20
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 140, Aprili, 2019 ISSN 0856-874X Mwakyembe apingwa Mbunge apongeza MCT, LHRC na THRDC Baraza lazindua vitabu Uk5 Uk 20 Uk 7 Kampeni yaanzishwa kumtafuta Azory Gwanda

Kampeni kumtafuta Azory Gwanda - MCT

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 140, Aprili, 2019ISSN 0856-874X

Mwakyembe apingwa

Mbunge apongeza MCT, LHRC na THRDC

Baraza lazindua vitabu

Uk5 Uk 20Uk 7

Kampeni yaanzishwa kumtafuta Azory Gwanda

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Mwandishi Azory Gwanda ambaye ametoweka na sasa zimepita zaidi ya siku 500 tangu alipotoweka Novemba 21, 2017.

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Tupiganie uhuru wa kweli wa habari na wa kujielezaWakati tunaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Duniani (WPFD) Mei 3, 2019 kwa hapa Tanzania inakumbusha hali mbaya ambapo uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza unazidi kusinyaa.

Woga na hofu vimetamalaki huku hatua za kujidhibiti wenyewe zinakwaza vyombo vya habari. Ili kuweza kumudu kuwepo katika hali ya sasa, wamiliki na wahariri wanajidhibiti kwa kuchapisha habari salama na kusifia.

Hii inadhihirishwa na tabia inayochukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kujifungia vyenyewe baada ya kuripoti habari wanazoshuku kuwa hazikuwapendeza wenye mamlaka.

Hatua kama hizo zimechukuliwa bila ya wenye mamlaka kulalamika.

Hali ilivyo hapa nchini inakinzana na kauli mbiu ya maadhimisho ya hayo ya siku ya Uhuru wa habari duniani ambayo ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia: Uandishi na Uchaguzi katika Zama za Upotoshaji”.

Maadhimisho hayo katika ngazi ya Kitaifa, yanafanyika Dodoma.Ni muhimu hata hivyo, vyombo vya habari vijidhatiti

kuendeleza shughuli zake licha ya vikwazo kwa kuwa uhuru haupatikani kirahisi.

Utaratibu wa kujidhibiti unaofanywa na vyombo vya habari kutokana na aina ya habari wanazoandika na kuchapisha na sheria mbaya zilizopo zikiwemo ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na Sheria ya Takwimu, zinakwaza shughuli za vyombo vya habari na hata uzalishaji mapato. Matokeo ya hali hii mbaya , vyombo vingi vya habari vina matatizo ya kutimiza majukumu yao kama kulipa mishahara na hata kulipia gharama za uchapishaji.

Wakati tunaandika maoni haya, baadhi ya vyombo vikubwa vya habari vimeshatoa notisi kwa watumishi wao kuwaeleza nia ya kuwapunguza.

Wakati vyombo vikubwa vya habari vinakabiliwa na matatizo kama hayo, kundi la vyombo vingine vya habari linapeta kwa kuandika habari bila kuzingatia maadili ya taaluma na havikemewi.

Wenye mamlaka wanachukua hatua dhidi ya vyombo vingine vya habari ikiwa pamoja na kusimamisha leseni jambo ambalo linaonyesha upendeleo huku wakisema kuwa watu wanaona wanakerwa na magazeti hayo mengine waende mahakamani.

Pia wakati tunaadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani mwaka huu, mwandishi Azory Gwanda bado hajulikani aliko zikiwa ni zaidi ya siku 500 tangu atoweke huku wenye mamlaka hawachukui hatua ya kufanya uchunguzi na kueleza ukweli kuhusu mwandishi huyo.

Hii imefanya wanahabari na wadau wa habari kuanzisha kampeni ya kushinikiza wenye mamlaka waeleze wapi alipo Azory Gwanda.

Pia tunavyoadhimisha siku hii muhimu, wanahabari na wadau tujitutumue kuhakikisha kuwa hali inakuwa nzuri nchini mwetu ambapo michango ya wanahabari inakuwa muhimu kwa maendeleo.

Lazima tukatae kutishwa na kusalimu kwa wadhibiti wa habari.Ni muhimu kuchukua hatua na kuwa makini dhidi ya

kutumiwa kwa kuwa mwa huu kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Na Mwandishi wa Barazani

Ni zaidi ya siku 500 tangu Azory Gwanda, mwandishi wa kujitegema aliyekuwa akifanya kazi kutoka

Kibiti, Mkoa wa Pwani ali-potoweka November 21, 2017.

Wenye mamlaka wameshindwa ku-fanya uchunguzi kujibu swali hili: Azory yuko wapi?

Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) umeanzisha kampeni ya kupata saini kushinikiza wenye mamlaka ku-

chukua hatua Umoja huo katika maombi yake ya

kutafutwa kwa Gwanda umeeleza ya-fuatayo:

Mosi, Wizara ya Mambo ya Ndani itamke waziwazi kuwa Azory Gwanda ametoweka.

Pili, Serikali iviwezeshe vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina kutoweka kwa Gwanda kulingana na Kanuni za Polisi Na. 232 kuhusiana na watu waliotoweka.

Tatu, Vyombo vya usalama, hasa Jeshi la Polisi vitoe taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya uchun-

guzi huo.Nne, Vyombo vya habari vitangaze

taarifa zake kama mtu aliyepotea.Tano, Wamiliki wa vyombo vya

habari washirikiane kuandaa utarat-ibu wa wanahabari wanaotoweka ikiwa pamoja na kupata taarifa kutoka mamlaka husika kwa asiji ya ma-wasiliano ya umma.

Sita, Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora (CHRAGG) itekeleze wa-jibu wake kufuatilia kutoweka kwa Gwanda na mamlaka husika.

Saba, Mkuu wa Mabalozi wa-naowakilisha nchi zao Tanzania awe ta-yari kutoa msaada kwa uchunguzi wa serikali kuhusu kutoweka kwa Gwanda.

Kama unaunga mkono kampeni hii ya kumtafuta Gwanda tia saini kupi-tia kiunganishi hiki http://bit.ly/Azory-Petition

Gwanda’ alikuwa akiripoti kuhusu mauaji pamoja na utekaji wa watend-aji wa serikali katika ngazi za mitaa na Polisi katika mkoa wa Pwani.

Habari zake zilichapishwa katika gazeti la Mwananchi na The Citizen.

Mke wake Anna Penoni alikuwa mtu wa mwisho kumwona kabla ya ku-toweka kwake, November 21, 2017.

Aliondoka na watu wasiojulikana waliokuwa katika gari la aina ya Toy-ota Land Cruiser lililokuwa na rangi nyeupe.

Alimuaga mkewe kuwa angerudi baada ya siku moja lakini hadi sasa hajaonekana tena.

CoRI yazindua kampeni kumtafuta Azory Gwanda

Mwandishi Azory Gwanda aliyetoweka tangu Novemba 21,2017 – Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CORI) waanzisha kampeni ya kumtafuta.

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Utaratibu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

16

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

• Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

• Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

• Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

BARAZA LA HABARI TANZANIA

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mi-chezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwamba

watu wasiendelee kuulizia kuhusu alipo mwandishi wa habari Azory Gwanda, kwa kuwa watu wengine kadhaa pia wametoweka, imepingwa vikali.

Akizungumzia kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa vitabu vilivyochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) Aprili 24, 2019 Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga, alisema watu wanahaki kupata taarifa kuhusu jamaa zao waliotoweka.

Alisema inasikitisha kuwa taarifa kama hiyo imetolewa na

mtu msomi - mwanasheria na waziri.

Mukajanga, alisema hatuwezi kuzuiwa kuulia alipo Azory Gwanda. Tutaendelea kuuliza mpaka tupate ukweli.

Hatuwezi kunyamazishwa katika hili, alisema.

Mukajanga alisema kuwa juhudi zimekamilishwa ku zindua mtandaoni kampeni ya kupata saini ikiwa ni jitihada za kuulizia alipo Gwanda kushinikiza wenye

mamlaka

kuchukua hatua. Licha ya Mukajanga, kauli ya Waziri huyo kuhusu Gwanda aliyoitoa Bungeni, ilipingwa na watu mbalimbali.

Baadhi ya wahariri walielezwa kushutushwa na masikitiko katika mitandao ya kijamii huku wengine wakihoji kama waziri ana ubinadamu.

Mapema katika maelezo yake wakati wa unzinduzi wa vitabu alisema kuwa hofu imetamalaki katika jamii - wahariri wanajidhibiti wenyewe na wakati mwingine vyombo vya habari vinajifungia.

Wenye mamlaka pia wanafungia vyombo vya habari vikubwa, akitoa mfano wa gazeti la The Citizen lililofungiwa kwa wiki moja.

Mwakyembe apingwa kwa kauli dhidi ya Gwanda

5

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Wahariri wakiwa kwenye mkutano mjini Tanga

Na Mwandishi wa Barazani

Kuanzia Aprili 10 hadi 13, 2019 wanachama hai wa Jukwaa la Wahariri Tanza-nia (TEF) walikutana Tanga

kwa mkutano wa ambao wenyewe wanauita fungate ambao safari hii ulikuwa kama darasa.

Wawakilishi kutoka taasisi mbalim-bali walizungumzia shughuli za taasisi zao faida yake kwa umma na umuhimu

kwa jumla. Wawakilishi hao walitoka kampuni

ya Shell, Benki ya TIB Corporate , Mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi, Mifuko ya Jamii ya NSSF na PSSF , Haki Elimu na Bodi ya Manunuzi na Ugavi.

Wengine walitoka Benki ya TPB na Mamlaka ya Kodi ya Tanzania (TRA).

Licha ya kupewa mwangaza kuhusu masuala ya mashirika mbalimbali waha-riri hao pia walikuwa na fursa ya kufaha-mishwa juu ya jambo muhimu kwao la Uendelevu wa kiuchumi wa Vyombo vya

Habari. Mshauri wa masuala ya habari, Alex Kanyambo alisisitiza kwanini ni muhimu kwa wahariri kuwa na mipango ya kuongeza ukusanyaji mapato katika vyombo vyao.

“ Lazima mfikiri nje ya boksi ”, Kan-yambo ambaye aliwahi kufanyakazi ka-tika Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) aliwaambia wahariri hao.

Badala ya kukaa maofisini wakisubiri matangazo kama waIivyozoea, wahariri lazima wapange mipango na mawazo kushawishi watoa habari kuweza kukub-ali kutoa matangazo.

Alisema ni muhimu kubuni njia za ku-vutia watangazaji, watazamaji, wasomaji na wasikilizaji katika hali ya ushindani mgumu.

Zaidi ya hapo alishawishi vyombo vya habari kuanzisha miradi mingine isiyo ya kihabari ili kusaidia kukuza bi-ashara ya vyombo vyao vya habari.

Katika mkutano huo wahariri waliamua pia kuimarisha TEF Jamii ambao ni utaratibu wa kuchangia na ku-saidia pale wanachama watakapopata changamoto za kifamilia kama vile ku-fiwa. Wahariri waliambiwa katika mku-tano huo kuwa ripoti za utendaji za Jukwaa zitatolewa katika mkutano mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Wahariri wapewa mwanga kuhusu shughuli za taasisi mbalimbali

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na

Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) yamepongezwa Bungeni kwa

kushinda kesi dhidi ya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambayo inalau-miwa kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza na haki za binad-amu.

Pongezi hizo zimetolewa na Joseph Mbilinyi, Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini.

Aliliambia Bunge, katika kikao kilichoongozwa na Naibu Spika Tulia Ackson, kwamba hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki kwamba vipengele kadhaa vya sheria ya MSA 2016 vinakiuka makubaliano ya ushirikiano wa Afrika Mashariki, imelifedhehesha Bunge.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyotolewa Machi 28, 2019 ilisema vifungu 16 vya MSA vinakiuka vipengele 6(d) na 7(2) vya Makubaliano ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mahakama pia imeamuru serikali ya Tanzania kuchukua hatua stahiki ili sheria hiyo ya Huduma ya Vyombo vya Habari iendane na Makubaliano ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kipengele 6(d) cha Makubaliano ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kinaelezea kanuni za msingi za kusimamia mafanikio na malengo ya Jumuia kwa mataifa wanachama ambazo ni pamoja na : (d) Utawala Bora unajumuisha kuzingatia kanuni

7

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Mbunge apongeza MCT, LHRC, THRDC kwa ushindi wa kesi ya MSA 2016

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akizungumza Bungeni.

Endelea Ukurasa wa 8

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga na Mratibu wa Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo ole Ngurumwa ambao walifungua kesi dhidi ya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016.

za demokrasia, uwazi, haki ya kijamii, fursa sawa, usawa wa kijinsia pamoja na kutambua na kukuza haki za watu kulingana na Mkataba wa Afrika kuhusu haki za Binadamu.

Kwa upande wake kipengele cha 7(2) kinaeleza kuwa Nchi wanachama zitazingatia kanuni za utawala bora, ikiwa pamoja na kufuata kanuni za demokrasia, utawala wa sheria, haki za jamii na viwango vinavyokubalika vya haki za binadamu.

Vifungu vinavyokiuka Mkataba wa Afrika Mashairiki ni 7(3)(a), (b), (c), (f), (g), (h), (i) na (j).

Vifungu viningine ni 19, 20 21, 35, 36, 37, 38, 39 , 40, 50 54, 52, 53, 58 na 59.

Katika mchango wake Bungeni, Mbilinyi ambaye pia anafahamika kwa jina lake la kimuziki wa Bongo Flava kama Sugu alisema, “ Sisi wabunge tunakaa hapa tunatunga sheria mbaya inatufanya kuonekana vibaya”.Mbilinyi, ambaye alisimamishwa mara mbili wakati akichangia kutoa nafasi kwa wabunge kutoa taarifa za kumkosoa, awali alisema hata kukatisha uchangiaji wa wabunge ni sehemu ya ubinyaji wa haki ya kujieleza.

Mbunge huyo pia alipuuza madai ya kuwepo magazeti mengi nchini kudhihirisha uhuru wa habari na wa kujieleza, akieleza kuwa kinachojalisha ni ubora na siyo wingi.

Haijalishi , alisema, kuwa na

idadi kubwa ya magazeti ambayo yanaweza kufutwa mara moja na Waziri au Mkurugenzi wa Idara ya habari.

Mbilinyi alikumbusha kwamba shambulio la kwamza kwa uhuru wa kujieleza na habari lilikuwa uamuzi wa serikali kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwenye runinga.

Ingawa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwenye runinga yalisimamishwa lakini sasa yanatumiwa na “Mkuu”, huku wabunge wengine wakisema anatangazwa moja kwa moja asubuhi, mchana na usiku. Mbilinyi pia alihoji uamuzi wa serikali wa kujitoa katika Umoja wa Uwazi wa Serikali (OGP), chombo cha kimataifa kinachohamasisha uwazi na utawala bora.

“Kama serikali inadai kuwa ina uwazi kwa nini ilijitoa OGP?”, Mbunge huyo wa Chadema, anayejulikana kwa misimamo yake, aliuliza.

Katika mchango wake , Mbilinyi alikumbishia jina la Rais mstaafu Kikwete kwa kusema kuwa alitufikisha mbali katika maendeleo na sasa tunarudi nyuma.

Mbunge apongeza MCT, LHRC, THRDC kwa ushindi wa kesi ya MSA 2016 Inatoka Ukurasa wa 7

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Umuhimu wa kuwa na taifa linalozungumza umesisitizwa katika mkutano wa siku moja uliojumuisha wahariri, wana-

harakati na wanasheria.Akizungumza katika mkutano

huo uliofanyika Machi 30, 2019 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, alisisitiza kwa nini taifa linalozungumza ni muhimu kwa kuwa taifa lisilozungumza ni taifa mfu.

Madhumuni ya mkutano huo, ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania, ni kukomesha ukiukaji wa uhuru wa habari na kukuza uhuru wa kujieleza. Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki 40.

Mukajanga, akizungumza wakati wa uchangiaji katika mkutano huo alisema uandishi mbaya hauwezi kurekebishwa na sheria mbaya.

Alisema uandishi mbaya si sahihi na haki na kwamba sheria nzuri lazima ziwepo lakini zisiwe sheria za kukandamiza uandishi na kuukebehi au kuudhalilisha.

Alieleza kusikitishwa na wenye mamlaka kuchukua hatua za kusimamisha magazeti na hata kuwaonya wahariri wa magazeti makubwa lakini hawachukui hatua dhidi ya magazeti uchwara kama vile Tanzanite au Jamvi la Habari ambayo hayazingatii taaluma katika uandishi wake.

Pia alizungumzia hukumu ya

Mahakama ya Afrika Mashariki kuitaka serikali kuifanyia marekebisho sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 ili ikidhi matakwa ya Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki na kueleza matumaini kwamba hukumu hiyo italeta mabadiliko chanya.

“Hakuna namna wenye mamlaka wanaweza kupuuza hukumu ya mahakama hii ambayo iko juu ya mahakama za kitaifa”, alisema.

Kuwezesha umma kuwa makini na kutambua umuhumi wa kukomesha ukiukaji wa uhuru wa habari na kukuza uhuru wa kujieleza kwa njia ya kuhamasisha mshikamano miongoni mwa wahusika mbalimbali ni miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano huo.

Mshauri wa masuala ya habari, Pili Mtambalike na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena

waliongoza mjadala wa Wajibu wa Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari katika kukomesha ukiukaji wa uhuru wa habari na wa kujieleza, wakati mjadala wa Wajibu wa Wanasheria uliongozwa na wakili Geline Fuko.

Kucheleli Machumbana kutokaTanlap aliongoza majadiliano kuhusu vyama vya kiraia.

Wakili Humphrey Mtuy kutoka MCT na Jones Sendodo kutoka Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) waliwasilisha hali ya ukiukaji wa uhuru wa habari na nini kimefanyika.

Sendodo aliueleza mkutano huo matukio mbalimbali ambapo wanahabari walinyanyaswa na kukamatwa na hatua zilizochukuliwa na taasisi kama MCT na THRDC, ikiwa ni pamoja na kuwapatia mawakili wale walioshitakiwa mahakamani.

9

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Tunahitaji taifa linalozungumza – Mukajanga

Baadhi ya wahariri, wanasheria na wanaharakati waliohudhuria mkutano uliotishwa na Baraza la Habari Tanzania kuhusu kukomesha ukiukaji wa uhuru wa habari na kukuza uhuru wa kujieleza.

Habari

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa waandishi wa habari na wahariri kukisoma ili kuelewa takwimu na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi katika habari

10

Kitabu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Tanzania imezidi kuporomoka katika orodha ya viwango vya uhuru wa habari duniani, kwa mujibu wa taarifa ya Waandishi

wasio na Mipaka.Kwa mwaka 2019 Tanzania

imeporomoka nafasi 25 hadi kuwa nchi ya 118 katika viwango vya uhuru wa habari.

Katika Afrika Mashariki Kenya ni ya 100 wakati Uganda ni ya 125.

Tanzania imekuwa ikiporomoka

katika orodha ya viwango vya uhuru wa habari tangu 2016, miezi michache tangu kuingia madarakani utawala wa saa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba , 2015.

Namibia ni ya 23, ambapo Ghana ni ya 27 zikiwa nchi pekee za Afrika zilizo katika viwango vya juu vya uhuru wa habari. Norway inaongoza ikiwa namba moja ikifuatiwa na Finland na Sweden.

Chini kabisa katika namba 180 ni Turkmenistan, ikifautiwa na Korea Kaskazini 179 na Eritrea ikiwa ya 178.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa

vitabu vitatu vya Baraza la Habari (MCT), Katibu Mtendaji, Kajubi Mukajanga alisema “ lazima tujali jinsi wenzetu wanavyotuona”.

Alisema “ tusijifanye kuwa hatujali wenzetu wanavyotuona”.

Kwa miaka mitatu iliyopita, tulianguka nafasi 10 kwa maana ya kupitwa na nchi 10 na tukaanguka nafasi 12, alisema.

Orodha kamili ya nchi na alama zao katika Viwango vya Uhuru wa Habari ni

11

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Endelea Ukurasa wa 13

Tanzania yaporomoka katika orodha ya uhuru wa habari

Mwandishi Silas Mbise wa Wapo FM akipigwa na polisi

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

Na Mwandishi wa Barazani

Vituo viwili vya redio – Radio Free Africa na Magic FM vimeonywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

(TCRA) kwa kukiuka agizo la Waziri kuhusu kusoma taarifa kwenye mag-azeti.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Dk. Harrison Mwakyembe Mei 3, 2018 alitoa agizo kuzuia vituo vya redio kusoma maudhui ya habari kwenye magazeti katika vipindi vyao vya kupitia magazeti.

Waziri, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani alisema redio ziko huru kusoma vichwa vya habari tu vya magazeti.

Hatua hiyo ya TCRA kwa vituo hivyo viwili ilitangazwa Aprili 15, 2019 na kuripotiwa kwenye magazeti siku iliyofuata. Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka, amesema vituo hivyo viwili vimekiuka agizo la serikali katika nyakati tofauti.

Wakuu wa vyombo hivyo walipoitwa TCRA walikiri kutenda kosa.

Radio Magic FM ilidai kuwa kosa hilo lilifanyika kabla ya kubadilika kwa mmiliki wa kituo hicho ambacho sasa kinamilikiwa na CCM.

Kufuatia matatizo ya uendeshaji na upungufu wa wafanyakazi, wakati mwngine watangazaji wasio na uzoefu na wasiofahamu kanuni na taratibu hutumiwa kuendesha vipindi. Kituo hicho kimeahidi kutorudia kosa hilo.

Msoka ameripotiwa akisema kuwa tabia ya kukiuka maagizo ya serikali inajirudia rudia na akatupilia mbali maelezo ya kubadilika kwa umiliki wa kituo kuwa sababu ya msingi.

Kamati ya Maudhui, kulingaana na Msoka, imewashauri viongozi wa redio hizo mbili kuimarisha na kuboresha usimamizi wa vipindi vyao na wachukue hatua za makusudi kuhakikisha makosa hayo hayarudiwi. Kwa wafuatiliaji wa masuala ya vyombo vya habari, pamoja na kutopenda kusimamiwa kiserikali, tabia ya kusoma habari yote kama ilivyochapishwa kwenye gazeti, siyo nzuri.

Pamoja na dhamira ya kutaka kuwa na wasikilizaji kwa upande mwingine hatua hiyo inaathiri ununuzi wa magazeti.

Nani katika akili ya kawaida baada ya kusikiliza habari yote kwenye redio atakayenunua gazeti… kwa ajili gani, kulihifadhi?

Kutokana na ushindani mkali kuvutia wasomaji, ambao nao wamekwazwa kiuchumi kwa kuwa biashara nyingi zinachechemea na hata wafanyakazi hawajapata nyongeza za mishahara, biashara ya magazeti inapitia katika kipindi kigumu.

Suala la vituo vya redio na runinga kusoma habari za magazeti zote limezungumzwa sana hata kabla ya miaka ya awali ya 90 ya ulipoibuka utitiri wa vyombo vya habari.

Kwa kutangaza agizo hilo mwaka jana, ingawa lilichelewa, Waziri alichukua hatua stahiki kulinda mauzo na soko kwa magazeti.

Kutokana na matatizo ya ukata magazeti mengi yameshindwa kutimiza majukumu yake kiuchumi ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara wafanyakazi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Valery Msoka

Vituo viwili vya redio vyaonywa

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

13

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Habari

kama ifuatavyo::1 Norway 7.822 Finland 7.903 Sweden 8.314 Netherlands 8.635 Denmark 9.876 Switzerland 10.527 New Zealand 10.758 Jamaica 11.139 Belgium 12.0710 Costa Rica 12.2411 Estonia 12.2712 Portugal 12.6313 Germany14.6014 Iceland 14.7115 Ireland 1516 Austria 15.3317 Luxembourg 15.6618 Canada 15.6919 Uruguay 16.0620 Surinam 16.3821 Australia 16.5522 Samoa18.2523 Namibia 18.9524 Latvia19.5325 Cape Verde 19.8126 Liechtenstein 20.4927 Ghana 20.8128 Cyprus 21.7429 Spain 21.9930 Lithuania 22.0631 South Africa 22.1932 France 22.2133 United Kingdom 22.2334 Slovenia 22.3135 Slovakia 23.5836 Burkina Faso 24.5337 Andorra 24.6338 Papua New Guinea 24.7039 Trinidad and Tobago 24.7440 Czech Republic 24.8941 South Korea 24.9442 Taiwan 24.9843 Italy 24.9844 Botswana 25.0945 Tonga 25.4146 Chile 25.6547 Romania 25.6748 United States 25.6949 Senegal 25.8150 OECS 26.0451 Guyana 26.6352 Fiji 27.1853 Belize 27.5054 Madagascar 27.76

55 Dominican Republic 27.9056 Comoros 27.9157 Argentina 28.3058Mauritius28.4659 Poland 28.8960 Georgia 28.9861 Armenia 28.9862 Haïti 2963 Bosnia-Herzegovina 29.0264 Croatia 29.0365 Greece 29.0866 Niger 29.2667 Japan 29.3668 Malawi 29.3669 Seychelles 29.4170 Mongolia 29.5171 Côte d’Ivoire 29.5272 Tunisia 29.6173 Hong Kong 29.6574 Northern Cyprus 29.6775 Kosovo 29.6876 Togo29.6977 Malta 29.7478 Lesotho 29.7479 Panama 29.7880 Bhutan 29.8181 El Salvador 29.8182 Albania 29.8483 Kyrgyzstan 29.9284 Timor-Leste 29.9385 Peru 30.2286 Sierra Leone 30.3687 Hungary 30.4488 Israel 30.8089 Guinea Bissau 30.9590 Serbia 31.1891 Moldova 31.2192 Gambia 31.3593 Liberia 31.4994 Mauritania 31.6595 Republic of Macedonia 31.6696 Benin 31.7497 Ecuador 31.8898 Maldives 32.1699 Paraguay 32.40100 Kenya 32.44101 Lebanon 32.44102Ukraine32.46103Mozambique32.66104Montenegro32.74105Brazil32.79106Nepal33.40107Guinea33.49108Kuwait33.86109Angola34.96110Ethiopia35.11

111Bulgaria35.11112Mali35.23113Bolivia35.38114Nicaragua35.53115Gabon35.60116Guatemala35.94117Congo-Brazzaville36.04118Tanzania36.28119Zambia36.38120Nigeria36.50121Afghanistan36.55122Chad36.71123Malaysia36.74124Indonesia36.77125Uganda39.42126Sri Lanka39.61127Zimbabwe42.23128Qatar42.51129Colombia42.82130Jordan43.11131Cameroon43.32132Oman43.42133United Arab Emirates43.63134Philippines43.91135Morocco / Western Sahara43.98136Thailand44.10137Palestine44.68138Myanmar44.92139South Sudan45.65140India45.67141Algeria45.75142Pakistan45.83143Cambodia45.90144Mexico46.78145Central African Republic47.27146Honduras48.53147eSwatini49.09148Venezuela49.10149Russia50.31150Bangladesh50.74151Singapore51.41152Brunei51.48153Belarus51.66154Democratic Republic of Congo51.71155Rwanda52.43156Iraq52.60157Turkey52.81158Kazakhstan52.82159Burundi52.89160Uzbekistan53.52161Tajikistan54.02162Libya55.77163Egypt56.47164Somalia57.24165Equatorial Guinea58.35166Azerbaijan59.13167Bahrain61.31168Yemen61.66169Cuba63.81170Iran64.41171Laos64.49172Saudi Arabia65.88173Djibouti71.36174Syria71.78175Sudan72.45176Vietnam74.93177China78.92178Eritrea80.26179North Korea83.40180Turkmenistan85.44

Tanzania yaporomoka katika orodha ya uhuru wa habariInatoka Ukurasa wa 11

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Wanahabari wasiwe kisingizio kususiwa BungeNa Gervas Moshiro

Mzozo wa CAG waingiza

wanahabari

Siku ya pili baada ya Siku ya Wajinga Duniani (Aprili 1), Spika wa Bunge, Job Ndugai alikuwa kwenye habari kwa

kile kilichohofiwa kuwa kingeleta mgogogro wa kikatiba kwa kutangaza kuwa Bunge halitafanya kazi tena na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Bunge lilipitisha azimio hilo kutokana na matamshi ya CAG, wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Umoja wa Mataifa Januari mwaka huu, kuwa Bunge ni ‘dhaifu’ kutokana na kushindwa

kuidhibiti serikali kufuatia kasoro zinazoibuliwa na ripoti zake za ukaguzi.

Siku mbili baada ya tamko hilo la kumsusa CAG, baadhi ya wabunge walirudia kauli hiyo ya CAG na kutamka bungeni kuwa ‘Bunge ni dhaifu’. Spika alichefuka na mara moja akawatoa nje ya kikao.

Kana kwamba hiyo haitoshi, wabunge waliotimuliwa waliamriwa wasizungumze na vyombo vya habari, na wanahabari nao wasiwahoji wabunge hao la sivyo Spika atabatilisha vibali vyao vya kuandika habari za bunge.

Nimekuwa kwenye tasnia ya habari kwa zaidi ya miongo minne sasa. Tamko la Spika kutaka

kuwatia adabu na kudhibiti mienendo ya wanahabari katika maeneo na hata nje ya Bunge limenistua, hasa kwa vile limetolewa na mtu ambaye Jamii imemwamini na kumdhamini kuchukuwa madaraka na mamlaka ya kuendeleza na kutetea tunu za taifa ilivyo katika katiba ya nchi.

Makala haya yanachambua kitendo cha Spika kudhibiti taaluma ya wanahabari kwa visingizio nitakavyoeleza na pia tafakuri yangu kuhusu suala zima la habari katika huduma za bunge.

Kwa nini Ndugai anawachukia wanahabari

Spika Job Ndugai si mtu mgeni

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Inatoka Ukurasa wa 14

bungeni. Amekuwa mbunge toka mwaka 2000 na Naibu Spika wakati wa bunge la 2010 – 2015 kabla ya kuchaguliwa nafasi aliyo nayo sasa ya spika 2015. Kabla yake walikuwepo spika mashuhuri wengi tu (miaka waliohudumu katika mabano): Chief Adam Sapi (28), Erasto Mang’enya (2), Pius Msekwa (11), Samuel Sita (5) na Anna Makinda aliyekuwa na Ndugai kama Naibu wake (5). Ndugai ni msomi mzuri na mtendaji kazi wa kusifika. Katika ripoti moja iliyoandikwa kwenye gazeti la Daily News (Oktoba 19, 2010) Ndugai anatajwa kuwa ndiye aliyekuwa amilifu zaidi kuliko wote katika Bunge la 9. Ni Dhahiri, kwa hiyo, kuwa analosema na kutenda huchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu zaidi kuliko wengine kwa vile ni mheshimiwa kwa kila hali.

Kinachonishangaza hata hivyo ni mkabala wake wa sakata la CAG kwa kulihusisha na utendaji wa wanahabari. Aliagiza wabunge waliotimuliwa bungeni wasizungumze na waandishi wa habari, na wala waandishi wasiwahoji chochote. Agizo hilo, nionavyo mimi, halina uhalali wa kisheria wala utaratibu wowote rasmi isipokuwa ni matakwa binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 4 kutaka kufafanua agizo lile la Bunge la kutofanya kazi na CAG lililotolewa Aprili 2, 2019 Ndugai anadai kuwa waandishi walishindwa (au kukataa?) kutofautisha kati ya neno ‘Ofisi ya CAG’ na Prof. Mussa Assad, mwenyewe kama mtu binafsi, ambaye ndiye lile azimio lilimlenga, na sio kuacha kufanya kazi na ofisi ya CAG.

Tofauti anayotaka Ndugai tuione kati ya Prof. Assad kama mkuu wa ofisi na ofisi ya CAG bila kiongozi huyo, bado inatatiza wengi, wakiwemo wasomi na

wanataaluma, hasa inapokuwa ni taasisi ya umma. Uamuzi unapotolewa kutokana na matakwa binafsi bila kuzingatia misingi ya uendeshaji ofisi ya umma, basi ubinafsi unatawala na hilo halitakiwi.

Kuhusu kukataza wanahabari wasizungumze na wabunge wanaotolewa bungeni, Ndugai anadai kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akishuhudia kila anapowatoa wabunge nje kunatokea rabsha fulani inayosimamisha shughuli za bunge kwa muda wakati wanahabari nao wakitoka kuwafuata wabunge hao ili kuwahoji. Hali hii inaweka kituo kingine cha majadiliano nje ya utaratibu rasmi wenye kumbukumbu za Bunge, na ambayo huwafikia wananchi kupitia vyombo vya habari, japo hayakurekodiwa rasmi.

Chukizo jingine analoona Ndugai ni kwamba wananchi wanaamini sana taarifa za vyombo vya habari kuliko taarifa zilizo kwenye kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard). Hili, kwa mujibu wa Ndugai, hupendelewa sana na baadhi ya wabunge ambao hupenda kusema kwenye vyombo vya habari kuliko kuzungumza mbele ya wabunge wengine. Inaanza kuwa tabia ya baadhi ya wabunge kuchochea vurugu na uasi ili kuvuta na kutaka huruma ya wanahabari. Ndugai anasema tabia hii haina budi kukemewa na kukomeshwa kabisa.

Kwa upande mwingine, wabunge waelewe kuwa kwa kukumbatia vyombo vya habari, ni sawa na kukubali kuwa wao ni dhaifu katika kutoa hoja wakiwa wamekabiliwa na upande mwingine wa upinzani. Inahitaji uvumilivu na kuheshimu maoni ya wengine, kitu ambacho, Ndugai anadai kuwa hawana. Kadhalika Ndugai anadai kuwa baadhi ya wabunge wana matatizo ya kisaikolojia na ndio maana wanasababisha vurumai

bungeni, kuzomea na kutoka nje wakati wa vikao, vitu ambavyo wanahabari hupenda kuandika, na kwa kufanya hivyo kukuza tabia na umaarufu hasi wa wabunge.

Kwa mujibu wa Ndugai, tabia hizi mbaya ni matokeo ya kuweko wanahabari Bungeni, na ili kuikomesha, wabunge wasizungumze na wanahabari na wanahabari wasiwahoji wabunge!

Makatazo mwarobaini wa kusu-sia Bunge

Maoni ya Spika niliyoandika hapo juu yanatokana na mkutano aliofanya na waandishi wa habari Aprili 4, 2019 kufafanua azimio la bunge kumsusia CAG, baada ya baadhi ya wabunge wa upinzani kurudia kauli ile ile ya CAG bungeni kuwa ‘Bunge ni dhaifu’, kitu kilichomchafua zaidi Ndugai na kuamua kuwatoa nje ya kikao na kuagiza wasikutane na waandishi wa habari na waandishi wa habari wasiwahoji kwa minaajili ya kupata taarifa, la sivyo nao watanyang’anywa vibali vya kukusanya habari eneo la Bunge.

Haya ni majanga mara mbili. Yawezekana hayana msingi kisheria, lakini kutokana na hali tete nchini wanayofanyia kazi wanahabari ya kutakiwa kuunga mkono utendaji wa serikali tu na kuacha dhima yake kuu iliyopewa na jamii ya kuwa kioo cha jamii, basi kwa vyovyote wanahabari watatii amri hiyo. Licha ya utatanishi wa amri hiyo, vibaya zaidi ni kwamba hakuna chombo cha kisheria – kitaaluma au ndani ya mfumo wa sheria, kitakachojitokeza kuhoji uhalali kikatiba wa amri ya Spika Ndugai.

Wanahabari walionja machungu ya utawala wa Ndugai mara tu alipochaguliwa kuwa Spika wakati alipokubali matakwa ya mhimili wa utawala yaliyokataza vyombo vya habari visioneshe mbashara majadiliano ya wawakilishi wa wananchi bungeni, hasa mijadala ile inayohusisha kuhoji vitendo vya serikali. Kwa hiyo amri hii mpya ni mwendelezo tu wa machungu hayo yanayozidi kuminya uhuru wa habari nchini.

Wanahabari ni wataalamVyombo vya habari ni taasisi za

jamii zinazotoa huduma kwa umma kulingana na mfumo mkuu wa mgawano wa majukumu ambapo imegawanywa kwenye sekta mbalimbali kama afya, elimu, maji,

15

Maoni

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Inatoka Ukurasa wa 14

Wanahabari wasiwe kisingizio kususiwa Bunge

Endelea Ukurasa wa 16

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Maoni

habari, nyumba na nyingine. Huduma zake ni muhimu kwa uhai wa jamii na ndiyo maana huduma hizo zimetajwa kwenye katiba ya nchi kama haki ya msingi.

Habari imetajwa kwenye kifungu cha 18 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na japo taasisi hizo hazikutajwa mahususi kwenye katiba, kutambuliwa kwake ni dhahiri, kwani serikali na Bunge hutunga sheria mbalimbali kuwezesha utekelezaji wa taasisi hizo katika kutoa huduma zilizotajwa kwenye katiba ya nchi.

Huduma zote za jamii, habari ikiwemo, hutolewa na taasisi zilizoundwa maalum kwa madhumuni hayo na hutambuliwa kisheria. Taasisi hizo zina watoa huduma ambao ni wataalam kwenye fani husika. Wataalam hao, licha ya miaka mingi ya elimu kinadharia na vitendo, pia hufunzwa maadili ya taaluma na ya jamii ili yawaongoze katika utendaji wao. Kati ya maadili hayo, na ambayo yanaheshimiwa na kuzingatiwa sana, ni yale yanayotawala ukusanyaji wa habari za Bunge kwani chombo hicho ni cha heshima kubwa.

Kilab jumuiya ya wanahabari duniani kote ina masharti na maelekezo ya namna ya kutekeleza wajibu wake au maadili na kutokana na umuhimu wa maelekezo hayo, Serikali za nchi nyingi hutoa maelekezo hayo na mahali pengine hutolewa na tasnia ya wanabari wenyewe. Tanzania tuna yote mawili.

Tofauti kati ya mtu mweledi wa taaluma na mwingine asiye, hutokana pamoja na mengine na uzingatiaji wa maadili. Waandishi wa habari walio na ithibati, kwa maana ya walioruhusiwa rasmi kufanya kazi hiyo na kupewa kibali na serikali, kama hao Ndugai anaotaka kufuta vibali vyao, ni

weledi sana na wanafahamu vizuri taratibu zote za kuandika habari za Bunge. Hawahitaji kabisa makaripio kutoka kwa wasio wataalam na hasa wanasiasa.

Mwalimu Julius Nyerere, baba wa taifa, aliwahi kusema kuwa « siasa sio kazi ». Inafaa Ndugai akatambua kuwa hawezi kuelekeza wanahabari namna ya kutenda kazi zao. Wakiona mbunge ametoka au kutolewa nje ya Bunge kwa namna isiyo kawaida, kwao ni tukio la kihabari na watamfuata popote atakapokuwa hadi wamepata cha kusimulia kwani linahusu mamia ya wananchi waliomchagua mwakilishi huyo.

Spika Ndugai amekataza wanahabari wasiwe wanawafuata wabunge wanaotoka nje ya bunge kupinga mwenendo fulani. Hili ni mwendelezo wa kuminya habari zisitoke bungeni, mtindo ulioanza kwa kunyima matangazo mbashara ya majadiliano ya wabunge mwanzoni mwa utawala wa Ndugai baada ya uchaguzi wa 2015. Ni katika majadiliano hayo wabunge huhoji na kuishauri serikali katika mambo mbalimbali kwa lengo la kuidhibiti ilivyo matakwa ya katiba.

Wakati mwingine majadiliano huwa moto sana na wajumbe wanapoona kuwa hawatendewi haki na Spika au kuonewa kiubaguzi, ndipo inapokuwa hawana budi bali kutoka nje ya Bunge kama ishara ya kupinga uonevu huo. Kwa mujibu wa maelezo ya Ndugai, wabunge hutoka nje kwa sababu ya kukosa uvumilivu wa kuwasikiliza wengine.

Kuna wakati mwingine Ndugai anahisi kuwa baadhi ya wabunge wako chini ya viwango vya kustahili kuwa mbunge na anatoa mfano wa kanuni zinazotawala taratibu bungeni. Ndugai anasema kuwa hawakuona haja ya kuzipa maelezo ya kina kwa kuwa walidhani mambo mengine

yanaeleweka na mtu yeyote mwenye wadhifa wa kuwa mbunge kwani ni mstaarabu katika kiwango fulani, ila anasikitika kuwa hawako hivyo walivyotarajiwa.

Kusema kuwa wabunge wanasaidiwa na wanahabari kwa kuwa uandishi wa habari unapenda matukio ya vurugu au kudai kuwa kama waandishi wa habari wataacha kuwafuata wabunge hawatatoka tena nje, nadhani ni kutotafakari pa kutosha. Kwa sababu zozote zinazoleta vurugu bungeni, Ndugai awe na mkabala wa kisayansi zaidi na kutafuta kiini cha baadhi ya wabunge kutowavumilia au kuheshimu mawazo ya wenzao na vile vile ni kwa nini hawataki kutii kanuni za bunge.

Hata hivyo hii haiwasamehe wanahabari baadhi ya makosa tunayoona kwenye uandishi wa habari za bunge. Bunge ni mahali patakatifu. Ni mali ya wananchi na linawajibika kwa wananchi na ndio sababu limepewa kulinda na kuendeleza tunu za taifa hili kama zilivyoainishwa katika katiba. Mafunzo ya taaluma ya habari yanapaswa kutilia mkazo eneo hili kuhakikisha kuwa mfumo, muundo na utekelezaji wa bunge unaeleweka vema kwa wanahabari. Hali kadhalika, wanahabari wanatakiwa wajisomeshe vizuri kuhusu muundo, utekelezaji na kanuni zinazotawala mihimili mingine ya dola : utawala na sheria. Ili kuweza kuwa jicho la jamii ipasavyo, wanahabari wanapaswa kudhihirisha kuwa wanaelewa vizuri utendaji wa mfumo mzima wa serikali.

Wabunge ni chanzo muhimu cha habari

Agizo la Spika Ndugai kuwa wanahabari wasiwafuate wabunge, pia halina mashiko. Maadili ya uandishi wa habari yanamwelekeza mwandishi asiwahoji watu waliolazimishwa jambo kwa sababu ukweli hautasemwa, watoto kwa sababu uwezo wao wa kuelewa ni mdogo na walio kwenye msongo kwani wamechanganyikiwa. Tahadhari hizi zinachukuliwa kulinda uadilifu wa ukweli wa taarifa na utu wa mtu. Wabunge wanaofukuzwa bungeni wapo kwenye kundi lipi kati ya haya ili wasifuatwe? Kamwe wanahabari hawataacha kutafuta stori kwa kuwa Spika anataka hivyo. Kumradhi. Hawakufundishwa hivyo.

Wanahabari wasiwe kisingizio kususiwa BungeInatoka Ukurasa wa 15

17

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

Washington, DC:

Baada ya kutumia mkutano wake wa kwanza mwaka huu uliofanyika Februari 7, ku-panga jinsi ya kujiimarisha,

wanachama wa Umoja wa Haki ya Ku-pata Habari (CoRI) walikuwa na kikao kigumu zaidi walipokutana kwa mku-tano wa pili mwaka huu uliofanyika Aprili 25, 2019.

Mkutano huo, uliofanyika chini ya Mwenyekiti wa Umoja huo, Kajubi Mukajanga, ulikabiliwa na masuala mazito na nyeti ambayo yanatishia kuathiri shughuli za baadhi ya taasisi wanachama CoRI.

Sheria ya Takwimu iliyofanyiwa marekebisho ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa kwa kirefu katika mkutano huo huku baadhi ya washiriki wakieleza wasiwasi

kwamba inatishia kuathiri shughuli za baadhi ya mashirika ambayo kazi zake ni za utafiti na takwimu.

Kulingana na sheria hiyo ya takwimu iliyofanyiwa marekebisho, matokeo ya tafiti lazima yapitishwe na taasisi za kiserikali kama vile Shirika la Taifa la Takwimu kabla hazijatangazwa.

Wanachama wa CoRI walikubaliana kuwa lazima waendeleze mazungumzo kuhusisha vyombo hivyo mbalimbali ili matokeo ya tafiti yaweze kutangazwa.

Masuala mengine yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa pili wa CoRI ni kufanya mazungumzo na serikali kuhusu kufanyia marekebisho Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 kufuatia hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki kuwa baadhi ya vipengele vya sheria hiyo vinakiuka mkataba wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwa sheria hiyo

inabinya uhuru wa kujieleza na haki za binadamu pia. Mkutano huo ulielezwa pia kuhusu ziara ya ujumbe wa taasisi ya habari ya Kimataifa (IPI) ambao ulikutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisson Mwakyembe na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr.Hassan Abbas.

Mkutano huo wa CoRI ambao ulikuwa na mahudhurio mazuri, pia ulijadili ushiriki wa umoja huo katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yatakayoadhimishwa Dodoma Mei 3, 2019.

Suala la kutoweka mwandishi Azory Gwanda pia lilijadiliwa na wanachama waliangalia njia mbalimbali za kufuatilia suala hilo.

Mkutano huo wa pili wa CORI kwa mwaka huu ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Jamii Forum, Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Umoja wa Watetezi wa haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Twaweza, Sikika na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Katika mkutano wake wa kwanza uliofanyika Februari 7, 2019 umoja huo ulikubaliana kuimarisha shughuli zake ikiwamo kuongeza idadi ya wanachama na kukuza ushiriki wa umma.

CoRI yajadili changamoto na masuala ya kitaifa

Baadhi ya washirika wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) wakiwa katika kikao cha umoja huo.

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

Na Saidi Nguba.

Baraza la Habari Tanzania likiwa pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na wanaharakati wengine wa haki za binadamu, limeonyesha njia. Ni

baada ya Mahakama ya Afrika Mashariki kuamua Machi 28 mwaka huu kuwa Sheria ya Vyombo vya Habari nchini iliyokuwa inapigiwa kelele ina vipengele vinavyobana na kwa kweli inakwenda kinyume na baadhi ya vifungu vya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuitaka Serikali ya Tanzania iifanyie marekebisho.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya miaka mi-wili ya mapambano ya kisheria katika Ma-hakama hiyo kutokana na taasisi hizo zisizo za kiserikali kulalamikia changamoto za Sheria ya Vyombo vya Habari iliyopitishwa nchini mwaka 2016. Sasa, baada ya hukumu hiyo, baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeamua kuifuata Ma-hakama hiyo iangalie sheria nyingine inay-opigiwa kelele – Sheria ya Vyama vya Siasa, ambayo baadhi ya wanaharakati wanadai inaw-abana watu na siyo ya haki.

Nani alisema kuwa kwenda kwenye Ma-hakama hiyo siyo jambo zuri. Hapana, la hasha. Waziri wa Habari, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza katika Bunge kuhusiana na hu-kumu

hiyo ya Mahakama ya Afrika Mashariki alisema “wananchi wana uhuru kwenda popote pale kutafuta na kudai haki…tulilipigania sana jambo hili tulipokuwa tunatengeneza mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Jambo lote hili lilianza baada ya Bunge kuu-pitisha Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari nchini na Rais kuukubali kuwa Sheria, Novemba 16, mwaka 2016. Baadhi ya wana-habari, wanaharakati wa haki za binadamu na wadau wengine, waliiona sheria hiyo haikukaa vizuri. Sheria hiyo ina vipengele vilivyotarajiwa kuendeleza taaluma ya habari, imeanzisha Bodi ya Usajili wa wanahabari, imeanzisha Baraza Huru la Habari na imeweka mfumo wa kuisi-mamia tasnia ya habari na masuala mengine yanayohusiana na huduma hiyo. Wanahabari na wadau wengine walishirikishwa katika hatua za awali za utungaji wa sheria hiyo kabla ya mus-wada kufikishwa bungeni. Lakini kilichotokea baadaye na jinsi sheria hiyo ilivyokuwa inatu-mika kuvidhibiti vyombo vya habari, ndicho kili-choleta ukinzani huu.

Sheria ya Vyombo vya Habari, miongoni mwa madhumini yake, pia ni kuondokana na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo ili-kuwa inavuma kwa ubaya. Lakini baadhi ya vi-fungu vya sheria hiyo ya zamani, kwa mfano, vinavyompa Waziri wa Habari na wakala wen-gine wa serikali, madaraka ya kuamua yaliyo makubwa kupita kiasi, bado vinaonekana vipo na kuwa na nguvu kupindukia. Vifungu vingine vinavyoleta ubishi katika Sheria ya Vyombo vya Habari vinahusu shuruti ya kuwasajili waandishi wa habari, kuyafanya makosa ya kashfa na uchochezi kuwa ni makosa ya jinai na kudhibiti utoaji wa habari, maelezo na taarifa.

Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), walifikisha shauri lao katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki, baada ya kuona kuwa baadhi ya vifungu vya Sheria ya Vyombo vya Habari ya Tanzania, vinakwenda kinyume na vifungu vya Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, vinavyohusiana na utawala bora, uhuru wa kutoa maoni na haki za binadamu. Waliiambia Mahakama kuwa Sheria ya Vyombo vya Habari, katika hali yake ilivyo sasa, "ni uban-aji usiokuwa wa haki wa uhuru wa kutoa mawazo ambao ni msingi wa kanuni za de-mokrasia, utawala wa sheria na uwajibikaji, uwazi na utawala bora” ambao Tanzania imeapa kuzingatia, kupitia Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mikataba min-gine ya kimataifa.

Katika hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki, iliyoketi Arusha, Majaji waliamuru: ”Baada ya kupitia masuala yaliyokuwepo mbele yetu kwa uamuzi, tumebaini kuwa ni dhahiri baadhi ya vifungu vilivyoonyeshwa hapa vya Sheria ya Vyombo vya Habari inayolalamikiwa, viko kinyume na kanuni zilizomo kwenye vi-fungu 6(d) na 7 (2) vya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki”. Vifungu hivyo vinavyokwenda kinyume ni 7(3) (a), (b), (c), (f), (g), (h), (i) na (j); ibara za 35,36, 38 na 40; ibara za 50 na 54; ibara 52 na 53 na 58 ba 59 za Sheria ya Vyombo vya Habari.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, Ma-hakama imeagiza, “inaamriwa kuchukua hatua kadri inavyowezekana, kuifanya Sheria ya Vyombo vya Habari ya Tanzania ikubaliane na Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Wakati vumbi lililotimka baada ya hukumu

hiyo linatuwama na hakuna anayejua wazi wazi na kwa uhakika hatua zitakazochukuliwa kwa maelekezo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, bado kuna sheria nyingine zinazozua ubishi. Moja ya sheria hizo ni ya Vyama vya Siasa na nyingine ni zile zinazohusu matumizi mabaya ya mtandao na ya takwimu.

Wakati dunia nzima inajielekeza katika utawala bora na kuzingatia haki za binadamu sisi nchini Tanzania lazima tusonge mbele kwa kasi kuelekea mwelekeo huo kwa kuwa na sheria nzuri na siyo za kuwabana watu.

Itabidi tujikumbushe Tume ya Nyalali. Mwaka 1991, Rais Mwinyi, aliteua Tume ya Rais kuhusu kuchambua na kutoa mapendekezo kwa nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi au kuendelea na mfumo wa chama kimoja. Tume hiyo iliyoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Fran-cis Nyalali ikiwa na watu wengi mashuhuri, baada ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ilijielekeza kutoa marekebisho yaliyokuwa yakihitajika ka-tika sheria “kutokana na ukweli kwamba baadhi ya sheria hizo ama ziliwanyang’anya wananchi uhuru wao na haki zao za msingi au wakati mwingine kuathiri uhuru wa haki za watu”. Sheria 40 zilibainika kuwa ni “kandamizi” na zilizoonekana kwenda kinyume cha katiba na baadhi yake zimepitwa na wakati.

Ingawa sina orodha kamili ya hizo sheria “mbaya” ikionyesha zile ama zilizofutwa au zilizofanyiwa marekebisho, inaonekana kama vile baadhi ya sheria hizo zinarejea kimya kimya katika sura nyingine kwa kupitia marekebisho fulani fulani au kuja mpya kabisa. Inabidi tufanye mapitio ya mapendekezo ya Nyalali na hizo sheria 40 mbaya.

Hata hivyo, sheria zifuatazo zilizotajwa na Tume ya Nyalali, kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi, zimefanyiwa marekebisho au zimefutwa: Sheria ya kuwafukuza watu wasiotakiwa nchini (Cap. 38); Sheria ya Kuendesha Mashitaka ya Serikali, Na. 16 ya mwaka 1967; Sheria ya Shirika la Habari la Tanzania, Na. 14 ya mwaka 1976; Sheria ya Magazeti, Na. 3 ya mwaka 1976; Sheria ya Adhabu (Cap. 337); Sheria ya Kutaifi-sha Majengo, ya mwaka 1971; Sheria ya Uan-dikishaji wa Vyama (Cap. 337); Sheria ya Usalama wa Taifa, Na. 3/70 na Sheria ya Kuwa-fukuza Watu wasiohitajika (Cap. 39).

Inafahamika kuwa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini, nayo imekuwa na kazi ya kupitia sheria mbalimbali na kupendekeza marekebi-sho. Zoezi hili lazima liendelee kwa sababu siku zote tumekuwa tukipigania utawala bora na utawala wa sheria.

• Mwandishi ni Mwanahabari mkongwe nchini Tanzania. Anapatikana kupitia

Simu: 0754-388418 na Barua-Pepe: [email protected]

Tuipitie upya orodha ya Jaji Nyalali ya Sheria 40 mbovu

BAADA YA MAHAKAMA KUU YA AFRIKA MASHARIKI KUIKOSOA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI NCHINI…

wanahabari mkoani humo. Mwanahabari wa Songea, , Geofrey

Nilahi aliandikia MCT akidai kuwa waandishi walitumika kukanusha habari aliyoandika kuhusu changamoto za maendeleo katika jimbo la Peramiho.

Pia alidai kuwa wanahabari walim-tuhumu kutunga habari yake.

Baraza, kwa kuwezeshwa na katiba yake, huchunguza masuala muhimu ya

jamii na kuchapisha ripoti yake. Lilit-euwa wanahabari watatu kuchunguza suala hilo.

Katika uchunguzi wao walibaini ku-wepo jitihada za kukanusha alichoripoti Nilahi, lakini pia ilibainika ripoti ya mwandishi huyo ilikuwa ya upande mmoja.

Akizungumza katika uzinduzi huo alilipongeza Baraza kwa kuchapisha vi-tabu hivyo na pia alisema kuwa sha-

baha kubwa ya kutetea wanahabari ni kuhakikisha kuwa wananchi wanahabar-ishwa.

Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari iliandikwa na Dk. Joyce Bazira, Ally Uki na Henry Muhanika, wakati Kitabu cha Makosa ya Kawaida kimeandikwa na Pu-denciana Temba na Attilio Tegalile na kitabu cha Ruvuma kimeandikwa na Hamis Mzee, Lucas Liganga na Florence Majani.

Vitabu hivyo vitabu vilipitiwa na Pili Mtambilike, Absalom Kibanda na Attilio Tegalile.

Mapema Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema Baraza limepania kuchapisha Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari kila mwaka.

Nakala za vitabu hivyo ziligawiwa kwa walioshiriki katika hafla ya uzin-duzi. Pamoja na vitabu hivyo vitatu, Ri-poti ya Ukiukaji wa Uhuru wa habari kwa kipindi cha Oktoba 2017 hadi 2018, pia ilisambazwa..

Inatoka Ukurasa wa 20

Habari

Toleo la 140 , Aprili, 2019

19

Baraza la Habari lazindua vitabu

Baadhi ya waliohudhuria uzinduzi wa machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakichukua nakala ya vitabu vili-vyozinduliwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Juxon Mlay, akionyesha moja ya vitabu vitatu vya Baraza katika sherehe ya uzinduzi wake. Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga (kushoto) na waandishi wawili wa vitabu hivyo, Hamis Mzee (wa pili kushoto) na Attilio Tegalile (kulia).

20

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Vitabu vitatu – Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari kwa miaka 2017/2018, Makosa ya Kawaida Katika Vyombo

vya Habari na Ripoti ya Ukwazaji wa Uandishi wa Habari Mkoani Ru-vuma – vimezinduliwa.

Vitabu hivyo vilizinduliwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kisenga Jijini Dar es Salaam Aprili 24 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya

Baraza la Habari Tanzania (MCT), jaji mstaafu Juxon Mlay.

Ripoti ya Hali ya Habari ni kitabu muhimu kinachochapishwa na Baraza kwa miaka 11 sasa.

Kinaelezea maendeleo ya vyombo vya habari, mafanikio na matatizo, mafunzo, masuala ya maadili na kinapendekeza maboresho na maendeleo ya jumla ya vyombo vya habari.

Kitabu cha Makosa ya Kawaida amba-cho kinahusu ufuatiliaji wa vyombo vya habari unaofanywa na Baraza, kinalenga kuonyesha makosa katika vyombo vya habari kwa lengo la kurekebisha na ku-ondoa.

Kitabu kuhusu Ruvuma ni matokeo ya uchunguzi wa kiuandishi kuhusu migongano ya kimaslahi na matatizo ya

Baraza la Habari lazindua vitabu

Endelea Ukurasa wa 19