32
HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. SAID ALI MBAROUK (MBM) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA 2011/2012 1.0 UTANGULIZI 1.1 Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako tukufu, likae kama Kamati ili kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2011/2012. 1.2 Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana tukiwa katika hali ya afya na kutujaalia amani na utulivu katika nchi yetu. Kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Zanzibar akiwa Rais wa Awamu ya Saba chini ya Serikali yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa. Pia napenda kuwapongeza Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Kwa hakika kikosi hichi cha viongozi hawa watatu wa juu wa nchi yetu kinaleta matumaini makubwa kwa wananchi wote na timu inayoheshimika sana hata nje ya nchi yetu. 1.3 Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuchaguliwa tena kwa mara nyengine kuliongoza Baraza hili na kwa juhudi zako za makusudi unazochukua kuliendesha vizuri Baraza hili ukisaidiana na Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa wenyeviti wa Baraza hili, Katibu wa Baraza na maafisa wa Baraza wanaokusaidia katika kazi zako. Aidha, napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Baraza pamoja na Wajumbe wote kwa michango yao na ushirikiano mzuri wanaotoa kwa Wizara yangu. Kamati hizi zimekuwa ni chachu muhimu sana katika kushajiisha wafanyakazi wa Wizara yangu pamoja na wafugaji, wavuvi, wakulima wa mwani na wadau wengine wa sekta hizi katika kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi. 1.4 Mheshimiwa Spika, niruhusu kutoa shukrani za pekee na kuipongeza Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari ya Baraza la Wawakilishi, kwa ushauri na maelekezo yao ya msingi na

HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI,MHE. SAID ALI MBAROUK (MBM)

KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YAWIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA 2011/2012

1.0 UTANGULIZI

1.1 Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naomba kutoa hoja kwambaBaraza lako tukufu, likae kama Kamati ili kupokea, kujadili nakupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo naUvuvi kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

1.2 Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwakutuwezesha kukutana tukiwa katika hali ya afya na kutujaalia amanina utulivu katika nchi yetu. Kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara yaMifugo na Uvuvi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Zanzibarakiwa Rais wa Awamu ya Saba chini ya Serikali yenye mfumo waUmoja wa Kitaifa. Pia napenda kuwapongeza Mheshimiwa MaalimSeif Sharif Hamad kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Raisna Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kwa kuteuliwa kuwa Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar. Kwa hakika kikosi hichi cha viongozi hawawatatu wa juu wa nchi yetu kinaleta matumaini makubwa kwawananchi wote na timu inayoheshimika sana hata nje ya nchi yetu.

1.3 Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi kwakuchaguliwa tena kwa mara nyengine kuliongoza Baraza hili na kwajuhudi zako za makusudi unazochukua kuliendesha vizuri Baraza hiliukisaidiana na Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa wenyevitiwa Baraza hili, Katibu wa Baraza na maafisa wa Barazawanaokusaidia katika kazi zako. Aidha, napenda kuwashukuruWaheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Baraza pamojana Wajumbe wote kwa michango yao na ushirikiano mzuri wanaotoakwa Wizara yangu. Kamati hizi zimekuwa ni chachu muhimu sanakatika kushajiisha wafanyakazi wa Wizara yangu pamoja nawafugaji, wavuvi, wakulima wa mwani na wadau wengine wa sektahizi katika kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi.

1.4 Mheshimiwa Spika, niruhusu kutoa shukrani za pekee nakuipongeza Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari yaBaraza la Wawakilishi, kwa ushauri na maelekezo yao ya msingi na

Page 2: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

busara zao katika kuielekeza Wizara yangu. Uzoefu wa siku nyingiwa Mwenyekiti wa Kamati hii Mheshimiwa Bi Asha Bakar Makamena umahiri wa wajumbe wa Kamati hii unanisaidia sana mimi nawatendaji wa Wizara yangu.

1.5 Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kukipongezaChama changu cha Wananchi CUF kwa kunipa imani nakupendekeza jina langu katika nafasi ya kuwa msimamizi miongonimwa Wizara ndani ya Serikali hii yenye mfumo wa umoja wa Kitaifa;Aidha namshukuru Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein kwa kukubalianana mapendekezo hayo, kwa hakika mimi na kwa niaba ya wananchiwa Jimbo la Gando kupata fursa hii ya kuwatumikia Wazanzibarikatika serikali yenye mfumo huu ni heshima kubwa na kwaWazanzibari nina deni la utumishi kwao.

1.6 Mheshimiwa Spika, kama tunavyojua, Serikali yetu ya Mapinduzi yaZanzibar ya Awamu ya Saba imeanzisha Wizara hii ya Mifugo naUvuvi kwa lengo la kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi kwa ufanisizaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao yamifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguzaumasikini na hatimae kuongeza pato la Taifa.

1.7 Mheshimiwa Spika, Mapinduzi katika Sekta ya Uvuvi na Mifugokama yalivyoelekezwa katika hotuba muhimu ya Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uzinduzi wa Baraza laWawakilishi hapo Novemba 2010, ambayo ilizingatia Dira, Ilani,Mikakati ya kupunguza umasikini, Sera na ahadi mbali mbali ninyenzo zitazotumika katika kufanikisha malengo yetu.

2.0 HALI YA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI NCHINI2.1 Sekta ya Mifugo2.1.1 Mafanikio katika sekta ya mifugo

2.1.1.1 Mheshimiwa Spika, sekta ya mifugo imeweza kupata mafanikiokadhaa kati yao ni kama yafuatayo: -

(a) Kupatikana kwa mtambo wa kuzalisha "liquid nitrogen". Hiiimesababisha kiwango cha upandishaji ng'ombe kwasindano kuongezeka kutoka ng'ombe 500 hadi kufikiang'ombe 1,275 kwa mwaka.

Page 3: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(b) Kuanzishwa viwanda vidogo vidogo vya usindikaji wamaziwa ambavyo vinazalisha samli, siagi, mtindi na maziwaya kunywa.

(c) Muamko wa ufugaji wa mbuzi wa maziwa umeongezekakwa wananchi wengi na kupelekea ongezeko la mahitaji yambuzi hao.

(d) Muamko wa wafugaji kuwapatia wanyama wao hudumabora za kinga na tiba umeongezeka. Hivyo kupunguzahasara na vifo vya mifugo kwa wafugaji

(e) Kuongezeka kwa muamko wa wafugaji juu ya matunzobora ya wanyama kwa kujali haki zao za kuwapatia mahitajimuhimu wanayostahili.

2.1.2 Hali ya sekta ya mifugo

2.1.2.1 Mheshimiwa Spika, sekta ya mifugo ina umuhimu mkubwakiuchumi hapa Zanzibar. Mchango wa sekta hiyo katika pato laTaifa umeongezeka kutoka asilimia 4.5 hadi kufikia asilimia 4.7sawa na ongezeko la asilimia 0.2. Hii inatokana na kuongezekakwa uzalishaji wa mazao ya mifugo kulikotokana na kuongezekakwa mahitaji ya bidhaa hizo katika soko la ndani. Kwa hivi sasajumla ya kaya 45,684 zinajishughulisha na ufugaji wa ng'ombewakati kaya 78,428 zinajishughulisha na ufugaji wa kuku.Kutokana na kipaumbele iliyopewa Wizara yangu, na kwa mikakatituliyoiweka, nina matumaini makubwa kuwa Wizara yangu itainuahali za maisha ya wananchi pamoja na kukuza uchumi wa nchikwa ujumla.

2.1.2.2 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeandaa mikakati maalum yakuinua zaidi sekta hii hapa nchini ikiwemo kuzidisha ushauri wakitaalamu kwa wafugaji, sambamba na huduma bora za utabibuwa mifugo zitakazopelekea kuongeza idadi ya mifugo na ubora wamazao ya mifugo. Wizara yangu inafanya juhudi za makusudikatika kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo vyausindikaji wa mazao ya mifugo ikiwemo kuku na maziwa. Hivi sasajuhudi zinafanywa kushajiisha wawekezaji wa kati na wakubwa wandani na wa nje kuwekeza katika sekta ya mifugo na kuwekautaratibu wa ufugaji wa makubaliano "contract farming" kwa

Page 4: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

madhumuni ya kulinda soko la ndani na kuisaidia Serikali katikakuwaendeleza wafugaji wadogo wadogo.

2.1.2.3 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatilia mkazo sana uanzishajiwa tafiti ndogo ndogo zinazowashirikisha wafugaji wenyewe ilikupata mbinu bora za uzalishaji na mifugo bora yenye sifa zauzalishaji zaidi na kuhimili maradhi yaliopo nchini.

2.1.3 Changamoto katika sekta ya mifugo

2.1.3.1 Mheshimiwa Spika, sekta ya mifugo inakabiliwa na changamotombali mbali zikiwemo uhaba wa nyenzo za kutolea elimu kwawafugaji ikiwemo vyombo vya usafiri na uchache wa wataalamuambao wengi wao wana elimu ndogo. Aidha, taaluma ndogo kwawafugaji, uwezo mdogo wa kununulia teknolojia na pembejeo kwawafugaji na wasindikaji, maradhi ya mifugo, nasaba duni zamifugo yetu kiuzalishaji, uhaba wa malisho, wanajamii kukhalifusheria za mifugo na utesaji wa wanyama ni miongoni mwachangamoto zinazoikabili sekta hii. Wizara yangu tayari imeandaamikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.

2.1.4 Mtazamo wa baadae katika sekta ya mifugo

2.1.4.1 Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuimarisha sekta ya mifugonchini, Wizara yangu imejizatiti kuongeza ufanisi wa watendajikwa kuwawekea mazingira mazuri ya kazi ikiwemo usafiri, vifaavya kutendea kazi, kuwaendeleza kitaaluma wafanyakazi waliopopamoja na kuwashajiisha vijana kuendelea na masomo yao katikafani za mifugo. Aidha, Wizara yangu inalenga kuboresha mfumowa elimu ya ushauri kwa wafugaji ikiwemo kuendeleza skuli zawafugaji, kuwaunganisha wafugaji na taasisi za fedha, nakuanzisha vituo vya kujiendeleza kitaaluma kwa wafugaji hao.

2.1.4.2 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendelea kuhamasisha jamiijuu ya utumiaji wa gesi inayotokana na samadi ambao unachangiakwa kiasi kikubwa kuhifadhi mazingira kwa kupunguza matumizimakubwa ya kuni na mkaa katika visiwa vyetu. Hali hii itapunguzasana athari ya mabadiliko ya tabia nchi kunakotokana na ukatajimkubwa wa miti.

2.1.4.3 Mheshimiwa Spika, katika kutilia mkazo masuala ya utafitiWizara yangu imejipanga kuanzisha programu maalumu yakuimarisha miundombinu ya mifugo pamoja na kuhimiza tafiti

Page 5: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

mbali mbali za mifugo kwa lengo la kubadilisha mfumo wa ufugajiuliopo hivi sasa ili uwe wa kibiashara zaidi.

2.1.4.4 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inakusudia kuimarishamahusiano zaidi kati ya Wizara, wafugaji wadogo wadogo na wakati, wafanyabiashara wa mazao ya mifugo, wawekezaji wa ndanina nje, Jumuiya za kikanda na Kimataifa zinazohusiana na sektaya mifugo, pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuongezauzalishaji na tija. Aidha, Wizara yangu itashirikiana na ZAASO,ZALWEDA, WSPA na Jumuiya nyengine za kitaifa na kimataifazinazotetea haki na ustawi wa wanyama.

2.2 Sekta ya Uvuvi

2.2.1 Mafanikio katika sekta ya uvuvi

2.2.1.1 Mheshimiwa Spika, Sekta ya uvuvi imepata mafanikio makubwakatika kipindi hichi. Miongoni mwa mafanikio ya sekta ya uvuvi nikama yafuatayo: -

(a) Kuongezeka kwa wavuvi na kiwango cha samakiwanaovuliwa,

(b) Kuongezeka ukulima wa mwani, ufugaji wa samaki namazao mengine ya baharini.

(c) Kuongezeka kwa mchango wa sekta ya uvuvi katika pato laTaifa kutoka asilimia 5.2 mwaka 2009 hadi asilimia 6.1mwaka 2010.

(d) Jumla ya wanajamii 200 kati ya hao, 127 wanawake na 73wanaume wamepatiwa mafunzo mbali mbali yakiwemo yaujasiriamali, uongozi, usimamizi na uendeshaji wa miradi.Mafunzo hayo yalitolewa kwa wanajamii wote wa ukandawa pwani hasa wanaotekeleza miradi yao.

(e) Kuongezeka kwa kiwango cha zana za kuvulia kwawanajamii, ambapo jumla ya mashua 17 za uvuvi na nyavuza kuvulia 17 zilikabidhiwa kwa vikundi 22 kutoka vijiji 31vya Unguja. Kwa upande wa Pemba jumla ya vikundi 21vinavyojishughulisha na shughuli za uvuvi, upandaji miti naufugaji nyuki vimepatiwa vifaa. Katika msaada huo jumla yamashua 18 na mashine 18 zilitolewa. Aidha, ujenzi wamasoko ya kuuzia samaki katika maeneo mbali mbali hapa

Page 6: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

nchini kama vile Nungwi, Matemwe na Pwani Mchanganikwa upande wa Unguja na Ole, Mvumoni, Wesha, na Kilindikwa upande wa Pemba ulitekelezwa, Na ujenzi wa soko laTumbe unaendelea.

(f) Mafanikio makubwa yamepatikana kwa kuwepo maeneo yahifadhi yanayopelekea matumizi mazuri na endelevu yarasilimali za baharini pamoja na upatikanaji wa mapatoyanayotokana na rasilimali hizo ambapo jumla ya shilingi167,396,150 zilipatikana.

(g) Kuongezeka kwa shughuli za ufugaji wa samaki, ambapojumla ya vikundi 35 kwa Unguja na 40 kwa Pemba vyaufugaji wa samaki, kaa, chaza na lulu vimeanzishwa.

2.2.1.2 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imepata mshauri muelekezikutoka FAO kutupatia ushauri juu ya namna bora ya ufugaji naukulima wa mazao ya baharini na hivi sasa tunasubiri ripoti yake.

2.2.1.3 Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Baraza lako Tukufu kuwahivi sasa makampuni yote ya ununuzi wa mwani nchiniyamekubali kuongeza bei ya mwani mwembamba kutoka Shilingi250 kwa kilo na kununua kwa Shilingi 400 kwa kilo. Hivi sasawakulima wa mwani nchini wameshaanza kufaidika na bei hiyo.

2.2.1.4 Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mamlaka ya KusimamiaUvuvi wa Bahari Kuu mafanikio kadhaa yamepatikana kamayanavyojionyesha hapo chini:-

(a) Kupatikana kwa jengo la ofisi ya Mamlaka ambalolinategemewa kumalizika hivi karibuni.

(b) Kufanya doria za angani na majini kwa kushirikiana naKMKM, Polisi Marine, Jeshi la Majini na Anga. Hii imesaidiakupunguza uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira.

(c) Kusimamia utoaji wa leseni kwa pamoja za uvuvi wa BahariKuu na kusimamia mgao wake.

2.2.2 Hali ya sekta ya uvuvi

2.2.2.1 Mheshimiwa Spika, hali ya sekta ya uvuvi kwa sasa iko kamaifuatavyo: -

Page 7: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(a) Kiwango cha uvuvi wa samaki kimeongezeka kutoka tani25,396 zenye thamani ya shilingi 47,714,069,596 mwaka2009 hadi kufikia tani 25,693,080 zenye thamani ya shilingi61,784,309,912 kwa mwaka 2010 zilizouzwa na wavuvi.

(b) Ukulima wa mwani umeongezeka kutoka tani 10,248 zenyethamani ya shilingi 1,665,542,469 katika mwaka 2009 hadikufikia tani 12,500 zenye thamani ya shilingi 3,125,000,000kwa mwaka 2010 zilizouzwa na wakulima wa mwani.

(c) Mchango wa sekta katika pato la Taifa umeongezeka kutokaasilimia 5.2 kwa mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 6.1 kwamwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 0.9

2.2.3 Changamoto katika sekta ya uvuvi

2.2.3.1 Mheshimiwa Spika, sekta ya uvuvi inakabiliwa na changamotombalimbali zikiwemo: -

(a) Kuongezeka kwa wavuvi kutoka ndani na nje ya Zanzibarkatika maeneo ya hifadhi, kuwepo kwa wavuviwanaojihusisha na uvuvi haramu na kukithiri ukataji wamikoko katika fukwe unaopelekea kupunguza mazalia yasamaki.

(b) Mabadiliko ya hali ya hewa (kuongezeka kwa joto baharini)kunakosababisha kupauka kwa matumbawe "coralbleaching" inayosababisha mtawanyiko wa samaki baharini.

(c) Kuwepo migogoro baina ya wavuvi, wawekezaji nawakulima wa mwani, kunaathiri sana shughuli za uvuvi.

(d) Uwezo mdogo wa jamii kuwekeza katika ufugaji wa mazaoya baharini, ukosefu wa utaalamu na uelewa katika fani yaufugaji wa mazao ya baharini na uhaba wa wafanyakaziwataalamu wa fani ya mazao ya baharini.

(e) Kupungua kwa mapato ya Bahari Kuu kunakotokana natishio la uharamia baharini.

(f) Kutokuwa na wavuvi wazawa wanaovua kwenye Ukanda waUchumi wa Bahari Kuu.

Page 8: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(g) Kutokuwa na miundo mbinu ya uvuvi wa bahari kuuinayosababisha meli zinazopewa leseni za uvuvi wa baharikuu kutolazimika kutia nanga kwenye gati zetu, jambo hilihukosesha nchi yetu mapato mengi.

2.2.4 Mtazamo wa baadae katika sekta ya uvuvi

2.2.4.1 Mheshimiwa Spika, mtazamo wa baadae katika sekta ya uvuvi nikuendeleza uvuvi kwa kushajiisha uanzishaji wa kampuni zawazawa za uvuvi na ukulima wa mazao ya baharini kwa vikundi.Kutafuta njia na mbinu zitakazowezesha wavuvi wetu kuvua katikaukanda wa uchumi pamoja na kuhamasisha wawekezaji kutokanje kwa ajili ya uvuvi wa viwanda. Aidha kufanya tafiti ili kutambuamaeneo bora ya uvuvi (potential fishing grounds).

2.2.4.2 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inakusudia kuimarishamahusiano zaidi kati ya Wizara, wavuvi, wakulima wa mwani,wafanyabiashara wa mazao ya baharini, Taasisi ya Sayansi zaBahari, Jumuiya za kikanda na Kimataifa zinazohusiana na bahari,pamoja na wadau wengine ili kuongeza uzalishaji na tija. Aidha,ufugaji wa samaki utaimarishwa badala ya kutegemea samakiwanaovuliwa moja kwa moja kutoka baharini. Miundombinu nataaluma ya ufugaji wa mazao mengine ya baharini itaimarishwakwa lengo la kuongeza tija kwa wafugaji wa mazao hayo na kwakuangalia ubora wa viwango vya mazao ya bahariniyanayozalishwa.

3.0 TAARIFA YA MALENGO NA UTEKELEZAJI KWA MWAKA2010/2011 NA MALENGO YA MWAKA 2011/2012

3.1 Mheshimiwa Spika, kufuatia mabadiliko ya muundo wa Wizara,Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeundwa na Idara sita ambazo niIdara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Uendeshaji naUtumishi, Idara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo, Idara yaUzalishaji Mifugo, Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Idara ya Mazaoya Baharini na Ofisi Kuu ya Wizara Pemba.

3.2 IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

3.2.1 Majukumu ya Idara

Page 9: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

3.2.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara hii ina wajibu wa kuratibu, kubuni nakuandaa mipango ya maendeleo ya sekta ya mifugo na uvuvi,kusimamia, kutayarisha na kufanya mapitio ya Sera, Mikakati,Programu na Miradi ya Maendeleo kwa sekta hizi na kuratibu kaziza utafiti. Vilevile Idara hii ni kiungo baina ya taasisi za ndani, zakikanda na za kimataifa.

3.2.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.2.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idara yaSera na Mipango, chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Mifugo naMazingira kwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi ilikuwa na malengoyafuatayo:-

(a) Kukamilisha taratibu za uwasilishaji sera na sheria mbalimbali za Wizara na kusimamia utekelezaji wake.

(b) Kuratibu mashirikiano na taasisi mbali mbali za kitaifa nakimataifa na utayarishaji wa miradi.

(c) Kufanya mapitio ya mpango mkakati wa sekta ya mifugo nauvuvi (Strategic Plan).

3.2.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.2.3.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idarailitekeleza mambo yafuatayo:-

(a) Sera mpya ya mifugo imeshatayarishwa na kuwasilishwakatika ngazi za juu za uongozi wa Wizara.

(b) Idara imeandaa mapendekezo ya miradi ya miundo mbinuya uvuvi na mifugo, uchambuzi yakinifu wa ufugaji wasamaki, viwanda vya ukaushaji wa dagaa pamoja naprogramu ya kuwaendeleza wavuvi Zanzibar nakuziwasilisha Serikalini na kwa washirika wa maendeleo.

(c) Rasimu ya mpango mkakati wa sekta ya mifugo na uvuviimeshatayarishwa na kuwasilishwa Ofisi ya Rais, Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo.

(d) Idara imefanya mapitio ya sekta (sector review) ya mifugona uvuvi.

Page 10: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(e) Uchambuzi yakinifu wa ufugaji wa samaki na viumbe vyabaharini (feasibility study on marine aquaculture)umeshafanywa kwa kushirikiana na Idara ya Mazao yaBaharini pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umojawa Mataifa (FAO).

3.2.4 Malengo ya Mwaka 2011/2012

3.2.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 Idara inalengakutekeleza malengo yafuatayo:-

(a) Kukamilisha taratibu za uwasilishaji wa Sera ya Mifugo nakuzipitia sheria ndogo ndogo za mifugo na uvuvi pamoja nakusimamia utekelezaji wake.

(b) Kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Uvuvi,kutayarisha Mpango Mkuu wa Kuendeleza Uvuvi (FisheriesMaster Plan).

(c) Kuimarisha ukusanyaji wa takwimu na mapato yatokanayona sekta za mifugo na uvuvi.

(d) Kuanzisha kitengo cha habari, pamoja na kutoa nakala 1,000za "Jarida la Mvuvi na Mfugaji" na kulisambaza kwa wadau.

(e) Kuratibu mashirikiano na taasisi mbali mbali za Kitaifa naKimataifa.

(f) Kubuni na kutayarisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

(g) Kuratibu kazi za utafiti za sekta ya mifugo na uvuvi.

3.2.4.2 Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idaraitatekeleza mradi mmoja wa Kuimarisha Miundo Mbinu ya Mifugo,ambao utaendeshwa kwa fedha za Serikali (Kiambatisho na. 1)

3.2.4.3 Mheshimwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idara yaMipango, Sera na Utafiti kwa Unguja inaombewa jumla ya shilingi327,462,819 kwa kazi za kawaida na shilingi 243,000,000 kwakazi za maendeleo. Kati ya fedha za kazi za kawaida shilingi106,009,000 ni kwa matumizi mengineyo.

Page 11: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

3.3 IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI3.3.1 Majukumu ya Idara

3.3.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara hii ndio kiungo kikuu cha Wizara hasakatika kusimamia na kuratibu taasisi za Wizara, kusimamiauendeshaji wa kazi za kila siku za Wizara ikiwa ni pamoja nauwekaji wa kumbukumbu za wafanyakazi wa Wizara, utunzaji wamali za Serikali, kuhakikisha haki na wajibu wa wafanyakazipamoja na kufanya jitihada za kuwaendeleza kitaalumawafanyakazi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Aidha, kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na UtawalaBora, Idara inasimamia uajiri na maslahi ya wafanyakazi.

3.3.1.2 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa hivi sasa ina jumla yawafanyakazi 731, kati ya hao, wenye elimu ya kiwango chashahada ya kwanza kwenda juu ni 38 tu (Kiambatisho na. 6). Hiiinaonesha dhahiri idadi ndogo ya wataalamu tuliyonayoikilinganishwa na wingi wa wafugaji, wavuvi na wakulima wamwani wenye matarajio makubwa ya kupata huduma kutokakwetu. Wizara kwa sasa inajipanga kuwaendeleza wafanyakazikielimu pamoja na kuajiri wataalamu zaidi.

3.3.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.3.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idara yaUendeshaji na Utumishi ambayo ilikuwa ni sehemu ya Idara yaSera na Mipango ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Mifugo naMazingira ilikuwa na lengo la kuendelea kutoa mafunzo kwawafanyakazi kwa mujibu wa mahitaji ya taasisi zilizo chini yaWizara.

3.3.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.3.3.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idara yaUendeshaji na Utumishi ilitekeleza yafuatayo:-

(a) Jumla ya wafanyakazi 42 wanaendelea na masomo katikavyuo vya nje na ndani. Kati ya hao 11 ni wa kiwango chacheti, nane stashahada, 21 shahada ya kwanza na wawili nishahada ya pili. Miongoni mwao 15 ni wanawake na 27 niwanaume (Kiambatisho na. 7).

Page 12: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(b) Kusimamia ukarabati wa jengo la Wizara liliopo Maruhubiiliyokuwa Idara ya Maendeleo ya Mifugo. Hivi sasa Wizaraimehamia katika ofisi zake hizo kwa muda.

(c) Jumla ya wafanyakazi 95 wa Wizara walijitokeza kwa hiarikupima afya zao, pamoja na kupatiwa ushauri nasaha.

3.3.4 Malengo ya Mwaka 2011/2012

3.3.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 Idara inalengakutekeleza yafuatayo:-

(a) Kuimarisha uwekaji wa kumbukumbu za wafanyakazi waWizara.

(b) Kuwaendeleza wafanyakazi kielimu katika maeneo yao yakazi na kutafuta fursa za masomo kwa wafanyakazi haokutoka taasisi mbali mbali zinazotoa fursa za masomo ndanina nje ya nchi.

(c) Kuendelea kusimamia haki na maslahi ya wafanyakazi nakuhakikisha wafanyakazi hao wanatekeleza wajibu wao kwakufuata sheria za utumishi Serikalini.

(d) Kutunza mali za Serikali zinazomilikiwa na Wizara.

(e) Kufuatilia upatikanaji wa hati miliki kwa maeneo yote yaSerikali yanayomilikiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

(f) Idara itashirikiana na taasisi nyengine katika kuendeleakuwashajiisha wadau wake kubadili tabia ili wajikinge namaambukizo ya maradhi ya ukimwi, madawa ya kulevya nakutowanyanyapaa wale waliopata maambukizo. Hii itasaidiakukuza sekta ya uvuvi na ufugaji.

(g) Kuimarisha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi ili kuwezakutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwa wananchi ikiwemokuwapatia vitendea kazi.

(h) Ujenzi wa josho la kwanza katika wilaya ya Mkoani kisiwaniPemba katika Shehia ya Mjimbini.

Page 13: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(i) Kuendelea na utaratibu wa kuzifanyia ukarabati nyumba zaWizara zilizoko Mkoroshoni kisiwani Pemba na Mkwajunikisiwani Unguja.

3.3.4.2 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idara yaUendeshaji na Utumishi kwa Unguja inaombewa jumla ya shilingi306,740,870 kutoka Serikalini ili kutekeleza kazi zake za kawaida.Kati ya fedha hizo shilingi 85,151,000 zimetengwa kwa matumizimengineyo.

3.4 IDARA YA UZALISHAJI MIFUGO3.4.1 Majukumu ya Idara

3.4.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara ya Uzalishaji Mifugo ina jukumu lakupanga, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mikakati naprogramu za maendeleo ya mifugo. Aidha, Idara hii hutoa taalumaya ufugaji bora kwa lengo la kuongeza uzalishaji na ubora wamifugo na mazao yake, ili kuleta tija kwa wafugaji na wananchikwa ujumla. Pia Idara ina jukumu la kuimarisha uzalishaji wamifugo ya asili kwa kubadilisha vinasaba (cross breeding).

3.4.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.4.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idaraililenga kutekeleza yafuatayo:-

(a) Kuendelea kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu kwawafugaji ili kuongeza uzalishaji.

(b) Kushajiisha wananchi kutumia samadi inayotokana namifugo kwa kuzalisha nishati mbadala kwa matumizimbalimbali.

(c) Kuimarisha upatikanaji wa huduma za kupandisha ng'ombekwa sindano kwa matumizi ya mbegu bora za ng'ombe nambuzi wa maziwa.

3.4.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.4.3.1 Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa malengo haya hatuambali mbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na yafuatayo:-

(a) Katika kuhakikisha wafugaji wanapatiwa huduma bora zaushauri jumla ya wafugaji 14,288 Unguja na Pembawametembelewa na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.

Page 14: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

Makundi yaliyopatiwa ushauri ni pamoja na wafugaji wakuku, wazalishaji wa vifaranga, wafugaji wa ng'ombe wamaziwa, wafugaji wa mbuzi na jumuiya mbalimbalizinazojishughulisha na ufugaji. Aidha, wananchiwanaotarajia kuwekeza katika ufugaji wa ng'ombe, mbuzi nakuku walitembelewa na kupatiwa ushauri wa awali.

(b) Kwa kushirikiana na programu ya ASSP/ASDP-L, Idarailiendelea kutoa taaluma kupitia mashamba darasa 172Unguja na Pemba. Aidha, kwa kushirikiana na programuinayoratibiwa na (ILO/JP5/CoopAfrica), Idara imetoamafunzo kwa ushirika wa ufugaji ng'ombe wa maziwa"JUWAPO" uliopo Fuoni, "Ungalipo" uliopo Chaani naushirika wa kuku "Kupata Si Nguvu" uliopo Birikau-Pemba,pamoja na baadhi ya wafugaji wengine katika maeneo yakaribu.

(c) Idara ya Uzalishaji wa Mifugo, kwa kushirikiana na jumuiyaya kiraia ya kizalendo "ZALWEDA" na Jumuiya ya kiraia yakigeni "DANTAN" kwa pamoja ziliendesha ushajiishaji wamatumizi ya nishati mbadala inayotokana na samadi yamifugo kwa matumizi ya nyumbani. Zoezi hili limeanzakisiwani Pemba ambapo semina iliyojumuisha wafugaji 50waliotegemewa kuwa wadau wa mpango huu iliendeshwa.Kwa upande wa Pemba mtambo mmoja (1)umekwishafungwa katika eneo la Shumba Viamboni namiwili (2) imefungwa Unguja katika eneo la Machui.

(d) Jumla ya ng'ombe 1,274 walipandishwa kwa sindano.Kuimarika kwa huduma hii inatokana na kufungwa kwamtambo wa kuzalishia "liquid nitrogen" katika kituo chaMaruhubi.

(e) Utaratibu wa ununuzi wa madume ya ng’ombe bora wamaziwa wawili wa aina ya (Jersey) na ukarabati wa sehemuya maabara ya kituo cha kuzalisha mbegu boraumekamilika.

3.4.4 Malengo ya Mwaka 2011/20123.4.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, Idara

itatekeleza malengo yafuatayo:-

Page 15: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(a) Kushajiisha vijana kujiajiri katika kazi za ufugaji wakibiashara.

(b) Kuendelea kuimarisha kituo cha upandishaji ng'ombe kwasindano Maruhubi kwa kukarabati jengo la ofisi nakulizungushia uzio eneo hilo la kituo, na kutayarisha ardhikwa kupanda majani kwa ajili ya malisho ya ng’ombe wambegu.

(c) Kuendeleza kazi za upandishaji ng'ombe kwa sindanoambapo ng'ombe 6,000 wanatarajiwa kupandishwa.

(d) Kufundisha taaluma ya upandishaji wa mbuzi kwa sindano,kwa wapandishaji (CAHW’s) Unguja na Pemba nakuendeleza utafiti wa mbuzi bora. Katika hili la utafiti,naomba kutoa taarifa kwamba mwekezaji Sheikh AliYousouf amekubaliana na Idara ya Uzalishaji Mifugo,kufanya utafiti wa pamoja juu ya kabila ya mbuzi bora kutokaCyprus ambao wanauwezo wa kuzaa ndama watatu kwampigo na kutoa maziwa lita 6 hadi 8 kwa siku.

(e) Kuimarisha ufugaji wa kuku wa kienyeji wanaofugwa nawananchi wengi walio masikini kwa kuwahamasisha juu yautumiaji wa majogoo bora ili kuongeza uzalishaji wa mayaina ukuaji wa kuku wanaozaliwa pamoja na kushajiishamatumizi ya chanjo ya mahepe.

(f) Kuanzisha kampeni ya unywaji wa maziwa na ulaji wa mayaikatika jamii yetu.

(g) Kuanzisha utafiti shirikishi wa kuku katika kupata kukuwanaokua haraka, wanaotaga zaidi na wanaostahamilimaradhi.

(h) Kuimarisha mfumo wa elimu kwa wafugaji kwa kutumiamashamba darasa, redio na televisheni, vijarida navipeperushi, pamoja na kuongeza idadi na uwezo wakitaaluma kwa wataalamu wa fani hiyo. Jumla ya wafugaji15,000 watapatiwa elimu kupitia njia hizo.

(i) Kushajiisha ufugaji wa kuku wa kisasa kwa mashirikianobaina ya wawekezaji wa ndani na wafugaji wenyewe ilikuongeza uzalishaji wa ndani wa mayai na nyama. Naombanitoe habari njema kwamba Kampuni ya Sheikh Ali Youssuf

Page 16: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

na Wizara yangu zimo katika hatua ya kutayarisha hati yamakubaliano ya uanzishaji uekezaji mkubwa wa ufugaji wakuku wa mayai hapa Zanzibar. Ni imani yangu kwa SheikhAli Youssuf tunavyomfahamu hasa sisi Wajumbe wa Barazalako tukufu, uekezaji wake utaleta mapinduzi makubwakatika sekta ya mifugo hapa Zanzibar.

(j) Kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji WananchiKiuchumi na Ushirika pamoja na Wizara ya Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Idaraitashajiisha uundaji wa jumuia za ufugaji na kuzipatiamafunzo ya fani ya mifugo na uendeshaji.

(k) Kuzidisha mwamko wa usindikaji na matumizi ya mazao yamifugo (nyama, maziwa, mtindi, jibini, siagi na samli) pamojana kushajiisha wafugaji kuanzisha viwanda vidogo vidogovya kisasa vya kusindika mazao ya mifugo sambamba nakutoa mafunzo ya usindikaji na masoko.

(l) Kuendeleza ushajiishaji wa matumizi ya gesi itokanayo nasamadi na kufunga mitambo mitano (5) mipya kwa wafugajiwataojitokeza.

(m) Kukiimarisha kituo cha mbegu za majani Kizimbani,kuendelea na mazungumzo na waekezaji kwa kuyaendelezamashamba ya Kipange, Kitumba, Hanyegwa mchanaChamanangwe, Magome na mengineyo.

3.4.4.2 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idaraitatekeleza na kusimamia Mradi wa Kupandisha Ng'ombe kwaSindano (Kiambatisho 2).

3.4.4.3 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011, Idarahii ilikuwa sehemu ya Idara ya Maendeleo ya Mifugo ambayoilipangiwa kupata shilingi 848,636,000. Kati ya hizo matumizimengineyo yalipangiwa jumla ya shilingi 145,000,000 kutokaSerikalini. Hadi kufikia April 2011, shilingi 84,414,850zimepatikana ambazo ni sawa na asilimia 58.2 (Kiambatisho na.11). Kwa upande wa miradi ya maendeleo Idara ilipangiwa jumlaya shilingi 147,000,000 kutekeleza mradi wa kupandisha ng'ombe

Page 17: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

kwa sindano. Hadi kufikia mwezi wa Aprili Mradi ulipatiwa shilingi135,500,384 ambazo ni sawa na asilimia 92.2 (Kiambatisho na. 9).

3.4.4.4 Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza malengo ya 2011/2012Idara ya Uzalishaji Mifugo kwa Unguja inaombewa jumla yashilingi 226,248,000 kwa kazi za kawaida na shilingi 141,500,000kwa kazi za maendeleo. Kati ya fedha za kazi za kawaida shilingi89,448,000 ni kwa matumizi mengineyo.

3.5 IDARA YA HUDUMA ZA UTABIBU WA MIFUGO

3.5.1 Majukumu ya Idara

3.5.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo inajukumu la kuhakikisha mifugo yote inayofugwa nchini inastawi nainakingwa na maradhi mbalimbali ya mifugo. Aidha, kuhakikishamifugo yetu haienezi maradhi kwa binadamu kwa kufanya ukaguziwa wanyama na bidhaa zao. Vilevile, Idara hii ina jukumu lakuondosha ukatili dhidi ya wanyama, kusimamia utoaji wa tiba nakinga kwa maradhi mbalimbali ya mifugo pamoja na kuzuiamagonjwa yasiyo na mipaka "Transbaundary Animal Diseases"kuingia katika nchi yetu, kufanya uchunguzi wa mwenendo wamaradhi ya kuambukiza na yenye kuathiri mifugo yetu, kubunimbinu za kukabiliana na maradhi hayo na kufanya utafiti wamaradhi ya mifugo.

3.5.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.5.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idara hiiilikuwa ni sehemu ya Idara ya Maendeleo ya Mifugo ya iliyokuwaWizara ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na iliwekewa malengoyafuatayo:-

(a) Kuendelea kutoa huduma za kinga, tiba, na ushauri wakitaalamu kwa wafugaji.

(b) Kuendelea kuimarisha karantini na ukaguzi wa mifugo namazao yake kwa lengo la kuikinga mifugo na binadamu dhidiya maradhi yanayoweza kuletwa na mifugo au bidhaa zakekutoka nje ya nchi.

Page 18: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(c) Kuimarisha maabara za uchunguzi wa maradhi kwakuzipatia zana na nyenzo za kufanyia uchunguzi wa maradhihayo.

(d) Kuimarisha majengo yalioko katika chinjio kuu la Kisakasakapamoja na uwekaji wa umeme katika kituo hicho na uwekajiwa uzio katika eneo la karantini.

(e) Kuanzisha eneo la karantini ya wanyama huko Pemba.

3.5.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.5.3.1 Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Idarailitekeleza yafuatayo:-

(a) Kwa kushirikiana na Programu za ASSP/ASDP-L, Idarainaendelea na zoezi la kuchanja kuku wa kienyeji dhidi yaugonjwa wa mahepe ambapo jumla ya kuku 223,573wamepatiwa chanjo hiyo.

(b) Jumla ya wanyama 213,047 walikaguliwa na kuruhusiwakuingia nchini. Kati ya hao, ng'ombe ni 6,586, mbuzi 648,kondoo 11, kuku (vifaranga) 205,791 na wanyama wengine11. Aidha, bidhaa za mifugo zilizoingizwa nchini ni pamojana mayai 138,229, nyama ya kuku kilo 6,565, nyama yang'ombe kilo 8,225, nyama ya mbuzi kilo 14,065 na nyamaya kondoo kilo 13,765.

(c) Matengenezo ya maabara ndogo ya mifugo iliopo Chakechake Pemba na matengenezo ya sehemu ya maabara yaMaruhubi yamekamilika.

(d) Jumla ya eka kumi za eneo la karantini Kisakasakazimefanyiwa usafi na kuzungushiwa miti hai. Sambamba nahayo matengenezo ya chinjio la Kisakasaka yameanza.

(e) Eneo la kuanzisha karantini ya wanyama Pembalimeshapatikana huko Nziwengi, ambapo kwa sasa Wizaraipo katika hatua za kulipima na kupata hatimiliki ya eneo hilokabla ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu. Aidha Wizaraimeunda kamati ya pamoja baina ya maofisa wa Wizara,Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, pamoja nawafanyabiashara wa mifugo wa Mkoa wa Kaskazini Ungujaili kufanya utafiti ili kuangalia uwezekano wa kuanzisha

Page 19: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

kituo cha Karantini ya wanyama katika Mkoa KaskaziniUnguja.

(f) Kitengo maalum cha kuzuia ukatili dhidi ya wanyama chenyejukumu la kutoa elimu, ushauri na maelekezo juu yamatunzo mazuri ya wanyama kimeanzishwa. Jumla yawashiriki 50 kutoka vyombo vya ulinzi na usalama naHalmashauri za Wilaya walipata mafunzo juu ya haki zawanyama, uzuiaji wa mateso kwa wanyama na kinga dhidiya ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Aidha, washiriki 120wakiwemo watoa huduma za msingi za mifugo (CommunityAnimal Health Workers), walipewa mafunzo juu ya sheria zarasilimali ya mifugo, haki za wanyama na uzuiaji wa kichaacha mbwa. Vilevile mikutano mengine kumi na moja yakuwaelimisha wananchi kuhusu kichaa cha mbwa ilifanyikana kuhusisha washiriki 296 Unguja na Pemba.

(g) Jumla ya washiriki 2,500 kutoka Unguja na Pembawamehudhuria mafunzo juu ya tahadhari ya kujilinda namaradhi mbali mbali ya kuambukiza. Aidha, wataalamuwanne wa Idara wamehudhuria mafunzo mbali mbali yakuimarisha taaluma zao, ikiwa ni pamoja na namna yakubaini vimelea vya mafua makali ya ndege katika maabara.

(h) Kliniki za mifugo za wilaya zilizopo Kengeja, Konde,Maruhubi na Mangapwani ziko katika hatua ya mwisho yamatengenezo.

3.5.4 Malengo ya Mwaka 2011/2012

3.5.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 Idara inalengakutekeleza yafuatayo: -

(a) Kuendelea kutoa huduma za tiba, kinga na uchunguzi wamaradhi ya mifugo kwa nia ya kuboresha afya za mifugoyetu nchini.

(b) Kuendelea kuimarisha karantini na ukaguzi wa mifugo namazao yake kwa lengo la kuikinga mifugo na binadamu dhidiya maradhi yanayoweza kuletwa na mifugo au bidhaa zakekutoka nchi za nje.

Page 20: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

(c) Kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo, kuziendelezamaabara za uchunguzi wa maradhi kwa kuzipatia zana nanyenzo nyengine za kufanyia uchunguzi wa maradhi.

(d) Kufanya ukarabati wa kliniki ya mifugo ya Dunga na ujenziwa kliniki ya mifugo Unguja - Ukuu.

(e) Ununuzi wa vifaa na vitendea kazi vya kliniki 5 za mifugozilizofanyiwa ukarabati.

(f) Kuendelea na uimarishaji wa mazingira ya kituo chakarantini Kisakasaka.

(g) Jumla ya dozi milioni moja za chanjo ya mahepezitanunuliwa na kuchanjwa kuku wa kienyeji Unguja naPemba.

(h) Kuendelea na utaratibu wa kupata hatimiliki ya eneo laKarantini Nziwengi Pemba pamoja na vituo vyengine vyamifugo, pia kuendelea kukamilisha hatua za uanzishaji waeneo la Karantini huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.

(i) Kutoa taaluma kwa wafugaji juu ya kuwakinga wanyamawao na maradhi ya kuambukiza kupitia vyombo vya habari,vijarida, vipeperushi pamoja na semina.

(j) Kuendelea kutoa taaluma kwa jamii juu ya kuepukana natabia ya ukatili wa wanyama, na kushirikiana na taasisizisizo za kiserikali kama ZALWEDA na ZAASO ya mamaAnna iliyopo Kiyanga ya kupiga vita ukatili wa Wanyama.

(k) Kutayarisha mpango wa tahadhari ya mapema juu yamagonjwa ya miripuko katika sekta ya mifugo kwakushirikiana na "FAO" kupitia programu ya Maendeleo yaUmoja wa Mataifa.

3.5.4.2 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idaraitasimamia utekelezaji wa miradi miwili ambayo ni:-

(a) Mradi wa Kudhibiti Kichaa cha Mbwa unaotekelezwa naSMZ ikishirikiana na "World Society for Protection of

Page 21: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

Animals" (WSPA) kwa Unguja na "World HealthOrganization" (WHO) kwa Pemba (Kiambatisho 3).

(b) Mradi wa Kudhibiti Mafua Makali ya Ndege na Nguruweunaoendeshwa kwa ushirikiano wa SMZ na Shirika la Umojawa Mataifa la "UNICEF" na "European Union" (Kiambatisho4).

3.5.4.3 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2010/2011 mapatoyatokanayo na huduma ya utabibu wa mifugo yalikadiriwa kuwashilingi 48,000,000 kwa Unguja. Hadi kufikia mwezi wa Machijumla ya shilingi 27,628,560 zimekusanywa ambazo ni sawa naasilimia 57.6 ya lengo (Kiambatisho na 8). Kwa mwaka wa fedha2011/2012 mapato yanayotokana na huduma za Utabibu wamifugo kwa Unguja yanakadiriwa kuwa niShilingi 48,000,000.

3.5.4.4 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 Idara hiiilikuwa sehemu ya Idara ya Maendeleo ya Mifugo kamailivyoelezwa kwenye Idara ya Uzalishaji Mifugo. Katika kasma yamaendeleo, Mradi wa Kudhibiti Mafua ya Ndege uliombewashilingi 67,000,000. Mpaka kufikia mwezi wa Aprili 2011, mradiumetiliwa shilingi 53,854,949 sawa na asilimia 80.4. Mradi waKichaa cha Mbwa uliombewa shilingi 65,000,000 na mpaka kufikiamwezi wa Aprili 2011 umetiliwa shilingi 27,644,667 sawa naasilimia 42.5 (Kiambatisho na. 9).

3.5.4.5 Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza malengo ya mwaka2011/2012 Idara ya Utabibu wa Mifugo kwa Unguja inaombewajumla ya shilingi 283,619,416 kwa kazi za kawaida na shilingi150,000,000 zimeombewa kwa kazi za maendeleo. Kati ya fedhaza kazi za kawaida shilingi 60,431,000 ni kwa matumizimengineyo.

3.6 IDARA YA MAENDELEO YA UVUVI3.6.1 Majukumu ya Idara

3.6.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara hii ina majukumu ya kuwahudumiawavuvi pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha nauvuvi kwa ajili ya kuinua hali zao kiuchumi. Aidha, Idara inajukumu la kuhakikisha kuwa rasilimali za baharini zinalindwa kwakuzingatia matumizi bora na endelevu sambamba na jukumu la

Page 22: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni za uvuvi kwa lengo lakuhakikisha matumizi bora ya rasilimali za bahari.

3.6.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.6.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/2011 malengo ya Idara yaUvuvi yalikuwa kama yafuatayo:-

(a) Kuendelea kuishirikisha jamii katika uhifadhi wa rasilimali zabaharini na mazingira yake.

(b) Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ya baharikwa jamii ya ukanda wa pwani.

(c) Kuwashajiisha wavuvi vijana kuacha kuvua katika maeneoya hifadhi na badala yake kwenda kuvua katika kina kirefu.

(d) Kudhibiti matumizi ya nyavu zenye macho madogo katikamaeneo ya hifadhi na kupiga marufuku matumizi ya nyavu za"monofilament".

(e) Kuendeleza kazi za doria katika maeneo ya hifadhi kwakushirikiana na jamii.

3.6.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.6.3.1 Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza malengo ya 2010/2011Idara ilifanya yafuatayo:-

(a) Kuendelea kushirikisha jamii katika uhifadhi wa maeneo yahifadhi ya rasilimali za baharini kwa kuimarisha kamati zawavuvi pamoja na kamati za doria vijijini. Jumla ya kamati 61kwa Unguja na 28 za Pemba zimeshiriki kikamilifu katikadoria za kukabiliana na uvuvi haramu na shughuli za kitalii.Jumla ya vyombo viwili na vifaa vyake vya uvuvi haramu(nyavu sita, mashine moja na bunduki nne) vilikamatwa nahatua za kisheria zimechukuliwa.

(b) Doria 48 maalum za kudhibiti uvuvi haramu katika maeneoya hifadhi za kisiwa cha Mnemba na Ghuba ya Chwaka"MIMCA", Ghuba ya Menai "MBCA" na Mkondo wa Pemba"PECCA" zimefanyika kwa kushirikiana na wanajamii, askariPolisi pamoja na KMKM. Katika doria hizo jumla ya vipande

Page 23: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

11 vya nyavu za macho madogo na bunduki nne pamoja navyombo vitatu vilikamatwa na mashauri yao kufikishwa katikavyombo vya sheria.

(c) Jumla ya doria 270 za kawaida zenye lengo la kudhibiti nakukagua leseni pamoja na harakati za kitalii zinazoendeleakatika maeneo ya hifadhi ya kisiwa cha Mnemba, ghuba yaMenai na mkondo wa Pemba zilifanyika

(d) Idara iliandaa mafunzo kuhusiana na mpango wa usimamiziwa athari za kimazingira kwa jamii (Community MitigationAction Plans) katika Shehia 10 zilizopo katika eneo lahifadhi ya kisiwa cha Mnemba na ghuba ya Chwaka na kilashehia iliwakilishwa na wanavijiji 10.

(e) Mafunzo kuhusiana na umuhimu wa kuwahifadhi nakuwalinda wanyama walio hatarini kutoweka wakiwemopomboo, nyangumi na kasa yalitolewa. Mafunzo hayoyalitolewa kwa wamiliki wa mahoteli, wapelekaji watalii katikamaeneo ya hifadhi pamoja na wavuvi waliokuwepo katikamaeneo ya hifadhi za kisiwa cha Mnemba na Ghuba yaMenai. Jumla ya washiriki 220 walihudhuria mafunzo hayo.

(f) Jumla ya mikutano 48 imefanyika kwa shehia zote za"MBCA", "MIMCA" na "PECCA" kwa lengo lakuwahamasisha wanajamii juu ya umuhimu wa uhifadhi wamazingira ya bahari na ukanda wa pwani na athari yamatumizi ya nyavu katika maeneo ya uhifadhi.

(g) Sheria mpya ya Uvuvi No. 7 ya mwaka 2010 imeshapitishwana kutiwa saini na Mhe. Rais Mstaafu wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi wa Awamu ya Sita mnamo tarehe 26 Julai 2010.

(h) Ujenzi wa ofisi mpya za Idara ya Uvuvi Unguja na Pembaunaendelea na ujenzi wa majengo matatu ya maeneo yahifadhi ya kisiwa cha Mnemba na Ghuba ya Chwaka, Ghubaya Menai na Mkondo wa Pemba umekamilika nayameshahamiwa.

(i) Kazi ya kuanzisha wigo wa maeneo mapya ya hifadhi yavisiwa vya Changuu na Bawe "CHABAMCA", Tumbatu

Page 24: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

"TUMCA" na Kojani "KOMCA" pamoja na kuyatangazakisheria imeanza.

3.6.4 Malengo ya Mwaka 2011/2012

3.6.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012malengo ya Idara ya Maendeleo ya Uvuvi ni kama yafuatayo:-

(a) Kufanya ukaguzi wa maeneo ya uvuvi kwa lengo la kudhibitiuvuvi haramu kwa kushirikiana na kamati za wavuvi za jamii.

(b) Kuendesha mafunzo kwa wanajamii juu ya umuhimu wakulinda na kuhifadhi mazingira ya bahari na rasilimali zake.Jumla ya vijiji 60 na wavuvi 1,200 watafaidika na mafunzohaya.

(c) Kuendesha mafunzo kwa wanajamii juu ya uelewa nakuwashirikisha katika uhifadhi wa wanyama wa bahariniwaliohatarini kutoweka kama pomboo, nyangumi na kasa.

(d) Kuainisha maeneo madogo maalum yenye umuhimu kwauhifadhi wa rasilimali za bahari katika ngazi ya jamii.

(e) Kuendesha mafunzo kwa wadau mbali mbali wa utalii kwalengo la kuhifadhi rasilimali za bahari na mazingira yake.

(f) Kununua vifaa kwa ajili ya ofisi hizo zilizokamilika za“MENAI”, “MIMCA”, na “PECCA”, na pia kukamilisha ujenziwa ofisi za Idara Unguja na Pemba pamoja na kununua vifaavya ofisi hizo.

(g) Kusimamia ujenzi wa soko la Kisasa Tumbe.

(h) Kuanzisha mafunzo kwa wavuvi wazalendo kuvua kwenyemaji ya kina kirefu, na kutafuta boti za kisasa kwa ajili yamafunzo hayo. Mheshimiwa Spika, katika kufanikishamafunzo haya ambayo ni muhimu katika kuanzisha “fleet” yawavuvi wazalendo, wizara yangu inafanya mazungumzo naWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuona namna yakuanzisha mtaala wa uvuvi wa Bahari Kuu katika vyuo vyetuvya amali vilvyopo Mkokotoni na Vitongoji.

3.6.4.2 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idaraitasimamia na kutekeleza mradi mmoja wa Usimamizi wa

Page 25: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani "MACEMP"(Kiambatisho na. 5).

3.6.4.3 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2010/2011 mapato yaleseni za vyombo na za wavuvi yalikadiriwa kuwa shilingi20,000,000 kwa Unguja. Hadi kufikia mwezi wa Machi jumla yashilingi 8,780,100 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia43.90 ya lengo. Kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 mapatoyanayotokana na leseni za uvuvi kwa Unguja yanakadiriwa kuwani shilingi 20,000,000.

3.6.4.4 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/2011 jumla ya shilingi669,344,000 ziliombwa kutekeleza kazi za kawaida na zamaendeleo. Kati ya hizo shilingi 401,678,000 zilikuwa kwa kazi zamiradi ya maendeleo na hadi kufikia mwezi wa Aprili shilingi115,000,000 zimepatikana ambazo ni sawa na asilimia 28.6(Kiambatisho na. 9). Kwa kutekeleza kazi za kawaida jumla yashilingi 267,666,000 ziliombwa ambapo shilingi 51,678,000 kwamatumizi mengineyo. Hadi kufikia mwezi Aprili 2011 shilingi11,000,000 zimepatikana kwa matumizi mengineyo ambazo nisawa na asilimia 21.3 (Kiambatisho na. 11).

3.6.4.5 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idara yaMaendeleo ya Uvuvi kwa Unguja inaombewa jumla ya shilingi201,185,375 kwa kazi za kawaida na shilingi 216,000,000 kwakazi za maendeleo. Kati ya fedha za kazi za kawaida shilingi60,338,000 ni kwa matumizi mengineyo.

3.7 IDARA YA MAZAO YA BAHARINI

3.7.1 Majukumu ya Idara

3.7.1.1 Mheshimiwa Spika, Idara ya Mazao ya Baharini ina majukumu yakuwahudumia wafugaji wa mazao ya baharini, wakulima wamwani pamoja na wadau wengine wanaojishughulisha na mazaoya baharini kwa ajili ya kuinua hali zao kiuchumi. Aidha, Idara inajukumu la kukuza, kuendeleza, kudhibiti na kufuatilia shughuli zoteza ufugaji na ukulima wa mazao ya baharini kwa madhumuni yakuwa na ufugaji bora pamoja na kuimarisha ubora na thamani yamazao ya baharini.

Page 26: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

3.7.2 Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.7.2.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/2011 Idara ilikuwa namalengo yafuatayo:-

(a) Kuendelea kuishirikisha jamii katika uhifadhi wa rasilimali zabaharini na mazingira yake.

(b) Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ya baharini kwa jamiiya ukanda wa pwani kwenye maeneo ya ufugaji viumbe vyabaharini na ukulima wa mwani.

(c) Kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya mazao ya baharini.

3.7.3 Utekelezaji wa Malengo ya Mwaka 2010/2011

3.7.3.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/2011 Idara ilitekelezamambo yafuatayo:-

(a) Kutoa elimu ya mazingira kwa wanajamii wa shehia zote zamwambao wa bahari kwa Unguja na Pemba kwa kutumianjia mbali mbali zikiwemo mikutano na semina. Jumla yamikutano na semina 25 zilizowashirikisha wanajamii 4,000zilifanyika.

(b) Juhudi za kuwahamasisha wavuvi kujihusisha na ufugaji wasamaki na mazao mengine ya baharini zimeendeleakuchukuliwa kwa kushajiisha uanzishwaji wa mabwawa yaufugaji wa samaki katika maeneo ya Chukwani, BumbwiniMakoba, Fukuchani na Mangapwani kwa Unguja na Kiwani,Chambani, Makombeni na Mtangani kwa Pemba. Katikajuhudi hizo jumla ya mabwawa manane yametayarishwa nakuanzishwa.

(c) Kazi ya kutoa taaluma ya ufugaji wa mazao ya baharinikama vile ufugaji wa chaza, samaki, kaa pamoja na ukulimana uanikaji wa mwani zinaendelea kutolewa. Kwa hivi sasakuna jumla ya vikundi 75 vyenye wanachama 1,500wanaojihusisha na ufugaji wa mazao ya baharini kama vilesamaki, chaza, kaa na kasa.

(d) Kuhamasisha wakulima wa mwani kujiunga na jumuiya zaoza uzalishaji. Idara kwa kushirikiana na wakulima wa mwaniimeanza utaratibu wa kuanzisha jumuiya ya wakulima wa

Page 27: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

mwani Zanzibar (Zanzibar Seaweeds Farmers Association)itakayowawakilisha wakulima wa mwani katika jumuiya yawafanya biashara na wenyeviwanda na Kilimo Zanzibar(Zanzibar Chamber of Commerce, Industry and Agriculture).

3.7.4 Malengo ya Mwaka 2011/2012

3.7.4.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Idara yaMazao ya Baharini imepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

(a) Kuhamasisha matumizi ya mwani ikiwemo kutengenezasabuni na usarifu mwengine kwenye matumizi ya vyakulambali mbali.

(b) Kutoa elimu kwa wakulima juu ya ukulima bora wa mwaniutakaopelekea kuzalisha mwani bora na wa kiwango chajuu, na pia kutoa taaluma juu ya ujuzi wa ufugaji wa mazaoya baharini. Naomba kutoa habari njema kwamba katikakutekeleza azma hii, kundi la mwanzo la vijana 30litaondoka wakati wowote kwenda Jamhuri ya Watu waChina kwenda kuchukua ujuzi wa ufugaji wa mazao yabaharini. Vijana hawa 30 wametoka kwenye majimbo yawaheshimiwa wajumbe wa Baraza hili, mara kundi hililitaporudi, makundi mengine yataandaliwa na kupewamafunzo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutoa taaluma hiimuhimu kwa wananchi wetu.

(c) Kuhamasisha wakulima wa mazao ya baharini kuundavikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa ili kuwa na mitajiambayo itawawezesha kuanzisha vyanzo vya ziada vyakujiongezea kipato na kuwainua kiuchumi.

(d) Kuhamasisha wanajamii kujihusisha na ufugaji wa samaki,chaza, uzalishaji wa lulu na kaa, pamoja na kuimarishausarifu na uuzaji wa mazao hayo katika masoko ya ndani nanje ya nchi.

(e) Kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi ya Baharini ya ChuoKikuu cha Dar-es- Salaam kuendeleza utafiti wa mwanimnene ambao unastahamili hali ya hewa na wenye tija zaidi,pia kufanya utafiti wa mazao ya kamba na majongoo bahari.

3.7.4.2 Mheshimiwa Spika, mapato yatokanayo na ushuru wa usafirishajiwa mazao ya baharini nje ya Zanzibar yalikadiriwa kuwa shilingi

Page 28: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

40,000,000 kwa Unguja. Hadi kufikia mwezi wa Machi 2011 jumlaya shilingi 32,635,000 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia81.6 ya lengo (Kiambatisho na. 8). Kwa mwaka wa fedha2011/2012 mapato yanayotokana na mazao ya baharini kwaUnguja yanakadiriwa kuwa Shilingi 40,000,000.

3.7.4.3 Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 Idara yaMazao ya Baharini ilikuwa haijaundwa, hivyo haikuwa na bajetirasmi. Katika kutekeleza malengo ya mwaka wa fedha wa2011/2012 Idara hii kwa Unguja inaombewa jumla ya shilingi120,667,732 kutekeleza kazi za kawaida. Kati ya fedha hizoshilingi 46,122,000 ni kwa matumizi mengineyo.

3.8 OFISI KUU PEMBA

3.8.1 Mheshimiwa Spika, Ofisi Kuu ya Wizara ya Mifugo na UvuviPemba ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa kazizote za Wizara kwa upande wa Pemba kwa kushirikiana na Idarambali mbali zilizomo katika Wizara hii. Kwa mwaka wa fedha2010/2011, kazi zilizotekelezwa na Ofisi Kuu Pemba ni miongonimwa kazi zilizokwisha elezwa chini ya Idara zote ziliomo katikaWizara hii.

3.8.2 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2010/2011 Ofisi KuuPemba ililenga kukusanya mapato ya jumla ya shilingi15,000,000/- kutokana na utoaji leseni za uvuvi, mazao yabaharini na ada ya huduma za utibabu. Hadi kufikia mwezi waMachi ilikusanya jumla ya shilingi 6,623,000/- sawa na asilimia 44ya lengo. Kati ya fedha zilizokusanywa, Idara ya Uvuvi ilikusanyashilingi 1,905,700, Idara ya Mazao ya Baharini ilikusanya shilingi1,689,000 na Idara ya huduma za Utabibu ilikusanya shilingi3,028,300. Kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Ofisi Kuu Pembainakadiria kukusanya jumla ya mapato ya Shilingi 12,000,000.Mapato haya yatatokana na huduma za utibabu wa mifugo(7,000,000), leseni za uvuvi (3,000,000) na mazao ya baharini(2,000,000).

3.8.3 Mheshimiwa Spika, kwa kutekeleza malengo yaliolezwa katikaIdara mbali mbali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Ofisi KuuPemba imekadiriwa kutumia jumla ya shilingi 623,075,788 kwakazi za kawaida. Kati ya hizo shilingi 352,501,000 ni kwa matumizi

Page 29: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

mengineyo, ambapo Idara ya Mipango, Sera na Utafiti imekadiriwakutumia shilingi 37,044,000, Idara ya Uendeshaji na Utumishiimekadiriwa kutumia shilingi 68,656,000, Idara ya Mazao yaBaharini imekadiriwa kutumia shilingi 79,135,000, Idara yaMaendeleo ya Uvuvi imekadiriwa kutumia 82,374,000, Idara yaUzalishaji wa Mifugo imekadiriwa kutumia shilingi 33,871,000 naIdara ya Utabibu wa Mifugo imekadiriwa kutumia shilingi51,421,000. Mchanganuo wa makisio kwa Idara zote za Wizara yaMifugo na Uvuvi ziliopo Pemba unaonekana katika kiambatishona. 12.

4.0 MUHTASARI WA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA2010/2011

4.1 Ukusanyaji wa Mapato 2010/2011

4.1.1 Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2010/2011, Wizarailipangiwa kukusanya mapato ya shilingi 1,048,474,000. Hadikufikia mwezi wa Machi 2011 Wizara ilikusanya mapato ya shilingi333,168,796.30, ambayo ni sawa na asilimia 32 ya lengolililowekwa (Kiambatisho na. 8). Mapato kidogo yaliyokusanywayamesababishwa zaidi na kushuka kwa mapato ya leseni za uvuviwa bahari kuu. Hali hii inatokana na kuwepo kwa maharamia wabaharini katika pembe ya Afrika Mashariki.

4.2 Matumizi ya Fedha 2010/2011

4.2.1 Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 sekta zamifugo na uvuvi zilikuwa ni sehemu ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Mazingira. Sekta hizo ziliidhinishiwa jumla ya shilingi1,796,980,000 ambapo shilingi 1,116,302,000 zilikuwa kwa kazi zakawaida na shilingi 680,678,000 kwa kazi za maendeleo. Kati yafedha za kawaida shilingi 196,678,000 zilitengwa kwa matumizimengineyo. Hadi kufikia mwezi wa Aprili, fedha zilizopatikana nishilingi 95,414,850 kwa matumizi mengineyo ambayo ni sawa naasilimia 48.5. Aidha, jumla ya shilingi 332,000,000 zilitolewa kwamatumizi ya maendeleo sawa na asilimia 48.8 (Kiambatisho 9, 10 &11).

Page 30: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

5.0 MAKADIRIO YA MAKUSANYO YA MAPATO NA MATUMIZI YAWIZARA KWA MWAKA WA 2011/2012

5.1 Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Wizarainakadiria kukusanya jumla ya shilingi 1,020,000,000 kutoka katikavyanzo vyake mbali mbali vya mapato (Kiambatisho 8). Sambambana makusanyo hayo, Wizara yangu inatarajia kutumia jumla yashilingi 11,628,445,000. Kati ya hizo shilingi 8,788,945,000 ni fedhakutoka kwa washirika wa maendeleo kwa kutekeleza miradi miwili yamaendeleo (Mradi wa Kichaa cha Mbwa na Mradi wa MACEMP) nashilingi 2,839,500,000 ni kutoka SMZ. Katika fedha za SMZ, jumlaya shilingi 2,089,000,000 zimetengwa kwa kazi za kawaida naShilingi 750,500,000 kwa kazi za maendeleo. Kati ya fedha za kaziza kawaida jumla ya shilingi 1,289,000,000 ni kwa mishahara nashilingi 800,000,000 ni za matumizi mengineyo, (Kiambatanisho 9hadi 12).

6.0 HITIMISHO

6.1 Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kwa niaba ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kuzishukuru taasisi za Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Serikali ya Marekani, Jamhuri ya Watu waChina, Jamhuri ya Watu wa Korea, Serikali ya India, Serikali yaIsrael, Serikali ya Japan, Serikali ya Misri, Serikali ya Uholanzi,Serikali ya Uingereza na Ufalme wa Oman kwa kushirikiana nasikatika kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi. Aidha, napendakuyashukuru mashirika ya maendeleo yakiwemo "GEF", "KOICA","SADC", "UNICEF", "WHO", "WSPA", “USAFRICOM”, Benki yaDunia, Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika "AU", Shirika la ChakulaDuniani "FAO", Shirika la Maendeleo la Japan "JICA", Mfuko waKimataifa wa Maendeleo ya Kilimo "IFAD", Shirikisho la Nchi zaMashariki ya Afrika "EAC", na Umoja wa nchi za Ulaya "EU" Vile vilenapenda kuchukua fursa hii kuzishukuru Wizara za SMZ, taasisi zaSerikali na zisizo za kiserikali kama Taasisi ya Sayansi ya Baharini, ”Indian Ocean Marine Affairs Society” na “Zanzibar Society forProtection of Animal” ambazo zinasaidia kuleta maendeleo katikasekta za Mifugo na Uvuvi.

6.2 Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru kwadhati na kuwapongeza Katibu Mkuu Dk. Kassim Gharib Juma, NaibuKatibu Mkuu Dk. Omar Ali Amir, Afisa Mdhamini Pemba,

Page 31: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae

Nd. Mayasa Ali Hamadi, Wakurugenzi, wataalamu na wafanyakaziwote wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioko Unguja na Pemba kwautendaji wao mzuri unaoongeza ufanisi katika Wizara na kukubalikwao kufanyakazi katika mazingira magumu. Vile vile napendakuwapongeza, wafugaji, wavuvi, wakulima na wafanyabiashara wamwani, na wadau wengine wa sekta ya mifugo na uvuvi kwa jitihadana mashirikiano yao wanayotoa katika kuendeleza sekta hizi pamojana changamoto zinazowakabili. Napenda kuwahakikishia kwambamchango wao tunauthamini sana na tutaendelea kuyafanyia kazimapungufu yanayojitokeza kulingana na vipaumbele na nyenzozilizopo.

6.3 Mheshimiwa Spika, nitakuwa mkosefu wa shukurani iwapositawashukuru Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Madiwani,Masheha, Kamati za Maendeleo za Shehia, Kamati za Wavuvi,Vikosi vya SMZ na vyombo vya habari kwa mashirikiano yao mazuriwaliyoyatoa kusaidia utekelezaji wa kazi zetu. Vile viletunawashukuru wananchi wote kwa kuitikia wito wa kutumia mazaoya mifugo na uvuvi katika milo yao na tunawashajiisha wale bidhaaza ndani ili kuimarisha afya zao na kuwainua wazalishaji wetukimapato. Hivyo basi, kwa niaba ya Wizara yangu napendakuchukua fursa hii adhimu kuwaomba wananchi kuongeza juhudikatika uzalishaji na matumizi ya bidhaa hizo ili kuchangia katikasuala zima la kufikia uhakika wa chakula hapa nchini kwetu.

6.4 Mheshimiwa Spika, mwisho nawaomba waheshimiwa wajumbe waBaraza lako tukufu waipokee na kuijadili na kuikubali bajeti yaWizara yangu na watupe maoni, ushauri na mapendekezo katikakuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi kwa manufaa ya wafugaji,wavuvi na wananchi na Taifa hili kwa ujumla. Aidha, naliombaBaraza lako tukufu liidhinishe jumla ya shilingi 11,628,445,000 kwaajili ya matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Kati ya fedha hizoshilingi 2,089,000,000 ni kwa ajili ya kazi za kawaida na shilingi9,539,445,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kazi za maendeleo.

7.0 MHESHIMIWA SPIKA, NAOMBA KUTOA HOJA

MHE. SAID ALI MBAROUK (MBM)WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI

ZANZIBAR

Page 32: HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, · zaidi, ili ziweze kuchangia katika uhakika wa chakula kwa mazao ya mifugo na uvuvi, kuongeza kipato cha wananchi, kupunguza umasikini na hatimae