,
Zanzibar, kamati, Mungu.
Majibu:
AINA ZA NOMINO NOMINO
Nomino za Pekee Ashura, Januari, Zanzibar,
Nomino za Kawaida Mbuzi, kijiko,
Nomino za wingi Matatizo,
Nomino za Jamii Jeshi, kamati,
Nomino dhahania Usingizi, Mungu
83. Changanua sentensi ifuatazo kwa kutumia njia ya jedwali.
Mwizi aliyeiba jana amekamatwa
Majibu:
S. Changamano
K
A
KN
KT
N
V
E
T
Mwizi aliyeiba ja
n
a
amekamatwa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 47
84. Moja ya faida za misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mfano mmoja wa misimu zagao
iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo:
Majibu:
(a) Miaka ya Azimio la Arusha
Kabaila
Bwanyenye
Ukupe
Mchumia tumbo
Ujamaa
Kujitegemea
(b) Njaa ya mwaka 1974/1975
Unga wa yanga
Kufunga mkanda
kumbakumba
(b) Kipindi cha mfumo wa vyama vingi
Ngangari
Wapambe
Wakereketwa
Wafurukutwa
(c) Awamu ya tano ya serikali ya Tanzania
Hapa kazi tu
Vyuma vimekaza
85. Sentensi zifuatazo zina makosa, zichunguze kwa makini kisha uziandike kwa usahihi.
Majibu:
a) Ninyi wote mmechelewa
Sahihi: Nyinyi nyote mmechelewa
b) Wanafunzi waliyosoma wamefaulu
Sahihi: Wanafunzi waliosoma wamefaulu
c) Ngombe zake zimeuzwa
Sahihi: Ng’ombe wake wameuzwa
www.mwalimuwakiswahili.co.tz || MWL. MAEDA || 0717104507 48
d) Walimu wamewakilisha michango yao
Sahihi: Walimu wamewasilisha michango yao.
UFAHAMU NA UTUNGAJI
86. (a) Eleza maana ya ufahamu.
(b) Taja aina za ufahamu.
Majibu: