12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1079 SHAABAN 1434, IJUMAA , IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013 BEI TShs 500/=, Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Tuzingatie aliyosema DCI Manumba Mwanafunzi aliza waumini Mtambani Adai kupigwa teke na mwalimu akienda kuswali Wanafunzi Wakristo wasimama kidete kumtetea Wakumbukeni kwa Dua Masheikh walioko ndani Allah awape Subra, malipo mema Wanaodhulumu wajitathmini upya Wakumbuke, ipo siku ya Hukumu MWANAFUNZI Abubakar Ally. Kesi ya Victor imeishia wapi? Tanzania tusimame imara kuinusuru nchi Mwenzako akinyolewa, tia kichwa chako maji Tutizame Pakistan ilikofikishwa sasa inatukanwa Ilianza na kudai Masheikh, ‘Uamsho’ ni magaidi Sasa Taifa la nyuklia, limegeuzwa mwanasesere Uk. 7 Uk. 3 Uk. 3 Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeanza maandalizi yake kwa ajili ya HIJJA 2013 kwa lengo la KUONGEZA UFANISI KATIKA IBADA ZA MAHUJAJI WETU kwa gharama za Dola 4300. Lengo letu ni kukamilisha mipango yetu kabla ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani.Tafadhali wasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117. (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ramadhan Sanze akiongea na vyombo vya habari katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika katika Hoteli ya Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

(22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

  • Upload
    others

  • View
    87

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

ISSN 0856 - 3861 Na. 1079 SHAABAN 1434, IJUMAA , IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013 BEI TShs 500/=,

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Tuzingatie aliyosema DCI Manumba

Mwanafunzi aliza waumini MtambaniAdai kupigwa teke na mwalimu akienda kuswaliWanafunzi Wakristo wasimama kidete kumtetea

Wakumbukeni kwa Dua Masheikh walioko ndani

Allah awape Subra, malipo memaWanaodhulumu wajitathmini upyaWakumbuke, ipo siku ya Hukumu

MWANAFUNZI Abubakar Ally.

Kesi ya Victor imeishia wapi?Tanzania tusimame imara kuinusuru nchi

Mwenzako akinyolewa, tia kichwa chako majiTutizame Pakistan ilikofikishwa sasa inatukanwaIlianza na kudai Masheikh, ‘Uamsho’ ni magaidiSasa Taifa la nyuklia, limegeuzwa mwanasesere

Uk. 7

Uk. 3Uk. 3

Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeanza maandalizi yake

kwa ajili ya HIJJA 2013 kwa lengo la KUONGEZA UFANISI KATIKA IBADA ZA MAHUJAJI WETU kwa

gharama za Dola 4300. Lengo letu ni kukamilisha mipango yetu kabla ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani.Tafadhali wasiliana

nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

(22) AHLU SUNNA WAL JAMAA

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ramadhan Sanze akiongea na vyombo vya habari katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika katika Hoteli ya Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Page 2: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

2 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Makala

Tanzania tusimame imara kuinusuru nchiMAPEMA wiki hii tume iliyokuwa imeundwa kuchunguza tukio la k i k o s i m a a l u m c h a M a r e k a n i k u v a m i a m a k a z i y a l i y o d a i w a kuwa ya Usamah Bin Laden na kumuuwa (The Abbo�abad Commission) imetoa taarifa yake. Katika uvamizi huo uliofanyika usiku wa tarehe 1 Mei, 2011, inadaiwa kuwa ser ikal i ya Pakistan ilikuwa haina habari kabisa kwamba tukio kama hilo litafanyika, wala kuwa na taarifa kuwa Usama Bin Laden alikuwa akiishi eneo hilo.

Pamoja na taarifa ya Tume kuonyesha kuwa viongozi wa Ser ikal i kuanzia Rais na hata Waziri wa Ulinzi hawakuwa na habari wala kuarifiwa rasmi baada ya uvamizi kufanyika, taarifa hiyo ya kurasa 336 inasema kuwa hata polisi waliofika eneo la tukio baada ya kufanyika m a u w a j i w a l i z u i w a kufanya chochote kwa hiyo hapakuwa na taarifa yoyote ya kipolisi kuhusu uvamizi na mauwaji hayo.

Katika taari fa hiyo imeelezwa kuwa kitendo cha askari wa Marekani kufanya uvamizi katika ardhi ya Pakistan bila ya kuomba ruhusa wala kuar i fu vyombo vya kiusalama na kijeshi, ni kitendo cha uhalifu wa kivita na kukiuka sheria za kimataifa. Lakini pia ni kitendo kinachodhihirisha k u wa Pak i s t an k u n a serikali kama hakuna, kuna jeshi na Idara ya Usalama kama hakuna. Wote, wanasiasa, viongozi wa serikali na taasisi za kijeshi na usalama wa nchi, zimefanywa kuwa hazina maana yoyote. Kaputi!

Serikali imelaumiwa, I d a r a y a U s a l a m a i m e l a u m i w a , P o l i s i wamelaumiwa na kila waliokuwa wangeweza kuhusika kwa namna moja

au nyingine. Ufupi wa maneno, taarifa imesema kuwa Pakistan, tai fa lililofikia kuwa na silaha za nyukili, limegeuzwa kuwa mwanasesere na kiroja cha karne. Limekosa heshma na kudharaulika kabisa kiasi cha watu kutoka nchi nyingine, kuingia na kufanya harakati za kijeshi bila kujali kuwa hiyo ni nchi huru yenye serikali na Rais wake.

R i p o t i h i y o inayopatikana katika mtandao wa Aljazeera na iliyochambuliwa kwa marefu na mapana katika kituo cha televisheni cha Aljazeera kuanzia Jumanne hadi hii leo, inamnukuu Waziri wa Ulinzi wakati huo Chaudhry Ahmed Mukhtar, akisema kuwa hakujua chochote juu ya uvamizi wa Marekani na wala hakuambiwa kilichotokea baada ya uvamizi. Akihojiwa na Tume hiyo alisema kuwa yeye alijua kuwa kikosi cha makomandoo wa Marekani wameingia na kufanya uvamizi na kumuuwa Usama Bin Laden kupitia magazeti.

Anasema baada ya kus ik ia k i l i chotokea kupi t ia vyombo vya habari, akapata pia simu kutoka kwa binti yake anayeishi New York, Marekani akimuuliza juu ya tukio hilo.

R i p o t i i n a f i c h u a z a i d i k u w a h a t a b a a d a y a u v a m i z i , Serikali ya Marekani haikushughulika kutoa taarifa kwa Serikali ya Pakistan. Kilichofanyika ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani (US Chairman of the Joint Chiefs of Staff Commi�ee) Admiral Mike Mullen, kunyanyua simu na kumwarifu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Pakistan, (Pakistani Chief of Army Staff ) General Ashfaq Pe ve z K a ya n i . S a s a

ilikuwa ni kazi ya Kayani kumwarifu Rais wake au kuacha. Kwa mujibu wa taarifa ya Tume, Generali Kayani alitoa taarifa kwa serikali masaa kadhaa baada ya tukio na kuongeza kuwa uchunguzi wao umebaini kuwa serikali yote na vyombo vyake vya dola vilikuwa kizani na waliofanya uvamizi, walifanya kana kwamba hakuna serikali au Idara za Usalama na Ulinzi za Pakistan. Kama kuna al iyetumika, anasema C h a u d h r y A h m e d Mukhtar, alitumika kama ‘kachero’; mtumishi wa CIA na unaweza kusema kuwa msaliti wa Pakistan.

Kama alivyonukuliwa Mkuu wa Idara ya Usalama (ISI), Lt-Gen Ahmed Shuja Pasha akisema, yote hayo ikijumuishwa na madai kuwa Usama Bin Laden aliweza kuishi Pakistan kwa miaka 9 bila serikali kujua mpaka alipouliwa na Wamarekani, ni ushahidi tosha kuwa serikali na vyombo vyake vimelemaa na kufeli kabisa.

Akionyesha wasiwasi wake kuwa huenda hiyo i n a t o k a n a n a w e n g i katika watendaji muhimu kununuliwa na kutumikia masilahi ya nchi nyingine badala ya kuitumikia Pakistan, anatoa mfano wa Saeed Iqbal, Kanali wa jeshi mstaafu ambaye alionekana akivinjari eneo lililodaiwa kuwa makazi ya Usama akipiga picha huku akitembea na gari lisilopenya risasi. Anasema Iqbal alitoweka mara baada ya tukio na uchunguzi unaonyesha kuwa alikuwa mtumishi wa CIA.

Akielezea ilichovuna Pa k i s t a n k a t i k a h i k i kinachodaiwa kuwa urafiki na ushirikiano na Marekani ambao ndio kilichopelekea haya ya Abbo�abad, Pasha anasema:

“We are a very weak state, also a very scared state.”

Taifa ambalo limefikia h a t u a y a k u w e z a kutengeneza bomu la nyukilia, limefanywa kuwa “very weak and very scared state.” Na kwamba kufeli huku:

“not so much of specific individual or institutional failure, but with a problem of collective and systemic failure”.

Lakini la kutisha zaidi mkuu huo wa Idara ya Usalama ya Pakistan, Lt -Gen Ahmed Shuja Pasha, anasema kuwa baada ya kufanywa nchi yao ifikie mahali kuwa

sasa ni taifa na serikali iliyofeli na iliyodhalilika, hao hao waliowafikisha hapo sasa wanawakejeli na kuwatukana.

Anasema, wanada kuwa serikali yote ya Pakistan na vyombo vyake vya usalama imenunuliwa na CIA na wanatamba wakisema kuwa kila mmoja wao ana bei yake, tena rahisi sana.

“He also claimed that the US CIA had been able to “deeply penetrate” Pakistani society, quoting a US intelligence officer as having allegedly told him:

“You are so cheap… we can buy you with a visa, with a visit to the US, even with a dinner… we can buy anyone.”

Amenukuliwa Pasha akitoa ushahidi katika Tume hiyo iliyoundwa na serikali ya Pakistan.

“We are a failing state, even if we are not yet a failed state.”

Luteni Generali Ahmed S h u j a Pa s h a a l i s e m a akihit imisha maelezo yake.

Swali la msingi ni je, Pakistan imefikaje hapo? Mchezo wote huu umeanzia katika inayoitwa vita dhidi ya ugaidi. Serikali ya Pakistan wakati huo chini ya Generali Perves Musharaff, iliaminishwa kuwa ndani ya Pakistan kuna magaidi na ikatakiwa kufungua milango yake kwa makachero na askari wa Marekani kusaidia kupambana na magaidi hao. Pakistan ikasifiwa sana na Marekani kuwa ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya ugaidi. Na ikawa inapewa misaada mbalimbali mingi ikiwa ya kikachero na kijeshi. Ikafikia mahali askari na makachero wa Marekani kufanya Pakistan kama uwanja wao wa nyumbani. Wanaweza kufanya lolote bila kuulizwa.

Kupitia ushirika huu, wa n a n c h i w e n g i wa Pa k i s t a n wa m e u l i wa wakiwemo watoto wa M a d r a s a , wa n a f u n z i shuleni , akina mama mitaani, sokoni na mahali pengi ambapo yalifanywa mashambulizi ikidaiwa kuwa wanaopigwa ni magaidi.

Ni kupitia ushirikiano h u u , m a k a c h e r o n a a s k a r i wa M a r e k a n i walifunguliwa milango na kufanya wanavyotaka huku matukio yaliyodaiwa kuwa ni mashambulizi ya kigaidi nayo yakizidi. Kwa maana nyingine, ushirikiano huo, ndio uliozua balaa zaidi kwani wameuliwa watu wengi wasio na hatia,

hasa katika kipindi hiki cha kutumia ndege zisizo na rubani (drone). Kabla ya hapo hapakuwa na mauwaji ya kiwango hicho. Na hii ni moja ya vielelezo kuwa kila ushirika huu ulipoanzishwa, ndio ulileta balaa zaidi kama ambavyo h i v i s a s a I r a q k u n a mauwaji zaidi ya kikabila na kidini, mambo ambayo hayakuwepo kabisa wakati wa Saddam Hussein.

Tumelieleza tukio hili kwa urefu kwa sababu kwa muda mrefu sasa kumekuwa na jitihada za kuisajili nchi yetu kuwa ni nchi yenye makundi ya kigaidi. Juhudi hizi zilianza kwa vitisho na tahadhari zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya balozi za nje hapa nchini au serikali zao. Wakati huo, serikali z e t u , k wa m a a n a ya muungano na Zanzibar, zilikuwa zikifanya juhudi kukanusha habari hizo za kuwepo kitisho cha ugaidi wakisema Dar es Salaam na Zanzibar ni salama kwa hiyo watalii waje.

Hali hiyo imekwenda mpaka sasa imefikia mahali viongozi wetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaimba wimbo huo huo-kuwa kuna kitisho cha ugaidi! Nchi si salama!

Jambo la kukumbukwa na kuzingatia hapa ni kuwa vitisho hivi vilianza, hata al Shabab wenyewe hawakuwepo.

Lakini ukiacha vitisho na tahadhari iliyokuwa ikitolewa kupitia balozi na nchi za nje juu ya hatari ya ugaidi Tanzania na Afrika Mashariki, kulikuwa na zile taarifa ambazo zilikuwa zikipandikiza chuki kati ya Waislamu na Wakristo. Hicho ni kipindi ambapo tulikuwa tukisikia habari za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi ndio yakaibuliwa haya ya al Shabab na tuhuma za kulipua makanisa na kuangamiza watu wa dini nyingine.

Tunachotaka kusema hapa ni kuwa ukitizama taarifa kama zile za madai ya mtoto wa Kiislamu kuingia ubalozi wa Marekani na kigaloni cha mafuta ya taa, madai ya kuingia nchini waliodaiwa magaidi akina Fazul na haya ya sasa hivi ambapo jitihada zimekuwa zikifanyika kuunganisha baadhi ya Masheikh na taasisi za Kiislamu na kinachoitwa ugaidi wa al Shabab au Boko haram;

Inaendelea Uk. 4

Page 3: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

3 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Habari

Mwanafunzi aliza waumini MtambaniM W A N A F U N Z I Abubakar Ally, amewaliza Wa i s l a m u b a a d a y a kuelezea mkasa wa udini unaowakumba wanafunzi wa Kiislamu katika shule ya Sekondari Kahororo, Mkoani Kagera.

Abubakar alisimama mbele ya Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, I jumaa wiki iliyopita, baada ya kutakiwa na Imam Hamza Omari, kutoa ushahidi jinsi kadhia ya Udini, ilivyokithiri shuleni hapo dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu.

Katika maelezo yake Abubakar, aliye muhitimu wa k i d a t o c h a s i t a , amesema kuwa kuna baadhi ya walimu ambao kinyume kabisa na maadili ya kazi yao, wamekuwa wakidhihirisha chuki dhidi ya wanafunzi Waislamu.

Akitoa mfano alisema k u w a y e y e b i n a f s i al ipigwa teke bila ya kosa hali iliyosababisha hata wanafunzi Wakristo kuingilia kati kumtetea.

Alisema, siku ya tukio alikuwa akienda msikitini kuswali I jumaa lakini akazuiwa na mwalimu kwa madai kuwa hakutakiwa kuvaa kanzu.

Alisema, mwalimu wa nidhamu ( Jailo) ndiyo kero kwa wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo, kwani hataki hata kuona Waislamu wakiswali.

“Pale Shuleni kuna Kanisa kubwa sana kwa sababu shule hiyo zamani ilikuwa ni ya Kanisa, lakini sisi kuna chumba tu na hata hiyo adhana yenyewe huadhiniwa taratibu bila kutumia spika lakini bado iinaonekana kuwa ni kero”. Alisema.

Alisema, siku ya Ijumaa h u a m b i wa wa s i t o k e kwenda Msikini mpaka wapate kibali maalum na mwalimu ana uwezo w a k u w a r u h u s u a u kuwakatalia.

Lakini alidai, wenzao Wakristo siku za jumamosi na jumapili ni ruksa kutoka tu kwenda kwenye ibada bila kibali chochote.

“ I la s i s i Wais lamu huambiwa siku ya Ijumaa mpaka tuombe ruhusa kwanza na kupat iwa k iba l i maalumu kwa ajili ya kwenda kuswali

Na Bakari Mwakangwale swala ya Ijumaa”. Alisema Abubakar.

Alisema, wakati wao wakikatazwa kuvaa Kanzu na kofia (Baraghashia) iwe nje au darasani, wenzao Wakristo huvaa rozali wakiwa nje na darasani, bila bughudha yoyote.

A k i e l e z e a m k a s a uliomkumba, Abubakar a l i s e m a , a l i p o k u w a anatoka bwenini akiwa ndani ya kanzu yake, kabla hajamaliza mazingira ya shule alikutana na mwalimu aliye mtaja kwa jina moja la Jailo.

Alisema, aliulizwa na mwalimu huyo kwamba anakwenda wapi, naye alimjibu kwamba leo (siku hiyo) ni I jumaa hivyo anaelekea kuswali.

Abubakar, aliendelea kusimulia mahojiano na mwalimu huyo kwamba alimuuliza kuwa hilo alilovaa ni vazi gani, naye alimjibu kuwa hiyo ni kanzu.

“Akaniuliza, ‘kwani hilo vazi limeruhusiwa kuja nalo hapa shuleni’?

Nikamwambia, ‘katika fomu ya kujiunga hapa shule imeeleza tuje na nguo za nyumbani za heshima, hivyo na hii kanzu ni miongoni mwa vazi la heshima’. Alisema akirejea mahojiano yake na mwalim Jailo.

Akasema, baada ya kumjibu hivyo mwalimu huyo alihamaki, na kuhoji kwa kusema, ‘hilo ni vazi la heshima?’ ambapo alimjibu ‘ndiyo ni vazi la heshima na ndio maana naenda nalo katika ibada’,

Alisema, mwalimu huyo akaendelea kumhoji kama hajawahi kupewa maelezo kuhusu vazi hilo shuleni hapo, huku akimjibu kuwa hajaona sehemu ambayo wamezuiliwa kuvaa vazi kanz

“Mwalimu yule, akaona sasa amwite mwalimu wa nidhamu, alipofika pale nae kwa ukali aliuliza hilo ni vazi gani, nami nikamjibu hii ni kanzu, hapo hapo alirusha teke na kunishambulia katika sehemu za korodani , nikaanguka chini, yeye akaondoka”.

Alisema huku alikilia na kufanya Waislamu waliokuwa wakimsikiliza kugugumia kwa vilio.

A b u b a k a r, a l i s e m a alisikia maumivu makali, jambo ambalo lilifanya

w a n a f u n z i w e n z a k e wengi wakiwa Wakrtisto, kufika katika eneo la tukio na kumuinua na kwenda kumuombea ruhusa i l i wampeleke hospitali.

A l i s e m a , w a l i m u walionyesha kutokuwa tayari kutoa ruhusa. Waligoma k u t o a r u h u s a , j a m b o ambalo liliamsha hasira za wanafunzi.

“Kwa tukio l i le hata Wakristo hawakufurahishwa nalo na ndio walikuwa mstari wa mbele kwa kuwa Waislamu wengi walitoka kwenda kuswali, walisimama kidete wakisema lazima niende hospitali, kwani nilikuwa nalalamika maumivu makali.” Alisema Abubakar.

Alisema, baada ya muda,

alipewa ruhusa na kupewa kiasi cha shilingi elfu kumi kwa ajili ya matibabu huku baadhi ya walimu wakimtaka kutosema kuwa amepigwa na mwalimu bali alieleze kuwa amepigwa na mpira.

A l i s e m a w a l i p o f i k a wal ie leza ukwel i kuwa amepigwa teke na mwalimu, akatakiwa kwenda Polisi kwa ajili ya kupata fomu ya matibabu (PF3), na alipofika Polisi alipewa kisha akarudi hospitali.

“Kufika hospitali, PF3, i l i z u i l i wa k u m b e y u l e mwalimu aliyenipiga alikuwa ameshafika hapo hospitalini cha ajabu wahudumu (manesi) walianza kunishawishi kuwa yaishe tu, kwa kuwa mimi ni mwanafunzi tena nipo kidato

cha sita.” Alisema Abubakar.Alisema, katika mazingira

hayo, hakupewa fomu hiyo ya Polisi na alipoingia kwa daktari baada ya kumueleza tatizo lake alipinga kunipa matibabu bila PF3, na kumtaka aende kuidai.

“Aliniambia niifuate, kwa kuwa wanafunzi wenzagu wal ikuwepo pale , wote tulirudi kwa mhudumu yule (nesi) na kumzonga atoe PF3, akaitoa ndipo nilipoendelea kupata matibabu”. Alisema.

Pamoja na madai hayo, hadi tunakwenda mitamboni, mwandishi wa habari hizi hakuweza kufanikiwa kupata maelezo ya upande wa pili kwa maana ya uongozi wa shule na mwalimu Jailo mwenyewe.

Wakumbukeni kwa DuaWAISLAMU wametakiwa kuleta dua kwa wingi kuwaombea Masheikh wa Uamsho waliowekwa ndani, Allah awape subra na malipo mema kutokana na mtihani uliowakuta.

Wakitoa wito huo kwa nyakati tofauti, baadhi ya Waislamu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’an, Sheria na katiba ya nchi, Masheikh hao hawajapatwa na hatia yoyote na hivyo hawastahiki kuadhibiwa, na kinachowakuta ni moja ya mitihani ambayo Allah ndiye atakayewalipa.

“Kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu, kama wanadamu wangesikilizwa kwa madai yao, wangedai damu na mali za watu wengine. Kwa hiyo ni wajibu wa mdai kuleta ushahidi kuthibitisha madai yake.”

Amesema Ustadh Shakir akisisitiza kuwa mpaka sasa hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuwatia hatiani Masheikh hao na kwamba kuwashikilia bila ya dhamana ni kama kuwaadhibu bila ya kosa kuthibiti.

Katika hali hiyo akasema kuwa, ingekuwa ni vyema kwa walioshikilia mpini na wenye madaraka ya kuwazuiya Masheikh hao, wakatizama upya Sheria zilizopo, iwapo wanachowafanyia Masheikh wa Uamsho ni sawa, haki na ubinadamu.

Akasema, anayasema hayo akihofia kuwa kama kuna namna yoyote ya dhulma, wenye madaraka wasidhani kuwa dhulma hiyo itapita bure bure, lakini wajue kuwa yupo ‘Mfalme wa Siku ya Malipo’ na huyo ndiye Hakimu wa mahakimu.

Na Mwandishi Wetu Ustadh huyo akiongea na mwandishi anasema ameona atoe wito na nasaha hizo kwa sababu hata kama wa n a o wa s h i k i l i a wa n a mamlaka kwa mujibu wa sheria kuamuru mtu awekwe ndani bila ya dhamana, lakini wenye mamlaka hayo wangetakiwa kutizama pia ubinadamu.

“Masheikh wetu wanafunga R a m a d h a n i w a k i w a korokoroni, hatujui hali ya futari, daku na ibada zao za tarawehe na witri, zitakuwaje; n a h a ya wa n a f a n y i wa wakiwa ni watuhumiwa tu, pengine kwa Ramadhani hii wangetakiwa hao wenye madaraka, kama ni Waislamu, wakati wakifuturu na wake zao, wakumbuke kuwa kuna watoto ambao wamekosa huduma ya futari kutoka kwa baba zao na kuna wake ambao wamekosa furaha ya kufuturu na waume zao.”

A m e s e m a m u u m i n i mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Mustafa na kuongeza kuwa “kama mtu amepatwa na hatia na kufungwa, hilo ni jambo jingine, lakini sio katika hali hii ambayo mtu ananyimwa dhamana huku kukiwa na malumbano ya kisheria iwapo ni haki na ni katika sheria kuwafanyia hivyo.”

“Mi nadhani katika hali kama hii ya malumbano, kama ilivyojitokeza katika kesi hii juu ya suala la dhamana, nadhani wenye mamlaka wangeshika ile busara kuwa ni bora ukafanya kosa la kumuacha huru mkosaji (kama ushahidi una utata), kuliko ukamuadhibu mtu asiye na hatia. Wanajisikiaje wakisimama katika tarawehe

wanaswali huku katika fikra zao ikiwajia picha ya watu walio ndani kutokana na kauli na amri zao?” Alisema na kuhoji.

Kwa upande mwingine Ustadh Shak i r ambaye a m e s e m a k u w a y e y e hazungumzi kama mtu mwenye wadhifa katika taasisi yoyote ya Kiislamu, bali kama Muislamu wa kawaida, amesema kuwa anadhani itakuwa vyema kwa taasisi za Kiislamu kutafuta namna ya kusaidia katika jambo hili.

A m e s e m a , l e n g o s i o kuingilia uhuru na mamlaka ya mahakama wala kuvunja sheria, bali kujaribu kufanya kazi ya kiwakil i kuona kama kuna uwezekano wa kurahisisha Masheikh hao kupata haki yao ya dhamana.

“Moja ya mafunzo ya Ramadhani n i ku jenga moyo wa huruma, hebu tuwahurumie wenzetu walio ndani kwa kutizama ni kwa vipi tunaweza kuwasaidia kupata haki yao ya dhamana, itakuwa haionyeshi udugu na mshikamano wa Kiislamu kama tutakaa kimyaa bila kufanya juhudi yoyote.” Amesema.

Waislamu ni kama mwili mmoja ambapo kiungo kimoja tu kikipata tatizo, mwili mzima hupata maumivu, basi tukifutari tuhakikishe kuwa na familia za Masheikh walio ndani nao wamefuturu.

Aidha, kama sheria na taratibu zinaruhusu, basi tuhakikishe kuwa Masheikh na Maimamu wetu walio ndani, nao wanafutari vizuri kama tunavyofutari sisi.

Page 4: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

4 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013HABARI

Kongamano Masjid Tungi - TemekeBaraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania linawaalika wanawake wote

wa Kiislamu katika Kongamano litakalo fanyika Inshaallah Msikiti wa Tungi

Temeke Jumamosi Tarehe 13/07/2013 Saa 2:30 hadi saa 7:00 Mchana ,Mada

swaumu. Tuzingatie Muda. Ukipata Taarifa hii Mwaambie na

mwenzio.

Naibu katibu TaifaBi. Mayasa Sadallah.

Tanzania tusimameInatoka Uk. 2u t a o n a k u wa k i l e kilichofanyika Pakistan n d i o k i n a t a k i k a n a kufanyika Tanzania.

Zinasambazwa habari kuwa kuna mtandao wa magaidi wa al Shabab, lakini hakuna maelezo kuwa wapo wapi, ni akina nani na hawakamatwi n a k u f i k i s h w a m a h a k a m a n i . Tafsiri yake ni kuwa ukishajenga hoja hiyo, siku yoyote panaweza kufanyika shambulio na kumkamata yoyote na kudai kuwa ndio yale makundi ya kigaidi yaliyodaiwa kuwepo nchini. Na hili, hakuna litakapotupeleka ila kwenye machafuko na mauwaji ambayo p e n g i n e i t a k u w a rahisi kuona mwanzo wake, lakini hatma yake itakuwa ngumu kufikiwa.

Mwandishi Murtaza Hussa in ak iandika kutoka Toronto, Canada anatukumbusha akisema kuwa ni wakoloni wa Kibeligiji waliokuwa wakitawala Rwanda waliopandikiza chuki za kikabila kati ya Watutsi na Wahutu, ambapo baadae walipatikana w a p u m b a f u waliozichochea zikazaa mauwaji ya Kimbari m w a k a 1 9 9 4 n a kuangamiza takribani roho milioni moja za Wanyarwanda.

Katika nchi ambazo ukabila hauna nguvu kama nchi za Kiislamu (Kama Pakistan na Iraq) anasema wanatumia u-Shia na u-Usunni. Ambapo kwa nchi kama Tanzania, watatumia Ukristo na Uislamu.

Sasa ni wajibu kwetu s o t e , t u n a p o s i k i a baadhi ya wenzetu wakija na madai kuwa wamekamata komputa mpakato zenye maneno y e n y e k u c h o c h e a kuangamizwa watu wa d i n i n y i n g i n e , t u w a a m b i e , watuonyeshe na sisi tuyasome maneno hayo na watuthibitishie kuwa hawakuandika wao.

Yote hii ni katika

kuchukua tahadhari za kuinusuru nchi yetu maana tunajua kuwa kama kuna mtu anataka kuleta balaa la vita ya wenyewe kwa wenyewe, mlango wa kupit ia Tanzania utakuwa wa kidini. Ni kwa sababu hii, sisi kama chombo cha habari, tunaona tuna dhima kubwa na deni kubwa kwa nchi hii, kuhakikisha kuwa kama kuna chochote tunachoweza kufanya kuiepusha nchi hii na balaa hili, tunalifanya. Ndio maana tunatoa wito kwa Waislamu na Watanzania wote, kuwa macho na wapiga filimbi hawa wa ugaidi pamoja na watu watakaopita mitaani na Misikitini wakitangaza sera za ki-al Shabab.

Kuyasema haya ndiyo Jihad na zawadi yetu An nuur kwa nchi hii, kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla. Na kama kutakuwa na baya lolote litakalotufika, basi ni kwa ajili ya kuiepusha nchi hii na balaa tunaloliona mbeleni.

Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi. Allah anashuhudia kuwa tumefikisha. Na hatukufanya haya kwa nia ya kuleta uchochezi, bali kwa lengo la kuinusuru nchi hii na maafa.

T u m e f a n y a h a y a kuwanusuru waja wa Allah wasitumbukizwe katika mchezo wa kuuwana au kuuliwa ili kutimiza malengo ya mabeberu kama inavyotokea Syria, Iraq, Afghanistan, Pakistan, Yemen na Somalia.

Tu m e ya s e m a h a ya tukihofu , i s i j e kuwa na s i s i tukachezewa k a m a i l i v yo c h e z e wa Pakistan, mwisho wa y o t e w a n a t u k a n w a wakiambiwa:

“You are so cheap… we can buy you with a visa, with a visit to the US, even with a dinner… we can buy anyone.”

Tu n a a m i n i k u wa Watanzania ni watu na heshma zao, wazalendo w e n y e k u j a l i u t u wao na ubinadamu wao. Hawatakubal i kufikishwa huko.

Tumefikisha. Isi je k u s e m w a k u w a hatukusema.

Wabillahi Tawfiq

WA I S L A M U w a m e a s w a kujenga Misikiti kwa ajili ya kuimarisha umma wa Kiislamu na si kubomoa, kwani Misikiti kama hiyo isipewe nafasi katika jamii.

Hayo yamesemwa na Sheikh Abdulkadir Mohammed, akitoa nasaha zake mbele ya Waislamu katika uzinduzi wa Masjidi Taqwa, Ilala Jijini Dar es Salaa, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Alisema, Misikti ambayo ipo kwa ajili ya kuweka mikakati ya kubomoa jamii, Misikiti hiyo haina nafasi katika jamii, bali msikiti ijengwe kwa ajili ya manufaa kwa umma na jamii kwa ujumla.

“Misikiti ijengwe kwa ajili ya kuimarisha umma na si kubomoa, kwani hata Mtume alisema, Misikiti hiyo haina nafasi katika jamii”. Alisema Sheikh Mohammed.

Shkh. Mohammed, alisema Msikiti ni sehemu ya kujenga watu kielimu, kwamba iwe ni kituo cha elimu isiwe ni sehemu ya kiibada tu.

Alisema, katika tukio moja

Misikiti iimarishe umma sio kuleta faraka-ImamNa Bakari Mwakangwale Mtume (s a w) aliingia Msikiti

kukuta vikundi viwili, kimoja kikimtaja Mwenyezi mungu, ikiwa si jambo dogo hata kidogo na kikingine kikijisomea.

“Mtume (s a w) baada ya kuwaona alichagua kundi la wanaosoma na akasema hao wa n a m u o m b a M we n ye z i Mungu, huenda wakakubaliwa au wasikubaliwe katika wanayo yaomba, lakini hawa wanaosoma nafasi ya kukubaliwa ni kubwa zaidi, kwa sababu wanachofanya ni kitu bora”. Alisema Shkh. Mohammed.

A i d h a a l i s e m a , n a f a s i nyingine ya Msikiti ni kujenga amani kwani Uislamu unahimiza sana amani kutona na Mwenyezi Mungu kushusha aya kadhaa zikitaja amani.

Sheikh Mohammed, alisisitiza kwamba Misikiti isiwe sehemu ya mizozano, magomvi na mifarakano, kuvurugana baiana ya Waislamu kwa Waislamu au na wanajamii.

Alisema, Mtume katika kuonyesha heshima ya Misikiti alifika akasema kwamba ndani ya Msikiti anayesoma Qur an na aisome pasi ya kunyanyua sauti

yake kiasi kwamba akamkera mwingine.

“Sasa ikiwa tu kuisoma Qur an, kwa kunyanyua sauti Mtume hapendi vipi sasa ikiwa utanyanyua sauti kwa mizozano na faraka ndani ya Msikiti, kosa kubwa sana hatuna budi Waislamu kuepukana nalo.” Aliasa.

A k i e l e z e a n a f a s i y a Msikiti katika Uislamu, Shkh. Mohammed, alisema mara tu baada ya Mtume kufika Madina, akitoka katika mji wa Makka, cha kwanza alichokifanya ni kujenga Msikiti.

“Hii ni kuonyesha kwamba Msikiti ni kituo kikuu cha watu, kwani maswahaba kama Ally, Othama na Abubakar walijengwa kiimani Msikitini.” Alisema Shkh. Mohammed.

Alisema, ukiona Msikiti umeimarishwa ujue watu hao ni wale waliojengeka kiimani, kwani katika surat Tawba Allah anasema kuwa wale wanaoimarisha Miskiti ya Allah ni wale ambao wameamini siku ya mwisho na kusimamisha swala na hao ndio wanaoimarisha Misikiti.

WAISLAMU wametakiwa kuupokea Mwezi Mtukufu w a R a m a d h a n i , k w a kuzingatia mafundisho ya Uislamu na miiko ya ibada hiyo ili waweze kuwa wachamungu.

Wito huo umetolewa n a I m a m w a M a s j i d i Mtambani, Ustadhi Suleiman, akiwahutubia Waislamu

Tufanye mema katika RamadhaniNa Bakari Mwakangwale katika hotuba yake ya swala

ya Ijumaa wiki iliyopita.Imam Suleima, alisema

Waislamu tayari wameukabili M w e z i M t u k u f u w a Ramadhani hivyo ni wajibu wao kuzingatia na kufuata misingi ya ibada hiyo ili waweze kufikia lengo la funga.

“Waislamu mwezi wa Ramadhani umetukabili, mwezi ambao umekusanya

kila aina ya kheri ambazo unazozijua na usizo zijua, tuupokee Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa bashasha ili mwisho tuwe ni wenyewe kufutiwa madhambi na kufikia lengo la funga.” Alisema Imam Suleiman.

Alisema, ukifuatilia katika Qur an, kheri za Mwezi wa Ramadhani, zilizomo kwa siku moja, mbili hata mwezi mzima hutoweza kuzielezea zikaisha, hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuhimizana, kukumbushana na kuhamasishana ili kuweza kuzipata kheri hizo.

Akisherehesha hadithi ya Mtume (s a w), Imam S u l e i m a n , a m e s e m a miongoni mwa anayepata khasara katika Mwezi huu ni yule ambaye inamdiriki R a m a d h a n i , m p a k a inamalizika hakufutiwa madhambi yake.

“Mimi na wewe, je tutakuwa katika kundi hili au tutakuwa ni wenye kushindana katika kheri ili tuweze kuepukana kuwa katika kundi la wenye kupta hasara.” Alisema Imam Suleiman.

Alisema, Mwezi huu kila ulipokuwa ukimfikia Mtume (s a w), alikuwa akiacha shughuli zake zote akifunga kibwebwe kufanya ibada kuliko alivyokuwa akifanya siku za kawaida.

Page 5: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

5 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Habari za Kimataifa/Tangazo

Ahlul Daawa Hajj And Travel AgencyINAPENDA KUWA TAARlFU MAHUJAJI WAKE WOTE NA WAISLAMU KWA JUMLA KUA:-

IDADI YA MAHUJAJI WAO WA MWAKA HUU 2013 IMEPUNGUZWA KUTOKA MIA TATU MPAKA MIA MOJA NA SABINI TU. KWA HIVYO;- (a) WALE WOTE W ALIOJIANDIKISHA W A WAHl KUMALIZA KULIPIA GHARAMA ZAO. (b) W ALIOJIANDIKISHA TU NA HAW AJALIPIA W AJE KULIPIA AU TUT A WAONDOSHA KWENYE ORODHA NA KUW APA NAFASI W ALIOKUW A TAYARI. (c) KUWASILISHA PASSPORT AU KOPI ZA PASSPORT KWA MUDA HUU. (d) PICHA MBILI PASSPORT SIZE KW A AJILI Y A VISA. 2. (a) BEl YETU NI US DOLA 3550 TU.

(b) UKIWAHI KULIPIA SA SA NA KUMALIZA TARATlBU ZOTE PUNGUZO NI ASILIMIA SITA KWA HIVYO UT ALIPIA US DOLA 3337 TU NA KABLA Y A TAREHE 25 JULAY 2013. 3. KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI KWAO;-

(a) DAR ES SALAAM MTAA W A DOSI NA MKADINI NYUMBA NAMBA 26 MKABALA NA SHOW ROOM Y A MAGARI TEL 0713 730444 AU 0785 930444 AU 0773 930444. (b) ZANZIBAR MTAA WA RAHA LEO TEL 0777484982 AU 0777413987 AU WASILIANA NA. ( c) MAALIM SElF HUMOUD KIJICHI ZANZIBAR TEL 0777417736. (d) ABDALLA SALEH MAZRUI (HOKO) TEL 0715724444 AU 0773 724444 AU 0784 724444 (e) SHEIKH DAUDI KHAMIS SHEHA PEMBA 0777 679 692(f) SHEIKH ABUBAKARI MAULANA MARKAZ KIWALANI 0784 453 838 NA BEl NAFUU KULIKO WOTE NA HUDUMA BORA KULIKO WENGI USISAHAU AHLUL DAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

REUTERSMsemaji wa kiongozi wa mpito nchini Misri, Adly Mansour, amearifu kuwa mchakato wa kumpata Waziri Mkuu wa taifa hilo bado unafanyika.

Wakati kiongozi huyo akitoa kauli hiyo kumekuwa na tetesi za kutaka kuteuliwa Dk. Mohamed Elbaradei, ambaye amekosolewa vikali kwa kudaiwa kutofaa kushika wadhifa huo.

Taarifa za ndani zilimtaja Dk. ElBaradei , ambaye alikuwa kiongozi wa zamani wa masuala ya usimamizi wa nyuklia katika Umoja wa Mataifa-UN kushika wadhifa huo.

Ta a r i f a z a k u t a k i wa kuteuliwa kwake zimekuwa zikikosolewa kwa madai kuwa kiongozi huyo asingefaa kwa chochote.

Hata hivyo Dk. Mohamed al Baradei ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini humo, amekataa pendekezo la kuwa

AU yasitisha uanachama wa MisriTarehe ya Uchaguzi yatangazwaElBaradei apingwa, ajitoa

Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.

M b a l i n a k u k a t a a pendekezo hilo, Al-Baradei amependekeza wadhifa huo uchukuliwe na Ziyad Bahaud-Din. Aidha kiongozi huyo wa upinzani, ametaka kuchukua wadhifa wa Naibu wa Waziri Mkuu katika masuala ya kisiasa.

Wakati hali ikiwa hivyo, Rais wa serikali ya mpito ya Misri Adly Mansour, a m e t a n g a z a k w a m b a uchaguzi wa Bunge nchini humo utafanyika mwaka 2014.

Rais Mansour ameongeza k u wa , m a r a b a a d a ya kufanyika uchaguzi wa Bunge, itatangazwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa Rais. Rais wa serikali ya mpito ya Misri ana kipindi cha miezi sita cha kuifanyia marekebisho kat iba ya nchi hiyo ambayo hivi sasa imesitishwa.

Wakati huohuo, Msemaji wa Rais wa serikali ya mpito wa Misri amesema kuwa, matukio yaliyojiri jana mjini Cairo hayawezi kuzuia uundwaji wa serikali mpya.

Ahmad al Musalmani, amesema kuwa mapigano yaliyotokea kati ya wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin na vikosi vya usalama mbele ya makao ya Gadi ya Rais Mashariki mwa Cairo, hayawezi kuzuia juhudi za kuundwa serikali mpya au kutekelezwa mpango uliobuniwa na jeshi la nchi hiyo.

Ta k r i b a n w a t u 5 3 wameuliwa wengi wao wakiwa ni wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood na kiongozi aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi, nje ya kambi ya Jeshi jijini Cairo mwanzoni mwa wiki.

Chama cha Morsi, Muslim Brotherhood, kilichoongoza maandamano dhidi ya Jeshi na Mapinduzi dhidi ya Kiongozi wao, wamelitupia lawama Jeshi na Polisi kwa kupoteza maisha ya watu hasa wafuasi wa Chama chao.

I k h wa n u l M u s l i m i n imesema kuwa, wafuasi wake wameuawa wakati jeshi la Misri lilipoushambulia umati wa watu waliokuwa wameketi chini nje ya kambi

zao wakipinga kitendo c h a k u p i n d u l i wa R a i s Muhammad Morsi.

Watu wal ioshuhudia wameeleza kuwa, jeshi lilitumia silaha za moto kuwatawanya wafuasi wa Muhammad Morsi katika mji wa Nasr, Mashariki mwa Cairo.

Jeshi nalo limetupa lawama kwa makundi waliyoyaita ya kigaidi. Nacho chama cha upinzani Freedom and Justice (FJP), kimetoa wito wa kupinga wale wote wanaojaribu kuiba mapinduzi yao kwa nguvu.

Wa f u a s i wa M u s l i m Brotherhood wameapa kuzidi kuendesha maandamano ya amani mpaka kiongozi wao atakaporejeshwa katika nafasi yake. Waandamanaji pia wametaka aachiliwe huru yeye na baadhi ya viongozi wa Ikhwanul Muslimin wanaoshikiliwa na jeshi la nchi hiyo.

FJP kimeiomba Jumuia ya Kimatai fa kuingi l ia kati kuhakikisha mauaji yanakoma nchini humo na kuzuia hali ya mambo kwani inaonekana itakuwa mbaya zaidi kama ilivyo nchini Syria.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amekemea mauaji yaliyotokea nchini Misri na kutoa wito kufanyika uchunguzi ulio huru ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya Sher ia waliohusika.

M o r s i a n a y e d a i w a k u s h i k i l i wa n a j e s h i ,

hajatokea hadharani tangu a l ipopindul iwa , l ak in i imearifiwa kuwa amewataka wafuasi wake kupigania haki yao kwa kiongozi wa l i ye m c h a g u a k a t i k a uchaguzi wa kidemokrasia.

Tayari Umoja wa Afrika AU umesitisha uanachama wa Misri katika Umoja huo na kusema, hautambui m a p i n d u z i h a y o k w a sababu Morsi alichaguliwa kidemokrasia baada ya kuondolewa kwa Rais wa zamani Hosni Mubarak.

Wakati Katibu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon, akiwataka viongozi kuhakikisha waandamanaji wa n a l i n d wa n a k u wa salama, serikali ya Marekani na mataifa makubwa nayo imeingilia kati kwa kuwataka viongozi wa Misri kukomesha ghasia.

N a ye R a i s V l a d i m i r Putin wa Urusi, ameonya juu ya hatari ya machafuko ya n a y o e n d e l e a n c h i n i M i s r i k u wa ya n a we z a kuitumbukiza nchi hiyo k w e n y e m a p i g a n o y a wenyewe kwa wenyewe.

Ra is Put in amesema tayari Syria imetumbukia vya kutosha katika vita vya ndani na kuwa, jambo la kusikitisha ni kuona hatari ya kutumbukia Misri katika mgogoro kama huo.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya siasa wanabainisha kuwa, kuangushwa kwa serikali ya Morsi imekuwa ni faraja kwa mataifa ya Magharibi kwani hawakuwa wakimuunga mkono Morsi na wala hakuwa chaguo lao.

MILANGO yafunguka kwa Edward Snowden ya kupata hifadhi katika mataifa kadhaa ya Amerika Kusini.

Bolivia imekuwa nchi ya tatu kujitolea kumuhifadhi Edward Snowden, huku Rais wa nchi hiyo Evo Morales, akisema yupo tayari kumuhifadhi mkimbizi huyo kama akihitaji.

Bila sjaka hatua hiyo ya Rais Morales, ambaye ni mpingaji mkubwa wa siasa za mataifa ya kibeberu, inakuja kufuatia ndege yake kukamatwa na kukaguliwa nchini Ufaransda hivi karibuni, ikidaiwa kuwa ilikuwa inasadikiwa kumbeba Bw. Snowden.

Hatua hiyo iliwakasirisha s a n a w a n a n c h i w a Bolivia, wakidai Rais wao kadhalilishwa. Hali hiyo i l i i l a z i m i s h a U f a r a n s a kuomba radhi kwa Bolivia kufuatia tukio hilo.

Hatua hiyo ya Bolivia inaongeza matumaini kwa Snowden kwamba huenda akaweza kuondoka Moscow, ambapo amekwama kwa zaidi ya siku 14, kufuatia kutafutwa na Marekani kwa kosa la kuvujisha siri za kijasusi za Taifa hilo.

Nafasi hiyo inakuja ikiwa ni muda mfupi tu, tangu Rais wa venezuela Nicolas Maduro, kuthibitisha uamuzi wa serikali yake kumpatia hifadhi ya kisiasa mfanyakazi huyo wa zamani wa shirika la kijajusi la CIA, Edward Snowden, anayesakwa baada ya kuvujisha siri za ndani za

Matumaini ya Snowden kupata hifadhi yaongezeka

Marekani.Maduro ameweka wazi

uamuzi huo wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Venezuela, yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.

Rais wa Nicaragua Daniel Ortega, naye amesema kuwa nchi yake inaweza kumpa hifadhi salama Bw. Edward snowden akihitaji.

Mlolongo wa nafasi za kupata hifadhi kwa jasusi huyo wa zamani, unakuja baada ya kukataliwa na mataifa mengi kati ya 21 ambayo Bw. Snowden aliomba hifadhi juma lililopita.

Snowden amekuwa katika Jijini Moscow toka alipowasili akitokea Hong Kong kwa takribani majuma mawili yaliyopita.

Snowden anayejitahidi k u e p u k a m k o n o w a Marekani, alituma maombi ya hifadhi kwa takribani nchi 27, lakini nchi nyingi za Ulaya zimekataa ombi lake huku zile za Amerika Kusini zilizoonyesha nia ya kumpokea.

S a k a t a l a S n o w d e n limeendelea kuzua utata katika siku za hivi karibuni, ambapo Marekani imeendelea k u h a h a k u h a k i k i s h a inamtia nguvuni ili akajibu mashtaka yanayomkabili kufuatia kuvujisha siri za ndani za shirika la kijasusi la CIA, kwamba limekuwa l ikirekodi mawasi l iano mbalimbali yanayofanywa ya ki-electronic.

Page 6: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

6 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013TANGAZO

www.amanabank.co.tz

Katika mwezi Mtukufuwa Ramadhan matawi

yetu yatafanya kazikuanzia Saa 3 asubuhi

hadi Saa 9 alasiri kila siku

Tunawatakiamwezi wa

Kheri na Baraka

Ramadhan Kareem

Main BranchGolden Jubilee TowerTel: +255 22 2129014Fax:+255 22 2129013

Tawi la NyerereJengo la DRTCTel: +255 22 2863724Fax: +255 22 2863725

Tawi la TandamtiKariakoo(Mkabala na soko)Tel: +255 22 2185474Fax: +255 22 2185475

Tawi la LumumbaKariakooTel +255 22 2180101fax +255 22 218410

Tawi la ArushaJengo la Hugo PlazaTel: +255 27 254 7496Fax: +255 27 254 7497

Tawi la MwanzaBarabara ya KenyattaTel. +255 282 541 921Fax: +255 282541922

Dar es Salaam Arusha MwanzaNEWNEWNEW

Page 7: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

7 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Makala/Tangazo

K A T I K A j u m l a y a h a b a r i k u b w a zilizopewa umuhimu m k u b w a m w i s h o n i mwa wiki iliyopita ni ile ya kukamatwa mtu mmoja katika mpaka wa Tanzania na Malawi akituhumiwa kwa kosa la ki-Uhamiaji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa n a M k u r u g e n z i w a Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na hati mbili za kusafiria, moja ya Tanzania na nyingine ya Uingereza.

Katika hati ya Tanzania,

Bomu Kanisani Arusha:

Kesi ya Victor imeishia wapi?Uchunguzi tulioahidiwa umebaini nini?Tuzingatie aliyosema DCI Manumba

Na Omar Msangi AB 651926, mtuhumiwa ametajwa kwa jina la Adili Ally Patel wakati katika ile ya Uingereza jina ni Iqbal Hassan Ally.

Habari zaidi za DCI Manumba zinasema kuwa waliwasiliana na Serikali ya Uingereza ikathibitisha kuwa Iqbal Hassan Ally ni raia wa Uingereza na kwamba mtu huyo anatafutwa kwa tuhuma za ugaidi.

D C I M a n u m b a aliendelea kudai kuwa mtuhumiwa Iqbal Hassan Ally alikutwa na komputa mpakato (lap top) ambayo ilipochunguzwa ilikutwa na maneno ya kukashifu dini nyingine.

“Baada ya kushukiwa na kupekuliwa, alikutwa na…komputa mpakato yenye maandishi mengi ya kichochezi dhidi ya dini asizoziabudu. Maneno katika komputa yake yanasisitiza kuteketezwa k w a w a t u w a d i n i nyingine (hakuzitaja).” Amenukuliwa Kamishna Robert Manumba akidai.

D C I M a n u m b a akaongeza kudai kuwa maneno kama hayo ya uchochezi na kutaka kuteketezwa watu wa dini nyingine, yalikutwa pia kwa mwanafunzi a n a ye d a i wa k u s o m a

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.Inaendelea Uk. 8

Page 8: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

8 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Makala

Kesi ya Victor imeishia wapi?Inatoka Uk. 7Sudan ambaye anadaiwa pia kuwa mshirika wa Iqbal.

Katika kutoa tahadhari juu ya kitisho cha ugaidi, tuk io la kukamatwa M u i n g e r e z a h u y o , liliunganishwa na mabomu yaliyolipuliwa Arusha na DCI Manumba akaenda mbali kwa kuunganisha na kitisho cha Al Shabab na Boko Haram.

Alisema, habari za ki-intelijensia zinaonyesha k u w a Ta n z a n i a s i o sa lama kutokana na kuwepo vikundi vya kigaidi vinavyojificha chini ya mwavuli wa dini na kwamba hivi sasa kuna taarifa za kuwepo “kikundi cha kigaidi cha al Shabab, ambacho kimekuwa kikizunguka A f r i k a M a s h a r i k i , kutafuta mwanya wa udhaifu na kushambulia.” (HABARILEO)

Kutokana na taarifa hizi za DCI Robert Manumba, Shirika la Utangazaji BBC nalo li l iremba habari hizo kwa mtindo wake na kuziunganisha na mabomu ya Arusha.

“Authorities in Tanzania are concerned at the growth of an Islamist movement accused of links to Somalia’s al-Shabab.”

Zilisema taarifa kama zilivyopatikana katika mtandao zikisherehesha habari za kukamatwa Ally na kuzihusisha na mabomu ya Arusha na kuhitimisha kwa madai kuwa mwisho wa siku ni kitisho cha “Islamists” (Waislamu) walio na uhusiano na al Shabab.

Kwa upande mwingine baadhi ya vyombo vya h a b a r i h a p a n c h i n i , Jumamosi viliibuka na habari vikidai kuwa gaidi limekamatwa Tanzania.

“ G a i d i m b a r o n i ” , n d i v yo l i l i v yo r i p o t i gazeti la NIPASHE huku l ikikoleza na kichwa kidogo kinachosema, “ M t a n z a n i a a d a k wa akidaiwa kumsaidia.”

H a t a h i v y o , k w a mujibu wa taarifa ya gazeti la HabariLeo la Jumamosi Julai 6, 2013 ukurasa wa 31 ambao kwa kawaida ni ukurasa wa michezo, imeelezwa kuwa Muingereza huyo amepandishwa kizimbani kat ika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu,

akiunganishwa katika kesi ya wizi wa hati 26 za kusafiria.

Iqbal anaunganishwa katika kesi hiyo kwa sababu hati aliyokuwa

nayo inadaiwa kuwa m i o n g o n i m wa h a t i zilizoibwa kutoka Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Wakati hayo yakijiri,

bado Watanzania wapo kizani juu ya lile bomu lililolipuliwa katika Kanisa Arusha na kuuwa watu watatu. Katika tukio hilo lililotokea Mei 5, 2013

Victor Ambrose Calist alikamatwa akituhumiwa kurusha bomu kwenye K a n i s a K a t o l i k i l a Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha, na alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashitaka 21 ya kuua na kujaribu kuua.

Mbele ya Hakimu Mkazi, D e v o t h a K a m u z o r a , mtuhumiwa huyo, Victor Ambrose (20), dereva wa Bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo, A r u s h a a l i s o m e w a mashitaka hayo yakiwamo matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki katika tukio hilo lililotokea Mei 5, mwaka huu.

Mawakili wa Serikali, Zachariah Elisaria na H a r u n a M a t a g a n e walidai kuwa Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua.

Kuacha taarifa hizo za awali za kufikishwa mtuhumiwa mahakamani, bila kuathiri mwenendo wa kesi mahakamani, bado hakujasikika taarifa zozote za uchunguzi kama Serikali ilivyokuwa imeahidi kuwa itafanya uchunguzi na kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo la kigaidi.

Mtuhumiwa ni nani, amefanya peke yake au kuna mtandao wa ndani pekee au ndani na nje ya nchi. Mtandao una ukubwa gani na unawahusisha watu gani. Je, nini malengo, siasa za ndani au za kimataifa au kutaka tu kuleta vurugu. Je, bomu hilo linahusiana kwa namna yoyote na taar i fa z inazoto lewa kila uchao kuwa kuna chuki za kidini na hizi za sasa za DCI Manumba kuwa kuna ‘komputa mpakato zenye maneno y e n y e k u h a m a s i s h a kuangamizwa watu wa dini za watu wengine.’

Hayo ni baadhi ya mambo yal iyotakiwa kufanyiwa uchunguzi na kufahamika. Lakini mpaka leo kimyaa!! Na hata huko mahakamani, haijulikani nini kinaendelea maana inaonekana jambo lenyewe l imekuwa siri kubwa toka siku ya mwanzo mtuhumiwa alipofikishwa mahakamani . Baadhi ya taarifa zinadai kuwa

JULAI 7, 2005 yalifanyika mashambulizi yaliyodaiwa ya kigadi katika jiji la London. Mashambulizi hayo yaliyotokea katika vituo vya gari moshi, tena katika muda uliokuwa na watu wengi, yalidaiwa kufanywa na Waislamu watatu raia wa Uingereza wenye asili ya Pakistan na mmoja mwenye asili ya Jamaica aliyefanya kusilimu.

Tukio hi lo l i l ipigiwa zumari sana na likafanya ule mshikamano wa Marekani na Uingereza katika vita dhidi ya ugaidi kuimarika zaidi. Viongozi wa Uingereza wakatamba na kupata kupumua wakijenga hoja kuwa wana kila sababu ya kupigana huko Iraq na Afghanistan ili kuzuiya magaidi kuingia London na Ulaya kwa ujumla.

Unapozungumzia ugaidi

Mabomu London 7/7Uingereza, katika ulimwengu huu wa leo wa ‘crusade’ iliyotangazwa na Geoge W Bush baada ya Septemba 11, 2001; “London Bombing” ndio tukio pekee kubwa linalopigiwa ngoma sana.

Hata hivyo, hata kabla ya sherehe ya vyombo vya habari vyenye mrengo wa kuchangamkia habari za kuwabambika Waislamu ugaidi haijamalizika, watu wenye ak i l i zao huru , walianza kuhoji na kuonyesha mashimo yanayozua wasiwasi wa kuwepo usanii katika tukio hilo.

Wachambuzi mbalimbali wa n a j e n g a h o j a k u wa shambulio hilo lilikuwa la kupangwa ili kuwaunganisha Waingereza katika kuunga mkono Serikali yao katika vita Iraq. Katika kujenga hoja zao wanasema kuwa shambulio hilo lilitanguliwa

na kuvuja habari kutoka Ofis i ya Wazir i Mkuu, Uingereza, kwamba George Bush, aliliongopea Bunge la Congress katika madai yake kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamizi ili kupata kibali cha kuvamia Iraq.

Ni baada ya kuvu ja habari hizo, wananchi wa Uingereza walizidi kupaza sauti wakitaka wanajeshi wao warejeshwe nyumbani. Blair alikuwa katika hali ngumu na Bush naye alikuwa katika wasiwasi mkubwa wa k u m k o s a m s h i r i k a wake mkuu kule Iraq na Afghanistan.

Ni ka t ika mazingi ra hayo, likatokea shambulio la 7/7 London na kwa muda likabadili hali ya hewa. Waingereza wakawa na hasira dhidi ya Waislamu na

Inaendelea Uk. 9

KUMEKUWA na kauli nyingi sana kuhusu al Shabab, lakini nyingi zikitoa taswira kuwa hiki ni kikundi cha kigaidi ambacho kimeanzishwa rasmi kwa lengo la kufanya ugaidi Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, na hata kimataifa. Al Shabab p a m o j a n a a l Q a i d a , i m e k u w a m i s a m i a t i inayotumiwa kuwakilisha unaodaiwa kuwa Ugaidi. Ukisikia maneno ‘Islamists’ au Waislamu wenye siasa/msimamo mkal i , bas i hao mara nyingi utasikia ikidaiwa kuwa wanahusiana na ama al Shabab au al Qaidah.

Taarifa ya Mkurugeni wa Upelelezi wa Makosa ya J inai nchini , Robert Manumba kwamba Tanzania kuna kitisho cha magaidi wa al Shabab wanaovinjari kutafuta shabaha za kupiga, ni ushahidi kuwa hapa nchini, rasmi inachukuliwa kuwa al Shabab ni kundi la kigaidi lililosambaa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kufanya ugaidi na kwa namna nyingine kwamba wana washirika wao nchini ambao ndio hao wanaodaiwa kubeba komputa mpakato zinazohimiza kuangamizwa

Nani al Shababwatu wa dini nyingine.

Katika hali kama hii kuna kila sababu kwa Waislamu kwanza kujua hali hii, pili kujua kwa uhakika nani al Shabab na tatu kuchukua tahadhari, wasije wakajikuta wakitumiwa bila kujua na kujiangamiza kwa mikono yao wenyewe.

Nani al Shabab, tujiulize k a m a a n a v y o j i u l i z a C h r i s t o p h e r A n z a l o n e anapouliza: “Who are Somalia’s ‘al-Shabab?” (Wednesday, August 3, 2011).

Christopher Anzalone ambaye ni mtafiti katika kitengo cha Islamic Studies, Chuo Kikuu cha McGill, amejiuliza swali hili kufuatia kauli nyingi zinazotolewa kuwahusisha al Shabab na ugaidi pamoja na madai kuwa wao ni ndugu moja na al Qaida.

Baada ya utafiti wake Christopher anasema kuwa k u n a u wo n g o m w i n g i unasambazwa kuhusu al Shabab ikilinganishwa na ukweli juu ya kundi hilo.

Ukweli unaoepukwa na wengi wanaopiga propaganda ya al Shabab ni wa namna mbili: Moja ni kuwa al Shabab ni taasisi ndani ya Somalia ambayo inapigania Somalia kutawaliwa na Wasomali

wenyewe na muhimu zaidi i tawaliwe na Sheria za Kiislamu (Shariah). Al Shabab hawataki kuona serikali kama iliyopo hivi sasa wanayodai kuwa ni serikali kibaraka inayowakilisha masilahi ya mabeberu. Na kwa hiyo hawataki kuona majeshi ya nje yakiingia Somalia kusaidia kuiweka na kuilinda serikali hiyo wanayodai kuwa ni kibaraka wa madui wa Somalia.

U k w e l i w a p i l i usiozungumzwa ni kuwa waliopandikiza machafuko yaliyopo hivi sasa Somalia pamoja na kuibuka al Shabab, ni mabeberu wakiitumia Ethiopia. Ni maarufu kwa walimwengu wote kuwa baada ya vurugu, ujambazi, mapigano, mauwaj i na kukosekana serikali kwa zaidi ya miaka 15, ambapo juhudi za kikanda na kimataifa zilifeli kabisa kuleta amani; Wasomali wenyewe walifikia mahali wakapata ufumbuzi.

Kabla ya kurejea amani kwa muda, Somalia ilikuwa imeshikiliwa na wababe wa kivita (warlords) jumuiya ya kimataifa ikiwa imeshindwa kabisa kuleta amani.

I l ikuwa ni baada ya Jumiya ya Kimataifa na jeshi

Inaendelea Uk. 9 Inaendelea Uk. 9

Page 9: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

9 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Makala

Kesi ya Victor imeishia wapi?Inatoka Uk. 8mtuhumiwa alishapewa dhamana.

Pengine badala ya kutegemea taarifa za kupewa na Uingereza na washirika wao na kisha kuibuka na taarifa za kuwatisha Watanzania juu ya al Shabab na komputa mpakato zenye habari za kutaka watu wa dini nyingine kushambuliwa n a k u a n g a m i z w a , tungezingatia kwanza taarifa zilizotokana na uchunguzi wetu wenyewe k a t i k a k u k a m a t w a mtuhumiwa Victor Calist Ambrose na uchunguzi wa lile bomu lililolipuka katika mkuano wa CHADEMA Arusha na kuuwa watu watatu.

Nani Victor, bomu analotuhumiwa kurusha kalipata wapi, kapewa na nani, nani wapo nyuma yake na mambo kama hayo. Au kama si yeye aliyelirusha kutokana na ushahidi utakaowasilishwa m a h a k a m a n i , l a k i n i ukweli unabaki kuwa kuna bomu lilirushwa Kanisani likauwa watu. Nani alihusika? Kwanini? Kwa malengo gani?

Kama tuna nia ya kujua ukweli juu ya kitisho cha ugaidi Tanzania, na hakuna agenda ya siri, uchunguza juu ya bomu la Arusha, na tukiufanya sisi wenyewe bila kutegemea akili na maelekezo ya watu wengine, ingetusaidia sana kuliko hizi habari za kuambiwa na Uingereza/FBI. Na sababu yake ni moja tu lakini ya msingi na yenye kujitosheleza:

‘ H a wa t u n a o d h a n i kuwa wana utaalamu hata tukawaita kutusaidia, washapoteza s i fa ya kuaminika, hasa katika m a t u k i o k a m a h a ya yanayodaiwa kuwa ya kigaidi.’

Mpaka hivi sasa lile tukio la “London bombing” limekuwa mwiba kwa serikali ya Uingereza kutokana na maswali na ushahidi unaoibuka kujenga wasiwasi kuwa huenda tukio lile lilikuwa la kupangwa na serikali yenyewe.

“Terror Expert: London Bomber Was Working For MI5

Khan used as informant for security services”.

“What’s Behind the London A�acks?”.

“Report: Israel Was Warned Ahead of First Blast.”

“7/7 links with British intelligence agencies don’t

end with Khan. Terror expert John Loftus told Fox News.”

“Dayside show that alleged London bombing m a s t e r m i n d H a r o o n Rashid Aswat was an MI6 intelligence asset that British security helped protect and hide before the bombings.”

“The bombing of the London Underground was a false-flag operation designed to keep the West mired in war. Don’t believe otherwise.”

Hivi n i baadhi ya vichwa vya habari na baadhi ya sehemu za makala na uchambuzi wa wataalamu mbalimbali

wakihoji na kutoa hoja zao madhubuti kuonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio linalodaiwa la kigaidi lililotokea London Julai 7, 2005 ni la kupangwa na kwamba lengo kubwa ilikuwa ni kuwaunganisha wananchi wa Uingereza na Ulaya kwa ujumla

w a m u u n g e m k o n o Waziri Mkuu Tony Blair katika kuendelea kuweka wanajeshi wa Uingereza kule Iraq na Afghanistan. Wakati huo wananchi wa Uingereza walikuwa wameanza kuchachamaa kupinga vita Iraq.

K w a m u j i b u w a wachambuzi hao, kipigo cha kweli cha kigaidi, n a u k a w a h u s i s h a watuhumiwa wa Kiarabu/Wahindi, (Waislamu), kingeweza kuwafanya Waingereza kuona mantiki na umuhimu wa wanajeshi wao kupigana Iraq.

Wiki iliyopita niliandika makala nikisema kuwa k u t o k a n a n a h a l i inavyokwenda hivi sasa juu ya kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi, Waislamu wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa juu ya watu wanaojitokeza na kuweka darsa za siri na kuanza kujadili harakati za al Shabab au vikundi vyovyote ambavyo hivi sasa vinatumiwa na Marekani kama k i s ing iz io cha kuwabamiza Waislamu. Na hii ni kwa sababu kumekuwa kukifanyika mchezo wa kupandikiza makachero misikitini na katika taasisi za Kiislamu wakijifanya mujahidina, kisha kupandikiza silaha na mashambulizi (false terror attacks) ambapo vijana wa Kiislamu hukamatwa na kupachikwa kesi za ugaidi.

Baada ya makala ile mtu mmoja alinipigia s imu akiongea huku kakasirika sana. Yeye yote yaliyosemwa katika makala ile hakuyaona wala kuzingatia nini yalikuwa maudhui ya makala ile. Yeye aliloona ni pale tu nil iposema Waislamu waepuke darsa za siri. Alitumia muda mrefu sana akidhani ananipa darsa juu ya Darul Arqam.

Kilichonisikitisha ni ule ufinyu wa uelewa wa mambo na kutokufahamu watu wanaishi katika mazingira gani, kuelewa MUKTADHA wa sasa na wapite wapi ili wasalimike n a wa f a n ye D a ’ wa h yenye manufaa kama inavyodhihiri katika Sira ya Mtume (s.a.w).

Bomu l imel ipul iwa K a n i s a n i , A r u s h a . Limeuwa na kujeruhi watu wasio na hatia. Taarifa ya Ser ika l i imesema kuwa ni shambulio la kigaidi. Vyombo vya Dola vimetoa kauli kali lakini za matumaini kwa wananchi, vikiahidi kuwa uchunguzi

Mabomu London 7/7Inatoka Uk. 8

Waarabu. Blair akapumua kidogo.

“They are trying to use the slaughter of innocent people to cow us, to frighten us out of doing the things that we want to do. They “should not and they must not succeed,” – Tony Blair.

“The war on terror goes on.”-Bush

Walinukuliwa viongozi hao na vyombo vya habari wakionyesha walivyofaidika na tukio hilo la 7/7.

B a a d h i y a t a a r i f a zinafahamisha kuwa Israel ilikuwa inajua juu ya kutokea kwa shambulio hilo siku moja kabla na kwamba Waziri wake wa Fedha Binyamin Netanyahu, ambaye alikuwa London, alibaki hotelini kwake na hakutoka kabisa kuendelea na program zake za siku hiyo.

K a t i k a m a k a l a ya k e “Bombing Mastermind A s wa t Wo r k s f o r M I -6” (August 2 2005), Kurt Nimmo, ananukuu habari

ya Fox News, ikisema kuwa wakati vyombo vya dola vya Uingereza vikisema kuwa vinahangaika kumtafuta mtuhumiwa namba moja wa ulipuaji bomu London, Haroon Rashid Aswat, kwa upande mwingine vyombo hivyo vilikuwa vikimlinda na kumhifadhi mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa ni mtumishi wa Shirika la kijasusi la Uingereza MI-6.

K a t i k a m a k a l a n a uchambuzi wake, Kurt Nimmo, ananukuu pia gazeti la “The Times” likisema kuwa Aswat alitumiwa kufanya kazi na Osama bin Laden katika kambi ya mafunzo iliyokuwa imeanzishwa na CIA-ISI, kama kituo cha mafunzo cha al Qaida (al-Qaida training camp, Afghanistan).

Gazeti hilo likasema kuwa limepata nyaraka za FBI zikionyesha kuwa Haroon Rashid Aswat, alipelekwa Marekani mwaka 1999 ambapo alipewa mafunzo ya matumizi ya silaha na kuuwa kwa kutumia sumu.

Uchambuzi wa mwandishi Kur t Nimmo ak i tumia

nyaraka mbalimbali anasema al Qaida ni taasisi bandia ya kigaidi (a fake terrorist front organization) iliyobuniwa na mashirika ya kijasusi ya CIA, ISI na MI-6. Na kwamba lengo ni kutumia taasisi hiyo kupandikiza ugaidi, mauwaji, vurugu na ghasia ili kuupiga vita Uislamu na kuzuiya kabisa kupatikana kwa umoja miongoni mwa mataifa ya Kiislamu.

K a m a a m b a v y o imeandikwa na Paul Joseph Watson akinukuu taarifa ya gazeti la Guardian, Usamah bin Laden mwenyewe alikuwa akipewa fedha kutoka MI6 na kwamba pamoja na kuwa Abu Qatada anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wakubwa wa al Qaida, lakini aliwahi kuhifadhiwa na MI-6 kama ilivyoripotiwa na BBC mwaka 2002.

Ni kutokana na taarifa kama hizo, mwandishi Griffin Tarpley, anasema kuwa:

“There is every reason to believe that London is one of the main recruiting grounds

Inaendelea Uk. 10

Nani al ShababInatoka Uk. 8

Inaendelea Uk. 10

la kulinda amani kutoka Marekani kuondoka Somalia katika miaka ya mwanzo ya 1990s, na kuiacha nchi mikononi mwa wababe wa kivita, hali ilizidi kuwa mbaya. Kila koo ikiwa na wanamgambo wake na mahakama yake.

H a r a k a t i z a k u p a t a ufumbuzi wa ndani zilianza zikiwaunganisha vijana na wafanyabiashara waliokuwa wamechoshwa na vitendo vya kiharamia. Harakati hizo zikashika kasi miaka ya 2003 na 2004 ambapo vijana waliunganisha koo wakipigania kusimamisha Sheria za Kiislam. Kwa muda mfupi kabisa wakafanikiwa k u v u n j a m i t a n d a o ya kijambazi na kiharamia nchi ikawa na amani. Kutokea hapo ndio wakapata kuungwa sana mkono na wananchi mpaka wakafanikiwa kuunda serikali.

Hata hivyo, hali hiyo haikuifurahisha Marekani. Ikitumia kisingizio kuwa ICU itakuwa serikali ya kigaidi

itakayogeuza Somalia mahali pa kuzalisha magaidi, Serikali ya Marekani ilianza kuwapa silaha wababe wa kivita waliokuwa wameshindwa na Umoja wa Mahkama za Kiislamu (ICU).

Mwaka 2006 aliyekuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati huo Sean McCormack, alidai kuwa kamwe Marekani haitakubali kuona Somalia ikigeuzwa kuwa kiwanda cha kuzalisha magaidi ikiwa ni kama namna ya kujibu lawama zilizokuwa zikitolewa ni kwa nini Marekani inaunga mkono wababe wa kivita dhidi ya Serikali ya UIC iliyofanikiwa kuleta amani Somalia.

I l i kuwa kama k i in i m a c h o n a u s a n i i w a kisiasa kwa propaganda za kimataifa, wababe wa kivita wanaosaidiwa na Marekani wakatakiwa kuanzisha kitu kinachitwa: Alliance for the Restoration of Peace and Counter-Terrorism (ARPCT) ili ionekane kuwa ni ‘watoto wazuri’ wanaopambana na

ugaidi. Hata hivyo katika h a r a k a t i z a o wa k a wa wanashambulia nyumba za Maimamu wa misikiti na wale wanaowakamata wakawa wanawakabidhi kwa Wamarekani.

Ilikuwa ni katika kipindi hicho, Februari 2006, Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) nao wakatangaza Jihad dhidi ya ARPCT. Ilichukua muda mfupi sana ARPCT kushindwa.

Kutokana na matokeo ya kazi iliyofanywa na ICU, i l ikuwa sio rahisi tena kuwatumia Wasomal ia kupambana na ICU, ndio wa k a t u m i wa E t h i o p i a kuvamia nchi hiyo. Serikali ya Umoja wa Mahakama ya Kiislamu ikaondolewa madarakani na baadae Marekani ikatangaza kuwa al Shabab ni kundi la kigaidi.

Kilichotokea nini? Vijana waliokuwa ndani ya serikali ya Islamic Courts Union (ICU), wakashika silaha kupambana na serikal i i l iyowekwa madarakani pamoja na majeshi ya nje yaliyoko Somalia kulinda ser i k a l i h iyo . N a k wa

Inaendelea Uk. 10

Page 10: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

10 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Makala

Kesi ya Victor imeishia wapi?Inatoka Uk. 9

Mabomu London 7/7Inatoka Uk. 9

Nani al ShababInatoka Uk.9

wa k i n a u t a f a n y i k a i l i ukwel i u jul ikane. Amekamatwa Victor Calist Ambrose kwa kudaiwa kuonekana akirusha bomu hilo.

Hakuna hata taarifa moja, iwe ya Polisi au ya vyombo vya habari i l i y o s e m a : “ G a i d i lililorusha bomu Kanisani lakamatwa.”

Kama ni kutajwa Victor, alitajwa kama mtuhumiwa na hata alipofikishwa m a h a k a m a n i , a m e s h i t a k i w a k w a mauwaji.

Ila kwa kukamatwa mtuhumiwa wa kughushi pasi ya kusafiria, Iqbal Hassan Ally, tunaambiwa “Gaidi mbaroni.” Halafu a n a u n g a n i s h w a n a mabomu Arusha huku tukiambiwa kuwa habari za ki-intelijensia zinaonyesha kuwa magaidi wa al Shabab wapo mitaani wakitafiti sehemu za kushambulia!

Nil ichosema katika makala ile na ambacho nazidi kusisitiza hapa ni kuwa kwa muda sasa kumekuwa na jitihada za kupandikiza kitisho cha ugaidi wa al Qaida na al Shabab. Na yote hii, japo inaonekana katika sura yake ya nje ni kuwatafutia sababu Wais lamu na k u wa b a m i z a . L a k i n i itatuathiri Watanzania wote kama ambavyo mabomu ya ndege zisizo na rubani (drone) yasivyochagua mtu wa kuuwa kule Pakistan, Yemen na Somalia.

T u j u e n j a m a z a kupandikiza kitisho cha uga id i k ik i fan ik iwa , tutakuwa na kibarua kingine cha kukidumisha ili wenye agenda yao wazidi kupata sababu ya kuendeleza malengo yao. Kila uchao maguruneti na mabomu yatakuwa yakichukua ushuru wa roho za Watanzania wasio na hatia.

J e , h a y a n d i y o w a n a y o y a l i l i a w a l e wanaoshabikia kuwepo ugaidi Tanzania kwa vichwa vyao vya habari, “ G a i d i l a k a m a t w a Tanzania?”

Mahmoud, kijana wa Kisomal i anatumikia kifungo Marekani baada ya kushitakiwa kwa kesi ya ugaidi. Lakini kama n i l i v y o e l e z a k a t i k a makala iliyopita, ugaidi ule ulikuwa mchezo wa kuigiza uliofanywa na watu wanaotumiwa na FBI wakaja misikitini na kuanzisha darsa za jihad kisha kuwaahidi vijana kuwapeleka katika kambi

za siri na kuwapa silaha. Darsa za namna hii

na mfano wake ndio

nilizosema tujihadhari nazo isije ikawa ndio yale yale ya kutaka mambo

ya kuth ib i t i sha ya le yal iyosemwa na DCI Robert Manumba kwamba “zipo taarifa za kuwapo

kikundi cha kigaidi cha a l S h a b a b , a m b a c h o kimekuwa kikizunguka Afrika Mashariki kutafuta mwanya wa udhaifu na kushambulia.”

for patsies, dupes, fanatics, double agents, and other roustabouts of the terrorist scene.” (9/11: Synthetic Terror, p. 156).

Akimaanisha kuwa kuna kila sababu ya kuamini kuwa Uingereza imekuwa moja ya kambi kubwa ya kutoa mafunzo kwa ‘magaidi bandia’ , ambao baadae hutumika kupandikiza kitisho cha ugaidi (false terror a�acks) sehemu mbalimbali duniani.

Na tukumbuke kuwa kwa hapa Tanzania wanatuambia kuwa:

“Authorities in Tanzania are concerned at the growth of an Islamist movement accused of links to Somalia’s al-Shabab.”

Kwa sababu hii, nilisema katika makala yangu iliyopita kuwa Waislamu tuwe makini sana na watu wanaopita Misikitini au mitaani na agenda za kuanzisha darsa za siri za kuhamasisha Jihad, kwani wanaweza kuwa ni akina Haroon Rashid Aswat na Abu Qarada.

Na ieleweke wazi hapa kuwa hoja sio kujadili dhana ya “Jihad” kama ilivyokuja katika Uislamu, bali namna m a a d u i w a U i s l a m u wanavyowatumia baadhi ya watu wenye majina ya

Kiislamu au hata baadhi ya wanaharakati wa Kiislamu, kuuangamiza Uislamu na Waislamu.

Jana gazeti la RAI, katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa cha habari: “Siri nzito Arusha.”

Kisha kufuatiwa na vichwa vidogo vinavyosema: “Mamia ya vijana wapelekwa Somalia, Darfur”, “Watajwa kupewa mafunzo ya kigaidi.”

“Wakati Jiji la Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vi jana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan, kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi.”

Limesema gazeti hilo katika ufunguzi wa habari hiyo na kuongeza likisema kuwa:

“Chanzo cha habari kutoka katika duru za usalama mkoani Arusha kimesema kuwa, vijana wanaodaiwa kwenda Somalia kwenye kambi za kundi (la) Al-Shabab na Darfur ni wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea.”

L i l i l o l a u h a k i k a n i kuwa, hakuna uwezekano wakatoka vijana 200 hapa

na kwenda kusomea ugaidi Somalia na Darfur, bila ya vyombo vya dola kujua. Kwa hiyo kama kungekuwepo na vijana wanaokwenda Somalia na Darfur kwa ajili ya kujifunza ugaidi, vyombo vya usalama vingekwisha w a k a m a t a w a h u s i k a kuanzia wal iopekekwa mpaka wanaowarubuni na kuwapeleka. Na kama v ina jua , h a la fu hav i j a wa k a m a t a m p a k a R A I inaripoti, ni kwamba hao ni watu wao wanaowaandaa kwa ‘kazi maalum’.

Maana kama habari hizi ni kwa mujibu wa duru za usalama, kama gazeti lilivyodai, ni kuwa Idara ya Usalama inajua. Sasa swali ni je, kwa nini haijachukua hatua na badala yake ikaona ivujishe taarifa kwa gazeti?

Ta a r i f a k a m a h i z i zinachoeleza bila kusema ni kuwa kuna uwezekano wa vijana kuchukuliwa na kupelekwa katika kambi zinazodaiwa kuwa ni za al Shabab, kisha baada ya kukusanya ushahidi na vielelezo, ndio wahusika wa k a m a t w e n a k u t o a vielelezo hivyo kuwa kweli kuna watu wanasomea ugaidi. Lakini ukweli ukiwa

kuwa vijana hao wamefanya kupandikizwa na pengine kwa kuzugwa wakiaminishwa kuwa wanapekewa kupigana Jihad.

K w a c h a m b o h i k i wakatokea watu watakaojiona kuwa ‘wameiva’ tayari kwa Jihad wakanaswa. Na hawa ndio baadhi ya waandishi wa kimataifa wanawaita kuwa ni ‘Wapumbavu wenye kudanganyika kwa wepesi’ (gullible idiots).

Kama wapo watu walioiva barabara, tunataka kuwaona wakija na miradi ya kuwa na hospitali kila mkoa na kila wilaya, vyuo vikuu, televisheni na magazeti ya kila siku, miradi ya kilimo na uchumi ili kuwatoa Waislamu na Watanzania kwa ujumla katika njaa na umasikini.

Tu n a t a k a k u w a o n a wakie lekeza J ihad yao kukabiliana na ujinga wa baadhi ya watu wanaokataza mabint i na vi jana wao k u s o m e a u d a k i t a r i n a utaalamu mwingine, lakini wenyewe wanapeleka wake zao kwa John wakatibiwe magonjwa ya wanawake huku wenyewe wakikaa nje kwenye benchi!

L a k u s i s i t i z a h a p a kwa Watanzania wote ni kuwa kama tutakubal i kupandik iz iwa k i t i sho cha ugaidi, tutaumia sote. Kwanza ili kitisho hicho kikubalike, itabidi kiwe cha kweli. Watu wauliwe na mali kuharibiwa. Lakini baada ya hapo, itabidi pia kiendelezwe. K i l a b a a d a y a m u d a tutakuwa tukikumbana na mashambulizi ya maguruneti na mabomu kudumisha kitisho kwa manufaa ya wenye malengo yao.

Kwa wale wanaoshabikia taarifa za “gaidi adakwa”, inapokuwa mtuhumiwa ni Ally, lakini wakigwaya anapokuwa ni Victor, wajue kuwa hi l i l inalotakiwa l i k i t i m i a , h a t a w a o hawatasalimika.

K u l e Pa k i s t a n , j a p o inadaiwa kuwa walengwa ni magaidi, lakini makombora kutoka Drone, yameuwa m a e l f u ya wa n a wa k e , wazee, wanafunzi wa shule na watoto wasio na hatia wakati waliodaiwa kuwa wanalengwa idadi yao hata 20 haifiki.

K o m b o r a l a d r o n e halichagui nyumba wala roho ya kuangamiza. Na maadhali ugaidi unaoliliwa kupandikizwa ni wa kidini, hapana shaka tutaumia sote Waislamu na Wakristo.

kuamini kuwa wanapigana kwa niaba na kwa masilahi ya Wasomali, al Shabab wamekuwa wakifanya juhudi kuwahusisha viongozi wa koo mbalimbali na kila kada katika jamii.

Kwa mujibu wa tafiti za waandishi mbalimbali na wasomi ambao wametafiti na kuandika juu ya al Shabab, ki la ambapo al Shabab wamefanik iwa kuweka uongozi wao, huweka gavana (wali) kama mkuu wa wilaya, mahakama (Shari’a court), ofisi ya Zakat na idara ya ulinzi na polisi. Kunakuwa pia na idara za huduma kwa jamii na uchumi zikihusika na ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja, shule, hospitali na kilimo.

Katika kipindi cha njaa miaka ya 2009 na 2010 al Shabab walifanya kazi kubwa kukusanya chakula, sadaka na Zaka kutoka kwa matajiri na kuwasaidia wananchi we n ye n j a a . Wa l i p i g a m a r u f u k u m i s a a d a ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kuingia Somalia wakisema kuwa WFD walikuwa wakisambaza chakula kilichopita wakati wa kutumiwa (expired) na pia kutumia misaada hiyo kwa masilahi ya mabeberu

na vibaraka wao.Kuhusu madai kuwa Al-

Shabab ina uhusiano na Al-Qaeda, watafiti mbalimbali wanasema kuwa, al Shabab sio al Qaida, bali kama ni kuhusiana ni kutokana na ukweli kuwa baadhi ya viongozi wake walikuwa wapenzi wa kauli na wito wa Usama, ila ukweli unabaki kuwa al Shabab ni taasisi ya Somalia yenye malengo ya kuiokomboa Somalia kwa mtizamo wao. Wanasema pia kuwa hata kama kuna wapiganaji wa nje, basi ni wapiganaji walioingia kwa kuona wanataka kusaidiana n a a l S h a b a b k a t i k a kusimamisha Shariah.

M a e l e z o z a i d i yanasema kuwa hata pale ilipodaiwa kuwa al Shabab walishambulia nje ya Somalia kama ilivyodaiwa kuwa walifanya Kampala (kama ni kweli walipiga wao) 2010, basi i takuwa walifanya vile kwa kupata mafanikio ya ndani, kwa maana ya kuishinikiza Uganda itoe jeshi lake Somalia.

M t a f i t i C h r i s t o p h e r Anzalone ak ih i t imisha uchambuzi wake anasema kuwa pamoja na kuwa hivi sasa al Shabab wanakabiliwa na changamoto nyingi, lakini bado wanashikilia sehemu

kubwa ya nchi ya Somalia na hakuna dalili kwamba watatoweka kwa siku za karibuni. Anasema, moja ya changamoto ni kutengwa na jumuiya ya kimataifa, kukosa msaada wa maana kutoka kwa jumuiya hiyo na kuingia kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki.

Hata hivyo anasema kuwa udhaifu ndani ya serikali (TFG), unaotokana na rushwa, ufisadi, ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe na kukosa uoni unaotoa uongozi na matumaini kwa Wasomalia, bado al Shabab wataendelea kupata uhalali wa kuwepo na kutegemewa na Wasomali wengi. Propaganda kuwa ni magaidi na kwamba wanatawala kwa sheria kali za Kiislamu, inashindwa kufanya kazi katika maeneo wanayotawala na ndani ya Somalia kwa ujumla, kwa sababu haionekani nafuu yoyote kutoka kwa TFG. Bali kudumu kwa TFG ni kutokana na msuli wa kijeshi wa majeshi ya Kenya, Uganda, Ethiopia na Burundi.

(Makala hii imeandikwa kwa kutumia utafiti wa mtafiti Christopher Anzalone (Institute of Islamic Studies at McGill University), makala za wasomi mbalimbali na taarifa za Aljazeera)

Page 11: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

11 AN-NUURSHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013Makala

M W E Z I m t u k u f u w a R a m a d h a n i u m e a n z a . Ramadhani ni fahari kwa mja na anapaswa kuipokea hidaya hii vyema ili apate malipo mema kutoka kwa Allah (sw).

Ramadhani ni siku 29 au 30 tu, katika mwaka. Na kumi la awali la mwezi ni la Rehma panapo majaliwa Mwenyezi Mungu atuvushe salama.

Katika mantiki yake, mwezi huu ni wa kujifunza, kujisafisha na kujizoesha kuendelea kufanya mema kutokana na matokeo mema yanayopatikana ndani yake.

Ramadhani humfanya mja kuongoka na kuwa n a m wa n z o m z u r i wa kubadilisha maisha yake, kuanzia mtazamo, tabia na matendo yake. Mwezi huu unazowesha mfungaji kurejea yale mema na yaliyoridhiwa na Mola wake na kuachana na yale yote mabaya na

`Kumi la kwanza Ramadhaniyalikatazwa.

Hii ni Ramadhani mwezi wa s wa u m u u n a h i t a j i mazingatio ndani yake na hata baada ya kwisha kwake. Ni wakati wa Muislamu kutulia, kufikiri na kisha kupima matokeo ya matendo yake. Mola wetu tutakabalie swaumu zetu na utukunjulie rizki ya halali, Amin.

Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ni nguzo ya nne kati ya tano zinazosimamia dini ya Kiislamu, ambapo mtu mwenye kubalehe au kuvunja ungo hutakiwa kuitimiza.

Mwezi huu una historia ya kipekee katika dini ya Kiislamu, kwa sababu ndiyo mwezi ambao kitabu kitukufu cha Qur-an kilishushwa katika usiku unaoitwa ‘Laila-tul Kadir.’

Swaumu au kufunga ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa waumini wa dini ya

Kiislamu kupitia kwa Mtume Muhammad (S.A.W).

Amri hiyo ya Mwenyezi Mungu imetajwa katika aya ya 182 ya sura ya pili Baqarah 183, ndani ya kitabu kitukufu cha Qur-an.

Katika aya hii, Allah (SW) anawaambia Wais lamu kupitia Mtume Muhammad ( S . A . W ) k u w a , “ E n y i mlioamini, mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama w a l i v y o l a z i m i s h w a wal iokuwa kabla yenu i l i mpate kuwa wacha Mungu.”

Kwa mujibu wa aya hii, utagundua kuwa lengo k u b wa k wa Wa i s l a m u kulazimishwa kutekeleza ibada hii ya funga ni kwa wao kuweza kufikia ngazi au daraja la ucha Mungu wa kikwelikweli.

Kwa maana kwamba endapo mja ataitekeleza ibada hii kwa kufuata sharti zote kikamilifu, dhahiri kiwango chake cha imani kitapanda.

M w e z i m t u k u f u wa

Ramadhani umegawanyika katika makundi matatu ambayo yana siku kumi kila moja. Kila kundi moja la kumi, lina faida zake kwa mwenye kutimiza kile kilichoagizwa na Mwenyezi Mungu.

K u m i l a k w a n z a linajulikana kwa jina la Rehma (rehema), la pili Magh-fira (kusamehewa madhambi) na lile la mwisho linaitwa kumi la kuachwa huru na moto.

Tumeianza Ramadhani kwa kuanzia na kumi la Rehma. Kat ika kipindi mja hurehemewa sana na Allah (sw) kwa kila jema analolifanya. Kwa kifupi ni kwamba kumi la kwanza ni kumi la mja kurehemewa na Mola wake.

I t o s h e k u f a h a m i k a kwamba kila jema analofanya mja, hulipwa zaidi kuliko ambavyo analipwa katika siku za kawaida. Ndiyo maana wakati huu unaweza kushuhudia watu wakifurika katika nyumba za ibada.

MPAKA alipopinduliwa Rais Morsi wa Misri wiki i l iyopi ta , watu wengi waliounga mkono njia iliyotumiwa na ‘Ikhwan M u s l i m i n ’ k u i n g i a m a d a r a k a n i , a m b a y o walidhani ni mafanikio makubwa kwa kundi hilo la harakati za Kiislamu, sasa wameshatia akili kwamba njia hiyo haikuwa muafaka, na ilikuwa ni kupoteza tu malengo sahihi ya waasisi wa kundi hilo.

Mwaka jana niliandika makala ya kutahadharisha kuhusu methodolojia hii na changamoto zake na jinsi ilivyowaangusha Waislamu wa Algeria, Uturuki na Palestina (Hamas). Watu wengi, ama hawakuelewa au walijifanya hawaelewi. S h a n g w e y a u s h i n d i n a m a t u m a i n i h e w a , iliwaondolea maarifa hata ya kuona ukweli ulio wazi.

Methodolojia iliyotumiwa na ‘Ikhwan Muslimin’ ya kuingia kwenye uongozi wa dola kupitia mlango wowote, na kisha kuanza kutekeleza Uislamu baada ya kuingia madarakani inafahamika vyema. Njia hii inamaanisha kuwaandaa watu hatua kwa hatua kiitikadi, kisaikolojia, kimaadili na kijamii, ili wakubali na kisha kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika nyanja zote za maisha yao.

Wanaoshabikia njia hii wana hoja zao ingawa hazina mashiko ya kisheria. Msingi mkuu wa hoja yao ni kwamba Uislamu haukufunuliwa kwa Mtume Muhammad (saw)

Mafunzo kutoka mapinduzi ya MisriNa Said Rajab wote kwa mara moja. Kwa

hiyo, kila hatua ya Uislamu i l ivyoku ja wakat i u le , inatumika kama ushahidi wa matumizi ya methodolojia hii. Mifano inayotumika zaidi ni jinsi Swala ilivyoshuka, Funga na amri ya kukataza ulevi.

Kwa hiyo, wanasema, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha sheria yake kwa binadamu kidogo kidogo. Basi na sisi tukitaka kuirejesha, inabidi tufanye hivyo. Hapo maana yake binadamu ndiyo wanaoamua jinsi gani na lini sheria ya Mwenyezi Mungu itekelezwe! Hilo ni kosa.

Taasisi za utawala wa umma hazikuanguka wakati Hosni Mubarak alipoanguka nchini Misri . Na Morsi alikabiliana na upinzani mkali kutoka Mahakama ya nchi hiyo, vyombo vya habari vya umma, jeshi na polisi. Taasisi ambazo kimsingi hazipaswi kupingana na mkuu wa dola, isipokuwa zinatakiwa kumtii. Hakuwa na uwezo wa kuzifanyia marekebisho taasisi hizi kama kiongozi mkuu wa nchi.

N c h i i l i k a b i l i wa n a migogoro mikubwa ya kiuchumi wakati Morsi al ipoingia madarakani , lakini masikini ya mungu, hakuwa na nyenzo wala mamlaka anayopaswa kuwa nayo Rais, katika kurekebisha uchumi wa nchi. Wapinzani wake wa kisiasa wa kisekula, walitilia shaka sifa zake za kidemokrasia, na wapinzani wake wengine wa kisiasa “Waislamu” walitilia shaka sifa zake za Kiislamu. Ikawa ugali moto, mboga moto kwa Mohammed Morsi!

Hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Misri, ingeweza kumpa wakati mgumu kiongozi yeyote mahiri wa kisiasa, ambaye taasisi zote za dola ziko chini yake, wachilia mbali Mohammed Morsi, ambaye hakuwa na uwezo hata wa kuamrisha jeshi, wakati yeye ni Amiri jeshi mkuu! Kwa hiyo kushindwa kwake kusimamia baadhi ya mambo, lilikuwa ni jambo la wazi kabisa.

Lengo la siasa katika Uislamu ni kushughulikia na kusimamia masuala ya umma. Uislamu umeweka misingi ya kisiasa na kiuchumi na taratibu madhubuti za kushughulikia matatizo ya kijamii. Misri inakabiliwa na mgogoro mzito wa kiuchumi pamoja na matatizo ya kiusalama na ufisadi wa kisiasa.

Kwa kugeukia ufumbuzi wa kibeberu wa matatizo hayo (kama vile mikopo ya IMF), ili kutatua mgogoro wa kiuchumi nchini Misri, Serikali ya bwana Morsi imejenga mtazamo mbele ya umma, kwamba ubeberu ndiyo wenye fikra sahihi za kuimarisha uchumi wa Misri. Sasa kama Uislamu hautekelezwi wakati wa kutatua migogoro kama hiyo, utatekelezwa wakati gani?

Dhana kwamba matatizo y a n a w e z a k u t a t u l i w a kwa kutumia ufumbuzi usiokuwa wa Kiislamu, ili baadaye Uislamu uweze kutekelezwa kikamilifu siyo sahihi. Kujiamini kunaweza kujengwa kwenye ufumbuzi wa Kiislamu, kwa kuona ufumbuzi huo ukifanya kazi na siyo ufumbuzi huo

kutupwa wakati wa matatizo. Tatizo lolote linalopatiwa ufumbuzi kwa kurejea mfumo usio wa Kiislamu, maana yake ni kujenga mtazamo kwamba Uislamu hauhitajiki.

Serikali ya Misri chini ya bwana Morsi, ilionekana k u t o a u m e m e wa b e i nafuu Gaza, wakati Cairo ikikabiliwa na changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara. Mwaka mmoja umepita, Misri imekumbwa na upungufu wa chakula, petroli, umeme, maji na ukosefu wa ajira, wakati hali ya usalama ikidorora.

Serikali ya Misri chini ya M o h a m m e d M o r s i , haikutekeleza hata ufumbuzi mmoja wa matat izo ya kiuchumi kwa kuzingatia fikra ya Kiislamu, lakini bado taswira inayojengwa duniani ni kwamba Uislamu wa Morsi ndiyo ulioporomosha uchumi wa Misri. Matatizo na changamoto zote za Misri sasa anabebeshwa Morsi na ‘Uislamu’ wake, wakati inajulikana wazi alipokuwa Rais, hakuweza kutekeleza Uislamu hata kidogo katika ngazi ya dola, kutokana na mfumo ulioshindwa wa kisekula unaotawala Misri.

Kiuhalisia, kushindwa kwa bwana Morsi kuitawala Misri Kiislamu, ingawa aliingizwa madarakani na umma unaotaka kutawaliwa Kiislamu, kulimfanya Rais h u yo k u wa k i b o g o yo . Ndiyo maana ameondolewa madarakani kirahisi mno na kujenga picha duniani kwamba Uislamu haufai kutawala. Lakini tathmini sahihi ya kufaa au kutofaa

k wa U i s l a m u k w e n y e utawala na uongozi wa dola, haiwezi kutolewa na wale wanaopinga Uislamu nchini Misri!

I n a f a h a m i k a v y e m a kwamba wafuasi wengi wa ‘Ikhwan Muslimin’ nchini Misri walikuwa wakitumai kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu nchini humo, ingawa walijua wazi kwamba utawala wa Morsi usingeweza kuwafikisha kwenye malengo hayo. Kujua kwamba malengo yako makuu ya kisiasa yanatofautiana kabisa na sera za kisiasa unazotekeleza, inakufanya wakati wote u e n d e s h e m a m b o k wa mashaka.

Hali hii imejitokeza zaidi kwenye kipindi cha mwisho cha utawala wa ‘Ikhwan Muslimin’ nchini Misri, ambao ulikuwa ukituhumiwa vikali kwa “Uislamu wa Siasa Kali,” hata pale sera walizotekeleza zilipokuwa “Usekula wa Siasa Kali.” Kwa hiyo kusimamisha Uislamu kidogo kidogo katika ngazi ya dola, kama walivyofanya ‘ I k h w a n M u s l i m i n ’ , kunaashiria udanganyifu, ingawa nia inaweza kuwa njema. Qur’an imetuonya kuhusu utekelezaji nusu nusu wa sheria za Mwenyezi Mungu:

“Na (baadhi ya) ambao tuliwapa Kitabu wanafurahia uliyoteremshiwa. Na katika makundi yao mengine w a k o w a n a y o y a k a t a a baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa kumuabudu M w e n y e z i M u n g u t u wa l a n i s i m s h i r i k i s h e . Ninaita Kwake viumbe wenzangu waongoke (kama nilivyoongoka). Na ni kwake marejeo yangu” Qur(13:36).

“ N a n a m n a h i v i tumeiteremsha (hii Qur’an), hali ya kuwa ni hukumu (ya Mungu iliyoteremka) kwa (lugha ya) Kiarabu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya kukufikia Ilimu hii, hutakuwa na rafiki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu” Qur(13:37).

Mara nyingi Mwenyezi Mungu anatupigia mifano ya Waislamu wa mataifa ya l i yo p i t a , i l i t u we z e kuj i funza kutokana na makosa yao. Wanaharakati wa Kiislamu duniani, lazima walinganie ‘Utekelezaji wa Uislamu Wote’ kama mfumo, na watafute ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayowahusu binadamu kutoka ndani ya mfumo huo. Kusiwe na matarajio hewa kwamba tukishika madaraka, basi Katiba itakuwa ya Kiislamu na mambo yote yataendeshwa Kiislamu. Hilo halijawahi kuwa na wala halitakuwa!

Page 12: (22) AHLU SUNNA WAL JAMAA Mwanafunzi aliza waumini ... · za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi

12 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR12 SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

Maimamu Tanga waichambua rasimu ya katibaNa Abu Ayub

IMAM Hamza Omar, amewahimiza Waislamu kusimama imara katika kutetea haki.

A m e s e m a , wanalotakiwa kufahamu Waislamu ni kuwa katika kupigania haki kuna gharama zake na kwamba hilo lisiwatishe.

I m a m H a m z a , a m e b a i n i s h a h a y o , Ijumaa ya wiki iliyopita akiwahutubia Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa, katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Katika mawaidha yake

MAIMAMU wa misikiti mbali mbali ya jijini Ta n g a w a m e k u t a n a kwenye ukumbi wa Simba Mtoto katikati ya jiji hilo kwa madhumuni ya kuangalia makosa y a l i y o m o k w e n y e rasimu ya katiba mpya na kutoa mapendekezo yao yatakayopelekwa kwenye Baraza la Katiba la Kiislamu litakalokaa tena huko jijini Dar es Salaam siku za mbele.

Wa k i o n g o z w a n a mwakilishi wa Baraza hilo kwa mkoa wa Tanga, S h e i k h A l i N a s s o r , Maimamu hao baada ya mada ya ufunguzi iliyotolewa na mtaalamu wa masuala ya katiba, Sheikh Salim Barhiyaan walikaa vikundi vikundi kuvijadili vipengele 21 vilivyotajwa kuwa ni kandamizi zaidi kwa imani ya Kiislamu nchini.

Baada ya kamati hizo kuangal ia v ipengele hivyo wasemaj i wao walisimama mbele na kueleza kwa hamasa kile kila kikundi kilichokiona

Imam Hamza ahimizaWaislamu kutetea hakiNa Bakari Mwakangwale

IMAM Hamza Omar.

Imam Hamza amesema kuwa anaamini kuwa kisa cha yeye kukamatwa, kufunguliwa kesi huku dhamana yake ikizuiliwa, ni kutokana na msimamo wake na juhudi aliyokuwa akifanya kupigania haki.

Akitoa mfano juu ya yale yaliyojiri wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipofika Geita kufuatilia mgogoro wa uchinjaji, alisema kuwa Waislamu akiwemo yeye mwenyewe, walisimama kusema kweli na kueleza wazi kuwa hawapo tayari kuona wakibaguliwa na kudharauliwa.

Akasema kuwa ilikuwa pale Mheshimiwa Waziri

Mkuu alipoonyesha kuwa hayupo tayari kusikiliza madai ya Waislamu, ndipo walipoamua kutoka katika kikao na hiyo ikiwa ni kuonyesha hisia zao kuwa hawaridhiki na mambo yanavyoendeshwa.

Imam Hmzana alisema, baada ya kikaoa na Waziri Mkuu, haikupita muda alikamatwa, na kuwekwa ndani huku dhamana yake ikizuiliwa.

Akasema, yeye binafsi anahisi kuwa kuzuiliwa h u k o k wa d h a m a n a kunatokana na msimamo wake wa kusema kweli na kupigania haki.

kwenye rasimu hiyo.Kikundi kilichoitwa

A b u b a k a r S i d i q r. a k i l i s e m a k i n a t a k a katiba mpya kuruhusu maeneo yenye Waislamu wengi kama Zanzibar kuwa huru kujitawala kwa Sheria za Kiislamu na kusema kuwa kwa uzoefu wa nchi nyengine kama Nigeria jambo hilo wala halitozikwaza haki za raia mwengine yoyote. Zaidi ni kuwa utaratibu huo utapunguza manung’uniko kwa raia wa eneo husika wanaopenda kujitawala kwa imani za dini zao.

Kikundi cha Omar ibn Khattab r.a kilisema kifungu cha 5 cha ibara ya 31 ya rasimu kuhusu kilichoitwa uchochezi kwa kutetea imani ya dini kinapingana na kifungu cha 2 chenye kutoa uhuru wa kuchagua na kutangaza imani ya mtu. Yale yote yanayoruhusiwa na kifungu cha 2 ndiyo hayo hayo yanayopingwa na kifungu cha 5 cha ibara hiyo.

Awali katika mada ya ufunguzi, Sheikh Salim alisema kuwa ibara hiyo

ya rasimu inaonekana kama imewekwa kutetea imani ya Kikristo akigusia huko nyuma katika kesi i l iyomuhusu Ra jabu Dibagula.

D i b a g u l a a l i p e wa hukumu ya kutumia kifungo jela kwa kusema kuwa Yesu si Mungu jambo linaloitwa ni kashfa kwa Wakristo. Baadae hukumu hiyo ilitenguliwa pale Waislamu walipokata rufaa wakitumia kipengele cha katiba inayomalizika.

Ilibainishwa kuwa kabla hata rasimu hiyo haijapita, tayari kumekuwa na k a m a t a k a m a t a y a kuhusisha mawaidha ya

Waislamu yanayopatikana kwenye mikanda ya aina mbali mbali zikiitwa ni kanda za kichochezi na kashfa.

Katika maelezo yake, Sheikh Salim Barhiyaan a l i s e m a Wa i s l a m u h a w a t a k i w i k u k a t a t a m a a h a t a k i d o g o kwani Mwenyezi Mungu subhaanahu wataala anaona kila walifanyalo hivyo mafanikio yanaweza kuja hata dakika za mwisho. Lakini hata hivyo ikiwa kutakuwa na matokeo kinyume chake basi kila mwenye kufanya juhudi ajue atalipwa n a h a t a u l i z wa k wa kukosekana mafanikio.

Pichani ni kiongozi wa kikundi kimojawapo akiwa na maimamu wenzake . Alikumbusha kwamba

Mtume swalaLlaahu alayhi salaam aliendelea kumlingania Ami yake, bwana Abu Talib hadi wakati wa sakaraatul mauti.

Pamoja na hivyo ami yake huyo alikufa katika imani ya kishirikina na kwa hilo hatoulizwa juu ya ami yake huyo kufa katika ukafiri.

Baada ya kumalizika kwa mijadala hiyo na majumuisha wawakilishi wa Baraza la Katiba la Waislamu walichukua mapendekezo hayo na kuahidi kuyaweka sawa kwa ajili ya kuyapeleka mbele kunakohusika.

“TAQWA ORPHANS TRUST TANZANIA” inawakaribisha waislamu wote kushiriki na kuchangia katika program maalum ya ‘futar kwa yatima’-Pemba na Pwani kwa mwaka 1434A.H /2013.Kwa maelezo zaidi:Piga simu namba;0658 225 998/0683 225 998/0713 300 417 au tembelea ofisi zetu zilizopo kwenye jengo la Red Cross lililopo kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi, mkabala na jengo la NSSF.

2nd floor, Red Cross Bldg, Bibi Titi / Morogoro Rd,PO Box 7079 DSMPhone: 255 658 225998/ 255 683 225998Email: [email protected]: www.taqwaorphanstrust.org