16
MAONESHO YA KWANZA (1) YA KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA Taarifa ya Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika Tarehe 16 23 Novemba 2014, Viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam, Tanzania Afrika Mashariki JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LTD Imeandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Ltd S.L.P 90447 Dar es Salaam, Tanzania. Simu ya Mkononi: + 255756147487 Barua pepe: [email protected]

Ripoti Ya Maonesho Ya Tiba 2014 (1)

Embed Size (px)

DESCRIPTION

TAARIFA YA MAONESHA YA KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA

Citation preview

  • MAONESHO YA KWANZA (1) YA

    KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA

    Taarifa ya Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya

    Mwafrika Tarehe 16 23 Novemba 2014, Viwanja vya

    Mnazi mmoja Dar es Salaam, Tanzania Afrika Mashariki

    JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LTD

    Imeandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Ltd

    S.L.P 90447

    Dar es Salaam, Tanzania.

    Simu ya Mkononi: + 255756147487

    Barua pepe: [email protected]

  • 1

    Yaliyomo.

    uk

    1.0 UTANGULIZI ................................................................................................................................. 2

    2.0 MALENGO MAKUU YA MAONESHO ..................................................................................... 4

    3.0 MAANDALIZI YA MAONESHO ...................................................................................................... 6

    3.1 Uhamasishaji wa Ushiriki ................................................................................................................... 7

    3.2 Uchapishaji wa Majarida na Mabango ya Kunadi Maonesho .......................................................... 8

    3.3 Uundwaji wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi .................................................................................. 8

    4.0 UDHAMINI WA MAONESHO .................................................................................................... 9

    5.0 WASHIRIKI WA MAONESHO ................................................................................................. 10

    6.0 ULINZI NA USALAMA WAKATI WA MAONESHO ............................................................ 10

    6.1 VIONGOZI NA WAGENI MASHUHURI WALIOTEMBELEA MAONESHO ........................................... 10

    7.0 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE ............................................................................... 11

    8.0 WALIOCHANGIA MAFANIKIO YA MAONESHO .............................................................. 12

    9.0 KUFUNGA .................................................................................................................................... 13

    10.0 HITIMISHO .................................................................................................................................. 14

    Kiambata:....Ripoti ya fedha

  • 2

    JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LIMITED

    RIPOTI YA MAONESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA

    TIBA ASILI YA MWAFRIKA, 2014

    1.0 UTANGULIZI

    Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yalifanyika

    katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, vilivyopo kwenye Manispaa ya Ilala

    Mkoani Dar es Salaam, Tanzania kuanzia tarehe 16 23 Novemba, 2014.

    Lengo lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano wa huduma ya Tiba Asali na Tiba

    ya kisasa katika kuimarisha huduma ya Afya ili kuleta Maendeleo endelevu

    na kutengeneza mtandao wa huduma ya Tiba Asili, Kutoa Elimu kwa Umma

    kuhusu Tiba Asili, Utafiti na uboreshaji wa dawa Asili kwa kuzingatia sera,

    Sheria, kanuni na miongozo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala na kuyafanya

    Maonesho haya kuwa ya Kimataifa na kufanyika kila mwaka.

    Maonesho yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Novemba, 2014 na Mheshimiwa

    Dkt Seif Seleman Rashid (Mb), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

    akiwakilishwa na Ndugu Dunford Makala, Kamishna wa Ustawi wa Jamii

    Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii. Pamoja naye alikuwepo Dr Liggyle

    Vumilia, Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

    Wageni wengine walioambatana na Mgeni Rasmi walikuwa kama ifuatavyo:

    Bi Lucy Samweli, Mfamasia wa Idara ya Tiba, sehemu ya Tiba Asili na Tiba

    Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Gertrude Ngweshemi,

    Afisa Mwandamizi Ukuzaji Masoko na Huduma za Ukuzaji Biashara toka

    Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na wageni

    wengine waalikwa. Mgeni Rasmi alipata fursa ya kutembelea mabanda ya

  • 3

    washiriki wa Maonesho na kupata maelezo kuhusu dawa, bidhaa, huduma na

    matibabu mbalimbali yanayotolewa na Washiriki wa Maonesho hayo.

    Baada ya hapo ndugu Boniventura Mwalongo Mwenyekiti wa Kamati ya

    Maandalizi alisoma Ujumbe wa Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba

    Asili ya Mwafrika. Katika ujumbe wake Mwenyekiti alimkaribisha Mgeni

    rasmi, wageni waalikwa na washiriki wa Maonesho katika maonesho haya

    muhimu ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika ambayo yalifanyika kwa

    mara ya kwanza hapa nchini.Nakufanya kuwa tukio la kihistoria katika nchi

    yetu, Pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa

    Maonesho hayo.Kisha akamkaribisha Mgeni rasimi, kwa hotuba ya ufunguzi,

    Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwanza alitoashukrani kwa kuwa

    mgeni rasmi wa kwanza wa Maonesho haya Makubwa ya Biashara ya

    Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika ambayo yamefanyika kwa mara ya

    kwanza hapa nchini kwetu. Katika hotuba yake alipongeza Jukwaa la Tiba

    Asilia Tanzania kwa kuanzisha Maonesho ya Tiba Asili ambayo yataleta

    Manufaa makubwa kwenye sekta ya Afya ikizingatiwa kuwa Tiba Asilia

    husaidia wananchi wengi Mijini na Vijijini, alitoa rai kwa Jukwaa la Tiba

    Asilia Tanzania kuyaendeleza Maonesho haya kufikia kiwango cha Kimatifa

    na kuyafanya Maonesho hayo kila Mwaka.Na aliwataka washiriki kutumia

    fursa nzuri waliyoipata kubadilishana uzoefu kutoka kwa washiriki wanje ya

    nchi na Aliwaambia wananchi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya na

    Ustawi wa Jamii inaitambua huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala.

    Pia alitoa pongezi kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara

    Tanzania,(TanTrade) kwa kutambua umuhimu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala

    hapa nchini na kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha maonesho

    haya ya Kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yanafanyika katika

  • 4

    ngazi za Kimataifa kwa kutumia utaalam walionao. Pia aliahidi kuwa Wizara

    ya Afya na Ustawi wa Jamii iko tayari kutoa ushirikiano thabiti ili

    maonesho haya yafanyike sambamba na maadhimisho ya siku ya Tiba Asili

    ya Mwafrika na kushirikisha wadau wengine.

    Aidha aligusia changamoto zilizopo katika Tiba Asili,na kwamba Serikali

    inasisitiza waganga na watoa huduma wote wa Tiba Asili na Tiba Mbadala

    kufuata sheria Na. 23 ya mwaka 2002 kama usajili wa waganga na vituo

    vyao, kutojihusisha na Uzuzaji, Uchawi, ushirikina na upigaji wa ramli, vile

    vile na matangazo ya kwenye redio, Televisheni na magazeti pamoja na

    uwekaji wa mabango barabarani.

    Kauli Mbiu ya Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya mwafrika

    Mwaka 2014 ilikuwa Kuimarisha Ushirikiano wa Tiba Asili na Tiba ya

    Kisasa katika Kuimarisha Huduma ya Afya Afrika, Kauli Mbiu hii

    ilichaguliwa Mahsusi ili kuhamasisha uboreshaji wa huduma ya Tiba Asili na

    kuziingiza Dawa za Asili kwenye utoaji wa huduma za Afya ili kuleta

    maendeleo endelevu katika sekta ya Afya nchini Tanzania.

    2.0 MALENGO MAKUU YA MAONESHO

    Lengo kuu la Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asilia ya

    Mwafrika ni kuhamasisha uboreshaji na uendelezaji wa utoaji huduma ya

    Tiba Asili katika Sekta ya Afya kwa kuzitangaza, kuboresha na kuziingiza

    dawa za asili kwenye mfumo wa kisasa wa utoaji huduma za Afya na kutoa

    Elimu kwa umma kuhusu Tiba Asili na Utafiti kwa kuzingatia Sera, Sheria,

    Kanuni na Miongozo ili kuleta maendeleo endelevu katika Sekta ya Afya

    nchini, Afrika na duniani kwa ujumla.

  • 5

    Maonesho ya Kimataifa ya Tiba Asili yalilenga kutoa fursa zifuatazo:-

    i. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kuwa Jukwaa la kuwawezesha

    Washiriki wa maonesho ya kwanza kuimarisha ushirikiano wa Tiba

    Asili na Tiba ya kisasa, na Watowa huduma wa Tiba Asili, Watafiti

    wa dawa Asili, Wavumbuzi, Wasindikaji wa Dawa Asilia kuonesha

    bidhaa na huduma wanazotoa kwa jamii.

    ii. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa jukwaa la kuunganisha pamoja

    Asasi, Taasisi, Kampuni, na Watu kutoka nchi mbalimbali kukutana

    na kufahamiana kwa lengo la kutengeneza mitandao ya Kibiashara,

    kujifunza, kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kimaendeleo

    katika Tiba Asilia kwa lengo la kuboresha huduma ya afya.

    iii. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kuwa jukwaa la Kutoa taarifa sahihi

    kuhusu umuhimu wa TIBA ASILI NA TIBA MBADALAili

    kubadilisha mtazamo wenye kasumba potofu uliotokana na

    kutawaliwa na wakoloni na ukoloni mamboleo ambao umesinyaza

    Tiba Asili na kuhusishwa na Imani za kichawi na Ushirikina hivyo

    kupelekea kudharauliwa kwa watabibu wa Tiba Asili. hivyo

    maonesho yanatusaidia kubadilisha na kupanua wigo wa ufahamu

    katika taaluma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala

    iv. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa Jukwaa la kukutanisha watoa na

    wapokea huduma , wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za Asili jambo

    litakalowezesha Washiriki wa Maonesho kupata mrejesho wa moja

    kwa moja kutoka kwa watumiaji huduma na bidhaa (wahitaji) wao

    kuhusu maoni na mtazamo wao kutokana na huduma na bidhaa

    wanazozitoa. Jambo hili litamsaidia mzalishaji au mtoa huduma kujua

  • 6

    ni wapi panahitaji marekebisho na maboresho katika kutoa huduma au

    bidhaa zake kwa Jamii.

    v. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa Jukwaa la Kujenga mtandao wa

    ushirikiano na kupeana ujuzi mbalimbali kwa kuwa kila mmoja ana

    ujuzi wa pekee ambapo kwa pamoja yatapatikana matokeo yenye

    ufanisi na Kuchochea fursa za Utafiti wa maendeleo.

    3.0 MAANDALIZI YA MAONESHO Maandalizi ya Maonesho yalifanyika chini ya uratibu wa Jukwaa la Tiba

    Asilia Tanzania ambapo Vikao vinne (4) vya Maandalizi vilifanyika. Vikao

    hivyo ni:

    Kikao cha Kwanza

    Kikao cha Mkutano Mkuu chenye wajumbe 56 kutoka katika vyama 12 vya

    Watabibu wa Tiba Asili. Kikao hiki kilijadili masuala ya kuandikisha

    Jukwaa la Tiba Asili kisheria, na kuweka bayana maandalizi ya Maonesho

    ya Tiba Asilia ya Mwafrika.

    Kikao cha Pili

    Kikao cha pili kilikuwa cha wajumbe 20, katika vyama 12 vya Tiba asili kila

    chama kilitoa mjumbe mmoja na wajumbe 8 kutoka Kamati Kuu. Kikao hiki

    kiliazimia kupanga utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano Mkuu,

    Kikao cha Tatu

    Kikao cha tatu kilikuwa na wajumbe 11 kikiwa na dhumuni la kufuatilia na

    kufanikisha maazimio ya vikao vyote vya juu na kutekeleza maazimio hayo.

    Kikao cha Nne

    Kikao cha nne kilikuwa cha ushirikiano wa wataalam kutoka Jukwaa la Tiba

    Asili Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Mamlaka ya

    Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambacho pamoja na maazimio

  • 7

    mengine kiliwachagua viongozi wa kamati ya wataalam kwa maandalizi ya

    Maonesho ambapo Boniventura Mwalongo aliyekuwa Mratibu Jukwaa la

    Tiba Asili Tanzania alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya

    Maandalizi ya Maonesho, Bi Lucy Samweli Mfamasia wa Idara ya Tiba,

    sehemu ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

    alichaguliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho na Bi

    Gertrude Ngweshemi Afisa Mwandamizi, Ukuzaji Masoko, na Huduma za

    Ukuzaji Biashara toka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

    (TANTRADE) alichaguliwa kuwa Mhazini wa kamati ya Maandalizi ya

    Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika. Maazimio

    mengine yalikuwa kuandaa bajeti ya maonesho, Mawasiliano pamoja na

    kutoa Utaalamu katika kufanikisha Maonesho ya Kwanza ya kimataifa ya

    Tiba Asili ya Mwafrika, kuyasajiri na kuyaingiza katika kalenda ya

    Maonesho nchini.

    KATIKA MAANDALIZI, MAMBO YAFUATAYO YALIFANYIKA;

    3.1 Uhamasishaji wa Ushiriki Maandalizi yalianza kwa uhamasishaji wa Serikali na Taasisi zake,

    Taasisi za Kimataifa, Asasi za Kijamii na Kimataifa, pamoja na wadau

    kushiriki katika Maonesho hayo. Mbinu zilizotumika kuhamasisha ni

    pamoja na kufanya kampeni ya mlango kwa mlango (door to door) kwa

    kuyatembelea makampuni mbali mbali, Jumuiya zao na Balozi za nchi

    za nje zilizopo Tanzania, kuwasiliana na Balozi za Tanzania zilizo nchi

    za nje, kutuma barua pepe na barua za kawaida za mialiko pamoja na

    kutumia vyombo vya habari. Hata hivyo, matokeo ya uhamasishaji

  • 8

    hayakuwa na matunda tarajiwa kwakuwa maandalizi yamefanyika katika

    muda mfupi sana.

    Aidha, iliandaliwa kampeni ya matangazo kupitia mitandao ya Kijamii

    na vyombo mbalimbali vya habari kwa kushirikiana na makampuni

    mengine yaliyoshiriki katika Maonesho. Wawakilishi mbalimbali

    walikwenda kwenye vituo vya televisheni na redio na kutoa taarifa na

    maelezo kuhusiana na Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba asili

    na Tiba mbadala.

    3.2 Uchapishaji wa Majarida na Mabango ya Kunadi Maonesho Ili kuimarisha utoaji taarifa za Maonesho hayo kwa umma majarida,

    vipeperushi na mabango (Promotional Material) ya kunadi Maonesho

    yaliandaliwa na kuchapishwa.

    3.3 Uundwaji wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi Kamati ya Kitaifa iliundwa ikijumuisha Mjumbe kutoka Jukwaa la Tiba

    Asili Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na TanTrade

    ambapo Boniventura Mwalongo Mratibu Jukwaa la Tiba Asili Tanzania

    alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho,

    Bi Lucy Samweli Mfamasia wa Idara ya Tiba, sehemu ya Tiba Asili na

    Tiba Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii alichaguliwa kuwa

    Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho na Bi Gertrude

    Ngweshemi Afisa Mwandamizi, Ukuzaji Masoko, na Huduma za

    Ukuzaji Biashara toka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

    (TANTRADE) alichaguliwa kuwa Mhazini wa kamati ya Maandalizi ya

    Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika kwa ajili

    ya zoezi zima la kuratibu, kusimamia na kuandaa taratibu zote za

    Maonesho ili kuhakikisha kuwa maandalizi yanakwenda ipasavyo na

  • 9

    yanakuwa shirikishi. Kamati hii ilifanya kazi kutokana na maazimio

    yaliyotolewa na Mkutano Mkuu pamoja na Kamati Kuu.

    4.0 UDHAMINI WA MAONESHO

    Wadhamini na Wafadhili mbalimbali walijitokeza kuunga mkono Maonesho

    ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika, udhamini huo ulichangia

    kwa kiasi kikubwa kufanikisha Maonesho hayo. Ufadhili huu ulitolewa na

    Wadau wafutao: - (Wilfred Jumanne Mwazini) kutoka Kituo cha Huduma ya

    Uponyaji, JKBRS International, Boresa Traditional Medicine Company

    Limited, Adulkharim Mambo Saleh na Cocacola Kwanza Limited. TanTrade

    pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zilitoa ufadhili wa utaalam

    (technical assistance).

    Picha za matukio mbalimbali

    zikionyesha sehemu ya ufungaji wa

    maonesho. Ndugu Simba A . Simba

    muwakilishi wa mgeni rasmi katika

    kufunga maonesho ya Kwanza ya

    Kimataifa ya Tiba Asili ya mwafrika

    akiwa na Viongozi mbalimbali wa

    jukwaa la Tiba Asili Tanzania.

  • 10

    5.0 WASHIRIKI WA MAONESHO

    Jumla ya washiriki 58 walishiriki katika Maonesho ya Tiba Asili ya

    Mwafrika hii ikiwa ni pungufu kulinganisha na matarajio ya kamati ya

    maandalizi ambapo kamati ilitarajia kuwa na washiriki wapatao 100.

    Upungufu huu ulitokana muda mfupi wa maandalizi ingawa juhudi za ziada

    za kuhamasisha zilizofanyika. Washiriki walikuwa ni pamoja na Watabibu

    wa Tiba Asili, watengenezaji wa Dawa Asili,Wakunga wa Tiba Asili,

    Kampuni za Dawa Asili na Vipodozi vya Dawa Asili, Wasambazaji wa

    Vifaa Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa Vyakula Asili, Kliniki

    za Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na kazi za mikono(sanaa).

    6.0 ULINZI NA USALAMA WAKATI WA MAONESHO

    Masuala ya Ulinzi, Usalama yalisimamiwa na Jeshi la Polisi kwa

    kushirikiana na Walinzi wa MG Manispaa ya Ilala ambao walilipwa malipo

    kwa siku.

    6.1 VIONGOZI NA WAGENI MASHUHURI WALIOTEMBELEA

    MAONESHO.

    Baadhi ya Viongozi na Wageni Mashuhuri waliotembelea Maonesho ni

    kama wafuatao: -

    i. Nd. Dunford Makala Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizara ya

    Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye alimwakilisha Mgeni Rasmi Mhe.

    Dkt Seif Seleman Rashidi (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

    katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho.

    ii. Dr Liggyle Vumilia, Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya na

    Ustawi wa Jamii.

  • 11

    iii. Nd. Masalida Zephania, Afisa Maendeleo ya vijana kutoka Ofisi ya

    mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam.

    iv. Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru, aliyekuwa Mjumbe wa Bunge

    Maalum la Katiba aliwakilisha Tiba Asili na Mlezi wa Tiba Asili.

    v. Nd Josephat Rweyemam Mwenyekiti wa CISO Afrika Mashariki.

    vi. Eng. Armin Zedlitschka kutoka Ujerumani na

    vii. Eng. Siliwat Jodelist kutoka Ujerumani.

    viii. Ndugu Simba Abdulrahman Simba Tabibu Asili aliyemuwakilisha

    Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb)

    katika kufunga Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya

    Mwafrika.

    7.0 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE

    Yafuatayo ni mapungufu yaliyojitokeza katika maandalizi na usimamizi wa

    Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika na hatua za

    ufumbuzi wake;

    7.1 Kulikuwa na mwitikio mdogo wa washiriki hivyo kupelekea Maonesho

    kuhudhuriwa na washiriki wachache sana kinyume cha matarajio.

    Washiriki hawakuwa na uelewa wa umuhimu wa kushiriki Maonesho

    kwa ajili ya kutangaza bidhaa na huduma zao. Hii inatokana na ukweli

    kuwa, maandalizi ya Maonesho yalifanyika kwa muda mfupi sana, hivyo

    mawasiliano hayakuwafikia walengwa wengi katika muda muafaka.

    Katika Maonesho ya mwaka huu 2015 Kamati ya Maandalizi

    inashauriwa kuanza maandalizi mapema na taarifa itolewe kwa washiriki

    kuhusu umuhimu wa kushiriki katika Maonesho kama njia muhimu ya

    kutangaza bidhaa na huduma zao pamoja na manufaa mengine.

  • 12

    7.2 Mahudhurio ya watembeleaji hayakuwa yakuridhisha kutokana na

    Maonesho kutofanyiwa matangazo mapema. Matangazo yaliyofanyika

    yalifanyika katika muda mfupi na hiyo haikutosha kuwafikia

    watembeleaji wa kutosha. Maonesho yajayo Kamati ya Maandalizi

    inashauriwa ihakikishe matangazo yanafanyika mapema ili kuwafikia

    wananchi wengi.

    7.3 Jukwaa la Tiba Asili Tanzania liweke nguvu katika kujitangaza, kuwa na

    machapisho yanayoelimisha na kuendana na wakati na yenye ubora wa

    kuvutia matumizi bora na salama ya Tiba Asili na Dawa Asili. Mikakati

    ifanyike ya kutoa elimu kwa wananchi na wadau Tanzania kuhusu

    shughuli za Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa kupitia machapisho, radio,

    television, magazeti na midahalo mbalimbali. Watanzania na Ulimwengu

    wanahitaji kupata uelewa kwa kuwa kwa sasa wanaichukulia Tiba Asili

    ni ushirikina, ulamari, na uchawi na hivyo imesababisha baadhi ya watu

    waichukie na kutoipa kipaumbele.

    8.0 WALIOCHANGIA MAFANIKIO YA MAONESHO

    Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Limited tunatoa shukrani za dhati kwa

    Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Viwanda na Biashara,

    Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ofisi ya Mkuu

    wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi

    mbalimbali, Vyombo vya Habari, Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Idara ya

    Habari Maelezo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Bunge la Jamhuri ya

    Muungano wa Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, pamoja na

    Taasisi kutoka sekta ya Umma na sekta binafsi zilizochangia kufanikisha

    Maonesho haya.

  • 13

    Vilevile, kwa namna ya pekee Jukwaa linapenda kutambua mchango

    mkubwa wa Nd Wilfreid Jumanne Mwazini wa Kituo cha Huduma ya

    Uponyaji, JKBRS International, Boresa Traditional Medicine Company

    Limited, Tabibu Abdulkarim Mambo Saleh Tiba Asili za kisunah, Coca-

    Cola Kwanza Ltd waliodhamini shughuli mbalimbali za Maonesho.

    9.0 KUFUNGA

    Maonesho yalifungwa saa 11:30 jioni na Waziri wa Viwanda na Biashara

    Dkt. Abdallah O. Kigoda (MB) ambaye kutokana na sababu zilizo nje ya

    uwezo wake.Aliwakilishwa na Ndg. Simba Abdulrahman Simba Tabibu

    Asili na Mjumbe wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania, ambapo alipofika katika

    viwanja vya Maonesho alipokelewa na Uongozi wa Jukwaa na Mafisa wa

    Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya

    Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kisha alitembelea

    Ngoma ya Asili ya Wamakonde ya kikundi cha Mchabwede, na Mabanda ya

    washiriki, alipomaliza alikaribishwa Jukwaa kuu akapokea risala ya

    washiriki,Ujumbe wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania na

    Arafa ya Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho. Kwanza alitoa

    shukrani na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata fursa ya kipekee ya

    kumuwakilisha Mgeni rasmi kufunga Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya

    Tiba Asili ya Mwafrika, pili akawashukuru Viongozi wa Jukwaa la Tiba

    Asili Tanzania na Kumtakia kheri Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

    Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa akipata matibabu nchini

    Marekani ili apone haraka na kuendelea katika ujenzi wa Taifa, pia

    aliwataka washiriki wote kwenda kuboresha huduma na vituo vyao ili

    kuendelea kuiletea heshima huduma ya Tiba Asili na kuziingiza Dawa Asili

    kwenye utoaji wa huduma za Afya ili kuleta Maendeleo endelevu katika

    huduma za Afya nchini. Alitoapongezi kwa kuandaa Jukwaa la Tiba Asili

    Tanzania pia alitoapongezi kwa wadau waliohusika kwa maandalizi na

    ushiriki wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Mamlaka ya Maendeleo ya

    Biashara Tanzania (TANTRADE) kwaniaba ya Waziri wa Viwanda na

    Biashara. Aidha alisema kwamba ni matarajio yake kwamba Maonesho haya

    ambayo niyakwanza kufanyika nchini yatasajiliwa rasmi ili yaweze

    kufanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya siku ya Tiba Asili ya

    Mwafrika inayoadhimishwa 31 agosti kila mwaka katika nchi 46 barani

  • 14

    Afrika. Kwani yataleta tija kwa Watanzania hususani wadau wa Tiba Asili

    na Tiba Mbadala ambao wamekuwa na shahuku yakuona wanakuwa na

    maonesho kama haya na kuonesha bidhaa na huduma zao za Asili.

    Alisema hivyo kwa sababu pamoja na huduma ya Tiba Asili katika

    maonesho haya, pia kuna kazi za mikono ambazo zinawakilisha bidhaa asili

    za hapa nchini. Fursa nzuri na ya kipekee kabisa hivyo msisite kuitumia

    endapo itatokea tena hapo mwakani. Aliahidi , Wizara ya Viwanda na

    Biashara ipo tayari kutoa mchango wa hali na mali kuona Sekta hii inakuwa

    na kuboreshwa ipasavyo na hivyo kuhudumia soko la ndani, la kikanda na

    hata la kimataifa. Na aliwasilisha shukrani za Mhe Dkt. Abdallah O. kigoda

    (MB) kupata taarifa mapema kabisa na kuahidi Wizara itashirikiana na

    Jukwaa la Tiba Asili Tanzania ipasavyo hapo mwakani. Aidha amekubali

    ombi la kuwa Barozi wa Tiba Asili Tanzania, nakuomba kukutana na

    uongozi wa Jukwaa la Tiba Asili kupata ufafanuzi juu ya majukumu

    yanayoendana na Ubarozi wa Tiba Asili.

    Aidha alisema anatambua umuhimu wa Tiba Asili na changamoto zinazo

    ikabili Tiba Asili nchini. Na kuhimiza utoaji wa elimu endelevu kwa Umma

    kupitia machapisho, vyombo vya Habari, semina na Makongamano. Pia

    alilitaka Jukwaa la Tiba Asili kuitangaza Tanzania kimataifa kwa Tiba Asili

    nzuri tulizonazo.

    Kuhusu Viwanda vya kusindika dawa za Tiba Asili nchini vyenye kiwango

    cha kimataifa alisema nitawaomba viongozi wa Jukwaa watembelee Ofisini

    kwake ilikuongea zaidi juu ya maombi yote haya ikiwa nipamoja na

    kuchochea uwepo wa viwanda kwajili ya dawa Asili nchini.

    MWISHO

    Ndg Simba Ablahman Simba alifunga rasmi Maonesho ya kwanza ya

    kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika na aliahidi kufikisha risala,Arafa na

    Hotuba kwa Mhe. Dkt Abdallah O. Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.

    10.0 HITIMISHO Tunaomba kuwasilisha ripoti ya Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba

    Asili ya Mwafrika yaliyofanyika tarehe 16-23 Novemba 2014

    Kiambata Ripoti ya Fedha

  • 15

    Picha ya Pamoja ya baadhi ya washiriki na viongozi wakati wa kufunga maonesho ya kwanza ya kimataifa yaTiba Asili ya

    mwafrika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam, tanzania

    Bonivetura Ferdinandi Mwalongo

    MWENYEKITI JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LIMITED.

    Februari, 2015