24
Awamu ya 2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

CP - CRK FAW July to Printer 2013 lw - ccp.jhu.educcp.jhu.edu/documents/CP Facltr Guide 2013.pdf · mahitaji yao ya maisha, kuleta furaha na maelewano mazuri na mwenza wako nyumbani

Embed Size (px)

Citation preview

Awamu ya2MWONGOZO WA MWEZESHAJI

Awamu ya2MWONGOZO WA MWEZESHAJI

Yaliyomo

UtanguliziSehemu ya

Uk

Sehemu ya

Sehemu ya

Sehemu ya

Sehemu ya

Sehemu ya

Sehemu ya

1

2

3

4

5

6

7

1

2

3

4

5

6

7

Simulizi 1

Majadiliano kuhusu simulizi1.

Simulizi 2

Majadiliano kuhusu simulizi 2

Kujitoa katika Mtandao wa ngono

Hitimisho

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

Mwezeshaji:Karibisha washiriki, waeleze kuwa hiki ni kipindi kuhusu mitandao ya ngono, waeleze pia katika kipindi hiki watajifunza jinsi gani mtu aliye kwenye mtandao wa ngono anaweza kuchukua maamuzi ya kujitoa katika mitandao hiyo. Swala hili ni nyeti na linaweza kuibua mijadala mingi.

Wahimize kusikiliza simulizi kwa makini na wawe wazi katika kuchangia. Pia wakumbushe kuwa simulizi hii inahusisha majina ambayo ni ya kubuni. Na endapo itatokea yupo mtu miongoni mwao ambaye jina lake linafanana na jina la mmoja wa wahusika katika simulizi hii, asijione kuwa amelengwa.

Sehemu ya 1: Utangulizi

1

2

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

Mwezeshaji panga mtandao wa ngono kwa kushirikisha washiriki kama ifuatavyo;

Nitasoma simulizi. Kila nitakapomtaja mshiriki nitamchagua mtu mmoja kutoka miongoni mwenu. Nikikuchagua nitaomba uje mbele na umshike mshiriki (au washiriki) unaounganishwa nao. Tafadhali kumbuka jina la mshiriki ambalo utapewa. Baadaye tutakuwa na majadiliano.

Huyu ni Pendo. Pendo ni mama wa nyumbani.

Huyu ni Mashaka. Pendo na Mashaka wamekuwa wanandoa kwa miaka mitano. Kwa sasa Pendo ni mjamzito. Mashaka anampenda mke wake, lakini ana mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine.

Huyu ni Sofia. Sofia ni mwanafunzi wa sekondari. Mashaka na Sofia hufanya ngono.

Huyu ni Maua. Maua ni mpenzi wa Mashaka lakini pia hufanya mapenzi na Amani.

Huyu ni Amani. Marafiki wa Amani humwita kiwembe, ana wapenzi wengi.

Huyu ni Tumaini. Tumaini husafiri mara kwa mara kwa ajili ya kazi zake. Maua pia yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na Tumaini.

Huyu ni Anita. Anita hufanya ngono na Tumaini.

Huyu ni Zawadi. Zawadi hufanya mapenzi na Tumaini pia hufanya mapenzi na Amani.

Huyu ni Bahati. Tumaini amemuajiri Bahati. Tumaini amemuahidi Bahati kumpandisha cheo kama atafanya nae ngono, Bahati amekataa.

Huyu ni Faraji. Faraji ni mpenzi wa kweli wa Bahati na anataka kumwoa. Tangu ampate hajawahi kuwa na mwanamke mwingine.

Sehemu ya 2: Simulizi ya 1

3

4

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

1. Je, hali kama hii ya mahusiano ya kingono inatokea katika jamii yenu?

2. Kwanini watu wanakuwa na mahusiano ya kingono na mtu zaidi ya mmoja? Majibu:

a. Kipato

b. Starehe

c. Tatizo la mawasiliano na mahusiano mabaya nyumbani

d. Kutoridhishwa katika tendo la ngono

e. Shinikizo rika

3. Ni yapi madhara ya kuwa na mahusiano ya kingono na mtu zaidi ya mmoja?

4. Kama mmoja wapo miongoni mwa hao walio katika mtandao ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, hali itakuwaje?

Sehemu ya 3: Majadiliano kuhusu simulizi 1.

5

Hawa ni Bahati na Faraji:

• Bahati na Faraji wameoana na kwa sasa Bahati ni mjamzito. Siku zote Bahati na Faraji hujadili na kupanga mambo yao na kuyatekeleza kwa pamoja. Faraji humsindikiza Bahati kila anapopaswa kuhudhuria kiliniki.

Mwezeshaji, soma wasifu wa kila mshiriki kama ilivyooneshwa hapo chini, kwa kufuata mtiririko kama ulivyoanza kuwapanga washiriki katika mtandao wa ngono.

Sehemu ya 4: Simulizi ya 2

6

Huyu ni Mashaka,

• Mashaka ni mume wa Pendo, lakini pia Mashaka amekuwa na mahusiano ya kingono na Maua, Sofia na wanawake wengine.

• Pendo kwa sasa ni mjamzito. Faraji na Mashaka ni marafiki na hucheza bao pamoja nyakati za jioni baada ya kazi.

• Faraji amekuwa akimshauri Mashaka mara kwa mara juu ya umuhimu na faida ya kumsindikiza mkewe Pendo kliniki ikiwemo kupata elimu juu ya afya ya mama mjamzito na mtoto aliye tumboni na umuhimu wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aliye tumboni na ushauri nasaha na kupima kwa pamoja. Japo mwanzoni alikuwa mbishi, hatimaye aliona umuhimu wa kufanya hivyo na kukubali.

• Huko kliniki, Mashaka alipata elimu juu ya tabia hatarishi zinazochangia mtu kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI ikiwemo kuwa na mahusiano ya kingono na mwanamke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja . Pia umuhimu wa kujilinda yeye mwenyewe mke wake na mtoto aliye tumboni dhidi ya maambukizi ya VVU. Elimu hii iliwashawishi yeye na mkewe kupima kwa pamoja.

• Tukio hili la kupima VVU na mkewe lilimfanya atafakari sana juu ya tabia na athari za yeye kuwa na mahusiano ya kingono na wanawake wengine, hadi kumfanya afanye maamuzi magumu ya kuvunja mahusiano ya kingono na wanawake wengine aliokuwa nao.

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

7

Mwezeshaji: Mtenganishe Mashaka na Sofia, kisha na Maua kwa kuonyesha ishara ya kukata/kuachana na mtandao, na waruhusu waondoke, kisha endelea

Huyu ni Sofia.

• Sofia alipokuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari alikuwa na mahusiano ya kingono na Mashaka.

• Sofia alibahatika kufaulu na kwa sasa amejiunga na masomo ya chuo kikuu katika kitivo cha Uhandisi.

• Kama ilivyokuwa wakati akiwa shule ya sekondari, baada ya kuwa ameachwa na Mashaka kwa sasa hapo chuoni ana mahusiano ya kingono na Sikioni ambaye ni mwanachuo mwenzake wa mwaka wa kwanza.

• Mbali na kuwa na mahusiano ya kingono na Sikioni pia ana mahusiano ya kingono na Mkombozi ambaye ni mfanya biashara maarufu.

• Matokeo ya mtihani kwa muhula wa kwanza wa masomo yameonyesha kuwa Sofia hajafaulu vizuri hivyo inamlazimu kurudia masomo matatu.

• Hali hii imemshitua sana Sofia kiasi cha kumfuata Mwalimu Kiboko na kumshawishi ili wafanye naye ngono kwa masharti ya kupewa upendeleo katika mtihani wa somo lake ambalo linasemekana kuwa gumu kufaulu, japo bado ni mtihani kwa masomo yaliyobaki ambayo anafikiria kufanya njia hiyo hiyo kufaulu kama itawezekana.

• Tangu wamekuwa kwenye mahusiano na Mkombozi, Sofia anaamini kabisa kuwa yuko pekee yake.

8

• Lahaula!!/La!!/Du!! Alikaribia kuzimia siku alipokwenda nyumbani kwa Mkombozi na kumkuta anafanya tendo la ngono na mwanafunzi mwingine aitwaye Sikujua

• Kitendo hiki kilimfanya afikirie sana kuhusu afya yake na hatimaye Sofia aliamua kwenda katika kituo cha afya. Huko kwenye kituo cha afya Sofia alipata elimu kuhusu Ukimwi na namna ya kujilinda ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mahusiano ya kingono na watu wengi kwa wakati mmoja, kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na aliyepima.

• Elimu hii ilimshawishi Sofia kupima na matokeo yakaonyesha hana VVU.

• Tukio la kupima na kujikuta hana VVU lilimfanya atafakari sana tabia zake za mahusiano ya kingono na wanaume wengi na hatari zake.

• Hili lilimshitusha sana na kumfanya kuamua kuvunja mahusiano yake ya ngono na wanaume wote aliokuwa nao ili kulinda afya yake na kuendelea na masomo yake.

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

9

Huyu ni Maua

• Maua alikuwa na mahusiano ya ngono na Mashaka

• Pia wakati mwingine alikuwa akifanya ngono na Amani na Tumaini

• Baada ya Maua kuelezwa na Mashaka sababu ya maamuzi ya kuachana naye, ambayo ni kulinda afya yake na ya mkewe Pendo ambaye ni mjamzito pamoja na mtoto wanayemtarajia ili kujikinga wasipate maambukizi ya VVU, Maua aliamua kubaki na Amani na Tumaini.

• Maua aliamini kabisa kwamba amebakia katika mahusiano na watu wawili tu. Lakini alichanganyikiwa siku alipomfumania Amani akifanya mapenzi na rafiki yake wa karibu.

• Kitendo cha Maua kumfumania Amani, kilimfanya kufikiria matokeo ya mwenendo wa tabia ya Amani kwa afya yake na madhara yanayoweza kumpata, alitia shaka kuwa huenda hata Tumaini pia akawa ana tabia kama za Amani .

• Hivyo aliamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuwaacha wote wawili, na hivyo kujitoa katika mtandao wa wapenzi wengi kwa wakati mmoja.

10

Mwezeshaji: Mtenganishe Maua na Tumaini na Amani kwa kuonyesha ishara ya kukata/kuachana na mtandao, na waruhusu Maua na Amani kuondoka, kisha endelea.

Huyu ni Tumaini

• Baada ya Tumaini kuachwa na Maua aliumia sana na kuanza kutafakari jinsi alivyomgharimia kimaisha halafu leo anamuacha ghafla hivi.

• Mawazo mengi yalimjia huku akitazama ujumbe mfupi wa simu aliotumiwa muda mfupi uliopita, mmoja ukitoka kwa Anita kimada wake aliyetaka alipiwe kodi ya nyumba na Zawadi hawara yake aliyeomba asaidiwe kulipiwa ada za shule na fedha za kulimia shamba.

• Haya yote yalimchanganya kimawazo hatimaye alichukua uamuzi wa kuwaacha wote.

Mwezeshaji: Mtenganishe Tumaini na Anita na Zawadi kwa kuonyesha ishara ya kukata/kuachana na mtandao, na waruhusu waondoke. Mtandao utakuwa umekwisha.

Mwezeshaji uliza washiriki:

Mmeona na mmejifunza nini katika igizo hili?

• Tumejifunza kwamba unaweza kudhani hauko kwenye mtandao kumbe mwenza wako anakuingiza kwenye mtandao wa ngono bila kujijua

• Tumejifunza sababu mbalimbali zinazowafanya watu wajiingize katika mitandao ya ngono

• Tumeona kwamba ni rahisi sana kupata maambukizi ya VVU na magonjwa ya ngono ukiwa kwenye mtandao wa ngono

• Tumeona kwamba kujitoa katika mitandao ya ngono inawezekana

• Tumejifunza kuishi maisha ya uaminifu kama Bahati na Faraji

• Tumejifunza kuishi maisha ya kusikilizana, kusaidiana, kutumia huduma za afya kama Bahati na Faraji.

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

11

12

1. Je unafikiri ni kwa nini Mashaka, Sofia, Maua, Tumaini walichukua uamuzi wa kuachana na mitandao ya ngono?

Majibu:• Baada ya kupata elimu alijua kuwa tabia yake inamuweka katika hatari ya kupata

maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,na angeweza kumwambukiza mke wake na mtoto wao aliye tumboni.(Mashaka)

• Baada ya kumfumania Amani na kugundua kuwa anafanya ngono na wanawake wengine Maua alijiona kuwa yuko kwenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU akaamua kujilinda kwa kuwaacha wote. Alimuacha Tumaini pia kwa sababu alihisi Tumaini anaweza kuwa na tabia kama hizo.(Maua)

• Tumaini aliona ni usumbufu kujiingiza kwenye gharama zisizo za msingi (Tumaini).

2. Wewe ungekuwa ni mmoja wa wahusika ungefanya uamuzi kama walioufanya wao? Unadhani ni rahisi?

Majibu:• Ndiyo.• Kwa kuelewa madhara yake, faida, na hatimaye kukufanya uchukue uamuzi sahihi wa

kujitoa kwenye mtandao wa ngono. (Mwezeshaji awaeleze washiriki kuwa inawezekana japo mabadiliko ya tabia ni

mchakato)

Sehemu ya 5: Majadiliano kuhusu simulizi ya 2

Kisha mwezeshaji endelea kuuliza maswali yafuatayo.

13Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

3. Unafikiri ni faida zipi wahusika watazipata kwa kujitoa katika mtandao? Majibu:

• Wataepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa mengine ya ngono na mimba zisizotarajiwa.

• Wataepuka gharama zisizokuwa za lazima.

4. Je ni nini kifanyike ili watu walio na tabia za kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja kama walizokuwa nazo wahusika wa igizo hili, waweze kuziacha?

Majibu:• Waelimishwe juu ya athari za kuwa katika mitandao ya ngono.• Waelimishe juu ya umuhimu wa wenza kujadiliana katika masuala yao ya mapenzi ili

kuwa na maamuzi yanayoridhiwa na pande zote mbili ili kuepusha mitafaruku

14

FungaZIPU!

1. Wanaume au wanawake walio katika mitandao ya ngono wanachukuliwaje na jamii inayowazunguka?

2. Je Anita na Zawadi wafanye nini baada ya kuachwa na Tumaini ili wasiingie kwenye mtandao mwingine?

i. Wajiunge kwenye vikundi vya kijamii (hisa, ujasiriamali n.k.) ili waweze kupata mikopo na kuanzisha shughuli zitakazowaingizia kipato

ii. Wajiunge na vikundi vya imani za dini ili kufuata maadili ya dini zao kuhusu kuwa waaminifu na kuacha uzinifu

3. Taja mambo ambayo unaweza kuyafanya wewe na mwenza wako kwa pamoja na yakawafanya wote mkatulizana pasipo mtu mwingine kutoka nje ya mahusiano yenu.

• Mawasiliano – Kuwa na mawasiliano ya wazi• Kuridhishana katika mahusiano ya kimapenzi ikiwemo mahusiano ya ngono

4. Utamshauri nini rafiki, ndugu au jamaa yako unapogundua ana mahusiano ya kingono na watu wengi?

5. Je ni nani katika simulizi au igizo hili amekuwa ni mfano wa kuigwa katika jamii? Kwa vipi? Jibu: Wote. (mbali na Faraji na Bahati pia wote waliojitoa kwenye mtandao ni mfano wa kuigwa)

6. Kama kuna mtu katika mtandao huu amepima akakutwa ameambukizwa VVU je na yeye anatakiwa kujitoa kwenye mtandao? Jibu: Ndiyo, anatakiwa kujitoa ili aepuke kupata maambukizi mapya na vile vile kutowaambukiza wengine

7. Je kuna mtu kati yenu amewahi kuwa kwenye mtandao na kuamua kujitoa? Je ni sababu zipi zilizokufanya ujitoe?

Sehemu ya 6: Kujitoa katika Mtandao wa ngono

Awamu ya2 MWONGOZO WA MWEZESHAJI

15

• Ni muhimu kwa wapenzi kuwa na mawasiliano mazuri na kuridhishana ili kuepuka kuingia katika mitandao ya ngono.

• Ni muhimu kwa wanajamii kujua hali za afya zao.

• Ni jambo jema kuwashauri na kuwasaidia jamaa zetu kutoka katika mitandao ya ngono.

• Kuna faida nyingi za kujitoa kwenye mitandao ya ngono zikiwemo kuepuka hatari ya kupata maambukizi ya VVU, kumlinda mwenza wako dhidi ya maambukizi ya VVU, kuepuka gharama zisizo za lazima za kuhudumia wanawake wengi kwa wakati mmoja katika kukidhi mahitaji yao ya maisha, kuleta furaha na maelewano mazuri na mwenza wako nyumbani

Sehemu ya 7: HitimishoMwezeshaji: kabla hujahitimisha waulize washiriki kama wana maswali kutokana na yale waliyojadiliana na kisha fanya majumuisho kwa kurejea yafuatayo

16

Hitimisha kwa kuwaeleza washiriki kuwa ukishajiuliza

Jitoe mtandaoni kisha

................... bila mitandao ya ngono inawezekana

17

FungaZIPU!