Download pdf - ANNUUR 1037

Transcript
Page 1: ANNUUR 1037

ISSN 0856 - 3861 Na. 1037 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Rungu la NECTA lawaponda tena WaislamuSafari hii ni kwa Walimu wa StashahadaNi mchezo wa kuondoa Dini baada ya Qubah (?)Zanzibar nayo kubanwa au wawe na NECZA yao

DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania.

WITO umetolewa kwa Waisamu Jijini Dar es Salaam, kujitoa na kwenda

Sensa ilikuwa BarakaKumbe ilisilimisha Mkristo mmojaWaislamu watakiwa kutembelea wafungwa

Inaendelea Uk. 3

Ubaya Ubaya sasakuleta balaa Unguja

Uamsho watakiwa kuanzia Jihad Jang’ombeWaje kwa Baraza la Mji Zanzibar ing’are

Uk. 3

Na Bakari Mwakangwale Magerezani kuwatembelea Waislamu, kwa ajili ya kuwasaidia kwani wengi walioko huko wanahitaji

Washenga wa maadui wa Zanzibar watolewe serikalini

Aanze kuondoka Mwinyihaji MakameAu aseme Bububu adui alikuwa nani?Wanadhani fitna, farka itawapa Urais 2015

Uk. 4

MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Julius Mtatiro katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita. Habari kamili Uk. 16.

Tapeli ajizolea fedha kutoka kwa Waislam

Uk. 7

Page 2: ANNUUR 1037

2 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Tangazo

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0754 260241 Fax: 2450822 Dar es Salaam

E-mail: [email protected]

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu.Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana.Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. English Language3. Arabic Language4. Mathematics6. Introduction to ComputerNi programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012)Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu.

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE

Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107

MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU

Wabillah TawfiiqMKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

HIVI sasa Waislamu, wake kwa waume kutoka nchi mbalimbali duniani wanaelekea nchini Saudi Arabia kwa aj i l i ya kutekeleza nguzo ya tano ya Uislamu, ambayo ni ibada ya Hija.

Hapa kwetu Tanzania kadhalika, ndugu zetu w a K i i s l a m u a m b a o w a m e j a a l i w a k u p a t a masurufu ya kutekeleza ibada hiyo, nao wamekuwa katika hatua za mwisho kuelekea Saudia kwa lengo hilo hilo.

Uislamu umejengwa k a t i k a n g u z o t a n o . K u s h u h u d i a k w a m b a hakuna Mola anayestahiki k u a b u d i w a k w a h a k i isipokuwa Allah na Bwana M t u m e M u h a m m a d (SAW) ni mjumbe wake, kusimamisha sala tano, kutoa zaka, kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwenda Hijja. (Bukhari na Muslim).

K w a b ah a t i mb ay a Waislamu wengi tunazisoma na kuzikariri nguzo hizi bila ya kuzingatia uzito na umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku.

Uislamu haumkubali mtu yoyote ambaye hakutimiza nguzo za Dini, inapokuwa mtu huyo amepewa na Mwenyezi Mungu uwezo wa kuzitimiza.

Mwenyezi Mungu (SW) anaamuru ifuatavyo: “Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” (Al-Baqara, 2:196)

Hapa Mwenyezi Mungu (SW) anataka Waislamu wai teke leze ibada na nguzo ya Hijja. Na kwa wale wanaokwenda Hijja, anawataka waitimize ibada hiyo kwa ukamilifu.

Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia w a t u w a f a n y e H i j j a katika nyumba hiyo kwa yule awezaye kwenda huko. Na atakayekufuru (atakayekanusha) basi

Kila la kheri mahujaii wetu

Mwenyezi Mungu si mhitaji kuwahitaji walimwengu.” (Al Imran, 3:97)

Kwa maneno mengine, ni wajibu kwa kila mwenye uwezo kwenda Hijja kwa ajili ya Mola wake. Mwenyezi Mungu (SW) anaichukulia Hijja kuwa ni haki yake kutoka kwa viumbe vyake waliomuamini na ambao amewapa uwezo. Na kwa kuwa anayetoa uwezo ni yeye Mwenyewe (SW), basi anamjua kila aliyempa uwezo na asiyempa. Hivyo, kwa ambaye amepewa uwezo na kwa sababu yoyote ile, hakwenda kuhiji Makka, basi ajue kuwa Mola wake hamuhitajii kwa lolote.

Tuna hakika kwamba Waislamu wengi wanajua faida za Hijja. Hivyo M u i s l a m u h a n a b u d i kutanguliza kwenda Hijja kwanza kuliko kwa mfano, kufanya harusi inayogharimu thamani ya Hijja zaidi ya moja.

K a t i k a H a d i t h i i l iyopokelewa na Abu Huraira (RA), Mtume (SAW) amesema: “Mwenye kufanya Hijja bila ya kusema maneno machafu na bila ya kufanya vitendo vichafu, atasamehewa madhambi yeke atakaporudi kama siku aliyozaliwa na mama yake.” (Bukhari, Muslim).

Kwa mapenz i yake subhanahu Wataala, Rehema za Allah hazisimami kwa yule anayekwenda kuhiji peke yake. Bali wapenzi wote wa Mahujaji wananufaika kwa uhakika kutokana na dua watakazoombewa na Hajji.

Hoja hii imebainishwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (SAW) ka t ika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira (RA) kama ifuatavyo:

“Husamehewa madhambi yake mwenye kuhiji pamoja na wale watakao-ombewa na mwenye kuhiji.” (Al-Bazzari, At-tabraany, Ibn

Khuzaimah, na Al-Hakim). Wako miongoni mwetu

Waislamu wanaojizuil ia kwenda Hijja kwa dhana ya kuwa wanachohitaji kutoa ni kingi na hakirudi. Hii ni dhana potofu haiendani na mafundisho ya Dini. Ni potofu kwa sababu lengo la Uislamu ni kupata radhi za Mola, kuepukana na moto, na kupata pepo. Hijja inamhakikishia Muislamu haya yote kwa mpigo.

Lakini pia dhana hiyo ni potofu kwa sababu anachokitoa mtu kwa kufunga safari ya Hijja au Umra hakipotei; kinarudishwa na kuzidishwa. Katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Malik (RA), Mtume(SAW) amesema:

“Mwenye kufanya Hijja na mwenye kufanya Umra ni wageni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hupewa wanachoomba, na (Allah) a n a j i b u d u a z a o , n a hurudishiwa walivyotoa, dirham (au shilingi) moja kwa dirham (au shilingi) milioni moja”. (Al-Baihaqy).

Nguzo ya kwanza katika nguzo za Hijja ni kuhirimia. Wanaume wote kubadili nguo na kuvaa nguo za aina moja. Mashuka mawili meupe, moja juu mabegani na la pili kufunga kiunoni.

Hapa tunajifunza kitu kimoja muhimu. Nacho ni usawa kwa binadamu. Hakuna nafasi ya kuwepo alama alama zinazowatofautisha watu kwa mataifa yao, utajiri wao, vyeo vyao, n.k. na zinazowafanya wajinasibishe na cheo, kabila, mali, utaifa au kundi fulani. Hali hii inatoa nafasi ya mtu kujijua zaidi. Kiburi, majivuno, kujiona, chuki, miongoni mwa maasi yaliyo ndani ya moyo wa mtu yanakuwa havana nafasi.

Mtu anapata nafasi ya kupata hisia ya utu wake, na hali itakavyokuwa siku y a k u f u f u l i w a . H i v y o Hijja ni fursa kubwa sana inayomsaidia mtu katika kukumbuka mwisho wake, kujenga Uislamu wake, na kumkumbuka sana Mola wake.

Kis imamo cha Arafa kinatoa wasaa zaidi watu milioni tatu hukutana katika uwanja mmoja. Huo ni mfano wa siku ya Qiyama ambapo Allah atatukusanya wanadamu wote walioumbwa na kuishi katika uso wa ardhi pamoja katika uwanja mmoja. Wenye akili wanatakiwa wanufaike na mkusanyiko huo kwa kuikumbuka siku hiyo ya kiyama.

Watu wote wanaokwenda Hijja kwa ajili ya Allah (SW) ni vyema wakaweka mapatano baina ya watu waliokuwa wamekhasimiana. Haji mtarajiwa anatakiwa

asuluhishane na kila Mwislamu aliyekuwa amekhasimiana naye. Kwa maneno mengine, anatakiwa akamilishe imani yake kwa kuondoa chuki, hasama , kuondosheana kinyongo, kusuluhishana na kupeana radhi na Waislamu wenzake ambao ndio ndugu zake wa kiroho.

Ibada ya Hijja inaanzia mtu anapokuwa nyumbani kwake na katika nchi yake. Muislamu anatakiwa aondoke kwa safari ya Hijja akiwa amelipa madeni yake yote anayodaiwa, na amewaridhisha watu wake wa nyumbani kwa kuwaachia mahitaji yao ya maisha kwa muda wote anaotarajiwa kuweko safarini.

Hivi ndivyo Muislamu anatakiwa anapoondoka kuelekea Makka kuitikia wito wa Mola wake, anatakiwa aondoke huku ndani ya moyo wake ukiwa umejaza mapenzi kwa Mola wake (SW), Mtume wake Muhammad (SAW), na ndugu zake Waislamu wote.

Ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu (SW) ametuwekea Hijja ili tujenge umoja wa Kiislamu kimataifa. Swali la kujiuliza ni je, sisi tunaotoka nchi moja tunajuana? Je, tunashirikiana? Je, tuna mshikamano?

N i vyema sa f a r i h i i mahujaji wakajenga umoja na kufahamiana kabla ya

kuondoka kwenda Hijja ili kujenga umoja unaofahamika katika nchi yetu kwanza. Ni ajabu taasisi za kusafirisha na kuhudumia mahujaj i nchini kusafirisha Mahujaji na kutekeleza ibada zote huko Makka na kurejea nyumbani bila ya Mahujaji wa taasisi moja kujuana na wa taasisi nyingine hali ya kuwa wanatoka Taifa moja. Si kisimamo cha Arafa wala Minna, kote huko kupishana tu. Hutokezea wachache miongoni mwao wakajuana kwa bahati. Lakini bado hakuna juhudi inayochukuliwa kujenga mtandao angalau wa wale waliobahatika kwenda Hijja wakafahamiana vizuri.

Katika hal i hi i kweli l i le lengo kuu la Hij ja linapatikana? Vipi kuhusu falsafa ya Hijja tunaifahamu? Kuna haja ya waandaaji wa Hija kulishughulikia tatizo hili. Mahujaji wafahamiane na kushikamana tangu nyumbani.

Tumalizie kwa kusema, kama ambavyo Mwenyezi Mungu amewajaalia afya njema, masurufu na wasaa kwa aji l i ya kutekeleza ibada ya Hija, tunamuomba awajaalie pia Hija njema na iliyokamilika. Hija maq buul.

Page 3: ANNUUR 1037

3 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Habari

Rungu la NECTA lawaponda tena WaislamuM G O G O R O k a t i y a Waislamu na Baraza la Mitihani Tanzania unazidi kupanuka baada ya Baraza hi lo kuzuiya matokeo ya baadhi ya wanachuo kwa madai kuwa NECTA haitambui somo la Maarifa ya Uislamu.

Baadhi ya wanafunzi waliozuiwa masomo yao wanasema kuwa kat ika mitihani yao ya kidato cha sita walifanya masomo ya ‘arts’ pamoja na Islamic Knowledge na kufaulu kwa kiwango cha kuwa na sifa za kuchukua Mafunzo ya Ualimu kiwango cha Stashahada (Diploma) na kwamba waliwalisha vielelezo vyao NECTA wakasajiliwa.

Hata hivyo wanasema kuwa, baada ya kufanya mtihani wa kumalizi kozi yao ya masomo wakiwa wamefanya masomo mawili ya kufundishia, moja likiwa Elimu ya Dini ya Kiislamu, Baraza la Mitihani limezuiya matokeo yao likidai kuwa somo la Maarifa ya Uislamu halitambuliki.

Wal imu hao Tara ja l i w a m e s e m a k u w a wameshangazwa na hatua hiyo ya NECTA kwani tangu wakati wa Usajili mpaka kufanyika mtihani Baraza liliwakubali kama wanachuo wenye sifa, sasa wanashangaa hii kanuni imekuja kutoka wapi.

Kwa upande wa baadhi ya wakufunzi wal iotoa maoni yao wamesema kuwa wameshangazwa na kitendo hicho cha NECTA kwani ilivyo Baraza hutahini mtihani wa Maarifa ya Uislamu kwa O Level na A Level, sasa “walimu wa kufundisha somo hilo watapatikana kutoka wapi kama Baraza halitambui somo hilo katika kiwango cha kusomesha walimu?” Wamehoji.

“ H i z i n i n j a m a , h iv i wana taka wa l imu wanaosomesha Elimu ya Dini ya Kiislamu wasiwe na Maarifa ya Uislamu na Ualimu japo wa Diploma ili wapate kisingizio cha kuwatukana Waislamu kuwa walimu wa Madrasa ndio wanaosomesha sekondari! Kama hawataki wasomi Waislamu, mbona katika mitihani ya kidato cha nne na sita, hawachukui tu Waislamu mitaani na kuwapa kutunga na kusahihisha mitihani ya kidato cha nne na sita?” Alihoji Mwalimu mmoja ambaye hata hivyo

Na Mwandishi Wetu hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Mwalimu huyo anasema kuwa kisingizio cha NECTA kuwa kuna Waraka wa Wizara usiotambua Islamic knowledge hayana mashiko kwa sababu yapo pia masomo mengine ambayo hivi sasa yanatambuliwa na Baraza la Mitihani Tanzania kuwa yana fanya miungan iko (Combinations), wakati katika Waraka huo hayakutajwa.

Kwa upande mwingine akasema kuwa katika mitihani ya kidato cha sita (ACSEE), kwa upande wa Zanzibar, wanafunzi wanafanya Islamic Knowledge kama somo mojawapo katika combination ya masomo ma ta tu ya Principal Pass.

Swali ni je, kwa msimamo huo Baraza na kwa kuzingatia kuwa Baraza hi lo ndio linasimamia pia mitihani kwa Zanzibar, kwa maana kuwa ni suala linalosimamiwa na Serikali ya Muungano, “je, ina maana NECTA itafuta matokeo ya wanachuo wote kutoka Zanzibar?”

Kwa upande wa baadhi ya Wamiliki wa Shule na Vyuo vya Ualimu vya Kiislamu w a m e s e m a k u w a , w a o mchepuo wao mkuu ni Somo la Dini ya Kiislamu kama ilivyo kilimo kwa shule za kilimo.

K w a h i y o , B a r a z a kutotambua somo hilo ni sawa na kuwazuiya Waislamu kusomesha walimu wenye sifa wa kusomesha somo hilo.

“Shule na Vyuo vyetu wamevisajili kwa kuvitambua kuwa ni vya kidini, kutotambua somo la dini, maana yake ni kutukataza kusomesha walimu wataalamu ili baadae watumie kisingizio cha kutokuwa na walimu wenye sifa kufunga shule na vyuo vyetu.” Amesema Mkuu mmoja wa Chuo.

Hata hivyo, baadhi ya Waislamu waliotoa maoni yao kuhusu sakata hi l i wamekumbushia ule Waraka ulitolewa miaka ya 1980s baada ya kuanzishwa shule za kwanza za seminari za Kiislamu uliosema kuwa shule za seminari si shule na kwamba wanafunzi wake wakimaliza kidato cha nne hata wakifaulu hawatachaguliwa kuingia kidato cha tano katika shule za seriikali.

K a b l a W a i s l a m u hawajaanzisha Qubah na Jabal Hira, ilikuwa wanafunzi kutoka shule za seminari za Kikristo wakichaguliwa kuingia High School za

serikali na kisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wanasema, ilikuwa baada ya kuona Waislamu nao wanaanzisha seminari ndio Waraka huo ukatoka.

Hata hivyo wanasema k u w a , W a r a k a h u o ulitelekezwa kinyemela, kwa maana kuwa haukutekelezwa baada ya kuonekana kuwa haukuwaka t i sha t amaa Waislamu na ‘mfumo’ ukaona kuwa watakaoathirika zaidi ni Wakristo kwa sababu ndio walikuwa na seminari nyingi.

“Walidhani kuwa kwa kutoa Waraka huo, Waislamu wangevunjika moyo wafunge shule zao na wazazi wa Kiislamu wasingepeleka watoto wao katika shule hizo wakati Waraka wa Serikali hauzitambui, lakini walipoona zinaendelea wakauficha.” Amesema mwanaharakati mmoja wa Kiislamu.

Kwa rekodi hiyo, baadhi ya Waislamu waliokuwa katika harakati za kuanzisha seminari za kwanza za Kinondoni, Jumuiya, Masjid Qubah na Jabal Hira, wanasema kuwa, huenda hatua hii ya

Baraza la Mitihani Tanzania, ni mkakati wa kuwakatisha tamaa na kuwawekea vikwazo Wais lamu wasisomeshe wa l imu wenye s i f a za kusomesha Somo la Dini ya Kiislamu katika ngazi ya sekondari na hata Vyuo Vikuu.

Ta a r i f a t u l i z o z i p a t a wakati tukienda mitamboni jana zilifahamisha kuwa Walimu Tarajal i ambao matokeo yao yamezuiwa, ilikuwa wawasilishe barua ya malalamiko yao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Sensa ilikuwa BarakaInatoka Uk. 1

msaada wa hali na mali.Wito huo umeto lewa

na Ustadhi Ally Mbaruku akiongea na Mwandishi wa habari hizi akielezea hali ya Waislamu magerezani na wafungwa kwa ujumla.

Ust. Mbaruku amebaini hayo baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi, mwezi Septemba, mwaka huu kisha kuwekwa rumande katika Gereza la Segerea kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kosa la kugomea zoezi la Sensa ya watu na Makazi.

Mbali ya Ust. Mbaruku kubaini hali hiyo, lakini pia alidai yeye pamoja na wenzake watano, wakiwa gerezani huko walifanikiwa kumsilimisha mtuhumiwa mmoja waliyemtaja kwa jina la Yona Edward Pius.

Mbaruku amesema, kuna watuhumiwa Waislamu wengi wanaohitaji msaada wa hali na haswa namna ya kuwawekea dhamana ambazo anadai wengi wao wamekwama kwa hila na dhulma tu.

Alisema, siku chache a l i z o k u w a g e r e z a n i , amejifunza mengi na kubaini

kwamba Waislamu wengi waliopo huko wapo kwa makosa ya kubambikiwa au kukosa uwezo wa ndugu zao kuwasimamia katika masuala ya dhamana.

Kwa maana hiyo, aliwataka Wa i s l a m u w a k i w e m o wanasheria, kuweka utaratibi wa kufika magerezani kuongea na watuhumiwa.

Alisema, yeye baada ya kutoka kwa dhamana na wezake kufuatia sakata hilo la Sensa, ameshafanya juhudi kwa kuwasimamia mahabusu Waislamu wapatao watano na kufanikiwa kuwatoa kwa dhamana.

Kuhusu Bw. Yona Edward, waliyemsilimisha akiwa gerezani, al isema awali walikutana naye katika selo ya kituo cha Polisi cha Oysterbay, ambapo wakijadili suala la sensa na Uislamu humo kituo cha polisi, Bw. Yona, alivutika nayo.

Baada ya hapo, walitoka na baadaye walikutana tena katika mahabusu ya Segerea, ambapo jamaa (Edward) aliwaeleza nia yake ya kusilimu, ambapo walimuona Sheikh Mkuu wa mahabusu, aliyemtaja kwa jina la Sheikh Ally Jabir na

kumsilimisha.Baada ya kusilimu, alisema,

Yona, alichagua jina la Ismail, na kisha kuanza kumfundisha masuala ya dini huko huko gerezani na viongozi wa Kiislamu Mahabusu walioko humo.

Alisema, walianza kutoka wao kwa dhamana kisha alimsimamia Bw. Islamil (Yona) kwa kuwafua ta wazi wake ambao walitoa ushirikiano hatimaye naye alitoka kwa dhamana.

Bw. Ismail (Yona) ambaye alipitia mafunzo ya dini katika Chuo Cha Biblia (Bible School) na kuhitimu masomo hayo mwaka 2003, a l ikabidhiwa chet i cha kusilimu chenye namba 1201, cha Baraza Kuu.

Mbali ya chet i hicho Islamil amepata hati ya kiapo cha kusilimu cha Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya K i n o n d o n i , y a t a r e h e 25.9.2012, iliyosainiwa na Hakim E. M. Kihiyo.

Kwa sasa Bw. Ismail, anapata elimu ya dini yake mpya ya Kiislamu katika Madrasa Istiqama, iliyopo jirani na Masjidi Rahman Makangira Msasani.

DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji NECTA.

Page 4: ANNUUR 1037

4 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Habari

Washenga wa maadui wa Zanzibar watolewe serikalini

VIKUNDI vya Uporaji, ukabaji na upigaji wa wananchi vimeibuka kwa kasi kubwa Zanzibar huku wananchi mbali mbali wakiwa na wasiwasi mkubwa wa maisha yao na mali zao.

Vikundi hivyo vilivyopewa jina la Ubaya Ubaya, vimekuwa wakionekana katika maskani mbali mbali, na vimekuwa gumzo kubwa visiwani hapa huku wananchi mbali mbali wakiliomba Jeshi la Polisi na serekali kuvidhibiti ili wananchi waweze kuishi kwa amani na utulivu.

Kwa upande mwingine, Jumuiya ya Uamsho imeombwa kuanzia Jihad yake katika maeneo yaliyokithiri uhalifu huo kwa kutoa Da’wa na kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuisafisha jamii hii ya Kiislamu na uchafu.

“Nadhani Uamsho wanaweza kusaidia sana kusafisha jamii kama wataelekeza nguvu zao katika kubadili nyoyo za watu badala ya kukimbilia kupambana na wanasiasa wenye bunduki na majeshi, watu wakibadilika ndio hao hao watakuwa viongozi wema ambao hawataruhusu siasa za kikafiri au kula mali za umma huku miji ikiwa michafu haisafishwi.”

Amesema mwananchi mmoja ambaye anasema kuwa anakerwa na hali ya uhalifu unaozidi kukua Zanzibar huku serikali ikionyesha kutokujali.

“Maadhali wahalifu hawa, Ubaya Ubaya hawa hawagusi masi lahi yao , hutawaona wanasiasa wetu wakijali kama ambavyo hawajali kuona mji huu wa Waislamu ukiwa mchafu, ila utawaona wakicharukwa Uamsho wakiwagusa, mimi naona Uamsho wangeelekeza juhudi zao katika kusafisha nyoyo za Wazanzibari, wasafishe Ubaya Ubaya na kuazisha harakati za kusafisha mji, ile Al Islam Nadhiif ionekane mtu akiingia Unguja.” Aliongeza mwananchi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Bilal.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda wa wiki mbili sasa, wananchi mbali mbali wameonyesha hofu zao juu ya kikundi hicho ambao kimekuwa gumzo katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Mjini Unguja.

Wahalifu hao hucharuka zaidi wakati wa usiku na wakati mwengine hufikia kufanya uhalifu wao huo hata wakati wa mchana bila ya kupata kikwazo chochote.

Maeneo ambayo yameatihirika zaidi na kikundi hicho ni Maeneo ya M-bori borini Jimbo la Kwamtipura, Maeneo ya Mwembeladu, Jangombe, Migombani na Mwanakwerekwe Makaburini.

Maeneo mengine ni eneo

Na Mwandishi Wetu

la soko la Mwanakwerekwe, U w a n j a w a M p i r a K w a BaMgeni (Fuoni), Magomeni Jitini na maeneo mengine yanayozunguruka Mji wa Zanzibar.

Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuenea kwa vijana wengi wanaotumia Madawa ya Kulevya na uvutaji wa bangi na kuanzishwa kwa magenge na maskani nyingi za vijana katika maeneo ya wazi na yaliojificha.

Hapo ndio kumeibua kundi hili la wahalifu huku baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakiomba Serekali kuwa macho na maskani na magenge kama hayo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi , wananchi mbali mbali wameshtushwa na matukio ambayo yameanza kujitokeza kwa kasi huku mengine yakitokea mbele ya jamii yanayodaiwa kufanywa na Kikundi hicho.

Akitoa mfano, Mkazi mmoja wa Mwanakwerekwe Makaburini amedai yeye ameshuhudia baadhi ya watu wakikabwa na kunyanganywa vitu vyao wakati wa mchana katika eneo la Mwanakwerekwe bila ya wahalifu hao kuchukuliwa hatua na wapita njia.

“ H i c h i K i k u n d i c h a kinachoitwa Ubaya Ubaya kimekusanya watu wengi na kina mtandao mkubwa, kimekuwa tishio sana kwa amani na mali zetu, wanafanya uhalifu bila hata woga na wakati mwengine hufanya uhalifu wao hata katika soko kuu la Mwanakwerekwe tena Mchana, tunaomba serekali ivishughulikie vikundi hivi ili wananachi tuweze kuishi kwa amani.” Alisema mkazi huyo.

Nae mkazi mmoja anaeishi Kijito Upele Jimbo la Fuoni amedai kwamba kuibuka kwa vikundi kama hivi visiwani Z a n z i b a r , k u m e w a f a n y a akina mama na watoto kujaa hofu kubwa wakati wa usiku w a n a p o k u w a w a n a r u d i matembezi.

Amesema tayari baadhi ya akina mama wameathirika na vitendo vya vikundi hivo katika maeneo ya Uwanja wa Mpira kwa Ba Mgeni ambapo matukio ya Uporaji na upigwaji kwa wanawake umekuwa ukifanyika kwa kasi na bila ya woga wowote.

Aliliomba Jeshi la Polisi kuharakisha kufungua Kituo cha Polisi cha Kijito Upele Mashine ya Maji ili kiweze kusaidia kukidhibiti kikundi hicho.

Pia baadhi ya wananchi wamewaomba viongozi wa dini hasa Jumuia ya UAMSHO na mihadhara ya Kiislamu

kulikemea kundi hili ambalo limekuwa likifanya wanachi wa Zanzibar kuishi kwa woga mkubwa.

“Uhalifu kama huu sio wa kufumbia macho kabisa, tunaomba UAMSHO katika mihadhara yao walikemee kundi hili la wabaya wabaya ili jamii

tuweze kuishi kwa amani na utulivu, utadhani tupo Yombo, Manzese na Tandika huko Dar es Salaam jinsi ya vijana hawa wanavyofanya uhalifu bila ya Woga.”

Alisema mkazi mmoja wa Kwamtipura ambae mara kwa mara amedai akifanya safari zake Unguja na Dar es Salaam kufanya biashara.

Msemaji wa jeshi la Polisi Zanzibar hakuweza kupatikana kuzungumzia kuibuka kwa uhalifu wa aina hii.

Ubaya Ubaya sasa kuleta balaa Unguja

WITO umetolewa kuwa wale wote wanaojitokeza kama washenga wa maadui wa Zanzibar wang’olewe serikalini.

H a y o n i k w a s a b a b u wanadaiwa kuitafuna serikali na Zanzibar kwa ujumla ndani kwa ndani hali inayowafanya kuwa hatari zaidi kuliko adui wa nje.

A k i t o a n a s a h a h i z o , Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Said Soud Said amemuomba Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kumuondoa kat ika wadhifa wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame kwa kile alichodai kusababisha vurugu na utumiaji wa mabavu katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu.

Aidha alimtaka Rais Shein Kuunda Tume huru kuchunguza utumiwaji wa magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ katika harakati za Uchaguzi wa Jimbo hilo ambalo watu kadhaa walijeruhiwa kwa risasi za moto na wengine kupigwa na vikosi vya usalama.

Soud a l iyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana n a m a m b o m b a l i m b a l i yanayoikabili Zanzibar katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mjini Zanzibar.

Alisema Dk. Mwinyihaji Makame ambaye ni msimamizi wa Vikosi vya SMZ ambavyo vilishiriki kuuharibu uchaguzi wa Bububu anapaswa kujiuzulu kutokana na kuchangia kwa makusudi matumizi ya nguvu yaliyofanywa na vikosi hivyo.

Alisisitiza kuwa Chama cha AFP kinatoa muda wa miezi mitatu kujiuzulu kwa Waziri huyo kabla ya kuitisha maandamano ya wananchi wa Zanzibar kwenda Ikulu kushinikiza kujiuzulu huko.

Alisema, Uchaguzi wa Bububu umetoa picha mbaya kwa mustakabali wa Serikali ya Umoja ya Kitaifa na kwamba kwa vile risasi na mabomu vilitumika ambapo alisema inaashirikia hali mbaya zaidi na ya hatari wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu kuwa na vurugu kubwa iwapo serikali haitakuwa

Na Mwandishi wetu Zanzibar

makini na vitendo kama hivyo vinavyofanywa hivi sasa na baadhi ya watu.

“Ni jambo la kushangaza sana kuwa silaha zinanunuliwa kwa kodi ya wananchi kwa ajili ya kujilinda na maadui, sasa katika uchaguzi ule wa Bububu tunajiuliza adui alikuwa nani hata zikatumika silaha za moto”. Alisema na kuhoji Soud.

Aliongeza kuwa kuna watu wameandaliwa kwa makusudi kwa lengo la kuja kuichafua Serikali ya Umoja wa Kitaifa a m b a y o i m e s i m a m a n a kuonesha mafanikio makubwa ya kuwatumikia wananchi lakini watu hao hufanya juhudi za kuihujumu Serikali hiyo.

S o u d a l i s e m a k a m w e Wazanzibar i was iwaunge mkono watu waovu wa aina hiyo ambayo lengo lao ni kuwarejesha wananchi walipotoka kwani vishio hivyo vinaonesha dhahiri kwamba mustakabali wa umoja Zanzibar unaweza kutoweka mara moja kutokana na vitendo hivyo vinavyofanywa na watu wa aina hiyo.

Alisema baadhi ya watu hao ambao hata wakati wa mchakato wa uanzishwaji wa Serikali hiyo hawakuwepo nchini lakini wamepata bahati ya kuingizwa katika uongozi wa GNU sasa ndio wamekuwa chanzo cha mifarakano na bughudha nchini.

Alifahamisha kuwa Viongozi hao bila hata ya kuona aibu bado wanatumia silaha ya kuchochea mifarakano katika jamii za Wazanzibari kwa ajili ya kujirahisishia njia ya kugombea Urais jambo ambalo ni hatari kubwa.

“Hawa ambao hawaitakii mema Serikali ya Umoja wa kitaifa na kuchochea mifarakano kwa kisingizio cha kutaka kugombea Urais tunawaambia wahame Zanzibar, sisi tunahitaji amani bwana.” Aliongeza Soud.

Ak izungumz ia kuhusu Jumuiya ya MUAMSHO na Mihadhara ya Kiislamu Soud aliitaka Jumuiya hiyo kufanya kazi zake kwa kufuata sheria bila kuhatarisha amani iliyopo nchini.

Alisema amani ina umuhimu wa kipekee na kwamba kama itaondoka itakuwa ngumu kuirejesha hivyo kuiomba J u m u i y a h i y o k u t o k u w a kichocheo cha vurugu na kuhatarisha amani.

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kutokuwashambulia wafuasi wa Jumuiya hiyo ambao amedai ni Wazanzibari wanaodai madai ya msingi kwa mustakabali ya nchi yao.

“AFP inaitambua Jumuiya ya Uamsho kihalali na tunaliomba Jeshi la Polisi kuwaheshimu Uamsho wasithubutu kabisa k u w a h u j u m u , h a w a n i Wazanzibari bwana na hakuna asiyetaka kupumua.” Aliongeza Soud.

A l i s e m a U a m s h o wanachofanya ni kuitanabahisha jamii ya Kizanzibari juu ya Dini yao na mambo ambayo yanahusu mustakabali wa Uchumi na maendeleo ya nchi yao hivyo hakuna haja ya kuwaingilia kama ikiwa hawajavunja sheria.

“Jeshi la Polisi liiheshimu Uamsho na kuacha kuwahujumu kwa kisingizio cha kutekeleza amri za Mkereketwa mmoja tu asiyeipenda jumuiya hiyo..Imefika wakati lazima tupumue bwana.” Aliongeza Soud.

Kuhusu ongezeko la ukosefu wa ajira, Soud alisema Chama chake kinasikitishwa na ongezeko hilo na kwamba hali ni mbaya Zanzibar na kumtaka Dk. Shein kuyafanyia kazi mazungumzo ambayo waliyafanya naye Ofisini kwake Ikulu ikiwemo uanzishwaji wa Viwanda vya Minofu ya Samaki Zanzibar ili kupunguza tatizo hilo.

“Inasikitisha kuona bilioni .2.4 zinaenda Tanganyika kila mwaka kwa ajili ya kununulia mboga mboga tu, jambo ambalo linaweza kufanywa na vijana wa hapa Zanzibar ikiwa wataandaliwa mazingira mazuri ya kufanya kazi za kilimo cha mboga mboga.” Alitanabahisha Soud.

Kuhusu mchakato wa maoni ya Katiba mpya Mwenyekiti huyo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kwa kuruhusu mchakato huo na kwamba hiyo ni nafasi adhimu ambayo wananchi wanapaswa kuitumia vyema. Amewataka wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwenda kutoa maoni yao bila ya jazba huku wakiweka maslahi ya Taifa mbele badala ya vyama.

Page 5: ANNUUR 1037

5 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Habari za Kimataifa

1. Algebra ni shule ya BWENI na KUTWA kwa WAVULANA NA WASICHANA2. Inaongozwa kwa maadili ya Kiislamu na Iko Kigamboni - Kibada3. MAHALI PENGINE ZINAKOPATIKANA FOMU Mtambani (0715 – 866 887), UBUNGO ISLAMIC (0712 - 033 556) na ANNUR (0713 -110148)4. Maabara, Kompyuta na Maktaba vimeongezwa ili kuongeza ubora 5. Tumesajiliwa kwa namba S.4198 Tunajua tunakoenda na namna ya kufika huko

CHAGUA ALGEBRA ISLAMIC SEMINARY, INSHAALLAH HUTAJUTIA UAMUZI WAKO

ALGEBRA ISLAMIC SEMINARYP.O. BOX 36262 KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

TEL: 0715 – 299 945, 0714 – 112 083, 0655 – 260 241, 0714 - 593 897

NAFASI ZA MASOMO 2013Kidato cha Kwanza

Israel haitokuwepo tena baada ya miaka kumi Henry Kissinger, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, ambaye pia ni mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe wa nchi hiyo amesema kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo Israel haitokuwepo tena.

Kwa mujibu wa makala i l iyoandikwa na Kevin Barret, katika safu ya makala za kisiasa ya mtandao wa televisheni ya Press TV, si mwiko tena sasa kusikia afisa rasmi wa Marekani akisema wazi wazi kwamba suala la kuporomoka kwa Israel ni jambo lisiloweza kuzuilika.

Kwa mujibu wa Barret, ripoti ya utafiti uliofanywa mapema mwaka huu na Jumuiya ya Mashirika ya K i j a s u s i y a M a r e k a n i inayojumuisha mashirika 16 ya nchi hiyo iliyokuwa na anuani isemayo, “Kujiandaa kwa Mashariki ya Kati ya baada ya Israel”, nayo pia imethibitisha maelezo ya Kissinger, ambaye yeye mwenyewe pia ni Myahudi.

Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa amesema ripoti hiyo imesisitiza kwamba serikali ya Marekani haina uwezo tena wa kijeshi na kifedha wa kuisaidia Israel

kukabiliana na matakwa ya watu zaidi ya bilioni moja katika nchi zilizo jirani yake na kushauri kuwa Washington itapaswa kufikiria maslahi yake ya kitaifa na kuuacha kuunga mkono utawala huo wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Kevin Barret, kuna sababu kadhaa ambazo z imesababisha kujitokeza hali hiyo ikiwemo wanasiasa na wanaharakati

wa Marekani kuchoshwa na sera zinazovuka mipaka za Israel na kutokuwepo tena umoja ndani ya jamii ya Kiyahudi ya Marekani katika suala la kuunga mkono utawala huo wa Kizayuni.

Henry Kissinger

Abbas ataka Palestina ipewe uanachama kamili UN Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, amesema ataomba kupigiwa kura kuundwa taifa huru la Palestina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

A b b a s p i a ametahadharisha kuwa hatua ya Israel ya kuendelea kupanua vitongoji vyake vya walowezi wa Kizayuni inamaanisha kuwa wakati wa kutekelezwa suluhisho la kuundwa nchi mbili katika ardhi ya Palestina unayoyoma.

I k i w a n i m w a k a mmoja tangu awasilishe pendekezo la Palestina kupewa uanachama kamili Umoja wa Mataifa, Abbas sasa amelielekea Baraza Kuu la Umoja huo na

kutahadharisha kwamba hatua zinazochukuliwa na Israel zinaonyesha kuwa inapinga kuundwa nchi mbili katika ardhi ya Palestina.

Kiongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina aidha ametahadharisha kwamba, kuendelea siasa za kupenda kujipanua Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kunaonyesha kwamba utawala wa Kizayuni unakusudia kutekeleza dhahma nyingine dhidi ya Wapalestina.

Abbas amesema hayo k a t i k a h o t u b a y a k e kwenye mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Gaddafi aliuliwa kwa amri ya Sarkozy R I P O T I i l i y o t o l e w a na gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza imeeleza kwamba kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, aliuliwa na wakala wa siri wa Ufaransa kwa amri ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy.

Inasemekana kuwa jasusi huyo wa Ufaransa alijipenyeza kwenye kundi moja la vikosi vya wanamapinduzi wa Libya lililomkamata mateka Gaddafi kwenye bomba la majitaka katika mji alikozaliwa wa Sirte na kumpiga risasi.

Likinukuu vyanzo vya Libya, Daily Mail limeandika k u w a j a s u s i h u y o w a Ufaransa aliamriwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo Nicholas Sarkozy kumuua Gaddafi ili kumzuia asije akafichua mahusiano yao endapo angesailiwa.

Kabla ya kuuawa na kufuatiwa na mashambulio ya anga yaliyofanywa na shirika la kijeshi la NATO nchini Libya, Muammar Gaddafi alitishia hadharani kwamba angefichua kwa undani uhusiano wake na rais huyo wa zamani wa Ufaransa.

Sarkozy, ambaye aliwahi kumwita Gaddafi kuwa ni ‘kiongozi ndugu’ wakati

alipofanya safari nchini Ufaransa, inasemekana kuwa alipokea kutoka kwa Gaddafi kitita cha Euro milioni 50 kusaidia kampeni zake za uchaguzi wa rais wa mwaka 2007.

Gazeti la Kitaliano la Corriere della Serra, nalo pia limeripoti kuwa vyanzo nchini Libya vimeeleza kwamba muuaji wa kigeni mwenye uraia wa Ufaransa ndiye aliyemuua Gaddafi.

Muammar Gaddafi

Page 6: ANNUUR 1037

6 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Habari

SAKATA la Sensa ya Watu na Makazi lililomalizika hivi karibuni, limeacha changamoto na kupelekea Waislamu wa Bwakila na Mvuha Wilayani Morogoro kuunda Umoja wao ili kukabiliana na maswala ya kijamii.

Hayo yamebainishwa na Ustadhi Pesa Mohammed Pesa, akiongea na gazeti hili katikati ya wiki hii, juu ya kuundwa kwa umoja wa Waislamu uliojumuisha Tarafa za Bwakila na Mvula Wilayani Morogoro.

Ustadhi Pesa alisema Waislamu wamefungua ukurasa mpya kuanzia Octoba mosi, mwaka huu, baada ya kukutana na kuunda chombo kitakachojulikana kama ‘Umoja wa Misikiti Morogoro Kusini’ (UWAMMOKU) kupitia Tarafa hizo.

Ust. Pesa, akieleza sababu za kuundwa kwa umoja huo hivi sasa, alisema yapo mambo mengi ambayo Waislamu wanatakiwa kuwa na muongozo wa pamoja iwe kwa Muislamu mmoja mmoja, kikundi au wote kwa ujumla, akitolea mfano k u y u m b a k i m s i m a m o miongoni mwao katika zoezi la Sensa lililopita.

Lakini pia alisema, kutoa muongozo kwa Waislamu k u w a n a k a u l i m o j a kuunga mkono masuala ya kimaendeleo, kijamii na hususani kwa wao kama umoja wa Kiislamu kwa manufaa yao na Uislamu kwa Ujumla na hata katika kutoa maoni, hapa akitolea mfano maoni kuhusu undwaji kwa Katiba mpya.

“Umoja huu una malengo mengi, kwanza kuwa na kauli moja kuhusu Waislamu na Uislamu katika eneo husika pindi inapotokeza Muislamu kuonewa, kuhakikisha vijiji vyenye Waislamu wengi kuwatembelea wenzao walio wachache katika baadhi ya vijiji na kuwafikishia Daa’wa na kuwashajihisha katika masuala ya Uislamu.” Alisema Ust. Pesa.

A l i s e m a , w a m e o n a umuhimu wa umoja huo kuwepo haswa kupitia zoezi la

Sensa yaunganisha Waislamu Morogoro

Ni wale wa vijiji vya Bwakila, MvuhaNa Bakari Mwakangwale Sensa, kwani alidai Waislamu

walikuwa wakikamatwa hovyo na kwamba kukosekana kwa umoja katika maeneo husika ilipelekea uonyonge, pamoja na kwamba Waislamu waliit ikia msimamo wa kususia Sensa kwa asilimia mia moja ku toka kwa Masheikh wa juu.

Ust. Pesa, alisema pamoja na kuwa ni Diwani wa Bwakila chini, yeye kwake imani ya dini yake iko mbele kwani alidai yeye kama Muislamu ni miongoni mwa wale ambao hawakuhesabiwa katika sensa.

A l i s e m a , s a k a t a l a Sensa limewapa fundisho Waislamu na kutoa msukumo kwa upande wao kuwa na chombo ambacho kitakuwa ni kiunganishi baina ya Waislamu wa maeneo hayo husika na kupokea kauli za Masheikh wa Juu na kupeleka juu masua la yahusuyo Waislamu katika tarafa hizo.

Alisema, kwa sasa katika masuala ya kitaifa kuhusu Wa i s l amu , wanasub i r i

maelekezo na msimamo nini cha kufanya kuhusiana na sakata la Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Alisema, kupitia umoja huo viongozi wana jukumu la kulifikisha ngazi ya chini suala la NECTA, ili Waislamu waelewe madhara ya kuwa na chombo cha Taifa kilicho hodhiwa na dini moja na yepi madhara kwao.

U s t . P e s a , a l i s e m a , umoja huo uliundwa kwa kuwakutanisha Maimamu wakuu na wasaidizi wake katika kijiji cha Bonye, Kata ya Bwakila Chini, kutoka Miskiti 35 ya Tarafa hizo mbili.

U s t . P e s a , a l i s e m a katika umoja huo yeye ni Mkurugenzi wa Uhusiano, huku akiwataja viongozi wengine waliochaguliwa kuongoza umoja huo kuwa Mwenyekiti ni Amir wa Shura ya Maimam, Ust. Salum Kiserewende, Katibu ni Hamisi Mpendu, na mweka hazina ni Juma Ndevu.

WANAWAKE wa Kiislamu nchini, wametakiwa kujenga tabia ya kujitolea kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na Uislamu kwa ujumla, kabla ya kukimbilia wafadhili.

M b a l i y a k u j i t o l e a , p i a wametakiwa kujenga umoja, mshikamano sanjari na kuheshimu na kuwatii viongozi wao pale wanapowaongoza katika njia za kheri, ili kuleta mshikamano wa kweli.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa juma lililopita na Bi. Naima Chonde, akiwahutubia wanawake wa Kiislamu katika Kongamano la uzinduzi wa Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Wilayani Mkuranga , Mkoan i Pwan i , uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara na Kompyuta.

Katika uzinduzi huo, Bi. Chonde, aliongoza harambee kutoka kwa kina mama hao, chini ya viongozi wa Baraza hilo Taifa na kuweza kufanikisha kupatikana kiasi cha Shilingi 1,529,900/-, kwa ajili ya

Jitoleeni kabla ya wafadhiliBi Naima awaambia wanawake wa KiislamuNaye Bi Sururu ahimiza maendeleo, umoja

Na Bakari Mwakangwale maendeleo ya Baraza hilo.Bi. Chonde, alisema pamoja

na changamoto zinazowakabili w a n a w a k e w a K i i s l a m u Ulimwenguni kote, bado wanayo nafasi ya kusonga mbele iwapo watakuwa mstari wa mbele katika kujitolea, kuchangia na kuwatii viongozi wao.

Bi. Chonde, ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Adam Kighoma Malima, alikuwa msatari wa mbele kuhamasisha kuchangia akiwa na wanaharakati mbalimbali wa Kiislamu wa kike waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Diwani wa viti maalum, Hajat Aisha Sururu, huku naye akihimiza kina mama kutoa michango yao kwa ajili ya maendeleo ya Dini yao.

A i d h a , H a j a t S u r u r u , aliwashajihisha kina mama kote nchini kuliunga mkono Baraza hilo, kwa kusema kwamba ndicho chombo pekee kwa sasa nchini, kilichoonyesha dhamira ya dhati kuwa na mikakati ya kuwaendeleza wanawake wa Kiislamu katika nyanja za elimu, uchumi na kijamii.

“Zipo Taas i s i ny ing i , za wanawake hapa nchini, lakini hakuna hata moja ambayo mpaka sasa imeonyesha kuwa na nia ya kuwainua na kuwatetea wanapopata idhilali wanawake wa Kiislamu. Hivyo kina mama wenzangu tuliunge mkono Baraza letu, kwa manufaa yetu.” Alisema Hajat Sururu.

Awali, Katibu wa Baraza hilo Wilayani Mkuranga, Bi. Mariamu Lusasa, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, alisema Baraza lake linalaani vikali filamu iliyolenga kumkashfu Mtume Muhammad (s a w).

Katika risala hiyo, kina mama hao wa Kiislamu walimuomba Allah (sw) awashushie laana wale wote waliohusika katika kuitayarisha, kuicheza na hata kuisambaza filamu hiyo.

Baraza Kuu la Wanawake T a n z a n i a , n i c h o m b o kinachotambulika kisheria, ambacho miongoni mwa malengo yake ni kuwaunganisha wanawake wote wa Kiislamu nchini.

Baraza hilo pia lina lengo la kutoa elimu ya utambuzi kupitia mihadhara, warsha semina, makongamano pamoja na usambazaji wa vitabu vya maadali ya Kiislamu.

Lakini pia, Baraza limejikita katika kuhakikisha kinamama wa Kiislamu kote nchini wanajikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu ya ujasiliamali kila wanapopata fulsa ya kufanya hivyo.

V I O N G O Z I w a J u m u i a zinazoandaa safari za hijja hapa Nchini wametakiwa kuunganisha baadhi ya Jumuia zao zinazofanana ili kuwa na Taasisi chache zenye nguvu na uwezo mkubwa wa kutekeleza kazi hiyo kwa umakini na ufanisi zaidi.

Nasaha hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwaaga Mahujaji watarajiwa wa Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Makka, Saudi Arabia kwenda kutekeleza ibada ya Hijja Mwaka huu.

Hafla ya kuwaaga mahujaji ilifanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri Mjini Zanzibar.

Katika hafla hiyo, Balozi Seif alisema hatua ya kuungana taasisi itasaidia kuwapunguzia gharama nyingi na kupelekea kupatikana kwa lengo kuu la Hijja.

Alieleza kuwa Jamii inaendelea kushuhudia idadi kubwa ya Mahujaji kutoka Mataifa ya Bara la Asia na nyengine za Kiafrika wanavyojipanga mapema kupitia jumuia zao chache lakini madhubuti na kuwezeshana kutimiza Ibada hiyo.

“ Kwa wenzetu hili halikuja kwa sadfa, bahati au kujitokezea tu. Juhudi kubwa ilipita ya uelimishaji na uhamasishaji hadi watu wakafahamu, wakahamasika na kuanza kujipanga mapema na kuwawezesha kutimiza ibada hii”. Alifafanua Balozi Seif.

Aliomba Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar { UTAHIZA } ni vyema ukaangalia uwezekano wa kuziunganisha baadhi ya

Taasisi za kusafirisha Mahujaji ziungane - Balozi SeifNa Alghaithiyyah,

ZanzibarJumuiya zilizodhaifu kiutendaji na hatimaye kupata nguvu za pamoja na kuimarisha Jumuiya hizo kwa pamoja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mahujaji w a t a r a j i w a k w a m b a h i y o waliyoipata ni neema kubwa ambayo inahitaji shukrani na w a n a p a s w a k u m s h u k u r u Mwenyezi Muungu.

Aliwataka Mahujaj i hao watarajiwa watakapojaaliwa kurudi salama wazingatie na kuzilinda Hijja zao kwa kumudu katika twaa ya Allah.

“Al lah {SW} awajaa l ie muende salama na mrudi salama na mrudi na hidaya ya uongofu pamoja na hidaya { zawadi }, kwani wengi huenda wakarudi na hidaya {zawadi} bila ya hidaya ya uongufu”. Alisisitiza Balozi Seif.

Mapema Mwenyekiti waTaifa wa Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar {UTAHIZA } Sheikh S u l t a n K h a m i s M b a r o u k ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutaka kununua Meli kubwa kwa ajili ya usafirishaji wa Wananchi kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Sheikh Sultan alisema ni vyema Meli itakayonunuliwa iwe na uwezo pia wa kuandaliwa mazingira ya kuwasafirisha Mahujaji wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kwa gaharama nafuu utaratibu ambao hufanywa na baadhi ya Mataifa Duniani kusafirisha Mahujaji wao.

“Kuna malalamiko kutoka kwa Waislamu kuhusu kupanda kwa gharama za nauli ya Hijja kila mwaka na kutupiwa lawama Taasisi za Hijja”. Alisema Sheikh Sultan na kufafanua kwamba hilo si sahihi kwa ongezeko hilo husababishwa na kupanda kwa bei ya gharama za usafiri wa ndege, Nyumba panoja na Mahema huko Saudi Arabia.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar ameishauri Serikali kuimarisha na kuipauwezo zaidi Taasisi inayounganisha shughuli za Hijja kati ya Wizara ya Hijja ya Saudia na Tanzania {BIITHA} ili itekeleze kwa upeo zaidi kazi zake.

Alisema Zanzibar hivi sasa ndio yenye mamlaka ya kuiongoza Taasisi hiyo ya Biitha kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Saudia Arabia za kutaka Chombo kinachosimamia masuala ya Hijja kiongozwe na Mtu asiyepunguwa wadhifa bwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Serikali.

Kwa upande wake Kiongozi wa Taasisi inayounganisha shughuli za Hijja Kati ya Tanzania na Wizara ya Hijja ya Saudi Arabia { BIITHA } Sheikh Khalid Mohd Mrisho alisema kwamba Tanzania hivi sasa ina Taasisi karibu 25 ambapo Zanzibar pekee ina Taasisi 7 zinazoshughulikia safari za Hijja.

Sheikh Khalid alifahamisha kwamba Timu ya Uongozi wa Taasisi hiyo inatarajiwa kuondoka Nchini Wiki ijayo kwa ajili ya kujiandaa kuwapokea Mahujaji watarajiwa wa Tanzania watakaowasili Saudia kwa ajili ya Ibada hiyo.

Jumla ya Mahujjaji wa Tanzania wapatao 2,700 kati ya hao 1000 kutoka Zanzibar wanatarajiwa kuondoka Nchini katika makundi tofauti yatakayoanzia Tarehe 8 na 16 Oktoba mwaka huu.

Page 7: ANNUUR 1037

7 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Makala/Habari

S H U K U R A N I z o t e anastahik i Mwenyez i Mungu Mola wa viumbe wote. Rehema na Amani z imfikie Mtukufu wa Mitume.

Ama baada ya utangulizi huu. Katika mambo yasio na shaka kwamba kuwa mwanamke ana majukumu katika kila nyanja kwenye jambo muhimu, kwani mwanamke ni nusu ya Jamii. Na Mtume alitilia nguvu hili pale aliposema (Kwa hakika Mwanamke ni ndugu wa Mwanaume) na Uislamu umempa mwanamke haki zake kamili bila mapungufu yoyote kwani kabla ya Uislamu jinsia ya kike ilikuwa ni yenye kudharauliwa na madhila.

U i s l a m u u m e k u j a k u t a n g a z a k u o n d o a

Mwanamke wa Kiislamu kushikamana na elimu ni lazima na ni muhimuunyanyasaji huo na dhuluma z i l i z o k u s a n y i k a k w a mwanamke.

N a y a m e o n e k a n a majukumu ya mwanamke katika malezi maalumu kama ni miaka ya mwanzo katika umri wao yanatupwa majukumu katika kuwalea watoto kwa sahihi.

Na vyanzo vyote vya Uislamu vilivyo vizuri hapo watoto watakuwa katika uadilifu na usawa katika mambo yao yote ya kimaisha na kuwapa mafunzo ya tabia nzuri ambazo zinaendana na Dini ya Kiislamu pia zinamuepusha mbali kabisa na kutoka nje ya Dini na kukaa pembeni na mafunzo kwa kuaxha kutekeleza yake yaliopo katika maneno ya Mtume (S.A.W) kwamba (Nyote ni wachunga na kila mchunga ataulizwa kwa kile alichokichunga. Mwanamke ni mchunga katika Nyumba ya mumewe naye ataulizwa kwa kile alichokichunga, basi ni wajibu kwao kutekeleza amana hii kwa namna na kiasi anacho kiweza. Lakini inabidi tujue vipi anaweza

mwanamke kus imamia jukumu hili kubwa kwa uhakika ili tujue namna gani anaweza mwanamke kusimamia majukumu haya makubwa katika kuelimisha vyanzi hivi na namna hii inahitaji mambo mawili, nayo ni;

Kuwepo mawasiliano kati ya mwanamke na utamaduni wa Dini na Mji wenyewe (Mazingira). Hili ni jambo muhimu sana hapana budi kuwepo mambo haya hii ni kwa sababu ya kuandaa Ratiba ya masomo na kuelewesha juu ya ufahamu sahihi wa Jamii yenye uadilifu (Usawa) ambao husmaidia mwanamke kuwa na utulivu ili kupelekea ujumbe umfikie kwa urahisi na kuleta athari na kunyoosha tabia na kuzikuza falsafa hizi za uwastani unaoshikamana na kufanya watu wanakuwepo katika Ratiba zote Msikitini na Vyuoni na Mashuleni kwa kuhakikisha juu ya usalama wa ujumbe wenyewe katika kuuandaa na pia kuwaandaa watoto wa kike kwa kujua haki na wajibu kwa kwenda sambamba na matukio ya

SHEIKH WAHEED MANSOOR MOHAMED

maisha.Kwa hivyo wamegawanya

wanachuoni wetu katika mafungu matatu;

1. K u s h i k a m a n a mwanamke na Elimu ya lazima na yaliomuhimu tuu. Kisha akae nyumbani kwake na asitoke isipokuwa kwa haja maalumu.

2. A s h i k a m a n e n a mafunzioya kike kisha bila ya masharti au pingamizi za kitamaduni.

3. Uwastani na kuamini mafunzo ya Uislamu na pasiwe na mipaka na shiriki kazi nje ya nyumba yake pale anapotaka kufanya hivyo pamoja na kuchunga adabu za Uislamu.

La p i l i : - kurudisha uhai wa mahusiano kati ya mwanamke na nyumba ya Mwenyezi Mungu (Msikiti) katika Swala Tano na Idi na nyinginezo.

Na hili jambo ni muhimu sana kabisa kwani watu wengi wanawazuia wanawake wasiende Misikitini, lakini unahimiza Uislamu wanawake kwenda Msikitini na hasa katika zama hizi ambazo

wanaume wameshughulishwa na kazi mbali mbali na kushindwa kuwafundisha wake zao mambo ya Dini.

Na Mtume (S.A.W) aliweka mlango maalumu katika Msikiti wa Makka na akauita mlango wa wanawake: na akasema (msiwazuie waja wa kike wa Mwenyezi Mungu) waende na wajifunze na wao wawafundishe watoto wao na wawafikishie wanawake wenzao kwa kui fanyia kazi kauli yake Mwenyezi Mungu (Sema hii ni njia yangu nina lingania kwa Mwenyezi Mungu tena kwa ujuzi (umakini) na amehimiza Mtume (S.A.W) Masahaba wake na umati wake kuwa wajifunze bali wachukue nusu ya Dini kwa mama Aisha (R.A) akasema (chukueni nusu ya Dini toka kwa huyu cheupe naye ni mwanamke ambaye al ikuwa akiwafundisha wanaume na wanawake hivyo aliwafundisha uma wote na akawa ni mfano kwa wanawake wote na waweze kupata elimu hii ya Kiislamu na kuwafundisha watoto ili waelewe Uislamu sahihi.

KIJANA mmoja ‘amesilimu’ mara nyingi na kujizolea f e d h a k u t o k a k w a Waislamu.

K i j a n a h u y o aliyejitambulisha kwa jina la Peter John, akidai ni Mmasai kutoka Simanjiro, alifika Ifakara na kudai kwamba yeye ni Muinjilisti lakini ameona ukweli na kwamba anataka kusilimu.

Hiyo ilikuwa ni Alhamisi ya tarehe 27 Septemba, 2012 saa 12 jioni katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa ambapo alisilimishwa na Amiri wa kundi la Tabligh Sheikh Nassor lililo kuwa Msikiti Mkubwa wa Ifakara Wilaya ya Kilombero.

Habari kutoka Ifakara zinafahamisha kuwa baada ya kusilimishwa kijana huyo alipendelea jina la Ismail.

Katika maelezo yake kijana akizungumza kwa sauti ya upole ya kipadiri, alinukuu vifungu alivyodai kuwa ni vya Biblia vilivyokuwa na maelezo yanayofanana na Aya za Qur’an.

Ha l i h iyo i l iwavu t i a Waislamu wakawa wananukuu aya hizo na kisha kumchangia shilingi 210, 700.

Hata hivyo, walionakili vifungu hivyo walipokuja

Tapeli ajizolea fedha kutoka kwa WaislamAdai alikuwa Muinjilisti MmasaiAsilimu zaidi ya mara saba

Na Mwandishi Wetu

kutizama katika Biblia walikuta kuwa havipo, vifungu hivyo si sahihi.

Habari zaidi zinafahamisha kuwa siku ya Jumamosi Septemba 29, Peter aliwaaga Waislamu akisema kuwa anaelekea Morogoro ili arudi Arusha.

Hata hivyo akashukia Ruaha ambapo alisilimu tena kwa maelezo yale yale ya awali na kuchagua jina lile lile la Ismail.

Hapo Ruaha aliingia katika Msikiti mkubwa ulioko kando kando ya barabata ambapo alichangiwa shilingi 5,000.

Peter alilala hapo na Jumapili akaondoka akidai kwenda Morogoro lakini akashukia Kiberege akaenda

Msikiti uliopo Kiberege k a n d o y a b a r a b a r a n a kujitambulisha tena kuwa n i Muin j i l i s t i anaomba asilimu akasilimishwa. Hata hivyo baadhi ya Waislamu waliomsil imisha Ifakara wa l i kuwepo na kuanza kufuatilia nyendo zake bila ya

kumstua.Taarifa zinasema kutoka

Kiberege, Peter alikwenda

Mikumi ambapo alisilimu tena na kuchangiwa shilingi 14,000 na kutoka hapo akaenda

Mahenge ambapo kwa mtindo wa kusilimu alichangiwa shilingi 60,000.

Alirejea Ifakara stendi ya mabasi majira ya saa moja na nusu asubuhi na kukata tiketi ya kuelekea Morogoro katika basi la Mvumi tiketi hiyo iliandikwa jina la James Peter na kukaa katika kiti no. 25 na hapo ndio Waislamu wakamkamata na kumfikisha Kituo Kikuu cha Police Ifakara na kumfungulia Jalada IFA/RB/3099/2012 IFA/IR/1963/2012 kwa kosa la KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.

Hiyo ilikuwa Oktoba 3, 2012 ambapo baada ya kuangaliwa simu yake ikakutwa na jumla ya Tsh 380,000.

Ki jana huyo a l iomba Waislamu wamsamehe na kwamba atawarudishia pesa zote alizochukua.

Wakati huo huo, mtu mmoja mashuhuri katika wahadhiri (jina tunalo) alifika Ifakara mwishoni mwa mwaka jana na kuchangiwa jumla ya shilingi laki nne akidai kuwa ni gharama za kwenda kuwaleta wahadhiri wazungumze na Waislamu juu ya masuala ya Katiba Mpya.

Mpaka hivi sasa mhadhiri huyo hajarudi Ifakara na wahadhiri waliodaiwa kwenda kutoa somo hilo hawajafika.

Peter John kijana anayedaiwa kuwatapeli Waislamu.

Page 8: ANNUUR 1037

8 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Makala

Na Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir

KUANZIA mwezi wa Septemba mwaka huu, Dun ia imegub ikwa na ghasia kubwa kwa sababu ya mtu mmoja tu. Kuna walio muunga mkono mtu huyo chini ya mwavuli wa kile kinacho itwa hivi leo “Uhuru wa kutoa maoni/kujieleza”.

Na wapo waliokerwa na ghasia hiyo kwa sababu ya kuutumia vibaya uhuru huo wa kutoa maoni na kutokuwepo na mipaka ya uhuru huo. Matokeo ya uhuru huo usio na mipaka wa mtu mmoja, ni kugongana na uhuru wa kuabudu wa umma mzima.

Kadhia ya Muamerika mwenye asili ya Kiyahudi, aliyetengeneza filamu y a k u m s h u t u m u n a kumdhalilisha Mtume Muhammad (s .a .w.) , filamu iliyo sababisha ghasia (maandamano na vifo kwa baadhi ya watu) Duniani. Ni kadhia ambayo leo ndio gumzo la Waislamu na wapenda amani Ul imwenguni kote. Ni kadhia iliyopewa umuhimu hadi huko Amerika katika mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika katika mwezi wa Septemba mwaka huu.

Rais Obama alisisitiza sana suala la watu kupewa uhuru wa kutoa maoni, na akalaumu vikali sana mauaji yaliyotokea Libya ya Balozi na watumishi w a t a t u w a U b a l o z i huo wa Amerika, huko Benghazi.

Lakini uhuru mwingine (uhuru wa kuabudu) hakuugusia kamwe. Kwa msingi huo hakuweza

Uhuru wa kutoa maoni unapo gongana na uhuru wa kuabudu

kutangaza hatua ambazo Amerika itazichukua dhidi ya Muamerika huyo al iyesababisha ghasia hizo, ambazo ndizo zilizopelekea mauji na kujeruhiwa kwa watu wa Taifa lake na mataifa mengine.

Pia ameshindwa hata k u c h u k u a h a t u a y a maneno akaomba radhi kwa niaba ya nchi yake ambako ndiko chimbuko la ghasia hizo.

Ni nchi nyingi leo hapa duniani zinazo zungumzia uhuru wa kuabudu kwa raia wake, lakini siku uhuru huo unapo gongana na uhuru wanao utaka wao, dhaahiri shaahiri wanakuwa tayari kuulinda, kuutetea na kuushabikia huo uhuru wanao utaka wao.

Uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake yaliyomo moyoni mwake bila ya mipaka, tena bila ya kujali kuwa maoni yake hayo yanajeruhi imani na hisia za watu wengine. Huu ni uhuru uliowekwa na

watu wenye kusukumwa na matashi na malengo dhaifu ya kibinaadamu.

L a k i n i u h u r u w a k u a b u d u , n i u h u r u uliowekwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.), hana nafasi mtu yeyote duniani kuukosoa. Kumshutumu M t u m e M u h a m m a d (s.a.w.) na kumdhalilisha ni kosa kubwa sana katika dini ya Kiislamu. Mwenye kufanya kosa hilo adhabu yake n i kuuawa na kuitekeleza adhabu hiyo ni haki kabisa.

Katika wakati wake Bwana Mtume (s.a.w.) alipata kutoa amri ya k u m u u a m t u a l i y e mtukana , lak in i p ia alikuwa akitoa nafasi kwa ambaye anataka kuomba radhi na msamaha baada ya kosa hi lo . Dal i l i kubwa leo ya madola ya nchi za Magharibi, Amerika na Ulaya katika kuufanyia uadui Uislamu na Waislamu, ni kukosa jambo hilo.

Hawako tayari hata

mara moja wanapofanya makosa kuomba msamaha wao au kumlazimisha aliyefanya kosa hilo yeye mwenyewe aombe msamaha. Wako tayari kumteteta kwa hoja zozote aliyefanya kosa hilo au kumlinda kwa gharama yoyote.

Hali ile ile iliyotokea kwa Salman Rushdie, ndio hiyo hiyo inayojitokeza leo kwa Same Bathel (Muamerika mwenye asili ya Uyahudi). Haya ndiyo matatizo yanayotokana na sheria za kutungwa na wanaadamu; wajawa m a p u n g u f u w a n a o sukumwa na matashi na malengo binafsi katika kuzi tunga , na k isha zikashabikiwa na madola makubwa.

Sheria wanayoitunga wao wanaona ndio sheria pekee ya haki na uadilifu i n a y o w e z a k u k i d h i mahitaji ya watu wote na wa itikadi zote, hata kama sheria yao hiyo inagongana na sharia au

itikadi za dini kuu zilizopo Duniani.

Kwa muda huu, sisi Waislamu tunasubiri utekelezaji wa pendekezo l i l i lo tolewa na Rais Muhammad Mursi wa Misri katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, y a k w a m b a U m o j a huo uweke sheria ya kuzuia uhuru unaoweza kushutumu itikadi za waumini, ingawa hatuna tamaa kubwa Waamerika wataweza kulikubali pendekezo hilo.

Lakini pendekezo kama hili hili, lingekubaliwa na Amerika bali na Nato yote kama lingekuwa ni kwa ajili ya kudhibiti uhuru wa kutoa maoni wa Rais Ahmad Najad wa Iran, la kutaka kuifuta Dola ya Israel katika ramani ya Mashariki ya kati. Au kukanusha baadhi ya yaliyomo katika historia ya Wayahudi walipokuwa Ujerumani.

Wabillah taufiq.

Page 9: ANNUUR 1037

9 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Makala

LICHA ya kwamba Ta n z a n i a n i n c h i yenye Waislamu wengi katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, bado imeendelea kuwa na mahuja j i haba wanaokwenda Hija kila mwaka.

Wakati kiwango cha Waislamu wa Tanzania kinachotolewa na serikali ya Saudia Arabia kwa ajili ya kwenda hija kila mwaka hakizidi Mahujaji 2,500, wanaokwenda kutekeleza ibada ya Hija wanakadiriwa kuwa ni 2,200 kwa mwaka huu.

Ka t ika t aas i s i 22 zilizosajiliwa nchini kwa ajili ya kusafirisha Mahujaji, wastani wa kila taasisi ni kusafirisha Mahujaji 100-150 tu.

Taasisi ya kusafirisha mahujaji hairuhisiwi k u p e l e k a m a h u j a j i iwapo itashindwa kifikia kiwango cha kuhudumia mahujaji 100. Iwapo itatokea taasisi kushindwa kufikia idadi hiyo ya Mahujaji, basi hulazimika kupeleka mahujaji wake katika taasisi nyingine iliyotimiza idadi hiyo ili kuwasafirsha na kuwapa huduma nyingine za Hija.

Na hata usafirishaji wenyewe unategemea zaidi kutumia mashirika ya ndege ya nchi za nje, sio ATC wala Precission Air.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Waislamu wa hapa nchini, zaidi ya Wairani 75,000 wameripotiwa kuwa watashiriki katika ibada ya Hija mwaka huu. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, safari za ndege za Hija zimeanza Septemba 24 na kila siku Mahujaji 3,000 wanasafirishwa kuelekea Madina na Jeddah . Kinyume na miaka ya huko nyuma, Mahujaji wa Iran watasafirishwa kupitia Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wa k a t i m a h u j a j i w a k i w a h a b a h a p a

Mahujaji Tanzania bado haba

Na Shaban Rajab

Ta n z a n i a , S e r i k a l i y a S a u d i A r a b i a imeihakikishia India kufanyia kazi masuala y a n a y o h u s i a n a n a kuwahudumia Mahujaji kutoka India. Saudia imetangaza kuchukua hatua hiyo kufuatia ombi la Krishna la kutaka kuongezwa idadi ya Mahujaji kutoka

India kwa robo moja hadi kufikia Mahujaji 200,000. Serikali ya Saud ia ime tangaza kulipa kipaumbele ombi hilo la Waislamu wa India. Inakadiriwa kuwa India hupeleka mahujaji wanaofikia 150,000 kila mwaka.

Kufuatia kufanyiwa k a z i m a o m b i y a

India, Kamati za Hija nchini humo tayar i zinaandaa orodha ya mwisho ya Mahujaji, ambayo imee lezwa kuwa itaongeza idadi ya mahujaji wa India w a t a k a o r u h u s i w a kwenda Hija safari hii.

Ibada ya Hija ni nguzo muhimu ya Uislamu na ni kongamano kubwa zaidi

la Waislamu kutoka kona zote za dunia. Huko Nigeria, kwa mara ya kwanza tangu kuingia Uislamu nchini humo, Mamlaka za Saudi Arabia mapema wiki hii zimewarejesha Nigeria Mahujaji wanawake kutoka Nigeria wanaokadiriwa kufikia 1,000 ikidaiwa kuwa wameingia Saudia kwa ajili ya ibada ya Hija bila ya kuambatana na maharimu wao. Mamlaka za Maeneo Matukufu zimedai kuwa kiutaratibu, mahujaji hao wanawake lazima wawe wameambatana na maharimu wao wa kiume kama vile baba, kaka au hata mtoto wa kiume au mume.

Kufuatia adha hiyo kwa mahujaji wanawake wa Nigeria, Masheikh nchini humo wamepinga

vikali hatua hiyo ya Saudia na kueleza kuwa hatua hiyo haikufuata kwa kina udhuru wa wanawake kuhiji kwa makundi.

Nigeria ni miongoni mwa nchi za bara la Afrika zinazoongoza kwa kuwa na mahujaji wengi wanakwenda Hija Saudia.

Page 10: ANNUUR 1037

10 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Tangazo

The Deanship of Graduate Studies at King Fahd University of Petroleum and Minerals (KFUPM) is pleased to invite your attention that application to Graduate Studies at KFUPM is now open online from the link http://www1.kfupm.edu.sa/gs/application/preonline.asp until October 8, 2012. KFUPM provides full MS and PhD scholarships for distinguished graduate applicants who demonstrate high potential for conducting original research in the fields of Engineering, Sciences and Business.

Distinguished Partnership of KFUPM with International InstitutionsKFUPM has very strong collaborative partnership on conducting innovative research

with the following international institutions:• MIT: Clean Water and Clean Energy.

• Stanford: Oil, Gas and Geosciences.

• California Institute of Technology (Caltech): Petrochemicals and Polymers.

• Technical University of Munich: Refining and Petrochemicals.

• Cambridge University: Oil and Gas.

• Georgia Institute of Technology (Georgia Tech): Geo-signal Processing and Smart Grids.

• National University of Singapore: Refining and Petrochemicals

• KAUST: Many research disciplines in Engineering and Sciences.

• Saudi Aramco (the largest oil company worldwide): Many research disciplines.

• SABIC (one of the leading petrochemical companies worldwide): Refining, Petrochemical and Polymers.

• In addition to many world-class universities and industries on different research fields.

Centers for Research Excellence at KFUPM To provide extreme support for research in areas of excellence, KFUPM has established

National Centers for Research Centers for Research Excellence at KFUPM To provide extreme support for research in areas of excellence, KFUPM has established

National Centers for Research Excellence in the following areas:• KFUPM-MIT Collaboration Center on Clean Water and Clean Energy (http://

ccwce.mit.edu/).

• Nanotechnology (http://www2.kfupm.edu.sa/cent/).

• Renewable Energy (http://corere.kfupm.edu.sa/).

• Refining and Petrochemicals (http://core-prp.kfupm.edu.sa/).

• Corrosion (http://www2.kfupm.edu.sa/corec/).

• Transformative Research in Petrochemicals and Polymers (http://cid-rpp.kfupm.edu.sa/).

• Maintenance (http://se.ikfupm.com/department/ce/ceim/).

• Supply Chain Management (http://se.ikfupm.com/department/ce/cescm/).

• Carbon Capture and Sequestration. The Research Institute The Research Institute is the cornerstone of applied research activities at KFUPM,

solving critical scientific and technical problems as well as working on turning knowledge into practice. More details are available on the website of the Research Institute at the link: http://www.kfupm.edu.sa/ri/

Research Groups at KFUPM To provide special support for research in focused areas of interest to Saudi Arabia,

KFUPM has established 13 Research Groups in Science and Engineering areas. More details are available on the website of the Deanship of Scientific Research at the link: http://www.kfupm.edu.sa/dsr/

Graduate programs offered at KFUPMDISCIPLINE DEGREESAerospace Engineering M.Sc.Applied Statistics M.Sc.Architectural Engineering M.Sc.Business Administration M.B.A.Chemical Engineering Ph.D., M.Sc.Chemistry Ph.D., M.Sc.

KING FAHD UNIVERSITY OF PETROLEUM & MINERALS (KFUPM)DEANSHIP OF GRADUATE STUDIES

Dhahran, Saudi ArabiaCity & Regional Planning M.C.R.P.Civil Engineering Ph.D., M.Sc.Computer Engineering M.Sc.Computer Networks M.Sc.Computer Science M.Sc.Computer Science and Engineering Ph.D.Construction Engineering & Management M.Sc.Electrical Engineering Ph.D., M.Sc.Environmental Science M.Sc.

Geophysics M.Sc.Industrial & Systems Engineering Ph.D., M.Sc.Materials Science & Engineering M.Sc.Mathematical Sciences Ph.D., M.Sc.Mechanical Engineering Ph.D., M.Sc.Medical Physics M. Med. Phys.Petroleum Engineering Ph.D., M.Sc.Physics Ph.D., M.Sc.Software Engineering M.Sc.Systems Engineering Ph.D., M.Sc.Security & Information Assurance M.Sc.Telecommunication Engineering M.Sc. Online Admission System The online graduate admission application for the coming Spring Semester 2012-

2013 (Starting in Jan. 2012) will be available until Oct. 8, 2012, 2012 through this link: http://www1.kfupm.edu.sa/gs/application/preonline.asp

After submission a complete online application, mandatory documents need to be uploaded before Oct. 15, 2012 through the Upload System using the same Login ID and PIN created for the online application using this link: http://adgs.kfupm.edu.sa/

Mandatory documents for application (without which application will not be processed)

• Copy of identification (Passport for international applicants / National ID for Saudi nationals / Iqama for residents of Saudi Arabia).

• Complete official transcripts for BS degree (and MS degree if applying to PhD).

• Statement-of-Purpose (a one-page essay focusing on career and research goals at KFUPM).

• Recommendation Letters from academic referees through the online recommendation system after submitting the online application.

• Certificates for BS degree (and MS degree if applying to PhD) if degrees granted.

• GMAT score (for international MBA applicants).Other supporting documents (needed for final decision)

• TOEFL score (min. is 68 IBT for MS and 79 IBT for PhD) or IELTS score (min. is 6 for MS and 6.5 for PhD).

• Acceptable GRE General score (min. Quant. is 720 (or 156 on the new scale), min. Analytical is 4.0).

• Upon approval, original/certified copies of degree certificate(s) and transcript(s) are to be sent through postal mail.

Application Deadlines• TOEFL score (min. is 68 IBT for MS and 79 IBT for PhD) or IELTS

score (min. is 6 for MS and 6.5 for PhD).

• Deadline for submitting the online application is Oct. 8, 2012.

• Deadline for uploading mandatory documents is Oct. 15, 2012.

• Deadline for recommendation letters to be received via the online recommendation system is Oct. 15, 2012.

If there are any questions or further clarifications are required, please feel free to contact us at [email protected] or Telephone : +966-3-860-2800 begin_of_the_skype_highlighting +966-3-860-2800 end_of_the_skype_highlighting, or check our website at: http://www.kfupm.edu.sa/gs

We wish you the best in your endeavor.

Page 11: ANNUUR 1037

11 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Tangazo

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:• Mkuzo Islamic High School - (Songea) - BWENI TU.• Kirinjiko Islamic Sec. School – (Same) - BWENI TU• Nyasaka Islamic Sec.School – (Mwanza) - BWENI TU.• Ubungo Islamic High School –(Dar es Salaam) - KUTWA NA BWENI

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya Kiislamu.2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Qur’an na mafunzo yake, Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics,

Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book – keeping na Commerce.3. Patakuwa na mtihani tarehe 01/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11 /20125. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

• Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni -0763 282 371/ 0784 406 610• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha – 0654 723 418 - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075• Tanga - Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 - Ofisi ya Islamic Education Panel - Mwanza -Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin – 0785 086 770• Musoma - Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni-0714587193• Kagera - Bukoba: Alhuda Café Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA.-0688 479 667

• Shinyanga - Msiikiti wa Majengo-0718866869 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 • Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 - Ofisi ya Islamic Ed.Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin-0655144474• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086• Singida - Ofisis ya Islamic Ed. Panel –karibu Nuru snack Hotel-0714285465• Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575• Kigoma - Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860 - Kasulu: Murubona Isl.ss 0714710802• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663• Mtwara - Amana Islamic S.S 0786 729 973• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU—0715 68 1 701/0716791113 - Mkuzo Islamic High School. 0716 791113• Mbeya - Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole-0713 200209 - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209

• Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122

• Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331

• Unguja - Madrasatul –Fallah: 0777125074- • Mafia - Ofisi ya ust.Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu – 0653705627

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA – 2013

Page 12: ANNUUR 1037

12 AN-NUURBarua/Shairi Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012

Ni tarehe thamania, mnaanza mitihaniMwezi wa Oktobia, na siku ya IthinaniMwaka mnautambua, ni ziro moja na thaniMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Kalam mkizishika, jambo moja tambueniAdui yenu ni NECTA, hivyo msuli pigeniNi machinjio hakika, katu acheni utaniMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Jambo la kuzingatia, mpo katika JihadiKaa chini fikiria, onesha yako juhudiJibu huku metulia, tumkamate FisadiMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Mwafelishwa makusudi, hili hapa tambueniKatu msije jirudi, pambaneni kwa juhudiHii ni yenu Jihadi, mlofunzwa darasaniMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Uanzapo kuandika, umuombe Mola wakoAtie zake Baraka, unusuru dini yakoMbele muweze kufika, kutetea dini yakoMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Mwisho naiomba dua, Mwenyezi awajalieNyote muweze pasua, na mbele muendeleeKafiri anosumbua, Allah mpe dhilalieMema tunawatakia, nyote Kidato cha Nne.

Mwl. Mohammed MakimuUITC-DAR ES [email protected]

MH: WAZIRI TWAJA TENABado tunakukumbuka, sidhani tumekutupaDhulma inofanyika, mipakaye imechupaDamu itaja mwagika, na kuanza tapatapaKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Waziri Katibu wako, ni nyie ninawatajaTwataka mabadiliko, si midomo kubwabwajaNECTA sio ya kwako, wala si ya kundi mojaKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

NECTA si parokia, wala genge la wahuniKile mlotufanyia, ukweli tumebainiData tumewapatia, ukweli tumebainiKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Kama ni malalamiko, ambayo tunawambiaNa hoja zisomashiko, mwasema tunazitoaNinyi zenu wapi ziko, mbona hamjatoa?Kidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Mepita mtandaoni, nikaliona tamkoHoja zenu ni laini. wala hazina mashikoAcheni wenu udini, zitoeni hoja nzitoKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Hizo ni zangu salam, ila bado tupo soteNinyi ni wataalam, mbona mwawa kama mate?Mwaua Waislamu, vijana wao wasoteKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Kile mlotufanyia, hasa kidato cha sitaKama mtakirudia, mazito yatawafataMatokeo twangojea, jueni tutawafataKidato cha Nne waja, hebu haki itendeke

Jela kwa Muislamu, ni sunna za manabiaHaokopwi mwanadamu, ila ALLAHU JaliaHata tupigwe mabomu, nanyi pia mtajifiaUkishindwa kufikiri, hutaweza kuamua !!

Mwl. Mohammed MakimuUITC-DAR ES [email protected]

KILA LA KHERI KIDATO CHA NNE HAKI hakii! Uadilifu! Mataifa makubwa yenye nguvu za ve to kama Marekani yanapaswa kufanya haki. Kwa nini nchi ndogo na dhaifu hasa za Kiafrika hupelekwa machinjioni Ulaya kwa kile kinachoitwa uhalifu wa kivita? Marekani jee haonekani anayoyatenda? I k i w a y a M a r e k a n i hayaonekani , nahofu walimwengu tumekuwa v i p o f u . H A K I n a UADILIFU vidumishwe duniani kote. Marekani t a i f a k u b w a S U P E R POWER tafadhali taifa hili nalo linastahili kudumisha haki ili lijenge heshima yake kwa wanyonge.

Marekani ni kinara wa kuvunja haki za binaadamu. Kauli hiyo ni dhahiri shahiri haitaki tochi. Ya nini tumulike kurunzi mchana kweupe na mambo yote yako wazi tena hadharani?.

M a r e k a n i m b a b e anaejipachika umwamba wa kuwaonea wembamba. Anadhani anatamba lakini ulimwengu ana unanga (anauharibu) adhulumu, ahujumu hakuna wa kumzidi anajitia uhavinambi hata ak i fahamishwa ha ja l i . M a r e k a n i a n a t i s h a , a n a o g o p w a k a m a OCTOVIAN CIZARE Mkuu wa wachawi kisa cha yote ni mkubwa ana maguvu ya kijeshi. Akiwatisha, ak iwa t imba ana j ivuna kwa vile anaona atashinda anafanya anavyotaka, kwani mwenye nguvu mpishe.

Mimi katu sitompisha akionea watu nitambisha.

Mjini Hiroshima Japan, 1945, Marekani aliiangamiza jamii kwa kuupiga mji huo bomu la atomic. Athari iliyotokea haielezeki kwa kalamu wala kwa ndimi zenye ladha ya nahao. Bado kitendo kile ulimwengu hautakisahau. Vizazi vya huko vinaathirika hadi zama hizi tulizo nazo.

Vietnam yalifanyika ni ya utwana tena ya kinyama nyama hayasahauliki mpaka kiama. Watoto na kinamama walikatwa katwa maziwa hayo niliyashuhudia kwenye picha mbali mbali mnamo 1968 wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa darasa la sita.

Marekani ni taifa lenye sifa ya “Double face”. Taifa lenye nyuso mbili upande hujipa wema na huruma kumbe ni taifa zandiki na nafiki. Haya niliyashuhudia mwaka 1963 nilipokuwa mwanafunzi wa darasa la

Marekani ni kinara wa uafriti duniakwanza. Nililia sana pale alipouliwa Rais wa Marekani Kenedy, kwa vile nilidhani Marekani ni taifa jema kwa vile tulipewa misaada ya maziwa ya unga ya bure. Tukiwa skulini zama hizo tul ikunywa maziwa ya Marekani. Nilikuja kujuwa kumbe Marekani si mwema baada ya kugundua unyama uliofanyika nchini Vietnam.

Mpaka hivi sasa, sera za Marekani ni zile zile kugawa vyandarua vya bure lakini huku Marekani anawauwa kwa makombora watu wa nchi nyingine wasio hatia.

Afghanistan, Iraq na Libya bwana mkubwa huyu mwenye milki, uluwa na faka ya mamlaka anafanya ushenzi anautaka.

M a r e k a n i t a i f a lililotunukiwa nguvu na Allah. La kuhuzunisha na kusikitisha linalindwa kuzitumia kwa manufaa ya viumbe wenzake mwaka 1990 BUSH aliipiga mabomu mazito Iraq katika vita vinavyojulikana kitaalamu “Stars war” Iraq nchi ambayo ilikuwa juu sana kiuchumi imeporomoka mpaka hivi sasa.

Mwisho wa yote, Rais wa Iraq Marehemu SADAM HUSSEIN walimtumbua damu kama vile wanaouwa kunguni. Nchini Libya vyanda vya Marekani vilimbanja Gadafi kama vile walikuwa wanauwa chawa.

Marekani huyo huyo ndie kinara wa uonevu u n a o f a n y w a d h i d i y a Wapalestina. Marekani siku zote hufurahia na kuunga mkono maovu yanayofanywa na Wayahudi.

Marekani ana wivu, anaona gere kuona nchi nyingine zinapiga hatua kimaendeleo. Leo maendeleo ya Nchi nyingine kama vile Iran, Korea na China yanampa kiherehere. Marekani haachi kupiga kelele. Mara Iran ana NUCLEA, uwongo mtupu na uzandiki ana kijiba cha roho kwa kuona wengine nao wanapiga hatua.

Lengo la Marekani ni kutaka yeye awe bwana pekee yake wengine wawe wa twana . Ki sa mkasa yalipotokea ya September 11 Bwana Mkubwa analia yoo! Yoo! Mpaka leo kisa nae alionjwa kidogo. Kumbe Masky Scraper yake nayo yanaweza kuporomoka kama anavyoviporomoa vijumba vya wengine kwa mabomu? Hebu angalia uchungu al ionao dhidi

ya kifo cha Balozi wake, Chriss Stevens kilichotokea Libya hivi karibuni, kwa Amerika Mmarekani ndie mtu, watu wengine ni sawa na wanyama mwitu. Matamu hayoo? Hayo hayanipi hamu. Iweje roho ya Mmarekani ionekane tamu ya wengine iwe chungu kama shubiri? Nina kawaida ya kutoridhia uonevu na ukandamizaji na mwisho huulani.

Dunia kizungu mkuti, wanaojidai kutetea amani ndio wanaivunja . Wao huwaonea wanyonge akina Raisi Omar Al-Bashir wa Sudan kutaka kuwapeleka k a t i k a m a h k a m a z a o kumbe wanaovunja amani ya dunia hatu hawaguswi, sababu wamejipa Veto wamejipachika ukubwa. Wakubwa wa dunia hawa Wazungu wanaachwa akiuwa watu hasa wanyonge wan chi zetu za ulimwengu wa tatu. Kwani kuna siri gani ya huku kuumbwa Wazungu na kujifananisha na miungu?

TAKBIR! Takbir kufru zimezidi dunia ati kuna hiki kikasisi feki kikaragosi uchwara cha mathehebu ya kiprotestan nchini Marekani Terry Jones kimetangaza nia kumfungulia mashitaka M t u m e w e t u m p e n z i Muhammad ( s.a.w). Jeuri hiyo ameipata wapi bwana huyu? Si bure nadhani ametumwa au asitumwe mimi sitaacha kumwambia kama kufunguliwa mashtaka inapasa taifa la Marekani listakiwe limefanya uhalifu mwingi wa kivita. BUSH wote wawili na Obama wao wanastahili kupandishwa machinjioni kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Watu wa Iraq, Afghanistan na Libya hivi sasa iko haja kukaa pamoja tena waimbe kwa nguvu zao zote.

Marekani ana kwao kwa nini awe mvamizi mlowezi wa nchi nyingine. Historia inatwambia kuwa Wazungu ni wazowefu wa kuyavamia mataifa mengine. Hata huko Marekani wenyeji wake wa asili ni Wahindi Wekundu “ Red Indianis” lakini walowezi wa Kizungu waliwafisidi watu hawa na kuwafanya si chochote si lolote.

Haki! Hakii mataifa makubwa yenye nguvu za veto nayo yafanye haki.

Mzee Hassan Mkwenda Hassan

Zanzibar.

Page 13: ANNUUR 1037

13 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Tamko/Tangazo

The fifth graduation ceremony will be held at the campus of the Muslim University of Morogoro on SATURDAY, 17th November, 2012. The ceremony is expected to start at 2.00 pm and end at 4.30 pm.

Students eligible to attend the ceremony are undergraduates who successfully completed their studies in 2012.

Parents, relatives and guests of the students as well as interested members of the general public are welcome to attend the graduation ceremony. Guests are expected to dress modestly and decently. Lady guests attending the ceremony are advised to wear the hijab or any dress that does not expose the body other than the face, hands and feet.

All eligible students are requested to attend the occasion, regardless of whether or not they bring guests. However, they must inform the office of DVC (Academic) of their intent to participate in the ceremony NOT LATER THAN 30th October, 2012. Preferably call or email by a phone call or by electronic mail.

Academic costumes (gowns, hoods and caps) are available for hire by the graduands but they must be booked by at least 5th November 2012. The University cashier’s office must receive from each of the participating students a total of Ts. 35,000 (Ts. 20,000 for hiring the costumes, Ts. 10,000 deposit security which is refundable, and Ts. 5,000 convocation fee).

MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGOROP.O. BOX 1031 Morogoro, Tanzania.

Tel: +255 23 2600256; Fax: +255 23 2600286E-mail address:[email protected]

Website: www.mum.ac.tz

FIFTH GRADUATION CEREMONY FOR UNDERGRADUATE DEGREESCONFERMENT 2012

Graduands, who do not have academic costumes on, will not be allowed to participate in the Ceremony.

Graduands are required to bear in mind that the hired gowns shall have to be returned after the ceremony. A heavy fine will be imposed in case the costumes are damaged, or not returned and/or in time. A hiring Contract Form will be provided for completion by those intending to hire the costumes.

For the safety of all participants and their guests, close-up picture taking and video recording of the graduation ceremony is restricted. Pictures may be taken before and after the ceremony.

REHEARSAL

Since the rehearsal is an integral part of the ceremony, all graduands who wish to attend the graduation ceremony MUST attend the rehearsal which is scheduled on Saturday morning (17th November, 2012) at 8.30am at the graduation site. Failure to attend all rehearsals by students will result in immediate cancellation of their eligibility to participate in the graduation ceremony.

Certificates and transcripts of the graduands will not be given at the ceremony. These can be received at another convenient day from the Office of the DVC (Academic) upon signing register books and presenting an ID card.

DEPUTY VICE CHANCELLOR (ACADEMIC)

BARAZA kuu la Jumuiya za Answaru Sunnah Tanzania (BASUTA) limefuatilia kwa karibu na kwa umakini mkubwa utovu wa adabu na umomonyokaji wa maadili uliyooneshwa na genge la watu wenye chuki na Uislam na Mtume Mtukufu wa Waislamu; Pamoja na tukio hilo BASUTA imeshuhudia k u p a m b a m o t o k w a ghasia na maandamano ya Waislamu na wapenda haki na amani kote duniani; na ambayo baadhi yake yamepelekea vifo kwa watu wasiyo na hatia, uharibifu wa baadhi ya balozi na majengo ya ibada ya dini nyingine.

Mungu anasema: ( I k i w a n y i n y i

hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika

TAMKO LA BASUTA KWA WAISLAMU KUHUSU FILAMU NA VIBONZO VYA KUMDHALILISHA MTUME MUHAMMAD

wawili walipokuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima). Attawbah: 40.

K u t o k a n a n a s a k a t a hilo Baraza linatoa tamko lifuatalo:-

1. B a r a z a K u u L a J u m u i y a Z a A n s w a r u Sunnah Tanzania (BASUTA) linapinga vikali matumizi mabaya ya uhuru wa kutoa habari unaolenga kuchochea ghasia, kuhatarisha amani kwa kudhihaki hadhi za Mitume wa Mungu na matukufu ya watu wengine.

2. Baraza linawahimiza na kuwataka Wais lamu kote nchini kuwa watulivu na kutopoteza muda wao kwa kushughul ishwa na chokochoko za mamluki hawa, kinyume chake tumieni fursa hii ya kumnusuru Mtume Muhammad kama; kichocheo cha kufuata sunnah sahihi za Mtume Muhammad kwa mujibu wa uelewa wa wema waliyotangulia, kuiga nyendo zake sanjari na kuwaelimisha watu wa dini nyingine uzuri wa Uislamu.

3. Baraza linawaomba Waislamu wote wa nchini japo si suluhisho; kupitia mchakato wa katiba mpya unaoendelea h iv i sasa , wapendekeze vifungu vitakavyoainisha kutambuliwa kwa dini, kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, maana ya uhuru wa kuabudu kwa maana ya neno, mipaka ya uhuru wa habari, na mwisho z i p e n d e k e z w e k a n u n i

zitakazolinda na kuheshimu m a t u k u f u y a w e n g i n e , angalau mwisho wa siku sote tuishi kwa kuvumiliana na kuheshimiana.

4. B a r a z a l i n a t o a angalizo; vitendo hivi vya kichokozi vinavyofanywa na mahasidi hawa, kamwe havitaathiri heshima iliyotukuka aliyopewa Mtume Muhammad na Mola wake, na anayoendelea kutunukiwa na watu waadilifu wa dini mbalimbali duniani kwa kuthamini mchango wake katika historia ya dunia na maendeleo ya binaadamu, na katu chuki zao hazitapunguza mapenzi yetu kwa Mtume Muhammad.

5. Baraza linawataka watu wote wafahamu; Ni haki ya Waislamu kote duniani kupinga vitendo hivi viovu na mfano wa hivi kwa kutumia nyenzo mbalimbali zisizokinzana na maadili ya Uislamu na bila

ya kusababisha madhara kwa watu wasiyohusika - kwa kulizingatia neno la Allah: “Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine”. Al-israa: 15.

6. Baraza linawataka Waislamu wachunge ndimi na lugha zao kila wanapohemkwa- kwani:- Swahaba Abi Hureyrah al isema: Mtume al iwahi kutakiwa awaapize washirikina (baada ya kumjeruhi vibaya), akasema: “Kwa hakika mimi sikutumwa kuja kulaani (watu) hakika mimi nimeletwa kuwa ni rehema”.Muslim 8/24.

Mwisho: Rehema na amani ya Allah zimshukie kipenzi wetu Mtume Muhammad, Swahaba zake na wote waliyomfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho.

Shaabani MussaKatibu Mkuu

Page 14: ANNUUR 1037

14 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012Makala

“NABII ana haki zaidi kwa Waislamu (waliomfuata) kuliko nafsi zao, (lazima wamkinge hata kwa kutoa roho zao)…”.

Hiki ni kipande cha Aya ya sita ya suratul Ahzab (Tafsiri ya Al-Farsy).

Inasimuliwa kwamba baada ya Aya hii kushushwa, Khalifa Mtukufu Umar Ibn Khatab (RA) alikwenda kwa Mtume SAW na kumwabia ukweli toka moyoni mwake kwamba bado hajisikii kama yuko tayari kufa kwa ajili ya kumhami Mtume SAW, kama inavyotamka Aya. Mtukufu wa daraja Mtume Muhammad SAW akamjibu kuwa bado hajaamini/kwamba imani haijajikita bado katika kifua cha Umar Ibn Khatab (RA).

Inaendelea kusimuliwa kuwa baada ya muda kupita Umar Ibn Khatab alikwenda tena kwa Mtume SAW na kumwambia kuwa kwa muda huo alikuwa anajihisi yuko tayari kuutoa muhanga uhai wake kwa ajili ya kumhami Mtume SAW, na hapo Mtume SAW akamwambia kwa muda huo alikuwa amekwisha amini/kwamba kwa muktadha huo, imani ilikuwa tayri imechukua nafasi ysake katika kifua cha Umar (RA).

Kwa mujibu wa Aya na ka mujibu wa kisa hiki tunapata mafunzo kwamba ili tuwe miongoni mwa walioamini, basi yatakakana tuwe tayari kumhami Mtume Muhammad SAW. Na kwa kuwa yeye hayupo kwa sasa, basi tunawajibika kulihami jina lake na heshima yake pale maadui wa Uislamu wanapotaka kumchafua kama ambavyo wanajitahidi kufanya kila uchao. Aidha tunatakiwa kukihami kile alichokuja nacho yaani uislamu; kwa maana ya Quran na sunna.

Aya ya 59 ya su ra t Annisaa inasema hiv i : “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, waliokatika nyie (Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo inamatokeo bora kabisa.”

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu baada ya kututaka tuwe tayari kufa kwa ajili ya mtume SAW, anatuambia tuna wajibu wa kuwatii vingozi wetu katika dini, wale tuliowaweka mbele ili watuongoze. Anasema Mola mlezi tumtii yeye, Mtume na viongozi wetu. Kwa

Tuwatengeneze akina Nasralallah wetu

Na Rajab Nkawa

maneno mengine ni kuwa viongozi wetu ni bora kwetu kuliko nafsi zetu. Twatakiwa kuwahami na kuwalinda dhidi ya maadui wa uislamu na Waislamu.

Aidha kat ika Aya 10 mpaka ya 11ya suratul Saff, Mola wetu mlezi anatuambia; “ E n y i m l i o a m i n i ! J e nikufahamisheni biashara itayokuokoeni na adhabu i u m i z a y o ? M u a m i n i Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu ikiwa mnajua (kuwa ni bora, basi fanyeni).”

K a t i k a A y a h i z i Mwenyezi Mungu Mtukufu, anatufahamisha juu ya umuhimu wa jihadi katika njia yake, na kwamba kwa kufanya hivyo pekee ndiko kutatuepusha na adhabu yake siku ya hesabu. Kwamba lazima dini ipiganiwe, na hao watakaofanya hivyo basi atawalipa Pepo, kinyume chake atawatia motoni. Hivyo ndugu zanguni katika imani jihadi ni jambo la lazima, na ni lazima tulifanye tutake tusitake maadam tumekuwa ni waumini.

Aya h iz i t a tu n i l i zo zitanguliza ndizo zitakuwa msingi wa makala hii ya leo. Kwamba tunapaswa au tunawajibu au ni faradhi kwetu kujitoa muhanga kwa ajili ya kuihami dini ya Mungu, na kuihami dini maana yake ni kumhami Mtume SAW na viongozi wetu, wale ambao sisi wenyewe t u m e a m u a k u w a w e k a mbele ili watuongoze katika

mapambao ya kuipigania dini hii ya Mwenyezi Mungu.

Sasa jambo kubwa kuliko yote hapa ndugu yangu katika imani ni mimi na wewe kujiuliza je nafsi zetu ziko tayari kufa kwa ajili ya kumhami Mtume SAW na viongozi wetu katika dini. Umar Ibn Khatab (RA) alimwambia wazi Mtume kwamba bado kwanza. Lakini imani ilipokaa sawa akamfuata Mtume na kumwambia yuko tayari. Na hapo ndipo Mtume SAW alipomwambia sasa umeamini. Je mimi na wewe msomaji nafsi zetu ziko tayari katika hili, au nasi bado bado kwanza? Kama bado bado kwanza, kwa mujibu wa Mtume, sisi imani haijakaa bado katika vifua vyetu.

Je, nini faida ya kuwahami vingozi wetu kwa nafsi zetu? Rejea kidogo katika k i n d u m b w e n d u m b w e kinachoendelea duniani kote hivi sasa baada ya kutengenezwa kwa filamu inayomdhalilisha Mtukufu wa daraja Mtume Muhamad SAW. Waislamu dunia nzima tumeonesha hasira zetu na kwamba tuko tayari kulinda heshma ya Mtume wa Mungu. Kila atayetaka kujaribu tena upuuzi huu atakuwa na kumbukumbu nzuri kuwa jambo hilo halita pita kimya kimya, bali litakabliana na upinzani mzito toka kwa waislam dunia nzima.

Tukirejea hapa kwetu Tanzania, alhamdulillah, nuru imenza tena kufunguka na sasa imekuja katika sura bora zaidi; kwanza ni kule kuwaleta pamoja Masheikh tunaowajua kuwa hawa ni viongozi wetu

tangu zamani na pili ni jinsi waislamu kwa umoja wetu tunavyowaitikia wakituita. Kumbuka kuwa pamoja na kuwepo kuandikisha sensa kwa ku laz imishana na kutishana na maeneo mengine chini mtutu wa bunduki, bado tulitii amri ya viongiozi wetu ya kutoshiriki sensa ya mwaka 2012. Au angalia jinsi maandamano yale ya kuelekea Wizara ya Mambo Ndani kushinikiza kuachiliwa huru kwa Waislamu waliokuwa wamezuiliwa kolokoloni kwa kukataa kuhesabiwa, yalivyoitikiwa na watu wengi. Aidha angalia jinsi uwanja wa Kidongo Chekundu ulivyojaa Waislamu, tena basi kwa taarifa za muda mfupi tu, wakati walipomiminika katika uwanja hu kuwalaani w a l e w a l i o t e n g e n e z a na kuisambaza filamu ya kumdhalilisha kipenzi chetu Mtume Muhammad SAW.

Hii ni namna ya kiwango cha juu sana ya kuwahami vingozi wetu. Viongozi wanapotuita tuzidishe kutoka kwa wingi twende tuwaitikie wito wao na wakituagiza ya kufanya tufanye kwa nguvu moja. Huku ndiko kuwahami vingozi wetu, na ninaamini kama tutaweza kufanya hivi basi tutaweza kuzitoa nafsi zetu kwa ajili yao. Kwanini? Kwasababu imani haingii mara moja ikaa kifuasni kwa mtu. Inaingia taratibu, rejea kisa cha Khaalifa Umar Ibn Khatab (RA) nilichokitanguliza mwanzo.

Tunapotoka kwa wingi kuwaitikia viongozi wetu, maadui wanapata picha ya

nguvu walizonazo viongozi w e t u . Wa n a j u a k u w a tukiwavunjia heshma hawa, basi kuna watu nyuma yao watapinga na watapambana. Hata kamata kamata ya m a s h e i k h p a l e p o l i s i wanapojisikia tu kufanya h ivyo i tapotea kabisa . Ule uhuni aliyofanyiwa Sheikh Nurdin Kishiki kwa kugaragazwa chini na Polisi utakoma. Yale makusudio ya kutaka kumuua Sheikh Farid kwa kumiminia risasi gari yake hayataweza kurejewa tena. Upuuzi wa kuwaita Polisi viongozi wa Waislamu n a k u w a h o j i u t a k u w a his tor ia . Watawafanyia heshma viongozi wetu na kuwachukulia kwa tahadhari kubwa.

K w a w a l i o a n g a l i a maandamano yaliyoitishwa na Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hizbullah, katika jiji la Beirut nchini Lebabon, waliona nguvu ya kiongozi huyu aliye mwiba kwa Mayahudi na Marekani. Maandamano yale yalihudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Waislamu bila kujali wao ni Shia au Sunni. Unadhani Nasrallah anagusika tu hovyo hovyo? Hapana, kwasababu ana watu nyuma yake, waliotayari kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kiongozi wao. Hizbullah c h i n i y a u o n g o z i w a Nasrallah ililisambaratisha jeshi la Israel katika vita ya mwaka 2006, mpaka kupelekea kujiuzulu kwa Waziri wa Ulinzi wa taifa hilo la kizayuni. Msimamo wake ni kuwa Hizbullah haiwezi kukabidhi silaha mpaka hapo itakapoona kuwa Lebanon ina jeshi la kuweza kuilinda nchi, vinginevyo Hizbullah itendelea kuilinda Lebanon. Msimamo huo unajulikana na Marekani na washirika wake, mbona hawamgusi! Wanajua kuwa kumgusa ni kutupia njiti ya kibiriti iliyowashwa katika dibwi la petroli. Nasi lazima tuwape nguvu masheikh wetu wa pande zote mbili Zanzibar na Bara. Na kwamba mshikamano wetu ndio nguvu zetu na ndio nguvu ya kuwahami viongozi wetu. La Bara ndiyo liwe la Zanzibar na la Zanzibar ndiyo liwe la Bara, Inshaallah tutawashinda.

Tuk iwa na v iongoz i tuliyowatanguliza mbele huku tukiwahami na kama t u k i w a t a y a r i k u j i t o a muhanga nafsi zetu kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu, upuuzi u le u l iofanywa pale Sekondari ya Ndanda usingefanyika. Wala upuuzi ule wa kuwafelisha kusudi watoto wa Kiislamu pale Baraza la Mitihani la Taifa, NECTA, usingeendelea.

Page 15: ANNUUR 1037

15 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012HABARI

Vurugu za kisiasa zaipokonya Chadema wanachama Arusha

Inatoka Uk. 1

Bw. John Bayo.Bw. Bayo, amekihama

chama hicho sambamba na wanachama wengine kutoka vyama vya CHADEMA na CCM, ambao kwa pamoja walikabidhi kadi kwa Mwenyekiti wa CUF, Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba.

P r o f e s a L i p u m b a , pia amempokea Kasim C o r l i n , a n a y e d a i w a kuwa aliyekuwa mdau na mpambe mkubwa wa karibu wa Godbless Lema, aliyevuliwa Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA), pamoja na mjane wa Ismail Omari aliyeuwawa na Polisi katika vurugu za maandamano ya CHADEMA, yaliyozuiliwa na Polisi Jijini humo, Januari mwaka 2011.

Akizungungumza mbele ya umati wa watu, mara baada ya kupokea kadi ya Chama chake kipya cha CUF, Bw. Bayo, alisema amelazimika kukihama chama chake kutokana na kuweka mbele masuala ya ubabe na maandamano

“ K u n a v i o n g o z i ndani ya CHADEMA, bila vurugu na kuitisha maandamano hadhani kuwa siasa zinawezekana, hali hiyo ni hatari kwa

jamii na hayapendezi name nimeamua kuhama.” Alisema Bw. Bayo.

A m a k w a u p a n d e wa mjane wa muhanga w a m a a n d a m a n o y a CHADEMA, Bi. Asia, alisema ameamua kujiunga na CUF, baada ya kutengwa pamoja na kupewa ahadi hewa za kusaidiwa na viongozi wa Chama kilicho itisha maandamano, na kusababisha kifo cha mumewe.

A k i w a k a r i b i s h a wananchama hao wapya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Bw. Salim Bimani, alisema msingi na dhana ya CUF, ni kusimamia siasa za kistarabu, pamoja na haki za msingi za maisha ya wananchi.

Alisema, Chama cha siasa ambacho viongozi wake wanatumia nguvu katika kusimamia itikadi zao, ni dhahiri viongozi hao huwa hawana busara.

“Huwezi kusimamia vurugu hata kwa jambo a m b a l o l i n a w e z a kuzungumzika wakati wanaoathi r ika kat ika vurugu hizio ni wananchi, na viongozi wa namana hiyo lazima wati l iwe mashaka.” Alisema Bw. Biman.

Akiwahutubia wakazi wa Jiji la Arusha, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba, alisema Tanzania inahitaji kuwa na viongozi wenye dira watakaoweza kuzitumia rasilimali za nchi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Profesa Lipumba ametoa changamoto hiyo katika viwanja vya Levolosi Jijini Arusha mapema wiki hii, alipokuwa akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho, ikiwa ni sehemu ya ‘Operesheni Mchakamchaka had i 2015’.

O p e r e s h e n i h i y o ilizinduliwa Septemba 9, mwaka huu Jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Jangwani ambayo imekusudiwa kuzunguka katika mikoa mbali mbali nchini, chini ya viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho.

P r o f e s a L i p u m b a , a m e s e m a Ta n z a n i a ime jaa l iwa kuwa na rasilimali nyingi zikiwemo jiografia yake, Bahari na Madini ambazo bado h a z i j a t u m i k a v i z u r i kuwanufaisha Watanzania wanaoendelea kuishi katika hali ngumu ya maisha.

Akinukuu jar ida la

Kimataifa, liitwalo Finance Time, Profesa Lipumba, alisema jarida hilo limeitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi pekee yenye vivutio vingi vya utalii na mtu a n a w e z a k u p u m z i k a kutokana na mandahari na vivutio vyake.

“Tunahitaji viongozi wenye dira watakaoweza kuzisimamia rasilimali za Watanzania kwa maslahi ya Watanzania wenyewe”, alisema Profesa Lipumba na kuongeza,

“ W a t a n z a n i a tumeshindwa kuzitumia ras i l imal i tu l izonazo kwa maendeleo yetu, tunayo mazao mengi ya mboga mboga, tunayo madini mengi, bandari na kadhalika ambazo zote hizi zikitumika vizuri tunaweza kujikwamua kiuchumi”.

Alifahamisha kuwa, Watanzania wanahitaji k u j i p a n g a k u l e t a mabadiliko ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali z i l i z o p o p a m o j a n a maendeleo ya teknolojia, na kwamba iwapo kutakuwa na mipango imara ni wazi kila Mtanzania anaweza kunufaika moja kwa moja na rasilimali za nchi.

P r o f e s a L i p u m b a , aliye bingwa wa Uchumi duniani, aliwachambulia wakazi wa Jiji la Arusha u ta j i r i unaoizunguka Tanzania kuwa ni pamoja na vivutio vya utal i i vikiwemo milima mikubwa kama vile Kilimanjaro na Meru, Visiwa vya Zanzibar pamoja na rasilimali za mafuta na gesi.

Vyote hivyo Profesa L i p u m b a , a l i s e m a vikisimamiwa vizuri ni vyanzo vizuri vya kuinua Uchumi wa mwananchi na Taifa kwa ujumla na kumuwezesha mtanzania kuondokana na umasikini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CUF M a a l i m S e i f S h a r i f Hamad aliwashangaa wale wanaobeza maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa Zanzibar, na kwamba maridhiano hayo yalikuwa ni maamuzi ya Wazanzibari w e n y e w e n a h a i f a i kuyabeza.

Alisema, maridhiano h a y o y a l i y o p e l e k e a kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, yameifanya Zanzibar kuwa mfano wa kuigwa kwa Tanzania na nchi nyingine

za Afrika Mashariki.“Chama Cha CUF kina

malengo ya kuwaunganisha Watanzania wote na ni chemchem ya amani , s i o k a m a v y a m a vingine vyenye sera za maandamano, kususa na migomo pamoja na sera za kibaguzi (Majimbo)”, alisema Maalim Seif na kuongeza,

“Siasa si lelemama wala si vurugu, bali viongozi wa kisiasa wanatakiwa washindane kwa hoja sio kuwabagua wananchi kwa misingi ya udini na ukabila au ukanda na wajue kuwa hili linavuruga umoja wa Kitaifa, ambao CUF ndio msingi wake mkuu”. Alisema.

Aliwashukuru wananchi wa Arusha kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wao kusikiliza sera za CUF, na kwamba kuanzia sasa Chama kitajikita katika Mkoa huo kuhakikisha kuwa k inawakomboa wananchi wa eneo hilo kwa siasa za kistaarabu.

“Nasema hakuna mtu wala chama chenye hati miliki ya Mkoa huu, bali Mkoa huu ni wa wananchi wote wa Arusha, na kuanzia sasa tutajikita kisiasa katika mkoa huu hadi kieleweke”, alibainisha Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Maalim Seif, aliwasihi wananchi wa Arusha kuwa makini na propaganda zinazoenzwa dhidi ya chama hicho na kwamba propaganda hizo lengo lake ni kuwagawa Watanzania badala ya kuwaunganisha.

Mapema, akisoma risala ya wanachama wa CUF mbele ya viongozi wakuu wa CUF, Katibu wa Chama hicho Wilaya, Bw. Hassan Zakaria Zani, alisema wananchi wa Arusha wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za Kiuchumi, ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na siasa za vurugu.

M k u t a n o h u o p i a u l i h u d h u r i w a n a kuhutubiwa na viongozi kadhaa wa CUF wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa Machano Khamis Ali na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, Julius Mtatiro.

Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Page 16: ANNUUR 1037

16 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012

V U R U G U n a M a a n d a m a n o y a n a y o d a i w a k u s i m a m i w a n a viongozi wa Chama Cha CHADEMA nchini, yameanza kutoa taswira mpya, baada ya baadhi ya wafuasi wake kuanza kukihama chama hicho, wakidai kuchoshwa na mwenendo huo.

Hali hiyo imejidhihirisha katika mkutano mkubwa wa hadhara wa Chama Cha Wananchi (CUF), u l i o f a n y i k a k a t i k a viwanja vya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita, na kuhutubiwa na viongozi wa Kitaifa wa Chama hicho.

Wa k a t i h u o h u o , Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, ametoa somo kwa vyama vya siasa vinavyodhani kuwa siasa ni maandamano na vurugu huku akiwataka warejee somo la siasa za vyama vingi.

Kwa mujibu wa mpasha habar i wetu a l iyeko Jijini Arusha, Maalim Seif ameyasema hayo wakati akishiriki katika operesheni ya CUF ya ‘Mchakamchaka hadi 2015, Jijini humo, ambapo chama hicho kimevuna wanachama kutoka baadhi ya vyama vya siasa na kupa ta wananchama wapya.

Katika mkutano huo Prof. Lipumba alimkabidhi kadi ya CUF aliyekuwa Diwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Ererai Mkoani Arusha

Vurugu za kisiasa zaipokonya Chadema wanachama Arusha

Maalim Seif ampa Slaa somo la vyamaAwaponda wanaobeza umoja Zanzibar

Na Bakari Mwakangwale

“KWELI nimeamini kabla hujafa hujaumbika, kwa hatua hii sina cha kufanya zaidi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani kuwa kilema si ugonjwa.”

Hii ni moja ya kauli ya Mama Hussein ambaye ni mkazi ya mjini Bagamoyo.

Mama huyu hivi karibuni alipata mtihani wa kukatwa mkono wake wa kul ia uliosababishwa na mwiba wa samaki uliomchoma katika kidole chake cha mkono.

Akiongea na mwandishi wetu akiwa amelazwa wodini katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo, Mama Hussein amesema kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Mama Hussein ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo amesema siku moja akiwa katika harakati za biashara zake kwa bahati mbaya alichomwa na mwiba wa samaki ambao ulikatikia kwa ndani.

L a k i n i k a d i r i s i k u z inavyokwenda mkono wake ukawa kama anapooza ndipo alipotoa taarifa kwenye kliniki yake ya kisukari, madak t a r i wakashau r i ahamishiwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya uchunguzi ikabainika kuwa kutokana na hali ya kisukari alichonacho mwilini, analazimika kukatwa mkono wote kwani sumu yake ilikuwa imeshasambaa sehemu kubwa ya mkono wake.

Hivi sasa Mama huyo anauguza kidonda katika hospitali ya Bagamoyo akiwa hana mkono mmoja kuanzia begani.

Mwiba wa samaki wasababisha akatwe mkono

Na Mwandishi Wetu

Inaendelea Uk. 15

Usikose nakala yako ya

AN-NUUR kila Ijumaa

LABAIKAH LLAHUMA LABAIKA!

Soma habari kamili Uk. 2 , 6 & 9

Wanachama na wapezi wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita.