Upload
vancong
View
717
Download
62
Embed Size (px)
Citation preview
Ijue Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya
Mifugo
(Livestock Training Agency - LITA)
Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training
Agency - LITA) ni miongoni mwa wakala tatu za Wizara ya
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Kuanzishwa kwa LITA ni moja
ya utekelezaji wa programu ya Mageuzi kwa Umma (PSRP II)
ya kuanzisha Wakala wa Serkali ambazo huchukuwa maju-
kumu ya kutekeleza kazi mbalimbali kwa niaba ya Serikali.
Lengo likiwa ni kuboresha utendaji na uwajibikaji katika
taasisi za umma. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo
ulianzishwa tarehe 1 September, 2011.
Wakala huu ulianzishwa kwa kuunganisha Vyuo Sita vya Ma-
funzo ya Mifugo (Livestock Training Institutes -LITIs) sam-
bamba na kupanua majukumu ambayo yalifanywa na LITIs,
kulingana na Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agen-
cies Act Cap 245 - R.E. 2009). Wakala ina malengo ya kutoa
mafunzo bora ya mifugo, kufanya tafiti, ushauri, na uzalishaji
wa mazao mbalimbali ya mifugo ili kukidhi mahitaji ndani na
nje ya nchi.
Mgeni rasmi Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya \mifugo na
|Uvuvi Mh. Dr. Titus Mlengeya Kamani (MB) akizindua
rasmi Baraza la Wafanyakazi wa LITA, Uzinduzi ulifanyika
tarehe 2/4/2014, Morogoro Hotel
Baraza la wafanyakazi wa LITA katika picha ya pamoja pamoja
Baraza la wafanyakazi wa LITA katika picha ya pamoja pamoja
na Mh. Dr. Titus Mlengeya Kamani (MB) baada ya uzinduzi wa
Balaza la Wafanyakazi wa LITA
Kiongozi Mkuu wa Wakala ni Mtendaji Mkuu (CEO) ambaye
huteuliwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Mtendaji
Mkuu anasaidiwa na wakurugenzi watatu ambao ni; Mkurugenzi
wa Uzalishaji (DP), Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Ushauri
(DTRC) na Mkurugenzi wa Huduma (DBS). Pia Wakala ina vitengo
huru viwili ambavyo ni; Ukaguzi wa ndani chini ya usimamizi wa
Mkaguzi Mkuu wa ndani (Principal Internal Auditor), na kitengo cha
Manunuzi kinachosimamiwa na Mkuu wa Manunuzi (Principal Sup-
plies Officer)
Wakala una Kampasi kuu sita na vituo viwili kama ifuatavyo;
Tengeru (Arusha) Mpwapwa (Dodoma), Morogoro, Madaba
(Ruvuma), Buhuri (Tanga), Temeke (Dar es Salaam), Kituo cha Ma-
buki (Mwanza) and Kituo cha Kikulula (Kagera). Katika ngazi ya
Kampasi Mtendaji Mkuu ana wakilishwa na Mkurugenzi wa Kam-
pasi au Mkuu wa Kituo husika. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya
Mifugo inayo Bodi ya ushauri (Ministerial Advisory Board) ambayo
humshauri Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
kuhusu muelekeo na utendaji wa wakala kwa ujumla.
Dira
Kuwa taasisi inayotoa mafunzo bora ya mifugo na huduma zina-
zoendana ifikapo 2025.
Majukumu ya Wakala
Jukumu kubwa la Wakala ni kutekeleza malengo ya maendeleo ya
sekta ya mifugo kama ilivyo ainishwa katika Sera ya Taifa ya Mifugo
ya mwaka 2006. (National Livestock Policy 2006) na Mpango
Mkakati wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Majukumu
ya Wakala ni kama ifuatavyo:
Kutoa mafunzo bora juu ya uzalishaji na afya ya mifugo;
Uzalishaji bora wa mifugo na mazao yake;
Uzalishaji bora wa mifugo na mazao yake;
Kutoa ushauri bora juu ya uzalishaji na afya ya mifugo;
Kufanya utafiti juu ya uzalishaji, afya ya mifugo na masuala
yanayohusiana.
Lengo Kuu
Lengo la LITA ni kutoa maarifa na ujuzi juu ya uendelezaji wa
mifugo kwa umma kwa njia ya mafunzo, utafiti na huduma za
ushauri pamoja na uzalishaji ili kuifanya sekta ya mifugo iwe
endelevu.
Malengo Mahsusi
Aidha, malengo mahsusi ya LITA ni kama ifuatavyo:
Kuongeza udahili wa wanafunzi wa muda mrefu na mfupi kwa
ajili ya program za mafunzo ya uzalishaji na afya ya mifugo;
Kuboresha na kuongeza uzalishaji katika mashamba ya Wakala;
Kufanya utafiti na huduma za ushauri bora juu ya uzalishaji na
afya ya mifugo;
Kuimarisha miundo mbinu ya kutoa mafunzo na uzalishaji;
Kuboresha usimamizi wa fedha na rasilimali za Wakala;
Kuimarisha usimamizi wa rasilimali watu;
Kuimarisha mifumo ya usimamizi wa utendaji katika wakala;
Kushughulikia masuala mtambuka mfano VVU/UKIMWI, jinsia,
utawala bora, na mazingira.
Jengo la Utawala la Kampasi ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo
Tengeru—Arusha
Udahili wa wanafunzi
Chati 1 hapo juu inaonyesha udahili wa wanafunzi tangu
mwaka 2000. Ni dhahiri kumekuwa na ongezeko la wana-
funzi waliodahiliwa tangu LITA ilipoanzishwa. Idadi ya wana-
funzi waliodahiliwa iliongezeka toka 1622 (2011) mpaka
2216 (2013). Wakala inakusudia kuongeza idadi ya udahili
mwaka hadi mwaka kulingana na upanuzi na ukarabati wa
miundo mbinu katika Vituo/Kampasi zake, sambamba na
kuongeza idadi ya wakufunzi.
Idadi ya wahitimu tangu mwaka 1998
Chati 2 hapo juu inaonyesha idadi ya wanafunzi walio-
hitimu tangu mwaka 2000, ni dhahiri kwamba idadi ya wa-
hitimu imeongezeka tangu Wakala ilipoanzishwa. Miradi
mbalimbali imetekelezwa katika Kampasi za LITA mfano
ujenzi wa hosteli na madarasa pamoja na ukarabati. Maa-
bara mpya zimejengwa na zingine kukarabatiwa ikiwa ni
pamoja na kuweka vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa ma-
funzo bora.
Wakala una mikakati ya kujenga madarasa, hostel na maa-
bara mpya ili kuongeza udahili. Vitengo vya uzalishaji vitai-
marishwa kwa ajli ya mafunzo kwa vitendo na kuongeza
pato la Wakala. Kufikia malengo yake Wakala unatumia
mikakati mbalimbali ili kuiwezesha Wakala kukua.
Madarasa ya Kampasi ya Temeke iliyoko Dar es Sa-
laam
Kufikia malengo yake Wakala unatumia mikakati
mbalimbali ili kuiwezesha Wakala kukua. Umuhimu
wa kuimarishwa kwa LITA na ungezeko la udahili ni
dhahiri, kwani sekta ya mifugo nchini inahitaji maaf-
iza ugani wa mifugo 17,325, wakati walioko ni 5,157
(30%). Lengo la Wakala ni udahili wa wanafunzi 5,000
kwa mwaka ifikapo mwaka 2016.
Madarasa ya Kampasi ya Temeke iliyoko Dar es Sa-
laam
Kuboresha mafunzo ni miongoni mwa jitihada za Wa-
ziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.
Dr. Titus Mlengeya Kamani (MB). Picha hapo juu ni
Waziri (kulia) akielezewa jambo na Kaimu Mtendaji
Mkuu Mama M. Pallangyo, wakati waziri alipokitem-
belea Kituo cha Kikulula
Kozi zinazotolewa na Wakala wa Vyuo vya Mafunzo
Stashahada ya uendeshaji wa nyanda za malisho na udhibiti
wa ndorobo (DRMTC)
Stashahada ya uendeshaji wa nyanda za malisho na
udhibiti wa ndorobo (DRMTC)
Astashahada ya afya na uzalishaji wa mifugo –
CAHP
Astashahada ya ufundi sanifu wa maabara ya vet-
erinari – CVLT Kozi maalumu zinatolewa pia kulin-
gana na mahitaji ya wateja
Wanafunzi wa Kampasi ya Tengeru katika ma-
funzo kwa vitendo
Wanafunzi wa Kampasi ya Tengeru wakichoma
sindano ya madini ya chuma kwa vitoto vya ngu-
ruwe na kukata meno (tooth clipping)
Kozi fupi kwa wakulima wafugaji zinazotolewa na
LITA:
Ufugaji bora wa ngómbe wa maziwa;
Ufugaji bora wa ngómbe wa nyama;
Unenepeshaji wa ngómbe wa nyama (Beef Fatten-
ing);
Ufugaji bora wa nguruwe;
Ufugaji bora wa mbuzi wa maziwa;
Ufugaji bora wa kuku wa kisasa na kienyeji;
Usindikaji wa maziwa;
Uboreshaji wa ngozi na mazao yake;
Kutoa Mafunzo kwa Wakulima-wafugaji
Kampasi za LITA zinatoa mafunzo kwa wakulima wa-
fugaji tangu mwaka 1984, wengi kati yao wakiwa wa-
kulima wadogo toka maeneo mbalimbali ya nchi ya
Tanzania. Wakulima-wafugaji huendesha shughuli za
kilimo na ufugaji ili waweze kujikimu katika maisha
yao ya kila siku. Wengi wao hupata tatizo la uhaba
wa chakula kila mwaka haswa wakati wa kiangazi.
Mafunzo kwa wakulima-wafugaji yameleta manufaa
kwao kwani yameendeshwa kwa vitendo (kujifunza
kwa kufanya).
Mafunzo kwa Wafugaji
Wakulima wafugaji hupata mafunzo katika Kampasi
za Wakala katika maeneo mbalimbali ya ufugaji
mfano ufugaji bora wa ngómbe wa maziwa, kusindika
maziwa, uboreshaji wa malisho, ufugaji bora wa
kuku, Uhudumu wa afya ya mifugo katika jamii,
kilimo hai n.k. Mafanikio katika kozi hizo fupi yanato-
kana na ushirikiano wa LITA na wadau wengine
mfano World Vision, KKKT-Mradi wa Mitamba, Heifer
International Tanzania, Halmashauri mbalimbali za
miji Tanzania n.k. LITA inakusudia kuimarisha kozi za
wakulima-wafugaji kwa kupanua na kukarabati mi-
undo mbinu yake sambamba na kutafuta wadau
mbalimbali ambao wanaweza kufadhili mafunzo kwa
wakulima-wafugaji. Mafunzo kwa wakulima-wafugaji
yameboresha maisha ya wafugaji kutokana na uzal-
ishaji kuongezeka, na hivyo kuongeza kipato na
usalama wa chakula katika kaya.
Uzalishaji katika Vitengo na Mashamba ya LITA
LITA ina eneo la Hekari 4,731.4 ambazo ziko
kwenye Kampasi mbalimbali za LITA; Tengeru
(320.4 ha), Mpwapwa (500 ha), Morogoro (50
ha), Madaba (1,400 ha), Buhuri (855 ha), Temeke
(6 ha), Mabuki (500 ha) and Kikulula (1,600 ha).
Mashamba ya Wakala hutumika kuzalisha mifugo
mfano; ngómbe wa maziwa, ngómbe wa wan-
yama, kondoo, mbuzi, mabata, nguruwe, farasi.
Mashamba hayo pia hutumika kuzalisha malisho
kwa ajili ya kulishia wa mifugo pamoja na kuuza
ziada kwa wafugaji walio jirani. Mazao ya chakula
ya aina mbalimbali pia huzalishwa katika
mashamba ya LITA mfano mahindi, alizeti na ma-
harawe. Mashamba ya Wakala pia yana misitu ya
asili na ya kupandwa.
Ngómbe wa maziwa kampasi ya Tengeru
Uzalishaji wa Mabata Kampasi ya Mpwapwa
Uzalishaji Malisho
Ili uzalishaji wa ngómbe wa maziwa na nyama una
tija endapo malisho ya kutosha yanazalishwa
kufikia kiwango cha mahitaji ya mifugo. Ili kukidhi
mahitaji ya msingi ya mnyama LITA imetekeleza
miradi ya umwagiliaji ili kuwezesha uzalishaji wa
malisho ya kutosha hasa katika misimu ya kian-
gazi. Miradi ya umwagiliaji wa malisho umeon-
geza na kuboresha uzalishaji wa malisho ya kuto-
sha na kupunguza athari za kiangazi na ukame.
Ngómbe wameweza kutoa maziwa mengi bila ku-
pungua uzito katika msimu wa kiangazi. Pia mal-
ekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika pato la taifa na
haswa kwa jamii zilizoko vijijini, hivyo kuimarishwa
kwa sekta hii kutaleta mchango mkubwa kwa maisha
vijijini na umma wa Tanzania kwa ujumla. Uzalishaji
wa mifugo ulio thabiti nchini utaiwezesha jamii ya
Tanzania kuwa na maisha bora, na kustahimili changa-
moto za ukame utokanao na mabadiliko ya tabia nchi
ambazo hufanya mazao kukauka shambani au ku-
sombwa na mafuriko wakati wa mvua nyingi. Hivyo
uzalishaji bora wa mifugo huchangia kwa kiasi ki-
kubwa usalama wa chakula katika kaya.
Uzalishaji wa malisho Kampasi ya Tengeru
Utengenezaji wa Hei (Hay baling) Kampasi ya
Morogoro
Sera ya matokeo makubwa sasa (BRN) inaweza pia
kuweka mipango mkakati ya kuongeza uzalishaji wa
malisho nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya
umwagiliaji wa malisho. Kwa kufanya hivyo malisho
yatapatikana wakati wa kiangazi. Mipango hiyo
inaweza kwenda sambamba na kuhifadhi pamoja na
kumboresha masalia ya mazao mbalimbali mfano ma-
salia ya maharagwe, mahindi, ngano n.k. Mafunzo kwa
wakulima-wafugaji wadogo juu ya uzalishaji wa mal-
isho bora, kuhifadhi/kuboresha masalia ya mazao ita-
saidia kupunguza athari za ukame kwa mifugo. Mifugo
ikiwa na afya nzuri hata wakati wa kiangazi itawezesha
ngómbe wa nyama kupata bei nzuri na wale wa
maziwa kuendelea kutoa maziwa vizuri. Unenepeshaji
Dume la Mbegu – kwenye Kampasi ya Buhuri
Utafiti na Huduma za Ushauri
Utafiti pamoja na huduma za Ushauri juu ya Afya
na Uzalishaji wa Mifugo ni muhimu sana katika
kuboresha na kuleta maendeleo katika sekta ya
mifugo. LITA ni mdau mpya katika nyanja ya uta-
fiti kwani kabla ya LITA kuanzishwa LITI haziku-
jishughulisha na kazi za utafiti. Baada ya LITA
kuanzishwa na kuongeza majukumu yake utafiti
imekuwa ni moja ya majukumu ya Wakala. Hata
hivyo shughuli za utafiti zinahitaji fedha nyingi,
hivyo ushirikiano na taasisi zingine zinazofadhili
tafiti ni muhimu. Katika kufanya utafiti na
huduma za ushauri Wakala utaongeza kasi ya ku-
leta maendeleo katika sekta ya mifugo. Wakala
imefanya mchakato wa kuboresha na kuongeza
uwezo wa wakufunzi wake kwa kuwapa mafunzo
ya muda mfupi.
LITA inatoa huduma ya ushauri katika maeneo
mbalimbali ya ujuzi kama ifuatavyo:
Ufugaji wa ngombe wa maziwa na nyama,
Ufugaji wa mbuzi wa maziwa na nyama,
Usindikaji wa maziwa,
Kutathimini miradi kwa mbinu shirikishi,
Mafunzo ya mbinu bora za ufundishaji kwa wa-
kufunzi,
Jinsia na maendeleo
Uzalishaji wa mifugo na hifadhi ya mazingira,
Ufugaji/kilimo hai
LITA inafanya tafiti katika maeneo mbalimbali
kama ifuatavyo:
Kuboresha uzalishaji wa kuku wa kienyeji,
Kuboresha afya na uzalishaji wa mifugo,
Maendeleo endelevu ya sekta ya mifugo,
Mifumo ya masoko na kuongeza thamani,
Picha ya pamoja baada ya kuhitimu mafunzo ya kuende-
sha tafiti
Vituo na Kampasi za LITA
SN Kampasi/Kituo
Mkoa/Eneo
Anuani
KAMPASI YA TENGERU
ARUMERU ARUSHA
S. L. P. 3101, Arusha
KAMPASI YA MPWAPWA
S. L. P. 51, Mpwapwa
DODOMA
KAMPASI YA MOROGORO
S. L. P.603, Morogoro
KAMPASI YA MADABA
S.L.P 368
MADABA SONGEA
KAMPASI YA BUHURI
S.L.P
TANGA
KAMPASI YA TENMEKE
S.L.P
TENEKE - VETENARY