Upload
others
View
11
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
MIANYA YA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
i
MUHTASARI (EXECUTIVE SUMMARY)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya utafiti kwa lengo la kutoa
ushauri kwa Mamlaka zinazohusika juu ya namna bora ya kudhibiti vitendo vya rushwa katika
Chaguzi nchini. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: (i) Kubaini mianya ya rushwa katika
mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014; (ii) Kutathmini uelewa wa wananchi kuhusu
haki na wajibu wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa; (iii) Kuainisha vitendo vya rushwa
vilivyojitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014; na (iv) Kushauri namna ya kuziba
mianya ya rushwa itakayobainika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Utafiti huu ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kuhusisha jumla ya wahojiwa
1332. Aidha katika kila Wilaya, kata mbili zilichaguliwa na katika kila kata, ilichaguliwa
mitaa/vijiji viwili. Makundi ya wadau waliohojiwa ni: wananchi, wagombea na wasimamizi wa
uchaguzi. Aidha, taarifa za msingi za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya mahojiano/usaili na
kwa kuangalia matukio (Observation) ambapo madodoso na orodha ya ukaguzi (checklists)
zilitumika. Taarifa za upili zilikusanywa kwa kupitia nyaraka zilizohusu uchaguzi.
Matokeo ya utafiti huu kabla, wakati na baada ya uchaguzi ni kama ifuatavyo: Kabla ya
uchaguzi, baadhi ya wasimammizi wa uchaguzi hawakutoa orodha ya majina ya wapiga kura,
hawakuonesha mipaka ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji; baadhi ya wapiga kura kutotaka
kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, baadhi ya wagombea kutoidhinishwa na vyama
vyao vya siasa, kukosekana kwa barua za wadhamini na nyaraka za pingamizi za wagombea
ambao hawajaridhika na uendeshaji wa zoezi la uchaguzi. Aidha sababu za mapingamizi kwa
baadhi ya wagombea kutowekwa wazi (bayana), kampeni kufanyika zaidi ya muda
unaokubaliwa kisheria, chama kimoja kuingilia kampeni ya chama kingine cha siasa, uelewa
mdogo wa wapiga kura kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi pamoja na matumizi ya
lugha za matusi, kashfa na kejeli.
Aidha, utafiti unaonesha kuwa wakati wa zoezi la upigaji kura, baadhi ya wapiga kura
walisafirishwa toka eneo moja kwenda eneo lingine kinyume na taratibu, majina ya baadhi ya
wagombea kutooneka vituoni, kutokuwepo kwa eneo la faragha la kupigia kura, upungufu wa
vifaa zikiwemo karatasi za kupigia kura (ballot papers), kuendelea kwa kampeni hata wakati wa
kupiga kura, kutokufunguliwa kwa wakati vituo vya kupiga kura, picha za baadhi ya wagombea
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
ii
kuchanwa pamoja na kukosekana/kutokuwepo kwa mawakala kwa baadhi ya vyama vya siasa.
Vilevile, utafiti umebaini uwepo wa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
ambavyo ni ugawaji wa fedha taslimu, kanga, mashati, kofia, vinywaji na vyakula, mifuko ya
saruji na jezi za michezo, kwa lengo la kuwashawishi wapiga kura. Aidha baadhi ya vituo
vilichelewa kuhesabu na kutoa matokeo hali iliyo sababisha vurugu na fujo. Vitendo vya rushwa,
ukiukwaji wa Sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi huenda ni kati ya mambo yaliyosababisha
uchaguzi kurudiwa katika baadhi ya maeneo.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu mambo yafuatayo yanapendekezwa ili kuziba mianya ya
rushwa katika chaguzi zijazo: kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mpiga kura katika
mchakato mzima wa uchaguzi; Kuimarisha vyombo vinavyohusika na usimamizi wa Sheria na
taratibu za uchaguzi; vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
na Uchaguzi Mkuu vinapaswa kuzingatia maadili wanayokuwa wameyaridhia kwa pamoja kama
wadau maalumu wa kukuza demokrasia nchini; wasimamizi wa uchaguzi wanapaswa kutekeleza
wajibu wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi; na kujiepusha na itikadi za
kisiasa au vitendo vinavyoashiria upendeleo,rushwa au ushabiki wa kisiasa.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
iii
SHUKRANI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa shukrani zake za dhati kwa
wale wote walioshiriki katika kufanikisha Utafiti huu. Kwa kuwa si rahisi kuwataja wote
waliofanikisha utafiti huu, shukrani za pekee ziwaendee Wananchi, Wasimamizi wa Uchaguzi,
Mawakala na Waangalizi wa Uchaguzi kwa kushiriki kikamilifu katika utafiti huu.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
iv
YALIYOMO
MUHTASARI (EXECUTIVE SUMMARY) .................................................................................. i
SHUKRANI ................................................................................................................................... iii
YALIYOMO .................................................................................................................................. iv
ORODHA YA CHATI ................................................................................................................. vii
ORODHA YA VIFUPISHO .......................................................................................................... ix
SURA YA KWANZA .................................................................................................................... 1
1.0 UTANGULIZI ...................................................................................................................... 1
SURA YA PILI ............................................................................................................................... 3
2.0 MAPITIO YA MAKALA ..................................................................................................... 3
2.1 MUONGOZO WA UCHAGUZI WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA... 4
2.2 Rushwa katika Siasa ......................................................................................................... 7
2.3 Athari za Rushwa katika Uchaguzi .................................................................................. 9
SURA YA TATU ......................................................................................................................... 11
3.0 MBINU ZA UTAFITI .................................................................................................... 11
3.1 Maeneo na Muda wa Utafiti ....................................................................................... 11
3.2 Ukusanyaji wa Taarifa ..................................................................................................... 11
3.2.1 Taarifa za Msingi .......................................................................................................... 11
3.3 Upatikanaji wa Sampuli wakilishi. ............................................................................. 11
3.4 Ukubwa wa Sampluli.................................................................................................. 12
3.5 Uchambuzi na Unyambulisho wa Taarifa .................................................................. 12
SURA YA NNE ............................................................................................................................ 13
4.0 MATOKEO YA UTAFITI............................................................................................. 13
4.1 Wasifu wa Wahojiwa .................................................................................................. 13
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
v
4.2 Vitendo vya Rushwa Katika Michakato ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa .............. 14
4.3 Elimu kwa wapiga kura ................................................................................................... 34
SURA YA TANO ......................................................................................................................... 37
5.0 MAPENDEKEZO NA HITIMISHO ............................................................................. 37
5.1 Mapendekezo .............................................................................................................. 37
5.2 Hitimisho .................................................................................................................... 38
6.0 MAREJEO .............................................................................................................................. 39
6. VIAMBATANISHO ................................................................................................................. 40
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
vi
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali 1: Mchanganuo wa mwitikio wa wahojiwa kuhusu wasifu wao
Jedwali 2: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kujiandikisha na orodha ya wapiga kura
Jedwali 3: Mwitikio kuhusu kuwepo kwa barua za wadhamini na mapingamizi kwa wagombea
Jedwali 4: Taarifa kwa wadau kuhusu mapingamizi mbalimbali
Jedwali 5; Mapingamizi kwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika mikoa iliyojaza hojaji
Jedwali 6: Mwitikio wa Wahojiwa Kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa 2014.
Jedwali 7: Mwitikio wa Wahojiwa kuhusu uwepo Rushwa na aina zake katika Uchaguzi
Jedwali 8: Majina na Namaba Wapiga Kura Kuonekana Vituoni
Jedwali 9: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu mwenendo wa upigaji kura katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa 2014.
Jedwali 10: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu elimu ya uchaguzi na aina ya elimu waliyopata
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
vii
ORODHA YA CHATI
Chati 1: Nafasi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014
Chati 2: Majina na mipaka ya mitaa, vijiji na vitongoji siku 50 kabla ya uchaguzi
Chati 3: Wagombea kuidhinishwa na vyama vyenye usajili wa kudumu
Chati 4: Uwepo wa mapingamizi katika uteuzi wa wagombea
Chati 5: Taarifa za kuwafahamisha wapingaji kuhusu kupokelewa kwa mapingamizi
Chati 6: Taarifa za kuvifahamisha vyama vya siasa kuhusu uamuzi wa mamlaka za uteuzi
kuhusu mapingamizi yaliyopokelewa
Chati 7: Ushiriki katika mikutano ya kampeni
Chati 8: Kampeni kufanyika baada ya saa kumi na mbili jioni
Chati 9: Chama kuingilia kampeni ya chama kingine
Chati 10: Wananchi waliosafirishwa kwenda katika vijiji/ mitaa mingine kupiga kura
Chati 11: Uchaguzi kufanyika sehemu faragha
Chati 12: Karatasi zote za kupigia kura zilikuwa karatasi maalum
Chati 13 Vituo vyote vya kupigia kura vilikuwa na mawakala wa vyama vya siasa
Chati 14 Matokeo ya Wenyeviti wa vijiji kwa mikoa 14
Chati 15 Matokeo ya Wenyeviti wa Vitongoji kwa Mikoa 24
Chati 16: Kupata elimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa
Chati 17: Maoni ya wadau kuhusu kusuia vitendo vya rushwa na kuboresha chaguzi za
serikali za mitaa
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
viii
ORODHA YA PICHA
Picha 1: Baadhi yai wananchi wakihakiki uwepo wa majina yao kwa kutumia tochi za
simu
Picha 2: Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili ya kupiga kura
Picha 3: Wapiga kura katika kituo cha kupigia kura
Picha 4 Fomu ya kupiga kura
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
ix
ORODHA YA VIFUPISHO
ACT Alliance for Change and Transparency
CCM Chama cha Mapinduzi
CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHAUMA Chama Cha Ukombozi wa Umma
CUF Civic United Front
DP Democratic Party
NCCR-M National Convention for Construction and Reform- Mageuzi/Change
NEC National Election Commitee
NLD National League for Democracy
NRA National Reconstruction Alliance
PPT Progressive Party of Tanzania
TADEA Tanzania Democratic Alliance Party
TLP Tanzania Labour Party
TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
UDP United Democratic Party
UMD United for Multparty Democracy
UPDP United People’s Democratic Party
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
1
SURA YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo iliyopewa
dhamana kuzisimamia mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini. Sera mbalimbali zimekuwa
zikitekelezwa na TAMISEMI ikiwemo ile ya Ugatuaji wa Madaraka (Decentralization by
Devolution) kwa lengo la kuboresha mfumo wa Serikali za Mitaa. Ugatuaji huo wa majukumu
ukihusisha fedha, rasimali watu na vitendea kazi, kutoka Serikali Kuu kwenda Serikali za Mitaa
na kutoka Serikali za Mitaa kwenda ngazi za chini za utawala. Katika kutekeleza dhana ya
utawala bora, suala la usimamizi wa fedha kwenye mamlaka hizo lina umuhimu wa kipekee
kwani fedha za ruzuku za maendeleo zimekuwa zikipelekwa moja kwa moja kwenye
halmashauri hizo.
Serikali za Mitaa ndiyo mamlaka za wananchi ambazo kwa mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 mamlaka hizo huundwa, huendeshwa na
huwajibika kwa wananchi ambao ndiyo chimbuko la mamlaka yote katika nchi. Aidha, kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 146, Katiba inazitambua
Mamlaka ya Serikali za Mitaa kama vyombo vya haki vyenye mamlaka ya kuwashirikisha
wananchi kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma muhimu. Hizi
ndizo mamlaka za kiutawala zilizo karibu zaidi na wananchi. Hivyo basi mamlaka hizo ndizo
zilizopewa dhamana kikatiba katika kuhakikisha zinasimamia utoaji huduma za kijamii kama
vile ile ya elimu, maji, afya, kilimo, ufugaji na uvuvi, barabara, maliasili na utalii n.k. Aidha,
mamlaka hizo zipo kwa lengo la kukuza demokrasia kwa kuwashirikisha wananchi kuchagua
viongozi wao. Kwa mantiki hiyo ushiriki wa wananchi katika chaguzi za vyama vingi zilizo huru
na haki (kidemorkasia) ni nguzo muhimu ya kukuza utawala bora.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini ulifanyika tarehe 14 Desemba mwaka 2014, ukiwa ni
uchaguzi wa tano kufanyika chini ya mfumo wa vyama vingi kuwachagua viongozi wa Vijiji,
Vitongoji na Mitaa. Mamlaka za Serikali za Mitaa zilirejeshwa mwaka 1984 kwa sheria ya
Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya
Miji) sura ya 288 ambapo, uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi za Mitaa, Kijiji na Kitongoji
umekuwa unafanyika kila baada ya miaka minne. Uchaguzi huu ni muhimu kwani matokeo yake
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
2
yanaweza kusaidia kukuza demokrasia nchini kwa kuitambua mianya ya rushwa na kupendekeza
namna inavyoweza kuzibwa.
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, ambapo hadi sasa kuna vyama vya siasa 18 vyenye usajili wa
kudumu. Katika mfumo wa kidemokrasia, viongozi hupatikana kupitia uchaguzi ulio huru na
haki. Hata hivyo, zimekuwepo kasoro kadhaa katika uendeshaji na usimamizi wa chaguzi hizi.
Sababu mbalimbali zimekuwa zikitajwa zikiwemo zile za kunga’ang’ania kukaa madaraka,
ubinafsi, ukabila, urafiki, ujinga, umaskini na rushwa. Aghalabu, uwepo wa tuhuma za rushwa
katika uchaguzi huondoa imani ya wapiga kura, kutoaminiwa kwa serikali na hata kusababisha
machafuko.
Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kupambana na vitendo vya rushwa katika
uchaguzi kwa kutunga na kurekebisha sheria. Sheria hizo ni; Sheria ya Vyama vya Siasa namba
5 ya mwaka 1992, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007,
Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010; Sheria ya Uchaguzi, kwa kuondolewa
kwa kifungu cha takrima na kutungwa kwa Kanuni za uchaguzi za mwaka 2009 (mfano kanuni
namba 18) zinazozuia vitendo vya rushwa katika uchaguzi za Serikali za Mitaa. Kwa mujibu wa
Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa namba 4 ya mwaka 1979, uchaguzi wa Serikali za
Mitaa unasimamiwa na Halmashauri za Majiji/Manispaa/Miji/Wilaya chini ya usimamizi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Hata hivyo, pamoja na jitihada zote
hizo za Serikali katika kusimamia chaguzi mbalimbali nchini, vitendo vya rushwa vimeendelea
kuongezeka. Kwa sababu hiyo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
ilifanya utafiti kwa lengo la kubaini mianya ya rushwa katika uchaguzi na kisha kushauri njia
bora ya kudhibiti vitendo vya rushwa.
Aidha, madhumuni mahsusi ya utafiti huo yalikuwa kama ifuatavyo:
i) Kubaini mianya ya rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014;
ii) Kutathmini uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika uchaguzi wa Serikali
za Mitaa
iii) Kuainisha vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na;
iv) Kushauri namna ya kuziba mianya ya rushwa itakayobainika katika uchaguzi wa Serikali
za Mitaa.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
3
SURA YA PILI
2.0 MAPITIO YA MAKALA
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini husimamiwa na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa namba 4 ya mwaka 1979 sura namba 292 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
Pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo, uchaguzi za Serikali za Mitaa huendeshwa pia kwa
uzingatia kanuni zitokanazo na sheria za Serikali za Mitaa za mmlaka za miji sura ya 288 na
mamlaka za wilaya sura ya 287. Kanuni hizi zinatoa taratibu na masharti yanayotakiwa
kuzingatiwa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Aidha, tarehe 5/9/2014 Waziri mwenye
dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia Gazeti la Serikali
namba 320,321,322 na 323, alitoa tangazo la kufanyika kwa uchaguzi huo Decemba, 2014
ambapo Waziri husika alitangaza pia kanuni nne (4) zitakazotumika kusimamia uchaguzi huo:
Kanuni hizo ni pamoja na:
i) Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Mijii Midogo za
Mwaka, 2014, zilizotungwa chini ya kifungu cha 201A zinazotokana na sheria ya
Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) sura ya 287.
ii) Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na
Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za Mwaka, 2014 zilizotungwa chini
ya kifungu cha 87A zinazotokana na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura
ya 288.
iii) Kanuni za Uchaguzi za Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika
Mamlaka za Miji za Mwaka, 2014 zilizotungwa chini ya kifungu cha 87A zinazotokana
na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288.
iv) Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na
Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya Za Mwaka 2014, zilizotungwa
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
4
chini ya kifungu cha 201A zinazotokana na sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za
Wilaya) sura ya 287.
Tarehe 16 Oktoba, 2014 ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilitoa
mwongozo wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi za Vijiji, Vitongoji na Mitaa ambapo mambo
kadhaa yalitolewa ufafanuzi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi huo, kama inavyooneshwa
hapo chini.
2.1 MUONGOZO WA UCHAGUZI WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA
a) Kutangaza majina ya Vijiji, Vitongoji, Mitaa na Mipaka ya maeneo yake
Taratibu za uchaguzi zinaelekeza wazi kuwa kila Msimamizi wa Uchaguzi alitakiwa kutangaza
majina ya maeneo na mipaka ya kila Mtaa, Kitongoji au Kijiji kwa wakazi wa maeneo yake
katika muda wa siku 50 kabla ya siku ya uchaguzi ili kuwawezesha wakazi wa maeneo hayo
kuyatambua na kufahamu wanaowajibika kupiga kura.
b) Ratiba ya Shughuli za Uchaguzi
Kila Msimamizi wa Uchaguzi/ Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ahakikishe kuwa shughuli zote
za Uchaguzi zinaanza na kukamilika katika muda uliowekwa katika Kanuni, kuzingatia ratiba,
kutoa elimu kwa umma kuhusu uchaguzi na kufahamu idadi ya Vijiji, Vitongoji au Mitaa
itakayohusika kufanya uchaguzi na kufahamu idadi ya wakazi ili iweze kupeleka idadi sawa ya
karatasi zinazohitajika kwenye upigaji kura.
c) Kutoa maelezo kuhusu Uchaguzi
Wasimamizi wa uchaguzi watatoa maelekezo kuhusu Uchaguzi siku 28 kabla ya siku ya
uchaguzi yaani tarehe 16 Novemba, 2014. Maelezo hayo yataeleza masuala ambayo ni tarehe ya
uchaguzi, mahali na muda uchaguzi utafanyika, zoezi la ujiandikishaji, nafasi za
zinazogombewa, tarehe, muda na mahali pa kuchukulia fomu na kurudisha, uteuzi wa
wagombea, muda wa kuwasilisha pingamizi na mikutano ya kampeni.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
5
d) Uteuzi wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi
Wasimamizi wa Uchaguzi watateua wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi kwa kila Mtaa,
Kitongoji na Kijiji kutoka miongoni mwa maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa na ni pamoja na
Afisa yoyote wa umma atayeteuliwa na msimamizi wa uchaguzi wakati wa uchaguzi kwa
kuzingatia sifa zifuatazo wasiwe na dhamana ya au uongozi wa chama chochote cha siasa, wawe
watumishi wa umma na waadilifu. Wasimamizi wasaidizi na maafisa wengine watapaswa
kuhudhuria semina za mafunzo kuhusu mwongozo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.
e) Uandikishaji wa Wapiga Kura
Msimamizi wa Uchaguzi atamteua Afisa wa Umma au mtu mwingine yoyote mwenye sifa na
uadilifu ambaye ataandikisha na kuandaa orodha ya wapiga kura. Uandikishaji utafanyika
kwenye maeneo husika kwa siku 21 kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa siku saba
kuanzia tarehe 23 hadi 29 Novemba, 2014. Uandikishaji utafanyika kwenye majengo ya umma
au sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa
vyama vya siasa kuanzia saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 10 jioni kwa kuwaorodhesha wakazi
wenye sifa tu. Vyama vya siasa vitaruhusiwa kuweka wawakilishi wao wakati wa uandikishaji
kwa gharama za chama husika, ambapo baada ya siku saba za uandikishaji wapiga kura
Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi atabandika orodha ya wapiga kura ili kutoa muda kwa
wananchi kukagua orodha ya wapiga kura. Pingamizi dhidi ya mtu kuandikishwa kuwa mpiga
kura litawasilishwa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ambaye atalitolea uamuzi na
kurekebisha orodha hiyo kwa muda wa siku 5 yaani kuanzia tarehe 6 Decemba hadi tarehe 10
Dcemba 2014. Orodha ya mwisho ya wapiga kuraa itabandikwa siku 3 kabla ya siku ya kupiga
kura yaani kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 13 Decemba, 2014
f) Kuchukua fomu za kugombea uongozi
Wasimamizi wa Uchaguzi wataandaa fomu za kutosha za kugombea nafasi zilizotajwa, fomu
hizo zitatolewa siku 27 kabla ya siku ya Uchaguzi na zoezi la kutoa fomu litafanyika kwa siku 7
yaani kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 22 Novemba, 2014. Fomu hizo zitatolewa bila masharti wala
malipo yoyote, nakala moja ya fomu hizo itabandikwa kwenye ubao wa matangazo ili mgombea
yoyote mwenye pingamizi aweze kujitokeza.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
6
g) Idadi ya wajumbe watakaochaguliwa
(i) Mwenyekiti wa Kijiji/ Mtaa
(ii) Wenyeviti wa Vitongoji walio katika eneo la kijiji
(iii) Wajumbe wa viti maalumu wanawake
(iv)Wajumbe mchanganyiko wanawake na wanaume
h) Uteuzi wa Wagombea
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za uongozi ngazi
zote siku zisizopungua 20 kabla ya tarehe ya uchaguzi yaani tarehe 24 Novemba, 2014 na
mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa ni saa 10 jioni siku ya uteuzi ya uteuzi
i) Kamati ya Rufaa
Makatibu Tawala wa Mikoa watateua wajumbe wa Kamati za Rufaa siku 7 kabla ya siku ya
uteuzi yaani tarehe 17 Novemba 2014. Wajumbe wa kamati hiyo utamuhusisha Katibu Tawala
wa Wilaya au afisa mwingine wa umma atakayeteuliwa ambaye atakuwa mwenyekiti, afisa
yoyote kutoka taasisi ya umma iliyoko katika wilaya husika ambaye atakuwa mjumbe na afisa
yoyote wa umma anayefanyakazi katika ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ambaye atakuwa
Katibu.
Mgombea au Mwakilishi wake ambaye hataridhika na uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi kuhusu uteuzi atakuwa na haki ya kukata rufaa kwenye kamati ya ?Rufaa katika muda
usiozidi siku 4 kuanzia tarehe ya uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi. Kamati ya
Rufaa itasikiliza na kutoa uamuzi kuhusu uteuzi wa mgombea katika muda usiozidi siku 4 tangu
siku ya kupokea rufaa yaani kuanzia tarehe 26 Novemba hadi tarehe 29 Novemba, 2014
j) Kampeni za Uchaguzi
Kampeni za uchaguzi zitafanyika siku kumi na nne za mwisho na zitamalizika siku moja kabla
ya siku ya uchaguzi, kampeni zitaanza 30 Novemba 2014 na kumalizika tarehe 13 Desemba
2014 ambapo wagombea wa nafasi za ngazi tofauti au mwakilishi wake au chama cha siasa
kinaweza kuitisha mikutano ya kampeni kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi kwa kufuata ratiba
iliyowasilishwa na mgombea, mwakilishi wake au chama cha siasana kuratibiwa na Msimamizi
wa Uchaguzi ambapo kampeni zitaanza saa 2 asubuhi na zitamalizika saa 10 jioni ya kila siku ya
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
7
kampeni. Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Jeshi la Polisi vitatumika katika kuhakikisha
kunakuwepo na usalama na utulivu katika mikutano ya kampeni na wakati wa uchaguzi. Vikundi
vya jadi, ushabiki vimepigwa marufuku kuwepo maeneo ya mikutano ya kampeni au ya
uchaguzi. Aidha, vikundi vya uhamasishaji pia vimepigwa marufuku kujihusisha na kazi ya
ulinzi wa amani au chimbuko la fujo kwenye mikutano hiyo.
k) Utaratibu wa kupiga kura
Kwa kutegemea hali na mazingira ya kila eneo muda wa kuitisha mkutano wa uchaguzi
umepangwa kuwa wakati wote kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni. Kutakuwepo na sanduku
maalumu la kupigia kura ambalo kabla ya uchaguzi litahakikiwa likiwa wazi kabla ya kufungwa
kwa lakiri na kuanza kwa zoezi la upigaji kura. Kabla ya Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi
hajampatia mpiga kura karatasi za kupigia kura, atajiridhisha kama jina la mpiga kura
liorodheshwa karika orodha ya wapiga kura na baada ya kuridhiks atamtaka mpiga kura
ajitambulishe kwa kutumia kitambulisho kinachotambuliwa. Kura zitapigwa katika majengo ya
umma au sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ataiteua baada ya kushauriana na
wagombea, wawakilishi wao au vyama vya siasa isipokuwa majengo ya vyombo vya usalama,
taasisi za dini na vyama vya siasa.
l) Utaratibu wa kuwasilisha taarifa na matokeo ya uchaguzi
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika mitaa, vitongoji na vijiji watapeleka taarifa kwa
maafisa watendaji wa kata/ Vijiji kama idadi ya watu waliojiandikisha, idadi ya wakazi
waliojitokeza katika uchaguzi na majina ya wagombea walioshinda. Matokeo ya uchaguzi kwa
ngazi tofauti yatajazwa kwenye fomu maalumu ambayo itasainiwa na wagombea au wawakilishi
wao pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.
2.2 Rushwa katika Siasa
Haibishaniwi kuwa uwepo wa rushwa huweza kusababisha athari mbaya katika jamii katika
maeneo tofauti tofauti. Zipo tafiti zinazobainisha athari ya rushwa kwenye ukuwaji wa uchumi,
utulivu na biashara (Merton 1957; Leff 1964; Nye 1967; Huntington 1968; Mo 2001), Usawa
(Li, Xu, and Zou 2000, Gupta, Davood, and Alonso- Terme 2002) Uwekezaji (Mauro 1995; Wei
2000) Uaminifu kati ya mtu na mtu (Seligson 2002) na Imani ya wananchi juu ya demokrasia
(Phar na Putnam 2002).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
8
Mbali ya ukweli kwamba chaguzi ndiyo msingi mkuu wa demokrasia, michakato ya uchaguzi
imekuwa hatarini kwa vitendo vya rushwa na udanganyifu. Kwa kuwa chaguzi nyingi zimekuwa
zikifanyika mara kwa mara, kumejitokeza jitihada za siri za kuhakikisha chaguzi hizo
zinakumbwa na vitendo vya rushwa. Kote duniani rushwa inachangia katika kuondoa uhalali wa
kisiasa na mifumo ya kitaasisi (Rock; Sung 2004). Chaguzi zilizofanyika kwenye miji mikongwe
huko Athens na Sparta miaka mingi iliyopita (Staveley, 1972: chap 5) na pia katika miaka ya
hivi karibuni kote duniani inaonesha kuwa chaguzi hizo zilikumbwa na vitendo vya ununuzi wa
kura na udanganyifu (Posada- Carbo, 1996; 2000).
Rushwa ni neno kongwe katika historia ya maisha ya mwanadamu na limekuwa likipewa maana
tofauti katika nyakati mbalimbali za historia. Ipo tafasari inayoielezea rushwa kuwa ni matumizi
mabaya ya raslimali za umma kwa ajili ya kujipatia manufaa binafsi (Shleifer and Vishney
1993). Lipset na Lenz (2002, 112) kwamba rushwa ni kujipatia manufaa kwa kutumia gharama
ya umma na kwa Rose – Ackerman’s ametafasiri kuwa rushwa ni matumizi ya mabaya ya ofisi
kuhalalisha maslahi yanayotokana na mifumo yenye urasimu. Ipo tafasiri inayoielezea rushwa
kuwa ni tabia mchepuko toka ile ya utaratibu rasmi wa utendaji wa majukumu ya umma kwa ajili
ya manufaa binafsi, marafiki wa karibu au yale ya kikundi binafsi (Nye 1967: 420).
Herdenheimer et al (1989:10) ameeleza kwamba rushwa inatokea pale ambapo afisa mwenye
dhamana ya ofisi ya umma ameshawishika kwa kupokea fedha au manufaa mengine ili aweze
kuchukua hatua kukidhi dhamira ya mtoaji wa fedha au manufaa hayo na hivyo kuathiri maslahi
ya umma. Kwa Niccolo Machiavelli (1513) hii ilimaanisha kuporomoka kwa maadili na ile hali
ya kutokujali maslahi ya raia. Kwa Montesquieu (van Blerk, 1996) ilimaanisha kupotoshwa kwa
mfumo wa siasa bora na kuingia kwenye mfumo muovu. Kwake Jean- Jacque Rousseau (van
Blerk, 1996), hali hii ilitokea bila kuepukika kutokana na mapambano ya kugombea madaraka.
Kostadinova (2003) katika utafiti wake ameeleza kwamba kuvunjwa moyo kwa wananchi
kutokana na kukithiri kwa rushwa kunachangia wapiga kura kutojitokeza wakati wa zoezi la
upigaji kura.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
9
Birch, 2009, kwa wepesi wa uelewa, rushwa katika uchaguzi upo katika sura tatu, ambazo ni
hila katika sheria (manipulation of rules), hila katika orodha ya wapiga kura (manipulation of
voters) na ile ya hila katika zoezi la upigaji kura (manipulation of voting). Hila katika sheria
hujitokeza pale ambapo sheria/ kanuni zinazotawala/ kuongoza uchaguzi zinapokiukwa kwa
makusudi (distorted) ili kutoa upendeleo kwa chama kimoja au mgombea mfano kuzuia sehemu
idadi fulani ya watu wazima kushiriki katika zoezi la uchaguzi.
Hila katika wapiga kura (manipulation of voters); aina hii ya rushwa hubadili machaguo ya
wapiga kura (voters preferences) na juhudi kubwa kufanywa ili kubadili nia/ dhamira za wapiga
kura. Aina hii hufanywa kwa njia tofauti kama vile kukengeuka katika sheria za gharama za
uchaguzi, matumizi ya raslimali za umma, upendeleo katika matumizi ya vyombo vya habari,
ununuzi wa kura na vitisho kwa wapiga kura kwa manufaa ya chama kimoja au kwa mgombea.
Hila katika zoezi la upigaji kura (manipulation of voting); aina hii ya rushwa inahusisha
ucheleweshaji au upelekaji wa vifaa pungufu kwa kwenye vituo vya kupigia kura hasa maeneo
ambayo ni ngome ya upinzani na kukosekana kwa dhana ya uwazi katika taasisi zinazosimamia
uchaguzi.
Hivyo basi, sababu yoyote itakayochangia kutokea kwa uchaguzi mbovu, haiwezi kubishaniwa
kuwa zoezi la uchaguzi linapoharibika demokrasia na utawala bora huathirika kwa kiasi kikubwa
na huchukua muda mrefu kubadili hali hiyo.
2.3 Athari za Rushwa katika Uchaguzi
Rushwa huleta changamoto kubwa katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
Katika siasa, rushwa hudumaza demokrasia na utawala bora katika nchi uvunjifu na upindishaji
wa sheria au taratibu zilizowekwa. Rushwa katika siasa husababisha viongozi wanaowekwa
kutokuwa na uwajibikaji na kutokuwa na uwakilishi ufaao katika kufanya maamuzi (Wikipedia,
2010).
Aidha, athari nyingine za rushwa katika uchaguzi ni kuondoa uhuru wa mpiga kura, wagombea
wenye vipaji na uwezo wa kuwakilisha hushindwa kushiriki kugombea katika uchaguzi kwa
kukosa uwezo wa fedha, huharibu dhana nzima ya uwakilishi kwa kuwa wanaochaguliwa
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
10
hawana ridhaa kamili ya mpiga kura, viongozi waliochaguliwa kwa njia ya rushwa hawawezi
kusimamia mapambano dhidi ya rushwa wakiwa madarakani na usimamizi wa shughuli za
maendeleo hukwama kutokana na vitendo vya ubadhilifu wa rasilimali za umma. Rushwa katika
Uchaguzi inazuia wananchi kuwapigia kura viongozi wanaowataka na hivyo kupata viongozi
wabovu na kudidimiza demokrasia na kuzuia uchaguzi ulio huru na wa haki (NEC, 2010).
Mwaka 2010, Sheria ya Gharama za Uchaguzi Namba 6 ya mwaka 2010 ilipitishwa kwa lengo la
kutambua kisheria mchakato wa uchaguzi ndani ya vyama na kuusimamia kisheria, kuweka
utaratibu wa kisheria wa kudhibiti, kusimamia na kuratibu mapato na matumizi ya gharama za
kampeni kwa vyama vya siasa na wagombea katika uchaguzi, kudhibiti zawadi kutoka nje ya
nchi, kuweka utaratibu na mfumo wa uwajibikaji wa mapato na matumizi ya fedha za uchaguzi
kwa upande wa Vyama vya Siasa na wagombea. Sheria hii imeweka utaratibu wa kudhibiti
matumizi ya fedha wakati wa kampeni kwa kumtaka kila mgombea na kila chama
kitakachoshiriki katika chaguzi kutoa taarifa ya matumizi na vyanzo vya fedha inayotarajia
kutumika kama gharama ya uchaguzi.
2.4 Muhtasari wa Mapitio ya Nadharia (Summary of Literature Review)
Pamoja na kwamba zipo tafiti nyingi kuhusu Serikali za Mitaa, matokeo ya tafiti hizo
zinaonyesha kwamba rushwa bado ni tatizo sugu kwenye nchi zinazoendelea. Hata hivyo, tafiti
zinaonyesha nchi zinazoendelea na hasa nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara
ndizo zimeathirika zaidi kuliko nchi za Ulaya. Moja ya sababu kubwa ni tamaa ya kung’ang’ania
kukaa madarakani ili kujineemesha pamoja na kujilimbikizia mali. Hata hivyo ukubwa wa tatizo
unatofautiana kutoka nchi moja na nyingine. Kwa sababu hiyo, bado kuna haja ya kuendelea
kufanya tafiti kwenye eneo hili ili kukuza uelewa kwa lengo la kukuza Demokrasia.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
11
SURA YA TATU
3.0 MBINU ZA UTAFITI
3.1 Maeneo na Muda wa Utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika Mikoa ya Tanzania Bara ambapo mikoa 19 ilijaza hojaji. Utafiti
ulifanyika wakati wa kutangaza majina na mipaka ya vijiji na vitongoji, uteuzi wa wagombea,
kampeni za uchaguzi, uchaguzi na baada ya uchaguzi. Utafiti ulifanyika katika kipindi cha
kuanzia Novemba 2014 hadi Desemba 2014. Aidha, katika mikoa hiyo wilaya zote zilihusishwa
ambapo katika kila wilaya, zilichaguliwa kata mbili na katika kata hizo, vilichaguliwa vijiji
viwili au mitaa miwili.
3.2 Ukusanyaji wa Taarifa
Katika utafiti huu, taarifa za msingi na za taarifa za upili zilikusanywa.
3.2.1 Taarifa za Msingi
Taarifa za msingi zilikusanywa kwa kutumia mahojiano/usaili na kwa kuangalia matukio
(Observation). Mahojiano kwa njia ya usaili (interview schedual) pamoja na checklist orodha ya
ukaguzi (checklist).
3.2.2 Taarifa za Upili
Taarifa za upili zilikusanywa kwa kuchambua Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo
inayohusiana na chaguzi. Pia, kazi za watafiti kama machapisho, makala na majarida kuhusu
chaguzi za Serikali za Mitaa.
3.3 Upatikanaji wa Sampuli Wakilishi.
Wahojiwa katika utafiti huu walipatikana kwa kutumia njia/ mbinu zifuatazo:-
Sampuli kwa mpangilio/makusudi maalum (Non Random Sampling/Purposive
Sampling)
Njia hii ilitumika kuwapata walengwa kutokana na majukumu yao katika uchaguzi.
Walengwa waliohojiwa ni wagombea katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji/mitaa,
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
12
kitongoji, na mjumbe wa halmashauri ya Kijiji pamoja na wasimamizi na wasimamizi
wasaidizi wa uchaguzi.
Sampuli bila Mpangilio Maalum (Random Sampling)
Njia hii ilitumika kuwapata wahojiwa walio katika makundi makubwa. Wahojiwa
waliopatikana kwa njia hii ni wananchi katika wilaya, kata na vijiji/mitaa iliyotembelewa
kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara.
3.4 Ukubwa wa Sampuli
Ujazaji wa dodoso katika utafiti huu ulifanyika katika mikoa 19 kati ya mikoa 25 ya Tanzania
Bara iliyofanyiwa utafiti. Katika mikoa hiyo iliyojaza madodoso, utafiti ulifanyika katika Wilaya
69, kata 275 na vijiji/mitaa 402 ambapo jumla ya wadau 1332 walishiriki. Wadau walioshiriki ni
wasimamizi wa uchaguzi wilaya (84), wasimamizi wa Uchaguzi wasaidizi kata (155), wagombea
wa nafasi za mwenyekiti wa Mtaa/Kijiji (162), wagombea wa nafasi za mwenyekiti wa kitongoji
(190), wagombea wa nafasi za ujumbe katika Halmashauri za Kijiji/mtaa (242) na wananchi
(499).
3.5 Uchambuzi na Unyambulisho wa Taarifa
Taarifa zilizokusanywa kwa njia ya madodoso na orodha ya ukaguzi zilisafishwa (data cleaning),
kuchambuliwa (editing), kuwekewa alama (coding), na kunyambuliwa kwa kutumia programu
maalumu ya Statistical Package for Social Science (SPSS).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
13
SURA YA NNE
4.0 MATOKEO YA UTAFITI
Sura hii inatoa matokeo ya utafiti na uchambuzi ikihusisha wasifu wa waliojaza dodoso na
wahojiwa. Aidha, sura hii inachambua mianya ya rushwa katika mchakato mzima wa uchaguzi
wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na mwenendo wa kampeni katika uchaguzi na upigaji kura,
elimu na uelewa kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mapungufu katika uchaguzi na matukio
yaliyoathiri zoezi zima la uchaguzi kwa ujumla.
4.1 Wasifu wa Wahojiwa
Wasifu wa wahojiwa katika utafiti huu, unajumuisha mgawanyiko wao kwa umri, elimu
waliyofikia na jinsia. Utafiti huu ulilenga kufanya mahojiano na wananchi ambao kwa umri wao
wanastahili kutumia haki yao ya kupiga kura, yaani kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea.
Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa asilimia 71.0 ya wahojiwa walikuwa wanaume na
asilimia 29.0 walikuwa wanawake (Jedwali 1) ambapo wanaumme walikuwa wengi zaidi
kutokana na makundi ya wagombea na wasimamizi yaliyochaguliwa kwa utaratibu maalum
(Non random sampling). Aidha, wahojiwa walikuwa na umri wa miaka 18 hadi 35 walikuwa
asilimia 36.3 ambapo zaidi ya nusu (50.8%) ya wahojiwa walikuwa na umri wa miaka 36 hadi
55 na wachache (13%) walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 55. Kiwango cha elimu cha
wahojiwa kilitofautiana ambapo, asilimia 51.2 ya wahojiwa walikuwa na elimu ya msingi,
asilimia 33.0 walikuwa na elimu ya sekondari, asilimia 15.2 ya wahojiwa walikuwa na elimu ya
juu na asilimia 0.7 walieleza kuwa walikuwa hawajasoma.
Jedwali 1: Mchanganuo wa Mwitikio wa Wahojiwa kuhusu Wasifu Wao
Jinsi Elimu Umri
Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia
Wanaume 71.0 Msingi 51.2 Miaka 18 hadi 35 36.3
Wanawake
29.0
Sekondari 33.0 Miaka 36 hadi 55 50.8
Elimu ya juu 15.2 Zaidi ya miaka 55 13.0
Sijasoma 0.7
Jumla 100.0 100.0 100.0
Chanzo: Utafiti 2014
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
14
Matokeo haya yanaashiria kuwa wapiga kura wengi walikuwa wananchi wenye umri wa kati
ambapo kuna uwezekano kuwa, ufahamu wao na uzoefu katika kupiga kura ni mkubwa
ikizingatiwa kuwa ni kundi ambalo limeshiriki katika chaguzi nyingine zilizopita. Hata hivyo
kundi la wahojiwa lenye elimu ya msingi ni zaidi ya asilimia 50. Hali hiyo inaweza kuathiri
uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi hivyo elimu ya kutosha inapaswa kutolewa
kuhusu taratibu, haki na wajibu wa mpiga kura.
Mahojiano ya ujumla yalifanyika katika mikoa ya Tanzania Bara ambapo washiriki 1332
walijaza madodoso katika mikoa 19 ya Tanzania Bara. Katika ujazaji wa hojaji asilimia 6.3
walikuwa wasimamizi wa uchaguzi wilaya, asilimia 11.6 ulihusisha wasimamizi wasaidizi wa
uchaguzi kata, asilimia 12.2 ulihusisha wagombea katika nafasi za wenyeviti wa vijiji na mitaa,
asilimia 14.3 ulihusisha wagombea wa nafasi za wenyeviti wa vitongoji, asilimia 18.2 ulihusisha
wagombea wa nafasi za wajumbe wa halmashauri za vijiji na asilimia 37.5 ulihusisha wananchi
wapiga kura kama inavyochanganuliwa katika chati 1 hapa chini:
4.2 Vitendo vya Rushwa Katika Michakato ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Sehemu hii inatoa matokeo ya mianya na vitendo vya rushwa katika hatua mbalimbali za
uchaguzi Serikali za Mitaa. Hatua hizo ni pamoja na utangazaji wa majina na mipaka ya Mitaa,
Vijiji na Vitongoji, kujiandikisha na maandalizi ya orodha ya wapiga kura; uteuzi wa
wagombea katika nafasi mbalimbali, na kampeni za wagombea
4.2.1 Utangazaji wa Majina na Mipaka ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji
Kanuni ya 6 ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 inaelekeza kuwa wasimamizi wa uchaguzi
wanapaswa kutoa tangazo la majina na mipaka ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji siku 50 kabla ya
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
15
siku ya uchaguzi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa baadhi ya mamlaka hazikutangaza majina
na mipaka ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Aidha, utafiti ulibaini kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa na migogoro iliyohusiana na mipaka ya
mitaa. Migogoro hiyo ilisababishwa na baadhi ya wanasiasa waliosababisha kukinzana kwa
mipaka iliyotangazwa. Aidha, katika baadhi ya maeneo, baadhi ya Wabunge na Madiwani
walisababisha kukinzana huko, ili kupata wapiga kura wanaowalenga katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015. Wanasiasa hao walitumia uelewa mdogo wa wapiga kura kuhusu mipaka ya vijiji,
vitongoji na mitaa ili kupata wapiga kura wengi. Utafiti ulibaini pia katika baadhi ya maeneo
Viongozi wa Serikali walishirikiana na wanasiasa kuchochea migogoro hiyo. Kwa ujumla,
ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika zoezi la kutangaza majina na mipaka ya mitaa,
vitongoji na vijiji ni chanzo kikubwa cha migogoro katika baadhi ya maeneo.
4.2.2 Kujiandikisha na Orodha ya Wapiga Kura
Kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ni hatua muhimu katika uchaguzi. Hatua hiyo
inawawezesha wapiga kura kujiandikisha na hatimae kutumia haki yao ya kidemokrasia ya
kupiga kura. Mwananchi anaruhusiwa kupiga kura baada ya kuandikishwa na kuwa katika
orodha ya wapiga kura siku 21 kabla ya siku ya Uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni ya 8 na 9 ya
Kanuni za Uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za 2014.
Utafiti ulitaka kujua iwapo wahojiwa walijiandikisha kupiga kura kwenye daftari la wapiga
kura. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa asilimia 89.3 ya wananchi waliohojiwa,
walijiandikisha katika daftari la Wapiga Kura na asilimia 10.7 hawakuwa wamejiandikisha.
Aidha, matokeo yanaonyesha kuwa asilimia 94.5 ya wahojiwa walisema orodha ya wapiga kura
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
16
ilibandikwa mahali pa matangazo ambapo asilimia 3.4 wanasema hapana na asilimia 2.1 hawajui
(Jedwali 2). Asilimia 93.8 ya waliojaza hojaji wameonyesha kuwa maandalizi ya orodha ya
wapiga kura yalifanyika Novemba 2014, ambapo inaonyesha ni kipindi cha cha wiki tatu kabla
ya uchaguzi kama inavyoelekeza Kanuni ya 9 ya Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014.
Jedwali 2: Mwitikio wa Wahojiwa Kuhusu Kujiandikisha na Orodha ya Wapiga Kura
Kama wamejiandikisha Orodha ya wapiga kura kubandikwa mahali pa
matangazo
Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia
Ndiyo
Hapana
89.3
10.7
Ndiyo
Hapana
Sijui
94.5
3.4
2.1
Jumla 100.0 100.0
Chanzo: Utafiti 2014
Katika baadhi ya maeneo utafiti ulibaini orodha ya majina ya wapiga kura, ilikuwa na majina ya
watu wasio wakazi wa maeneo husika, majina mengine yalijirudia zaidi ya mara moja na majina
mengine, ilielezwa kuwa ni ya wakazi lakini walikuwa na umri chini ya miaka 18.
Kutokujiandikisha kupiga kura kunaashiria kuwa, huenda baadhi ya wananchi hawakuwa na
elimu ya kutosha kuhusu haki na wajibu wa mpiga kura. Elimu kwa wapiga kura inapaswa
kutolewa mapema, kabla mchakato wa uchaguzi haujaanza ili kuwachagua viongozi bora. Aidha,
kutojiandikisha huenda kumesababishwa pia na wananchi kutokuwa na ari ya kujiandikisha ili
wapige kura. Hali hiyo, inaweza kusababishwa na kutokutekelezwa kwa ahadi zinazotolewa na
baadhi ya viongozi baada ya kuchaguliwa. Aidha, ubandikaji wa orodha ya wapiga kura mahali
pa matangazo ni muhimu kwa kuwa uwazi huondoa mianya ya rushwa na malalamiko.Pia
wasimamizi wa uchaguzi wanapaswa na kuweka orodha ya wapiga kura kama inavyoelekezwa
kwenye kanuni na sheria za uchaguzi.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
17
4.2.3 Uteuzi wa Wagombea
Uteuzi wa wagombea ni msingi wa kupata wagombea wenye sifa na hatimaye kupata viongozi
bora. Aidha, kila mgombea anatakiwa kuteuliwa kutoka kwenye chama cha siasa chenye sifa ya
kushiriki uchaguzi. Asilimia 12 ya wahojiwa walieleza kuwa wagombea hawakuidhinishwa na
vyama vya siasa. Hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na uelewa mdogo wa taratibu za
uchaguzi na kukosekana kwa uwazi katika zoezi la uteuzi wa wagombea. Aidha, Utafiti ulibaini
kuwa usiri katika zoezi la uteuzi wa wagombea umesababisha malalamiko kutoka kwa baadhi ya
waombaji. Katika baadhi ya maeneo, taratibu za uteuzi wa wagombea umevigharimu baadhi ya
vyama vya siasa kutokana na wagombea kuvihama vyama hivyo wakipinga taratibu za uteuzi. Ni
vyema vyama vya siasa kuwa na taratibu na kanuni za uteuzi zitakazowawezesha kupata
wagombea bora na hatimae kuleta maendeleo kwa wapiga kura wao na taifa kwa ujumla (Chati
3).
Utafiti ulibaini ukiukwaji wa utaratibu katika baadhi ya maeneo ambapo barua za wadhamini na
nyaraka za mapingamizi hazikuonekana. Utafiti uliangalia uwepo wa mapingamizi kwa
wagombea na iwapo taratibu zilifuatwa katika kutoa na kushughulikia mapingamizi hayo. Katika
baadhi ya maeneo, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wagombea wa vyama vya
siasa walio wekewa mapingamizi na au kuenguliwa wakilalamikia ukiukwaji wa kanuni za
kuwekewa pingamizi. Katika baadhi ya maeneo, vyama vya siasa havikuweka wagombea na
hivyo kupunguza ushindani. Aidha vyama vingi havikupata viti katika baadhi ya maeneo
(Viambatanisho 1&2). Kwa ujumla, vyama vyote vya kisiasa ni muhimu kujijenga na
kujiimarisha kuanzia katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Hata hivyo, uteuzi makini wa wagombea
ni msingi wa kupata ushindi katika chaguz (Jedwali 3).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
18
Utafiti ulibaini kuwa baadhi ya wasimamizi hawakuwa wanatumia sheria na kanuni za uchaguzi
kutoa maamuzi, badala yake walitumia mamlaka waliyo nayo kutoa maamuzi yaliyokuwa na
msingi upendeleo na rushwa.
Jedwali 3: Mwitikio kuhusu kuwepo kwa barua za wadhamini na mapingamizi kwa wagombea
Zilipati
kana
Hazikup
atikana
Zilithib
itishwa
Hazikuthibiti
shwa
Barua za udhamini za
wagombea wenyeviti
wa vijiji/mitaa
87.4 12.6 Nyaraka za pingamizi
wagombea wenyeviti
wa vijiji/mitaa
63.4 36.8
Barua za udhamini za
wagombea wenyeviti
wa vitongoji
71.6 28.4 Nyaraka za ingamizi
wagombea wenyeviti
wa vitongoji
76.4 23.6
Barua za udhamini za
wagombea wajumbe
wa halmashauri
76.6 23.4 Nyaraka za ingamizi
wagombea nafasi za
ujumbe
81.7 18.3
Chanzo: Utafiti 2014
Aidha, asilimia 30.3 ya wahojiwa walieleza kuwepo kwa mapingamizi, asilimia 58.6 walieleza
kuwa hakukuwepo mapingamizi na asilimia 11 walikuwa hawajui kama mapingamizi
yalikuwepo kwa wagombea walioteuliwa na vyama vya siasa, (Chati 4).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
19
Kanuni ya 14 na 15 ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 zinatoa maelekezo kuhusu uteuzi wa
wagombea na endapo kuna mapingamizi. Katika baaadhi ya maeneo utafiti ulibaini kuwepo kwa
wagombea ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na hivyo kutoa mapingamizi kwa
wagombea.
Katika baadhi ya maeneo, utafiti ulibaini kuwa mapingamizi hayakufuata utaratibu wa
wagombea kujaza fomu za pingamizi za kuwataka Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kupitia
upya maamuzi yaliyokwishafanyika. Aidha, utafiti ulibaini matumizi ya nyaraka zisizo rasmi
kama barua na fomu za mapingamizi.
Ukiukwaji wa taratibu umesababisha kuwepo kwa malalamiko/mapingamizi mengi yasiyo ya
lazima kutoka kwa wagombea (Jedwali 4). Pia katika baadhi ya maeneo wasimamizi wasaidizi
walilalamikiwa kukiuka taratibu za mapingamizi ambapo waliandika barua za kuwaengua baadhi
ya wagombea kwa kutumia nafasi zao na si kwa mujibu wa kanuni na taratibu za uchaguzi.
Utafiti ulibaini kuwa ukiukwaji huo ulisababisha baadhi ya wananchi kuhisi upendeleo kwa
baadhi ya vyama na vitendo vya rushwa.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
20
Jedwali 4: Taarifa kwa Wadau kuhusu Mapingamizi
Taarifa kujulisha: Hazikupatikana
(%)
wapingaji kupokelewa kwa mapingamizi kwa wenyeviti wa Vijiji/Mitaa 14.2
wapingaji kupokelewa kwa mapingamizi kwa wenyeviti wa Vitongoji 6.8
wapingaji kupokelewa kwa mapingamizi kwa wagombea ujumbe wa
Halmashauri
1.4
Chanzo: Utafiti 2014
Katika baadhi ya maeneo utafiti ulibaini kuwa mamlaka za uteuzi hazikuvifahamisha vyama vya
siasa kuhusu maamuzi yaliyotolewa baada ya mapingamizi.Kwa mfano kuna maeneo ambayo
taarifa za pingamizi zilitolewa siku ya kupiga kura, tarehe 14 Desemba 2014, baada ya wapiga
kura kuhoji kutokuwepo kwa wagombea wao katika orodha ya wapiga kura na kuelezwa kuhusu
pingamizi. Aidha, baadhi ya maeneo, hayakuzitunza taarifa kuhusu mapingamizi ipasavyo. Hali
hii inaashiria upungufu wa uwazi, hivyo kuwa mwanya wa rushwa na chanzo cha malalamiko
katika maeneo hayo.
Kiasi cha mapingamizi kilitofautiana kati ya eneo moja na jingine hali inayoashiria tofauti ya
mwamko wa kisiasa, uelewa wa wadau wa kanuni na taratibu za uchaguzi na uzingativu wa
kanuni, sheria na taratibu za uchaguzi (Jedwali 5)
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
21
Jedwali 5; Mapingamizi kwa Wagombea wa Nafasi Mbalimbali Katika Mikoa Iliyojaza Dodoso
Chanzo: Utafiti 2014
Sababu mbalimbali zimetolewa kuhusiana na mapingamizi kwa wagombea. Sababu zilizotolewa
ni pamoja na baadhi ya wagombea kuwa na makosa ya jinai (2.9%), wagombea kutokuwa
wakazi wa maeneo wanayogombea (28.2%), utata wa umri (5.6%) na fomu zilijazwa bila
kufuata taratibu (23.8%). Sababu nyingine za mapingamizi ni wagombea kutoidhinishwa na
vyama vya siasa (10.6), kuchelewa kuwasilisha fomu (10.3), na uhasama wa kisiasa (2.6%).
Aidha, asilimia 16 ya wahojiwa walieleza kuwa mapingamizi mengine yalitokana na wagombea
MIKOA Mapingamizi katika uteuzi wa wagombea Jumla
Ndiyo Hapana Sijui Hakuna jibu
Arusha 30 54 7 4 95
Kilimanjaro 15 91 12 5 123
Ilala 3 3 0 0 6
Temeke 13 0 2 4 19
Morogoro 24 46 10 3 83
Dodoma 24 63 10 2 99
Geita 9 22 3 0 34
Njombe 16 42 7 4 69
Rukwa 16 38 12 4 70
Iringa 16 35 3 0 54
Mbeya 76 76 10 5 167
Katavi 10 22 0 0 32
Mtwara 21 36 3 5 65
Lindi 12 30 0 0 42
Ruvuma 3 7 4 3 17
Tabora 32 80 10 0 122
Tanga 7 12 2 0 21
Simiyu 45 57 3 0 105
JUMLA 404 780 105 43 1332
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
22
kutokurudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na au kughushi
nyaraka.
4.2.4 Kampeni katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014
(a) Muda wa kujinadi
Kanuni ya 18 ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 inaelekeza kampeni kufanyika siku kwa
14 kabla ya uchaguzi. Aidha, katika kipindi hicho cha kampeni vyama vyote vinatakiwa
kufanya kampeni kwa kufuata ratiba na taratibu zilizowekwa, na kwa kufuata makubaliano na
kanuni za maadili zilizosainiwa na vyama vya siasa vilivyosajiliwa. Utafiti ulipata maoni
mbalimbali ya wahojiwa walioshiriki katika kampeni kama inavyoonekana katika chati.
Utafiti uliangalia mwenendo wa wagombea katika kampeni za uchaguzi ambapo ulifuatiliwa ili
kubaini endapo kuna kampeni zilizoendelea zaidi ya saa kumi na mbili za jioni kama kanuni ya
18 ya Uchaguziwa Serikali za Mitaa 2014 inavyoelekeza. Katika baadhi ya maeneo kampeni
zilifanyika zaidi ya saa kumi na mbili za jioni.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
23
Mgombea, mwakilishi wake au chama cha siasa kinaweza kuitisha na kuhutubia mikutano ya
kampeni kwa kufuata ratiba itakayowasilishwa na wagombea, wawakilishi wao au vyama vya
siasa na kuratibiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Asilimia 10 ya wahojiwa walieleza kuwa
kampeni zilifanyika zaidi ya saa 12 jioni. Kufanyika kwa kampeni zaidi ya saa 12 za jioni
inaashiria uwepo wa vitendo vya rushwa na pia kuwa chimbuko la fujo na vurugu katika baadhi
ya maeneo.
(b) Mwenendo wa Kampeni
Katika kampeni za uchaguzi Mgombea, Mwakilishi wake au chama cha siasa hakiruhusiwi
kuendesha kampeni za Uchaguzi kwa kutumia rushwa, takrima, kashfa, lugha za matusi,
ubaguzi wa kijinsia, kidini na ukabila. Kwa ujumla, utafiti ulibaini kuwa ingawa vyama vya
siasa vilijitahidi kuzingatia kanuni za uchaguzi, baadhi ya vyama vya siasa vilikiuka kanuni za
uchaguzi na hivyo kusababisha kampeni za uchaguzi kuvurugika na hata kusababisha fujo.
Mathalani, asilimia 16.3 ya wahojiwa walieleza kuwa, chama kimoja cha siasa kiliingilia
kampeni za chama kingine kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
24
Aidha, utafiti ulibaini kuwa baadhi ya wagombea walijinadi kwa kutumia lugha za kejeli, matusi
na kashfa ili kuwashawishi wapiga kura. Pia asilimia 9.7 ya wahojiwa walieleza kuwa picha za
wagombea zilichanwa, asilimia 3.7 walieleza kuwa kulikuwa na kampeni katika makanisa na
misikiti na asilimia 12.6 walieleza kuwepo kwa fujo na vurugu katika kampeni (Jedwali 6).
Jedwali 6: Mwitikio wa Wahojiwa Kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa 2014.
Ka
mp
eni k
atik
a
misik
iti na
ma
ka
nisa
Uw
ep
o w
a v
uru
gu
na
fujo
ka
tika
ka
mp
eni
Ch
am
a k
uin
gilia
ka
mp
eni y
a ch
am
a
kin
gin
e
Ma
tum
izi ya
lug
ha
za
ka
shfa
Pich
a za
wa
go
mb
ea
zilicha
nw
a
Ndiyo (%) 6.1 25.6 18.3 35.4 9.7
Hapana (%) 85.4 70.7 78.0 62.2 74.5
Sijui (%) 8.5 3.7 3.7 2.4 5.2
Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0
Chanzo: Utafiti 2014
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
25
c) Vitendo vya Rushwa
Vitendo vya rushwa katika kampeni za uchaguzi hudumaza demokrasia na ni adui mkubwa wa
utawala bora. Ili kubaini vitendo vya rushwa wananchi walihojiwa iwapo walishuhudia vitendo
vya rushwa katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 ambapo, asilimia 54.2
walieleza kuwa hakukuwa na vitendo vya rushwa na asilimia 42.9 walieleza kuwepo kwa
vitendo vya rushwa asilimia. Aidha, asilimia 32.9 ya wahojiwa walieleza kuwa kulikuwa na
vitendo vya rushwa vilivyohusiana na ugawaji wa fedha taslimu, asilimia 9.8 walieleza kuwepo
kwa ugawaji wa kanga na Tshirt na asilimia 26.8 walieleza kuwa wapiga kura walipewa
vinywaji na vyakula (Jedwali 7).
Jedwali 7: Mwitikio wa Wahojiwa kuhusu uwepo Rushwa na aina zake katika Uchaguzi
Uwepo wa rushwa Aina za rushwa
Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia
Ndiyo 54.2 Kupewa fedha taslimu 32.9
Hapana 42.9 Kupewa vinywaji na vyakula 26.8
Sijui 2.9 Kanga na Tshirt 9.8
Vitendo Vingine
Jumla 100.0 *
Chanzo: Utafiti 2014
Vitendo vingine vya rushwa vilivyobainishwa katika mchakato wa kampeni za Serikali za Mitaa
ni vitendo vilivyohusisha ugawaji wa mifuko ya saruji, ugawaji wa mipira ya miguu, harambee
kanisani, kutoa pikipiki na michango katika misiba. Utafiti ulibaini pia kuwa, katika baadhi ya
maeneo vitendo vya rushwa vilijidhihirisha kwa ugawaji wa chumvi na vitu vingine vya thamani
siku ya kupiga kura. Ugawaji huu ulifanyika kwa kupelekwa majumbani kwa wapiga kura au
wakati wapiga kura wanaelekea vituoni kupiga kura. Katika matukio hayo, utafiti ulibaini kuwa
shughuli hizo ziligharamiwa na baadhi ya wagombea na katika baadhi ya maeneo, mawakala wa
wagombea walitumika.
Utafiti ulibaini kuwa katika baadhi ya maeneo Madiwani na Wabunge walishirikiana na baadhi
ya wagombea kuwahonga wapiga kura. Madiwani na wabunge hao, walishirikiana na baadhi ya
wagombea kwa matarajio kuwa watakaposhinda watawasaidia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
26
2015. Ili kupata viongozi bora katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa viongozi wa kisiasa hasa
madiwani na wabunge wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha maadili, kanuni na
sheria za uchaguzi zinazingatiwa. Aidha, elimu ya kutosha inapaswa kutolewa kwa wanasiasa
kuhusu wajibu wao katika kuhakikisha viongozi bora wanapatikana.
4.2.5 Upigaji wa kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014
Upigaji wa kura unapaswa kufanyika katika eneo ambalo mpiga kura alijiandikisha. Ni kinyume
cha utaratibu kupiga kura eneo ambalo mpiga kura hakuandikishwa. Matokeo ya utafiti
yanaonesha kuwa katika baadhi ya maeneo wananchi walisafirishwa kwenda kwenye maeneo
mengine kinyume na kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Utafiti ulibaini kuwa katika baadhi ya maeneo, majina ya wapiga kura hayakuonekana vituoni.
Aidha, katika baadhi ya vituo kulikuwa na majina ya wapiga kura wenye umri chini ya miaka 18
na katika baadhi ya vituo orodha ya majina ya wapiga kura ilikuwa na majina yalijirudia zaidi ya
mara moja (Jedwali 8).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
27
Chanzo: Utafiti 2014
Pia matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa kanuni na taratibu katika
baadhi ya maeneo ambapo upigaji wa kura uliofanyika baada ya muda wa kupiga kura kupita
(10.4%), kutokufunguliwa kwa vituo vya kupiga kura kwa wakati (19.4%) na kuendelea na
kampeni hata wakati wa zoezi la kupiga kura (13.3%).
Aidha, katika baadhi ya maeneo wananchi waliendelea kupiga kura usiku na hivyo kuwalazimu
kutumia simu zao zenye tochi ili kuwawezesha kusoma majina yao katika orodha ya wapiga kura
(Picha 1).
Jedwali 8: Majina na Namba za Wapiga Kura kuonekana Vituoni
Mkoa Ndiyo Hapana Sijui Hakuna
jibu
Jumla
Arusha 80 13 1 1 95
Kilimanjaro 87 20 10 6 123
Ilala 5 1 0 0 6
Temeke 12 6 0 1 19
Morogoro 57 13 2 11 83
Dodoma 79 14 1 5 99
Geita 22 5 5 2 34
Njombe 52 9 7 1 69
Rukwa 50 10 6 4 70
Iringa 39 10 5 0 54
Mbeya 124 27 10 6 167
Katavi 29 3 0 0 32
Mwanza 86 17 5 1 109
Mtwara 49 7 9 0 65
Lindi 40 1 1 0 42
Ruvuma 9 6 2 0 17
Tabora 84 25 10 3 122
Tanga 17 1 3 0 21
Simiyu 87 14 3 1 105
Jumla 1008 202 80 42 1332
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
28
Picha 1: Baadhi ya wananchi wakihakiki uwepo wa majina yao kwa kutumia tochi za simu
baada ya saa kumi na mbili jioni
Baadhi ya maeneo yaliendelea kupiga kura zaidi ya saa kumi na mbili za jioni kutokana na vituo
kuchelewa kufunguliwa, upungufu wa vifaa vya kupigia kura, maeneo ya kupigia kura kutokuwa
na nafasi na ubora unaowezesha zoezi la upigaji kura kwenda haraka, ufanisi mdogo kwa
wasimamizi wasaidizi na vurugu. Uwepo wa rasilimali za kutosha na zenye ufanisi ni muhimu ili
kuhakikisha upigaji kura unaanza na kukamilika kwa wakati ili chaguzi ziwe zenye amani na
utulivu. Aidha, mazingira mazuri ya upigaji kura yatatoa fursa kwa wananchi wengi kujitokeza
kupiga kura na hatimae kupata viongozi bora.
Picha 2: Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili kupiga kura
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
29
Aidha, 11.2% wamebainisha kuwa kuna picha za wagombea zilichanwa wakati wa upigaji kura
na baadhi ya vituo havikuwa na mawakala wa vyama vya siasa 13.5%. Matokeo yanaonesha pia
kuwepo kwa vurugu na fujo wakati wa kupiga kura (18.9%). Hali hii inaashiria ukiukwaji wa
sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ambapo vitendo vya rushwa vinaweza kuwa chimbuko la
hali hii. (Jedwali 9)
Katika baadhi ya maeneo utafiti ulibaini kuunganishwa vituo zaidi ya kimoja vya kupigia kura
hivyo kusababisha mlundikano, kukosekana kwa faragha na usiri wa kupiga kura, kama
tunavyoona kwenye picha hapa wapiga kura wawili tofauti wote wakipiga kura sehemu moja
kama inavyoonekana katika picha 3
Jedwali 9: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu mwenendo wa upigaji kura katika Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa 2014. Mw
itikio
Up
iga
ji wa
ku
ra b
aa
da
ya
mu
da
wa
ku
pig
a
ku
ra k
wish
a
Vitu
o v
ya
ku
pig
ia k
ura
ha
vik
ufu
ng
uliw
a k
wa
wa
ka
ti
Ka
mp
eni k
atik
a v
ituo
vy
a k
up
igia
ku
ra
Pich
a za
wa
go
mb
ea
zilicha
nw
a w
ak
ati w
a
up
iga
ji ku
ra
Uw
ep
o w
a v
uru
gu
na
fujo
wa
ka
ti wa
up
iga
ji
ku
ra
Ndiyo (%) 10.4 19.4 13.3 11.2 18.9
Hapana (%) 81.5 68.5 74.0 74.6 74.5
Sijui 5.0 8.4 9.5 10.0 3.4
Haihusiki (%) 3.1 3.6 3.2 4.2 3.2
Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0
Chanzo: Utafiti 2014
4.2.6 Masuala yaliyojiri wakati na baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Utafiti uliangalia kama uchaguzi ulifanyika mahali pa faragha na kwa kutumia karatasi maalum.
Matokeo yanaonesha kuwa katika baadhi ya maeneo upigaji kura haukufanyika katika mahali pa
faragha hali iliyowawezesha wapiga kura kujadili wakati wakiwa katika upigaji kura (picha 3)
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
30
Picha 3: Wapiga kura katika kituo cha kupigia kura
Ni muhimu sehemu ya kupigia kura kuwa sehemu ya faragha ili mpiga kura awe huru
kumchagua mgombea anayemtaka. Utafiti ulibaini kuwa baadhi ya maeneo hayakuwa na sehemu
ya faragha kwa ajili ya kupiga kura (28.60%) kama inavyoonekana katika Chati 11.
Kukosekana kwa faragha ni kuvunja Kanuni ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa 20 (10)
inayoelekeza kuwa kura zitakuwa za siri na zitapigwa katika majengo ya umma au sehemu
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
31
ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ataiteua baada ya kushauriana na wagombea au
wawakilishi wao au vyama vya siasa isipokuwa majengo ya serikali.
Kanuni ya 21 inabainisha kuwa karatasi za kupigia kura zilipaswa kuwa maalum zikiwa pamoja
na: Jina la Mgombea; Jina la Chama; Nembo ya Chama; na Nembo ya Halmashauri husika.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa katika baadhi ya maeneo karatasi za kura hazikuwa maalum
(6%). Matumizi ya karatasi maalum za kupigia kura huondoa malalamiko na migogoro. Aidha,
matumizi ya karatasi zisizo maalum huashiria uwepo wa mianya ya rushwa na matokeo yake ni
kuvuruga uchaguzi au matokeo ya uchaguzi husika kutiliwa shaka.
Utafiti umebaini kuwa katika baadhi ya maeneo karatasi za kupigia hazikuwa maalum na
nyingine zilikosewa kama inavyoonekana katika Picha 4 inayoonesha makosa katika fomu ya
kupigia kura ambapo jina la mgombea wa CCM linaonekana katika sehemu ya mgombea wa
CHADEMA na jina la mgombea wa CHADEMA kuonekana katika sehemu ya mgombea wa
CCM
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
32
Picha 4. Fomu ya kupigia Kura iliyokosewa Majina ya Wagombea.
Lengo la mawakala kuwepo kituoni ni kuhakikisha kuwa zoezi la kuchambua na kuhesabu kura
linaendeshwa kwa uwazi na haki. Matokeo yanaonesha vituo vingi vilikuwa na mawakala
ingawa kuna baadhi ya vituo havikuwa na mawakala wa vyama vya siasa (13.4%) kama
inavyooneshwa katika chati 13. Utafiti umebaini pia kwamba baadhi vyama ambavyo
havikushindanishwa katika baadhi ya maeneo, havikuweka havikujihusha kuona hali na
mwenendo wa uchaguzi katika maeneo hayo (Kiambatanisho 1)
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
33
4.2.7 Kuhesabu Kura na kutangaza Matokeo
Mchakato wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo ni muhimu ambapo taratibu na kanuni
zisipozingatiwa zinaweza kusababisha athari kubwa. Muda wa kuhesabu kura baada ya zoezi la
upigaji kura ni suala la kuzingatiwa ili kuleta ufanisi na tija. Utafiti ulibaini kuwa katika vituo
vya kupigia kura, kura zilihesabiwa kwa muda tofauti baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Utafiti ulibaini uwepo wa vurugu katika baadhi ya maeneo kutokana na ukiukwaji wa taratibu za
kuhesabu na utangazaji wa matokeo. Ukiukwaji huo ni pamoja na ucheleweshaji wa makusudi
katika kutangaza matokeo ya uchaguzi. Hali hiyo ilisababisha hisia za uchakachuaji wa matokeo
na hivyo kusababisha vurugu na fujo katika baadhi ya maeneo. Matokeo yanaonesha baadhi ya
vyama vya siasa havikufanya vyema katika uchaguzi huu (Kiambatanisho 1& 2). Kwa kuwa
Serikali za Mitaa ni msingi wa demokrasia na maendeleo, vyama vyote vyenye usajili wa
kudumu vinapaswa kujijenga kuanzia katika ngazi hiyo.
Serikali ya Mtaa ndiyo Serikali iliyo karibu zaidi na jamii. Matokeo yanaonesha kuwa baadhi ya
vyama vya siasa havikushindana na vingine kupata ushindi kidogo sana (Chati 15) . Ukiukwaji
wa kanuni na taratibu za uchaguzi na vitendo vya rushwa vinaweza kuwa sababu ya baadhi ya
vyama vya siasa kuacha kushindanisha wagombea au kupata viti vichache. Ili kujenga Serikali za
Mitaa zitakazoweza kuleta maendeleo yanayotarajiwa vyama vyote vya siasa vinapaswa
kujijenga kutoka katika ngazi za mitaa na hatimae kuwa na uwiano mzuri wa ushindi
unaojengwa na uchaguzi ulio huru na haki (Kiambatanisho 2).
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
34
4.3 Elimu kwa wapiga kura
Elimu kwa wapiga kura ndiyo msingi wa wapiga kura kufahamu sheria na kanuni za kupiga
kura; ikiwemo haki na wajibu wao katika uchaguzi. Utafiti ulitaka kufahamu iwapo wahojiwa
waliwahi kupatiwa elimu wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014. Matokeo
yanaonesha kuwa asilimia 66.1 ya wananchi waliohojiwa walieleza kuwa walipatiwa elimu na
asilimia 33.9 ya wahojiwa walieleza kuwa hawajawahi kupata elimu hiyo kama inavyooneshwa
katika Chati 16. Aidha, elimu ya kutosha kwa viongozi na wanasiasa ni muhimu ili waweze
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
35
Utafiti unaonesha kuwa elimu iliyotolewa ilihusu: kujiandisha katika daftari la wapiga kura
(65.9%); Sheria za Uchaguzi (58%); Sheria ya Gharama za Uchaguzi 27.7%); Haki ya Mpiga
Kura (64.3%) na Athari za Rushwa katika Uchaguzi 55%). Aidha, wahojiwa walieleza kuwa
walipata elimu kupitia vipindi vya radio (65%); vipindi vya televisheni (53.9%); magazeti
(50.5%); warsha na semina (43.1%); na vipeperushi na vijarida (42.1%) (Jedwali 10). .
Jedwali 9: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu elimu ya uchaguzi na aina ya elimu waliyopata
Kama wamepatiwa elimu Aina ya elimu waliyopata Njia iliyotumika kutoa
elimu
Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia Mwitikio Asilimia
Ndiyo 66.1 Kujiandikisha katika
daftari la wapiga
65.9 Radio 65.0
Hapana 31 Sheria za uchaguzi 58.0 Televisheni
(luninga)
53.9
Hakuna jibu 0.8 Gharama za uchaguzi 27.7 Magazeti 50.5
Haki ya mpiga kura 64.3 Warsha na
semina
43.1
Athari za rushwa
katika uchaguzi
55.7 Vipeperushi na
vijarida
42.1
Chanzo: Utafiti 2014
Asilimia theluthini na moja (31%) ya wahojiwa walieleza kuwa hawakupata elimu ya uchaguzi.
Kutokupata elimu ni chanzo kikubwa cha migogoro katika chaguzi hapa nchini. Aidha, uelewa
mdogo hukwamisha ushiriki mpana wa wananchi kwenye chaguzi hizo.
4.4 Maoni ya Wadau kuhusu mambo ya kufanya ili kuzuia rushwa na kuboresha uchaguzi
wa Serikali za Mitaa
Vitendo vya rushwa huathiri mchakato wa uchaguzi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa
rushwa bado ni tatizo. Vitendo hivyo ni kama vile kuwapa wapiga kura pesa, vyakula, vinywaji,
mavazi, ahadi za uongo, na vitisho. Aidha, vitendo vingine vinavyolalamikiwa ni wizi wa kura
na udanganyifu katika kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi. Ili kukabiliana na vitendo
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
36
vya rushwa katika uchaguzi, maoni yafuatayo yalitolewa ikiwa ni pamoja na: kuongeza bajeti ya
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (29%); kuboresha daftari la wapiga kura (0.4%); wananchi
wapewe elimu ya kutosha kuhusu taratibu za uchaguzi, haki na wajibu wa wapiga kura (17.5%);
kutoa adhabu kali kwa wanaojihusisha na vitendo vya rushwa (14.6%); polisi kusimamia
taratibu za uchaguzi kwa usawa na haki (19%) na Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa
Serikali za Mitaa (15.2%) (Chati 15)
Maoni mengine katika kuboresha mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni pamoja na
kuongeza maslahi ya wasimamizi wa uchaguzi, matokeo ya uchaguzi yatangazwe mapema
iwezekanavyo mara baada ya kumaliza kuhesabu kura ili kuepusha vurugu na kuondoa hisia za
udanganyifu. Aidha, uwazi na elimu ya mpiga kura ipewe kipaumbele ili kudumisha na kukuza
demokrasia nchini. Aidha,Vyama vya Siasa, Serikali na Asasi za Kiraia pamoja na Mashirika
yasiyo ya kiserikali, wote wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha elimu ya mpiga kura inatolewa
kwa utaratibu ulio endelevu.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
37
SURA YA TANO
5.0 MAPENDEKEZO NA HITIMISHO
5.1 Mapendekezo
NA. TATIZO MAPENDEKEZO
1. Uelewa mdogo wa
wananchi kuhusu haki na
wajibu wa mpiga kura
katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Elimu ya haki na wajibu wa mpiga kura itolewe kwa
wananchi.
Elimu ya rushwa, gharama za uchaguzi na uraia itolewe
katika ngazi zote za elimu nchini.
Serikali itenge bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuelimisha
wananchi.
Ushirikiano wa wadau wote katika kutoa elimu ya uraia
na mpiga kura kwa wananchi uimarishwe.
Kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zinazohusiana na
uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinapatikana kwa urahisi
na lugha inayoeleweka kwa wananchi.
Serikali iongeze fedha kwa ajili ya kuelimisha wananchi.
2. Usimamizi dhaifu wa
Sheria na taratibu za
uchaguzi wa Serikali za
Mitaa.
Kuviimalisha kielimu, kifedha na vifaa Taasisi na vyombo
vinavyohusika na usimamizi wa Sheria ya Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Kufanya tathmini ya uchaguzi na kuwachukulia hatua
watakaobanika kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi
huu.
Kuboresha usimamizi wa maadili ya uchaguzi.
Kuandaa/kuimarisha uwajibikaji wa wadau katika
kutekeleza taratibu za uchaguzi.
Serikali iongeze Maslahi ya wasimamizi wa uchaguzi.
3. Uzingativu mdogo wa
maadili. Kuimarisha na kusimamia utekelezwaji wa kanuni za
maadili(code of conducts) kwa vyama vya siasa,Taasisi na
vyombo vinavyohusika na usimamizi wa uchaguzi.
Kutoa elimu ya maadili kwa wadau wa uchaguzi.
Viongozi wa dini, kisiasa na Serikali wawe mfano katika
mapambano dhidi ya rushwa. (Uteuzi wa viongozi wa
kisiasa na Serikali uzingatie ushauri wa vyombo
vinavyohusika na maadili ambavyo ni
TAKUKURU,Usalama wa Taifa,Tume ya maadili ya
viongozi,tume ya haki za binadamu na Utawala Bora).
Kuongeza uwazi katika uteuzi wa wagombea ndani ya
vyama, wakati wa kuhesabu kura na kutoa matokeo ya
uchaguzi.
Kuwachukulia hatua wanaokiuka maadili.
.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
38
5.2 Hitimisho
Mapambano dhidi ya rushwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa yanahitaji mikakati
madhubuti ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa wa wananchi juu ya haki na wajibu wa mpiga
kura. Pia ni muhimu kuimarisha usimamizi wa Sheria na taratibu za uchaguzi wa Serikali za
Mitaa na Uzingativu wa maadili kwa wanasiasa na vyombo vyote vinavyohusika na uchaguzi
wa Serikali za Mitaa. Aidha, kuweka mikakati inayowabana wanasiasa wanaojihusisha na
vitendo vya rushwa na kuwajibika kwa matendo yao ni muhimu katika mapambano haya.
Endapo mikakati hiyo itaandaliwa na kutekelezwa na wadau, tatizo la rushwa katika uchaguzi
litapungua au kwisha kabisa.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
39
6.0 MAREJEO
Agenda Participation 2000 (2010): Elimu ya Uraia na Mpiga Kura Uchaguzi 2009-2010. Issue No.
009/10. Agenda Paricipation 2000. Dar es Salaam.
Blechinger, Venera (2002): Corr)uption and Political Parties. Sectoral Perspective on Corruption. MSI
and USAID, DCHA/DG. From www.usaid.gov .
Gymah-Baadi (2004): Remarks at the Ghana Integrity Initiative (GII) Symposium on Political
Corruption in Ghana, April 27, 2004. From www.cddghana.org visited on 12/09/2014.
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/773740-yaliyojiri-katika-uchaguzi-serikali-za-mitaa-dec-
14-2014-
Klitgaard, R (1988), Controlling Corruption. Berkeley. University of California Press.
Polisi (2010): Haki na Wajibu wa Mpiga Kura. Ulinzi Shirikishi katika Mchakato wa Uchaguzi. Dar es
Salaam.
Rose-Ackerman, S. (2001), Trust, Honesty, and Corruption: Theories and Survey Evidence from Post-
Socialist Societies, Toward a Research Agenda for a Project of the Collegium Budapest. Prepared
for the Workshop on Honesty and Trust in Post-Socialist Societies at Collegium Budapest, May
25-26, 2001. Draft of April 24, 2001. (Available for downloading at www.colbud.hu/honesty-
trust/rose/pub 01.pdf. Sept 12, 2014).
TAKURU & IDS (2002): Uchaguzi wa Vyama vingi na Rushwa katika Tanzania….
URT (1979): The Local Authorities (Elections) Act No.4, Dar Es Salaam.
URT (1982): The Urban Authorities Act, Dar Es Salaam.
URT (1985): The National Election Act No.1, Dar Es Salaam.
URT (2007): The Prevention and combating of Corruption Act No.11/2007, Dar Es Salaam.
URT (2010): The Election Expenses Act No.6, Dar Es Salaam.
Yerevan, A (2006): The concepts of Civic Education, Electoral Education and Voters Awareness.
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
40
6. VIAMBATANISHO
Kiambatanisho 1: Matokeo ya Wenyeviti wa Vijiji kwa Mikoa 14
MKOA IDA
DI Y
A V
ITI
VYAMA VILIVYOSHINDANISHWA
CC
M
CH
AD
EMA
CU
F
NC
CR
TLP
NLD
AC
T
UP
DP
UD
P
AP
PT
NR
A
CH
AU
MA
DP
TAD
EA
AD
C
UM
D
ARUSHA 399 326 73
DODOMA 570 509 27 33 1
GEITA 473 367 94 12
IRINGA 354 347 7
KAGERA 664 477 172 13 2
KATAVI 136 97 38 1
KIGOMA 304 206 47 6 38 4 1 1 1
K/NJARO 514 336 143 27 8
LINDI 520 358 15 146 1
MARA 487 333 149 2 2 1
MBEYA 843 701 140 2
MANYARA 440 344 95 1
MOROGORO 666 527 114 24 1
MTWARA 779 616 24 135 1 1 2
JUMLA 7149 5544 1138 375 71 10 2 5 2 0 0 1 0 1 0 0 0
Chanzo: Utafiti 2014
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
41
Kiambatanisho 2: Matokeo ya Wenyeviti wa Vitongoji kwa Mikoa 24
MKOA
IDA
DI
YA
VIT
I
VYAMA VILIVYOSHINDANISHWA
CC
M
CH
AD
EM
A
CU
F
NC
CR
TL
P
NL
D
AC
T
UP
DP
UD
P
AD
C
AP
PT
NR
A
NL
D
CH
AU
MA
DP
TA
DE
A
UM
D
ARUSHA 1462 1134 327 1
DODOMA 3317 2959 187 169 1 1
GEITA 2235 1682 512 41
IRINGA 1837 1765 72
KAGERA 3703 2574 1066 53 4 6
KATAVI 704 531 167 5 1
KIGOMA 1844 1286 282 36 185 47 1 3 1 3
K/NJARO 2249 1485 603 1 126 33 1
LINDI 2387 1676 83 624 3 1
MARA 2680 1827 808 17 15 7 1 3 2
MBEYA 4455 3596 835 17 1 4 2
MANYARA 2008 1599 397 6 6
MOROGORO 3415 2664 609 141 1
MTWARA 3416 2650 151 603 4 6 2
MWANZA 3437 2529 825 65 2 3 13
NJOMBE 1826 1688 133 1 4
PWANI 1995 1596 42 356 1
RUKWA 1842 1402 436 2 2
RUVUMA 3817 3442 169 206
SHINYANGA 2746 2154 552 35 1 1 3
SIMIYU 2639 1711 848 27 2 50 1
SINGIDA 2257 1830 389 36 1 1
TABORA 3565 2967 453 128 17
TANGA 4605 4422 81 102
JUMLA 64441 51169 10027 2671 354 58 2 72 0 69 6 3 3 0 2 4 1 0
Chanzo: Utafiti 2014
RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
42
Kiambatanisho 3: Matokeo ya Wenyeviti wa Mitaa kwa Mikoa 24
MKOA
IDA
DI
YA
VIT
I
VYAMA VILIVYOSHINDANISHWA
CC
M
CH
AD
EM
A
CU
F
NC
CR
TL
P
NL
D
AC
T
UP
DP
UD
P
AD
C
AP
PT
NR
A
NL
D
CH
AU
MA
DP
TA
DE
A
UM
D
ARUSHA 154 78 76
DSM 556 398 89 69
DODOMA 169 160 8 1
GEITA 60 24 36
IRINGA 222 156 65 1
KAGERA 66 35 29 2
KATAVI 42 34 8
KIGOMA 176 123 20 20 12 1
K/NJARO 60 29 31
LINDI 117 84 33
MARA 151 72 78 1
MBEYA 252 130 120 2
MANYARA 35 24 11
MOROGORO 294 256 33 5
MTWARA 180 104 25 45 5 1
MWANZA 345 202 136 7
NJOMBE 82 55 27
PWANI 73 62 10 1
RUKWA 166 65 101
RUVUMA 95 69 24 2
SHINYANGA 86 40 45 1
SIMIYU 92 48 40 2 2
SINGIDA 50 50
TABORA 148 97 20 29 1 1
TANGA 258 192 3 63
JUMLA 3929 2587 1035 260 30 1 0 12 0 3 0 0 0 0 0 0 0 1
Chanzo: Utafiti 2014