36
KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOT African Lead Paint Elimination Project 2015

KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

  • Upload
    others

  • View
    20

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOT

African Lead Paint Elimination Project

2015

Page 2: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

ii

KUTABARUKU

Tunachukua fursa hii kuwashukuru wote waliohusika katika kukusanya na kuandaa kitabu hiki kinachohusu uangamizaji wa rangi yenye sumu ya madini ya risasi (lead).

Shukrani za dhati ziliendee shirika la kimazingira la Global Environment Facility kwa kutoa msaada wa kifedha. Tunashukuru pia shirika la UNEP kwa ushauri na mwelekeo kwa ushirikiano na IPEN katika uandishi na uchanganuzi wa nakala hii. Pia tunatambua juhudi nyingi za Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO) yanayoshirikiana na IPEN barani Afrika na kote duniani katika kuangamiza rangi yenye sumu ya madini ya risasi. Shukrani za kipekee ziwaendee wafanyakazi wa IPEN ambao kazi yao ilifaulisha kukamilika kwa kitabu hiki.

Kitabu hiki kiliandaliwa kama sehemu ya Mradi wa Kuangamiza rangi yenye sumu ya risasi barani Afrika. Mradi wa Kuangamiza rangi yenye sumu ya risasi barani Afrika huendesha shughuli zake za kishabaha katika mataifa manne– Cameroon, Cote d’Ivoire, Ethiopia na Tanzania – ili ku-komesha sumu ya risasi kwenye rangi.

Mradi huu unafadhiliwa na shirika la kimazingira la Global Environment Facility; Shirika la Umoja wa Mataifa lnalohusika na Mipango ya Maz-ingira (UNEP) ndilo Shirika la Utekelezaji wa Mradi huu; nalo shirika la IPEN ndilo Shirika Linaloendesha Mradi huu. Hata hivyo, matini ya kitabu hiki ni jukumu la kibinafsi la IPEN.

Chapisho hili ni mchango wa Ushirika wa Kimataifa wa Kuangamiza Rangi yenye Sumu ya Risasi. http://www.unep.org/noleadinpaint/

IPEN www.ipen.org

Ushirika wa Kimataifa wa Kuangamiza Rangi yenye Sumu ya Madini ya Risasi:

http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Home/tabid/197/chemical-sandwaste/LeadCadmium/PrioritiesforAction/GAELP/tabid/6176/De-fault.aspx

Page 3: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) iii

Dibaji ............................................................................................... iv

Utangulizi .........................................................................................2

Kutagusana na madini ya Risasina Athari zake kwa Afya ..................4

Athari za kiuchumi za Mtagusano na Sumu ya Risasi ........................9

Vianzo vya madini ya Risasi katika Rangi .........................................11

Vibadala vya Madini ya Risasi katika Rangi ..................................... 13Rangi ya Kunakshisha ................................................................................. 13Industrial Paints ........................................................................................... 14

Muongozo wa Kukomesha Rangi yenye Sumu ya Risasi .................. 16Mwongozo wa Kimataifa wa Kumaliza Rangi ya Sumu ya Risasi:

Muungano wa Kimataifa wa Kukomesha Rangi ya Sumu ya Risasi (GAELP) .................................................................................................... 16

Mwogozo wa Kitaifa wa Kukomesha Rangi zenye Sumu ya Risasi ....... 17Ufuatiliaji na Uzingatiaji Sheria ................................................................ 19

Rangi yenye Sumu ya Risasi Katika Mataifa ya Cameroon, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Tanzania ............................................. 20

Hitimisho ........................................................................................22Miongozo ya Kisheria ................................................................................. 22Hamasisho kwa Umma .............................................................................. 22Juhudi za Kujitolea na Uwekaji Lebo ...................................................... 23

Kiambatisho ....................................................................................24

YALIYOMO

Page 4: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

iv

DIBAJI IPEN na mashirika mengineyo yamedhihirisha kuwa rangi zilizotiwa sumu ya risasi kwa matumizi ya nyumbani zinaendelea kutengenezwa kwa wingi, kuuzwa na kutumiwa katika mataifa yanayoendelea licha ya kuwa mataifa mengi yaliyostawi yalipiga marufuku rangi zenye sumu ya risasi kwa matumizi ya nyumbani zaidi ya miaka 40 iliyopita. IPEN pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Mipango ya Maz-ingira (UNEP), Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika mengine yanaendelea kushirikiana ili kuhamasisha kwamba ni tatizo kubwa kwa watoto kutagusana na rangi yenye sumu ya risasi, hatua ambayo imeimar-isha juhudi za kitaifa katika mataifa kadhaa yanayostawi, na zinazolenga kukomesha rangi yenye sumu ya risasi na hivyo kuwalinda watoto.

Mnamo 2007 na 2008, Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) na mtandao wa IPEN yalikusanya na kuchanganua rangi za kunakshisha/kurembesha nyumba (rangi za matumizi ya nyumbani) zilizomo masokoni katika mataifa 11 yanayoendelea, pamoja na yale yenye uchumi una-okaribia kustawi. Matokeo yake yakawa ya kushangaza. Katika kila moja ya mataifa haya, rangi nyingi ziligunduliwa kuwa na viwango hatari na vya juu vya sumu ya madini ya risasi. Katika kukabiliana na hali hiyo, IPEN il-izindua kampeni ya kimataifa ya kuangamiza rangi yenye madini ya risasi. Tokea hapo, NGO zinazoshirikiana na IPEN pamoja na mashirika men-gine yameteua na kuchanganua rangi mbalimbali sokoni katika mataifa yapatayo 40 yenye uchumi wa chini na wa wastani.1 Tafiti kumi na mbili kati ya hizo ziliendeshwa kwa msaada wa UNEP.2

Katika mwaka wa 2009, matokeo (data) mapya yaliyoorodhesha kuwa rangi yenye madini ya risasi bado inatumika kwingi katika mataifa yanayoendelea na yale yenye uchumi unaokaribia kustawi, yalichangia maamuzi ya Kongamano la Pili la Kimataifa kuhusu Matumizi ya Ke-mikali (ICCM2) kwa dhamira ya kuhimiza juhudi za kuangamiza rangi yenye sumu ya risasi duniani. Kutokana na maamuzi hayo ya kongamano la ICCM2, UNEP na WHO ziliunda shirika la Global Alliance kwa lengo la kuangamiza Rangi yenye Sumu ya Risasi (GAELP), ukumbi ambapo mashirika ya serikali, IPEN, NGO za kitaifa, wawakilishi wa viwanda vya kutengeneza rangi na mengineyo hushirikiana ili kuendeleza dhamira ya kukomesha rangi yenye sumu ya risasi.

1 Habari kuhusu mataifa yaliyoonyeshwa pamoja na tafiti zake zinapatikana katika Annex A ya ripoti hii.

2 Ibid.

Page 5: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 1

Leo hii, IPEN inajumuisha mashirika 700 kutoka mataifa 116, hasa yanayoendelea na yale yenye uchumi unaokaribia kustawi. IPEN huyaleta pamoja makundi maarufu ya kimazingira na afya ya umma kote duniani ili kuyahusisha katika juhudi za kimataifa za kupunguza na, ikiwezekana, kuangamiza kemikali hatari zenye sumu katika ngazi za kimataifa na hata kitaifa.

Page 6: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

2

UTANGULIZI Madini ya Risasi ni chuma chenye sumu kinachopatikana katika baadhi ya rangi.

Rangi yenye madini ya risasi hutengenezwa kwa kutumia mseto wa metali zenye madini ya risasi ili kuipa rangi aina mbalimbali za muonekano (rangi), kupunguza kutokea kwa kutu kwenye vyuma, au kuwezesha rangi kukauka harak.3 Metali zenye madini ya risasi zinaweza pia kupatikana katika mipako mbalimbali kama vile vanishi, gundi ya lacquers, utomvu katika rangi, enameli, rangi za kinamu au rangi majimaji ya awali kabla ya kupaka rangi yenyewe. Madini ya Risasi yanaweza pia kupatikana kama kichafuzi katika malighafi mengineyo ambayo hutumika kutengeneza rangi na bidhaa nyinginezo. Kwa sababu hiyo, lazima watengenezaji wa-fuatilie kwa karibu jumla ya madini ya risasi kwenye bidhaa.4

Nchi nyingi zilizostawi zilishakumbatia sheria na kanuni zinazodhibiti kiwango cha madini ya risasi katika rangi za kunakshisha – rangi zinazo-tumiwa ndani na nje ya majengo, shule, na mijengo mingineyo kunak-oishi watoto- kuanzia miaka ya 1970 hadi 1980. Mataifa mengi kati ya hayo pia yaliweka vidhibiti kuhusu kiwango cha madini ya risasi katika rangi zinazotumiwa kutengeneza wanasesere (doli) na vifaa vinginevyo vinavyoweza kuchangia watoto kutagusana na sumu ya risasi. Hatua hizi za kisheria zilichukuliwa kutokana na matokeo ya tafiti za kisayansi na kimatibabu kwamba madini ya risasi ndiyo chanzo kikuu cha watoto kuta-gusana na sumu ya risasi mbali na kwamba kutagusana kwa watoto na sumu ya risasi husababisha madhara makubwa, hasa kwa watoto wenye umri wa miaka sita na chini yake. Kutagusana na sumu ya risasi pia ku-nadhuru watu wazima, hasa wale wanaofanya kazi zinazohusisha uwepo wa kiwango cha juu cha madini ya risasi. Madini ya risasi katika rangi yanaweza kuchangia hatari kuu ya kikazi kwa wapaka-rangi wanaotagusa-na na sumu ya risasi, watengenezaji wa ‘miili’ ya magari, wanaofanya kazi za ujenzi zinazohusisha unaksishaji wa mijengo na kadhalika.

3 Metali za madini ya risasi ambazo hasa huongezwa kwenye rangi zinajumuisha, japo si hizo tu: lead carbonate (madini meupe ya risasi), lead chromate, Lead chromate oxide, Lead chromate molybdate sulphate red, Lead sulpho-chromate ya rangi ya njano, Lead 2-ethylhexanoate, Lead molybdate, Lead naphthenate, Lead nitrate, Lead monoxide, Lead oxide, Lead octanoate, Lead peroxide, Lead sulphate, na Tri lead-bis (carbonate)-dihydroxide.

4 Global Alliance to Eliminate Lead Paint (GAELP), What is Lead Paint [Rangi yenye Madini ya Risasi ni nini], http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Lead_Cadmium/images/Lead-PaintFlyerJM121016_Web.pdf; Pia tazama Muongozo wa Kiutendakazi wa GAELP, aya za 6 & 7: http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Lead_Cadmium/images/GAELP_operational-framework-full-JM120725.pdf

Page 7: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 3

Ukusanyaji wa data kuhusu kiwango cha sumu ya risasi kwenye rangi katika mataifa yanayoendelea na yale yenye uchumi unaokaribia kustawi, ulianzishwa mwaka 1999 na makundi ya Vyuo vikuu pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs). NGOs nyingi zilianza kwa kuainisha na kuchanganua rangi za kuuzwa katika mataifa yao katika mwaka wa 2007 baada ya ripoti maradufu kutokea kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, hali iliyozua hofu kuhusu doli zilizopakwa rangi zenye madini ya risasi zilizotengenezewa barani Asia na kampuni kubwa za Amerika ya Kaskazini na Magharibi mwa Ulaya ili ziuzwe.

Katika miaka ya majuzi, NGOs zinazoshirikiana na IPEN pamoja na ny-inginezo zimechanganua zaidi ya aina 2,000 za rangi zilizonunuliwa ka-tika angaa mataifa 40 yenye uchumi mdogo na wa kadri.5 Katika mataifa kumi na mbili kati ya haya, tafiti hizi zilifadhiliwa na UNEP.6

Katika mataifa yaliyofanyiwa utafiti, pale ambapo hapakuwa na sheria au kanuni za kitaifa za kudhibiti kiwango cha madini ya risasi katika rangi na pale ambapo rangi yenye sumu ya risasi haikuwa hoja, nyingi ya rangi za kupaka zilizokuwa na enameli, zilikuwa na viwango vya sumu ya risasi vinavyozidi vipande 600 kwa milioni moja (ppm). Nyingi ya rangi zilikuwa na madini ya risasi inayo-zidi ppm 10,000 na hivyo zingepigwa maru-fuku kuuzwa au kwa matumizi katika angaa mataifa yote yaliyostawi. Katika matokeo hayo yote, hata hivyo, mteja hakuwa na njia ya kutofautisha ni rangi zipi zenye enameli zilizokuwa madukani ambazo zilikuwa na ma-dini ya risasi na zipi hazikuwa nayo.

5 Annex A ya kitabu hiki Inaorodhesha tafiti kuhusu rangi katika mataifa 40, tafiti nyingi ambazo ziliendeshwa na IPEN na NGOs shirika. Tafiti katika mataifa kumi na mawili ziliendshwa kwa ush-irikiano na UNEP. Dkt Scott Clark alisaidia IPEN kufanikisha tafiti nyingi.

6 Ibid.

Page 8: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

4

KUTAGUSANA NA MADINI YA RISASINA ATHARI ZAKE KWA AFYAKwa jumla watoto huwa hawatagusani na sumu ya madini ya risasi pale rangi hiyo inapokuwa kwenye gudulia/mkebe wake au rangi hiyo in-apopakwa kwenye kuta ambazo hazikuwa zimewahi kupakwa. Ila mtagu-sano na madini ya risasi kimsingi hufanyika baada ya rangi yenye sumu ya risasi kukauka kwenye ukuta au kwenye sehemu nyingineyo iliyopakwa rangi.

Baada ya muda, rangi iliyopakwa kwenye sakafu fulani hubambuka, ku-zeeka au kufifia. Hii hufanyika haraka iwapo sehemu iliyopakwa inakabili-ana na jua au inasuguliwa au kugusana (na vitu vingine kama vile madiri-sha na milango).

Madini yoyote ya risasi yaliyokuwa kwenye rangi hiyo inayofifia hudondo-shewa kwenye uchafu/vumbi na mchanga ulio kwenye nyumba au karibu na nyumba, shule, au maeneo mengineyo yaliyo mahali palipopakwa rangi. Ikiwa sakafu iliyokuwa imepakwa rangi yenye madini ya risasi imebambuliwa au kufutwa kwa matayarisho ya kupakwa rangi upya, kiwango kikubwa cha uchafu uliochanganyika na sumu ya risasi hutokea na kusambaa.

Kisha watoto wanaocheza ndani au nje ya nyumba hugusana na uchafu au mchanga huo na kisha kuuingiza mwilini kupitia shughuli zinazogu-sisha mikono kwenye mdomo. Iwapo uchafu wa nyumbani au mchanga umechanganyana na sumu ya risasi, watoto huingiza madini hayo mwil-ini. Shughuli zinazohusisha mkono na mdomo kugusana ni nyingi mion-goni mwa hasa watoto wenye umri wa miaka sita na chini yake, ambalo ni rika linalodhurika kwa urahisi na mtagusano na sumu risasi. Kwa kawaida mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja hadi sita huingiza mwilini kati ya miligramu 100 na 400 za uchafu utokao nyumbani na machanga kila siku.7

7 “The amount of soil and house dust that a typical 1–6-year-old child ingests is said to be 100 mg/24 h, but a more conservative estimate of 200 mg/24 h with an upper percentile of 400 mg/24 h has also been suggested.” World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, page 18. http://www.who.

Page 9: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 5

Katika matukio mengineyo, watoto huokota mibambuko ya rangi na kuiweka vinywani mwao moja kwa moja. Hali hii inaweza kuwa hasa na madhara kwa kuwa viwango vilivyomo kwenye mibambuko vinaweza kuwa vya juu kuliko vile vinavyopatikana katika uchafu au mchanga. Pale doli, samani za chumbani au vifaa vinginevyo vinapopakwa rangi yenye madini ya risasi, watoto wanaweza kutafuna vifaa hivyo na hivyo kuin-giza mwilini rangi kavu yenye sumu ya risasi. Hata hivyo, njia maarufu

int/ceh/publications/leadguidance.pdf (2010)

Istilahi za Rangi yenye madini ya Risasi

Kama zilivyotumika kwenye kitabu hiki:

• “Rangi” inajumuisha vanishi, lacquers, rangi zenye utomvu, enameli, rangi za kinamu, rangi ya awali au mipako inayotumiwa kwa madhumuni mbalimbali. Rangi kwa kawaida huwa mchanganyiko (mseto) wa utomvu wa resini, rangi asili, viimarisha rangi, viyeyushi, pamoja na kemikali/viungo vinginevyo.

• “Rangi yenye Madini ya Risasi” ni rangi ambayo aina moja au zaidi ya metali za risasi zimeongezwa.

• “Rangi asili za madini ya risasi” ni metali za madini ya risasi zinazotumiwa kuipa bidhaa ya rangi muonekano (rangi) wake.

• “Madini ya risasi kama kizuia kutu” ni metali za risasi zinazotumiwa kuzuia chuma kupata kutu au aina nyingi-nezo za kuchakaa.

• “Lead driers” are lead compounds used to make paint dry more quickly and evenly.

• “Madini ya Risasi kama kikaushi” inarejelea rangi ambazo zinatengenezwa kwa ajili ya kupakwa kwenye kuta za ndani au nje pamoja na sakafu za nyumba, shule, mijengo ya kibiashara na mingineyo kama hiyo. Rangi za kurembesha hutumiwa mara nyingi kwenye malango makuu, madirisha, pamoja na kupaka samani za nyumbani kama vile vitanda na madema ya watoto, meza na viti.

• “Rangi ya enameli” ni rangi inayotiwa mafuta au viyeyusho fulani.

• “PPM” Inamaanisha kiwango cha jumla cha madini ya risasi kinachohesabiwa kama sehemu (vipande) fulani ya milioni moja kwa kutumia kigezo cha uzani wake, katika rangi Iliyokauka.

Page 10: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

6

ya watoto kuingiza mwilini sumu ya risasi ni kupitia uchafu au mchanga wenye sumu ya risasi ambao hushika mikono yao.

Japo mtagusano na madini ya risasi pia una madhara kwa watu wazima, mtagusano na sumu ya risasi hudhuru hasa watoto hata inapokuwa katika viwango vidogo, na kwa jumla madhara yake ya kiafya huwa hayawezi ku-ponywa, hivyo basi kuzua athari ya kudumu.8 Uchanga wa mtoto, huvutia madhara makuu ya madini ya risasi, nao watoto wenye matatizo ya lishe hubwia madini ya risasi kwa kiwango kikubwa.9 Kitoto kilichomo tumbo-ni ndicho kilichomo kwenye hatari kubwa zaidi, na mwanamke mjamzito anaweza kukipokeza sumu ya madini ya risasi iliyokusanyika mwilini mwake. Madini ya risasi pia hupokezwa kupitia maziwa ya mama iwapo madini hayo yamo kwenye mama anayenyonyesha.

Pindi madini ya risasi yaingiapo mwilini mwa mtoto kupitia kumeza au kupumua au kupokezwa wakati wa ujauzito, yanakuwa na uwezo wa kuharibu mifumo na viungo kadhaa vya mwili. Viungo muhimu vinavyod-hurika huwa mfumo mkuu wa neva (uti wa mgongo) na ubongo, lakini pia madini hayo huweza kudhuru mfumo wa damu, figo na pingiti zima.

Imeafikiwa kwa jumla kuwa sifa hatari zaidi katika madini ya risasi ni uwezo wake wa kufifisha madini ya calcium katika mfumo wa kusambaza hisia, protini na kiambajengo cha mifupa, na kubadilisha utendakazi wake na umbo lake na hivyo kusababisha madhara makuu zaidi ya afya. Sumu ya madini ya risasi pia inajulikana kuathiri na kuharibu mfumo wa chem-bechembe (seli).10

Watoto wako katika hatari kuu ya kupata madhara ya madini ya risasi kuliko watu wazima kwa sababu mbalimbali, ikiwemo:11

• Ubongo wa mtoto mdogo hupitia ukuaji wa haraka, ustawi na uz-idishaji, nayo madini ya risasi huvuruga harakati hizi. Kwa mfano imeonyeshwa kwamba mtagusano wa kawaida wa kiwango cha madini ya risasi (5 hadi 40 ug/dL) mtu awapo mchanga unahusishwa na kupungua kwa kiwango cha sehemu ya kijivu ya mfumo wa neva miongoni mwa watu wazima. Kiasi cha kadri cha damu kimehusishwa na uwezekano wa juu wa kuvurugwa kiutambuzi na kiutendakazi, kuzua hisia kali, hasira na tabia za kitoto. Kupotea kwa sehemu ya kijivu kunahusishwa na mtagusano na sumu ya risasi.12 Kuharibika

8 Ibid., ukurasa 12.9 Ibid., ukurasa 48.10 Verstraeten, S.V., et al, Aluminium and lead: molecular mechanisms of brain toxicity, (Archives of

Toxicology 82:789–802. DOI 10.1007/s00204-008-0345-3, 2008)11 World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, http://www.who.int/ceh/publications/lead-

guidance.pdf, 201012 Cecil, K.M., et al., Decreased Brain Volume in Adults with Childhood Lead Exposure, (PLOS Medicine

Page 11: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 7

kwa ubongo kunakosababishwa na kutagusana na sumu ya risasi kwa kiwango hatari, cha chini, hakuwezi kurekebishwa na kutibiwa.

• Kutagusana na madini ya risasi mapema katika maisha ya mtu ku-naweza kupangua mpangilio wa chembechembe za jeni, hali ambayo inaweza kusababisha kuvurugika kwa utendakazi wa jeni na kuongeza hatari ya kupata magonjwa baadaye maishani. Kwa mfano mvurugo wa jeni unaotokana na mtagusano na madini ya risasi wakati wa ujauzito umehusishwa na ongezeko la ugonjwa wa kusahausahau almaarufu Alzheimer.13

• Mpenyo wa madini ya risasi mwilini kupitia kwa uoevu wa gesi katika matumbo hufanyika utotoni. Hadi asilimia 50 ya sumu ya risasi huingia mwilini mwa watoto, ukilinganisha na asilimia 10 ya watu wazima. (Wanawake wajawazito pia wanaweza kubwia sumu nyingi ya risasi ya iliyoingia mwilini kuliko watu wengine wazima.)14

(2008) 5(5): e112. DOI:10.1371/journal.pmed.0050112)13 Mazumdar, M., et al., Prenatal Lead Levels, Plasma Amyloid β Levels, and Gene Expression in Young

Adulthood, (Environmental Health Perspectives (2012) 120 (5))14 World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, http://www.who.int/ceh/publications/lead-

guidance.pdf, 2010

Mtagusano na Sumu ya Risasi hupunguza Kiwango cha akili

Mtagusano na madini ya risasi miongoni mwa watoto unaweza kupimwa katika viwango vya maikrogramu kwa desilita ya damu (µg/dL) au maikrogramu ya madini ya risasi kwa lita moja ya damu (µg/L). Katika upande wa chini wa mduara wa mtagusano na madini ya risasi, kuongezeka kwa kiwango cha madini ya risasi katika damu miongoni mwa mtoto mwenye umri wa kuenda shule kutoka chini ya 1 µg/dL hadi 10 µg/Dl kunahusishwa na kupungua pointi sita kwa kiwango cha werevu yaani IQ (Intellectual Quotient). Kwa watoto ambao kiwango chao cha madini ya risasi kiko katika viwango vya 10-20 µg/dL, hupoteza kati ya robo hadi nusu ya werevu wao kwa kila kuongezeka kwa 1 µg/dL ya sumu ya risasi katika damu. (World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, page 25, 2010)

Page 12: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

8

Kulingana na WHO: “Madini ya risasi hayana jukumu lolote muhimu mwilini mwa mwanadamu, na sumu ya risasi inachangia karibu 0.6% ya jumla ya magonjwa duniani.”15 Ushahidi wa kupungua kwa akili kunakosababishwa na sumu ya madini ya risasi kunakotokana na kuta-gusana kwake na madini hayo umelifanya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuorodhesha kudumaa kwa ukuaji wa akili kama ugonjwa unaot-ambulika. WHO pia inaorodhesha ugonjwa huo miongoni mwa magon-jwa 10 makuu ambayo mzigo wake wa kiafya kati ya watoto unatokana na sababu za kimazingira zinazoweza kubadilishwa.16

Katika miaka ya hivi majuzi, watafiti wa kimatibabu wamekuwa waki-orodhesha madhara kiasi ya kiafya miongoni mwa watoto kuanzia kwa wanaotagusana na kiwango cha chini cha madini ya risasi.17,18 Kulingana na Shirika la Afya Ulimwengunii: “Hakuna viwango salama vya sumu ya risasi vinavyojulikana.”19

15 World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, 2010, page 11: http://www.who.int/ceh/publi-cations/leadguidance.pdf

16 A. Prüss-Üstün and C. Corvalán, World Health Organization, Preventing Disease Through Healthy Environments: Towards an estimate of the environmental burden of disease, 2006, page 12: http://www.who.int/quantifying_ehimpacts/publications/preventingdisease.pdf

17 Herbert Needleman, Lead Poisoning,(Annual Review of Medicine 2004, http://www.rachel.org/files/document/Lead_Poisoning.pdf)

18 World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, page 26 (citing the work of Lanphear et al., 2000): http://www.who.int/ceh/publications/leadguidance.pdf, 2010

19 World Health Organization, Frequently Asked Questions, International Lead Poisoning Awareness Campaign, Week of Action, 19-25 October, 2014, page 1: http://www.who.int/ipcs/lead_campaign/faq_lead_poisoning_prevention_campaign_en.pdf?ua=1

Page 13: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 9

ATHARI ZA KIUCHUMI ZA MTAGUSANO NA SUMU YA RISASIMtoto mdogo anapotagusana na sumu ya risasi, madhara kwa mfumo wake wa neva huzidisha uwezekano kuwa mtoto huyo atakuwa na mata-tizo shuleni na pia atahusika katika vitendo vya hasira na ghasia.20 Mtagu-sano na madini ya risasi miongoni mwa watoto wadogo pia unahusishwa na ongezeko la viwango vya kuwa na hisia kali, kukosa kumakinika, kukosa kufuzu katika shule ya upili, tabia mbovu, kupotoka kwa watoto, matumizi ya dawa za kulevya na hata kufungwa jela.21 Madhara ya kuta-gusana na madini ya risasi huendelea maishani mote na huwa na athari ya kudumu kwa matokeo ya mtoto, na -kwa wastani – yanahusiana na kupungua kwa mafanikio ya kiuchumi kwa kigezo cha mapato ya muda mrefu maishani.

Utafiti wa hivi karibuni uliochungua athari za kiuchumi kwa watoto waliotagusana na madini ya risasi katika kiwango cha uchumi wa kitaifa miongoni mwa mataifa yenye uchumi mdogo na kadri ulikadiria jumla ya mzigo wa $977 bilioni dola za kimataifa22 kwa mwaka.23 Utafiti huo ulizingatia athari ya ustawi wa mfumo wa neva (neuro) miongoni mwa watoto waliotagusana na madini ya risasi, kwa vigezo vya kupungua kwa pointi za IQ, na ikahusisha mapungufu ya IQ yanayotokana na mtagusa-no na madini ya risasi miongoni mwa watoto na kupungua maishani mote kwa uzalishaji wa kiuchumi kwa kigezo cha mapato katika maisha yote ya mhusika. Utafiti huo ulitambua vyanzo vingi vya mtagusano na madini ya risasi miongoni mwa watoto, huku mtagusano na rangi yenye madini ya risasi ukubainika kuwa chanzo kikuu. Kwa viwango vya kimaeneo, mzigo

20 Mielke, H.W. and Zahran, S., The urban rise and fall of air lead (Pb) and the latent surge and retreat of societal violence ( Environment International. 43 (2012) 48-55)

21 World Health Organization, Childhood Lead Poisoning, ukurasa wa 28: http://www.who.int/ceh/pub-lications/leadguidance.pdf, 2010

22 Dola ya Kimataifa ni sarafu inayotumiwa na wanaiktisadi na mashirika ya kimataifa kulinganisha thamani ya sarafu mbalimbali. Hutumia dola ya Amerika kuakisi kiwango cha ubadilishanaji wa pesa, tofauti za uwezo wa kiuchumi (PPP) na bei ya wastani ya bidhaa katika kila nchi husika. Kulingana na Benki ya Dunia, “Dola ya Kimataifa ina uwezo sawa wa kiuchumi kwa kurejelea GDP na uwezo wa Dola ya Amerika nchini Amerika” Thamani za dola ya kimataifa katika ripoti hii zilikadiriwa kuto-kana na jedwali la Benki ya Dunia ambalo huorodhesha GDP kwa kila pato la wastani la raia katika nchi kutegemea tofauti za uwezo wa kiuchumi na kufafanuliwa kwa vigezo vya dola za kimataifa. Data kutoka katika jedwali (lililo katika: http://data.worldbank.org/indicator/NY.GDP.PCAP.PP.CD) ziliangaliwa na waandishi wa ripoti hii mnamo Februari 2012.

23 Teresa M. Attina and Leonardo Trasande, Economic Costs of Childhood Lead Exposure in Low- and Middle-Income Countries, (Environmental Health Perspectives; DOI:10.1289/ehp.1206424; http://ehp.niehs.nih.gov/1206424/ )

Page 14: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

10

wa kiuchumi wa mtagusano wa watoto na madini ya risasi kama unavyo-kadiriwa na utafiti huu ulipatikana kuwa:

• Afrika: $134.7 bilioni ya hasara ya kiuchumi au 4.03% ya Jumla ya Mapato (GDP)

• Amerika ya Kilatino na Karibi: $142.3 bilioni ya hasara kiuchumi au 2.04% ya GDP

• Asia: $699.9 bilioni ya hasara ya kiuchumi au 1.88% ya GDP

Page 15: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 11

VIANZO VYA MADINI YA RISASI KATIKA RANGIRangi huwa na sumu ya risasi pale mtengenezaji wake anapoongeza metali moja au zaidi ya madiniya risasi kimakusudi katika rangi yake kwa sababu fulani. Bidhaa za rangi pia inaweza kuwa na kiwango fulani cha madini ya risasi ikiwa viungo vya rangi vilivyochafuliwa na madini ya risasi vimetumika au uchafuzi unapofanyika kutokana na bidhaa nyingi-nezo zinazotengenezwa katika kiwanda hicho kimoja.

Metali za madini ya risasi zinazoongezwa kwenye rangi hasa huwa rangi asilia. Rangi asilia hutumiwa kuipa rangi mwonekano (rangi) wake; kuzuia rangi kupenyeza jicho (ndipo ishike vizuri); na kulinda rangi na ukuta/sakafu kuchakaa kunakosababishwa na jua. Rangi asilia zinazohu-siana na madini ya risasi wakati mwingine hutumiwa peke yake na wakati mwingine hutumika kwa pamoja na rangi nyingine asilia.

Metali za risasi pia zinaweza kuongezwa kwenye rangi zenye enameli (yenye mafuta) kwa matumizi ya kukausha (wakati mwingine zinaitwa vikaushi au vizidishaji). Rangi zenye enameli hukauka zikawa na sakafu ngumu na laini kupitia harakati inayojumuisha mgongano wa kemikali ambapo viungo vya rangi vinavyoitwa binders plymerize hukamatana. Vi-kaushi hivyo hutumiwa kama vizidishaji ambavyo huzidisha harakati hiyo na kuifanya rangi kukauka haraka na kwa ulaini zaidi. Metali za madini ya risasi zinazopotumiwa kama vikaushi, huwa hasa havitumiwa peke yake, ila huchanganywa na vikaushi vingine, ikiwemo metali za manganese, cobalt na kadhalika.

Metali za madini ya risasi wakati mwingine pia huongezwa kwenye rangi zinazotumika katika sakafu ya vyuma ili kuzuia kutu au kuchakaa. Maaru-fu kati ya hizi ni lead tetroxide, ambayo wakati mwingine huitwa red lead (madini mekundu ya risasi) au minium.

Rangi zisizoasilia, rangi-gundi na pia viungo vinginevyo vinavyotumika katika kutengeneza rangi zinaweza kupatikana kutokana na malighafi ya kiasilia, yanayopatikana ardhini na zinaweza kuwa zimechafuliwa zaidi au kidogo na madini ya risasi kutegemea sifa za kijiolojia katika eneo husika ambapo yaliyochimbwa. Viungo vilivyochafuliwa na madini ya risasi vinapotumika katika kutengeneza rangi, hivi vitachangia katika kiwango cha madini ya risasi kwenye rangi.

Tamati, mtengenezaji wa rangi anapotumia metali za madini ya risasi zilizoongezwa katika utengenezaji wa baadhi ya rangi zake (kama vile

Page 16: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

12

rangi za viwandani), rangi nyinginezo zinazotengenezewa hapo zinaweza kuchafuliwa na madini ya risasi iwapo utunzaji mzuri wa kiwanda hicho na utaratibu wa kukisafisha hautafuatwa.

Page 17: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 13

VIBADALA VYA MADINI YA RISASI KATIKA RANGIRangi asilia zilizokuwa na madini ya risasi, vikaushi na vizuia kuchakaa vimekuwepo kwa wingi kwa muda wa miongo mingi na hutu-miwa na watengenezaji wa rangi ya ubora wa juu. Mara nyingi, kwa kuepuka kutumia rangi asilia zenye madini ya risasi, vikausho vya madini ya risasi pamoja na metali nyinginezo zilizoongezwa katika kiwango cha kimataifa, mtengenezaji rangi hutengeza rangi yenye viwango vya madini ya risasi vilivyo chini sana ya 90ppm na ambayo in-aweza kuuzwa katika nchi nyinginezo duniani.

Panapotokea hali ambapo bidhaa yenye madini ya risasi imechunguzwa na kupatikana kuwa na kiwango cha madini ya risasi kinachozidi 90ppm, ila mtengenezaji wa rangi hiyo akawa anadai kuwa aliepuka matumizi ya metali za madini ya risasi yaliyoongezwa katika kiwango cha kima-taifa, chanzo cha madini hayo kinaweza kuwa kichafuzi kikuu cha kiungo kimoja au zaidi cha rangi hiyo. Viungo vilivyochafuliwa kwa kiwango kikubwa vinaweza kuepukwa kwa urahisi zaidi na mtengenezaji wa rangi ambaye hutumia harakati bora za kudhibiti na hiyo huwajuza wauzaji wake kuwa viungo vya rangi vilivyo na kiwango cha juu cha madini ya risasi havikubaliki.

Rangi ya Kunakshisha

Mataifa yaliyostawi zaidi katika bara la Amerika Kaskazini, Magharibi mwa Ulaya na kwingineko yamedhibiti kwa dhati kiwango cha madini ya risasi katika rangi zote za kunaksisha zinazouzwa na kutumiwa katika ma-taifa yao kwa miongo sasa. (Pia yamedhibiti kiwango cha madini ya risasi katika rangi zinazotumiwa kwenye doli za watoto na matumizi mengineyo yanayoweza kuchangia kutagusana kwa watoto na madini ya risasi). Hata bila kuwepo kwa sheria na kanuni mahsusi, baadhi ya watengenezaji rangi katika mataifa yenye uchumi mdogo au wa kadri, hutengeneza rangi zisizokuwa na sumu ya risasi zinazoshindana vyema katika masoko, mbali na kwamba viungo mbadala vinavyofaa vinapatikana kwa wingi.

Japo vizuizi vinavyohusishwa na kuangamizwa kwa viungo vyenye sumu ya risasi katika utengenezaji wa rangi za kutia nakshi vinaonekana kuwa

LEAD SAFE KIDSPromo Materials

Draft

Page 18: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

14

vichache, panaweza kuwapo vizuizi vya kiufundi au vya gharama vina-vyohusishwa na kuangamiza matumizi ya metali za sumu ya risasi katika baadhi ya kategoria za rangi ya viwandani. Kwa sababu hii na nyinginezo, serikali zinazowazia kukumbatia sheria, kanuni halali, viwango na/au harakati za kudhibiti utengenezaji, ununuzi, uuzaji na matumizi ya rangi yenye sumu ya risasi, umuhimu unaweza kupewa vidhibiti vinavyokabili-ana na rangi za nakshi na rangi za matumizi mengineyo ambazo zinaweza hasa kuchangia katika mtagusano wa watoto na sumu ya risasi. Hata hivyo, kiwango cha sumu ya risasi katika kategoria zote za rangi kinafaa kudhibitiwa.

Industrial Paints

Rangi zenye sumu ya risasi zinazotu-miwa katika baadhi ya shughuli za vi-wandani zimefahamika sana kuchangia mtagusano wa kikazi na sumu ya risasi miongoni mwa wafanyakazi. Kadhalika, kuna hali ambapo rangi za viwandani zenye sumu ya risasi zimechangia katika mtagusano wa watoto na sumu ya risasi (kwa mfano, wakati ambapo rangi za kiviwandani zenye madini ya risasi zinatumika visivyofaa kwenye vifaa vinavyotumiwa michezoni au kupakwa kwenye madaraja na mijengo mingineyo iliyo karibu na mahali ambapo watoto huchezea). Japo mataifa yaliyostawi zaidi hayana historia thabiti ya kudhibiti kwa dhati kiwango cha sumu ya risasi katika rangi zote za matumizi ya viwandani, hili linaonekana kuanza kubadilika.

Kuanzia mwezi Mei 2015, Muungano wa Ulaya utaanza kudhibiti kwa dhati utengenezaji na ununuzi kutoka nje ya nchi wa rangi asilia zenye sumu ya risasi na matumizi yake katika kategoria zote za rangi na mipako. Hili limechangia kwa watengenezaji wa rangi asilia barani Ulaya kukoma utengenezaji wa rangi asilia zenye sumu ya risasi kote barani Ulay,24 na bila shaka hilo litachangia watengenezaji wengine wa rangi ya matumizi

24 Uwasilishaji wa nafsi ya tatu wa maelezo kuhusu vibadala vya Matumizi kwa ajili ya Kuidhinishwa na BASF kwa shirika la European Chemicals Agency (ECHA): Nambari ya Mashauriano: 0012-01 to 0012-06 http://echa.europa.eu/documents/10162/18074545/a4a_comment_380_1_attachment_en.pdf

Page 19: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 15

ya viwandani wanaouza rangi zao barani Ulaya kukoma matumizi ya sumu ya risasi katika kutengeneza bidhaa zao zote za rangi na mipako.

Hata ingawa umuhimu unaweza kupewa vidhibiti vinavyoshughulikia rangi ya kutia nakshi pamoja na rangi za matumizi mengineyo ambazo zinaweza kuchangia watoto kutagusana na sumu ya risasi, rangi za kivi-wandani zenye sumu ya risasi pia zina madhara yanayoweza kuepukika na hivyo zinafaa ziondolewe haraka iwezekanavyo.

Page 20: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

16

MUONGOZO WA KUKOMESHA RANGI YENYE SUMU YA RISASIMkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya risasi nyeupe uliid-hinishwa katika Kongamano Kuu la Shirika la Kimataifa la Leba (ILO) na ukaidhinishwa na mataifa 63 tangu 1921. Mataifa mengi yaliyostawi kiviwanda yalipitisha sheria, kanuni mbalimbali na viwango vya lazima, zinazolenga kulinda afya ya raia katika miaka ya 1970 na 1980. Kwa jumla sheria hizi zinaharamisha utengenezaji, uagizaji, uuzaji na matumizi ya rangi ya risasi kupaka nyumba za makazi, shule na majengo mengine yanayotumiwa na watoto. Kulingana na viwango vilivyowekwa na Ameri-ka, rangi inayotumiwa kupaka majengo ya makazi na aina nyingi za rangi zinapaswa kuwa na kiwango cha sumu ya risasi ya kisichozidi 90 ppm. Mataifa mengine yamekumbatia viwango vya 90 au 600 ppm vya sumu hiyo ndani ya rangi.

Data kutoka tafiti zilizofanywa kuhusu rangi zinaonyesha kuwa katika mataifa ambako hamna sheria za kuharamisha sumu ya risasi, aina mbalimbali za rangi zinazounzwa huwa zimesheheni viwango vya juu vya sumu hiyo. Hii ni ithibati tosha kwamba uwepo wa sheria na kanuni husika huchangia pakubwa katika kudhibiti matumizi ya rangi yenye sumu ya risasi.

Mwongozo wa Kimataifa wa Kumaliza Rangi ya Sumu ya Risasi: Muungano wa Kimataifa wa Kukomesha Rangi ya Sumu ya Risasi (GAELP)

Katika kikao cha pili cha Kongamano la Kimataifa kuhusu Usimamizi wa Kemikali (ICCM) kilichofanyika mnamo 2009, masuala mengi ya kemikali yalitambuliwa kwa kauli moja kama ambayo yanayafaa kupewa umuhimu katika ngazi ya kimataifa. Mojawapo ya masuala hayo ilikuwa uwepo wa sumu ya risasi ndani ya rangi. Iliamuliwa kwamba suala hilo lichukuliwe kuwa suala ibuka la linalofaa kuundiwa sera kimataifa.25 Ku-fuatia uamuzi wa ICCM, Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP) na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kwa pamoja, yalibuni

25 http://www.saicm.org/images/saicm_documents/iccm/ICCM2/ICCM2%20Report/ICCM2%2015%20FINAL%20REPORT%20E.doc)

Page 21: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 17

ushirikiano kwa lengo la kukomesha utengenezaji wa rangi iliyosheheni sumu ya risasi. Hatua hii ililenga kulinda mazingira na afya ya umma.

Ushirikiano huo unaitwa Muungano wa Kimataifa wa Kumaliza Rangi ye-nye Sumu ya Risas (GAELP).26 Wajibu mpana wa GAELP ni kukomesha utengezezaji na uuzaji wa aina mbalimbali za rangi zilizoshehemu sumu ya risasi na hatimaye kuondoa madhara ya rangi kama hizo.27

Mwogozo wa Kitaifa wa Kukomesha Rangi zenye Sumu ya Risasi

Ni muhimu kwa serikali za mataifa mbalimbali kushughulikia tatizo la uwepo wa sumu ya risasi katika rangi kwa kuweka mfumo wa sheria wa kudhibiti utengenezaji, uagizaji, uuzaji na matumizi ya rangi za kunakshi-sha zenye sumu ya risasi ambazo zinaweza kupitisha sumu hii hadi kwa binadamu. Mifumo ya sheria ya kudhibiti matumizi ya rangi yenye sumu itatofautiana toka taifa moja hadi jingine. Lakini wadau kama vile seri-kali, kampuni za kutengeneza rangi na mashirika ya kijamii hushirikishwa katika uundaji wa sheria hizo.

Takriban mataifa yote yaliyostawi yana sheria au kanuni zilizoanza ku-tumika kuanzia miaka ya 1980 au kabla, kwa ajili ya kudhibiti viwango vya sumu ya risasi ndani ya rangi za kunakshisha. Mnamo 2008, kufuatia hofu kwamba watoto wangedhurika kutokana na sumu ya risasi pamoja na dhihirisho jipya la athari ya viwango vidogo vya sumu hiyo, Amerika ilibuni sheria iliyopunguza viwango vya sumu hiyo katika rangi kutoka 600 ppm hadi 90 ppm.28 Kiwango hicho kipya kinahusisha rangi na nakshi nyinginezo zinazotumika katika doli, na vifaa vingine ambavyo hutumiwa na watoto, na aina fulani za samani (fanicha). Sheria hiyo inahusu rangi zinazotumiwa kupaka majengo ya makazi, shule, hospitali, bustani, maeneo ya watoto kuchezea na majengo ya umma ambapo wateja wanaweza kutagusana na sakafu zilizopakwa rangi.29 Taifa la Canada pia limeidhinisha viwango hivyo vya chini vya sumu ya risasi katika rangi. Na mnamo 2009 Muungano wa Ulaya (EU) uliweka masharti makali kuhusu utengenezaji na matumizi ya rangi zenye sumu ya risasi.30 Katika mataifa ya Argentina, Uruguay na mataifa mengine, masharti ya hivi karibuni ni

26 http://www.unep.org/hazardoussubstances/LeadCadmium/PrioritiesforAction/LeadPaints/tab-id/6176/Default.aspx

27 http://www.unep.org/hazardoussubstances/LeadCadmium/PrioritiesforAction/GAELP/GAELPOb-jectives/tabid/6331/Default.aspx

28 United States Consumer Products Safety Commission, FAQs: Lead In Paint (And Other Surface Coat-ings) (http://www.cpsc.gov/en/Business--Manufacturing/Business-Education/Lead/FAQs-Lead-In-Paint-And-Other-Surface-Coatings/

29 Ibid.30 See European Chemicals Agency, Candidate List of Substances of Very High Concern for Authori-

sation: http://echa.europa.eu/candidate-list-table; For a short explanation see: FIRA; REACH Substance Sheet 4: http://www.fira.co.uk/document/reach-substance-sheet-4--lead-chromates.pdf

Page 22: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

18

kwamba kiwango cha juu cha sumu ya risasi kinachoruhusiwa kuwa ndani ya rangi za kurembesha vyombo vya matumizi nyumbani kinafaa kuwa 600 ppm. Pia mataifa hayo yamepiga marufuku utengenezaji na uagizaji wa rangi zilizosheheni viwango vya sumu ya risasi vilivyozidi kiwango hicho kilichowekwa.31

Katika mataifa mengine, Wizara ya Mazingira ama ile ya Afya zinaweza kuwa na mamlaka ya kutoa sharti, au amri ya kudhibiti viwango vya sumu ya risasi katika rangi mbalimbali. Mataifa mengi yameanzisha mipango mahsusi kuhusu Usimamizi wa Kimataifa wa Kimkakati kuhusu Usi-mamizi wa Kemikali (SAICM). Yanatekeleza mipango hiyo kupitia sheria mbalimbali na uanzishaji wa kamati zenye wawakilishi kutoka wizara mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha juhudi zao za kudhibiti sumu hiyo katika rangi. Katika baadhi ya mataifa, mashirika ya kukadiria viwango vya ubora wa bidhaa yana mamlaka ya kuamua kiasi cha sumu ya risasi ambacho kinapaswa kuwepo ndani ya rangi.

Ipo haja ya kupunguza madhara ya kiafya yanayosababishwa na sumu ya risasi ili kulinda jamii ambazo zimo katika hatari ya kudhurika na sumu ya risasi. Njia bora za kupunguza athari za sumu kwa mwanadamu zenye gharama ya chini ni kudhibiti kitaifa utengenezaji, uagizaji kutoka nje, uuzaji, matumizi na uuzaji nje wa rangi zenye sumu ya risasi. Aidha, sheria zinahitajika ili kuzuia matumizi ya rangi hizi kwa ajili ya kulinda binadamu na mazingira.32

Kabla ya kutengeneza au kurekebisha sheria za kudhibiti kiasi cha sumu ya risasi ndani ya rangi, serikali husika inapaswa kuangalia upya mahitaji yake ya wakati mahsusi. Utayarishaji wa sheria mpya utahitajika tu ikiwa sheria zilizopo hazitoshi kulinda afya ya umma.33 Mifumo ya kisheria na udhibiti inapaswa kuoanishwa na mfumo wa kisheria katika ngazi ya kitaifa kuhusu usimamizi wa kemikali.

Muungano wa Kimataifa wa Kumaliza Rangi yenye Sumu ya Risasi, un-apendekeza kuundwa kwa sheria na mifumo ya usimamizi itakayolenga kufanya yafuatayo:

• Kuzuia utengenezaji, uagizaji, matumizi na uuzaji nje wa rangi zenye sumu ya risasi;

31 For Argentina, see: ARG/166/Add.3 at: http://www.puntofocal.gov.ar/formularios/registro_arg04.php; For Uruguay see: http://www.mvotma.gub.uy/images/Decreto%2069-011%20Diario%20Ofi-cial.pdf

32 Global Alliance for the Elimination of Lead Paint, The Elements of a National Legal and Regulatory Framework for the Elimination of Lead in Decorative Paints, http://www.unep.org/chemicalsand-waste/Portals/9/Lead_Cadmium/docs/GAELP/GAELP%20Documents/NRFflyer-.pdf

33 Ibid.

Page 23: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 19

• Utayarisha wa mfumo maalum wenye njia bora ya kuhakikisha utekelezaji wa sheria hizo.

• Kuzipa asasi husika uwezo wa kuhakikisha sheria na/au kanuni husika zinatekelezwa.34

Ufuatiliaji na Uzingatiaji Sheria

Ingawa kuundwa kwa sheria ya kitaifa, kanuni, amri na viwango vya kudhibiti uwepo wa sumu ya risasi ndani ya rangi ni muhimu, hatua hiyo pekee haitoshi. Pia ni muhimu kutenga majukumu ya kutekeleza vipen-gee kadhaa vya sheria. Ni muhimu kujenga uwezo wa mashirika yenye majukumu ya kufanikisha utekelezaji wa sheria hizo, mbali na kuyapa rasilimali muhimu. Serikali za mataifa zinapaswa kubuni mipango ya uchunguzi inayojumuisha ukaguzi wa kila mara kuhakikisha sheria na kanuni zilizowekwa zinazingatiwa wakati wa utengenezaji na uuzaji wa rangi. Sampuli mbalimbali za rangi pia zinafaa kuchunguzwa kila mara ili kuhakikisha kuwa kiasi cha sumu ya risasi katika rangi hizo kinaafiki viwango vilivyowekwa.35

Harakati ya kukomesha rangi yenye sumu ya risasi pia inaweza kuchangi-wa na mikakati ya kujitolea kama vile mipango ya kuidhinisha na kuweka lebo rangi za kampuni nyingine za kiwango cha chini. Chini ya mpango huo kampuni zinazoshiriki hukubaliana kwamba hazitaweka sumu ya ri-sasi katika rangi zao. Pia kampuni hizo zinaweza kuafikiana kuuza bidhaa ambazo zina kiasi cha sumu ya risasi kisichozidi viwango vilivyoruhusiwa (kwa mfano, 90 ppm). Kampuni zitakazoshiriki katika mpango huu pia zitakubaliana kuweko lebo za idhini kwenye mikebe ya rangi zao kuonye-sha kuwa rangi hazina sumu ya risasi nyingi kupita kiasi kilichokubaliwa. Baadaye makundi ya wateja wa bidhaa hizo kwa ushirikiano na wadau wengine, watashirikiana kuwahimiza wateja kuzingatia lebo wanapocha-gua rangi. Itakuwa ni jukumu la wasimamizi wengine kuhakikisha kuwa rangi zinafanyiwa uchunguzi wa kila mara kuhakikisha kuwa zinaafiki viwango vilivyowekwa na sheria husika.

Hatua ya kampuni nyingine ndogo kuidhinisha rangi huzuia tofauti za vi-wango vya rangi za kampuni zinazouza rangi zisizokuwa na sumu ya risasi pale ambapo sharia za kitaifa zinahimiza hivyo, na rangi yenye sumu ya risasi pale ambapo hakuna sheria ya kudhibiti hilo, kama ilivyodhihirika katika utafiti uliofanywa Kusini mwa Asia.36

34 Ibid.35 Ibid.36 Toxics Link, Double Standard: Investigating Lead Content In Leading Enamel Paint Brands In South

Asia (http://toxicslink.org/docs/Double_Standard_Lead_Paint_29_June_2011.pdf)

Page 24: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

20

RANGI YENYE SUMU YA RISASI KATIKA MATAIFA YA CAMEROON, CÔTE D’IVOIRE, ETHIOPIA NA TANZANIAMnamo 2013, sampuli za rangi za kurembesha vyombo (za emameli) zilizokuwa zikiuzwa katika mataifa ya Côte d’Ivoire na Ethiopia zilic-hunguzwa ili kubaini kiwango cha sumu ya risasi ndani ya rangi hizo. Hii ilikuwa ni sehemu ya utafiti uliofadhiliwa na UNEP pamoja na IPEN.37 Sampuli ishirini za rangi zilikusanywa nchini Côte d’Ivoire na Shirika lisilo la Kiserikali la Jeunes Volontaires pour l’Environnement (JVE). Sampuli kumi na tatu kati ya sampuli hizo zote (yaani, asilimia 65) zil-ipatikana na sumu ya risasi iliyozidi kiwango cha 600 ppm. Sampuli tano (zinayowakilisha asilimia 25) zilibainika kuwa na kiwango cha sumu ya risasi kilichozidi 10,000 ppm.

Sampuli ishirini na tatu za rangi zilikusanywa nchini Ethiopia na NGO ijulikanayo kama Pesticide Action Nexus Association

(PAN). Sampuli 19 kati ya hizo (83%) zilikuwa na sumu ya risasi iliyozidi kiwango cha 600 ppm. Sampuli tano kati ya hizo (25%) zilibainika kuwa na kiwango cha sumu ya risasi kilichozidi 10,000 ppm.

Mnamo 2011, sampuli za rangi za kunakshisha zilizokuwa zikiuzwa sokoni nchini Cameroon zilichunguzwa ili kubaini viwango vya sumu ya risasi katika uchunguzi uliofadhiliw na NGO inayoendesha shughuli zake nchini humo kwa jina Centre de Recherche et d’Education pour le Développe-ment (CREPD) kwa ushirikiano na NGO nyingine kutoka Amerika (U.S) kwa jina Occupational Knowledge International (OKI).38 Sampuli 61 za chapa 15 tofauti za rangi zilinunuliwa. Sampuli 39 (yaani asilimia 64) zilibainika kuwa na kiwango cha sumu ya risasi kilichozidi vipimo vya 600 ppm. Sampuli 15 katika sampuli hizo (yaani asilimia 25) zilikuwa na kiwango cha sumu ya risasi kilichozidi vipimo vya 10,000 ppm.

37 UNEP and IPEN; Lead in Enamel Decorative Paints; National Paint Testing Results: A Nine Country Study, 2013: http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Mercury/Documents/publications/Lead_in_Enamel_decorative_paints.pdf

38 The Research and Education Centre for Development (CREPD); Lead Concentrations in New Resi-dential Paints in Cameroon, 2011 http://www.okinternational.org/docs/Report%20on%20Paint%20Sample%20Analyses%20FINAL%20English.pdf

Page 25: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 21

Mnamo 2009, sampuli za rangi mbalimbali zilizokuwa zikiuzwa sokoni nchini Tanzania zilichunguzwa kubaini viwango vya sumu ya risasi. Uc-hunguzi huo uliendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali kwa jina AGENDA for Environment and Responsible Development (AGEND).39 Sampuli ishirini kati ya sampuli hizo zilikuwa za rangi zinazotumiwa kupaka vyombo vya matumizi ya nyumbani. Sampuli 19 (yaani asilimia 95) kati ya sampuli hizo zilikuwa na kiwango cha sumu ya risasi kilichozidi vipimo vya 600 ppm. Tano kati ya sampuli hizo (yaani asilimia 25) zilikuwa na kiwango cha sumu hiyo kilichozidi vipimo vya 10,000 ppm.

39 Toxics Link and IPEN; Lead in New Decorative Paints; 2009: http://ipen.org/sites/default/files/documents/global_paintstudy-en.pdf

Page 26: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

22

HITIMISHORangi yenye sumu ya risasi ni hatari kwa afya ya mwanadamu, hasa rangi hiyo inapotumiwa mahala ambapo watoto wanaweza kutagusana na sumu hiyo.

Rangi za kunakshisha na zile ambazo hutumiwa katika bidhaa za watoto zinaweza kutengenezwa kwa njia rahisi bila kuweka chembechembe za sumu ya risasi, vikaushi vyenye sumu hiyo na kemikali za kuzuia kuchakaa.

Watengenezaji rangi wanaweza kubadilisha rangi za kurembesha wan-azotengeneza ili kuzuia matumizi ya chembembe za sumu ya risasi bila kushusha ubora wa rangi huku gharama ya uzalishaji ikiongezeka kwa kiasi kidogo mno.

Watengenezaji rangi ambao wakati huu wanatengeneza rangi za kunaksh-isha zenye sumu ya risasi na zile za kutumika katika shughuli nyinginezo ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya watoto, wanahimizwa kubadili-sha mbinu ya kutengeneza rangi hizo kwa kutotumia viungo (kemikali) zenye sumu ya risasi.

Miongozo ya Kisheria

Juhudi za kitaifa zinapaswa kuhimizwa ili kuwezesha ubunaji wa mion-gozo ya kitaifa ifaayo ili isaidie kudhibiti utengenezaji, uagizaji, uuzaji nje, uuzaji na matumizi ya rangi zilizo na sumu ya risasi na bidhaa zilizopakwa rangi zenye sumu hii. Kuwakinga watoto dhidi ya hatari inayosababishwa na rangi hizo kunafaa kupewa umuhimu wakati wa kuratibu mbinu na muda wa kutekeleza ukomeshaji wa rangi hizo.

Wakati wa kutayarisha mbinu za kumaliza utengenezaji na uuzaji wa rangi zenye sumu ya risasi, masuala ya uzingativu, usimamizi na utekelez-aji sheria husika yafaa kutiliwa mkazo.

Hamasisho kwa Umma

Kutokana na madhara ya utotoni ambayo sumu ya risasi inayo kwa mustakabali wa watu binafsi na taifa, pana haja ya kuanzisha kampeni za kuhamisisha kuhusu athari hizo katika nchi ambako uchunguzi umebaini kuwa rangi zenye sumu hii zinauzwa. Kampeni hizi zinafaa kufahamisha umma kuhusu hatari ya watu kufikiwa na sumu ya risasi, hasa watoto; uuzaji na matumizi ya rangi zenye sumu hii; rangi yenye sumu ya risasi kama chanzo cha kutagusana na sumu hii utotoni; na kuwepo kwa rangi nyingine zenye ubora unaofaa na salama kwa wanadamu. Pia pana haja

Page 27: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 23

kwa wananchi kufahamu umuhimu wa kuwa waangalifu wanaponakshi-sha kuta au vyombo kwa kuvipaka rangi upya; umuhimu wa wapakaji rangi kufundishwa kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya madhara pale wanapofanya marudio ya upakaji rangi; haja ya uwepo wa rasilimali za kuendesha mafundisho kama hayo.

Mashirika ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya ki-jamii, wataalamu wa kiafya na wadau wengine, wanahimizwa kuendesha uhamasishaji katika nyanja zilizotajwa hapo juu. Wadau wanahimizwa kupiga jeki juhudi za watengenezaji rangi, waagizaji na wauzaji, za kum-aliza matumizi ya sumu ya risasi katika bidhaa zao hata kabla ya kuanza kutekelezwa au kutumika kwa sheria yoyote ya kitaifa.

Juhudi za Kujitolea na Uwekaji Lebo

Katika mataifa mengine, baadhi ya watengenezaji wa rangi wameamzisha mikakati ya kijitolea kwa lengo la kukomesha utumiaji wa metali zenye sumu ya risasi wakati wa kutengeneza rangi zao. Watengenezaji rangi wote katika mataifa ambako hamna sheria za kudhibiti rangi ya sumu ya risasi, wanafaa kuhimizwa kujitolea kuondoa chembechembe za sumu hiyo wanapotengeneza rangi zao- hasa rangi zao zinazotumiwa kunakshi-sha bidhaa na rangi nyinginezo zinazoweza kupitisha sumu ya risasi kwa watoto na watu wengine.

Watengenezaji rangi pia wanahimizwa kushiriki, kwa kujitolea, katika mipango inayoendeshwa na mashirika mengine ya kuweka lebo za kuon-yesha kuwa rangi zao hazina sumu ya risasi. Hatua hii itawezesha wateja kutambua rangi ambazo hazina viwango vya juu vya sumu ya risasi. Vilevile, watengenezaji rangi wanaweza kutoa habari kwenye lebo za kufahamisha kuhusu hatari inayoweza kusababishwa na vumbi la sumu ya risasi linalotoka wakati wa utayarishaji wa eneo lililopakwa rangi zamani kwa upakaji upya.

Page 28: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

24

KIAMBATISHOTAFITI NA RIPOTI ZILIZOCHAPISHWA KUHUSU RANGI YENYE SUMU YA RISASI

Tafiti zifuatazo zilizochapishwa pamoja na ripoti zinatoa data kuhusu sumu ya risasi katika sampuli 2,349 za rangi zilizokusanywa na kuchan-ganuliwa katika mataifa 40.

Asia

Idadi ya sampuli za rangi zilizofanyiwa uchunguzi: 1,536 Idadi ya mataifa ambapo chunguzi kuhusu rangi zimeendeshwa: 12

Nchi Bra

shi z

enye

Su

mu

1

Su

mu

ya

Ris

asi K

atik

a R

angi

za

Ku

nak

shis

ha 2

Viw

ango

Vis

ivyo

tosh

ana:

Uch

un

-gu

zi w

a K

iwan

go c

ha

Mad

ini y

a R

i-sa

si (

Pb)

Kw

enye

Sam

puli

Maa

rufu

za

Ran

gi y

enye

En

amel

i En

eo la

A

sia

Ku

sin

i 3

Rip

oti y

a K

imae

neo

ya

Asi

a 4

Tafiti nyingine zilizochapishwa

Bangladesh 6 90

India 31 29 6 250 26Uchunguzi wa viwango vya sumu ya risasi katika rangi mpya za enameli katika nchi nne zenye historia tofauti za kudhibiti sumu ya risasi katika rangi5

72 Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enemeli za nyumbani, kutoka Asia, Afrika na Amerika Kusini6

24Kuzuia kuathiriwa na sumu ya risasi na & Matibabu: Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa katika Nchi Zinazoendelea7

25Sumu ya risasi katika rangi8

Indonesia 78 11Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli za matumizi nyumbani, kutoka Asia, Afrika, Asia, na Amerika9

Page 29: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 25

Nchi Bra

shi z

enye

Su

mu

1

Su

mu

ya

Ris

asi K

atik

a R

angi

za

Ku

nak

shis

ha 2

Viw

ango

Vis

ivyo

tosh

ana:

Uch

un

-gu

zi w

a K

iwan

go c

ha

Mad

ini y

a R

i-sa

si (

Pb)

Kw

enye

Sam

puli

Maa

rufu

za

Ran

gi y

enye

En

amel

i En

eo la

A

sia

Ku

sin

i 3

Rip

oti y

a K

imae

neo

ya

Asi

a 4

Tafiti nyingine zilizochapishwa

Nepal 6 49 24 Uchunguzi wa rangi ya sumu ya risasi nchini Nepal10

75 Sumu ya risasi katika rangi, Nepal11

Ufilipino 25 122

Sri Lanka 33 94

Thailand 27 120 31Iliripotiwa katika: Uchunguzi kuhusu athari katika afya ya mwanadamu na mazingira barani Asia na Pacific kuhusu biashara ya bidhaa zenye sumu ya risasi, cadmium na zaibaki (mercury), KiambatishoII12

China 64Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli kutoka Asia, Afrika na Amerika ya Kusini 13

58Sumu ya risasi katika rangi za nyumba: chanzo ambacho hakizingatiwi kama isababishayo hatari kwa watoto nchini China14

15Viwango vya sumu ya risasi katika Rangi za Enameli ya Nyumba nchini Taipei, Tai-wan vikilinganishwa na zile za China15

Lebanon 15 Ripoti ya Viwango vya Sumu ya Risasi katika Rangi za Kurembesha za Enameli nchni, Paraguay na Urusi16

Jordan 17Kuondoa sumu ya risasi katika rangi kupi-tia hamasisho na ufundishaji wa umma17

Page 30: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

26

Nchi Bra

shi z

enye

Su

mu

1

Su

mu

ya

Ris

asi K

atik

a R

angi

za

Ku

nak

shis

ha 2

Viw

ango

Vis

ivyo

tosh

ana:

Uch

un

-gu

zi w

a K

iwan

go c

ha

Mad

ini y

a R

i-sa

si (

Pb)

Kw

enye

Sam

puli

Maa

rufu

za

Ran

gi y

enye

En

amel

i En

eo la

A

sia

Ku

sin

i 3

Rip

oti y

a K

imae

neo

ya

Asi

a 4

Tafiti nyingine zilizochapishwa

Malaysia 72Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli zinazotumika kutoka Asia, Afrika na Amerika18

Singapore 41Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli zinazotumika nyumbani kutoka Asia, Afrika na Amerika Kusini19

Idadi ya jumla ya rangi

31 114 18 803 570

Page 31: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 27

Asia1 Toxics Link, Brush With Toxics; 2007: http://toxicslink.org/docs/lead_in_paints/Lead_in_Paints_

Brush_with_toxics.pdf2 Toxics Link and IPEN; Lead in New Decorative Paints; 2009: http://ipen.org/sites/default/files/

documents/global_paintstudy-en.pdf3 Toxics Link; Double Standard: Investigating Lead Content In Leading Enamel Paint Brands In South

Asia, 2011: http://toxicslink.org/docs/Double_Standard_Lead_Paint_29_June_2011.p4 The results of national studies carried out in 2012 and 2013 are summarized in: IPEN; Asia Regional

Paint Report, Dr. Sara Brosché et al,2014: http://ipen.org/sites/default/files/documents/Asia%20Regional%20Paint%20Report%20final.pdf

5 C. Scott Clark, et al, Examination of lead concentrations in new decorative enamel paints in four countries with different histories of activity in lead paint regulation, Environmental Research; Ac-cepted 7 March 2014

6 Clark, C.S., Rampal, K.G., Thuppil, V., Roda, S.M., Succop, P., Menrath, W., Chen, C.K., Adebamowo, E.O., Agbede, O.A., Sridhar, M.K.C., Adebamowo, C.A., Zakaria, Y., El-Safty, A., Shinde, R. M., and Yu, J. (2009) Lead levels in new enamel household paints from Asia, Africa and South America, Environmental Research 109:930-936. {Includes data for China, India, Malaysia and Singapore presented in Clark et al (2006) Environmental Research 102:9-12.; and data for Nigeria presented in Adebamowo, Clark et al (2007) presented in Science of the Total Environment 388:116-120.)

7 Van Alphen, M. (1999) Lead in Paints and Water in India, pgs. 265-272, in Lead Poisoning Preven-tion & Treatment: Implementing a National Program in Developing Countries, A.M. George (Ed), The George Foundation, Bangalore, India.

8 Johnson S, Salkia N, Sahu R (2009) Lead in Paints, Centre for Science and Environment, PML/PR-34/2009, New Delhi India.

9 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.10 Ram Charittra Sah and Kameshwar Yadav, Study of Lead Paints in Nepal, by; 201011 Perry Gottesfeld et al, Lead in new paints in Nepal, by; EnvironmentalResearch132 (2014); 70–7512 UNEP, Study on the possible effects on human health and the environment in Asia and the Pacific

of the trade of products containing lead, cadmium and mercury, Annex II. 2010;,http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Lead_Cadmium/docs/Trade_Reports/AP/UNEPLeadPb-CaicedoCompila-tion110601.pdf

13 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.14 Lin G Z, Peng R F, Chen Q, Wu Z G, Du L (2008) Lead in housing paints: an existing source still not

taken seriously for children lead poisoning in China, Environmental Research 109, 1-5.15 Ewers L, Clark C S, Peng H., Roda Sandy M, Menrath B, Lind C, Succop P (2011). Lead Levels in

New Residential Enamel Paints in Taipei, Taiwan and Comparison with Those in Mainland China, Environmental Research 111:6, 757-760.

16 IPEN and University of Cincinnati, Report on Total Lead Concentration (ppm) of New Enamel Deco-rative Enamel Paints in Lebanon, Paraguay and Russia; (2012)

17 IPEN and Land and Human to Advocate Progress (LHAP), Phasing out lead in paint through advo-cacy and awareness raising; 2010; http://ipen.org/sites/default/files/documents/LHAP%20final%20ISIP%20Lead%20in%20Paint%20report.pdf

18 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.19 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.

Page 32: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

28

Africa

Idadi ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi: 450 Idadi ya nchi ambako chunguzi kuhusu rangi ziliendesha: 14

Nchi

Sumu ya Risasi Kwe-nye Rangi za Kurembesha 20

Sumu ya risasi katika Rangi za Enameli za Kurembe-sha21 Tafiti nyingine zilizochapishwa

Tanzania 26

Afrika Kusini 29

Nigeria 30

Senegal 30

Kenya 31 Sumu ya Risasi Katika Rangi za Nyum-bani Kenya22

Cameroon 61Viwango vya sumu ya risasi na Uwekaji Lebo Rangi, nchini Cameroon23

Uganda 50 Ukusanyaji wa Rangi zenye Sumu ya Risasi, Uganda24

Cote d’Ivoire 30

Ethiopia 30

Ghana 30

Tunisia 30

Misri 20Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli kutoka Asia, Afrika na Amerika Kusini25

Nigeria 25Viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli kutoka Asia, Afrika na Amerika Kusini 26

Ushelisheli 28Viwango vya sumu ya risasi katik rangi za enameli kutoka Asia, Afrika na Amerika Kusini 27

Idadi ya Jumla ya Rangi

115 120 215

Page 33: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 29

Africa20 Toxics Link and IPEN, Lead in New Decorative Paints, 2009: http://ipen.org/sites/default/files/docu-

ments/global_paintstudy-en.pdf21 UNEP and IPEN, Lead in Enamel Decorative Paints; National Paint Testing Results: A Nine Country

Study, 2013: http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Mercury/Documents/publications/Lead_in_Enamel_decorative_paints.pdf

22 Nganga C, Clark S, Weinberg J (2012), Lead in Kenyan Household Paint, September, 2012, iLima, Nairobi, Kenya, University of Cincinnati http://ipen.org/sites/default/files/documents/lead%20in%20kenyan%20household%20paint%20sept.%202012.pdf

23 P. Gottesfeld , G. Kuepouo , S. Tetsopgang & K. Durand (2013): Lead Concentrations and Labeling of New Paint in Cameroon, Journal of Occupational and Environmental Hygiene, 10:5, 243-249

24 UNETMAC and IPEN Collection of Lead Based Paint Samples in Uganda, 2010 http://ipen.org/documents/isip-report-collection-lead-based-paint-samples-uganda

25 Clark, C.S., Rampal, K.G., Thuppil, V., Roda, S.M., Succop, P., Menrath, W., Chen, C.K., Adebamowo, E.O., Agbede, O.A., Sridhar, M.K.C., Adebamowo, C.A., Zakaria, Y., El-Safty, A., Shinde, R. M., and Yu, J. (2009) Lead levels in new enamel household paints from Asia, Africa and South America, Environmental Research 109:930-936. (Includes data for China, India, Malaysia and Singapore presented in Clark et al (2006) Environmental Research 102:9-12.; and data for Nigeria presented in Adebamowo, Clark et al (2007) presented in Science of the Total Environment 388:116-120.)

26 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.27 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.

Amerika Kusini28 Toxics Link and IPEN; Lead in New Decorative Paints; 2009: http://ipen.org/sites/default/files/

documents/global_paintstudy-en.pdf29 UNEP and IPEN; Lead in Enamel Decorative Paints; National Paint Testing Results: A Nine Country

Study, 2013: http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Mercury/Documents/publications/Lead_in_Enamel_decorative_paints.pdf

30 C. Scott Clark, et al, Examination of lead concentrations in new decorative enamel paints in four countries with different histories of activity in lead paint regulation, Environmental Research; Ac-cepted 7 March 2014

31 IPEN and University of Cincinnati, Report on Total Lead Concentration (ppm) of New Enamel Deco-rative Enamel Paints in Lebanon, Paraguay and Russia (2012)

32 Clark, C.S., Rampal, K.G., Thuppil, V., Roda, S.M., Succop, P., Menrath, W., Chen, C.K., Adebamowo, E.O., Agbede, O.A., Sridhar, M.K.C., Adebamowo, C.A., Zakaria, Y., El-Safty, A., Shinde, R. M., and Yu, J. (2009) Lead levels in new enamel household paints from Asia, Africa and South America, Environmental Research 109:930-936. (Includes data for China, India, Malaysia and Singapore presented in Clark et al (2006) Environmental Research 102:9-12.; and data for Nigeria presented in Adebamowo, Clark et al (2007) presented in Science of the Total Environment 388:116-120.)

33 Clark, C.S. et. al., Environmental Research, loc. cit.

Page 34: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

30

Amerika Kusini

Idadi ya sampuli za rangi zilizofanyiwa uchunguzi: 206 Idadi ya nchi ambako chunguzi kuhusu rangi ziliendeshwa: 8

Nchi

Sumu ya risa-si katika rangi za urembe-shaji 28

Sumu ya risasi katika Rangi za Enameli za Urembeshaji29 Tafiti nyingine zilizochapishwa

Mexico 30

Brazil 31 20 Examination of lead concentra-tions in new decorative enamel paints in four countries with dif-ferent histories of activity in lead paint regulation30

Paraguay 15 Report on Total Lead Concentra-tion (ppm) of New Enamel Decora-tive Enamel Paints in Lebanon, Paraguay and Russia31

Argentina 30

Chile 30

Uruguay 30

Ecuador 10Lead levels in new enamel house-hold paints from Asia, Africa, and South America32

Peru 10Lead levels in new enamel house-hold paints from Asia, Africa, and South America33

Idadi ya Jumla ya rangi

61 90 55

Page 35: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

Komesha Sumu ya Madini ya Risasi katika Rangi: Linda Afya ya Watot (2015) 31

Ukanda wa EECCA

Idadi ya sampuli za rangi zilizofanyiwa uchunguzi: 157 Idadi ya nchi ambako chunguzi kuhusu rangi ziliendeshwa: 6

Nchi

Sumu ya risasi ka-tika rangi za urembe-shaji34

Sumu ya risasi katika Rangi za Enameli za Urembe-shaji35 Tafiti nyingine zilizochapishwa

Belarus 30

Urusi 15 Ripoti kuhusu viwango vya Sumu ya Risasi (ppm) katika Rangi Mpya za Enameli za Urembeshaji, katika nchi za Lebanon, Para-guay na Urusi36

Azerbaijan 30

Kazakhstan 26 Uchunguzi wa viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli za katika mataifa manne zenye historia tofauti katika usi-mamizi wa rangi zenye sumu ya risasi37

Kyrgyzstan 30

Armenia 26 Uchunguzi wa viwango vya sumu ya risasi katika rangi za enameli za katika mataifa manne zenye historia tofauti katika usi-mamizi wa rangi zenye sumu ya risasi38

Idadi ya Jumla ya rangi

30 60 67

Ukanda wa EECCA34 Toxics Link and IPEN, Lead in New Decorative Paints, 2009: http://ipen.org/sites/default/files/docu-

ments/global_paintstudy-en.pdf35 UNEP and IPEN, Lead in Enamel Decorative Paints; National Paint Testing Results: A Nine Country

Study, 2013: http://www.unep.org/chemicalsandwaste/Portals/9/Mercury/Documents/publications/Lead_in_Enamel_decorative_paints.pdf

36 IPEN and University of Cincinnati, Report on Total Lead Concentration (ppm) of New Enamel Deco-rative Enamel Paints in Lebanon, Paraguay and Russia, (2012)

37 C. Scott Clark, et al, Examination of lead concentrations in new decorative enamel paints in four countries with different histories of activity in lead paint regulation, Environmental Research; Ac-cepted 7 March 2014

38 C. Scott Clark, et al, loc. cit.

Page 36: KOMESHA SUMU YA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA …

www.ipen.org

[email protected]

@ToxicsFree

GEF (www.thegef.org) ni zao la juhudi za ushirikiano wa kima-taifa ambapo nchi 183 zinafanya kazi pamoja na taasisi za kimatai-fa, mashirika ya kijamii na sekta ya kibinafsi, kwa lengo la kushu-ghulikia masuala ya kimazingira ulimwenguni.

UNEP (www.unep.org) ndiyo kipaza sauti cha masuala ya mazin-gira katika Umoja wa Mataifa (UN). UNEP hutekeleza wajibu wa mtetezi, mfundishaji na mshirikishi katika uendelezaji wa masuala ya kimazingira ulimwenguni.

IPEN (www.ipen.org) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) la kima-taifa linalofanyakazi kwa ushirikiano na mashiriki 700 yanayoen-deleza sera na shughuli kuhusu matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kulinda afya ya mwanadamu na mazingira. Mashirika hayo yanaendesha kazi hii katika mataifa 116 ulimwenguni.