45
Majina Ya Makufuru ` Asante, Ndugu Neville. Jambo hili lilikuwa kwa namna fulani la_la kustaajabisha kwangu. Sikutegemewa kuwepo hapa leo; bali usiku wa leo ni usiku wa Ushirika, nami_nami niliona ningeshuka nije asubuhi ya leo. Basi nilimpigia simu Ndugu Neville, naye akasema, “Vema sasa, kama unashuka kuja,” kasema, “mbona usituzungumzie kidogo.” Nami nikawaza, “Vema, kama ningeshuka, na iliwezekana, sitakuwa nikihubiri, bali ningalitaka tu kuzungumza na kanisa kidogo juu ya mambo ambayo, mwajua, ambayo nafikiri yangeliliimarisha kanisa.” Tumerudi hivi karibuni kutoka kwenye ninii yetu_kutoka kwenye mawindo yetu ya msimu wa mwisho wa mwaka (mimi na hawa ndugu hapa), nasi tulikuwa na wakati mzuri mno pamoja na^Tunashukuru sana. Sote tulishiba na_na_na tukapata wanyama pori tuliokuwa tunawinda. Na_nami pamoja na mchungaji wetu tunajua ya kwamba nyama ya kulungu ni nzuri sana, sana. Na kwa hiyo, tulikuwa na kulungu wazuri. Nami nilipata dubu na kulungu wawili. Ndipo tukarudi, na huu unapaswa kuwa ndio ule wakati ninaopaswa kuzungumza juu ya zile Muhuri Saba za mwisho. Nao hawakumaliza kujenga kanisa. Na kuna kitu, kizuizi, ambacho kimesababisha jambo hilo, ambacho^Nafikiri hili jiji linatupa wakati mgumu, kwa sababu ya kutokuwa na nafasi ya kutosha ya kuegeshea magari kwa ajili ya wingi wa watu ambao tuna_ambao kanisa litaenea. Tunataka kanisa jipya lijengwe hapa, na tuna kiasi cha fedha cha kutosha kilichokwisha kutengwa na_na kwa ajili ya kujenga ka_kanisa kubwa zaidi. Bali tunapokuwa na ibada hizi, mbona, mnafahamu ni nini. Ni jambo la kusikitisha sana: watu wamesimama kwenye kuta, huko nje kwenye mvua, na_ na_na ni jambo baya sana. Na hata shutuma hutoka kwa marafiki zangu, likasema, “Ndugu Branham, inaonekana kana kwamba wao^” Daktari fulani rafiki yangu alisema, “Inaonekana kana kwamba ungalipata mahali fulani ambapo unge-^ ninasikitika,” kasema, “^nipitapo.” Nesi fulani jirani yangu alisema, “Mbona, nilipitia kule alfajiri moja kwenye saa 11. Ulikusudiwa kuwapo pale,” kisha kasema; “watu tayari wamekusanyika kwenye hilo kanisa hapo kwenye saa 11 alfajiri. Ulikuwa uwe pale kwenye sasa 3:30.” Kwa hiyo, mnaona? Na inalifanya kuwa jambo gumu.

Majina Ya Makufurudownload.branham.org.s3.amazonaws.com/pdftranslations/SWA62-110… · tunaishi katika siku za mwisho_tunaamini kwamba_kwamba mahali ambapo ninii_tunapaswa kuwa tukifundisha

  • Upload
    doantu

  • View
    514

  • Download
    32

Embed Size (px)

Citation preview

MAJINA YA MAKUFURU 1

Majina Ya Makufuru

` Asante, Ndugu Neville. Jambo hili lilikuwa kwa namnafulani la_la kustaajabisha kwangu. Sikutegemewa

kuwepo hapa leo; bali usiku wa leo ni usiku wa Ushirika,nami_nami niliona ningeshuka nije asubuhi ya leo. Basinilimpigia simu Ndugu Neville, naye akasema, “Vema sasa,kama unashuka kuja,” kasema, “mbona usituzungumziekidogo.”

Nami nikawaza, “Vema, kama ningeshuka, na iliwezekana,sitakuwa nikihubiri, bali ningalitaka tu kuzungumza na kanisakidogo juu ya mambo ambayo, mwajua, ambayo nafikiriyangeliliimarisha kanisa.”

Tumerudi hivi karibuni kutoka kwenye ninii yetu_kutokakwenye mawindo yetu ya msimu wa mwisho wa mwaka (mimina hawa ndugu hapa), nasi tulikuwa na wakati mzuri mnopamoja na^Tunashukuru sana. Sote tulishiba na_na_natukapata wanyama pori tuliokuwa tunawinda. Na_namipamoja na mchungaji wetu tunajua ya kwamba nyama yakulungu ni nzuri sana, sana. Na kwa hiyo, tulikuwa nakulungu wazuri. Nami nilipata dubu na kulungu wawili.

Ndipo tukarudi, na huu unapaswa kuwa ndio ule wakatininaopaswa kuzungumza juu ya zile Muhuri Saba za mwisho.Nao hawakumaliza kujenga kanisa. Na kuna kitu, kizuizi,ambacho kimesababisha jambo hilo, ambacho^Nafikiri hilijiji linatupa wakati mgumu, kwa sababu ya kutokuwa nanafasi ya kutosha ya kuegeshea magari kwa ajili ya wingi wawatu ambao tuna_ambao kanisa litaenea.

Tunataka kanisa jipya lijengwe hapa, na tuna kiasi chafedha cha kutosha kilichokwisha kutengwa na_na kwa ajili yakujenga ka_kanisa kubwa zaidi. Bali tunapokuwa na ibadahizi, mbona, mnafahamu ni nini. Ni jambo la kusikitisha sana:watu wamesimama kwenye kuta, huko nje kwenye mvua, na_na_na ni jambo baya sana. Na hata shutuma hutoka kwamarafiki zangu, likasema, “Ndugu Branham, inaonekana kanakwamba wao^”

Daktari fulani rafiki yangu alisema, “Inaonekana kanakwamba ungalipata mahali fulani ambapo unge-^ninasikitika,” kasema, “^nipitapo.”

Nesi fulani jirani yangu alisema, “Mbona, nilipitia kulealfajiri moja kwenye saa 11. Ulikusudiwa kuwapo pale,” kishakasema; “watu tayari wamekusanyika kwenye hilo kanisahapo kwenye saa 11 alfajiri. Ulikuwa uwe pale kwenye sasa3:30.” Kwa hiyo, mnaona? Na inalifanya kuwa jambo gumu.

2 LILE NENO LILILONENWA

Nasi tunataka kanisa ambalo lina nafasi, na mahaliambapo kila mtu anaweza kuketi chini. Nasi tunafikiritunaishi katika siku za mwisho_tunaamini kwamba_kwambamahali ambapo ninii_tunapaswa kuwa tukifundisha kanisajuu ya_juu ya mambo haya yanayokuja: mambo ambayoyametabiriwa, baadhi yao, maelfu ya miaka; na kwa yapatamiaka ishirini na mitano na thelathini moja kwa moja katikakanisa hili, ambayo yamekwisha tabiriwa yangetimia. Na sasa,tunayo yakija kutimia moja kwa moja. Kwa hiyo tunapaswakuwa tukifanya upya mambo haya, bali hatuna nafasi yakutosha.

Kwa hiyo asubuhi ya leo^Ningeninii, nikipiga simuzangu na kadhalika jana, nami nikapata ninii_wenginekufanya alasiri ya leo na kadhalika. Halafu basi, nilikuwa naninii_watu waliotaka kuingia: jamaa mdogo ambaye anaugonjwa wa fadhaa, ndugu mhudumu hudumani; na lo, wengiwa namna hiyo; na ndugu fulani kutoka Norway. Nasi_nasitulikuwa na mahojiano madogo kule nyuma kwenye chumbacha nyuma, nami nikasema, “Vema sasa, tutatoka tu nje.”

Naye Ndugu Neville akasema, “Vema, tungetoka nakusema mambo machache ya kulihuisha kanisa kidogo.”

La kwanza_moja ya mambo ya kwanza ambayo natakakusema^Niliandika mambo fulani hapa kwenye karatasi, ilinifikapo kanisani, nilitaka kusema. Jambo moja nililokuwanimeandika lilikuwa kuhusu kuaga dunia kwa Ndugu Taylortulipokuwa tumeondoka.

Ndugu Taylor alikuwa anahudhuria kanisa hili kwa miakana miaka. Sote tulimjua, nina hakika. Bali kama kungekuwana wageni hapa, ilikuwa ni yule mzee muungwana ambayedaima alikutafutia kiti cha kuketi, Ndugu Taylor. Mara yamwisho niliyomwona, naam, mpaka nilipomwona nikiwakijana, alikuwa anasimama pale mlangoni yapata Jumapilitatu ama nne zilizopita. Akasema, “Ningetaka kuchukuavitabu, Ndugu Branham. Ningetaka kuvisambaza vitabu hivi.”

Kwa hiyo sisi^Yeye^Ninavyofahamu mimi, alikuwaana kisukari akazirai na haku-_bila kujua alikuwa nakisukari_naye alikuwa^Akafa. Hakufa; alienda tu kuwapamoja na Bwana Yesu.

Naye alikuwa ndugu mwaminifu na wa ajabu, daimaakiwajali watu wengine. Na furaha yake ilikuwa kujaribukumtafutia mtu fulani mahali pa kuketi walipokuja kanisani.Nanyi mwajua, labda tutakapovuka kwenye ile nguzo, silitakuwa jambo zuri kumwona Ndugu Taylor, kule,akitutafutia mahali pa kuketi kwenye ng’ambo ya pili?

Nafikiri katika kumkumbuka Ndugu Taylor^Sikuwekohumu kuzungumza kwenye_pamoja na Ndugu Neville kwenye

MAJINA YA MAKUFURU 3

mazishi yake, bali nataka kutoa rambirambi zangu kwa mjanewake. Dada Taylor, nadhani, yuko hapa mahali fulani asubuhiya leo. Nautakia heri moyo wake mwaminifu.

Ndugu Taylor, siku moja alisema, “Panda uje kunisalimu.Ninalo bwawa dogo lililochimbwa kule. Niliweka samakiwachache mle kwa hiyo ungekuja ukavue samaki.” Daimaalimjali mtu mwingine, na kulikuwa na Mtu fulani aliyemjaliyeye; huyo alikuwa Kristo, kumpa wokovu. Nami nafikiri kwaajili ya kumbukumbu ya kanisa hili, linapokusanyika kamamwili mmoja tena asubuhi ya leo, na tusimame pamoja nakuinamisha vichwa vyetu mbele za Mungu.

Baba yetu wa mbinguni, sisi kama wanadamu asubuhi yaleo na_na wanaohudhuria mahali hapa pa kuabudia^Mkono Wako mkuu umetenda kazi miongoni mwetu nakumwondoa kwetu mmoja wa ndugu zetu wa thamani, ambayetunampenda na tunajua ya kwamba Wewe ulimpenda. Naweulikuwa na sababu kwa ajili ya haya yote, Bwana, la sivyohaingalitukia namna hii, tukijua ya kwamba Biblia yetuinatwambia ya kwamba mambo yote hutendeka kwa manufaaya hao wanaompenda Mungu; na hilo alifanya.

Nasi tunaangalia kila mahali ulimwenguni, na tunaonama_maumbile, kwa kila njia, yakitwambia ya kwamba kaburihaliwezi kumzuia, kwa kuwa duniani alitimiza kusudi ambaloulimtuma humu kutimiza. Alikuwa ndugu mzuri namwaminifu.

Nasi tunaona ya kwamba katika uhai wa maisha yamimea, na katika maisha ya jua ambalo huchomoza asubuhikutupa nuru^ Na mchana linafikia umri wa makamu,halafu, jioni linakufa tena, kisha linafufuka tena asubuhiinayofuata likiwa changa na jipya, kwa maana lilitimizakusudi la Mungu.

Tunaona maua yanapochanua, na kuipamba nchi, nakuzipamba kumbi za mazishi na sehemu za kufanyia arusi, nakutumikia kusudi fulani: likifungua moyo wake na kutoa kwamoyo mkunjufu, asali kwa nyuki, na manukato kwa mpitaji,na uzuri kwa anayetafuta; linatoa yote liliyo nayo kwa ajili yautumishi wa Mungu, kisha linainamisha maskini kichwachake. Bali majira ya kuchanua yajapo linainuka tena, kwakuwa lilitimiza kusudi la Mungu.

Halafu mbele ya maumbile yote, na Biblia, ile Ahadi, naRoho Mtakatifu, tunaweza kufurahi moyoni mwetu kwa kujuaya kwamba Ndugu yetu Taylor, vivyo hivyo, Bwana, alitimizakusudi la Mungu. Basi kusema kwamba yeye hatafufuka tenaingekuwa ni kuikana Biblia, Mungu wetu, na mambo yoteambayo Mungu ametupa kuangalia, kujua ya kwamba kunakufufuka. Kwa hiyo tunautazamia wakati ambapo tutamwonatena, wakati yeye ni kijana na mwenye afya na hatakuwamgonjwa tena wala kuzeeka.

4 LILE NENO LILILONENWA

Mbariki mke wake wa thamani, huyo mwenziwemwaminifu. Jinsi tutakavyowakosa kwa muda mrefu, Bwana,tunapowaona wakienda pamoja kwenye kile kidimbwi, nawakiketi kwenye zile mbao za kukalia kule, wakivua samakina kuzungumza, na jinsi walivyokuwa wanapendana.

Basi sasa, tunajua ya kwamba kuna siku kuu inayokujawakati wale mashujaa wa imani watakapopita wakitembeachini ya tao kuu la ushindi, nao Malaika wa_wakiwa nanyimbo za sifa watajaa hewani. Tutawaona tena mahali pale.

Hata wakati huo, Bwana, tupe ujasiri. Tubariki nautusaidie. Tutamkosa Ndugu Taylor, na kila mmoja anayekujakwenye kanisa hili, jinsi angesimama mlangoni na kutafutamahali kwa ajaye kusikia Neno la Mungu, apate kuketiamestarehe na kupumzika.

Na hivi majuzi wakati alipoaga dunia, Bwana, niliomba yakwamba Malaika Mkuu wa Mungu aliyesimama pale mlangonikumtafutia mahali pia, Bwana, ambapo angeweza kuketi chini.Kwa maana imeandikwa katika Biblia, “Wenye rehemawatapata rehema.” Mpaka tutakapomwona, Bwana, jalia ilekumbukumbu iendelee kuwa tamu mioyoni mwetu, mpakasiku moja tutakapokutana tena kwenye ile nchi nyingine.Katika Jina la Yesu Kristo tunaomba. Amina.

Yeye atakosekana kwa muda mrefu kati yetu sisi namiongoni mwa wageni na kadhalika wanaohudhuria kanisaletu ama jengo letu hapa kuabudu. Nafsi yake na ikae katikaamani mbele za Mungu hata siku ile. Siku moja pia, kilammoja wetu ataondoka mmoja mmoja, mpaka tutakapoingiamstarini namna iyo hiyo. Hebu nasi sasa, wakati tuna wakatina tunaweza, na tujitayarishe wenyewe kwa ajili ya wakati uleujao; kwa kuwa hatujui itakuwa lini. Hatujui ni naniatakayefuata. Na tuishi ili kwamba kila siku, ya kwambakama huo utawahi kuja, utakuwa kwa ajili yetu, tutakuwatayari.

Sasa tungetaka kutoa matangazo. Sasa hivi karibuni,huenda ikawa labda^Sijazungumza na wadhamini tanguniliporudi, kuhusu hali ya kujenga ka_kanisa hapa, amatunachopaswa kufanya baadaye juu ya kupata kanisa letukusudi tuweze kufanya mikutano yetu. Kisha nitaendelea(samahani) na zile_zile Muhuri Saba. Halafu, kuna vile VitasaSaba na_na mambo mengi bado ambayo yatupasa kuyaingiliamara moja.

Na sasa, Jumapili ijayo asubuhi huko_ninapaswa kuwaElizabethtown, Kentucky, pamoja na Ndugu L. G. Hoover,kwenye ibada ya kuweka wakfu. Na hiyo ni kuweka wakfumaskani mpya_ama maskani ambayo wamenunua kuleElizabethtown, Kentucky: moja kwa moja kwenye ya 62 hatautakapofika Elizabethtown_ama moja kwa moja kule chini_

MAJINA YA MAKUFURU 5

namaanisha ya 31, ama kule chini kwenye kituo cha kodi yabarabara. Kwenye tu mahali pa kugeukia inakupeleka mpakaElizabethtown. Ni kama saa moja; ni kama maili thelathini natano, arobaini kule chini. Nafikiri yapata maili arobaini kwanjia ya_ya 31, na yapata maili thelathini na tano ama kitukama hicho kwenye ile njia nyingine, ukishuka kwenda karibuna kituo cha kodi ya barabara. Iko kwenye Barabara yaMulberry. Ile ibada ya kuweka wakfu^

Ndugu Hoover atakuwa na shule ya Jumapili ya kawaidasaa 4, nami ninapaswa kuhubiri ibada ya kuweka wakfukutoka saa 5 hadi saa 6, Jumapili hii ijayo, Novemba 11.

Kwenye ubao wa matangazo kule nje kuna_ni tangazolake, na itakuwa kwenye^Unaweza kupata njia kutoka papohapo. Yako kwenye Barabara ya Mulberry, ama wao_waowanatoa maelezo kwenye^Yako kwenye ubao wa matangazokule nje mbele ya kanisa.

Halafu mnamo_mnamo ta_tarehe 22 Novemba,i_inanibidi kuwa Shreveport, Louisiana, kwenye tarehe 22, 23,24, 25, na 26_siku tano, nafikiri, huko Shreveport, Louisiana,kwenye Maskani ya Uzima. Hiyo ni pamoja na Ndugu Moore.Wao wanasherehekea sikukuu ya ukumbusho wa mwaka waowa hamsini. Baraka za Pentekoste zilishuka huko Shreveport,Louisiana, miaka hamsini iliyopita, tarehe 22 ya mwezi huu.Miaka hamsini, ujumbe wa kwanza wa Kipentekosteulihubiriwa, na kushuka_Roho Mtakatifu alishuka Louisiana.Nao wana ukumbusho wa jambo hilo, na huu ndio ukumbushowa mwaka wa hamsini. Nami ninapaswa kuhubiri yubile hii,siku tano usiku pamoja na Ndugu Moore kule Shreveport,Maskani ya Uzima.

Kama mna marafiki karibu na kule, mbona (ambaomnataka kuwaandikia ama cho chote kile), tungefurahia kuwanao kule. Basi waambieni tu juu ya hiyo mikutanao ijayo.

Nayo Maskani ya Uhai, endapo mtu ye yote amewahi kuwakule pamoja na Ndugu Moore, yeye ni mtu mzuri sana. Piakuna kundi la watu wazuri sana. Hao wa Kusini wa tangu sikunyingi, ni vigumu kuwashinda. Na kwa hiyo, Maskani yaUzima, ye yote aliye karibu na Shreveport anawezakukwambia mahali ilipo. Shreveport ina karibu watu 200,000,na ni mji mzuri na kuna malazi mengi, kwa hiyo^

Nayo hayo maskani ni maskani makubwa, maskanimakubwa sana. Yana orofa, roshani, na sakafu ya chini, nahalafu sakafu chini yake; na kuna nafasi tele kweli, na mojakwa moja upande wa pili wa_kutoka kwenye ukumbi wa jijiambao unakaa watu elfu tano_kama_kama tu kuvukabarabara hapa kwenda kwenye ukumbi wa jiji.

Naye Kasisi Jack T. Moore ama_ama aidha Maskani yaUzima kule Shreveport, Louisiana^ Hiyo inaanza tarehe 22.

6 LILE NENO LILILONENWA

Hiyo itakuwa Alhamisi hadi Jumapili: Alhamisi, Ijumaa,Jumamosi, Jumapili, siku nne badala ya tano, nasikitika. Hiyoingekuwa tarehe 22, 23, 24, na 25 (nafikiri hivyo ndivyo ilivyo)ya_ya Novemba.

Halafu, tutaona basi vipi kuhusu_kile tumefanya kuhusukanisa hapa, tuone jinsi kanisa limeendelea juu ya kupatajengo lake. Makandarasi wanatwambia wanaweza kuwekawatu wa kutosha katika shughuli hiyo, mpaka yapata karibusiku kumi wanaweza kulitayarisha hivi kwamba tunawezakuingia ndani yake. Mnaona? Upesi sana. Nao wanangojea tujiji litie sahihi^ Mwajua, nasi tunapaswa kuwa na kiasifulani cha mahali pa kuegeshea magari, kiasi fulani cha hili;na loo, jamani, ni kupitia mambo mengi rasmi, kabla yakuanza kujenga cho chote.

Lakini ningetaka kufika kanisani kabla sijarudi hudumanitena. Naam, nina mwito kwenda Tanganyika, Uganda, nakupitia kule. Joseph ametayarisha mikutano itakayoanzaFebruari.

Na jana nilipoingia, kulikuwa na baadhi ya ndugu na DadaToms na hao wengine kutoka nchi za ng’ambo waliokuwawamekuja, nami nilikuwa_nilipata kijikaratasi mlangonimwangu_ama_ama mwaliko kutoka kwenye shi_shirika mojakule Afrika Kusini. Kwa hiyo ninawaandikia kuona tulinaloweza kufanywa. Labda nitakapokuwa umbali huo,ninaweza kwenda Afrika Kusini, labda, kwenye sehemu yamwisho ya Februari na Machi mnamo wakati huo.

Nasi tunakusudia kulijenga kanisa, kusudi niwezekuingiza hizi Nyakati za Kanisa kabla_kabla majira yakipupwe hayajaanza, ikiwezekana. Kama haiwezekani, amainaponibidi kurudi kutoka kule, kama Bwana Yesuakikawia^

Nilikuwa nikisikiliza jana nilipokuwa ninachukua_naamini ilikuwa ni juzi_kwenye kanda. Nilifikiri niliisikiaikicheza hapa asubuhi ya leo. Maskini ndugu fulani wa Kusinialikuwa^Mama yake alikuwa amehudhuria mkutano;alikuwa na ugonjwa wa kufisha kwenye titi lake, naye alikuwaametiwa uvuli wa mauti. Ndipo Roho Mtakatifu, katika mmojawa mikutano ya hivi karibuni kule_Southern Pine, naaminiilikuwa huko, ama mahali fulani, alimwambia, kasema juu yaugonjwa wake wa kufisha, na Yeye alikuwa ni nani, naalikotoka; kisha kasema alikuwa na mvulana aliyekuwaamerudi nyuma, naye angepata ajali kisha ashtakiwe kwamauaji yasiyo ya kukusudia, na mambo mengi sana ya namnahiyo.

Basi huyu jamaa^Yote yalitukia tu vile^ Na ugonjwawake mbaya sana wa kansa_au kivimbe cha kufisha, hasa,ulimwacha (ambacho, kivimbe cha kufisha ni kansa, mwajua).

MAJINA YA MAKUFURU 7

Kwa hiyo basi kili_kilimwacha, na mvulana wake alikuwaameshtakiwa kwa mauaji yasiyo ya kukusudia, na kila kitujinsi Roho Mtakatifu alivyosema. Naye aliongozwa kwaKristo_akarudi tena. Naye akafanya kanda yake, nami_naminiliisikia ikicheza. Hivi mlifurahia hayo mazungumzo madogoya Kusini? Kasema, “Hapa chini North Caroliner^,”akasema. [Ndugu Branham anaiga kukokoteza sauti kwandugu huyo wa Kusini_Mh.] Loo, ninapenda tu jambo hilosana, hao watu wa Kusini. Naye alikuwa^Bwana ndiyokwanza ambariki kwa jambo hilo. Kasema, “Najua unasemahuhubiri fundisho, Ndugu Branham, ila kwa kusanyiko lakotu,” kasema; “sisi ni sehemu ya kusanyiko lako.” Kwa hiyohilo lilikuwa jambo zuri sana kwake kusema hivyo.

Basi sasa, kuna picha^Nafikiri labda ipo kwenye ubaowa matangazo asubuni ya leo. Kama haipo, Billy ataiwekakule. Mara nyingi imesemwa, nilipoanza kuzungumza hayowao walisema, “Unawazia tu, Ndugu Branham, ya kwambaunaona Nuru hiyo, ile Nuru.”

Labda ni vigumu^Huenda ikawa kuna wenginewaliosalia hapa, watu wa zamani ambao wanakumbuka kulenyuma, kabla picha Yake hata haijawahi kupigwa. Kuna yeyote hapa ambaye anakumbuka mimi nikisema jambo hilo,muda mrefu sana uliopita? Angalieni! Yapata tu mikono minneama mitano: Dada Spenser hapa, na Ndugu na DadaSlaughter, na_na Ndugu hapa, Ndugu kule. Kuna tu kamawatano ama sita wa wale wa zamani waliosalia.

Vema sasa, baada ya kitambo kidogo, jicho la mitambo yakamera ile lilipiga picha ile. Kwa hiyo ikaenda Washington,D.C., kisha ikapitia kwa wachunguzi halafu ikarudi, na ha_hakuna kupigwa picha mara mbili wala cho chote kile.Kasema, “Nuru iliguza lenzi.” Huyo ni George J. Lacy. Mnayosahihi ya jina lake. Mnaona?

Vema basi, mara nyingi unasikia, naangalia kule nje nakusema, “Kuna kivuli cheusi juu ya mtu huyu. Ametiwa uvuliwa mauti.” Ni wangapi wamenisikia nikisema jambo hilo maranyingi (mnaona?), mara nyingi? Vema, ilitukia kwamba kamerailishika jambo hilo. Na kwa hiyo tunayo hiyo hapa.

Mwanamke fulani aliyemjia dada fulani na alikuwaamemwambia katika mkutano kule_kule Carolina, ambakotulikuwa na mkutano mzuri sana kule Southern Pines^ Nakule, yule bibi alikuwa akifa kwa kansa iliyokuwa kwenyematiti yote mawili. Nao madaktari walikuwa wamemkatiatamaa wamemwacha afe. Ndipo yule bibi alinyosha mkono nakumpiga picha mara tu nilipokuwa nikimwambia alikuwanani na mahali alipotoka; nami nikasema, “Kuna kivuli cheusijuu yako. Umetiwa kivuli cha mauti.” Naye yule bibi akapigatu picha ya jambo hili, na hiyo pale kwenye^Jicho lakimitambo la kamera limekipiga picha kivuli cha mauti.

8 LILE NENO LILILONENWA

Kuna mmoja wenu ameona ile Amri Kumi na kuonamalaika wa mauti, jinsi alivyoingia, kile kivuli cheusikinachoonekana cha huzuni? Kiko kwenye picha hii. Naminafikiri iko kwenye ubao wa matangazo sasa. Kama haiko, Billyanaweza kunisikia, mbona, mwambieni aiweke kwenye ubaowa matangazo. Nayo ina mshale unaoelekeza kwa huyo mtu.Naye huyo mtu^Hicho kivuli kilimwacha huyo mwanamkena^akaponywa kimiujiza. Lakini kuna kama kifuniko chamoshi mweusi kilichomzunguka na kufanya kifuniko juu yahuyo bibi, na kikining’inia juu ya kansa hiyo, namna hiyo,kikitoka kwenye hicho. Bila shaka hicho ni kivuli ambamomauti inatiririkia ndani yake kutoka kwenye ile kansa.

Vema, haidhuru ni jinsi gani unavyojaribu kuwaambiawatu kweli, kuna mtu fulani atakayekuwa na shaka kwamba sikweli. Na iwapo daima unasema kweli, basi unajua wewe_wewe u sahihi.

Nina rafiki ambaye ni m_mfugaji kule Magharibi. Na_naHifadhi ililipa yapata $4,000 kwa ajili ya gari la barafukuhesabu kundi la kulungu wakubwa waliosalia huko kwenyeBonde la Troublesome. Bw. Jefferey, aliyeketi humu kanisani,nilimwongoza kwa Kristo_kafiri kwelikweli. Nanyimmenisikia nikisimulia hadithi ya sisi kupanda farasi pamoja.Naye hakuamini ya kwamba_hakuamini kitu ila maadili yaDarwin, na yule Mtoto Mchanga, aliyezaliwa na bikira,ilikuwa ni upuuzi. Nasi tulipiga kambi pale pale hasaalipompokea Kristo.

Na kwa hiyo basi, mtu huyu akamwambia; akasema,“Sasa, mimi_si lazima ununue gari hilo_gari hilo la barafu.”Kasema, “Nitakwambia ni kulungu wangapi hasa waliokokule.” Kasema, “Kuna kumi na tisa.” Kasema, “Kulikuwekona ishirini_kulikuweko na ishirini na mmoja, nami nikauawawili wao.” Naye alikuwa anazungumza na mlinzi wawanyama pori. Hupaswi kuua ila mmoja. Kwa hiyo akasema,“Kulikuweko na ishirini na mmoja, nami nikawaua wawili.Wanasalia kumi na tisa.”

“Naye akasema, “Naam, Jeff, najua uliua wawili.”

Akasema, “Niliwaua!”

Vema, wakachukua gari la barafu wakapanda wakaendakule, na kulikuwa na kulungu wakubwa kumi na tisa.Akasema, “Billy, mwambie tu mtu kweli; hataamini.” Kwahiyo hivyo tu ndivyo ilivyo. Unaweza kuwaambia watu kweli,na hata hivyo wao^Kumekuweko na kutoelewa kwingi sanana_na kusema uongo kuhusu mambo, mpaka wao hawaaminiya kwamba unasema kweli wakati unapowaambia kweli.Mnaona?

Lakini tunashukuru sana ya kwamba tuna Baba wambinguni ambaye huthibitisha Kweli hiyo kwa uthibitisho. Ni

MAJINA YA MAKUFURU 9

Kweli. Kwa hiyo basi, kama hii itakuwa siku yangu ya mwishoduniani, ile^Hata utafiti wa sayansi na mathibitishoyamethibitisha ya kwamba nimesema kweli kuhusu mambohaya. Hiyo ni kweli; ni kweli. Kwa hiyo labda itakuwa kwenyeubao wa matangazo. Billy, umo humu chumbani humu? Unayomkononi mwako, ile picha? Na iwapo unayo, basi ilete hapa,halafu unaweza kuiweka hapa, nao labda wanaweza kuiona.Vema, sijui. Kutakuweko na nuru kwenye_kwenye ubao.

Na hii hapa ile_hii hapa ile picha papa hapa. [NduguBranham anaonyesha ile picha_Mh.] Nadhani hamwezikuiona, bali papa hapa mnaweza kuona kile kifuniko chakivuli cha mauti juu ya kichwa cha mwanamke yule. Na hapakuna maandishi juu yake huku nyuma, ambapo yule bibialipiga ile picha na_kuona kama kweli ilionyesha; na hiyohapo ku_kule. Ni kifuniko cha kivuli cha mauti. Mnakiona juuya yule. Umekiona nadhani. Ndugu Neville?

Kwa hiyo Billy labda ataiweka kwenye ubao wamatangazo, tafadhali. Billy atakuja aichukue, na kuipelekakule upande wa mbele, na kuiweka kwenye ubao, ili kwambakila mtu aweze kuiona wanapotoka nje. Yeye ama Doc, mmojawao. Sasa, nilifikiri labda ingeweza kuonyesha dhahiri vyakutosha kwamba mngeweza kukiona, bali kuna giza jingi sanakwa picha ya namna hiyo. Bali ataiweka kule ili kwambampate kuiona mnapotoka nje.

Sasa, kumbukeni matangazo yote.

Na sasa, asubuhi ya leo nilifikiri labda kwambatungezungumza kwa muda kidogo juu ya kitu fulani kulitiamoyo kanisa, kitu ambacho kingewapa ninyi ni_ninii zaidi^

[Ndugu Branham anazungumza juu ya tochi na nduguyake, Edgar_Mh.] Naam, Doc, kama ukiweza. Huenda ikawani zuri. Nataka kutumia hii hapa. Nilikuwa^Wengine waohawakuiweka kwa ajili ya juma lililopita, kwa hiyo tukafikirilabda ingetoa vizuri zaidi kwa leo. Nilitaka kuzungumziajambo hilo, kwa maana linahusu ndo_ndoto aliyoota dadafulani.

Sijui kama Dada Shepherd yuko kanisani asubuhi ya leo.Nilikutana naye juzijuzi usiku. Na mara yangu ya kwanzaniliyopata kumwona huyo mwanamke. Kweli, hata sikujuaalikuwa ni nani. Je! yeye^? Nadhani yeye si^Naam.Tafadhali, lingekuwa jambo baya kama nikirejea kwenyendoto hiyo? Dada Shepherd, usingejali sivyo? Vema, ni sawa.Na kabla hatujaliendea jambo hilo, na tuinamishe vichwavyetu sasa, tena.

Baba wa mbinguni mwenye rehema, Kwako tunatoa sifakwa wema Wako wote na rehema. Na sasa, tutulize, Bwana,kusudi tupate kulisoma Neno la Mungu Aliye Hai, kamalinavyotujia katika ono na linathibitishwa na Roho Mtakatifu,

10 LILE NENO LILILONENWA

huku likiungwa mkono na Biblia. Kwa hiyo tunaomba yakwamba Wewe utatupa ufahamu, kusudi tupate kujua lakufanya katika siku hizi za mwisho tunapoziona nguvu zauovu zikituzunguka sasa. Vile vita, vile vita vya mwisho, vikokaribu sana kupiganwa. Tusaidie, Bwana. Kama mashujaahalisi, wenye nguvu, na tuiinue ngao ya imani juu pamoja naNeno la Mungu, ule Upanga, na tupige hatua kwenda mbele.Katika Jina la Yesu. Amina.

Sasa, tukiwazia juu ya kusonga mbele, kwa vita, kama vi_vita vilivyoandaliwa, tayari kupiganwa, vita ha_halisikupigana vita vya imani^

Dada Shepherd, hapa, na Ndugu Shepherd, ambao ni rafikiwetu wazuri sana, na ambao wanahudhuria maskani hii^Nao ni watoto wa thamani wa Mungu. Basi_basi huyu DadaShepherd^Nilipokuwa nikichukua barua zangu (ambazoBilly anaweza kujibu, zile za mtu kusema tu, “Nitumie lesokadha za maombi.” Nami huziombea; yeye anazijibu tu. Baliikiwa ni barua ya kibinafsi, sina budi kuijibu mimi mwenyewe.Mnaona?)^ Kwa hiyo nikachukua barua zangu za kibinafsi.Na kwa hiyo nilikuwa nikizichukua kwenda nazo nyumbani,nami nilikuwa nikisoma mle; ilisema, “Kutoka kwa DadaShepherd.” Nayo ilikuwa ni ndoto aliyokuwa ameota miezikadha iliyopita. Naye asingeweza kuifahamu mpaka Jumapilimbili ama tatu zilizopita wakati nilipofundisha juu yahizi_hizi Nyakati Saba za Kanisa na_na yale_yale matundasaba_2 Petro, jinsi inavyopasa ku- (2 Petro 1)_kuongezeakwenye imani yetu. Mnaona?

Kwanza: kimsingi, ni imani. Pili: tia kwenye imani yako,nguvu: kwenye nguvu zako, maarifa; kutoka kwenye maarifa,kiasi; kutoka kwenye kiasi, saburi; kwenye saburi, utauwa; nakutoka kwenye utauwa, upendano wa ndugu_wema wandugu; na halafu upendo ukiwa ndio jiwe la kufunika juu_saba ya mambo hayo. Nyakati saba za kanisa (mnaona?), nanyota saba za nyakati saba za kanisa, na zote hizozinachanganywa pamoja na Roho Mtakatifu.

Sasa, hayo ndiyo yanayohitajika kuwa mtumishi waKristo. Kristo hulijenga Kanisa Lake katika nyakati saba zakanisa, Bibi-arusi Wake, Mtu fulani, Mwanamke, Kanisa.Nyakati saba za kanisa zinamuumba na kumfanya Bibi-arusi:wengine kutoka kwenye wakati huu, na wengine kutokakwenye wakati ule, na wengine kutoka kwenye wakati ule, nawote pamoja, na kuliumba Hilo kama piramidi.

Kama vile Henoko alivyojenga zile piramidi, ambazotunaamini^Na jiwe la kileleni kamwe hakikuwekwa juu yahizo, kwa maana jiwe la kichwani lilikataliwa.

Na tunalichukua sasa, si kama fundisho, bali ili kufahamu,kwa ajili tu ya kanisa hapa, ili kwamba hawa^

MAJINA YA MAKUFURU 11

Mungu hujifanya Mwenyewe mkamilifu katika tatu.Hujifanya mkamilifu katika Baba, Mwana, Roho Mtakatifu,afisi tatu za Mungu mmoja. Hujifanya mkamilifu katikaKuhesabiwa Haki, Kutakaswa, Ubatizo wa Roho Mtakatifu;zinakuwa kazi kamilifu za neema. Yeye hujifanya mkamilifukatika kuja kutatu: mara ya kwanza kumkomboa Bibi-ArusiWake, mara ya pili kumpokea Bibi-Arusi Wake, mara ya tatukatika ule Utawala wa Miaka Elfu pamoja na Bibi-arusi Wake.Na kila kitu hukamilishwa katika tatu-tatu. Na saba ni nambaya Mungu ya ibada; Mungu huabudiwa katika saba,kumalizika. Sasa imekamilika na imemalizika.

Na jambo la ajabu lilikuwa (si kuingiza jambo hili, balikuwaonyesha tu), kulungu wa mwisho niliyempata alikuwa nancha tano upande mmoja na tatu kwenye ule mwingine(mnaona?): neema na ukamilifu.

Sasa angalieni juu ya jambo hili, ya kwamba Kristo^Mungu aliandika Biblia tatu. Biblia ya kwanza ilikuwa angani,inayoitwa zodiaka. Naam, kama hujui kitabu cha Ayubu,sahau hilo, maana_kwa maana Ayubu ndiye anayelielezea:jinsi alivyoangalia juu, kisha akavipa majina vitu hivyoangani.

Basi angalia, katika zodiaka, ilianza na kitu gani? Kitu chakwanza katika zodiaka ni bikira. Kitu cha mwisho katikazodiaka ni Leo yule Simba: kuja kwa kwanza kwa Kristokupitia kwa bikira; kuja kwa pili, Leo yule Simba, Simba waKabila la Yuda.

Ndipo Henoko akamaliza katika siku zake, ama kulenyuma katika hizo, lile piramidi. Na, bila shaka, hatunawakati wa kuliwekea msingi na kuonyesha jinsi piramidi hilolilivyokuja kupitia kwenye vile vyumba na kadhalika.Inazungumza moja kwa moja hata kwenye wakati wa mwishosasa. Wao wako kwenye chumba cha mfalme sasa kwa vilevipimo. Bali jiwe la kichwani halikuwekwa kamwe kwenye lilepiramidi. Na hiyo inakaa ikiwa kamilifu kabisa kiujenziama_ama kiuashi, mpaka hata we_wembe mdogomwembamba^ Nao hawajui jinsi wao walivyopata kulijenga,hawaelewi_jinsi wembe ungeweza kamwe kupita katikasehemu ambazo zingeungwa kwa chokaa, na hakuna chokaandani yake. Ni kamilifu tu, imewekwa pamoja.

Kwa hiyo hivyo ndivyo ilivyo wakati Kristo na Kanisawanapokuwa mmoja. Hakuna chokaa katikati; hakuna kilichokatikati, ni Mungu tu na huyo mtu_ Mungu, Kristo, na huyomtu.

Sasa, lakini lile jiwe la kichwani, wao hawajalipata bado.Mnajua lile Jiwe la Skonsi walilo nalo kule Uingereza lakutawazia wafalme_ama ku_kuwatia taji na kadhalika? Balilile jiwe la kichwani^

12 LILE NENO LILILONENWA

Angalia kwenye noti ya dola ya Marekani; utaiona kwenyenoti ya dala ya Marekani. Kwenye upande mmoja, upande wakushoto, kuna Muhuri wa Marekani, tai aliyeshika mikuki.Kwenye upande wa pili^Hii inaitwa Muhuri ya Marekani.Bali kwenye upande wa pili kuna piramidi, na juu yake, jichokuu. Halafu chini hapa inasema, “Ile Muhuri Kuu.” Mbona iweni Muhuri Mkuu katika taifa hili, hata juu ya Muhuri ya taifaletu? Mnaona, haidhuru utafanya jambo gani, Munguanaifanya inene jambo lile hata hivyo. Mnaona? Yeyehumfanya mwenye dhambi kunena juu ya jambo hilo; Yeyehuyafanya mataifa kunena juu ya jambo hilo; kila kitu hakinabudi kuzungumza juu Yake, kama u_unataka kuamini jambohilo ama hutaki. Liko papo hapo.

Sasa angalia, kuna jicho kwenye hiyo_jicho la Mungu. Nakwa sababu hicho kifuniko hakikutoka, ile Muhuri yaKichwani, kwa sababu ilikataliwa, ambapo ilikuwa ni Mwanawa Mungu, Jiwe la Pembeni la hilo jengo, Muhuri ya Kichwaniya lile piramidi, na haya yote.

Sasa, sasa, mimi^Sitaki ku-^Wakati mwingine waohunasa mambo haya, na yanatoka nje miongoni mwa ndugumakanisani_wa makanisa mengine. Nao wanapofanya jambohilo, ndipo hao ndugu wakati mwingine wanapata mawazomabaya, ya kwamba ninasema jambo fulani juu ya hao ndugu.Bali sisemi. Mimi^Kama mngalisikiliza tu na kufahamu(mnaona?), mimi sineni juu ya ndugu ye yote, maana jambohilo halifai kwa hao ndugu kunena kuhusu_mmoja juu yamwingine. Inatupasa kushuhudiana mazuri, si kusemana. Balininapozungumza wakati mwingine juu ya madhehebu fulanikama vile Presbiteri, Methodisti, ama kadhalika, waowanasema, “Mnaona, anayapinga.” Mimi simpingi ndugualiyemo mle wala dada aliyemo mle. Utaratibuunaoutenganisha undugu ndio ninaonena dhidi yake. Watotowa Mungu ni familia moja na si_si makundi mbalimbali.

Na baadhi yao wanasema, “Sitahusika nalo, kwa sababuhilo ni la Presbiteri nami ni Mmethodisti.” Mnaona? Sasa, hilosilo^Mnaona, ni huo utaratibu wa madhehebu hayounaovunja huo undugu. Mnaona? Sasa hilo^

Kama nilivyosema: Kama ulikuwa kwenye mto ukitelemkakatika mashua inayoonekana bovu na ya kale na ulikuwaunaenda kujaribu kuvuka maporomoko, nami najua yakwamba jambo hilo halitafanikiwa, vema basi, mimi sipigimakelele, kukukemea; ninajaribu kukutoa kwenye mashuahiyo (mnaona?); kwa maana mashua ndiyo itakayovunjika,nawe_nawe_nawe utaachwa umeketi peke yako majini. Kwahiyo_kwa hiyo si_si yule ndugu katika ile mashua, balininampigia makelele yule ndugu kumwonyesha yaleyatakayotukia.

MAJINA YA MAKUFURU 13

Vema, taratibu hizi zote, ambazo wanadamu wameundakatika ufanisi wao, hazina budi kuvunjika. Hivyo tu. Lazimawafikie^Hatuna budi kufikia kwenye umoja, kwenyeundugu. Hilo limekuwa^Kusudi la maisha yangu ni kujaribukuunganisha wala si kuyavunja madhehebu, bali hebu waowaache mawazo yao na wawe ndugu kwa kila Mkristoaliyezaliwa mara ya pili. Wazo ndilo_ndilo hilo; hapo ndiponimesimama.

Vema sasa, kama wandugu wangeangalia jambo hilo,mimi^Wengi wa ndugu zetu, hata kwenye safu zetu za InjiliYote, wao hawaamini ya kwamba Wabatisti, na Wamethodisti,na Waluteri, na hao wengine wana nafasi. Bali mimi^Sasa,huenda wanasema kweli, bali mimi sikubaliani na jambo hilo.Naamini ya kwamba ule wakati hapa, wa Wakati wa Waluteri,na wakati huu hapa ulioitwa, naamini, Wakati wa Sardi,halafu Wakati wa Filadelfia kwa ajili ya Wamethodisti, halafuWapentekoste, Wakati wa Laodikia^ Naamini hizo ninyakati, naye Mungu katika kila mmoja wa nyakati hizoalichukua watu walioteuliwa. Na katika hilo, kama vile_Waebrania 11 isemavyo ya kwamba hao pasipo sisihawakamilishwa. Mnaona? Lakini sasa, Kanisa limekujakutoka kwenye hili, likija katika walio wachache wakati wote,hata limefikia katika Wakati wa Kipentekoste.

Sasa, sababu ya kusema jambo hili: ni kwamba mpatefununu juu ya kile yule dada alichoota. Nayo ndoto yake kweliinalingana na_na yale niliyokuwa nikifundisha.

Angalia, sasa hapa, sasa mambo haya yote ambayo I Petroaya ya 6 na ya 7 inawaambia, yaliyoletwa na imani yenu, hiyondiyo ya kwanza. Sasa, nasema ya kwamba watu wanadaikuwa na sifa hizi bila hata kuzaliwa mara ya pili. Naminaamini nilitoa tamshi la kijeuri na kusema ni kama ndegemweusi akijaribu kujibandika manyoya ya tausi na kujifanyatausi; hawezi kufanya jambo hilo. Yawapasa kuwa ni unyoyawa kawaida ulioota toka kwake. Mwili wake hauna budi kutoaunyoya huo.

Na daima_na daima nimeshtakiwa kuwa mkali kwa dadazetu juu ya kuwa na nywele zilizokatwa, na kujipodoa nyusonimwao mwote, na kadhalika. Daima nimelaumiwa kuwa nimkali kwa dada zetu. Si kwamba nina kitu dhidi ya jambohilo. Sisemi mwanamke huyo si mwanamke mzuri, ya kwambayeye ni ninii_kahaba wa mitaani ama cho chote kile. Hiyo siyonia yangu. Bali hivi ndivyo ilivyo: wakati yeye anapoweka vituchungu nzima vya bandia kwa nje, inaonyesha kuna ubandiamwingi mno humo ndani (mnaona?), mahali ambapopanapaswa kujazwa na Kristo. Kwa maana nje daimahuonyesha kile kilicho ndani. “Kwa matunda yaomnawatambua.” Mnaona? Na ambapo Kristo anapaswa kuwahumo ndani, na kushughulikia ninii_Mungu, na kushughulikia

14 LILE NENO LILILONENWA

mambo mengine, badala ya uzuri mwingi wa bandia, na_na,ninyi mwajua, kope za kijani, na yasiyoonekana kama ni yakibinadamu, na takataka zote za namna hiyo^Mimisiyapendi mambo hayo; wala siamini Biblia inayakubali. Kwahiyo mimi_mimi napenda tuwe tu jinsi tulivyo.

Angalia sasa, kama yeye hana kucha zo zote za vidole naanataka kuweka chache, iwapo hana meno yo yote na anahitajimachache, huna mkono na unataka mmoja, huna nywele naweunataka nyingine, huna vitu hivi, hilo ni jambo lingine. Baliunapong’oa meno yako ya kweli na mazuri, kwa sababu ati simeupe kama yanavyopaswa kuwa, basi umefanya makosa.Kama una nywele nyekundu nawe unataka nyeusi, naweunashuka unaenda hapa chini na kuzitia rangi nyeusi, kwasababu tu^Umefanya makosa. Naam, nafikiri hivyo. Balijambo muhimu^Hakuna Maandiko kwa ajili ya jambo hilo,ni kukata nywele zako tu, kuna Andiko juu ya jambo hilo, ninamengi ya hayo. Kwa hiyo basi, tunataka kuhakikisha kabisa yakwamba jambo hilo ni kweli. Sasa.

Sasa, sasa, dada yetu katika kuota, aliota ya kwambayeye^Vema kwanza, alifadhaika: “Kuna haja gani yakuendelea na kujaribu kujitahidi katika maisha kama Munguanatutaka tumpokee Roho Mtakatifu nasi hatuna Huyo?”

Sasa, sidhani^Huenda wao wananasa huu, bali kamahawaunasi_kama wanaunasa, ni kwa ajili ya kanisa pekeyake. Mnaona? Sasa, na iwapo ndugu fulani ataupata huu,nawe usikie sauti yangu, ndugu, juu ya jambo hili, kumbuka,ninafundisha tu kanisa langu. Wewe daima, mbele yakusanyiko lako^Chunguza hizo_hizo kanda, na endapohutaki kusanyiko lako lizisikilize, usiwaruhusu wazisikilize.Bali mimi_mimi ninajaribu tu kuliambia kundi hili dogo hapaya kwamba mimi_ambalo mimi na Ndugu Neville, kwa RohoMtakatifu, tunajaribu ku_kuwachunga na kuwafundisha^

Sasa, kuna baadhi ya mambo haya ambayo huendamkayapinga vikali. Kwa hiyo kama yapo, kama tu nilivyosemadaima juu ya kula kuku aliyekaangwa: Unapofikia kwenyemfupa humtupilii mbali huku, unatupa tu mfupa. Kwa hiyofanya hivyo daima. Ukila sambusa ya tunda jekundu na ukutepunje, hutaitupa hiyo sambusa, utatupa tu hiyo punje. Kwahiyo fanya jambo lilo hilo katika kuusikiliza huu.

Sasa, na_naamini ya kwamba_ya kwamba sa_sababu yakuwa na kuchanganyikiwa kwingi leo juu ya Roho Mtakatifu,Hilo halijafundishwa sawasawa. Ninaamini ya kwambaubatizo unafundishwa, na kusema tu, “ubatizo,” lakini basiuwe^Kama vile ukisema, “motokaa.” Lakini sasa, ninamafundi wengi wa magari katika kanisa hili, nami sijui chochote juu yake, kwa hiyo kama nikifanya kosa, ndugu,mimi^Kumbukeni mimi si fundi wa magari.

MAJINA YA MAKUFURU 15

Hapana budi kuwe na koili, na plagi, na pointi, na vilango,na kila kitu kinginecho kinachoifanya motokaa. Naunapozungumzia kuhusu Ubatizo wa Roho Mtakatifu, kunamambo mengi yanayoambatana na huo. Mnaona? Kuna mengiyanayoambatana na huo. Na jambo hili ndilo linalonifanyanifikiri ya kwamba Mungu anathibitisha Roho Mtakatifu yukohapa. Mnaona?

Basi, Petro alisema kwanza, imani. Sasa angalia jambo hilokwa makini sana sasa. Tutafundisha jambo hili kwa dakikachache. Imani, sasa, ndiyo ya kwanza kwako. Tia katika imaniyako, nguvu; katika nguvu zako, maarifa; katika maarifa yako,kiasi; katika kiasi chako, saburi; katika saburi yako, utauwa;katika utauwa wako, upendano wa ndugu, fadhili za kindugu,halafu upendo. Na mtu ye yote anajua ya kwamba upendo niMungu. Mungu ni upendo. Mnaona?

Sasa kwa kuwa_halafu kutoka katika jambo hili, halafukuleta jambo hili kwenye zile Nyakati Saba za Kanisa, Munguanajenga katika nyakati saba za kanisa Bibi-arusi kwa ajili yaKristo. Kupitia kwenye wakati wa Filadelfia, wa Thiatira, waPargamo, na wa Smirna, Efeso, wakati wa kanisa ambao Yesualisema, “Kama_kama Bwana Arusi akija katika zamu yakwanza ama zamu ya saba, wanawali hawa wote waliamka.”Wao walikuwa_wao waliamka, wanawali wa Efeso, Smirna,Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia, na Laodikia. Umeonahilo? Ilikuwa ni wakati wa saba ambapo alikuja nakuwaamsha hao wanawali waliolala. Jambo hilo linawaletakutoka kote kote huko nyuma mpaka hapa (mnaona?), kwakuwa katika jambo hili, kupitia katika miaka, nyakati, Yeyeamejenga Bibi-arusi, akamzaa Bibi-arusi, akamzaa Bibi-arusiduniani kwa ajili ya Kristo. Na kwa njia ile ile anayomzaaBibi-arusi huyu, amewazaa watu binafsi.

Sasa, ninawekea jambo hili msingi, ili kwamba mwonewakati ile ndoto ya dada inaposimuliwa.

Sasa, mambo haya hapa hasa hayana budi kuwa ndani yaMkristo daima kabla Roho Mtakatifu hajawatia muhuri kablahiki hakijaja upande wa juu na kufanya kitu kimojakikamilifu.

Sasa, ndoto ya dada yetu sasa. Yeye alipata wasiwasi kamaana Roho Mtakatifu ama hana. Wakati alipolala kwenyeKitanda cha watu wawili, ambapo mumewe alikuwa anasomagazeti (na ana watoto, kama nilivyo nao mimi, nao daimawanafanya makelele na kadhalika), na kwa hiyo katika jambohili, alilala usingizi kwa kama dakika kumi ama kumi na tano;ndipo akaota. Naye kamwe asingeweza kuielewa walakuikumbuka tangu mwaka mmoja uliopita, karibu, mpakaujumbe huu ulipofundishwa. Ndipo wakati nilipokuwaninaufundisha, yote ikamrudia.

16 LILE NENO LILILONENWA

Naye aliota ya kwamba alikuwa anaomba. Alikuwaanatembea sakafuni kwanza, kabla hajaota ndoto, na kusokotamikono yake, na kuwaza, “Bwana, hivi mimi nina RohoMtakatifu? Unaweza kunithibitishia. Wengine wanasema ati_ati kwa sababu nilipiga makelele, ama wengine walisema atikwa sababu nilinena kwa lugha. (Nasi tunaamini katika hayoyote.) Lakini hivi kweli mimi ninaye?”

Ninaamini katika mambo hayo yote, sifa hizo: kunena kwalugha, na kupiga makelele, na kila namna ya madhihirisho.Ninaamini katika kila moja ya hayo. Bali kama yako bila hili,kuna kasoro. Unaona? Sasa, mnaona? Wewe^Unaona, unaganda.

Angalia, naye alikuwa amefadhaishwa na jambo hilo, kwahiyo alilala tu chini kukingama kwenye kile Kitanda cha watuwawili, ambapo mumewe alikuwa anasoma, ndipo akaingiausingizini. Basi akaota alikuwa juu ya mlima fulani. Na katikamlima huu^Ninii bora sana^Sina ile karatasi mbeleyangu, bali nafikiri ni namna hii: Yeye aliota ya kwambaaliona ki_kitu kama sanduku la mwamba, kama jukwaalimewekwa moja kwa moja juu ya mlima huu. Naye bwanawake alikuwa nyuma yake. Ndipo akaona mtu mkubwaamesimama pale amevalia nguo za kazi, mikono ya lile vaziimekunjwa, akiteka maji safi sana aliyowahi kuona nakuyamwaga kwenye sanduku hili, sanduku hili la mwambalililokuwa juu ya ule mlima. Nalo sanduku hilo la mwambahalikuweza kushikilia hayo maji; nayo yalitiririka yakatokamle na kuchemsha taka zote na vijiti na kila kitu mle ndani, nakuvichemsha, kisha yakatiririka mlimani. Nayo yakatiririkiakwenye miguu yake, naye alikuwa amesimama katikati ya takahizo; ila tu hazikumchafua. Ndipo_ndipo basi akauliza kwanini lile sanduku halikuyazuilia, ndipo yule mtu akasema,“Hayo si maji. Huyo ni Roho Mtakatifu,” na akasema; “hakunakitu kinachoweza kumzuilia Huyo.”

Kisha kasema, “Ndipo akarudi akachukua ndoo nyinginekubwa_nayo ilikuwa imejaa asali_halafu akaimwaga ile asalimle na kusema, ‘Sasa, itaizuilia hii.’” Naye alifikiri yakwamba lile sanduku lilikuwa_lile sanduku la mwambalingepasuka na kuimwaga ile asali, bali halikupasuka.Hatimaye ilishikamana na likaizuilia.

Akageuka akashuka mlimani. Alipokuwa anashukamlimani, alisimama chini ya ule mlima na kuangalia nyuma.Akaona vijito vitano vya maji haya masafi kabisa,yasiyochafuliwa na vitu ambavyo yalikuwa yamevipitia,yangali mazuri na masafi, yakija mbio. Kisha yakapunguzamwendo; halafu karibu kutoweka. Naye alikuwa akishangaakama yatawahi kufika chini ya ule mlima_vijito vitano_ndipoakaamka. Nafikiri hiyo ni karibu na kuwa sawa, sivyo, DadaShepherd?

MAJINA YA MAKUFURU 17

Sasa, mara nilipoichukua ile barua na kuifungua, kablasijaisoma, nikaona ile ndoto yake. Sasa, hivyo ndivyo ndotozinavyofasiriwa. Sasa, wengi wenu mmenijia na ndoto na_nakuniambia mambo juu ya ndoto. Ninasema, “Ngoja kidogo.Hukuisimulia yote” (mnaona?); nami narudi nyuma nakuichukua. Basi kama huwezi kusimulia ulivyoota, unajuajefasiri hiyo ni kweli ama si kweli? Mnaona? Huna budi kuwana_huna budi kuiona hiyo ndoto. Ono halina budi kuonyeshahiyo ndoto. Basi unapoiona hiyo ndoto ambayo huyo mtualiota, nawe ungeweza kuwaambia kabla hawajakwambia,basi unajua hiyo fasiri^

Vema, naamini hiyo iko katika Maandiko pia. Danieliwakati mmoja (hiyo si ilikuwa ni kweli?) alisema^Naam,naamini^Imetukia kwamba nimewazia juu ya jambo hilobasi. Mnaona? Bali daima unaona hiyo ndoto, sasa, iwapo hiyotafsiri ni kweli. Mtu fulani akianza kukusimulia ndoto,unawakatiza tu, unasema, “Ngoja kidogo. Na ilikuwa fulani,pamoja na fulani, kuongeza fulani.”

Kisha unasema, “Hiyo ni kweli kabisa.” Unaona?

Mtu fulani, juzijuzi, alikuwa anajaribu kunisimulia ndotoaliyoota. Akasema, “Vema,” akasema^

Nikasema, “Sasa, ndugu, mbona uliacha ile sehemunyingine?”

Akasema, “Sehemu nyingine gani?”

Nikasema, “Uliota ya kwamba ulitupa jiwe hewani, naminikalipiga risasi na vingine vikaingia kwenye jicho langu.”

Akasema, “Hiyo ni kweli kabisa, Ndugu Branham.”

Nao walichukua ile sehemu yake ya mwisho jana. Kwahiyo ndiyo hivyo. Mnaona? Mnaona? Mbona huachilii^Wewesema kweli juu ya jambo hilo. Lakini, mnaona, daima inafunuakile_inakuambia ndoto yako, kile ulichoota. Ndipo unajua nikweli.

Naam, hii hapa fasiri ya ndoto yake. Yeye alisumbuka juuya Roho Mtakatifu. Naam, kwa vile aliona lile sanduku juu yaule mlima lilikuwa la mwamba, sanduku la mwamba ni“kukiri kwa mwamba.” Sasa, kama vile Yesu alivyosemakatika Maandiko, Yeye alisema^Petro alisema^Yesualisema, “Watu hunena Mimi, Mwana wa Adamu, kuwa ninani?”

Mmoja alisema, “Wewe ndiwe Eliya, na Musa, nakadhalika.”

Basi Yeye akasema, “Lakini nanyi mwaninena ya kuwaMimi ni nani?”

18 LILE NENO LILILONENWA

Akasema, “Wewe Ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu AliyeHai.”

Sasa, watu wengine husema^Sasa, kanisa Katolikihusema, Kanisa Katoliki la Kirumi linasema ya kwamba niniiYake_kile ule mwamba ulikuwa ndicho ambacho Yesualisema, “Juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa Langu walamilango ya kuzimu haitalishinda Hilo,”^ Wao walisemaulikuwa ni juu ya Petro, na Petro alikuwa huo mwamba, kwamaana Petro linamaanisha “jiwe dogo.” “Na juu ya jiwe hilidogo nitalijenga Kanisa Langu.” Na juu ya Petro wao_uhalifawa kimitume_wao walilijenga kanisa.

Halafu kanisa la Kiprotestanti linasema, “Hilo ni kosa,” yakwamba alilijenga Kanisa juu Yake Mwenyewe.

Sasa, si kuwa asiyekubaliana, bali mimi_nionavyo mimi,wote wamekosea, kwa maana Yeye hakulijenga kamwe juu yaPetro, wala hakulijenga juu ya nafsi Yake; bali ni juu yaufunuo wa Petro kwamba Yeye alikuwa ni Nani. Mnaona?“Watu hunena kwamba Mimi, Mwana wa Adamu^”

“Wewe Ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Aliye Hai.”

“Heri wewe, Simoni, mwana wa Yona: mwili na damuhavikukufunulia hili (seminari fulani. Mnaona?); bali BabaYangu aliye Mbinguni amekufunulia. Wewe ndiwe Petro, juuya mwamba huu (wa kukiri, juu ya ufunuo huu) nitalijengaKanisa Langu.”

Na hiyo imekuwa^Kila wakati wa kanisa umekuwa nakuungama huko kwa mwamba mpaka kwenye mwamba huuwa kuungama wa Laodikia. Na sasa, huwezi kufanya kanisatakatifu. Hakuna kitu kama kanisa takatifu wala madhehebumatakatifu. Roho Mtakatifu anaweza kuhubiriwa ndani yake,bali mle ndani unakuta wazuri na wabaya, wapotovu,wasiojali, na cho chote kile. Kwa hiyo madhehebuhayatabeba^ Huwezi kusema, “Tunaye; hakuna wenginewalio Naye.” La, bwana! Roho Mtakatifu humiminwa juu yawatu binafsi. Ni mtu binafsi.

Kwa hiyo basi, ule mwamba^Kanisa hili la Pentekoste lasiku za baadaye, ambalo limempokea Roho Mtakatifuwaliyempokea hapo awali^ Kote kote katika nyakati, waowalimpokea Roho Mtakatifu, bali si kwa kipimo walicho Nayesasa; maana ni kurudishwa kwa ule wa kwanza.Tunapochukua kinara cha taa, Alfa na Omega, jinsiwalivyouwasha ule mshumaa wa kwanza: ulizidi kupanda nakupanda juu, kisha ukazidi kufifia, halafu ukarudi tena(mnaona?), wa kwanza na wa mwisho na kadhalika.

Sasa, bali katika wakati huu wa kanisa Ujumbeunamwagwa katika kanisa. Bali mwili wa kanisa, wenyewe,kwa jumla^Kama vile_maskani hii, tutasema; hapo ndipo

MAJINA YA MAKUFURU 19

yeye anapokuja kanisani kuabudu. Maskani hii si maskani yaRoho Mtakatifu. Hakuna kitu kama hicho. Watu binafsiwanaohudhuria kanisa hili ndio maskani ya Roho Mtakatifu.Hao ndio maskani iliyo na Roho Mtakatifu, bali si kanisakatika jamii ya kundi. Kwa hiyo Huyo anamwagika.

Lakini basi, mtu huyu aliyekuwa anamimina yale maji,yule mjumbe kwa kanisa, akiumwaga Ujumbe kanisani.^Bali yale maji yalikuwa yanafanya nini? Yalikuwayakichemsha taka zote zilizokuwa ndani yake. Hicho ndichoRoho Mtakatifu anachofanya: anazichemsha.

Sasa, sasa, asali iliwakilisha upendano wa ndugu, fadhiliza kindugu, ambao ni wakati huu. Ndiyo kwanza nimalizekuwaambia (mnaona?) juu ya fadhili za kindugu, wakatitunaoishi sasa.

Sasa, unaweza kusema, “Angalia, hakika si_si_simpendiNdugu Neville,” ama, “Kweli simpendi Ndugu Jones; simpendiNdugu Fulani,” na kitu kama hicho. Bali acha kitu fulanikimpate; ndugu, moyo wako unavunjika. Jambo hilo nusuralikuue. Unaona? Tunaweza kupata fadhili za kindugu nakuhurumiana. Mnaona? Bali kuzidumisha katika kundi lawatu^

Mbona unamjali ndugu huyo? Kwa sababu ulimega mkatepamoja naye hapa madhabahuni, kama utakavyofanya usikuwa leo; unashiriki pamoja naye; ulimpa mkono; unaabudupamoja naye. Yeye ni ndugu yako. Naye anaweza kufanyajambo fulani katika mwili ambalo usingekubaliana nalo, kwasababu kwa namna fulani unakaa (jambo ambalo halikupasikufanya lakini)_unajiepusha naye kidogo. Lakini katikakilindi cha moyo wako, kama kitu fulani kingelimpata huyondugu, nusura kingekuua, ama dada huyo.

Mimi_mimi ni mzee. Wakati mmoja nilikuwa kijana lakinisasa ni mzee. Nimeona jambo hilo likitukia kila wakati.Kuwasikia watu wakisema, “Vema, sitajishughulisha tu nayetena.” Na jambo fulani linampata mtu huyo, nusura limwue;anawaza, “Ee, Mungu, nimemwacha ndugu yangu mpendwaaondoke bila kupatana naye (unaona?) tena.” Unaona?Unaona, ni upendano wa ndugu. Unaonekana kama hutanata,bali unanata. Asali, inanata.

Sasa, kwa kuwa alitoka kule, akashuka kwenye kile kilimaakaenda chini ya kilima^ Sasa, maji haya yenye utukufuyalikuwa yakibubujika kutoka juu ya kile kilima katika vijitovitano. Sasa, tano ni namba ya neema: J-e-s-u-s, I-m-a-n-i,N-e-e-m-a. Mnaona? Tano ni namba ya neema. Vijito vitanovilikuwa vikitiririka kutoka hapa juu kwenye kihori nakutiririkia kupitia hapa. Na kila mmoja wa nyakati hiziulikuwa na huo mwamba wa kuungama. Watakatifu wanalala,wanaendelea kungoja, kungoja, kungoja, kungoja (mnaona?) na

20 LILE NENO LILILONENWA

kuendelea hata kwenye wakati huu, bali hivi karibuni RohoMtakatifu, akimwagwa kutoka kwa Kristo, atakuja na atalitiaKanisa muhuri, kisha Kanisa litanyakuliwa. Litakuwa kitukimoja kikamilifu cha Mungu, Bibi-arusi wa Kristo,atakayekuwa kichwa cha mambo yote. Mnanifuata sasa?

Sasa, alikuwa akishangaa^Sasa, katika ndoto yakealikuwa anashangaa, je! kijito hiki kidogo, kijito hiki kidogokitawahi kufika kule chini. Mnaona? Kilikuwa kinakauka.Sasa, kwa kuwa yeye mwenyewe^ Sasa hapa ndiponinapotaka mfikie sasa. Yeye mwenyewe alikuwa anashangaajuu ya nafsi yake. Je! alikuwa na Roho Mtakatifu?

Sasa, nilijiepusha na kusema jambo hili siku chachezilizopita, nikifikiria ya kwamba kanisa lingekuwa la kirohovya kutosha kulipata (na labda yanipasa kufunga kinasasautihiki sasa hivi, lakini_kwa sababu sitaki itoke iende miongonimwa ndugu); bali ungaliweza kunena kwa lugha, ungaliwezakupaza sauti, ungaliweza kucheza, ungaliweza kutoa pepo,kufanya lo lote utakalo, na bado usiwe na Roho Mtakatifu.

Je! hao wanafunzi hawakuja wakifurahi na kupigamakelele, kwa sababu pepo walikuwa wanawatii? NayeYesu^Moja kwa moja miongoni mwao alikuweko Yuda? Je!Yesu hakusema katika siku hiyo alipokuja, ya kwamba “Wengiwatakuja Kwangu na kusema, ‘Bwana, mimi sikutoa pepo nakatika Jina Lako nikafanya kazi kubwa,’ Nami nitasema,‘Ondokeni Kwangu, ninyi mtendao maovu, sikuwajua mimi.’”Mambo hayo si dalili ya Roho Mtakatifu. Kwa matunda yaomtawatambua.

Sasa, mnasema, “Ndugu Branham, hivi sisi_inatupasakunena kwa lugha?” Kweli, hizo ni karama za Mungu. Balikarama hizo za Mungu, bila ya sifa hizi ndani yake, hufanyajiwe la kujikwaa kwa asiyeamini. Mungu hakubali jambo hilo.Hizi hazina budi kutangulia. Na unapokuwa na imani, nguvu,maarifa, kiasi, saburi, utauwa, na upendano wa ndugu, ndipoRoho Mtakatifu anashuka na kukutia muhuri kama kitukimoja, sawasawa na anavyozitia muhuri nyakati za kanisakama kitu kimoja. Jinsi anavyomfanya Bibi-arusi Wake ndivyoanavyomfanya mtu Wake binafsi: anafanywa kwa vitu vile vile,kama vile Hawa alivyofanywa kutokana na Adamu, ubavukutoka ubavuni. Hivi hapa vitu ambavyo huna budi kuwanavyo kwanza. Huwezi kujifanya unazo; huwezi kuviigiza;havina budi kuwa vimetumwa na Mungu na kuzaliwa naMungu. Kuigiza kunasababisha tu kuchanganyikiwa.

Ni kama nilivyosema: Ungeweza kuwazia kumwonakipanga, akiketi pale na unyoya wa hua umechomekwakwenye mabawa yake, aseme, “Mnaona, mimi ni hua.” Yeye sihua, yeye ni kipanga, koho.

MAJINA YA MAKUFURU 21

Ungeweza kuwazia ndege mweusi akiwa na manyoya yatausi kwenye mabawa yake na kusema, “Unaona^?” Hichoni kitu alichokichomeka mle ndani. Bali haina budi kutokandani ije nje, na izae Ukristo. Mungu, kwa nguvu za RohoMtakatifu^

Dada yetu alikuwa amelowa miguu alipofika kule chini.Sisi sote tunamjua Dada Shepherd kuwa mwenye fadhili^Nyumba yake imefunguliwa. Yeye na Ndugu_sijali kama nimzururaji, mwombaji, ama ye yote yule, wao watamlisha,wafanye lo lote wawezalo kumsaidia. Loo, Mungu alikubalijambo hilo, sehemu yake ya msingi. Na hapa kuna^

Sasa, shika somo hili: Hili hapa kosa la_la^(Sipaswikufungulia kwa ajili ya jambo hili.) Kosa la Maskani yaBranham ndilo hili. Mnaona? Kuna namna mbili za imani;kuna namna mbili za nguvu, kama nilivyosema juzijuzi; ainambili mbalimbali za maarifa; aina mbili mbalimbali za kiasi.Mmoja anafikiri ni kukatazwa. Wao wana^Hicho sicho kiasiambacho Mungu anazungumzia habari zake. Ni hiyo hasiraisiyo ya kitauwa na isiyozuilika uliyo nayo, na mambo yaupande huo, hamaki kali, kuzozana.

Saburi, na kadhalika, kuna mwigo wake, kujifanya, imaniinayotokana na maumbile, nguvu zinazotokana na maumbile.Kuna kiasi kinachotokana na maumbile. Na mambo haya yotehutokana na maumbile.

Na sehemu kubwa sana ya imani yetu ni imani ya akili.Kwa kusikia Neno, sisi^kunatuleta kwenye kumtambuaMungu kiakili. Bali kama hii inatoka juu, loo ndugu, kamakamwe itaigusa hii, kuna imani ya kiungu, ya kiroho. Basi hiyoimani inafanya nini? Imani hiyo inatambua Neno peke yake.Haidhuru kitu kingine cho chote kinasema nini, inatambuaNeno peke yake, kwa maana Hapo mwanzo kulikuwako Neno,Naye Neno alikuwako kwa Mungu, Naye Neno alikuwa Mungu.(Naye Neno angali Mungu.) Naye Neno alifanyika mwili,akakaa kwetu^ Na wakati Neno lenyewe linapomiminikakatika imani yetu, imani yetu ya akili inakuwa ufunuo wakiroho^ “Na juu ya msingi huu nitalijenga Kanisa Langu,”mnaona, si juu ya dhana ya akili ya kujiunga na kanisa, dhanaya akili ya jambo hilo, bali juu ya ufunuo. Wakati hivyo vijitovya neema vinamiminika ndani ya imani hiyo ya akili uliyonayo, halafu juu ya huu, ufunuo wa kiroho, “NitalijengaKanisa Langu na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda.”Mnaona? Hiyo inaonyesha italipinga, bali haitashinda. Loo, nijambo tukufu jinsi gani.

Sasa, mnaona, imani, mito hii mitano^ Nilikuwa nakipande cha choki hapa, bali nafikiri hakukileta. Bali hivivijito vitano mnavyoona vikishuka kupitia hapavinaichanganya hii pamoja. Imekuwa ni Roho Mtakatifu

22 LILE NENO LILILONENWA

aliyelifanya kanisa la Efeso. Roho Mtakatifu ndiye aliyelioshakanisa la Smirna. Roho Mtakatifu ndiye aliyelitoa kanisa laPergamo na kanisa la Thiatira katika zile Nyakati za Giza.Roho Mtakatifu ndiye aliyemjenga Bibi-arusi huyo, yuleMteule ambaye ametoka kwenye taratibu zote za madhehebukote kote katika nyakati namna hiyo. Na kuna Bibi-arusi waYesu Kristo aliyeteuliwa na kuchaguliwa tangu zamani,ambaye Roho Mtakatifu amemwita atoke, yule Mteule. Naimekuwa ni Roho Mtakatifu katika wakati huu, wakati ule,wakati ule, ule, ule, ule, ule, ule na kuendelea hata juu; RohoMtakatifu.

Basi sasa, kama vile katika watu binafsi, wema huu nakadhalika vina_(maarifa na kiasi)_vinatiwa kwenye imaniyetu, ndipo Jiwe la Kileleni linapokuja, Roho Mtakatifuanavishikamanisha pamoja. Huo ndio Ubatizo wa RohoMtakatifu. Hiyo ndiyo sababu ni haba sana leo.

Hebu nione hapa. Nina vifungu vilivyoandikwa hapa chini.Hebu tuone. Nilikuwa na picha iliyochorwa hapa ku_kwa ajiliya ndoto yake. Mnaona? Hamwezi kuiona kutoka huko.

Sasa, kikitoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini kinachokuja?Ndipo atakupa imani ya kimbinguni, imani ya kiroho, hii hapachini. Ndipo imani hiyo ya kiroho hutambua tu Neno pekeyake. Haidhuru mtu mwingine ye yote anasema nini, hai_haifai kitu. Hiyo inajua Neno tu. Kama mtu fulani akisema,“Siku za miujiza zimepita,” imani hiyo inajua Neno peke yake.

Mtu fulani anasema, “Hakuna kitu kama ubatizo wa RohoMtakatifu.” Imani hiyo inajua Neno peke yake. Hiyo ndiyoimani halisi ya kiroho. Mnaona? Hiyo ni kweli. Mnaona? Inajuatu Neno.

Halafu, hiyo ilikuwa namba moja. Namba moja, ikijakwako, imani yako ya akili, papa hapa, anakuja RohoMtakatifu, akishuka na kuingia katika imani yako ya akiliakiifanya ya kiroho. Ndipo hiyo imani ya kiroho hukubaliNeno peke yake.

Sasa, na namba mbili_tatu: Ndipo utakuwa na ya kiroho,utakuwa_utampata Roho Mtakatifu, na atavitia muhuri vituhivi vyote ndani yako, wakati Roho Mtakatifu anapoifunikahii. Kutoka kwenye imani yako hadi kwa Roho Mtakatifuanakutia muhuri ndani pamoja na Kristo; ndipo mnakuwammoja. Amina! (Ondoa kitu hiki mbele yangu. Ni kizitokwenye mikono yako.) Mnakuwa mmoja. Mnaona, wewe naKristo mnaishi pamoja. “Katika siku hiyo mtajua ya kwambaMimi niko ndani ya Baba, Baba ndani Yangu, Mimi ndaniyenu, nanyi ndani Yangu.” Mnaona? Ndipo hicho ni kitukimoja kilichotiwa muhuri cha Bwana Mungu. Sasa, halafuvinathibitishwa na kuwekwa. Hapo wakati huo unapowadia,wao wanakuwa wana na binti za Mungu waliothibitishwa.

MAJINA YA MAKUFURU 23

Mnakumbuka katika Kitabu cha Mathayo, sura ya 17, ayaya kwanza hadi ya 5, Yesu kwenye ule Mlima wa Kugeuzwa?Mmenisikia mimi^Msikieni Yeye, huo ujumbe ambao ndiyokwanza, hapa yapata mwaka mmoja uliopita, nikahubiri huoukapendwa sana na watu, Msikieni Yeye. Kufanywa mwanamwenye mamlaka katika Waefeso 1:5 pia: “Munguametuchagua tangu zamani tufanywe wana wenye mamlaka.”

Mnaona, familia^Mwana anapozaliwa kwake, ni mwanawakati huo. Bali huyo mwana alikuwa na waalimu wa kumlea.Na iwapo huyo mwana hakufanyika_hakufanyika mwana wanamna iliyo halisi, hakufanywa mrithi kamwe. Bali kamaalikuwa mwana halisi, na mwana ambaye angemtii babaye,basi huyo mwana alifanywa mwana mwenye mamlaka amaakawekwa mahali pake. Anakuwa mrithi wa kile alichokuwanacho babaye.

Na hivyo ndivyo Mungu alivyokuwa akifanya kwenyeMlima wa Kugeuzwa. Wakati alipomchukua MwanaweMwenyewe, baada ya kuthibitishwa kuwa Mwana halisi(mnaona?), na alikuwa amestahimili majaribu yote, Yeyealimpandisha kwenye Mlima wa Kugeuzwa kisha akamtiauvuli.

Mnajua, katika Agano la Kale walimchukua mwana,wakamvalisha mavazi mazuri na ya kupendeza, kishawakamweka mbele ya hadhara. Nao walikuwa na sherehe zakumweka mahali pake, ama tunaziita kufanywa mwanamwenye mamlaka. Katika Wagalatia pale, kwa namna fulanininafikiri Paulo anakuita kufanywa wana wenye mamlaka.

Naam, kwa kumweka mwana^Wahudumu watafahamu,na wasomaji wa kiroho wa Biblia, ku_kumweka huyu mwanamahali pake. Kwa maneno mengine, huyo mwana alikuwamwana alipozaliwa.

Hapo ndipo watu wetu wa Kipentekoste walifanya kosalao. Kuzaliwa katika familia na Roho Mtakatifu, hiyo ni kweli,lakini basi hatuna budi tuwe wana halisi, waliofunzwa namwalimu afaaye. Mnaona?

Sasa, kama mtu huko nyuma katika nyakati za kalealimpenda mwanawe, naye alimtaka awe mwana halisi,alitafuta mwalimu mzuri sana aliyeweza kumpata, mwalimumzuri kuliko wote; maana alitaka mwanawe akue awe kamababaye. Mnaona? Kwa hiyo akamchukua mwalimu afaaye.

Naam, kama mtu duniani angefikiria juu ya mwalimu aliyebora sana, na Mungu je! Baba yetu? Sasa, Yeye hakuwachukuamaaskofu, na makadinali, na makasisi; Yeye alimchukua RohoMtakatifu kuwa Mwalimu wetu. Naye Roho Mtakatifu ndiyeMwalimu wetu. Naye yu_yuko Kanisani, Naye humpelekeaBaba ujumbe.

24 LILE NENO LILILONENWA

Halafu, vipi kama baba_yule mwalimu alikuja akasema,“Vema, Baba^” Naam, Yeye hataenda na kuchukua namnafulani ya mwalimu ambaye anataka jani kavu kwenye kofiayake, mwajua, unyoya, kama tusemavyo; aseme, “Loo, kamanikimwambia Baba kitu fulani kuhusu^Maskini mvulanahuyo ni mtukutu kwa vyo vyote, lakini kama mimi_kamanikimwambia Baba, huenda Baba akanipandisha cheo.” Huyosi mwalimu anayefaa. Mwalimu afaaye ni mwaminifu, husemakweli. Naye Roho Mtakatifu hunena kweli anapokuja mbele zaMungu, kwetu. Naam.

Kwa hiyo Yeye huja. Unafikiri nini? Yeye angekunja usoleo kusema, “Binti Zako wote wanakata nywele zao, Naweuliwaambia wasifanye hivyo. Wanao wana mawazo yakimadhehebu sana hata tu hawawezi kufahamiana, na hiyoni^ Nao wanachukua hiki badala ya kile na hiki badala yakile.” Jinsi hana budi kukunja uso. Bali jinsi huyo Mwalimuangependa kuja na kusema, “Loo, jamani! Huyo mwana nimwana halisi. Yeye ni kama Baba Yake kabisa.” Loo, jinsiangependa kusema jambo hilo. Mnaona?

Ndipo Baba anajaa fahari na kusema, “Huyu nimwanangu.”

Hivyo ndivyo Mungu alivyofanya hasa kwenye Mlima waKugeuzwa. Unatambua palitokea Musa na Eliya. Naye Petro,akiwa ameshtushwa sana, ya kimbinguni yalikuwayamefanywa, kile^Petro ameshtuka; akasema, “Na tujengevibanda vitatu: kimoja Chako, na kimoja cha Musa, na chaEliya.”

Alipokuwa katika kusema, Mungu akamnyamazisha.Akasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa Wanguninayependezwa Naye. Msikieni Yeye.” Mnaona? Mungualijiweka mwenyewe kule nyuma na, “Huyu ni Mwanangu.”

Musa aliwakilisha torati. Manabii waliwakilisha hakiYake. Tusingeweza kuishi kwa torati Yake. Tusingewezakuishi kwa haki Yake. Siombi haki; nataka rehema, si haki.Mimi siwezi kuweka sheria Yake, wala siwezi kutimiza hakiYake; bali nahitaji rehema Yake. Naye Mungu alisema sheriana haki vimetimizwa katika Yeye. “Yeye ni Mwanangumpendwa Wangu. Msikieni Yeye. Huyo Ndiye, huyo NdiyeMwenyewe.”

Basi, katika Agano la Kale wakati huyo mwanaalipofanywa mwana mwenye mamlaka ama kuwekwa mahalipake katika familia, jina lake lilifaa vile vile kwenye hundikama la baba yake lilivyofaa. Naam, bwana! Hawakuwa na^Walikuwa na pete katika siku hizo, i_ishara, muhuri; naowangeitemea mate [Ndugu Branham anafanya sauti ya kutemamate kisha anapiga mimbara kwa ngumi yake_Mh.], wanaitia.

MAJINA YA MAKUFURU 25

Hiyo ilikuwa muhuri. Hiyo ilikuwa tu^Yeye alivaa pete yababaye, muhuri ya_yake; na hiyo ilikuwa bora tu kama yababa yake.

Basi, baada ya Yesu kuwa mtiifu, Yesu kwa Mungu, Mungualimweka mahali Pake: “Huyu Ndiye.”

Naam, wakati mshiriki amezaliwa na Roho Mtakatifukatika familia ya Mungu naye amethibitishwa kuwa na sifahizi ndani yake, kwamba Mungu anaweza kuona nguvu,maarifa, kiasi, saburi, fadhili za kindugu, na utauwa ndaniyake, basi Mungu humtia muhuri ama anamweka mahali pake.Basi hapo, hapo ndipo unapowaona wana na binti za Mungu.

Halafu Waefeso 4:30 inasema, Msimhuzunishe yule RohoMtakatifu wa Mungu, ambaye kwa yeye mlitiwa muhurimpaka siku ya ukombozi wenu. Naam, baadhi yenu Wabatistimnaotaka kwenda hata kwenye usalama wa milele, naam,kama mtafikia kiwango hicho, nitasimama pamoja nanyikwamba ni usalama wa milele, kama mtafikia mahali hapo.Bali kusema tu, mtu ye yote anasema, “Nitaenda kujiunga nakanisa la Kibatisti”; “Mimi ni Mpresbiteri”; “Nina usalama wamilele”; hilo ni kosa. Maisha yako mwenyewe yanathibitishaya kwamba huna. Mpaka HIZI ziwemo na Mungu amekufanyamwana na amekutia muhuri kwa Roho Mtakatifu ukaingiakatika ufalme Wake^ Basi hakuna kutoka ndani yake. Weweni salama milele.” “Aminini_Msimhuzunishe Roho Mtakatifuwa Mungu, ambaye kwa yeye ninyi nyote na sifa zenu zakitauwa mmetiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

Ninaamini kuna Bibi-arusi aliyechaguliwa tangu zamani.Ninaamini Mungu alisema Yeye angekuwa na Kanisa lisilo nawaa wala kunyazi. Ninaamini katika kuchaguliwa tanguzamani: ya kwamba Bibi-arusi amechaguliwa tangu zamani;Yeye hana budi kuwepo. Ninatumaini niko pamoja Naye. Hiyoni^Mnaona? Niko pamoja Naye. Sasa, ni juu yangu kutimizawokovu wangu na Mungu mpaka mambo haya yamekubaliwana Mungu halafu yakatiwa muhuri katika Ufalme wa Mungu.Huyo hapo Roho Mtakatifu. Hizo hapo kazi halisi za Mungu.Imetiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

Hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake. Nilifikiri ilikuwa nzuri.

Sasa, basi, wakati Hilo linapofanya hivyo, wakati Kanisahilo litakapofikia mahali hapa, ama huyo mtu binafsi^Kanisa litakuwepo. Hebu niliseme vizuri sana kusudi mlipate:Kanisa limechaguliwa tangu zamani kuwepo. Nataka kuwapamoja Nalo, bali njia pekee nitakayokuwa pamoja Nalo, nikuwa sehemu Yake.

Ninakuwaje sehemu Yake? Kwa kuwa ndani Yake.Ninaingiaje ndani Yake? Kwa ubatizo, kwa Roho mmoja. IWakorintho 12: “Kwa Roho Mmoja sote tumebatizwa kuwaMwili mmoja,” Mwili mmoja, tumebatizwa ndani Yake.

26 LILE NENO LILILONENWA

Bali huwezi kuvishikamanisha vitu hivi vidogo, useme,“Nilinena kwa lugha. Nimempata Huyo.” Unatoka unaendahapa nje, nawe una hasira, na unaapa, na kufanya yasiyofaa(mnaona?), huko ni kutia manyoya ya tausi kwenye_kwenyendege mwenye milio. Mnaona? Huwezi kufanya jambo hilo.Maisha yako mwenyewe yanathibitisha ya kwamba sivyoilivyo. Bali wakati vitu hivi vinafanya kazi ndani yako kwanjia ya Mungu, basi umetiwa muhuri. Ndipo basi hakuna kuigakuhusu hilo. Wewe ni wewe tu. Hapo ndipo maono, kazikamilifu za Roho Mtakatifu wa Mungu, kila kitukinadhihirishwa. Kwa sababu gani? Wewe na Kristo mnakuwammoja (natumaini jambo hilo linaeleweka), wewe na Kristomnakuwa mmoja.

Nilikuwa na kitu kingine nilichokuwa nimeandika hapanilichotaka kuwazia. Anatuleta kwenye mahali pa Uzima,ndipo unakuwa_unakuwa na Uzima wa Milele.

Sasa, nina Kamusi ya Kiyunani hapa, The EmphanticDiaglott. Nilisoma juzijuzi juu ya neno fulani.

Naam, katika Yohana 14_ama Yohana 3:16, tunaonamahali pamoja panasema, “yuna Uzima wa kudumu daima”;mahali pengine panasema, “yuna Uzima wa Milele.” Balikatika_katika tafsiri ya Kiyunani, katika Kiebrania inasema,“Uzima usio na mwisho.” Katika neno la Kiyunani, yunaA-i-n-i-o-a-n^Karibu kama “aeon.” Aeon ni wakati ambaohauwezi^Ni hesabu isiyoweza kuhesabiwa. Imepitamamilioni, matrilioni, mabilioni. Bali huu ni aionion yawakati: Uzima wa Milele. Na neno la Kiingereza kwalo nimilele dawamu. Tunalijua kama milele, Aionion ama Uzimausio na mwisho. Mnaona?

Na iwapo una Uzima usio na mwisho, unawezajekuangamia? Umekuwa sehemu ya Milele, na kuna kitu kimojatu cha milele. Shetani si wa milele. La! Yeye_yeye alifanyikaShetani. Kuzimu si kwa milele. Kuzimu kuliumbwa; si kwamilele. Na miili hii si ya milele; iliumbwa. Bali Roho waMungu ni wa Milele. Hakuwa na mwanzo, wala hana mwisho.Na njia pekee tunayoweza kuwa na Uzima wa Milele(kutokana na neno hilo la Kiyunani Zoe, ambalo maana yakeni “uzima wa Mungu Mwenyewe”), tuna_tunakuwa sehemu yaMungu tunapokuwa wana na binti za Mungu nasi tuna Uzimawa Aionion. Kwa hiyo sehemu inayoishi, sisi, ambayoinatambua Neno hili kutoka hapa mpaka pale, inayotambua,ni Uzima wa Aionion, Uzima usio na mwisho. Ni Uzima waMungu Mwenyewe ndani yetu. Amina. Whiu.

Juzijuzi, kwenye safari, nilikuwa na mazungumzo; Shahidiwa Yehova. Sasa, si kutoijali imani ya mtu ye yote. Tunawaongofu wengi sana wanaoketi hapa kutoka kwa Shahidi waYehova. Mmoja wa wadhamini wetu wa kanisa ni Shahidi wa

MAJINA YA MAKUFURU 27

Yehova_alikuwa, kisha akaokoka, yeye na jamaa yake. Babayake alikuwa msomaji, Ndugu Wooods na hao wengine. Nduguzake wote na dada zake sasa, karibu wote wameingia nakumpokea Roho Mtakatifu, kwa sababu ya maono ya Munguyakiwaambia yale waliyofanya na yale wao^Mnaona? Hilolilisababisha jambo hilo.

Sasa, bali hapa Shahidi wa Yehova katika kitabu chao,kinasema ya kwamba pumzi unayovuta ndiyo nafsi. Sasa, hiyohaiwezi kuwa sahihi. Pumzi unayovuta siyo nafsi. Kama ndiyo,wewe ni_wewe ni nii^Wakati mmoja wewe ni nafsi yanamna fulani; wakati mwingine wewe ni ninii^Mtumwingine amevuta nafsi hiyo. Angalia mahali ungalikuwa.Sasa, ile pumzi ni upepo, nao upepo ndio unaovuta ndani yatundu la pua yako.

Sasa, wao wanachukua Andiko kutoka kule nyuma, “KishaMungu akapulizia pumzi ya uhai katika pua yake, naye akawanafsi iliyo hai.” Sasa, nataka kuwaulizeni jambo fulani. Kamaalikuwa mtu, alikuwa akipuliza pumzi ya namna gani kablaMungu hajampulizia ndani mwake pumzi hii ya uhai? Mnaona?Ni pumzi ya namna gani^Yeye alikuwa mtu anayepumua,mtu anayeishi. Vema basi, kama hivyo ndivyo ilivyo, basi kilamnyama ni nafsi iliyo hai, maana wao wanavuta nafsi yabinadamu, na nafsi yetu, na vyote pamoja. Basi isingalimpasaYesu kufa; kafara ya mnyama ingalikuwa imetosha. Mnaona?Kwa hiyo, ndugu, hiyo hoja haiji.

Lakini alivyofanya Mungu, Yeye alimpulizia pumzi yaUzima wa Milele (Amina!), ndipo akawa nafsi iliyo hai, nafsiisiyoweza kufa. Sasa angalia sasa. Tutaingia kwenye asalimoja kwa moja hadi kwenye viko vya mikono yenu. Angalia,akampulizia pumzi ya Uzima wa Milele puani mwake. Nayeakawa nafsi ya milele, maana Mungu alipulizia (si kilemaumbile yalifanya, bali aliyofanya Mungu)_ akapuliziapumzi ya uhai puani mwake, naye akawa nafsi iliyo hai.

Halafu unaniambia mimi, “Adamu alikufa, NduguBranham.” Lakini kumbuka, kabla Adamu hajakufa alikuwana mwana-kondoo aliyemkomboa. Haleluya! Wale aliowajuatangu zamani aliwaita. Alimchukua mwana-kondoo apatekuwakomboa.

Yeye alikuwa ni mfano. Adamu alianguka. Kisha mwana-kondoo akatolewa kwa ajili ya Adamu, kwa sababu tayarikatika pua yake kumekuwa na pumzi ya Mungu wa Milele;naye akawa nafsi iliyo hai. Yeye alikuwa mwana wa Mungu. Sipumzi yake, kama lile neno la Kiafrika (sijui neno lake laKiyunani ni lipi sasa hivi, lakini^)_neno la Kiafrika waowanaiita Amoyah, ambalo maana yake ni “upepo, nguvuisiyoonekana.” Wanyama wanavuta Amoyah. Wenye dhambiwanavuta Amoyah.

28 LILE NENO LILILONENWA

Basi kwa nini sisi imetupasa kujitahidi kupata Uzima waMilele kama hiyo ndiyo nafsi ya milele iliyopuliziwa ndaniyetu kwa pumzi. Kwa nini imetupasa kujitahidi kwa ajili yaUzima wa Milele? Inapingana, ndugu. Mnaona? Ha_haiwezikufanya hivyo kamwe. Bali Mungu hasa, juu ya Adamu,alipumua pumzi ya Uzima wa Milele, naye akawa mtu wamilele pamoja na Mungu. Alikuwa na nguvu kama Mungu:alikuwa mungu aliye mdogo. Alikuwa mungu wa dunia, siMungu wa Mbinguni sasa, mungu wa dunia.

Na siku moja wana wa Mungu watakuwa miungu tena.Yesu alisema hivyo: “Je! haikuandikwa katika torati yenu,‘Ndinyi miungu’? Basi kama mnaweza kuwaita wale Yeyealiowaita miungu, ambao Mungu aliwazuru, mnawezajekunihukumu Mimi, kusema, ninaposema Mimi ni Mwana waMungu?” Mnaona? Naam, tunaingia kwenye kitu fulani chenyekilindi. Sasa, angalieni jambo hili tunapolifafanua.

Naam, hawa hapa. Yeye sasa ni mwana wa Mungu, balianafanya kosa. Yeye anajua anafanya kosa. Sasa kumbuka,Adamu hakudanganywa. Biblia ilisema hivyo: ITimotheo 3:“Adamu hakudanganywa, bali mwanamke ali_alidanganywa,alikuwa makosani.” Adamu alikwenda pamoja na Hawa, kwamaana alikuwa mkewe. Vivyo hivyo na Kristo,hakudanganywa na Shetani, bali aliingia katika mauti pamojana Bibi-arusi. Yeye alienda kuwa pamoja na Bibi-arusi, apatekulikomboa Kanisa.

Adamu alijua alikuwa amekosea, kwa hiyo alitoka tuakaenda pamoja na Hawa. Mnaona? Bali kulikuweko namwana-kondoo aliyetolewa kwa ajili yao, kwambawalikombolewa. Na hawa wana-kondoo leo, ambaowalijulikana tangu zamani na Mungu na Mungu amewaita,kuna Mkombozi. “Hakuna mtu awezaye kuja Kwanguasipovutwa na Baba Yangu; na wote alionipa Baba watakujaKwangu.” Hiyo ni kweli?

Kwa hiyo kuna Mwana-Kondoo aliyetolewa tangukuwekwa misingi ya dunia, ambapo majina yao yamewekwakwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Mwana-Kondoo alitolewa kufanya njia ya neema kusudi kila mmojawao apate kufufuliwa. Mwana-kondoo aliyetolewa, mwana-kondoo wa Adamu.

Sasa angalia, kama vile Adamu alivyokuwa na mwana-kondoo aliyetolewa. Sasa, ndivyo na Kanisa leo. Simaanishika_kanisa. Mnajua nini? Sisemi kwa kukufuru, wala sitakilimuudhi mtu ye yote. Mimi siko hapa kufanya jambo hilo,maana tayari nimejieleza mwenyewe; niko hapa kusaidia. Balikile ninachojaribu kufanya^Mnajua nini? Kwa kwelimakanisa haya si Makanisa. Kuna Kanisa moja tu. Haya nimaloji (mnaona?); ni maloji. Sina kitu^Ni sawa, lakini

MAJINA YA MAKUFURU 29

na_nataka kuwathibitishia jambo hilo mnamo dakika chache,ya kwamba hayo ni maloji. Wewe ni mfuasi wa loji laMethodisti, loji la Wapresbiteri, ama loji la Wapentekoste,kulingana na jambo hilo, hiyo ni^Mnaona? Maloji! Mnaona?Hamwezi^Mnaona, makanisa kweli ni maloji ambamo watuwalio na wazo lile lile wanachukuliwa pamoja. Bali Kanisa nimoja. Nawe huwezi kujiunga na Kanisa; unazaliwa ndaniYake. Na unapozaliwa ndani Yake, wewe ni mshiriki Wake.

Ni kama tu jamaa yangu. Nimekuwa katika jamaa yaBranham kwa miaka hamsini na mitatu; wao kamwehawakuniomba nijiunge na hiyo jamaa. Kwa nini? Sina hajana kujiunga na hiyo jamaa. Nilizaliwa Mbranham. Naweunazaliwa katika Kanisa. Sasa, haya mengine ni maloji.Uliwahi kuwazia jambo hilo? Naam, bwana!.

Siku moja nilikuwa ninakata nyasi, nami nilikuwanikiwazia juu ya, vema, kanisa kuu takatifu la Katoliki,wanavyoliita. Nilikuwa nikiendelea namna hiyo, nikikatanyasi, na kitu fulani kikanisimamisha wima kabisa, kasema,“Usiliite hilo namna hiyo.” Nami nikaangalia kila upande.Nikaanza kuendelea kukata nyasi, na kikanisimamisha tena,kasema, “Usiyaite namna hiyo.” Kasema, “Hayo ni malojikama mengine. Wao si Kanisa. Kuna Kanisa moja.” Mnaona?Wao ni wafuasi wa loji, maana unaweza kujiunga na loji, balihuwezi kujiunga na lile Kanisa. Lile Kanisa, unazaliwa ndaniYake. Unakuwa mshiriki Wake kwa kuzaliwa upya, halafummoja wa ile jamaa, ndugu au dada ndani Yake.

Naam, hebu niwasomee kutoka kwenye Emphatic Diaglotthapa kitu fulani, kwenye Ufunuo 17:3, katika Ufunuo waEmphatic Diaglott hapa, nanyi angalieni tu jambo hili, jinsihili linavyosema na jinsi_jinsi linavyolingana vizuri na jambohilo: Ufunuo 16-17. Vema! Sasa, hebu tusome hapa kwa mudakidogo tu. Sikilizeni jambo hili kwa makini sana. Ufunuo 17:3:

Na mmoja wa hao Malaika saba wenye^vitasasaba akaja na kusema nami,^ (Ninawasomea kutokakwenye kamusi.)^akiwa, “Njoo, nitakuonyeshahukumu ya kahaba huyo mkuu, aketiye juu ya majimengi;^ (Nasi sote tunajua huyo ni Vatican.)

Hapa tuna Our Sunday Visitor kule ndani kutoka kwenyekanisa Katoliki, likituambia hiyo ni nini hasa. Mnaona? Najibu hili kwake lilisema, “Lakini ngoja kidogo.” Kasema,“Kumekuwako na majina ya kila namna,” kasema, “ambayoyangefanya nambari 666.”

Nikasema, “Lakini ngoja kidogo!”

Kasema, “Jina lako lingefanya mia sita, siti_”

Lakini nikasema, “Mimi siketi juu ya milima sabanikiutawala ulimwengu hata hivyo.” Mnaona? Mnaona, hiyo nikweli. Mnaona?

30 LILE NENO LILILONENWA

“^kuonyesha^hukumu ya yule kahaba mkuu,aketiye juu ya maji mengi;^ (Maji, Ufunuo 17:15, niwingi na umati wa watu. Mnaona?) ambaye wafalmewa nchi wamezini naye, nao wakaao juu ya nchiwamelevywa kwa mvinyo ya_ya uasherati wake.”^(Sasa angalia.)

Akaniongoza, katika Roho, hata jangwani;^(Emphatic Diaglott sasa. Mnaona?)^nikaonamwanamke ameketi juu ya mnyama aliyevikwa nguonyekundu sana, amejaa majina ya makufuru,^

Naam, katika ile ya Mfalme James inasema,^amejaamajina ya kukufuru. (Hebu kidogo. Naam, nitalipata hapamuda kidogo tu. Ufunuo aya ya 3.) Vema, hii hapa. Vema,Ufunuo, nilimaanisha 17, si 7, 17. Sasa isikilizeni aya ya tatu:

Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaonamwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana,mwenye kujaa majina ya kukufuru,^

Hivyo ndivyo Kiingereza kinasema, bali kiyunani asilikutoka kwenye The Diaglott kinasema hivi katika Ufunuo 17:3.Sasa sikilizeni.

Akaniongoza, katika yule Roho, hata jangwani;nikaona mwanamke ameketi juu ya mnyamamwekundu sana, mwenye kujaa majina yamakufuru,^

Hiyo ni tofauti sana, kutoka kwenye “majina ya kukufuru”hata kwenye “majina ya makufuru.” Ni nini?

Nasi_na sasa, yeye alikuwa mama wa makahaba. Sotetunajua jambo hilo. Sasa, ni nini? Haikubidi kuwa^Vema,hiyo ni kweli. Hilo lingechukua kanisa Katoliki la Kirumi, balilimejaa majina ya makufuru: Methodisti, Batisti, Presbiteri,Luteri, na yote, yanayojiita makanisa ya Mungu_majina yamakufuru. Tofauti kubwa kati ya “majina ya kukufuru” na“majina ya makufuru.” Wanajiita wenyewe Kanisa la Munguna kujianika wenyewe mbele ya ulimwengu, na karamu zakadi, na kunywa pombe na kufanya yasiyofaa, na supu zajioni, na cho chote kile, na upuuzi wa kila namna hata^Kuna Kanisa moja tu. Unazaliwa ndani Yake. Huingii mle,mpaka umesafishwa katika Damu ya Mwana-Kondoo nakutiwa muhuri na Roho Mtakatifu.

Ni tofauti jinsi gani kati ya “majina ya kukufuru” na“majina ya makufuru.” Mnalipata? Nililipata hilo asubuhi yaleo nilipokuwa nikisoma hapa kule_niliposhuka. Kitu fulanikikaniambia tu, “Nenda katika chumba chako; chukua TheDiaglott.” La, ni utii tu, hivyo tu. Nikaingia, nikafunguaUfunuo 17. Nikawaza, “Kwa nini unanitaka nisome hili?”Nami nikaanza kusoma. Mara nilipolifikia hilo, “Hilo hapo.”Nikachukua penseli nikaandika. Nikasema, “Hilo hapo.”

MAJINA YA MAKUFURU 31

Sasa, wao wanapiga makelele juu ya mimi kuyapingamadhehebu. Ni majina hayo ya makufuru yanayojiitaMakanisa ya Mungu, na Makanisa ya Kristo, na makanisa yaMethodisti, na makanisa ya^ Ni maloji, si makanisa. Kanisamoja, ambalo ni Kanisa la Bwana Yesu Kristo. Basi ni Lipi?Mwili wa kisiri wa Yesu Kristo ukitenda kazi duniani,uliofanywa kwa mfuasi wa yo yote ya makusanyiko haya,ambaye angekuwa mshiriki wa Mwili wa Kristo. Huna budikuzaliwa ndani Yake; si kujiunga Nalo. Na ku_kujiunga Naloni majina ya makufuru.

Mwanamke huyu, mwanamke huyu, nguvu zake^ Nanyimnaona hivi sasa mahali watakapowapeleka watu wote waliona mawazo tofauti juu ya dini na kuwapeleka Alaska. Mmeonahayo. Imani zetu zote tofauti^ Na kile_ni kitu gani? LileBaraza, Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Na Katoliki inashughuli zao kubwa zinazoendelea kule Vatican sasa, kuleambako wanajaribu^ Na maaskofu hawa wote na kadhalika,wao wanajaribu kufikia mapatano kuupinga ukomunisti,ulimwengu ukiupinga ukomunisti na huku unaungana tu naUkatoliki.

Na ni kama tu vile ilivyo leo: sisi hapa, kama nilivyosema,tuna-^Dhahabu^Karibu tumefilisika. Tunakopa,tunatumia fedha sasa katika kodi zitakazolipwa miakakumi na minne tangu sasa. Hivyo ndivyo tulivyokwisha. Ninani aliye na pesa za ulimwengu? Kanisa Katoliki.Zingekopeshwaje Marekani? Kuhifadhi makampuni haya yatumbaku na wiski na kadhalika. Hakika wao watazikopakutoka kwa^Watakapofanya hivyo, wao watauza haki yaoya mzaliwa wa kwanza moja kwa moja kwa kanisa Katoliki laKirumi. Tutaungana. Tazama jambo hili lililo dhahiri vivyohivyo, dhahiri kuliko kusoma gazeti; hili hapa. Mnaona?

Wao ni Wamethodisti, Batisti, Presbiteri, na kadhalika,wakijiita kanisa la Mungu. Katoliki, na upuuzi wote wa namnahiyo, ni nguvu za mnyama huyu mwenye kujaa majina yamakufuru. Ukijiita mwenyewe, “Mimi_mimi ni^”

Nilisema^Nilienda hospitalini hapa si muda mrefuuliopita, nilikuwa nikienda kumwombea mtu fulani.Nikasema, “Tuta-^”Ilikuwa ni mama yangu. Nikasema,“Tutamwombea Mama.”

Ndipo huyo bibi akasema, “Fungeni pazia hiyo.”

Nikasema, “Hivi wewe si ni Mkristo?”

Akasema, “Sisi ni Wamethodisti.”

Nikasema, “Asante. Nilifikiri labda wewe ni muumini.”Nami nikafunga pazia karibu nami basi. Mnaona? Kwa hiyokama Wewe si Mkristo hilo ni jambo lingine (mnaona?), lakini“Sisi ni Wamethodisti.” Hiyo ni kukufuru!

32 LILE NENO LILILONENWA

Yule mnyama, makanisa, yanayojiita makanisa, hayo simakanisa. Hebu nihakikishe jambo hilo liko kwenyekumbukumbu. Hayo si makanisa; ni maloji. Watu wanajiunganayo, bali huwezi kujiunga na Kanisa la Mungu aliye Hai.Unazaliwa ndani Yake kwa Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Naunapobatizwa na Roho Mtakatifu, sifa hizi zinatiwa muhurindani yako na Roho Mtakatifu; na kwa hiyo, “Yeye aliyezaliwana Mungu hatendi dhambi.” Hawezi. Haya basi. Loo, jamani!Tungeweza kuzungumza mchana kutwa, sivyo?

Kanisa ni Mwili wa kisiri wa Kristo, uliozaliwa kwa pumziya Mungu. Mlilifahamu jambo hilo? Kanisa la Mungulimezaliwa kwa pumzi ya Mungu. Mungu alipulizia kiroho,pumzi puani, mwa Adamu, akawa nafsi iliyo hai. MlijuaWapentekoste, ama Kanisa la kweli la Kipentekostelimezaliwa kwa pumzi ya Mungu? Hebu niwasomeeni jambofulani kwa muda kidogo tu, juu ya jambo hilo tu. Hebu nionekidogo tu. Yohana Mt., ninaamini, ninakoelekea, nasi tutaonakama kanisa la Mungu ndivyo lilivyo ama sivyo lilivyo. YohanaMt.^Hebu tuone, naamini hiyo ni kwenye 16, 19, 20. Vema.Hapa, naamini tutalipata papa hapa. Vema. Hebu niwasomeenimwone kama Kanisa limezaliwa kwa pumzi ya Mungu au la,kama Adamu alivyokuwa hapo mwanzo. Angalia.

Na ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, palewalipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwahofu ya Wayahudi; Yesu akaja, akasimama katikatiyao, akawaambia, Amani iwe kwenu.

Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mkonowake na ubavu wake. Waka_Basi wale wanafunziwakafurahi walipomwona Bwana.

Naye Yesu_Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwekwenu; kama Baba alivyonituma mimi,^ naminawapeleka ninyi.

Angalia! Baba aliyempeleka aliingia ndani Yake. NayeYesu, anapomtuma mwanafunzi, Yeye huingia ndani yake, mtuyule yule aliyetumwa!^

Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akasema,Pokeeni Roho Mtakatifu^(Kanisa lililozaliwa kwapumzi ya Mungu.)

Wakati kimo hiki kimejifinyanga chenyewe pale katika ilehali, pumzi ya Mungu inapopuliziwa, wanampokea RohoMtakatifu. Ndipo wewe ni mwana wa Mungu. Unawezakujiunga na cho chote unachotaka, bali umezaliwa katikaKa_Kanisa la Mungu Aliye Hai, umezaliwa kwa pumzi yaMungu. Mungu aliwapulizia akasema, “Pokeeni [NduguBranham anatoa sauti ya kupulizia_Mh.] Roho Mtakatifu.”Loo, jamani, haya basi. Si “Njoo ukajiunge, andikisha jinalako pale,” na pamoja na supu zenu za jioni na kila kitu

MAJINA YA MAKUFURU 33

kinachoadamana nayo. Unajiunga na loji. Unaweza kujiungana loji, Kimethodisti, loji la Kibatisti, loji la Kipresbiteri, lojila Kikatoliki, ama loji la Kipentekoste, kitu cho choteunachotaka kujiunga nacho, bali unajiunga na loji. Baliunapokuwa mwana wa Mungu, umezaliwa kwa pumzi yaMungu. Amina! Afadhali tuliache papo hapo sasa. Vema.

Uzima wa Mungu pia umo ndani yenu. Yesu alisema (hebukidogo)_Yesu alisema, “Mimi ndimi Mzabibu, nanyi ni tawi.”Sasa angalieni. Ugomvi wao na Yesu ulikuwa nini? Ugomviwao na Yesu, kwa sababu Yeye alikuwa Mwanadamuakijifanya Mwenyewe Mungu. Yeye alikuwa Mungu. Mungualikuwa ndani ya Kristo. Mnaona? Naye aliwaambia, akasema,“Msiniangalie Mimi. Si Mimi; ni Baba Yangu, Naye anakaandani Yangu.” Mnaona?

Sasa, wao walikuwa wakiangalia maskini mwili huo mdogouliozaliwa na Mariamu. Mnaona? Huo haukuwa Mungu; huoulikuwa ni Mwana wa Mungu, bali Mungu alikuwa katikamwili huo. Ilikuwa ni Mungu. Yeye alisema, “Kama sizitendikazi za Baba Yangu basi nihukumuni Mimi. Bali ni yupi katiyenu anayeweza kunihukumu Mimi kwa ajili ya dhambi(kutokuamini Neno)? Ni Neno gani Mungu amenena ambalohalijatimizwa ndani Yangu Mimi? (Dhambi ni kutokuamini.) Ninani kati yenu ananishuhudia kwamba nina dhambi? (Dhambini kutokuamini.) Nionyesheni Mimi. Kama sizitendi kazi zaBaba Yangu, basi msiniamini. Bali kama nikifanya kazi za naniiYangu^ingawa hamwezi kuniamini Mimi, aminini kazinizitendazo kwa kuwa zinashuhudia.” La sivyo, “Baba yumondani Yangu, akishuhudia kwa nafsi Yake,” maana Mungualikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu kwa nafsiYake. Mnalipata? Vema sasa, uhai ule ule ulio kwenye mzabibuuko pia kwenye tawi. Utajiungaje na huo? Huwezi.

Niliona mti fulani si muda mrefu uliopita katika bustani yaNdugu Sharrit kule Arizona, ulikuwa na matunda tisambalimbali ya namna ya mchungwa ndani yake. Ilikuwa ninini? Ulikuwa m_ulikuwa mti wa mchungwa, chungwa lenyekitovu, bali ulikuwa_ulikuwa na li_limau, chenza, kangaja,na balungi; ulikuwa na kila namna. Nami nikasimama,nikautazama mti huo, nami nikasema, “Ndugu Sharrit,unataka kuniambia ya kwamba mti huo ni mchungwa?”

Kasema, “Hakika.”

Nami nikasema, “Vema vipi_imekuwaje?” Nikasema,“Ninaona balungi hapa, na chenza hapa, na kangaja hapa, nalimau hapa, na matunda haya mengine yote. Yamekujaje?”

Akasema, “Vema, unaona, yamepandikizwa.”

“Loo.” Nikasema, “Vema, ninataka kukuuliza jambofulani. Sasa, unachuma balungi hili na limau hili. Sasa, mwakaujao utafanyaje? Utazaa basi chungwa kutoka kwake?”

34 LILE NENO LILILONENWA

“Loo, la!” Kasema, “Utazaa limau!”

“Loo.” Nikasema, “Asante.” Mnaona?

Huwezi kufanya jambo hilo. Huwezi kujiunga mle. Balialisema kila wakati mti huo unapokuwa mwaka mmoja zaidina unatoa tawi mpya, litazaa machungwa, kama huo mzabibuwenyewe ukizaa tawi.

Na jambo ambalo tumejaribu kufanya ni kuwa wafuasiwaliojiunganisha Kwake, nasi tunaishi chini ya jina la Ukristo;kwa sababu sisi ni (kama ilivyo_katika msemo wa kawaida)_“Sisi ni tunda la namna ya mchungwa,” kanisa la Kikristo.Bali wakati mzabibu wenyewe unapotoa tawi, litakuwa kamatawi la kwanza ulilozaa. Kama Mzabibu wa kwanza ulipotoa,wao waliandika Kitabu cha Matendo nyuma yake, kamaukipata kuzaa lingine, utaandika Kitabu cha Mitume nyumayake. Hiyo ni kweli.

Kwa hiyo unajiunga tu na maloji. Bali unapozaliwakutokana na mzabibu^ Una tunda; hiyo ni kweli. Una tunda,bali unafanya nini nalo? Una mfano wa utauwa na kukanaNguvu zake. Unakana ishara; unakana maajabu; unamkanaRoho Mtakatifu. Unakana kunena kwa lugha; unakana maono;unakana unabii. Unakana kuponya, na hata hivyo unajiita jinafulani. Si ajabu Roho Mtakatifu alisema, “Nguvu za_makundiya watu waliojaa majina ya makufuru (hakika!), wakijiitawenyewe Wakristo, wakiwa na mifano ya utauwa lakiniwakikana Nguvu zake. Hao nao ujiepushe nao, kwa maanakatika hao wamo wale wanaowachukua wanawake wajingawaliochukuliwa na tamaa za namna nyingi.”

Kila namna ya madhehebu, kanisa linalobeba mengi sanaya mambo ya shirika la namna hii na shirika la namna ile. Vipikuhusu shirika la Yesu Kristo? Mnaona? Tuna mambo hayamengine yote, na tunalemeza kanisa. Sasa, haya basi.

Huwezi ukajiunga na Kanisa kamwe; unajiunga na loji.Wewe ni mfuasi wa loji, kundi la watu kama vile loji lilivyo.“Tunaamini hivi; tuna taratibu zetu, na tuna siri zetu nakadhalika.” Unafanya jambo lile lile wakati_wakatiunapojiunga na linalojiita kanisa, bali huwezi kujiunga naKanisa. Wewe ulijiunga na loji la wafuasi bali si Kanisa, kwakuwa unazaliwa katika Kanisa hilo. Na mzabibu wenyewesasa^Ngoja kidogo. Angalia! Nami nitafunga baada yakitambo kidogo.

Angalieni! Tafadhalini, si_sikumaanisha kusema jambohilo. Angalieni. Kama Mungu alimuimarisha Bibi-arusi huyuna Roho huyo, basi jambo hilo liliimarisha huyo mtu binafsi naRoho huyo. Mnaona? Ndipo umezaliwa kuwa katika Ufalmehuo, halafu Uhai ule ule uliokuwemo ndani ya Kanisa hilikatika Kanisa lile, na lile, lile, lile, lile. Na Uhai ule uleuliokuwemo katika lile ganda, ule Mzabibu, Yesu, umo katika

MAJINA YA MAKUFURU 35

mshirika aliyemzaa Yeye. Utukufu! “Kwa mambo yale yaleniyafanyayo, kazi nizifanyazo, ninyi nanyi mtazifanya.” Huyohapo mshiriki wa kweli wa Mwili wa Kristo; hakuna namnafulani ya jina lililobandikwa kwake. Kazi zenyewe za huyomtu binafsi zinathibitisha anakotoka. Hayo hapo Maishayanayoshuhudia yeye ni nini.

“Wewe ni_wewe ni^Ni mfuasi_wewe ni wa kundigani?”

“Mwili wa Kristo!”

“Vema, ulijiunga Nao wapi?”

“Sikujiunga; nilizaliwa Mle.” Mnaona? “Nilizaliwa Mle.’

Huna lazima ya kumwambia. Wao wanajua kilichotukia.Wewe tu^“Unawezaje kuwasha mshumaa na kuufunika kwapishi?” Yeye alisema. Mnaona? La, la!

Unapozaliwa kuwa katika Ufalme huo wa Mungu, basiUzima, Uzima uliokuwemo katika Yesu^ Ndipo unawapendawatu. Ndipo haikubidi kuwashawishi watu wajemadhabahuni. Huna haja ya kumshawishi mtu fulani kujakuomba pamoja na wale walioko madhabahuni. Vi_vi_vituhivyo vinabubujika vyenyewe tu, kwa maana umetiwa muhurindani yako. Wewe ni kitu kizima cha Mungu. Umetiwa muhurina Roho Mtakatifu.

Sasa, mnajua maana ya Roho Mtakatifu? Haimaanishiniliruka juu na kupiga makelele, na nilipata hisi za ajabu.Hayo ni sawa. Nimeruka juu na kupiga makelele na nikawa nahisi za ajabu. Nilinena kwa lugha. Ninaamini Roho Mtakatifuhunena kwa lugha. Hakika! Nimefasiri. Naam, bwana!Ninaamini jambo hilo pia. Bali hilo silo. Hilo siloninalozungumzia. Kunaweza kuwe na kuvuja hapa mahalifulani. Kunaweza kuwe na kuvuja hapa katika saburi yako.Hebu mtu fulani akupige kofi shavuni. Unaligeuza lile lingine?Lakini unasema, “Mnafiki mchafu yule.” Basi kuna kuvujamahali fulani kumeanza. Afadhali tuachilie mbali jambo hilo.Vema. Lakini mnajua ninalomaanisha? Bali unapotiwa muhurikuwa katika Mwili wa Kristo, basi umejazwa Roho, nawe nimwana wa Mungu.

Loo, laiti ningalikuwa na kama dakika kumi kusoma kitufulani hapa, lakini mimi^ Mngenivumilia kwa dakikaziingine kumi? Ninataka kusoma jambo fulani. Kidogo tu sasa.Nita-^Kweli, maharagwe hayataungua; nitawahakikishia tu(mnaona?), kama tutasoma tu hili kwa dakika chache tu. Ni zurisana hatuwezi kuliacha lipite. Nimepata mambo machachehapa yaliyoingia moyoni mwangu hivi punde ambayo ningetakakusema. Hebu tufungue Yohana Mt. sura ya 3, inayozungumzajuu ya Uzima wa Milele. Hebu tuone inavyosema juu ya swalihili la Uzima wa Milele pamoja na Uzima wa Mungu. Sasa, sasaangalieni hapa.

36 LILE NENO LILILONENWA

Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jinalake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

Huyo basi alimjia Yesu usiku, akamwambia, Rabi,twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu;^hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi^isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

Sasa, wao_hiyo halmashauri ya Wazee, wao walitambuaya kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Walijua jambohilo. Hapa alikuwepo mkuu wao papa hapa akimwambia Yeye,“Tunajua ya kuwa U mwalimu umetoka kwa Mungu, kwamaana Uzima ule ule wa Mungu unatiririka ndani Yako.”Mnaona? “Tunajua ya kwamba mafundisho Yako si Yakomwenyewe; ni ya Mungu, kwa maana Mungu anathibitishajambo hilo.” Mnaona? “Uzima wa Mungu unatiririka moja kwamoja ndani Yako.” Sasa angalieni!

Yesu akijibu akamwambia, Amin,^, nawaambia,Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalmewa Mungu^ (Loo, jamani! “Usipojiunga na kanisalangu^” Loo, mnaona jinsi mnavyopotea? Mnaona,mnaona?)

Ndipo Yesu_Yesu akijibu akamwambia, Amin, amin,nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na^Roho,hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Kilichazaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwakwa Roho ni roho.

Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budikuzaliwa mara ya pili.

Upepo unavuma upendako,^ (Mnaona? Moja kwamoja tena. Mnaona? Akirudi. Mnaona?)^ Upepounavuma upendako, na sauti yake huwezi kuisikia_kusikia sauti yake, lakini hujui mahali unakotoka,wala mahali unakokwenda; kadhalika na hali yakekila mtu ambaye amezaliwa kwa Roho.

Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwamambo haya?

Yesu akajibu, akamwambia, Je! wewe u mwalimu waIsraeli, na mambo haya huyafahamu?^ (Angaliapale, ndugu, D.D., Ph.D., L.L.D. Mnaona?), na mambohaya huyajui?

Amin,̂ , nakuambia kwamba, Lile tulijualotwalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; walaushuhuda wetu nyinyi hamwukubali^ (Tunayajuamambo haya. Tumeyaona; tunajua jambo hilo, walahata hamwukubali ushuhuda wetu, mjiunga nakanisa. Mnaona?)

MAJINA YA MAKUFURU 37

Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, walahamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo yambinguni?^ (Sasa, sikilizeni jambo hili hapa. Sasa,angalieni!)

Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeyealiyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana waAdamu, aliye mbinguni.

Wazia jambo hilo. Mnajua wakati mmoja Yeye alisema,“Mnafikirije juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?”

Wao wakasema, “Mwana wa Daudi.”

Akasema, “Basi kwa nini Daudi, katika Roho,anamwambia Yeye, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu, “Uketimkono Wangu wa kuume”’?” Awezaje kuwa Bwana Wake naMwanawe? Hakuna mtu aliyemwuliza jambo lingine lo lote.

Katika Ufunuo Yeye alisema, “Mimi ni Shina na Mzao waDaudi.” Mnaona? “Mimi ni Mzabibu na Tawi. Mimi nimwanzo. Nilikuweko kabla ya mwanzo; nilikuwa mwanzo,na_na nilikuwa Mzao wake pia.”

Sasa, hapa Yeye alisema, “Hakuna mtu aliyeshuka kutokaMbinguni, ila Mwana wa Adamu aliye sasa Mbinguni.”

Bibi fulani aliniuliza wakati mmoja, swali, nikasema,“Nijibu hili.”

Kasema, “Yesu alimwomba Nani katika bustani yaGethsemane?”

Nikasema, “Yeye alikuwa akinena juu ya Nani wakatialiposema, ‘Hakuna mtu aliyepaa Mbinguni, ila Yeyealiyeshuka kutoka Mbinguni, yaani Mwana wa Adamualiye_aliye sasa Mbinguni’?”

Huyu hapa, amesimama papa hapa juu ya nyumbaakizungumza na Nikodemo, kisha akasema, “Mimi nikoMbinguni.” Hiyo ni kweli? Hebu tuliache jambo hilo hadiusiku wa leo, mnaonaje? Muda unaenda sana. Loo, jamani!Hebu tuwazie tu jambo hilo kwa muda kidogo alasiri ya leo.

Unaingiaje Kanisani? Kuzaliwa! Na nini? Pumzi yaMungu!

Nipulizie, nipulizie;Roho wa Mungu Aliye Hai, nipulizie.

Hilo ndilo ombi langu. Acha tu Roho Mtakatifu apulizie.Loo, jamani, nina hamu ya pumzi ya Mungu. Ni nini? Kutiwamuhuri katika Ufalme wa Mungu, nikijua ya kwamba wakatinilipokiri kwanza, “Namwamini Yesu Kristo”^Naam.

Kisha kwenye imani yangu, natia nguvu, nguvu za kiungu.Halafu kwenye nguvu zangu, natia maarifa ya Neno. Kwenyemaarifa yangu natia kiasi, kuweza kujitawala. Ninaupendahuo, “Nchi yangu ni yako^Tia taji nafsi yangu kwa kuweza

38 LILE NENO LILILONENWA

kujitawala^Kutoka bahari hadi bahari inayong’aa.” Saburi.Loo, jamani! Kujaribiwa: usijali, Shetani atakujaribu na vituhivyo.

Ninapanda ile ngazi sasa. Mnaona? Nimetia nguvu,maarifa, kiasi; sasa sina budi kutia saburi. Bado sina RohoMtakatifu. Kisha baada ya kutia saburi, natia utauwa. Unajuahuo ni nini? Kuwa kama Mungu. Ninatia huo. Sifanyi matendomabaya; enenda kama Mkristo muungwana anavyopaswakuenenda. Hebu hilo lisiwe la kuigiza. Kitu fulani ndaniyangu, upendo wa Mungu unachemka tu^Mnaona, mnaona?Si kusema, “Mimi_mimi_mimi^Jamani, ningeweza kufanyajambo hilo, bali labda afadhali nisilifanye.” Mnaona? A-ha; A-ha! Liko pale hata hivyo. Ni kuzaliwa. Nimezaliwa katika hii,katika hili, katika hili, katika hili, katika hili, katika hili,katika hili, halafu upendo wa Mungu, Kristo, anashuka nakutia muhuri hayo yote ndani yangu kwa ajili ya utumishi.Mnaona?

Basi anafanya nini anaponipa Roho Mtakatifu?Anakuweka kule nje peke yako katika mahali palipotengwa,anakutia alama. Mnaona? Wewe ni mtu tofauti basi. Wewe siwa ulimwengu tena (mnaona?), umevikwa tofauti. Unavalianguo tofauti. Si nguo hii ya nje. La, la! Haikubidi kuwa mtutofauti na wa kipekee, pamoja na ukosi uliopinduliwa, na vasirefu kama la sherehe. La, la! Hufanyi hivyo. Unavaa kamakawaida ya mtu kama^Vazi_vazi refu la kiroho ndilo tu kitumuhimu. Umevalishwa vazi la arusi. Wewe ni nini? KamaYesu.

Angalia, Yeye alitiwa uvuli, na akageuka sura pale mbeleyao. Na vazi Lake likang’aa kama jua. Huyo hapo, Yesu,Mungu akimweka Mwanawe mahali Pake. Mnaona? Halafu,akaja Musa. Kisha akaja Eliya. Basi Petro akasema, “Mwajua,ni_ni jambo zuri kuwa hapa.” Unaona vile mwanadamuanavyokuwa? Loo, ya kimbinguni yalifanywa^Kasema,“Natujenge vibanda vitatu. Na tujenge kimoja kwa ajili yaMusa, na kimoja kwa ajili ya Eliya, na kimoja kwa ajili Yako.”

Basi kabla hajamaliza kusema, Mungu akafunga tu jambolote, kasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa Wangu. Katikamambo haya yote niliyomtaka Musa, na nikatoa amri kwa njiaya Musa, haki kwa njia ya manabii, Yeye ametimiza yote.Msikieni Yeye. Nitajiondoa sasa. Msikieni Yeye tu. MsikieniYeye tu.” Loo, jamani, ni jambo zuri jinsi gani.

Halafu, tunapotimiza masharti haya na kujaa wema waMungu na mambo ya Mungu, ndipo Roho Mtakatifuanaposhuka na kututia muhuri katika Ufalme. Msijali. Kilamtu atajua ya kwamba unaye Huyo. Hutakuwa na haja yakusema, “Vema, Mungu atukuzwe, ninajua ninaye; nilinenakwa lugha. Mungu atukuzwe, ninajua ninaye; nilicheza katika

MAJINA YA MAKUFURU 39

Roho wakati mmoja.” Huna haja ya kusema kitu juu yake; kilamtu atajua unaye; Usijali. Yeye atajishuhudia Mwenyewe.Atatangaza jambo hilo kati ya watu.

Mungu awabariki. Ninafurahi sana kuwa pamoja nanyiasubuhi ya leo na kuwa na wakati huu wa ushirika. Sikilizeni!Maskini kanisa letu ni dogo, na hata hivyo hatuna nafasi yakutosha kwa ajili ya watu wanaokuja hapa. Sisi si madhehebu.Sisi tunaamini na tunashiriki pamoja na kila madhehebu.Mnakuja tu hapa, kwa sababu kwamba mnataka kuja.Nanyi^Tunawapenda, na tunataka kila madhehebu, kilamtu^

Ninaamini ya kwamba kuna watu katika madhehebu hayoyote ambao ni Wakristo. Wao ni ndugu na dada katika Kristo.Kwa hiyo basi, hatuna masharti, hakuna kitu cha kujiunganacho, hakuna la kufanya, bali uwe tu Mkristo.

Kama alivyozoea kusema E. Howard Cadle, “Hatunasheria ila upendo, hatuna kitabu ila Biblia, hatuna kanuni yaimani ila Kristo.” Na hiyo ni kweli. Njoo ukatutembelee. Tunafuraha ku-^Tunaamini Injili Yote, kila sehemu ya Neno.Tunaamini tu vile hasa^Hatuongezi jambo moja Kwake,kuondoa lo lote Kwake, kuongeza upuuzi wo wote wakimadhehebu Kwake. Tunaliacha tu jinsi tu lilivyo. Naam.Nasi daima tunafurahi kuwapokea. Njoni mwe pamoja nasimwezapo. Tunawaombea wagonjwa. Tunaamini kila kituinachosema Biblia tufanye. Tunasahau “unyonge wetu, nyuma,nasi tunapiga mbio kuelekea mede ya wito mkuu.”

Sasa, jambo moja zaidi. Mtaruhusu lisemwe? Sikuiliyotangulia jana asubuhi^Mtaona kwenye_kwenye ubaowa matangazo kule nje ono. Nilipata ono. Ilikuwa kama saa 11,kama mke wangu kule nyuma ajuavyo, ama 12. Nilikuwanimeamka. Tulikuwa tumeamka kuwatayarisha watotokwenda shuleni. Ninapata haya mara kwa mara; nanyi nyotemnajua, kila mmoja wenu hapa, ya kwamba hayashindwi. Ni_ni makamilifu kabisa (mnaona?); hayashindwi.

Nami nilifikiri nilikuwa mtu mwenye furaha sananiliyepata kuona. Nilikuwa nimesimama kwenye jua, j-u-a,nami nilikuwa ni_nikihubiria Injili kusanyiko kubwa mno(nilitaka tu kuona kama yananaswa) ku_ku_kusanyikokubwa mno. Nao walikuwa wameketi msituni, na miali ya juailikuwa inawaangazia, hapa tu na pale, wakiipata, wakilipataNeno.

Nami, kama kawaida, daima nachukua wakati mrefu sana,nawachelewesha sana, nahubiri kwa muda mrefu sana. Nanikahubiri kwa muda mrefu sana, mpaka kusanyiko likawa nanjaa ya chakula cha kawaida. Nao, wengine wao wakachoka,kwa hiyo waliamka tu wakatoka wakaenda kujipatia chakula,wakaanza kutoka nje. Nikasema, “Msitoke, msitoke.”

40 LILE NENO LILILONENWA

Nilikuwa nina vipeo viwili nilivyotaka kufikia_nilivyotaka kufikia katika somo langu. Naye Bwana alikuwaamenipa hilo. Na mhubiri ye yote anajua wakati unajua kwelini_Mungu amekupa hilo, unakuwa na shauku sana yakuwaambia watu. Nami nilikuwa tu ninahubiri, “Charlie,”kwa nguvu tu nilivyoweza kuhubiri, nikiyaelezea tu, mwajua,na kusema, “Mambo haya yote makuu^Hivi ndivyo Munguanavyofanya, angalieni jambo hili. Yeye anatambua mawazoya moyo. Ni nini? Neno,” huku ninaendelea namna hiyo.

Ndipo lo, laiti ningalikumbuka niliyokuwa ninasema, somolangu lilikuwa nini. Siwezi kulikumbuka. Mnaona? Lakininilikuwa ninahubiri tu, nami nilikuwa nikijiangalia nikifanyajambo hilo. Ndipo basi, nilipokuwa nimesimama palenikitazama na kujiangalia mwenyewe nikilihubiri^Naminilikuwa nikihubiria “ambaye asingeamini.” Basi baada yamuda kidogo nikainuka, mwajua, kisha nikawaza, “Munguatukuzwe.” Nikasema, “Angalia mambo haya ya ajabu, na hili,lile^”

Moja kwa moja, nikaona watu wakianza kufanya kamakwamba walikuwa na njaa ya kawaida. Na kwa hiyowalikuwa na cha kutosha kiroho, kwa hiyo wakaanzakuondoka na wengine wao [Ndugu Branham anapiga miayokutoa mfano_Mh.] wakaanza kuondoka. Nikawaza, “Kunanini kwa kila mtu?” Na_nami nikaangalia na hapawalikuweko maskini wake na waume zao wanapita karibunami, ndipo nikanyamaza; nikasema, “Hebu kidogo, marafiki,hebu kidogo. Mtarudi tena wakati vivuli vya jionivitakapotua.” Mnaona? Nikasema, “Mtarudi tena.” Lakini,hebu niwape kipeo hiki cha kwanza. “Mambo haya yoteniliyowaonyesha hutoka wapi? Yametoka wapi?” Nikasema,“Haya hapa. Yako kwenye Neno la Mungu. Hayo ni BWANAASEMA HIVI, ahadi Yake, maana,” nikasema, “ninyi nyotemnanishuhudia, mnashuhudia jambo hili, ya kwamba agizolangu ni, ‘Kaa na Neno.’” Nikasema, “Ninyi nyote mna nini?Hivi hamwezi kulifahamu Neno? Hamna budi kulifahamu.”

Ndipo mtu fulani akasema, “Jamani, ningetaka kulabiskuti,” na kadhalika namna hiyo.

Vema, niliwaza tu, “Vema, Mungu atukuzwe. Iwapowanataka biskuti, na waende wakazichukue.” Kwa hiyo ni_nikageuka; nikawaza, “Loo, lakini wajua nini? Vivuli vitatuabaada ya kitambo kidogo. Mara moja.” Kisha nikasema,“Halafu usiku wa leo, wakati kusanyiko hilolitakapokusanyika tena^ Sasa, niliwawekea kipeo nakuwaambia ya kwamba mambo ambayo wameniona miminikiyafanya yanapatikana katika Neno la Mungu, si katikavitabu fulani vya kujibunia wala madhehebu fulani,yanapatikana katika Neno (mnaona?), kila sehemu yake katikaNeno, maana nimeagizwa kufanya jambo hilo.” Nikawaza,

MAJINA YA MAKUFURU 41

“Wajua, kila mmoja wao atarudi usiku wa leo. Kwa hiyo hivindivyo nitakavyofanya: nitaliwekea msingi, kuliwekea msingikwa namna fulani.” Mnajua jinsi ninavyofanya jambo hilokatika nyakati hizi za kanisa na kadhalika, kusema niliyosemahapo awali. “Nitaliwekea msingi kwa Neno, halafu kipeo hikikikubwa na cha ajabu sana^” Nikasema, “Utakuwa wakatiwa jinsi gani. Mungu asifiwe.” Nami nikajiona nikifanyikamdogo sana, ndipo nikasikia hiyo, “Mungu asifiwe.” Nikajionamwenyewe nikififia namna hiyo, nami huyu nimesimama pale.

Sasa, hii hapa fasiri yake. Mnaona? Jambo la kwanzanililofanya: Mambo ambayo yamefanywa yamekuwa ya kisirikwa watu_karibu wote. Simaanishi Injili Yote na watakatifuwa Mungu, bali ninamaanisha kwa watu walio wengi sana.Nanyi hamtaki kamwe kuangalia ulimwengu, Cosmos, kamaUjumbe wa Mungu. Mnapoingia, mnasema^

Kama vile Boze alivyosema, “Daima nime-^” Kasema,“Niliota ndoto miaka kadha iliyopita ya kwamba Mu_Mu_Mungu angenituma Chicago na kuutikisa Chicago kwautukufu wa Mungu.”

Nikasema, “Joseph, Yeye tayari amefanya jambo hilo.”

“Mbona,” akasema, “wao hawajatikiswa tangu siku zaMoody.”

Nikasema, “Hilo^Mimi ninazungumza juu ya Kanisa.Hao ni chakula cha mizinga huko nje. Hao ni mavumbi tu yaardhi; kundi hilo linalosongamana mitaani, na Mayezebeliwaliojipodoa, na kila kitu^” Nikasema, “Hao ni huko nje.Hayo ni maloji makubwa ya kale na kadhalika yataporomokana kuanguka mitaani huko.” Nikasema, “Yeye ananena juu yaKanisa. Kanisa limeona ufunuo wa Yesu Kristoukidhihirishwa, nao wanautambua. Huenda wasiweko kumi nawatano kutoka Chicago. Huenda wasiweko kumi katika kizazihiki kutoka katika jiji zima la Chicago na kadhalika.”

Ulipata kuwazia jambo hilo? Kama ilivyokuwa katika sikuza Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika kuja Kwake Mwana waAdamu, ambapo watu wanane waliokolewa. Ni wangapiwaliotoka Sodoma? Mnaona ninalomaanisha? Nina shakawatakuwa wachache sana. Mnaona?

“Lakini Kanisa lenyewe limekwishapata mtikiso. Waowametambua jambo hilo. Walijua Neno. Walilitambua Nenolilipokuwa likifanyika mwili, nao wakalishika. Sasa, angalienijambo hilo kwa muda kidogo.”

Sasa, na huu ujumbe wa kwanza, wakiisha kuuona, kilamtu aliufuata; kasema “Loo, Mungu atukuzwe. Loo, kamaningeweza kuona^hili, lile, na linginelo,” nao wangeondokamoja kwa moja, jinsi ile ile walivyoingia. Mnaona? Na sasa,

42 LILE NENO LILILONENWA

wao wanafikiri, “Vema, sijui. Ungejiunga na wapi? Kamasitakuja pamoja na hili, itakuwa namna hii; nami nitafukuzwanitoke hapa, nami sitakuwa na la kufanya hapa.”

Nao ndugu wanaketi na kusema, “Vema, ningefanyajekama mimi^?” Mnaona pale? Wao hawatakaa muda mrefuwa kutosha waone Hilo ni Neno ambalo Mungu aliahidi sasalinadhihirishwa (mnaona?), nao wakaondoka. Bali msijali,vivuli vimekaribia sana. Mnaona?

Niliporudi kwenye huduma^ Mnakumbuka usiku wajuzijuzi wa ujumbe alionipa huko nyuma nilipokuwa nikiwekajiwe la pembeni. Vile vile kabisa, kasema, “Fanya kazi^”Kasema, “Utakapotoka kwenye ono hili, soma 2 Timotheo 4.”Mnajua liko pale pale kwenye jiwe la pembeni_miakathelathini na mitatu iliyopita. Kasema, “Fanya kazi ya mhubiriwa Injili. Timiliza huduma yako, maana utakuja wakatiwatakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuatania zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundiwenye masikio ya utafiti, watajiepusha na hadithi za uongo_watajiepusha na yaliyo Kweli na kuzigeukia hadithi zauongo.” Kama hilo halijatukia neno kwa neno.

Lakini kumbukeni basi, usiku wa juzijuzi wakati sikusomayaliyosalia. Miaka thelathini na kitu ambayo nimehubirikwenye maskani haya, hata wakati mmoja sikuenda mbalizaidi ya hapo, nami sijui ni kwa nini. Mara nyinginimeshangaa, hata siku moja nikaona ambapo Yesu alitwaaGombo na kuanza kusoma, ndipo akasoma nusu ya unabii,kisha akasimama, ndipo akasema (kule Kapernaumu),akasema, “Basi leo, unabii huu umetimizwa.” Kwa ninihakusoma yaliyosalia? Yanahusu kuja Kwake kwa pili.Mnaona?

Na pale ningesoma hayo bila kujua^Nilitwaa hilo, nandilo hilo papo hapo mbele yangu kule Southern Pines,Carolina ya Kusini. Asubuhi hiyo, nikisimama palenikizungumza na Joseph Boze, niliegemea kwenye upandemmoja wa motokaa [Ndugu Branham anadata vidolevyake_Mh.], nikalipata. Paulo alisema, “Mimi^Watu wotewamenichukia. Hakuna mtu aliye pamoja nami. Demaameniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa. Na mimisasa^(angalia!) Naye mfua shaba ameonyesha ubaya mwingikwangu.”

Angalia yale hapana budi Dema aliwazia. “Mbona,nimemwona Paulo akihubiri Injili na kuwaponya wagonjwa;na huyu hapa ameketi akiugua yeye mwenyewe, akiambatanana daktari, Luka, kila mara anapoenda, akiambatana nadaktari, mtu anayehubiri Kiungu^ Mbona, nilimwonaakimpiga mtu upofu; kasema, ‘Bwana na akukemee, naweutakuwa kipofu kwa muda’; halafu anamwacha mfua shaba

MAJINA YA MAKUFURU 43

amfukuze mkutanoni. Nafikiri alipoteza nguvu za kumpofushamtu. Hatimaye alipoteza nguvu za kuponya Kiungu. Munguamemgeuka.”

Sidhani Dema alienda ulimwenguni, maana Dema alikuwawa^ Mwajua historia yake, alitoka kwenye jamaa kubwa natajiri; naye alitaka kuambatana na huo umati mwingine. BaliPaulo, maskini Paulo, ilikuwa ni nini? Mungu daima huachahuduma ifikie mahali kama hapo kisha anaitia taji. Yeyealimwacha Yesu afikie mahali (angalia pale!), ambapo Yeyealiweza kuwafufua wafu, ambapo angefanya lo lote alilotaka,kisha akamwacha askari wa Kirumi ang’oe ndevu kutokausoni Mwake na [Ndugu Branham anatoa sauti ya kutemamate_Mh.] kumtemea mate usoni Mwake. Wakampigakwenye^Wakamfunika uso kwa kitambaa na kusema, “Sasa,wajua, wao wananiambia ya kwamba wewe ni nabii^” Wotewalisimama karibu wakiwa na mianzi yao na [Ndugu Branhamanatoa mfano wa kumpiga Yeye_Mh.], wakampiga Yeyekichwani, wakasema, “Sasa twambie ni yupi aliyekupiga.”Yeye alijua ni nani aliyempiga. Hakika alijua! Mnaona? Balihuduma yake ilikuwa karibu kutiwa taji. Daima inafikiamahali hapo ambapo inaonekana kana kwamba ni nyonge sanasana, imekaribia sana kwisha, ndipo Mungu anaitia taji. Loo,Bwana, na itendeke. Na itendeke, Bwana. Na tuinamishevichwa vyetu.

Nampenda, nampenda,Kwani alinipenda kwanza, (Sasa, mwabuduni;

tumekuwa na mafundisho magumu!)Na kununua wokovu wangu mtini Kalvari.

Na tumwinulie Yeye mikono yetu sasa.

Nampenda, (Naam, iweni katika Roho.Mnaona? Nampenda.] Nampenda,

Kwani alinipenda kwanza,^ `

44 LILE NENO LILILONENWA

Majina Ya Makufuru, Vol. 8 No. 3

(Blasphemous Names, Vol. 3 No. 21)

Ujumbe huu wa Ndugu William Marrion Branham, uliohubiriwa hapo awali

katika Kiingereza mnamo Jumapili asubuhi, Novemba 4, 1962, katika

Maskani ya Branham kule Jeffersonville, Indiana, Marekani, hapo awali

ulitolewa kwenye kanda za sumaku na kupigwa chapa bila kufupishwa

katika Kiingereza. Hii tafsiri ya Kiswahili ilichapishwa mwaka wa 1996 na

Voice Of God Recordings.

VOICE OF GOD RECORDINGS

P.O. Box 950, Jeffersonville, Indiana 47131 U.S.A.

Just One MOre tiMe, LOrd 1

Copyright notice

All rights reserved. This book may be printed on a home printer for personal use or to be given out, free of charge, as a tool to spread the Gospel of Jesus Christ. This book cannot be sold, reproduced on a large scale, posted on any website other than www.branham.org, stored in a retrieval system, translated into other languages, or used for soliciting funds without the express written permission of Voice Of God Recordings®.

For more information or for other available material, please contact:

Voice of God RecoRdinGsP.o. Box 950, JeffeRsonVille, indiana 47131 U.s.a.

www.branham.org