62

Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

  • Upload
    others

  • View
    49

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab
Page 2: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

kitabu cha saumu

Kimeandikwa na:

Sayyid Muhammad Mahdi al-Musawy

Kimetolewa na Kimechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam - Tanzania

Page 3: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

Haki za kunakili imehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9976 956 21 5

Toleo la kwanza 1967, Nakala 3,000 Toleo la Nne 1987, Nakala 5,000 Toleo la Tano 2005, Nakala 2,500

Kimetolewa na Kuchapishwa na:BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM - TANZANIA

Page 4: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

YALIYOMO MLANGO 1 : SAUMU

Faida kwa kiwiliwili; Faida kwa roho; Faida kwa mwenendo na utamaduni; Faida kwa imani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2

MLANGO 2 : FADHILA YA RAMADHANI NA SAUMUFadhila ya Ramadhan; Fadhila ya Kufunga; Kumcha Mungu; Amali bora kabisa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8

MLANGO 3 : DARAJA ZA SAUMUDaraja ya kwanza; Daraja ya pili; Daraja ya tatu . . . . . . . . . . . . . . . 13

MLANGO 4 : SHURUTI ZA KUFUNGAShuruti za kufunga; Wakati wa kuweka nia;Walioruhusiwa wasifunge . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .16

MLANGO 5 : MAMBO YAVUNJAYO SAUMUMambo yavunjayo Saumu; Mambo yenye karaha . . . . . . . . . . . . . . 21

MLANGO 6 : NAMNA ZA SAUMUSaumu za faradhi; Saumu za haramu; Saumu za makruhu;Saumu za sunna . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25

MLANGO 7 : DUA NA AMALI ZA USIKUDua za kila siku; Dua za kufuturia; Th awabu ya Kufuturisha; Fadhila ya Laylatul-Qadri, Amali za Laylatul-Qadri; Amali za kumi ya mwisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .31

MLANGO 8 : KULIPA SAUMU NA KAFFARAMahala ambapo ni wajibu kulipa saumu tu; Maelezo ya kafara ya Ramadhani; Kafara ya saumu yaQadha; Kaff ara ya kuvunja kiapo, nadhiri au ahadi . . . . . . . . . . . . . 39

Page 5: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

MLANGO 9 : MATOKEO MUHIMU KATIKA MWEZI WA RAMADHAN . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 42

MLANGO 10 : MCHANGANYIKO WA MAMBO MUHIMU(a) Madhambi makubwa; (b) Itikafu; (c) Alama na njia za thibitisho za kuanza na kumalizika mwezi . . . . . . . . . . . . . . 45

MLANGO 11: ZAKAT-UL-FITRIAl-Fitra; Shuruti za kufaradhisha mtu kutoa zaka ya Fitri; kadri na kiasi cha zaka ya Fitri; wakati wa kutoa zaka ya Fitri; Matumizi ya zaka ya Fitri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .50

MLANGO 12 : SALA YA IDIMaelezo ya Sala ya Idi; Namna ya kusali; Dua ya Qunuut . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 54

Page 6: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

1

Mateuzi Kutoka Dibaji ya Chapa ya Kwanza

BISMILLAAHIR RAHMAANIR-RAHEEM

Kwa jinsi kitabu hiki kina maelezo na mafundisho ya maana juu ya kufunga na maamrisho yake, hata inambidi kila Mwislamu na asiye Mwislamu kuwa na kitabu hiki, na kukisoma, na hasa wale wanaotaka kujua Uislam.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa taufi ki ya kukitunga kitabu hiki ili wapate faida watu, na namwomba Mola kwa utukufu wa Muhammad na Ahlu Baiti wake (a.s.) na kwa baraka ya siku ya leo tukufu ya kuzaliwa Imam wetu Ameerul-Mumineen Ali (a.s.) mwezi kumi na tatu ya Rajab 1387 al-Hijra, anikubalie kwa takabali njema na aniwekee akiba yangu siku ya Qiyama. Na naomba kwa Mola atupe taufi ki mimi na Waislamu wote kuyafuata yaliyomo humu.

Vile vile napenda kumshukuru sana Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa kuchukua taabu ya kuipanga kwa uzuri milango na maelezo ya kitabu hiki.

al-Ahqar Muhammad Mahdi Musawy13th Rajab, 1387 DAR ES SALAAMI8th October, 1967

*****

Dibaji ya Chapa ya Pili

Chapa ya kwanza ya kitabu hiki kilitolewa mwisho wa 1971. Kwa jinsi kilivyopendwa hata katika muda ya miaka 24 nakala zote zikauzikana, lakini bado watu wanavitaka.

Kwa hiyo Bilal Muslim Mission inakichapisha kwa mara ya pili. Safari hii maelezo na Masail yote yamesahihishwa kwa mujibu wa Fatwa za Mujtahid wetu Ayatullah Agha e Sayyid Abul Qasim al-Khoui Dama-Dhilluhul Aali.

DAR ES SALAAM

Page 7: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

2

BISMIL-LAA-HIR-RAHMAA-NIR-RAHEEMNasoma kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha na kurehemu

MLANGO 1SAUMU

Saumu (kufunga) ni kitu gani na vipi inatubidi kufunga?

Maana ya saumu inavyoelezwa katika kitabu cha lugha (Kamusi) ni kujizuia kufanya jambo fulani. Na maana yake kwa kisharia ni hii:- Mtu kujizuia kutwa na mambo yafuatayo yanayovunja saumu; kuanzia alfajiri ya pili iitwayo Subh-Saadiq hadi magharibi ya kisharia.1

Ukikaribia kuja mwezi mtukufu wa Ramadhani, utawaona watu wengi wameshughulika kuandalia huo mwezi mtukufu kwa furaha, vile vile (utawagundua) utawaona baadhi ya watu wanatafuta masingizio ya kutokufunga. Laiti wangefi kiria faida ya kufunga na makusudio yake, ijapokuwa udhuru wenyewe wenye maana, na akajaribu kufunga. Ikiwa anafahamu fadhila na faida ya roho ambayo hupatikana kwa kufunga tu bila shaka hatawacha saumu hata siku moja.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wenye baraka nyingi, na bwana wa miezi yote, na huitwa mwezi wa Mwenyezi Mungu. Katika mwezi huu

1 Subh-Saadiq ni weupe wa mchana unaonekana kwenye mstari wa upeo wa macho upande wa mashariki wenye kutanuka kwa upana, na kuzidi kua mweupe mpaka linapotoka jua, na ndio wakati ambapo huwa haramu kula na kila kinachovunja Saumu kwa mwenye kutaka kufunga.Magharibi: Kwa kawaida magharibi ni wakati jua linapozama na kufi chika upeo wa macho, na kwa sharia ni wakati ule wekundu unaonekana upande wa mashariki baada ya kuzama juu ufi ke sawa na utosi mbinguni.

باسم االله تعالى

Page 8: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

3

Mwenyezi Mungu anawafungulia viumbe wake milango ya rehema, na rehema hizo kuwafi kia na huwazingia viumbe wake. Basi ndugu zangu tufanye bidii kama tuwezavyo tuziteke hizo baraka na rehema za mwezi huu. Neema bora na kubwa ya mwezi huu ni hiyo ya kufunga saumu.

Hakika mwezi wa Ramadhani huwazindua na kuwaamsha katika usingizi waovu na wahalifu na kuwatanabihisha kuyafahamu na kuyafuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu (mwenye hekima) ili kuepukana na yaliyo katazwa na dini ya Kiislam, wapate kujitenga nafsi zao kwa kutenda maovu, na kukimbilia kwa Mola wao, kwa kusali, kusoma dua, kulisha na kufanya utiifu mwingi.

Walevi wengi huwacha kulewa mwezi wa Ramadhani na wafasiki na waovu wengi hawatubii ila katika mwezi wa Ramadhani, na wasio amini wengi hawaoni huruma nyoyoni, lakini ukiingia mwezi huu mtukufu huruma inawajia na hulainisha nyoyo, na wenye mali (matajiri) wengi wasiowaonea huruma masikini ila ukiingia mwezi mtukufu ndipo huonyesha huruma.

Unapoingia mwezi wa Ramadhani tu basi huingia baraka, heri, na utiifu. Usiku na mchana wake hunawirika na kung’aa kwa ibada na utiifu wa watu. Misikiti na mahala pa ibada hujaa wachamungu wanaosujudu na kurukuu na huku wakiomba waghufuriwe. Wengine hushughulika kuisoma Qur’ani usiku na mchana, na kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mwenye huruma kwa nyoyo za unyongezi iliyo safi , huku macho yakilia na wakimwomba kwa sauti ya huzuni.

Huu ndio mwezi mtukufu wenye uzuri na jamala na kuwa bora kuliko miezi yote. Katika mwezi huu wanatubia wenye kutaka kutubia, na wanaomba kughufuriwa wenye kutaka kughufuriwa, na huo ndio msimu wa wenye kufanya ibada. Basi ewe mwenye kufanya ibada hima kimbilia kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu.

Usije mwezi mtukufu huu ukapita, ila nawe uwe na tamaa ya kuwa umekwisha ghufuriwa.

Page 9: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

4

Ewe tajiri, masikini, mwenye miliki, mkulima, na waungwana wakubwa na wadogo, msiwadhulumu walio chini yenu na msishindane na wakubwa wenu.

Ewe, mwislamu mahala popote ulipo, kimbilia kufanya mema ya kumridhisha Mola na Mtume, na pia waridhishe Maimamu “Maasumin” (a.s.) kwani mwezi huu ni mwezi ule ambao Mwenyezi Mungu huyafuta madhambi na huongeza juu ya hayo thawabu kwa viumbe, na huinua daraja zao; basi tukimbilie kumridhisha Mola, tukimbilie kufanya ibada, na tukimbilie kutubia kwa Mwenyezi Mungu.

Tukitaka kueleza kwa urefu manufaa yote ya saumu kwa kiwiliwili, kwa tabia na mwenendo, kwa roho, na kwa dini, itakuwa taabu sana. Hapa tutatoshelea kueleza kwa ufupi kwa kutoa mifano tu.

Faida kwa KiwiliwiliNi maalumu kwamba kiwiliwili cha binadamu ni kama mashine ambayo huhitajia mapumziko kidogo. Na mapumziko hayo hayawezi kupatikana hadi mtu ajizuie kula na kunywa kwa muda ambao ala ya kuyeyusha chakula (tumbo) itulie. Vile vile upatie moyo na vifaa vyote vya ndani mapumziko na kujisafi sha vyenyewe. Basi kwa kufunga saumu hupungua, na pengine hutoka kabisa maradhi.

Elimu ya afya siku hizi imethibitisha kwamba mtu kuweka siha yake vizuri, inampasa kwa uchache afunge saumu, siku moja katika kila wiki, au wiki moja kila mwezi na bora mwezi mmoja kila mwaka.

Vile vile imethibitisha elimu za sasa kwamba bidii za akili na nguvu ya mwili huzidi kwa kuuweka mwili katika hali ya njaa. Bila shaka faida na maendeleo yanaweza kupatikana kwa kufunga saumu, kuliko mtu anapokuwa amejaa tumbo na uvivu pia umemshika. Madaktari na matabibu katika maradhi mengi huwaongoza wagonjwa wao kufunga. Yapo baadhi ya maradhi kama mtu akifunga saumu tu, badala ya kutumia dawa, atapona kabisa. Baada ya kujua na kufahamu hayo yote, basi tutapata hakika kuwa

Page 10: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

5

Mwenyezi Mungu kwa njia na taratibu bora kabisa ametuamrisha kuwacha kula; na kitendo hicho kakifanya kuwa ni Ibada. Huu ni uthibitisho dhahiri wa huruma juu ya viumbe wake, isitoshe haya kakifanya hicho kitendo (kufunga) si faida ya duniani tu, bali kwa akhera pia. Juu ya hayo yote ikiwa tutahalifu, tutakuwa watu wajinga mno, tusio na mfano kwa kuzisahau hisani zake.

Si vibaya hapa tukisema kwamba baada ya kujua faida ya saumu kwa kiwiliwili, basi mtu haifai kwake ukifi ka usiku ale chakula kwa wingi kulipia njaa ya mchana, au kula vitu ambavyo vizito kwa tumbo na vyaweza kumletea taabu na maradhi. Kwa hiyo ni bora sana kutumia chakula chepesi anapofuturu ili apate faida kwa kiwiliwili na roho.

Faida kwa RohoTunaelewa vizuri kwamba makusudi ya kuumbwa kwetu ni kutupatia kufi kia ukamilifu wa roho. Na kwa ajili ya kutimiza makusudi hiyo roho kuelekea upande wa juu wa utakatifu; vile vile inapasa roho iangalie huku utaratibu na usalama wa kiwiliwili. Anapokuwa mtu yu macho, tena madhali tumbo lake limejaa, basi roho haijaliwi kupata wasaa kuelekea upande wa Mola kwa vile umeshughulika na mambo ya mwili; inaziwilika kuipata shabaha ya kuumbiwa kwake. Kwa hivyo mtu akifunga mchana kiwiliwili kinakuwa chepesi, na tukifanya mazowea usiku pia tule chakula chepesi na kiasi cha dharura tu, hapo roho itapata wasaa na faragha kwa upesi. Ijapokuwa kwa muda huo mdogo wa mwezi mmoja mfululizo bila ya taabu itaweza kushikamana uhusiano wake wa juu kwa furaha na kupata daraja tukufu za akhera.

Faida kwa Mwenendo na UtamaduniWapo viumbe wengi humu duniani ambao hawakupata chakula cha shibe yao; hao ni watu wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa fungu katika mali ya matajiri, na Mola amesema hivi: “Mali ni mali yangu na maskini ni watu wangu wa nyumbani, na matajiri ni wajumbe (wakili) wangu”. Matajiri na wenye mali hawawezi kuhisi na kujua taabu ya njaa inavyowapata maskini; ndipo Mwenyezi Mungu akafaradhisha saumu juu ya matajiri na maskini, ili

Page 11: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

6

matajiri waone taabu ya njaa, na wapate kujua inawapata taabu gani katika nyoyo za maskini na wahitaji. Imam Jafar as-Sadiq (Imam wa sita) amesema: “Saumu imefanywa faradhi kwa ajili ya kuwafundisha usawa katika kujionea njaa na kiu kati ya watu wote, wala hakuna tafauti kati yao, na vile vile matajiri wahisi maumivu ya njaa (hata wapate kuwasaidia na kuwahurumia kikweli maskini)”.

Mwezi wa Ramadhani huwazoeza watu utaratibu na kawaida katika maisha. Tunawaona wanafuturu kwa wakati mmoja kama wanavyojizuia kwa yavunjayo saumu kwa wakati mmoja pia.

Hakika mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kufungamana, wa ukarimu na upaji, ikiwa kuna uadui kati ya Mwislamu na mwenziwe, kama ugomvi au kuachana usuhuba, basi katika mwezi huu mtukufu hufanya bidii ya kupatana, na kuanza kupendana na kufanyiana hisani. Kwa kufahamu kwamba katika mwezi kama huu mtukufu na adhimu mtu hujipatia thawabu zaidi kwa kuwa ni mmoja katika aamali nzuri zenye kutukuka na kumfaa hapa duniani na kesho akhera. Th ibitisho juu ya jambo hili tunaona katika hadithi za Mtume (s.a.w.) alizohutubia kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, anasema hivi: “Enyi watu, mwenye kumfuturisha aliyefunga katika mwezi huu hupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu ya kumweka huru mtumwa na kughufi riwa madhambi yake yote yaliyopita.” Akasimama sahaba mmoja akasema: “Yaa rasula-llah, Siwote kati yetu twaweza kufanya hivyo (kufuturisha).” Mtume (s.a.w.) akajibu: “Jilindeni na moto (wa Jahannam) kwa nusu ya tende, jilindeni na moto kwa kumnywesha maji” Yaani, ikiwa huna uwezo wa kulisha basi hata nusu tende, au kunywesha maji kutafi dia.

Madhumuni na shabaha ya mambo hayo ni kuwafanya Waislamu wawe pamoja, na wapendane na kwa umoja wao waepuke na maovu na uchoyo, na kujipendelea raha ya binafsi, na hilo ni lengo kubwa la Islam.

Faida kwa ImaniMwenyezi Mungu kwa kuamrisha kufunga mwezi huu, ametayarisha

Page 12: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

7

mafundisho ya kuzoeza ugumu na taabu. Tunaelewa sote kwamba watu wanaokwenda kuchukua mafundisho ya aina yeyote, wakati wanapochukua hayo mafundisho hawawi na raha, bali wanapambana na taabu na mashaka mengi na inawabidi kustahimili. Kwa mfano, mwanajeshi anapokwenda kuchukua mafundisho usiku na mchana, saa ishirini na nne humpita kwa ilhali hafahamu; kula, kunywa na mambo yote inakuwa chini ya mipango na kanuni, wakati wa kulala na kuamka umewekwa, majaribio na kazi ngumu lazima kufanya. Huchukuliwa masafa makubwa kupita majabalini na misitu na mahala pa hatari, chakula na tandiko begani, mara mbio mara pole pole mara anahema, masikini huyo mwana jeshi lazima avumilie; pengine kwa uchovu anapenda kukaa, miguu imekuwa mizito, kwa hali hiyo yote yule mkuu wa amri (Commanding Offi cer) kumwona yule mwana jeshi katika hali hii pia haoni huruma bali humwamrisha ‘Quick March’. Kwa nini hivyo? Huyo mkuu anafanya hivi kwa kuwa ni adui wake? Sivyo, bali anamtakia katika mafundisho hayo ya taabu azowee kuvumilia ili wakati wa kazi ya ujeshi na kuwa askari wa vitani hata akipata taabu yeyote itakuwa ameshazoea na itakuwa kwake kutekeleza ni rahisi na kwa furaha ataifanya.

Vile vile Mwenyezi Mungu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati mtu amefunga, vitu vilivyo halali tumefanyiwa haramu. Kitu kama kula na kunywa ambavyo ni dharura ya maisha tumekatazwa. Ladha na mambo ya kufurahisha ambayo wakati mwingine ni ruhusa kuyafanya na labda baadhi ya wakati kutenda kwake ina thawabu, lakini siku hizi (Ramadhani) imekatazwa na imeharamishwa. Kwa nini? Yote haya tunafundishwa na kuzoweza kutii na kufuata maamrisho ya Mola, kujizuia na mambo mazuri na ya halali; katika mwezi huu tunafundishwa utiifu, na majaribio hayo yaendelee muda wa mwezi mmoja. Vile vile tujue kwamba Mwenyezi Mungu kadiri vitu alivyoturuhusu kufanya ni hisani yake Mola juu yetu, kama si hivyo angeweza vitu hivyo kuviharamisha maisha; lakini fadhili na upaji wake vitu vingi ametuhalalishia na kidogo sana ametuharamishia.

Kwa vyovyote utaratibu na utii huu katika mwezi wa Ramadhani, inatufundisha na kutupa faida ya kuvumilia kwa kujitenga na vitu vilivyo

Page 13: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

8

haramishwa na visivyofaa kufanya. Ikiwa kwa mwezi mmoja tunaweza kujitenga na vitu vya dharura na halali, basi baadaye kujitenga na vitu vya haramu na visivyodharura bali vyenye kudhuru roho na kiwiliwili tutakuwa na taabu gani?

Basi usemi wa Mwenyezi Mungu katika Qur’ani kwamba, “Imefanyiwa faradhi mfunge, ili mumche Mwenyezi Mungu (mwogope Mola).” Tuseme binadamu kwa baraka na utukufu wa Ramadhani, sehemu moja katika sehemu kumi na mbili (1⁄12) ya mwaka anapitisha katika uchaji na utii wa Mwenyezi Mungu, ni kama mtu ambaye sehemu ya kumi na mbili ya maisha yake ameishi utiini. Kwa hivyo ikiwa tumechukua faida sahihi ya kweli yamajaribio ya mwezi wa Ramadhani, basi siku zilizobaki tunaweza kustahiki kupata maridhio ya Mola, na sehemu ya kumi na mbili ya maisha ikazidi hadi ikafi ka nusu au maisha yote; lakini shuruti lilioko ni hili kuwa ule uvumi na ustawi na maombolezo uliokuwa nao katika kumtii Mola, athari na matokeo yake baadaye uendelee, usiwe mchemko wa soda unapofungua chupa kuchemka baadaye ikatulia.

MLANGO 2FADHILA YA RAMADHANI NA KUFUNGA

Hapa tunaeleza baadhi ya utukufu na fadhila za mwezi wa Ramadhani. Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani hivi:-Shah-ru-ramadana al-ladhee unzila fee-hil-quran hudal-lin-naa-si wa-bay-yi-naa-tim minal-hudaa wal-fur-qan (2:185)“Mwezi huo wa Ramadhani ambao hii Qur’ani ndipo imeteremshwa kuwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na ubatili)”.

Qur’ani ni kipimo baina ya haki na ubatili, na ni mizani ya kuangalia uzuri na ubaya. Kwa sababu kila kitendo na amali, ukiweka mbele ya Qurani, ikiwa

Page 14: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

9

inawafi kiana na Qur’ani basi hiyo ni haki na nzuri, na ikiwa haiafi kiani basi ni batili na mbaya.

Mtume (s.a.w.) alisema katika hotuba yake aliyohutubia kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Ijumaa ya mwisho wa Shabani (na iliyopokewa kwa Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s.) aliyoipokea kwa baba zake watukufu (a.s.) kutoka kwa Amir al-Muminin) hivi:“Ay-yuhan-nass In-nahu qad aq-bala ilay-kum shah-rul-laah bil-bara-kati war-rah-mati wal-magh-fi rah. Shah-run huwa in-dal-laah af-dha-lush-shu-huur wa ay-yaa-muhu af-dha-lul, ay-yaam; wa layaa leehi af-dha-lul layaa-lee wa saa-aatu-hu af-dha-lus-saa-aat; wa ama-lukum fee-hi maq-buul; wa du-a-akum feehi mus-ta-jaab. Fas-alul-laa-ha rab-bakum bi-niy-yaa-tin saa-diqa, wa qu-luu-bin, taa-hira an yuwaf-fi qa-kum lisiyaa-mihi wa ti-laa-wati ki-taa-bih, fain-nash-sha-qiy-ya man hur-rima ghuf-raa-nal-laahi fi haa-dha-ash-sha-ril-adheem”.

“Enyi watu, hakika mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu (Ramadhani) umekukabilini (umewadia) kwa Baraka, Rehema, na maghfi ra: Mwezi ambao kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko miezi yote; mchana wake ni bora kuliko mchana wote; na usiku wake ni bora kuliko usiku wote; Na saa zake (mchana na usiku) ni saa bora kabisa; na amali mtayoifanya inakubaliwa, na Dua mtazo ziomba zitakubaliwa. Basi mwombeni Mola wenu kwa nia ya ukweli (halisi), na nyoyo safi akuafi kini mfunge mwezi huu, na kusoma Qur’ani. Kwani hakika “Shaqiy” mkosefu ni yule ambaye atakosa kughufi riwa na Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu. Bila shaka mtu atakayekosa kughufi riwa na Mwenyezi Mungu katika mwezi huu ndiye “Shaqee” mpotevu na dhalili”.

Unapoingia mwezi mtukufu wa Ramadhani watu hujifunga kwa Ibada, utii, kufanya mema, na kila jambo la kheri kwa kiasi cha uwezo wao.

Fadhila ya KufungaMwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani tukufu:

Page 15: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

10

Yaa ayyuhal-ladhina aa-manu kutiba alay-kumus-siya-amu kamaa kutiba alal-ladhina min qab-likum; La’allakum tat-taquon; Ay-yaa-mam maa-duu-daat. (2:183-4)“Enyi mlioamini! mumefaradhishiwa kufunga saumu kama waliyo faradhishiwa wale walio kutangulieni, ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu. (Mfunge) siku maalum za kuhesabika. . . .”.

Zile siku maalum ndio mwezi huu wa Ramadhani ambao umefaradhishwa kufunga. Husemwa kwamba hekima ya kuainishwa mwezi huu wa Ramadhani minghairi (pasipo) ya miezi mingine ni kuwa Mwenyezi Mungu ameeneza uongozi wake katika mwezi huu, juu ya viumbe wake wote kwa jumla, na juu ya Waislamu kwa halisi alipoteremsha Qur’ani, kama tulivyo eleza mbele.

Katika hadithi iliyopokewa kwa Amir al-Muminin Ali (a.s) inasemwa: “Mtu wa kwanza ulimwenguni aliyefaradhiwa kufunga saumu ni baba yetu Adam (a.s.). Maana yake si kwa nyie Waislamu ndio mmefaradhishiwa kufunga tu, bali mtu wa kwanza, na umma wote waliopita, walifaradhishiwa kufunga, lakini tunatafautiana kwa wakati na namna ya kufunga.”

Katika mwisho wa aya 183, (la-al-lakum tat-taquun), yaani mjizuie (mwepukane) na uovu na Maasi, kwani inavunja nguvu ya matamanio ambayo ni sababu na njia kubwa ya maasi kama ilivyo katika hadithi (man lam yas-tati-il-baah fal-ya-sum), maana yake: asiyejiweza kujizuia na mambo ya matamanio basi afunge kwani saumu hupigana na mambo ya matamanio. “TAQWA” hasa inatoka moyoni na ni hali halisi ya roho iliyochanganyika na hadhari na hofu kumcha Mungu.

Umuhimu na fadhili za saumu hazina mfano wala makisio. Mwenyezi Mungu katika “Hadithul Qudsi” (hadithi takatifu) anasema as-swawmu lee wa ana ajzee alayhi, (Saumu hasa ni yangu na mimi ndiyo nitakaye toa jazaa na thawabu yake). Maana yake thawabu ya kufunga ina jinsi nyingi na adhimu, hata Malaika hawezi kukadiria au kujua kiasi cha thawabu yake. Basi Ibada kwa kiasi ilikuwa adhimu hata tukipata kidogo takalifu, tusifi kiri kitu bali tuteketeze inavyotakikana ili tustahiki kuipata jaza hiyo.

Page 16: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

11

Sababu na maana ya kufunga saumu ina thawabu adhimu kama hiyo yawezekana kuwa ni hii. Mwenye kusali anaposali anaweza kuonekana na watu wengine; kuhiji na kupigana jihadi (vita vya dini) huwa mbele na pamoja na watu hutendeka na wengine pia wakaweza kuona; kutoa khums na zaka au sadaka kwa vyovyote kama hawakujua watu, yule mustahiki maskini unayempa hiyo zaka atajua! Hivyo hivyo tukichukua Ibada zote lazima mtu au watu watajua; na katika Ibada hizo zote inaweza kuwa mtu kumwingia Riya (kujipendekeza) kuonesha watu. Lakini kufunga saumu ni Ibada ile ambayo haitakiwi jambo lolote kudhihirisha, bali inatosha kufanya nia tu na kujizuia na baadhi ya mambo. Kwa hiyo mpaka mtu aliyefunga asidhihirishe kuwa amefunga, mtu mwingine hawezi kujua kama fulani amefunga. Vile vile ni shida sana kwa mfunga saumu kumwingia Riya (kutaka kujipendekeza). Kwa yote hayo ndipo Mwenyezi Mungu kuita Ibada hii ya kufunga kuwa hasa ni yake, na kumjazi mwenye kufunga Yeye Mwenyewe.

Wapo baadhi ya watu miongoni mwetu, siku akifunga utamwona amenuna;utafi kiri kwa kufanya Ibada hiyo amewafanyia hisani wengine! Isitoshe haya, utaona kaghadhibika na watu wa nyumbani na watumishi, amejaa na uchungu! Hajijui maskini, kwa kufanya hivyo ile shabaha halisi kuwa ni Ibada ya siri inapotea; na watu wote wa mtaa wanajua kuwa fulani amefunga, kwa sababu leo anahamaki na kila mtu! Hakika tukitaka tufunge saumu kikweli kweli, basi lazima tuepukane na tabia mbaya kama hiyo, tuwe wapole na wenye huruma zaidi juu ya watu wa nyumbani na watumishi tunapofunga.

Zimepokewa hadithi nyingi kutokana na Mtume (s.a.w.) na Ahlul Bayti wake pamoja na Maimamu kumi na mbili (a.s.) juu ya Saumu, na kuhimiza kufunga, maelezo juu ya hekima za saumu, siri na adabu za mfungaji, na thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu. Hata mtu akiyaona maelezo au kuyasikia hayo atashangaa kwa kuona wingi wake.

Hapa tutaeleza zile hadithi zinazohimiza kudumisha na kushikilia kufunga, tulizozipata katika kitabu mashuhuri kinachoitwa, Wasail al-Shia.

Page 17: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

12

Imepokewa hadithi kwa Imam as-Sadiq (Imamu wa sita (a.s)) isemayo kwamba, Mwenye kufunga (Saumu) anakuwa katika ibada, hata kama amelala (anapata thawabu ya ibada) lakini ikiwa hakumsema mtu.

Vile vile imepokewa hadithi kwamba Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenye kuifi cha saumu (asihubiri mtu kama amefunga), Mwenyezi Mungu anawahubiri Malaiki hivi, ‘Kiumbe wangu ametaka alindwe na adhabu yangu, basi mlindeni’”. Mwenyezi Mungu amewaweka Malaika wakiamrishwa kumwombea mtu yeyote; hapana budi ila dua hiyo hukubaliwa.

Kumcha Mungu: Amali Bora KabisaAmali gani bora kabisa kutenda katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani?

Kila mmoja hujibu kwa mujibu wa maarifa yake na kiasi cha fi kra na elimu zake. Lakini ni bora mno tutazame na tuyafahamu maneno ya hotuba aliyoitoa Mtume (s.a.w.) katika Ijumaa ya mwisho wa Shabani kuwapa Waislamu maelezo, fadhila, utukufu na ufanyaji bora wa amali katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Anasema Amir al-Muminin Ali (a.s): Baada ya kumaliza Mtume (s.a.w.) hotuba hiyo, “nikasimama na nikamwuliza, ‘Ya Rasuu-lallaah, Amali gani bora kabisa katika mwezi huu mtukufu?’ Akajibu, ‘Uchaji wa Mwenyezi Mungu kwa kila kilichoharamishwa na kukatazwa’”.

Hakika uchaji ijapokuwa ni neno fupi na dogo, lakini maana na muradi wake ni kubwa mno na vigumu kwa vitendo. Kwa hivyo kusali suna, kufanya Ibada, kusoma Qur’ani, kulisha, kuvisha na mambo mengi yote ya kheri hayawezi kuwa sawa kabisa na Uchaji wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yote hayo ni sehemu moja ya uchaji nayo ni suna, lakini kujitenga na madhambi na alichoharamisha Mwenyezi Mungu ni jambo la wajibu, si mwezi wa Ramadhani tu bali maisha yake mtu yote, Mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwa kila alichoharamisha na kukataza, tutasema kwa yakini amefanya amali bora kuliko yote katika mwezi huu. Na hapana shaka akizifanya baada ya amali zote zingine suna zilizotajwa kuwa bora, basi mtu huyo kapata bahati nzuri sana. Tunaomba kwa Mwenyezi Mungu, kwa wasila ya Mtume wake (s.a.w.)

Page 18: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

13

na Ahlul Bait zake (a.s.), kwa baraka ya mwezi huu mtukufu awape Waislamu wote uwezo wa kufi kiria kumcha Mwenyezi Mungu, (Na kwa sadaka ya hao wote, mimi mtungaji pia asinisahau). Amini.

MLANGO 3DARAJA (VYEO) ZA SAUMU

Saumu (kufunga) ina daraja tatu:

Daraja ya Kwanza: Ni kwa watu wote, na hiyo ni kujizuia na vitu vinavyovunja saumu, navyo ni kumi, kama tutavyoeleza baadaye. Na daraja hizi za saumu faida yake hasa ni kuondoa Wajibu wako tu, na kujiepusha na adhabu iliyowekwa na Mwenyezi Mungu kwa wale wasiofunga. Lakini tusitoshelezwe na hayo tu, bali tujitahidi tuzipate daraja za mbele kama tuwezavyo ili tupate faida ya roho na baadhi ya thawabu waliowekewa wafunga saumu. Mtume (s.a.w.) amesema, “Katika vitu rahisi zaidi, alivyofaradhisha Mwenyezi Mungu juu ya mwenye kufunga katika kufunga kwake, ni kuwacha kula na kunywa”.

Wakati wa saumu hii, kama tulivyoeleza, huanzia Subh Sadiq mpaka Magharibi. Baadaye, mfunga ameruhusiwa kuvunja saumu yake.

Daraja ya Pili: Kufunga kwa mahsusi (ya peke yake) na hiyo ni kwanza kujizuia yavunjayo saumu yale kumi, na juu ya hayo kujizuia viungo vyake na mambo yaliyoharamishwa. Zimepokewa hadithi nyingi sana za Mtume (s.a.w.) na za Maimamu (a.s.) zinazotilia mkazo za kuhimiza jitihada kwa kila mwenye imani kuwa anafunga saumu kama hivyo na awe anajiepusha viungo vyake vyote kwa kila dhambi na ubaya aliokataza Mwenyezi Mungu viumbe wake.

Anahadithia sahaba Bw. Muhammad bin Ajlaan, kwamba amemsikia Imam

Page 19: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

14

Jafar as-Sadiq (a.s.) anasema, “Kujizuia kula na kunywa tu hakuitwi kufunga siyamu, lakini ukifunga, ujifunge masikio, macho, ulimi, tumbo, utupu wako pia, na uzuie mikono na miguu yako pia, kwa kila kinachokatazwa, na ujaribu kukaa kimya kama uwezavyo ila kwa jambo la kheri na uwe mpole na mtumishi wako”.

Aina hii ya saumu haimaliziki unapokucha jua; kwa sababu mwislamu haruhusiwi kutenda dhambi wakati wowote. Kwa hivyo wakati wa saumu ya daraja hii huanzia siku mtu anapobaleghe, na huishia wakati wa kufa kwake, kwani kanuni za sharia ni ya kufuatwa maisha yote ya binadamu.

Lakini saumu namna hiyo huharibika ikiwa mtu atatenda dhambi yoyote. Mtume wetu (s.a.w.) alimwona mwanamke mmoja aliyefunga saumu anamtukana mtumishi wake. Hapo Mtume akaagiza chakula na akamtaka yule bibi ale. Yule mwanamke akasema: “Yaa Rasuulal-llah, nimefunga mimi”. Mtume akamjibu: “Hukufunga, kwa sababu umemtukana mtumishi wako”.

Amehadithia sahaba mmoja wa Imam al-Baqir (a.s.) kwamba Imam alisema, “Uongo humfuturisha aliyefunga, na tazamo la pili2 na udhalimu kidogo au mwingi, yote hayo bila shaka humharibia saumu mfunga”.

Na zaidi ya hayo, Dini ya Kiislaam inampendelea kila Mwislamu, kwa kila ubaya na taabu atakayofanyiwa, aikabili na kustahimili kwa wema, hasa anapokuwa amefunga, kwa heshima ya saumu, na kujipatia hiyo daraja tukufu ya saumu.

Imepokewa kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba Mtume (s.a.w.) amesema, “Hakuna Kiumbe aliyefunga akiamka asubuhi na kuamkia huku anatukana na kusema nimefunga basi yule anaetukanwa akavumilia matusi hapo Mwenyezi Mungu huwaambia Malaika, ‘Mtumwa wangu kajilinda na saumu 2 Tazamo la Pili”. maana yake tazamo la haramu juu ya mwanamke asie wako. Binadamu

inapoanguka nadhari yake ya kwanza kwa ghafl a, au kwa kusahau, au kosa kujua, juu ya mwanamke (asie wake) au kitu kilichoharamishwa kutazama, na akitazama tena mara ya pili, basi hilo tazamo la pili ni haramu, asitazame.

Page 20: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

15

mbele ya Mtumwa mwenziwe, basi Nyie Malaika mlindeni na moto wangu wa Jahannam na mtieni Peponi” (Maana ya kujilinda na saumu ni kuwa isingekuwa yule mtu aliyetukanwa amefunga, angeliweza kulipa matusi, lakini kaikabili kwa utulivu kwa taadhima ya ile saumu); Kwa kuwa thawabu zote za kufunga saumu, na daraja na cheo cha akhera, vilivyo wekewa kwa ajili ya wanaofunga daraja hii, ndivyo mfunga saumu hujitenga na kila alichoharamisha Mwenyezi Mungu.

Basi binadamu juu ya kujizuia nafsi yake na madhambi, afanye juhudi awezavyo kupata wema wote ambao umsaidie mtu kuwa karibu na Mola. Lazima afanye bidii kutenda amali ya heri kwa nia safi .

Daraja ya Tatu: Kufunga mahsusi zaidi, naye kuepukana na kujitenga na yenye kuvunja saumu, na kila kilicho haramishwa na juu ya hayo kutenga moyo na tabia mbaya na dhamiri ya uovu, na mawazo ya mambo ya Dunia.

Mwenye kufunga saumu ya daraja hii bila shaka moyo wake husafi ka na kila kitu; hashughulikii jambo lolote isipokuwa la Mwenyezi Mungu; na anaondoa moyoni mahaba ya kila kitu kwa ajili ya mahaba ya Mola.

Daraja hii imeelezwa katika aya hii ya Qur’ani: Quli-llahu Thumma dhar-hum fee khawdhihim yal-aaboona (6:91) Sema: Mwenyezi Mungu (ndiye aliyekiteremsa); kisha waache wacheze katika porojo lao.

Kufunga hivi hawezi mtu isipokuwa yule aliye mwepusha Mwenyezi Mungu, kama Mitume na Maimam (a.s.).

Saumu hii haina kuishia na kumalizika. Roho tukufu ya Wali wa Mwenyezi Mungu hukaribia zaidi kwa Mola baada ya kifo, na usafi wake hukamilika zaidi. Kwa hivyo saumu namna hii haina kufuturu.

Page 21: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

16

MLANGO 4SHURUTI ZA KUFUNGA NA KUSIHI KWAKE

Huwa wajibu kufunga saumu juu ya watu wote kwa shuruti hizi:-1. Kwa kila Mwislamu aliye baleghe3, mwanamume au mwanamke, ni wajibu

afunge.

Na siwajibu kufunga kwa mtoto ijapo mwenye akili na anayepambanua; lakini huyo mtoto akifunga ni thawabu sana, na inawapasa wazee wa wazoeze watoto wao kufunga, ili wawe tayari kutimiza wajibu wao wakiwa wakubwa (baleghe). Mtoto yeyote akibaleghe wakati wa Ramadhani siku yeyote ile itampasa kufunga siku zote zilizobaki za mwezi tangu kubalehe, na siku zilizopita (kabla ya kubaleghe) ikiwa hakuzifunga haidhuru neno (kwani haikuwa fardhi juu yake). Ikiwa amebalehe kabla ya alfajiri, ni fardhi juu yake siku hiyo aanze kufunga, na ikiwa baada ya alfajiri kabaleghe na siku ile amefunga kwa thawabu tu, hapo ni lazima juu yake aendelee na hiyo saumu na haruhusiwi kufuturu mchana.

2. Katika shuruti za kufunga ni kuwa na (Akili); si wajibu (fardhi) mwenda wazimu kufunga.

3. Awe na siha (asiwe na ugonjwa wa kumdhuru saumu wakati anapojizuia kula na kunywa).

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’an tukufu:Wa Man Kaana Maree-Dhan Aw Alaa Safarin Fa-Id-Datum-Min Ay-Yaa-Min Ukhar. (2:185)“Na atakayekuwa mgonjwa (kwa maradhi yale ambayo akifunga saumu 3 Alama za ubalehe ni moja katika hizi tatu :

a. Kutoka manii (shahawa) macho au usingizini. Alama za kupambanua (kufafanua) manii, kwa mtu mzima (asiye mgonjwa) ni tatu. Kwanza, bidii ya moyo inapotoka shahawa. Pili, kumwaga kwa nguvu (kufoka). Tatu, ulegevu wa mwili baada ya kutoka.

b. Kuwa nywele nene (za kukwaruza) chini ya kitovu, juu ya dhakari. c. Kutimia umri miaka kumi na tano (15). Na alama ya ubalehe wa mtoto wa kike ni

kuingia miaka ya kumi (10) katika umri.

Page 22: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

17

itamdhuru au anahofi a kumdhuru au akifunga atachelewa kupona au ugonjwa utamzidi) au yuko safarini (kwa njia zote hizi haruhusiwi kufunga), basi itampasa (kulipa) idadi (yake) katika siku nyingine”.

Ikiwa mtu anajua kuwa saumu haimdhuru, hata akimwambia daktari kama itamdhuru, lazima afunge; na ikiwa anahakika au anawaza kwamba saumu akifunga itamdhuru, haruhusiwi kufunga, hata daktari akimwambia kwamba haitamdhuru; na akifunga saumu yake haitasihi; lazima ailipe saumu ile baadaye.

4. AL-IQAA-MA: Awe katika mji wake (asiwe safarini) au mahala (mji) ambapo haimpasi kupunguza sala zake, kwa mfano ikiwa katika safari kafi ka mahala na akanuia kukaa siku kumi (10) au zaidi basi kwa sharia, mtu huyo huitwa MUQEEM na itamlazimu afunge saumu ya Ramadhani.

Mwenyezi Mungu amesema juu ya jambo hili: Faman sha-hida min-kumush-shah-ra fal-ya-sum-hu wa-man kaana maree-dhan aw alaa safar-in faid-da-tun min ay-yaa-min ukhar. yu-ree-dul-laa-huu bikumul-yus-ra; walaa yu-ree-du bi-kumul-us-ra”. (2:185)“Basi mwenye kuwamo katika mwezi huu na aufunge, na ambaye alikuwa mgonjwa au yuko safarini (akala) basi itampasa (kulipa) idadi (yake) katika siku nyingine. Mwenyeezi Mungu huwatakieni yaliyo mepesi wala hawatakieni yaliyo mazito (Kwa sababu hiyo amekuamrisheni msifunge katika ugonjwa na safari)”.

Ikiwa shuruti za upungufu (Qasr) wa sala zimetimia (Tazama kitabu cha Sala, uk. 98), basi msafi ri haruhusiwi kufunga. Hukumu hii inachukuliwa kwa namna zote za safari, kama vile, kusafi ri kwa mguu, mnyama, reli, meli, au kwa ndege. Kusafi ri katika mwezi wa Ramadhani haikatazwi hasa ikiwa ni kwa ajili ya kazi. Lakini ikiwa ni kuikimbia saumu, safari hiyo ni makruhu. Hata hivyo ni lazima wote hawa wazilipe funga (saumu) zao baadaye. Ikiwa msafi ri ameshafi kia masafa tutayotaja, akifunga saumu basi haitasihi; bali atakuwa ameasi na lazima alipize baadaye saumu yake. Zimepokewa hadithi

Page 23: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

18

nyingi za Mtume (s.a.w.) na Maimamu (a.s.) kukataza dhahiri kufunga katika safari kama hivi:“As-Saimu Fi Shahri Ramadhan Fis-Safar, Kal-Muf-Tir Feehi Fil-Hadhar,” yaani “Kufunga saumu katika mwezi wa Ramadhani katika safari, ni kama yule ambaye hakusafi ri na hakufunga ingawa hana budi kufunga”.

Amesema Mtume (s.a.w.) katika hadithi mbili kwamba “Mwenyezi Mungu amenituza mimi na umma (wafuasi) pia, zawadi ambayo hakumtuza mtu yeyote katika umma wowote walio tangulia, na ni heshima kutokana na Mola juu yetu”. Wakasema watu, “Kitu gani hicho, Yaa Rasuul-lal-Laah?”, Akajibu, “Kufuturu (Kutokufunga) katika safari na kupunguziwa sala pia, na asiyefuata hayo basi atakuwa amerejesha tuzo kwa Mola!”.

Katika, hadithi moja Imam al-Baqir (Imam wa tano) (a.s.) amesema hivi, “Samma Rasuu-lul-laah (S.a.w.) Qaw-Man Saa-Muu Heena Aft ara Wa Qas-Sara Usaa-Tun.” Mtume (s.a.w.) aliwaita wale watu waasi (USAAT); ambao walisafi ri naye wakifunga wakati ambapo Mtume alikuwa akifuturu. Kwa hiyo wamekuwa waasi mpaka siku ya Qiyama.

Imeelezwa katika Sahih Muslim hadithi inayotokana na Jabir bin Abdullah, inasema, “Mwaka wa kuiteka Makka, Mtume (s.a.w.) alitoka Madina katika mwezi wa Ramadhani wakati watu wote walikuwa wamefunga. Hata alipofi ka mahala paitwapo Kuraa Gha-mi, mchana kabisa, Mtume akataka bakuli la maji, akalinyanyua hata wote wakaliona; na akafuturia kwa yale maji. Baadaye akapashwa habari kwamba baadhi ya watu (waliofuatana naye) hawakufuturu (hawakuvunja saumu yao), Mtume (s.a.w.) akasema kuwa mwenye kufanya vile (ambaye hakufungua saumu yake) basi amefanya dhambi na uhalifu naye ni MUASI.”

Ikiwa mwenye saumu kafanya safari baada ya adhuhuri, basi lazima siku hiyo aitimize mpaka magharibi, saumu yake itasihi, lakini ikiwa anasafi ri kabla ya adhuhuri wakati wowote ule, akifi ka kwenye “Had-dut-Tarakh-Khus” (mahali ambapo majumba ya huo mji atokao hayaoni au sauti ya adhana ya mji

Page 24: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

19

haisikiki) itampasa afuturu, na akifuturu kabla ya kufi ka mahali hapo itampasa alipe kaff ara pia.

Ikiwa msafi ri amefi ka mji wake kabla ya adhuhuri au mahala ambapo amepakusudia kukaa siku kumi au zaidi, na hakutenda mambo yavunjayo saumu siku hiyo, basi lazima siku hiyo afunge, na ikiwa amewahi kufanya moja katika yavunjayo saumu, kufunga siku hiyo kwake si fardhi, atailipa tu.

5. Mwanamke asiwe katika hedhi na nifasi (ujusi) kwa sababu haitasihi saumu yake. Hata kama ikimjia kwa muda mdogo kabla ya magharibi, saumu ya siku hiyo lazima ailipe pia.

6. AL-ISLAM: Uislamu ni shuruti moja katika shuruti za kukubaliwa saumu na ibada zote. Ijapokuwa juu ya kafi ri pia ni wajibu kufunga na kufanya ibada zote, lakini kwa vile yeye si Mwislamu basi haitasihi na kukubaliwa ibada zake.

Mwenyezi Mungu anaamrisha watu wasali lakini shuruti (watawadhe au watayammamu). Basi kafi ri pia inampasa afunge, lakini shurati za kusihi hiyo saumu yake ni kukubali Uislamu, na Kafi ri anaweza kusilimu.

7. Nia ni makusudio ya kutenda, nayo ni fardhi kwa kila ibada na ni sharti katika ibada zote. Lazima kunuia kujizuia na kila kinacho batilisha Saumu, na si lazima wakati wa nia kuzikumbuka zote kwa jina, inatosha kuweka nia ya kujitenga na kila kinacho haribu na kubatilisha saumu. Kuweka nia ni wajib. Ikiwa kwa mfano, siku moja kabla ya kuingia Ramadhani mtu bila ya Nia ya kufunga akalala na asizindukane ila baada ya magharibi ya usiku wa pili wa mwezi wa Ramadhani, basi kukosa kula na kunywa siku hiyo moja ya Ramadhni bila ya Nia haitasihi, na lazima baadaye ailipe.

Mtu anaweza kila usiku wa Ramadhani kuweka nia ya kufunga kesho yake, na nzuri usiku wa mwezi mosi Ramadhani aweke nia ya mwezi mzima.

Page 25: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

20

WAKATI WA KUWEKA NIA: Wakati wa kuweka nia ya saumu ni kutoka mwanzo wa usiku hadi adhana ya asubuhi (Alfajiri) kwa saumu za fardhi, ama saumu za sunna huanzia mwanzo wa usiku, hadi kiasi cha kunuwia kumebaki kufi kia magharibi, ikiwa mpaka wakati ule hakutenda kitu cha kuvunja saumu, basi hapo aweke nia ya saumu, na saumu itasihi. Ikiwa mtu bila ya kuweka nia kabla ya alfajiri akalala, na akaamuka kabla ya adhuhuri na hapo akiweka nia, saumu yake itasihi, ikiwa saumu ya fardhi au ya sunna; lakini akizindukana baada ya adhuhuri, basi hapo hawezi kuweka nia ya saumu ya fardhi. Ikiwa kabla ya alfajiri kanuwia na akalala na asiamke ila baada ya magharibi, saumu hiyo itasihi haidhuru neno.

8. AL-KHU-LUUS: Lil-Laahi Ta’Aala, maana yake, kufunga kwake iwe Lil-Laahi, Ta’ ala tu, au akiingiza Riya (kwa kujipendeleza) tu hapa saumu yake haitasihi.

Walioruhusiwa WasifungeWapo baadhi ya watu ambao wamesamehewa wasifunge. Nao ni hawa:1 na 2. (a) Mzee na kizee ambao si wagonjwa lakini kufunga saumu kwao ni

takalifu sana; wasifunge lakini watoe fi dia kwa kila siku ‘Mud’ moja (¾ kilogramu). (b) Ikiwa hawawezi kabisa kufunga basi kutoa hiyo fi dia si lazima. bali ni bora.

(3) Hivyo hivo hukumu hii kwa mgonjwa wa kiu (ambaye hawezi kustahmili kiu kabisa):

(a) Ikiwa takalifu sana, atoe fi dia ‘Mud’ moja. (b) Ikiwa hawezi kabisa, basi kutoa hiyo fi diya si lazima. bali ni bora. (Na hata hivyo asifanye fujo kwa kunywa maji). Na baadaye akiweza azilipe saumu hizo.)

(4) Mwanamke mwenye mimba aliye karibu kuzaa (a) Ikiwa anahofi a mimba yake asifunge, lakini atoe fi dia ‘Mud’ moja kwa kila siku; na baadae atazilipa saumu hizo

Page 26: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

21

(b) Ikiwa anahofi a nafsi yake, asifunge, wala hana fi dia lakini baadae azilipe saumu.

(5) Mwanamke mwenye kunyonyesha aliye na maziwa machache (akiwa anamnyonyesha mwanawe au mwana wa mwingine.

(a) Ikiwa kufunga kutamdhuru mtoto anyoyae, basi asifunge, lakini atoe fi dia ‘Mud’ moja kwa kila siku. (b) Ikiwa saumu itamdhuru yeye binafsi, asifunge, na ni bora atoe fi dia pia; na baadae azilipe saumu zote alizo ziacha kwa sababu zote mbili hizo.

MLANGO 5 MAMBO YAVUNJAYO SAUMU

Mambo yavunjayo Saumu, ambayo kila mwenye kufunga ni lazima aepukane nayo (asitende) ni kumi:Jambo la Kwanza na la Pili: Kula na kunywa makusudi kitu chochote. Hakuna tafauti ikiwa kitu kile kinaliwa kama mkate au maji, au hakiliwi kama udongo au mafuta ya taa; wala hakuna ukomo wa uchache. Vile vile hakuna tafauti ikiwa unakula na kunywa kwa mdomo kama desturi au kwa pua, au kwa njia ya kupigwa sindano na kikafi ka tumboni. Lakini kupenyeza dawa kwa njia ya sindano katika mikono au paja au mahala popote pa kiwiliwili haitadhuru saumu. Kutia dawa machoni au sikioni haibatiliki saumu.

Ikiwa unapiga mswaki mara ukautoa, basi lazima upanguse mate mswakini ndipo urejeshe mswaki mdomoni, kwani ukirejesha vivyo hivyo bila ya kufuta yale mate kwenye mswaki na ukiyameza hubatilika saumu, kwa vile mate yale yanahesabiwa kitu cha nje; lakini mate yako ya mdomoni humo humo ukimeza haidhuru saumu. Mtu aliyefunga, ikiwa kwa kusahau akila au akinywa kitu chochote haibatiliki saumu yake, lakini akifahamu tu, hapo hapo

Page 27: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

22

itamlazimu awache kula na kutema kilicho kinywani; na akila kilicho bakia kinywani, basi saumu hubatilika.

Kutafuna chakula kwa ajili ya watoto au ndege, na kuonja chakula (kwa wapishi) ambao kwa desturi hakifi ki kwenye koo, na hata ikifi ka si makusudi, haitabatilisha saumu; lakini mtu akijua tangu mwanzo kwamba itafi ka kooni, hapo itabatilika saumu yake, lazima alipe na itampasa atoe kaff ara pia.

Na kama tulivyosema katika Kitabu cha Sala kwamba moja katika suna za kutawadha ni kusukutua mara tatu, basi katika hali ya saumu, ikiwa unatawadhia sala ya fardhi, na katika kusukutua maji yakamezeka, haitadhuru saumu, lakini ikiwa unasukutua kusafi sha mdomo tu, au kujipoza kwa joto basi yakimezeka maji hubatili saumu, na itakubidi ulipe hiyo saumu.

Kumeza kohiri (belghamu) inayotoka kifuani ikiwa haikufi ka kwenye ukingo wa mdomo haitadhuru saumu, lakini kamasi itokayo kichwani (ndani ya pua) ikifi ka mdomoni usiimeze. Jambo la Tatu: Kuingiliwa mtu na utupu; katika utupu wake saumu ya wote wawili hubatilika, hata kama hawakutoa manii (shahawa). Ikiwa mtu katika hali ya saumu amelala akaota usingizini na ikamtoka shahawa, saumu yake haitavunjika, bali itampasa kuoga janaba anapotaka kusali. Jambo la Nne: Istimna. Kutoa manii makusudi kwa njia yeyote, hata kama unafanya mahaba na mke wako. Lakini kama ukiwa na hakika kwa kufanya vile haitatoka na ikaja kutoka (si kusudi) saumu haitabatilika. Jambo la Tano: Kusema uwongo (kuwasingizia) juu ya Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.), Maimam kumi na wawili (a.s.) mmoja wapo, Bibi Fatima (s.a.), mitume wa haki wote na Awsiyaa (warithi) wao. Kwa kutoa hadithi hakuna tafauti katika kuwasingizia mambo ya dini au dunia.

Page 28: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

23

Jambo la Sita: Al Irtimaas. Kuzamisha kichwa chote katika maji makusudi. Hakuna tofauti ikiwa kiwiliwili kipo ndani au nje ya maji. Muradi wa kichwa ni upande wote wa juu ya shingo. Ikiwa umepiga mbizi kwa kusahau tu, haitabatilika saumu.

Jambo la Saba: Kufi kisha vumbi au moshi nzito au isio nzito kwenye koo makusudi (kwa kuwacha kinywa au pua wazi pasipo kuzuia kwa kitu kama leso, kiganja au kitu chochote). Ikiwa baada ya kujizuia ikapita vumbi hapo haitabatilika saumu kwani hukufanya makusudi.

Jambo la Nane: Kukaa na janaba hadi alfajiri makusudi hukuoga ni haramu, na saumu hubatilika na itakupasa kulipa kadha na pia kaff ara. Vile vile mwanamke ikiwa amefunga damu yake ya hedhi au nifasi usiku, na hakuoga kabla ya alfajiri itakuwa hukumu yake kubatilika saumu tu, ijapokuwa bora kaff ara vile vile alipe. Haibatiliki saumu yeyote ikiwa mtu kwa kuota usingizini mchana yakamtoka manii.

Ikiwa mtu ameshajiona kwamba anayo janaba usiku, na akalala pasipokuwa na dhamiri ya kuoga na hakuzindukana mpaka asubuhi, basi hukumu yake sawa na kukaa na janaba hadi alfajiri. Lakini ikiwa amelala kwa dhamiri ya kuoga kabla ya alfajiri na usingizi ukamchukua mpaka asubuhi mtu huyu saumu yake haibatiliki. Ikiwa mtu amelala akazindukana na akaona anayo janaba, kwa kuwa upo wakati mwingi hadi alfajiri, akalala tena kwa nia ya kuamka na kuoga kabla ya alfajiri, alipoamuka safari hii akaona bado upo wakati, akalala tena asiamke mpaka asubuhi, basi mtu huyo saumu yake hubatilika na lazima baadae alipe. Na ikiwa mtu huyo aliamka mara ya tatu na kwa kuona bado upo wakati akalala tena na hakuzindukana mpaka asubuhi, saumu itabatilika alipe kadha na juu ya hayo alipe kaff ara.

Ikiwa mtu amesahau kuoga janaba usiku, hadi ikapita siku moja au zaidi katika mwezi wa Ramadhani, basi saumu za siku zote hizi hubatilika na itampasa kuzilipa ikiisha Ramadhani. Ikiwa mtu usiku anajua akijitia janaba

Page 29: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

24

(akimwingilia mkewe) hana wakati wa kuoga au kutayammamu na akafanya, basi itakuwa hukumu yake sawa na yule aliyekaa makusudi na janaba hadi alfajiri. Lakini ikiwa ameweza (amewahi) kutayammamu hapo saumu yake itasihi ijapokuwa amefanya dhambi, na ikiwa hakuifanya hiyo tayammamu, saumu yake itabatilika na itamlazimu alipe baadaye.

Ikiwa kabla ya adhana ya sala ya asubuhi mwanamke imefunga damu yake ya hedhi au nifasi, na wakati wa kuoga hana, na anataka kufunga fardhi au kulipa kadha, basi hapo hapo lazima atayammamu, na lazima akae macho mpaka adhana ya asubuhi.

Jambo la Tisa: Kupiga bomba nyuma kwa kutilia dawa ya maji maji kwa mgonjwa (kwa ajili ya kujitibu) saumu hubatilika, itampasa kulipa. Lakini ikiwa anatia kitu kikavu kwa dawa basi haibatiliki saumu.

Jambo la Kumi: Kujitapisha makusudi, hata ikiwa kwa dawa kwa ajili ya kujitibu vile vile saumu hubatilika. Lakini mtu akitapika bila ya kusudi basi hapo haitadhuru saumu.

Mtu akila usiku kitu chochote ambacho anahakika kwa kula kitu hicho, mchana atatapika bila kutaka, basi saumu ya siku hiyo itambidi baadaye ailipe.

Mambo yote haya kumi yanavunja saumu kama tulivyo taja ikiwa mtu anafanya kwa makusudi basi bila shaka hubatilika saumu yake, na alipe kaff ara pia, wala hakuna tafauti kwa wale wenye kuzijua hukumu hizo, au kwa wasio jua.

Mambo yenye karaha katika hali ya SaumuNi karaha mchana: 1. Kucheza mtu na mke wake wa halali, au kumbusu ikiwa hakukusudia

kumwaga shahawa, au sitabia yake kwa kufanya hayo kumtoka. Lakini ikiwa anajua au ni tabia yake akifanya humtoka basi ni haramu kwake hata kama haikumtoka, kwani amekusudia kuvunja saumu;

Page 30: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

25

2. Kutia machoni wanja ikiwa ladha au harufu ya wanja inafi ka kwenye koo; 3. Kujitoa damu au kufanya jambo lolote lenye kumdhoofi sha; 4. Kunusa kila aina ya maua yenye harufu kali nzuri, 5. Kuvaa nguo majimaji au Kujilowesha nguo; 6. Kukaa mwanamke ndani ya maji; 7. Kung’oa jino; 8. Kusukutua bure; 9. Kusoma mashairi yoyote isipokua mashairi ya sifa, au masaibu juu ya

Mtume (s.a.w.) na Ahli Bayti wake (a.s.)

MLANGO 6NAMNA ZA SAUMU (KUFUNGA)

Saumu ipo namna nne: Kwanza, Wajib (fardhi); Pili, Haramu; Tatu, Makruuhu (yenye karaha); Nne, Mustahab (sunna).

Saumu zilizo Faradhi (Wajib)1. Saumu ya mwezi wa Ramadhani.2. Saumu ya Nadhiri, Ahadi na Yamini, ambazo funga hizo hufaradhika kwa

kuweka na dhiri, au ahadi au kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu.3. Saumu ya kadha (malipo ya mwezi wa Ramadhani kwa wale wasiofunga).4. Saumu ya kaff ara.5. Samu ya kufunga badala ya mtu aliyekufa kwa kulipiwa.6. Saumu badala ya kuchinja nyama katika Hija ikiwa mtu hana uwezo wa

kununua mnyama wa kuchinja, afunge siku kumi (Tatu huko Makka na saba akirejea nyumbani).

7. Saumu ya siku ya tatu katika siku za Itikafu.8. Saumu kwa mtoto mwanaume wa kwanza badala ya wazee wake ambao

walikufa kabla ya kuzilipa saumu zao.

Page 31: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

26

Saumu za Haramu (Zilizokatazwa Kufunga)1. Saumu ya sikukuu mbili (a) Idi ya Ramadhani (Idul-Fitri: siku ya kwanza

ya Shawwal (mfungo mosi)) na (b) Idul-Adh-Ha (Sikukuu kubwa, mwezi kumi mfungo tatu (Dhil-Hajji) sikukuu ya kuchinja).

2. Kufunga kwa watoto saumu za sunna bila ya radhi ya wazee; vile vile mke kufunga sunna bila ya radhi ya mumewe ikiwa kwa kufunga mke hatekelezi haki ya mume.

3. Saumu ya siku ya shaka baada ya kwisha siku 29 ya Shabani. Kwa sababu ya mvua na mawingu, mwezi tisa wa ishirini, mwezi haukuonekana na hukupata hakika ya kuandama kwa mwezi, siku hiyo ya pili ni siku ya shaka ilivyokuwa si mwisho wa Shabani wala si mwanzo wa Ramadhani. Basi haijuzu kufunga kwa nia ya Ramadhani bali unaweza kwa nia ya sunna tu.

4. Saumu Ay-Yaa-Mut-Tash-reeq: Siku tatu baada ya sikukuu kubwa (ya kuchinja) nazo ni tarehe kumi na moja, kumi na mbili, na kumi na tatu, mfungo tatu (Dhil-Hajji) kwa wale walioko Mina katika Makka wanapohiji.

5. Saumul Wisaal: Kufunga kwa mfululizo bila kufuturu usiku hadi alfajiri au siku ya pili magharibi. Lakini ikiwa hukutumia zivunjazo saumu si kwa nia ya kufunga, bali basi tu, haidhuru saumu yako.

6. Saumus-Samt: Kwamba anuwie katika saumu kukaa kimya kabisa mchana kutwa, au baadhi ya nyakati, ni haramu. Lakini ikiwa hakunuwia hivyo na ikatokeya sadfa siku hiyo kutwa hakuongea, basi haidhuru neno, kwani hakunuia hayo.

Saumu zilizo Makruhu (ya karaha)Maana ya makuruhu hapa (na katika Ibada yote) ina thawabu kidogo sana; na bora zaidi kuiwacha. Nazo ni hizi:

Page 32: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

27

1: Saumu siku ya Ashura: (mwezi kumi Muharram, mfungo nne). Imepokewa kwa baadhi ya wanavyuoni kwamba Banu Umayyah walikuwa wakiifurahia siku hiyo na wakiifunga kuonesha furaha yao kwa kumwua Imam Husain (a.s.) (Bwana wa Vijana wa Peponi) siku kama hiyo. Zimepokewa hadithi nyingi zilizosemwa na Ahlul Bait (a.s.) kulaumu kufunga siku mbili (mwezi tisa na kumi) ya Muharram na hasa siku ya Ashura. Hadithi nyingi wamemzulia Mtume (s.a.w.) kuonesha fadhila ya kufunga siku mbili na hasa Ashura ni hadithi za uzushi tu. Naam, ukiwacha kula na kunywa bila nia ya kufunga, kwa kuihuzunikia masaibu yaliyompata Sayyidinal Husain (a.s.) na Ahlul Bait wa Mtume (s.a.w.) siku hiyo, na kuikumbuka njaa na kiu chao, baada ya sala ya Alasiri ukifungua kinywa kwa maji tu, bila shaka ni kama unampa Mtume (s.a.w.) mkono wa rambi rambi.

2 na 3: Kufunga siku ya Arafa (mwezi tisa Dhil-Hajji, mfungo tatu) ikiwa sikuhiyo inatiliwa shaka kwamba ni Idi (mwezi kumi); na kwa yule anayeogopa kudhoofi ka kwa kufunga siku hiyo na akachelea kuzisoma Dua na kufanya Amali ambazo ni bora kuliko kufunga.

4: Kufunga saumu mgeni (aliyeshuka kwa mtu) bila ya idhini ya mwenyekumkaribisha.

Saumu za Sunna1. Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni sunna. Imepokewa hadithi kwamba

kufunga huko ni sawa na kufunga maisha; na inaondoa joto la kifua. Na njia bora ni kufunga hivi: afunge Alhamisi ya kwanza na ya mwisho wa kila mwezi, na Jumatano ya kwanza baada ya tarehe 10 ya mwezi. Na mwenye kuacha kufunga siku hizo, basi ni sunna azilipe, na akiwa hajimudu kwa uzee, basi inafaa afi die kwa kila siku Mud moja (kibaba kimoja) cha ngano au pesa.

2. Saumu ya Ay-yaamul Bayz: Kufunga tarehe 13, 14, na 15 ya kila mwezi

3. Kufunga kila Alhamisi na Ijuma pamoja, au Ijumaa tu.

Page 33: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

28

4. Saumu ya miezi ya Rajab na Shabaan (mfungo kumi na kumi na moja) siku zote, au baadhi ya siku, ijapokuwa siku moja katika kila miezi miwili hizo. Zimepokewa hadithi ya Imam Musa bin Jafar (a.s.) amesema hivi: “Rajab ni mwezi adhimu mtukufu. Mwenyezi Mungu huzidisha katika mwezi huu bakhshishi, na hufuta madhambi. Basi mwenye kufunga siku moja katika Rajab moto wa Jahannam huwa mbali naye mwendo wa mwaka mmoja, na mwenye kufunga siku tatu ataingia Jannah (Peponi).”

Na katika hadithi nyingine, al-Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenye Kufunga siku kumi na tano katika Rajab, Mwenyezi Mungu humpa atakayo, na akizidisha kufunga atamzidishia”

Na katika hadithi nyingine, Imam huyo amesema: “Mwenye kufunga siku moja katika Shabaani basi ataingia Jannah.”

Na katika hadithi nyingine, Imam huyo amesema: “Mtume (s.a.w.) alikuwa hafungi mwezi kamili katika miezi ya mwaka ila mwezi wa Shabaani na akiunganisha na mwezi wa Ramadhani”.

5. Saumu ya Mab’ath: Mwezi ishirini na saba ya Rajabu (mfungo kumi), ambao hapa kwetu ni maarufu sana, kuwa ni siku ya Miraji, lakini hakika ni siku ambapo Mtume (s.a.w.) alibashiriwa aanze kudhihirisha Utume wake. Na inayumkinika usiku wake kenda Miraji, ijapokuwa Mtume (s.a.w.) alikwenda Miraji mara nyingi. Imepokewa hadithi inayotokana na al-Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba alisema: “Usiwache mfungo wa mwezi ishirini na saba ya Rajabu, kwani ni siku ambayo aliteremshiwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) utume wa kuwafi kishia umma, na thawabu ya mfungo huo, ni kama kufunga miezi sitini”

6. Kufunga siku ya 15 wa mwezi wa Shabaan siku ambayo amezaliwa Imam wetu wa kumi na mbili, al-Iman Muhammad Mahdi (a.s.), mwaka 256 wa Hijra katika mji wa Samarra (Iraq).

Page 34: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

29

7. Kufunga siku ya nne mpaka tisa mwezi wa Shawwal (mfungo mosi).

8. Kufunga siku ya Dah-wul-Ardh: siku ya kuenewa ardhi (Dunia) kutoka chini ya al-Kaaba. Nayo ni siku ya ishirini na tano (25) wa mwezi wa Dhil-Qaada (mfungo pili). Imepokewa hadithi kwa al-Imam ar-Ridha (a.s.) (Imam wa nane), amesema kwamba mwenye kufunga siku hiyo anapata thawabu sawa na kufunga miezi sitini.

9. Kufunga siku ya ishirini na tisa (29) wa mwezi wa Dhil-Qaada (mfungo pili).

10. Kufunga siku ya kwanza ya mwezi wa Dhil-Hajji (mfungo tatu) au kila siku katika siku tisa za mwanzo. Imepokewa hadithi ya Imam Musa bin Jafar (a.s.) (Imam wa saba), amesema hivi: “Mwenye kufunga siku tisa katika kumi la mwanzo wa mfungo tatu anapata thawabu ya kufunga maisha”.

11. Kufunga siku ya Arafa (tarehe 9 ya mwezi wa Dhil-Hajji (mfungo tatu)) kwa yule ambaye kwa kufunga hatadhoofi ka kwa kufanya amali na dua.

12. Kufunga siku ya Ghadeer; nayo ni siku ambayo Mtume (s.a.w.) alimteua Sayyidna Ali (a.s.) kuwa ni Wasii na Wazir wake wa haki kwa amri ya Mwenyezi Mungu alipoteremsha aya ifuatayo njiani akirudi kutoka Hija ya mwisho kwenye mahala paitwao GHADEER-E-KHUM:

Yaa ay-yuhar-rasulu bal-ligh maa unzila ilay-ka mir-rab-bika wa-il-lam taf-al fa-maa bal-lagh-ta risaa-latahu (5:67) “Ewe Mtume! Fikisha ulioteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hukufi kisha ujumbe wetu”.

Baadaye akakamata mkono wa Sayyidna Ali (a.s.) na akasema, “Man Kuntu Maw-Laa-Hu Fa’hadha Aliy-Yun Maw-Laahu”. “Mwenye (kunikubali) kuwa mimi ni bwana wake, basi huyu Ali pia ni bwana wake”; na akasema maneno haya juu yake, “Al-Laa-Hum-Ma, Waa-Li Man,

Page 35: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

30

Waa-Laa-Hu, Wa Aa-Di Man, Aa-Da-Hu, Wan-Sur, Man Nasa-Rahu, Wakh-Dhul Man Khadha-Lah”, “Ee Mola wangu, mpende mwenye kumpenda Ali, mfanyie uadui mwenye kumfanyia Ali uadui, msaidie mwenye kumsaidia Ali mchukie mwenye kumchukia Ali”.

Nayo ni siku ya mwezi wa kumi na nane (18) wa Dhil-Hajji (mfungo tatu).

Imepokewa hadithi, kutokana na al-Imam as-Sadiq (a.s.), kwamba amesema; “Kufunga siku ya Ghadeer ni malipo ya fi dia ya miaka sitini”.

13. Kufunga siku ya “Mubaahila” (tarehe 24 ya mwezi wa Dhil-Hajji (mfungo tatu)). Nao ni siku ya kuamrishwa Mtume (s.a.w.) na Mwenyezi Mungu kwenda kuapizana Yeye na Ahlul Bayti wake mbele ya Makasisi wa Kikristo wa Najraani na kama inavyoeleza aya (3:61) hivi:

Faman hajjaka feehi min baaadi ma jaaka mina alaailmi faqul taaaal-aw nadaau abnaana wa abnaakum wa nisaana wa nisaakum wa anfu-sana wa anfusakum thumma nabtahil fanajaaal laaanata Allahi aaala alkathibeena“Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufi kilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo”.

14. Kufunga siku ya awali, ya tatu na ya saba wa Mwezi wa ya Muharram (mfungo nne).

15. Kufunga siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.) nao ni siku ya kumi na saba (17) wa mwezi wa Rabi-ul-Awwal (mfungo sita).

16. Kufunga siku ya kumi na tani (15) wa mwezi wa ya Jumaadal-Ula (mfungo nane).

Page 36: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

31

MLANGO 7DUA NA AMALI ZA USIKU

Sasa tutaeleza baadhi ya sunna za mwezi huu mtukufu ambazo ni thawabu sana kuzifanya; na ambazo zimepokewa kutoka kwa Mtume wetu (s.a.w.) na Ahlul Baiti wake (a.s.).

Dua za Kila Usiku1. Dua za Kufuturia: Ukisoma dua zifuatazo kabla ya kufuturu utapata

thawabu nyingi:

Katika hadithi tukufu nyingi za Mtume (s.a.w.) na Maimamu (a.s.) imesemwa kwamba kufuturia vitu vitamu, kama halua, sukari mawe au tende, kuna thawabu nyingi na pia ni suna ya Mtume (s.a.w.).

Vile vile kufuturu kwa maji ya moto kuna fadhila nyingi na faida kwa roho na kiwiliwili.

Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) amesema: “Kutanguliza sala (za Magharibi na Isha) kabla ya kufuturu kuna thawabu nyingi sana; huandikwa sala hizo thawabu za sala katika hali ya saumu”.

Lakini ikiwa mtu anakungojea, au umeshikwa na nja hutaweza kusali kwa utulivu, hapo bora kufuturu kwanza. Ujitahadhari usichelewe kusali katika nyakati za fadhila.

a. Al-llaa-humma laka sumtu wa ala riz-qikaa af-tartu wa alay-ka ta-wak-kal-tu.

b. Soma sura nzima ya al-Qadr (In-na an-zal-na).c. Kwenye tonge la kwanza, anzia na Bismillahi, na ufuatie maneno haya:

Yaa Wa-si-al-magh-fi rati Igh-fi r-lee. d. Soma dua hili ambalo Ameerul-mumeneen Ali (a.s.) alikuwa akisoma

wakati wa kufuturu: Bismil-lahi, alla-humma laka sumnaa wa ala riz-qi-ka af-tar-naa; fata-qab-bal minnaa, Inna-ka an-tas-sa-mee-ul-aleem.

Page 37: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

32

Thawabu ya KufuturishaAmehadithia Imam as-Sadiq (a.s.), kwamba: “Katika mwezi wa Ramadhani, Sudair as-Sairafi alikwenda kwa baba yangu (Imam Muhammad al-Baqir, (a.s.) Imam wa tano). Akamuliza Imam, ‘Ee Sudair, je wajua siku gani hizi?’ Akajibu, ‘Ndiyo, nakufi dia baba yangu, siku hizi ni siku za Ramadhani, kwani ni nini?’ Akamwambia Imam (a.s.), ‘Je unaweza kuweka huru watu kumi katika watoto wa Nabi Ismail (a.s.) kila usiku katika siku hizi?’ Akajibu Sudair, ‘Nakufi dia baba yangu na mama yangu, sina mali kiasi hicho’. Akaendelea Imam al-Baqir (a.s.) kuipunguza hata akafi ka kuweka huru mtu mmoja tu, na kila mara Sudair akamjibu, ‘Siwezi’. Basi akamwambia, ‘Je, huwezi kumfuturisha Mwislamu mmoja kila siku?’ Akajibu, ‘Naweza si mmoja tu, bali hata kumi’. Akamwambia Imam (a.s.), ‘Hiyo ndiyo ninayotaka (ndio shabaha yangu), Ee Sudair. Kumfuturisha ndugu yako Mwislamu ni sawa (thawabu yake) kama kumweka huru mmoja katika watoto wa Mtume Ismail’.”

Imepokewa hadithi kwa al-Imam as-Sadiq (a.s.), “Mwenye kumfuturisha Mumin mmoja, Mwenyezi Mungu huwaweka Malaika sabini wamtakase (wammuombee aghufi riwe) mpaka mwakani usiku kama ule”.

2. Asome dua hii yenye maneno machache, lakini maana yake adhimu. Basi mwenye kusoma dua hii kila usiku katika mwezi wa Ramadhani ataghufi riwa madhambi ya miaka sitini:

Al-laa-hum-ma Rab-ba shah-ri Ramadhan, al-lla-dhi an-zal-ta fee-hil Qur-aan; waf-tar-adh-ta ala ibaa-dika fee-his-siyaam; Sali-li alaa Muhamadin wa aali Muhammad; war-zuq-nee Haj-ja bay-tikal ha-raam, fee aami hadha wa fee kul-li aam; wagh-fi r-lee til-kadh dhu-nuu-bal-idhaam; fa-in-nahu la-yagh-fi ru-haa ghay-ruka; ya Rah-maanu, ya Al-laam.

3. Asome kila usiku dua mashuhuri inayoitwa Dua al-Ift itaah. Mwanzo wake ni hivi: Al-laa-humma in-nee af-ta-ti-huth-thanaa-abi-ham-dik.4

4. Wakati wa kula daku asome dua mashuhuri na adhimu ya Sahar,

4 Tazama Mafatih Al-Jinan, uk. 179

Page 38: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

33

inayoanza kwa maneno haya: Al-laa-hum-ma In-nee as-alu-ka min ba-haa-ika bi-ab-ha-hu, wa kul-lu ba-haa-ika ba-hee.5 Na baada ya kuisoma, amuombe Mwenyezi Mungu kila mambo mema anayotaka; Na anapotaka kula daku asiache kabisa kusoma sura ya al-Qadr.

Imepokewa hadithi kwamba Mtume (s.a.w.), amesema, “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake huwarehemu walao daku (katika mwezi wa Ramadhani) na wenye kuomba kughufi riwa, wakati wa daku, basi msiache kula daku ijapokuwa kinyweo cha maji.”

5. Abu Hamza Th umali (r.a.) amesema kwamba Imam Zaynul-Abideen (a.s.) alikuwa akisali sehemu ya usiku; na ukifi ka wakati wa daku akimwomba Mwenyezi Mungu kwa maneno haya: Ilaa-hi, laatu-addib-ni bi ukuu batik6 (mpaka mwisho). Dua hii inajulikana kwa jina la sahaba huyu Bwana Abu Hamza Th umaali (r.a.). Hakika dua hiyo ni hazina ya elimu na maarifa.

6. Kuoga (Ghusl) katika usiku wa witri (1, 3, 5, 7, na kadhalika) kuna thawabu sana. (Kwa namna ya kuoga tazama Kitabu chetu cha Sala uk.33).

Amali za Usiku za Laylatul-QadrUsiku ambao taadhima yake haina mfano; usiku ambao fadhila yake haiwezi kukadiriwa; Usiku ambao utukufu wake hauna kifani. Ni usiku ambao Qur’ani tukufu iliteremshwa na Mwenyezi Mungu; usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu; ibada katika usiku huo ni sawa na ibada ya miezi elfu.

Mwenyezi Mungu anasema katika usiku huo hivi:Bis-mil-laa-hir-rahmaa-nir-raheem. Innaa an-zal-naahu fee lay-latil-qadr. Wa maa ad-raa-ka maa lay-latul qadr. Lay-latul qadri khay-run min alfi shahr. Tanaz-za-lul mala-ikatu war-ruu-hu fee-ha bi idh-ni rab-bihim min kul-li amr. Sa-laa-mun, hiya hat-taa mat-lail-fajr. (97:1-5)

5 Tazama Mafatih Al-Jinan, uk. 1846 Tazama Mafatih Al-Jinan, uk. 186

Page 39: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

34

“Hakika tumeiteremsha (Qur’an) katika Laylatul Qadr (Usiku wa Heshima, Usiku wa Cheo Kitukufu). Na nini kitakujulisha Laylatul Qadr (usiku wa Heshima) ni nini? Laylatul Qadr (Usiku wa Heshima) ni bora kuliko miezi elfu. Hushuka Malaika na Jibril katika (usiku) huo kwa amri ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.”

Usiku huo ni usiku ambao hubainishwa kila jambo la hekima. Mwenyezi Mungu anasema: Inna anzalnahu fee laylatin mubarakatin inna kun-na munthireena. Feeha yufraqu kullu amrin hakeemin (44:3-4)“Kwa hakika tumeiteremsha (Qur’an) katika usiku uliobarikiwa, bila shaka sisi ni waonyaji. Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hekima.” Usiku huu ndio Mwenyezi Mungu huweka mambo ya viumbe wake mpaka mwaka mmoja. Kwa mfano, kila atakayezaliwa, atakaye kufa, atakaye tajirika, atakaye kuwa masikini, atakaye kuwa na cheo, atakaye dhalilika, atakaye shinda, atakaye shindwa, atakaye ongoka, atakaye potea, atakaye pona, atakaye kuwa mgonjwa, na mambo mengi kama hayo ambayo humsibu binadamu.

Amali nzuri usiku huo ni kusali, kutoa zaka, kutenda kila jambo zuri la khayri; kwani ukitenda usiku huu ni bora kuliko amali ya miezi elfu isiokua na Laylatul Qadr. Usiku huu huteremka Malaika pamoja na AR-RUUH ambaye ni Malaika alie adhimiwa kuliko Malaika wote, kwa amri ya Mwenyezi Mungu wanafi ka kwa al-Imam al-Mahdi (a.s.), na wanamwonesha kila alichokadiriwa yeye na watu wote na Mola, mwaka ujao mpaka Laylatul Qadr ijayo.

Kama ilivyo katika hadithi ya Laylatul Qadr hii, juu ya utukufu wake, na jinsi inavyokuwa inayo manzila (cheo), lakini bado hatuijui, na maarifa ya kuwekwa hiyo siku, na siku gani kwa hakika hiyo haikubaynishwa. Lakini inatumainiwa kuwa ni moja katika usiku wa tarehe kumi na tisa (19), ishirini na moja (21), ishirini na tatu (23). ishirini na tano (25) na ishirini na saba (27); na labda zaidi inatumainiwa sana kuwa katika usiku wa tarehe ishirini na moja na ishirini na tatu (21 na 23). Hadithi nyingi za Maimamu wetu (a.s.) zilizopokewa zinatilia nguvu sana kwamba Laylatul Qadr ni usiku mmoja

Page 40: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

35

katika siku hizo mbili (21 au 23). Mara nyingi watu wamewaomba al-Imam (a.s.) awaainishiye (dhihirishie) siku ipi katika hizo mbili? Imam hakuainisha, na akajibu, “Itakudhuru nini ukifanya mambo mazuri (Ibada) za usiku siku mbili hizi?”.

Imepokewa kwa Imam al-Baqir (a.s.) kutokana kwa baba zake watukufu (a.s.) kwamba wamesema hivi, “Mtume (s.a.w.) amekataza mtu kutojali usiku wa Ishirini na moja na Ishirini na tatu, na amekataza kulala mtu usiku wa siku hizo”. Vile vile amesema (a.s.) kwamba “Mtume (s.a.w.) alikuwa akikunja matandiko yake na akikaza kitambaa cha kiunoni (mshipi) katika siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhani (alikuwa akikesha kwa Ibada) na akiwafanya watu wake wa nyumbani wakeshe usiku wa Ishirini na tatu na akiwarushia maji usoni mwa wenye kulala. Na alikuwa Bibi Fatima (s.a.) hamwachi mtu yeyote katika watu wake wa nyumbani kulala usiku huo, na akiwatibu kwa kula kidogo (akiwaeleza kama kula kidogo hupunguza usingizi; na ukila sana huleta usingizi mwingi), na akijiweka tayari kwa Ibada ya usiku tangu mchana”.

Ala kulihali, usiku wa al-Qadr haimfalii mtu kuupuuza kulala, bali akeshe kwa Ibada ya Mwenyezi Mungu kwa kusali, kutubia, kufanya dhikri (kutoa uradi) na kila amali za sunna zilizowekwa na kupangwa kwa usiku huu. Usijidanganye nafsi yako kwa kusema nimechoka au ninaumwa kichwa na kuonesha uchovu. Kwa sababu haya yote hutokana na adui wetu mkubwa shetani, kukukosesha mafanikio na manufaa yote ya kheri za usika huu. Kama alivyosema Bibi Fatima (s.a.), “Mwenye kunyimwa ni yule mwenye kujinyima kheri zote za usiku huu”. Basi, ndugu zangu, msikose yote haya kwani hujui mwakani utakuwapo hai, upate kufi dia uliyo yakosa!!

Maelezo na Utaratibu wa Amali ya Laylatul Qadr1. Kuoga (Ghusl) usiku wa 19, 21 na 23. Ni bora uoge wakati linapozama

jua, hata upate kusali sala ya Magharibi na Isha kwa hiyo ghusli, lakini utawadhe pia.

Page 41: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

36

2. Ukeshe kucha usiku wa siku zote tatu za Laylatul Qadr kuomba dua, kunyenyekea, kuomba kughufi riwa.

Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba kila mwenye kukesha kucha Mwenyezi Mungu atamghufi ria madhambi yake yote hata yakiwa kwa idadi ya nyota zote, au majabali, au kiasi cha maji ya bahari zote (utaghufi riwa dhambi zako binafsi na Mola, si za watu kama umemwibia mtu).

3. Usali raka mbili katika usiku wa Laylatul Qadr (19, 21, 23). Katika kila rakaa, baada ya Sura ya Al-Hamdu, soma Sura (Qul-Huwal-Laah) mara saba na ukiisha maliza hiyo sala, hapo hapo soma mara sabini (70) hivi; As-tagh-fi rul-Laa-ha wa Atuu-bu-Ilay-hi.

Imepokewa hadithi tukufu inasema, ‘Mwenye kuzisali hizi rakaa mbili kama ilivyo elezwa, basi kabla ya kuondoka mahala pake Mwenyezi Mangu atamghufi ria yeye na wazee wake’.

4. Usome usiku wa mwezi 19, 21 na 23 mara mia moja (100): As-tagh-fi rul-laaha rab-bee wa atubu-ilayh.

5. Usiku wa 19 na 21, usome mara mia moja (100): Allaa-hum-mal-an qata-lata Ameeril-Muminin.

6. Ufunue Qur’ani tukufu, uiweke wazi mbele mikononi mwako na usome dua hii: “Al-la-hum-ma in-nee as-alu-ka bi ki-taa-bikal munzali wa maa fee-hi wa fee-his-mu-kal ak-baru wa as-maa-ukal hus-naa wa maa yukhaa fu wayur-jaa an taj-alanee min uta qaa-ika minan -naar”. Baadaye uombe maombi yako yote.

7. Tena uifunge Qur’ani na uiweke juu ya kichwa chako (Tahadhari isianguke) na useme maneno haya:

“Al-laa-hum-ma, Bi-haqqi ha dhaal-Qur’aan wa Bihaqi man ar sal-taho bih wa Bihaq qi kul-li mu-mi-nin ma-dah-tahu feeh wa Bi-haq-qika, alay-him, falaa ahada a’ rafu Bi-haq-qika minka”.

Page 42: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

37

Tena sema mara kumi hivi: Bika yaa Allaahu; mara kumi, Bi-Muhammadin (s.a.w.); mara kumi, Bi-Aliy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Faa-timata (a.s); mara kumi, Bil-Hasani (a.s); mara kumi, Bil-Husaini (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-y ibnil-Husain (a.s); mara kumi, Bi-Muhammad bin-Aliy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Jafar ibni-Muhammadin (a.s); mara kumi, Bi-Musa ibni-Jafarin (a.s); mara kumi Bi-Aliy-y ibni Musa (a.s); mara kumi, Bi-Muhammad ibni-Aliy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-y ibni-Muhammadin (a.s); mara kumi Bil-Hasan ibni-Aliy-yin (a.s); Hapo inuka katika hali ya kusimama mkono mmoja umeikamata Qurani ilioko juu ya kichwa, basi sema mara kumi Bi-Huj-ja (a.s); tena taja moyoni haja zako zote na utake kwa Mwenyezi Mungu baraka ya usiku huu wa Laylatul Qadr.

8. Kumzuru Imam Husain (a.s.) katika usiku wa Laylatul Qadr. Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba, “Huita muitaji (Malaika) kutoka mbingu ya saba kwenye Arshi hivi, ‘Bila shaka Mwenyezi Mungu amemghufi ria mwenye kuhudhuria (kuizuru) kaburi tukufu la Imam Husain (a.s)”. Basi zipo Ziyara mahsusi nyingi katika vitabu vya Ziyara, na ukisoma Ziyara mashuhuri kwa jina la Ziyaaratul Waaritha itatosha. Ziyara hii inaanzia kwa maneno haya: “As-salaamu alay-ka, yaa waa-ritha Aa-dama saf ’wa-til-Iaah” 7

9. Usali rakaa mia (100) katika kila usiku wa 19, 21 na 23. Kusali huko kuna thawabu mno; na bora kusali hivi: Katika kila rakaa, baada ya sura ya “Al-Hamdu”, soma sura ya Qul-Huwal-Laahu mara kumi. Vile vile unaweza kusali raka mia hizo kwa (kukidhi) kulipa sala zako za fardhi

7 Tazama Mafatih Al-Jinan, uk. 428/430.

Page 43: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

38

uloziwacha kusali kwa udhuru fulani fulani muda wa mwaka; kwa mfano ikiwa unadaiwa sala ya siku sita itakuwa rakaa mia moja na mbili (102) Kuanzia sala ya adhuhuri ya siku ya kwanza mpaka isha ya siku ya sita.

HADHARI Sala ya sunna yeyote haijuzu kusali kwa mafungu zaidi ya rakaa mbili, utazisali kama sala za asubuhi; vile vile huwezi kusali kwa Jamaa kabisa, isipokuwa sala za Idi na Salatu-Istisqaa (Sala ya kuombea mvua tu).

10. Usome usiku wa mwezi ishirini na tatu (23) Sura za Qurani zijazo: Al-Ankabuut. (J.20: S.29), Ar-Ruum (J.25: .30), na Ad-Dukhaan (J25:S.44). Katika hadithi tukufu amesema Imam as-Sadiq (a.s.): “Ninaapa, mwenye kuzisoma zile sura mbili (za mwanzo) usiku huu, ni mtu wa Peponi”

Amali za Kumi ya Mwisho wa Mwezi1. Kuanzia usiku wa ishirini na moja mpaka mwisho wa mwezi mtukufu

soma dua hii kila usiku. “A’udhu bi-jalali waj-hikal-Kareem, an yan-qa-dhi-ya an-nee shahru Ramadhan au yatlual-Fajru min lay-latee ha-dhi-hee walaka qi-balee dhan-bun au tabi-atun tuadh-dhi-buni alayh”.

2. Imam Zaynul-Abedeen (a.s.) (Imam wa nne) alikuwa akisoma dua hii usiku wa ishirini na saba (27) kila mara, nayo ni hii: al-laa-hum-mar-zuq-nee at tajaa-fi ya an daa-ril-ghu-ruur wal-inaa-bata Ilaa daa-ril-khu-luud wal is-tia-dada lil-mawti qabla hu-luu-lil-fawt.

Ewe Mola wangu nipe uwezo wa kujitenga na mambo usiyoyapenda yenye kunidanganya humu (duniani) na nifanye mambo mema ya kuniokoa huko akhera na adhabu yako, na nijiweke tayari kwa kufa kabla haikunijia mauti, (maana yake nifanye amali njema hata ikinijia mauti nisiwe na wasiwasi wa kukosa kutubia).

Usiache kuoga “GHUSL” usiku huu, na kukesha pia kwa Ibada, kama unaweza.

3. Usome Dua ya Al-Widaa (ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani) katika usiku wa mwisho, kama ilivyopokewa katika hadithi ya al-Imam

Page 44: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

39

Jafar bin Muhammad as-Sadiq (a.s) (Imam wa sita); nayo ni hii: Al-laa-ham-ma laa tajal-hu aa-khiral-ahdi min siyaa-mee li-shah-ri Ramadhan wa audhu bika an-yat-lua fajru haa dhi-hi?-lay-lati il-laa wa qad ghafarta-lee. Basi Mwenyezi Mungu atakughufi ria kabla ya asubuhi na atakujalia na kuruzuku utubiye madhambi yako.

Haya yote ni badhi ya dua na sala zilizopokelewa katika hadithi tukufu, na mwenye kutaka zaidi atapata katika vitabu vya Dua na Ziyara kama Mafaatee-hul-Jinaan na zinginezo.

MLANGO 8MAELEZO YA KULIPA SAUMU NA KAFFARA

Mahala ambapo ni wajibu kulipa Saumu tu:1. Kujitapisha makusudi mwezi wa Ramadhani (si kwa dawa). Ni bora hata

kulipa kaff ara.

2. Kulala makusudi na janaba (baada ya kujua unayo janaba) na bila ya kuwa na nia ya kuoga na usizindukane mpaka ikiingia asubuhi.

3. Mtu ijapokuwa hakutenda linalo vunja saumu, lakini nia ya saumu hakuweka, au alifanya Riya (kujipendekeza) au amenuia asifunge, au amenuia atende moja lenye kuvunja saumu.

4. Katika mwezi wa Ramadhani kasahau kuoga janaba na katika hali ya janaba amefunga siku moja au zaidi, basi azilipe zote.

5. Bila ya kuhakikisha kwamba asubuhi imeingia au bado, na akafanya moja katika yanayovunja saumu, baadaye akatambua kwamba ilikuwa asubuhi. Vile vile baada ya kuhakikisha kwa hali anadhani asubuhi imeingia na akatenda yavunjayo saumu, baadaye ikajulikana kwamba ilikuwa asubuhi; bali hata baada ya kuhakikisha akitia shaka kwamba asubuhi imeshakuwa

Page 45: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

40

au bado na akafanya yavunjayo saumu, baadaye akajua ilikuwa asubuhi, lazima alipe siku hiyo.

6. Mtu aseme kwamba asubuhi bado, na kwa usemi huyo, mtu atende yavunjayo saumu, na baadaye akajua ilikuwa asubuhi.

7. Mtu aseme kuwa sasa ni asubuhi, lakini wewe usemi wake hukuwa na yakini nao, au ufi kirie kwamba alikwambia hivyo kwa mzaha tu, ukitenda yavunjayo saumu, na baadaye ikajulikana kuwa ni asubuhi.

8. Kipofu, na mtu kama huyo, kwa kumsikia mtu akisema magharibi imekuwa na akafuturu, baadaye akajua kwamba haikuwa magharibi.

9. Ikiwa hali ya hewa safi , lakini kwa kuona kiza imjie yakini kwamba magharibi imeshaingia na akafuturu, baadaye ikajulikana haikuwa magharibi. Lakini ikiwa hali ya hewa ni mawingu mawingu, na akafuturu, baadaye ikajulikana haikuwa magharibi, haimpasi kulipa (lakini hali kama hiyo inambidi ahakikishe kwanza).

10. Kwa ajili ya kujipoza, au bila ya haja yoyote mtu akisukutuwa, na maji ikawa amemeza lazima alipe hiyo saumu. Lakini kwa kusahau kwamba yeye amefunga akameza maji, au alisukutuwa kwa ajili ya kutawadha na maji yakamezeka ikiwa ni ya sala ya fardhi haidhuru neon kama tulivyoeleza nyuma, lakini ikiwa sala ya sunna ni mushkili (ina matatizo) na bora alipe ile saumu.

MAELEZO YA KAFFARAKaffara za Mwezi wa Ramadhani:

Kama tulivyoeleza mwanzo kwamba mtu yeyote atakayetenda makusudi katika mwezi wa Ramadhani mambo kumi yanayovunja saumu basi itamlazimu kulipa ile saumu, au kaff ara pia, nazo ni hizi itampasa kufanya mojawapo:-a. Amuache huru mtumwa mmoja.

Page 46: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

41

b. Afunge miezi miwili (siku sitini).c. Awalishe masikini sitini, au awape kila masikini hao sitini mud (kibaba)

kimoja cha ngano au shayiri na kadhalika.

Mwenye kutaka kufunga siku sitini, lazima siku thelathini na moja (31) afunge mfululizo na zilizobaki anaruhusiwa kuzigawa.

Ikiwa mtu anataka kufunga hizo sitini za kaff ara, basi asianze kufunga wakati ambapo itaingia katika hizo siku thelathini na moja, siku ambayo kufunga kwake ni haramu, kwa mfano, siku kuu kubwa (Idi ya kuchinja nyama). Ikiwa mtu ambaye inampasa kufunga mfululizo siku thelathini na moja, akiachakufunga siku moja kati ya siku hizo, bila ya udhuru, hapo itambidi kuanza upya hizo siku thelathini na moja; lakini ikiwa umetokea udhuru (ambao kwa sharia unakubaliwa) kama mwanamke kumjia hedhi, au nifasi, au mtu akapata ugonjwa (na kufunga kutamdhuru) au imembidi kusafi ri, hawa wote baada ya kuondoka udhuru wao, haitawalazimu kuanzia mwanzo, bali watamaliza, siku zao zilizobaki.

Ikiwa mtu katika hizo kaff ara tatu hawezi kutimiza hata moja, basi lazima afunge mfululizo siku kumi na nane (18). Na ikiwa hawezi hata hiyo, basi atoe sadaka kwa kuwapa masikini awezayo mud (kibaba) kila mmoja, na ikiwa kufunga na kutoa chakula mud vile vile hawezi, basi atoe Istighfari kwa kusema AS-TAGH-FIRUL-LAAH, na itamlazimu akipata uwezo baadaye alipe hiyo kaff ara.

Ikiwa katika hali ya saumu mtu katenda moja katika vitu vinavyovunja saumu mara nyingi katika siku moja hiyo basi kaff ara yake kwa yote aliyoyatenda kwa siku hiyo ni moja katika tatu, isipokuwa kumwingilia mke wa halali na kutoa manii (shahawa) Istimna itarejea kaff ara kwa kila uingiliaji.

Ikiwa kwa kitu cha haramu kavunja saumu yake basi ni wajibu azilipe zote kaff ara tatu tulizozitaja hapo mwanzo. Hakuna tafauti kitu kile kiwe tangu asili ni haramu, kama, mvinyo, au kuzini, au kwa sababu fulani fulani kikawa haramu, kama kumwingilia mke wake wa halali katika hali ya hedhi

Page 47: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

42

au chakula cha halali ambacho akila kitamdhuru.

Ikiwa mtu anafunga (analipa) kadha, basi haruhusiwi kuvunja hiyo saumu baada ya adhuhuri, na akifuturu basi itambidi kutoa kaff ara kwa kuwalisha masikini kumi (10), kila maskini “Mud” moja, na kama hana uwezo huo basi afunge siku tatu mfululizo.

Ikiwa mtu kaweka nadhiri au ahadi au kaapa kufunga siku maalum, na siku hiyo makusudi kabatilisha saumu yake, hapo ni wajibu atoe kaff ara, kwa kumwacha huru mtumwa mmoja, au kuwalisha masikini kumi au kuwavisha; na ikiwa hawezi hayo, basi afunge siku tatu mfululizo.

Katika kaff ara yoyote haijuzu kulipa pesa badala ya kitu kinachotakiwa utoe.

MLANGO 9MATUKIO MUHIMU KATIKA MWEZI WA RAMADHANI

Mwezi wa Ramadhani umejaa kwa matukio adhimu ya historia ya Uislaam na yasiokuwa ya Uislaam. Mwezi huu mtukufu ni mwezi ambao viliteremshwa Vitabu juu ya Mitume na Marasuli. Inatosha katika utukufu wa mwezi huu na kuwa ni bora kuliko miezi mingine kwa kuterenishwa vitabu vitakatifu, ijapokuwa kuna mambo mengi yanayozidisha pia utukufu wa mwezi huu.

Huenda kwa ajili ya matukio muhimu, yaliyotokea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ndio ikafaradhishwa kufunga. Na sasa hapa tunakuleteeni baadhi ya matukio adhimu kwa mpango wa siku za Ramadhani.

Siku ya KwanzaSiku hiyo vilikuwa vita vya Tabuk kama ilivyo tajwa katika kitabu cha Waqai-ush-shuhuur-e-wa-ay-yaam. Navyo ni vita alivyo pigana Mtume (s.a.w) kwenye Tabuk, mahala ambapo walikusanyika jeshi la warumi kuushinda Uislaam na Waislaam. Tabuk ni mji kati ya Madina na Damascus.

Page 48: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

43

Siku ya PiliSiku hiyo ameteremshiwa Mtume Ibrahim (a.s) Sura tukufu za hukumu za Mwenyezi Mungu.

Siku ya Sita Siku hiyo katika mwaka 201 A.H., watu walimbaayi Imam wetu wa nane, al-Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s).

Siku ya KumiSiku hiyo ambapo alifariki Ummul Momineen Bibi Khadijah bint Khuwaylid (mke wa kwanza wa Mtume (s.a.w.)) mwaka 10 A.H.

Siku ya Kumi na TanoSiku hiyo ambapo alizaliwa Imam wetu wa pili al-Imam al-Hassan bin Ali bin Abi Talib (a.s) katika mwaka wa nne.

Siku ya Kumi na Saba Usiku wa siku hiyo, mwaka wa pili, yamekutana majeshi ya Mtume (s.a.w) na majeshi ya makafi ri kwenye ardhi inayoitwa Badri, na mchana wake ikapiganwa vita kubwa vya Badri ambavyo Mwenyezi Mungu aliwapa ushindi masahaba wa Mtume (s.a.w) juu ya mushrikiin. Na vile vile usiku wake (kama inavyo semekana) Mtume akaenda Miraji kutoka nyumba ya Ummu Haani, dada yake Amir al-Muminin Ali bin Abi Talib (a.s) katika Makka; ambapo akapanda Buraq na kuruka kwenda juu mbinguni, na Mwenyezi Mungu matukio hayo ameyataja mwanzoni mwa sura ya Is-raa katika Qur’ani. (juzu 15: S 17). Pia (kama inavyo semekana) siku hiyo alifariki Aisha bint Abi Bakr.

Siku ya Kumi na TisaSiku adhimu kwa Waislamu, siku ambayo imebomoka nguzo ya Kuongokea (Hidi) na asubuhi ya siku hiyo ikakatika kamba ya Urwatil Wuth-qa (kishiko chenye nguvu) na umoja wa Waislamu ukatawanyika. Hii ni siku ambayo Amir al-Muminin Ali bin Abi Talib (a.s) amepigwa kwa upanga katika

Page 49: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

44

Mihrabu ya Masjidul-Kufa (Iraq) alipokuwa akisali, pigo ambalo ndio sababu ya kufariki dunia. Amempiga mtu duni na mbaya kabisa, jina lake Abdur-Rehman bin Muljam al-Murady (Mwenyezi Mungu amlaani).

Siku ya IshiriniKatika siku hiyo, mwaka wa nane wa al-Hijra, Mtume (s.a.w) akauteka mji wa Makka bila ya vita. Na al-Imam Amir al-Muminin Ali (a.s) alipanda juu ya mabega ya mtume kuvunja masanamu yale yaliyokuwa yametundikwa kwenye Kaaba tukufu, akayavunja na akayatupa yote, kama alivyo yavunja baba yake Mtume Ibrahim (a.s) masanamu zama za kale.

Siku ya Ishirini na MojaSiku ya msiba na hasara kubwa; siku ya huzuni kubwa kwa Waislamu wote; kwani siku hiyo amefariki dunia al-Imam Amir al-Muminin Ali (a.s) hakika ni siku ya kusikitika na kulia.

Siku ya Ishirini na TatuUsiku wake ambao ni Laylatul Qadr, uliyo mashuhuri imeteremshwa al-Quranul-Hakeem, kitabu kitukufu cha jamii ya wanadamu wote, na Kanuni za Mwenyezi Mungu hapa Ulimwenguni.

Imeelezwa katika kitabu mashuhuri Majmaul Bayaan kwamba Ibn Abbas amesema, “Mwenyezi Mungu ameteremsha Qur’ani kwa jumla kutoka Al-Law-hul-Mah-fuudh kuletwa mpaka mbingu ya kwanza ya dunia katika usiku wa Laylatul Qadr, baadaye Jibril (a.s) kwa amri ya Mwenyezi Mungu aliteremsha juu ya Mtume Muhammad (s.a.w.) katika wakati makhsusi kidogo kidogo na ikachukua muda wa miaka ishirini na tatu, kuanza mpaka kwisha.

Siku ya Ishirini na NaneSiku ambayo Mtume (s.a.w.) alitengeneza jeshi la Waislamu kwenda kupigana na makafi ri katika vita vya Hunain, mwaka wa nane wa al-Hijra.

Siku ya ThelathiniSiku ambayo Mtume (s.a.w.) alitoka Makka, baada ya kuiteka, kwenda kwenye

Page 50: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

45

vita vya Hunain na majeshi elfu kumi na mbili (elfu mbili watu wa Makka waliobaki watu wa Madina).

Vile vile yapo matukio mengi ya mambo muhimu yaliyofanyika zaidi kuliko tuliyo yataja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, na anayetaka kujua yote hayo, avipitie vitabu vya tarikh na historia. Sisi hapa tumetaka kuandika kwa ufupi basi tukayawacha yote hayo.

MLANGO 10MCHANGANYIKO WA MAMBO MUHIMU

(A) Madhambi Makubwa

Tulieleza mbele kwamba jambo muhimu na la kwanza katika ‘Amal’ (vitendo) katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ni Taqwa (Kujitenga na yaliyo haramishwa).

Tusisahau kuwa Adabu na Adhabu ya kila dhambi katika mwezi huu, tukitenda huwa mara mbili. Kwa hivyo kwa kuwasaidia wasomaji wetu, tunaeleza hapa orodha ya madhambi makubwa (ambayo Mwenyezi Mungu ameahidi kumtia motoni mtendaji), nayo ni haya: 1. (Ash-Shirku Billaah) Kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika. 2. (Al-Ya’su min Rawhil-Laah) Kukata tamaa na rehema za Mola. 3. (Al-Amnu min Makril-Laah) Kutoogopa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. 4. (Uquu-Qul-Waa-lidayn) Kukosa radhi ya wazee na kuwaudhi. 5. (Qatlun-nafsil-muhtarama) Kuua. 6. (Qadhful-Muhsina) Kuwasingizia wanamke wema kwa kuzini. 7. Kula mali ya yatima kwa dhuluma. 8. Kukimbia katika kupigana Jihadi. 9. Kula riba. 10. Kuzini 11. Kulawiti

Page 51: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

46

12. Kutenda mambo ya uchawi. 13. Kuapa kiapo cha uwongo, juu ya jambo au kumkosesha haki ya mtu kwa

kuapa uwongo. 14. Kukataa kutoa zaka iliowajibu kutoa. 15. Kushuhudia uwongo. 16. Kufi cha na kukanusha ushahidi. 17. Kulewa (kunywa mvinyo wa aina yoyote) 18. Kuacha kusali sala ya fardhi au jambo lolote la fardhi makusudi. 19. Kuvunja ahadi. 20. Kukosa kumsaidia jamaa yako kwa jambo lolote la kheri. 21. Kukaa au kuhamia mahala ambapo utakosa mambo ya dini na Imani. 22. Kuiba. 23. Kukanusha mafundisho au jambo lolote la Dini. 24. Kusema uwongo, uwongo wa namna yoyote hasa juu ya Mwenyezi Mungu,

Mitume na Awsiyaa (warithi) wa Mitume. 25. Kula maiti (nyama ya halali aliyekufa au kachinjwa bila kutajwa jina la

Mwenyezi Mungu au hazikutimizwa shuruti za kumfanya mnyama aliyechinjwa awe halali kula).

26. Kula damu namna yoyote. 27. Kula nyama ya nguruwe. 28. Kucheza kamari. 29. Kula thamani ya uchafu. Maiti, mvinyo, ulevi, malipo ya uzinzi,

mirungura, mtabiri (mpiga ramli), kazi kwa mdhalimu, malipo ya kuimba mwanamke, Staranji (chess).

30. Kupunja (Kutoa kasoro kwa kipimo au mizani). 31. Kuzuia haki za watu pasipo na taabu. 32. Takabari (kuwa na kiburi). 33. (Al-Is-ra-fu) Kutumia kwa fujo. 34. Kudharau kwenda kuhiji Makka. 35. Kushughulika, au kwenda kwenye ngoma, muziki na kwenda sinema. 36. Kucheza ngoma (dance). 37. (Al-Gheebah) Kumsema mwenzio. 38. (At-Tuhma) Kutuhumu.

Page 52: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

47

39. (An-Na-Meemah) Uchongezi. 40. Kuwadhihaki Mumineen, kuwaudhi na kutoa siri ya wenzio. 41. Kumchungulia mke au mwanamke yeyote asiyekuhusu, na vile vile

mwanamke kumtazama mwanamme yeyote asiyemhusu au kutoka wanawake nje bila ya kujifunika.

42. Kuvaa mwanamume pete au kitu chochote cha dhahabu, na hariri safi . 43. Kufi cha vyakula vya mahitajio ya watu na kukataa kuuza wakati wa dhiki

kutaka faida nyingi.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani:Tilka, Hu-Duu-Dul-Laahi Fa-Laa Taq-Rabuu-Haa. (2:187)“Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie.” Hakika hizi hukumu za faradhi, haramu, halali, na suna, ndizo mipaka ya Mwenyezi Mungu na ukingo kati ya haki na batili; basi msikaribie kwa ku-kanusha na kuhalifu.

Katika hadithi ya Mtume (s.a.w.) amesema, “Hakika kila mfalme anao ulinzi, na ulinzi kwa Mwenyezi Mungu ni kujilinda na yaliyoharamishwa, basi mwenye kwenda karibu nazo ipo hatari ya kuanguka ndani yake”.

Mwenyezi Mungu amesema:In Tajtanibuu Ka-Baa-ira Maa Tun-Haw-Na An-Hu Nukaf-fir An-kum Say-yi-aa-Tikum Wa Nud-Khil-Kum-Mud Kha-Lan Karee-Maa (4:31)“Kama mkijiepusha na maovu makubwa mnayokatazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu”. Hapa inasema tukijiepusha na ile midhambi mikubwa tuliyo itaja juu, Mungu atatusamehe vile vile vijidhambi vidogo vidogo. Lakini tusiendelee nao wala tusiyadharao kuwa ni vidogo; kwani ukifanya hivyo unatenda dhambi kubwa.

(B) Itikafu

Itikafu ni kutia nia mtu kukaa msikitini muda usiopungua siku tatu na zaidi,

Page 53: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

48

kufanya ibada kama sala, dua, na kadhalika, na hufaa kufanya Itikafu kati ya mwaka mzima siku ambazo hujuzu kafunga saumu. Bora kabisa na ambayo ina thawabu nyingi ni kufanya Itikafu katika mwezi wa Ramdhani na hasa siku za mwisho. Hukaa humo msikitini isipokuwa kwa jambo la dharura sana kama kwenda chooni, kuoga janaba, na vile vile anaruhusiwa kwenda kumzuru mgonjwa, kumwosha na kumvalisha sanda maiti, na kumsalia maiti. Basi muda huo wa kuwa katika Itikafu hapana ruhusa kuingiliana na mkewe japo kuwa huo muda wa kwenda chooni.

Mwenyezi Mungu amesema:Wa-Laa, Tubaa-Shiruu Hun-Na Wa-An-Tum Aa-Kifuu-Na Fil-Masaa-Jid. (2:187)Wala msichanganyike nao (msiwaingilie) na hali mnakaa (Itikafu) misikitini.

(C) Alama na Thibitisho za Kuanza na Kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Ramadhani hudhihirika unapo andama mwezi, na humalizika kwa kuonekana mwezi wa mfungo mosi (Shawwal). Mwezi wa Ramadhani ukionekana tu, kifungo huwa ni wajib kwa wote wanaotakiwa kufunga. Mwezi wa mfungo mosi (Shawwal) ukiandama tu, Ramadhani humalizika.

Mtume (s.a.w.) alisema, “Su-muu li-ru-yati-hi wa af-tirou li-ru-yati-hi fa-in khafi ya fa, ak-miluu id-data sha-ban thala theena yaw-man”.“Fungeni mkiona mwezi na mfunguwe mtapoona mwezi; lakini ukifi chika, imalizeni Shabani kwa siku thelathini, vile vile ikiwa mwezi wa Shawwal haukuonekana kwa sababu ya hali mbaya ya hewa, Ramadhani iwe thelathini”

Njia za kuthibiti mwezi ni tano1. Mtu binafsi auone mwezi. Hapo itamlazimu (Wajib) afunge ikiwa ni mwezi

wa Ramadhani, na itampasa (wajib) afuturu (asifunge) ikiwa ni mwezi wa Shawwal ijapokuwa mtu mwingine hakuuona mwezi.

Page 54: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

49

2. Zipite siku thelathini kamili kwa mwezi wa nyuma. Basi ikiwa zimetimia siku thelathini ya Shabani, ni wajib afunge hata kama hakuona mwezi, na ikiwa zimefi ka siku thelathini za Ramadhani basi lazima siku inayofuata afuturu (asifunge) hata kama mwezi hakuuona.

3. Washuhudie wanaume wawili waadilifu kuwa wameuona mwezi kwa macho yao; (lakini hao waadilifu wasiwe wanahitalifi ana katika maelezo ya kuona mwezi, kwa mfano mmoja aseme umekaa hivi na mwembamba sana, na wa pili aseme ulikuwa juu sana na mnene; basi hapo shahada hizo hazithibiti). Hapo ni wajib afunge ikiwa ni mwezi wa Ramadhani, na itampasa kufuturu (asifunge) ikiwa ni mwezi wa Shawwali.

4. ASH-SHI-YAA. Kikundi cha watu au makundi ya watu washuhudie kwamba mwezi wameuona, na wewe kwa ushuhuda huo upate yakini ndipo itakulazimu kufunga au kufuturu; lakini ikiwa kwa ushahidi huo hukupata yakini basi huwezi kufunga au kufuturu.

5. Akihukumu Mujtahid (Mwanachuoni) mwadilifu kwamba kesho ni mwezi mosi na unao uhakika wa maelezo ya kuandama mwezi aliyoyapata sahihi (thabiti) basi ni wajibu watu wote wafuate.

Mwezi kuwapo juu sana au kuwa ni mkubwa au kuchelewa kuzama haiwi dalili na thibitisho ya kuwa usiku wa jana ilikuwa usiku wa mwezi mosi, na leo mwezi pili. Mwezi hauthibiti kwa kuandikwa magazetini au kwa kusemwa na wenye elimu ya nyota (Metreology). Haithibiti mwezi kwa sheria ikiwa wameona wanawake tu, wala akiuona mtu mmoja mwadilifu hata akiapa kiapo pia. Lakini ikiwa kwa jambo lolote inakuletea yakini na uthibitisho rohoni mwako kwa kuandama mwezi basi juu yako wewe tu, ni wajibu kuifuata, si mwenzio.

Ikiwa imethibiti mwezi katika mji mmoja, kwa watu wa mji wa pili haina faida, isipokuwa mji huo uwe karibu na mji wako, au wenye ‘ufuq (MATLAI) moja. ‘Ufuq (Matlai) moja ni miji ile ambayo ipo karibu na mji uliomo wewe. (Aga Khui haafi kiani hapa).

Page 55: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

50

MLANGO 11 ZAKAT-UL- FITRI

Al-Fitra

Moja katika maana yake ni kuumba (kuhuluku). Kama ilivyo kuwa kwa kutoa zaka ya mali, huingia baraka na ikazidi mali ya mtoa zaka, basi kwa kutoa zaka ya Al-Fitri husababisha kusafi ka roho na kukulinda na maut mbaya na humtakasa yule mtu na madhambi.

Imepokewa hadithi inatokana na al-Imam as-Sadiq (a.s) kwamba alimwamrisha mjumbe wake: “Nenda toa zaka ya Fitri ya watu wote wa nyumbani, wala usimwache hata mtu mmoja; kwani ukiwacha kutoa zaka ya mmoja katika hao, namwogopea kufa”.

Kutoa zaka ya Fitri ndio sababu ya kuifanya saumu yako ikamilike na ikubaliwe. Basi asiyetoa (mwenye kuweza kutoa) mtu huyo hana saumu, wala haitakubaliwa saumu yake. Katika hadithi iliyotokana na al-Imam Jafar as-Sadiq (a.s) inasema hiyi: “Ukamilifu wa saumu ni kutoa zaka ya Fitri, kama ilivyokuwa Kumsalia Mtume (s.a.w.) na Ahli Baiti wake (a.s.) katika sala ndio ukamilifu wa sala. Basi mtu akifunga na hakutoa zaka makusudi basi hana saumu, na akiwacha kumsalia Mtume (s.a.w.) na Ahli Baiti wake (a.s.) makusudi basi hana sala vile vile.”

Mwenyezi Mungu ameanzia kwa hiyo zaka, kabla ya kusali na akasema katika Qur’ani, katika sura ya A’ala (87:14 na 15): Qad-Aflaha Mantazakka. Wadhakari Sma Rabbihii Fa Swallaa.“Hakika amekwisha faulu mwenye kujitakasa (kwa kutoa zaka) na akakumbuka jina la Mola wake akasali.”

Shuruti za Kufaradhisha Mtu Kutoa Zaka1. Ubaleghe. Awe amebaleghe.2. Akili. Awe mwenye akili.

Page 56: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

51

3. Ghumia. Asiwe amezimia. (Aga Khui haafi kiani hapa).4. Uhuru. Asiwe mtumwa.5. Utajiri. Awe mwenye mali.

Shuruti za Kusihi Zaka ni Mbili:1. Uislamu. Asiwe kafi ri.2. Kutoa Lillahi Taala. Asitoe kwa Riya (kuonesha watu).

Kwa hivyo haitakuwa wajibu kwa mtoto asiyebalehe hata akiwa na pesa; wala mwenda wazimu; wala kwa mtu yule ambaye mwezi wa Shawwal (mfungo mosi) umeandama na yeye hali amezimia; wala kwa mtumwa; wala masikini.

Kwa Sharia Tajiri ni nani?Muradi na kipimo ni hiki: Mtu awe na mali au pesa ya kutosha mwaka mzima matumizi yake na watu wake wote wa nyumbani; haidhuru pesa hizo anazo kwa jumla au anacho kipato kama mshahara, kodi, biashara, ambacho kitatimiza mahitajio yake yote.

Basi kwa hiyo ikiwa katika njia hizo mbili hana hata moja, hapo mtu huyu huitwa masikini, na zaka ya Fitri haimlazimu kutoa, bali ni thawabu tu, na anaweza kufanya namna tutavyoeleza baadaye.

Ni wajibu kutoa zaka ya Fitri kwa kila mtu ambaye zimekamilika shuruti zote za kumfaradhisha. Atoe kwa nafasi yake, na kwa kila aliyekuwa ahali (jamaa) yake, wakati unapoingia usiku wa Idul-Fitri unapoandama mwezi wa mfungo mosi. Wala hakuna tofauti kwa wale wenye kuwatolea wawe katika wale ambao ni wajibu kuwalisha kama mke na watoto, au si fardhi kuwalisha kama ndugu, mgeni, na mtumishi, madamu wamo katika ahali hata kama sio jamaa au sio Mwislamu; hao wote lazima awatolee hata wakiwa mahala pengine. Mtoto aliyopo tumboni mwa mama yake hailazimu kutoa Fitri yake lakini akizaliwa kabla ya magharibi ya usiku wa Idi basi ni wajibu atolewe.

Akifa mtu baada ya magharibi ya usiku wa Idi ni lazima zaka yake pamoja na

Page 57: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

52

zaka za watu wa nyumba yake zitolewe katika mali yake. Na ikiwa amekufa kabla ya magharibi si fardhi kutoa zaka yake wala ya watu wake. (Ikiwa hao watu wake (maiti) wanazo shuruti za kufaradhika itawabidi watoe hiyo zaka katika mali zao).

Ikiwa umemkaribisha (alika) mtu usiku wa Idi kuja kufuturu kwako na baada ya magharibi kaja kufuturu kwako haitakulazimu (wajibu) kutoa Fitri ya huyo uliemwalika ijapokuwa ulimwalika tangu mchana. Lakini akifi ka kabla ya maghribi na ikiingia magharibi kwako hapo itakubidi utoe zaka yake.

Ikiwa mtu wakati wa magharibi wa usiku wa Idi, akiingiliwa na wazimu, kutoa zaka kwao si fardhi, lakini ikiwa kabla ya kuingia magharibi au wakati ule ule wa kuingia magharibi mwenda wazimu kapata akili, mtoto kabaleghe au maskini kapata mali na akawa tajiri, na ikiwa shuruti zingine pia zimetimia, basi itawapasa watoe zaka.

Ni suna kwa masikini asiyemiliki chakula kwa mwaka mmojo kutoa zaka ya Fitri hivi: Atoe sehemu iliyowekwa kwa nia ya zaka kisha ampitishie mkewe tena mtoto mmoja baada ya mwingine kwa nia hiyo hiyo hadi kwa kila mmoja wa nyumba yake. Hatimaye atoe sehemu ile kwa masikini. Kwa kufanya hivyo Mwenyezi Mungu atawakubalia wote wa nyumba hiyo kwamba wamelipa zaka zao.

Aina ya Vitu vya Kutolea Zaka ya FitriChakula kinacholiwa sana katika nchi, kwa mfano, ngano, mchele, shayiri, tende, zabibu, mahindi, unga na maziwa. Ni thawabu na ina fadhila sana kutoa zaka kwa tende. Ukitoa bei ya mojawapo ya vitu hivyo itajuzu; si lazima kutoa hasa kile kitu, bali wakati mwingine ni bora sana kutoa pesa kupewa yule maskini ili aweze kununua nguo yake au ya watu wake.

Kadri na Kiasi cha FitriKwa kipimo kilicho tajwa katika vitabu vya sharia ni ‘SAA’ moja ambayo ni sawa na kilo tatu na gram mia mbili (31⁄5 kilo) ambazo ni ratili sita na nusu kiasi.

Page 58: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

53

Wakati wa Kutoa Zaka ya FitriWakati wa kutoa zaka ya Fitri huanzia panapo zama jua siku ya mwisho wa Ramadhani. Wale wanaosali sala ya Idi inawapasa wasicheleweshe kutoa hiyo zaka mpaka wakati wa sala ya Idi, bali kabla yake iwe wameshatoa; na wasio sali sala ya Idi hawaruhusiwi kuahirisha kutoa hadi sala ya adhuhuri, bali waitoe kabla ya kuingia wakati huo.

Ikiwa mtu katenga zaka ya Fitri, basi haijuzu kubadilisha kile kitu au pesa. Na akichelewesha kumpa masikini, kwa hali aliweza kumfi kishia masikini, na ikaja potea, basi itamlazimu kulipa.

Na ikiwa hadi wakati huo hakutoa au hakutenga kiasi kinachombidi kutoa, basi sasa akitoa asinuwie kwa nia ya “adaa” au “qadhaa” bali atoe qurbatan illa-llah. Mtu akitenga (pesa au kitu) zaka huo wakati ulioainishwa na akazuwia kutoa kumngojea huyo masikini mahsusi aliemkusudia kumpa anaruhusiwa hivyo. Haruhusiwi kutoa zaka ya Fitri kabla ya mwezi wa Ramadhani; na hata katika mwezi wa Ramadhani huwezi kumpa masikini zaka hiyo ila kama unamkopa na baadae utapoingia usiku wa Idi, ile pesa uliomkopesha huyo masikini ukalipia hivi leo; ni bora zaidi ukimpa hiyo zaka mkononi mwake, na baadae huyo masikini akurejeshee kama analipa deni.

Matumizi ya Zaka ya Fitri Zaka ya Fitri wapewe masikini “MU-MIN” na bora kabisa jamaa zako masikini walio karibu na wewe sana, majirani Muumin, na wanafunzi wanaochukua elimu ya dini na sharia ya Kiislaam. Usimpe masikini chini ya kadri ya zaka ya mtu mmoja hata wakiwa wanaostahiki ni wengi au watakosa vilevile unaruhusiwa kumpa masikini zaidi ya zaka ya mtu mmoja. Huwezi kuwapa zaka ya Fitri wale ambao ni jamaa zako (wenye kukupasa kuwalisha) na umewatolea wewe Fitri zao. Unaweza kumpelekea Mujtahidi wako (ambaye unamfuata) hizo pesa zako za Zaka ya Fitri ikiwa hakuna masikini katika mji ukaao.

Page 59: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

54

MLANGO 12 SALA YA IDI

Sala ya Idul-Fitri na Idul-Adh-ha (sikukuu kubwa) asili yake ni faradhi; na mmoja katika shuruti zake muhimu ni kuhudhuria Mtume (s.a.w.) au mmoja katika Ma-Imamu kumi na wawili au Naibu wao mahsusi. Kwa vile sharti ya sala hiyo wakati huu haikutimu, basi sala hiyo sasa ni sunna tu.

Sala hiyo unaweza kusali peke yako na kwa jamaa pia; ni bora na ina thawabu nyingi kusali kwa jamaa. Wakati wa kusali sala za Idi ni wakati wa kutoka jua hadi adhuri.

Namna ya Kusali:Sala za Idi ni rakaa mbili tu. Baada ya kunuia na kutamka Takbeeratul Ihram, katika hali ya kusimama (Qiyaam) uta soma Sura ya Al-Hamdu na baadae Sura moja ya Qur’ani (Ni bora kabisa kusoma Sura ya Al-Aala (87:1-19) inayo anza kwa Sab-Bi-His-Ma Rab-Bikal-Aala). Ukiisha maliza Sura hiyo, utatamka takbira mara tano, na baada ya kila takbira utafanya Qunuut (unyanyue mikono yako juu sawa na uso wako kama tulivyoeleza katika mlango wa 14 wa kitabu cha sala) na utasoma dua ifuatayo. Tena utatamka takbira ya sita na utakwenda rukuu tena sajdah mbili. Hapo utainuka kwa rakaa ya pili na utasoma Sura ya Al-Hamdu na baadaye Sura moja ya Qur’ani (Ni bora sana kusoma Sura ya Wash-Shams (91:1-15)). Na baadae utatamka takbira nne mara hii, na baada ya kila takbira utafanya Qunuut, na utasoma dua ifuatayo. Tena utatamka takbira ya tano, na utakwenda rukuu, tena sajda mbili; baadaye utakaa utasoma ‘Tashah-hud’ na baadaye utamaliza sala kwa kutoa salaam kama desturi.

Unaweza vile vile katika sala ya Idi baada ya Sura ya Al-Hamdu, katika rakaa ya kwanza, usome Sura ya Wash-Shams na katika rakaa ya pili baada ya Sura ya Al-Hamdu usome Sura ya Ghaa-shiya ((88:1-26) inayo anza kwa Hal ataaka hadee-thul ghaa-shiya).

Page 60: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

55

Dua ya QunuutAl-laa-hum-ma ah-lal kib-riyaa-i wal-adhamah; wa ahlal juudi wal jaba-ruut; wa ah-lal-af-wi war-ra-rah-mah; wa ah-lat-taq-waa wal magh-fi rah; as-aluka bi-haq-qi ha-dhal yaw-mil-ladhi jaal-tahu lil-mus-limeena iy-daa, wali-Muhammadin, sal-lal-laa-hu alay-hi wa AA-lihi, dhukh-ran wa sha-ra-fan waka-ra-matan wama-zee-daa, an tu-sal-liya alaa Muhammadin wa Aa-li Muhammad wa-an-tud-khila-nee fee, kul-li khay-rin ad khalta fee-hi Muhammadan wa AA-la Muhammad, wa-an tukh-rija-nee min kul-li suu-in akh-rajta min-hu Muhammadan wa-AA-la Muhammad. Sala-waa-tuka, alay-hi wa alay-him. Al-laa-hum-ma in-nee as-aluka khay-ra maa sa-alaka bi-hee ibaa-dukas-saa-lihuun; wa au-dhu, bika mim-mas-ta-aa-dha min-hu Ibaa-dukal mukhli-suun.

Ikiwa mtu anasali sala za Idi kwa jamaa, lazima asisome Qara-at (sura ya Al-Hamdu na sura nyingine) kama anavyosali sala za fardhi kwa jamaa kila siku, kwa kuacha kusoma Qaraat tu, huku amsikie Imamu anazisoma; vitendo na masemo yaliyobaki yote lazima atende na ayasome yeye.

Ikiwa Maamumu kafi ka wakati ambapo Imam ameshazisoma baadhi ya Qunuut basi akienda Imam katika rukuu yeye azitimize zile Qunuuti asizoziwahi, ijapokuwa katika kila Qunuut akisema SUB-HAANAL-LAAH, au AL-HAMDU-LIL-LAAH. pia itatosha na baadaye amfuatie Imam.

Ikiwa mtu katika sala ya Idi kafi ka wakati ambao Imam yupo katika rukuu, basi baada ya nia na kusema Takbeeratul Ihraam tu, amfuate Imam (aingie katika rukuu).

Ni sunna baada ya sala ya magharibi, isha, usiku, kuamkia Idul-Fitri na baada ya Idul-Fitri kuzisoma takbeeraat hizi : Al-laa-hu akbar, Al-laa-hu-akbar, Laa-ilaa-ha il-lal-laa-hu wal-laahu-akbar, Al-laa-hu-akbar, walil-laa-hil-hamd, Al-laa-hu-akbar alaa maa hadaa-naa.

Na ikiwa Idul-Adh-ha basi Takbeeraat hizo ni sunna kuzisoma baada ya sala

Page 61: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

56

kumi (10) kuanzia sala ya adhuhuri ya tarehe kumi (mfungo tatu) hadi sala ya asubuhi ya tarehe kumi na mbili (mfungi tatu); lakini utaongeza Takbeeraat ya sikukuu hii maneno haya: Al-laa-hu akbar, Alaa maa razaqa-naa min bahee-matil an-aam, wal-hamdu-lillaahi alaa maa ab-laa-naa.

Na ikiwa Mwenyezi Mungu amemjaalia mtu awepo Hija katika Mina siku hiyo, basi Takbeerat ufululize hadi baada ya sala ya asubuhi ya tarehe kumi na tatu (mfungo tatu). Mwenyezi Mungu atujalie sote tuwepo huko kila mwaka. Amin.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani: Wali-tuk-milul-iddata, wali-tukab-birul-laaha ala maa hadaa-kum, wala-allakum tash-ku-ruun (2:185). “Na (pia anakutakieni) mtimize hiyo hesabu (wa kufunga), na (anakutakieni) kumtukuza Mwenyeezi Mungu kwa kuwa amewaongozeni (kwenye dini), na ili mpate kushukuru (kwa neema hiyo na neema zote).”

Katika hadithi inayotokana na al-Imam ar-Ridha (a.s.) (Imam wa nane), imesema hivi: “Kwa ajili ya hii, katika sala ya Idi imefanywa takbira nyingi zaidi kuliko sala zote zingine; kwa sababu, takbira, hakika, ni taadhima kwa Mola na kumtukuza kwa namna alivyotuahidi na kutupa afya, kufuata alivyosema Mwenyezi Mungu katika Qur’ani.”

RABBANA TAQABBAL MINAAINNAKA ANTAS-SAMEE-UL-ALEEM

SUB-HAANAL-LAAHI WAL-HAMDU-LIL-LAAHIWALAA ILAAHA ILLA-LLAAHU

WA-LLAAHU-AKBAR

Page 62: Kitabu cha Saumu - Shia Maktab

Kimetolewa na Kuchapishwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P 20033Dar es Salaam

ISBN: 9976 956 21 5