4
TOLEO NAMBA 094 | JULAI 31, 2021 1 KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA KUPATA MITAJI SUMAJKT Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe (alievaa tai) akipokea zawadi kutoka Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali (Mstaafu) Farah Mohamed, baada ya kikao cha bodi, wengine ni Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele (wapili kutoka kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi (wakwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi.

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA …

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA …

TOLEO NAMBA 094 | JULAI 31, 2021

1

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA KUPATA MITAJI SUMAJKT

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe (alievaa tai) akipokea zawadi kutoka Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali (Mstaafu) Farah Mohamed, baada ya kikao cha bodi, wengine ni Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele (wapili kutoka kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi (wakwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi.

Page 2: KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA …

TOLEO NAMBA 094 | JULAI 31, 2021

2 2

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA KUPATA MITAJI SUMAJKT

K atibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt Faraji Mnyepe ameeleza namna ya kutatua changamoto ya kupata Mitaji kwa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa ( SUMAJKT).

Dkt. Mnyepe ameeleza hayo jana julai 30, 2021 kwenye kikao cha bodi ya SUMAJKT kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt Mnyepe amefafanua kuwa zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetengwa na Wizara ya Ulinzi na JKT kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya shirika hilo.

Dkt.Mnyepe amefafanua kuwa namna mbadala ya kutatua tatizo la fedha za Miradi ya maendeleo kwa SUMAJKT ni kuandika maandiko ya mitaji.

"Matatizo yote ya mitaji andikeni andiko mniletee, mimi na Waziri kazi yetu ni kutafuta fedha kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi na JKT " alisema Dtk. Mnyepe.

Pia, Dkt.Mnyepe amesisitiza watendaji wa JKT kuipitia bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT ambayo iliwasilishwa Bungeni tarehe 20 Mei 2021.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali ( Mstaafu) Farah Mohamed, ameeleza kuwa

katika kipindi chote bodi imeshuhudia mabadiliko ya Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo lakini hayakuweza kuathiri Shirika, nao kama bodi wataendelea kushirikiana na uongozi wa SUMAJKT kwa kutoa ushauri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Meja Jenerali Mohamed ameongeza kuwa kazi ya bodi ni kushauri, anashukuru katika kipindi cha uongozi wa bodi hiyo Shirika limekuwa linatekeleza ushauri wote ambao umekuwa unatolewa na bodi hiyo.

Naye Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt.faraji Mnyepe kwa namna wanavyopambana ili kuhakikisha Wizara inasonga mbele.

"Jeshini huwa hawajadili maelekezo bali hutekelezwa kama kuna sehemu utakwama utarudi kwa aliye kuelekeza ili akupe ufafanuzi zaidi" alieleza Brigedia Jenerali Rajabu Mabele

SUMAJKT linashughulika na Uuzaji na usambazaji wa zana za kilimo na vizuri vyake, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi na Uhandisi, Huduma za biashara pamoja na Viwanda.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe, (wapili kutoka kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali Farah Mohamed (wakwanza kushoto) Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele ( wapili kutoka kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi, wakiwa kwenye kikao cha bodi ya SUMAJKT kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Page 3: KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA …

TOLEO NAMBA 094 | JULAI 31, 2021

Matukio Katika Picha

3

Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali Farah Mohamed ( Mstaafu), akiongea na Wakurugenzi wa Idara, Kampuni za SUMAJKT pamoja na wajumbe wa bodi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe, akizungumza Wakurugenzi, wakuu wa Idara na Kampuni za SUMAJKT kwenye kikao cha bodi ya SUMAJKT kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru mwenge jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele, akiongea na Wakurugenzi wa Kampuni, Idara na Wakuu wa Miradi wa SUMAJKT katika kikao cha bodi kilichofanyika katika ukum-bi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi, akizungumza na Wakurugenzi wa Kampuni, Wakuu wa Idara na Miradi ya SUMAJKT katika kikao cha bodi ya SUMAJKT kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Page 4: KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI ATOA MWANGA WA …

TOLEO NAMBA 094 | JULAI 31, 2021

Matukio Katika Picha

4

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe (katikati) Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali ( Mstaafu) Farah Mohamed (wapili kutoka kushoto) Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele (wapili kutoka kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi (wakwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi baada ya kikao cha bodi mwenge jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Mnyepe (alievaa tai) Mwenyekiti wa bodi ya SUMAJKT Meja Jenerali (Mstaafu) Farah Mohamed (wakwanza kushoto) Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele (wapili kutoka kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Absolomon Shausi (wakwanza kulia) Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Hassan Mabena (wakwanza kutoka kushoto waliosimama nyuma) Mkuu wa Tawi la Sheria JKT Kanali Projest Rutahiwa ( wapili kutoka kulia) Msaidizi wa Mkuu wa JKT Kanali Laurence Lugenge (watatu kutoka kushoto) Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha bodi ya SUMAJKT.

Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Hassan Mabena (wapili kutoka kulia) Mkuu wa Tawi la Sheria JKT Kanali Projest Rutahiwa (watatu kutoka kulia) Msaidizi wa Mkuu wa JKT Kanali Laurence Lugenge ( wakwanza kulia) Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata, na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Miradi wakiwa katika kikao cha bodi kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mwendeshaji Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Mhandisi Morgani Nyonyi(watatu kutoka kushoto) Meneja Ujenzi Kanda ya Mashariki Kanali Samuel Machemba (wapili kutoka kushoto) Meneja Ujenzi Nyanda za juu Kusini Luteni Kanali Juma Mvumbo( wakwanza kulia) na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti SUMAJKT Luteni Kanali George Wang'ombe (wakwanza kulia), wakiwa na Wakurugenzi na wa wakuu wa Idara katika kikao cha bodi ya SUMAJKT kilichofanyika katika ukumbi wa Uhuru Mwenge jijini Dar es salaam.