HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    1/104

    1

    HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO

    KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA

    TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA

    KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE,

    DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015

     Mheshimiwa Spika;

    Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu

    mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha

    kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu

    na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi

    imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa

    Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia

    nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze

    kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini,

    shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na

    shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi

    rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    2/104

    2

    mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama

    salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari

    hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika

    uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza

    kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa

    kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake

    wakipewa nafasi wanaweza.

     Mheshimiwa Spika;

    Niruhusu pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati

    kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kazi kubwa na nzuri

    mliyoifanya. Mmetimiza ipasavyo wajibu wao wa Kikatiba

    wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukurukwa ushirikiano wenu na msaada wenu. Ni ukweli ulio

    wazi kuwa bila ya ninyi Wabunge wetu na Bunge hili,

    tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo tuliyoyapata.

    Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima kubwa

    mbele ya wananchi. Mmeitendea haki demokrasia ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    3/104

    3

    Tanzania na kuliletea heshima kubwa Bunge letu nchini,

    kikanda na kimataifa.

     Mheshimiwa Spika;

    Tarehe 30 Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa

    nilielezea mtazamo wangu kuhusu nchi yetu na kutaja

    majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya Awamu

    ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele

    hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16

     Julai, 2010 wakati wa kuvunja Bunge hilo nilielezea

    mafanikio tuliyopata na changamoto zilizotukabili katika

    kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa kuzindua

    Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya Serikali yaChama cha Mapinduzi katika kipindi changu cha pili cha

    uongozi wa nchi yetu na kuahidi kuvitekeleza kwa ari zaidi,

    nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama ilivyo ada, leo tunafikia

    mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba kutumia fursa

    hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali

    na yale mambo ambayo tuliahidi na kupanga kufanya.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    4/104

    4

    Umoja, Amani na Usalama

     Mheshimiwa Spika;

    Niliahidi kuwa katika kipindi cha uongozi wangu

    nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa Tanzania

    inaendelea kuwa nchi moja na watu wake wanaendelea

    kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya

    tofauti zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na

    ufuasi wa vyama vya siasa. Pia, kwamba nchi yetu

    itaendelea kuwa yenye amani, usalama na utulivu.

    Leo tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa

    Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa wamoja. Hata

    hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapana pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi

    yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta

    chuki baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya Wakristo

    na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya nchi na wengine.

    Bahati nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa

    Serikali zetu mbili wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    5/104

    5

    na ushirikiano na viongozi wa dini na wa jamii na uelewa

    wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu kushinda

    changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi

    zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa

    kwamba wanaozungumza hawagombani na

    wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.

     Mheshimiwa Spika;

    Niruhusuni, nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara

    nyingine viongozi wakuu wenzangu, Makamu wa Rais, Rais

    wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu

    wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais

    Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchiwote kwa ushindi tulioupata katika kudumisha umoja wetu.

    Hata hivyo, tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa

    kwani watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu au na umoja

    wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba hawajafaulu.

    Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni

    kuendelea kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    6/104

    6

    Muungano Wetu Umeimarika Zaidi

     Mheshimiwa Spika;

    Nafurahi kwamba namaliza kipindi changu cha

    uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na kuuimarisha

    Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika.

    Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kufungua

    Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande

    zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi

    wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili

    limefanyika chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais,

    akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara

    na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamuyangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika

    awamu hii.

    Mafanikio yaliyopatikana ni makubwa. Masuala

    mbalimbali ya zamani na mapya yamezungumzwa,

    yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa mfano,

    hadi mwaka 2005 zilikuwa zimebakia kero13za Muungano

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    7/104

    7

    zilizoainishwa na Tume ya Shelukindo, hivi sasa zimebaki

    kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja unakamilishwa

    kiutawala na tatu zimeshughulikiwa kwa ukamilifu katika

    Katiba Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa

    imefanyika na Katiba hiyo kupitishwa kungekuwa hakuna

    kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo. Lakini kwa vile

    kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea

    kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na

    kukubaliana tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya

    mafuta na gesi. Ndiyo maana katika Muswada wa Petroli

    hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia

    uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa

    kupitisha Muswada huo. Moja ya kero kubwa katika

    Muungano tumeimaliza.

    Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    8/104

    8

     Mheshimiwa Spika;

    Mtakumbuka kuwa nilizungumzia kusononeshwa

    kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo Zanzibar

    wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia

    kuuondoa. Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani

    ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka

    ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na

    mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya

    yote hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii

    yamekuwa bora zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya

    hapo.

    Ni matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibarwatayadumisha mafanikio haya ili waendelee kuishi kwa

    amani, upendo na udugu. Natambua kuwepo kwa

    changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali

    hiyo. Jambo linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe

    hayahusu muundo wa Serikali bali yanaletwa na watu

    kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    9/104

    9

     baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo

    yanayoweza kumalizwa kwa wadau kukaa kitako na

    kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.

    Amani na Usalama

     Mheshimiwa Spika;

    Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama kwa sababu

     Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea

    kutimiza ipasavyo jukumu lake la kulinda uhuru na mipaka

    ya nchi yetu. Katika kipindi hiki tumewekeza sana katika

    kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na zana za kisasa za kivita

    na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu, Anga na

    Majini. Utayari kivita wa jeshi letu ni mzuri tena wa hali ya juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya juu.

    Tumeboresha maslahi na makazi ya wanajeshi kwa kujenga

    nyumba mpya za kuishi. Utekelezaji wa mpango wa

    kuwajengea nyumba10,000unaendelea vizuri. Hadi hivi

    sasa nyumba6,064zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati

    yake nyumba3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    10/104

    10

    cha kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na

    Usalama kwa kujiamini kwamba “Tupo vizuri”. Pamoja na

    hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa

    kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu

    pale tulipopakusudia.

     Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya

    kupambana na uhalifu ili kulinda usalama wa maisha na

    mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka kuwa mwaka

    2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya

    ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba

    yangu Bungeni kwamba hatutawaacha majambaziwaendelee kutamba. Hali ile imedhibitiwa. Ingawaje

    matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama

    ilivyokuwa wakati ule.

    Hali kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali

    yamepungua kutoka53,268 mwaka 2005 hadi43,808 mwaka

    2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    11/104

    11

    kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.

     Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za

     barabarani. Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.

    Niruhusuni niwatambue na kuwashukuru Inspekta Jenerali

    (mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali (mstaafu) Said

    Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa

    uongozi wao mzuri.

    Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali

    katika utakelezaji wa mpango wa maboresho ya Jeshi la

    Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu Saidi

    Mwema, IGP mstaafu. Jeshi la Polisi linaendelea

    kuwezeshwa kwa zana, vifaa na mafunzo. Taratibuzimekamilika za kulipatia Jeshi hilo magari ya kutosha ili

    kuongeza ufanisi.

    Pia, tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya

    kuishi Maafisa na Askari. Kwa ajili hiyo tumekarabati

     baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba kadhaa

    mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni. Mipango

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    12/104

    12

    imekamilika ya kuwezesha ujenzi wa nyumba 10,000

    ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa

    nyumba za kuishi katika Jeshi la Polisi.

     Mheshimiwa Spika;

     Jeshi letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza

    vizuri majukumu yake ya kulinda wafungwa na kurekebisha

    tabia zao. Aidha, huduma za malazi, mavazi, chakula na

    usafiri kwa wafungwa zimeendelea kuboreshwa.

    Changamoto kubwa ni msongamano wa wafungwa

    Magerezani. Naamini mipango ya kujenga magereza mapya

    na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo litaisha. Aidha,

    mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika nakutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na

    kuishi maafisa na askari, hivyo kupandisha morali wao na

    kuongeza ufanisi.

     Jeshi la Kujenga Taifa

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    13/104

    13

    Ahadi yangu ya kuanzisha upya utaratibu wa

    kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria katika Jeshi la

    Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana38,200

    wamekwisha hitimu mafunzo hayo wakiwemo

    Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza sana Waheshimiwa

    Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia

    sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi. Ni

    matumaini yangu kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi

    na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa pamoja kujadili namna ya

    kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo. Naamini

    zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila

    matatizo yoyote.

    Utawala Bora

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza

    dhamira yetu ya kujenga na kuimarisha utawala bora kwa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    14/104

    14

    sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa rasilimali watu.

    Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo

    yale yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano

    dhidi ya rushwa, maadili ya viongozi, ukusanyaji wa mapato

    na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na mgawano

    wa madaraka hati ya mihimili.

    Bunge la Jamhuri ya Muungano

     Mheshimiwa Spika;

    Serikali imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili

    mkuu wa dola wa Kutunga Sheria. Tulianzisha Mfuko wa

    Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya Bunge toka

    shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadishilingi bilioni173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili

    kuwawezesheni Wabunge kuchangia katika kutatua

    changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi wa

    majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu

    yake kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu

    Kamati teule zilizoundwa.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    15/104

    15

    Katika kipindi hiki miswada163 imepitishwa, maswali

    ya msingi7,544 na ya nyongeza22,632 yameulizwa na

    kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya ni mafanikio

    makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa

    na kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa

    chachu ya baadhi ya hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria

    na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali. Kwa kweli mnastahili

    pongezi nyingi. Huwezi kutaja mafanikio ya Serikali ya

    Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa Bunge hili.

    Mchakato wa Katiba

     Mheshimiwa Spika;

    Kama sote tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa naBunge hili, mwaka 2013 tulianzisha mchakato wa

    Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi yetu Katiba

    mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba

    mchakato huo ulituwezesha kupata Katiba

    Inayopendekezwa ambayo imekidhi matarajio hayo. Narudia

    kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    16/104

    16

    na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na nzuri

    waliyofanya. Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni ambapo sote

    tunasubiri maelekezo ya Tume ya Uchaguzi. Mimi naamini

    iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa itaimarisha

    zaidi taifa letu.

    Vyama vya Siasa

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa

    vikiendelea kuimarika na kujijenga nchini. Idadi ya vyama

    vya siasa imeongezeka kutoka18 hadi24. Vyama vya siasa

    vimefanya shughuli zake kwa uhuru. Viongozi na

    wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hatamaandamano kote nchini. Baraza la Vyama vya Siasa na

    TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya kazi nzuri ya

    kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.

    Yamekuwa majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya

    vyama vya siasa kwa masuala mbalimbali. Matatizo na

    changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi. Ni

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    17/104

    17

    matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa

    na kuimarishwa miaka ijayo.

    Huu ni mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo

    wahusika wakuu. Ni matumaini yangu kuwa vyama vya

    siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi. Hii

    itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa

    uchaguzi.

    Uchaguzi Mkuu

     Mheshimiwa Spika;

    Habari kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu.

    Tayari Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar

    (ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwa nisiku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya uchaguzi

    huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi

    inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa

    mfumo mpya wa teknolojia yaBiometric Voters Register (BVR).

    Hadi sasa zoezi la uandikishaji limekamilika katika mikoa13

    na linaendelea katika mikoa11 na katika mkoa wa Dar es

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    18/104

    18

    Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza mwezi

    huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari wamekwisha

    andikisha hadi sasa wapiga kuramilioni 11 kati ya lengo la

    kuandikisha wapiga kura kati yamilioni 21hadi 23.

    Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu

    wa kuiwezesha Tume kutimiza wajibu wake. Napenda

    kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya

    kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime tuhimize

    watu wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki yao hiyo.

    Uhuru wa Habari Mheshimiwa Spika;

    Mtakubaliana nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa

    habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umepanuka sana.

    Tanzania kuna magazeti ya kila siku16 na kati ya hayo ya

    Serikali ni2(Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya kila

    wiki yapo62. Aidha, kuna vituo vya redio115 na vya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    19/104

    19

    televisheni29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya

    kuchapishwa au kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani

    yangu kwamba ustawi wa demokrasia hutegemea sana

    uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua

    manufaa ya vyombo vya habari kuelimisha jamii,

    kupambana na maovu na kuhimiza uwajibikaji.

    Pamoja na hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua

    hatua pale uhuru huo ulipotumiwa vibaya na kutishia

    kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii au taifa. Au,

    pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu

    wetu wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa

    kuutimiza. Mheshimiwa Spika;

    Katika kuongeza uwazi na mawasiliano na wananchi

    mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya wananchi. Tovuti hiyo

    imeshapokea hoja117,243 na kati ya hizo zilizohusu Serikali

    zilikuwa78,258 na zote zimeshughulikiwa.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    20/104

    20

    Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania

    imeshahama kutoka mfumo wa analogia na kuingia kwenye

    mfumo wa digitali. Hii ni hatua kubwa muhimu kwa

    maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo

    nasikitika kuwa hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa

    Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa Habari na Sheria ya

    Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa

    mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake

    haukuweza kufika mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao

    washughulike nayo katika Bunge la 11.

    Vita dhidi ya Rushwa Mheshimiwa Spika;

    Vita dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia

    njuga katika Awamu ya Nne. Tumepata mafanikio ya kutia

    moyo katika mapambano dhidi ya rushwa ingawaje kazi

     bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza,

    tumetunga Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    21/104

    21

    Kupambana na Rushwa ambayo imeongeza nguvu ya

    mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya rushwa

    iliongezwa kutoka4mpaka24 na wigo wa wakosaji pia, kwa

    kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya upelelezi na

    uendeshaji mashitaka nayo imeimarishwa.

    Tumeunda chombo kipya TAKUKURU badala ya

    TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya kuzuia na

    kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake.

    TAKUKURU imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza

    mapambano haya. Taasisi imeendelea kuimarishwa kwa

    kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na

    rasilimali watu na mahitaji mengine. TumeiwezeshaTAKUKURU kufungua ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.

     Mheshimiwa Spika;

    Maboresho haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma

    za rushwa zinazofikishwa mahakamani kuongezeka kutoka

    kesi50mwaka 2005 hadi1,900mwaka 2014. Jumla ya

    shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali97

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    22/104

    22

    wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi

    mabaya ya ofisi zao baada ya ushahidi wa kijinai

    kukosekana. Kwa upande wa kupambana na rushwa

    kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya

    Kudhibiti Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili

    kutoa majibu ya kilio cha siku nyingi dhidi ya watu

    wanaotumia fedha kununua kura.

    Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali

     Mheshimiwa Spika;

    Nilieleza katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la

    Tisa tarehe 30 Desemba, 2005 kuwa tutatoa kipaumbele cha

     juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na nidhamu yamatumizi ya Serikali. Leo miaka kumi baadae ninaona

    fahari tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali

    yameongezeka kutokashilingi bilioni 177.1 mwaka 2005

    kwa mwezi hadi takriban shilingi bilioni 850. Hii

    imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutokatrilioni 4.13

    mwaka 2005/2006 haditrilioni 22.49 mwaka 2015/2016.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    23/104

    23

    Isitoshe imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya

    washirika wa maendeleo kutokaasilimia 42 ya Bajeti ya

    Serikali mwaka 2005 hadiasilimia 15 mwaka 2014/2015 na

    tumejipa lengo la kushusha zaidi hadiasilimia 8 mwaka

    huu wa fedha wa 2015/2016.

     Mheshimiwa Spika;

    Mafanikio haya yametokana hasa na kazi kubwa

    tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka ya Mapato ambao

    wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza

    kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa

    mianya ya kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na

    mamlaka nyingine za ukusanyaji mapato ya Serikali. Badoukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya kodi katika

    Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara

    zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo.

    Huku kuendelee kufanyiwa kazi.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    24/104

    24

      Kwa upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na

    mali za Serikali tulielekeza nguvu zetu katika kuimarisha

    utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi wa hesabu za

    Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,

    tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa

    Umma ili iweze kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti

    wa sheria hiyo na kanuni zake. Kama mjuavyo sehemu,

    kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi wa

     bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni

     jambo jema. Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali,

    tumechukua hatua za makusudi za kuimarisha Ofisi ya

    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

    Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi

    Ofisi hiyo. Aidha, tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    25/104

    25

    rasilimali watu. Ofisi8 za Mikoa zimejengwa na2

    zinaendelea kujengwa.

    Nafurahi kwamba maagizo yangu kwa viongozi na

    watendaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu

    Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

    kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa zinasomwa,

    zinajadiliwa na hatua kuchukuliwa kwa kasoro

    zilizoonekana. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali

    imefanya kazi nzuri. Wezi na wabadhirifu wanaobainika

    kuchukuliwa hatua za kisheria mara makosa

    yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni

    kwa muda wa kutosha. Mheshimiwa Spika;

    Niliamua pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa

    Ndani wa Serikali na kuwaweka Wakaguzi wa Ndani wote

    wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka yake

    na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria

    na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    26/104

    26

    zinaheshimiwa. Pia, katika ufuatiliaji na utekelezaji wa

    mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa ukaguzi wa ndani na

    ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali kuwa

    nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu

    zinazidi kupungua Serikalini. Kwa mfano katika

    Halmashauri za Wilaya na Miji, hati safi zimeongezeka

    kutoka56 mwaka 2006 hadi150 mwaka 2014. Hati zenye

    mashaka ni13 na hakuna Hati isiyoridhisha. Kazi ya

    kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima

    iendelezwe.

    Maadili ya Viongozi wa Umma

     Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka 10 hii tumeimarisha mfumo wa

    kusimamia maadili ya viongozi. Tumefanya hivyo kwa

    kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya kiongozi

    na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    27/104

    27

    Maadili na kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria

    ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya 1995.

    Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi na

    familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la

    Mali la kila mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa

    kiongozi kuficha mali kwa mgongo wa mwenza wake au

    mtoto.

     Mheshimiwa Spika;

    Kamati ya Maadili sasa si tu inapokea fomu na

    kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi wa mali za viongozi na

    kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali fedha. Hili

    litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa yakimaadili wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili.

    Sote tumeshuhudia kazi nzuri iliyofanywa na Baraza hilo

    wakati wa sakata la Escrow. Bado kazi ya kuimarisha

    Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,

    majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.

    Muhimili wa Mahakama

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    28/104

    28

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi cha miaka10 hii tumefanya jitihada

    kubwa za kuimarisha mhimili wa Mahakama. Miongoni

    mwa mambo mengine, tumefanya mambo muhimu kwa

    madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa

     jukumu lake la msingi la utoaji haki.

    Kwanza, tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za

    utawala. Tumeunda Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama

    ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala. Hivyo basi,

    Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki.

    Mpaka sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa

    makubwa kwa Mahakama kwani yameboresha utekelezaji

    wa majukumu katika Mahakama.Pili, tumeanzisha Mfuko

    wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika

    kuendesha shughuli zake. Sambamba na hilo tumeongeza

     bajeti ya Mahakama kutokashilingi bilioni 36.6mwaka

    2006/07 hadishilingi bilioni 87.6mwaka 2014/15. Jambo

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    29/104

    29

    linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati ili

    shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.

     Mheshimiwa Spika;

     Jambo latatu,ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji

    wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu Wakazi na

    Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Lengo letu ni

    kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri.

    Kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo

    wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya Sheria. Hivi

    sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama

    hizo kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na

    2015 tumeongeza Majaji wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005

    hadi16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka37 hadi81

    katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya

    Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo5na

    katika Mahakama Kuu wapo32 na kufanya jumla yao kuwa

    37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu Wakazi1,266 katika

    ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao534 sawa naasilimia

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    30/104

    30

    35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake

    hivi sasa ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.

     Mheshimiwa Spika;

    Kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu

    Mohamed Chande Othman Mahakama zimepiga hatua

    kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.

    Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na

    kuamua mashauri yasiyopungua220 kwa mwaka na kila

    Hakimu Mkazi mashauri250 na wale wa Mahakama ya

    Mwanzo mashauri260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo,

    kuanzia Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015

    yalifunguliwa mashauri177,586 na Mahakama ilisikiliza na

    kuamua mashauri 179,962. Maana yake ni kuwa

    zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma.

    Bila shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia

    kuwa historia katika kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza

    sana Majaji na Mahakimu kwa kazi nzuri waifanyayo.

    Kwa upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu,

    wamekamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu za

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    31/104

    31

    Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama Kuu

    Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya

    Mahakama za Wilaya na12 ya Mahakama za Mwanzo nayo

    yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi unaendelea wa majengo ya

    Mahakama Kuu9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za Wilaya

    9 na za mwanzo25.

    Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki

     Mheshimiwa Spika;

     Jambo lingine ambalo tumefanya katika nia ya

    kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na kupunguza malalamiko ya

    wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni kutenganisha

    kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wamashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya

    yote sasa watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi

    wa Mashtaka ndiyo inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za

    Mkurugenzi wa Mashtaka zimekwishafunguliwa katika kila

    Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha, tumeboresha Ofisi

    ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    32/104

    32

    vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji

    wa ofisi hiyo muhimu sana. Kuna haja ya kuendelea

    kuongezea rasilimali fedha na vitendea kazi ili ufanisi

    uongezeke zaidi.

    Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za

    Binadamu na Utawala Bora kwa kuiwezesha kwa nyenzo,

    rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi katika

    eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na

    utumiaji wa mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi

    mengi zaidi yanafikishwa kwenye Tume na mengiyanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko

    yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka9,455mwaka

    2006 hadi 25,921 mwaka 2014 na uwezo wa Tume

    kushughulikia malalamiko kwa mwaka umeongezeka

    kutoka malalamiko3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko

    18,501 mwaka 2014.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    33/104

    33

    Utendaji Serikalini

    Maeneo ya Utawala

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa nia ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha

    mikoa mipya4 ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavina

    wilaya mpya19. Pia,tulianzisha Halmashauri45, kata 1,432,

    vijiji1,949, Mitaa1,379 na vitongoji8,777. Nimeamua

    kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya

    na Wilayasita kama ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi,

    Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es Salaam, Songwe

    mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani

    Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwasasa tufanye haya.

    Maslahi ya Wafanyakazi

     Mheshimiwa Spika;

    Serikali ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu

    suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa Serikali. Karibu

    kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha chini cha

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    34/104

    34

    mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara

    kimeongezeka kutokashilingi 65,000 mwaka 2005 hadi

    shilingi 265,000 mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia

    shilingi 300,000. Najua bado hakikidhi mahitaji lakini

    ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki tumeongeza sana

    mishahara ya wafanyakazi. Vile vile, tumeendelea

    kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutokaasilimia

    18 mwaka 2005 hadiasilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu

    ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa wafanyakazi. Vile vile,

    tumewapandisha vyeo watumishi 233,876 na kulipa

    malimbikizo ya watumishi422,348 ya kiasi chashilingi

    bilioni 384.8. Mheshimiwa Spika;

    Tumetekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wilaya

     jambo ambalo limelazimu kuongeza rasilimali fedha na watu

    kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa ajili hiyo ruzuku

    kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutokashilingi bilioni

    780 mwaka 2005/2006 hadishillingi trilioni 4.69 mwaka

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    35/104

    35

    2015/2016. Aidha, tumeimarisha utumishi katika

    Halmashauri kwa kuajiri watumishi wengi wa kada

    mbalimbali.

    Usawa wa kijinsia

     Mheshimiwa Spika;

    Mwaka 2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa

    kuzindua Bunge la Tisa, kuwa tutaongeza ushiriki wa

    wanawake katika shughuli na nyanja mbalimbali za maisha

    ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi. Ninyi na

    mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi

    ya Wabunge wanawake imeongezeka kutoka62mwaka 2005

    hadi127.Hivi sasa hamsini kwa hamsini ni rasmi katikaKatiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya kwanza katika

    historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika

    mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.

    Wanawake wameongezeka katika ngazi zote kuu za

    uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri wanawake10, Naibu

    Mawaziri wanawake5, Majaji wanawake37 na Wakuu wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    36/104

    36

    Wilaya wanawake wako53. Kwa upande wa Makatibu

    Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,

    Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka. Katika

    elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya

    wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na

    sekondari. Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya

    wanafunzi wa kike imeongezeka kwa kasi kutoka10,039

    mwaka 2005 hadi78,800 mwaka 2014.

    Hali ya Uchumi

     Mheshimiwa Spika;

    Wakati ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi

    Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo

    kujenga uchumi ulio imara na shirikishi. Hususan, nilisema

    nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka

    misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira,

    kuongeza Pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    37/104

    37

    miaka kumi iliyopita tumeendelea kusimamia kwa kiwango

    kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi katika ngazi

    ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.

     Jitihada zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo.

    Katika kipindi hiki, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa

    takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa10

    ya Afrika na20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa

    kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara

    tatu kutokashilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia

    trilioni 79.4mwaka 2014. Hivyo basi, pato la wastani la

    Mtanzania nalo limeongezeka kutoka shilingi 441,030

    mwaka 2005 hadishilingi 1,724,416 mwaka 2014. Mheshimiwa Spika;

    Mauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za

    Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani

    bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu ya fedha

    za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    38/104

    38

    nchi kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.1 kama

    tulivyopanga. Mfumuko wa bei niasilimia 6.1.

     Mheshimiwa Spika;

    Kama mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira

    ya Taifa ya Maendeleo ya hadi mwaka 2025. Mwaka 2010

    tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long Term

    Perspective Plan) wa (2010 – 2025) wa kuongoza utekelezaji

    wa Dira kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake

    katika Mipango mitatu ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila

    mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za utekelezaji wa

    Mpango wa Kwanza, (2011/12 – 2015/16) na kuandaa

    mpango wa pili (2016/17 – 2021/22).Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali

    nilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

    Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na kusimamia

    utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    39/104

    39

    kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa

    wakati. Tuliamua kuanza na sekta sita zaElimu, Nishati,

    Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato ya Serikali. Baadae

    sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji

    ziliongezwa.

    Katika kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa

    wenye manufaa. Mambo katika sekta zilizojumuishwa katika

    BRN yameanza kwenda vizuri. Changamoto yetu kubwa

    imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa wakati

    kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo isingekuwepo

    mambo yangekuwa mazuri zaidi.

    Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Spika;

    Kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza

    uchumi, kuzalisha ajira, kuongeza mapato na kupunguza

    umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua hatua thabiti za

    kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    40/104

    40

    ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa

    kuwekeza.

    Mwaka 2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya

    Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public

    Private Partnership—PPP). Lengo letu ni kuweka mazingira

    mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali

    katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya

    utaratibu huu ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza

    katika baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi inaweza

    kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu inaongeza kasi ya

    maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha ambazo

    inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine. Juhudi zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji

    zinaendelea kuzaa matunda mema. Kati ya 2005 na 2014,

    Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi7,159

    yenye thamani yaDola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya

    miradi hiyoasilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani,

    asilimia 23.41 ni wawekezaji wa kutoka nje naasilimia 27.18

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    41/104

    41

    ni miradi ya ubia baina ya Watanzania na wawekezaji wa

    kigeni. Ajira16,000 zilipatikana. Ukuaji huu wa uwekezaji

    umeongeza mapato ya Serikali.

    Kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda na Biashara

    Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania inaongoza

    Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. IlipataDola za

    Marekani bilioni 2.142 sawa naasilimia 31.5 ya uwekezaji

    wote katika Jumuiya yetu.

    Sekta za Uzalishaji

    Sekta ya Kilimo

     Mheshimiwa Spika;Kuendeleza kilimo ilikuwa ni moja ya mambo

    tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha yetu kuu ni kutaka

    kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima wapate

    mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri

    ili mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile

    vile wao na taifa lijitosheleze kwa chakula.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    42/104

    42

    Kwa ajili hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka

    7 ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector

    Development Programme—ASDP). Katika Programu hiyo,

    matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa

    mdogo yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa

    kuyatatua. Serikali pia ilianzisha mikakati, programu na

    mipango mingine ya kuongeza msukumo katika kuleta

    mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa

    Kilimo Kwanza, Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika

    Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mpango wa

    Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP), Sera ya

    Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu yaMageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika.

     Mheshimiwa Spika;

    Pamoja na hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya

    kilimo kutokashilingi bilioni 233.3 mwaka 2005/06 hadi

    shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15. Kuongezwa kwa

     bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    43/104

    43

    pembejeo kuongezeka kutokashilingi bilioni 7.5mwaka

    2005/06 hadishilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/14.

    Matrekta makubwa na madogo yameongezeka kutoka7,491

    mwaka 2005 hadi16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo

    matumizi ya jembe la mkono yamepungua kutokaasilimia

    70 hadiasilimia 62. Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379

    mwaka 2005 hadi7,974 mwaka 2014.

    Vituo vya utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali

    fedha, watu na vitendea kazi. Aidha, tumeanza safari ya

    kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha sekta

     binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika

    kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu(Agricultural Seed Agency – ASA) na kuongeza uzalishaji wa

    mbegu bora kutoka tani10,477.17 mwaka 2005 hadi tani

    32,340mwaka 2014.

     Mheshimiwa Spika;

     Juhudi za Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda

    mazuri. Tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    44/104

    44

    chakula imeongezeka. Kwa upande wa mazao ya chakula

    uzalishaji umeongezeka kutoka tanimilioni 9.66 mwaka

    2005 hadi tanimilioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili

    limeliwezesha taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa

    asilimia 125 mwaka 2014 ikilinganishwa naasilimia 95

    mwaka 2005. Uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara

    umeongezeka toka tani427,738 mwaka 2005 hadi tani

    569,054mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta

    umeongezeka karibu ya mara4 toka tani1,389.9 mwaka 2005

    hadi tani5,545.6mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa matunda

    nao umeongezeka toka tanimilioni 1.2mwaka 2005 hadi

    tani milioni 4.4mwaka 2014 na maua toka tani5,862 haditani10,790.

     Mheshimiwa Spika;

    Upatikanaji wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa

    mazao ya wakulima bado ni changamoto. Pia kuna tatizo la

    upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao. Jitihada

    zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    45/104

    45

    kisasa nchi nzima. Programu ya Mageuzi na

    Modenaizesheni ya Ushiriki ilianzishwa ili kutatua tatizo la

    masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya kuanzisha soko la

     bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.

    Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa

    SACCOS na kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa itatoa

    mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya mapinduzi ya

    kilimo.

    Mifugo

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanzasafari ya kuleta mageuzi katika sekta hii. Safari hiyo

    tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya

    Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya

    sekta hii zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa

    utekelezaji. Katika kipindi hiki malambo1,008, majosho

    2,364na maabara104za mifugo zimejengwa. Visima virefu

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    46/104

    46

    101 vimechimbwa, malambo 370 na majosho 499

    yamekarabatiwa katika kipindi hiki cha miaka10.

    Ukarabati na ujenzi wa majosho umeongeza idadi

    kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi3,637 mwaka 2015.

    Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka2,270 mwaka 2005 hadi

    6,041 mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo

    kutoka kituo1 mwaka 2005 hadi vituo8mwaka 2015 na

    kuwezesha ng’ombe955,360 kuhamilishwa katika miaka 10

    hii.

     Mheshimiwa Spika;

    Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi

    tuliyoyajenga yamewezesha viwanda vya kusindika nyama,maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda vya

    kusindika maziwa vimeongezeka kutoka22 mwaka 2005

    hadi74 mwaka 2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya

    mifugo vimeongezeka kutoka viwanda6mwaka 2005 hadi

    80mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tanimilioni

    1.4za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    47/104

    47

    machinjio ya kisasa9 vimejengwa katika kipindi hiki.

    Usindikaji wa ngozi pia umeongezeka kutoka vipande

    790,000mwaka 2005 hadi vipandemilioni 3.78 mwaka 2014.

    Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)

    umefikia marobota957,860 ikilinganishwa na marobota

    178,100 mwaka 2005.

    Safari yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji

    kwenda kwenye ufugaji imeanza. Vijiji vingi vimeandaa

    mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo vimetenga

    maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji

    vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo

    ya malisho mbali na mazao ya wakulima. Pia, tuhimizeuhamilishaji kama mlango wa kuingilia kwenye kuboresha

    kosafu za mifugo yetu.

    Uvuvi

     Mheshimiwa Spika;

    Wakati nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005

    nilisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    48/104

    48

    kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika kutekeleza hayo

    tumefanya yafuatayo.Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya

    Mifugo na Uvuvi.Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili

    kuwawezesha wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa bei

    nafuu zaidi.Tatu, tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi sasa

    vina uwezo wa kudahili wanafunzi1,215 ikilinganishwa na

    wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii imetuwezesha kuongeza

    wagani wa uvuvi kutoka103 mwaka 2005 hadi540 mwaka

    2014.Nne, tumeongeza sana juhudi za kupambana na uvuvi

    haramu ili kutunza mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia

    kuvuliwa au kuuawa kwa samaki wadogo.

    Tumeimarisha maabara ya Taifa ya Samaki paleNyegezi kwa vifaa vya kisasa na wataalamu ili iende na

    wakati.Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza ufugaji

    wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka

    kutoka13, 011 mwaka 2005 hadi20, 325 mwaka 2014.

    Uvuvi haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi

    yameongezeka kutokashilingi bilioni 351.6 mwaka 2005

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    49/104

    49

    hadishilingi trilioni 1.8 mwaka 2013.Bado tuna kazi kubwa

    ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato ya

    wavuvi na taifa.

    Utalii

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za

    kuiendeleza sekta hii muhimu. Tumeongeza kutangaza

    vivutio vya utalii vya nchi yetu katika masoko makubwa

    duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani waasilimia 7.1

    na imechangiaasilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.

    Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii612, 754mwaka

    2005 hadi watalii1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitandakatika mahoteli imeongezeka kutoka15,828 hadi21,929.

    Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za Marekani

    milioni 823.05 mwaka 2005 hadiDola za Marekani bilioni 2

    mwaka 2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka

    32,673 hadi686,130 na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    50/104

    50

    165,883 hadi1,318,109. Haya ni mafanikio makubwa na ya

    kujivunia.

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la

    ujangili wa wanyamapori hasa wa ndovu kutokana na

    kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei kuwa

    kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la

    ujangili lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu nchini

    na dunia nzima. Tukaamua kuchukua hatua za kuidhibiti

    hali hiyo. Tumefanya operesheni tatu kukabiliana na tishio

    hili. Yakwanza, iliendeshwa na Idara ya Wanyamapori na

    Misitu wakishirikiana na TANAPA na NgorongoroConservation Area. Hii hasa ilihusu kupambana na ujangili

    katika hifadhi na mapori ya Kaskazini mwa Tanzania.

    Mafanikio makubwa yalipatikana.

     Mheshimiwa Spika;

    Operesheni yapili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi

    katika hifadhi na sehemu nyingine za Tanzania. Operesheni

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    51/104

    51

    Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata mafanikio. Na yatatu,

    Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya ulinzi

    na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi

    zimesaidia sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo

    yake katika sensa ya ndovu iliyofanyika mara ya mwisho,

    ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na mapori mengine ina

    muelekeo mzuri.

    Kuundwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA)

    yenye mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia sekta ya

    wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano

    ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani,

    naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.Viwanda

     Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea

    kukua kwa kasi nzuri ya kutia moyo. Viwanda vikubwa, vya

    kati na vidogo vimeongezeka kutoka11, 544 mwaka 2005

    hadi viwanda51,224mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005 na

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    52/104

    52

    2014 na miradi751 imepewa leseni za kudumu na BRELA ya

    kuanzisha viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda katika

    Pato la Taifa umefikiaasilimia 7.3  mwaka 2014 kutoka

    asilimia 6.8mwaka 2005. Mchango wa viwanda kwenye

    mauzo ya nje umeongezeka kutokaasilimia 9.3 mwaka 2005

    hadiasilimia 23.3 mwaka 2014.

    Tunategemea ukuaji mkubwa wa viwanda katika

    Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka5 kutokana na

    misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza.

    Ujenzi wa kiwanda cha chuma kule Liganga na makaa ya

    mawe cha Mchuchuma, unatarajiwa kuanza mwaka huu na

    kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza baada ya taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika.

    Hivi ni viwanda vya msingi na mama ambavyo vitachochea

    kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi kwa jumla.

    Madini

     Mheshimiwa Spika ;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    53/104

    53

    Sekta ya Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa

    kuingiza fedha nyingi za kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia

    upya sera, sheria na mikataba ya madini iliyokuwepo na

    kutengeneza sera na sheria mpya. Halikadhalika,

    tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo

    hatimaye yalizaa marekebisho ya mikataba yao na hivyo

    kuboresha maslahi ya taifa.

    Kufuatia marekebisho hayo, makampuni husika ya

    madini yanalipa kodi ya mapato. Bila ya hivyo huenda

    mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi. Kutumika

    kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na

    kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato yaSerikali. Aidha, tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini

    Tanzania (TMAA) ambao umewezesha kukagua mahesabu

    ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na

    kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa

    makampuni hayo.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    54/104

    54

    Mabadiliko haya pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji

    katika sekta hii yamewezesha mchango wa sekta ya madini

    katika Pato la Taifa kuongezeka kutokaasilimia 2.9 mwaka

    2005 hadi kufikiaasilimia 3.5mwaka 2014. Thamani ya

    mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka kutokaDola

    za Marekani milioni 655.5 mwaka 2005 hadi kufikiaDola za

    Marekani bilioni 1.794 mwezi Desemba 2014. Mambo

    yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu isingeshuka

    katika kipindi hiki.

     Mheshimiwa Spika;

    Serikali ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezeshaShirika letu la Madini (STAMICO) kuanza tena kazi ya

    utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia kampuni zake

    tanzu. STAMICO kwa kupitia kampuni yake ya

    STAMIGOLD imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje.

    Vilevile, tumejiunga na Mpango wa Uwazi wa Uvunaji wa

    Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika kuongeza

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    55/104

    55

    uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika

    ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye makampuni ya

    madini.

    Katika kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa

    nayo ni Migodi ya dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga) na

    New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka

    (Ruvuma). Aidha, miradi mikubwa mingine 8

    imeendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi

    ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Mradi wa

    Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa

    Mchuchuma (Njombe). Pia, ajira rasmi kwenye migodi

    mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517mwaka 2005 hadi waajiriwa15,000 mwaka 2014. Hali

    kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi wa

     bidhaa na huduma hapa nchini (local procurement) kutoka

    Dola za Marekani milioni 230.41mwaka 2005 hadiDola za

    Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    56/104

    56

    Katika kipindi hiki pia, tumetengamaeneo 8 kwa ajili

    ya wachimbaji wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha

    wachimbaji wadogo kuchimba madini bila bughudha.

    Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya

    uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili

    ya wachimbaji wadogo. Tumeanzisha mfuko wa

    kuwakopesha wachimbaji wadogo pale Wizarani ili kutoa

    fursa kwa wachimbaji wadogo kupata mikopo ya

    kuendeleza shughuli zao.

    Nishati

     Mheshimiwa Spika;Wakati naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania

    ilikuwa inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababisha

    upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na upungufu

    mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha

    umeme kukosa maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha

    watu zaidi ya milioni3,776,000 na kukodisha mitambo ya

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    57/104

    57

    kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni tuliamua kuchukua

    hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa

    kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya

    mawe, mionzi ya jua na upepo.

    Ujenzi umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi

    kutoka Mtwara na Songo Songo litakaloongeza kiasi cha gesi

    kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji wamegawati

    3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya

    kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam.

    Umeme huo utakidhi mahitaji ya umeme sasa na miaka

    kadhaa ijayo.

     Mheshimiwa Spika; Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme Vijijini

    (REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya

    kusambaza umeme kwa vijiji5,336 kati ya vijiji12,423 nchini.

    Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa na ile ya

    mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata umeme

    kutokaasilimia 10 hadiasilimia 40 mwaka 2015. Uamuzi

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    58/104

    58

    uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa kukusanya fedha

    kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta ya petroli,

    utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini.

    Gesi Asilia

     Mheshimiwa Spika;

    Tumepata mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi

    asilia. Kuanzia mwaka 2010 nchi yetu imepata bahati ya

    ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari kuu. Mpaka sasa

    zimegundulika futi za ujazotrilioni 47.08.Ukijumlisha na

    futi za ujazotrilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40

    iliyopita kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali

    ya gesi asilia nchini ni futi za ujazotrilioni 55.08. Kazi yautafutaji inaendelea na wataalamu wanasema kuwa

    Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazotrilioni 200.

    Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni kikubwa na

    kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa kuipatia dunia

    nishati hii.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    59/104

    59

    Gesi asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri

    itaiwezesha nchi yetu na watu wake kupata maendeleo

    makubwa na kuondokana na umaskini. Ni fursa ya aina

    yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha

    kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake.

    Lakini, ili hayo yaweze kufanyika hapana budi pawepo

    usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu za mnyororo wa

    thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji, uuzaji wa

    gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali

    ghafi ya viwanda upande mmoja. Upande mwingine

    inategemea sana matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na

    rasilimali hiyo. Mheshimiwa Spika;

    Ni kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo

    yanakuwa hivyo ndiyo maana tumetunga Sera ya Gesi Asilia

    na kuwasilisha katika Bunge hili ile Miswada miwili yaani

    wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato ya

    Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    60/104

    60

    kuipitisha Miswada hii nami nitaitia saini mara

    nitakapoletewa.

    Usafirishaji na Uchukuzi

    Barabara

     Mheshimiwa Spika;

    Serikali ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu

    kwa uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji na

    uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na barabara, reli, bandari,

    usafiri wa majini na usafiri wa angani. Tumeendeleza kazi

    ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa

    mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na

    zile zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kaziya ujenzi inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po

    pote nchini kwenda Dar es salaam unafika siku hiyo hiyo,

    tofauti na ilivyokuwa zamani watu walichukua zaidi ya siku

    moja. Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa

    Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    61/104

    61

    Katika mkakati wetu wa kupanua mtandao wa

     barabara za lami nchini, tulitambua barabara za urefu wa

    kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami. Baadae

    tuliongeza barabara nyingine na kufikishakilomita 17,742

    katika mpango huo. Utekelezaji wake upo katika hatua

    mbalimbali. Tayari ujenzi wakilomita 5,568 kwa upande wa

     barabara kuu nakilomita 535kwa barabara za mijini

    umekamilika. Ujenzi wa kilomita 3,873 unaendelea.

    Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara

    za urefu wakilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana

    fedha ujenzi uanze. Baadhi ya barabara hizo zimo katika

     bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za urefu wakilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu

    wa kina.

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki pia, madaraja madogo7,200 na

    makubwa12 yamejengwa na mengine16 yapo katika hatua

    mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja makubwa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    62/104

    62

    yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa

    ni daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja

    haya yalikuwa miongoni mwa matano yaliyopangwa

    kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa

    Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani

    la Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003.

    Kwa upande wa vivuko, tumeongeza vipya15 na kufikisha

    idadi ya28 kote nchini mwaka 2014.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumeongeza sana fedha katika mfuko wa barabarakutokashilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/06 hadishilingi

    bilioni 866.63 mwaka 2015/16. Hii itasaidia katika

    matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga

    nyingine mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha

     barabara za udongo na changarawe wilayani na vijijini

    ziweze kupitika wakati wote. Katika kipindi hiki barabara

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    63/104

    63

    za changarawe zimeongezeka kutokakilometa 9,424hadi

    kilometa 22,089.

     Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani

    magari, bajaji na pikipiki imeongezeka kutoka1,696,088

    mwaka 2005 hadi3,313,254 hivi sasa. Ongezeko hili

    linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri

    limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi

    nchini. Katika jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa

    zaidi na Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali

    kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa baadhi ya

     barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) nasasa tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine

    (flyovers). Tulianzisha matumizi ya treni katika reli za

    TAZARA na TRC kusafirisha abiria. Hivi sasa reli hizo

    zinasafirisha abiriamilioni 2,804,269 kwa mwaka ambao

    wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    64/104

    64

    kuendeleza matumizi ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa na

    tumeanza kuutafutia fedha.

    Usafiri wa Reli

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta

    ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili reli zetu za TAZARA

    na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa zinakabiliwa na

    matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na

    uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli

    hizi ambazo kila moja inaweza kusafirisha tanimilioni 5

    kwa mwaka zinasafirisha kati yatani 200,000 na300,000tu.

    Hivyo basi, mizigo mingi husafirishwa kwa barabara nakutishia uhai wa barabara ambazo tumezijenga kwa

    gharama kubwa.

    Kwa upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya

    Dar es Salaam na Tabora unakaribia kukamilika na

    utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza. Wakati huo huo

    mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    65/104

    65

    (standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza

    mwaka huu kutegemea kukamilika kwa majadiliano na

    mabenki yaliyoonyesha utayari wa kutukopesha pesa za

    ujenzi.

     Mheshimiwa Spika;

    Azma yetu ya kufufua reli ya TAZARA nayo

    tumeiwekea mkakati. Sisi na Zambia tumekubaliana

    kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa

    matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki

    zetu wa China nao wamekubali kutusaidia katika mipango

    yetu hiyo. Ni matumaini yangu kuwa safari hii tutapata

    ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo yanayoathiri ufanisi wareli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na ustawi wa

    uchumi wa nchi zetu na watu wake.

    Bandari

     Mheshimiwa Spika;

    Tumeboresha na kuimarisha huduma katika bandari ya

    Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa. Mwaka 2014

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    66/104

    66

     bandari yetu ilihudumiatani milioni 14.4 ukilinganisha na

    tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia

    tanimilioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwasaa 24 na

    kasi ya kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka

    sana na wizi umepungua sana. Hata wale walioacha

    kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.

     Mheshimiwa Spika;

    Kuanza kutumika kwa mfumo wa Single Custom’s

    Territoryunaorahisisha upakuaji na upakiaji mizigo ya nchi

    za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza zaidi ufanisi.

    Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao

    wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.Kuongezeka kwa usafirishaji wa mizigo inayopita

    nchini kuna faida kwani sekta ya usafirishaji inachangia

    zaidi yaasilimia 15 ya pato la taifa. Hali kadhalika, ujenzi

    wa gati za 13 na14 katika bandari ya Dar es Salaam

    unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya

    makasha kuongezeka kutoka makasha600,000 hadi makasha

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    67/104

    67

    1,200,000. Mipango ya kuboresha bandari za Mtwara, Tanga

    na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu na ujenzi wa

     bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania kunufaika na

    fursa ya jiografia yake.

    Usafiri wa Anga

     Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya

    kuwekeza kwenye ukarabati, upanuzi na ujenzi wa viwanja

    vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa Ndege wa

    Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo

    wa kuhudumia kutoka ndege7 hadi30 hivi sasa. Aidha

    tunajenga jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo lenyeuwezo wa kuhudumia abiriamilioni 3.5. Ujenzi huo

    unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

    Kukamilika kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa

     Julius Nyerere kuhudumia abiriamilioni 6na ndege nyingi

    zikiwemo ndege kubwa za kisasa za Airbus 380.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    68/104

    68

    Vile vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja wa

    Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa sekta

    ya utalii ya ukanda wa kaskazini. Uwanja mpya wa ndege

    wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi sasa

    unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja

    vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora,

    Mwanza na Bukoba.

    Ujenzi, upanuzi na ukarabati huu tulioufanya,

    umechangia sana katika ongezeko kubwa la safari za ndege

    na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini zimeongezeka

    toka safari78 mwaka 2005 zilizokuwa zinatolewa na

    kampuni 29 za usafiri wa ndege hadi safari175 zinazotolewana kampuni55mwaka 2014. Aidha, abiria wanaoondoka na

    kuwasili katika viwanja vya ndege wameongezeka kutoka

    2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria4,670,380mwaka 2013.

    Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka

    kwa kasi kubwa.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    69/104

    69

     Jambo ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la

    kufufua Shirika letu la Ndege. Tumefanikiwa kulifanya lisife

    lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata kwenye ile hali

    yake ya zamani. Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu

    mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa

    Menejimenti imepewa jukumu la kuandaa mpango wa

     biashara unaoeleweka na unaokopesheka, kisha Serikali

    itaona namna ya kulisaidia shirika.

    Utabiri wa Hali ya Hewa

     Mheshimiwa Spika;Sambamba na hayo, tumeboresha huduma za utabiri

    wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa imepatiwa vifaa

    vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa utabiri

    unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata cheti

    cha utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya

    taarifa zake kutambuliwa kimataifa.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    70/104

    70

    Mawasiliano

     Mheshimiwa Spika;

    Tumepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya

    habari na mawasiliano. Tumejenga Mkongo wa Taifa wa

    Mawasiliano wenye urefu wakilometa 7,560 unaounganisha

    miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa

    mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na Pemba, ujenzi

    wake utakamilika mwezi ujao. Katika Awamu ya Pili, Mkoa

    wa Simiyu na wilaya zote nchini zitaunganishwa.

    Ujenzi wa mkongo huu umechangia katika kuongeza

    ubora na kasi ya mawasiliano, na kushusha gharama za

    mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simuzimeshukakutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005

    hadishilingi 34.92 mwaka 2014 na gharama za intaneti

    zimeshuka kutoka wastani washilingi 36,000 kwa Gigabyte

    moja mwaka 2005 hadi wastani washilingi 9,000 kwa

    Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014. Hii imeshusha pia

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    71/104

    71

    gharama za biashara kwa kurahisisha mawasiliano na

    malipo kati ya mabenki na kwa njia ya mtandao na simu.

    Kwa upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka

    lainimilioni 2.96mwaka 2005 hadimilioni 28mwaka 2014.

    Watu wanaotumia intaneti wameongezeka tokamilioni 1.6

    hadimilioni 9.3mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya

    simu kumewezesha watumiajimilioni 12.3 kupata huduma

    ya fedha kupitia simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na

    Aprili 2014 jumla ya miamalamilioni 972.6 ilifanyika yenye

    thamani yashilingi trilioni 28. Huu ni wastani wa zaidi ya

    shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania

    kuongoza duniani kwa huduma hii. Mheshimiwa Spika;

    Tulitambua kuwa makampuni binafsi ya simu

    hayapendi kuwekeza vijijini ambako biashara si kubwa kama

    mijini. Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya

    mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo

    huo. Kwa sababu hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    72/104

    72

    kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha kata na vijiji vyote

    nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo

    umekwisha wezesha jumla ya kata52 na vijiji314kufikiwa

    na huduma hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano

    kupitia Mfuko huo zinaendelea kwa kata nyingine163 zenye

    vijiji922, ambapo wananchimilioni 1.2 watanufaika.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumechukua hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya

    kodi inazibwa na kwamba makampuni yanalipa kodi stahiki

    kwa kununua na kufunga mtambo wa Kusimamia

    Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha

    Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu halisiza mawasiliano yanayofanywa. Tangu kuanza kutumika kwa

    mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza kukusanya

    shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo zisingepatikana.

    Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika ya Mashariki

    kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali. Karibu

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    73/104

    73

    tutakamilisha kwa mikoa yote. Tunazipokea nchi kadhaa

    zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji wa zoezi hili.

    Ardhi na Makazi

     Mheshimiwa Spika;

    Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na

    kuboresha makazi ya watu. Sote tunafahamu kuwa makazi

    ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la kuboresha

    huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio

    makubwa. Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu

    zaidi na wananchi kwa kuanzisha Kanda nane za kusimamia

    upangaji, upimaji na utoaji hatimiliki. Uamuzi huu

    umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata hatimiliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati164,275zimetolewa,

    vijiji10,500 vimepimwa na kati yake vijiji10,341 vimepatiwa

    hatimiliki.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumetunga Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji

    wa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    74/104

    74

    pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba (Mortage Finance)

    na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa

    kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria

    hizi kwa ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi

    kupata mikopo ya kujenga au kukarabati nyumba zao na

    kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya jengo.

    Mabadiliko hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba

    kukua kwa kasi kubwa na majengo na nyumba za kisasa

    kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es Salaam ya

    leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la

    Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya

     Jamii nayo imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenziwa nyumba katika kipindi hiki.

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa watumishi wa serikali kuwa na

    nyumba mwaka 2008 tulianzisha Mfuko wa Mkopo kwa

    watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya

    shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi1,169. Pia, tumeanzisha

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    75/104

    75

    Kampuni ya Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa

    umma ambayo tayari imeanza kazi.

     Mheshimiwa Spika;

    Ninayo furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia

    yameendelea kuwa bora. Takwimu za Sensa ya Watu na

    Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi ya nyumba

    zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutokaasilimia 46

    mwaka 2002 hadiasilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha

    nyingine nyumba zilizoezekwa makuti na nyasi zimezidi

    kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia moyo na

    hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.

    Utafiti Mheshimiwa Spika;

     Jambo lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni

    eneo la utafiti. Hili ndilo eneo ambalo ilitalivusha taifa letu

    kwenda katika maendeleo makubwa zaidi. Niliamua Serikali

    ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli za utafiti

    ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu. Niliamua

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    76/104

    76

    kuwa Serikali ianze safari ya kutenga fedha za kutosha kwa

    ajili ya utafiti. Tulianza nashilingi bilioni 10na kuendelea

    kuongeza mwaka hadi mwaka na kufikashilingi bilioni 60

    mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi kufikiaasilimia 1

    ya bajeti ya Serikali na hatimayeasilimia 1 ya pato la Taifa

    kwa ajili ya shughuli za utafiti.

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi

    wetu 344 wamepata ufadhili wa masomo ya shahada ya

    Uzamili na173 wa shahada ya Uzamivu. Miradi70 ya utafiti

    imefadhiliwa, kati ya hiyo22 ni ya kilimo. Fedha hizi pia

    zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojiakuanzisha viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha

    vijana wetu kubuni na kuvumbua teknolojia zenye manufaa

    kwa maendeleo ya jamii na taifa. Wamezalisha ajira na

    kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni mfano

    mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.

    Huduma za Jamii

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    77/104

    77

    Elimu

     Mheshimiwa Spika;

    Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa mwaka

    2005 nilisema kuwa, “ Hakuna Taifa lililopata maendeleo

    bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza elimu nchini

    itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne”.

    Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka kumi

     bajeti ya sekta ya elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko za

    sekta nyingine zote. Mwaka huu 2015 bajeti ya elimu

    imefikiashilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa nashilingi

    bilioni 669.5 za mwaka 2005.

    Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani

    ya miaka 10 hii ni ya kutia moyo. Tumeongeza shule za

    msingi kutoka14,257 mwaka 2005 hadi16,538 mwaka 2015

    na wanafunzi wameongezeka kutoka 7,541,208 hadi

    8,202,892. Upanuzi huu umewezeshaasilimia 98 ya watoto

    wanostahili kupata elimu ya msingi sasa kuandikishwa.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    78/104

    78

    Kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi

    tumeongeza Shule za Sekondari kutoka Shule1,745 mwaka

    2005 hadi Shule4,753mwaka 2015. Idadi ya wanafunzi

    imeongezeka kutoka524,325 mwaka 2005 hadi1,804,056

    mwaka 2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi

    vimeongezeka kutoka184mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015

    na wanafunzi katika vyuo hivyo wameongezeka kutoka

    40,059 hadi145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio

    makubwa sana.

    Kwa nia ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua

    hatua thabiti za kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu,

    vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya kujifunzia nakufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,

    Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi

    ya walimu wa Shule za Msingi kutoka135,013 mwaka 2005

    hadi202,752 mwaka 2015, na walimu wa Shule za Sekondari

    kutoka18,754 mwaka 2005 hadi88,908 mwaka 2015. Uhaba

    wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    79/104

    79

    kutosha. Tuna upungufu wa walimu20,141wa masomo wa

    sayansi na hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu

    za kusomesha walimu wa sayansi vyuoni zilizopo, katika

    miaka michache ijayo tatizo hili nalo tutalipatia ufumbuzi.

    Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014

    kimeanza kudahili wanafunzi5,000 wa ualimu wa masomo

    ya sayansi.

     Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa maabara za sayansi, katika shule za

    sekondari za kata tayari maabara5,979 zimejengwa na

    nyingine4,410ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.

    Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wavifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa

    vitabu tumeweza kuboresha upatikanaji wake kwa

    mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka uwiano wa1:5

    mwaka 2005 hadi1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari

    uwiano ni1:2ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    80/104

    80

    Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia upanuzi

    mkubwa wa elimu ya juu nchini. Idadi ya vyuo vikuu

    imeongezeka kutoka vyuo26 mwaka 2005 hadi52 mwaka

    2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha

    Dodoma na cha Nelson Mandela cha Arusha ambavyo

    vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Tumeanza

    mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha

    Kilimo kule Butiama. Vyuo hivi ni fahari ya nchi yetu kwani

    tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe bila msaada kutoka

    kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi ya

    wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi40,719 mwaka

    2005 hadi218,959mwaka 2014. Idadi ya wanafunziwanaonufaika na mikopo nayo imeongezeka kutoka

    wanafunzi16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi99,590

    mwaka huu.

    Afya

     Mheshimiwa Spika;

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    81/104

    81

    Tumepata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa

    kuboresha na kupanua huduma ya afya nchini. Tuliazimia

    kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa

    kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na

    kuimarisha vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya

    kutolea huduma za afya2,175 vimejengwa. Kati yake

    hospitali19, vituo vya afya 168 na zahanati1,883

    zimejengwa.

    Tumeimarisha hospitali ya Taifa ya Muhimbili,

    Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na Wilaya kwa

    kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,

    Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa yaAfya ya Jamii ambayo inatumika kama maabara ya

    Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC. Tumeimarisha

    maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya

    uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina

    uwezo wa kubaini virusi vya Ebola jambo ambalo miezi

    michache iliyopita tulikuwa tunapeleka sampuli Nairobi.

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    82/104

    82

    Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza kufanya uchunguzi

    wa mwenendo wa figo na ini.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumeboresha huduma ya Afya ya Kinywa katika

    Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga mashine26 za kisasa

    za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza meno

     bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa

    kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashuri91. Hivi

    sasa hospitali136, vituo vya afya63 na zahanati3 zinatoa

    huduma hiyo nchini.

    Tumeanza kupata mafanikio katika dhamira yetu ya

    kujenga uwezo wetu wa ndani wa kuchunguza na kutibumaradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya fahamu

    ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa

    mfano, tangu Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale

    Muhimbili wagonjwa 71,963 wamepatiwa matibabu

    wakiwemo 692 waliofanyiwa upasuaji. Watu hao

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    83/104

    83

    wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu

    utaongezeka sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumebadilisha utaratibu wa kusambaza dawa kutoka

    Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba

    kutokashilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadishilingi

    bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na

    Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya

    wameongezeka kutokaasilimia 3 mwaka 2005 hadiasilimia

    19 mwaka 2014.

    Katika kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika

    kupambana na maradhi makubwa ya kuambukizayanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha

    kampeni ya kupambana na malaria nchi nzima kwa

    kubadilisha dawa ya kutibu malaria na kugawa vyandarua

    26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa akina

    mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia

    dawa ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    84/104

    84

    ya ziwa. Matokeo ya jitihada hizo ni kupungua kwa

    maambukizi ya malaria kwaasilimia 51 na vifo kwa

    asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua

    viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya

    kutokomeza malaria hapa nchini ni ya uhakika.

     Mheshimiwa Spika;

     Juhudi zetu katika kupambana na ukimwi

    zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya ukimwi kutoka

    asilimia 7.7mwaka2005 hadiasilimia 5.1 mwaka 2012.

    Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka

    kutoka365,189 mwaka 2005 hadi25,468,564mwaka 2014.

    Aidha, tumewezesha vituo5,244na asilimia 97 ya vituovyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya kuzia

    maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

     Mheshimiwa Spika;

    Kati ya mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa

    wanafunzi katika vyuo vya afya kutoka3,025 mwaka 2005

    hadi11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho wataalamu wa

  • 8/20/2019 HOTUBA YA KUAGANGA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015 - FINAL.doc

    85/104

    85

    afya55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya kada

    mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya madaktari

    imeongezeka kutoka madaktari1,048 mwaka 2006 hadi

    madaktari2,325 mwaka 2014. Halikadhalika, madaktari

    wasaidizi wameongezeka kutoka1,223 hadi1,914, wauguzi

    kutoka15,961hadi22,942 wataalamu wa Maabara kutoka

    1,277 hadi2,378 mwaka 2014. Hivi sasa uwiano wa Daktari

    kwa wagonjwa ni 1:6,666ikilinganishwa na 1:35,714 mwaka

    2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa wagonjwa umeshuka

    kutoka1:2,347 mwaka 2005 hadi1:2,008 mwaka huu.

     Mheshimiwa Spika;

    Tumeendesha kampeni ya kub