20
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 149, Januari, 2020 ISSN 0856-874X Kufuatia watu wasiojulikana Kwanini waathirika wako kimya? IPI yataka Kabendera apewe dhamana Uk 7 Uk 15 Uk 9 Hofu yaua habari za uchunguzi

Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 149, Januari, 2020ISSN 0856-874X

Kufuatia watu wasiojulikana

Kwanini waathirika wako kimya?

IPI yataka Kabendera apewe dhamana

Uk 7 Uk 15Uk 9

Hofu yaua habari za uchunguzi

Page 2: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Ukiukaji wa uhuru wa habari ukomeshweVitisho dhidi ya waandishi wa ahabari, utekaji,

kunyimwa habari na mashambulizi ya kimwili yameripotiwa kutokea na kurekodiwa katika Rejista ya Ukiukaji wa Uhuru wa Habari

inayosimamiwa na Baraza la Habari Tanzania. Lakini mambo yaliyoibuliwa katika ripoti mbili

zilizotolewa na Baraza hivi karibuni yanaonyesha ukubwa wa matatizo yanayowakabili wanahabari na tasnia ya habari nchini.

Ripoti ya Uchunguzi wa Ongezeko la Vitisho na Kuingiliwa kwa Uhuru Uhariri na Ripoti ya Ukiukaji wa Uhuru wa Habari zimethibitisha mambo yanayosemwa kwamba siyo simulizi za kupuuzia.

Wanaofanya ukiuakaji huo dhidi ya vyombo vya habari na wanahabari ni wenye mamlaka na ujasiri wao wa kufanya vitendo hivyo unatokana na kauli na amri za wakubwa wenye mamlaka.

Matokeo yake waandishi wanakamatwa na kubambikiwa kesi na wakati mwingine hata wanapigwa.

Kutokana na uchunguzi uliowezesha kutolewa ripoti hizo, ni muhimu kwa wenye mamlaka kubadilisha tabia zao kwa wanahabari hasa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Vyombo vya habari vioga na vilivyobanwa havina maana kwa sasa kwa kuwa vitakuwa havitoi hali halisi ya yanayotokea nchini bali mambo yanayowafurahisha wakubwa.

Kinachotakiwa kwa vyombo vya habari ni kuwa makini, huru na kutoegemea upande wowote na hivyo kuwa chachu ya kukuza demokrasi, utawala bora, uwajibikaji, uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari.

Ingawa siku zote changamoto zimekuwepo katika uhuru wa habari Tanzania hali ya sasa haijawahi kutokea. Vitisho dhidi ya wanahabari na hata hatua za kukomoa na zingine si za haki kabisa, imefikia hatua ambapo hazijafikiwa hata kwenye mfumo wa siasa ya wa chama kimoja.

Ni muhimu zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote, kwa wenye mamlaka kuacha kuwa na mtazamo hasi kwa vyombo vya habari na kuwa na mtazamo chanya kwa mahusiano ya pande hizi mbili.

Kama ilivyoelezwa katika ripoti zilizotolewa na Baraza kuwa vyombo imara na huru vya habari ni muhimu kwa kuendeleza na kuimarisha demokrasi na ustawi wa taifa, ukiujkaji wa uhuru wa habari uzikwe.Tuweke hali ya kuwa na vyombo uhuru vya manufaa.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Wanahabari wakiwa katika chumba cha habari

Page 3: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 149, Januari, 2020

Na Mwandishi wa Barazani

Hofu ya kuchukuliwa hatua kali na wenye mamlaka imesababi-sha wanahabari na

vyombo vya habari kujidhibiti na kuua uandishi wa habari za uchunguzi nchini.

Vyombo vya habari vinachukua tahadhari kwa kuchapisha habari zinazowafurahisha wenye mamlaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi kuhusu kuongezeka kwa vitisho na kuingiliwa uhuru wa uhariri iliyotolewa karibuni na Baraza la Habari Tanzania

(MCT), wanahabari na wahariri wana wasiwasi.

Wanadhoofisha maudhui ya habari siyo kwa kuhofia vyombo vyao kufungiwa na kunyang’anywa leseni zao za kufanyakazi, bali pia kupoteza ajira na kubambikiwa kesi za uhalifu.

Kulinngana na ripoti hiyo, wamiliki wa vyombo vya habari wanaingilia maudhui ya habari za vyombo vyao ili kulinda biashara zao na kuhakikisha kuwa hawanyang’anywi leseni zao.

Gazeti la The Citizen lilifungiwa kwa wiki moja baada ya kuchapisha habari ambayo serikali haikuipenda.

Gazeti lingine, la Kiswahili – Nipashe Jumapili lilifungiwa na mmiliki wake kwa miezi mitatu baada ya kuchapisha habari ambayo haikuwapendekeza wenye mamlaka ambao waliafiki kuchukuliwa kwa hatua hiyo.

“Ukizingatia hali ya kiuchumi inayoendelea nchini,

Hofu, vitisho vyaua uandishi wa uchunguzi

Wahariri waliohudhuria mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Baraza na baadhi ya wawezeshaji wa mafunzo hayo.

Endelea Ukurasa wa 4

Page 4: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

mmiliki yeyote makini, hawezi kufanya jambo ambalo litasababisha chombo chake kufungiwa na watumishi kupoteza ajira” ripoti hiyo imeeleza ikimnukuu mmoja wa watu waliohojiwa.

Angalia matukio makubwa yanavyoripotiwa, inayonyesha kwa kiasi fulani vyombo vya habari vimeingiwa na hofu, mtu mwingine aliyehojiwa anaeleza katika ripoti hiyo.

Akizungumzia ripoti mbili za hali ya vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza zilizotolewa na Human Rights Watch na Shirika la Haki za Binadamu la Kimataifa zilizozinduliwa Nairobi, Kenya Oktoba 2019, alisema walishangazwa jinsi ripoti hizo hazikutumiwa na vyombo vingi vya habari Tanzania.

Vyombo vya habari vilivyochapisha habari za ripoti hizo zilizokuwa na vichwa – Bei Tunayolipa:Kulengwa kwa kuwa na mawazo tofauti na serikali ya Tanzania… kadri ninavyonyamaza, niko salama: na Vitisho kwa vyombo huru vya habari na mashirika yasiyo ya kiserikali, vilikuwa makini jinsi vilivyoandika habari zao na lugha waliyotumia.

Kuhusu vyombo vya habari kujidhibiti hali inayofanyika katika vyombo vya habari, ripoti hiyo imeeleza kuwa ilichokusanya kutoka kwa watu waliohojiwa wanahabari hawataki kubishana na serikali na kuitwa mara kwa mara katika Idara ya Habari MAELEZO kutokana na kuandika habari zinazoikera serikali.

Kuongezeka vitisho kwa vyombo vya habari kunavikwaza

kufanya uchunguzi na kuibua masuala nyeti na ripoti hiyo imeongeza kuwa, hali hii inakwamisha kuwepo na mawazo mbadala kupitia vyombo vya habari.

Wakati vitisho vinaelekezwa kwa vyombo muhimu vya habari, vyombo vingine vinavyochukuliwa na wenye mamlaka kuwa ni vya kimkakati vinapewa uhuru zaidi kuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii.

Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti vinavyotumiwa dhidi ya magazeti hayo na wenye mamlaka wanawaambia watu wanaokerwa navyo waende mahakamani lakini vyombo vingine hufungiwa vinapoandika habari zisizowapendeza wenye mamlaka.

Wahariri ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania waliohudhuria mkutano mkuu wa jukwaa hilo uliofanyika Desemba 9, 2019 Jijini Dar es Salaam.

Hofu, vitisho vyaua uandishi wa uchunguziInatoka Ukurasa wa 3

Page 5: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kwa kuwa vyombo vya habari huru na imara ni muhimu kwa kukuza demokrasi na mafanikio ya taifa, ni vyema

vitendo vya ukiukaji wa uhuru wa habari vikaepukwa na kuzuiwa kabisa.

Ripoti ya uchunguzi wa kuongezeka vitisho na kuingiliwa kwa uhuru wa uhariri iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) hivi karibuni imewataka watu, makundi, taasisi na waliohusika katika vitendo vya ukiukaji dhidi ya uhuru wa habari kuacha mara moja ili kudumisha amani, utulivu kati ya vyombo vya habari na serikali.

Imesisitizwa katika ripoti hiyo kwamba kuendelea kudorora uhusiano wa kikazi kati ya serikali na vyombo vya habari, vyombo ambavyo kwa kawaida vinategemewa kuwa wabia katika kuhamasisha maendeleo, sio jambo zuri.

Kwa wadau wa habari ripoti hiyo imewataka kubaini na kurekebisha makosa na udhaifu wao na kwa maofisa wa serikali na vyombo vya dola, waweke kando maslahi yao ya kisiasa, wazingatia taaluma zao na wazingatie jinsi ya kufanya kazi na vyombo vya habari bila kuwa na migogoro.

Mapendekezo ya ripoti hiyo ni pamoja na kuwa na taratibu itakayohakikisha kuendelea mazungumzo na kuboresha

ushirikiano kwa kuzingatia ajenda sawa, tunu za kitaifa na kuheshimu majukumu na malengo kinyume na hali ya sasa.

Mapendekezo mengine ni kama ifuatavyo: • Kuhimizwa kujisimamia vyombo

vya habari • Kuhimizwa weledi – hii itasaidia

kuzuia wanahabari kutokiuka maadili

• Kuelewa sheria na kanuni ambazo tafsiri yake na utumiaji wake unasababisha migongano.

• Kuhimiza marekebisho ya sheria na kanuni zinazoweza kutumiwa vibaya.

• Kushirikiana na kuzungumza na wadau muhimu kwa lengo la kuwa na msimamo wa pamoja katika masuala nyeti.

• Majukwaa ya kitaifa kufanya majadiliano na kuonyesha namna ya kuendelea yanapendekezwa.

Mapendekezo hayo yanatokana na maoni ya waliohojiwa wakati wa uchunguzi wa ripoti hiyo. Mawazo yaliyotolewa katika ripoti hiyo ni kama ifuatavyo:-

Wanahabari lazima wafanye: -• Wafanye kazi kwa weledi,

waandike habari zenye maudhui bora kuweza kukuza imani ya umma na kuungwa mkono kwa kukuza usambazaji na kupata

5

Habari

Toleo la 149, Januari, 2020

Ukiukaji wa uhuru wa habari lazima uzuiwe

Endelea Ukurasa wa 6

Page 6: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga (wa pili kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo MCT, Jukwaa la Wahariri (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) walitoa kauli ya pamoja kupinga utaratibu unaoshika kasi wa kukamata hovyo waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile,wa tatu ni Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa na kulia ni Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo.

matangazo. Kupata imani ya wananchi siyo tu kutafanya vyombo vya habari kuwa imara, bali pia kutawazuia maofisa wa serikali na watu wengine wenye mamlaka kufanya ukiukaji dhidi ya vyombo vya habari na kuingilia uhuru wa uhariri.

• Wasome sana kuelewa sheria zote, kanuni, sera, mikataba na makubaliano yahusuyo vyombo vya habari – hii itasaidia kuzuia wenye mamlaka kuchukua hatua dhidi yao na wajisimamie kuzuia hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

• Wafanyekazi pamoja kutetea wanahabari wanaokabiliwa na hatua za kisheria- kesi dhidi ya chombo cha habari ama mwanahabari za mtandaoni ichukuliwe kama kesi dhidi ya tasnia. Na hata ushindi uchukuliwe kama hivyo.

• Wanahabari wanapo kabiliwa na tatizo la kisheria, wachambue kesi husika na wajidhirishe kuwa suala hilo linahusiana na kazi zao kitaaluma na kuona kama mwanahabari katika kesi husika amekosea ama la kabla ya kutoa taarifa za kulaani. Hii itafanya serikali kutambua kama maofisa wao wamekosea .

• Kuwa na mkakati jinsi ya kushirikisha mashirika ya nje. Badala ya mashirika hayo kuunga mkono vyombo vya habari kwa kulaumu serikali kwa kutoa taarifa, viwasiliane na wanahabari wa Tanzania kuchunguza na kupata ushahidi kamili kuhusu suala linalolalamikiwa. Pia yanaweza kusaidia kuboresha uwezo wa wanahabari na kuondoa tabia zisizo za kitaaluma.

• Kuwaelimisha viongozi wa serikali jinsi ya kufanyakazi na vyombo vya habari na namna gani wanaweza kutumia sheria na kanuni zinazohusu vyombo vya habari bila kusababisha migogoro.

• Kufanyakazi pamoja kama timu, kushirikisha wadau wengine na kuanzisha mazungumzo na vyombo vya kisheria na serikali katika ngazi tofauti na kuwa na msimamo wa pamoja jinsi ya kufanya kazi pamoja.

Kuwa na majukwaa yakitaifa kujadili hali iliyopo na jinsi ya kusonga mbele.

• Kuhamasisha marekebisho ya sheria ama na kanuni hasa vifungu vinavyoweza kutumiwa vibaya.

• Kuweka kando manufaa ya kisiasa na kuzingatia taratibu za

taaluma zao. • Kujifunza jinsi ya kuwa wabunifu

na kuwa na mifumo mbalimbali ya biashara kuweza kuwa endelevu na kuwa huru. Itasaidia kukabiliana na shinikizo kutoka kwa watangazaji na wafadhili.

Kwa maofisa wa serikali na , vyombo vya kisheria lazima waf anye yafuatayo;-• Waweke kando maslahi yao ya

kisiasa na kufanyakazi kuzingatia taaluma.

• Wajifunze jinsi ya kushughulikia vyombo vya habari na kutekeleza sheria bila kusababisha migongano.

• Kusoma kwa upana na kuelewa sheria zote, kanuni, sera, mikataba na makubaliano kuhusu vyombo vya habari.

• Kupitia mashauri dhidi ya wanahabari na kuchukua hatua kwa maofisa waliokosea

• Kushirikiana na wanahabari na wadau kwa lengo la kuwa na mijadala kwa masuala yenye mgogoro.

• Kuanzisha mapitio ya sheria na kanuni, hasa vifungu vinavyobana na kandamizi.

• Kuhakikisha kutenganisha kwa madaraka miongoni mwa mihimili mitatu. Mihimili yote ifanye kazi kwa uhuru bila kuingiliwa kwa aina yoyote.

Ukiukaji wa uhuru wa habari lazima uzuiweInatoka Ukurasa wa 5

Page 7: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Tangu atoweke mwandishi wa habari za uchunguzi Azory Gwanda zaidi ya miaka mwili iliyopita sasa, usemi wa watu

wasiojulikana umezoeleka katika jamii na vyombo vya habari.

Gwanda, mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, alionekana mara ya mwisho akiwa na watu wasiojulikana Novemba 21, 2017 na hajaonekana tena.

Kufuatia matukio zaidi ya waandishi kutekwa na watu wasiojulikana ambao wakati mwingine huwa ni polisi waliovaa kiraia, Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilianzisha uchunguzi kujua chanzo cha suala hilo ambalo limeibua hofu na kuvifanya vyombo vya habari kuwa “mbwa waangalizi” wasio na meno.

Licha ya Gwanda ambaye mahali alipo hapajulikani hadi sasa, Julai mwaka jana watu wasiojulikana ambao baadaye walitambulika kuwa ni polisi wanaovalia kiraia walimchukua kibabe mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kutoka nyumbani kwake kwa namna iliyowatia hofu majirani zake waliolazimika kufuatilia

kujua hatma ya jirani yao. Baada ya awali kukataa kuwa wamemkamata Kabendera, Polisi walikiri baadaye kuwa wanamshikilia. Kabendera alifunguliwa mashtaka ya uhalifu wa uchumi yanayomtesa rumande hadi sasa bila kuwa na uwezekano wa kupata dhamana.

Mei 28, 2018 mwandishi mwingine alitekwa na Polisi mkoani Kigoma na watu wasiojulikana. Awali alikuwa ameitwa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel aliyemwambia mwandishi huyo kuwa alikuwa ameshinda zawadi na kumtaka aende kuichukua. Alipofika mahala alipotakiwa kwenda kuichukua zawadi yake aliwakuta watu wawili walimpakia kwenye gari.

Alikutwa ametupwa Jijini Dar es Salaam mwezi mmoja badaye. Bila shaka kutokana na yaliyomkuta mwandishi huyo hakuwa tayari kueleza yaliyomsibu.

Licha utekaji na vitisho vingine kama vile unyanyasaji, kupigwa, kukamatwa bila kosa wanahabari pia wanabambikiwa kesi , wanapewa maonyo makali na watendaji wakubwa wa serikali na vyombo vya habari navyo kupewa barua hali inayowafanya

mameneja wa vyombo vya habari, wahariri na wamiliki kuogopa na kujidhibiti wenyewe katika habari zao na kuchapisha habari za kusifu tu wenye mamlaka.

Kauli ya Rais John Magufuli Machi, 2017 akionya vyombo vya habari : “Angalieni. Kama mnafikiri mko huru, haumko kiasi hicho”, ni kauli inayotisha vyombo vya habari ambayo haijawahi kutolewa na mkuu wa nchi.

Ni msimamo wa bahati mbaya na mabadiliko kabisa kwa mtu ambaye wakati wa kampeni za kuwania urais aliahidi kusaidia vyombo vya habari kwa kutambua mchango wao muhimu kwa jamii.

Vyombo vya habari vya mitandaoni navyo havijasalimika kwa kuwa vinapata mashambulizi kadhaa ya kimtamdao na kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi katika kipindi cha mwezi mmoja tu wa Septemba 2019, Jamii Forum walibaini mashambulizi 14,474 wakati Oktoba 31, 2019 yalifanyika majaribio ya mashambulizi ya kimtandao zaidi ya 2,400.

Sheria za habari na kanuni zinawezesha ukiukwaji wa uhuru wa habari kama uchunguzi ulivyobaini ambapo baadhi ya watu waliohojiwa walieleza kuwa vitisho, mashambulizi, kufuatilia habari za vyombo, uchukuaji wa zana za kazi, kukamatwa bila makosa, kushitakiwa, tuhuma za kubuniwa na kuvipachika majina vyombo vya habari kuwa wasaliti na vibaraka na kuingilia maudhui ya habari ni mambo yanayopewa nguvu na sheria zilizopitishwa karibuni na hali mbaya sasa ya kisiasa.

Hadidu rejea za uchunguzi huo ambao umetolewa mtandaoni ni pamoja na kuwahoji wahariri wa vyombo vikuu vya habari, vyombo vya mtandaoni na vinginevyo ili kufahamu kiasi cha vitisho na uingiliaji katika uhuru wa uhariri; kuwahoji wadau wengine wa habari kubaini aina ya kiwango cha vitisho; kubaini kama kitisho chochote na uingiliaji umeripotiwa polisi na mamlaka zingine husika; kubaini pia kwa kiasi gani vitisho na uingiliaji umeathiri uhuru wa uhariri na kwa upande wa biashara katika tasnia ya habari.

Matokeo muhimu ya uchunguzi huo ni kama ifuatavyo:-

• Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kuwa vyombo vya habari Tanzania vinakabiliwa na aina mbalimbali ya ukiukwaji katika utendaji wake wa kazi ikiwemo vitisho na kuingiliwa katika uhariri.

• Kuna mambo mengi yanayopelekea hali ya sasa ya hofu nchini Tanzania, na baadhi ya mambo hayo yanatokana na sheria zisizo rafiki na utawala wa kisiasa wa sasa, ambapo zingine zinatokana na

7

Habari

Toleo la 149, Januari, 2020

…Kufuatilia watu wasiojulikana

Mwandishi wa habari za uchunguzi Azory Gwanda ambaye ametoweka tangu Novemba 21, 2017

Mwandishi Erick Kabendera anayekabiliwa na mashataka ya utakasishaji fedha

Endelea Ukurasa wa 9

Page 8: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Utaratibu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

16

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

• Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

• Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

• Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

BARAZA LA HABARI TANZANIA

Page 9: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

9

Toleo la 149, Januari, 2020

Habari

Na Mwandishi wa Barazani

Wakati matukio ukiukaji ya uhuru wa habari yanaripotiwa kuongezeka, jambo la

kushangaza ni kwamba hayaripotiwi kwa mamlaka husika.

Kwanini inakuwa hivyo. Uchunguzi uliofanywa kuhusu kuongezeka kwa vitisho na kuingiliwa kwa uhuru wa uhariri na

ripoti yake kutolewa na Baraza la Habari Tanzan ia (MCT) imebainisha sababu mbalimbali zinazowafanya waathirika kuamua kukaa kimya.

Kukosa imani na vyombo vya dola ni moja ya sababu kubwa ya ukimya wa waathirika hao.

Pia imeelezwa kuwa baadhi ya maofisa wa polisi wanatuhumiwa kwa ukiukwaji, hivyo kuathiri kushughulikiwa kwa matukio ya ukikwaji. Suala lingine kama

vyombo vinavyosimamia sheria vya dola vikisuasua katika kushughulikia matukio yaliyofanyika mchana kweupe, watawezaje kushughulikia masuala yanayofanyika kwa kificho.

Suala la Azory Gwanda, mwandishi wa habari za uchunguzi wa gazeti la Mwananchi limetolewa mfano kwamba sasa ni zaidi ya miaka miwili imepita tangu alipotoweka akiwa na watu wasiojulikana ambapo hakuna uchunguzi unaoeleweka ama taarifa za kuaminika zilizotolewa na wenye mamlaka.

Kuchelewa kufanywa uchunguzi na ukamilishaji wa kesi pamoja na kutolewa kauli tata kunasababisha waathirika wa ukiukwaji wa uhuru wa habari kukosa imani na wenye mamlaka.

Shaka kuhusu uhuru wa vyombo vya dola na uwezo wao wa kuchelewesha matukio kama hayo pia kunafanya waathirika kutoripoti, ripoti hiyo imeeleza ikitoa mfano wa mwanahabari mmoja alieleza jinsi alivyoacha kufuatilia maendeleo ya malalamiko yake aliyowasilisha polisi. Anasema alikatishwa tamaa kuendelea kufuatilia shauri lake kwa mbinu za kuchelewesha za polisi.

Pia kuna wasiwasi wa kuwepo ajenda iliyofichika dhidi ya baadhi ya wanahabari na vyombo vya habari zinazowalazimisha kutowasilisha malalamiko ya ukiukwaji. Kwa mujibu wa waliohojiwa, baadhi ya vyombo vya habari vinaitwa mbele ya Idara ya Habari hata pale ambayo habari zao hazina makosa ya kitaaluma.

Wasiwasi kwamba mambo yatawageuka yanafanya baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari kutoripoti matukio ya ukiukwaji wa uhuru wa habari.

Kwanini waathirika hukaaa kimya?

Mwandishi wa Wapo Radio, Silas Mbise akipigwa na Polisi.

udhaifu wa wanahabari wenyewe.• Aina za ukiukwaji kwa wanahabari

na vyombo ni tofauti na ambao hufanywa na watu tofauti wakiwemo maofisa wa serikali , wanasiasa na vyombo vya dola.

• Ukiukwaji mwingi hauripotiwi kwa sababu ya watu wanaoathirika kukosa imani na vyombo vya sheria vya dola. Pia matukio machache yaliyoripotiwa hayashughulikiwi;

• Baadhi ya ukiukwaji na vitisho vimerekodiwa na kuthibitishwa . Matukio ya ukiukwaji yaliyorekodiwa yamejadiliwa kwa kina katika ripoti;

• Hali hii imeathiri vyombo vya habari kwa njia mbalimbali ikiwemo kujidhibiti kwa kupitiliza, kukosekana uandishi wa habari za uchunguzi na vikwazo vya kupata habari .

Baraza la Habari limefanya uchunguzi huu kutokana na matakwa ya katiba yake kifungu 3(a) na 3(e)

ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:Kifungu cha 3 (a) “Kukuza, kusaidia,

kutetea na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na aina nyingine za mawasiliano ya umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” kifungu 3(e) “ Kuweka rejista ya matukio yanayoweza kukwaza upatikanaji wa habari za manufaa kwa umma,kufuatilia na kuchunguza mwenendo na tabia za watu, mashirika na vyombo vya serikali na kupanga matokeo yake”.

…Kufuatilia watu wasiojulikana Inatoka Ukurasa wa 7

Page 10: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Mfanyakazi wa Baraza la Habari Tanzania, Bi. Shifaa Said Hassan ameteuliwa kuwa

Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar.

Uteuzi wa Bi. Shifaa ambaye ni Ofisa Programmu Mwandamizi wa Baraza katika ofisi ya Zanzibar, ulitangazwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Bw. Mahmoud Thabit Kombo mwezi Desemba, 2019.

Akiwafahamisha wafanyakazi wengine wa Baraza kuhusu uteuzi huo, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema:” Ninayo furaha kukujulisheni kuwa mnamo Desemba 2019 Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Bw. Mahmoud Thabit Kombo alimteua mwenzetu Bi. Shifaa Said Hassan kuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar.Uteuzi huo ulianza tarehe 20 Desemba 2019.”

“Nachukua nafasi hii kumpongeza Bi. Shifaa

na kumwomba Mwenyezi Mungu amjalie uwezo na busara za kutimiza majukumu hayo kwa ufanisi”, amesema Mukajanga katika taarifa yake.

Wafanyakazi wa Baraza kwa ujumla wao wamempongeza na kumtakia kheri Bi. Shifaa katika utekelezaji wa majukumu yake kufuatia uteuzi huo.

Akizungumzia uteuzi wake,Bi. Shifaa alisema amefurahi hasa kwa vile aliwahi kufanyakazi katika gazeti la Serikali la Zanzibar Leo.

Alisema alijiunga na Baraza la Habari akitokea Zanzibar Leo mwaka 2003.

Alisema anauchukulia uteuzi huo kama fursa muhimu na chachu ya kuhamasisha maboresho ya utendaji katika magazeti na pia kutekeleza majukumu na malengo ya Baraza .

Shirika la Magazeti ya Serikali linachapisha magazeti manne

likiwemo Zanzibar Leo. Mengine ni Zanzibar Mail, Zanzibar Leo Jumapili na Zaspoti.

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri ni Salim Said Salim, Dk. Juma Mohamed Salum,, Khalfan Sheikh Saleh na Said Hassan Said.

Pamoja na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Serikali,

Waziri pia aliteua wajumbe wa Chuo

cha Uandishi wa Habari na

Shirika la Utangazaji.

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Mfanyakazi MCT ateuliwa Mjumbe Bodi ya Magazeti ya Serikali Z’bar

Ofisa Programu Mwandamizi wa Baraza la Habari Tanzania, Shifaa Hassan.

Page 11: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

11

Kitabu

Toleo la 149, Januari, 2020

Kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa waandishi wa habari na wahariri kukisoma ili kuelewa takwimu na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi katika habari

Page 12: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Fursa

Mfanyabiashara maarufu , Ali Mufuruki aliyefariki akipata matibabu Afrika Kusini.

ISO-D-PROD-03-03 Award Criteria Sheet Humanity v2 1/5

WORLD TV AWARDS 2020 CATEGORY HUMANITY

The Best TV Documentary on Youth – Charting the Future

CRITERIA AND REGULATION Genre: Documentary Length: Maximum of 60 minutes

All the entries will be judged according to the following criteria: 1. The programme must focus on creating deeper awareness among the audience on

the theme of youth as ‘critical agents of change’ by highlighting the role of youth in shaping the world as a stakeholder at all levels.

2. The programme must focus on the importance of having youth oriented viewpoints and youth themselves, who are changing the world by their experience, innovation and expertise. It also must highlight issues faced by the youth and show effective solutions to over-coming these challenges, while highlighting the opportunities present as well.

3. The programme could either focus on a local, regional or on global point of view.

4. The programme should be creative and innovative with the ability to capture audience attention, and offer excellent production values.

5. The programme must have been aired or must be scheduled for broadcasting in its originating country on national and/or any private TV network (broadcasting sheet to be provided).

6. The programme must have been produced within the last 12 months before the date of submission.

7. The programme must be either in English or if in any other language with English subtitles. It can also be a non-narrative piece.

8. The programme must be the original work of the entrants. Entrants must be able to demonstrate that they have full copyright clearance on all music, image, artwork and other audio-visual elements used in the programme.

Page 13: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

13

Toleo la 149, Januari, 2020

Fursa

Endelea Ukurasa wa 13

ISO-D-PROD-03-03 Award Criteria Sheet Humanity v2 2/5

Who can submit an entry? Television producers from public service broadcasting organisations, private networks, freelancers etc. are invited to participate in this competition. How many entries can be submitted? Each producer/organisation can submit up to 2 entries. Format requested: Programmes can be submitted DVD format or as softcopy*

3 DVDs are requested for each programme submitted.

* All softcopy entries must be of high quality without any playback issues. Successful submissions will receive an email to this effect.

Shipping information: The DVDs and the submission forms should be sent to Ms. Fathimath Leeza at the following address: Asia–Pacific Institute for Broadcasting Development (AIBD)

2nd Floor, Bangunan Teknologi (IPPTAR Lama) Kompleks Angkasapuri, 50614 Kuala Lumpur, Malaysia

Deadline: The entry forms and the DVDs should reach AIBD no later than: Friday, 17th April 2020 Jury: Jury members are senior media professionals from various countries and regions. Winner Prize: US$5,000.00 cash in favor of the producer and/or broadcasting organisation A trophy and a certificate presented by the Asia-Pacific Institute for Broadcasting Development (AIBD) A trip to Attend Asia Media Summit 2020 to receive the trophy and the certificate on 4 June 2020, a global media gathering. Note: The names of the winner and runner-up will be announced at the AMS 2020. The AIBD Director and representatives of the sponsors will hand over the prize to the winner during the AMS. A video clip of the winner’s programme will be screened during the AMS as well as during the AIBD General Conference in Laos in 2020. Information: More information on World TV Awards is available at: www.aibd.org.my/worldtv

Page 14: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Mwandishi aliyekuwa "moto” kushikiliwaNa Mwandishi wa Barazani

Mwandishi wa habari , Jessy Mikofu , wa Mwanza aliachiwa na polisi Januari 15, mwaka

huu saa chacahe baada kukamatwa kufuatia shinikizo kutoka kwa vyombo mbalimbali vya habari.

Mikofu anayeandikia gazeti la Mwananchi alikamatwa mchana kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi .

Aliachiwa bila masharti jioni siku hiyo kutoka kituo cha Polisi cha Igogo ambako alikuwa akishikiliwa pamoja na watu wengine watatu.

Mikofu alikamatwa wakati akipiga picha za vurugu zilizotokea wakati watu wakiwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa mjini humo walipolalamikia kuhusu zoezi hilo kufanyika kwa taratibu.

Kulingana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi ya Mwanza, Edwin Soko, mwandishi huyo alikuwa ametumwa kuandika habari kuhusu zoezi hilo na siku hiyo kwa bahati mbaya umeme ulikuwa umekatika jambo lililozua malalamiko kutoka

watu waliokuwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata vyeti vyao vya uraia.

Baada ya kukamtwa kwa Mikofu ambaye ni mwanachama wa klabu ya waandishi ya Mwanza, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Soko ,

aliwasiliana na Mkuu wa Wilaya akitaka mwandishi huyo aachiwe lakini jitihada zake ziligonga mwamba baada ya Mkuu wa wilaya kusema aache utaratibu uendelee.

Mkuu huyo wa wilaya alishikilia msimamo huo na hivyo Mikofu alipelekwa na watuhumiwa wengine katika kituo cha polisi cha Igogo.

Picha ambazo Mikofu alizipiga kwa kutumia simu

yake zilifutwa na Polisi. Baada ya vituo

mbalimbali vya habari kuanza kuatangaza kukamatwa kwa mwandishi huyo, Mkuu wa Wilaya aliwasiliana na Soko na Mikofu aliachiwa bila masharti.

Watu wengine waliokuwa

wameshikiliwa nao waliachiwa.

Mwanishi Jessy Mikofu

Page 15: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Vienna,

Serikali ya Tanzania imetakiwa kumpa dhamana kwa ajili ya matibabu , mwandishi aliye rumande

Erick Kabendera.Mwito huo umetolewa na taasisi

ya kimataifa ya habari –IPI. “Tunaitaka serikali ya Tanzania

kuruhusu mara moja Erick Kabendera kuachiwa kwa dhamana ili aweze kupata msaada wa matibabu,” amesema Mkurugenzi wa Uragbishi wa IPI Ravi R. Prasad katika taarifa iliyotolewa Vienna, Austria.

Kabendera, mwandishi wa kujitegemea aliyekuwa anaandikia magazeti mbalimbali duniani, alikamatwa Dar es Salaam Julai 2019 na amekuwa rumande kwa miezi sita akikabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha na uhalifu wa kiuchumi, ambayo hayana dhamana nchini Tanzania.

Kwa muda wote huo kesi yake imekuwa ikiahirishwa na mahakama kwa mara 13 ambapo wakili wa Kabendera ameripoti kuwa afya ya mteja wake ilikuwa mbaya na kusisitiza apatiwe matibabu.

Licha ya ushahidi wa kudhoofika kwa afya ya Kabendera kiasi kwamba hawezi kutembea vizuri, mahakama imemkatalia kumpa ruhusa kupata matibabu.

Majaribio zaidi ya kutumia utaratibu wa kukiri ili asamehewe ambao ungemwezesha kupata matibabu pia umekataliwa.

“Hali hiyo mbaya isiyo ya kibinadamu imechukua muda mrefu sana”, amesema Prasad.

IPI imeeleza katika taarifa yake kuwa kesi hiyo iliahirishwa hivi karibuni Januari 27 ambapo waendesha mashtaka wa serikali wamesema uchunguzi haujakamilika. Kesi hiyo imepangiwa tena Februari 10, 2020.

Shirika hilo huko nyuma

limefikisha suala la Kabendera katika Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika (ACHPR).

Miongoni mwa magazeti ya nje ambayo Kabendera amekuwa akiyaandikia ni pamoja na The Guardian na The Times ya

Uingereza. Inadaiwa kuwa tuhuma anazokabiliwa nazo zinalenga kumnyamazisha.

Uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania umedorora chini ya serikali ya sasa ya Rais John Magufuli.

15

Habari

Toleo la 149, Januari, 2020

Mwandishi Erick Kabendera akiwa mahakamani

IPI yaomba Kabendera apewe dhamana atibiwe

Page 16: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Fursa

Page 17: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

17

Habari

Toleo la 149, Januari, 2020

MALIPO KWA KUPIGWA PICHA BILA RIDHAA

Maria Agostino Eliasi, Mkazi wa Magomeni Kagera akipokea sh. 50,000 kutoka kwa Meneja wa Fedha wa Baraza la Habari, Mustapha Tarimo. Bi Maria ambaye shughuli zake ni mama lishe, alipewa fedha hizo baada kushinda katika malamiko aliyowasilisha dhdi ya gazeti la Mtanzania katika Kamati ya Maadili ya MCT baada ya gazeti hilo kumpiga picha na kuichapisha bila ridhaa yake. Alipigwa picha akiwa amebeba watoto wake wawili na maelezo yakiwa “Kulea ni kazi”.Aliiambia kamati hiyo kuwa baada ya kutoka tu picha ile, alipata usumbufu mkubwa na kudhalilika.Shauri lake liliamuliwa Oktoba mwaka jana. Alipata fedha hiyo mapema Januari, 2020. Fedha hizo zimetolewa na gazeti la Mtanzania ambalo liliamriwa pia kumuomba radhi mama huyo.Fedha hizo ni kumlipa kwa ajili ya kushughulikia malalamiko hayo.

vikubwa vya habari na redio za jamii.

Florence Majani wa gazeti la Mwananchi alikuwa mwanamke wa kwanza kuvunja rekodi ya washindi wa jumla wanaume kwa kushinda mwaka 2016, akifuatiwa na Vivian Pyuza wa CG FM Tabora mwaka 2017 na 2018 ilikuwa zamu ya Salome Kitomari.

Mashindano ya mwaka huu ni ya 11 ambapo washirika wanayoyasimamia ni Baraza la Habari Tanzania, Wakfu wa

Habari (TMF) Taasisi ya habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISATan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), HakiElimu, AMREF, SIKIKA, Agricultural Non-State Actors Forum (ANSAF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mukajanga alisema pia katika uzinduzi wa EJAT kuwa mwaka huu Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Uandishi wa Habari (LAJA)

itatolewa. Wanaowania Tuzo hii ni wenye rekodi ya umahiri wa uandishi wa habari na kuunga mkono taaluma na kuwa na ari na dhamira ya kutetea uhuru wa habari.

Hakuna kazi inayotumwa kuwania Tuzo hiyo ambayo inaweza kutolewa kwa mtu aliye hai ama aliyefariki ama mstaafu. Waliotunikiwa Tuzo hiyo huko nyuma ni Fili Karashani (2011), Hamza Kasongo (2012), Mariam Mohamed Hamdan (2013), Jenerali Ulimwengu (2014) na Rose Haji Mwalimu (2015).

Kazi zaidi za kuwania EJAT zawasilishwaInatoka Ukurasa wa 20

Page 18: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Fursa

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18ISO-D-PROD-03-03 Award Criteria Sheet v1 1/5

WORLD TV AWARDS 2020 CATEGORY SCIENCE/ENVIRONMENT

The Best TV Programme on Climate Action – Zooming in on Forests

CRITERIA AND REGULATION

Genre: TV Documentary, Short documentary/TV report, Docu drama, Edutainment/Infotainment TV programme, Public Service Announcement/TV Spot Length: A maximum of 60 minutes

All the entries will be judged according to the following criteria: 1. Large swathes of forests are lost every day due to direct and indirect human

actions. Managing forests landscapes or halting the loss or degradation of forests and restoring them can help climate change mitigation. The programme must focus on the importance of forests and look into ways that can restore, maintain and create these life-sustaining natural resources.

2. The programme should describe concrete actions and/or practices which create awareness on the harm deforestation and what can be done to mitigate the problem.

3. The programme could either focus on a local, regional, sectoral or on global point

of view.

4. The programme should be creative and innovative with the ability to capture audience attention, and offer excellent production values.

5. The programme must have been aired or must be scheduled for broadcasting in its originating country on national and/or any private TV network (broadcasting sheet to be provided).

6. The programme must have been produced within the last 12 months before the date of submission.

7. The programme should use an engaging and easily understandable style. Information presented in the video must be factually accurate.

8. The programme must be either in English or in any other language with English subtitles. It can also be without words.

9. The programme must be the original work of the entrants. Entrants must be able to demonstrate that they have full copyright clearance on all music, image, artwork and other audio-visual elements used in the programme.

Page 19: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Fursa

Toleo la 149, Januari, 2020

19ISO-D-PROD-03-03 Award Criteria Sheet Humanity v2 2/5

Who can submit an entry? Television producers from public service broadcasting organisations, private networks, freelancers etc. are invited to participate in this competition. How many entries can be submitted? Each producer/organisation can submit up to 2 entries. Format requested: Programmes can be submitted DVD format or as softcopy*

3 DVDs are requested for each programme submitted.

* All softcopy entries must be of high quality without any playback issues. Successful submissions will receive an email to this effect.

Shipping information: The DVDs and the submission forms should be sent to Ms. Fathimath Leeza at the following address: Asia–Pacific Institute for Broadcasting Development (AIBD)

2nd Floor, Bangunan Teknologi (IPPTAR Lama) Kompleks Angkasapuri, 50614 Kuala Lumpur, Malaysia

Deadline: The entry forms and the DVDs should reach AIBD no later than: Friday, 17th April 2020 Jury: Jury members are senior media professionals from various countries and regions. Winner Prize: US$5,000.00 cash in favor of the producer and/or broadcasting organisation A trophy and a certificate presented by the Asia-Pacific Institute for Broadcasting Development (AIBD) A trip to Attend Asia Media Summit 2020 to receive the trophy and the certificate on 4 June 2020, a global media gathering. Note: The names of the winner and runner-up will be announced at the AMS 2020. The AIBD Director and representatives of the sponsors will hand over the prize to the winner during the AMS. A video clip of the winner’s programme will be screened during the AMS as well as during the AIBD General Conference in Laos in 2020. Information: More information on World TV Awards is available at: www.aibd.org.my/worldtv

Page 20: Hofu yaua habari za uchunguzikuwa na uandishi wa ajabu kwa kuchapisha uongo, kutunga habari na kutukana watu mashuhuri katika jamii. Kwa mshangao wa wana habari, kuna viwango tofauti

Na Mwandishi wa Barazani

Kasi ya kuwasilisha kazi za kuwania Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)

2019 inaongezeka wakati siku ya mwisho ya kuziwasilisha Januari 31, 2020 inapokaribia.

Ofisa Programu wa Baraza la Habari ambalo ni mshirika kiongozi wa EJAT, Paul Mallimbo amesema ni kawaida kuwa kazi nyingi huwasilishwa tarehe ya mwisho inapokaribia na kwamba nyingi zaidi zitawasilihswa katika wiki ya mwisho.

Hata hivyo hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya kazi ziliziopokelewa kwa kuwa zingine zinawasilishwa kwa njia ya posta na nyingine zinafikishwa kwa mkono katika ofisi za Baraza.

Mwaka huu EJAT ina makundi 20, ambapo matatu ni mapya. Ilizinduliwa Oktoba 21, 2019.

Makundi mapya ni Ubunifu Maendelo ya Binadamu ambapo Hedhi Salama na Afya ya Uzazi.

Makundi mengine ni Biashara na Fedha, Utamaduni na Michezo, Kilimo na Biashara ya Kilimo, Utalii na Uhifadhi, Elimu, Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Uandishi wa Habari za Data, Utawala Bora, Mpiga Picha Bora , Mpiga Video Bora, Mchora Vibonzo Bora, Uandishi wa Jinsia, Mafuta, Gesi na Usimamizi wa Madini, Usalama wa Barabara na Kundi la Wazi.

Tuzo hizo zimeibua na kukuza wanahabari wengi kutoka vyombo vikuu vya habari na hata redio za jamii amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga wakati wa uzinduzi.

Alisema kuwa Tuzo hizo zimekuza waandishi wa habari wanawake ambapo katika miaka mitatu mfululizo washindi wa jumla walikuwa wanawake waliotoka katika vyombo

Ofisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania, Paul Mallimbo akipitia kazi zilizowasilishwa kuwania Tuzo za Umahiri wa Uandishi Habari Tanzania (EJAT) 2019.

20

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Kazi zaidi za kuwania EJAT zawasilishwa

Endelea Ukurasa wa 17