Upload
kassim-hussein
View
1.099
Download
7
Embed Size (px)
Citation preview
Figa la tabia katika elimu ya juu: Tusomeshe
nini, tusomeshaje?
Kassim Hussein, PhD
[email protected] Cell: 0754360174
Maudhui • Katika mchakato wa kusoma na
kusomesha, sufuria ya ya elimu huwekwa juu ya mafiga matatu:
–Maarifa (knowledge)
–Stadi (skills)
–Tabia (behaviors)
Msukumo • Yako mambo kadhaa yamenipa msukumo:
– Kwanza tukiunda mitaala huwa rahisi kuanisha maarifa na stadi zinazotakiwa kusoma au kusomesha.
Mathalani:
– Tunafahamu kazi za mhasibu na ili mhasibu au awe na maarifa husika tunaoorodhesha yanayohitajika. Mitaala yetu hutaja maarifa pia huoorodhesha vitabu vya kiada na vya kurejelea kufikia malengo hayo.
Msukumo • Kuhusu tabia, mitaala yetu huwa
kimya na hakuna malengo wala, tabia husika hazijaooridheshwa na hakuna hata vitabu vya kiada au machapisho ya kurejelea.
Msukumo • Katika kuanzisha mwaka mpya wa
masomo na hata wakati wa mahafali, wageni rasmi husisitiza tabia njema kwa wanafunzi au wahitimu. Aghlabu tabia zenyewe huwa haziwekwi wazi.
Msukumo • Niliombwa na wenzagu
niwape nasaha na uzoefu wangu, nikawa sina. Ila nikatoa ahadi na leo ninatimiza kwa maswali mawili.
Msukumo • Maswali ni juu ya tabia:
tusomeshe nini na tusomesheje? Maswali ambayo nikaona yanahitaji kuanzisha mjadala juu ya tabia ili kuyatafutia majibu
Msukumo • Itakuwa nimefungua mlango
wa kutambua, kuchagua na kuzisoma/kusomesha tabia husika.
Msukumo • Ilikuwa haja yangu kujaribu tafiti
shirikishi kuhusu jambo la msingi katika elimu ya Tanzania.
• Hivi ni nini kimefanya wanafunzi kuandika matusi au bongo flavour katika mitihani?
Msukumo • Ni nini kinafanya wahitimu
wengine wapendelewe katika soko la ajira ?
Tabia - maana • Ni sehemu ya elimu iliokamilika au
UWEZO
• Inahusika na tathmini ya utu, vitu, mambo au matukio
– Inaelekeza fikira (cognitive function)
– Inashawishi hisia (affective function)
– Inaathiri hatua (conative function)
Organizational Behavior 12
USAWA WA BAHARI TABIA
MIKO – VIGEZO – UAMUZI
Mtazamo DHAMIRA – MAADILI - IMANI
Wengine huiona
Wengine hawaioni
Nadharia ya tabia • Hulka ambazo mtu huzaliwa nazo….
Vipaumbele juu ya kufikiri, kutoa maamuzi, mahusiano na nishati ya mwili.
• Kuna tabia zitokanazo na malezi, upendo na mazingira ya mtu kutokana na wazazi na jamii aliyokulia.
• Kuna tabia zianzofunzwa sambamba na taaaluma yaani kuzisoma na kusomesha.
Asiefunzwa na ……, hufunzwa na ….
•Katika nadharia ya tatu, juu ya tabia katika mchakato wa elimu ya juu, kuna orodha ndefu ya tabia stahiki.
Asiefunzwa na ….., hufunzwa na ….
• Tabia zote ni muhimu, ila kwa wahadhiri kuna haja ya kuziainisha, na kuamua kuziiingiza baadhi kwenye mitaala rasmi au iliokubalika na wengi.
Kuna haja, ulazima wowote?
• Chimbuko la haja: hutokana na wasomi wenyewe; yaani msomaji na msomeshaji
• Wadau wengine: taasisi, serikali, jamii nk
Kuna haja? • Dunia ni soko la ajira inahitaji wahitimu
walioelimika yaani wenye uwezo (maarifa + stadi + tabia)
• Uwezo ( au competency) ni jumuisho la maarifa (applied), stadi za kazi na tabia (attributes/ behaviours/attitudes) ili kufanya kazi nzuri zaidi ya kiwango cha kawaida. (McClelland, 1973)
Haja za Wasomi •Kuna nadharia moja ya
muundo, tabia na utendaji (S – C – P) kwamba utendaji wa mtu unaathriwa na tabia na inatokana na muundo.
Haja za Wasomi • Muundo huenda ukawa umiliki,
vyanzo vya mapato, kipimo (ukubwa), jiografia, wakati , jinsia nk hulazimisha kusoma au kusomesha tabia fulani.
• Mathlani kuhusu umiliki: kuna vyuo vya serikali , vya dini au vya binafsi?
Mifano – vyuo vya dini
• Vyuo vya taasisi za dini hutaka kutambuliwa kuwepo kwa mungu, kujenga tabia za dini husika na hairuhusu kufuru kwa mfano dhana za Charles Darwin kuhusu asili ya binadamu.
Mifano – vyuo vya dini
• Vyuo hivi hufundisha tabia zinazo endana na imani za dini kama vile haramu, halali , makuruhu, utumishi wa mungu nk
Mifano – vyuo vya dini
• Kwa mfumo huu, chuo ni zizi, walimu na wachungaji na wanafunzi ni wachungwa. Kwa hiyo wachungaji ni masuuli – wataulizwa mbele ya mungu juu ya dhima ya tabia za waliowachunga kama zimeenda kombo
Mifano: Vyuo vya serikali • Vyuo vya serikali hustawisha fikra ya kutafuta
ukweli na kuruhusu imani mbalilmbali na hata zile zinazo kubali kuwepo kwa mungu na zile zinazokataa kuwepo kwa mungu.
• Wakati wa kupigania uhuru, au wa ukombozi vyuo hivi hukazania fikra za walioshika uongozi wa serikali.
• Mathlani serikali ya kijamaa ilizaa watu wenye tabia za uzalendo, wapenda haki na utu na haya yalikuwepo ndani ya mitaala.
Vyuo binafsi
• wadhamini huwa na malengo ya kufikia ndoto za walengwa na hulenga kufanikiwa, kushinda, na ujasiria mali. Tabia zinazowekwa makazo ni pamoja na kuwa mshindani, mjasiriamali, kiongozi nk
Vyuo binafsi
• Sera za vyuo zimeelemea kuwa mwanafunzi ni mteja na mteja anahaki ya kuchagua atakachotaka kusoma au kusomeshwa.
Vyuo binafsi
• Msomeshaji anawajibu wa kumridhisha kila mteja, mara ya kwanza na kila mara. Elimu ni bidhaa na kwa hiyo mfumo wa masomo ni wasoko huria.
Vyuo binafsi
• Mwanafunzi huamua atakacho soma yeye na msomeshaji atalazimika kumridhia mteja wake. Kwa maana hii, tabia hata figa la tabia katika elimu ni uchaguzi wa msomi mwenyewe.
Vyuo binafsi • Tabia nazo huwa katika bidhaa kama
vile Entrepreneurship, Diversity, nk.
• Wasomeshaji/ wahadhiri hufanikiwa kama wanasajili wanafunzi wengi na kutathminiwa kuwa wanawajali na kuwaridhisha wateja wao.
Swali letu la msingi
• Tufundishe nini, tufundishaje?
–kuandaliwa orodha ya tabia muhimu zinazostahiki kila mhitimu awe nazo
–Tuainishe zile za muhimu,
–Tuzifundishe vipi?
Jitihada za kuanisha ‘Tabia’
• Azimio la UNESCO juu ya tabia ni pamoja na uraia, tabia za kushirikiana na jamii, uwezo, kuchunga haki za binadamu, maendeleo endelevu, demokrasia, na amani katika misingi ya haki.
• Nyingine ni utamaduni wa kujiendeleza na kuleta maendeleo
Jitihada za kuanisha ‘tabia’ – JKN (Elimu ya Kujitegemea)
• Mwalim alibainisha tabia za kujitegemea, tabia za kuhudumia umma na tabia za kutatua au kuwaondelea watu (wananchi) matatizo na migogoro.
Ameainisha:
• Ushirikiano ( na sio maendeleo ya mtu binafsi)
• Fikra za usawa
• Wajibu wa kutoa huduma
Jitihada za kuanisha ‘tabia’ – JKN (Elimu ya Kujitegemea)
• Akili ya kuchunguza
• Uwezo wa kujifunza
• Uwezo wa kukataa au kukubali vitu wanavyofanya wengine kufuatana na mahitaji binafsi
• Kujiamini kama mtu sawa na huru
• Anaethamini wengine na anathaminiwa … kwa anachokifanya na si anachokipata
Jitihada za kuanisha
• SAUT- “To prepare and mould men and women of integrity, devotion, commitment, principled, accountable, capable of taking risk; for future performance of leadership roles in society, and occupying positions of influence in public life, professions, industry and commerce in order to be able to realize the ideals of a good and just society”
Jitihada za kuanisha
• SAUT……. ‘In other words to have personnel who are mentally and morally fit. ... to us, through the Word of God, Catholic Tradition and Teaching of the Church’
MUM works to produce highly educated and well trained human
resources inculcated with the appropriate aptitudes and attitudes for
the material, moral and spiritual development of the society through:
Knowledge Seeking
Community Built on Respect and
Tolerance
Academic freedom,
Creativity and Innovation
Integrity and
Prudence
Collegiality and
Collaboration
Spiritual and
Academic Balance
Excellence Responsibility
and Accountability
Trust and Teamwork
1. Kufanya kazi katika timu
2. Kuwezana na wafanyakazi
wengine
3. Kuheshimika na wengine
4. Kujieleza kimaandishi
5. Kujieleza kwa kusema
6. Usiikvu na kuelewa
7. Kujifunza na kuwafundisha
unaowasimamia
8. Kupangana kupangilia
9. Kuongoza, kuhamasisha na
kutatua migogoro
10.Kuanzisha na ubunifu
11.Kuwasilisha kazi sahihi kwa
wakati
12.Bidii na kutochoka
13. Kuridhisha unachohitajika kutimiza
14. Kufanya kazi za ziada
15. Kukubali majukumu na kuyatimiza
16. Kufanya maamuzi sahihi
17. Kuwahudumia wateja
18. Kuonyesha unafuata na wasaidiza
wako
19. Kuwasaidia viongozi wako
20. Utii wa maelekezo halali ya viongozi
wako
21. Kutumia muda wa kazi kufanya
mambo ya kazi
22. Kutoa huduma bora bila ya kichocheo
chochote
Serikali katika OPRAS inataka tabia hizi
Tufundishe ‘Utu’ • Utu au kwa lugha za kusini “ubuntu” ni
ufundi au tasnia ya a kuwa binadamu (Ivorgba, 2009).
• Utu au “ubuntu” kwa semi za Zulu: “umuntu ngumuntu ngabantu”, inamaanisha utu wa mtu unapatikana toka kwa mtu mwingine
Tufundishaje? • Kwanza: Tukumbuke kuwa
huwezi kufundisha usichokijua au kuwa nacho!!
• Haja ya kujiandaa/kuandaliwa kuwa na tabia husika.
Tufundishaje?
• Pili, maandalizi ni pamoja na njia za kufundisha, kupima na kutathmini tabia
• Tatu, kuikimu nidhamu na kuiweka hali shwari ya kusoma na kusomesha. Kowalski, (2003) anatoa mifano ya tabia za kitoto, za kuudhi na inajumuisha kuchelewa, kuundoka kabla ya wakati, kuongea pembeni, kuchelewesha kazi, udanganyifu, kujipatia alama zisizo haki.
Tufundishaje? • Boice (1998) anaona tabia hizi
pia huchangiwa na wasomeshaji kwa kutoweka misingi ya nidhamu na kuisimamia.
Tufundishaje? • Tabia za kuharibu uendeshaji wa
masomo, usumbufu, kuwapunguzia wasomaji wengine ari na kuwavunjia heshima.
• Tunasimamia vipi nidhamu?
Tufundishaje? • Wasomeshaji, wajifunze tabia
husika
• Watayarishaji wa mitaala…. Ziwekwe vipi? Zipimwaje?
Tufundishaje? • Kuweka masomo maalumu yenye kufundisha
tabia husika
• Baadhi ya tabia ziwe ni sehemu ya masomo mengine
• Njia za kuwasilisha somo juu ya tabia zitokane na utaalamu wa msomeshaji na ari ya msomaji
Hitimisho • Haja ya kuzitambua tabia husika
• Kuziweka katika mitaala
• Kuwaandaa walimu kuzisomesha
• Kuwaandaa wanafunzi kujifunza
Marejeo
• Boice, R. (1998). "Classroom incivilities." In K. A. Feldman & M. B. Paulson (Eds.), Teaching and learning in the college classroom (2nd ed.) (347-369). Needham Heights, MA: Simon & Schuster Custom Pub
• Kowalski, R. M. (2003). Complaining, teasing, and other annoying behaviours. New Haven, CT: Yale University Press.
• Ivorgba, E.A. (2009) Values in African thought. (http://valuesinworldthought.authorfriendly.com/pages/p....) • McClelland, D. (1973). Testing for competence rather than
for "intelligence." American Psychologist, 28, 1-14 • McClelland, D. (1978) Guide to Behavioral Event
Interviewing, Boston: McBer and Company.
Marejeo
• Nyerere, J. Elimu na Kujitegemea, Oxford University Press
• Nyerere, J. Uhuru na Maendeleo. Oxford University Press 1968
• UNESCO. 1998. The Role of Higher Education in Society: Quality and Pertinence. Paris, UNESCO.
• URT, OPRAS form