10
1 NKINGA INSTITUTE OF HEALTH SCIENCES (NIHS) P.O.BOX 60, NKINGA. TABORA –TANZANIA 16.10.2020. [email protected] Phone +255 765120032 / +255754 063 064 Kwa Bwn/Bi/, YAH.NAFASI YA KUJIUNGA NA KOZI KATIKA TAASISI YA SAYANSI ZA AFYA NKINGA MWAKA WA MASOMO 2020/2021. Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza na kukutaarifu kwamba wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE ) ,imekuchagua kujiunga na mafunzo katika taasisi hii ya kikristo ya Kanisa la Pentekoste FPCT ( Free Pentecoste Churches of Tanzania ) katika kozi ya Utabibu ( Ordinary Diploma in Clinical Medicine ),ngazi ya astashahada (cheti) mafunzo haya ni kwa muda wa miaka mitatu ( 3 ). Chuo kitafunguliwa tarehe 08 November,2020. Kutokana na uchache wa nafasi za masomo,nafasi yako itahesabika kupotea kabisa na kujazwa na mtu mwingine,endapo hutafika katika kipindi cha wiki mbili baada ya chuo kufunguliwa. Tafadhali unatakiwa kufika na vyeti vyako halisi vya kuhitimu masomo ya sekondari, na kuviwasilisha unapofika chuoni ili vipelekwe wizarani kuhakikiwa ULIPAJI WA FEDHA Gharama za chuo zitafuata utaratibu wa kulipa ambayo hutolewa kila mwaka.Mchanganuo wa gharama hizo umeainishwa kwenye jedwali.

1.,1*$ ,167,787( 2) +($/7+ 6&,(1&(6 1,+6 3 2 %2; 1.,1*$ 7 ......o .XYDD Q\ZHOH ]D EDQGLD DX ]LOL]RVXNZD KHOHQL PDVLNLRQL DX Q\ZHOH NXNDULNLWL QD EDQJLOL 0LNXIX LWDND\RUXKXVLZD NXYDOLZD

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • 1

    NKINGA INSTITUTE OF HEALTH SCIENCES (NIHS) P.O.BOX 60, NKINGA.

    TABORA –TANZANIA

    16.10.2020.

    [email protected]

    Phone +255 765120032 / +255754 063 064

    Kwa Bwn/Bi/,

    YAH.NAFASI YA KUJIUNGA NA KOZI KATIKA TAASISI YA SAYANSI ZA AFYA NKINGA MWAKA WA MASOMO 2020/2021.

    Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza na kukutaarifu kwamba wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE ) ,imekuchagua kujiunga na mafunzo katika taasisi hii ya kikristo ya Kanisa la Pentekoste FPCT ( Free Pentecoste Churches of Tanzania ) katika kozi ya Utabibu ( Ordinary Diploma in Clinical Medicine ),ngazi ya astashahada (cheti) mafunzo haya ni kwa muda wa miaka mitatu ( 3 ).

    Chuo kitafunguliwa tarehe 08 November,2020. Kutokana na uchache wa nafasi za masomo,nafasi yako itahesabika kupotea kabisa na kujazwa na mtu mwingine,endapo hutafika katika kipindi cha wiki mbili baada ya chuo kufunguliwa.

    Tafadhali unatakiwa kufika na vyeti vyako halisi vya kuhitimu masomo ya sekondari, na kuviwasilisha unapofika chuoni ili vipelekwe wizarani kuhakikiwa

    ULIPAJI WA FEDHA

    Gharama za chuo zitafuata utaratibu wa kulipa ambayo hutolewa kila mwaka.Mchanganuo wa gharama hizo umeainishwa kwenye jedwali.

  • 2

    MWAKA WA KWANZA UTABIBU ASTASHAHADA

    MAELEZO MUHULA WA I MUHULA WA II JUMLA

    ADA YA MAFUNZO 760,000.00 760,000.00 1,520,000.00

    GHARAMA ZA KUFUATILIA BIMA YA AFYA(NHIF) 5,000.00 - 5,000.00

    MITIHANI YA NDANI 100,000.00 100,000.00 200,000.00

    UTUMIAJI WA MAKTABA 45,000.00 45,000.00 90,000.00

    UANACHAMA WA JUMUIA YA WANACHUO 10,000.00 - 10,000.00

    KITAMBULISHO 5,000.00 - 5,000.00

    KITABU CHA MAFUNZO YA VITENDO 80,000.00 - 80,000.00

    USAJILI - NACTE 25,000.00 - 25,000.00

    KOMPYUTA 25,000.00 25,000.00 50,000.00

    MICHEZO 10,000.00 - 10,000.00

    MALAZI 250,000.00 250,000.00 500,000.00

    SARE - - -

    USAJILI CHUONI 20,000.00 - 20,000.00

    JUMLA 1,335,000.00 1,180,000.00 2,515,000.00

    Fedha zote zinatakiwa kulipwa mwanzoni mwa muhula husika. Inasisitizwa kulipa benki katika akaunti za chuo zilizotajwa kabla ya kufika chuoni. Unatakiwa kuwa umelipa pesa benki,kabla ya kufika chuoni,kiasi cha pesa kilichoelekezwa katika jedwali.

    Mara ufikapo chuoni wasilisha nakala ya malipo ya kutoka benki ili uweze kupokelewa. Hautapokelewa kama hutakuwa umekamilisha malipo.Akaunti za chuo ni hizi zifuatazo:

    Jina la akaunti - Nkinga School of Nursing,yenye akaunti namba 51103500019 iliyopo National Microfinance Bank (NMB),SWIFT CODE:NMIBTZTZ

    Jina la akaunti - Nkinga School of Nursing,yenye akaunti namba 025103002760,iliyopo National Bank of Commerce (NBC),SWIFT CODE:NLCBTZTX

    Jina la akaunti - Nkinga School of Health laboratory and Health Sciences,yenye akaunti namba 056101001007, iliyopo National Bank of Commerce ( NBC ),SWIFT CODE:NLCBTZTX

    Pesa zote zilipwe kati ya akaunti zilizotajwa hapo juu, isilipwe pesa tofauti na akaunti hizo,wala hakuna malipo yatakayofanyika chuoni kwa kulipa pesa taslimu au kumpa mtu yeyote mkononi.

    Kuna fedha ya mtihani wa wizara ambayo italipwa kwenye akaunti ambayo itatolewai mara mwanafunzi atakapofika chuoni. Kiasi kinacholipwa kila mwaka ni shilingi laki moja na elfu hamsini ( 150,000/=).

  • 3

    Tafadhali ieleweke kuwa gharama hii ya mitihani ni mitihani ya mwisho inayohusika na wizara na siyo gharama ya mitihani ya chuoni ( mitihani ya ndani ).

    Fedha ya chakula mwanafunzi atajitegemea mwenyewe, hivyo mzazi / mlezi au mfadhili anatakiwa kumpa mwanachuo husika pesa ya chakula moja kwa moja kulingana na siku atakazokuwepo chuoni.Chuo kimefanya mazingira mazuri ya kupata chakula kwa kununua katika migahawa ya chuo kwa bei nafuu,kwa wastani wa shilingi 3,500/= kwa siku.

    Kuhusu matibabu, Kama huna kadi ya bima ya Afya, unatakiwa kulipa kiasi cha shilingi hamsini elfu na mia nne (Tshs. 50,400=) kwa ajili ya kukata bima ya Afya. Malipo haya yafanyike katika akaunti za chuo zilizotajwa. Kiasi hicho cha pesa ya bima ya Afya ni nje ya pesa ya ada. Hautapokelewa kama utakuwa hujalipa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya bima ya afya. Pia kama unakadi ya bima ya afya unatakiwa kuiwasilisha chuo kwa ajili ya uthibitisho wa kadi yako.

    Kabla ya kuja chuoni hakikisha umepimwa afya yako na daktari ambaye atajaza fomu yako iliyoambatanishwa na barua hii. Fomu hiyo utaiwasilisha chuoni ili iwekwe mwenye jalada lako.

    MALIPO YOTE YATAFANYIKA KATIKA AKAUNTI ZA CHUO ZILIZOTAJWA. UKIMPA MTU YEYOTE PESA NJE YA AKAUNTI ZA CHUO HAUTAHESABIKA KAMA UMELIPA. PESA IKISHAINGIA KATIKA AKAUNTI KWA MALIPO HAITARUDISHWA.

    Wakati wote utakapokuwa chuoni, utatakiwa kutii sheria na taratibu za nchi na zile zilizowekwa na Wizara ya Afya Maendeleo na Ustawi wa Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,ambazo ni sawa na sheria za chuo.Vile vile ieleweke kwamba,masuala yote ya mwanafunzi unapokuwa chuoni yatashughulikiwa na uongozi wa chuo,endapo itakuwa lazima suala la mwanafunzi kushughulikiwa na makao makuu ya wizara kupitia idara ya mafunzo,itabidi maombi yote yapitie kwa mkuu wa chuo kabla ya kuwasilishwa wizarani.

    SHERIA NA TARATIBU ZA MAVAZI

    Taasisi ya Tayansi za Afya ni ya kikristo ya kanisa la kipentekoste FPCT ( Free Pentecoste Churches of Tanzania ), inasimamia na kuendeleza maadili na kulinda utu na mtazamo wa kikiristo na jamii kama chuo kinavyoelekeza.

    Mwanachuo katika taasisi hii anatakiwa kuva mavazi yaliyo nadhifu, wakati wote awapo chuoni na nje ya chuo kama inavyoelekeza katika sheria na taratibu ya chuo.

  • 4

    MWONGOZO WA UVAAJI MAVAZI KWA WANCHUO

    UVAAJI WA MAVAZI USIZOKUBALIKA KWA WASICHANA/WANAWAKE

    o Gauni au sketi zinazobana na zina urefu wa juu ya goti la mvaaji o Nguo zinazovaliwa na kuonesha mavazi mengine yaliyo ya siri kwa ndani ya mwili o Nguo zilizo na mkato uliokatwa hadi juu ya magoti au maungo o Nguo zote zilizombana na kushikiria mwili mvaaji o Nguo zinazoonesha tumbo,maziwa,kiuno,mapaja na nguo nyingine ndogo za kuvaa kwa

    kupachika na mipasuko o Skafu ( nguo zinazovaliwa kama vipachiko shingoni ),bangili,na mapambo yanayofanya

    mvaaji anaonekana mlimbwende o Nguo za aina zote zilizofupi kama mini o Kilemba,baibui na hijabu wakati wa darasani na idarani wakati wa mazoezi ya vitendo

    UVAAJI WA MAVAZI USIZOKUBALIKA KWA WAVULANA/WANAUME

    o Suruali na kaputula zivaliwazi na kuwa mlegezo zinazovaliwa na kuonesha nduo za ndani

    o Nguo za aina zote zinazovaliwa na kuwa fupi o Nguo kama mashati yanazovaliwa bila kufungwa na vishikizo o Nguo zote zinazovaliwa na kuonesha kiwiliwili o Kofia za soksi kuvaliwa kichwani,kofia,na mifungio ya kiume kichwani o Miwani inayovaliwa kama miwani ya jua iliyo mieusi sana o Nguo zenye mikunjo mikunjo ya hovyo hovyo na suruali kubwa au kaputula

    kubwa,michoro katika mwili kama mbavuni au mikononi au kukarikiti nywele o Kuvaa nywele za bandia au zilizosukwa,heleni masikioni,au nywele kukarikiti,na

    bangili.Mikufu itakayoruhusiwa kuvaliwa ni ile yenye maudhui ya dini za kikristo yenye msalaba au medali

    o Kilemba kuvaliwa peke yake au juu ya kofia

    NAMNA YA KUVAA KWA WOTE ( WAVULANA /WANAUME NA WASICHANA / WANAWAKE ),WANACHUO NA WAFANYAKAZI WOTE WANATAKIWA KUTOKUVAA HIVI:

    o Mavazi yaliyo na maudhui ya kisiasa,au ujumbe usiokuwa na maana au wa yanayotarajia kutokea

    o Aina ya nguo fupi,jinsi katika siku na sehemu zenye kukusanyika katika mahubiri,sherehe ya ufunguzi,kumbukumbu au mahafali

  • 5

    o Miwani mieusi ya jua o Kujichora michoro katika mwili kama mbavuni au mikononi au kukarikiti nywele o Aaina ya nguo tofauti au nguo maalum zitavaliwa kulingana na tangazo maalum

    litakalotolewa na kutfuatia tukio kwa maelekezo kwa kuvaa nguo hizo. o Mavazi yenye kuwa na matangazo yasiyo rasmi,yenye ujumbe wenye picha yenye dira

    na maono ya kutangaza ubora wa kutumia pombe,sigara,madawa ya kulevya. o Viatu vya ngozi lazima vivaliwe muda wa saa za kazi o Wavulana / wanaume wasijiwekee madoido zaidi katika uvaaji na wasichana / wanawake

    wasijipodoe sana kuzidi kiasi

    AINA ZA SARE

    UVAAJI KWA WANACHUO WASICHANA / WANAWAKE AMBAO INABIDI KUFIKA NAZO CHUONI WAKATI WA KUANZA MAFUNZO ISIPOKUWA WANACHUO WA KAZI ZA UUGUZI NA AFYA YA JAMII WAO WATASHONEWA CHUONI SARE ZAO.

    GAUNI.

    o Urefu lazima uwe katikati ya magoti na visigino o Isiwe imebana na isiwe na mapindo kama ilivyoelekezwa na wizara ya Afya Ustawi wa

    Jamii,Maendeleo,Jinsia,Wazee na Watoto o Urefu wa mikono ufikie kwenye kiwiko cha mikono o Rangi iwe nyeupe wanachuo wa maabarana utabibu na pinki kwa wanachuo wauuguzi

    JAKETI

    o Iwe na rangi ya bluu kwa wanachuo wa maabara na isiwe na michoro wala mistari ya michirizi kama ya jezi za michezo

    o Iwe sweta ya mikono mifupi au mirefu ya rangi ya pinki katika kada ya uuguzi

    VIATU

    o Viwe vya ngozi na view vya kufunga au kutumbukiza,visiwe na visigino virefu,view vyeusi au rangi ya ugoro vivaliwe na soksi nyeupe au pinki

    MAVAZI KWA WANACHUO WAVULANA / WANAUME WA MAABARA/TABIBU.

    MASHATI

    o Meupe ya mikono mifupi,itakuwa yatakuwa yanawekwa ndani ( kuchomekea ) ndani ya suluari na iwe na mfuko mmoja juu upande wa kushoto

    o Ziwe imetosha vizuri zisizoshika mwili

  • 6

    SURUALI

    o Ziwe za rangi ya khaki,ndefu hadi kwenye kisigino,na ivaliwe na mkanda mweusi kama ilivyoelekezwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii,maendeleo,jinsia,wazee na watoto

    o Zwe inavaliwa vizuri zisivaliwe mlegezo au zisishike mwili

    KOTI

    o Iwe ya mikono mirefu,ivaliwe muda wote wakati wa mazoezi ya vitendo idarani au wakati wa masomo ya vitendo chuoni

    o Urefu wake ufike kwenye magoti o Iwe na mifuko mitatu ( miwili chini mmoja kila upande na mmoja juu upande wa

    kushoto

    JAKETI

    o Liwe la mikono mirefu au mifupi rangi ya bluu,isiwe na kofia nyuma ya kuvaa kichwani,

    VIATU

    o Viwe vya rangi nyeusi au rangi ya ugoro,visiwe na visigino virefu,vivaliwe na soksi za rangi nyeusi au nyeupe au zambarau

    MAVAZI BAADA YA SAA ZA KAZI.

    MAENEO YA CHUONI

    o Kuvaa nguo binafsi zilizo safi na ziwe za kawaida zisizoonesha maungo

    NYWELE

    WANACHUO WA KIUME

    o Ziwe safi na nadhifu zisizidi nchi moja kwa urefu.Heleni,bangili na ndevu hazitakiwi

    WANACHUO WA KIKE

    o Ziwe safi na nadhifu zisizidi nchi moja kwa urefu,ziweze kuchanwa kwa urahisi. o Nywele zichanwe kwa kwenda nyuma ( kubana ) o Hereni zinaweza kuvaliwa za kupachika na si zile ndefu o Kupaka rangi mdomoni,kwenye kucha hakutakiwi uwapo darasani na idarani wakati wa

    kufanya mazoezi ya vitendo o Wanachuo wanaruhusiwa kusuka mistari ya nyuma ya nywele na hawaruhusiwi kusuka

    rasta na kuchana michano mingine isiyotajwa hapa.Kusuka nywele zisukwe mistari ya nyuma isiyozidi saba ( 7 ) na isipungue mitatu ( 3 ) na siyo rasta

  • 7

    UTEKELEZAJI NA UHIMIZAJI WA UVAAJI WA MAVAZI KWA WANACHUO

    Utekelezaji na uhimizaji wa kuvaa sare za chuo ni kwa mjibu wa jamii iliyopo karibu na taasisi,wakufunzi,na uongozi wa taasisi:

    o Kuwafuatilia wanaovunja taratibu au wasiovaa inavyotakiwa na taasisi wawapo chuoni au anapokuwa akitoa huduma wakati wa mafunzo

    o Aidha kuvunja sheria za uvaaji mavazi yanayostahili kwa sheria zilizowekwa kwa kuvaa mavazi,inaweza kutolewa taarifa kwa mlezi wa wanachuo/mkuu wa idara au mkuu wa taasisi,na ishughulikiwe kwa kuchukuliwa hatua kali.Taarifa hii pia inaweza kutolewa katika kamati ya nidhamu ya taasisi,kwa hatua zaidi ya kinidhamu.

    o Mwana chuo yeyote atakayeenda kinyume cha taratibu au sheria za uvaaji mavazi,iliyoainishwa hapa kisheria,atahesabika kuvunja sheria iliyowekwa na afisa/maafisa au uongozi wa taasissi.

    KUVUNJA SHAERIA YA UVAAJI MAVAZI CHUONI

    Atakayevunja sheria ya mavazi,katika sheria ya uvaaji wa mavazi chuoni kwa kuvunja au kurudia rudia kwa makusudi uvunjifu wa sheria hii atahesabika mkosaji wa makosa ya kuvunja sheria.Kwa kuwa na ukosaji wa namna hiyo,mkosaji atahesabika kuwa amefanya kosa kwa mara moja au makosa yote kwa mara moja au yote kwa pamoja kuwa:

    o Atakayekosa mara ya kwanza atahesabiwa kutenda kosa anawezapata onyo la mdomo au kwa maandishi na kuonywa kuwa,lisitokea tena kosa jingine la jinsi hiyo

    o Kwa kutenda kosa mara ya la pili au la tatu,anapokuwa katika muda wa matazamio,kutoka alipotenda kosa,akifanya kosa tena ndani ya muda wa matazamio,kosa litahesabika kuwa kubwa zaidi.Mkosaji anaweza kupelekwa kujadiliwa katika kamati ya nidhamu ya chuo,na haitazuia kufukuzwa au kuachishwa masomo.Muda wa matazamio,utakuwa utatolewa na mamlaka / uongozi wa chuo kulingana na kosa.

    o Mwisho,tamko la kuachishwa au kufukuzwa chuo linaweza kuamuliwa kama mkosa atakuwa ameendelea kufanya kosa tena,na kuamliwa atoke chuoni baada ya kuwa amepewa onyo,na kupewa adhabu ya kuachishwa masomo katika muhula husika,kadri kamati ya nidhamu au uongozi wa chuo utakavyoamua.

  • 8

    VITU VINGINE BINAFSI NA MUHIMU VYA KUJA NAVYO CHUONI

    Utakapokuwa unakuja chuoni,unaombwa kufika na vifaa vifuatavyo:

    Jozi mbili za viatu vyeusi au vyenye rangi ya ugoro vya ngozi,visivyo na visigino virefu wala havina mapambo ya rangi tofauti tofauti

    Sweta la rangi ya bluuau jaketi kwa wavulana na sweta za rangi ya pinki kwa wasichana Blanketi 1,foronya 1 na funiko lake,taulo 1 na shuka 3,chandarua na saa ya mkononi ya

    mishale

    Madaftari ya kuandikia ya wastani ya kati yawe 10 Tochi 1,ndoo 1,chupa ya chai 1 Picha ndogo 3 za mkato Bp mashine na manati yake (sthethoscope),kipima joto ( thermometer) kwa wanachuo

    wauguzi na tabibu

    Mwanvuli.

    TAASISI YA SAYANSI ZA AFYA INAKOPATIKANA

    Taasisi ya sayansi za afya Nkinga,iko katika hospitali ya rufaa ya Nkinga,kilomita 120 kaskazini mashariki ya manispaa ya Tabora ambapo ni makao makuu ya mkoa na kilomita 47 kutoka mjini Nzega.Wanaosafiri kutoka mikoa ya kaskazini mwa nchi wanaweza kuteremka Nzega mjini na kupanda bus au mabas madogo yanayokuja Nkinga.

    Wanaosafiri kwa gari moshi toka mikoa ya Kigoma,Mwanza au Dar Es Salaam watateremka Tabora na kupanda magari yanayopita Nkinga kwenda Igunga au kuja Nkinga.Pia wanaweza kupanda mabus yanayoenda Nzega ambapo watapata usafiri wa mabus au bus ndogo kuja Nkinga.

    Watakao kuwa wanasafiria mabus kutoka Mwanza mabus yanayoenda Dar Es Salaam,Arusha,Moshi,Singida,Dodoma,Morogora,Iringa au Mbeya wateremke Nzega,watapata mabus au bus ndogo zinazo kuja Nkinga.Watakaotumia mabus yanayotoka Dar Es Salaam,wapande mabus yanayoenda Mwanza,Kahama au Kigoma na wakifika Nzega wateremke wapande mabus au bus ndogo zinazokuja Nkinga.

    HONGERA SANA KARIBU KATIKA TAASISI YA SAYANSI ZA AFYA NKINGA.

  • 9

    MEDICAL EXAMINATION CERTIFICATE

    SURNAME…………………………………..OTHER NAMES………………………….………

    AGE…………………………………………..SEX…………………………………………………..…

    MARITAL STATUS…………………………CITIZENSHIP……………………………..…….

    PERSONAL HISTORY

    Is the examinee suffering from any of the following? Indicate Yes or No.

    1. Allergy disorder………………………………………………………………………………...

    2. Heart Disease…………………………………………………………………………………...

    3. Kidney or urinary disease………………………………………………………………...

    4. Diabetes…………………………………………………………………………………………..

    5. Epilepsy…………………………………………………………………………………….……..

    6. Deformity………………………………………………………………………………..………

    7. Psychotic……………………………………………………………………………………..….

    8. Eye disorder……………………………………………………………………………….……

    PHYSICAL EXAMINATION

    1. Height ………………………… 2. Weight…………………………………….

    3. Skin disease…………………… 4. Eye Conjunctivae

    Pupils……………………………………

    Vision Right……………………………

    Left……………………………………..

    5. Please state condition of Ears (If any discharge)…………………………………..

    Nose……………………………………………………………………………………………………..

    6. Any Abnormality…………………………………………………………………………..……..

    7. Cardiovascular system…………………………………………………………….…………..

  • 10

    Blood Pressure: Systolic……………............................................................

    Heart: Any Murmur? Diastolic……………………………………………………..……....

    8. Abdomen……………………………Hernia………………………………………….…………..

    Masses…………………………………………………………………………………………….…….

    Liver…………………………………………………………………………………………………….…

    Kidneys………………………………………………………………………………………..…………

    Any clinical evidence of hyperacidity or gastric duodenal ulcer...................

    LABORATORY INVESTIGATION

    1. Urine albumin…………………………………………………………………......................

    Sugar……………………………………………………………………………………………………..

    Bilharzia…………………………………………………………………………………………….…..

    2. Stool: special emphasis on WORMS…………………………………………………………

    3. Blood examination: Hb Level…………………………………………………………………..

    4. Serology: VDRL……………………………………………………………………………………….

    5. Pregnancy Test ……………………………………………………………………………………...

    CONCLUSION

    ………………………. ………………………… …………………………..

    Name Signature Qualification

    ………………… ………………….

    Date Official Stamp

    I have examined Mr./Mrs./Miss/Sir/Br/Fr/………………………….and Considered that he/she is/physically/ not physically and mentally fit to be admitted to higher studies