132
ULINGANISHI CHANGANUZI WA MOFU NJEO ZA KIKARA NA KISWAHILI JANUARY PETER NYAWEMA MAGESA TASNIFU ILIYOWASILISHWA KUKAMILISHA MASHARTI YA SHAHADA YA UZAMILI YA KISWAHILI KATIKA ISIMU YA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA, DAR ES SALAAM 2017

JANUARY PETER NYAWEMA MAGESArepository.out.ac.tz/1611/1/TASINIFU_YA_Magessa-21-01-2017.pdf · Mofu ni dhana ya mofolojia ambayo imechambuliwa na baadhi ya wanaisimu . 2 mbalimbali

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • ULINGANISHI CHANGANUZI WA MOFU NJEO ZA KIKARA NA

    KISWAHILI

    JANUARY PETER NYAWEMA MAGESA

    TASNIFU ILIYOWASILISHWA KUKAMILISHA MASHARTI YA

    SHAHADA YA UZAMILI YA KISWAHILI KATIKA ISIMU YA

    CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA, DAR ES SALAAM

    2017

  • ii

    UTHIBITISHO WA MSIMAMIZI

    Mimi J.S.Mdee, ninathibitisha kwamba nimesoma tasnifu hii iitwayo ‘Ulinganishi

    Changanuzi wa Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili’ na nimeridhika kuwa tasnifu hii

    imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuhudhurishwa kwa utahini wa Shahada

    ya Uzamili (M.A) ya Kiswahili katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es

    Salaam.

    Prof. James S. Mdee

    (Msimamizi)

    ……………………………….

    Tarehe

  • iii

    HAKI MILIKI

    Sehemu yoyote ya kazi hii ya Tasnifu hairuhusiwi kubadilishwa kwa ajili yoyote

    iwayo ya kietroniki, kunakilisha, kurudufu, katika hali yoyote, bila ya kupata idhini

    ya maandishi kutoka kwa mwandishi wa Tasnifu hii au chuo Kikuu Huria cha

    Tanzania kwa niaba yake.

  • iv

    TAMKO

    Mimi, Magesa Peter Nyawema January, ninatamka na ninathibitisha kwamba,

    Tasnifu hii iitwayo Ulinganishi Changanuzi wa Mofu Njeo za Kikara na

    Kiswahili ni kazi yangu mimi mwenyewe kwamba, haijawahi kuwasilishwa na wala

    haitawasilishwa katika chuo kingine chochote kwa ajili ya kutunikiwa shahada

    yoyote.

    ………….………

    Saini

    ………….………

    Tarehe

  • v

    TABARUKU

    Naitabaruku kazi hii kwa mama yangu Mecktrida Wegesa Nombe wa Ukerewe kwa

    kunipeleka shule.Pia mke wangu Sia Donath, kwa kunipa ushirikiano wa karibu

    katika kukamilisha shahada ya uzamili kwa kunitia moyo na kuniombea kwa Mungu

    nilipokuwa ninakata tamaa. Bila kuwa sahau wanangu Mercy, Metusela, Marcus na

    Mikayahu kwa kunivumilia muda wote ambao nilikuwa na fanya kozi hii kwa

    kukosa muda wa kuwa nao.

  • vi

    SHUKURANI

    Kazi hii imekamilika kutokana na michango ya watu wengi walioshirikiana nami

    katika kufikisha kazi hii kama ilivyopangwa. Sina budi kutoa shukurani zangu za

    dhati kwa watu wote hao ambao walinisaidia katika kufikisha utafiti huu na kuuona

    hivi jinsi ulivyo. Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Mungu muumba mbingu na

    nchi kwa kunitia nguvu, uzima na kuniwezesha kukamilisha kazi hii na kuifikisha

    katika hatua hii kama inavyoonekana.

    Pili, napenda kutoa kongole zangu kwa msimamizi wangu Profesa James Salehe

    Mdee amekuwa nami bega kwa bega katika kuhakisha kuwa utafiti huu unafanyika

    katika kiwango hiki.

    Tatu, kongole zangu ziwaendee wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili katika chuo

    Kikuu Huria cha Tanzania kwa mchango wao walionipa: Prof. Mdee, Prof. Sengo,

    Prof. Mbogo, Dkt. Zelda, Dkt. Simpassa, Dkt. Lipembe, Dkt. Omary, na Dkt Mreta

    Mungu awape uzima na neema za kipekee ili waendelee kutoa mchango wa

    kitaaluma kwa Taifa letu na nje ya nchi.Nne, shukurani zangu za dhati kwa

    wanafunzi wote wa shahada ya uzamili ya Kiswahili wa mwaka wa masomo

    2014/2015.

    Tano, shukurani zimwendee Mkurugenzi wa TATAKI Dkt. Mosha, E na

    Bi.Msighwa, E wa chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kwa kunipa kibali kutumia

    Makavazi na Maktaba ya TATAKI. Bila kuwasahau David Simon Kilangi, Leonard

    Benard Kulwijira na Innocent Lukondo Mataba walionitajamali.

  • vii

    IKISIRI

    Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza, kubaini na kulinganisha mofu njeo za

    kitenzi cha Kikara na za Kiswahili ili kujua idadi yake, mazingira zinapotokea na

    athari ya maumbo yake inayotokana na mazingira zilimo. Utafiti huu ulifanywa

    katika kata za Bukiko na Nyamanga wilaya ya Ukerewe kwa kuwatumia watoa

    habari 45 waliosailiwa na kujibu maswali. Utafiti huu umetumia nadharia ya Ulalo

    ya Reichenbach ambayo huchunguza, hubainisha na kulinganisha mofu njeo katika

    lugha ya Kikara na Kiswahili. Aidha nadharia hii inahusisha maumbo ya mofu njeo

    kwa kuonyesha wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Mbinu ya utafiti

    iliyotumika katika kukusanya data ilikuwa ni usaili na dodoso. Katika utafiti huu

    watoa taarifa waliteuliwa kwa kuzigatia kigezo cha usampulishaji lengwa na nasibu.

    Uchambuzi wa data ulibainisha kuwa lugha zilizochunguzwa zilikuwa na idadi

    tofauti ya mofu njeo. Kikara kina jumla ya mofu njeo saba ilihali Kiswahili kina

    mofu njeo tano. Utafiti huu uligundua mazingira ya kutokea kwa mofu njeo hizi

    katika vitenzi yalikuwa tofauti kwa baadhi ya mofu njeo na kufanana kwa mofu

    nyingine. Aidha maumbo ya mofu katika vitenzi yaliathiriwa na mazingira

    yalimokuwa, ambazo husababishwa na muungano wa irabu zinazokabiliana katika

    kingo zake.

  • viii

    YALIYOMO

    UTHIBITISHO WA MSIMAMIZI .......................................................................... ii

    HAKI MILIKI ........................................................................................................... iii

    TAMKO ..................................................................................................................... iv

    TABARUKU ............................................................................................................... v

    SHUKURANI ............................................................................................................ vi

    IKISIRI ..................................................................................................................... vii

    UFUNGUO WA ISHARA NA VIFUPISHO ......................................................... xii

    ORODHA YA MAJEDWALI ................................................................................ xiv

    ORODHA YA VIELELELZO ................................................................................ xv

    SURA YA KWANZA ................................................................................................. 1

    1.0 UTANGULIZI ................................................................................................ 1

    1.1 Usuli wa Tatizo ................................................................................................ 2

    1.2 Kauli Kuhusu Tatizo ........................................................................................ 7

    1.3 Lengo kuu la Utafiti ......................................................................................... 8

    1.3.1 Malengo Mahsusi ............................................................................................. 8

    1.4 Maswali ya Utafiti ............................................................................................ 8

    1.5 Umuhimu wa Utafiti ......................................................................................... 9

    1.6 Mipaka ya Utafiti ............................................................................................. 9

    1.7 Fasili ya istilahi zilizotumika katika kazi hii .................................................. 10

    1.8 Hitimisho ........................................................................................................ 11

    SURA YA PILI ......................................................................................................... 12

    2.0 MAPITIO YA MATINI ZINAZOHUSIANA NA MOFU NJEO ............ 12

    2.1 Utangulizi ....................................................................................................... 12

  • ix

    2.2 Mofu Njeo ...................................................................................................... 12

    2.3 Pengo la Utafiti ............................................................................................... 39

    2.4 Kiunzi cha Nadharia ....................................................................................... 40

    2.4.1 Nadharia ya ulalo ya Reichenbach ................................................................. 40

    2.5 Hitimisho ........................................................................................................ 42

    SURA YA TATU ...................................................................................................... 43

    3.0 USANIFU NA MBINU ZA UTAFITI ........................................................ 43

    3.1 Utangulizi ....................................................................................................... 43

    3.2 Usanifu wa Utafiti .......................................................................................... 43

    3.3 Eneo la Utafiti ................................................................................................ 43

    3.4 Mbinu za Utafiti ............................................................................................. 44

    3.4.1 Usaili .............................................................................................................. 44

    3.4.2 Dodoso ........................................................................................................... 44

    3.5 Aina ya Data Iliyokusanywa .......................................................................... 45

    3.5.1 Data ya Msingi ............................................................................................... 45

    3.5.2 Data ya Upili .................................................................................................. 45

    3.6 Sampuli na Usampulishaji .............................................................................. 46

    3.6.1 Sampuli ........................................................................................................... 46

    3.6.2 Usampulishaji ................................................................................................. 46

    3.6.3 Usampulishaji Lengwa ................................................................................... 46

    3.6.4 Usampulishaji Nasibu .................................................................................... 47

    3.6.5 Usampulishaji Makusudio .............................................................................. 47

    3.7 Uchambuzi wa Data ....................................................................................... 48

    3.8 Ukusanyaji wa Data ....................................................................................... 49

  • x

    3.9 Hitimisho ........................................................................................................ 50

    SURA YA NNE ......................................................................................................... 51

    4.0 UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA ZA MOFU NJEO

    ZA KIKARA NA ZA KISWAHILI ............................................................ 51

    4.1 Utangulizi ....................................................................................................... 51

    4.2 Uwasilishaji wa Data ...................................................................................... 51

    4.2.1 Nafasi ya Mofu Njeo Katika Kitenzi cha Kikara ........................................... 52

    4.2.2 Mofu njeo ya Kikara Wakati Uliopo (njeopo) ............................................... 58

    4.2.3 Mofu Njeo ya Kikara Wakati Ujao (Njeojao) ................................................ 65

    4.2.4 Mazingira ya Mofu Njeo na Jinsi Inavyoathiriwa na Umbo la Kitenzi cha

    Kikara ............................................................................................................. 78

    4.3 Nafasi ya Mofu Njeo Katika Kitenzi cha Kiswahili....................................... 86

    4.3.1 Mofu Njeo za Wakati Uliopita ....................................................................... 86

    4.3.2 Mofu Njeo za Wakati Uliopo (Njeopo) .......................................................... 90

    4.3.3 Mofu Njeo za Wakati Ujao (Njeojao) ............................................................ 93

    4.3.3.1 Nafasi ya Mofu Njeo ya Wakati Ujao Katika Kitenzi cha Kiswahili ............ 94

    4.3.4 Idadi ya mofu njeo za kitenzi cha Kiswahili .................................................. 96

    4.3.5 Mazingira ya Mofu Njeo na Jinsi Inavyoathiriwa na Umbo la Kitenzi cha

    Kiswahili ........................................................................................................ 96

    4.4 Kulinganisha mofu njeo za Kikara na Kiswahili ........................................... 98

    4.4.1 Nafasi ya mofu njeo katika kitenzi cha Kikara na Kiswahili ......................... 99

    4.4.2 Idadi ya mofu njeo za Kikara na Kiswahili .................................................. 103

    4.5 Hitimisho ...................................................................................................... 105

  • xi

    SURA YA TANO ................................................................................................... 107

    5.0 MUHTASARI, MAPENDEKEZO NA HITIMISHO ............................. 107

    5.1 Utangulizi ..................................................................................................... 107

    5.2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti ................................................................. 107

    5.3 Mchango wa Utafiti ...................................................................................... 109

    5.4 Mapendekezo ya Tafiti Zijazo ...................................................................... 109

    5.5 Hitimisho ...................................................................................................... 110

    MAREJEO .............................................................................................................. 111

  • xii

    UFUNGUO WA ISHARA NA VIFUPISHO

    - : Mpaka wa mofu

    ( ) : Mabano ya jumla

    / : Ni zote

    / /: Uwasilishaji wa fonimu

    { }: Mabano ya mofu njeo

    + : Ukiongeza

    : Inakuwa

    amm: alama ya muda wa mazungumzo

    amr: alama ya muda rejelewa

    amt: alama wa muda wa tukio

    Dkt: Daktari

    ir.mw : irabu mwisho

    kan: mofu kanushi

    ks: kiambishi sioukomo

    mr: muda rejelewa

    mt: muda wa tukio

    mz: muda wa mazungumzo

    mzz: mzizi

    nfs: nafsi (1= kwanza, 2= pili, 3= tatu)

    njeojao: mofu njeo wakati ujao

    njeopita: mofu njeo wakati uliopita

    njeopo: mofu njeo wakati uliopo

  • xiii

    Prof.: Profesa

    TATAKI: Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili

    Ts: kitenzi kisaidizi

    um: umoja

    wi: wingi

  • xiv

    ORODHA YA MAJEDWALI

    Jedwali 1.1: Mpangilio wa Mofu na Idadi ................................................................ 4

    Jedwali 4.1: Kusawazisha Matamshi Baina ya Irabu /a/ na / i / huzua

    irabu / e / ............................................................................................. 68

    Jedwali 4.2: Nafasi za Mofu Njeo Za Kitenzi Cha Kikara Na Kiswahili

    Zinapotokea Wakati Uliopita ............................................................. 99

    Jedwali 4.3: Nafasi ya Mofu Njeo za Kitenzi cha Kikara na Kiswahili Wakati

    Uliopo ............................................................................................... 100

    Jedwali: 4.4: Kufanana kwa Nafasi za Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili

    Wakati Ujao ...................................................................................... 101

    Jedwali 4.5: Kufanana kwa Nafasi za Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili

    Wakati Ujao Mofu Kanushi.............................................................. 101

    Jedwali 4.6: Tofauti ya Nafasi ya Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili Wakati

    Uliopo Mofu Kanushi ....................................................................... 102

    Jedwali 4.7: Tofauti ya Nafasi ya Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili Wakati

    Ujao Mofu Kanushi .......................................................................... 103

    Jedwali 4.8: Idadi ya Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili Katika Wakati

    Uliopita ............................................................................................. 104

    Jedwali 4.9: Idadi ya Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili Wakati Uliopo ............ 104

    Jedwali 4.10: Idadi ya Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili Wakati Ujao ............... 105

  • xv

    ORODHA YA VIELELELZO

    Kielelezo 2.1: Uwasilishaji wa Muda ........................................................................ 12

    Kielelezo 2.2: Uwasilishaji wa Muda ........................................................................ 13

    Kielelezo 2.3: Uwasilishaji wa Muda ........................................................................ 13

  • 1

    SURA YA KWANZA

    1.0 UTANGULIZI

    Utafiti huu unahusu uchunguzi wa mofu ya lugha ya Kikara na Kiswahili kwa lengo

    ya kuzilinganisha na kubaini idadi yake na mazingira zinamotokea katika vitenzi vya

    lugha hizi. Katika sura hii tunaeleza usuli wa tatizo, kauli kuhusu tatizo, lengo kuu la

    utafiti na malengo mahsusi ya utafiti. Aidha maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti

    huu kwa jumuiya ya akademia na kwa jamii na mipaka ya utafiti ni mambo

    yatakayoelezwa hapa pia. Kabla ya kufanya hivyo tutaeleza kwa ufupi kuhusu lugha

    ya Kikara na Kiswahili.

    Kikara na Kiswahili ni lugha za Kibantu. Kikara ni lugha inayozungumzwa na

    Wakara wanaoishi katika kisiwa cha Ukara kilicho katika ziwa Viktoria. Kwa mujibu

    wa LOT, (2009) Kisiwa cha Ukara kina kadiliwa kuwa na wazungumzaji 114,990.

    Kisiwa hiki cha Ukara ni moja ya visiwa 21 vinavyounda wilaya ya Ukerewe. Lugha

    ya Kikara ambayo hujulikana pia kama Kiregi kwa mujibu wa Mekacha (2000)

    akimnukuu Nurse na Hinnebusch (1993) kipo katika kundi la E.25 Suguti ambalo

    hujumuisha lugha za Kijita, Kikwaya, Kiruri na Kikara chenyewe (Kiregi). Kiswahili

    ni lugha ya watu wa pwani na visiwa vinavyopakana na pwani ya Afrika Mashariki,

    lakini sasa imeenea nchi nzima ambapo inafahamika kama lugha ya kwanza na ya

    pili pia. Kwa mujibu wa uainishaji wa Guthrie (1948) Kiswahili kipo katika ukanda

    wa kijiografia wa G kundi la 40 namba G 42.

    Mofu ni dhana ya mofolojia ambayo imechambuliwa na baadhi ya wanaisimu

  • 2

    mbalimbali katika mitazamo tafauti. Wanaisimu baadhi walioshughulikia mofu ni:

    Katamba na Stonham (2006) wanasema mofu ni umbo la nje linalowakilisha mofimu

    katika lugha. Habwe na Karanja (2007:74-76) wanaifasili mofu kama kipashio

    kidogo kabisa cha neno chenye kusitiri maana.Wanaendelea kusema kuwa uhusiano

    kati ya mofu na mofimu ni ule wa umbo na yaliyomo au kiashiria na kiashiriwa.

    Hata hivyo, kuna vitabu vingine vya isimu na mofolojia vimekuwa vikijadili zaidi

    mofimu na aina zake pamoja na alomofu bila kubainisha mofu. Rubanza (1996: 13-

    80) anasema mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha kiisimu ambacho kina maana.

    Alomofu ni maumbo zaidi ya moja ambayo huwakilisha mofimu moja. Besha

    (1994:59-66) anasema mofimu ni vipashio vidogo sana vya msingi vinavyotumika

    katika kuunda maneno ya lugha. Wesana-Chomi (2013:7, 28) anasema kuwa mofimu

    ni kiambajengo cha neno, ni umbo lenye maana na ambalo linachangia muundo wa

    kimofolojia wa neno. Kuhusu alomofu Wesana-Chomi, (ameshatajwa) anasema

    kuwa ni maumbo tofauti yanayowakilisha mofimu moja yakiwa na maana ya mofimu

    hiyo hiyo.

    Mdee (1999: 8) anasema kuwa mofimu ni kipashio kidogo kuliko vyote katika lugha

    chenye maana kisarufi. Anaendelea kusema kuwa mofimu ni kipashio kidogo kuliko

    neno na ndicho kinachojenga neno. Mfaume (1984:28) kwa upande wake anasema

    mofimu ni maumbo madogo kabisa ambayo yana maana na hayawezi yakagawika

    katika maumbo madogo zaidi yakaleta maana.

    1.1 Usuli wa Tatizo

    Mofu ni umbo la nje linalowakilisha mofimu katika lugha, (Katamba na Stonham

  • 3

    2006:24). Habwe na Karanja (2007:74-76) wanaifasili mofu kama kipashio kidogo

    kabisa cha neno chenye kusitiri maana.Wanaendelea kusema kuwa uhusiano kati ya

    mofu na mofimu ni ule wa umbo na yaliyomo au kiashiria na kiashiriwa.

    Mfano 1:

    a-na-lim-a

    nfs- 3 um - njeopo- mzi-irabu mwisho

    Katamba na Stonham (2006:24) wanasema kuwa mofu ni umbo la nje

    linalowakilisha mofimu katika lugha.

    Mfano: 2

    she- park- ed ( park)

    nfs 3um -mzi- njeopita

    ‘a - li- egesh- a’

    Mofu imefasiliwa pia kama ni vipande vya neno ambavyo vimesetiri mofimu.

    (Mareale (1978) Kwa mujibu wa Mareale (keshatajwa) kila mofu ina maana

    maalumu inapokuwa katika neno.

    Mfano: 3

    a-na-imb-a (anaimba). Neno hili lina mofu nne na kila moja ina maana.

    {a-} mofu nafsi ya tatu ya mtenda; umoja

    {-na-} mofu njeo,wakati uliopo

    {imb-} mofu mzizi wa neno

    {-a} mofu dhamiri ya tendo

  • 4

    Fasili zote hizi zinafanana. Wanazuoni wote wanakubaliana kuwa mofu ni kipashio

    cha kimaumbo ambacho hakiwezi kugawanywa katika sehemu ndogo zaidi zenye

    kuleta maana. Kwa maana hii kila kiambishi ni mofu na kila mzizi wa neno ni mofu.

    Kama inavyoonekana katika jedwali la 1.1 hapa chini.

    Jedwali 1.1: Mpangilio wa Mofu na Idadi

    Neno Mofu Idadi

    a) kalamu kalamu - - - - - 1

    b) alimpigia a li m pig i a 6

    Chanzo: Mtafiti

    Baada ya kueleza maana ya mofu, sasa tutafafanua mofu za njeo na jinsi

    zinavyojidhihirisha katika kitenzi. Mofu njeo kwa mujibu wa Crystal (1991:348) ni

    sehemu ya umbo la kitenzi ambalo huelezea umbo na muda unaolejerea taarifa.

    Lindfors (2003) anaieleza mofu njeo kama msimbo wa uhusiano nukuzi kati ya

    sehemu mbili za mhimili za mahali pa muda. O’Grady na wenzake (1997:733)

    wanaifasili mofu njeo kama kategoria ya kimofolojia ambayo hurejelea uhusiano kati

    ya wakati na muda wa mazungumzo. Kutokana na fasili hizi twaweza kusema kuwa,

    mofu njeo ni umbo la kimofolojia ambalo hurejelea uhusiano kati ya muda wa

    mazungumzo na tukio katika lugha.

    Tafiti zilizofanywa kuhusu mofu njeo katika lugha za Kibantu ni chache. Baadhi ya

    tafiti hizo ni kama vile, Besha (1985) Mreta (1998), Beaudoin-Lietz (1999), Nurse

    (2008) na Walker (2013). Besha (1985) alishughulikia mfumo wa njeo na hali na

    kugundua kuwa lugha ya Kishambala ina mofu njeo nane na mofu hali moja. Mreta

    (1998) alichunguza mofu njeo na hali katika lugha ya Chasu na kugundua kuwa

  • 5

    lugha ya Chasu ina mofu njeo 7 na mofu hali 6. Beaudoin-Lietz (1999) alifanya

    utafiti juu ya miundo ya mofu njeo, hali na ukanushi katika uundaji wa vitenzi vya

    Kiswahili sanifu. Katika utafiti huu, aligundua kuwa Kiswahili kina mofu njeo 3 na

    mofu hali 7.

    Nurse (2008) alichunguza mofu njeo na hali za Kibantu katika mapitio mbalimbali

    kwenye lugha 100 za Kibantu alizochunguza. Kwa mujibu wa Nurse (ameshatajwa)

    mofu njeo hizi alizigawa katika makundi matatu ya wakati uliopita, wakati uliopo na

    wakati ujao. Lugha za kibantu zinatofautiana kimuundo na zipo katika viwango

    mbalimbali. Wakati uliopita una viwango kuanzia kiwango 1 hadi 5, wakati uliopo

    una mofu njeo kuanzia 1 hadi 2 na wakati ujao una mofu njeo kuanzia 1 hadi 4.

    Mofu njeo hizi ni: Mofu njeo za wakati uliopita katika viwongo tofauti ni hizi: -á-, -

    a-, -ka-,-aka-,- -,–li-, a…-ile,-iti,-i, e-..í, hi-,-ku-, na a..-zu, sá-,

    Baadhi ya mofu njeo za wakati uliopo katika Kibantu ni: -a-, -ma-, ø-, -ό- na mofu

    njeo wakati ujao katika viwango tofauti ni: ngá-,-ka-,-aku-,-la-,-laa-, -ra-,-ri-,- dzá-,

    - ci-...-e, -e- zinatofautiana kimuundo kama zitakavyofafanuliwa katika sura ya 2

    Tafiti za kulinganisha mofu njeo za lugha mbili au zaidi tofauti ni chache sana.

    Baadhi ya tafiti linganishiza lugha mbili au zaidi zimehusisha lugha za Kibantu na

    lugha za kigeni kama alivyofanya O’Grady na wenzake (1997), Katamba na

    Stonham (2006:24-34,241) na Walker (2013).

    O’Grady na wenzake (1997) walilinganisha lugha ya Kibemba (lugha yenye toni) na

    Kiingereza na kugundua kuwa lugha ya Kibemba ina mofu za njeo 6 ambazo ni: (-

  • 6

    ὰlí-) juzi,(-ὰlíí-) jana,(-ὰcí-) leo mofu njeo ijayo ambazo ni: (-kά-)kesho kutwa,(-kὰ)

    kesho, na (-léé-) leo baadaye.

    Katamba na Stonham (2006:24-34,241) walichunguza na kulinganisha mofu njeo

    katika lugha ya Kiganda na Kiingereza na kugundua kuwa Kiganda kina mofu za

    njeo 3 ambazo ni:-li- (wakati ujao),-a- (wakati uliopita) na -ø- (wakati uliopo) au

    (mofu ya hali).

    Mfano: 4

    (a)Tu-li-laba vitabu

    “tu-ta-ona vitabu”

    (b) ba-a-laba kitabu

    “wa-li-ona vitabu”

    (c) (ba-ø-kola) bakola

    “wa-na-fanya au

    ‘hufanya’

    Hakuna hadi sasa utafiti wa kulinganisha mofu za njeo za lugha za Kibantu peke

    yake uliokwisha kufanywa unaofahamika. Utafiti tunaoufahamu wa kulinganisha

    mofu za njeo ni wa Walker (2013) ambaye alifanya utafiti wa kulinganisha mofu

    njeo na hali katika lugha ya Kiingereza, lugha ya Kiswahili na Kiikizu, Kizanaki,

    Kiikoma, Kikabwa na Kisimbiti ambazo zote ni lugha za mkoa wa Mara za kundi

    (40). Kwa mujibu wa mwanazuoni huyu mofu njeo za lugha hizi zipo 9 na mofu hali

  • 7

    zipo 4 kama zitakavyoelezwa katika sura ya 2. Mofu njeo hizi ziko katika mgawanyo

    ufuatao: yaani mofu njeo iliyopita ambayo ina kuwa katika nyakati nne tofauti kama

    ifuatavyo; mofu njeo iliyopita zamani, mofu njeo iliyopita jana, mofu njeo iliyopita

    leo ambayo inagawanyika katika nyakati mbili (zaidi ya masaa matano yaliyopita na

    dakika chache zilizopita). Mofu njeo iliyopo na mofu njeo ijayo ambayo ina nyakati

    nne tofauti kama ifuatavyo; mofu njeo ijayo kuanzia kesho kutwa, mofu njeo ijayo

    kesho, mofu njeo ijayo saa chache zijazo leo na mofu njeo ijayo ndani ya masaa

    mawili. Mofu njeo za lugha hizi zinatofautiana kimuundo kama zitakavyoelezwa

    katika sura ya 2.

    Utafiti wa kulinganisha mofu njeo za Kikara na za Kiswahili kama lengo la utafiti

    huu linavyoeleza haujafanyika. Japokuwa Kikara na Kiswahili ni lugha za Kibantu

    mofu njeo zao zinaelekea kutofautiana kwa idadi na hata mazingira zinapotokea.

    Utafiti utakaoibua tofauti hizi ni muhimu kufanyika ili kuonyesha tofauti hizi za

    kiisimu katika lugha za Kibantu.

    1.2 Kauli Kuhusu Tatizo

    Kama ilivyoelezwa juu, utafiti wa kulinganisha mofu njeo na hali za lugha tofauti za

    Kibantu tunaoufahamu ni ule wa Walker (2013) ambaye alilinganisha njeo na hali ya

    lugha ya Kiikizu, Kizanaki, Kiikoma, Kikabwa na Kisimbiti za mkoa wa Mara kwa

    kuzilinganisha na Kiingereza na Kiswahili. Hizi lugha za Mara ni za kundi moja la

    E.40 na mfanano wake ni dhahiri. Lugha ya Kikara ipo katika kundi la (E.25) Suguti

    ambalo lina Kijita, Kikwaya, Kiruri na (Kiregi) Kikara.

  • 8

    Hakuna utafiti uliokwishafanywa wa kulinganisha mofu njeo za lugha ambazo zipo

    katika makundi tofauti kama vile ya Kiswahili (G 42 ) na Kikara (E.25 Suguti) na

    kuonyesha tofauti na mfanano wa vipengele vya kiisimu katika lugha hizi ambavyo

    kama tulivyoeleza juu zina mwelekeo wa kutofautiana. Kwa hivyo kutokana na hali

    hii ni dhahiri kuwa kuna haja ya kuchunguza Kiswahili na Kikara ili kuona ni kwa

    kiasi gani kipashio hiki kinajidhihirisha katika lugha hizi.

    1.3 Lengo kuu la Utafiti

    Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza, kubainisha na kulinganisha mofu njeo za

    Kikara na za Kiswahili ili kujua idadi yake na mazingira zinapotokea.

    1.3.1 Malengo Mahsusi

    Kuchunguza nafasi ya mofu njeo katika kitenzi cha Kikara na cha Kiswahili ili

    kuona mazingira zinamotokea.

    Kubainisha idadi ya mofu njeo za Kikara na za Kiswahili ili kubaini iwapo ni

    sawa au la.

    Kubaini mazingira ya mofu njeo na jinsi inavyoathiriwa na umbo la kitenzi

    ambamo mofu inatokea.

    Kulinganisha mofu njeo za Kikara na Kiswahili ili kuona iwapo zinatokea

    katika nafasi ile ile au la.

    1.4 Maswali ya Utafiti

    Je mofu njeo za Kikara na za Kiswahili zikilinganishwa huonekana kuwa hutokea

    katika nafasi ile ile au la?

  • 9

    Mofu njeo za Kikara na za Kiswahili hutokea katika mazingira gani katika

    kitenzi?

    Je Kikara na Kiswahili zina idadi sawa ya mofu njeo?

    Je mazingira ya mofu njeo za kitenzi cha Kikara na za Kiswahili zinaathiriwa na

    umbo la kitenzi?

    1.5 Umuhimu wa Utafiti

    Utafiti huu una umuhimu mkubwa katika isimu ya lugha za Kibantu.Umuhimu huo

    umo katika maeneo makuu manne:

    Kwanza, utafiti huu unalenga kuwasaidia wanazuoni, walimu na wanafunzi

    wanaojifunza lugha za kibantu katika dhana za mofu njeo katika lugha za Kibantu.

    Pili, matokeo ya utafiti huu yatasaidia watafiti wa baadaye watakaotumia kama rejeo

    katika isimu.

    Tatu, utakuwa kichocheo kwa watafiti wengine hususani wazawa wa lugha hii

    kushawishika kutafiti na kuandika Makala na vitabu juu ya lugha hii kwa nia ya

    kuikuza, kuitunza, na kuimarisha ili kuipa hadhi.

    Nne, mofu za njeo katika lugha ya Kikara haijachunguzwa na kuandikwa, kwa hali

    hiyo kazi hii itafanya hilo na kutoa mchango katika taaluma.

    1.6 Mipaka ya Utafiti

    Utafiti huu una lengo la kulinganisha vipengele vya kimofolojia vya mofu njeo za

    Kikara na za Kiswahili tu. Utafiti huu hautashughulikia mofu nyingine za lugha hizi

  • 10

    kama vile mofu kanushi, mofu hali, mofu patanishi, mofu sharti, mofu rejeshi, mofu

    yambwa, na kadhalika.

    1.7 Fasili ya istilahi zilizotumika katika kazi hii

    alomofu ni maumbo tofauti yanayowakilisha mofimu moja yakiwa na maana hiyo

    hiyo.

    mofu ni umbo la nje linalowakilisha mofimu katika lugha.

    mofu njeo ni kategoria ya kimofolojia ambayo hurejelea uhusiano kati ya wakati wa

    muda wa mazungumzo.

    njeo ni umbo la kimofolojia ambalo hurejelea uhusiano kati ya muda wa

    mazungumzo na tukio katika lugha.

    wakati uliopita kitambo katika (Kikara) huelezea matendo yaliyotendeka au

    kutotendeka siku mbili kabla ya muda wa mazungumzo nakurudi nyuma kama juma,

    mwezi, miezi na miaka iliyopita.

    wakati uliopita wa karibu katika (Kikara) hutumika katika kuelezea matendo

    yaliyotendeka au kutotendeka siku moja kabla ya muda wa mazungumzo.

    wakati uliopo katika (Kikara) hutumika kuelezea matukio yanayotokea au

    hayatokei sambamba na muda wa mazungumzo.

    wakati ujao kitambo katika (Kikara) hutumika kuelezea matukio yatatokea au

    hayatatokea kuanzia miaka miwili na kuendelea hadi miaka mingi ijayo baada ya

    muda wa mazungumzo.

    wakati ujao kitambo kiasi katika (Kikara) hutumika kuelezea matukio yanayotokea

    au hayatokei kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja baada ya mazungumzo.

  • 11

    wakati ujao wa karibu katika (Kikara) hutumika kuelezea matendo

    yatakayotendeka au kutokutendeka muda mfupi baada ya mazungumzo hadi masaa

    machache yajayo kabla ya siku inayofuata.

    wakati uliopita katika (Kiswahili) hutumika kueleza kuwa tendo lilitendeka au

    halikutendeka kabla ya kutolewa kwa taarifa.

    wakati uliopo katika (Kiswahili) hutumika kuelezea kuwa tendo linafanyika au

    halifanyiki wakati ule ule ambao tendo linaendelea kufanyika.

    wakati ujao katika (Kiswahili) hutumika kueleza tendo ambalo litafanyika au

    kutofanyika katika wakati wote ujao.

    1.8 Hitimisho

    Sura hii ilitalii usuli wa tatizo, kauli kuhusu tatizo, malengo ya utafiti, maswali ya

    utafiti, umuhimu wa utafiti na mipaka ya utafiti. Sura inayofuata inaelezea mapitio

    ya matini zinazohusiana na mofu njeo. Mapitio yalipitiwa yalisaidia katika kufikia

    lengo la utafiti huu.

  • 12

    SURA YA PILI

    2.0 MAPITIO YA MATINI ZINAZOHUSIANA NA MOFU NJEO

    2.1 Utangulizi

    Sehemu hii inabainisha maandiko mbalimbali yanayohusiana na mada hii.

    Machapisho ambayo tumeyazingatia ni yale yanayoelezea dhana ya mofu, alomofu,

    mofu njeo na kiunzi cha nadharia.Tumetumia nadharia ya ulalo ya Reichenbach

    ambayo inasema kuwa muda unarejelea alama tatu ambazo ni muda wa

    mazungumzo, muda wa tukio na muda rejelewa. Nadharia hii inaonyesha alama tatu

    muhimu za kuzingatia wakati wa kuelezea mahusiano ya nyakati katika lugha.

    Alama hizi ni alama ya muda wa mazungumzo (mz) muda ambao usemi unatamkwa,

    alama ya muda wa tukio (mt) muda ambao tukio linatokea, na alama rejelewa (ar)

    alama ya wakati uliopo kati ya muda wa mazungumzo na muda wa tukio.

    (li) uliopita -na-(uliopo) (-ta-)ujao

    mz ar mt

    Kielelezo 2.1: Uwasilishaji wa Muda

    Chanzo: Reichenbach (1947)

    2.2 Mofu Njeo

    Kama tulivyoeleza katika sura ya kwanza, mofu njeo ni sehemu ya umbo la kitenzi

    ambalo huelezea umbo na muda unaolejerea taarifa (Crystal 1991). Comrie (1985)

    anasema kuwa wakati unaweza kuwasilishwa na mstari mnyoofu, wenye wakati

  • 13

    uliopita upande wa kushoto na wakati ujao kulia.” Katika uwasilishaji wake, wakati

    uliopo (alama) Ο kwenye mstari mnyoofu.

    Wakati uliopita Ο wakati ujao

    wakati uliopo

    Kielelezo 2.2: Uwasilishaji wa Muda

    Chanzo: Comrie (1985)

    Comrie (1985) anaeleza kuwa mchoro wa muda huwasilisha utoshelevu kwa

    kuelezea mofu njeo katika lugha ya mwanadamu. Kwa mujibu wa Lindfors (2003)

    nadharia ya Reichenbach ya mofu njeo ina sehemu mbili ambazo ni uhusiano mahali

    rejeshi (umr) na muda wa tukio (mt). Makosa yanayojitokeza katika (umr)

    inapendekeza kuwa ni tukio lililoambatana na muda wa mazungumzo (mz).

    Uhusiano huo umepangwa katika mfumo ufuatao:

    Kielelezo 2.3: Uwasilishaji wa Muda

    Chanzo ni kutoka Lindfors (2003)

    Mstari huu mkubwa mweusi huwakilisha tukio la muda

    uliopita uliopo ujao

    ---------------- --------------- --------------- --------------- --------------- ------------

    Muda wa usemi

  • 14

    Lindfors (ameshatajwa) hueleza kuwa njeo inajitokeza katika makundi makubwa

    matatu kama kielelezo hapo juu kinavyoonesha. Kwanza ni wakati uliopita, ambao

    tukio la muda lililotokea kabla ya muda wa mazungumzo, uliopo ambao tukio la

    muda linaendelea na mwisho wakati ujao ambao muda wa tukio hufuata muda wa

    mazungumzo kabla ya tukio.

    Besha (1985:198-279) aliyefanya utafiti juu ya mfumo wa njeo na hali katika lugha

    ya Kishambala alibainisha mofu njeo 8 na mofu ya hali 1 katika Kishambala. Besha

    (ameshatajwa) ameonyesha kuwa wakati uliopita una mofu njeo 4 na mofu ya hali 1

    ambazo zina uhusiano kwa karibu na muda wa mazungumzo. Ili kujua tofauti ya

    muda unaorejelewa, wazungumzaji sharti wawe na maarifa ya nyuma yanayofanana.

    Mofu za njeo za wakati uliopita zinazofafanuliwa na vielezi vya wakati ni:

    a) - iyé jana

    b) -za-siku ya jana,

    c) -ὰ- siku ile wakati uliopita na

    d) -άά-siku nyingi zilizopita zamani.

    Kwa kutumia vielezi vya wakati kama vile; ghulo (jana), ghulo nakiyo (jana usiku),

    lelo (leo), lelo makelo (asubuhi hii), zuzi (siku kabla ya jana), haya kale (siku nyingi

    zilizopita), keloi ushwelo (jioni) katika Kishambala huonyesha wakati, kama mfano

    ufuatao:

    Mfano: 1

    a) ti-di-iyé maboko (ghulo) ‘tulipika ndizi (jana)’ (njeo ya wakati uliopita)

  • 15

    b) ti-zὰ-dika maboko (ghulo) ‘tulipika ndizi (jana)’ (njeo ya wakati uliopita)

    c) t-ὰ-dika maboko (uja mushi) ‘tulipika ndizi (siku ile) (njeo ya wakati uliopita)

    d) t-άά-dika maboko (uju mushi) ‘tulipika ndizi (siku ile zamani)’ (njeo ya wakati

    uliopita zamani)

    Besha (ameshatajwa) amefafanua kuwa kuna mofu 3 zinazobainisha wakati uliopo

    ambazo ni:-ø-wakati uliopo -ta- wakati uliopo wa kawaida na -aa- wakati uliopo wa

    kuendelea. Kwa mfano

    Mfano: 2

    a) (ivi aha) ni- ø-onda ghembe ‘(sasa hivi) ninatafuta jembe’ (njeo ya wakati uliopo)

    b) (ivi aha) uko nyumba-i ti-ta-dika manga‘(sasa hivi) tuko nyumbani tunapika

    mihogo’ (njeo ya wakati uliopo)

    c) (ivi aha) (uko nyumbai) waghani w-aa-j-a ‘sasa hivi huko nyumbani wageni

    wanakula’ (njeo ya wakati uliopo)

    Ameeleza kuwa wakati ujao una mofu njeo moja ambayo ni: -ne- (kesho)-nee- (siku

    zijazo)

    Mfano: 3

    a) ne-ti-dik-e (maboko) (keloi) ‘tutapika (ndizi) (kesho)’

    b) nee-ti-dik-e (maboko) (iyo mushi yeiza) ‘tutapika ndizi siku zijazo’

    ne- ina tumia vielezi vya wakati vifuatavyo: mushi (mchana), ushwelo (jioni), keloi

    (kesho) na kishindo (siku baada ya kesho) na nee- ina tumia vielezi vya wakati

    vifuatavyo: iyo mushi yeiza (siku zijazo) iyo myezi yeiza (miezi ijayo) ayo mavuli

  • 16

    yaza (miaka ijayo) Mofu ya wakati uliopo wa kuendelea ambayo ni -aa- haina toni

    isipokuwa inafanana na ile ya wakati uliopita ambayo huwa ina toni juu -άά-.

    Pamoja na hayo, Besha (ameshatajwa) anataja jana mara mbili inawezekana ni

    makosa ya kiuandishi. Maana ameeleza kielezi (juzi) lakini hajatoa mfano kuhusu

    juzi. Huenda mojawapo inahusika na juzi.

    Katika utafiti huu, mtafiti alionyesha kuwa mofu njeo za wakati uliopita moja

    hutokea mwishoni mwa kitenzi kama kiambishi tamati.

    Mfano: 4

    ti-di-iyé maboko (ghulo) ‘tulipika ndizi (jana)

    Mofu njeo tatu zilizobaki wakati uliopita hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi.

    Mfano: 5

    a) ti-zὰ-dika maboko (ghulo) ‘tulipika ndizi (jana)

    b) t-ὰ-dika maboko (uja mushi) ‘tulipika ndizi (siku ile)

    c) t-άά-dika maboko (uju mushi) ‘tulipika ndizi (siku ile zamani)

    Katika wakati uliopo mofu njeo zote tatu hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi kama

    kiambishi awali.

    Mfano: 6

    a) ni- ø-onda < ni-na-tafuta

    b) ti-ta-dika < tu-na-pika

    c) iii) w-aa-j-a

  • 17

    Katika wakati ujao mofu njeo hutokea mwanzoni mwa kitenzi kabla mofu nafsi.

    Mfano: 7

    i) ne-ti-dik-e t- ὰ-dika (uju mushi) ‘tulipika (siku ile )

    b) ti + άά-dika > t- άά-dika (uju mushi) ‘tulipika (siku ile zamani)

    c) wi- + aa-j-a > w-aa-j-a < wa-na-kula (wakati uliopo)

    Mreta (1998) alichunguza mofu njeo na hali katika lugha ya Chasu.Katika utafiti

    wake alibaini kuwa lugha ya Chasu ina mofu njeo 7 na mofu hali 6.

    Mfano 9: Mofu njeo wakati uliopita

    a) é - ð- ie yό (wakati uliopita leo)

    nfs3 um- / njeojao- mzz- ir.mw leo

    ‘alikuja leo’

    b) á- na- im- a ighuo (wakati uliopita kuanzia jana)

    nfs3 um/-njeopita- mara moja- mz-ir.mw jana

    ‘alilima mara moja jana’

    c) é- im - ie ishamba lakwé (wakati uliopita wa kawaida)

  • 18

    nfs3 um/-njeopita- mzz- ir.mw shamba lake

    ‘alilima shamba lake’

    d) é- im - íe he mghunda (wakati uliopita zamani kiasi)

    nfs3 um/-njeopita- mzz- ir.mw ndani ya makaburi

    ‘alilima ndani ya makaburi’

    e) é-!kí- im - íe hé- mghunda (wakati uliopita zamani sana)

    nfs3 um/-njeopita- mzz- ir.mw. ndani ya makaburi

    ‘alilima ndani ya makaburi zamani sana’

    Katika wakati uliopita mofu njeo zote tano hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi kama

    kiambishi awali.

    Wakati uliopo katika Chasu una mofu njeo 2, ambazo ni: { - ø -} na {é- ra-}.

    Katika wakati uliopo {- ø -} huonyesha tendo linaendelea muda wa mazungumzo.

    Mfano: 10 Mofu njeo wakati uliopo

    a) é- ø - tόng- a yό (wakati uliopo ambao tendo linafanyika leo)

    nfs3um njeopo mzz- ir. mw leo

    ‘anaenda leo’

    b) é- ø - tόng- a yaßo ( wakati uliopo tendo litafanyika kesho)

    nfs3um njeopo mzz- ir. mw kesho

    ‘anaenda kesho’

    c) é - ra- im- a- ishamba lakwé ( wakati uliopo unaendelea hajafikia kikomo)

    nfs 3um bado- mzz- ir.mw shamba lake

  • 19

    d) ‘bado analima shamba lake’

    Katika wakati uliopo mofu njeo hizi zote hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi kama

    kiambishi awali.

    Katika wakati ujao Chasu una mofu njeo 2 ambazo huonyesha tendo litatendeka

    baadaye.

    Mofu njeo -ne- ya wakati ujao inaonesha tendo litatokea muda mfupi baada ya muda

    wa mazungumzo.

    Mfano: 11

    a) é- ne- im- a ishamba lakwé (wakati ujao baadaye baada ya mz)

    nfs3 um -njeojao- mzz- ir.mw shamba lake

    ‘atalima shamba lake ’

    b) é- ne- im- a miÕi yeðie (wakati ujao siku nyingi zijazo)

    nfs3 um -njeojao- mzz- ir.mw siku zijazo

    ‘atalima siku zijazo’

    Mofu njeo -ra- huelezea tendo litakalotokea baadaye katika wazo fulani.

    Mfano: 12

    a) é- ra- ok-a mwalimu. (wakati ujao siku zijazo)

    nfs3 um -njeojao- mzz- ir.mw mwalimu

    ‘atakuwa mwalimu’

    b) é- ra- bá-a ngwii.

  • 20

    nfs3 um -njeojao- mzz- ir.mw

    ‘atakata kuni’

    Katika wakati ujao pia mofu njeo hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi kama kiambishi

    awali.

    Kwa mujibu wa Mreta (ameshatajwa) kuna mambo matatu yanayojitokeza kati

    Chasu. Kwanza, maumbo ya kimofolojia yanayotumika katika mofu njeo kimaana

    hayaendi sawia na hali halisi ya kile kinachoelezwa na maumbo yanayotumiwa na

    mofu njeo. Hii ina maana kuwa mofu njeo {-ø -} ya wakati uliopo inatumika pia

    katika mofu hali. Katika Chasu mofu njeo {-ra-} inatumika wakati uliopo na ujao.

    Katika mfano 12b kuna maana mbili: maana ya kwanza inatokea katika wakati

    uliopo ‘bado anakata kuni’ na maana ya pili inatokea katika wakati ujao ‘atakata

    kuni’. Pili, katika kitenzi kunakuwa na maumbo mawili yanayoonesha mofu njeo.

    Mfano wakati uliopita mofu njeo.

    {é-} huonesha wakati uliopita na {- ie} huonesha ukamilifu wa tendo lenyewe. Tatu,

    mofu hizi za njeo zinahusiano sana na vielezi kwa kurejea maana nyingine.

    Kuna athari za kiisimu ambazo zinatokana na kitenzi husika kuwa na toni au

    kutokuwa na toni kwenye irabu ya mwisho / íe / katika wakati uliopita zamani kiasi

    na wakati uliopita wa kawaida irabu ya mwisho /- ie /.

    Platt (1972) alichunguza umbo la vitenzi vyenye toni katika lugha ya Kikuyu. Katika

    utafiti wake alibaini kuwa lugha ya Kikuyu ina mofu njeo 4. Platt (ameshatajwa)

  • 21

    ameonyesha kuwa wakati uliopita una mofu njeo 1 inayojitokeza katika wakati

    uliopita wa muda mrefu na wakati uliopita wa muda mfupi. Katika wakati ujao una

    mofu njeo 3, wakati ujao wa karibu, wakati ujao kitambo kiasi na wakati ujao wa

    kitambo.

    a) Mofu njeo katika Kikuyu wakati uliopita hujitokeza katika wakati uliopita wa

    muda mrefu na wakati uliopita wa muda mfupi. íré

    i) Mofu njeo iliyopita muda mrefu (–íré)

    Mfano: 13

    i) o-tem-iré ‘u-li-kata’

    ii) ά-gόr-iré ‘a-li-nunua’

    ii)Mofu njeo iliyopita muda mfupi (–íré)

    Mfano: 14

    i) άᵭondék-íré `a-li-shona`

    ii) άniin-íré ‘a-li-naliza`

    b) Mofu njeo ijayo

    Mofu njeo ijayo imegawanyika katika nyakati tatu

    i) Mofu njeo ijayo wa karibu (-ré-, ά )

    Mfano: 15

    i) o – ré - niin - ά > o-ré-niin-a ‘u-ta-maliza’

    ii) a - ré- gor - ά > a-re-gόr-a ‘a-ta-nunua’

    ii) Mofu njeo ijayo kitambo kiasi (-ko-,-ά )

  • 22

    Mfano: 16

    i) [ό [ko[άn ek ά > okwάnékά `utaeneza`

    ii) [ό [ko [ᵭὸndekά > όkόᵭondékά `utategeneza`

    iii) Mofu njeo ijayo kitambo muda mrefu (–ka-, -a)

    Mfano: 17

    i) o-ka-tem-ά ‘u-ta-kata’

    ii) a-ka-gόr-a ‘a-ta-nunua’

    Katika utafiti huu tunaona kuwa mofu njeo ya wakati uliopita hutokea baada ya

    mzizi wa kitenzi kama kiambishi tamati.

    Mfano: 18

    i) άά-ndek-iré ‘a-li-andik-a’

    ii) o-tem-iré ‘u-li-kata’

    Katika wakati ujao mofu njeo hutokea kabla ya mzizi kama kiambishi awali.

    Mfano: 19

    i) a - ré- gor - ά > a-re-gόr-a ‘a-ta-nunua’

    ii) [ό [ko [ᵭὸndekά > όkόᵭondékά `utategeneza`

    iii) a-ka-tem-ά ‘u-ta-kata’

    Athari inayoonekana ya kiisimu ambayo inasababishwa na msigano wa sauti za irabu

    zinapofuatana katika mofu njeo ijayo kitambo kiasi.

    Mfano: 20

    [ό [ko [άnekά > okwάnékά.

  • 23

    Aidha anaeleza kuwa, athari za kiisimu hujitokeza pale ambapo mofu njeo ambayo

    ina irabu yenye toni ya juu inapokaribiana na mzizi wa kitenzi ambao huanza na

    irabu husababisha irabu yenye toni kudondosha toni na irabu iliyo katika mzizi

    hupokea toni.

    Mfano: 21

    i) a- ré- gor- ά > aregόra ‘a-ta-nunua’.

    Walker (2013) alifanya utafiti wa kulinganisha njeo na hali katika lugha ya

    Kiingereza, Kiswahili na Kiikizu, Kizanaki, Kiikoma, Kikabwa na Kisimbiti ambazo

    zote ni lugha za mkoa wa Mara za Kundi E.40. Kwa mujibu wa mwanazuoni huyu

    mofu njeo zipo 9 na mofu hali zipo 4.

    a) Mofu njeo iliyopita

    Mofu njeo iliyopita ipo katika viwango vinne tofauti.

    i) Mofu njeo iliyopita zamani

    Mofu njeo -ka-, hutumika katika Kiikizu na Kizanaki,-a (a) - hutumika katika

    Kikabwa na Kisimbiti na Kiikoma haijaoneshwa na mtafiti wa kazi hii.

    Mfano: 22

    i) Kizanaki: tu-ka-gaamb-an-a na-we (ekare) ` tuliongea naye (zamani) `

    ii) Kisimbiti: (n-kare) tw-aa-shumaash-ire na-we. `Tuliongea naye (zamani) `

    iii) Kikabwa: tw-a-hair-a na-we (akare). `Tuliongea naye (zamani)`

    iv) Kiikizu: tu-ka-gaamb-an-a na-wi (ikari).` tuliongea naye (zamani) `

    ii) Mofu njeo iliyopita jana

  • 24

    Mofu njeo -ka-, hutumika katika Kiikizu na Kizanaki,-a (a) - hutumika katika

    Kisimbiti, Kikabwa hutumia –a- na Kiikoma haijaoneshwa. (Walker 2013) alitoa

    mfano 1 wa Kikabwa (uk 44) kama ilivyo katika mfano 23 hapo chini.

    Mfano: 23

    Kikabwa: tw-a-bhin-iri (ejo) `tulicheza (jana)

    (iii) Mofu njeo iliyopita leo

    Mofu njeo iliyopita leo and Mofu njeo iliyopita inayotokea muda mfupi ndani ya

    masaa mawili tangu muda wa mazungumzo.Katika lugha hizi tano inajitokeza katika

    Kikabwa na inatumia vielezi vya wakati (nyenkyo inu) (asubuhi hii).

    Mfano: 24

    i) Tu-bhin-iri nyenkyo i-nu. “tulicheza asubuhi hii”

    Walker (ameshatajwa) anasema kitu kimoja ambacho ni kigumu kabisa katika

    uthibitishaji wa usemaji juu ya wakati uliopita leo katika Kiswahili ni kweli kuwa

    maelezo ni yale ya wakati uliopita kuanza masaa mawili leo ambayo kiuhalisia

    inatokana na mofu ya hali –me-.Hii ni kwa sababu uhusiano wa mofu hali katika

    Kiswahili ni vigumu kutambua kama umbo la –me- linakuwa katika mofu njeo

    kwani uthibitishwaji wake upo katika mofu za hali. Anaendelea kusema kuwa, huu ni

    utata ambao hakuna uthibitishaji wa usemaji kutoka katika Kiswahili kwani ni

    vigumu sana kutofautisha aina hizi katika lugha nyingi za Kibantu (Nurse 2008: 94-

    99).

    b) Mofu njeo iliyopo.

  • 25

    Mofu njeo iliyopo ina mofu njeo zifuatazo kulingana na lugha husika.

    Mfano: 25

    i) Kikabwa: tw-aa-gy-a Darisaraamu `` tunaenda Dar-ES salaam” (wakati

    uliopo)

    ii) Kiikizu: tw-aa-j-a Daresaraamu `` tunaenda Dar-ES salaam” (wakati uliopo)

    iii) Kiikoma:to-ø- gha-ye Darisaraamu `` tunaenda Dar-ES alaam” (wakati

    uliopo)

    iv) Kisimbiti:to-ra-y-a Daresaramu`` tunaenda Dar-ES salaam” (wakati uliopo)

    v) Kizanaki: tu-ra-gy-a Darisaraam`` tunaenda Dar-ES salaam” (wakati uliopo)

    c) Mofu njeo ijayo

    Mofu njeo ijayo imegawanyika katika nyakati nne ambazo ni: leo ndani ya masaa 2

    yajayo, baadaye leo, kesho na kesho kutwa na kuendelea.

    i) Mofu njeo ijayo kuanzia kesho kutwa

    Mofu njeo ijayo ambayo inatokea kuanzia kesho kutwa na kuendelea ni zifuatazo:

    Kiikizu na Kizanaki kinatumia -ra-, Kiikoma kinatumia -ko- na Kikabwa na

    Kisimbiti kinatumia -ri-

    Mfano: 26

    Kizanaki: Tu-ra-keranh-a na-we o-mwaka gu-no gu-kuz-a.

    `Tutaongea naye mwaka ujao`

    Kiikizu: Tu-ra-gaamb-an-a na-wɨ u-mw-aaka gu-nu gu-ku-uz-a.

    ‘Tutaongea naye mwaka ujao’.

  • 26

    Kiikoma: N-to-ko -siiker-a na-we mo-mo-oka u-no o-ku-uch-a.

    ‘Tutaongea naye mwaka ujao.’

    Kisimbiti: O-mo-oka ghu-yö ghu-ku-ush-a n-tu-ri-shumaash-a nawe.

    ‘Tutaongea naye mwaka ujao.’

    Katika lugha hizi tano za Mara ni lugha mbili tu ambazo ni Kikabwa na Kisimbiti

    ambazo mofu njeo ni –ri-

    (ii) Mofu njeo ijayo kesho

    Mofu njeo ijayo inatokea katika matukio yanayotegemea kutokea kesho. Katika

    Kiikizu na Kizanaki hutumia –ra-, Kiikoma hutumia –ko-, Kikabwa –aka- na

    Kisimbiti hutumia -ri-.

    Katika lugha hizi tano za Mara, Kizanaki na Kiikizu ndizo zinatumia -ra- lugha

    tatu zinazobaki kila moja ina mofu njeo yake.

    Mfano: 27

    Kikabwa: Tw-aka-hair-e na-we ejo. ‘Tutaongea naye kesho.’

    Kizanaki: Izo tu-ra-keranhia nawe. `kesho tutaongea naye`

    Kiikoma: N-to-ko-siikera nawe. ` tutaongea naye`

    Kisimbiti: N-tu-ri-shumaasha nawe. `tutaongea naye`

    Kiikizu: Tu-ra-gaamb-an-a nawi. `tutaongea naye`

    (iii) Mofu njeo ijayo saa chache zijazo leo

    Mofu njeo ijayo saa chache zijazo leo ni tukio linalotegemea kutokea saa chache

    zijazo tangu muda wa mazungumzo.

  • 27

    Kiikizu na Kizanaki hutumia –ra-, Kiikoma hutumia –ko- , na Kikabwa na Kisimbiti

    hutumia -aka-.

    Mfano: 28

    Kisimbiti: Mo-ghorobha n-tw-aka-shumaash-e na-we.‘Tutaongea naye jioni hii.’

    Hakuna mfano mwingine uliotolewa na mtafiti wa kazi tangulizi katika lugha zingine

    (walker 2013: 46)

    iv ) Mofu njeo ijayo leo ndani ya masaa mawili

    Mofu njeo ijayo leo ni tukio linalotegemea kutokea ndani ya muda wa masaa mawili

    yajayo tangu muda wa mazungumzo lakini tukio hutokea kama ilivyopangwa.Hii ni

    katika Kisimbiti na Kikabwa (Mwita 2008: 47). Katika Kiikizu na Kizanaki hutumia

    –ra-, Kiikoma hutumia –ko- , na Kikabwa na Kisimbiti hutumia -raa-.

    Mfano: 29

    Kisimbiti: Ha-no se-raa-het-e se-dakika i-kömi n-to-raa-shumaash-e na-we.

    ‘Tutaongea naye baada ya dakika kumi.’

    Katika utafiti huu wa ulinganishi wa mofu njeo na hali katika Kiingereza, Kiswahili

    na lugha tano za mkoa wa Mara zilizo kundi (40) yaani, Kiikizu, Kizanaki, Kiikoma,

    Kikabwa na Kisimbiti, Walker (2013) anasema, mofu njeo za wakati uliopita

    zinatofautiana kimuundo. Lugha zilizo kusini mwa Mara ni: Kiikoma, Kiikizu, na

    Kizanaki na zilizo kaskazini ni: Kikabwa na Kisimbiti.

    Katika mofu njeo iliyopita zamani, jana na leo Kiikizu na Kizanaki zinatumia mofu

    –ka- ilhali Kikabwa na Kisimbiti zinatumia mofu –a(a)- zamani na jana bali Kiikoma

  • 28

    kinatumia –iri. Katika utafiti (Walker 2013) pamoja na kueleza kuwa Kiikoma

    kinatumia –iri hakuna mfano wowote uliotolewa kuthibitisha alichoeleza.

    Kizanaki na Kisimbiti zinatumia mofu njeo –ra-, Kiikizu na Kikabwa zina mofu –aa-

    na Kiikoma kina mofu njeo –ø- katika wakati uliopo.Wakati ujao Kiikoma, Kiikizu

    na Kizanaki zinatumia mofu njeo-ra-,Kikabwa na Kisimbiti zinatumia mofu njeo 3

    ambazo ni -raa-, -aka- na -ri-.

    Athari inayoonekana katika lugha hizi ni kuwa, mofu njeo –aa- ya wakati uliopita

    katika lugha ya kizanaki hutumika pia wakati uliopo katika lugha ya Kikabwa na

    Kiikizu. Mofu njeo -ra- ya wakati ujao katika lugha ya Kiikizu na Kizanaki

    hutumika pia wakati uliopo katika lugha ya Kizanaki na Kisimbiti.

    Beaudoin-Lietz (1999) alifanya utafiti juu ya miundo ya mofu njeo, hali na ukanushi

    katika uundaji wa vitenzi vya Kiswahili sanifu. Mtafiti huyu alitumia uchanganuzi

    mofosemantikia na nadharia ya Guillaumian ilitumika katika kazi hii. Katika utafiti

    wake amesema kuwa katika Kiswahili sanifu mofu njeo hutokea kabla ya mzizi, hii

    ni tofauti na lugha nyingine za Kibantu. Katika kazi yake hii amebainisha kuwa

    Kiswahili kina mofu njeo 3 na mofu hali zipo 7.

    Mofu njeo ya wakati uliopita unaonekana wazi kuwa tendo linaloelezewa limepita.

    Mfano: 30

    a) wa- li- imb- a (wakati uliopita katika uyakinishi)

    nfs3um-njeopita-mzz- ir.mw

  • 29

    b) ha- wa- ku- imb- a (wakati uliopita katika ukanushi)

    kan- nfs3um- njeopita- mzz- ir.mw

    Mofu njeo ya wakati ujao tukio lake halijakuwepo au halijafanyika.

    Mfano:31

    a) wa- ta- imb- a

    nfs3um-njeojao- mzz- ir.mw

    b) ha- wa- ta- imb-a (wakati ujao katika ukanushi)

    kan- nfs3um-njeojao- mzz- ir.mw

    Katika kazi yake, Beaudoin-Lietz ameonyesha kuwa mofu –na- ni miongoni mwa

    mofu hali katika lugha ya Kiswahili.Katika utafiti huu mtafiti alitofautiana naye

    (tazama 4.3.2) kwa kuiona mofu hii kama mofu katika wakati uliopo. Katika utafiti

    huu umechangia katika isimu ya lugha kwa kutambua kuwa nafasi ya mofu njeo za

    Kiswahili sanifu hutokea kabla ya mzizi, pia mtafiti litamsaidia sana kwa sababu ni

    mojawapo ya lengo mahsusi la kuchunguza nafasi ya mofu njeo. Ingawa hivyo, bado

    kazi hiyo haikukidhi haja iliyokusudiwa na utafiti huu.

    Nurse (2008) alichunguza mofu njeo na hali za Kibantu katika lugha 100 za Kibantu.

    Katika utafiti wake aligundua kuwa katika lugha za kibantu mofu njeo zake zina

    tofautiana katika viwango. Kwa mfano, zipo lugha ambazo wakati uliopita una

    viwango vitano. Wakati uliopita kitambo sana, wakati uliopita kitambo, wakati

    uliopita kitambo kiasi, wakati uliopita wa karibu na wakati uliopita wa karibu kiasi.

    Tuangalie mfano 32 lugha ya Kikongo-zombo hapa chini.

  • 30

    Mfano:32

    Kikongo-Zombo

    a) Wakati uliopita kitambo sana

    tú- ø -súmba / tú-ø-súmb-idi / tu- ø -súmb-id-il-ing-i

    ‘tulinunua’ (wakati uliopita zamani sana)’

    b) Wakati uliopita kitambo

    tu- ø -súmba

    ‘tulinunua’ (muda uliopita kuanzia miezi miwili hadi miaka miwili)

    c) Wakati uliopita wa karibu

    tu- ø -súmb-idi

    ‘tulinunua’

    d) Wakati uliopita wa karibu kiasi

    tu- ø -sumb-idi

    ‘tulinunua’ (leo)

    e) Wakati uliopita wa karibu

    tu- ø -fuma-sumb-i au (tu- ø -fuma sumb-i)

    ‘tumenunua’( leo baada ya muda wa mazungumzo’

    Pia zipo lugha zenye viwango vinne katika wakati uliopita. Viwango hivi ni: wakati

    uliopita kitambo, wakati uliopita kitambo kiasi, wakati uliopita wa karibu na wakati

    uliopita wa karibu kiasi.Tuangalie Mfano 33 katika Kinomaande hapa chini.

    Mfano: 33

    Kinomaande:

  • 31

    a) Wakati uliopita kitambo

    tↄ- a-sↄsↄmb-ák-a (siku nyingi)

    ‘ulificha’

    b) Wakati uliopita kitambo kiasi

    nↄ-a-nↄ námb-ak-a ( zamani jana)

    ‘ulificha’

    c) Wakati uliopita wa karibu

    e- ’á-meta’g-ák-a (mapema leo)

    ‘nilizungumza’

    d) Wakati uliopita wa karibu kiasi

    e) tↄ-ma-sↄ lↄgↄk-ↄ (saa chache zilizopita)

    ‘tulikuita’

    Mofu njeo za wakati uliopita, lugha za kibantu zenye viwango vitatu ambavyo ni:

    wakati uliopita kitambo, wakati uliopita kitambo kiasi na wakati uliopita wa

    karibu.Tuangalie Mfano 34 katika Kipimbwe hapa chini.

    Mfano: 34

    Kipimbwe:

    a) Wakati uliopita kitambo

    tw-á-lí tu-g´ud-ile

    ‘tulinunua’

    b) Wakati uliopita kitambo kiasi

    (tw-á-lí) tu-ká-gud-íle

  • 32

    ‘tulinunua’

    c) wakati uliopita wa karibu kiasi

    (tw-a-ti) tu-gud-ile

    ‘tulinunua’

    Mofu njeo wakati uliopita, lugha za kibantu zenye viwango viwili ambavyo ni:

    wakati uliopita kitambo na wakati uliopita karibu.Tuangalie Mfano 35 katika lugha

    ya Kikundi hapa chini.

    Mfano: 35

    Kikundi

    a) fu-dza-gula

    ‘tulinunua’ (wakati uliopita jana na kuendelea)

    b) f-á-gula

    ‘tulinunua’ (wakati uliopita leo baada wa muda wa mazungumzo)

    Nurse (ameshatajwa) anasema katika Kiswahili mofu njeo –li- na –ta- zinaonesha

    wakati uliokamilika lakini wakati uliopo mofu –na- hauna wakati asili bali

    hutegemea mofu njeo iliyo katika maneno. Wakati uliopo katika lugha nyingi za

    Kibantu hazina mofu za kipekee zinazoonesha wakati uliopo. Tuangalie Mfano 36

    katika Kiduala hapa chini ambayo inawakilisha lugha zingine. Katika Kiduala wakati

    uliopo unaelezwa kwa kutofautisha mofu njeo zinazowekwa kwenye vitenzi ila ni

    wakati uliopo.

  • 33

    Mfano: 36

    Kiduala

    i) na-ma-bol-a ‘ni-na-to-a’

    ii) na-ø-bol-a ‘ni-na-to-a’ (rudia kutoa)

    iii) ná-ø-bol-a ‘ni-na-to-a’ (rudia kila siku kutoa)

    iv) na-ό-bol-a ‘ni-na-to-a’ (kutoa muda huo huo)

    Wakati ujao katika lugha za Kibantu zifuatazo ni mofu njeo zinazotumika ambazo ni:

    -ngá-,-ka-,-aku-,-la-,-laa-, -ra-,-ri-,- dzá-, - ci-...-e, -e-

    Katika Mfano 37 hapa chini ni baadhi ya lugha za Kibantu zilizotumia hizo mofu

    njeo.

    Mfano: 37

    Kiswahili: wa-ta-zungumza

    Kilucazi: tu-ka-ímb-a ‘ataimba’

    Kimbundu: tu-ka-land-a ‘tutanunua’

    Kikele: tó-la-kol-aka ‘tutafanya kazi

    Kiruri: ci-laa-gul-e ‘tutanunua’

    Kichewa: a-dzá-fik-a ‘atakuja’

    Kimwera: ci-tu-o-lim-e ‘tutalima’

    Kinyoro: tu-ra-gúr-a ‘tutanunua’

    Kinyoro: tu-ri-gúr-a ‘tutanunua’

    Kilamba: tw-aku-cit-a ‘tutafanya’

  • 34

    Katika wakati ujao pia lugha za kibantu zipo ambazo zina viwango vinne. Wakati

    wakati ujao kitambo, wakati ujao kitambo kiasi, wakati ujao wa karibu na wakati

    ujao wa karibu kiasi. Tuangalie mfano 38 lugha ya Kisena hapa chini.

    Mfano: 38

    Kisena:

    a) Wakati ujao kitambo

    ndi-na-ti ndi-dy-e

    ‘nitasema’ (wakati ujao wa kitambo)

    b) wakati ujao kitambo kiasi

    ndi-na-dya

    ‘nitakula’

    c) wakati ujao wa karibu

    ndi-sa-funa ku-dya

    ‘nitataka’

    d) wakati ujao kiasi

    ndi-na-dza ka-dya

    ‘nitakwenda kula’

    Katika lugha za Kibantu zipo zenye viwango vitatu vya wakati ujao ambavyo ni:

    wakati ujao kitambo, wakati ujao kitambo kiasi na wakati ujao wa karibu. Tuangalie

    Mfano 39 katika Kipimbwe hapa chini.

    Mfano: 39

    Kipimbwe:

  • 35

    a) Wakati ujao kitambo

    tu-lu-gul-ánga

    ‘tutanunua’ (mwezi ujao nakuendelea)

    b) Wakati ujao kitambo kiasi

    tu-lu-gul-á

    ‘tutanunua’ (kesho hadi mwezi ujao)

    c) Wakati ujao wa karibu

    tu-gud-ile

    ‘tutanunua’ (leo)

    Mofu njeo wakati ujao, lugha za kibantu zenye viwango viwili ambavyo ni: wakati

    ujao kitambo na wakati ujao wa karibu.Tuangalie Mfano 40 katika lugha ya

    Kimatumbi hapa chini.

    Mfano: 40

    Kimatumbi

    a) Wakati ujao Kitambo

    n-aa-lúwa-t´uumuka

    ‘nitaanguka’

    b) Wakati ujao wa karibu

    ni-luwa-t´uubuka

    ‘nitaanguka’

    Nurse (ameshatajwa) anasema mofu njeo za lugha za Kibantu hutokea kabla ya mzizi

    na nyingine baada ya mzizi katika kitenzi.

  • 36

    Tuangalie Mfano 41 hapa chini katika ya lugha ya Kipogolo na Kichiriku.

    Mfano: 41

    Kipogolo:

    tu- ø- hemer-iti

    nfs1wi-mofu kapa-mzz- njeopita

    ‘tulinunua’

    Kidchiriku:

    ngá- tu- ø- ping-a

    njeojao -nfs 1 wi - mofu kapa- mzz- ir.mw

    ‘tutarithi’

    Baadhi ya mofu njeo katika lugha za Kibantu hutokea kabla ya kitenzi na wakati huo

    huo hutokea baada ya mzizi.Tuangalie pia Mfano 41 katika lugha ya Kiyanzi na

    Kilunda hapa chini.

    Mfano: 42

    i) Kiyanzi (n´e)- e- s- í

    nfs2um njeopita-mzz-njeopita

    ‘uliweka’

    ii) Kilunda: hi- tu- ku-y-a

    njeojao-nfs1wi-njeojao-mzz-ir. Mw

    ‘tutaenda’

  • 37

    Mofu njeo huleta tofauti katika wakati kutokana na toni zinazojitokeza katika

    kitenzi.Tuangalie Mfano 43 katika lugha ya Kinyali, Kiewondo na Kiumbundu hapa

    chini.

    Mfano: 43

    i) Kinyali: k-á-kora ‘tulinunua’ wakati uliopita

    k-á-korá ‘tunanunua’ au ‘tutanunua’wakati uliopo au wakati ujao.

    ii) Kiewondo: ma-á-dí ‘nilikula’ wakati uliopita

    m-a-dí ‘ninakula’ wakati uliopo

    iii) Kiumbundu: tw-a-land-éle ‘tulinunua’ wakati uliopita siku nyingi

    tw-a-land-á ‘tulinunua’ wakati uliopita hivi karibuni

    Nurse (ameshatajwa) kazi hii inaonyesha mchango katika utafiti huu, kwani kuna

    lugha za kibantu ambazo mofu njeo hutokea kabla ya mzizi na zipo zinazotokea

    baada ya mzizi.

    Athari inayoonekana katika lugha hizi ni kuwa, mofu njeo –á- ya wakati uliopita

    katika lugha ya Kinyali hutumika pia wakati ujao katika lugha hiyo ya Kinyali, pia

    hutumika wakati uliopita katika lugha ya Kiewondo. Katika utafiti wa Nurse tunaona

    athari inayotokea ni kuwa toni zina athiri mofu njeo na kuleta maana nyingine katika

    kitenzi husika. Kwa mfano mofu njeo iliyo katika kitenzi ‘madi’ inakuwa “ma-á-dí

    ” ‘nilikula’ wakati uliopita inakuwa “ m-a-dí ” ninakula wakati uliopo.

    Mofu njeo –na- wakati uliopo lugha ya Kiswahili hutumika katika lugha ya Kisena

    katika wakati ujao.

  • 38

    Wesana-Chomi (2001, 2003) na amesema wakati ni sifa ya kitenzi ambayo huonesha

    wakati wa kufanyika kwa tendo au jambo. Anasema kuwa Kiswahili kina nyakati

    tatu na kila moja inaoneshwa kwa viambishi awali katika vitenzi. Katika kazi yake

    ameonesha mofu njeo 7 na mofu hali 5. Kwa mujibu wa Wesana – Chomi

    (ameshatajwa) wakati uliopo una mofu njeo 1 ambayo ni: {-na-}, wakati uliopita una

    mofu njeo 4 ambazo ni: {-me-},{-li-},{-ka-} na {-ku-} na wakati ujao una mofu njeo

    2 ambazo ni: {-ta-} na {-taka-}. Tuangalie Mfano 44 hapa chini.

    Mfano: 44

    Kiambishi Wakati Mifano

    -na- wakati uliopo anasoma, anapika

    -ta- wakati ujao atasoma, atapika

    -taka- wakati ujao katika vitenzi rejeshi nitakaporudi

    -me- wakati uliopita muda mfupi amepika, ameoga

    -li- wakati uliopita muda mrefu alikwenda sokoni

    -ka- wakati uliopita katika mfululizo wa matendo nikanunua samaki nikarudi

    Nyumbani nikapika,

    nikala halafu

    nikapumzika.

    -ku- wakati uliopita katika vitenzi kanushi hakusoma, sikusoma

    Katika uainishaji huu wa Wesana – chomi una kasoro zifuatazo: Kwanza,

    kuunganisha mofu njeo {-ta-} pamoja na mofu rejeshi {-ka-}na kuisema ni mofu nje

    ya wakati ujao

  • 39

    {-taka-} kawaida mofu njeo hutokea moja tu katika kitenzi cha Kiswahili. Katika

    neno hili –taka- si mofu njeo bali ni kidahizo. Pili, uainishaji mofu hali {-me-} kuwa

    ni mofu njeo ya wakati uliopita siyo sahihi. Katika mfano wake wa mofu hali

    hauoneshi tofauti ya wakati uliopita na hali timilifu. Katika kazi yake ametoa mfano

    ufuatao: ‘mama amefua nguo’ kwa mujibu wa Wesana- Chomi hii ni mofu hali

    lakini amepika au ameoga anasema ni mofu njeo ya wakati uliopita. Tatu, mofu {-ka-

    } hutumika katika usimulizi wa matukio yanayojitokeza kwa kufuatana hii siyo mofu

    njeo ya wakati uliopita.

    Kwa hiyo, katika utafiti huu tutaeleza zaidi katika sura ya nne juu ya mofu njeo

    (tazama 4.3.2).

    Kutokana na kazi hizi tangulizi mtafiti alikuwa na shauku ya kufanya utafiti katika

    kipengele cha mofu njeo peke yake maana wanaisimu hawazitofautishi na mofu

    hali.

    2.3 Pengo la Utafiti

    Kutokana na mapitio hayo mbalimbali mtafiti ameona kuwa, tafiti nyingi zimeelezea

    kuhusu mofu njeo na hali. Ulinganishi wao ulijikita katika mfumo wa mofu njeo na

    hali, mofu njeo na hali au kazi yoyote iliyofanywa ikihusisha mofu njeo za lugha za

    Kibantu. Katika tafiti hizi hakuna zilizoelezea kuhusu ulinganishi changanuzi wa

    mofu njeo za lugha za makundi tofauti ya Kibantu kama vile Kikara na Kiswahili.

    Hivyo basi, ni lengo la utafiti huu kufanya ulinganishi changanuzi wa mofu njeo za

    Kikara na Kiswahili.

  • 40

    2.4 Kiunzi cha Nadharia

    Katika sehemu hii ya kutalii kazi tangulizi, tutajikita katika kubainisha kiunzi cha

    nadharia ambayo tutaitumia tunapochunguza mofu njeo, aina zake na mazingira ya

    kutokea kwake. Kiunzi cha nadharia tutakayoizingatia ni nadharia ya ulalo ya

    Reichenbach.

    2.4.1 Nadharia ya ulalo ya Reichenbach

    Nadharia ya ulalo ya mahusiano ya nyakati katika lugha iliasisiwa na Reichenbach

    (1947) kushughulikia masuala ya nyakati katika lugha ya Kiingereza. Kwa mujibu

    wa nadharia hii nyakati katika lugha huelezwa kwa alama tatu muhimu: a) alama ya

    muda wa mazungumzo (amm), b) alama ya muda wa tukio (amt) na c) alama ya

    muda rejelewa (amr).

    Reichenbach (ameshatajwa) alionyesha tofauti zilizopo katika mofu njeo za lugha ya

    Kiingereza kwa kuangalia uhusiano unaokuwepo kati ya alama hizi tatu za wakati.

    Ameeleza kuwa uhusiano wa alama hizi unaweza kuwa wa usambamba au wa

    kufuatana. Amefafanua kuwa, si lazima alama rejelewa iwe wakati uliopo

    unaobainishwa katika sentensi au usemi fulani bali alama rejelewa huweza

    kubainishwa kwa kuangalia muktadha katika kubainisha muda wa tukio. Kwa mujibu

    wa Reichenbach, njeo huweza kubainishwa kwa kuangalia matini nzima. Hivyo,

    ameonyesha kuwa mahusiano ya nyakati si lazima yatazamwe katika kiwango cha

    sentensi bali huweza kutazamwa kwa kuzingatia matini nzima. Kwa maelezo haya

    inaonyesha kuwa si kila mara muda rejelewa ni wakati uliopo bali unaweza

    kubainishwa kwa kuzingatia maarifa waliyonayo wazungumzaji.

  • 41

    Pili, nadharia hii inahusisha maumbo ya njeo na maumbo mengine ya kisarufi

    ambayo yangeweza kuainishwa kama dhamira au hali. Mfano wa dhamira ni:

    ninaimb-a, imb-a, imb-eni, usiimb-e. Mfano wa hali ni: nimeimba, sijaimba,

    akanunua, akicheza.

    Smith (1978) aliboresha nadharia hii kwa kubadilisha alama rejelewa

    iliyopendekezwa na Reichenbach na kuwa muda rejelewa (mr) ambao ni muda

    mahususi wa tukio.Pia aliona ni vema kutumia neno tofauti za wakati badala ya

    alama za wakati pindi tunapozungumzia mahusiano ya nyakati katika lugha.

    Wakati unaweza kuwasilishwa katika sentensi kwa kufuata uhusiano wa kigezo

    bainifu cha ukweli ambao huendana na ulimwengu kwa kufuata aina tatu za wakati

    ambazo ni: wakati uliopo, kipindi cha muda fulani/ kati ya muda fulani (muda

    rejelewa wa mazungumzo) na muda ujao (Johnson (1977). Aidha, anaendelea

    kusema kuwa katika kutambulisha wakati mofu njeo ujitokeza katika njia tofauti kwa

    masharti ya kufasili sentensi ili ilete ukweli, unaofanya kazi ndani ya mfumo wa

    semantikia. Kwa hali hii, katika Kikuyu mofu njeo inajumuisha wakati uliopita: siku

    nyingi zilizopita, wakati uliopita (jana), mapema ndani ya siku ya

    mazungumzo.Wakati uliopo na wakati ujao: muda ujao saa chache baada ya muda

    wa mazungumzo na muda ujao mrefu kuanzia kesho na kuendelea.

    González (2003) anakubaliana na nadharia hii ya Reichenbach, mofu njeo huonesha

    wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Katika utafiti huu, mtafiti

    hakushughulikia mofu hali bali mofu njeo, hivyo, hakuendelea na mofu hali ya kama

    alivyotafiti González.

  • 42

    Utafiti huu unatumia nadharia ya ulalo katika kuchambua mofu njeo katika lugha ya

    Kikara na Kiswahili ili kujua mahusiano ya nyakati.Hata hivyo, mtafiti atatumia

    tofauti za wakati kama alivyopendekeza Smith (ameshatajwa) badala ya alama za

    wakati zilizotumiwa na Reichenbach.

    Kwa ujumla, nadharia hii imekuwa na manufaa sana katika utafiti huu kwa sababu

    inatuwezesha kuchunguza nafasi ya mofu njeo, kubaini tofauti ya idadi ya mofu njeo

    na mazingira yanayojitokeza baina ya lugha hizo mbili na hivyo kulinganisha mofu

    njeo za Kikara na za Kiswahili. Nadharia hii hudhihirisha upekee wa kila lugha na

    hutumika katika mofu njeo, tumechunguza lugha hizi mbili tukajua idadi, nafasi na

    mazingira mofu njeo zinapotokea.

    2.5 Hitimisho

    Sura hii ilipitia machapisho mbalimbali kuhusu mofu njeo ambayo yalitoa

    changamoto kwa mtafiti kuweza kufanya utafiti wa kiisimu kwa kulinganisha mofu

    za njeo za Kikara na za Kiswahili. Mapitio ya machapisho hayo yalionesha jinsi

    mofu njeo hutofautiana katika nafasi zinapotokea, idadi na mazingira zinapotokea.

    Sura inayofuata inaelezea mbinu za utafiti na nadharia ya utafiti

    iliyotumika.Nadharia na mbinu za utafiti zilisaidia katika uwasilishaji na uchambuzi

    wa data na kufikia hitimisho.

  • 43

    SURA YA TATU

    3.0 USANIFU NA MBINU ZA UTAFITI

    3.1 Utangulizi

    Sura hii inaeleza usanifu na mbinu za utafiti zilizotumika katika mchakato wa utafiti

    huu. Mbinu za utafiti zinajumuisha eneo la utafiti, sampuli na usampulishaji, mbinu

    za kukusanya data, aina ya data iliyokusanywa, zana za kukusanyia data na

    uchambuzi wa data.

    3.2 Usanifu wa Utafiti

    Usanifu wa utafiti ni mpango unaoonyesha jinsi utafiti utakavyofanywa katika

    kuchunguza tatizo la utafiti. Usanifu wa utafiti hueleza mbinu za utafiti

    zitakazotumiwa, namna data itakavyokusanywa, zana za utafiti za kukusanyia na

    uchambuzi wa data.Kothari (2004).

    Usanifu wa utafiti huonyesha jinsi ambavyo vipengele mbalimbali vya utafiti

    hujumuishwa pamoja. Kwa hivyo usanifu wa utafiti ni utaratibu wa kuchunguza

    tatizo kisayansi. Kwa mujibu wa Kombo na Tromp (2006) usanifu wa utafiti ni

    mpangilio wa taratibu zinazotumika kukusanya na kuchambua data kwa namna

    inayounganisha data zinazopatikana na malengo ya utafiti.

    3.3 Eneo la Utafiti

    Utafiti huu ulifanyika katika kata za Bukiko na Nyamanga, tarafa ya Ukara wilaya ya

    Ukerewe, mkoa wa Mwanza. Eneo hili liliteuliwa kwa sababu lina wasomi wenye

    umri mkubwa ambao wanafahamu Kikara na Kiswahili vizuri. Pia kata hizi

  • 44

    zilizingatiwa kwa kuwa Nyamanga ni sehemu ya makao makuu ya Kanisa Katoliki

    (parokia) waliosoma semenari ni wengi na Bukiko ni sehemu ambayo mtemi alikuwa

    akiishi.

    3.4 Mbinu za Utafiti

    Mbinu za utafiti zimefafanuliwa na Kothari (2004) kuwa, ni jumla ya mbinu

    zinazotumiwa katika kukusanyia data. Mbinu za kukusanyia data ni mbinu zile

    ambazo mtafiti huzitumia ili kupata taarifa za utafiti. Katika utafiti huu mtafiti

    alitumia mbinu ya usaili, na utumiaji wa dodoso katika kukusanya data.

    3.4.1 Usaili

    Mbinu hii inahusisha uwasilishaji wa maswali kwa watafitiwa.Maswali hayo

    yatajibiwa kwa mdomo wakati huohuo mtafiti atarekodi majibu hayo katika tepu ya

    kurekodia au ataandika katika daftari la kumbukumbu.Kwa mujibu wa Kothari

    (2004) na Mligo (2012) mbinu hii inamruhusu mtafiti kuuliza maswali ya nyongeza.

    Hatimaye husaidia kuweka bayana jambo ambalo halieleweki kwa watu

    wanaoulizwa maswali. Hivyo basi, katika utafiti huu usaili ulitumika ili kupata data

    ya mofu njeo za Kikara. Pamoja na hayo, katika mbinu hii mtafiti alitumia zaidi

    usaili maalumu ambao watafitiwa waliulizwa maswali ya msingi ya aina moja na

    yaliyo katika mpangilio ulio sawa. Mtafiti aliandaa maswali ambayo yalilenga

    kukusanya taarifa za aina moja kwa kila kundi la watafitiwa.

    3.4.2 Dodoso

    Kwa mujibu wa Kothari (2004) na Mligo (2012) dodoso ni mbinu ya utafiti ambayo

    mtafiti anaandaa maswali yake yanayolenga kupata taarifa kuhusu jambo

  • 45

    fulani.Katika utafiti huu mtafiti aliwapa watafitiwa dodoso yenye lugha ya Kikara na

    Kiswahili wanaoifahamu na kuielewa vizuri kwa usahihi. Dodoso hizi ziliandikwa

    vitenzi peke yake katika lugha ya Kiswahili na sentensi za Kiswahili peke yake ili

    ziandikwe katika lugha ya Kikara na sentensi za Kikara ziliandikwa kwa

    Kiswahili.Kwa kutumia mbinu hii ilisaidia katika kulinganisha data za mofu za njeo

    za Kikara na za Kiswahili.

    3.5 Aina ya Data Iliyokusanywa

    Data hupatikana kutokana na vyanzo mbalimbali kama inavyoelezwa hapa. Kothari

    (2004) na Mligo (2012) wanakubaliana kuwa, zipo aina kuu mbili za data ambazo ni

    data ya msingi na data ya upili.

    3.5.1 Data ya Msingi

    Data ya msingi ilikusanywa uwandani wakati mtafiti alipowahoji watafitiwa kuhusu

    mofu njeo za Kikara. Data hii ilikusanywa na mtafiti moja kwa moja kutoka kwenye

    eneo la utafiti.Kwa mujibu wa Mligo (2012:104) na, Kombo na Tromp (2006:100)

    data ya msingi ni taarifa ambazo hukusanywa moja kwa moja kutoka kwa watafitiwa

    Kothari (ameshatajwa:95) anafafanua zaidi kwa kusema kuwa data ya msingi ni data

    ambazo zinakusanywa kwa mara ya kwanza, ni halisi, na hutokea kuwa asilia. Data

    ya msingi ilikusanywa uwandani kisiwani Ukara na mtafiti moja kwa moja kutoka

    kwa watafitiwa ambao ndio wazungumzaji wa lugha hii kupitia mbinu za usaili na

    dodoso.

    3.5.2 Data ya Upili

    Data upili ni data ambazo tayari zimekusanywa na mtu mwingine na ambazo tayari

  • 46

    zimepitia mchakato wa kitakwimu Kothari (ameshatajwa: 95). Utafiti huu utatumia

    data ya msingi tu kwani hakuna data ya upili iliyopo ambayo mtafiti angeitumia.

    3.6 Sampuli na Usampulishaji

    3.6.1 Sampuli

    Mligo (2012:60) anasema sampuli ni kundi la watu ndani ya mkusanyiko mkubwa

    wenye uelewa unaofanana kuhusu tatizo analoshughulika nalo mtafiti. Kothari

    (2004) anasema kwamba sampuli humaanisha watu walioteuliwa kujibu maswali ya

    utafiti kutoka katika kundi husika.Uteuzi wa sampuli ni muhimu kwa sababu si rahisi

    kwa mtafiti kuwahoji watu wote wanaoishi eneo husika.

    3.6.2 Usampulishaji

    Ni mchakato wa kuchagua sampuli ya watoa habari kutoka katika kundi lengwa la

    utafiti. Katika mchakato huu mshiriki yeyote katika kundi lengwa anakuwa na fursa

    ya kuchaguliwa. Usampulishaji ni wa aina tatu: usampulishaji lengwa, usampulishaji

    makusudio na usampulishaji nasibu.

    3.6.3 Usampulishaji Lengwa

    Kwa mujibu wa Kothari (2004) kundi lengwa ni jumla ya watu wote ambao

    huhusishwa katika kazi ya utafiti.Walengwa waliohusishwa katika utafiti huu ni

    walimu, wazee, wasomi wa zamani wa shule za seminari na wananchi, kutoka katika

    kata hizo mbili za Bukiko na Nyamanga ambazo zipo katika tarafa ya Ukara wilaya

    ya Ukerewe mkoani Mwanza. Kundi hili watafitiwa katika utafiti huu liliteuliwa

  • 47

    kulingana na sifa na umuhimu wa kila kundi. Katika utafiti huu, walimu ambao wana

    uzoefu na maarifa katika lugha kutoka kata hizo walihusishwa. Hivyo basi, utafiti

    huu uliliona kundi hilo kuwa ndilo lenye uwezo wa kutoa data sahihi juu ya mofu

    njeo za Kikara kwa kuandika vitenzi walivyopewa kwenye dodoso.Pia kigezo cha

    wasomi waliosoma seminari kilimfanya mtafiti kuliona kundi hili kuwa ni rasilimali

    ya kutosha katika utoaji wa data. Wazee na wananchi waliteuliwa kwa sababu wao

    wana umilisi wa lugha zote mbili.

    3.6.4 Usampulishaji Nasibu

    Kwa mujibu wa Kothari (2004) usampulishaji nasibu ni mbinu ya kuchagua sampuli

    ambayo kila mshiriki katika kundi ana fursa sawa ya kuchaguliwa. Kwa maneno

    mengine usampulishaji nasibu na usampulishaji lengwa ni mbinu ya kuchagua

    sampuli ambayo huegemea zaidi uamuzi wa mtafiti na hauwezi kutoa matokeo

    jumuishi kuhusiana na kundi lengwa. Hii ina maana kuwa, ni mbinu ya kuchagua

    sampuli ambayo sehemu ya watafitiwa huchaguliwa kwa kuzingatia zaidi upatikanaji

    wao kuliko uwakilishi wao.

    3.6.5 Usampulishaji Makusudio

    Hii ni mbinu ya kuchagua sampuli ambayo mtafiti huichagua huku akiwa na

    matarajio kuwa itawakilisha kundi lengwa.

    Utafiti huu ulitumia usampulishaji usio nasibu kwa maana ya uteuzi wa kukusudia.

    Mtafiti aliamua kutumia aina hii ya sampuli katika utafiti wake kwa sababu aliamini

    kuwa kundi hili ndilo lenye uwezo wa kutoa taarifa sahihi katika kufikia malengo ya

    utafiti huu. Pia uteuzi wa sampuli kimaeneo ulizingatia maeneo ya kiutamaduni, na

  • 48

    kielimu katika tarafa ya Ukara. Maeneo haya yalichaguliwa kwa sababu ya wingi wa

    watu waliosoma shule.

    Sampuli ya utafiti ilikuwa na watafitiwa 45 ambao watafitiwa 10 miongoni mwao

    walikuwa walimu wazawa waliofundishwa Katekisimu ya Kikatoliki katika lugha ya

    Kikara na ambao walikuwa walimu wa shule za msingi na sekondari. Hawa

    waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji lengwa. Sampuli lengwa iliteuliwa kwa

    sababu wao wanajua lugha zote mbili kwa ufasaha.Watafitiwa 15 walikuwa ni wazee

    waliojifunza Katekisimu kwa lugha ya Kikara na ambao bado wanahudhuria katika

    ibada zao katika kata ya Bukiko na Nyamanga ambao waliteuliwa kwa kutumia

    usampulishaji nasibu. Watafitiwa 5 wenye umri kati ya miaka 60 hadi 69 waliosoma

    zamani katika shule za seminari waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji lengwa.

    Watafitiwa 15 walikuwa wananchi wanaozungumza Kikara na Kiswahili.

    3.7 Uchambuzi wa Data

    Baada ya kukamilika kwa mchakato wa ukusanyaji wa data, mtafiti alichambua data.

    Katika mchakato huu, data iliwasilishwa kwanza na halafu ilichambuliwa. Kothari

    (2004) anafafanua kuwa kuchambua data ni kitendo cha kuchanganua, kufupisha na

    kupangilia vizuri data zilizokusanywa kwa namna ambayo zitasaidia kujibu maswali

    ya utafiti husika.Uchambuzi wa data ni hatua muhimu katika kutafuta majibu ya

    tatizo la utafiti. Kwa msingi huu uchambuzi wa data utaongozwa na mbinu ya

    uchambuzi wa kimaelezo katika kuchambua data za utafiti huu. Mbinu hii ya

    kiuchambuzi, huruhusu utolewaji wa maelezo ya kina juu ya data zilizokusanywa na

    mtafiti kwa namna ambayo iliweza kukidhi na kujibu maswali ya utafiti husika.

  • 49

    Inafaa ieleweke kwamba, mtafiti anapozungumza kuhusu mbinu ya kimaelezo ana

    maana kwamba alichambua data kwa kuzitolea ufafanuzi wa kimaelezo usiohusisha

    kanuni zozote za kitakwimu. Data zilizokusanywa zilipangwa vizuri katika makundi

    mbalimbali yanayofanana ili kurahisisha uchambuzi wa data.Uchambuzi wa data

    ulifanywa kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti

    3.8 Ukusanyaji wa Data

    Data zilikusanywa katika jamii ya Wakara wanaoishi katika Kata za Bukiko na

    Nyamanga. Kata hizi zilizingatiwa kwa kuwa Nyamanga ni sehemu ya makao makuu

    ya Kanisa Katoliki (parokia) na Bukiko ni sehemu ambayo mtemi alikuwa akiishi na

    sehemu zote hizi zina watu wengi na wasomi. Kwa sababu hii zilimsaidia mtafiti

    kukusanya data kwa urahisi. Ukusanyaji wa data za utafiti huu ulifanyika katika

    sehemu ndogo sana katika tarafa ya Ukara. Usaili wa ana kwa ana ulihusika wakati

    wa kukusanya data ya msingi. Hii ni kwa sababu baadhi ya data za kiutendaji

    haziwezi kupatikana bila kukutana na watafitiwa ambao ndio wenye kutoa data

    toshelevu na za kina zilizohitajika. Mtafiti aliwapa watoa habari dodoso

    zilizoandikwa vitenzi 9 vya Kiswahili, sentensi 15 za Kiswahili ili watafsiri katika

    Kikara na sentensi 11 za Kikara ili watafsiri katika Kiswahili. Watafitiwa walishiriki

    vizuri kwa kujaza dodoso walizopewa na mtafiti.

    Mtafiti alinukuu kwenye daftari yale mambo yote muhimu yaliyomwezesha kufikia

    malengo ya utafiti.

  • 50

    3.9 Hitimisho

    Katika sura hii tumeeleza mbinu mbalimbali zilizotumika katika ukusanyaji wa data

    na namna ya uwasilishaji na uchambuzi wa data.Mbinu hizo ndizo zilizoongoza

    uchakataji wa data na kuweza kukamilisha kazi hii ya utafiti. Mbinu zilizojadiliwa

    katika sura hii zilisaidia katika uwasilishaji na uchambuzi wa data kama

    tutakavyoona katika sura ya nne. Sura inayofuata inaeleza uwasilishaji wa data za

    mofu njeo za Kikara na za Kiswahili.

  • 51

    SURA YA NNE

    4.0 UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA ZA MOFU NJEO ZA

    KIKARA NA ZA KISWAHILI

    4.1 Utangulizi

    Sura hii inawasilisha na kuchambua data zinazohusu mofu njeo za Kikara na za

    Kiswahili. Uwasilishaji na uchambuzi huu wa data umefanywa na kuongozwa na

    malengo na maswali ya utafiti. Data ziliwasilishwa kwa maelezo na kufafanuliwa

    kwa mifano ya mofu njeo husika. Katika mjadala huu tunawasilisha na kuchambua

    mofu njeo za Kikara na Kiswahili na kisha kuzilinganisha kwa mujibu wa malengo

    yetu ya utafiti. Kabla ya kuwasilisha data yafaa turejelee malengo ya utafiti huu

    ambayo ni:

    i) Kuchunguza nafasi ya mofu njeo katika kitenzi cha Kikara na cha Kiswahili ili

    kuona mazingira zinamotokea.

    ii) Kubaini idadi ya mofu njeo za Kikara na za Kiswahili ili kubaini iwapo ni sawa

    au la.

    iii) Kuonyesha mazingira ya mofu njeo na jinsi inavyoathiriwa na umbo la kitenzi

    ambamo mofu inatokea .

    iv) Kulinganisha mofu njeo za Kikara na Kiswahili ili kuona iwapo zinatokea katika

    nafasi ile ile au la.

    4.2 Uwasilishaji wa Data

    Katika uwasilishaji huu tutaanza kuangazia mofu njeo za Kikara na kisha mofu njeo

    za Kiswahili. Uwasilishaji na uchambuzi wa data utafanyika kwa kuzingatia lengo

  • 52

    kuu na malengo mahsusi ya utafiti wa mada hii pamoja na maswali ya utafiti

    yanayoambatana na hayo malengo. Tutaanza na lengo mahsusi la kwanza hadi la

    nne, halafu tutalinganisha mofu njeo za lugha hizi.

    4.2.1 Nafasi ya Mofu Njeo Katika Kitenzi cha Kikara

    Katika sura ya kwanza tulieleza kuwa mofu njeo ni umbo la kimofolojia ambalo

    hurejelea uhusiano kati ya muda wa mazungumzo na tukio katika lugha.Tulieleza pia

    kuwa mofu njeo katika lugha ni za aina tatu a) mofu njeo ya wakati uliopita, b) mofu

    njeo ya wakati uliopo, na c) mofu njeo ya wakati ujao.

    Mofu njeo katika Kikara hutofautishwa katika wakati uliopita, uliopo na ujao. Mofu

    njeo katika Kikara hugawanyika katika makundi mawili ambayo hujitokeza katika

    uyakinifu na ukanushi. Lugha ya Kikara ina mofu njeo za aina tatu pia ambazo ni: a)

    mofu njeo ya wakati uliopita, b) mofu njeo ya wakati uliopo, na c) mofu njeo ya

    wakati ujao. Katika sehemu inayofuata tunawasilisha mofu njeo za Kikara za wakati

    uliopita.

    4.2.1.1 Mofu Njeo ya Kikara Wakati Uliopita (Njeopita)

    Mofu njeo ya wakati uliopita ya vitenzi vya Kikara ni:{ -ile }na kibadala chake {-

    ele}, na {-ma-}na kibadala chake {-me-}. Uwepo wa mofu njeo mbili za wakati

    uliopita katika Kikara unamaanisha kuwa lugha hii ina viwango viwili vya wakati

    uliopita ambavyo huwakilishwa na mofu njeo (2) tofauti. Viwango hivi vya wakati

    uliopita ni: wakati uliopita kitambo na wakati uliopita wa karibu ambao kila moja

    huwakilishwa na mofu njeo mahsusi kwake, yaani mofu njeo wakati uliopita kitambo

  • 53

    na mofu njeo wakati uliopita wa karibu kwa mfuatano huo. Tuanze na mofu njeo

    wakati uliopita kitambo.

    (i) Mofu njeo wakati uliopita kitambo

    Wakati uliopita kitambo ni wakati unaoelezea matendo yaliyotendeka zaidi ya siku

    mbili kabla ya muda wa mazungumzo kama vile juma, mwezi, miezi na miaka

    iliyopita. Mofu njeo ya wakati uliopita kitambo katika vitenzi ina maumbo mawili:

    {-ile} na {-ele}

    Mfano: 1

    i) na- kam- ile

    nfs1um -mzz-njeopita

    ‘nilikama’

    ii) wa- sek- ele

    nfs 2 um- mzz- njeopita

    ‘ulicheka’

    iii) a- sing- ile

    nfs 3 um- mzz- njeopita

    ‘alishinda’

    iv) cha- mot- ele

    nfs1wi- mzz- njeopita

    ‘tulifua’

    v) mwa- suβ- ile

    nfs 2 wi- mzz- njeopita

    ‘mlirudi’

  • 54

    Mofu njeo ya wakati uliopita kitambo kama data ya Mfano: 1 juu inavyoonyesha ni

    {-ile} na {-ele}. Kwa kuzingatia mazingira ya kutokea mofu hizi, ni dhahiri kuwa

    mofu {-ile} na {-ele} ni mofu moja yenye maumbo tofauti kwani zote hutokea katika

    mazingira yale yale ya kitenzi. Tofauti za maumbo haya zinatokana na umbo la irabu

    iliyo katika mzizi wa kitenzi husika. Mofu njeo {-ele} huambatana na kitenzi chenye

    irabu /e/ au /o/ katika mzizi wake, na mofu njeo {-ile} hufuatana na kitenzi chenye

    irabu /a/, /i/ au /u/ kwenye mzizi wake. Mofu {-ile} ina mawanda mapana zaidi

    kuliko mofu {-ele} kwa hivyo tunaibainisha kama umbo la msingi. Kwa hali hii, {-

    ile} ndiyo mofu na {-ele} ni alomofu ya {-ile}

    (ii) Mofu njeo ya wakati uliopita wa karibu

    Wakati uliopita wa karibu ni wakati unaoelezea matendo yaliyotendeka siku moja

    kabla ya siku ya mazungumzo kama vile jana. Mofu njeo ya wakati uliopita wa

    karibu katika vitenzi ina maumbo mawili: