4
Mwalimu JK. Nyerere na Kikwazo cha Uongozi na Urafiki Urafiki Urafiki ni hali ya watu kuwa na mahusiano ya karibu na kusaidiana,kushirikiana katika raha na shida.Binaadamu hufarijika zaidi pale anapomshirikisha jambo Fulani rafiki yake na hasa anapokuwa na matatizo na kwakufanya hivyo hujisikia kama vile tatizo/huzuni imepungua. Wanasaikolojia wanashauri sana ukiwa na jambo mjulishe rafiki yako utapata ahuweni na huenda ama nae kisha kumbwa na tatizo hilo au anajua aliekwisha pata na utatuzi wake ulikuwaje ………kila tatizo/jaribu lina mlango wake wa kutokea!! Kwa nchi ambazo zipo katika dimbwi la ufukara,faraja kuu ipo kwa ndugu na marafiki.Muda mwingi hutumika kwa kuwa pamoja ama katika maongezi,sherehe,huzuni na hata kazi za kijumuia.

JK.nyerere Na Urafiki Na Uongozi

Embed Size (px)

DESCRIPTION

'Kuwe na mipaka baina ya Urafiki na Uongozi.Rafiki aheshimu kiongozi na kufuata taratibu za kazi hata kama kiongozi husika ni rafiki yake'Rafiki yako atafurahi zaidi na urafiki utaimarika zaidi pale utakapotenda ipasavyo kwa mujibu wa taratibu.

Citation preview

Mwalimu JK. Nyerere na Kikwazo cha Uongozi na UrafikiUrafikiUrafiki ni hali ya watu kuwa na mahusiano ya karibu na kusaidiana,kushirikiana katika raha na shida.Binaadamu hufarijika zaidi pale anapomshirikisha jambo Fulani rafiki yake na hasa anapokuwa na matatizo na kwakufanya hivyo hujisikia kama vile tatizo/huzuni imepungua.Wanasaikolojia wanashauri sana ukiwa na jambo mjulishe rafiki yako utapata ahuweni na huenda ama nae kisha kumbwa na tatizo hilo au anajua aliekwisha pata na utatuzi wake ulikuwaje kila tatizo/jaribu lina mlango wake wa kutokea!!Kwa nchi ambazo zipo katika dimbwi la ufukara,faraja kuu ipo kwa ndugu na marafiki.Muda mwingi hutumika kwa kuwa pamoja ama katika maongezi,sherehe,huzuni na hata kazi za kijumuia.Hivyo haitarajiwi rafiki yako anapokukosea ukamwadhibu kwa zihaka, ufedhuri,uzandiki au kwa hali yoyote ile bali kinachotakiwa ni kukutana na kuonyana na ikishindikana hatua ya kuliweka mbele ya Wazee hufanyika na mwafaka kufikiwa.Jamii nyingine Urafiki huenda mbali zaidi kwa kuchanja damu kwa kila mmoja na kisha kila mmoja kunyonya damu ya mwenzie na kuweka agano la kusaidiana na kamwe kutosalitiana katika Urafiki wao huo na koo zao pia kuungana katika agano hilo.urafiki si unafiki bali urahisi wa kusaidiana katika kila jambo maishani.

Uongozi na UrafikiKutokana na maelezo hapo juu, mila za kiafrika na utamaduni wetu unatufanya rafiki na ndugu kuwa vigumu kufanya nao kazi kwasababu moja tu..ni nadra na kinyume kumchukulia hatua ndugu yako/rafiki kwavyovyote vile iwayo!! Kufanya hivyo ni kukosa utu,kujidai kutothamini ndugu /rafiki na kuwa wewe unajiona umefika hapo ulipo wakati wengi wamepita tu.!! Kwani nani ambaye hakosei? Huo uongozi si mali yako ni dhamana tu utarudi uraiani tutaonana , n.k.Hizi ni baadhi tu ya tambo za wanajamii pale utakapo mchukulia hatua rafiki/ndugu yako.Zaidi ya hapo, inatarajiwa rafiki yako alikusaidia mambo mbali mbali katika mchakato wa maisha, sasa unaanzaje kumchukulia hatua?Hapa ndipo dhana ya Uongozi na Urafiki inapotuelekeza kujizuia zaidi kuwa na ukaribu wa kimajukumu wewe kiongozi na ndugu yako au rafiki yako.Mwalimu JK.Nyerere alikumbana na kuliona tatizo hili katika hatua ya awali kabisa ya Uongozi wake.Katika harakati zake za kisiasa Mwalimu alipata msaada mkubwa sana kwa wakazi wa Dar es Salaam wa hali na mali.Wakazi hao walimkirimu kwa kiasi kikubwa mno ikiwa ni pamoja na kumsaidia makazi,chakula na fedha za kujikimu pale alipoacha kazi na kuingia katika siasa za moja kwa moja.Baada ya kuwa Rais wa nchi, ilikuwa vigumu sana kwake kuwapa Uongozi wale watu wakaribu sana maana alilitambua tatizo husika la Urafiki na Uongozi..!! unamkemeaje mtu aliekupa masaada wa hali na mali? Katika machapisho na Makala mbali mbali watu wameelezea sana na kulalamika jinsi Mwalimu alivyo waacha watu wakaribu sana katika Uongozi wake..sababu kuu ni hii.Je ,sote kwa pamoja katika ngazi za chini hadi ngazi ya kitaifa, tunazingatia hili? Tujiandae kufanya mabadiliko ya kifikira na kushauriana kutatua jambo hili pindi linapojitokeza .mgogoro wa Urafiki na Uongozi nchini. Na Gilay Shamika