9
Kenya MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP Empowered lives. Resilient nations. Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

Kenya

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP

Empowered lives. Resilient nations. Empowered lives. Resilient nations.

Miradi ya EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

Page 2: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Muliru Farmers Conservation Group, haswa mwongozo na mchango wa James Ligare. Picha ni za Muliru Farmers Conservation Group, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ZiadaUnited Nations Development Programme. 2012. Muliru Farmers Conservation Group, Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

Page 3: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

MAELEZO KUHUSU MRADI HUUKikundi cha wakulima wahifadhi wa Muliro ni shirika la kijamii linalopatikana karibu na msitu wa Kakamega magharibi mwa Kenya. Kikundi hiki hujipatia riziki kwa kuuza dawa ya kienyeji inayoitwa Naturab ambayo hutengenezwa kutokana na mti spesheli. Shughuli hizi za kikundi zimesaidia katika uhifadhi wa msitu wa Kakamega. Wengi wa wanachama wa kikundi hiki ni wanawake ambao huchuma riziki kwa kuuza dawa hii. Aidha, baadhi ya pesa zinazopatikana kutoka biashara hii hutumika kulipia utafiti kuhusu msitu huu na uhifadhi wake kwa kijumla.

MUHTASARIULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2010

ULIANZISHWA: Mwaka 1997

ENEO: Mkoa wa Magharibi, Kenya

WANAOFAIDI: Kaya 360

MAZINGIRA: Msitu wa Kakamega

3

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUPKenya

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 5

Matokeo ya Kimazingira 7

Matokeo ya Kijamii 7

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 8

Maono 8

Wahisani 8

Page 4: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

4

Msitu wa Kakamega ndio msitu asilia ulionusurika kutokana na uharibifu wa kibinadamu. Msitu huu wenye miti aina tofauti hupatikana mkoa wa magharibi. Msitu huu ndio tegemeo la wakaaji wa eneo hilo. Wenyeji hutegemea msitu huu kwa mbao, kuni, chakula cha ng’ombe, miti ya ujenzi na miti ya kutengeneza dawa za kienyeji. Msitu huu ndo chanzo cha maji safi ya eneo hili pamoja na shughuli zote za kibiashara. Msitu Kakamega (kama ilivyo kawaida kwa msitu mingine nchini Kenya) huko karibu kuangamizwa na shughuli za kibinadamu kama vile: ukulima na ujenzi, mbao ,uchomaji makaa na utengenezaji wa madawa ya kienyeji. Idadi ya watu karibu na msitu inaendelea kuongezeka huku eneo la kilomita moja kukaliwa na watu takriban 1200. Hapa, kiwango cha umasikini ni cha juu huku watu 35,000 wakitegemea msitu huu.

Kukuza na kuhifadhi mti wa dawa

Baadhi ya miti inayopatikana katika msitu Kakamega ni Ocimum Kilimandscharicum. Tangu jadi mti huu umekuwa ukitumiwa na wenyeji kwa kutibu mafua na kikohozi. Mti huu huwa na mafuta yenye mnuko spesheli. Matawi yake yamekuwa yakichemshwa na kutumiwa kutibu magonjwa ya kupumua. Matumizi mengine ni kama: kufukuza mbu, kutengeneza asali (nyuki), viungo vya vyakula na kufukuza wadudu wanavamia ghala za mahindi.

Kikundi cha Muliru kiliundwa mnamo mwaka wa 1997 kikiwa na lengo la kukuza mti wa Ocimum Kilimandscharicum ambao wangeutumia kama mbinu ya kuhifadhi msitu wa Kakamega na kuwapa kitega uchumi majirani wa msitu huu. Kikundi hiki kimechanganya elimu ya zamani na ile ya kisasa yakiteknolojia na sayansi na kupata washika dau wa kipekee - wakulima wa mashinani, asasi za utafiti na sekta ya kibinafsi – ili kuongeza ubora wa mti huu wa dawa. Kikundi hiki hushirikiana sako kwa bako na wakulima wa mashinani kuunda bidhaa tofauti tofauti kutokana na mti huu ambao huuzwa kwa kutumia nembo na jina la usajiri la Naturub. Naturub imesajiriwa kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali.

Kikundi hiki kina malengo manne makuu:

i. Kuimarisha ukuzaji wa kibiashara wa Ocimum Kilimandschirium miongoni mwa wachochole wanoishi mkabala na msitu wa Kakamega

ii. Kuunda na kutafutia soko bidhaa zinazotokana na mti huu ndiposa wakulima wa mashinani wajipatie mapato

iii. Kuhamasisha wakulima kuhusu umuhimu wa kuutunza msitu wa Kakamega

iv. Kuwakusanya majirani wa msitu huu ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuhifadhi msitu huu.

Historia na Mandhari

Page 5: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

55

Kikundi cha Muliru huwaleta pamoja majirani wa msitu Kakamega ili kupanda miche ya Ocimum Kilimanscharicum. Ukulima wa mti huu huwa biashara muhimu kwa wakulima waliotengwa wa eneo hii. Wakulima hufunzwa namna ya kutayarisha na kuvuna mti huu nyumbani mwao. Mti huu huvunwa kwa kukatia sehemu karibu na mizizi na kisha kuchuma matawi yake. Kitambo, utoaji wa mafuta ulifanyiwa nyumbani, lakini mnamo mwaka wa 2005, Muliru ilijenga mtambo wa kazi hiyo katikati mwa eneo hilo. Wakulima husaidiwa na kikundi kukusanya na kusafirisha matawi mitamboni. Hapa matawi hupimwa na kukaushwa. Matawi haya makavu hutengenezwa mafuta maalum ambayo huuzwa kwa nembo ya Naturub.

Utengenezaji na uuzaji wa Naturub

Tangu kuzinduliwa mtambo wa utengenezaji wa mti wa Ocimum tani 770 zimetengenezwa na kilo 700 za mafuta kidawa yametolewa. Aidha takriban vidonge 400,000 vya Naturub vimeuzwa mijini na mashinani kote nchini Kenya. Bidhaa hizi za Naturub zimekubaliwa vyema masokoni ingawa vimepata ushindani mkubwa kutoka bidhaa za kimataifa. Kipato cha mradi huu ni takribani dolla 70,000 za kimarikani. Hivi sasa wakulilma kama 360 wanakuza mti huu mashambani mwao. Ukulima wa mti huu umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika eneo hili.

Licha ya kukuza na kuuza bidhaa za Naturub, shirika hili la uhifadhi wa msitu huandaa warsha za kimasomo kwa wenyeji wa eneo hili wakiwafunza juu ya umuhimu wa kuyatunza mazingira na raslimali asilia kama misitu. Shirika hili hutayarisha miche ya miti asili ambayo hukabidhiwa wakulima ili kuipanda mashambani mwao.

Ubunifu usiosahaulika wa kikundi hili ni ule wa kuanzisha mradi uliosajiri dawa, kuunda na kisha kuifanya biashara muhimu ya kunufaisha wakulima wachochole. Licha ya kuhimiza ukulima wa mti huu, kikundi kilienda hatua moja zaidi kwa kuanzisha mtambo uliomilikiwa na kuendeshwa na wakulima wenyewe. Isitoshe, wakulima wamepata ujira wa kudumu na kuinua viwango vya maisha yao.

Uongozi

Kikundi hiki kinaingozwa na bodi iliyoundwa na; mwenyekiti na naibu wa mwenyekiti, katibu na naibu wa katibu, mwekahazina, katibu mwandalizi na wanakamati wane, ambao uchaguliwa na vikundi vya wakulima kuhudumu kwa miaka fulani. Bodi ndiyo inayo usemi wa mwisho katika kikundi hiki cha Muliru. Jukumu kuu la bodi ni kuhakikisha kuwa maslahi ya wakulima yanazingatiwa na kupata ujira mwema wa mauzo yao. Kikundi kina nyapala mkuu ambaye anaendesha shughuli zote za kikundi hiki na kuripoti kwa bodi.

Shirika hili lina vitengo kadha vyenye kushughulikia mambo tofauti tofauti; mfano, kitengo cha mauzo ambacho huijishughulisha na kuuza bidhaa za kikundi hiki katika maduka makuu nchini Kenya, kitengo hiki vile vile ushirikiana na makampuni ya kibinafsi ili kutangaza bidhaa za shirika hili. Mwisho kikundi huwa na vitengo vitatu katika ngazi ya mashinani. Mwakilishi wa vikundi vya wakulima ambaye hutoa maoni ya wakulima wakati wa mikutano. Ngazi ya pili, huwa na mwendesha mtambo ambaye husaidiwa na vijana tisa katika kutoa mafuta malighafi. Ngazi ya mwisho ni askari gongo mkuu ambaye hushirikiana na utawala wa mkoa ili kuchunga mali yote ya kikundi.

Majukumu Makuu na Ubunifu

Page 6: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

66

Fig. 1: Jendwali la Uongozi

Bodi ya Usimamizi

Nyapala Mkuu

Kitengo cha Uundaji

Msimamizi wa Mtambo

Kitengo cha Mauzo

Askari gongo Mkuu

Kitengo cha Mafunzo

Mwakilishi wa Wakulima

Chanzo: Kikundi Cha Wakulima Wahifadhi Cha Muliru

Page 7: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

7

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRAMatokeo makuu ya mradi huu ni matumizi na uhifadhi mwema wa msitu Kakamega na vilevile kulinda takribani ndege 350 na mimea 380 inayopatikana humo. Aidha, mradi huu umesaidia wenyeji kuwa na fikra chanya kuhusu uhifadhi wa msitu pamoja na miti - mradi huu vilevile umechukuliwa kama kielelezo chema cha uhifadhi wa msitu na, chama cha msitu cha jamii ya Mwileshi.

Chama cha msitu cha jamii ya mwileshi

Chama cha kitaifa kinachosimamia msitu (KWS) kiko mbioni kuhusisha jamii za mashinani katika uhifadhi wa misitu. Msitu wa Kakamega ulichaguliwa ili kufanyia majaribio hayo ambapo ushirikiano kati ya jamii za mashinani pamoja na kikundi cha Muliru wamepanda miche 10,000 mnamo Septemba 2010 pekee. Vyama hivi vilivyokusanywa pamoja hufunza jamii kuhusu umuhimu wa msitu na namna ya kuitunza misitu kwa jumla.

Kubadili mtizamo kuhusu uhifadhi wa misitu

Utafiti uliofanywa na kikundi cha MuIiru ,ukihusisha wakulima wa Ocimum 360 ulionyesha wazi kuwa wakulima asilimia 85 huhifadhi msitu. Matokeo kamili ya utafiti huo ni kama ifuatavyo; Asilimia 49 ya wakulima hao husambaza elimu ya uhifadhi wa misitu kwa wenzao, asilimia 59 wamepunguza ukusanyaji kuni , chakula cha ng’ombe na mbao msituni humo, asilimia 37 wamewakataza wanajamii wengine dhidi ya kutumia msitu vibaya na asilimia 5 ya wakulima wameripoti visa vya uwindaji haramu kwa utawala wa mkoa. Uvunaji wa Ocimum hauharibu mazingira, mimea ya Ocimum humea tena baada ya kukauka na hivyo jamii hupata kipato kisichoisha. Bidhaa za Naturub huwa na onyo na mawaidha ya kuhimiza uhifadhi wa mazingira.

MATOKEO YA KIJAMIIKikundi cha Muliru kimetanda miongoni mwa wilaya 5 zinazouzunguka msitu wa Kakamega ,na idadi ya watu ni kama2,500 na wanachama wa kikundi wakiwa ni 360.Wengi wa watu katika eneo hili wametengwa kiuchumi na wengi ni wachochole walio na mashamba madogo mno yasiyoweza kuwakimu kimaisha. Kikundi hiki cha Muliru kimebadili hii hali kwa kuwapa wenyeji fursa ya kazi na njia ya kujipatia riziki. Takribani watu 8 wa eneo hili wamepata kazi ya kudumu mitamboni . Isitoshe takribani wakulima 900 wana kazi ya kulima mmea huu hadi sasa vidonge 400,000 vimeuzwa kote nchini hususan kwenye maduka makuu kama vile; Uchumi,Turskeys na Eastmat. Naturub vilevile hupatikana kwenye maduka ya dawa nchini Kenya. Wakulima hupata marupurupu yao mara tatu kwa mwaka na wameona kipato chao kikiongezeka kwa asilimia 300 tangu mradi huu kuanzishwa.

Faisa Nynginezo

Kutokana na utafiti wa awali uliofanywa na kikundi hiki cha Muliru, kulipatikana faida nyinginezo kama; asilimia 31 ya wakulima hutumia hela walizozipata kutoka kwa mradi huu kuanzisha biashara ndogo ndogo na hivyo kuongezea kipato chao. Isitoshe , asilimia 83.5 hutumia hela zao ili kununulia familia zao chakula . Asilimia 57 hulipia watoto karo ,asilimia 26 hujinunulia nguo, asilimia17.65 hutumia pesa hizo kukarabati nyumba zao. Wenyeji vilevile wamenufaika na elimu ya kibiashara wanaopewa na mashirika mengine. Mradi huu vilevile umeinua kiwango cha maisha ya wenyeji. Wakulima nao ni kati ya washika dau wa shirika hili . Wakulima kwa sasa wana ufahamu mkuu kuhusu kilimo, uwekaji pesa na kuhusu umuhimu wa mshikamano wa kijamii.

Mradi huu aidha umehimiza usawa wa kijinsia ambapo jamii ya hapa imekubali ukweli kuwa uchumaji ni kazi ya mke na mume .Wanawake pia wanastahili kuchaguliwa kwenye nyadhifa za uongozi

Page 8: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

8

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUKikundi cha Muliru kilikua na mpango wa miaka kumi ya matumizi ya faida inayotokana na mauzo ya Naturub. Mpango wenyewe ulikua kama ufuatao; asilimia 10 kusaidia katika uhifadhi wa msitu wa Kakamega, asilimia 10 iingie kwenye mfuko wa maendeleo ya jamii inayozunguka msitu Kakamega, asilimia 60 kupewa wanachama wa kikundi cha Muliru, na asilimia 20 kuingia kwenye mfuko wa kusaidia utafiti. Kikundi kinachokisia kuwa shirika hili litajisimamia kifedha na kukua zaidi. Naturub ndiyo dawa pekee ya kienyeji kupata usajili wa kiserikali pamoja na shirika la madaktari linalosimamia dawa na sumu nchini. Upelelezi wa siri kuhusu Naturub umeonyesha kuwa dawa hii inazaa takribani shilingi million 100 kwa kila mwaka mijini. Kikundi cha Muliru kimetegemea mashirika ya nchini na kimataifa katika kufikia malengo yake. Muliru imewahi kushirikiana na kampuni kadhaa za matangazo na utangazaji katika kuendeleza malengo yake. Mashirika mengine ambayo yamefadhili Muliru ni kama chuo kikuu cha Nairobi, kituo cha dunia cha misitu, shirika la wanyama pori la Kenya (KWS) na mengineyo. Maono mengine ya kikundi ni kuongeza usalishaji, kutafuta masoko mengine ya nchini na kitaifa, kufanya utafiti zaidi kuhusu mmea huu kuwapa mafunzo zaidi wakulima na kuimarisha na kuhimiza wanawake na vijana kuunga mkono mradi huu.

MAONOKikundi hiki kimebadilisha mawazo ya mradi na wanajamii wa nchi kama Uganda, Tanzania, Afrika kusini na Nigeria na vilevile jamii zingine za humu nchini. Zaidi ya watu 830 wametutembelea ndiposa wapate masomo ya moja kwa moja . Mafunzo yanayopatikana kutoka kwa mradi huu yamesambazwa kupitia kwa mihadhara ,uigizaji, utambaji na matembeleano. Isitoshe , mradi huu umeonyeshwa na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kama redio na televisheni. Kutokana na utangazaji huo, mradi wetu umeigwa na jamii kadhaa mfano kikundi cha kuifadhi misitu cha mashariki ya Usambara nchini Tanzania na kikundi kinachohifadhi misitu ya

Budongo nchini Uganda. Kulingana na maoni ya kikundi cha Muliru, mafunzo yanayobadilishwa miongoni mwa watu wenye rika moja huzama na kueleweka zaidi

WAHISANI• Kituo cha kimataifa cha uchunguzi wa Wadudu• Chuo Kikuu cha Nairobi• Shirika la Dunia la Misitu• Taasisi ya Utafiti waMisitu la Kenya [KEFRI]• Shirika la Wanyama Pori la Kenya [KWS]• Shirika la[GBDI]• Wakfu wa Ford• Wakfu wa Bio Vision• Wakifu wa Macarthur• Huduma za kiuduma za Kijerumani [DED]• PACT-Kenya/USAid• WHO Multilateral Initiative on Malaria/Research and Training in

Tropical Diseases (TDR)

Page 9: MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - …...kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na wadudu na miteguko mbalimbali. Kikundi hiki kina malengo manne makuu: i. Kuimarisha

MAREJELEO YA ZIADA

• Muliru Farmers Conservation Group PhotoStory (Vimeo) vimeo.com/15780379• Video on Muliru Farmers Conservation Group (Vimeo) vimeo.com/43207923

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa: