9
DHIMA YA MENEJIMENTI KABLA NA BAADA YA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA Eng.Gilay Charles Kilayi Shamika ‘Ilituendelee tunahitaji taasisi imara na endelevu zenye Wataalamu wanao jiamini na wenye weledi usio na shaka pamoja na Vyama vya siasa sikivu kwa taasisi na Wataalamu husika na si kinyume chake.’ Hivi ndivyo walioendelea walifanya na wanaendelea kufanya.

Dhima Ya Menejimenti Kabla Na Baada Ya Karne Ya Ishirini Na Moja by Gilay Shamika

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Taasisi Imara ni zao la Menejimenti Imara.Hatuna budi kuwa na menejimenti imara kwaajili ya kupata Taasisi Imara na hivyo kurahisisha maendeleo ya nchi.Ulegevu wa kitaasisi ni chanzo pia cha ulegevu wa maendeleo ya nchi.

Citation preview

DHIMA YA MENEJIMENTI KABLA NA BAADA YA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA

Eng.Gilay Charles Kilayi Shamika

Ilituendelee tunahitaji taasisi imara na endelevu zenye Wataalamu wanao jiamini na wenye weledi usio na shaka pamoja na Vyama vya siasa sikivu kwa taasisi na Wataalamu husika na si kinyume chake. Hivi ndivyo walioendelea walifanya na wanaendelea kufanya. Eng.Gilay Charles Kilayi Shamika

1.0 UTANGULIZI

Uimara wa kampuni au taasisi kwa kiasi kikubwa unategemea uimara wa Menejimenti husika katika kuwashirikisha wafanyakazi wao kufanya maamuzi.Ukaribu wa menejimenti na wafanyakazi hufanya wafanyakazi kufanya kazi kwa uhuru,kutoa maoni na ubunifu ili kuongeza ufanisi zaidi.Kuwa mbali na wafanyakazi hakuongezi heshima yako kuwa sababu wewe ni mkuu, huhitaji kuwa karibu na wafanyakazi wa chini na huoni nini watachangia kimawazo.Kwakufanya hivyo unajishushia heshima zaidi na ufanisi wa kazi.

Ufanisi kazini ni majumuisho ya kazi zote za kila mfanyakazi.Hivyo tuzingatie teamwork na kuisaidia wafanyakazi katika mambo yote kazini na yale ya kibinafsi kadri mfanyakazi atakavyohitaji msaada wa kimenejimenti.

2.0 MWELEKEO WA DHIMA YA MENEJIMENTI KABLA NA BAADA YA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA Dola ya Uingereza mpaka sasa ndiyo inayoaminika kwa kuwa nguli/weledi wa mambo ya menejimenti.Mabadiliko yoyote yale yanayoendana na nyaja hii huasisiwa katika dola hiyo.Warumi ndiyo waasisi wa masuala ya falsafa katika nyaja zote ila dola ya Uingereza ikaenda mbali zaidi katika kutafsiri falsafa za kimenejimenti. Itakumbukwa pia hata masuala ya ubinafsishwaji wa mashirika na taasisi za umma ya lianza kwa kuasisiwa na malkia wa uingereza na kupewa jina la Iron Lady baada ya kuonesha msimamo wa kile ambacho kwa Waingereza wengi hawakutarajia kinge asisiwa na familia ya kifalme ambayo ndiyo hufaidika zaidi na mali za serikali ya uingereza.Aidha taasisi za elimu za Uingereza ndiyo zipo daraja la juu kwa kutoa elimu bora ya masuala ya menejimenti.

2.1 MWELEKEO WA DHIMA YA MENEJIMENTI KABLA YA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA Kabla ya karne ya ishirini na moja, menejimenti katika maeneo ya kazi,dhumuni lake kubwa ilikua ni kuandaa kanuni na taratibu za kuhakikisha wafanyakazi wanatenda kadri ya taratibu na kanuni hizo bila kujali masuala yote yanayo muhusu mfanyakazi ambayo haya athiri utendaji wake moja kwa moja.Masuala ya afya na ujuzi ndiyo yaliyozingatiwa tu sababu yana athiri utendaji wa mfanyakazi mojakwa moja. Hivyo basi jukumu la menejimenti ilikuwa nikumdhibiti mfanyakazi aendane na kanuni na taratibu katika eneo lake la kazi baada ya hapo menejimenti haihusiki. Mantiki hiyo iliitwa personnel management ikiongozwa na falsafa ya personnel monitoring.

Mashiko yake ikiwa ni kufuatilia uwajibikaji wa mfanyakazi kama unakidhi malengo,kanuni na taratibu bila kujali kiundani mambo mengine anayokabiliana nayo mfanyakazi ili kuongeza ufanisi, zaidi ya mafunzo na afya. 2.2. MWELEKEO WA DHIMA YA MENEJIMENTI BAADA YA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA Baada ya karne ya ishirini na moja,mwelekeo wa menejimenti ulibadilika na kujikita zaidi ya masuala ya kazini tu yamuhusuyo mfanyakazi. Mfanyakazi aliangaliwa zaidi ya kuwa mfanyakazi tu bali rasilimali inayohitaji kutunzwa,kuendelezwa na kuihusisha na mazingira ya ndani na nje ya maeneo ya kazi.Dhumuni likiwa mfanyakazi ni rasilimali kama rasilimali nyingine ambazo kwayo,huhitaji umakini wa ziada wa kuitunza kwa namna zote,ndani ya maeneo ya kazi na nje ya eneo la kazi ikiwa namaana ya kumuwezesha mfanyakazi aweze kukabiliana na mazingira yanayo mzunguka akiwa kazini na anopokuwa nje ya kazi.

Dhima ya kutomtofautisha mfanyakazi na matatizo yote yanayo muhusu ikawekewa mashiko katika kanuni na taratibu za kimenejimenti.Suala la kuwa na official and personal issues likawekewa angalizo.Dhima ya menejimenti ikawa shirikishi zaidi kwa maana kwamba matatizo ya mfanyakazi yote yanaihusu menejimenti tofauti itakuwepo tu ya jinsi ya kuyatatua. Matatizo yanayomuhusu mfanyakazi yaliyo ndani ya kanuni na taratibu za kikazi yatatatuliwa na menejimenti kwa mujibu wa hizo kanuni na taratibu.Na kwa yale ambayo yapo nje na taratibu,menejimenti itoe ushirikiano wa kuyatatua kadri mfanyakazi atakavyoomba msaada wa kimenejimenti.Kabla ya karne ya ishirini na moja mtazamo huu ulifumbiwa macho.

Mantiki ya sasa inaitwa human resources management ikiongozwa na falsafa ya teamwork.

Mashiko yake ikiwa ni kuwa haiwezekani kutenganisha ufanisi wa mfanyakazi(ambae ni rasilimali) na matatizo yanayo muhusu,iwe ya kikazi au kibinafsi.Menejimenti ishirikiane na mfanyakazi kulingana na madhila yanayo muhusu mfanyakazi lengo likiwa ni kumfanya mfanyakazi asiwe na jambo lolote litakalo kwamisha ufanisi wake. Hayo pia yatawezekana kama wafanyakazi hawatakuwa na matabaka na hivyo kufanya kazi kwa kutegemeana (teamwork).

Msingi mkubwa wa falsafa hii ulitokana na wanasaikolojia kutafiti ufanisi wa michezo ambapo kila mchezaji akitimiza wajibu wake ipasavyo na kocha kuwashirikisha bila kubagua,matokeo yake huwa ni ushindi.Kocha anatakiwa kuonesha wachezaji wote ni muhimu ila kipekee anaweza kutambua kipaji zaidi bila kuonesha waziwazi upendeleo. Falsafa hii pia inatoa pendekezo la eneo la kazi liwe sawa na sehemu ya michezo!! Kwa maana ya kwamba ofisi/kiwanda iwe wazi ili mfanyakazi mmoja aweze kumuona na kuwasiliana na mwingine kama ilivyo kwa wachezaji uwanjani.Dhana hii kwa baadhi ya ofisi/viwanda walikubaliana nayo japo wanafalsafa wengine waliipinga.Wanakubali teamwork ila sio pool office. Ofisi iliyowazi kwa kila mfanyakazi kumuona mwezake anavyojituma au kuzembea na hivyo kiongozi kuweza kuona kwa urahisi na kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo kirahisi.

Hivyo basi kutokana na mabadiliko ya dhima ya kimenejimenti tuliyonayo sasa (karne ya Ishirini na moja) inashauriwa ,eneo la kazi linapaswa kuwa eneo rafiki,eneo shirikishi na eneo lisilo na mipaka ya kimawasiliano kati ya mfanyakazi na mkuu wake wakazi.

Msingi wa hoja hii ni kuwa kwa sasa kutokana na mabadiliko ya tekinolojia ya mawasiliano na tofauti ndogo ya kiwango cha taaluma kati ya mfanyakazi na mkuu wake,hakuna tofauti ya uelewa wa kanuni na taratibu za kikazi na kiungozi.Hivyo basi mazingira shirikishi ni muhimu ili kufikia maamuzi sahihi yanayoendana na kanuni na taratibu ambazo wote mfanyakazi na mkuu wake wanazifahamu kwa dhati. Kabla ya karne ya ishirini na moja,ilikuwa ni vigumu mfanyakazi kujua kanuni na taratibu za kazi sababu kanuni na taratibu hizo ilikuwa ni siri na upatikanaji wa kanuni na taratibu hizo ilikuwa aidha ni vigumu na vile vile ni kosa kuwanazo mfanyakazi wa kawaida. Kukuwa kwa teknolojia ya mawasiliano kumeondoa mipaka hii na hivyo upatikanaji wake kuwa wawazi.Hivyo basi yote anayoyajua mkuu wa kazi kwa maana ya kanuni na taratibu,vivyohivyo yanajulikana na wafanyakazi husika walio chini yake.Maamuzi yanapofanyika ni ukweli usiopingika kuwa mfanyakazi atajiridhisha kwa kudurusu kanuni na taratibu zilizo pelekea maamuzi husika.Hivyo basi ni mwito kwa menejimenti kwa ujumla wake kulijua hili kuwa hakuna maamuzi yanayofanywa na menejimenti na wafanyakazi wasijiridhishe na maamuzi hayo.Aidha ni uamzi wa wafanyakazi kutoa dukuduku au kuamua kukaakimya wasipo ridhishwa na uamzi/maamuzi ya kimenejimenti.Hapa ndipo mantiki ya teamwork inapokuwa na mashiko zaidi. Kuwa baada ya maamuzi, inapaswa yafikishwe na kushirikishwa kwa wafanyakazi wote watoe mawazo yao kuhusu maamuzi yaliyofikiwa na menejimenti. Kwa kufanyi hivyo, hakutakuwa na mgongano wa kimaamuzi kati ya menejimenti na wafanyakazi.Aidha pale ambapo maamuzi ya menejimenti yanakinzana na wafanyakazi, menejimenti haina budi kuendelea kuwaelimisha mantiki ya uamzi huo na taratibu wafanyakazi wataridhia.

Menejimenti ni kama kocha wa timu.Ili kocha aweze kuwajua wachezaji wake ni lazima kwapamoja washirikiane katika mazoezi ili aelewe mapungufu na ubora wa kila mchezaji. Hii itasaidia katika kuwapanga wachezaji wake katika mashindano.

Lugha hii ya picha inaonesha Menejimenti lazima iwe karibu na wafanyakazi ili kuwajua na kuweza kupanga majukumu kwa ufanisi zaidi. Makampuni na mashirika yote yanayofanya vizuri menejimenti ipo karibu na wafanyakazi kwa kufanya vikao vya kila siku kupata maoni mawazo na ubunifu kutoka kwa wafanyakazi husika.Hakuna namna yoyote ile ya kufanya vizuri kwa kampuni au taasisi kama menejimenti iko mbali na wafanyakazi wake kwa kuto fanya vikao vya kuwashirikisha na kuweka mipaka ya mawasiliano kati ya wafanyakazi na menejimenti.

HITIMISHO Hakuna jambo dogo katika uongozi kwa sababu wafanyakazi wanamtazamo tofauti.Jambo dogo kwa utawala laweza kuwa kubwa kwa wafanyakazi.Vivyo hivyo jambo dogo kwa mfanyakazi laweza kuwa kubwa kwa uongozi.Kila mmoja atende impasavyo kwa kuzingatia dhima ya menejimenti ya karne ya Ishirini na moja; (human resources management and teamwork which encompasses both official and personal issues); Rasilimali lazima itunzwe Ili uitunze hunabudi kuwa nayo karibu uone namna nzuri ya kuitunza Kukua kwa rasilimali husika ndiyo faida mahususi ya mtunzani wa rasilimali.