Transcript
  • 1

    TANZANIA PORTS AUTHORITY

    www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 25 23 - 29 Disemba, 2013

    Matukio mbalimbali ya Michezo Uk. 13

    Bila tija na ufanisi hakuna michezo - Massawe Uk.3

    Wanamichezo Wastaafu Waagwa rasmi Uk.4

    Na Focus Mauki

    Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imefanikiwa kutetea ubingwa wake katika michezo ya Bandari, ‘Inter-Ports Games’ kwa kufanikiwa kuibuka washindi wa jumla wa mwaka 2013. Inaendelea Uk. 2

    Dar Port mshindi wa Jumla Inter-Ports• Mshindi Nidhamu-Bandari za Maziwa• Mshindi Ushangiliaji-Bandari ya Tanga

    Wachezaji na mashabiki wa Bandari ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe na Mwenyekiti na DOWUTA Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Athuman Mkangara.

    Furaha ya ushindi

  • 2

    Bandari ya Dar es Salaam wameibuka mabingwa kwa kupata alama 108, mbele ya Bandari ya Tanga ambayo imekuwa mshindi wa pili kwa kupata alama 74. Timu ya Makao Makuu nayo imeshika nafasi ya tatu kwa kupata alama 33, huku Bandari za Maziwa ikishika nafasi ya nne kwa kupata alama 17 na Bandari ya Mtwara kuambulia nafasi ya nne kwa kupata alama 7.

    Matokeo hayo yameifanya Bandari ya Dar es Salaam kupata na vikombe vingi zaidi na kuibuka washindi wa jumla. Katika mpira wa miguu, Dar Port waliibuka washindi wa kwanza kwa kujinyakulia alama 12 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Bandari za Maziwa iliyopata alama 9, huku

    ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga waliopata alama 6.

    Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kamba wanawake ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam ambayo ilipata alama 8 na Bandari ya Mtwara ilishika nafasi ya pili kwa kupata alama 6 huku mchezaji Bora akiwa ni Rubby Jaffari wa Bandari ya Mtwara.

    Mchezo wa bao nao umeshuhudia timu mbili zikiibuka na ushindi ambapo Bandari ya Dar es Salaam imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 12 na Makao Makuu wakishika nafasi ya pili kwa kupata alama 5, huku mchezaji bora wa mchezo wa bao akiwa ni Omary Saidi wa Bandari ya Dar es Salaam.

    mchezaji Bora wa soka akiwa ni, Mrisho Biboze wa Makao Makuu. Kwa upande wa mpira wa pete mshindi ni Bandari ya Dar es Salaam aliyepata alama 6 na nafasi ya pili imenyakuliwa na Bandari ya Tanga iliyopata alama 4 huku mchezaji bora wa mchezo huo akiwa ni Nuru Fundi.

    Kwa upande wa mchezo wa kikapu timu ya Makao Makuu imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa kupata alama 8 huku Bandari Tanga ikishika nafasi ya pili kwa kupata alama 7 na mchezaji bora wa kikapu akiibuka kuwa ni Gerald Baru (Mgaya).

    Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya wanaume Bandari ya Dar es Salaam imetetea nafasi yake kwa kunyakua alama 8 na nafasi

    Inatoka Uk. 1

    Toleo Maalum la Michezo

    Timu ya riadha ya Bandari ya Dar es Salaam.

  • 3

    Toleo Maalum la Michezo

    Bila tija na ufanisi hakuna michezo - Massawe

    • Katibu DOWUTA Taifa asifu ushirikiano

    Katibu Mkuu Dowuta Taifa, Bw. Jonathan Msoma (kulia) akiweka saini katika mpira, huku mwamuzi wa kimataifa wa mpira wa miguu Othman Kazi (kushoto) akishuhudia.

    Na Focus Mauki

    Michezo ya ‘Inter-Ports Games’ imelizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Sigara (TCC Club), ambapo wanamichezo 400, wafanyakazi wa Bandari mbalimbali zilizo chini ya Mamlaka, walishiriki michezo ya mpira wa miguu, pete, kikapu, riadha, bao, kuvuta kamba, kurusha tufe na mkuki.

    Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine kwa washindi, Katibu Mkuu wa DOWUTA Taifa, Bw. Jonathan Msoma ameushukuru Uongozi wa Mamlaka kwa kukitambua chama na kukipa nafasi ya kufunga michezo hiyo iliyofaana.

    “Hili ni jambo la kihistoria haijawahi kutokea kwa DOWUTA kupata nafasi hii muhimu ya kuwa mgeni rasmi, katika michezo hii napenda kuushukuru Uongozi kwa kutupa nafasi hii na sisi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuona Bandari zetu zinafanikiwa katika kiwango cha juu,” amesema Msoma.

    Msoma amewakumbusha wafanyakazi kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujenga afya zao lakini kubwa zaidi wakumbuke kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

    Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe ambaye alimwakilisha Kaimu

    Mkurugenzi Mkuu Eng. Madeni Kipande, amewakumbusha wafanyakazi kwamba wamepewa dhamana kubwa na Taifa ya kusimamia Bandari hapa nchini na kuongeza kuwa ni wajibu wetu sote kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa.

    “Napenda niwakumbushe

    kwamba uamuzi na hatima ya michezo hii ipo mikononi mwetu wote, mkiongeza tija basi tutakuwa na uhakika wa michezo hii kuendelea, lakini kama tija itashuka basi itakuwa ni hatima ya michezo hii, hivyo wote tufanye kazi kwa bidii, uadilifu na ufanisi ili michezo hii iendelee kuwepo,” amefafanua Massawe.

  • 4

    Toleo Maalum la Michezo

    Na Mwandishi Wetu

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Eng. Madeni Kipande amezawadiwa tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa michezo ya Inter-Ports kwa mwaka 2013.

    Tuzo hiyo imetolewa na Kamati Kuu ya Michezo kwa kutambua mchango wa Eng. Kipande, katika kusimamia na kutekeleza michezo ndani ya Mamlaka.

    Tuzo hiyo ya heshima ilipokelewa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu kwenye hafla ya kufunga michezo hiyo.

    Kaimu Meneja Mawasiliano, Bi. Janeth Ruzangi amenukuliwa akisema, “kamati kuu imeamua kutoa tuzo hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutokana na ukweli kwamba ameshiriki kwa karibu katika kuhakikisha kwamba michezo ya mwaka huu iliyofanyika jijini Dar es Salaam inafanikiwa kwa kiwango kikubwa.”

    Na Focus Mauki

    Wanamichezo Wastaafu wameagwa rasmi wakati wa kufunga michezo ya Bandari iliyomalizika Disemba 14 katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

    Wanamichezo ambao wanakaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria ni pamoja na mchezaji wa Riadha, Sikujua Saidi na William Kakusa kutoka Makao Makuu.

    Wanamichezo wengine na michezo wanayocheza katika mabano ni kutoka Bandari ya Tanga, Twaha Shali (kamba), Bakari Kombo (bao), Saidi Rajab (bao) na Alifa Juma (bao).

    Kwa upande wa Bandari ya Mtwara ni Hassani Madafu ambaye ni mchezaji wa mpira wa miguu na Exoud Minja mchezaji wa Kikapu kutoka Bandari za Maziwa.

    Eng. Kipande apewa tuzo ya heshima ya

    mwanamichezo Bora Inter-Ports 2013

    Wanamichezo Wastaafu

    Waagwa rasmi

    Eng. Madeni Kipande

  • 5

    Toleo Maalum la Michezo

    Wanamichezo Wastaafu wakipokea zawadi zao

  • 6

    Toleo Maalum la Michezo

    Na Focus Mauki

    Selemani Malwilo kutoka Bandari ya Dar es Salaam na Amina Kubo kutoka Bandari ya Tanga wameibuka kuwa wachezaji bora wa ridha katika michezo ya Bandari 2013.Mchezo wa riadha ulishindaniwa katika riadha mita 100, mita 200 na mita 400, ambapo mita zote hizo zilikuwa na timu za wanaume na wanawake.

    Kwa upande wa riadha mita 100 (wanaume), nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Selemani Malwilo (Bandari ya Dar es Salaam), nafasi ya pili ilichukuliwa na Almancius Vedasto (Bandari za Maziwa) na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Luhinda Mtambalike (Bandari ya Dar es Salaam).

    Riadha mita 100 (wanawake) nafasi ya kwanza imechukuliwa na Fadhila Yusuph (Bandari ya Dar es Salaam), nafasi ya pili imekwenda kwa Nuru Fundo (Bandari ya Dar es Salaam) na nafasi ya tatu imechuliwa na Ramla Hamisi (Makao Makuu).

    Mchezo wa riadha mita 200 (wanaume) nafasi ya kwanza imechukuliwa na Selemani Malwilo (Bandari ya Dar es Salaam), nafasi ya pili imekwenda kwa Salimu Bakari (Bandari ya Dar es Salaam) na Josephat Ezekiel (Bandari ya Tanga) ameshika nafasi ya tatu.

    Kwa upande wa ridha mita 200 (wanawake), Ramla Hamisi (Makao Makuu) ameshika nafasi ya kwanza, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Edith Msami (Bandari ya Dar es Salaam) na ya tatu ikienda kwa Lucy Kakologwe (Bandari ya Dar es Salaam).

    Malwilo na Kubo vinara wa Riadha

    Mchezaji bora wa riadha wanaume, Selemani Malwilo kutoka Bandari ya Dar es Salaam akipokea zawadi ya ushindi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Awadhi Massawe na Katibu Mkuu wa DOWUTA Taifa, Bw. Jonathan Msoma.

  • 7

    Toleo Maalum la Michezo

    Nafasi ya kwanza ya riadha mita 400 (wanaume) imekwenda kwa Mrisho Harambe (Makao Makuu), huku Josephat Ezekiel (Bandari ya Tanga) akishika nafasi ya pili na Florian Kamugisha (Bandari ya Dar es Salaam) akishika nafasi ya tatu.

    Kwa upande wa wanawake mita 400, nafasi ya kwanza imekwenda kwa mfukuza upepo mahiri, Lucy Kakologwe (Bandari ya Dar es Salaam), nafasi ya pili ikishikwa na Zuwena Ibrahim (Makao Makuu) na Victoria Ligidagiza (Bandari ya Tanga) akishika nafasi ya tatu.

    Kwa upande wa mchezo wa kupokezana vijiti relay mita 100 wanaume, timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa kwanza, mbele ya Tanga huku Bandari za Maziwa ikishika nafasi ya mwisho.

    Mchezo wa ‘relay’ mita 100 wanawake, timu ya Bandari ya Dar es Salaam wanawake imepata ushindi wa kwanza, nafasi ya pili ikiienda kwa Bandari ya Tanga na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Makao Makuu.

    Mchezo wa tufe nao haukubaki nyuma ambapo tufe wanaume mshindi ni Mohamed Fazal (Bandari ya Tanga), nafasi ya pili ni Joseph Mwambipile (Bandari ya Tanga) na nafasi ya tatu imekwenda kwa Siraj Yusuf wa Bandari ya Dar es Salaam.

    Nao wanawake kwenye mchezo wa tufe hawakubaki nyuma ambapo mshindi wa kwanza wanawake ameibuka kuwa ni Amina Kubo (Bandari ya Tanga), nafasi ya pili imekwenda kwa Oliver Ngomuo (Bandari ya Dar es Salaam) na nafasi ya tatu imekwenda kwa Jaliobeth Palangyo wa Bandari ya Tanga.

    Mchezo wa kurusha mkuki nao ulikuwa na hamasa ambapo washindi kwa upande wa wanaume ni Siraj Yusuf (Bandari ya Dar es Salaam), Mbwana Hatibu (Bandari ya Tanga) amepata ushindi wa pili huku Abdallah Mtandu (Bandari ya Dar es Salaam) akipata ushindi wa tatu.

    Washindi wa kurusha mkuki wanawake ni Amina Kubo (Bandari ya Tanga) na nafasi ya pili imekwenda kwa Modesta Kaunda kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

    Mchezaji bora wa riadha wanawake, Amina Kubo akipongezwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Awadhi Massawe kabla ya kupokea tuzo yake kutoka kwa Katibu Mkuu wa DOWUTA Taifa, Bw. Jonathan Msoma.

  • 8

    Matukio mbalimbali ya michezo katika picha

    Mshindi wa kwanza wa kurusha tufe, mkuki na mwanariadha bora, Amina Kubo akijiandaa kurusha tufe katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivi karibuni.

    Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Maabad Hoja akizungumza na wanamichezo.

    Timu ya Kamba wanawake Mtwara ikiwa kazini.

    Wacheazaji wa timu ya pete ya Bandari ya Tanga wakiwa katika picha pamoja kuanzia kushoto ni Anjella Kapaya, Mwanahamisi Ramadhani, Jane Palghyo, Amina Kubo, Beatrice Siriwa, Sina Juma Martha Mwakabambo.

  • 9

    Matukio mbalimbali ya michezo katika picha

    Timu ya Kamba wanawake Mtwara ikiwa kazini. Mashabiki wa Bandari ya Tanga wakiipeperusha vyema bendera ya timu yao.

    Wacheazaji wa timu ya pete ya Bandari ya Tanga wakiwa katika picha pamoja kuanzia kushoto ni Anjella Kapaya, Mwanahamisi Ramadhani, Jane Palghyo, Amina Kubo, Beatrice Siriwa, Sina Juma Martha Mwakabambo.

    Wachezaji wa timu ya kamba kutoka Bandari ya Tanga wakiwa katika picha ya pamoja kuanzia kushoto ni kocha mkuu wa timu hiyo Ngugu Damian Mabena, Mbwana Hatib, Twaha Shali, Joseph Mwakimbile, Moses Kisanga, James, Kayoka, Abdalah Wazira, waliochuchumaa kuanzia kulia ni Abushe Ramadhani, Mohamed Hamza, Musa Lah, Ndewa Nasiri pamoja na Hassani Mikidadi.

  • 10

    Toleo Maalum la Michezo

    Na Cartace Ngajiro

    “Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mashindano ya interport Games salama licha ya changamoto tulizokutana nazo uwanjani hasa mchezo wa kuvuta kamba ambao ulikuwa na changamoto kubwa sana mwaka huu, Pili napenda kuupongeza Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kwa kuwezesha michezo hii” hivi ndivyo alivyoanza kusema mchezaji huyu wakati wa mahojiano haya.Anaitwa Joseph Mwikabe kutoka kitengo cha ulinzi Bandari ya Dar es Saalam, lakini kwa jina la utani anaitwa Gazza alipewa jina la Gazza kwa sababu alikuwa anacheza sana mpira wa miguu na wakamfananisha na Gazza.

    Ukibahatika kukutana na Gazza katika eneo lake la kazi akiwa amevalia mavazi ya kazini huwezi kujua huyu kijana ni msakata kabumbu mzuri sana uwanjani anayechezea namba 7 yaani kiungo wa pembeni, mbali na kuimudu vizuri namba 7 pia anaweza kucheza vyema namba 10 akiwa kama mshambuliaji wa kati.

    Mchezaji huyu alifanya mahojiano hivi karibuni na mwandishi wa makala hii na kuongea mengi. Hii ni sehemu ya maswali na majibu ya mahojiano ya nyota huyu aliyefunga magoli matatu katika michezo ya mwaka huu.

    Swali: Unazungumziaje mi-chezo ya Inter-Ports Games mwaka huu?

    Jibu: Mashindano ya mwaka huu yalikuwa magumu sana sababu kila timu ilikuwa imejiandaa vizuri na kila timu

    ilikuwa inataka iondoke na ubingwa ndio maana kulikuwa na ushindani mkubwa.

    Swali: Unajisikiaje kuwa mchezaji uliyefunga magoli mengi zaidi katika mchezo wa mpira wa miguu

    Gazza: nyota iliyong’araInter-Ports Games 2013

  • 11

    Toleo Maalum la Michezo

    Jibu: Kwakweli najisikia furaha sana kuwa mchezaji niliyefunga magoli mengi tofauti na wachezaji wengine walioishia kufunga goli moja au mawili.Pia nafikiri nilicheza vizuri na kufuata maelekezo ya mwalimu wangu.

    Swali: Umewezaje kucheza kwa kiwango hicho ulichokionyesha?

    Jibu: Kwanza kabisa ni kujiepusha na vishawishi kama vile ngono na ulevi, pili ni kujua jukumu lako mbeleni na kujitambua na kufuata misingi ya uchezaji.

    Swali: Ni mechi ipi ilikuwa ngumu kwenu pia ni mchezaji gani ulikuwa unamkubali zaidi katika mashindano hayo?

    Jibu: Mechi iliyokuwa ngumu ni siku ya fainali tuliocheza na timu ya Maziwa Makuu, kwakweli ilikuwa mechi ngumu kwasababu timu zote zilikuwa na pointi sawa isipokuwa tofauti ya magoli hivyo ilitubidi tucheze kwa akili sana ili kuweza kupata pointi tatu za ushindi.

    Kwa upande wa mchezaji ninayemkubali ni Karimu Sabu kwa sababu ana nguvu na akili nyingi uwanjani na ana mbio sana.

    Swali: Unazungumziaje ushirikiano uliopo kati ya viongozi na wachezaji?

    Jibu: Kwa upande wetu ushirikiano ni mzuri kwa kweli labda timu zingine, upande wetu sisi viongozi wanatusikiliza vizuri na wanaukubali ushauri tunaowapa.

    Swali: Unawezaje kupanga muda wa kazi na mazoezi?

    Jibu: Inategemeana na shifti ya kazini, kama naingia kazini asubuhi jioni nafanya mazoezi na wenzangu katika klabu yetu ya michezo “Haurbours sports club” na kama naingia kazini jioni basi asubuhi naenda kufanya mazoezi.

    Swali: Ni timu ipi unaikubali zaidi?

    Jibu: Naikubali zaidi timu ya makao makuu kwasababu tunajuana na makao makuu ni watani wetu wa jadi na muda mwingine tunakutana katika mechi zetu za mtaani.

    Gaza (jezi ya njano) mazoezini.

    Michezo: Tunasaka ushindi

    Inaendelea Uk. 12

  • 12

    Toleo Maalum la Michezo

    Swali: Nini Mtarajio yako ya baadae?

    Jibu: Matarajio yangu ya baadae ni kufanya kazi kwa bidii ili kuleta ufanisi na kulitangaza shirika letu ndani na nje ya mipaka yetu kwa kutumia michezo.

    Swali: Unamaoni gani kwa Uongozi kuhusu michezo ya Inter-Ports ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka?

    Jibu: Maoni yangu kwa manejimenti kwanza, naomba waweke zawadi za wafungaji bora katika timu zote ili kutupa hamasa sisi wachezaji tofauti na ilivyo sasa ambapo anapewa mchezaji bora tu uwanjani, pili tupewe muda mwingi wa kupumzika, tatu posho ziongezwe hasa kwa

    wenyeji wa mashindano, nne tuboreshe viwanja vyetu vya Harbours Club ili tuvitumie katika michezo kama hii.

    Swali: Unawashauri nini vijana wenzio kuhusu janga la ukimwi ambalo limekuwa likizima ndoto za vijana wengi?

    Jibu: Ukimwi ni janga la kitaifa linalorudisha maendeleo ya vijana nyuma nawashauri wajilinde na ngono zembe na kuwa na mpenzi mmoja, pia watumie vizuri nafasi wanayoipata katika michezo ya Inter-Ports hasa wanaosafiri waepukane na vishawishi pia wajitunze pindi wanapoenda mkoa mwingine kushiriki michezo hiyo.

    Wahitimu wa mafunzo ya huduma kwa mteja wakiwa katika picha ya pamoja

    Wahitimu wa warsha ya mafunzo ya huduma kwa mteja kutoka Bandari mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhititimu mafunzo yao mjini Bagamoyo hivi karibuni.

    Inatoka Uk. 11

  • 13

    Toleo Maalum la Michezo

    Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Bandari za Maziwa.

    Washindi wa Pili wa jumla Bandari ya Tanga.

    Washindi mbalimbali katika picha

  • 14

    Mafunzo/Mv. Cubango

    Vikombe vya Ushindi

    Mchezaji wa timu ya kuvuta kamba wanawake, Rubby Jaffari kutoka Bandari ya Mtwara akipokea kikombe cha ushindi wa pili wa mchezo huo.

    Kapteni wa timu ya kuvuta kamba wanawake Asha Omary kutoka Bandari ya Dar es Salaam akipokea kikombe cha ushindi wa kwanza wa mchezo huo.

    Kapteni wa mpira wa miguu kutoka Bandari za Maziwa Almachius Vedasto akipokea kikombe cha ushindi wa pili wa mpira wa miguu.

    Mwakilishi wa Bandari ya Dar es Salaam, Emmanuel Bohama akipokea kikombe cha ushindi wa jumla kwa Bandari ya Dar es Salaam.

  • 15

    Ziara

    Hafla ya kufunga michezo Harbours Club

    Mshindi wa shindano la kuimba akibebwa na mashabiki wake.

    Wafanyakazi wakishindana kucheza kwaito wakati wa sherehe za kufunga michezo ya Bandari. Mshindi aliibuka kuwa Neema Mushi kutoka Idara ya Ukaguzi wa Ndani, Makao Makuu.

    Mshindi wa kwanza kurusha Mkuki wanawake kutoka Bandari ya Tanga, Amina Kubo akipokea medali yake kutoka kwa Katibu Mkuu wa DOWUTA Taifa, Jonathani Msoma.

    Mshindi wa pili kurusha Tufe wanawake kutoka Bandari ya Dar es Salaam, Oliver Ngumuo akipongezwa na Katibu Mkuu wa DOWUTA Taifa, Jonathani Msoma

  • 16

    HONGERA WAHISANI BANDARI LANGO LA UCHUMI

    Tunalianza shairi, kulisoma hadharaniFuraha imekithiri kuja kwenu kusiniKaribuni kwa pamoja karibuni Hongera wahisani Bandari lango la Uchumi.

    Ndege wana viota, Mbweha wao na mapangoWalimu wetu waota, kupata pesa za pangoBandari mkatuota, kuja kufungua LangoHongera wahisani Bandari lango la Uchumi.

    Tiginya kafikiria, akili kang’amua Bandari Darisalama, barua kuiandaaBila hofu akatua Ofisini wasilisha,Hongera wahisani Bandari lango la Uchumi.

    Huruma ikaingia, Mamlaka ya BandariHundi mkaiandika, nyumba walimu wapateHongera wahisani Bandari lango la Uchumi.

    Leo tumekusanyika, Walimu na Wanafunzi,Tuwe wote mashuhuda, Kupokea yetu hundi,Kutoka kwa Mamlaka ya Bandari TanzaniaHongera wahisani Bandari lango la Uchumi. Wote tunaahidi, Ujenzi anza mara moja, Mafundi waahidi, Majengo jenga imaraShukrani tunatoa, walimu kupata nyumbaHongera wahisani Bandari lango la Uchumi.

    Mwisho tumefikia, Shairi twalikatiza Bandari mmetufikiria, Kweli tunawatukuzaSiku tuliyofikiria, Leo mmeitimiza, Hongera wahisani, Bandari lango la Uchumi.

    Limetayarishwa na Shule ya MsingiKurasini-Dar es Salaam.

    Malenga/Huduma kwa Jamii

    Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Bi. Janeth Ruzangi (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi ya Kurasini, Bw. Selemani Kiwanga (wa tatu kulia) kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo.