16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1131 SHAABAN 1435, IJUMAA , JUNI 27 - JULAI 3, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz facebook: [email protected] Wasichana wavaa uchi wazomewe - Profesa Wanawake wasikubali kufanywa bidhaa Utu ni muhimu kuliko umaarufu wa kijinga Vyombo vya habari vikome kuwapamba Unguja tulivu, Pemba shauri yao Mapinduzi Daima, nani mchochea vurugu? Kisonge wanamtia majaribuni Rais Shein Walilia kurejea yale ya ‘melody’, Janjaweed Uk. 4 INSHA'ALLAH, Nitafurahi kuona kwa kiasi fulani sehemu kubwa ya watoto wangu na wajukuu wote wanakuwa Waislamu. Sikuwahi kujuta kuwa Muislamu na ninamwomba Mwenyezi Mungu anipe imani kama ile ya Maswahaba Hatujafanya Da’wah kabisa Hatujawafikia wenye kiu ya Mwongozo wa Mtume (s.a.w). Sema: Hakika Bwana wangu ameniongoza katika njia iliyonyooka (dini ya kweli) njia ya Abraham, inayoegemea ukweli. Na hakuwa miongoni mwa wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu. (Soma Uk. 8, 9) Jaji ajitoa kusikiliza rufaa ya Sheikh Ponda Mahakama yakubali rufaa kufanyiwa marekebisho Uk. 2 Uk. 3 BAADHI ya akinamama wa Kizungu wanaosilimu kwa juhudi zao wenyewe. Kulia ni Yvonne Ridley. Karibu Ramadhan Uk. 16

An Nuur 1131

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: An Nuur 1131

ISSN 0856 - 3861 Na. 1131 SHAABAN 1435, IJUMAA , JUNI 27 - JULAI 3, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz facebook: [email protected]

Wasichana wavaa uchi wazomewe - Profesa

Wanawake wasikubali kufanywa bidhaaUtu ni muhimu kuliko umaarufu wa kijingaVyombo vya habari vikome kuwapamba

Unguja tulivu, Pemba shauri yaoMapinduzi Daima, nani mchochea vurugu?Kisonge wanamtia majaribuni Rais SheinWalilia kurejea yale ya ‘melody’, Janjaweed

Uk. 4

INSHA'ALLAH, Nitafurahi kuona kwa kiasi fulani sehemu kubwa ya watoto wangu na wajukuu wote wanakuwa Waislamu.

Sikuwahi kujuta kuwa Muislamu na ninamwomba Mwenyezi Mungu anipe imani kama ile ya Maswahaba

Hatujafanya Da’wah kabisaHatujawafikia wenye kiu ya Mwongozo

wa Mtume (s.a.w).Sema: Hakika Bwana

wangu ameniongoza katika njia iliyonyooka (dini ya kweli) njia ya Abraham, inayoegemea ukweli. Na hakuwa miongoni mwa wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu. (Soma Uk. 8, 9)

Jaji ajitoa kusikiliza rufaa ya Sheikh Ponda

Mahakama yakubali rufaa kufanyiwa marekebishoUk. 2

Uk. 3

BAADHI ya akinamama wa Kizungu wanaosilimu kwa juhudi zao wenyewe. Kulia ni Yvonne Ridley.

Karibu Ramadhan

Uk. 16

Page 2: An Nuur 1131

2 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari

J A J I a l i y e k u w a akisikiliza rufaa ya Sheikh Ponda katika mahakama Kuu jijini Dar es Salaam Shaban Lila amejitoa kusikiliza rufaa hiyo jana.

Jaj i huyo amesema M a h a k a m a n i h a p o kwamba amelazimika kujitoa kusikiliza rufaa hiyo kwasababu dhamira yake inamfunga asiweze kuendelea kusikil iza rufaa hiyo.

Kufuatia kujitoa Jaji Shaban Lila kusikiliza rufaa ya Sheikh Ponda Issa Ponda, ambayo awali iliwasilishwa na wakili wake Bw. Juma Nassor, Jaji Stephen Kaduri ndiye ambaye amekabidhiwa faili la rufaa hiyo na ndiye atakayesikiliza shuri hilo.

Kufuatia hali hiyo, Wakili Juma Nassor, a l i iomba mahakama hiyo imruhusu kufanya marekebisho ya hati ya rufaa yake aliyoiwasilisha na kuirejesha mahakamani h a p o k w a a j i l i y a mahakama kuendelea kuisikiliza, jambo ambalo wakili wa serikali alipinga ombi hilo.

Pamoja na wakili wa serikali kupinga hoja ya wa k i l i N a s s o r o , Mahakama ilikubaliana na hoja kat ika ombi la wakili Nassoro na kumkubalia kufanya marekebisho ya hati yake ya rufaa aliyoiwasilisha awali.

Kufuatia kukubaliwa h u k o , M a h a k a m a i m e p a n g a k u w a marekebisho ya rufaa h i y o y a w a s i l i s h w e mahakamani hapo Julai 8 mwaka huu ambapo Agosti 4, hoja za rufaa hiyo zitasikilizwa mahakamani hapo mbele ya Jaji Kaduri.

Kabla ya rufaa hiyo kusikilizwa hapo jana, Mei 2, 20014 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda, a l igoma kwenda Mahakamani kutoka mahabusu ya gereza la Morogoro, akitaka haki itendeke

Jaji ajitoa kusikiliza rufaa ya Sheikh PondaMahakama yakubali rufaa kufanyiwa marekebishoNa Shaban Rajab

katika kesi yake.S iku h iyo She ikh

P o n d a a l i t a k i w a kwenda kusikiliza kesi yake ya msingi ikitajwa katika Mahakama ya mjini Morogoro, kama i l i v y o p a n g w a n a Mahakama hiyo.

Ilielezwa kuwa Sheikh Ponda, aligoma kwenda Mahakamani akikusudia k u f i k i s h a u j u m b e kwamba, anachofanyiwa kat ika kesi hiyo ni kinyume na haki zake kikatiba.

K u g o m a h u k o kulitokana na Sheikh Ponda kuona anaendelea kudhulumiwa badala ya kufatwa sheria, hasa kutokana na rufaa yake aliyokata Mahakama Kuu Dar es Salaam ya kutaka kurejea uamuzi wa kesi iliyohukumiwa Mahakama ya Kisutu

i l i y o m p a k i f u n g o c h a n j e u r e j e w e , l a k i n i u k i c h e l e w a kufanyika hadi kifungo chenyewe kikiwa tayari kimemalizika.

I m e e l e z w a k u w a S h e i k h P o n d a anaona mazingira ya mashauri yake mawili y a n a v y o p e l e k w a , yaani hilo la rufaa na kesi yake ya Morogoro, y a m e g u b i k w a n a mashaka.

Kufuatia kuchelewa kwa kusikilizwa shauri la rufaa hiyo, Mahakama ya Morogoro imekuwa ikitaja na kuahirisha kesi yake mahakani hapo kwa kuwa haiwezi kulazimisha fai l i la Sheikh Ponda lipelekwe Morogoro, na hawawezi pia kusema chochote mpaka pale Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi wa rufaa hiyo.

SHEIKH Ponda Issa Ponda.

Al-MARHUM Profesa Kigoma Ally Malima, katika uhai wake aliwahi kuwausia Waislamu nchini k wa k u s e m a m a n e n o machache lakini yenye uzito mkubwa.

Profesa Malima, aliwaasa Waislamu wawe ni watu wa kujiratibu na kisha kufanya kazi kwa malengo, wadai haki yao zao badala ya kulalamika na kwa kufanya hivyo, shida zao zitaondoka na haki zao watazipata.

Usia huu tukiutafakari, tunaona haujafanyiwa kazi ipasavyo. Wenye wajibu wa kusimamia usia huo, ambao ni viongozi wa Waislamu, bado hawajaamua kikamilifu kuufanyia kazi.

Tunasema hivyo kwa sababu umma wowote au kundi lolote haliwezi kufanya mambo yake kwa ufasaha na kwa ufanisi bila ya kuwa na viongozi wa kuratibu mambo kisha kuyawasilisha kwa hao wanaowaongoza kwa ajili ya utekelezaji.

Kutokana na mfumo wa kiutawala wa nchi ulivyo, Wais lamu wanatakiwa kujiratibu kiimani na kisiasa na kufanyia kazi kisayansi kile walichokiratibu, ili waweze kujiimarisha zaidi kiimani na vilevile kujiiza na kujiimarisha kiasiasa hususan katika mamlaka za maamuzi katika mfumo wa kiutawala.

Tumeamua kukumbushia hoja hii kwasababu hivi sasa Waislamu tunaingia katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. K wa k a wa i d a , k a t i k a mwezi huu Waislamu huwa wanajitahidi kujikurubisha sana na ibada, kipindi hiki Waislamu hujitokeza zaidi kuonyesha na kudhihirisha Uislamu wao. Katika kipindi hiki mapenzi, kuhurumiana na kupendana Waislamu hujionyesha.

Kwa msingi huo basi, t u n a c h u k u a f u r s a h i i kuwakumbusha viongozi w e t u w a K i i s l a m u , M a s h e i k h , M a i m a m u , W a n a z u o n i , k a t i k a Ramadhani hii kujitokeza kwa wingi kulingania umoja katika Uislamu nchini.

T u n a s e m a h i v y o k w a s a b a b u t a y a r i Ramadhani imeturahisishia k a z i k w a k i w a n g o kikubwa, sehemu iliyosalia ikitekelezwa kikamilifu

Ramadhani njia sahihi ya umoja wa kudumu wa Kiislamu

na viongozi wetu, basi utakuwa mwanzo mzuri wa jamii ya Kiislamu nchini kushikamana na kuwa kitu kimoja hata baada ya Ramadhani.

Kwa miaka mingi umoja umekuwa ugonjwa mkubwa katika jamii ya Waislamu n c h i n i . K a m a k a t i k a Ramadhani hii tunafunga pamoja, tunaswali pamoja, t u n a f u t u r u p a m o j a , h a t u t e n d e a n i u o v u , tunatubu madhambi yetu, kwanini tusitumie nafasi hii ya utukufu wa Ramadhani, kumaliza tofauti zetu za kitaasisi, kimadhehebu na tukarejea kuwa kundi moja la Waislamu.

Tunawashauri viongozi wetu wa kiimani, maulamaa, wanazuoni, Masheikh na Maimamu, kubuni mbinu sahihi za kurejea umma wa Kiislamu katika umoja kipindi hiki.

Tu s i i s h i e k u a n d a a mashindano ya kuhifadhi Qur’an tu, makongamano, Warsha, darsa, futari za pamoja, zote hizo ni njia sahihi za kukusanya umma wa Kiislamu pamoja na kujadili masuala ya msingi katika imani na hata katika medani za huduma za kijamii na kisiasa.

Ramadhani ni ukombozi kwa Waislamu kimaisha hapa duniani na kesho akhera. Ndani ya Ramadhani tunarehemewa na Allah (sw), ndani ya Ramadhani tunanusuriwa na ibilisi na sheitwan, ndani ya Ramadhani tunasamehewa dhambi zetu kwa kutubu makosa yetu, ndani ya Ramadhani tunaachwa huru, ndani ya Ramadhani tunal ipwa her i nyingi hususan kwa kupatwa na usiku wa Lailatul Kadir.

Ndani ya Ramadhani t u n a o n g e z a m a p e n z i miongoni mwa Waislamu hata kwa sio Waislamu. Ndani ya Ramadhani tunasaidiana, tunasameheana, tunaoneana huruma, tunapendana.

Kama tunafaidika na yote hayo kupitia chuo Ramadhani, kwanini ndani ya Ramadhani Waislamu w a s h i n d w e k u o n d o a mgawanyiko uliopo na kuwa na umoja wa kweli hata baada ya kwisha Ramadhani?

Page 3: An Nuur 1131

3 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari

Wasichana wavaa uchi wazomewe - ProfesaWANAWAKE wametakiwa kujali zaidi utu wao kuliko kukimbilia senti na umaarufu wa kijinga.

Wito huo umetolewa n a P r o f e s a P e n i n a Mlama wakati akiongea na wanahabari Juni 24, 2014, Kimalang’ombe, B a g a m o y o , k a t i k a Kongamano la maadili ya wanahabari lililoandaliwa n a B a r a z a l a H a b a r i Tanzania (MCT).

P r o f e s a M l a m a a m e s e m a k u w a wanawake wamekuwa w a k i j i d h a l i l i s h a huku baadhi ya watu wakiwafanya kama bidhaa.

Kwa upande mwingine akavikemea vyombo vya habari akisema kuwa vimekuwa vikiendeleza na kupamba upuuzi huo kwa kushabikia habari na picha za wasichana wacheza uchi katika kumbi za starehe.

Akasema, baadhi ya wananchi nao wameingia ujinga kwamba badala ya kuwazomea wacheza uchi katika kumbi hizo huwashangilia.

Katika hali hiyo akasema kuwa, vyombo vya habari nchini v ina mchango mkubwa katika biashara ya kubidhaisha wanawake badala ya kuwaelimisha wajue utu wao ili wakatae kufanywa bidhaa.

Prof. Mlama alisema kuwa suala hilo kwa sasa ni moja ya changamoto zinazovikabili vyombo vya habari na kuvitaka kuliangalia suala hilo kwa umakini kwa kuzingatia dhima ya vyombo vya habari katika jamii.

“Katika hili vyombo vya habari vina mchango mkubwa sana ka t ika kubidhaisha wanawake, kwa hiyo ninachoomba n i k u w a t u i a n g a l i e h iyo changamoto , i l i muweze kulifanyia kazi kwa kuwaelimisha wale wanaokubali kuwa bidhaa ili waweze kujitambua, kujiamini, kujithamini na kuona kuwa utu wao n i m u h i m u , k a m w e wasikubal i kufanywa bidhaa”. Alisema Prof. Mlama.

A l i s e m a , h a l i h i y o inakuwa ni changamoto kwa vyombo vya habari kwa kule kubidhaisha wa n a wa k e k wa h a l i ya juu kwa kuwa kuna

Na Bakari Mwakangwale, Bagamoyo.

watu wameona mwili wa mwanamke ni bidhaa unayoweza kuiuza kwa urahisi.

Alisema, ukiangalia katika Tanzania ya sasa, kwa hivi sasa kuna hali ya kumfanya mwanamke kuwa bidhaa kwa hali ya kiwango cha juu na hali hiyo inajionyesha katika matukio mengi.

Prof. Mlama, alisema wale wenye kutengeneza pesa wametengeneza miradi ya kubidhaisha wanawake kwa sababu kupitia wao wanatengeneza pesa, huku akiyataja mashindano mbalimbali ya urembo (Miss), na kufafanua kuwa hayo ni katika biashara ya kubidhaisha miili ya wanawake.

Mbali na mashindano ya urembo, lakini pia Profesa Mlama, akawataka wadau wa habari kuangalia pia masuala ya sanaa kwani akadai hivi sasa nazo zinabidhaisha wanawake.

“Wote ni mashahidi hapa, mnaona hivi sasa yanayoendelea katika sanaa ni minengue na ngono kwa wingi. Ukiangalia pia suala la urembo, jambo ambalo limekuwa ni bidhaa kubwa kwa kumtumia mwanamke kupitia vyombo vya habari kama vile magazeti, redioni na Televisheni”. Alisema Prof. Mlama.

Akahoji, “hivi vipindi katika Televisheni, radio na magazeti ambayo kila wakati yanambidhaisha mwanamke, je hiyo ndiyo dhima yao? Na je, huo ndio uwajibikaji wao kama vyombo vya habari?”.

Alisema, mara zote u k i a n g a l i a k a t i k a maonyesho katika kumbi m b a l i m b a l i u t a k u t a wanawAke wanacheza uchi jukwaani na wale watu waliojaa ukumbini wanaushangilia kwa nguvu zote uchafu ule na cha ajabu vyombo vya habari wanarusha na kuripoti upuuzi huo.

A l i s e m a , a n a d h a n i kwamba upo umuhimu wa kuliangalia tatizo hilo kwa mapana yake ili katika mikakati ya kubadilika huko isiwe tu ni kwa vyombo vya habari au waandishi wa habari lakini pia na kwa walaji wao (wasomaji).

Hivyo basi Prof. Mlama, akasema kazi kubwa i l iyopo kwa vyombo vya habari ni kuelimisha

au kuhamasisha walaji (wasomaji) na endapo wakielimika hakutakuwa n a m t u a t a k a e we z a k u c h a p i s h a g a z e t i lenye mambo machafu likanunuliwa.

Kwa mfano, alisema ukiangalia maonyesho katika kumbi mbalimbali w a t u w a m e j a a n a kuwashangilia kwa nguvu wanawake wanaocheza nusu uchi, lakini akasema w a s h a n g a l i a j i h a o wangekuwa wanawazomea wasingekuwa wanavaa

nusu uchi wanawake hao.Akavitaka vyombo vya

habari kurudi katika dhima yake ya kuwaelimisha wanawake wanaokubali kuwa bidhaa ili waweze kujitambua na kujithamini na kuona kuwa utu wao ni muhimu na wasikubali kufanywa bidhaa kwa manufaa ya watu wengine.

Lakini, Prof. Mlama, akatahadharisha kwamba k a t i k a k u l i k o m e s h a suala hilo mapambano yatakuwa makubwa kwani wale wanaowabidhaisha

wanawake wanapata faida kupitia biashara hiyo, hivyo wanaweza kutumia kila mbinu kuhakikisha kuwa wanawake hao wanabaki kuwa wajinga ili wabaki kuwa bidhaa kwao.

Ili kuepusha mgongano na vita katika hilo, alisema ni vyema pia hao ambao w a n a b i d h a i s h a n a o wakaelimishwa na kufanya nao kazi kwa nguvu ili waweze kutafuta pesa kwa mbinu nyingine na sio kwa kudhalilisha utu wa hao wanao wafanya bidhaa.

SHIRIKA la Kimataifa l a K u t e t e a H a k i z a Binadamu la Human Rights Watch, limetoa ripoti inayoonyesha kuwa waasi wanaopigana na serikali nchini Syria na katika nchi jirani ya Iraq, wanawapa watoto wadogo mafunzo ya kijeshi na kisha kuwatumia kama wanajeshi kwenye medani ya vita.

HRW limesema watoto walio chini ya umri wa miaka 15, wamekuwa wa k i p e wa s i l a h a n a kutakiwa kupigana na wanajeshi wa serikali katika nchi hizo, jambo l inalokiuka sheria za kimataifa zinazowalinda watoto.

Shirika hilo limetaja makundi ya Jabhat al-N u s r a , D a e s h , F r e e

Waasi wawatumia watoto vitani SyriaKuna hatari Marekani kupeleka jeshi Iraq

Syrian Army na Islamic Front Coalit ion kuwa miongoni mwa makundi yanayowatumia watoto kwenye vita.

Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, alifanya mkutano na Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, Jumatatu na kusisitiza umuhimu wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

R a i s wa M a r e k a n i Barack Obama amesema anaangalia uwezekano wa kuisaidia Iraq kukabiliana n a m a s h a m b u l i z i ya wanamgambo wa Kiislam waonadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq .

Aidha wanamgambo hao wamedhibiti eneo kubwa la Mashariki mwa jimbo la Diyala huku vikosi

vya serikali vikiendela ma mashambulizi ya anga ya magharibi mwa eneo la Samara kuijaribu kudhibi eneo hilo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani , Jen Psaki , ametoa ufafanuzi akidai k u wa wa t a l a a m wa o bado wanaendelea na majadil iano na kudai kwamba, si nia ya nchi yake kurejesha vikosi vyake Iraq japokuwa nchi hiyo inaona haja ya kutoa msaada kwa nchi hiyo kutokomeza makundi hayo.

Hata hivyo katika ziara yake nchini Iraq, Bw. Kerry hakutamka wazi ni hatua gani zitachukuliwa na Washington kuisaidia Iraq.

Wengi wanaamini ziara ya mwanadiplomasia huyo wa Marekani inaashiria

Inaendelea Uk. 5

Profesa Penina Mlama.

Page 4: An Nuur 1131

4 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari

Unguja tulivu, Pemba shauri yaoW A T U w a m e k u w a wakihoji baadhi ya watu wanapata wapi kibali cha kupika fitna na faraka katika jamii na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Kuhoji huko kunafuatia ujumbe ambao umekuwa ukiandikwa mara kwa mara katika ubao wa matangazo wa Kisonge ambao mara n y i n g i u m e k u wa wa kuchochea chuki na fitna.

“ M i m i n a s h i n d w a kufahamu hasa hii Maskani ya Kisonge ina kibali gani cha kupika Fitna,Chuki na Ubaguzi na kuwagawa wananchi wa visiwa hivi na huku Serekali ya SMZ ikachindwa kukemea au kuifunga Fitna ya Maskani hii?”

Huyo n i mmoja wa wananchi ambaye anahoji na kuweka maoni yake katika mtandao.

K a t i k a m a o n i ya k e m w a n a n c h i h u y o anaonyesha wasiwasi wake kuwa hali inavyokwenda ni kana kwamba viongozi wa serikali wameridhia kupikwa fitna hiyo, wakati wakiwa katika majukwaa ya siasa wanakemea chuki na kuhimiza umoja.

Anasema, “kila kukicha Maskani ya CCM Kisonge kuwabuguzi Wapemba kwa kuwasimanga kwa matusi na dharau kama vile ni wahamizi tu katika Zanzibar na huku SMZ ikiwa kimya bila kuwachukulia hatua za kisheria.”

Kisha anahoji, “viongozi w a S M Z / C C M , h i l i munaliona ndio uhuru wa kuzungumza au ndio demokrasia ya kulinda amani na utulivu?”

Kat ika nasaha zake mwananchi huyo amesema kuwa SMZ/CCM wafahamu kuwa siasa hizo za chuki ndio zinaigharimu CCM hata ikakosa kuungwa mkono na wananchi walio wengi na hivyo kulazimika kutumia nguvu za dola.

Anasema, “kila shari ina heri yake ndani , kumbukeni Micheweni Pemba kulikua ni CCM watupu na maeneo m e n g i t u ya Pe m b a , lakini ulipoanza ubaguzi wa kuwavunjia nyumba Wapemba kwa chuki za kisiasa na kuwasimanga kwa kuwatukana wende kwao ,Wapemba walianza kuichukia CCM na kuona sio Chama cha maana kwao ni chama cha kibaguzi.”

Kwa upande mwingine, anapewa heko Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa kurudiarudia d h a m i r a ya k e , l a b d a ahadi zaidi, ya kuilinda serikali ya umoja wa kitaifa anayoiongoza . Umma unautambua mchango wake huu.

Ila sasa, hata anapotamka hayo, akilenga kuenzi kitu

Na Jabir Idris, Mwandishi Wetu

adhimu kwa maendeleo ya watu wake, Wazanzibari, na mustakabali wa nchi ya o , k wa k u j i v u n i a a n a y o i t a m a f a n i k i o makubwa yaliyopatikana kutokana nayo, wanatokea baadhi ya watu kumtia katika majaribu.

H i v i k a r i b u n i , alipokaribisha mabalozi wapya Ikulu, aliwaambia anaienzi serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na mafanikio chini ya uongozi wake.

Anaamini mfumo huo wa serikali unasaidia nch i kwenda mbele . Nao wakamhakikishia kuendeleza ushirikiano k a m a w a l i v y o k u w a mabalozi wanaoondoka.

Rais anatoka hadharani k u t e t e a m a m l a k a yaliyotokana na maamuzi ya Wazanzibari ya kufuta siasa chafu na kujenga, badala yake, siasa mpya za maridhiano kwa lengo la kuibadili nchi ifute ufukara miongoni mwa watu wake.

Lakini tizama baadhi ya watu wanavyomvuta. Wanamyumbisha Rais. Wanaivunja misingi ya amani na utengamano iliyojengeka tangu 2010. Wanachafua s iasa za maelewano, umoja na ushirikiano.

M a t u k i o m a w i l i yenye mshabaha mmoja: Watu hao wanaviz ia m k u s a n y i k o w a Waislamu waliohitimisha mhadhara wa kusaidia kukumbushana mema na kukatazana maovu.

Wa n a t u p a b o m u . Mlipuko unaoelezwa na wataalamu kutokana na bomu la kivita la kutupa kwa mkono, unakata roho ya mwananchi. Unaumiza wananchi wengine kadhaa.

M a s h e t a n i h a w a wanatumia mbinu kali kupanga na kutekeleza matukio. Wanapanga kwa siri na mtendaji – ambaye amekosa ubinaadamu – akivaa koti la uharamia.

Ni vigumu kuwadhibiti, labda Jeshi la Pol is i lisimame imara na kwa ukakamavu. Liache siasa na kasumba. Litafanikiwa l i k i j a l i w a n a n c h i wanaoweza kujua michoro ya mashetani hawa.

Wa m e t u m i a k i v u l i c h a m k u s a n y i k o wa Waislamu kwenye Msikiti wa Darajani – maarufu Msikiti wa Muzamil – kupata sabuni ya roho kutoka kwa maulamaa waliotoka Tanga.

Mhadhara ul ikuwa umekwisha, waumini w a n a t o k a k u r u d i nyumbani, ghafla mlipuko. Bomu linalipuka nyanda tu kutoka walipo. Fadhaa na hofu – mahangaiko.

Wapo hawa wa tukio la pili: Wanachama wa CCM wanaouvaa ujinga na kujitoa fahamu kwa kuandika maneno ya uchochezi kwenye ubao wa matangazo. Ni Sauti ya Kisonge, tanuri halisi lililochimbwa Maskani ya M u e m b e k i s o n g e , M i c h e n z a n i , m j i n i Zanzibar.

Tanuri hili, kulingana na msomaji aliyepiga picha ya ubao huo na kunitumia; ak in ishaur i n i i tumie kuinua sauti ya wasio na sauti, bila ya hofu, linapika kasumba za kurudisha siasa chafu, fit ina na upotoshaji zilizokusudiwa kukoma na kurithiwa na siasa za maridhiano.

A n a a n d i k a k a t i k a ujumbe alioambatanisha na picha hii: “Tafadhali muandishi, tumia picha n i l i y o i p i g a k w e n y e maskani ya CCM mapema leo (siku hiyo), kuasa Wazanzibari waitunze amani iliyostawi kwa gharama kubwa na muda.”

U b a o wa S a u t i ya Kisonge unaambia watu: “PEMBA IWE SALAMA, U N G U J A Z O G O T U M E C H O K A : 2 0 1 5 MARIDHIANO YAISHE; UNGUJA IWE SALAMA. MAPINDUZI DAIMA.”

Wanakisonge wanahoji ni kwanini Pemba, ngome kuu ya Chama cha Wananchi (CUF), mbia wa CCM katika ser ika l i , kuwe mahala salama, bali Unguja kila siku zogo (vurugu). Wamechoka na wanatoa indhari ifikapo mwaka 2015, mwaka wa uchaguzi mkuu wa pili tangu maridhiano yaafikiwe, maridhiano basi.

K w a m a t a k w a y a o Wanakisonge, maridhiano yanachochea vurugu Unguja. Wanasema kama i l ivyo Pemba amani siku zote, Unguja ina haki ya kuwa salama.

K w a m b a k a b l a y a maridhiano ambayo msingi wake ulitandikwa na Amani Abeid Karume wa CCM, alipokuwa Rais wa Zanzibar, na Maalim Seif Sharif f Hamad wa CUF, walipofanya mazungumzo ya faragha Ikulu, Zanzibar palikuwa salama.

Inaingia aki l ini mwa Wanakisonge , kwamba kwa vile Pemba ambayo wangependa iwe peke yake siyo ndugu na Unguja kama ilivyo, imebakia salama, Unguja nayo, ishamiri amani. Kwao, Mapinduzi Daima ni Unguja tulivu, Pemba shauri yao.

Kwanza si kweli kuwa Pemba ina amani daima. Hatujasahau athari za siasa za fitina zilivyozama Pemba. Ni Pemba ambako watu wakidhalilishwa kwa sababu za kisiasa.

Wanawake walibakwa, t e n a b a a d h i m b e l e ya watoto zao. Familia zao z i k a n ya n g ’a n y wa m a l i kama mashada ya dhahabu baada ya watu waliodaiwa kutoka vikosi vya SMZ wakishirikiana na Janjaweed, kuvamia majumbani mwa wananchi wat i i fu kwa upinzani.

Ni Pemba ambako watu walikuwa hawaendeani kwenye misiba kwa kuwa

tu wanachagua upinzani. Ni Pemba ambako watu waovu wanaotumiwa na wanasiasa waovu walibeba vipolo vya vinyesi na kuvipakaza kwenye majengo ya serikali, skuli na vituo vya afya, lengo kusingizia wapinzani kuwa ni wao wametenda ili waswekwe gerezani.

P e m b a k a b l a y a maridhiano, kila kukifanyika u c h a g u z i u l i o i s h i a n a u c h a f u z i , w a t u w a k e walijiandaa kupigwa mijeledi kama vile chokora walio madarasani wakifundishwa alifu bee. Wakiita melody! Leo melody wapi?

Ni Pemba ambako kabla ya maridhiano, serikali iliyoundwa na viongozi k u t o k a C C M p e k e e , i l ikuwa ik iwadhulumu wamiliki wa karafuu haki ya kuuza watakavyo kwa kulazimishwa kuuza mali yao kwa bei ya dhulma.

Karafuu ikiuzwa kwa bei ya chini ya asilimia 20 ya bei halisi ya soko. Kutokana na siasa chafu, serikali iliamua kutumia mapato yaliyotokana na karafuu, kuijenga Unguja na kunenepesha viongozi wa kisiasa wa CCM.

P e m b a w a l i n y i m w a ajira waliostahili kupatiwa na walinyimwa nafasi ya kusonga mbele kielimu kwa waliokuwa na uwezo. Pale serikali ilipowafukuza wa n a f u n z i wa l i o k u wa wakiishi dakhalia zilizoko Unguja mwaka 1995, watoto wa familia za Wazanzibari waliotoka Pemba, ndio waliathirika zaidi.

Hawa walidai haki ya kupiga kura ili kuchagua v i o n g o z i w a w a t a k a o . Walikusanyika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) k u d a i w a a n d i k i s h w e ili wapige kura wakiwa Unguja wanakosoma na watakakokuwa wakati wa uchaguzi.

Pemba haikuwa salama kabla ya maridhiano. Ilikuwa s e h e m u a m b a y o wa t u waliishi kwa hofu. Watawala wa k i i t u m i a k u n e n e p a . Wapemba waliambiwa urais watausikia.

Dk. Shein anatoka Pemba. M s a i d i z i wa k e m m o j a Mpemba. Lakini baadhi ya hawajatulia. Wanataka Pemba na Unguja zitengane japo wanajua kihistoria na kijiografia, zi mamlaka moja.

Um ma u n a t a k a R a i s aongoze serikali kudhibiti wa t u h a wa b a d a l a ya kuwachekea kama watu wema. Ni kujidanganya kudhani yupo jini mwema. Hakuna popote ilipoelezwa jini ana huruma. Anayeamini ni mshirikina.

H a t u a s t a h i k i z i s i p o c h u k u l i w a , n i k u r u h u s u wa n a n c h i kuangamizwa, nchi yao kuharibiwa.

Page 5: An Nuur 1131

5 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari za Kimataifa

JAJI aliyetoa hukumu ya kunyongwa kwa Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, amekamatwa na kuhumiwa kifo na wapiganaji wa ISIS wa Iraq.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.lankasrinews.com mwaka 2006, Jaji Rauf Abdul Rahman (69), aliyetoa adhabu ya kifo kwa Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein, 16 mwaka huu alikamatwa na wapiganaji hao na baada ya siku mbili aliuliwa.

Wapiganaji hao wa Sunni hivi sasa wamekamata sehemu kubwa ya Iraq kuhu mapambano bado yakiendela kati yao na majeshiya serikali.

Jaji aliyemnyonga Saddam auliwaImeelezwa kuwa Jaji

huyo alikuwa akijaribu kuwatoroka wapiganaji hao, lakini jitihada zake zilishindwa na hatimaye alikamatwa na kuuliwa.

Katibu wa Saddam Hussein, aliyetajwa kwa jina la Ishad Ibrahim Al-noori, aliaandika ujumbe katika anuani yake ya mtandao wa Facebook na kwa mujibu wa ujumbe huo, mwaka 2006, Saddam Hussein alihukumiwa adhabu ya kifo na Jaji Rauf Abdul Rahman, kwa makosa ya kutumia silaha za sumu katika vita.

Alieleza katika mtandao huo kuwa, “Na sasa naye amekamatwa na wapiganaji wa I.S.I.S. Nao

wamemhumumu adhabu ya kifo”.

Kutokana na ujumbe huo wa Facebook, habari hizi zimefichuka lakini mpaka sasa serikali ya Iraq haijathibitisha rasmi kuuliwa kwa Jaji huyo, wala haijakanusha habari hizo.

H a t a h i v y o k u n a taarifa kwamba baadhi ya maofisa wa Serikali ya Waziri Mkuu Nuri Al Maliki, wamekiri kuwa vikosi vya wapiganaji dhidi ya serikali (ISIS) wamemtia mkononi Jaji Rauf Abdirrahmaan na kisha kumchinja.

Mwaka 2007 Jaji Rauf Abdul Rahman, ambaye ni mtu wa jamii ya Kurdish,

Jaji Rauf Abdul Rahman (kushoto) , Saddam Hussein (kulia)

Waasi wawatumia watoto vitani Syria

CAIROMahakama ya Mansoura katika jimbo la Nile Delta nchini Misri, imewahukumu wanachama wasiopungua 83 wa harakati ya Ikhwanul M u s l i m i i n a d h a b u ya kifungo cha maisha jela.

Mahakama hiyo imedai kuwa, watu hao walipatikana na makosa ya mauaji, kuzuia utekelezaji wa majukumu ya polisi na kufunga barabara za mji huo.

Taarifa ya Mahakama ya Mansoura imeeleza kuwa, wafuasi 83 wa Ikhwanul Muslimin wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela na wengine 62 wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu hadi kumi.

J u m a m o s i i l i y o p i t a mahakama moja katika mji wa Minya, Kusini mwa Misri ilitoa adhabu ya kifo kwa wafuasi 200 wa chama cha

baada ya kutoa hukumu kwa Saddam Hussein, a l i o m b a h i f a d h i y a ukimbizi wa kisiasa, kwa ajili yake na familia yake kwa serikali ya Uingereza.

I m e e l e z w a k u w a k i o n g o z i m m o j a wa kikabila anayetoka katika koo ya Saddam Hussein, aliwahakikishia wandishi wa habari kuwa Jaji Rauf, aliyewahi kutoa hukumu ya kunyongwa Saddam Hussein mwaka 2006 ameuliwa na vikosi vya wapiganji wa Kiislam nchini Iraq.

"16,Jun1 2014 nyakati za usiku wapiganaji walimtia m k o n o n i J a j i R a u f Abdirrahmaan, aliuawa nyakati za usiku alipojaribu kutoroka na mwisho wa kila aliyefanya mauji dhidi ya Waislam utakuwa ni mbaya", alisema kiongozi huyo wa kikabila Khaliil A'diyyah.

Gazeti la the Daily Mail la Uingereza lilinukuu vyanzo muhimu vya kuaminika na kudhibitisha kuuliwa Jaji huyo.

S a d d a m H u s s e i n al iyekuwa kiongozi wa Iraq kwa miaka mingi , alikamatwa na vikosi vya Marekani ilipofanya uvamizi nchini Iraq na kumkabidhi kwa serikali ya Iraq na kisha kumhukumu kifo, ambapo alinyongwa na kuonyeshwa tukio hilokatika vyombo vya habari katika sikukuu ya Waislam ya Eid, ambayo kwa kawaida inasherehekewa duniani kote.

Al Sisi aanza kuwashughulikia Ikwanul MuslimiinMamia wahukumiwa kifo, maisha Yumo Mohammad al Badie

Ikhwaanul Muslimin.Mohammad al Badie,

kiongozi mkuu wa harakati hiyo, ambaye yumo katika gereza moja lililopo nchini M i s r i c h i n i ya u l i n z i mkali, ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.

H u k u m u h i z o zimekosolewa na kupingwa vikali na Jumuiya za kimataifa na makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu.

Taari fa z imebainisha kwamba Kadhi Mkuu wa Mahakama nchini Misri tayari ametangaza uamuzi wa mwisho wa mahakama hiyo, utakaotekelezwa dhidi ya viongozi hao waliotuhumiwa kwa kile kilichotajwa katika M a h a k a m a h i y o k u wa

vitendo vya Kigaidi.V y o m b o v ya h a b a r i

nchini Misri vimeripoti k u w a f u n g w a h a o waliohukumiwa kunyongwa wamechambuliwa kutoka idadi ya watu 529 waliowahi kuhukumiwa kunyongwa hapo awali.

Baada ya Jumamosi , siku ya Jumatatu wiki hii, mahakama ya Misri ilitoa hukumu ya kuwafunga jela waandishi watatu wa habari wa televisheni ya Al-Jazeera.

Mahakama hiyo iliwakuta na hatia Siku ya Jumatatu, mahakama j i j in i Ca i ro iliwakuta waandishi Peter Greste, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed na makosa ya kusambaza taarifa za

uongo na kuwahukumu vifungo vya kati ya miaka 7 na 10 gerezani.

B w . G r e s t e a m b a y e n i r a i a wa Au s t r a l i a , amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuripoti habari za uongo pamoja na kushirikiana na kundi la Ikhwanul Muslimin, ambalo limewekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi nchini Misri.

Mohamed Fahmy pia alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela huku Baher akihukumiwa jela miaka kumi.

Waandishi wote watatu walikataa hukumu hiyo na wanatarajiwa kukata rufaa.

S e r i k a l i m b a l i m b a l i , mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari duniani vimelaani uamuzi wa mahakama hiyo.

uwezekano wa nchi yake kurudisha tena majeshi yake nchini Iraq, jambo ambalo linapingwa na wengi ndani na nje ya nchi hiyo.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba mapema mwezi huu, Rais Barack Obama wa Marekani, aliidhinisha kutumwa huko I raq mamia ya wanajeshi wa oparesheni maalumu ili kuisaidia Baghdad katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh.

Itakumbukwa kuwa chanzo cha kuvurugika hali nchini nchini Iraq, ni matokeo ya Marekani kuivamia nchi hiyo kwa kisingizio cha uongo, kwamba utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo marehemu Saddam H u s s e i n , u l i k u w a unamiliki silaha za sumu.

H a t a b a a d a y a wachunguzi wa silaha hizo kutoka Umoja wa Mataifa kuthibitisha kuwa hakuna silaha hizo, bado Marekani ilivamia nchi hiyo kimabavu.

Tangu wakati huo, hadi sasa, hali ya kisiasa katika Taifa hilo la Iraq haijatulia huku milipiko na mauaji yakiendelea kulianda taifa hilo hadi leo.

Sasa kumeibuka kundi la Waasi wa Daesh ambalo l inataka kuondolewa utawala wa sasa wa nchi hiyo.

Katika taarifa nyingine, Baghdad imedai kuwa haijaafiki kuwapatia kinga ya kutofikishwa mbele ya vyombo vya mahakama vya Iraq, wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo.

Serikali ya Iraq imepinga madai hayo baada ya ripoti kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kueleza kuwa, I r a q i m e i h a k i k i s h i a Washington kwamba, a s k a r i wa Ma r e k a n i h a w a t a k a b i l i w a n a uwezekano wa kushtakiwa katika mahakama za Iraq.

A f i s a m m o j a w a serikali ya Iraq ambaye h a k u t a k a j i n a l a k e litajwe katika vyombo vya habari ameongeza kuwa, kuwapatia kinga wanajeshi wa Marekani ni madai yasiyo na msingi wowote yaliyobuniwa na baadhi ya vyombo vya habari.

(irib.ir).

Inatoka Uk. 3

Page 6: An Nuur 1131

6 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari

VIKUNDI na vyama v y a k i r a i a v y a Kenya na Wabunge

wanataka kujiuzulu haraka au kufukuzwa kazi kwa maofisa waandamizi wa u s a l a m a k u t o k a n a n a kuongezeka kwa hali ya kukosekana usalama katika nchi.

Wabunge na Wanaharakati wametoa wito kwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali, Joseph ole Lenku, Katibu wake Mutea Iringo, Inspekta Mkuu wa Pol is i David Kimaiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Upelelezi la Taifa Michael Gichangi, kuwajibika wao binafsi na kujiuzulu na kwamba kama watakataa, wamesema Rais anapaswa kuingilia kati na kuwafukuza.

S h i n i k i z o h i l o l imeongezeka dhidi ya wakuu hao wa usalama kufuat ia shambul io la Juni 15-16 katika mji wa Mpeketoni na karibu na kijiji cha Poromoko katika Kaunti ya Lamu, ambapo kwa mujibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya lilisababisha watu zaidi ya 60 kufariki dunia na wakazi 800 kukosa makazi.

Licha ya hakikisho la serikali kwamba polisi zaidi watasambazwa katika eneo hilo, Chama cha Msalaba Mwekundu kilisema bado kuna wasiwasi mkubwa katika eneo hilo na wenyeji w a n a k i m b i a k u o g o p a mashambulio zaidi.

Eric Mutua, mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK), alisema kuendelea kwa matukio ya kukosekana kwa usalama kunakofanywa na vikundi v y a w a n a m g a m b o a u kama matokeo ya vurugu za kikabila, kulikuwa na dalili za kushindwa kwa uongozi ndani ya mamlaka za usalama.

Alisema shambulio la Mpeketoni, bila kujali nani alipanga na kutekeleza, l i n a o n y e s h a k w a m b a watumishi wa usalama siyo mahiri au hawana uwezo.

"Hii ndiyo sababu LSK inatoa wito wa kujiuzulu mara moja kwa Lenku, Iringo, Kimaiyo na Gichangi," Mutua aliuambia mtandao wa Sabahi.

K a t i k a t a a r i f a k w a vyombo vya habari Juni 17 Bw. Mutua alisema LSK inawapa Lenku na Kimaiyo wiki mbili kujiuzulu na kwamba, baada ya hapo LSK itaanzisha ama mchakato wa mahakama au katiba kwa ajili ya kuondolewa kwao katika nafasi hizo.

"Ongezeko la mashambulio lililoshuhudiwa katika miezi mitatu iliyopita ni ushahidi kwamba watu wawili ama hawakuwa na udhibiti wa hali ya usalama au ni watumishi wasiofaa," sehemu ya taarifa yao ilisema.

Mashambulizi mfulululizo KenyaWakuu wa usalama watakiwa kujiuzulu

MAITI za wananchi wa Kenya waliouliwa katika shambulio lililofanyika Mombasa hivi karibuni.

Na Rajab Ramah, Nairobi

K u n d i l a w a b u n g e lililoongozwa na Mbunge wa Mvita, Abdulswamad Nassir, walisema walikuwa wanapanga kuwasilisha hoja Bungeni kutaka kumshitaki Bw. Lenku na kuwapunguzia kazi Kimaiyo, Iringo na Gichangi.

"Siku ya Alhamisi (Juni 19) tulikutana na Rais na kumwambia kwamba maofisa hao wamezembea katika kazi zao na matokeo yamekuwa vifo visivyokwisha kwa Wak enya , " Bw. N ass i r aliiambia Sabahi.

Alisema wao wanatarajia R a i s a c h u k u e h a t u a lakini kama atashindwa, watawasilisha hoja yao na kuwafanya waondolewe n a k u o n g e z a k wa m b a alikuwa na matumaini hoja itapitishwa bungeni.

" W a k e n y a w a k i w a katika hali ya mgawanyiko wa kisiasa, wanateseka kutokana na mashambulio ya kigaidi, hivyo sitarajii wenzangu wataiangalia hoja hii kwa mitizamo ya Jubilee au CORD; ni hoja ya kuwaokoa Wakenya wote kutokana na kutofaa kwao," alisema Nassir, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Orange Democratic, ambacho kinahusiana na chama cha upinzani cha Coalition for Reforms and Democracy (CORD).

Aidha, Tume ya Taifa ya haki za Binadamu nchini Kenya (KNCHR), Tume ya Kimataifa ya Wanasheria nchini Kenya (ICJ) na Kituo cha Kimataifa cha Sera na Migogoro (ICPC), wametoa wito wa uchunguzi wa vifaa vya usalama.

Makamu mwenyekiti wa KNCHR, George Morara, alitoa wito kwa Rais Uhuru K e n ya t t a , k u m f u k u z a

Kimaiyo, Gichangi na Lenku kama njia ya kuchukua jukumu la kis iasa kwa makosa ya kiusalama.

"Wakenya wamekuwa wakishikiliwa mateka sio na magaidi tu, bali pia na makundi mengine ya wahalifu ambayo yanavamia katika miji yetu mikubwa pamoja na vijijini.

"Mambo yanaonekana kutuzidi nguvu sasa, lakini kuwahakikishia Wakenya haki zao kwa usalama, Rais anapaswa kuchukua hatua na kuwafukuza maofisa hao ili kuingiza mawazo mapya na nguvu katika namna ulinzi wetu unavyoendeshwa." Bw. Morara aliiambia Sabahi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ICPC Ndung'u Wainaina, alisema kushindwa kwa pol is i kuzuia shughuli za uhalifu kunaonyesha upungufu katika kukua kwa intelijensia.

Bw. Wainaina alisema

kama kungekuwa na mfumo mzuri wa kiinteli jensia, kusingekuwa na magenge na magaidi ambao wanapanga na kufanya mashambulizi kwa mafanikio.

Aliongeza kuwa ki la wakati wanaposhambuliwa, wanashtukizwa bi la ya kuwepo taarifa na kwamba, hiyo ni ishara kuwa mifumo ya serikali imeshindwa na inapaswa kuangaliwa kwa upya, kubadilishwa na viongozi wapya kupangwa upya kukabiliana na matukio ya uhalifu yasiyobadilika nchini humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ICJ Bw. George Kegoro, alisema serikali imeshindwa kuwahakikishia raia wake usalama na shirika lake l inapanga kuwas i l i sha waraka wake bungeni, kudai umma kudadisi kuhusu kutokuwepo kwa usalama.

A l i s e m a w a n a t a k a udadisi wa umma kukagua

vyanzo vya kutokuwepo kwa usalama, ufanisi wa maofisa katika kushughulikia usalama na kuchukuliwa hatua ili kukabiliana na kutokuwepo hali ya usalama.

Akijibu ukosoaji huo, B w . K i m a i y o a l i s e m a kutokuwepo kwa usalama hakupaswi kulaumiwa kwa jeshi la polisi lililopo.

" H u w e z i k u r u s h a lawama kwa maofisa wote, kuna wachache tu ambao wanazembea kazini lakini u m e o n a , t u m e c h u k u a hatua kwa maofisa ambao wanatakiwa." Alijitetea Bw. Kimaiyo.

Hata hivyo, Kimaiyo alikataa kujibu maswali ya iwapo atajiuzulu au la.

Bw. Lenku naye alitupilia mbali kukosolewa utendaji wake na LSK ak i sema kwamba, kikundi hicho k i m e m z u l i a u o n g o n a kwamba atalipeleka suala hilo kwa wanasheria.

Hata hivyo Iringo na Gichangi hawakupatikana kutoa maoni ju ya tuhuma za udhaifu wao kiutendaji, kiasi cha hali ya usalama kutoweka nchini humo.

W a k a t i W a b u n g e , wanasiasa wa vikundi vya kiraia vikilalamikia viongozi wa mamlaka za kiusalma kwa kushindwa kudhibiti machafuko, UN wamesema kuwa takriban watu 60 wameuliwa na wengine zaidi ya 75,000 kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na machafuko yaliyojiri katika maeneo ya Wajir na Mandera huko Kaskazini na Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Ripot i ya Umoja wa Mataifa (UN) imebainisha kuwa, mapigano ya kikabila kati ya makabila hasimu ya Degodia na Gare katika eneo la Wajir, yamelazimisha watu wasiopungua elfu sitini kuwa wakimbizi.

Maeneo ya Wajir, Mandera na Garissa yaliyopo Kaskazini Mashar ik i mwa Kenya yanayopakana na Somalia, mara kwa mara yamekuwa yakikabiliwa na mapigano ya kikabila na mashambulio y a n a y o t e k e l e z w a n a wanamgambo wa kundi la al Shabab la kutoka Somalia.

I K I WA n i w i k i m o j a imepita tangu watu sitini kuuawa huko Mpeketoni, watu wengine kumi na moja wameuawa katika shambulio jipya kwenye Kaunti ya Lamu ya Kenya, maofisa walisema Jumanne wiki hii.

Baadhi ya waathirika walikatwa na visu hadi kufa, wengine walipigwa risasi na kunyongwa hadi kufa bila huruma, mbinu ambazo zimetumika katika shambulio lililotangulia ambalo lilidaiwa kufanywa na al-Shabaab, AFP iliripoti.

Shambulio hilo lilifanyika usiku katika kijiji kidogo kilichopo karibu na mji wa Witu, kilometa 50 kuelekea maeneoya bara Magharibi mwa Lamu. Kiji j i hicho

Kumi na moja wauliwa katika mashambulio jipya Lamuk i n a r i p o t i wa k u wa n a mchanganyiko wa vikundi vya makabila ya Kenya.

Awali Mkuu wa Wilaya wa Kaunti ya Lamu Stephen Ikua alisema miili mitano ilipatikana, lakini chanzo cha polisi baadaye kilisema miili sita zaidi ilipatikiana na kufanya idadi kufikia kumi na moja.

"Tumewatuma maofisa wetu kwenda kwenye eneo hilo kupata taarifa zaidi... wako kat ika eneo hi lo kuwatafuta washambuliaji," alisema Bw. Ikua.

Diwani wa eneo hilo, Athaman Badi, al isema watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo na kupelekwa hospitali za karibu kupata matibabu.

"Mtindo wa kushambulia

ulikuwa sawa sawa na ule wa Mpeketoni, inaonekana kama lilifanywa na wanaume wale wale," alisema Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Benson Maisori.

Hata hivyo hakuna madai ya waliohusika na mauaji hayo yaliyopatikana mara moja.

Al-Shabaab ilidai kuhusika na shambulio la wiki iliyopita, i n g a wa j e R a i s U h u r u Kenyatta alisema ziliandaliwa na kuhamasishwa kisiasa na kufanywa na mitandao ya kisiasa ya ndani.

Tuhuma za Kenyatta zimezidisha wasiwasi wa upinzani wa kisiasa, ambao tayari upo baina ya serikali na vyama vya upinzani na kuibua hofu ya kuanza tena kwa mvutano wa kikabila.

Page 7: An Nuur 1131

7 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari

WA T A A L A M wa masuala ya kiuchumi nchini

Kenya wanaamini kuwa, kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi na mivutano ya kisiasa, kunaathiri v i b a y a u c h u m i n a maendeleo ya nchi hiyo.

Shirika la Habari la Xinhua limewanukuu wataalamu wa uchumi na wafanyakazi wa viwanda nchini Kenya wakisema k u w a , k u o n g e z e k a mivutano ya kisiasa na tishio la ugaidi nchini humo, ni chanzo cha kuharibika uchumi wa Kenya.

Bw. Bethwel Kinuthia, mtaalamu wa masuala ya uchumi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, ni mmoja wa weledi waliohojiwa na shirika hilo la habari ambapo alisema kuwa, mivutano kati ya vyama vya siasa inatia dosari uchumi wa nchi.

K a t i k a w i k i m b i l i zilizopita Kenya imekuwa ikishuhudia mivutano ya m a n e n o k a t i ya wanachama wa chama tawala ‘Jubilee’ na kile cha upinzani ‘CORD’, mivutano ambayo juu ya hali ya vurugu katika Taifa hilo.

Kambi ya upinzani inayoongozwa na Raila Odinga, aliyewahi kuwa

KINACHOENDELEA Iraq sasa ni machafuko

na mapigano ya kila siku. Vile vita vya Washia na Wassuni sasa ndio vimepamba moto, wakati Wassuni wanaendelea na mapambano Washia nao wanatoka majumbani kwao na kujitolea kuingia katika jeshi la serekali ili kupigana na Wassuni.

Haya yamepangwa y a t o k e e n a t a y a r i w a l i o p a n g a wameshafanikiwa na sasa wanajisifu na kuona ndio sasa wamefanikiwa, watu wanachinjana. Pengine pia inatafutwa sababu mpya ya kuingia tena Iraq kwa Waingereza na Marekani kwenda kufanya yao kama yale ya 2003.

Mwenyekiti wa the Christian Democratic U n i o n , G e r m a n y Volker Kauder, wakati a n a z u n g u m z a n a gazeti la Kijerumani la Hannoversche Allgemeine Zeitung today, alisema k u w a Wa m a r e k a n i , kutokana na uvamizi wao

Machafuko yaathiri uchumi wa Kenya

Raia wa kigeni wakiondoka nchini Kenya kufuatia machafuko yaliyoikumba nchi hiyo siku za hivi karibuni.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, anaitaka serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kukaa na wapinzani kwenye meza moja ya mazungumzo ya kitaifa, kwa lengo la kuikwamua nchi katika hatar i za k iusalama, ufisadi na kuongezeka kwa gharama za maisha nchini Kenya.

Katika hatua nyingine,

Marekani imezuia raia wake kusafiri kwenda K e n ya k u t o k a n a n a kuwepo hofu za kiusalama.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani , imewaonya Raia wake w a n a o t a k a k u s a f i r i kwenda nchini Kenya, kuahirisha kufanya hivyo kufuatia kushuhudiwa

kukidhir i machafuko nchini humo.

Marekani imesema wamepata taar i fa ya k i j a s u s i i n a y o l e n g a kushambulia maslahi ya Marekani, hivyo hakuna budi kuzuia wananchi wa k e w o t e k u s a f i r i kwenda nchini Kenya.

" K u t o k a n a n a mabadiliko ya kiusalama

y a l i y o p o n c h i n i K e n ya , i m e t u l a z i m u kuwahamisha wafanyakazi wa Ubalozi wetu hivyo tunawaonya raia wetu kutosafiri kwenda katika nchi hiyo", ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na Wizara ya Masuala ya Nje wa Marekani.

Mashirika ya Usalama wa Marekani wameonya uwezekano wa kutokea mashambulio kama lile la wiki uliopita kwenye mji wa Mpeketoni kisiwani Lamu, iliyowaua watu zaidi 70.

Miji ambayo Marekani imetoa onyo kali dhidi ya raia wake kusafiri kwenda, ni pamoja na Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu na Katika mkoa wa Tana River.

Upande mwingine , Wa z i r i w a M a m b o ya n d a n i wa K e n ya a m e w a t a h a d h a r i s h a wananchi wa Kenya, k u t o k w e n d a k w e n y e mikusanyiko hasa sehemu za kuangalia mechi za kandanda za fainali za kombe la dunia zinaoendelea nchini Barazil.

O n y o h i l o l a K e n ya limekuja ikiwa ni tahadhari ya kiusalama kutokana na kuwepo shaka ya kutokea mashambulio makubwa k a t i k a s i k u z a u s o n i , hususan katika sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu.

Blair, USA wamefanikiwa wanajisifu sasaNa Rashid Abdallah

TONY Blair.

wa awali Iraq, wanabeba jukumu lote juu ya hali inayoendelea Iraq.

Kila mtu anawalaumu m a h a s i d i h a w a w a Kimarekani hata wale wenzi wao, basi wanakiri kuwa Wamarekani ndio sababu ya kuichafua Iraq. Tumsikilize huyu naye ana maoni gani juu ya hili.

Meya wa jiji la London Boris Jonson anasema kuwa, Tony Blair (Waziri Mkuu wa zamani wa U i n g e r e z a ) m w i s h o a m e k u w a m w e n d a wazimu kwa kudai kuwa uvamizi wa mwaka 2003 kule Iraq sio sababu ya machafuko ya sasa.

Kabla ya Meya huyo kuyasema hayo Tony Blair amekuwa akishambuliwa s a n a k u t o k a n a n a k i n a c h o e n d e l e a I r a q sasa na wanaomlaumu wanasema kuwa yeye alikuwa ndio sababu ya yanayotokea sasa Iraq.

M t a n d a o w a T h e independent umeandika mengi, lakini ya muhimu ni kuwa Blair amekataa na kusema kuwa kama Marekani na Uingereza wangekataa kuivamia Iraq

na kumuondosha Saddam, basi Mashariki ya Kati ingekuwa mbaya zaidi ya sasa. Hiyo ni katika aya ya mwanzo lakini ninachokiona mimi hizi ni sifa huyu mtu anajisifu k u w a t u m e i h a r i b u Mashariki ya kati. Eti sehemu iliyokuwa salama halafu wao wakaichafua ndio anasema kama si kuichafua wao ingekuwa chafu zaidi. Huu ni ujinga mtu anaongea hizi ni sifa anajisifu kuwa tumeharibu sisi.

Kat ika aya ya p i l i anasema ni ajabu kuamini k u w a u v a m i z i w a Marekani ndio umeleta m a c h a f u k o ya s a s a . Jamani tuko pamoja? Munamuelewa Blair? Anajisifu kwa njia hizi yeye na kuongeza kuwa wao wameleta ukombozi kule Iraq.

Baada ya kuyasema hayo katika tovuti yake ndipo Johson naye mbaye kama tulivyosema awali n i Meya wa London katika Daily Telegraph Jonson anasema kuwa Blair na Bush ni wahalifu na waovu wanaostahiki

kuhukumiwa kwa uovu waliofanya Iraq.

Ni usia nzuri mno lakini usia kama huu u w e n d e k w a w a t u wenye akili na huruma sio kina Bush,Obama au Blair na wenzake, watakuona kama adui unayetaka kuwapokonya t o n g e m d o m o n i . Hawatokuelewa na wala hawatojali. Jonson sio wa mwanzo kuyasema kama haya wamepita wengi na wote wanayasema kama haya lakini kila uchao wa n y o n g e wa n a z i d i kunyongeka na kutiwa kwenye matatizo yasiyo ya lazima.

Wamefanikiwa na sasa wanajisifu na kujipongeza kwa mivinyo ya bei kali katika meza zao huku Wa i r a q wa k i e n d e l e a k u a n g a m i a . B l a i r anauwambia Ulimwengu kuwa wamefanya kazi nzuri mno Iraq na kama si wao basi Iraq ingekuwa pabaya zaidi. Ujinga hata hauingii akilini!

Ema : [email protected] 0773526254

Page 8: An Nuur 1131

8 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Makala

PROFESA Khadija Watson, alikuwa mwana Theologia,

Missionary, Mchungaji, Mkristo mhafidhina na kamwe hakuonekana kama angeweza kuwa muumini wa Kiislamu. Miaka sita iliyopita, katika maisha yake yote, alilelewa katika maisha ya Ukris to (awali kama muumini wa Roman Katoliki na baadae Mlokole). Alihitimu stashahada ya uhubiri (Standard Ministerial Diploma), shahada ya Theology na shahada ya uzamili ya Divinity.

Lakini pamoja na hayo yote, hatimaye aligeukia Uislamu na kusilimu! Ni jambo gani lililomfanya Prof. Khadija kufanya

Alivyosilimu Prof. Khadija Watson-2

Na Khadija Watson m a b a d i l i k o h a y o yaliyowashtua wengi, i k i l i n g a n i s h w a n a msimamo na elimu ya Ukristo aliyokuwa nayo?

W i k i i l i y o p i t a tulisimulia sehemu ya kisa cha kusilimu Prof. Khadija Watson. Katika makala hii tunamalizia sehemu ya mwisho . Endelea…

KI L A k i t u n i l i c h o j i f u n z a kuhusu Uislamu

wakati nasoma shahada ya n g u ya u z a m i l i , kilifutwa katika darsa za Kiislamu nilizokuwa n a h u d h u r i a . K a m a Mkristo, hatukufahamu k wa m b a Wa i s l a m u wanaamini kuhusu kuzal iwa Yesu bi la ya baba. Hatukufikiri kabisa kama wanaweza k u m w a m i n i Ye s u . N i l i s h t u k a z a i d i kufahamu kwamba

Waislamu wanaamini kuwa Yesu amepaa mbinguni na atarejea tena!

M a r i a , ma ma wa Yesu ana sura nzima katika Quran Tukufu na ikapewa jina lake. B a d o W a i s l a m u h a w a m u a b u d u kama wanavyofanya W a k a t o l i k i n a Protestanti. Biblia ina sehemu ndogo sana iliyomuelezea Maria wakati Qur’an Surah Maryam ni sura nzima kuhusu mama wa Yesu.

Niliporea nyumbani n i l i j iu l iza maswal i mengi kuhusu yale niliyojifunza darasani. Ukristo ulizua maswali mengi akilini mwangu, lakini Uislamu ulinipa m a j i b u . K i l a s i k u nilihudhuria mhadhara na kila siku nilisoma Biblia na kila usiku n i l i o m b a M u n g u , anionyeshe kama huu Uislamu ni dini ya kweli. Wakati mwingine nilisita kusema Jesus, nilisimama kusema roho mtakatifu, nisimama k u s e m a “ b a b a ” . Nilikuwa sema Mungu ( V y o v y o t e u l i v y o ) nionyeshe kama hii ni kweli.

Sio rahisi kubadili dini yako. Sikutaka kupoteza uokovu wangu, lakini n i n i c h a k u p o t e z a kama hakuna uokovu nitakaopoteza?

Usiku mmoja katika miezi miwili tangu mara ya kwanza nilipoanza k we n d a k i t u o c h a Kiislamu, nilisali sala hii kama nilivyokuwa nafanya na kwenda kulala.

Wakati fulani katika hali ya kuzinduka na kulala, nilijisikia kitu fulani ndani ya moyo wangu. Nilikaa ghafla kitandani na kusema kwa nguvu:

"Allah, ninaamini kuwa wewe ni Mungu m m o j a n a M u n g u mmoja pekee”.

Hii i l ikuwa mara y a n g u y a k w a n z a kutumia j ina Allah. Ingawa nilisikia wengine wakilitumia, mwenyewe

sikuwahi kulitaja hadi siku hiyo. Baada ya kusema hivyo, nilipata amani . Alhumdulillah haikunikosa hadi leo.

U a m u z i w a n g u h a u k u n i a c h a b i l a m a l i p o . Wa k r i s t o ambao wamethibitisha kumpenda Yesu na a m b a o n i w e p e s i kuwashutumu wengine k w a k u w a a d h i b u wengine wanaojiunga na Ukristo, walikuwa wa kwanza kuniadhibu. Iko wazi, mara moja ajira yangu ya kufundisha v y u o v ya K i k r i s t o ilisitishwa.

Unaweza kuwa na Mkristo anafundisha k u h u s u U i s l a m u , lakini huwezi kuwa na Muislamu anafundisha kuhusu Ukristo. Tayari nimekuwa mjane kwa miaka saba wakat i nilipokuwa Muislamu

H i i i n a m a a n a ninajisaidia mwenyewe. Bado nina watoto watatu ambao nina majukumu kwao kati ya watoto tisa. Jambo jingine ambalo l imej ir i ni kwamba f a m i l i a y a m u m e wangu imenitenga. Mume wangu anatoka katika familia maarufu. Babu yake yupo katika vitabu vya historia aki tambul ika kama shujaa, na baba yake wakati fulani alikuwa Gavana.

Ingawa wote watatu walishafariki, nilikuwa na mahusiano ya karibu sana na familia yake, sana kiasi kwamba nilikuwa karibu nao kuliko hata familia yangu.

Baada ya kusilimu, niliambiwa mimi sio sehemu ya familia na siruhusiwi kujumuika katika hafla yeyote ya kifamilia. Kuna baadhi ya wanafamilia bado wapo katika medani ya siasa, hivyo hawawezi kuwa na Muislamu kat ika famil ia yao. Niliumizwa sana na hili hasa ikizingatiwa kwa miaka mingi nimekuwa nao karibu. Si kwasabau ya misingi ya Ukristo wangu, bali kwa sababu

nilikuwa sehemu ya familia. Mume wangu alipofariki, familia yake iliwajibika kusadia kulea watoto wangu, sasa ndio wamenitupa. Nililia kwa siku tatu, lakini kila niliposwali nilipata amani kwa kutambua kuwa nilifanya uamuzi sahihi.

Hivi sasa watoto w a n g u i s i p o k u w a kijana wangu ninayeishi naye, wapo Marekani. Nilipokuwa naenda I s l a m i c C e n t r e , n i l i w a s i l i a n a n a o kwa barua kuhusu nilichojifunza.

B a a d a y a k u w a Muislamu binti yangu m k u b w a ( a m b a y e a l i k u w a a k i f a n y a kazi makao makuu ya Kanisa nililokuwa nashughulika nalo kwa miaka 18) aliniandikia b a r u a n a k u s e m a , "Hujui kuwa Uislamu ni moja ya dini kuu za kishetani?" Nilimjibu k w a k u m t u m i a vijitabu, naye alijibu na kusema, "DON'T TRY TO CONVERT ME!" (Usijaribu kunibadili dini).

Nilimweleza kuwa t u m e k a t a z w a n a M w e n y e z i M u n g u k u m l a z i m i s h a m t u yeyote kuingia katika d in i , lak in i n i l i jua a n a w e z a k u h i t a j i kusoma kuona nini ninachokiamini.

K a m a m z a z i , u n a p o k u m b a n a n a matatizo na mtoto wako aliye mbali, mara nyingi unaitisha mkutano na ndugu wa karibu, (bibi, shangazi , mjomba) ambao wanaweza kuwa na athari katika hali ya tatizo lililopo.

Baadae niligundua k u w a w a n a n g u walikuwa na mkutano juu yangu! Mama ni tatizo na Uislamu ndio tatizo lenyewe! Kama ilivyo kwa familia nyingi kubwa, kulikuwa na mgawanyiko miongoni mwa watoto. Wakubwa watatu ni mabosi, watatu wa katikati wapambanaji na wadogo hawana

Inaendelea Uk. 9

MMOJA wa mama wa Kizungu aliyesilimu akiwa na vazi lake la Hijab.

Page 9: An Nuur 1131

9 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Makala

Alivyosilimu Prof. Khadija Watson-2Inatoka Uk. 8ubavu wa kusema. Wakati majadil iano yakipamba moto, watoto mkubwa walipinga hali yote, wale wa katikati walisema, "Huyu ni mama yetu na ni uamuzi wake. Hakutulazimisha kumfuata. Tunataka k u wa k a r i b u ya k e na tunamtaka yeye pia kuwa karibu na wanawake."

Baadae nilipokwenda M a r e k a n i , w a l e wakubwa waliweka ukuta wa kufanyika majadiliano yoyote. Upande mwingine wale wa katikati walikuwa na maswal i mengi . Hata hivyo, hatimaye majadiliano yaliendelea na kuwa ya mafanikio na maana na yalikuwa ya kawaida. Binti mmoja a l id i r i kutoa kaul i kuwa nimekuwa mama mzuri zaidi baada ya kuwa Muislamu kuliko nilivyokuwa Mkristo. Hili lilinishtua kwa sababu ni l ipokuwa M k r i s t o s i k u z o t e nilijaribu kuonyesha kile nilichokiamini.

Nilipokuwa Marekani niliendelea kuvaa abaya (hijab). Ndugu yake naye akatoa kauli nyingine. Alisema ataeleza namna wanaume wa Kiislamu wanavyomtizama mama yao wanapotembea mitaani. Nilipata hamu y a k u j u a k w a n i n i a l i k u j a n a k a u l i h i y o n a a m e wa j u a wanaume wa Kiislamu wanaomtizama wakati wanaume hao hawavai chochote kuwaonyesha w a o n i Wa i s l a m u (na wala wengi wao hawafugi ndevu).

A l i n i a m b i a , "Wanapokutizama, ni tofauti. Wanakutizama kwa heshima."

Baada ya miaka sita wanangu wakubwa wa kike hatimaye walikiri kuwa mimi ni Muislamu kwa uwezo wa Allah na s i tare jea kat ika

Ukristo na waliheshimu. Wengine walisema kuwa wanauona Uislamu ni njia ya maisha tofauti na Ukristo ambako huenda Kanisani na baadae kuendelea kufanya jambo lolote unalotaka. Kwa maneno mengine, U i s l a m u u n a t a k a mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Mwanangu wa kiume, ambaye nilikuwa naishi naye wakati naingia katika Uislamu, hakuwa anafuata imani ya dini yeyote wakati huo. Alikuwa na umri wa miaka 18 na dini haikuwa n a m a a n a k a t i k a maisha yake. Wakati mwingine nilipokuwa n i m e p o t e z a n a f a s i yangu ya kufundisha, niliombwa kuanzisha na kuendesha kitengo cha wanawake katika kituo cha Kiislamu. Kila wiki nilileta nyumbani vitabu na kuviweka mezani na kila siku viliendelea kuwepo pale kama vilivyo.

Wakat i mwingine nilivibadilisha nikitarajia angevisoma na kuniuliza

baadhi ya maswali . Hakuwahi kufanya hivyo. Mwaka ule , mara kadhaa niliwaleta rafiki zangu kutoka kituo cha Kiislamu na kuzungumza naye. Mara zote alikuwa mpole,

l a k i n i a k i o n e k a n a hayuko tayari. Siku moja nilizungumza naye na alionyesha hali ya kushawishika katika sura yake. Aliniuliza, "kwanini hukunieleza haya?" Nilishtuka na kumjibu kuwa nilikuwa naacha vitabu pale m e z a n i , n i k i t a r a j i kuwa angevisoma na kuniuliza maswali.

Baadae akaniambia nikiondoka nyumbani, yeye na rafiki zake w a t a v i s o m a n a kuvirejesha. Pia nilikuwa na saa yenye adhana (mwito wa swala) na aliniambia nilipokuwa sipo na kubaki peke yake, alikuwa akiichezea mara kwa mara i l i kusikia ile sauti.

Sasa hivi jina lake ni Omar. Yeye na rafiki zake waliachana na staili zao za zamani za maisha na hivi sasa anafanya kazi Saudi Arabia. Alifanikiwa zaidi kuliko mimi katika kuzungumza na dada zake wakubwa juu ya Uislamu. Kabla ya hapo, hakuna hata mmoja

katika familia alikuwa a k i f u a t a U i s l a m u . Lakini tunaendelea k u w a o m b e a d u a . Insha'Allah, Nitafurahi kuona kwa kiasi fulani sehemu kubwa ya watoto wangu na wajukuu w o t e w a n a k u w a Waislamu. Sikuwahi kujuta kuwa Muislamu n a n i n a m w o m b a M w e n y e z i M u n g u anipe imani kama ile ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w).

Sema: Hakika Bwana wangu ameniongoza katika njia iliyonyooka (dini ya kweli) njia ya Abraham, inayoegemea ukweli . Na hakuwa miongoni mwa wale w a n a o m s h i r i k i s h a Mwenyezi Mungu.

Sema: Hakika, sala yangu, sadaka yangu, uhai wangu na hatima yangu ni kwa ajili ya M we n ye z i M u n g u , muumba wa mbingu na ardhi. Hana mshirika. N a h a y a n d i y o niliyoamrishwa. Na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha (kwa M we n ye z i M u n g u ) (Surah Al-An'am: 161-16)

Prof. Khadija Watson.

Yvonne Ridley.

Page 10: An Nuur 1131

10 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014MAKALA/TANGAZO

SH U K R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi Mungu kwa kutuletea

tena Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao ni fursa nyingine kwetu kutafuta radhi na msamaha wake. H u u n i m we z i a m b a o tunapambana na silika na matamanio yetu. Ni

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGE

MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014 / 2015

Wafuatao wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti kwa Chuo cha Ualimu Kirinjiko Islamic Teachers’ College mwaka wa masomo 2014 / 2015.

MUHIMU• Maelekezo ya kujiunga na Chuo yanapatikana Kirinjiko

Islamic Teachers’ College (Same), Ubungo Islamic Teachers’ College (Dar es Salaam) na Nyasaka Islamic Secondary School (Mwanza).

• Usaili wa mara ya pili kwa wale waliochelewa kuchukua fomu utafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 19/07/2014 katika vituo vya:- Kirinjiko Islamic Teachers’ College (Same), Ubungo Islamic Teachers’ College (Dar es Salaam) na Nyasaka Islamic Secondary School (Mwanza) Inshaallah.

• Fomu zinaendelea kutolewa na zinapatikana kwa mawakala wetu kote nchini.

• Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkuu wa Chuo kwa simu namba 0787 188964 au 0657 705878.

Wabillah TawfiiqMKUU WA CHUO

Ramadhan ya Mtume - mwezi wa mapambano!Said Rajab mwezi ambao Waislamu

wanajipinda kutoka kwenye matamanio yao ya msingi na kujikurubisha zaidi kwa Muumba.

Muislamu anaidhibiti nafsi yake na vitu ambavyo inavipenda sana - chakula, v i n y w a j i , j i m a i n a vinginevyo. Anajizuia na furaha inayotokana na vitu hivyo ili apate furaha kubwa

zaidi - mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo hayo ya siku thelathini yamebuniwa kitaalamu, ili kumuweka binadamu katika daraja ya juu zaidi kiroho. Hii ndiyo maana ya taqwa ambayo Mwenyezi Mungu ameitaja kwenye Surah Baqarah:

" E n y i m l i o a m i n i Mmelazimishwa kufunga kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu" Qur(2:183).

Mwezi wa Ramadhan unatuonyesha sisi ni nani kama wanadamu. Ni binadamu tu ndiye mwenye uwezo wa kujinyima matamanio na silika yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hilo ndilo linalomtofautisha binadamu na mnyama. Silika zetu za kiroho zinapaswa kuwa juu ya silika za kivitu (material). Hii inatukurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kututofautisha na wanyama.

Kwa bahati mbaya, tunaishi kat ika ul imwengu leo , ambapo binadamu amekuwa mtumwa wa matamanio yake na silika. Hiyo ndiyo maana halisi ya kuishi kwenye ulimwengu unaodhibitiwa na mabeberu. Israfu ya vyakula, ngono, fedha na starehe ndiyo malengo ya maisha dunia nzima leo. Hayo yanawasilishwa kwetu kama mafanikio kat ika maisha. Kila mtu anatafuta hayo katika maisha. Hadhi ya binadamu imeshushwa na kufikia kiwango cha wanyama ulimwenguni leo.

Na hii ndiyo imesababisha fitna kubwa duniani, ambapo watu tofauti na mataifa tofauti, wanapambana vikali kudumisha matamanio yao ya kivitu (material desires). Uislamu kama Itikadi, umekuja kumuinua binadamu kutoka kwenye utumwa huo na mashindano, na kumuweka katika ngazi ya juu kabisa. Hiyo ndiyo thamani halisi ya kufunga na umuhimu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Ramadhan siyo tu mwezi wa kujinyima kula na kunywa. Ni mwezi wa mafunzo ambao unapaswa kumkomboa binadamu kutoka kwenye utumwa wa kupenda vitu, na kumuwezesha kudhibiti matamanio yake katika kiwango ambacho kitaleta amani na maelewano katika jamii za wanadamu. Hicho n d i c h o t u n a c h o p a s wa kuvuna katika mwezi huu wa mapambano dhidi ya nafsi zetu.

Mamilioni ya Waislamu dunia nzima wanapofunga mfungo wa Ramadhan, wanajionyesha ulimwenguni kwamba wao ni umma m m o j a , n a h a d h i ya o kama wanadamu, ambao wa m e j i k o m b o a k u t o k a k w e n y e u t u m w a w a matamanio ya nafsi, na kuelekea kwenye utumwa wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Lakini Ramadhan siyo tu ni mwezi wa kupambana na nafsi zetu. Vile vile ni mwezi

wetu wa kufanya tathmini ya mapambano mapana zaidi, ambayo yanaendelea katika ulimwengu tunaoishi. R a m a d h a n n i m w e z i ambao Mwenyezi Mungu ameiteremsha Qur'an Al - Kareem:

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wa z i z a u w o n g o f u n a upambanuzi" Qur(2:185)

Tangu mwanzo wake, hii Qur'an imekuja kama changamoto kwa mifumo mingine yote ya maisha hapa ulimwenguni. Qur'an haikuja ili isomwe tu na kupendezesha misikit i . Na wala haikuletwa i l i kukamilisha usomaji wa Juzuu thelathini katika siku 30 za Ramadhan - ingawa kufanya hivyo, bila shaka ni jambo jema linaloleta thawabu.

Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, ameiteremsha hii Qur'an kama Muongozo (Huda) na Kipambanuzi (Furqan) kwa wanadamu. M w e n y e z i M u n g u ametubainishia wazi kupitia Qur'an, jinsi ya kutofautisha Haki na Batili, Wema na Uovu, jinsi ya kuridhisha matamanio yetu na silika, na jinsi ya kuendesha masuala yetu ya kijamii na umma. Qur'an iliteremshwa kama muongozo wa kila kipengele cha maisha ya binadamu. Qur'an hii iliteremshwa mwezi wa Ramadhan kama rehema kwa wanadamu.

Masahaba walipokea A y a z a Q u r ' a n m j i n i Makkah wakati zilipokuwa zikishushwa na wakajipanga kupambana dhidi ya maadili yote, vigezo, sheria na mifumo iliyowekwa kutokana na ukafiri. Waliingia katika mapambano makal i ya kifikra dhidi ya mawazo na mitazamo yote potofu. Baada ya kupata ukweli wa Aya za Qur'an, hawakuishia kusoma tu na kubaki na fikra za Qur'an wao wenyewe.

N g u v u y a f i k r a z a Kiislamu, iliwalazimisha masahaba kushiriki kwenye j ami i i l iy owazu ng u k a , ambayo ilijengwa juu ya fikra na mawazo potofu ya kikafiri. Qur'an imeonyesha njia ya kitaaluma ya kuondoa mawazo potofu kwenye jamii. Mwenyezi Mungu amebainisha ndani ya Qur'an:

"Je? Wameumbwa pasipo kitu, au wao wenyewe ndiyo waliojiumba. Au wameumba mbingu na ardhi? Bal i hawana yakini (ya jambo lolote)"Qur(35:36).

"Na mali yake hayatamfaa atakapokuwa anadidimia (motoni humo) Qur(92:11).

" M a a n g a m i z o y a t a w a t h u b u t u k i a wapun jao (wenziwao) . Ambao wanapo j ip imia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani au (vinginevyo), wao hupunguza. Je! Wao hawaf ik i r i ya kwamba watafufuliwa. Katika siku iliyo kuu-" Qur (92:1-5)

"Wala hii si kauli ya Shetani aliyefukuzwa (katika rehema za Mwenyezi Mungu). Basi mnakwenda wapi? Haikuwa hii Qur'an ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote" Qur(81:25-27).

Leo hii mapambano kama hayo bado yanaendelea. Uislamu unashambuliwa na kudhalilishwa kila kona ya dunia. Fikra za Kiislamu zinaonyeshwa kuwa ni za kale na zilizopitwa na wakati. U is lamu unaonyeshwa kuwa ni dini ya kinyama na katili. Zaidi ya miaka 1400 iliyopita, Maquraysh walisambaza uongo dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakimkejeli na kumdhalilisha.

Mashambulizi kama hayo bado yanaendelea mpaka leo. Ukafiri hauna silaha nyingine dhidi ya Uislamu zaidi ya uongo na propaganda mbuzi! Lengo lao ni kuwatia mashaka watu kuhusu Uislamu, ili waendeleze dhulma na ubeberu wao. Wanataka Uislamu ubadilike na kufanyiwa 'mageuzi' ili ulingane na usekula wa kimagharibi.

Mapambano haya bado yangalipo kama yalivyokuwa wakati wa kipindi cha Mtume wa M we n ye z i M u n g u . Waislamu leo hawawezi kupuuza mapambano haya kwa kisingizio chochote kile. Kwa hakika tuna wajibu wa kukabiliana na changamoto hizi na kuiga njia ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliifuata katika kukabiliana na mashambulizi hayo ya propaganda.

Waislamu leo wanahitaji kuongozwa na Qur'an na kujenga uwezo wa kufikiri unaotokana na Qur'an, kama Waislamu wa awali walivyoweza kuondoa hoja za kijinga za Maquraysh. Tunahitaji kufuata muongozo wa Qur'an na kubainisha mgongano na unafiki uliopo kwenye mifumo ya kisekula, ili kufungua fikra za watu na kuwafanya wafikiri sawa sawa.

Dunia leo inateseka sana kutokana na Ubeberu . Familia zinasambaratika, ndoa zinavunjika, ukatili u m e o n g e z e k a , wa t o t o wanadhalilishwa, picha za ngono kila mahali, ubakaji, utapeli, kunyanyasa wazee na madawa ya kulevya, yote hayo ni matunda ya Ubeberu, ambao umejengwa juu ya msingi wa kupenda vitu (materialism), uchoyo na kusaka starehe kwa gharama yoyote.

Kat ika umasikini wa u l i m w e n g u w a t a t u , tunashuhudia utapiamlo, magonjwa, majanga ya kimazingira na vita vya wenyewe kwa wenyewe, vinavyolenga kuzivuruga

Inaendelea Uk. 14

JINA KAMILI MKOA ANAOTOKA1 ABAS OMARY KISOMA ME DAR ES SALAAM2 AMIRI I. TEMBA ME KILIMANJARO3 HATIBU ZAHABU ME TANGA4 IBRAHIMU E. SAIDI ME KILIMANJARO5 IDDY MOHAMED MUSSA ME DODOMA6 ISSA H. MNYONE ME KILIMANJARO7 JUMA WALII MFINANGA ME KILIMANJARO8 MASELI OMARI TAO ME KILIMANJARO9 MOHAMED N. ABDALLAH ME TANGA10 RASHID ALLY RASHID ME KILIMANJARO11 SHABANI MAULIDY MANGULA ME NJOMBE12 YASSIR HASSAN MSHIHIRI ME TANGA13 AMAN HAKIM ME MWANZA14 AISHA KIPINGU IMAMU KE TANGA15 ASHA SHEMKAY KE TANGA16 FADHILA LUKINDO KE TANGA17 FATMA JUMANNE MAYOGHO KE SINGIDA18 HADIJA I. MKUMBWA KE DAR ES SALAAM19 HALIMA ABDUL JUMA KE MOROGORO20 HAMIDA R. SUDI KE DAR ES SALAAM21 HAWA AMANI MFINANGA KE KILIMANJARO22 MARIAMU MSECHU KACHEMA KE KILIMANJARO23 MWAJUMA S. SALEHE KE TANGA24 MWAMINIE A. HASHIMU KE DAR ES SALAAM25 MWANAIDI ABASI MSANGI KE DAR ES SALAAM26 MWANAMKASI BAKARI MNYIKA KE TANGA27 NAYMA J. ALLY KE TANGA28 RAFIA HAJI KIMARO KE KILIMANJARO29 SAMILA KATAKWEBA KE MOROGORO30 SAUDA K. SAIDI KE KILIMANJARO31 SAUMU SAIDI NGOI KE SINGIDA32 SHIDA J. HASANI KE DAR ES SALAAM33 TATU ALLY KE TANGA34 ZAINABU T. ISSA KE DAR ES SALAAM

HADIJA HUSSEIN KONDO KE MWANZA36 MWAMINI JUMANNE KE MWANZA

Page 11: An Nuur 1131

11 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Makala/Tangazo

Uongozi wa Jukwaa la Vijana wa Kiislamu Tanzania unawaalika vijana wote wa Kiislamu kuhudhuria ufunguzi wa semina ya uongozi wa Jukwaa la Vijana Ijumaa (leo) 27/06/2014 itakayofanyika mara baada ya swala ya Alasir katika Misikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Saalam.

Nyote mnakaribishwa

Kwa mawasiliano zaidi piga kwa: Katibu 0713 495962

SEMINA YA UONGOZI WA JUKWAA LA VIJANA WA KIISLAMU

MS A F A R A w a wafanyabiashara u l i o k u w a

u k i e l e k e a M i s r i ulipumzika katika kisima kile na ukamgundua kijana mzuri wa kiume akiwa chini ya kisima hicho. Wafanyabiashara hao wakamuokoa Yusuph (as), na wakampeleka u t u m wa n i M i s r i n a kumuuza kwa Waziri Mkuu. Kwa muda mfupi sana, Waziri Mkuu wa Misri alitambua kwamba mtumwa Yusuph (as), hakuwa mtu wa kawaida na alikuwa na hazina k u b wa n d a n i ya k e . Kwa hiyo akamuagiza mke wake, Zulekha, kumtendea wema Yusuph ( a s ) n a k u m u we k e a mazingira mazuri. Bila shaka, huo ulikuwa ni mpango wa Mwenyezi Mungu, kama mwenyewe anavyobainisha:

" N a k a m a h i v y o , t u l i m m a k i n i s h a (tulimkalisha) Yusufu katika nchi ya Misri kwa raha, ili kumfundisha hakika ya (kila) maneno. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kushinda juu ya jambo lake lakini watu wengi hawajui" Qur(12:21).

M w e n y e z i M u n g u a l i t a k a k u m u o n d o a Yusuph (as) kutoka kwenye nchi yake ya Kaanan (eneo la Palestina, Syria na Jordan), na kumpeleka Misri kwa mustakabali mkubwa zaidi wa maisha yake. Mwenyezi Mungu M t u k u f u a l i w a a c h a ndugu zake Yusuph (as) wamfanyie ubaya, ikiwa ni sehemu ya mpango wake mkubwa zaidi.

Yusuph (as) atupwa gerezani: Kisa cha Yusuph (as) katika hatua hii , kinachukua mwelekeo mwingine mgumu, wakati mke wa Waziri Mkuu wa Misri, Zulekha, alipojaribu kumtaka k imapenz i . Kwa kuwa Yusuph (as) hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa ni mwanaume mzuri anayevutia mno. M w e n y e z i M u n g u a n a t u a r i f u k w a m b a wakati wanawake wa M i s r i wa l i p o m u o n a Yusuph (as), walisema: "Hasha Lillahi!", "Huyu si Mwanadamu; hakuwa huyu i la n i mala ika mtukufu" Qur(12:31).

Sitaingia ndani sana katika maisha ya Yusuph (as) kwenye hatua hii, ili kufupisha urefu wa kisa hiki. Ufupi wa maneno, Yusuph (as) alikabiliwa na mtihani mwingine mzito na kwa msaada

Kisa cha Nabii Yusuph - Lengo na umuhimu wake leo-2Yusuph (as) apelekwa Misri Said Rajab.

wa Mwenyezi Mungu a l i faulu . Ul ikuwa ni mpango wa Mwenyezi Mungu Yusuph aende gerezani, ili kumnusuru kutokana na uovu wa wanawake wale wenye tamaa za mwili!

Wakati akiwa gerezani, hadithi ya Yusuph (as) inaingia kwenye awamu yake ya tatu ya mitihani, a m b a p o a n a e n d e l e a na dhamira yake ya kitume ya Da'awah kwa wa f u n g wa we n z a k e . Yusuph (as) alikaa jela kwa miaka kadhaa kwa kosa ambalo hakulitenda. Hata hivyo, kulikuwa na hekima kubwa nyuma ya Yusuph (as) kukaa gerezani, ambayo baadaye ilibainishwa na Mwenyezi Mungu, Mbora wa wote wenye kupanga.

Ndoto ya mfalme wa Misri: Mfalme wa Misri aliota ndoto ya kutisha ambayo ilimfanya awe na hofu na ufalme wake. Alijitahidi sana kupata tafsiri sahihi ya ndoto ile bila mafanikio.Washauri wake wazito, wachawi, wapiga ramli na waganga wote walishindwa kutafsiri ndoto ile kwa usahihi. Hapo ndipo mtumishi mmoja nyumbani kwa mfalme alipomkumbuka Yusuph (as) na uwezo wake wa kutafsiri ndoto.

Mtumishi huyu alikuwa pamoja na Yusuph (as) gerezani na alinufaika na tafsiri ya ndoto yake iliyofanywa na Yusuph (as). Maafisa wa mfalme wakamsimulia Yusuph (as) kuhusu ndoto ya mfalme gerezani na akawaambia kwamba Misri itakabiliwa na miaka saba ya neema, itakayofuatiwa na miaka saba ya ukame. Yusuph (as) akamshauri mfalme kwamba katika miaka hiyo migumu ijayo, ni muhimu sana kusimamia vyema rasilimali za nchi na ugawaji wake.

Yusuph (as) alibainisha kwamba baada ya miaka hiyo 14, neema itarejea tena Misri na rasilimali z i t a k u wa n y i n g i z a kutosha kama zamani. Mfalme alipopata tafsiri hiyo alitulia na akaridhika. Mfalme alitambua uwezo wa Yusuph (as), elimu yake na maono yake ya mbali. Haraka sana akaamrisha Yusuph (as) atolewe gerezani. Hata hivyo, Yusuph (as) alikataa kuondoka gerezani mpaka jina lake litakaposafishwa n a i t a n g a z w e k u wa hakuwa na hatia.

Kwa hiyo uchunguzi wa

Yusuph (as) ukafanyika kwa amri ya mfalme, na haraka sana tuhuma zilizoletwa na Zulekha dhidi ya Yusuph (as) z ikabainika kuwa ni uongo. Mfalme, akitambua ukubwa na utukufu wa Yusuph (as), akaagiza a a c h i w e h u r u m a r a moja. Mwenyezi Mungu anasema:

Basi Mfalme akasema: " M l e t e n i k w a n g u , n imchague awe mtu w a n g u m w e n y e w e " B a s i a l i p o z u n g u m z a naye (mfalme) alisema, "Hakika wewe leo kwetu umeshakuwa ni mwenye heshima na muaminiwa" Qur(12:54)

Yusuph (as) alimuomba mfalme amteue kuwa Wazir i wa Fedha wa Misri, ambaye anasimamia u c h u m i , i l i a w e z e kutimiza vizuri jukumu la kusimamia mavuno, maghala na ugawaji wa rasilimali kwa ufanisi. Mfalme alikubali bila ya kipingamizi kwa sababu Yusuph (as) ndiye hasa al iyekuwa na sifa ya kufanya kazi ile.

Kwa hiyo, mpango wa Mwenyezi Mungu kumpaisha Yusuph (as) na kumfanya kigogo anayeheshimika Misri, ulizaa matunda baada ya miaka mingi ya subira na uvumi l ivu mbele ya mitihani migumu. M w e n y e z i M u n g u anasema:

" B a s i n a m n a h i v i t u k a m p a Y u s u f u cheo katika nchi hiyo (Misri); anakaa humo p o p o t e a n a p o p e n d a . Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala h a t u p u u z i m a l i p o ya wa f a n ya o m e m a " Qur(12:56).

L i c h a ya m i t i h a n i mikubwa i l iyompata Y u s u p h ( a s ) k a m a tulivyoona, Mwenyezi Mungu hakuacha subira ya mja wake huyu ipotee bure, na badala yake alimlipa ukubwa, ushindi na mamlaka. Kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni wa mwanzo wa Kiislamu, kutoka kundi la tabi'in, mfalme wa Misri alisilimu mikononi mwa Yusuph (as). Kwa hiyo, Mtume h u y u wa M we n y e z i Mungu, aliitawala Misri kwa kutumia Sheria za Mwenyezi Mungu.

Qur'an haizami sana katika kipande hiki cha maisha ya Yusuph (as). Kisa kinaingia kwenye a wa m u ya m w i s h o , ambapo Yusuph (as)

a n a u n g a n a t e n a n a ndugu zake. Makala hii haitazungumzia kipande hicho.

M w e n y e z i M u n g u Mtukufu amemfahamisha Muhammad (saw) kwamba katika visa vya Mitume kuna mafunzo kwa watu wa Umma huu: "Bila shaka katika hadithi zao hizi limo fundisho kwa wenye akili" Qur(12:111).

Leo hii, Umma wa Kiislamu duniani unashambuliwa kutoka kila kona. Katika ulimwengu wa Magharibi, Waislamu wanashambuliwa kifikra, wanadhalilishwa kupitia propaganda na sheria kandamizi za ugaidi, ambazo zinawalenga wao tu.

K a t i k a u l i m w e n g u wa Waislamu, Waislamu wanauawa kama wanyama. Kuanzia Somalia, Burma, Iraq, Yemen, Syria na hiyo ni mifano michache tu. Hali hii ya ukandamizaji na unyanyasaji siyo mpya kwa Waislamu. Kiukweli, Mitume wengi na mataifa yaliyotangulia, walikabiliana na mitihani na mateso kama hayo.

Lakini wao walifanikiwa kwa sababu waliamini na kumtegemea Mwenyezi M u n g u t u . Wa l i f a n ya matendo mema na kufuata Shariah ya wakati wao. Umma wa Kiislamu leo pia unahitaji kumuamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake. Kama tulivyoona kwenye makala hii, Mwenyezi Mungu ana mipango yake kwa waja wanaomtii kwa dhati na hatimaye atawapa ushindi, ingawa kwa sasa anawaachia waovu watambe:

"Hata Mitume walipokata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo i k a wa j i a n u s u r a ye t u , wakaokolewa tuwatakao. Na

adhabu yetu haitowawacha k a u m u y a w a k o s e f u " Qur(12:110)

Aya hiyo inafundisha kwamba Mwenyezi Mungu mara nyingi huleta ushindi wakati hali inapoonekana kuwa ngumu na mwelekeo haueleweki. Hiki ndiyo kipindi ambacho waumini wa kweli husubiri nusra ya Mwenyezi Mungu. Waislamu duniani leo wako katika kipindi kigumu mno. Ndiyo kile kipindi ambacho Mtume alisema kuwa Muislamu wa kweli ni sawa na kushika kaa la moto.

Hata hivyo, Waislamu t u n a h i t a j i k a k u f u a t a kikamilifu mafundisho ya dini yetu na sheria zake bila ya kulegeza msimamo hata kidogo. Kukimbilia njia za mkato, hakuwezi k u t u f i k i s h a k w e n y e ushindi. Iwapo tumejifunza chochote kutoka kwenye visa vya manabii, msaada wa Mwenyezi Mungu unakuja pale Waislamu wanapokamata sawasawa kamba ya Mwenyezi Mungu bila ya kulegeza m s i m a m o . N a s i l e o tunapaswa kufanya hivyo ili tuweze kuiweka dini ya Mwenyezi Mungu mahali pake inaspotahili.

Tuache kuwaogopa m a k a f i r i . M we n ye z i M u n g u a m e t u a m b i a m b i n u , m i p a n g o n a m i k a k a t i ya o d h i d i ya Waislamu ni dhaifu t u . Wa i s l a m u n d i y o wanaotakiwa kuwa sawa katika dini yao:

"Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima." Qur(14:46)

Page 12: An Nuur 1131

12 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Mashairi/Makala

SH U K U R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi M u n g u , M o l a w a

ulimwengu (dunia) na rehema na amani zimfikie yule aliye mbora wa Mitume Nabii Muhamad (SAW).

Ama baada ya utangulizi huo mfupi, kwa yakini M w e n y e z i M u n g u ameumba ulimwengu na akaudhalilisha kwa ajili ya binadamu na akamuumba binadamu kwa aj i l i ya kumuabudu yeye peke yake.

Na akaifanya ibada hii kuwa ni jambo muhimu katika maisha na kwa hivyo basi, amesema Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu, “Na sikuwaumba m a j i n i n a b i n a d a m u isipokuwa kwa kuniabudu” Dhariyat (56).

A m e s e m a k w e l i Mwenyezi Mungu, hivyo hapana budi tujue maana ya ibada kwa upana zaidi kuliko wanavyojua baadhi ya watu, kwani haikusudiwi kutekelezwa swala tano kila siku isipokuwa ina maana ya kila kitendo utakachokitenda kwa aj i l i ya Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe katika kila nyanja zote za maisha, iwe katika uzalishaji mali au kutoa huduma au kutoa msaada kwa watu au katika kuchunga maslahi ya watu.

N a k u w a f a n y i a mambo ya kheri watu na kuwapatia mahitaji yao na kuwawepesishia mambo yao hayo yote huhesabiwa kuwa ni ibada.

Hivyo Mtume wetu (SAW) amesema, “kwa hakika matendo yote hutegemea nia” na hutofautiana kati ya ada na ibada, kwamba unatekeleza jambo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kutaka radhi zake na k u h a k i k i s h a u n a k u wa kiumbe mkamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mola wa u l i m w e n g u w o t e . Kwa yakini amelazimisha

Uadilifu katika ibada ni alama za Uislamu

Na Sheikh Wahid Mansuri Mohamed

Mwenyezi Mungu ibada kwa Waislamu na akaweka mipaka maalum na wakati maalum, ili watu waweze kutekeleza kwa wakati wake bila ya kuchoka au kwa taabu, na kisha wakapata visingizio.

Kwa hakika ni uzuri ulioje kwa Uislamu kuweka uadilifu na kuchunga muda ili isilete baadhi ya nyakati uchovu, hivyo uadilifu ni jambo linalotakiwa na lenye kupendeza, kuchupa mipaka na kuzidisha hakutakiwi. Amesema Mwenyezi Mungu “Na vile vile tumekufanyieni umma wa Kati na kati” SURAT ALBAKARAT (143) kati na kati katika kila kitu bila kuzidisha wala kupunguza.

N a a l i k u wa M t u m e akiwalingania Masahaba zake juu ya ukati na kati na kujitenga na kuzidisha au kupunguza kwa hali yoyote itakayokuwa, kwani watu kwa pupa yao juu ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu, wakati mwingine hufikia kuongeza ibada na kuweka pembeni ile hali ya kati na kati, hivyo akaamrisha Mtume juu ya uadilifu na ukati na kati na akatolea mifano toka kwa Abii Harairat (RA), amesema Mtume (SAW) “jitahidini kwa ibada kiasi muwezacho na jisogezeni kwa Mwenyezi Mungu kwa ibada za muda wa usiku na kusudieni kufikia lengo”. Ameitoa Imamu Bukhari na Muslim.

Na akatoa mfano kwa yule anayerusha mshale, ajitahidi aweze kulenga na kupiga anachokusudia. Hivyo yampasa kila mtu afikie malengo na pale alipokuwa akiwafundisha Masahaba zake, hukumu za dini na sheria zake alikuwa anajua watapatikana wale watakaovuka mipaka ndio maana akatahadharisha sana juu ya hilo.

Na kusisitiza kushikamana na yule yaliyokuja katika dini bila ya kujilazimisha au kuongeza toka kwa Bin Abbas (RA) amesema, ameniambia mimi Mtume (SAW) kesho muagane naye akiwa juu ya mnyama wake, LETE, okota au niokotee, nikamuokoeta vijiwe vya kutupia kwenye nguzo tatu na pale nilipoviweka katika mikono yake mitukufu akasema, mfano wa vijiwe hivi.

Na j i tahadhar in i na k u v u k a m i p a k a , k wa y a k i n i w a m e a n g a m i a waliopita kabla yenu kwa kuzidisha kat ika dini , ametoa Nnasai na pale walipouliza juu ya matendo bora na anayoyapenda sana Mwenyezi Mungu, akasisitiza juu ya vyanzo vya uadilifu na kukusudia

na akawaamrisha kufanya kazi wawezavyo bila ya kujichosha wenyewe.

Kutoka kwa Aisha (RA) hak ika yake amesema “Aliulizwa Mtume (SAW) juu ya ibada anayoipenda mno Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema (SAW) ni ile yenye kudumu hata kama ni chache na akasema “J i lazimisheni kazi i le mnayoiweza”. Ameitoa Bukhari na Muslimu.

N a a m e s e m a k w e l i Mwenyezi Mungu pale aliposema “Na hakuifanya kwenu dini hii ugumu” Surat Al-Haji (78). Kwa maana hakufanya kwenye din i mashaka ( taabu) . Na kutoka kwa Jabiri Bin Samurta (RA) amesema, nilikuwa nikiswali pamoja na Mtume (SAW), ilikuwa swala yake ni ya wastani na ikadhihiri malezi haya kwa wanaomfuata Nabii Muhamad (SAW) miongoni mwa Masahaba zake na wafuasi wake, kwani wao walikuwa wakijifunza elimu ya dini na yale aliyokuja nayo miongoni mwa uadilifu na ukadiri wa kati na kati.

Tunayapata hayo kwa yaliyotokea baina ya watu wawil i miongoni mwa Masahaba zake, Abii Dardai na Salman Alfarisiy (RA) toka kwa Abii Juhaifa (RA) amesema, “Aliwafanyia udugu kat i ya Salman na ABII DARDAI (RA), akamtembelea Salman kwa Abii DARDAI na akamuona mama yake DARDAI amevaa hovyo ovyo akamwambia, mbona upo hivyo, akamjibu, ndugu yako baba DARDAI hana haja na dunia.

Akaja ABUU DARDAI akamtenganezea chakula a k a m w a m b i a k u l a , akasema mimi nimefunga, akamwambia basi na mimi si l i hadi na wewe ule, akala na ulipofika usiku aliondoka ABUU DARDAI kwenye kisimamo cha usiku akamwambia lala, akalala hadi ilipofika karibu na alfajiri akasema SALMAN, h i v i s a s a s i m a m a n a wakaswali, akasema Salman, kwa hakika Mola wako ana haki kwako na nafsi yako ina haki kwako na mkeo ana haki kwako, basi mpe kila mwenye haki haki yake. Akaja kwa Mtume (SAW) na akamuhadithia yote, akasema Mtume (SAW), “Amesema kweli Salmaani” ameitoa hadithi hii Imamu Bukhari.

Ewe Mwenyezi Mungu tupe elimu ya dini yetu na utuonyeshe aibu zetu tuziepuke.

AAMIIN

Salam zangu natuma, mijini na vijijini,Habari imeshavuma, amewasili mgeni,Leo mwezi kuandama, ni yetu matumaini,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu wa fadhila, na mwezi wa ihsani,Sio mwezi wa chakula, kushindilia tumboni,Au mwezi wa kulala, kukoroma kitandani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu wa ibada, na kusoma Qur-aani,Ni mwezi wenye faida, nyingi ziso na kifani,Si mwezi wa kawaida, ni mwezi wenye thamani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Imo siku ya Kudura, kwenye kumi za mwishoni,Hiyo siku ndio bora, kuliko zote yakini,Ni siku yenye kung'ara, Jibrili ni mgeni,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu mashetani, wana pingu mikononi,Minyororo ya shingoni, wametiwa huwaoni,Ona vipi Rahmani, mwezi Anauthamini!Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu Qur-aani, ilishuka ardhini,Kwa wahyi toka mbinguni, ni maneno ya Manani,Isomwe kila makani, itunawiri moyoni,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu tarawihi, ni Swala za Ramadhani,Usikose kuziwahi, ziswali msikitini,Mwenyewe utafurahi, utakuwa burudani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu mafakiri, pamoja na masikini,Uwaalike futari, wakaribishe nyumbani,Wape maneno mazuri, na sadaka mkononi,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu wa kufunga, kila kitu mdomoni,Sio mwezi wa kuringa, kujivuna mitaani,Ni mwezi wa kujikinga, na maasi duniani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu kujishika, kujizuia mwilini,Usiyavuke mipaka, yalokatazwa na dini,Na ibada shughulika, asubuhi na jioni,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu kula daku, mama aende jikoni,Ukiingia usiku, kula unavyotamani,Mchana ni marufuku, ila uwe safarini,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu inafungwa, milango yote motoni,Hapo inafunguliwa, milango yote peponi,Dua zinakubaliwa, ombeni ndugu ombeniKaribu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu wa kutubu, uyafute ya zamani,Uzikusanye thawabu, uombe na samahani,Uzungmze kwa adabu, na ndugu na majirani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu tenda mema, uchoyo weka pembeni,Tena uwe na huruma, kwa wale walioduni,Kama Mungu kawanyima, huo ndio mtihani,Karibu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Mwezi huu wa baraka, wa amani na imani,Tumuombe Mtukuka, pepo iwe maskani,Ni mwisho wa kuandika, nimefika kikomoniKaribu wetu mgeni, mtukufu Ramadhani.

Abdallaah Bin Eifanalhidaaya.com

Karibu wetu mgeni - Mtukufu Ramadhan

Page 13: An Nuur 1131

13 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Makala

KWA jina Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma na mwingi wa

ukarimu. Kila sifa njema a n a s t a h i k i M we n ye z i M u n g u k w a n e e m a zake a l izotuneemesha z e n y e k u o n e k a n a n a zisizoonekana.

“Basi kumbusha, hakika kukumbusha ndio bora, ataogopa mwenye kuamini na atajitenga muovu.”

Mpenzi msomaji, kila mwanadamu ni mkosaji na mmbora wa mkosaji ni yule anaekosea kisha akatubia makosa yake. Maneno haya ni yenye kutia moyo, yenye kuhadharisha na yenye kuthibitisha kuwa maumbile yake mwanadamu ni yenye kutiwa kasoro toka pale anapoingiwa na utimamu wa akili.

Kutokana na kasoro hizo ambazo mwanadamu ameumbwa nazo, suala la kukumbushana katika kufanya mema na kuyaacha maovu l imepewa uzito mkubwa katika Dini ili kupatikane jamii yenye kufuata maadili.

Kuamrisha mema ni maneno au kauli anayoitoa mtu akimtaka mtu au watu wengine wafanye mambo mazuri yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu. Amma kukataza maovu ni kumzuia mtu au watu wengine kufanya mambo mabaya na maovu yenye kumchukiza Mwenyezi Mungu (s.w).

Suala la kuamrisha mema na kukataza mabaya ndio usimamizi mzuri wa jamii, yaani watu wote kuwa ni wasimamizi wa mambo katika jamii, ni miongoni mwa ratiba na mipango a m b a y o i n a m p e l e k a mwanaadamu katika njia ya ukamilifu na ufanisi katika maisha, na watu wanapoacha kuamrishana mema na kukatazana mabaya humpelekea mwanadamu kat ika maangamiz i na upotevu mkubwa. Maneno haya yanathibitishwa na kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) aliposema:

“A m r i s h e n i m e m a n a k u k a t a z a m a o v u , k wa n i kinyume na hivyo, Mwenyezi Mungu atawafanya madhalimu wakutawaleni, madhalimu ambao hawatawaheshimu wazee na wala hawatawaonea huruma watoto wadogo."

Wakati umma wa Kiislamu u n a p o a c h a k u a m r i s h a mema na kukataza maovu, basi kuna uwezekano wa kushuka na kupungua kwa heshima na thamani yao. Katika upande mwingine, bila ya kuweko usimamizi wa wote katika jamii, yaani kila mtu kujihisi kuwa na

Wajibu wa kuamrisha mema na kukataza mabayaNa Hemed S. Marhoon jukumu juu ya yanayotokea

katika jamii, harakati ya mambo huondoka katika mikono ya watu wema, na badala yake watu wasio wema hushika usukani na kuutumbukiza umma katika misiba na masaibu makubwa.

S h a h i d i M u r t a d h a mwanafikra mkubwa wa Ki i s lamu kat ika kutoa ufafanuzi kuhusiana na thamani na udharura wa kuamrisha mema na kukataza maovu anaandika hivi:

"Katika Uislamu kuamrisha mema na kukataza mabaya ni msingi muhimu. Msingi huu huwafanya Waislamu wadumu na kubakia katika mapinduzi ya kifikra na harakati za kutaka mageuzi sambamba na kupambana na ufisadi na mambo maovu."

Katika Qurani tukufu M w e n y e z i M u n g u a m e t u f u n d i s h a k u w a maslahi ya mwanadamu yamo katika kuamrishana mema na kukatazana maovu, na kwamba ummati nyingi ziliangamizwa kwa sababu ya kuiacha faradhi hii.

Imam Ali bin Abi Talib A.S amesema: "Msiache k u a m r i s h a m e m a n a kukataza maovu, kwani k i n y u m e n a h i v y o , madhalimu na watu waovu watakudhibitini, wakati huo kadiri mtakavyopiga mayowe na kuomba msaada, hamtojibiwa."

U m m a u n a p o a c h a k u a m r i s h a m e m a n a k u k a t a z a n a m a o v u , M w e n y e z i M u n g u a t a wa f a n y i a v i o n g o z i n a w a t a w a l a w a o v u ambao watawadhibiti na kuwanyanyasa na ha l i ya kuwa hawatakuwa na msaada.

M b i n u y a k w a n z a i l iyotumiwa na Bwana Mtume (s.a.w) na Ahlul Bayt wake katika kueneza faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu ilikuwa ni kuleta ufahamu na uwelewa baina ya watu. Hapana shaka kuwa, ufahamu, maarifa na uwelewa wa haki na majukumu ni msingi na sharti muhimu la kuzingatiwa katika kufanya marekebisho katika jamii.

Kuweko sheria na kanuni kadiri zitakavyokuwa nzuri na zimekamilika, lakini hilo halitoshi, bali kuna ulazima kwa wanajamii kujua haki zao na vile vile kufahamu yanayopaswa na yasiyopaswa kufanywa kwa mujibu wa maadili. Shaksia wakubwa wa kidini walitumia maneno ya Mwenyezi Mungu katika kuwapa maarifa watu, na kwa msingi huo wakatumia aya za Qur'ani kuwabainishia watu hatima na matokeo mazuri ya matendo mema pamoja na matokeo mabaya ya dhambi na matendo maovu. Kwa kuzingatia kwamba, wao wenyewe walikuwa ni vigezo bora vya matendo na maagizo ya Qur'ani Tukufu waliweza kuwa na nia njema kwa waliokuwa wakiwalingania

AMIR wa Shura ya Maimamu nchini, Sheikh Mussa Kundecha.

kutenda mema na kuachana na maovu.

Imam Ali (a.s) anasema k a t i k a k u h u s i a n a n a udharura wa kuamrisha mema na kukataza maovu kwamba:

" M w e n y e z i M u n g u amewajibisha kuamrisha mema kwa ajili ya maslahi ya watu wote na kuwapeleka wao katika njia ya saada na ufanisi , na ametaka watu wakataze mabaya ili kuwazuia kutenda dhambi watu wasiotumia aki l i ipasavyo."

Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni jukumu ambalo kama litafanyiwa kazi ipasavyo katika jamii kwa maslahi ya jamii nzima kutawapelekea katika ufanisi na kuwaepusha na ghadhabu za Mwenyezi Mungu.

Katika kuti l ia mkazo jambo hili, Mtume (s.a.w) amesema katika hadithi yake mashuhuri:

"Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mchunga a taul izwa juu ya ki le alichokichunga".

Mbali na waja kujichunga wao wenyewe katika matendo yao na kujiepusha kutenda maovu, wana jukumu pia la kuwachunga wengine au kuwa na usimamizi kwa wengine katika jamii. Yaani katika Uislamu, mbali na dini hii tukufu kumtaka kila mtu kuwa ni mchunga wa amali na matendo yake binafsi na kujihesabu kwa anayoyatenda, unamtaka pia ahisi kuwa na majukumu pia kwa watu wengine.

Faradhi ya kuamrisha m e m a n a k u k a t a z a maovu ilikuwa na nafasi muhimu sana mwanzoni mwa Uislamu kwa ajili ya kuzifanya thamani za dini zikite mizizi na kuimarika. Katika harakati za kueneza utamaduni wa Kiislamu na kuzifanya thamani za kimaadili na kijamii kukita mizizi, Bwana Mtume (s.a.w) kwanza aliwafundisha watu misingi ya awali ya Uislamu na kisha akaomba msaada kupitia kuamrisha mema na kukataza mabaya na kulitaja

hilo kama ni jukumu la wote kwa ajili ya kuzifanya thamani za Kiislamu zikite mizizi. Usimamizi huu wa kijamii uliwafanya Waislamu wakubaliane na kuziheshimu sheria za dini ya Mwenyezi Mungu.

Kando ya us imamizi wa nje wa kijamii, yeye mwenyewe Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa ni kigezo cha kuigwa katika amali na matendo mema. Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w) nao wakimfanya Bwana Mtume (s .a .w) kuwa ni kigezo na ruwaza njema kwao walifanya bidii ya hali ya juu katika kuamrisha mema na kukataza maovu katika jamii kwa njia ya maneno na vitendo vyao.

Qur'ani Tukufu inautaja umma wa Kiislamu kuwa ni umma wenye heshima na bora kuwahi kutolewa kwa ajili ya wanaadamu. Lengo la kuletwa umma huu ni kumwokoa mwanaadamu na ni kwa ajili ya kuwatakia kheri watu. Amethibitisha Mwenyezi Mungu (s.w) jambo hili katika Kitabu chake kitukufu, pale aliposema:

“Ninyi ndio umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishiwa watu” (Al-imraan:110)

N a a k a s e m a t e n a Mwenyezi Mungu katika Surat Baqara:143:

“ N a v i v y o h i v y o tumekufanyeni umati bora, ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu.”

Jukumu kubwa la umma huu nalo ni kuamrisha mema na kukataza maovu na kuwa na imani thabiti juu ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa Waislamu hawatafanya harakati zozote za kuamrisha mema na kukataza mabaya, b a s i s i f a z a u o n g o z i zitawaondokea mikononi mwao.

Mpenzi msomaji, ibaada hii muhimu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya huanzia kat ika famil ia hususan malezi ya watoto, wazazi wana dhima kubwa kwa Mwenyezi Mungu juu ya watoto wao. Mwenyezi

Mungu ametubainishia njia za kuwalea watoto na Mtume (s.w.a) akatufafanulia njia hizo kwa maneno na vitendo ili tupate urahisi wa kuyatekeleza.

Maporomoko makubwa ya tabia na tamaduni za Kiislamu katika jamii kwa kiasi kikubwa yanaanzia katika malezi. Filamu za kuigiza zisizo na maadili, muziki, mpira, majarida, pombe, kamari, riba na zinaa ni katika mambo machafu na yenye kumchukiza Muumba lakini katika hali ya kawaida hivi sasa mtu kuyafanya hayo aidha kwa siri au hadharani si jambo la kushangaa. Hii ni kwa kuwa jamii imeacha misingi madhubuti iliyowekwa na Mola Muumba na kujibebesha mifumo isiyoendana na umbile la mwanadamu na yenye kubadilika kila kukicha. Wazazi na jamii kwa ujumla wamejivua jukumu la malezi ya watoto wao na kuwaacha watoto walelewe na watu wengine, jambo ambalo linachangia kuporomoka kwa maadili ya Dini. Jamii ya Kiislamu imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia watoto wao kufuata mifumo m i b o v u ya m a i s h a ya kidunia kinyume kabisa na ule alio uweka Muumba. Hawaamrishi mema wala hawakemei mabaya. Uovu unahalalishwa unapokuwa sambamba na kipato. Mzazi yuko radhi kumuacha binti yake aishi na mwanamume bila ya ndoa ikiwa tu anapata mahitaji yake na ikiwa binti ameridhia. Hii ni misiba inayotawala katika jamii zetu. Kukaa bila kuchukua hatua yoyote wakati unashuhudia u o v u u k i t e n d e k a n i kuacha kutekeleza wajibu ambao Mwenyezi Mungu amekupangia.

M w e n y e z i M u n g u amesema katika kitabu chake Kitukufu:

“ Na iogopeni adhabu ambayo haitawasibu wenye kudhulumu nafsi zao peke yao, bali itawasibu h a t a w e n y e k u n ya m a z a wanapoona uovu.”

Page 14: An Nuur 1131

14 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014Habari

Karibu RamadhaniInatoka Uk. 16hazitaweza kunyanyuka katika siku ya kiyama hadi aulizwe ameumaliza umri wake katika njia gani na ameutumia ujana wake katika nini.

Bw. Mziya aliongeza kuwa kongamano hilo, pia linakusudia kuiomba serikali kuweka mikakati mahsusi ya kuwasaidia vijana kiuchumi, kwa kuwa na sera zitakazowezesha kuongeza ajira kwa vijana na fursa mbalimbali za ujasiriamali.

Al isema Tai fa h iv i sasa linaelekea kubaya kwakuwa tu, baadhi ya watu wanaol iongoza wamekuwa wanatumia nafasi zao kwa ajili ya kujali maslahi yao binafsi au watu wa kikundi fulani, huku wakikosa utii wa imani na maadili mema, ambayo matokeo yake mfumo mzima wa maendeleo ya jamii, kisiasa na kiuchumi umeathirika.

Aliongeza kubainisha kwamba inawezekana k a b i s a k u p o r o m o k a maadil i kunakotokea sasa, kunaathiri jamii, ikiwemo ya Kiislamu yenye muongozo bora wa mfumo wa maisha ya binadamu.

A l i s e m a , u b i n a f s i u m e r u h u s u kutomuhusisha vyema ki jana katika sera na mipango ya kimaendeleo au kusahau majukumu makuu ya malezi kwa vijana katika kujenga j a m i i i m a r a y e n y e

taaluma na maadili mema, kama dini ya Kiislamu inavyofundisha.

Bw. Mziya alisisitiza kuwa wazazi wa sasa nao wamechangia kuharibu mustakabali wa vijana kwakuwa wamekuwa wakijishughulisha zaidi na kutafuta mali, kwa ajili ya maendeleo ya vitu na kusahau familia zao, kiasi kwamba hali hiyo baadae wanashtuka wanakuta vijana tayari wameshaharibika katika

vitendo vya umalaya, dawa za kulevya, ufisadi na tabia nyingine za hatari.

“Katika kongamano h i l i , t u n a t a r a j i a p i a kuiomba serikali, vyombo vya habari pamoja na wanaharakati mbalimbali, kujishughulisha zaidi na shida za vijana wa leo hasa kimaadili.”

“Kuhakikisha hazina ya vijana inakuwa ya Taifa kweli kwa sasa na huko mbeleni. Kufutwa kwa mifumo inayoonekana

kuwabagua vijana wetu kwa imani zao, hasa katika masuala ya ibada mashuleni, vyombo vya habari kurusha habari zinazoporomosha maadili kama vile kuonyesha vijana wa kiume wamevaa kama wanawake katika Television, wanaharakati k u s h a b i k i a m a m b o ambayo yanawafanya v i j ana wahamaki na kuwa wenye kulalamika k i l a s i k u b a d a l a ya kuwafanya waone fursa

z i n a z o w a z u n g u k a au kutetea mavazi ya baadhi ya vijana ambayo ya n a o n y e s h a wa z i kuwa yanahamasisha masuala ya ngono. Haya ni matatizo makubwa kwa vijana” alibainisha Bw. Mziya.

Aidha kongamano hilo litakuwa ukumbusho k wa wa n a t a a l u m a n a w a n a z u o n i w o t e wa K i i s l a m u j u u y a k u e n d e l e a k u m h a m a s i s h a ki jana kimaadili na k u m u e n d e l e z a , i l i kujenga jamii bora ya Kiislamu inayofuata maadili bora na sahihi, ambayo italeta athari kwa maendeleo ya Taifa.

P i a K o n g a m a n o l i n a k u s u d i a k u w a c h a c h u y a kuwakumbusha vijana kutosahau kutekeleza m a j u k u m u ya o ya Kiimani katika kipindi chao chote cha maisha, na kushir ikiana na wanazuoni ambao muda mwingi wanakuwa katika wakati mgumu kuendeleza jamii kiroho.

CUF warekebishaInatoka Uk. 16

ngazi ya mkoa kwa upande wa Tanzania Bara na kutaka ngazi za uongozi ziendelee kama kawaida kwa k u we p o n g a z i ya Wilaya ikifuatiwa na ngazi ya Taifa.

W a j u m b e h a o wamekataa pendekezo hilo kwa madai kuwa ngazi hiyo itaongeza utitiri wa viongozi wasiokuwa na ulazima kwa maendeleo ya chama.

Pendekezo jingine w a l i l o l i k a t a a n i uteuzi wa Makatibu wa Wilaya, ambapo w a m e k u b a l i a n a kuwa Makatibu wa ngazi hiyo waendelee k u c h a g u l i w a n a wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya.

M a r e k e b i s h o y a k a t i b a h i y o y a t a y o i n g i z w a kwenye Katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la 2014, yataanza kutumika kuanzia tarehe Agosti 2014.

Dk. Salha (kushoto) akizungumza kuhusu ulezi wa yatima katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani limefanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mapema wiki hii. Kongamano hilo lililoandaliwa na TAMPRO.

Ramadhan ya Mtume - mwezi wa mapambano!Inatoka Uk. 10nchi hizo, ili mababeru wapate mwanya wa kupora rasilimali za nchi hizo. Wakati asili ya Uislamu ni kudhibiti tamaa za kibinadamu, Ubeberu umezifungulia tamaa hizo na matokeo yake ndiyo hii vurumai tunayoiona leo. Mtu haiogopi kuangamiza nafsi ili apore mali!

Haya ni mapambano ya Kiitikadi katika zama zetu, ambayo kama Waislamu, hatuna budi kukabiliana nayo, kwa kutumia silaha ya kitaaluma ya ujumbe wa Qur'an. Badala ya kuomba radhi kwa ajili ya Uislamu wetu, tunahitaji kuwa mstari wa mbele na kuonyesha mapungufu ya mifumo yao ya maisha.

Tunahitaji kuwaonyesha kwamba mifumo yao ya maisha imejengwa juu ya fikra potofu na ndiyo sababu ya majanga yote katika jamii yao na duniani kwa ujumla. Tunahitaji kuwaonyesha jinsi Uislamu ulivyomkomboa

mwanamke kutokana na unyanyasaji wa kingono na jinsi ulivyomaliza tatizo la ubaguzi wa rangi na umasikini wa kutupwa.

Mtume wa Mwenyezi Mungu aliipanga jamii yake na dola kwa misingi ya Sheria za Mwenyezi Mungu, akisimamisha haki miongoni mwa watu, na kujenga jamii ya kipekee juu ya msingi wa Imani na Taqwa, badala ya msingi wa ukabila, rangi au hadhi ya kijamii. Aliwapa wasio Waislamu haki zao walizostahili kwa mujibu wa Uislamu. Mtume alionyesha Sunna ya kuwa mtu wa Serikali na kiongozi wa kisiasa mjini Madina.

Mtume aliunda jeshi la kisasa wakati ule, alipigana vita na kusaini mikataba, lengo likiwa kuimarisha dola ya Kiislamu katika eneo la Arabuni. Ilikuwa R a m a d h a n 1 7 w a k a t i Wa i s l a m u wa l i p o p a t a ushindi mkubwa kwenye vita vya Badr. Vita vingine

maarufu kama Khandaq na Tabuk vinaonyesha jinsi Waislamu walivyojiandaa na kupambana katika mfungo wa Ramadhan.

Vita hivi vinawasilisha mapambano ya kijeshi na kisiasa ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu na Masahaba wake walishiriki ili kuimarisha mamlaka ya Uislamu na kusambaza Da'awah ya Kiislamu kwa watu wa mataifa mengine.Walifahamu Qur'an hi i imekuja kama muongozo kwa watu wanadamu wote, hivyo hawakudhoofisha juhudi zao za kusambaza Uislamu kupitia Da'awah na hata Jihad kwa mataifa mengine. Hivyo ndivyo Waislamu wenzetu wa awali walivyoifahamu Qur'an na jinsi walivyotekeleza majukumu waliyokabidhiwa na Uislamu.

Imefika wakati Waislamu duniani kuifanya Ramadhan hii kuwa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mpaka

lini tutaisoma tu hii Qur'an na kusikiliza sauti yake ya kuvutia, bila ya kuifahamu na kuitekeleza? Je, tunautendea haki ujumbe wa Qur'an kwa kuisoma tu? Hivyo Swala na Funga ndiyo majukumu pekee Qur'an iliyotuletea Waislamu hapa duniani? Hivi tutaishia tu kupambana na nafsi zetu bila ya mapambano m a b a n a z a i d i a m b a y o Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyafanya?

Tu n a w e z a k u t a r a j i a madhambi yetu yasamehewe na Mwenyezi Mungu kwa kuifuata Qur'an nusu nusu? Imefika wakati wa kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mapambano yake yote. Popote tutakapokuwa, m we z i wa R a m a d h a n , pamoja na kufunga, kuswali taraweh na tahaj jud na kuomba dua sana, Ibada hizo lazima ziimarishe Imani zetu na Taqwa, ili tuweze kukabiliana na changamoto za kusimamisha Uislamu leo. Ramadhan ni mwezi wa ushindi. Mwenyezi Mungu aupe umma huu tawfiq, ili

Page 15: An Nuur 1131

15 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014LISHE

FUNGA ya Mwezi w a R a m a d h a n i i n a y o t a r a j i w a

kuanza s iku chache zijazo, ni lazima kila Muislamu balehe, mkazi wa mji, mwenye akili timamu na afya njema. Tujikumbushe wajibu huo kama Mwenyezi Mungu anavyo tujulisha. " E n y i m l i o a m i n i ! M m e l a z i m i s h w a kufunga (saumu) kama w a l i v y o l a z i m i s h w a waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu" (Quran: 2:183).

Kwanini tunafunga?Kwa mujibu wa aya hapo

juu, tunajifunza moja ya faida ya kufunga kuwa ni kumsaidia mja afikie ucha Mungu. Faida nyingine inayopatikana kutokana na funga ni kuimarisha afya ya kiwiliwili kama alivyotufundisha Mtume Muhammad (s.a.w) kwa maneno yake, "fungeni mtapata afya".

M o j a ya m u h i m i l i muhimu wa kujenga afya ya binadamu ni chakula.

Dini ya Kiislamu ina mwongozo kamili kwa m w a n a d a m u k a t i k a mambo yote ya maisha yake, iwe vyakula, lishe, afya, siasa, uchumi, jamii, elimu, afya, vita, mambo ya kiroho na kadhalika k w a m a e l e k e z o y a aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Msiba kwa Waislamu wa sasa

Waislamu wengi wa siku hizi hawafuati mafundisho ya Qur’an na Sunna za M t u m e M u h a m m a d ( s . a . w ) k u h u s u m l o bora. Hali hii inatokana na sababu kuu mbili. Kwanza ni kuufahamu Uislam vibaya. Kama vile dhana waliyokuwa nayo baadhi ya Waislamu kuwa masuala ya chakula bora ni ya kizungu na sio ya Kiislamu.

Sababu ya pili ni elimu ndogo ya mambo ya chakula na lishe. Hapa maana yake ni kuwa kuna baadhi ya aya za Qur’an na Hadith za Mtume (s.a.w) haiwezikani kuziingiza katika utekelezaji kwa kiwango cha kuridhisha bila ya kuwa na elimu ya chakula na lishe, hasa kat ika zama za sasa ambapo kuna udanganyifu mkubwa katika sekta ya vyakula.

Mlo bora kwa aliyefunga saumuNa Mujahidi Mwinyimvua Mfululizo wa makala

hizi unalenga kuchangia juhudi za kuwapa elimu Waislamu na wananchi wengine kwa ujumla, kuhusu chakula na lishe kama nguzo muhimu katika ujenzi wa afya ya kiwiliwili hasa wakati huu wa mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, inshaa Allah.

Makusudio yetu ni kuwa Waislamu watakapoingia katika kipindi cha kula mchana, wawe wanafuata miiko na taratibu nyingine katika vyakula na vinywaji kwa mujibu wa Uislamu, ili wawe na fya njema kama funga ilivyokusudiwa kuwafikisha katika lengo hilo.

Qur’an na utafiti wa vyakula“Hebu mwanadamu na

atazame chakula chake. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu (kutoka m a w i n g u n i ) . T e n a tukaipasuapasua ardhi. Kisha Tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe. Na mizabibu na mboga. Na mizeituni na mitende. Na mabustani, ( m a s h a m b a ) y e n y e mi t i i l iyosongamana barabara. Na matunda na malisho. Kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi n a wa n ya m a we n u ” (Qur’an: 80:24-32).Qur’an na uchaguzi wa vyakula

“Enyi watu kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala m s i f u a t e n y a y o z a shetani, bila shaka yeye kwenu ni adui dhahiri (Qur’an: 2:168). “Enyi mlioamini kuleni vizuri t u l i v y o k u r u z u k u n i , n a m u m s h u k u r u Mwenyezi Mungu, ikiwa m n a m u a b u d u y e y e peke yake”. (Qur’an: 2:172). “Na kuleni katika vile alivyokuruzukuni Mwenyezi Mungu vilivyo vizuri na halali na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi mnamwamini (Qur’an: 5: 88).

Qur’an na kula kiasi “...na kuleni (vizuri) na

kunyweni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao kiasi.” (Qur’an; 7:31).

Aya tu l izozinukuu hapo juu zinatupa msingi wa fani ya afya, hususan vipengele vya chakula na lishe. Aya zinatutaka tufanye utafiti ili tuone

chakula kinavyo zalishwa shambani na hatimaye kufika kwa mlaji na kuliwa na kutupa nguvu na afya kwa ujumla. Tukifanya hivyo tutaona uwezo mkubwa wa uumbaji wa Mola wetu.

Pia, tutaweza kuchunga miiko na taratibu nyingine za kula na kunywa na hatimaye kuwa sababu ya Mwenyezi Mungu kutujaalia afya njema.

Ratiba ya chakula Wakati wa mfungo wa

Ramadhani, ratiba ya chakula inabadi l ika . Tunaweza kuigawa milo ya mfungaji katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza mlo wa futari. Mlo wa pili ni ule wa usiku wa manane unaoitwa daku. Mlo wa futari nao una sehemu mbili. Kwa pale mfungaji anakata swaumu kwa tende, maji safi na salama au maziwa kama Mtume Muhammed (s.a.w) alivyotufundisha.

Kama mtu atakosa tende, maziwa au maji, anaweza kutumia juisi ya asili, chai, kahawa, tangawizi, togwa na uji kama mlo wa kufungua swaumu. Pia , matunda matamu kama vile chungwa, tikiti maji, ndizi mbivu, maji ya dafu, nanasi, embe, miwa, tufaa (apple), peasi na tango (kwa wasiotaka sukari).

Baada ya kukata swaumu n a k u s wa l i M a g h a r i b i mfungaji anakula futari kamili. Mlo huo lazima uwe laini na wenye sukari ya asili inayotokana na utamu wa vyakula vyenyewe. Vilevile, mlo huo wa futari kamili uwe wenye mafungu yote ya vyakula kama vile wanga,

mafuta, protini, madini, vitamini, maji ya kunywa na nyuzi lishe (dietary fibres). Ndio kusema mlo huo uwe ni mchanganyiko wa nyama au samaki au maharage, viazi, maboga, mihogo, vyakula vil ivyotengenezwa kwa ngano au mchele.

Mlo wa kabla ya kulala ni kwa mtu ambaye hawezi kuamka na kula daku usiku wa manane. Ikiwa mtu hawezi kuamka na kula daku ni vema kabla ya kulala ale vyakula mchanganyiko na vigumu. Mfano ugali, wali, chapati, vitumbua vikiwa na maharage au samaki au dagaa au nyama.

Mlo wa dakuMlo wa pili kwa mfungaji

ni ule unaoliwa usiku wa manane unaoitwa daku. Kwa mtu atakayeamka na kula daku ni vema asile kabisa wakati anapokwenda kulala. Vizuri anywe maji na ale matunda au mboga za majani kabla ya kwenda kulala.

Atakapoamka usiku wa manane, daku lake liwe chakula kizito kama ugali, wali, chapati, vitumbua vikiwa na maharage au samaki au dagaa au nyama. Lakini anapokula daku asishibe sana.

Pia, mlo wa daku usiliwe na chai, kahawa au juisi. Kwa sababu mchana utakapo fika mwili utapoteza maji mengi kwa njia ya mkojo.

Katika mlo wa futari au daku inasisitizwa kula na matunda na mboga za majani ili kupunguza tatizo la kujaa gesi na kiungulia mchana wa swaumu. Watu wengi

hata wale wenye uwezo kifedha hawana tabia ya kula matunda na mboga za majani. Huu ni ufahamu mbaya kwa sababu, mboga na matunda ni baadhi ya vyakula al ivyotuumbia Mwenyezi Mungu, ili tuvile na kujenga afya zetu kama i l ivyobainishwa kat ika Qur’an.

Kama mtu hawezi kuamka na kula daku, ni vema ale chakula chake kabla ya kulaka . Chakula hicho kinaweza kuwa ugali, wali, chapati kwa kiteoweo kama nyama, samaki, dagaa na maharage. Mboga za majani na matunda pia ni muhimu.

Miiko usiku wa saumuHali kadhalika, ni vema

wakati wa kufuturu mpaka a l f a j i r i , m f u n g a j i a we anakunywa maji ya kutosha. Ni muhimu sana kunywa maji ya kutosha ili kupunguza hatari ya mwili kukaa muda mrefu bila maji ya kutosha. Maji mwilini yanafanya kazi nyingi ikiwemo kuondoa sumu kutoka katika mwili.

Ili kupunguza upungufu wa maji mwilini vyakula vyote usiku wa Ramadhani v is iwe na sukar i wala chumvi nyingi. Chumvi nyingi mwilini inadhuru afya. Pia, chumvi nyingi inaufanya mwili upoteze maji mengi kwa njia ya mkoja au jasho. Tukumbuke kuwa kwa kawaida mwili hutunza chakula cha ziada, ukifunga au kufanya mazoezi chakula hicho hutumika na hatari ya kupata magonjwa kama kisukari au unene kupita kiasi inapungua sana.

Simu: 0655 654900

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia Majadiliamo katika Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani la Mwaka 2014 ukumbi Julius Nyerere Dar es Salaam hivi karibuni. Kongamano hilo liliandaliwa na TAMPRO.

Page 16: An Nuur 1131

16 AN-NUURSHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

AN-NUUR16 SHAABAN 1435, IJUMAA JUNI 27-JULAI 3, 2014

Soma Gazeti la AN-NNUR

kila Ijumaa

J U M U I Y A y a Wataaluma Waislamu Ta n z a n i a ( Ta n z a n i a Muslim Professionals Association-TAMPRO) imeukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya kongamano l i l i l o w a k u t a n i s h a wanataaluma wa fani na kada mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

K o n g a m a n o h i l o l i m e f a n y i k a k a t i k a ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mapema wiki hii , ambapo masuala mbalimbali ya kijamii na kidini yalijadiliwa.

A k i z u n g u m z a n a waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Jumuiya h i y o , B w . M u s s a Mziya, alisema lengo la Kongamano la mwaka huu ni kuhamasisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanataaluma wa Kiislamu na Waislamu w o t e k w a u j u m l a , hususan vijana kuona kuwa vijana kama kundi kubwa na muhimu katika jamii, wanapata malezi, nafasi na elimu sahihi ya mazingira na ya kidini, ili kumudu kuendesha harakati za kiuchumi na kidini kwa maana ya kuiweka jamii katika mustakbali wa maisha kama ilivyoamrishwa na dini yao.

Bw. Mziya aliongeza kuwa kauli mbiu “Our Yo u t h , O u r F u t u r e ” (Vijana wetu, Mustakbali wetu) ndio kauli mbiu ya kongamano la sasa la kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu 2014.

“ V i j a n a h a w a wanaokuwa hivi leo bi la shaka wao ndio umma wa kesho. Katika kongamano la mwaka h u u t u m e k u s u d i a kuzungumzia vijana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku, hususan maisha yao ya kidini na kiuchumi. Kwa maana hiyo basi, tumechagua anuani ya kongamano la mwaka huu kuwa “Vijana wetu, hazina yetu”.

K o n g o m a n o l a

Karibu RamadhaniTAMPRO wafanya kongamano la vijana

Na Mwandishi Wetu

kukaribisha Ramadhani limekuwa likifanyika kila mwaka katika siku ya Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Shaaban, ambapo kwa kipindi

cha miaka sita mfululizo, kongamano kama hilo l imefanikiwa kujadili na kupata majawabu ya masuala mbalimbali ya kijamii na kidini.

K i l a k o n g a m a n o limekuwa na kauli mbiu mbalimbali kila mwaka k u t o k a n a n a j a m b o mahsusi linalotakiwa kujadiliwa katika jamii.

B a a d h i y a k a u l i mbiu za makongamano yaliyowahikufanyika ni “Kufuta umasikini kupitia Zakah na Sadaqah”, “Nafasi ya elimu katika kuleta Maendeleo ya jamii”, “Athari za vyombo vya habari katika Jamii” na “Mifumo ya Benki za Kiislamu”, “Wanawake, nguzo kuu ya maendeleo ya Jamii”.

Bw. Mziya alisema kwa kutambua hali ya vijana kwa sasa kukabil iwa na changamoto nyingi katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uchumi, kijamii na kiteknolojia, T A M P R O i m e o n a umuhimu wa Waislamu hasa wanataaluma kama sehemu ya jamii, kukaa na kujadili ili kuona namna ya kuwasaidia vijana, hasa kwenye njanja za uchumi kama vile ajira, ujasiriamali na uwekezaji, pia nyanja za kijamii hasa kiimani ili kupata raia wema na waadilifu.

Alisema kuwa kipindi cha ujana ni muhimu sana kwa sababu ndio mustakabali wa umma na kutokana na sababu hiyo, mafundisho ya Kiislamu yanatilia mkazo sana katika kipindi hiki kutokana na umuhimu wake, kama hadith ya M t u m e M u h a m m a d ( S AW ) a l i p o s e m a , "Hakika nyayo za mja

CUF warekebisha katiba yaoNa Mwandishi Maalum

W A J U M B E w a M k u t a n o M k u u wa CUF Taifa wamepitisha m a p e n d e k e z o m b a l i m b a l i yaliyowasilishwa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho kuhusu marekebisho ya baadhi ya vipengele vya katiba ya chama hicho.

K a t i k a M k u t a n o Mkuu wa chama hicho unaoendelea kwa siku ya tatu katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, wajumbe hao pamoja na mambo

mengine wamekubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa chama hicho ufanyike mara moja katika kipindi cha miaka mitano badala ya miaka miwili na nusu kama ilivyopitishwa na Mkutano Mkuu mwaka 2009.

Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuona kuwa mapendekezo yaliyopitishwa mwaka 2 0 0 9 h a ya t e k e l e z e k i kutokana na ukosefu wa fedha unaokikabili chama hicho.

Hata hivyo amesema

kwa mujibu wa sheria hiyo, Mkutano Mkuu taifa unaweza kufanyika kwa dharura wakati wowote utakapohitajika.

Wajumbe wa mkutano huo pia wamekubali m a p e n d e k e z o y a kuongezwa ngazi ya uongozi ya Jimbo kwa upande wa Tanzania Bara ambapo kabla ya hapo, hawakuwa na ngazi hiyo.

Mapendekezo mengine yaliyopitishwa ni kwa Mwenyekiti wa chama hicho kupewa uwezo wa kuongeza wigo wa uteuzi kwa wajumbe wa kamati tendaji taifa, nje ya

wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kwa kadri anavyoona inafaa kwa maslahi ya chama.

Aidha wajumbe hao wamekubaliana kuwepo Kamati ya Nidhamu na Maadili kikatiba katika ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa, sambamba na mambo ya uchaguzi kuondolewa kwenye katiba na badala yake yabakie kwenye kanuni.

Kwa upande mwengine, wajumbe wa mkutano huo wamekataa pendekezo la kuwepo uongozi katika

Inaendelea Uk. 14

Inaendelea Uk. 14

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wataaluma Waislamu Tanzania (Tanzania Muslim Professionals Association-TAMPRO), Bw. Mussa Mziya (kushoto) akizungumza na Dk. Badamana wa Chuo Kikuu cha Nairobi katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mapema wiki hii.