28
KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 www.pccb.go.tz Kamati ya Bunge yaipongeza TAKUKURU kuokoa sh. bilioni 8.6 Ndani Waziri Lukuvi afichua rushwa mradi wa mji mpya Kigamboni

ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa1

Toleo la Januari - Machi 2016

KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Jarida la Taasisi ya

ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016

www.pccb.go.tz

Kamati ya Bunge yaipongeza TAKUKURU kuokoa sh. bilioni 8.6

Ndani

Waziri Lukuvi afichua rushwa mradi wa mji mpya Kigamboni

Page 2: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa2

Toleo la Januari - Machi 2016

Ukiwa na taarifa / maoni juu ya mapambano dhidi ya rushwa,

wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo:Mkurugenzi Mkuu,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) 16 Mtaa wa Urambo S.L.P. 4865 Dar es Salaam,Tanzania.

Simu: (022) 2150043 - 6, Nukushi: (022) 2150047, Baruapepe: [email protected] Wavuti: www.pccb.go.tz, Simu ya Bure 113

ARUSHA, S.L.P. 1055Simu: (027) 2503538/ 2507928Nukushi (027) 2505973Baruapepe: [email protected]

DODOMA, S.L.P. 1175Simu: (026) 2322003/ 2322695Nukushi: (026) 2320003Baruapepe: [email protected]

GEITA, S.L.P. 38Simu: (028) 2520004Nukushi: (028) 2520004Baruapepe: [email protected]

ILALA, S.L.P. 6420Simu: (022) 2132954Nukushi: (022) 2150047Baruapepe: [email protected]

IRINGA, S.L.P. 1575Simu: (026) 2700156Nukushi: (026) 2703014Baruapepe: [email protected]

KAGERA, S.L.P. 1138Simu: (028) 222084/ 2220491Nukushi: (028) 2220534Baruapepe: [email protected]

KAHAMA, S.L.P. 538Simu: (028) 2710936Nukushi: (028) 2710926Baruapepe: [email protected]

KATAVI, S.L.P. 275Simu: (025) 2820613Nukushi: (025) 2820613Baruapepe: [email protected]

KIGOMA, S.L.P. 880Simu: (028) 2802889Nukushi: (028) 2804928Baruapepe: [email protected]

KILIMANJARO, S.L.P. 1951Simu: (027) 2750885Nukushi: (027) 2750889Baruapepe: [email protected]

KINONDONI, S.L.P. 90397Simu: (022) 2170852Nukushi: (022) 2170852Baruapepe: [email protected]

LINDI, S.L.P. 1004Simu: (023) 2202456/ 222799Nukushi: (023) 22202215Baruapepe: [email protected]

MANYARA, S.L.P. 386Simu: (027) 530255/ 2530256/ 2530570Nukushi: (027) 2530448Baruapepe: [email protected]

MARA, S.L.P. 377Simu: (028) 2623030Nukushi: (028) 2623029Baruapepe: [email protected]

MBEYA, S.L.P. 1419Simu: (025) 25603566Nukushi: (025) 2502859Baruapepe: [email protected]

MOROGORO, S.L.P. 845Simu: (023) 22614302Nukushi: (023) 2614478Baruapepe: [email protected]

MTWARA, S.L.P. 213Simu: (023) 2334013Nukushi: (023) 2333726Baruapepe: [email protected]

MWANZA, S.L.P. 2599Simu: (028) 2500600Nukushi: (028) 2500602Baruapepe: [email protected]

NJOMBE, S.L.P. 629Simu: (026) 2782777Nukushi: (026) 2782777Baruapepe: [email protected]

PWANI, S.L.P. 30261Simu: (023) 2402658/ 2402284Nukushi: (023) 2402657Baruapepe: [email protected]

RUKWA, S.L.P. 273Simu: (025) 2802426/ 2802926Nukushi: (025) 2800312Baruapepe: [email protected]

RUVUMA, S.L.P. 926Simu: (025) 2600613Nukushi: (025) 2600663Baruapepe: [email protected]

SHINYANGA, S.L.P. 37Simu: (028) 2762630Nukushi: (028) 2763358Baruapepe: [email protected]

SIMIYU, S.L.P. 306Simu: (028) 2700371Nukushi: (028) 2700532Baruapepe: [email protected]

SINGIDA, S.L.P. 484Simu: (026) 2502305/ 2502550Nukushi: (026) 2502550Baruapepe: [email protected]

TABORA, S.L.P. 1020Simu: (026) 2604030/ 2604311Nukushi: (026) 2604039Baruapepe: [email protected]

TANGA, S.L.P. 1953Simu: (027) 2645186/ 078642280Nukushi: (027) 2647885Baruapepe: [email protected]

TEMEKE, S.L.P. 42325Simu: (022) 2850633Nukushi: (022) 2850635Baruapepe: [email protected]

Page 3: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa3

Toleo la Januari - Machi 2016

YaliyomoTahariri

RUVUMA, S.L.P. 926Simu: (025) 2600613Nukushi: (025) 2600663Baruapepe: [email protected]

SHINYANGA, S.L.P. 37Simu: (028) 2762630Nukushi: (028) 2763358Baruapepe: [email protected]

SIMIYU, S.L.P. 306Simu: (028) 2700371Nukushi: (028) 2700532Baruapepe: [email protected]

SINGIDA, S.L.P. 484Simu: (026) 2502305/ 2502550Nukushi: (026) 2502550Baruapepe: [email protected]

TABORA, S.L.P. 1020Simu: (026) 2604030/ 2604311Nukushi: (026) 2604039Baruapepe: [email protected]

TANGA, S.L.P. 1953Simu: (027) 2645186/ 078642280Nukushi: (027) 2647885Baruapepe: [email protected]

TEMEKE, S.L.P. 42325Simu: (022) 2850633Nukushi: (022) 2850635Baruapepe: [email protected]

Sheria iboreshwe ili kuongeza ukali wa adhabu kwa makosa ya rushwa

Moja kati ya changamoto zinazoikabili TAKUKURU katika kutekeleza kwa mafanikio jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa ni udogo wa adhabu zinazotajwa na kutolewa na Mahakama kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Sheria hii, mathalani, inaitaja adhabu kwa mtu atakayepatikana na hatia kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kuwa ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni saba ama kwenda jela kwa kipindi kisichozidi miaka mitano au adhabu zote mbili kwa pamoja. Kosa hili, kwa uzoefu wa matukio ya rushwa yaliyojiri limeigharimu Serikali hasara ya bilioni za fedha ambazo zingetumika kuboresha huduma za umma kama vile upatikanaji wa dawa hospitalini au maji safi na salama.

Isitoshe, chunguzi za makosa haya ya rushwa hutumia fedha nyingi ikilinganishwa na adhabu zinatotolewa kisheria, fedha ambazo pia zingeweza kutumika katika kuboresha huduma kwa umma. Ukweli huu hauna budi kutufanya tufikirie zaidi kuhusu ufanisi wa Sheria hii katika kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa.

Tujiulize: mtumishi mla rushwa akijipatia shilingi bilioni mbili kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri atashindwa kulipa faini ya shilingi milioni saba? Je, adhabu hizi zinazotajwa katika Sheria hii zinawaogopesha watu kutojihusisha na rushwa?

Mwaka 2010, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, katika kesi ya jinai Na.7/2010, ilimtia hatiani Bw. Michael Ngilangwa kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilingi 500,000. Bw. Ngilangwa, kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007 aliomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake aliyekuwa na miaka 13 ili ampatie alama za juu katika somo la Kiingereza. Pia, Mahakama hiyo ilimhukumu kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kujaribu kubaka kinyume na kifungu cha 132 cha Kanuni za Adhabu za Tanzania. Bw. Ngilangwa alianza kutumikia vifungo vyote viwili mara baada ya hukumu.

Mahakama ina wajibu wa kutafsiri Sheria kadiri zilivyotungwa na Bunge. Tunaamini hata kwa tafsiri ilizofanya na inazoendelea kuzifanya inatenda haki kwa washtakiwa. Hata hivyo, tunadhani ni wakati muafaka kutafakari ‘haki wanayopewa’ washtakiwa wa makosa ya rushwa kupitia hukumu iwapo ‘inawatendea haki’ wale waliowakosea. Ndiyo maana leo tunaungana na kauli ya hivi karibuni ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alipowaambia wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuwa upungufu katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 unawafanya mafisadi kuendelea kuliibia Taifa kwani wanafahamu watapewa adhabu ndogo watakapopelekwa Mahakamani. Sisi tunaamni kuwa adhabu hizo ‘hazitoi haki’ kwa waliokosewa na mafisadi hao.

Bw. Mlowola aliwaasa Wabunge hao akisema “…Tunaomba itakapofika wakati mswada wa mapendekezo yetu ya kuiboresha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 utakapowasilishwa mtuunge mkono na kuupitisha Bungeni”. Nasi leo tunatoa rai kwa kila mdau na mwananchi mwenye nia njema na Tanzania kutuunga mkono katika kufanikisha maboresho hayo. Tunaamini adhabu kali zikitamkwa katika Sheria, matukio ya watu kujihusisha na vitendo vya rushwa vinavyowanyang’anya wananchi haki za kibinadamu na ya kujipatia maendeleo kwa rasilimali za nchi yatapungua sana. Ni jukumu lako na langu kuzuia na kupambana na rushwa, tushirikiane!

1. Tahariri........................................................................Uk.32. Kamati ya Bunge yaipongeza TAKUKURU kuokoa sh. bilioni 8.6, kufungua kesi 98 za rushwa kubwa mahakamani................................................................Uk.43. TAKUKURU yapata Mkurugenzi Mkuu mpya.........Uk.64. Wanaojihusisha na rushwa waonywa...........................Uk.75. Mapambano dhidi ya rushwa: Kairuki aitaka TAKUKURU kutafakari mafanikio na changamoto ...................................................................................Uk.96. Waziri Lukuvi afichua rushwa mradi mji mpya Kigamboni..................................................................Uk.117. Wanafunzi waomba kuingizwa somo la rushwa katika mitaala ya elimu.........................................................Uk.138.Habari katika picha .............................................Uk.14&159.Wabunge mahakamani kwa rushwa...........................Uk.1610. Mwandishi wa habari ahukumiwa kwa kuomba na kupokea rushwa.........................................................Uk.1711. Mhasibu Mkuu Zimamoto ahukumiwa kwa kuhujumu uchumi.....................................................Uk.1712. TAKUKURU yawapandisha kizimbani Mkurugenzi ATCL, Ofisa Mtendaji Mkuu PPRA kwa makosa ya rushwa .....................................................................Uk.1913. TAKUKURU Njombe yaokoa shilingi bilioni 1.7 miradi ya maendeleo, mishahara hewa....................Uk.2014. Meneja Posta kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka..................................................................Uk.2115. TAKUKURU Mara yamshikilia Mhasibu NHIF kwa utakatishaji fedha.............................................Uk.2216. Shahidi kigeugeu jela miaka mitano kesi ya Uhujumu Uchumi.....................................................................Uk.2317. Madiwani Tunduma watakiwa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa........................................................Uk.2418. Magazetini ...............................................................Uk.26

19. Mashairi...................................................................Uk.27

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa1

Toleo la Januari - Machi 2016

KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Jarida la Taasisi ya

ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016

www.pccb.go.tz

Kamati ya Bunge yaipongeza TAKUKURU kuokoa sh. bilioni 8.6

Ndani

Waziri Lukuvi afichua rushwa Mradi wa Mji Mpya Kigamboni

28

Toleo la Januari - Machi 2016

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Jarida la Taasisi ya

ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016

www.pccb.go.tz

Jarida hili hutolewa na Kurugenzi ya Elimu kwa Umma ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

16 Mtaa wa Urambo, S. L. P 4865, Dar es Salaam. Simu: 022 2150043 - 6, Nukushi: 022 2150047

Wavuti:www.pccb.go.tz, Simu ya Bure:113, Baruapepe:[email protected]

AMKA MWANANCHI, LONGA NASI LONGA NA TAKUKURU KWA FAIDA YA TANZANIA

Page 4: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa4

Toleo la Januari - Machi 2016Habari

Na Deusdedit Mutekuruzi, Octavian Kafanabo, Dar es Salaam

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za

Mitaa imeipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuokoa shilingi bilioni 8.6 ambazo zingeingia kwenye mifuko ya wabadhirifu na kufungua kesi 98 za rushwa kubwa mahakamani kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Januari 2016.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Jason Rweikiza (Mbunge) wakati ilipotembelea TAKUKURU Makao Makuu kwa lengo la kufahamu majukumu na utendaji kazi wa Taasisi hii ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kamati hiyo kutembelea taasisi inazosimamia.

Awali, akiwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angela Kairuki aliwaeleza kuwa TAKUKURU inaendeleza jukumu lake

la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa nchini.

Alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana yamechangiwa na ushirikiano wa wadau mbalimbali katika vita dhidi ya rushwa. “Waheshimiwa wajumbe wa

Kamati tunaomba mzidi kutuunga mkono ili tuweze kuitokomeza rushwa katika jamii”, alisema Waziri Kairuki.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, akitoa taarifa ya utendaji

kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Januari 2016, alisema kuwa jumla ya shilingi bilioni 8.6 zimeokolewa kupitia chunguzi mbalimbali, fedha ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya baadhi ya watu wachache wasio waadilifu. “Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha ambazo kuokolewa kwake kutaiwezesha Serikali kuzifanyia kazi nyingine za maendeleo ya wananchi”, alisema Bw. Mlowola.

Bw. Mlowola pia alisema kuwa uchunguzi wa majalada 296 ulikamilika ambapo majalada 252

Kamati ya Bunge yaipongeza TAKUKURU kuokoa sh. bilioni 8.6, kufungua kesi 98 za rushwa kubwa mahakamani

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki (Mb) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala

Bora na Serikali za Mitaa walipotembelea Makao Makuu ya TAKUKURU Machi 16, 2016.

Page 5: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa5

Toleo la Januari - Machi 2016 Habari

yaliwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kuombewa kibali kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.

Pia alieleza kuwa TAKUKURU ilifungua kesi mpya 208 kwenye mahakama mbalimbali nchini kati ya hizo kesi 98 ni za rushwa kubwa. Aidha, kesi 113 washtakiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo au kulipa faini.

Vilevile, Mkurugenzi Mkuu alieleza kuwa Taasisi imeendelea kutekeleza jukumu la kushirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo takribani wananchi 495,616 walielimishwa kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa kupitia semina, mikutano ya hadhara, mijadala ya wazi matamasha. Pia kwa kipindi hicho TAKUKURU imerusha vipindi vya redio na televisheni 160.

Kwa upande wa jukumu la kuzuia rushwa na kuimarisha mifumo ili kudhibiti mianya ya rushwa, tafiti mbili zilifanyika ambazo zilihusisha kudhibiti mianya ya rushwa katika biashara ya vyuma chakavu na kubaini mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma ya maji.

Bw. Mlowola alieleza kuwa kwa kutekeleza majukumu hayo TAKUKURU imefanikiwa kuongeza uelewa wa wananchi

kuhusu rushwa na athari zake kwa jamii. Pia ari ya wananchi ya kushiriki kikamilifu katika mapambano hayo imeongezeka hatua inayowafanya kufuatilia zaidi masuala mbalimbali yanayohusu mapambano dhidi ya rushwa.

“Uchumi wa nchi umekua na pato la taifa limeongezeka na hivyo kuongeza uwezo wa Serikali kuhudumia wananchi wake. Wananchi wamepewa uwezo wa kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alieleza Bw. Mlowola.

Vilevile alieleza kuwa Taasisi imefanikiwa kuongeza ushirikishwaji wa wadau wote katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo masuala ya rushwa yanaongelewa kwa uwazi.

Aliongeza kuwa tabia ya uadilifu na uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi imeanza kujengeka.

Akieleza changamoto zinazoikabili TAKUKURU, Bw. Mlowola alisema kuwa adhabu zinazotolewa na Mahakama kwa wanaopatikana na hatia ya makosa ya rushwa ni ndogo kutokana na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kutotoa adhabu kali.

“Sheria hii inatoa adhabu ya juu

kabisa kuwa kifungo kisichozidi miaka saba jela au kulipa faini isiyozidi shilingi 15,000,000 ukilinganisha na ukubwa wa makosa yanayotendeka”, alisema Bw. Mlowola.

Akisisitiza juu ya changamoto hiyo na huku akitoa rai kwa wabunge hao, Bw. Mlowola alisema: “Mapungufu katika Sheria hii unawafanya mafisadi kuendelea kuliibia taifa hili kwani wanafahamu watapewa adhabu ndogo watakapopelekwa Mahakamani. Tunaomba itakapofika wakati mswada wa mapendekezo yetu ya kuiboresha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 mtuunge mkono na kuupitisha bungeni”.

Akieleza juu ya mambo mbalimbali iliyoelezwa kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Rweikiza (Mbunge) alisema kuwa kamati yake imechukua maoni yote ikiwa ni pamoja kutafuta namna ya kuisaidia TAKUKURU kutatua changamoto zinazoikabili katika utendaji kazi.

Pia aliongeza kuwa Kamati yake itaendelea kuunga mkono TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa tatizo la rushwa linamgusa kila mmoja katika jamii.

Page 6: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa6

Toleo la Januari - Machi 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John

Pombe Magufuli amemteua na kumuapisha Bw. Valentino Mlowola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanzia Machi 15, 2016.Taarifa iliyotolewa na Kaimu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Bw. Gerson Msigwa ilisema kuwa Rais Magufuli amemteua Bw. Mlowola kuchukua nafasi ya Dkt. Edward Hoseah aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU hadi Desemba 2015.

Bw. Mlowola aliapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.

Wakurugenzi Wakuu wengine waliowahi kuingoza Taasisi hii ni Dkt. Edward Hoseah (2006-2015), Meja Jenerali (mstaafu) Anatory Kamazima (1990-2006), Bw. Zakaria Maftah (1975-1990), Bw. Steven Rutayangirwa (1974-1975) na Bw. Geofrey Sawaya (1973-1974)

TAKUKURU yapata Mkurugenzi Mkuu mpya

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Valentino Mlowola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Aprili 15, 2016.

Page 7: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa7

Toleo la Januari - Machi 2016

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na

Rushwa (TAKUKURU) imewatahadharisha watumishi wa umma, wananchi na wafanyabiashara kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa kuwa chombo hicho hakitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na taratibu.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Januari 26, 2016, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola kipindi hicho akikaimu nafasi hiyo aliwataka watumishi wa umma wanaojihusisha na rushwa kwa maslahi binafsi waache tabia hiyo mara moja.

“Wananchi sasa hivi wana kiu ya kupata maendeleo na maisha bora, watumishi wa umma watambue kwamba wananchi wa jana siyo hawa wa leo kwani wamedhamiria kuunga mkono jitihada hizi za Serikali yao ya Awamu ya Tano za kuwaletea maendeleo na maisha mazuri. Hivyo yeyote yule atakayethubutu kuhujumu jitihada hizi za Serikali na kujihusisha na vitendo vya rushwa ataripotiwa tu, nasi hatutosita kuchukua hatua stahiki,” alieleza Bw. Mlowola.

Alifafanua kuwa watumishi

hao wa umma ni pamoja na watumishi watoa huduma katika ofisi za umma, maofisa maduhuli, wakusanyaji wa kodi, maofisa manunuzi na watumishi wengine wanaohusika na kutumia fedha za umma.

Alisema TAKUKURU itawachunguza na kuwafungulia mashtaka watumishi wote watakaotumia vibaya fedha na rasilimali za umma ikiwa ni pamoja

na kuwafilisi mali ili kurejesha hasara waliyoisababishia Serikali. “…tutachukua hatua mara moja na nawaomba wananchi watuunge mkono kwa kutupatia

taarifa,” alisisitiza Bw. Mlowola.

Akielezea mafanikio yaliyopatikana, Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU alifafanua kuwa mwitikio mkubwa wa wananchi kutoa taarifa za rushwa, ni matokeo ya jitihada za kuielimisha jamii kuhusu rushwa na madhara yake.

Alisema mwitiko huo umechangiwa na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa mstari

wa mbele kusambaza habari na elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Bw. Mlowola alieleza kuwa T A K U K U R U

Wanaojihusisha na rushwa waonywaNa Matai Kirumbi, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika TAKUKURU Makao Makuu

Januari 26, 2016.

Habari

Page 8: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa8

Toleo la Januari - Machi 2016Habari

inakamilisha uchunguzi wa majalada 36 ya rushwa kubwa.

Akifafanua kuhusu baadhi ya kashfa za rushwa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari, Bw. Mlowola alieleza kuwa mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ametakiwa kulipa kodi ya shilingi bilioni 8.5.

Kashfa ya Lake Oil ilikwepa kodi hiyo kwa kuuza mafuta ya petroli lita 17,461,111.58 katika soko la ndani kudanganya kuwa mafuta hayo yamesafirishwa kwenda katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Alieleza pia kuwa TAKUKURU inakamilisha uchunguzi wa kashfa ya rushwa inayohusu malipo ya fedha dola za kimarekani milioni sita kwa kampuni ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA) kwa madai ya kuisaidia Tanzania

kupata mkopo wa

fedha za kimarekani milioni 600.

Bw. Mlowola alifafanua kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa fedha hizo, dola za kimarekani milioni sita, zilitakatishwa kwa ushirikiano wa watumishi wa umma na wa sekta binafsi huku wakifahamu kuwa fedha hizo wamezipata kwa njia haramu.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU alieleza kuwa Taasisi inaendelea na imekamilisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za rushwa kuhusu Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Hizi ni pamoja na ile ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za kuwapata wazabuni katika ujenzi wa reli ya kisasa ya kimataifa (standard gauge) uliosimamiwa na Shirika Hodhi la Reli nchini (RAHCO) na ile ya ukiukwaji

wa Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 21/2014 wakati wa ununuzi wa mabehewa 25.

Alisema TRL iliagiza mabehewa hayo kutoka India ambayo hayakuwa katika viwango vilivyokubalika katika mkataba na bado ikamlipa mzabuni. Wahusika katika mchakato wa ununuzi huo watafikishwa mahakamani.

Bw. Mlowola aliwaambia waandishi wa habari kuwa TAKUKURU imejipanga kutekeleza majukumu hayo ya kisheria na azma na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kupambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo bila ya kumuonea wala kumwogopa mtu yeyote.

“Naomba nisisitize hapa kwamba Mheshimiwa Rais alipozungumza kwamba amejipa kazi ya ‘kutumbua majipu’ tambueni kwamba TAKUKURU ndiyo vidole vya Mheshimiwa Rais katika kuyatumbua ‘majipu hayo.’ Kasi ya kufanya shughuli hiyo ni yetu TAKUKURU na nataka muelewe kwamba mwenye vidole akishaamua kutumbua ‘jipu’ kazi ya vidole ni utekelezaji tu. Na niwahakikishie kwamba tuko tayari kwa hilo,” alisisitiza Bw. Mlowola.

Mwandishi wa habari wa Channel Ten Bw. David Ramadhani akiuliza swali wakati wa mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

uliofanyika TAKUKURU Makao Makuu Januari 26, 2016.

Page 9: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa9

Toleo la Januari - Machi 2016 Habari

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe.

Angela Kairuki ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutafakari mafanikio yaliyopatikana na kufanya tathmini kuhusu changamoto zinazoikabili Taasisi katika kupambana dhidi ya rushwa.

Rai hiyo ilitolewa wakati akifungua Mkutano wa Kazi wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika Makao Makuu, Februari 15 na 16, 2016.

Aliwaeleza washiriki kuwa madhumuni ya mkutano huo ni mazuri kwani yanatoa fursa kujadili kazi zilizofanyika kwa mwaka 2014/2015 na kutafakari mafanikio yaliyopatikana na changamoto zinazoikabili TAKUKURU katika vita hii.

“Fursa hii pia itumike kubadilishana uzoefu miongoni mwenu, juu ya namna mbalimbali za kukabiliana na kutatua changamoto hizo, na kwa

kufanya hivyo, mtajikuta wote kama Taasisi mnasoma ukurasa mmoja katika utendaji wenu”, aliwaeleza Waziri Kairuki.

Akipongeza jitihada zinazofanyika kupambana na rushwa nchini, Waziri Kairuki alisema kuwa kazi hiyo ni ngumu inayohitaji ujasiri na kujitolea. “Nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya, ni ngumu

sana inayohitaji ujasiri na kujitolea na ni ya lawama”, alisema Waziri Kairuki.

Alieleza kuwa ni jambo linalotia

moyo kwake na umma wa Tanzania namna Taasisi inavyopambana na vitendo vya rushwa na kushinda vishawishi wakati wa utekelezaji wa kazi zake. “Ni jambo linalotia faraja sana kwamba mnaweza kukabili vikwazo kwa umahiri mkubwa. Kuna vishawishi vingi mnakumbana navyo, nawasihi sana tunzeni heshima zenu na Taasisi kwa ujumla”, alisema Kairuki.

Aidha, alieleza kuwa TAKUKURU inastahili pongezi kwani kiasi cha fedha za Serikali zilizookolewa mwaka 2014/15 takribani shilingi bilioni saba (7) ni nyingi ambazo zingeishia mifukoni kwa watu wasio waadilifu.

Alieleza kuwa ili mafanikio yawepo ni vema kupima na kuchuja taarifa

za uchunguzi unaofanyika ili uwe na tija.

Alifafanua kuwa kuwa TAKUKURU inatakiwa ifanye kazi kwa ushirikiano wa

Mapambano dhidi ya rushwa: Kairuki aitaka TAKUKURU kutafakari mafanikio na changamoto

• Ahimiza kufuata sheria, kutomwogopa mtu

Na Deusdedit Mutekuruzi, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akiwa na Viongozi wa TAKUKURU mara baada ya kufungua mkutano wa kazi wa viongozi

uliofanyika Makao Makuu ya TAKUKURU Februari 15, 2016.

Page 10: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa10

Toleo la Januari - Machi 2016Habarikaribu na vyombo vya sheria, utoaji haki na utawala bora. “Shirikianeni na Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Sekretarieti ya Maadili, Polisi na Wakala wa Manunuzi wa Serikali”.

Waziri Kairuki alitoa wito kwa TAKUKURU kuendelea kuhamasisha jamii na wanafunzi kuwa mstari wa mbele kupambana na rushwa.

Aliongeza kuwa taasisi iendeleee kufanya kaguzi mbalimbali ili kugundua kama kuna ubadhirifu au la.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alimweleza Waziri Kairuki kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili, kupanga namna ya utendaji kazi wa TAKUKURU na kuweka mikakati ya kuzuia vitendo vya rushwa na ufisadi kulingana na falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Alieleza kuwa taasisi imefanya jitihada kubwa kupambana na rushwa kwani kwa kipindi cha mwaka 2014/15 kwa

upande wa uchunguzi na mashtaka, jumla ya kesi 314 zilifunguliwa Mahakamani ambapo ilishinda kesi 132 washtakiwa walihukumiwa vifungo au kulipa faini.

“Aidha, tulifanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni saba (7) zilizokuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache”, Bw. Mlowola alimweleza Waziri Kairuki.

Vilevile alieleza kazi za uelimishaji umma zilifanyika na kuwafikia wananchi 703,667 kupitia semina 2,933 na mikutano ya hadhara 1,870. Njia nyingine zilizotumika kuwafikia wananchi ni kushiriki kwenye maonesho 182, vipindi 243 vya redio na televisheni na kupitia mikutano ya vyombo vya habari.

Pia alieleza kuwa tafiti mbalimbali zimefanyika na kuchapishwa. Mathalan kuhusu utafiti wa migogoro ya wakulima na wafugaji unaendelea kwa lengo la kutafuta suluhisho na kuepuka kuathiri usalama na amani ya nchi.

Akieleza kuridhishwa uungwaji mkono na Rais, Dkt. John Magufuli katika kupambana na rushwa na ufisadi, Bw. Mlowola alisema kuwa TAKUKURU inashiriki katika hatua mbalimbali

za uanzishwaji wa Mahakama ya Rushwa na Ufisadi.

“Kuundwa kwa Mahakama ya Rushwa na Ufisadi kutarahisisha mapambano dhidi ya rushwa nchini”, alisema Bw. Mlowola.

Akitoa wito kwa viongozi walioshiriki mkutano huo alisema, “Nawahimiza viongozi wenzangu kufanya kazi kwa weledi na umakini mkubwa ili kuharakisha uchunguzi na mashauri mbalimbali”. Pia aliongeza kuwa wafuatilie mapato ya Serikali na kuhakikisha hayapotei. “Fuatilieni mapato ya Serikali na hakikisheni hayapotei na ifuatilieni miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu”, aliwaeleza Bw. Mlowola.

Wakati huo, Mkurugenzi wa Uchunguzi wa TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Kairuki alisema kuwa TAKUKURU itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya rushwa.

Alieleza kuwa Taasisi inahitaji ushirikiano wake na kuhimiza wadau na jamii kuzingatia maadili na utawala bora. Pia aliahidi kuwa Taasisi itazingatia yote aliyoeleza Mhe. Kairuki

Page 11: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa11

Toleo la Januari - Machi 2016 Habari

Waziri Lukuvi afichua rushwa mradi mji mpya Kigamboni• Ni baada ya kukataa rushwa ya shilingi bilioni tano• Aahidi kushirikiana na TAKUKURU kuvunja mtandao wa rushwa

Na Faisal Abdul, Dar es Salaam

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya

Makazi, Mhe. William Lukuvi amefichua na kukemea kukithiri kwa vitendo vya rushwa wizarani hapo na kuahidi kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( T A K U K U R U ) kuvunja mtandao wa vitendo vya rushwa katika sekta ya ardhi.

Mhe. Lukuvi aliyasema hayo Machi 7, 2016 katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa mji mpya wa Kigamboni wenye ukubwa wa takribani ekari 6,000 utakaojumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada na Somangila.

Mradi huo ulitarajiwa kugharimu shilingi trilioni 13 ambazo zingetolewa na Serikali lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi katika ujenzi wake.

Waziri Lukuvi alisema kuna wafanyabiashara waliwafuata

marafiki zake wa karibu na kudai kuwa wangempa rushwa ya shilingi bilioni tano ili afanikishe mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe shilingi bilioni tano ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi” alisema Waziri Lukuvi na kuongeza, “Wakati naingia tu wizara hii, nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni

ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri, nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili wafanyabiashara hao walipata taarifa wakaja mbio

kutaka kuniona.”

A l i s e m a wafanyabiashara hao walitaka walipwe kiasi cha shilingi milioni 141 kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa shilingi milioni tano kwa ekari jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa shilingi milioni tano kisha Serikali tumlipe shilingi milioni 141 kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa. Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji Waziri Lukuvi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

Page 12: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa12

Toleo la Januari - Machi 2016Habari

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya shilingi bilioni 84 kuwalipa wawekezaji hao kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

Aidha, alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa Wizara na kusema mtandao huo ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza vitendo vya rushwa.

Licha ya kukataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Mhe.Lukuvi alisema mtandao huo wa wafanyabiashara ni

hatari na kuahidi

kusaidiana na TAKUKURU kuwafichua na kuwapata wote waliohusika kutaka kumshawishi ili aweze kupokea rushwa.

Akizungumzia migogoro ya

ardhi, Waziri Lukuvi alisema amegundua migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na maofisa na viongozi wa wizara hiyo wasio waaminifu, lakini pia wawekezaji wenye tamaa ya kumiliki kiasi kikubwa cha ardhi hata kama hawana shughuli nayo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola alisema kuwa TAKUKURU imeanza kuchunguza taarifa zilizoripotiwa na Waziri Lukuvi kukataa kupokea rushwa ya shilingi bilioni tano iliyotaka kutolewa na wafanyabiashara.

Ramani ya Mji Mpya wa Kigamboni eneo la biashara

Ramani ya Mji Mpya wa Kigamboni eneo la viwanda

Page 13: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa13

Toleo la Januari - Machi 2016 Vijana

Rai imetolewa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

(TAKUKURU) kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kuandaa somo la elimu dhidi ya rushwa ili liingizwe kwenye mitaala ya elimu kuanzia shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu.

Hatua hiyo, imeelezwa kuwa i t a w a j e n g a zaidi wanafunzi kimaadili hivyo kuepuka vitendo vya rushwa wangali wadogo.

Ombi hili lilitolewa na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbeya, Bw. John Joseph kupitia risala aliyoisoma wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapinga rushwa kutoka shule za sekondari za Ivumwe, Iwalanje, Iyunga, Usongwe, Loleza na ile ya Mbeya. Mahafali hayo yalifanyika Machi 3, 2016 katika Shule ya Sekondari Mbeya, jijini Mbeya.

Risala hiyo iliainisha changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja na ile ya kutokuwepo kwa somo la rushwa katika mitaala ya elimu.

Bw. Joseph alisema somo la rushwa lingesaidia kuongeza uelewa wa wanafunzi wa masuala ya rushwa na madhara yake katika jamii.

Naye Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili (Kanda za Nyanda za Juu Kusini), Bw. Erick Mbembati, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, aliwashauri

wahitimu hao kutumia vyema elimu waliyoipata kwa kutojihusisha na vitendo vitakavyobomoa maadili yao ikiwemo vitendo vya rushwa.

Aliwataka kujihadhari na makosa ya jinai kama vile ujambazi au

biashara ya madawa ya kulevya na badala yake watumie ujana wao katika namna itakayolinufaisha Taifa.

Awali, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Bw. Xavery Mhyella akimkaribisha Bw. Mbembati alisema vitendo vya rushwa vimekithiri nchini kutokana na mmomonyoko wa maadili na kukosa uzalendo.

“TAKUKURU kwa kulitambua hilo

tumeamua kuwekeza nguvu kwenu vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kwani nchi hii ni ya kwetu na nyinyi ndiyo nguvu kazi ya Taifa, kama hatutakuwa na uzalendo na nchi yetu na kuwa na maadili, basi tatizo la rushwa litaendelea kulitafuna Taifa”, alisema Bw. Mhyella.

Wanafunzi waomba kuingizwa somo la rushwa katika mitaala ya elimu

Na Anangisye Mwateba, Mbeya

Wanachama wa Klabu za Wapinga Rushwa Shule za Sekondari jijini Mbeya, wakimsilkiliza Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi

wa Umma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Erick Mbembati (hayupo pichani) wakati wa mahafali yaliyofannyika katika Shule ya

Sekondari Mbeya, Machi 3, 2016.

Page 14: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa14

Toleo la Januari - Machi 2016

Wanafunzi na wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa

Shule ya Msingi Mweli iliyopo wilayani

Sengerema, wakionesha machapisho baada ya kupata elimu ya

mapambano dhidi ya rushwa

Januari 19, 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Bw.Valentino Mlowola akipata ufafanuzi kutoka kwa Afisa wa Mahakama (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika

viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es

Salaam, Februari 3, 2016.

Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt.Ramadhani Mlinga na

mwanasheria wa mamlaka hiyo Bi. Bertha Soka baada

ya kusomewa mashtaka katika Mahakama ya

Hakimu Mkazi Kisutu, Machi 15, 2016.

HABARI KATIKA PICHA

Page 15: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa15

Toleo la Januari - Machi 2016

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka

ya Uendelezaji wa Bonde la mto Rufiji

(RUBADA) Bw. Aloyce Masanja akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka,

Machi 15, 2016.

Kamishna Mkuu mstaafu wa TRA Bw. Harry Kitilya

(katikati) na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sio

Sumari (kushoto) na Bi. Shose Sinare (kulia) wakisubiri

kusomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari

ya Kata ya Mahongole iliyopo

Makambako yaliyojengwa bila kuwekewa "ring

beam".

HABARI KATIKA PICHA

Page 16: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa16

Toleo la Januari - Machi 2016

Na Waandishi wetu, Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

imewafikisha mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 30 kinyume na kifungu cha 15 (i) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

Wabunge hao, Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mvomero), Mhe. Victor Mwambalaswa (Lupa) na Mhe. Kangi Lugola (Mwibala), walifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Machi 31, 2016.

Akiwasomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Bw. Maghera Ndimbo akishirikiana na Bw. Emmanuel Jacob alisema kuwa Machi 3, 2016, kati ya saa mbili na saa nne usiku, katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam washtakiwa waliomba rushwa ya shilingi milioni 30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri

ya Wilaya ya

Gairo ili wamsaidie kuipitisha bila marekebisho taarifa ya utendaji kazi wa halmashauri hiyo iliyokuwa ijadiliwe na Kamati hiyo Machi 16, 2016.

Uchunguzi dhidi ya mashtaka haya bado unaendelea na washtakiwa wako nje kwa dhamana ya kila mshitakiwa kuwa

na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 14, 2016.

Wakati huohuo, Aprili 1, 2016, Mbunge wa Sumwe, Mhe. Richard Mganga Ndassa ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mtaji na Uwekezaji alifikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa

ya shilingi milioni 30 kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

Akimsomea mashtaka Mhe. Ndassa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro, Mwendesha Mashtaka

wa TAKUKURU, Bw. Dennis Lekayo akishirikiana na Bw. Emmanuel Jacob alisema kuwa Machi 13, 2016, mshtakiwa akiwa mjumbe wa Kamati hiyo, alimwomba rushwa ya shilingi milioni 30 Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme

Tanzania (TANESCO), Bw. Felchesmi Mramba ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati kuipitisha bila

kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.

Mbunge huyo amefunguliwa kesi namba 118/2016 na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyetakiwa kulipa shilingi milioni 10. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na kesi hii itatajwa tena Aprili 18, 2016.

Wabunge mahakamani kwa rushwa

Kutoka kushoto aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu

za Serikali za Mitaa Mhe. Kangi Lugola, Mhe. Sadik Murad na Mhe. Victor Mwambalaswa

wakiwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi za rushwa mahakamani

Page 17: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa17

Toleo la Januari - Machi 2016

Mw a n d i s h i wa habari wa kujitegemea jijini

Arusha, Bw. Joseph Ngilisho amehukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni mbili au kutumikia kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa.

Bw. Ngilisho alihukumiwa Februari 15, 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha na Hakimu Mkazi, Mhe. Devotha Msoffe baada ya kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya shilingi milioni mbili na kupokea shilingi milioni tano ikiwa ni sehemu ya hongo

aliyoomba jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

Akisoma hukumu hiyo dhidi ya mshitakiwa, Mhe. Msoffe alimtaka Bw. Ngilisho kulipa faini ya shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha miezi 24 jela kwa kosa la kwanza la kushawishi kupewa hongo.

Pia kwa kosa la pili la kupokea hongo, mshtakiwa alitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha miezi 24 jela. Bw. Ngilisho alilipa faini kwa

makosa yote mawili.

TAKUKURU ilimfikisha Bw. Ngilisho mahakamani kwa mara ya kwanza Januari 29, 2013 na kufunguliwa kesi ya Jinai Namba 31 ya mwaka 2013. Ilidaiwa mahakamani kuwa mshtakiwa huyo aliomba rushwa ya shilingi milioni mbili kutoka kwa aliyekuwa Afisa Mwandamizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Phili Makini Klerruu ili amsafishe kwa tuhuma alizomuandika katika gazeti la Dira la Januari 21-27, 2013. Bw. Klerruu alituhumiwa kufuja fedha za ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya hiyo lililopo jijini Arusha, Tanzania.

Mwandishi wa habari ahukumiwa kwa kuomba na kupokea rushwaNa Mwandishi wetu, Arusha

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam

imewahukumu kwa makosa ya uhujumu uchumi, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Kuzima Moto na Uokozi katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Bi. Naamini Henry Sangwa na Mkandarasi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, Bw. Webu Manoth Masawe.

Hukumu hiyo iliyosomwa Machi 24, 2016 na Hakimu Mkazi, Mhe.

Hassan Juma imemtia hatiani Bi. Naamini, ambaye alikuwa mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 06/2014 kwa makosa mawili ya matumizi mabaya ya madaraka ambapo alitakiwa kulipa faini ya shilingi laki tatu au kwenda jela miezi sita kwa kila kosa.

Mshtakiwa amelipa faini. Pia kwa kosa la kughushi nyaraka, mshtakiwa ametiwa hatiani na kuhukumiwa kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda wa miezi 12.

Bw. Masawe, aliyekuwa mshtakiwa wa tatu, Mahakama imemtia hatiani kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara ya shilingi milioni 68 ambapo amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu pamoja na kuirudishia Serikali kiasi hicho cha fedha.

Shtaka hili la kuisababishia Serikali hasara lilimhusu pia mshtakiwa wa pili, Bi. Naamini, ambaye hata hivyo hakupatikana na hatia yoyote kwa shtaka hilo.

Washtakiwa hawa na

Mhasibu Mkuu Zimamoto ahukumiwa kwa kuhujumu uchumiNa Mwandishi wetu, Ilala

Kesi za rushwa mahakamani

Page 18: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa18

Toleo la Januari - Machi 2016

mshtakiwa wa kwanza, Bw. Dotto Saleh Mgogo aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Kuzima Moto na Uokozi katika Wizara ya Mambo ya Ndani, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 14 2014 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 6/2014.

Bw. Mgogo alifariki dunia baadae mwaka 2014 na mashtaka dhidi yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria.

Washtakiwa hao kwa ujumla walishtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na kifungu 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007.

Mashtaka mengine yalikuwa ni kughushi nyaraka kinyume na vifungu 333, 335 (d) (1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 iliyorekebishwa mwaka 2002 na kuisababishia Serikali hasara kinyume na aya ya 10 (1) ya Jedwali la Kwanza, vifungu 57 (1) na 60 (1) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 iliyorekebishwa mwaka 2002.

Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Bw. Stanley Luoga

na Bw. Emmanuel Jacob, waliieleza Mahakama kuwa mnamo mwaka 2009, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa zabuni ya ujenzi wa uzio wa Chuo cha Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo-Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa kampuni ya Kiareni Investment Ltd yenye thamani ya shilingi milioni 82.

Hata hivyo, kwa kutumia madaraka yao vibaya, mnamo Agosti 27, 2009, Bw. Mgogo na Bi. Naamini walitoa zabuni kwa kampuni hiyo kinyume na kanuni namba 68 ya Manunuzi ya

Umma ya mwaka 2005 na kifungu 44 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 4 ya mwaka 2004 vinavyoelekeza kulinganisha gharama za wazabuni.

Pia ilidaiwa kuwa Agosti 27, 2009, katika kutekeleza majukumu, Bi. Naamini alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya Kiareni Investment

Ltd bila ya mkataba wa kazi (Local Purchase Order-LPO) kinyume na kifungu 55 (4) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 4 ya mwaka 2004.

Pamoja na kutolewa kwa zabuni kinyume cha sheria, kampuni ya Kiareni Investment Ltd ilifanya kazi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 13.7.

Ili kuwezesha malipo yote ya shilingi milioni 82 kufanyika, Bi. Naamini alighushi hati ya kuonesha kuwa kazi hiyo imekamilika (Certificate of Completion) ya Januari 5, 2012 kwa kuweka saini za Rashid Kichawele na Dotto Mgogo ili kuonyesha kuwa

ndiyo walioandaa na kuidhinisha hati hiyo jambo alililofahamu kuwa siyo kweli.

Kesi za rushwa mahakamani

Page 19: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa19

Toleo la Januari - Machi 2016

TAKUKURU yawapandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi ATCL, Ofisa Mtendaji Mkuu PPRA kwa makosa ya rushwa

Na. Mwandishi wetu , Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa ( T A K U K U R U ) ,

imewapandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Bw. David Mattaka, ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Ramadhani Mlinga na mwanasheria wa mamlaka hiyo Bi.Bertha soka Machi 15, 2016.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe.Respicius Mwijage, Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Timon Vitalis akishirikiana na mawakili wa T A K U K U R U Bw.Joseph Kiula na Stanley Luoga walisema washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuisababishia Serikali hasara kupitia ukodishaji wa ndege.

Aidha,Wakili Vitalis alidai kuwa

Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL, Bw. Mattaka alitumia madaraka yake vibaya kwa kutia saini mkataba wa ukodishaji ndege A320-214 iliyotengenezwa kwa namba 630 baina ya Wallis Trading Inc na ATCL.

Wakili Vitalis aliongeza kuwa Bw. Mattaka alifanya hivyo bila kuzingatia sheria za manunuzi ya Umma na kufata taratibu za

Zabuni, pia alidai Oktoba 27, 2007 alitumia madaraka yake vibaya kwa kutia saini cheti cha kuruhusu mchakato wa ukodishwaji wa ndege hiyo bila ya kufata ushauri wa kiufundi aliopewa na wataalam na kuisababishia Serikali hasara ya dola 772,402.08

za Marekani zilizolipwa kwa Kampuni ya Aeromantenimientos kama gharama za huduma ya matengenezo.

Aidha, Wakili Vitalis alisema washtakiwa wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Ramadhani Mlinga na mwanasheria wa mamlaka hiyo

Bi.Bertha, wanadaiwa kuwa Machi 19, 2008 katika ofisi za PPRA walighushi muhtasari wa kikao cha siku ukionyesha mamlaka hiyo ilijadili maombi ya ATCL juu ya kuidhinishwa kwa mkataba huo.

Hakimu Respicius Mwijage akiahirisha kesi hiyo hadi Machi

29, 2016, aliwakubalia na kuwaachia kwa dhamana Bw. Ramadhani Mlinga na Bi. Bertha kwani

dhamana yao ilikuwa wazi.

Aidha, David Mattaka dhamana yake ilikataliwa kwa madai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kumpa dhamana kwa kesi inayomkabili ila anaweza kudhaminiwa kupitia Mahakama kuu .

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania Bw. David Mattaka baada ya kusomewa

mashtaka dhidi yake Machi 15, 2016.

Kesi za rushwa mahakamani

Page 20: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa20

Toleo la Januari - Machi 2016

Na Joseph Singano, Njombe

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa

Njombe imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 1.7 zilizotengwa kwa ajili ya kugharamia mishahara na miradi ya maendeleo katika kipindi cha miezi mitatu tangu Januari hadi Machi 2016.

Mkuu wa TAKUKURU Njombe, Bw. Charles Nakembetwa aliyasema hayo Aprili 6, 2016 alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ambapo alieleza kuwa uchunguzi uliofanyika ulibainisha kuwa fedha hizo zilikuwa zimechepushwa kwa njia za rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Fedha hizo zimeokolewa baada ya TAKUKURU kuwaamuru watuhumiwa kuzirejesha na kurudishwa Hazina.

Alisema kati ya fedha hizo, shilingi milioni 82 zilikuwa zilipe mishahara ‘hewa’ ya ‘watumishi’ wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, kituo cha Ilembula.

Fedha hizo zimerejeshwa Hazina kama mishahara isiyolipwa

(unclaimed salary) na wahusika wamechukuliwa hatua za kinidhamu. Fedha nyingine, shilingi milioni 21 zilitumwa kwa ajili ya kulipa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe lakini hazikutumika kama ilivyopangwa na Serikali. Fedha hizo zimerejeshwa Hazina na kukatiwa stakabadhi ya Serikali (ERV).

Bw. Nakembetwa alifafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2013/2014, Halmashauri ya Mji Njombe ilituma shilingi milioni 11 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika Serikali za Mitaa na Vijiji vya Kata za Ramadhani.

Hata hivyo, fedha hizo zilizotokana na maduhuli ya Serikali ikiwa ni utaratibu wa halmashauri kurejesha asilimia 20 ya mapato yake kwa Serikali za Mitaa, vijiji na kata, zilitumika vibaya na watendaji husika. Fedha hizo zimerejeshwa Hazina na kukatiwa stakabadhi ya Serikali (ERV).

Pia alieleza kuwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha shilingi milioni 8 ulibainika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu zilizoko Makambako. Pia uchunguzi ulibaini kuwepo

kwa matumizi mabaya ya fedha shilingi milioni nne uliowahusisha baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Mpanga-Kipengele iliyopo wilaya ya Wanging’ombe. Fedha hizo zote zimerejeshwa Hazina na kukatiwa stakabadhi ya Serikali (ERV) na wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa TAKUKURU Njombe alisema uchunguzi mwingine uliofanyika ni wa ubadhirifu wa shilingi 330,100 uliomhusu Mtendaji wa Kijiji cha Kigala katika wilaya ya Makete.

Fedha hizo ambazo pia zimerudishwa na kukatiwa stakabadhi ya Serikali (ERV) zilikuwa zimechangwa na wananchi kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kufanya shughuli za usafi katika maeneo yao.

Pia, kulibanika kuwepo kwa ubadhirifu wa shilingi milioni 1.8 katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Maongele iliyopo Makambako, shilingi milioni 300 katika ujenzi wa mradi wa maji kwenye kijiji cha Rugarawa, Ludewa, shilingi

TAKUKURU Njombe yaokoa shilingi bilioni 1.7 miradi ya maendeleo, mishahara hewa

Kesi za rushwa mahakamani

Page 21: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa21

Toleo la Januari - Machi 2016

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa

Ilala imewafikisha mahakamani maofisa 3 waandamizi wa Shirika la Posta Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Meneja wa Mkoa Bw, Lawrence Mwasikili kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya 2007 Februari 22, 2016.

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Mhe. Respicius Mwijage, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Bi. Veronica Chimwanda aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Bi. Modester Fumbuka (Afisa Tawala) na Bi. Radegunda Massawe (Afisa

Manunuzi Mwandamizi).

Bi. Chimwanda aliieleza Mahakama kuwa kati ya Agosti 1, 2010 na Oktoba 31, 2010 washtakiwa hao wakiwa viongozi waandamizi wa Shirika la Posta Mkoa wa Dar es Salaam walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni ya huduma ya vibarua kwa kampuni binafsi ya Technical Merchantile Services bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 21 ya 2004.

Mwendesha mashtaka alidai katika shitaka la pili mnamo mwezi Septemba, 2011 washtakiwa hao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuongeza mkataba kwa kampuni ya Technical

Merchantile Services kinyume cha sheria. Katika shitaka la tatu, Bi. Chimwanda alidai kuwa Januari 1, 2012 washtakiwa hao waliongeza tena mkataba kwa kampuni hiyo bila kufuata sheria.

Kesi ya jinai Namba 59 ya 2016 ilifunguliwa dhidi ya washtakiwa hao ambapo waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni watumishi wa umma aliotakiwa kusaini dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja.

Kesi hiyo itatajwa tena Machi 2016 kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa.

milioni 79 za ujenzi wa daraja la kijiji cha Mpangala, Ludewa, shilingi milioni 605 za mradi wa umwagiliaji skimu ya Mkiu, Ludewa na ubadhirifu wa shilingi milioni 620 katika mradi wa bomba la maji lililopo Lugarawa, Ludewa. Baadhi ya mikataba ya

miradi hii imesitishwa na fedha kurejeshwa Hazina ambapo uchunguzi unaendelea kabla ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa.

Bw. Nakembetwa alifafanua kwamba pamoja na watuhumiwa wa uchepushaji wa fedha hizo

za miradi ya maendeleo na mishahara hewa kuzirejesha, hatua kali za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani baada ya kukamilisha kwa uchunguzi.

Meneja Posta kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Na. Raphael Mbwambo, Ilala

Kesi za rushwa mahakamani

Page 22: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa22

Toleo la Januari - Machi 2016Kesi za rushwa mahakamani

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara

(TAKUKURU) inamshikilia Mhasibu Mfuko wa Bima ya Afya tawi la Mkoa wa Mara (National Health Insurance Fund) Bw. Francis Mchaky kwa tuhuma za Uhujumu Uchumi na Utakatishaji fedha (Money Laundering) za Mfuko wa Bima ya Afya.

Akizungungumza na vyombo vya habari Machi 16, 2016, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Bw. Holle Makungu alisema Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, fedha zinazokaribia bilioni tatu za mfuko huo zimechepushwa kutoka akaunti ya mfuko na kuwekezwa kwenye miradi mbalimbali ya mtumishi huyo kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana

na Rushwa namba 11/2007.Aliongeza kuwa, kitendo cha Kuwekezwa kwenye miradi hiyo hutafsiriwa kuwa ni ufujaji na utakatishaji (Money Laundering) kinyume na Kifungu cha 12 cha Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha (Anti-Money Laundering Act, No 12 of 2006).

Aidha, Bw. Mchaky kwa nyakati tofauti amekuwa akiandaa hati za malipo kuonyesha kwamba walipwaji ni hospitali, zahanati na vituo vya afya mbalimbali vilivyoko mkoani Mara, hata hivyo hazikuwafikia walengwa bali alichukua fedha hizo toka Benki zikiwa ni fedha taslimu na kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ili jamii iweze kuaminishwa kwamba mtumishi huyo ameweza kujipatia fedha kutokana na biashara halali.

“Kwa maana ya sheria ya mapato yatokanayo na uhalifu (The Proceeds of Crime Act, 1991) neno mali imetafasiriwa kumaanisha vitu vinavyohamishika na visivyohamishika kama vile Viwanja, Majumba, Majengo, Uwekezaji katika Migodi, Mashamba, Biashara za aina mbalimbali kama vile maduka ya vipuri, maduka ya vileo, Nguo, Spea, hisa katika makampuni mbalimbali ndio maana tunamshikilia kwa utakatishaji wa fedha” alisema Bw. Holle.

Aliongeza kuwa “TAKUKURU inatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mali zenye kutiliwa mashaka zinazomilikiwa na Bw. Mchaky au jamaa zake wa karibu watoe taarifa ofisi za TAKUKURU Mara au ofisi zilizo karibu nao”

TAKUKURU Mara yamshikilia Mhasibu NHIF kwa utakatishaji fedha

Na Shani Ramadhani, Mara

“Naomba nisisitize hapa kwamba Mheshimiwa Rais alipozungumza kwamba amejipa kazi ya ‘kutumbua majipu’ tambueni kwamba TAKUKURU ndiyo vidole vya Mheshimiwa Rais katika kuyatumbua ‘majipu hayo.’ Kasi ya kufanya shughuli hiyo ni yetu TAKUKURU na nataka muelewe kwamba mwenye vidole akishaamua kutumbua ‘jipu’ kazi ya vidole ni utekelezaji

tu. Na niwahakikishie kwamba tuko tayari kwa hilo,”.

Bw.Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Nukuu Muhimu“Mapungufu katika Sheria hii unawafanya mafisadi

kuendelea kuliibia taifa hili kwani wanafahamu watapewa adhabu ndogo watakapopelekwa Mahakamani. Tunaomba itakapofika wakati mswada wa mapendekezo yetu ya kuiboresha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 mtuunge mkono na kuupitisha bungeni”.

Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Page 23: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa23

Toleo la Januari - Machi 2016

Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara imemhukumu

kwenda jela miaka mitano Bw. Hamidu Seleman Mayani baada ya kupatikana na kosa la kuyakana maelezo yake aliyokuwa ameyatoa kama shahidi katika kesi Na.130/2013 ya uhujumu uchumi Februari 25, 2016.

Akitoa hukumu katika kesi ya jinai Na.119/2014 Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Emmanuel Ngaile alimtia hatiani mtuhumiwa baada ya hapo awali kutoa maelezo ya kumtambua mtuhumiwa mbele ya maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kesi Na.130/2013 iliyofunguliwa na TAKUKURU.

Awali katika kesi hiyo, Bw. Hamidu katika maelezo yake ya awali alieleza kuwa alikuwa anamfahamu Bi. Scola Mossy na kwamba alimshawishi aweke sahihi mbele ya majina ya watu ambao hawafahamu kwenye karatasi ya malipo ya fedha za vibarua, Kitendo hicho kilipelekea jumla ya shilingi milioni 3.8

kuchepushwa kwa kisingizio zililipwa vibarua wa kuharibu karatasi zilizokuwa zimetumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo mwendesha mashitaka

wa TAKUKURU Bw. William Fusi alidai kuwa Bw. Hamidu akijua fika kuwa yeye ni shahidi kwenye kesi ya uhujumu uchumi Na. 130/2013 alipotakiwa kutoa ushahidi wake mahakamani aligeuka na kuyakana maelezo mahakamani kuwa hamfahamu Bi. Scola na kwamba alipewa kazi ya kuharibu karatasi zilizotumika katika uchaguzi 2010 na mtumishi

wa Halmashauri ya Wilaya aitwaye Julius Makwasa na kwamba kutokana na kazi hiyo alilipwa shilingi laki tatu kwa kazi hiyo!

Aliieleza Mahakama kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 162 cha Sheria ya Ushahidi (CAP 6 Re. 2002)” kinaeleza kuwa mtu yeyote ataitwa shahidi kigeugeu pale kwa nia njema kabisa na kwa kusaidia haki iweze kutendeka anatoa maelezo yake mbele ya vyombo vya dola kama vile Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,

Uhamiaji n.k. kuhusu kitendo cha uhalifu ambacho anaufahamu nacho”.

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU, Bw. Fusi aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa mashahidi wengine ambao ni vigeugeu, baada ya mshitakiwa kupatikana na hatia, Mahakama iliridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa hilo.

Shahidi kigeugeu jela miaka mitano kesi ya Uhujumu Uchumi

Na Shani Ramadhani, Mara

Bw. Hamidu Selemani Mayani

Kesi za rushwa mahakamani

Page 24: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa24

Toleo la Januari - Machi 2016Habari

Na Mwandishi wetu, Tunduma.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kituo

maalum Tunduma wamewataka Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma kutimiza wajibu wao katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli iliyofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lunch Time iliyoko eneo la Chapwa Januari, 26 – 27, 2016.

Wito huo ulitolewa na Afisa wa TAKUKURU, Bw. Faraja Uledi, wakati akitoa mada kwa Madiwani pamoja na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Tunduma.

Katika Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Momba, Bw. Mathias F. Mizengo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Uledi alisema Madiwani ni wasimamizi wa shughuli zote za Halmashauri kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya, Sura ya 287) na (Mamlaka za Miji, Sura ya 288) na kwamba wao ndio wanaounda Halmashauri

hizo za Serikali za Mitaa na ndiyo wenye Mamlaka ya kutekeleza majukumu ya Serikali za Mitaa.

Aliongeza kuwa, utekelezaji mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hufanyika katika ngazi ya Halmashauri na kiasi kikubwa cha fedha za umma hutolewa na Serikali ili kutekeleza miradi hiyo (mfano Busket fund, Road fund, TASAF, DADPS, nk), na kusema

kuwa jukumu kubwa la Serikali za Mitaa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwapatia huduma bora na kwa gharama nafuu.

Vilevile utekelezaji wa miradi hiyo mara nyingi umekuwa

ukiambatana na vitendo vya rushwa, ubadhirifu na ufujaji kiasi cha miradi hiyo kutokidhi viwango na kutofikia malengo yaliyokusudiwa kwa kushindwa kuwapatia wananchi huduma bora zenye gharama nafuu.

Bw.uled aliongeza kuwa Madiwani wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vyote vinavyohusiana

na rushwa au ubadhirifu katika utekelezaji wa miradi hiyo ili miradi hiyo ilete tija na wananchi waweze kupata maendeleo tarajiwa.

Aidha , Utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaweza kuathiriwa endapo rushwa, ubadhirifu na ufujaji vikiachwa vikashamiri kwani fedha zinazopangwa

kutumika katika miradi hiyo hutumika kinyume na malengo na pia wasimamizi wa miradi hiyo nao huweza kutumia fursa hiyo kutotimiza ipasavyo wajibu wao na hivyo kupelekea miradi hiyo kutekelezwa chini ya kiwango.

Madiwani Tunduma watakiwa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma wakimsikiliza Afisa wa TAKUKURU

(hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli

ya Lunch Time, Januari 26 & 27, 2016.

Page 25: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa25

Toleo la Januari - Machi 2016 HabariPia bw. Uledi alisema rushwa huathiri michakato ya utangazaji na upatikanaji wa zabuni mbalimbali katika Halmashauri kutokana na baadhi ya Watendaji wasio waaminifu kukiuka taratibu za kisheria na hivyo kutoa upendeleo wa namna fulani kwa baadhi ya Wazabuni baada ya kupewa au kuahidiwa kupewa rushwa na Wazabuni hao.

Aliongeza kuwa hata michakato ya ajira katika Halmashauri nayo huathiriwa na rushwa kutokana na nafasi za ajira kutotangazwa au kutolewa kwa upendeleo kwa sababu ya rushwa ikiwemo na rushwa ya ngono.

Bw.Uledi alibainisha kuwa rushwa ikishamiri katika Halmashauri basi hata mgawanyo wa rasilimali katika Halmashauri hautakuwa sawa kwani baadhi ya Madiwani wenye ushawishi au madaraka fulani kama vile Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Ha lmashau r i au Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Ha lmashau r i h u w e z a k u t u m i a m a d a r a k a yao hayo k u p e n d e l e a m a e n e o /Kata zao

wakati wa upangaji wa bajeti au miradi ya maendeleo na kuacha maeneo mengine.

Aidha, alisema baadhi ya sababu zinazopelekea kuwepo kwa rushwa katika Halmashauri kuwa ni pamoja na Watumishi kutokuwa na maadili ya kazi na hivyo kujihusisha na vitendo vya rushwa kama ni hali ya kawaida, uwepo wa urasimu katika utoaji huduma kwa wananchi wanaofika katika Ofisi/Idara mbalimbali za Halmashauri, kukosekana kwa uwazi wakati wa utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri nako huchangia uwepo wa rushwa.

Bw. Uledi aliwataka Madiwani hao kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa dhidi ya Watumishi wasio waaminifu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Alibainisha kuwa, kifungu cha 39 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, namba

11 ya mwaka 2007 kinamtaka mtu yeyote, wakiwemo na Madiwani kutoa taarifa kwa TAKUKURU juu ya vitendo vya rushwa vilivyotokea au vinavyotakiwa kutokea.

Uwepo wa Kamati ya Maadili katika Halmashauri hiyo nao ulisisitizwa na Afisa huyo kama moja ya njia ya kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inakuwa na chombo cha ndani cha kushughulikia Watumishi wote watakaokwenda kinyume na maadili yao ya kazi.

Suala la uwazi na uwajibikaji nalo lilipewa msisitizo katika mafunzo hayo kwa Madiwani hao kutakiwa kuhakikisha kuwa uendeshaji wa Halmashauri yao unafuata misingi yote ya Utawala bora, ikiwemo na uwazi katika utekelezaji wa majukumu yake,

mfano utangazaji wa nafasi za ajira, utangazaji wa zabuni, usomaji wa mapato na matumizi

ya Halmashauri katika vikao mbalimbali na ushirikishwaji katika uandaaji wa mipango ya maendeleo.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Mkoa mpya wa Songwe wakifuatilia mada iliyotolewa na Afisa wa TAKUKURU, Bw.

Faraja Uledi (hayupo pichani) Januari 26 – 27, 2016.

Page 26: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa26

Toleo la Januari - Machi 2016Magazetini

Nipashe Uk.9 Januari 10, 2016

Uhuru Uk.5 Januari 6, 2016

Page 27: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa27

Toleo la Januari - Machi 2016 Shairi

1. Napenda kuwa salimu, ndugu wageni wa kwetu, Nina mengi ya muhimu, yaliyopo nchini mwetu, Rushwa ndo jambo muhimu, laumiza nafsi zetu, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

2. Tena rushwa ni hatari, kila sehemu walia, Ukienda hata hospitali, wananch itunalia, Tena hao madaktari, wanapenda kazia, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

3. Bora ingekuwa homa, ningejua nitapona, Rushwa ni zaidi ya homa, sijui lini utakoma, Tena ni tatizo mama, halifai kuwa hazina, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

4. Kwenye ofisi za umma, tena huko ndo chanzo, Tena hawana huruma, wamekuwa ndo kioo, Hadi tunaumia ona, sababu ya zako kero, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma

5. Mahakamani nako pia, wamekuwa vichokozi, Wananchi twaumia, sababu yao viongozi, Nashindwa hata kuongea, nahisi kutokwa na chozi, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

6. Ngono zembe imekuwa, cheti ili kuipata kazi, Kina baba nama binti, wamekuwa ni viongozi, Kutwa kushinda gesti, warubuni waziwazi, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

7. TAKUKURU twashukuru, elimu kutuletea, Sasa nimekuwa huru, mpaka haya kuongea, Tangu enzi za uhuru, rushwa inaendelea, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

8. Lakini cha kushangaza, wananchi tumelala, Kazi zetu zaangaza, hasa kwenye daladala, Napenda kutangaza, kwa kuimba na kwa ala, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

9. Wana - njoss tuwe mfano, kimkoa kitaifa, Tuepukane na mawazo, kwa kuondoa mahafaa, Yatupasa jino jino, kwa hakika tunafaa, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma.

10. Ninapenda kumalizia, na washukuruni nyote, Mengi nimezungumza, pasipo kumeza mate, TAKUKURU tunaweza, tuwajibikeni sisi sote, Wewe rushwa kitu gani, mbona huna huruma..

1. Vita ninaitangaza, yatisha kote nchini, Jambo moja la kukaza, hilo nawatajieni, Usipokee angaza, ndiyo ngao ya vitani, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

2. Askari ndiyo sisi, shika sime na marungu, Vita hii yatuasi, yavuma kama ukungu, Majasiri twaikasi, kwa hasira na machungu, Wananchi tupambane, vita hii kushinda. 3. Sitawaficha daima, wapendwa wa Tanzania, Yatupasa kusimama, na kupambana kwa nia, Kutoa pia yachoma, acha we utaumia, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

4. Mwenzangu nakung’amua, vita hii tushinde, TAKUKURU saidia, wananchi wakupenda , Umepembua mabua, Tanzania zote pande, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

5. Nimejawa ujasiri, siwezi hata yumbishwa, Hii wala siyo siri, adui yetu ni rushwa, Naujenga umahiri, nchini dhidi ya rushwa, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

6. Uchaguzi twaingia, acha chumvi pia pesa, Mana haya ndiyo njia, adui aja papasa, Jenga njema yako nia, TAKUKURU yakuasa, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

7. Adui huyu atisha, hapa kwetu Tanzania, TAKUKURU yaamsha, Mapambano kukazia, Tujitume kudumisha, nia kwalio sinzia, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

8. Lifungue blanketi, kauli yangu kwa leo, Ukaze lako manati, umpe adui ngeo, TAKUKURU kunja shati, lengo kuishika ngao, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

9. TAKUKURU twatumika, huku ulipo tutuma, Watu wameshaamka, rushwa wanaifakama, Shime wanalalamika, rushwa yavunja hekima, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

10. Wapo walioelimishwa, pande zote Tanzania, Yale waliyofundishwa, ndiyo wanapambania, Kwa vitendo kuoneshwa, kuonyesha yetu njia, Wananchi tupambane, vita hii kushinda.

KLABU YA WAPINGA RUSHWA SHULE YA SEKONDARI NJOMBE (NJOSS ANTI - CORRUPTION CLUB)

TANZANIA BILA RUSHWA INAWEZEKANA VITA TUPAMBANE

WEWE RUSHWA KITU GANI HUNA HURUMA

Page 28: ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Kamati ya Bunge … · 2019. 6. 13. · Jarida la Taasisi ya ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016 Jarida hili hutolewa na

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa28

Toleo la Januari - Machi 2016

KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Jarida la Taasisi ya

ISSN: 0856 - 7670 Toleo la Januari - Machi 2016

Jarida hili hutolewa na Kurugenzi ya Elimu kwa Umma ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

16 Mtaa wa Urambo, S. L. P 4865, Dar es Salaam. Simu: 022 2150043 - 6, Nukushi: 022 2150047

Wavuti:www.pccb.go.tz, Simu ya Bure:113, Baruapepe:[email protected]