64
` Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini Tanzania: Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii na Uwezekano wa Matumizi February 2011

Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

  • Upload
    others

  • View
    47

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

`

Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama

nchini Tanzania:

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii na Uwezekano wa Matumizi

February 2011

Page 2: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini Tanzania:

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

na Uwezekano wa Matumizi

February 2011

Page 3: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Shukrani Kijarida hiki kimeandaliwa na kuandikwa na Tony Baker wa Idara wa Uchambuzi na Utetezi wa Sera ya HakiElimu. Alitiwa moyo na mkutano wa kikanda uliofanyika Cape Town, Afrika ya Kusini kuanzia Machi 23-25, 2010. Mkutano uliandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Ulinzi wa Kisheria wa Haki za Binadamu (INTERIGHTS), timu ya wanasheria wa haki za binadamu chenye makao yake London, Uingereza. Mkutano huu ulihudhuriwa na wawakilishi wa kisheria, mahakama, na asasi za kiraia kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Zimbabwe na Afrika ya Kusini, na wakakaa pamoja na baadhi ya wanasheria wa haki za binadamu kimataifa na Prof. Dk. Fons Coomeans, Mwenyekiti wa UNESCO katika Haki za Binadamu na Amani kwenye Idara ya Sheria za Kimataifa na za Ulaya katika Chuo Kikuu cha Maastricht, Uholanzi. Mkutano huu haukuwa mafunzo wala semina, bali yalikuwa ni majadiliano ya mezani ya siku tatu ya wataalam kumi na sita katika nyanja mbalimbali wenye lengo la kuvumbua faida za kesi za kimkakati katika kuhakikisha upatikanaji wa haki ya elimu katika nchi yoyote iliyowakilishwa kusini mwa jangwa la Sahara. Uchambuzi katika mjumuiko huu ulielezewa zaidi mkutano mwingine uliofuata kuhusu namna ya kufanya kesi za kimkakati mahsusi kwa ajili ya haki ya kupata elimu uliofanyika Dar es Salaam kuanzia Januari 25-28, 2011. Mkutano huu uliandaliwa na HakiElimu na INTERIGHTS, na uliwakusanya wanasheria, watetezi na wataaluma wa haki za binadamu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Swaziland, Afrika ya Kusini, Nigeria, Switzerland na Uingereza ili kujadili kesi na mikakati iliyopo na ijayo ya kudai haki ya kupata elimu kwa njia ya mahakama. Solomon Sacco wa INTERIGHTS anashukuriwa sana kwa mchango wake ambao umetia nguvu kijarida hiki, na Robert Mihayo wa bodi ya wahariri ya HakiElimu anashukuriwa sana kwa kuhariri kazi hii. Elizabeth Missokia, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, anashukuriwa sana kwa mwongozo wake wa mara kwa mara katika kuandaa jarida hili. © HakiElimu, 2011 ISBN 978-9987-18-028-8 HakiElimu S.L.P. 79401 Dar es Salaam, Tanzania Simu: (255 22) 2151852/3 Faksi: (255 22) 2152449 Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.hakielimu.org Picha za juu: Wanafunzi wa Shule ya Msingi Gidngwar, Babati Vijijini, Manyara (juu) Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam (chini kushoto) Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Arusha, Tanzania (chini kulia) Sehemu yoyote ya jarida hili inaweza kutolewa kwa namna yoyote kwa madhumuni ya kielimu na siyo ya kibiashara, kwa kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala mbili zitapelekwa HakiElimu. Maoni yanayoelezwa katika jarida hili si lazima yawe ni maoni ya HakiElimu.

Page 4: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Yaliyomo

Vifupisho .............................................................................................................................................. i

Dibaji ................................................................................................................................................... ii

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii .................................................................................... 1

1.0 Muundo wa Kisheria .......................................................................................................................... 1

1.1 Mikataba ya Umoja wa Mataifa ........................................................................................................ 1

1.1.1 Tamko la Dunia la Haki za Binadamu ............................................................................... 2

1.1.2 Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni ........................ 3

1.1.3 Mkataba Dhidi ya Ubaguzi katika Elimu ........................................................................... 9

1.1.4 Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake ........................ 9

1.1.5 Mkataba wa Haki za Mtoto .................................................................................................. 9

1.1.6 Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu ................................................................... 12

1.2 Mkataba wa Umoja wa Afrika ........................................................................................................ 12

1.2.1 Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu ...................................................... 12

1.2.2 Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto ......................................................... 16

1.3 Mikataba ya Jumuiya ya Afrika ....................................................................................................... 18

1.3.1 Mkataba wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ............................................... 18

1.3.2 Mkataba wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika juu ya Elimu na Mafunzo . 18

1.3.3 Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ....................................................................... 18

1.4 Sheria ya Ndani Tanzania ................................................................................................................ 19

1.4.1 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ............................................................... 19

1.4.2 Sheria ya Elimu .................................................................................................................... 19

1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ..................................................................................................... 21

1.5 Mazingatio Mengine Zaidi Kisheria .............................................................................................. 21

2.0 Mazingira ya Kisiasa ......................................................................................................................... 22

3.0 Muktadha wa Kijamii ....................................................................................................................... 24

Elimu ya Msingi ―Bure‖ .................................................................................................................. 26

Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito ...................................................................................... 32

Adhabu ya Viboko ........................................................................................................................... 38

Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II ....................................................................................... 42

Marejeo .............................................................................................................................................. 49

Page 5: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Vifupisho i

Vifupisho ACHPR Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu

ACRWC Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto

AEW Africa Education Watch – Mpango wa kuboresha uwazi na uwajibikaji katika elimu

ya msingi Afrika

AG Mwanasheria Mkuu

AU Umoja wa Afrika

CADE Mkataba dhidi ya Ubaguzi katika Elimu

CEDAW Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake

CRC Mkataba wa Haki za Mtoto

CRIN Mtandao wa Taarifa za Haki za Mtoto

CRPD Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu

CWT Chama cha Walimu Tanzania

EAC Jumuiya ya Afrika Mashariki

ICESCR Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni

ICRMW Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Haki za Wafanyakazi Wahamiaji Wote na Familia zao

MMEM Mpango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi

MMES Mpango ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari

MoEVT Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

MP Mbunge

NAO Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

OAU Umoja wa Muungano wa Afrika

RTE Haki ya Kupata Elimu

SADC Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika

TI Transparency International – Shirika la kimataifa linalopambana na rushwa

UDHR Tamko la Dunia la Haki za Binadamu

UN Umoja wa Mataifa

UNCESCR Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi,

Kijamii na Kiutamaduni

UNCHR Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu

UNESCO Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa

UNGA Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

UPE Elimu ya Msingi kwa Wote

URT Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 6: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

ii Dibaji

Dibaji Mtu anaweza kutetea haki zake kwa mafanikio iwapo tu anafahamu kuwa ni zipi na anajua kutumia njia iliyopo kikatiba katika kudai haki hizo….

Julius K. Nyerere, ―Uhuru na Maendeleo,‖ 1968 Elimu ni haki ya kibinadamu yenyewe kama ilivyo, na pia ni chombo cha lazima katika kujipatia haki zingine za binadamu. Ikiwa ni haki ya kutia nguvu, elimu ni chombo cha msingi ambacho watu wazima na watoto walioko pembezoni kiuchumi na kijamii wanaweza kutumia kuondoa umasikini na kujipatia njia za kushiriki kikamilifu katika jamii zao. Elimu ina kazi kubwa ya kuwajengea uwezo wanawake, kuwalinda watoto kutoka katika kazi nyonyaji na hatarishi na unyonyaji wa kingono, kuchochea demokrasia na haki za kiibinadamu, kulinda mazingira na kudhibiti ongezeko la watu. Zaidi sana, elimu ni ongezeko la mambo ambayo ni hazina ya ajabu Serikali inaweza kuwekeza. Lakini basi umuhimu wa elimu si tu katika matumizi yake: akili iliyoelemika, iliyotiwa nuru, iliyochangamka, yenye uwezo wa kufikiri kwa uhuru mirikishi ni mojawapo ya furaha na amali za kuwepo kwa mwanadamu.

Sehemu ya kwanza ya Maoni ya Jumla Na. 13: Haki ya Kupata Elimu ya Kamati ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni, 1999

Karibu katika Kijarida cha Maelezo ya Haki ya Kupata Elimu! Lengo la kijarida hiki ni kukujuza juu ya haki ya kupata elimu, mitazamo yake kisheria, kisiasa na kijamii na baadhi ya mifano yake ambayo yaweza kutumika katika kudai haki hii mahakamani. Wengi wetu bila shaka tumekwishasikia juu ya haki ya kupata elimu na yawezekana tunatumia msemo huu katika kuzungumza na jamii zetu, hata hivyo mara kwa mara haki ya kupata elimu hubaki kuwa ni jambo la kufikirika katika akili zetu na kwamba haki hii inatupatia tu baadhi ya aina za elimu. Kama tungelazimishwa kuelezea maana ya haki ya kupata elimu, wengi wetu tusingeweza kusema zaidi ya kwamba ina maana ya kuwa watoto wenye umri wa miaka saba ni lazima waende shule. Kimsingi, haki ya kupata elimu ni haki iliyo bayana, yenye malengo na majukumu yaliyoainishwa kwa wazi kabisa ambayo serikali katika dunia nzima zimekubaliana nayo kupitia mikataba au makubaliano ya kidunia, kikanda na hata ndani ya nchi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda unaozidi miaka 60 sasa. Ni lengo la chapisho hili kukuonesha mambo ya msingi kwa kina na mapana kuhusu haki ya kupata elimu ili kwamba isiwe tena ni dhana yenye mkanganyiko ndani yako bali iwe ni dira iliyoelezwa kwa kina ikaeleweka na kutambulika na ukajua kila ambacho tunafanyia kazi. Hata hivyo, kinachofuata si kwamba kinaeleza mjadala wote kwa mapana na marefu kuhusu nyanja zote za haki ya kupata elimu. Bali kimsingi, lengo ni kujadili matumizi yake, hasa kudai haki hii kwa njia ya mahakama, kwa sababu ni lengo la kijarida hiki kukuzoesha wewe nafasi au jukumu lako kama raia katika mfumo wa kisheria. Mara nyingi tunafikiri kwamba sheria zinaweza kujisimamia zenyewe—kwamba mara zinapotungwa basi zinatumiwa kama ipasavyo. Mara kwa mara tunafurahia kupitishwa kwa sheria mpya, yenye mwono wa mabadiliko, tunapotaharuki na kuangalia nyuma baada ya miaka kadhaa tangu sheria hiyo kupitishwa kuona kwamba hakuna mabadiliko yoyote. Hii ni kwa sababu hatutambui na kusimamia majukumu yetu kwa kutumia mifumo yetu ya sheria. Sheria si tu kwamba ni kanuni ambazo serikali inahakikisha zinafuatwa na watu; ni kanuni ambazo watu wanapaswa pia kuhakikisha serikali inazitimiza. Sheria hazibadilishi mambo kwa njia ya miujiza; ni vitendea kazi vya kutumia katika mahakama kuwajibisha wengine ili kuleta mabadiliko. Kwa mantiki hiyo, si makusudi ya chapisho hili kujaza kichwa chako na maelezo ya haki ambayo huwezi kuipata lakini ni kukuelimisha juu ya vitendea kazi vilivyopo na namna ambavyo unaweza kuvitumia ili kupata haki zako.

Page 7: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Dibaji iii

Mwisho kabisa, japokuwa chapisho hili lina msamiati wa kisheria na dhana za kisheria, halikuandikwa na mwanasheria na hivyo laweza kuwa na kurahisishwa sana kwa makosa. Hatimaye, ni matumaini kwamba kutakuwa na faida kwa sababu dhana za sheria zilizoandikwa na mtu asiye mwanasheria zinaweza pia kusomwa na kueleweka vizuri na mtu asiye mwanasheria.

Page 8: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 1

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii Watu wa Tanzania nzima wanafanya kazi kwa bidii ili kuboresha maisha yao na ya wale wanaowapenda. Suala la msingi katika maendeleo haya ni elimu. Elimu bora ni haki ya kikatiba kwa kila raia wa Tanzania, hata hivyo ni jambo la kawaida kuona kwamba haki hii inavunjwa. Kwa dhati kabisa, haki ni sheria yenyewe. Wakati sheria zinavunjwa, mara nyingi hatua za kisheria huchukuliwa. Hivyo basi, haki zinapovunjwa, kuna nyakati kwenda mahakama kuchukuliwe kama hatua mbadala. Tunapoangalia uwezekano wa kwenda mahakamani kupeleka shauri la kuvunjwa haki, mambo kadhaa ya msingi ni lazima kuangaliawa, hususan muktadha wa kisheria, kisiasa na kijamii. Masuala haya ni ya msingi sana kwa shauri lolote lile lakini zaidi sana kwa shauri la kimkakati, ambalo ndilo hasa linajadiliwa kwa kina hapa. Shauri la kimkakati linatofautiana na shauri la kawaida kwani lenyewe linategemea kutumia mahakama ili kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Wakati linatafuta kutetea haki ya mtu mmojammoja kama ilivyo kwa huduma za kisheria za kawaida, shauri la kimkakati linahusu haki ya kijamii. Ni mbinu ya kuleta mabadiliko katika sera au kuhakikisha utekelezaji wa sera kwa lengo la kutetea haki katika jamii kwa ujumla (CRIN, 2009). Hivyo basi, zaidi ya shauri la kawaida, shauri la kimkakati ni lazima lizingatie masuala ya kisheria, kisiasa na kijamii katika jitihada za kuleta mabadiliko endelevu ya kijamii.

1.0 Muundo wa Kisheria Japokuwa mazingira ya kisiasa na kijamii yanaweza kuwa na ushawishi zaidi katika mafanikio ya shauri la haki ya kupata elimu (RTE), hata hivyo muundo wa kisheria uliopo kimsingi ni wa kwanza kabisa kuangalia, kwa sababu unaainisha maana halisi ya haki ya kupata elimu, wajibu wa msingi wa serikali katika hilo na ukiukaji wake. Muundo huu unajumuisha sheria, mikataba na maridhiano ya kidunia, kikanda na kitaifa.

1.1 Mikataba ya Umoja wa Mataifa Tanzania ilipata uanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1961, na hivyo basi kuwa sehemu ya mfumo wa Tamko la Dunia la Haki za Binadamu (UDHR) (1948). Tangu wakati huo, Tanzania imetia saini na kuridhia mikataba kadhaa ya kimataifa, ikiwemo inayotamka bayana kwamba wanachama wake kutimiza haki ya kupata elimu. Kwa kufuata mtiririko na mwaka ambao mikataba hii iliridhiwa na Tanzania, ni hii ifuatayo: Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR) (1976), Mkataba dhidi ya Ubaguzi katika Elimu (CADE) (1979), Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) (1985), Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC) (1991) na Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRDP) (2009). Tanzania imeridhia mikataba yote ya Umoja wa Mataifa yenye masuala ya haki ya kupata elimu, isipokuwa Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Haki za Wafanyakazi Wahamiaji Wote na Familia zao (ICRMW). Maelezo zaidi katika lugha ili kuufanya mjadala ufuatao ueleweke zaidi: Katika mfumo wa mikataba ya kimataifa na pia katika mifumo mingine ya kisheria, kuna tofauti kati ya ‗kutia saini,‘ na ‗kuridhia.‘ Kutia saini mkataba ni alama tu ya kuukubali, wakati kuridhia ni kuhakikisha kwamba unatekeleza makubaliano ya mkataba na matakwa yake ya kisheria. Japokuwa la pili hufuata la kwanza, si lazima,

Page 9: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

2 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

na kuna ushahidi wa mataifa mengi kusaini na kuacha kuridhia mikataba fulani fulani.1 Pia, ‗kuukubali‘ mkataba ina maana iliyo sawa na ‗kuridhia,‘ na ina matokeo sawa kisheria. Nyakati zingine, mjadala unaofuatia huzungumzia ‗kuuchukua‘ mkataba, halafu ‗kuwekwa katika vitendo.‘ ‗Kuchukua‘ ni tendo la chombo, kama vile Umoja wa Mataifa, kuanzisha aina na maudhui ya azimio—kimsingi wakikubaliana juu ya maana ya azimio hilo. Katika hatua hii, azimio halina nguvu ma bado linahitaji kuridhiwa na baadhi ya wanachama ndipo pande za azimio zifungwe nalo kwa mujibu wa makubaliano. Mkataba au azimio ‗kuwekwa katika vitendo‘ huanza pale ambapo namba iliyowekwa na wanachama inatimia, ni mchakato ambao unaainishwa na azimio lenyewe kama wanachama walivyoazimia. Kwa mfano, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR) ulitamka kwamba ungeanza kufanya kazi miezi mitatu baada ya mwanachama wa 35 wa Umoja wa Mataifa kuingia au kuridhia. Kuanzia hapo ndipo mkataba huu ungewafunga wanachama wake walioridhia na wale watakaoridhia baada ya hapo. Kiujumla, kwanza mkataba unaandaliwa, halafu unawekwa wazi kwa nchi wanachama kutia saini na kuridhia. Pale ambapo wanachama wa kutosha wameridhia (ikionesha kwa dhati kabisa kwamba umekubaliwa na wengi kuwa ni mkataba halali wa Umoja wa Mataifa) unaanza kufanya kazi. Kwa wakati huo sasa ni mkataba rasmi wenye kuzibana nchi wanachama zilizoridhia. Kwa sababu mjadala huu unalenga zaidi katika vipengele vinavyohusu haki ya kupata elimu ambavyo kwavyo Tanzania inawajibika, ifuatayo inajadili tu mikataba ambayo Tanzania imetia saini na kuridhia/kukubali na ile ambayo inafanya kazi. 1.1.1 Tamko la Dunia la Haki za Binadamu Likichukuliwa kama hatua ya kwanza kubwa kabisa juu ya haki za binadamu na lililoanzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, Tamko la Dunia la Haki za Binadamu (UDHR) lilikubaliwa na Tanzania ilipokuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1961. Kifungu cha 26 cha Tamko hili kinaelezea bayana haki ya kupata elimu:

(UNGA, 1948)

1 Kwa mfano, Marekani wametia saini lakini wamekataa kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR), Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW), na Mkataba wa Kyoto.

Kifungu cha 26 (1) Kila mmoja ana haki ya kupata elimu. Elimu itatolewa bure, japo kwa

hatua za awali na msingi. Elimu ya msingi itakuwa ni ya lazima. Elimu ya ufundi na taaluma mbalimbali itakuwepo kwa ujumla na elimu ya juu itapatikana kwa wote kwa vigezo stahiki.

(2) Elimu itaelekezwa katika kuendeleza haiba kamili ya mwanadamu na katika kutilia mkazo heshima ya haki za binadamu na uhuru wake. Itachochea uelewa, uvumilivu na urafiki miongoni mwa mataifa yote, makundi ya rangi au ya kidini, na itachochea vitendo mbalimbali vya Umoja wa Mataifa vinavyodumisha amani.

(3) Wazazi wana haki ya kwanza kabisa ya kuchagua aina ya elimu ambayo itatolewa kwa watoto wao.

Page 10: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 3

Tangu kuanza kwa Tamko hili, haki ya kupata elimu inajumuisha vipengele kadhaa kama vinavyoainishwa na kifungu cha 26. Kwanza kabisa, uwepo na upatikanaji wa elimu umeainishwa. Haki ya kupata elimu ni kwa wote, na kuhusu viwango mbalimbali vya elimu, elimu ya msingi itakuwa ni ya bure na ya lazima, elimu ya ufundi itakuwepo, na elimu ya juu itakuwa ni kwa anayestahili. Pili, lengo la elimu limewekwa kuwa ni maendeleo kamili ya mwanadamu na kuheshimu haki za binadamu, uhuru, kutokuwepo ubaguzi, na amani. Na tatu, uhuru wa wazazi wa kuchagua aina ya elimu kwa watoto wao umeainishwa. 1.1.2 Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni Ukiwa umeanzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1966, kuanza kufanya kazi mwaka 1976, na kukubaliwa na Tanzania mwaka huohuo, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR) unawabana wanachama kufanya kazi ili kuhakikisha mtu binafsi anapata haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kama vile haki za kufanya kazi, za hifadhi ya jamii, za maisha ya familia, za hadhi stahiki ya maisha, za afya, za elimu na za kushiriki katika maisha ya kiutamaduni. Mpaka sasa nchi 160 zimeridhia mkataba huu ambapo nchi nyingine 6 zimetia saini lakini bado hazijaridhia. Kuhusiana na haki ya kupata elimu, mkataba huu unasema:

Kifungu cha 13 1. Nchi wanachama katika Mkataba uliopo zinatambua haki ya kila mtu kupata

elimu. Wanakubali kwamba elimu itailenga katika kumwendeleza kikamilifu mwanadamu na hisia ya utu wake, na itatilia mkazo heshima katika haki za binadamu na uhuru wa msingi. Na wanakubali kwamba elimu itawawezesha watu wote kushiriki kikamilifu katika jamii huru, kuchochea ufahamu, uvumilivu na urafiki miongoni mwa mataifa yote na makundi yote ya rangi, kabila na dini, na kuchochea vitendo vya Umoja wa Mataifa vinavyodumisha amani.

2. Nchi wanachama katika Mkataba huu zinatambua kwamba, zikiwa na mtazamo wa kufanikisha upatikanaji wa haki hii: (a) Elimu ya msingi itakuwa ni ya lazima na itapatikana bure kwa watu

wote; (b) Elimu ya sekondari katika aina zake tofauti, ikijumuisha elimu ya

sekondari ya ufundi stadi, itakuwepo kiujumla na kupatikana kwa wote kwa njia zote muafaka, hususan kuendelea kutoa elimu ya bure;

(c) Elimu ya juu itapatikana sawa kwa wote, kwa kuzingatia uwezo, kwa njia zote muafaka, na hususan kuendela kutoa elimu ya bure;

(d) Elimu ya msingi itatiliwa mkazo kama itakavyowezekana kwa wale ambao hawakuipata au hawakumaliza kipindi chao cha elimu ya msingi;

(e) Maendeleo ya mfumo wa shule katika ngazi zote yatatiliwa mkazo, mfumo mzuri wa kujiendeleza utaanzishwa, na mazingira ya kufundishia kwa walimu yataendelea kuboreshwa.

3. Nchi wanachama katika Mkataba huu zinadhamiria kuheshimu uhuru wa

wazazi na, inapobidi, walezi kisheria kuchagua shule za watoto wao, mbali ya zile zilizoanzishwa na mamlaka ya umma, ambazo zinakidhi matakwa ya kielimu kama inavyooneshwa au kuthibitishwa na serikali na kuhakikisha elimu ya dini na maadili ya watoto wao yanaendana na dhamiri zao.

Page 11: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

4 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

(UNGA, 1966)

Kama inavyoonekana, Mkataba huu unatoa sauti kubwa zaidi kuhusu haki ya kupata elimu kama inavyoainishwa katika Tamko la Dunia la Haki za Binadamu na inaainisha msingi bayana wa kile ambacho kimekuja kuwa viashiria vya msingi vya haki ya kupata elimu. Idadi ya vipengele vipya vinajitokeza: elimu ya sekondari na ya juu inatakiwa kuendelezwa ili itolewe bure; utolewaji wa ―elimu ya msingi‖ unaelezewa zaidi kujumuisha wale waliokosa elimu ya msingi kabisa au kwa sehemu; mifumo ya shule na mazingira ya walimu ya kufanya kazi yanapaswa kuendelezwa na kuboreshwa; haki ya wazazi ya kuchagua aina ya elimu ya watoto wao imeongezwa kwa walezi kisheria, na uhuru huu wa kuchagua unajumuisha masuala ya uhuru wa dini; kuanzishwa kwa shule za binafsi kumelindwa; na serikali ambazo hazijakidhi elimu ya msingi ya bure kwa wote zinalazimika kuandaa mpango ili kutimiza haki hii. 1.1.2.1 Mambo ya Msingi Mbali ya mikataba na makubaliano, maeneo mengine muhimu ya kuangalia wakati wa kufanya uchambuzi wa haki ya elimu katika mfumo wa sheria, kama ulivyoanzishwa na Umoja wa Mataifa, ni ripoti za kamati za Umoja wa Mataifa na za Mwakilishi Maalumu wa Haki ya Kupata Elimu. Kamati zinaanzishwa na Umoja wa Mataifa kufuatilia utekelezaji wa mikataba na pia kutoa tafsiri zaidi ya mikataba hiyo. Pale ambapo mkataba au maagano yanaweza kuwa na maelezo machache juu ya suala hili, kamati itajadili na kutoa taarifa juu ya maana halisi na nia ya maelezo hayo. Wawakilishi Maalumu ni watu ambao wamepewa mamlaka na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya ufuatiliaji kwa ujumla, kuchunguza ukiukaji, na kutoa mapendekezo juu ya masuala ya haki za binadamu. Ripoti za Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki ya Kupata Elimu, japokuwa ziko nje ya mfumo wa kisheria wa haki ya kupata elimu, kihistoria zimekuwa ni sauti ya nguvu inayoshawishi mwelekeo na maendeleo ya haki hiyo. Mnamo mwaka 1999, Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (UNCESCR) ilikaa kikao ili kutoa maana nzima ya Vifungu vya 13 na 14 vya Mkataba huu. Inasema kwamba, ―Kifungu cha 13, ambacho ni kirefu kuliko vyote katika Mkataba, ni kifungu kipana na chenye maelezo ya kina kuliko vyote kuhusu haki ya kupata elimu katika sheria za kimataifa za haki za binadamu‖ (UNCESCR, 1999b).

4. Ni marufuku kutafsiri kipengele chochote katika kifungu hiki ili kuingilia uhuru wa mtu binafsi au chombo chochote kuanzisha na kuelekeza taasisi za elimu, ambayo mara zote inapaswa kutii kanuni zilizoainishwa katika aya ya I ya kifungu hiki na kwa matakwa kwamba elimu inayotolewa katika taasisi hizi mara zote itafuata masharti ya msingi kama itakavyoainishwa na serikali.

Kifungu cha 14 Kila nchi mwanachama katika Mkataba huu ambao, muda ilipopata uanachama, haijaweza kupata katika himaya yake au maeneo mengine yaliyo chini yake elimu ya msingi ya lazima na ya bure, itafanyakazi ndani ya miaka miwili, itaanzisha mpango kazi kabambe kwa ajili ya utekelezaji, ndani ya miaka muafaka, kuwekwa katika mpango, kanuni ya elimu ya lazima na bure kwa wote.

Page 12: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 5

Katika kuelezea kwa wazi na kina kwa yale yanayojulikana kama ―mambo ya msingi‖ ya haki ya kupata elimu kama inavyoainishwa na Kifungu cha 13, Kamati inaelezea kile kinachoitwa mpango wa ―A-4‖ (availability, accessibility, acceptability na adaptabilty) wa haki ya kupata elimu, yaani: uwepo, upatikanaji, kukubalika, na kurekebishika. Kwanza ukibuniwa na Katarina Tomasevski, hayati mtaalam wa dunia juu ya haki ya kupata elimu na Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki ya Kupata Elimu kuanzia mwaka 1998 hadi 2004, mfumo wa ―A-4‖ ulichukuliwa na Kamati na umekuwa mfumo unaotumika zaidi katika kuleta uelewa wa mambo ya msingi juu ya haki ya kupata elimu. Ikifupishwa na Prof. Dr. Fons Coomans, Mwenyekiti wa UNESCO katika Haki za Binadamu na Amani kwenye Idara ya Sheria za Kimataifa na za Ulaya katika Chuo Kikuu cha Maastricht, Uholanzi, mfumo wa ―A-4‖ unaweza kuelezewa kama ifuatavyo:

uwepo (availability): taasisi na mipango ya elimu inayofanya kazi inapaswa kuwepo kwa idadi ya kutosha katika nchi, kupitia mfumo wa elimu ya umma na kuwaruhusu watu wa mashirika binafsi kuanzisha shule zisizo za serikali;

upatikanaji (accessibility): taasisi na mipango ya elimu inapaswa kupatikana kwa kila mmoja, bila ubaguzi wa aina yoyote ile, pia ikujumuisha kufikika kimwili na kiuchumi;

kukubalika (acceptability): muundo na maudhui ya elimu, ikijumuisha mitaala na njia za kufundishia, vinapaswa kueleweka, kufaa kiutamaduni na ubora mzuri wa kumfaa mtoto; pamoja na mazingira ya shule salama na safi;

kurekebishika (adaptability): elimu inapaswa kuwa yenye kuendana na mazingira, ili kwamba iweze kwenda sambamba na mahitaji ya jamii yanayobadilika, na kuitikia kwa mahitaji ya wanafunzi katika muktadha wao kijamii na kiutamaduni, pamoja na uwezo wa mtoto.

(Coomans, 2007) Tume ya Haki za Binadamu ya New Zealand, taasisi ya haki za binadamu ya serikali ya New Zealand, inaleta mwonekano unaowakilishwa na mchoro huu:

Page 13: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

6 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

(Tume ya Haki za Binadamu, 2010)

Yasiyoonekana katika chambuzi mbili hapo juu ni vile viwango vitatu vya upatikanaji ambavyo Kamati inaviainisha vikijumuisha kutokuwepo ubaguzi, upatikanaji wa kimwili na upatikanaji wa kiuchumi. Haki zote za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni zinapaswa kupatikana ―bila ubaguzi wa aina yoyote kwa kigezo cha rangi, jinsia, lugha, dini, maoni ya siasa au mengineyo, asili ya kitaifa au kijamii, mali, kuzaliwa au hadhi yoyote ile‖ [UNGA, 1966, §2(2)]. Kuhusu upatikanaji wa kimwili, elimu ni lazima iwe inafikika kwa salama, iwe ni kijiografia kama vile shule iliyo karibu au kiteknolojia kama vile kozi za kupitia mtandao. Mwisho kabisa, ngazi zote za elimu ni lazima zifikike kiuchumi, yaani elimu ya msingi iwe ni ya bure na elimu ya sekondari na ya juu iendelezwe kuwa ya bure [UNCESCR, 1999b, §6(b)]. Vipengele vya haki ya kupata elimu, kama vile ―A-4,‖ si tu kwamba ni mapendekezo au miongozo, bali ni majukumu na wajibu kwa nchi wanachama zilizoridhia Mkataba. Vigezo vilivyoainishwa katika Vifungu vya 13 na 14 kuhusu haki ya kupata elimu vinaunganishwa na Kifungu cha 2 cha Mkataba ili kuwajibisha serikali zilizoridhia.

(UNGA, 1966)

Na hii kwa taathira yake ndiyo msingi wa Mkataba – kwamba Serikali za nchi zinaahidi kufanya jambo fulani, katika suala hili ni haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Hoja kutoka kwa Kamati juu ya Vifungu vya 2, 13 na 14 vinavyofanya kazi pamoja vinaelezwa hapa chini.

Kifungu cha 2 1. Kila nchi mwanachama wa Mkataba huu inachukua hatua, kibinafsi na

kupitia msaada na ushirikiano wa kimataifa, hasa kiuchumi na kitaalam, kwa rasilimali zote ilizonazo, kwa mtazamo kufanikisha utekelezaji mzima wa haki zilizotambuliwa na Mkataba huu kwa njia zote sahihi, ikijumuisha hasa utungaji sheria.

Mfumo wa Haki ya Elimu

UWEPO

KUREKEBISHIKA

UPATIKANAJI

KUKUBALIKA

Waelimishaji

wenye ujuzi na elimu ya kutosha

wapo

Mgawanyo wa

r asilimali inakidhi matakwa ya

kielimu kwa wote

Vikwazo

vinavyozuia maendeleo kati ya

viwango vya elimu

na ubor a wake na

utumishi bora

vimeondolewa

Mbinu imara

huhakikisha utoaji elimu wakati wote

huhakikisha elimu

yenye viwango na

iliyo bor a

Mazingir a ya

elimu yanaleta hisia kiakili

kimwili ni salama

kiutamaduni na

inakuza

Wanaofanya

kazi za elimu wanakaa

katika

mazingir a

mazuri

Utolewaji wa elimu

huchochea upatikanaji sawa wa

elimu kwa wote

Vikwazo vya elimu

vimeondolewa

Elimu huchochea

kufikia ukamilifu wa kibinadamu

Page 14: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 7

1.1.2.2 Heshimu, Linda, Timiza Haki ya kupata elimu pia huleta kundi lingine la majukumu ya Serikali yanayoendana na haki za binadamu zote: majukumu ya kuheshimu, kulinda na kutimiza. Wajibu wa kutimiza hufuatisha wajibu wa kuwezesha na wajibu wa kutoa. Kama ilivyoelezwa na Kamati,

Jukumu la kuheshimu: Serikali isikwamishe au kuzuia haki ya kupata elimu.

Jukumu la kulinda: Serikali lazima iingilie kati kuzuia wale wanaoingilia haki ya kupata elimu.

Jukumu la kutimiza (kuwezesha): Serikali zinapaswa kuwezesha na kusaidia watu binafsi na jamii kufurahia haki ya kupata elimu.

Jukumu la kutimiza (kutoa): Serikali inawajibika kutoa haki ya kupata elimu wakati mtu binafsi au kundi halina uwezo wa kufanya hivyo wao wenyewe.

(Imechukuliwa kutoka UNCESCR, 1999b, §47) Majukumu haya yanaungana na muundo wa ―A-4,‖ yaani ni majukumu ya kuheshimu, kulinda na kutimiza uwepo, upatikanaji, kukubalika na kurekebishika kwa elimu. Kwa kuelekeza, ―Serikali lazima iheshimu upatikanaji wa elimu kwa kutozifunga shule binafsi‖ (UNCESCR, 1999b, §50, msisitizo umeongezwa). Au, Serikali ni lazima ilinde uwepo wa elimu kwa kuhakikisha kwamba wasichana hawazuiwi na watu wengine kwenda shule. Vile vile, Serikali lazima itimize (iwezeshe) kukubalika kwa elimu kwa kuhakikisha kuwa kuna mtaala unaofaa kiutamaduni na ―kutimiza (kutoa) upatikanaji wa elimu kwa kuendeleza kikamilifu mfumo wa shule, ikijumuisha kujenga madarasa, kutoa kozi, kutoa zana za kufundishia, kuwapatia mafunzo walimu na kuwalipa mishahara ya kiushindani‖ (§50, msisitizo umeongezwa). 1.1.2.3 Utekelezaji Endelevu Serikali zinazokubaliana na Mkataba huu zinakubali ―kuchukua hatua,‖ na katika suala la haki ya kupata elimu, hii inaelezwa zaidi na Kifungu cha 14 kinachosema kwamba ―mpango kazi‖ lazima utekelezwe ―ndani ya miaka miwili‖ kwa lengo la kupata elimu ya msingi ya bure kwa wote ―ndani ya kipindi muafaka cha miaka kadhaa.‖ Kwa ujumla huku ‗kuchukua hatua‘ kwa serikali kuelekea kutimiza haki inayotolewa na Kifungu cha 2 kunaitwa ―utekelezaji endelevu,‖ ikimaanisha kwamba, kwa sababu haki zingine ni ngumu kuzipata papo kwa papo na kwa sababu rasilimali zaweza zisitosheleze mahitaji, Serikali hazilazimishwi kutimiza madhumuni ya Mkataba papo kwa hapo lakini wanapaswa kuyafanyia kazi kwa uendelevu. Au, kwa matamshi ya Kamati, ―Utekelezaji endelevu unamaanisha kwamba serikali wanachama zinalo jukumu bayana na endelevu ‗kufanyia kazi kwa haraka na ufanisi ndani ya uwezo wao‘ ili kuhakikisha kuwa kuna utekelezaji kamilifu wa kifungu cha 13‖ (UNCESCR, 1999b). 1.1.2.4 Rasilimali Zote Zinazopatikana Pia, ni muhimu kutambua kwamba utekelezaji huu endelevu unapaswa kufanywa na Serikali ―kuzifikia rasilimali zote zinazopatikana.‖ Kamati inafafanua kwa kina kwamba jukumu hili linahusisha rasilimali za Serikali zenyewe na zile zinazopatikana kupitia misaada ya kimataifa. Kwa maneno mengine, Serikali haiwezi tu kuangalia bajeti yake na kusema kwamba mapato yake ya ndani yanaweza kukidhi hitaji la ―rasilimali zote zinazopatikana‖ bila kuangalia fedha za misaada ya kimataifa kama sehemu ya rasilimali zake kutumika kutimiza haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni katika nchi husika.

Page 15: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

8 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

1.1.2.5 Kutokuwepo Ubaguzi Kamati inatoa tofauti fulani juu ya masharti hapo juu, na mojawapo ni suala la ubaguzi. Inasema kwamba marufuku dhidi ya ubaguzi ―haitegemei utekelezaji endelevu wala rasilimali zote zinazopatikana.‖ Kutokuwepo ubaguzi katika elimu ni suala linalohitaji kutekelezwa ―kwa ufanisi na haraka‖ (UNCESCR, 1999b, §31). 1.1.2.6 Kiwango cha Chini cha Majukumu ya Msingi Wajibu ulioainishwa hapo juu unajumuisha kile kinachoitwa kiwango cha chini cha majukumu ya msingi. Majukumu haya ni yale ambayo, zaidi ya mengine yote, Serikali wanachama zinalazimika kuyatimiza angalau kwa kiwango cha kutosha na yanaweza kuwekwa kama ifuatavyo:

Upatikanaji usio na Ubaguzi: ―kuhakikisha haki ya kupata elimu katika taasisi na kozi za elimu za umma kwa misingi isiyo na ubaguzi;‖

Lengo la Elimu la Kuleta Maendeleo kwa Mwanadamu: ―kuhakikisha kwamba elimu inaendana na malengo yaliyoainishwa katika kifungu cha 13 (1);‖

Elimu ya Msingi ya Lazima na ya Bure kwa Wote: ―kutoa elimu ya msingi kwa wote kuendana na kifungu cha 13 (2) (a);‖

Mkakati wa Kitaifa wa Elimu: ―kuchukua na kutekeleza mkakati wa kitaifa wa elimu utakaojumuisha utoaji wa elimu ya sekondari, elimu ya juu na elimu ya msingi;‖

Uhuru wa Kuchagua: ―kuhakikisha uhuru wa kuchagua elimu bila kuingiliwa na Serikali au watu wengine, ikizingatia kuendana na ‗viwango vya msingi wa elimu‘ (vifungu vya 13 (3) na (4)).‖

(Imechukuliwa kutoka UNCESCR, 1999b, §57) 1.1.2.7 Majukumu Maalum ya Kisheria Hatimaye, Kamati inaainisha mchanganyiko wa majukumu mengine ya serikali kuhusiana na haki ya kupata elimu. Serikali zinapaswa kuelekeza mitaala kuendana na haki ya kupata elimu; kuanzisha miundo ya kufuatilia ili kuangalia utekelezaji wa malengo ya kielimu; kuanzisha, kudumisha na kufuatilia viwango na kanuni za elimu ambazo taasisi zote zinapaswa kufuata; na kutokomeza utumikishwaji wa watoto katika jamii na familia (UNCESCR, 1999b, §49-55). 1.1.2.8 Ukiukaji

Ukiukaji wa haki ya kupata elimu unaanzia katika majukumu ya Serikali ya kuitambua haki. Serikali yaweza kukiuka haki ya kupata elimu kwa kufanya au kutofanya jambo fulani, maana yake ni kwamba Serikali yaweza kukiuka kwa kufanya jambo fulani dhidi ya haki ya kupata elimu au kwa kushindwa kutimiza sehemu ya majukumu yake (UNCESCR, 1999b, §58). Kwa mfano, kupitia sheria, serikali ikibagua kundi fulani la watu katika elimu, mathalani, kutowaruhusu kujiandikisha, huo ni ukiukaji. Kupiga marufuku shule za binafsi au kushindwa kutambulisha elimu ya msingi bure kwa wote pia ni baadhi ya ukiukaji ambao Serikali inaweza kufanya. Yote haya yanakiuka kiwango cha chini cha majukumu ya msingi ya Serikali katika haki ya kupata elimu. Upo pia ukiukaji wa pekee ambao unahusu utekelezaji endelevu na rasilimali zote zinazopatikana, na huo ndio ukiukaji wa hatua za kurudisha nyuma. Huu hutokea wakati Serikali inapoamua kuchukua hatua kinyume na utekelezaji wa haki ya kupata elimu badala

Page 16: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 9

ya kuifuata. Katika rasilimali zinazopatikana, inamaanisha kwamba Serikali haijihusishi tena na kuweka vipaumbele vya rasilimali katika elimu na yawezekana inaweka fedha zake mahali pengine. Yawezekana kwa namna fulani Serikali yaweza kuthibitisha kwamba hali hiyo si ukiukaji na kwamba ilikuwa ni lazima ifanye kama ilivyopanga, lakini kiujumla hatua za kurudisha nyuma haziruhusiwi (UNCESCR, 1999b, §42).

1.1.3 Mkataba Dhidi ya Ubaguzi katika Elimu Ikichukuliwa kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) katika mwaka wa 1960 na kuwekwa katika vitendo mnamo mwaka 1962, Mkataba Dhidi ya Ubaguzi katika Elimu (CADE) uliridhiwa na Tanzania mnamo mwaka 1979. Mkataba huu hutafuta kuondoa ubaguzi katika eneo la elimu na huainisha majukumu ya Serikali ya kuondoa ubaguzi katika nyanja zote za kielimu kama vile utawala, uandikishaji na misaada. Wakati unalinda uanzishwaji kwa shule za pekee za umma au binafsi kwa ajili ya dini au lugha (UNESCO, 1960, §2), Mkataba huu unazuia ―elimu iliyo duni‖ (§1(b)). Mbali na ubaguzi kutokuwepo, Mkataba huu unatilia mkazo baadhi ya dhana za msingi za Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR) kama vile madhumuni ya elimu kulenga maendeleo kamili kwa mwanadamu, uhuru wa wazazi na walezi kuchagua shule za watoto wao, uwepo na upatikanaji wa ngazi zote za elimu, viwango vya elimu, na juhudi za kuwafikia wale wote ambao hawajamaliza elimu ya msingi. 1.1.4 Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake Vita dhidi ya ubaguzi katika elimu inaendelea na Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1979, ukatekelezwa mwaka 1981, ukatiliwa saini na Tananzia mwaka 1980 na kuridhiwa na Tanzania mwaka 1985. Kifungu cha 10 cha Mkataba huu huwapatia wanawake haki sawa na wanaume katika nyanja ya elimu na unahakikisha kuwa:

masharti sawa ya upatikanaji katika ngazi zote za elimu; mtaala na mitihani sawa; walimu, majengo ya shule na zana zenye sifa na viwango sawa; fursa sawa kwa ufadhili wa masomo, misaada, kozi za mafunzo zaidi na ushirikiano

katika michezo/elimu ya michezo. (Imechukuliwa kutoka UNGA, 1979, §10)

Mkataba huu pia unalenga kuondoa ―dhana za ubaguzi kuhusu majukumu kati ya wanaume na wanawake‖ katika mfumo wa elimu, hususan katika kuangalia upya vitabu vya kiada, mipango ya shule na mbinu za kufundishia [UNGA, 1979, §10(c)] wakati ukihitajika upatikanaji wa habari za afya na mpango wa uzazi [§10(h)]. Mwaka 1987, baada ya kupitia ripoti kutoka mataifa 34 na kuona utofauti wa viwango vya ubaguzi wa kijinsia kwa wanawake, Kamati ya Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake iliomba Serikali wanachama kuchukua hatua ya kutoa maelezo ya kina kuonesha usawa wa kijamii kwa wanawake (Kamati ya UN CEDAW, 1987). 1.1.5 Mkataba wa Haki za Mtoto

Miaka ya mwanzo ya 1990 ilishuhudia uanzishaji wa urasimishaji wa haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa watoto. Ukianzishwa mwaka 1989 na kutekelezwa mwaka uliofuatia, Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC) umeridhiwa na kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa isipokuwa Somalia na Marekani. Tanzania iliridhia Mkataba huu mwaka 1991.

Page 17: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

10 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

Mkataba wa Haki za Mtoto ni waraka mpana unaoshughulikia mahitaji na haki mbalimbali za watoto, wakielezewa kwamba ni binadamu walio chini ya miaka 18 (UNGA, 1989, §1). Kiini cha Mkataba huu kinalenga katika kuzuia ubaguzi, maslahi ya mtoto, haki ya kuishi, kuishi na maendeleo na haki ya kutoa maoni na kuyafanya yazingatiwe wakati vipengele vingine vinaainisha haki na wajibu wa wazazi, uhuru wa kujieleza, uhuru wa mawazo, haki ya kupata habari, haki za watoto walemavu, haki ya kupata elimu ya afya, haki ya kuwa na lugha na utamaduni wao kwa watoto wa jamii zenye watu wachache, na haki ya kupata elimu (Kamati ya UNCRC, 2001b). Mkataba huu unapanua mjadala kuhusu haki ya kupata elimu zaidi katika mantiki ya ubora, kuzungumzia zaidi nia na madhumuni ya elimu ikilenga maendeleo ya mwanadamu na haki za binadamu. Unafanya hivyo kwa kuonesha picha ya kipekee zaidi ya mazingiria sahihi ya kujifunzia, mitaala na njia za kufundishia, kama hapa chini:

Kifungu cha 28 1. Serikali wanachama wanatambua haki ya mtoto kupata elimu, na pamoja na

nia ya kufanikisha haki hii endelevu na msingi wa fursa sawa, hasa:

(a) Kufanya elimu ya msingi iwe lazima na kupatikana bure kwa wote; (b) Kuchochea maendeleo ya aina mbalimbali ya elimu ya sekondari,

ikijumuisha elimu ya sekondari kwa jumla na elimu ya ufundi, kuhakikisha uwepo wake na upatikanaji wake kwa kila mtoto na kuchukua hatua madhubuti, mathalani utambulisho wa elimu ya bure na kutoa misaada ya kifedha endapo itahitajika;

(c) Kufanya elimu ya juu ipatikane kwa wote kwa vigezo vya uwezo kwa njia yoyote ile;

(d) Kuhakikisha maelezo na mwongozo kuhusu elimu na ufundi upo na unapatikana kwa watoto wote;

(e) Kuchukua hatua ya kuchochea mahudhurio shuleni na kupunguza viwango vya wanaoacha shule.

2. Serikali wanachama watachukua hatua muafaka kuhakikisha kwamba nidhamu ya shule inasimamiwa kwa namna ambayo inaheshimu utu wa kibinadamu wa mtoto na kwa kufuata Mkataba huu.

3. Serikali wanachama watachochea na kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika masuala yanayohusu elimu, kimsingi ikiwa na mtazamo wa kuchangia kuondoa ujinga na kutokujua kusoma na kuandika katika dunia yote na kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisayansi na kiufundi na mbinu za kisasa za kufundishia. Katika hili, mahitaji ya nchi zinazoendelea yatapewa kipaumbele.

Kifungu cha 29 1. Serikali wanachama wanakubali kwamba elimu ya mtoto itaelekezwa katika:

(a) Maendeleo ya haiba, vipawa, na uwezo wa kiakili na kimwili kwa mtoto kufikia ukamilifu wake;

(b) Maendeleo ya heshima kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi, na kwa kanuni kama zinavyoainishwa na Hati ya Umoja wa Mataifa;

(c) Maendeleo ya heshima kwa wazazi wa mtoto, asili yake ya kiutamaduni, lugha na tunu zake, kwa tunu za nchi ambayo mtoto anaishi, nchi ya asili yake na kwa ustaarabu tofauti na wa kwake;

Page 18: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 11

(UNGA, 1989) Kama inavyoonekana hapo juu, Kifungu cha 28 cha Mkataba wa Haki za Mtoto kinanukuu baadhi ya majukumu ambayo tumekwishayaona: elimu ya msingi ni ya lazima na ni ya bure, maendeleo zaidi ili kuanzisha utoaji wa elimu ya sekondari bure, na elimu ya juu kwa wanaostahili kwa vigezo. Kinajumuisha pia nyanja zingine ambazo hazijaainishwa bayana hadi sasa, kama vile, kufuatilia mahudhurio na wanaoacha shule, nidhamu kwa kufuata ―utu wa kibinadamu‖, na ufuatiliaji wa karibu katika kujua kusoma na kuandika, sayansi na teknolojia na njia za kufundishia. Kifungu cha 29 ndipo tunapoona maendeleo ya vipengele vya ubora. Elimu inapaswa kuelekezwa katika maendeleo ya jumla ya mtoto katika nyanja za haiba na uwezo wake; heshima kwa haki za binadamu; amali za wazazi, tamaduni, jamii na taifa kwa ujumla; na kujali mazingira. Kamati ya Haki za Mtoto, jopo la wataalamu wanaojitegemea 18, hufuatilia utekelezaji wa Mkataba huu na pia kutoa tafsiri zaidi. Ni kupitia maneno ya Kamati ndipo tunapoona undani wa Mkataba huu unapozungumzia elimu:

(Kamati ya UNCRC, 2001b) Kamati inazungumzia kwa kirefu kuhusu aina ya elimu sahihi kama vile njia ya kufundishia yenye kumshirikisha mtoto zaidi, kurudia mitaala na mazingira ya shule yenye amani yasiyo na ubaguzi, ukijumuisha kuzuia adhabu ya viboko. Chini ya Mkataba wa Haki za Mtoto, Serikali wanachama wanawajibika kutoa ripoti kwa Kamati mara kwa mara juu ya utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Mkataba huo. Serikali wanachama

Elimu yenye mizizi katika amali za kifungu cha 29(1) ni kwa ajili ya kila mtoto zana ya lazima katika jitihada za zake za kufanikisha katika maisha yake mwitikio chanya ambao ni rafiki wa haki za binadamu na unaounga mkono mabadiliko ya msingi yanayosababishwa na utandawazi, teknolojia mpya na mambo yanayohusiana nayo. Changamoto hizi zinajuimuisha mvutano kati ya mambo ya kimataifa na ndani ya nchi; mtu binafsi na watu kama kundi; tamaduni za asili na za kisasa; mitazamo ya muda mrefu na muda mfupi; mashindano na usawa wa fursa; kupanuka kwa maarifa na uwezo wa kutumia maarifa hayo; na masuala ya kiroho na halisia. Na bado, katika sera na mipango ya taifa na kimataifa juu ya elimu ambao kimsingi inabeba vipengele katika kifungu cha 29(1) vinaonekana kutokuwepo mara kwa mara au kuwepo kama wazo la baadaye.

(d) Matayarisho ya mtoto ya kumfanya awajibike na maisha yake katika jamii huru, katika nia ya kuelewa, amani, uvumilivu, usawa wa jinsia na urafiki miongoni mwa watu wote, makundi ya makabila, ya kitaifa na ya kidini na watu wa asili yake;

(e) Maendeleo ya heshima kwa mazingira asilia. 2. Ni marufuku kutafsiri sehemu yoyote ya kifungu hiki au kifungu cha 28 ili

kuingilia uhuru wa mtu binafsi na wa vyombo mbalimbali kuanzisha na kuelekeza taasisi za elimu, mara zote kwa kufuata kanuni kama zinavyoainishwa na aya ya kwanza ya kifungu hiki na matakwa kwamba elimu inayotolewa katika taasisi hizi itafuatana na kukubaliana na viwango vya msingi kama vitakavyoainishwa na Serikali.

Page 19: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

12 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

zinapaswa kutoa ripoti hizi miaka miwili baada ya kuridhia Mkataba halafu kila baada ya miaka mitano (UNGA, 1989, § 44(1)). 1.1.6 Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu Hatimaye, ukiwa umeanzishwa mwaka 2006, kuwekwa katika vitendo mwaka 2008 na kuridhiwa na Tanzania mwaka 2009, Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) unapanua haki ya kupata elimu kwa watu wenye ulemavu katika maana halisi zaidi ya upatikanaji. Haizungumzii tu kutokuwepo ubaguzi na kutokuwepo ujumuishaji lakini pia hatua ambazo Serikali zinatakiwa kuchukua kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanajumuishwa katika elimu, ukijumuisha matumizi ya maandishi maalum (Braille), lugha ya alama na aina nyingine mbadala za mawasiliano darasani, pia kuajiri walimu, wakiwemo pia wenye ulemavu, ili kufundisha kwa kutumia aina ya mawasiliano yaliyotajwa hapo juu na kuwafundisha waelimishaji wengine katika haya.

1.2 Mkataba wa Umoja wa Afrika Mwaka 1963 ulishuhudia kuundwa kwa Umoja wa Muungano wa Afrika (OAU), ambao Tanzania ilikuwa mwanachama mwanzilishi. Ukibadilishwa na kuwa Umoja wa Afrika (AU) mnano mwaka 2002, taasisi hii ilianzisha mikataba miwili inayohusu haki ya kupata elimu: Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (ACRWC), Tanzania iliridhia mikataba hii miaka ya 1984 na 2003. 1.2.1 Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Ukichukuliwa na OAU mwaka 1981 na kuridhiwa na Tanzania mwaka 1984, Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) uliwekwa katika vitendo mwaka 1986 na umeridhiwa na kila taifa la Afrika isipokuwa Morocco ambayo si mwanachama wa Umoja wa Afrika. Mkataba huu unafanana na Tamko la Dunia la Haki za Binadamu (UDHR) katika ujumla na ujasiri wake. Kuhusu elimu, unasema tu, ―Kila mtu atakuwa na haki ya kupata elimu‖ (OAU, 1981, §17). Na kama ambavyo Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni inavyoleta maana zaidi ya ICESCR, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeunda lakini bado haijatekeleza Rasimu ya Kanuni na Miongozo ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu mwaka 2009. Japokuwa ni ndefu sana, fungu lake linalozungumzia haki ya kupata elimu inanukuliwa kwa kirefu hapa chini, si tu kwa sababu ni nia ya ripoti hii kuwa kama rejeo kwa msomaji lakini pia ni kwa sababu ni vizuri kwa msomaji kusoma na kuona mwenyewe matumizi ya lugha na undani wa haki ya kupata elimu katika muktadha wa Kiafrika wakati mjadala kuhusu mfumo huu kisheria unavyozidi kuikaribia Tanzania:

55. Kila mtu atakuwa na haki ya kupata elimu.

56. Elimu ni haki ya msingi inayoathiri makuzi, maendeleo na ustawi wa binadamu, hususan watoto na vijana. Kama haki ya binadamu, elimu ni chombo cha msingi ambacho watoto na watu wazima walioko pembezoni kiuchumi na kijamii wanaweza kutumia kuondoa umaskini na kujipatia njia za kushiriki kikamilifu katika jamii zao. Elimu ina kazi kubwa ya kuwajengea uwezo wanawake, kuwalinda watoto kutoka katika kazi au utumikishwaji hatari na unyonyaji na unyanyasaji wa kingono, kuchochea demokrasia na haki za kibinadamu, kulinda mazingira na kudhibiti ongezeko la watu.

Page 20: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 13

57. Haki zilizoanishwa katika fungu la 17, miongoni mwa zingine, zinaweka wajibu ufuatao kwa nchi wanachama: i. Kuhakikisha kwamba watoto wote wanafurahia haki yao ya kupata

elimu ya msingi bure na kwa lazima kwa wote. Ni marufuku mtoto yeyote kutopata haki hii kwa sababu tu ya kukosa ada au gharama zingine za elimu. Hatua mahsusi zaweza chukuliwa ili kuhakikisha kwamba watoto walio katika mazingira magumu na hatarishi wanapata elimu hii bure. Ili kufikia lengo hili serikali zinalazimika kuongeza mara kwa mara rasilimali za kitaifa zinazotengwa kwa ajili ya elimu.

ii. Kuanzisha mfumo wa shule katika viwango vyote ambao utahakikisha kwamba elimu inafikika kwa urahisi na kuwezekana kwa wote kiuchumi (ikijumuisha utoaji wa fedha, ujenzi wa shule na utoaji wa zana za kielimu), kuanzisha utaratibu wa ufadhili wa masomo au elimu kwa marafiki, kuhakikisha elimu endelevu kwa walimu na wakufunzi ikijumuisha elimu kuhusu haki za binadamu na kuendeleza hali bora ya kazi na kiwango cha mafunzo kwa walimu.

iii. Kutunga sera ili kuondoa au kupunguza gharama za kuhudhuria shule za msingi ambazo zinajumuisha kuondoa karo, kutoa motisha kwa wale watakaohudhuria shule, kuondoa sare za shule au kupata sare za shule bure ambapo zipo, kutoa vitabu bure, kutoa usafiri bure au milo bure shuleni kuwavutia wanafunzi maskini shuleni.

iv. Kuhakikisha kwamba mifumo ya elimu inaelekezwa katika: a) Kuchochea na kuendeleza haiba, vipawa na uwezo wa kiakili

na kimwili kwa mtoto ili kufikia upeo wao bila ya ubaguzi; b) Kukuza heshima kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi

kwa kurejea zile zilizoainishwa katika nyaraka mbalimbali za Afrika zinazohusu haki za binadamu na watu na mikataba ile ya kimataifa;

c) Kuhifadhi na kuimarisha maadili, tunu za kitaifa na utamaduni wa Kiafrika wenye mtazamo mzuri;

d) Kumwandaa mtoto ili aweze kuwajibika kimaisha katika jamii huru, katika mwono wa uelewa, usawa, uvumilivu, majadiliano, kuheshimiana na urafiki miongoni mwa watu wote;

e) Kuchochea umoja na mshikamano wa Afrika na mafanikio yake;

f) Kuendeleza heshima kwa mazingira na mali asili; na g) Kuchochea uelewa wa mtoto kuhusu afya yake.

v. Kuhakikisha utoaji wa mpango wa elimu ya saikolojia jamii kwa yatima na makundi mengine yaliyotengwa.

vi. Kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa elimu ya sekondari, pamoja na elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi ya sekondari, kwa wote kwa kutumia njia muafaka zote na hasa katika kuanzisha na kuendeleza elimu bure.

vii. Kuhakikisha elimu ya juu na elimu ya baada ya sekondari yaani vyuo kupatikana kwa wote kwa kuzingatia uwezo, kwa njia muafaka zote, kwa kuhakikisha misaada ya fedha na mingineyo kwa wanafunzi katika elimu ya juu na kuanzisha elimu bure endelevu. Elimu ya chuo kikuu na elimu ya juu ni lazima ielekezwe katika mafunzo na tafiti zinazotakiwa ili kuhakikisha Afrika inajitegemea kisayansi na kiteknolojia.

Page 21: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

14 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

viii. Kuhakikisha kwamba taasisi za elimu ya juu zinawajibika katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na ulinzi wa uhuru na utu. Taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu viwezeshwe ili viweze kuchangia katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, kisayansi na kibinadamu kwa njia ya kufundisha wataalamu wa viwango vya juu na kutilia mkazo tafiti.

ix. Kuhakikisha upatikanaji wa gharama nafuu wa mafunzo ya ufundi na elimu ya watu wazima kama mambo ya msingi kabisa katika haki ya kupata elimu.

x. Kuhakikisha kwamba mipango ya elimu ya watu wazima inalenga katika kuondoa ubaguzi ndani ya jamii na kuwawezesha watu wa Afrika kufahamu kwa kina matatizo ya dunia ya kisasa. Mipango hii pia ni lazima izingatie vipaumbele vya taifa na uhalisia wa mambo. Serikali ni lazima zihakikishe uanzishaji wa taasisi kwa ajili ya mafunzo ya walimu wa elimu ya watu wazima. Matumizi ya lugha za Kiafrika yanatiliwa mkazo katika elimu ya watu wazima bila ulazima wa kuacha matumizi ya lugha za kigeni. Elimu ya watu wazima iwe endelevu na si tukio la mara moja.

xi. Kufundishwa kwa lugha za kitaifa za Afrika, kuanzishwa katika ngazi rasmi za elimu, hasa elimu ya msingi. Serikali zihakikishe kwamba matumizi ya redio, luninga, zana za kufundishia kwa kusikia na kuona na zana za kufundishia zinazotengenezwa katika nchi husika vitumike katika elimu hii.

xii. Kuhakikisha kwamba mtoto ambaye anaadabishwa shuleni au na wazazi anatendewa kwa utu na kwa heshima ya utu wake kama mtoto.

xiii. Kuhakikisha kwamba watoto wote, pamoja na watoto wote walio katika mazingira magumu na waliotengwa, wanapata na kufurahia haki sawa ya upatikanaji na uendelevu katika mfumo wa elimu, ikijumuisha pia kuangalia vikwazo vya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni vinavyosababisha kushindwa kwa mtoto wa kike kufurahia sawa haki ya kupata elimu. Inapolazimu, Serikali zinapaswa kuchukua hatua mahsusi ili kuhakikisha kwamba watoto waliotengwa na walio katika mazingira magumu wanahudhuria shule.

xiv. Kuhakikisha kwamba wasichana wanaopata mimba kabla ya kumaliza shule wanapata fursa ya kuendelea na masomo. Kuhakikisha kwamba watoto wote walioacha shule wanapata fursa ya kuhitimu elimu yao.

xv. Kuhakikisha usalama wa watoto wa shule kwa kuchukua hatua muafaka ili kuondoa unyanyasaji wa jinsia na wa kimwili unaofanywa na wanafunzi wengine, walimu, wafanyakazi wengine au wakuu wa shule; kuhakikisha usalama wa watoto wa shule wakati wa kwenda na kurudi kutoka shule wakiwa njiani; na kuanzisha au kutekeleza uzuiaji wa adhabu ya viboko.

xvi. Kuheshimu uhuru wa wazazi na walezi kuanzisha na kuchagua shule kwa ajili ya watoto wao, mbali na zile zilizoanzishwa na mamlaka ya umma, zinazoendana na viwango vya msingi katika elimu vinavyowekwa na Serikali, na kuhakikisha elimu ya maadili na dini kwa watoto inafundishwa kulingana na dhamira zao.

Page 22: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 15

(Tume ya ACHPR, 2009)

xvii. Kuhakikisha kuwa elimu inaelekezwa katika kukuza heshima na maendeleo halisi ya haiba ya mwanadamu. Elimu lazima iimarishe kuheshimu haki za binadamu katika jamii na uhuru wa msingi katika jamii, ushirikishaji wa watu wote katika jamii na kuchochea uelewa, uvumilivu na urafiki. Mfumo wa elimu ni lazima ujumuishe elimu ya haki za binadamu.

xviii. Kuhakikisha kwamba mipango yote ya elimu ni ya viwango vya juu na muafaka kwa mahitaji ya jamii. Elimu ni lazima iwapatie wanafunzi maarifa yanayotakiwa na tunu za kushiriki na kuchangia maendeleo ya kitaifa na kimataifa na kupata fursa za ajira. Elimu na mafunzo ni lazima vilenge katika maendeleo yenye msingi katika uhalisia wa Kiafrika, hasa kuelekea maendeleo ya sayansi ya teknolojia. Mitaala ya shule lazima ihusishwe soko la ajira na mahitaji ya jamii ya teknolojia na kujitegema, wakati huo huo ikizingatia maendeleo binafsi ya mtoto.

xix. Kuhakikisha uhuru wa elimu katika shule zote za taasisi zote za elimu ya juu.

xx. Kusaidia kuhama kwa watu bila kubughudhiwa ili kuchochea kubadilishana kwa uzoefu na mahusiano ya kiuchumi. Kutoa kipaumbele kwa ushirikiano katika kubadilishana kwa wataalamu na ambao ni nguvu kazi, hususan katika elimu na mafunzo, na kukomesha mwenendo wa wataalamu wa Kiafrika kutafuta kazi nje ya Afrika na kuwashawishi wataalamu Waafrika wanaoishi nje kurudi nyumbani.

xxi. Kuhakikisha utolewaji wa elimu bora ya msingi kwa bure kwa watoto wote wenye ulemavu inayojumuisha upatikanaji wa elimu bora ya sekondari kwa watoto wote kwa vigezo sawa na wanajamii wengine. Serikali ni lazima zihakikishe kwamba watu wenye ulemavu wanapewa msaada wanaohitaji, katika mfumo wa elimu kwa ujumla, ili kuwezesha elimu bora kwao. Serikali zinapaswa kuhakikisha hatua madhubuti zinatolewa katika mazingira yanayoboresha masomo na maendeleo ya jamaii, yakizingatia kwa kina lengo la ushirikishaji.

xxii. Kupiga marufuku na kuzuia ubaguzi wa aina yoyote katika elimu dhidi ya watoto kwa kuangalia hali ya afya yao kwa kudhania au kwa ukweli kuhusu UKIMWI na kuchukua hatua ili kuimarisha uwezo wa familia katika kuwatunza watoto walioathirika na VVU/UKIMWI na kuwapatia elimu rasmi.

xxiii. Kuangalia uhusiano kati ya elimu na ajira kwa watoto kwa kuhakikisha vichocheo vinatolewa ili kuwaweka watoto shuleni, kupanua fursa za kielimu kwa watoto wanaofanya kazi na kuongeza juhudi za kuwaondoa watoto katika ajira mbaya ya watoto na kuhakikisha wanapata nafasi katika mipango sahihi ya elimu.

xxiv. Kuboresha matokeo ya nguvukazi ya nyumbani juu ya elimu ya mtoto, na kuhakikisha kwamba mtoto wa kike hazuiliwi kupata elimu bora kwa sababu tu ya kutoa nguvukazi hii.

xxv. Kuhakikisha kwamba wafungwa na watu wengine walioko kizuizini, hasa watoto, wanapewa elimu rasmi na elimu ya ufundi ili kuongeza ujuzi na uwezo wao wakati watakaporejeshwa tena katika jamii.

Page 23: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

16 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

Kama inavyoonekana, haki ya kupata elimu si tu kwamba ni wazo au maoni ndani ya Umoja wa Afrika; ni dhana pana yenye malengo na majukumu. Kama inavyoonekana, maendeleo ya haki ya kupata elimu kama inavyoainishwa na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ni mchanganyiko mpana wa mambo mbalimbali kutoka katika mikataba mingine kama vile Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, Maoni ya Jumla kutoka Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, Mkataba wa Haki za Mtoto, Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto, Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, na Tamko la Semina ya Pretoria juu ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Afrika. Kwa kuwa na vifungu vya nyongeza kuhusu lugha, utamaduni, na utambulisho wa Kiafrika, Rasimu ya Kanuni na Mwongozo wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu kwa namna mbalimbali ni aina ya Kiafrika ya kujumuisha yanayoimarishwa katika mikataba ya Umoja wa Mataifa kama tulivyokwisha kuona, ikiainisha mambo mengi kama vile elimu ya msingi ya lazima na ya bure, elimu ya juu iendelezwe kuwa bure, A-4, malengo ya elimu, kupiga marufuku adhabu ya viboko na kuondoa ubaguzi. Ulinganifu huu unaendelea kwa jinsi ambavyo Rasimu ya Kanuni na Mwongozo wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu inavyoonesha majukumu ya Serikali katika haki za binadamu. Hapa tena tunaona A-4 (ila safari hii inajumuisha uwepo, utoshelevu, unafuu na kukubalika); wajibu wa kuheshimu, kulinda, kutimiza na vilevile kuchochea; dhamira katika rasilimali zote zilizopo; utekelazeji endelevu; majukumu ya msingi; kutokuwepo ubaguzi na kupiga marufuku hatua za kurudisha nyuma (Tume ya ACHPR, 2009, Kifungu II: Aina ya wajibu wa nchi wanachama). Kwa kurudia tena, katika njia nyingi, Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu na Rasimu ya Kanuni na Mwongozo wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni ni namna ya Kiafrika ya kuifanya Tamko la Dunia la Haki za Binadamu na Maoni ya Jumla kutoka Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni ziwe za nyumbani zaidi. Kusema kweli, tanbihi 444 za Rasimu ya Kanuni na Mwongozo wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu zinarejea sana ICESCR na Kamati yake. 1.2.2 Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto Kukubalika kwa mikataba ya kimataifa barani Afrika kuliendelea mwaka 1999 ambapo OAU ilianza kutumia Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Watoto (ACRWC). Ukichuliwa na OAU mwaka 1990, ACRWC uliridhiwa na Tanzania mwaka 2003. Kama ambavyo Mkataba wa Haki za Mtoto unatoa haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, pia ACRWC inatoa haki hizo. Ibara ya 11 kuhusu elimu inasomeka kama ifuatavyo:

Kifungu cha 11: Elimu 1. Kila mtoto ana haki ya kupata elimu. 2. Elimu ya mtoto itaelekezwa:

(a) Kuchochea na kuendeleza haiba, vipawa na makuzi ya kiakili na kimwili ya mtoto kufikia malengo yake;

(b) Kuchochea heshima kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi mahsusi kwa zile zinazoainishwa katika vifungu vya mikataba mbalimbali ya Afrika juu ya haki za binadamu na watu na mikataba na matamko mbalimbali ya kimataifa;

(c) Kuhifadhi na kuimarisha maadili, mila na desturi safi za Kiafrika;

Page 24: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 17

(OAU, 1990) Kama inavyoonekana, Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto ni rejea ya Mkataba wa Haki za Mtoto lakini inaongeza msisitizo katika wasifu wa nje, utamaduni na umoja wa Kiafrika. Endapo mtu atalinganisha mkataba huu na dondoo za Mkataba wa Haki za Mtoto hapo juu, unaweza kuona kwamba mengi yanayoainishwa na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto kuhusu elimu yamenukuliwa neno kwa neno toka Mkataba wa Haki za Mtoto. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo ni mapya, hasa hatua madhubuti za kielimu kuchukuliwa ili kuhakikisha elimu kwa wasichana kwa ujumla na hasa kwa wao wanaopata mimba.

(d) Kumwandaa mwanafunzi ili kuwajibika kimaisha katika jamii iliyo huru, katika mwono wa uelewa, uvumilivu, mjadala, heshima kwa kila mmoja na urafiki miongoni mwa watu wa makabila yote, makundi ya kijamii na makundi ya dini;

(e) Kuhifadhi uhuru wa kitaifa na uadilifu wa mipaka yake; (f) Kuchochea mafanikio ya Umoja na Mshikamano wa Afrika; (g) Kuendeleza kujali mazingira na maliasili; (h) Kuchochea uelewa wa mtoto juu ya afya ya msingi.

3. Serikali Wanachama katika Mkataba huu zitahakikisha zinachukua hatua muafaka wakiwa na mwono wa kuitimiza haki hii na watafanya yafuatayo: (a) Kutoa elimu ya msingi bure: (b) Kuchochea maendeleo ya elimu ya sekondari katika aina zake zote

tofauti na kuiendeleza na kuifanya kuwa ya bure na kwa wote; (c) Kuifanya elimu ya juu ipatikane kwa wote kwa kuzingatia vigezo vya

uwezo kwa njia zote muafaka; (d) Kuchukua hatua ili kuchochea mahudhurio shuleni na kuondoa idadi

ya wanaoacha shule; (e) Kuchukua hatua mahsusi kuhusu wasichana, watoto wenye vipawa na

wao waliotengwa, kuhakikisha upatikanaji sawa wa elimu kwa makundi yote katika jamii.

4. Serikali Wanachama katika Mkataba huu wataheshimu haki na wajibu wa wazazi, na inapobidi, wa walezi kisheria, kuchagua shule kwa ajili ya watoto wao, mbali ya zile zilizoanzishwa na mamlaka za serikali, ambazo zinaendana na viwango vya lazima vilivyowekwa na Serikali, kuhakikisha elimu ya maadili na dini ya mtoto inazingatia makuzi na uwezo wa mtoto.

5. Serikali Wanachama katika Mkataba huu watahakikisha wanachukua hatua muafaka kuhakikisha kwamba mtoto anayeadabishwa shuleni au na wazazi anatendewa kwa utu na heshima yake inatunzwa kama mtoto na kuzingatia Mkataba huu.

6. Serikali Wanachama katika Mkataba huu watachukua hatua muafaka ili kuhakikisha kwamba watoto wanaopata mimba kabla ya kumaliza masomo yao watapata fursa ya kuendelea na masomo kwa kuzingatia uwezo wao binafsi.

7. Hakuna kipengele chochote katika Kifungu hiki kitatafsiriwa kwamba kinaingilia uhuru wa mtu binafsi na vyombo mbalimbali kuanzisha na kuelekeza taasisi za elimu kwa kufuata kanuni zilizoainishwa katika aya ya 1 ya Kifungu hiki na takwa la kielimu linalotolewa katika taasii hizi litazingatia viwango vya msingi vya elimu iliyowekwa na Serikali.

Page 25: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

18 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

1.3 Mikataba ya Jumuiya ya Afrika Tukitoka katika bara la Afrika kwa ujumla wake na kuelekea sehemu za Afrika Mashariki na Kusini, haki ya kupata elimu inaelekeza safari yake kwa Tanzania. Ikijumuisha Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Ushelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ilianzishwa mnamo mwaka 1992. Tanzania pia ni mwanachama mwanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ilianzishwa tena rasmi mwaka 2000 na inajumuisha Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania. 1.3.1 Mkataba wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Mkataba wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika ulianzishwa mwaka 1992, Tanzania ikiwa ni mojawapo ya nchi wanachama waanzilishi na ulianza kufanya kazi mwaka uliofuata. Mkataba huu hauainishi haki yoyote kuhusu elimu na huzungumzia kwa jumla ―haki za binadamu demokrasia na utawala wa sheria‖ (SADC, 2001, §4(c)) bila ya kuwa wazi au kurejea mkataba wowote kuhusu haki hizo. 1.3.2 Mkataba wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika juu ya Elimu na Mafunzo

Miaka mitano baada ya kuanzishwa kwa Mkataba wa SADC, Mkataba wa SADC juu ya Elimu na Mafunzo ulianzishwa. Mkataba huu ulitiwa saini mwaka 1997 na nchi 12 za SADC ambao ni wanachama, Tanzania ikiwamo, Tanzania iliridhia na nchi zingine nane na ukaanza kutumika mwaka 2000. Mkataba huu mdogo una lengo la kuchochea usawa wa kikanda katika masuala ya sekta ya elimu—msingi, sekondari, elimu ya juu, elimu ya watu wazima ufundishaji n.k.—katika nchi zote za SADC ili kuleta maendeleo ya juu kabisa katika rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii katika ukanda wote (SADC, 1997). Hata hivyo, unatoa mchango kidogo sana kuhusu haki ya kupata elimu. Kwa kutumia maneno ya Karola Hahn na Kitengo cha Uchumi Sera na Utafiti cha Namibia,

Tabia ya kisheria ya mkataba unafanana zaidi na ―tamko la nia ya ushirikiano‖ au Makubaliano ya Kiitifaki‖ kuliko agenda ya kisiasa yenye kuwajibisha Serikali na taasisi za elimu ya juu masuala yote muhimu na malengo yanaelezwa kwa miundo laini (itakuwa, itafanya, itatokea, itafanya kazi, itatunzwa n.k.).

(Hahn, 2005, uk. 15)

Kwa sababu ya lugha hii, Mkataba huu ―hauna nguvu rasmi kama ‗sheria ya kanda,‘‖ na pia ―hakuna majukumu au wajibu unaowabana wanachama kisheria, unaoweza kusomeka toka katika Mkataba‖ (2005, uk. 16). Vile vile, ―hakuna chombo cha kutekeleza adhabu au vikwazo‖ endapo mwanachama atashindwa au kukataa kutekeleza maelekezo ya mkataba (2005, uk. 16). 1.3.3 Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Waraka unaohuisha EAC, Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulianzishwa mwaka 1999 na kuanza kutumika mwaka 2000, Tanzania ikiwa ni nchi mwanzilishi. Japokuwa haitamki bayana kuhusu haki ya kupata elimu, inaziwajibisha nchi wanachama kwa ACHPR:

Page 26: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 19

(EAC, 2007, §6) Japokuwa hii inaichukua ACHPR katika kiwango cha juu zaidi, yaani EAC, kumbuka kwamba kile ambacho ACHPR inakisema kuhusu haki ya kupata elimu imewekewa mipaka sana (―Kila mtu binafsi atakuwa na haki ya kupata elimu‖ [OAU, 1981, §17]), na maana yake zaidi katika siku za usoni yaweza kunukuliwa toka ACHPR. Wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zaweza kufungwa na ACHPR, si lazima sana zifungwe na tafsiri ya Tume ya Afrika ya Mkataba huu.

1.4 Sheria ya Ndani Tanzania Hatimaye tumekuja katika sheria ya nchi yenyewe yaani Tanzania. Japokuwa haki ya kupata elimu haijaainishwa lakini kama ilivyo kimataifa, bado kuna mambo fulani ya msingi ya kuangalia. 1.4.1 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marekebisho ya mwaka 1984 kwa katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huainisha haki ya kupata elimu kama inavyoelezwa katika kifungu cha 11:

(URT, 1998, §11) Wakati hii inaonekana kama ndio mwanzo, haki ya kupata elimu katika Katiba ya Tanzania kwa bahati mbaya inaangukia katika vifungu vya katiba ambavyo haviwezi kudaiwa kwa njia ya mahakama (URT, 1998, §7(2)), na hivyo kuifanya haki ya elimu iwe jambo lisiloweza kutimizwa. 1.4.2 Sheria ya Elimu Sheria ya Elimu, ikianzishwa mnamo mwaka 1978, kufanyiwa marekebisho miaka 1995 na 2002 na sasa hivi inafanyiwa mapitio, ni sheria ya kwanza kabisa ya elimu nchini Tanzania. Wakati ikishughulikia zaidi muundo na masuala ya utawala, sheria hii inaainisha mambo kadhaa ya msingi kuhusu haki ya kupata elimu:

Kanuni za msingi ambazo zitasimamia utekelezaji wa malengo ya jumuiya na nchi wanachama zitajumuisha:… (d) utawala bora ukijumuisha kuzingatia kanuni za demokrasia, utawala wa

sheria, uwajibikaji, wazi haki za jamii, fursa sawa, usawa wa jinsia, na pia kutambuliwa kuchochea na kulinda haki za binadamu na haki za watu wote kwa kuzingatia vipengele vilivyoko katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu;

11. (1) Mamlaka za Serikali zitatengeneza vifungu muafaka ili kutimiza haki ya mtu kufanya kazi, kupata elimu, na huduma ya jamii wakati wa uzee wake, ugonjwa au kutokujiweza katika hali yoyote ile, bila kuathiri haki hizo zote. Mamlaka za Serikali zitahakikisha kwamba kila mtu anajipatia riziki yake. (2) Kila mtu ana haki ya kupata elimu na kila mtu atakuwa huru kujitafutia elimu katika eneo la chaguo lake hadi kiwango cha juu kwa kuzingatia au kulingana na uwezo wake na stahiki yake. (3) Serikali itahakikisha kwamba, kuna fursa sawa na za kutosha kwa watu wote, kuwawezesha kujipatia elimu na ufundi na mafunzo katika ngazi zote za shule na taasisi zingine za elimu.

Page 27: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

20 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

(URT, 1978, kama ilivyorekebishwa 2002) Wakati kuna vipengele vya msingi vinavyoenda sambamba na mfumo wa kisheria kuhusu haki ya kupata elimu ambayo tumekwishaona—mathalani elimu ya msingi kuwa ya lazima na bure kwa wote pamoja na swali la mahudhurio—kuna maswali mengi yanayoibuka kuhusu Sheria ya Elimu ambayo

35.-(1) Itakuwa ni lazima kwa kila mtoto aliyefikisha umri na miaka saba kuandikishwa shule kwa ajili ya elimu ya msingi.

(a) Bila kuathiri kipengele kidogo cha (1) ni marufuku kumkatalia usajili mtoto yeyote aliyetimiza miaka saba.

(2) Mzazi au wazazi wa kila mtoto aliyeandikishwa shule watahakikisha kwamba kila mtoto aliyeandikishwa shule ana hudhuria shule mara zote hadi atakapohitimu elimu yake ya msingi. (3) Kila mtoto aliyeandikishwa katika shule ya serikali atahudhuria shule mara zote katika shule aliyoandikishwa hadi atakapohitimu kipindi kilichoainishwa katika mtaala wa taifa, wa kiwango cha elimu ambacho anatakiwa kukikamilisha. (4) Waziri atatunga kanuni, zitakazochapwa katika gazeti la serikali, kwa nia ya kuhakikisha utimizaji wa malengo yaliyoainishwa katika sehemu hii, katika kanuni hizo, matendo au vitu ambavyo vitafanywa na mtu na adhabu endapo mtu atavunja kanuni hizo. 35A. Kila mtoto aliyetimiza miaka mitano atastahili kuandikishwa shule ya awali kwa kipindi cha miaka miwili. 56. (1) Kwa mujibu wa sera ya taifa kuhusu elimu ya taifa na kuhusu mipango mingine ya taifa na vipaumbele vyake vinavyotolewa mara kwa mara, kila raia atastahili kupokea aina hii ya elimu, na kiwango cha elimu ya taifa kama ambavyo uwezo wake utaruhusu. (2) Hakuna mtu yeyote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakayekataliwa aina yoyote ya elimu, au kiwango chochote cha elimu kwa sababu ya rangi yake, dini yake au msimamo wake kiimani au kisiasa. Ili mradi shule yoyote katika taratibu zake za kurajisi, itawapatia kipaumbele raia wa Jamhuri ya Muungano. (3) Kila shule itaweka somo la dini katika mtaala wake ili kufundishwa kwa wanafunzi wakiwa katika majengo ya shule, na pia hakuna mwanafunzi yeyote atakayelazimishwa kuhudhuria darasa la dini yoyote au ibada yoyote kinyume na dhamiri au matakwa yake binafsi kama amezidi umri wa miaka kumi na nane, au kinyume na matakwa ya wazazi au walezi wake kama hajafikisha umri wa miaka kumi na nane. (4) Hakuna kitu chochote katika sehemu hii kitatafsiriwa kana kwamba kinalazimisha au kufanya kuwa ni lazima kwa shule yoyote au walimu wa shule yoyote, katika nafasi zao rasmi kama walimu, kusimamia au kufundisha elimu ya dini au kuongoza ibada. 57. Ni marufuku kutoza michango au ada yoyote kama sharti la kumwandikisha mtoto shule au kuhudhuria shule katika shule yoyote binafsi bila ruhusa ya Kamishna. 58. Kwa amri ya maandishi, Waziri anaweza kupiga marufuku matumizi ya kitabu chochote shuleni au elimu fulani kwa sababu yoyote ile atakavyoona inafaa.

Page 28: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 21

yanahitaji kujadiliwa na kuainishwa. Kwanza, wakati sheria inahitaji elimu ya msingi kuwa lazima, haihitaji kuwa ni ya bure. Pili, ijapokuwa Tanzania imeridhia mikataba kadhaa kikanda na kimataifa, kama vile ICESCR, CADE, CEDAW, CRC, ACHPR na ACRWC, ambayo inapiga marufuku unyanyasaji wa kijinsia, Sheria ya Elimu ya Tanzania iko kimya katika hili (na aina nyingine za ubaguzi) katika kipengele chake kinachohusu ubaguzi (URT, 1978, §56(2)). Tatu, mamlaka kubwa sana ya kuchunguza na kusimamia yamewekwa kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, anayeweza yeye peke yake kupiga marufuku matumizi ya vitabu fulani bila kuwa na maamuzi ya busara—―kwa sababu yoyote atakayoona inafaa‖ (URT, 1978, §58). Hatimaye, badala ya kufuta adhabu ya viboko, marekebisho ya mwaka 2002 kuhusu Sheria ya Elimu kimsingi inairasmisha adhabu husika: ―kwenye mikono yake au kwenye matako yake ambayo kwa kawaida hufunikwa kwa kutumia fimbo nyepesi…‖ (URT, 2002b, GN 294). 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto Mnamo mwaka 2009, Tanzania ilipitisha Sheria ya Haki za Mtoto. Wakati sheria hii imeshuhudia kuingizwa katika sheria ya nyumbani mambo mengi ya CRC kama vile kulindwa watoto, makazi, matunzo, kusali, ajira kwa watoto na uzuiaji wake na haki ya kupata elimu pia, inashindwa kubeba uzito na maana sawa kama inavyoainishwa katika CRC. Sheria ya Haki za Mtoto inaelezea elimu kwa watoto, ikisema kwamba watoto wana haki ya kupata elimu, kwamba wazazi au walezi wana wajibu wa kuwapatia watoto wao elimu, kwamba mtu mwingine yeyote hana haki ya kuwanyang‘anya watoto hawa elimu au haki hiyo, kwa haki sawa, na mengine mengi yanayohusu matunzo ya watoto:

(URT, 2009c) Hata hivyo, kwa sababu ya utata wake, Sheria ya Haki za Mtoto kwa taathira yake inalinda haki ya mtoto kupata elimu wakati haielezi kwa kina: ―elimu ya msingi‖ inafafanuliwa kuwa ―elimu rasmi inayotolewa kwa mtoto kwa kiwango kinachotolewa mara kwa mara‖ (URT, 2009c, §3). Ikiwa mahakamani mtu anaweza kuitafsiri kuwa kile kinachoonekana kuwa elimu ya msingi, tafsiri hii na vifungu vyake juu ya elimu haitamki chochote kuhusu gharama zake. Zaidi sana, kwa sheria pana inayohusu mtoto na matunzo yake, na kulindwa kwa mtoto, haifuti adhabu ya viboko.

1.5 Mazingatio Mengine Zaidi Kisheria Mfumo huu wa mwisho nchini ni kikwazo kikubwa katika uwezekano wa kudai haki ya elimu Tanzania katika mfumo wetu wa mahakama. Vilevile kama Kenya na Uganda pamoja na Marekani na Uingereza, Tanzania inasimama katika mfumo wa sheria unaozingatia sheria za ndani na zile za kimataifa—tafsiri yake ni kwamba kuna tofauti kati ya sheria za nyumbani na za kimataifa na tofauti

8.- (1) Itakuwa ni wajibu wa mzazi, mlezi au mtu yeyote mwingine anayeishi na mtoto, kumtunza mtoto huyo, hasa wajibu huo unaompatia mtoto haki ya - … (e) Elimu na mwongozo; … (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumnyima mtoto haki ya kupata elimu, chanjo, chakula, nguo, malazi, huduma ya afya na tiba au kitu kingine chochote kinachotakiwa kwa ajili ya maendeleo yake. … (6) Mtoto mwenye ulemavu ana haki ya kupata matunzo maalum, matibabu, uwezeshaji wenye kumudu kwa ajili ya matibabu yake na fursa sawa ya elimu na mafunzo kila inapobidi ili kumwendeleza kwa kiwango cha juu kwa kadri ya uwezo wake ili aweze kujitegemea. 9.- (1) Mtoto atakuwa na haki ya kuishi, utu, heshima, furaha, uhuru, afya, elimu na malazi kutoka kwa wazazi wake.

Page 29: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

22 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

hiyo kimsingi inamaanisha kwamba sheria za kimataifa hazitumiki moja kwa moja mahakamani. Ijapokuwa zinaweza kurejewa kulitia nguvu shauri, kwa mkazo kabisa zaweza kutumika tu pale zinapokuwa zimeandikwa katika muktadha wa sheria za ndani ya nchi, kama ilivyo kwa CRC na Sheria ya Haki za Mtoto. Kukiwa na haki ya kikatiba ya kupata elimu ambayo huwezi kuidai mahakamani, sheria ya elimu ambayo baadhi ya haki hazijawekwa katika msingi wake na sheria ya haki za mtoto inayohakikisha kwamba watoto wana haki ya elimu isiyokuwa na mfumo wa uhakika, inatia shaka (ukiangalia tu muktadha wa sheria) endapo shauri la kutafuta haki ya elimu linaweza kufanikiwa katika mahakama za ndani kuliko labda shauri la kibaguzi katika kupata elimu ya msingi—kesi ya msichana aliyepewa mimba kufukuzwa shule ya msingi inaweza kuwa na mafanikio makubwa zaidi kwenye mahakama za ndani. Halafu, kuna mahakama za juu. Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, ilioanzishwa na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ina mamlaka juu ya tafsiri na matumizi ya Mkataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC, 2007, §27(1)), lakini kwa sasa haisikilizi kesi zinazohusu uvunjaji wa haki za binadamu, ijapokuwa inatarajia kuwa na mamlaka ya aina hii siku za usoni. Chombo kingine cha kikanda kinachofanana na hicho, Mahakama ya SADC, ijapokuwa ―si mahakama ya haki za binadamu katika mantiki yote…imeamua kwamba ina mamlaka ya kusikiliza kesi zinazohusu haki za binadamu kwani mojawapo ya kanuni za SADC ni kusimamia na kuangalia haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria‖ (Mahakama ya SADC, 2010, uk. 3; SADC, 2001, §§16(1), 4(c)). Hata hivyo, kanuni zisizowazi za ―haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria‖ kama zilivyotolewa na Mkataba wa SADC (SADC, 2010, §4(c)) zinaleta matarajio hafifu kuhusu matumizi yake kwenye mahakama. Mahala pengine pa kuongelea katika siku za usoni patakuwa ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, iliyoanzishwa mwaka 2004 (na itaunganishwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu). Tanzania yenyewe iliridhia mkataba wa kuanzisha Mahakama ya Afrika mwaka 2006. Kwa mujibu wa mkataba unaoanzisha Mahakama ya Afrika, kila nchi inayotaka kuruhusu raia wake kwenda moja kwa moja kwenye Mahakama ya Afrika hiyo lazima itoe rasmi tamko linaloruhusu watu wake kwenda moja moja kwenye mahakama hiyo. Tanzania bado haijatoa tamko hilo. Kwa sasa, hii inamaanisha kwamba kwa uzuri zaidi, kesi za haki za binadamu zinaweza kusikilizwa na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Tume ya Afrika inasikiliza malalamiko toka kwa watu binafsi na vyama vya hiari, kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu zinazolindwa na ACHPR, hutoa mapendekezo kwa nchi husika, na itashauri kesi husika kupelekwa katika Mahakama ya Afrika kama nchi husika watashindwa kutekeleza mapendekezo; Mahakama ya Afrika itasikiliza na kutoa maamuzi. Hata hivyo, Tume ya Afrika husikiliza malalamiko haya endapo tu njia au suluhisho zote zilizopo nchini zimefuatwa, maana yake ni kwamba kesi imepelekwa kwanza mahakama za nchi. Kwa hiyo, kesi, mathalani inayohusu adhabu ya viboko inaweza isifanikiwe katika mahakama za ndani ya nchini kwa sababu tu sera za nchi zinakubali adhabu hiyo lakini inaweza kupelekwa katika Tume ya Afrika, na hatimaye katika Mahakama ya Afrika kwa sababu imekuwa wazi kwamba inapingana na Kanuni na Miongozo ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika ACHPR (kama zimeridhiwa) zinazozungumzia ―kupiga marufuku matumizi ya adhabu ya viboko‖ (Tume ya ACHPR, 2009, §57(xv)). Hata hivyo, mara nyingi hakutakuwa na suluhisho kwa ajili ya ukiukwaji wa haki ya kupata elimu, ambayo inaweza kuwaruhusu wanaokwazika kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Tume ya Afrika.

2.0 Mazingira ya Kisiasa Ijapokuwa matarajio ya majibu bayana na utabiri vyaweza kufikiriwa wakati wa kuangalia muundo wa kisheria, ukweli unatisha, haijalishi ni katika nchi gani mtu anaishi. Nia ya mfumo huu ni

Page 30: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 23

kuhakikisha sera na sheria zipo wazi na zinaainisha mambo yote na matumizi yake pia, lakini si rahisi namna hiyo. Sheria haziwezi tu kuwekwa na kuchujwa ili kubainisha matokeo. Uimara wa mahakama, unyofu na uadilifu wa mahakama, usimamizi wa serikali, umahiri wa anayesimamia kesi, mitazamo binafsi na aina zingine za rushwa, kwa wepesi zaidi, vinafanya mambo kuwa magumu. Matokeo ya kesi, mathalani kesi dhidi ya Serikali, ambayo mara nyingi ni kesi ya kupigania haki ya kupata elimu, kwa kiwango kikubwa inategemeana na uimara wa mfumo wa mahakama. Je, inaona kwamba ina ubavu wa kuamua dhidi ya Serikali? Kama ndivyo, je, ina mbinu za kutosha kuhakikisha kwamba Serikali inatimiza amri za mahakama? Katika hili kuna suala la uadilifu wa majaji. Je, wanajua maana halisi ya haki ya kupata elimu na kwamba wataweza kuamua sawasawa? Je, wanafungwa na mitazamo ya kisiasa au ya kwao wenyewe? Je, wako tayari kulaumiwa kwa hili? Je, kuhusu Serikali? Inachukuliaje katika mfumo mzima wa mahakama? Je, inachukuliwa kama chanzo sawa na cha thamani kuhusu haki ya elimu au ni kikwazo na iko tayari tu kuendelea na agenda yake? Na wanasheria, je, wako tayari na wana uwezo wa kusimamia kesi hizi? Nchi inayopigania matokeo ya elimu, inapigania haki hii katika ngazi zote, hata kama mtu ni profesa, daktari, au wakili, na Tanzania haiondolewi katika kundi hili. Kwamba mtu fulani ni maarufu katika uwanja wa sheria, haina maana kwamba ana uwezo wa kusimamia kesi za aina hii—kwa kesi ngumu ya haki za msingi ambayo yaweza kuwa ni dhidi ya Serikali na anaweza kuipeleka katika mahakama ya kimataifa. Kuonesha ni kwa jinsi gani mambo haya ya kisiasa yanafanya kazi katika mahakama za Tanzania, hebu angalia kesi hii ya hivi karibuni: Mnamo mwaka 2006, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa maamuzi dhidi ya Serikali katika kesi iliyoomba Mahakama itamke kwamba marekebisho ya Katiba yaliyozuia mgombea binafsi kuwa ni kinyume cha Katiba, watu binafsi (ambao hawako na chama chochote) cha siasa wasiweze kugombea uraisi au ubunge, Serikali ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huu, na hoja za msingi zilitolewa na Naibu Mwanasheria Mkuu kwamba hakuna mahakama yoyote nchini Tanzania iliyo na mamlaka kuamua juu ya uhalali wa Katiba, kwamba Mahakama Kuu haikuwa na mamlaka ya kusikiliza juu ya marekebisho ya Katiba na kwamba ilivyofanya hivyo ilikosea kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa wakati wa kutolea maamuzi katika shauri hili. (katika hili ni UDHR). Mahakama ya Rufaa ilimpatia Naibu Mwanasheria Mkuu nakala ya Katiba, na pia kumsomea baadhi ya vipengele kwa sauti, ili kuainisha kile kilichoonekana kuwa wazi kabisa: kwamba Mahakama Kuu ndio hasa chombo chenye mamlaka ya kuamua kuhusu masuala ya Katiba, na kwamba inayo mamlaka ya kutamka kwamba kipengele fulani ni kinyume na Katiba kwa hiyo ni batili, na hata kipengele ambacho kimekuwa sehemu ya Katiba yenyewe (James, 2010). Naibu Mwanasheria Mkuu alionekana kuleta hoja kwamba kama Bunge linapitisha marekebisho ya Katiba, hayawezi tena kupingwa kwani sasa ni sehemu ya Katiba. Kusema kweli, kama mfumo ungekuwa hivi, kusingekuwa na uangalizi katika sheria ya wengi, na kwa sababu hiyo Mahakama Kuu ilianzishwa kwa mujibu wa Katiba ili kushughulikia masuala kama haya. Kwa UDHR, marekebisho ya Katiba yalikuwa yanakinzana na haki zenye kuweza kupiganiwa kama zinavyoainishwa na Katiba ya Tanzania, na hii ilinukuliwa katika uamuzi. Mahakama ilivyotamka UDHR ilirejea tu hoja za msingi kama zilivyowakilishwa na kesi husika. Katika muktadha wa kisiasa, kesi hii (ambayo ina umri wa miaka 16 malumbano ya kisheria yanayohusu kuwepo kwa mgombea binafsi wa urais na ubunge) ina maeneo mengi ya kuangaliwa. Kwanza, kama inavyoonekana hapa na katika vyombo vya habari, mbinu ya Serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu alionekana kutaka kuiburuza Mahakama—kuionesha Mahakama kwamba ―huna nguvu‖ kwa kuwa na matarajio kwamba malalamiko yao yapokelewe bila kuhojiwa tu, kwa sababu yanatoka kwa Serikali. Japo matarajio haya na tabia ya Serikali inashuhudia kwa kiwango fulani kuwa na Mahakama yenye kulegea (kwa mfano, mbinu hii yawezekana kabisa iliwahi kufanya kazi huko nyuma kama inatumika sasa hivi), hata hivyo Mahakama haikunywea na ikafanya kazi yake katika mfumo wa uwajibikaji. Pia, sababu za mbali za kijamii zaidi, Mahakama ilizonukuu katika uamuzi

Page 31: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

24 Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii

wake, inaleta matumaini kwamba upo uwezekano wa kushinda katika kesi ya haki ya kupata elimu nchini Tanzania katika mahakama za ndani. Katika kesi hii, si tu kwamba Mahakama iliona marekebisho kukinzana na haki fulani fulani zinazotolewa na Katiba ya Tanzania bali pia kwa ujasiri zaidi ilitamka kwamba ―ni vizuizi visivyo lazima na visivyo na sababu za msingi kuhusiana na haki za msingi za raia‖ (James, 2010). Mahakama iliendelea mbele kuelezea pia kuhusiana na UDHR, japo haikuwa lazima kisheria kuangalia mikataba hii wa kimataifa. Hata hivyo kesi hii haikukomea hapo. Mnamo tarehe 17 mwezi wa 6, Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu yake kuzuia uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu wagombea binafsi katika chaguzi kuu. Jaji Mkuu (wa wakati huo) Augustino Ramadhani alitamka, ―Suala la mgombea binafsi linapaswa kutatuliwa na Bunge kwa sababu ni suala la kisiasa na si kisheria‖ (Consesa, 2010). Uamuzi wake wa kujiondoa katika mfumo wa kuangaliana na kuwajibika uliibua maswali toka kwa wasomi, wataalamu wa sheria, wanasiasa, na wanaharakati wa haki za binadamu. ―Maamuzi ya Mahakama ya kurudisha katika Bunge suala linalohitaji tafsiri ya kisheria inamaanisha kwamba Mahakama imeshindwa kutumia mamlaka yake iliyopewa na Katiba,‖ Francis Kiwanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, aliripoti (Citizen Reporters, 2010). Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki na Chama cha Wanasheria Tanganyika walikutana na wasomi, wanasheria, watu wa mahakama, wanachama wa vyama vya hiari na wasajili wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, na mjadala wa kupeleka shauri hili katika Mahakama ya Afrika unaendelea. Mfano huu unaweza kutafsiri kuwa ni kesi halisi katika kuangalia uadilifu na umakini wa mahakama ya Tanzania, athari za misukumo ya kisiasa na uwezo katika kuamua haki, iwe ndani au kimataifa, kwa jinsi zinavyotumika katika mahakama za Tanzania. Muktadha huu ni lazima kukumbukwa wakati wa kutumia njia ya mahakama katika kupigania haki ya kupata elimu nchini, na kesi ya aina hii iwe tayari kupelekwa katika Mahakama ya Afrika kwani mahakama za ndani za Tanzania zaweza kuamua kwamba haki hii ni ―suala la kisiasa na si suala la kisheria.‖

3.0 Muktadha wa Kijamii Mojawapo ya mwitikio wenye nguvu sana kuhusu masuala ya kisiasa yenye upotofu kwa mfumo wa sheria; ni msukumo toka kwa raia. Raia kujua masuala haya na kuyaongelea ni jambo la msingi sana katika kuleta ufumbuzi nchini Tanzania. Kuwajibika kwa mtu binafsi ni adimu sana lakini mabadiliko ya kimfumo polepole yanatokea. Wakati jamii inauelewa na inaonesha kwamba inajua, Serikali itaanza kuifikia, haijalishi kwamba inataka kufanyia kazi vipaumbele vya umma au inajua kwamba sasa haiwezi kukwepa tena majukumu haya. Uelewa huu katika jamii, ni wa lazima; vinginevyo jamii yaweza tu kuambiwa uongo, kama inavyosemekana kwamba jambo hili limetokea katika Kampeni zingine za haki za binadamu—haki ya kupata taarifa. Mnamo Aprili 14, 2010, wakati wa vikao vya Bunge, Wabunge wawili waliuliza swali kuhusu ukomo wa Mbunge au wigo wa Mbunge katika kupata habari iliyo mikononi mwa Serikali. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Usimamizi na Mambo ya Bunge) alijibu, akielezea haki na wigo wa Wabunge katika kupata habari za umma. Halafu akaendelea kusema,

Ukomo unajumuisha yale niliyotaja katika jibu langu la nyongeza, lakini ikumbukwe kwamba kuna ongezeko kubwa la matakwa ya kupata habari za umma na ni kwa dunia nzima, palipo na mahitaji makubwa ya jamii, ukijumuisha na Wabunge wakitaka kupata habari toka ofisi za umma, mara zote kuna njia ya kuhakikisha hili ikiwa ni pamoja na sheria ikielezea kwa kina. Sheria ya namna hii mara nyingi inaitwa Sheria ya Uhuru wa Habari. Katika nchi yetu, kwa muda wote huu,

Page 32: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii 25

hatujaona msukumo au hitaji la Sheria hii kutoka kwa jamii, Wabunge au hata kutoka kwa tasnia ya habari. Na kwa sababu hiyo tumeendelea kutumia njia zilizopo.

(Mukajanga, 2010) Kumekuwepo kampeni za Muswada wa Haki ya Kupata Habari Tanzania kwa miaka minne (Baker, 2009a, b). Hata hivyo, kwa sababu mbinu za ushawishi zaidi sana zinajielekeza moja kwa moja kwa kushawishi Serikali kuu, jamii kwa kweli kabisa haijui nini kinaendela, na hivyo kukosa mwitikio, hivyo imeachwa nyuma katika hatari kubwa ya kutopata taarifa sahihi. Ili kuzuia hili kwa wote, Bunge na mahakama, ni lazima jamii ijue ikae tayari na pia iweze kutoa mwitikio. Japokuwa kuna kazi nyingi zinazohusu kuchochea uelewa kwa jamii, ni kidogo sana hupokelewa na jamii. Wakati masuala mbalimbali yanarushwa kwa njia ya radio, magazeti, mabango na vipindi vya luninga, Wananchi wanapashwa habari na wanaweza kuchukua hatua bila shaka, lakini kwa haraka sana, Serikali hupata taarifa kwamba jamii sasa inajua kuhusu masuala haya. Kama kulikuwepo kampeni kubwa kuhusu haki ya kupata habari, wawakilishi wa serikali wasingesema tena kwamba hakuna mtu ambaye amekuwa akisukuma haki ya kupata sheria ya haki ya kupata habari, kwa sababu wangekuwa na taarifa juu ya kampeni hii na kwamba wangejua kwamba jamii itajua kwamba matamshi haya si kweli. Katika mwono wa kupigania haki ya kupata elimu kwa njia ya mahakama, sekta ya kijamii iliyo makini inaipatia mahakama suala jingine la kuangalia—nini kinaonekana kuwa ni matakwa ya jamii. Wakati inapata msukumo kutoka kwa Serikali, mahakama itakuwa na msukumo uleule kutoka kwa jamii. Hata kwa mahakama ambayo haijalegeza maamuzi yake, hiyo ni nia ya kuhakikisha sura yake kwa jamii, mitazamo na maneno ya jamii yanaweza kwa njia moja au nyingine kuathiri maamuzi ya majaji kama wataamua dhidi ya Serikali. Ukiangalia mbele uwezekano wa kudai haki ya elimu kwa njia ya Mahakama, sababu zote za msingi katika nyanja hizi tatu—kisheria, kisiasa na kijamii—zinahitaji kuangaliwa katika kutathmini uwezekano wa mafanikio. Sehemu ifuatayo inatoa ufafanuzi na uchambuzi mfupi wa uwezekano wa kutumia shauri la kimkakati ili kusimamia haki ya kupata elimu nchini Tanzania.

Page 33: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

26 Elimu ya Msingi “Bure”

Elimu ya Msingi “Bure” Hakuna mjadala kwamba Tanzania katika miaka ya karibuni imefanya jitihadi kubwa sana kuhakihisha kuwa kuna upatikanaji wa elimu ya msingi kwa wote (UPE). Kwa sababu ya lugha ambayo imetawaliwa na malengo ya maendeleo ya milenia (MDG) (hususan lengo la pili kuhusiana na upatikanaji wa elimu kwa wote), elimu kwa wote imekuwa ni wazo la kila mmoja hasa katika upatikanaji na kuandikisha wanafunzi. Tanzania inasifika sana kimataifa (DFID, 2005; UNESCO, 2010) uandikishaji kwa kiwango cha asilimia 962 na hata ilipata tuzo ya MDG katika masuala ya elimu mnamo mwaka 2010 (Kamati ya Tuzo ya MDG, 2010). Wakati maendeleo haya yamefanyika, yanalinganishwa wakati wote na kufutwa kwa ada za shule mwaka 2002 ambako kulikuja pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM): ―Serikali itafuta ada za shule na michango yote ya lazima inayotolewa na wazazi kuanzia Julai 2001 ili pasiwepo mtoto yeyote atakayenyimwa haki ya kusoma‖ (URT, 2003a, uk. 7). Hivyo basi, kuonekana kukaribia 100% ya kuandikisha na shule za ―bure‖ za msingi inakuwa ni hatua ya mafanikio ya kile kinachoweza kuwa jukumu la msingi katika haki ya kupata elimu: ya lazima, bure, na elimu ya msingi kwa wote. Lakini hivi sivyo ilivyo. Wakati karo za shule, malipo ya masomo yamefutwa na kuongezeka kwa uandikishaji unaonesha matokeo mazuri, hata hivyo wazazi na jamii wameendelea kudaiwa michango kwa kigezo cha elimu ya msingi. Michango hii ya ziada ambayo kwa matokeo yake inafanya elimu ya msingi kuwa si bure tena na kuonekana katika sura mbili nchini Tanzania: michango ya elimu ya wazazi na michango ya maendeleo ya kijamii. Muulize mzazi yeyote nchini Tanzania kama elimu ya msingi ni bure kwa mtoto wake, na jibu lake ni hapana: sare za shule, vitabu, madawati, daftari, masomo ya ziada na ada za mitihani miongoni mwa mambo mengineyo ni lazima ilipiwe. Hizi ni gharama ambazo mzazi hubeba wakati anampeleka mtoto wake shule ya msingi, na wakati mwingine michango hii ni michango ya elimu ya wazazi inayoweza kabisa kumfanya mtoto asiende shule. Sambamba na gharama hizi za elimu kuna mfumo uliolazimishwa wa michango ya maendeleo ya jamii. Mpango huo huo unaozuia michango ya lazima kwa watoto/wazazi ndio huo huo unaochochea kuwepo michango ya lazima kwa jamii: ―Mamlaka za Serikali za Mitaa zitatakiwa kuhakikisha kuwa michango inatolewa na jamii zote zenye kumiliki shule za msingi‖ (URT, 2006b, uk. 12). Kwanza, sehemu kubwa ya MMEM unasisitiza ushiriki wa jamii na hata unarasmisha michango ya jamii kwa asilimia 20 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa (URT, 2006b, uk. 38). Japokuwa kushirikishwa kwa jamii ni sababu muhimu ya kuwa na elimu bora, mara kwa mara imegeuzwa kuwa ni wajibu na hulaumiwa wakati serikali inaposhindwa kusimamia haki ya kupata elimu. Mathalani, Mei 2010, taarifa kuhusu upungufu wa matundu ya vyoo ilitoka mkoani Mara. Mojawapo ya shule yenye wanafunzi 2,000 lakini mashimo 20 tu ya vyoo, kinyume na mashimo 80-100 yanayotakiwa kwa idadi hiyo ya wanafunzi kama inavyoainishwa na MMEM. Kama msichana mmoja wa darasa la saba alivyoomba,

2 Takwimu hizi zinapatikana kutoka shuleni na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na zimepokelewa bila kupingwa katika nchi na kimataifa pamoja na mgogoro wa wazi wa kimaslahi unaoweza kuchakachua namba hvi. Utafiti uliofanya na Taasisi ya Takwimu ya UNESCO unaolinganisha takwimu ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania na utafiti wa kaya, uligundua tofauti ya asilimia 25, ikimaanisha kwamba, wakati Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kuripoti asilimia 96 ya uandikishaji, hali halisi yaweza kuwa chini kabisa ya kiwango cha asilimia 71 (Utafiti wa Bruneforth katiki UNESCO, 2010).

Page 34: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Elimu ya Msingi “Bure” 27

Ni kama hatuna vyoo kwa sababu vingi vimejaa na vingine viko katika hali mbaya na hivyo kuhatarisha maisha yetu. Tunaomba serikali kujenga vyoo vipya katika shule yetu.

(Mwera, 2010) Hata hivyo, serikali iliona jukumu hili kwa mtazamo wa tofauti kabisa. Afisa Afya wa kata hiyo baada ya hapo aliitishia shule na nyingine tatu katika utawala wake kwamba zingefungwa endapo jamii husika wasingejenga vyoo. Kama ilivyoripotiwa,

Aliwataka watu wa jamii husika kuipatia elimu umuhimu wake kwa kuboresha mazingira ya shule ambayo, alisema ni ya kwao, alisema kwamba jamii wana wajibu wa kuhakikisha walimu na watoto wanakaa katika mazingira salama.

(Mwandishi wa Citizen, 2010) Mkanganyiko juu ya majukumu ya vipengele vya haki ya kupata elimu pia upo hata kwa walimu wenyewe. Katika manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam, wanafunzi wa shule ya msingi wapatao 54,000 wanakaa chini kwa sababu ya upungufu wa madawati. Katika shule ya msingi ya Mtakuja peke yake, wanafunzi wapatao 600 wanakaa chini. Mkuu wa shule Bi. Elizabeth Chiwambale anaripoti, ―Wanafunzi wengi hapa ni yatima au kila mmoja ana mzazi mmoja. Wengi wanaishi katika umaskini mkubwa chini ya kiwango cha chini kabisa na kwa hiyo hawawezi kabisa kuchangia maendeleo ya shule‖ (Agola, 2010). Hata hivyo, anahusisha upungufu wa madawati na ―ukosefu wa moyo wa kujitolea katika kushiriki miradi ya shule‖ (Agola, 2010). Hali hii ya kutokuwepo wazazi, kuwepo mmoja au wazazi wenye umaskini mkubwa kunamaanisha kwamba elimu yao itolewe na serikali na si mzazi au jamii yenyewe kuwajibika kwa mkuu wa shule ambaye ni mtumishi wa umma na mwajiriwa wa serikali, ni salama kwake kuitupia lawama jamii kuliko serikali, lakini ni matamshi kama haya yanayofanya jamii na serikali kupoteza mwelekeo wa majukumu yake. Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma uliofanywa kitaifa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (miongoni mwa mengine) na kutolewa mwaka 2010 ulibaini kwamba kwa wastani, ―Michango ya fedha na vitu kutoka kwa wazazi unafikia asilimia 1.0 ya michango yote ya shule na asilimia 7.7 ya vyanzo visivyokuwa vya fedha,‖ au kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 4 kwa mwaka, lakini ―takwimu hizi zimechakachuliwa kwa sababu shule nyingi hazitunzi kumbukumbu na hasa michango ya vitu‖ (Claussen na Assad, 2010, kar. 77-78, msisitizo uko kwenye chanzo). Utafiti wenye sehemu mbili unaonesha mwenendo wa gharama za elimu ambazo wazazi wanabeba nchini Tanzania. Utafiti uliofanywa Old Moshi mwaka 2000 (kabla ya ―kufuta‖ karo) na tena mwaka 2006 (baada ya ―kufuta‖ karo) uligundua kwamba wastani wa gharama za mwanafunzi wa darasa la sita kwa mwaka mwaka 2000 ulikuwa shilingi 13,660 wakati ule wa mwaka 2006 uliongezeka kufikia shilingi 38,700, ―kwa zaidi ya ongezeko tarajio katika gharama kwa sababu ya mfumuko wa bei‖ (Vavrus na Moshi, 2009). Lakini hili si tatizo tu la watu kulipia elimu ya msingi wakati haki ya kupata elimu inasema kwamba wasilipie, ni tatizo la haki ya upatikanaji wa elimu. Utafiti wa Bajeti ya Kaya uliofanyika nchini Tanzania unaonyesha kwamba asilimia 11 ya waliohojiwa walisema ―gharama‖ kama sababu ya kutopeleka watoto wao shule mwaka 2011 (kabla ya ―kufuta‖ karo), wakati asilimia 5 bado wanatoa sababu ile ile mnamo mwaka 2007 (baada ya ―kufuta‖) (NBS, 2008). Wazazi wa watoto wa shule wanapoacha kulipa ―michango,‖ makubaliano kati ya wazazi na mkuu wa shule yanawekwa, au wanaweza kupigwa faini, au watoto wao waweze kurudishwa nyumbani kwa lolote ambalo ni kawaida katika eneo husika.

Page 35: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

28 Elimu ya Msingi “Bure”

Katika mfumo wa elimu ambamo karo za shule zimefutwa lakini michango ya wazazi inatiliwa mkazo, malipo kwa ajili ya upatikanaji wa elimu kimatokeo unaendelea kuwepo na wakati mwingine wanafunzi ambao wazazi wao hawalipi wanarudishwa nyumbani. Mwanzoni mwaka 2011, vyombo kadhaa vya habari viliandika kuhusu hili (angalia Mlacky, 2011; Ilbadi, 2011). Katika shule moja mkoani Dar es Salaam, kila mwanafunzi alipaswa kuchangia matofali mawili, wakati baadhi ya wanafunzi walikwenda bila matofali, walirudishwa nyumbani. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aliingilia kati na kutamka kuwa marufuku kwa wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa kutotoa michango ya aina hiyo (Mlacky, 2011). Wakati tamko likitolewa kwamba ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata elimu na kwamba mtoto asikataliwe kupata elimu kwa sababu ya kukosa michango. Matamko haya yasichanganywe na yale yanayopiga marufuku michango ya lazima. Zaidi kwamba, tatizo linaloonekana katika suala hili na mengineyo ni lile la majukumu na wajibu—ukusanyaji wa michango ulikuwa unafanywa kati ya wanafunzi na walimu wakati, kama ilivyotiliwa mkazo na Naibu Waziri, kwamba ifanyike kati ya wazazi na kamati za shule. Japokuwa ujumbe unapelekea kwa baadhi ya waziri na wabunge kwamba watoto wasifukuzwe shule kwa sababu ya kukosa michango, wawakilishi wa shule na wazazi wakati mwingine wanaachwa katika mkanganyika kwasababu michango hiyo inaonekana kuwa ni ya lazima katika jamii. Ikiwa ni sehemu ya Africa Education Watch (AEW), mpango wa miaka mitatu (2007-2010) katika kusimamia fedha za umma katika shule za msingi, taasisi ya kimataifa ya kupambana na rushwa (Transparency International - TI) ilifanya utafiti katika nchi saba. Japokuwa Tanzania haikuwa miongoni mwa nchi hizo, matokeo ya utafiti yanaonekana kufanana mno:

AEW inaainisha tabia tatu zenye rushwa zinazowahusu wazazi: (i) matakwa mabaya ya karo zilizofutwa kisheria, (ii) ubadhirifu wa mali, na (iii) matumizi mabaya ya mamlaka kwa walimu au maofisa. Upo mkanganyiko, hasa miongoni mwa wazazi, kwamba ni matakwa yapi ya karo za shule ni halali. Upungufu wa bajeti mara nyingine unarahisisha shule kutafuta fedha za ziada, lakini kwa sababu ada za kuandikisha zinapaswa kuwa zimefutwa katika elimu ya msingi katika nchi zote zilizofanyiwa utafiti, inasikitisha kuona kwamba wastani wa asilimia 44 ya wazazi wanaripoti kwamba bado wanalipa ada hizo. Wastani ambao wazazi wanalipa ni dola za kimarekani 4.16 (shilingi za kitanzania 5,600) kwa mtoto kwa mwaka wa shule.

Kuongezeka kwa uandikishaji wa watoto miaka ya karibuni katika nchi zilizo kusini mwa Sahara Afrika kumerahisishwa na maamuzi ya serikali kuondoa karo ya shule katika elimu ya msingi. Elimu ya msingi bure mara zote haijumuishi vitabu vya bure sawa na zana zingine za shule. Gharama hizi zinabaki kuwa vichocheo hasi kwa masikini na vimeleta mkanganyiko fulani juu ya kile kinachotolewa bure na serikali na ambacho si bure.

(Antonowicz, Lesné, Stassen na Wood, 2010) Na ―mkanganyiko‖ ni sahihi. Kipi ni ―bure‖? Kwa vipi ―michango‖ idaiwe? Tanzania haiko pekee katika njozi hii ya ―vya bure‖; nchi nyingi duniani wanajikuta katika njozi hii wakati jamii ya kimataifa inatekeleza. Kwa kuwa ―katika mstari wa mbele katika mapambano ya haki ya kupata elimu‖ kwa miaka 6 kama Mfuatiliaji Maalum wa Ripoti za Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Kupata Elimu (Tomasevski, 2006), Katarina Tomasevski (ametajwa hapo juu kama mtunzi wa A-4) aliumizwa sana na hali hii na mnamo mwaka 2006 alihitimisha ripoti yake Bure au Karo: Ripoti ya Dunia ya mwaka 2006 kabla hajafariki ghafla. Kwa kuonja tu yaliyomo katika ripoti yake, na ile

Page 36: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Elimu ya Msingi “Bure” 29

huruma na upekee wa kile kilichokosekana, hebu angalia maneno ya mwanzo kabisa ya ukurasa wa juu wa tovuti yake:

Kusoma ripoti hii kutakufanya ukasirike. Inaonesha ni jinsi gani haki ya kupata elimu siku za leo ilivyo mahututi. Imekataliwa kimataifa, pamoja na kuwepo maneno mazuri ya umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu na maendeleo yenye kuwa na mizizi katika haki za binadamu. Kukataliwa kwake kunashuhudiwa na kuwepo kwa michango hata katika shule za msingi kunakosababisha walio maskini kuikosa. Ukweli huu wenye kuumiza katika ubaguzi wa kiuchumi katika shule za msingi unashuhudiwa na kuwepo kwa michango isiyopungua 22 ya aina tofauti kama ada katika shule za msingi ambapo kimsingi ilitakiwa kuwa bure. Watoto na vijana ni wahanga walio kimya wa ukiritimba dunia, ambao takwimu zake na misamiati yake vimeshindwa kuifanya ahadi zake kuwa halisi au kutimizwa. Sheria inayotamkwa kwamba elimu ya msingi iwe bure na lazima, imewekwa kando. Ni lazima elimu iwe ya bure lakini kinyume chake ni ya ―karo‖, Watu wenye bahati ya kuishi katika nchi ambayo elimu ya msingi hutolewa bure wanadhani kwamba hali ndivyo ilivyo kwingineko duniani. Watu katika nchi maskini wamelazimika kulipa karo za shule kwa ajili ya watoto wachache kiwango cha robo tatu ya vipato vyao. Mbaya zaidi, watoto wanalazimika kufanya kazi hata shuleni ili kulipia gharama za elimu yao ya msingi. Haya yote huwezi kuyapata katika ripoti rasmi. Soma ripoti. Pata hasira. Saidia kuibua na kupinga ubaguzi wa kiuchumi katika haki ya kupatikana elimu.

(Tomasevski, 2010) Ripoti hiyo inaonesha kwamba miongoni mwa nchi 45 za kusini mwa sahara ni nchi tatu tu—Mauritania, Sao Tomé na Principe, na Ushelisheli—ndio wanaotoa elimu ya msingi bure. Kwa sasa, nchi 19, Tanzania ikiwemo, zinazo elimu ya bure imeandikwa katika sera za serikali lakini kusema kweli wanatoza michango katika shule za msingi (Tomasevski, 2006). Tomasevski hajakanganikiwa na maana ya bure na pia si mfumo wa sheria wa haki ya kupata elimu. Karibu kila mkataba wa kikanda na kimataifa tulivyokwisha kuona hapo juu vinazungumzia elimu ya msingi bure: UDHR, ICESCR, CRC, CRPD, ACHPR (katika Kanuni na Mwongozo wa Tume ya Afrika), ACRWC na Mkataba wa Afrika Mashariki (kwa kutekeleza ACHPR). Mtazamo wa elimu ya msingi bure uko wazi na umeainishwa na mfumo wa sheria na si tu kwamba unahusu karo ya masomo. Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni inaelezea neno ―bure‖ kwa kina, na hata pia katika suala la kwamba serikali zinaweza kujaribu kusema kwamba kimsingi hazitoi elimu ya msingi bure:

(UNCESCR, 1999a)

7. Bila gharama. Chanzo cha hitaji hili lipo wazi kabisa. Haki hii imeelezwa wazi kabisa ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu ya msingi bure kwa mtoto, wazazi na hata walezi. Karo zinazoanzishwa na serikali, serikali za mitaa au shule, na gharama zingine za moja kwa moja zinachangia kuwa ni vichocheo hasi katika kujumuisha haki hii na vinaweza kuzuia upatikanaji wake. Na kwa taathira yake vinarudisha nyuma jitihada zote. Kuondolewa kwake ni suala ambalo linahitaji kufanywa kwa kuwepo kwa mpango kazi. Gharama zisizo za lazima za moja kwa moja, kama vile michango ya lazima kwa wazazi (wakati mwingine ikioneshwa kuwa ni ya hiari wakati kusema kweli siyo), au lazima ya kuvaa sare shule ambayo ni gharama kubwa, vyaweza kuangukia katika kundi moja.

Page 37: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

30 Elimu ya Msingi “Bure”

Haya yote yanasaidia lakini hakuna haja ya kufika hadi kwenye ngazi ya Umoja wa Kimataifa ili kupata maana iliyofafanuliwa na neno ―bure‖ kwenye haki ya kupata elimu. Tume ya Afrika, kwenye Rasimu ya Kanuni na Miongozo ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni katika ACHPR, zinasisitiza kwamba nchi husika zina wajibu wa msingi, aina mbili ya wajibu kati ya huo ni:

(Tume ya ACHPR, 2009) Yote haya yanathibitisha kwamba elimu bure ya msingi ina maana zadi ya ada ya masomo, na kuleta hoja ya kushughulikia jambo hili kutachukua muda na nguvu. Kwa kuzingatia mfumo wa kisheria, mafanikio yoyote huenda yakapatikana tu kupitia Mahakama ya Afrika kwa kutumia ACHPR. Kupatikana sera ya elimu bure kwenye shule za Tanzania haimaanishi kwamba kuna uhakika kisheria ya kutumia sera hiyo mahakamani, huenda kesi ya aina hiyo ingeshindwa na Serikali ndani ya nchi, kwa hiyo inabidi anayepeleka madai ajiandae kupitia na kumaliza hatua zote kwenye mahakama za ndani ya nchi ili aweze kuendelea hadi Mahakama ya Afrika. Kisiasa, kesi hii itakutana na upinzani kutoka Serikali. Kwanza kesi ya namna hii ingeharibu sura ya kimataifa ya Serikali. Kwa kushinda tuzo ya MDG kwa ajili ya elimu mwaka jana, kesi ya kushindana na misingi ya UPE ndani ya Tanzania ingeleta tishio la Tanzania kuaminika kimataifa. Kesi ya aina hii, huenda ingeonesha wazi jinsi Serikali ilivyokaa kimya juu ya mambo hayo au jinsi ilivyochangia kwenye michanganuo ya ―bure‖ inayoongelewa kwa sababu lazima watoe ripoti kwa wafadhili ya kuonesha kwamba wametekeleza UPE kikamilifu. Mathalani, katika Ripoti ya Tathmini ya Katikati ya MDG, imeandikwa, ―Maboresho [ya uandikishaji katika shule za msingi] yameletwa na kuondolewa kwa ada za shule, michango ya wazazi inayotokana na uandikishaji huo na utekelezaji mzuri wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM)‖ (URT, 2009d, uk.8). Hata hivyo, MMEM unasema wazi kwamba, ―Serikali itafuta ada za shule na michango yote ya lazima inayotolewa na wazazi‖ (URT, 2003a, uk. 7, msisitizo umeongezwa). Inasemwaje kwamba MMEM umekuwa na ―utekelezaji mzuri‖ wakati ―michango ya wazazi inayotokana na uandikishaji‖ imeondolewa wakati mambo mengine yote bado yapo? Kama ilivyotajwa hapo juu, MMEM unakataza michango ya lazima kutoka kwa wazazi lakini vilevile unalazimisha michango ya jamii (URT, 2006b, uk. 12). Je, hiyo inafanana kwa vipi na UPE au haki ya kupata elimu?

i. Kuhakikisha kwamba watoto wote wanafurahia haki yao ya kupata elimu ya bure ambayo ni ya lazima. Ni marufuku mtoto yeyote kunyimwa haki hii kwa sababu tu ya kukosa ada ya shule au gharama husika za elimu, kunahitajika hatua madhubuti ili kuhakikisha ya kwamba watoto wanaotoka kwenye vikundi duni na kwenye mazingira hatarishi wanaweza kupata elimu ya shule ya msingi iliyo bure ili kufikia malengo haya. Lazima nchi husika ziendelee kuongeza viwango vya rasilimali za mataifa yao walizotenga kwa ajili ya elimu.

… iii. Kutekeleza na kugawa sare ili kutokomeza au kupunguza gharama za

kusoma shule ya msingi ambazo ni pamoja na kuondoa ada, kutoa ruzuku kufuatana na mahudhurio shuleni, kuwapatia wanafunzi sare za shule bure au kuondoa swala la sare kabisa pale sare zinapotumika, kuwapatia wanafunzi vitabu vya masomo bure, kuwasajili bure shuleni au kuwapatia chakula cha bure mashuleni ili kuvutia wanafunzi maskini waweze kwenda shule.

Page 38: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Elimu ya Msingi “Bure” 31

Ya pili ni kwamba, pamoja na bajeti finyu kama ilivyo kwa wakati huu, kitu cha mwisho ambacho serikali inataka ni kuwa na matumizi mengine. Kushinda kesi ya aina hii kungesababisha kwamba gharama nyingine za elimu zingehamishwa kutoka kwa wazazi na jamii husika kwenda kwa serikali. Pamoja na kwamba michango ya fedha na misaada ya maendeleo inatolewa chini ya viwango kama ilivyo (rejea kifungu cha ―Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II‖), kuziongeza kufidia kile kinachotolewa kwa sasa na wazazi na jamii kunahitaji nidhamu na uwazi wa kifedha wa ziada na si kama ilivyo sasa kwenye ngazi mbalimbali za serikali ya Tanzania. Na pia mfumo wa kimahakama unaoleta matumaini ya kuwa na maendeleo hauwezi kufanya makubwa bila kuwa na sheria za kusaidia, hasa shinikizo la kisiasa. Kufuatana na hali ya ―kuchanganya‖ ya suala hili, kungetakiwa kuwa na kazi kubwa ya kufanya katika uwanja wa jamii. Pamoja na mfumo wa jamii ulioundwa na matakwa yasiyoisha ya michango ya jamii, wazo lile la kwamba elimu yote ya msingi iwe bure, kuzidi mafunzo peke yake, huenda ni mbali na fikra za baadhi ya watu. Utetezi mwingi ungetakiwa kuwepo ili kuelimisha raia juu ya haki zao na hasa maana ya kuwa na haki ya elimu. Wakati huo huo, jamii nyingi zimechoka kuombwa michango ya kila mara, na huenda kampeni au kesi ya kukomesha michango hiyo ingepokelewa vizuri na jamii. Hata hivyo, kwa kuangalia mazingira ya kisiasa na ya kijamii, kuna uwezekano kwamba jitihada za wanaharakati wa elimu zingeweza kwenda sambamba na za serikali. Moja kati ya ujumbe muhimu wa kutokupeleka kwenye kampeni ya aina hii ni kwamba wazazi na jamii waache kuchangia kabisa—kwa hiari yao—kwenye shule zao. Shule bora ni zile zilizopo ndani ya jamii ambazo wazazi na wakazi wengine wanaendeleza uhusiano wa karibu na maendeleo ya shule zao na wanafunzi wanaosoma humo. Ingependeza kama jamii zingechangia shule zao, lakini watoto wasirudishwe nyumbani kama wazazi wao hawajachangia shule. Haya yanakaribiana na yale ambayo tayari baadhi ya wafanyakazi wa serikali wanapendekeza, kinachopungua hapa, ambacho kingegeuza mambo haya yanayochanganya kuwa jibu sahihi ni kuwa na kanuni zinazoeleweka za kupelekwa mashuleni ambazo zingehamasisha michango na ukusanyaji wake wakati pia zikielimisha juu ya ukiukwaji wa kanuni hizo. Kama suala hili litaachwa juu juu na ikiwa kesi inayohusu michango na ubaguzi wa elimu itajitokeza, itakuwa vizuri kama itashugulikiwa na kikundi cha watu kuliko mtu binafsi. Itabidi pia kuonesha kwa uwazi uhusiano wa kina kati ya gharama za shule za msingi, kuzuiwa kupata elimu ya msingi, na athari hasi ambazo lazima tu zitakuwepo, si tu juu ya watu binafsi bali kwa jamii kwa ujumla. Kwa hiyo basi, watu wale wanaopasa kupeleka kesi mahakamani watatakiwa kuwa wale asilimia 5 waliotoa taarifa ya kwamba ―gharama‖ ziliwazuia kupata elimu kwenye Utafiti wa Bajeti ya Kaya ya mwaka 2007. Kwa kiwango hiki, watu wa jinsi hii watakuwa ni wachache na wa kutafuta. Mitandao ya kitaifa kama Marafiki wa Elimu wanaweza kuwa na nafasi muhimu sana ya kugundua wale waliotupwa pembeni na kuwaunganisha pamoja. Kwa ujumla, ijapokuwa uwezekano ni mdogo wa kesi ya aina hii kuwepo, hata hivyo ingekuwa ni uzembe kwa jarida linalohusu haki ya kupata elimu kutokuongelea ukiukwaji wa kinachowezekana kabisa kuwa ni matakwa ya msingi ya kuwa na haki ya kupata elimu: elimu ya bure na ya lazima.

Page 39: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

32 Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

HakiElimu inaamini kuwa elimu ni haki ya kila mtoto wakiwemo waliopata mimba. Mimba haiondoi haki ya kupata elimu kwa kuwa licha ya kuwa na mimba bado ni mtoto. Wasichana wajawazito wanahitaji elimu zaidi kuliko wengine. Ndio maana HakiElimu inatetea wasichana hao wapate fursa ya kupata elimu na watiwe moyo ili waweze kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Kuwafukuza watoto hao shuleni ni kuwanyanyasa wao na watoto watakaozaliwa ambao hawana makosa. Baadhi ya watoto wamepata mimba kwa kulazimishwa kufanya ngono au kubakwa. Elimu ndio njia nzuri ya kuwakomboa wanawake na wasichana katika jamii, hasa wale walioathirika na mimba. Kama alivyosema Mwalimu Nyerere,―Kwa watu masikini kama sisi elimu inatakiwa kuwa chombo cha ukombozi‖. Katiba ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC) pia inasisitiza watoto wote - wakiwemo na waliopata mimba - wana haki ya kupata elimu bila kubaguliwa.

(HakiElimu, 2004, uk. 16 [tafsiri ya mwandishi]) Tanzania ni nchi yenye tatizo kubwa la mimba kwa watoto. ―Asilimia 25 ya wanawake watanzania, chini ya miaka 18 tayari ni wazazi‖ (Bebien, 2010). Hoja hii inaandikwa sana katika vyombo vya habari yaani magazeti na kutangazwa pia, ni suala linalosumbua jamii au serikali za mitaa, na juhudi kubwa kwa mashirika yasiyo ya serikali. Maswali ya kila mara ni ―Kitu gani kinasababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni?‖ na ―Nini kifanyike juu ya jambo hili?‖ Tatizo si tu kwamba watoto wadogo wamebeba mimba na vipi kuhusu maisha yao lakini kimsingi ni juu ya elimu yao kwa sababu wengi wanafukuzwa shule. Hii yaweza kuwa ni kuacha shule kwa hiari—tathmini ya mazingira ya mmojammoja na majukumu mapya na vipaumbele vinavyopelekea mtoto kutolewa katika maisha ya shule na kwenda kuishi maisha ya nyumbani tu. Mara nyingi pia inahusisha ndoa za utotoni—msichana anaweza kuolewa akiwa mdogo halafu akapewa mimba, na maisha mapya ya kuolewa, maisha ya kimama yanaondoa kabisa thamani ya elimu. Hali hii ya ―hiari‖ inakuwa ya hatari wakati uamuzi wa kuendelea na elimu, waweza pia kuwa na hiari lakini mazingira yanayomweka msichana katika hali hii si ya hiari; mimba za aina hii mara ningi ni matokeo ya kulazimishwa au kubakwa, au kutokana na ndoa za kulazimishwa. Kinachofanya hali hii kuwa ngumu zaidi japo inaitwa kuwa ni kuacha shule ―kwa hiari,‖ ni ile hali ya kwamba hata kama msichana aliyepata ujauzito anataka kuendelea na shule, atafukuzwa shule mwisho wake. Katika miaka ya karibuni, Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la wanaoacha shule kwa sababu ya mimba (ambayo yaweza kuchukuliwa kuwa ni ―kufukuzwa shule‖ kwa sababu ni wazi kama haachi mwenyewe atafukuzwa shule). Kwa kuangalia elimu ya msingi na sekondari tu, mwelekeo unaonesha kama ifuatavyo:

Page 40: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

33

(URT 2008a, 2009a, 2010b, c)

(URT, 2010b, c) Wakati idadi ya jumla ya hawa wanaoacha shule ilikuwa ni wastani wa 4,000 kutoka mwaka 2003 hadi 2006, kwa sasa wastani huu umepanda sana na kufikia 8,000. Katika yote tangu mwaka 2003, karibia wasichana 50,000 wamelazimika kuacha shule kwa ajili ya ujauzito, na mara nyingi hawarudi shule.

3,218

9,788

0

2,000

4,000

6,000

8,000

10,000

12,000

2003 2004 2005 2006 2007 2008 2009 2010

“W

ali

oach

a” k

uto

kan

a n

a M

imb

a

Jumla ya “Walioacha” Shule za Msingi na Sekondari kutokana na Mimba

10

8

1,688

1,891

1,833

635

816

674

230

41

6

1

0

0 200 400 600 800 1000 1200 1400 1600 1800 2000

Kdt cha 6

Kdt cha 5

Kdt cha 4

Kdt cha 3

Kdt cha 2

Kdt cha 1

Drs la VII

Drs la VI

Drs la V

Drs la IV

Drs la III

Drs la II

Drs la I

“W

ali

oach

a” k

uto

kan

a n

a M

imb

a

“Walioacha” kwa Madaraja kutokana na Mimba mwaka 2010

Page 41: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

34 Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

Sababu zinazosababisha hali hii ni ngumu kuzielezea. Je, ni sera ya kufukuza au kuna sababu pekee zisizotabirika za mimba za utotoni? Au suala hili limeanza kuonekana kwanza, na halafu serikali ikaanza kutunza kumbukumbu kuliko hapo awali? Mkakati wa kujenga majengo ya sekondari ulioanza mwaka 2005 ulipelekea kuongezaka kwa uandikishaji kwa asilimia 51 kati ya mwaka 2006 na 2007 pekee; hii kwa wazi kabisa inahusisha kuongezeka kwa idadi halisi ya wanaoacha au kufukuzwa shule kwa sababu ya mimba. Hata hivyo wanaoacha shule kwa sababu ya ujauzito katika shule za sekondari idadi yao imeongezeka kwa haraka sana. Wakati imekuwa kati ya asilimia 5 hadi asilimia 10 kabla ya hapo, ilipanda hadi kufikia asilimia 22 mwaka 2007. Kama ongezeko lilikuwa tu sehemu ya kuongezeka kwa uandikishaji uwiano huu wa wanaoacha shule kwa sababu ya mimba ungetarajiwa kuendelea kuwa zaidi au sawia kama awali. Utaratibu wa kuwafukuza wanafunzi wajawazito umedumu takribani kwa miongo kadhaa, lakini wengi wanasema kwamba, sheria ya ufukuzaji wa wanafunzi wajawazito inayopatikana katika marekebisho ya sheria ya Elimu, Tangazo la Serikali Na. 295 ya mwaka 2002, inasema:

(URT, 2002b, msisitizo umeongezwa) ―Makosa dhidi ya maadili‖ kama vigezo vya kuwafukuza shule watoto yametafsiriwa kwa rejareja sana. Mantiki ni kwamba kama msichana ni mjamzito, basi amefanya ngono nje ya ndoa, kwa hiyo kwa wazi kabisa ―ametenda kosa kinyume na maadili‖ na kwa hiyo ni lazima afukuzwe shule (na kwa wale wanaofanya ngono ndani ya ndoa, hao wanafukuzwa pia kwa sababu ya kifungu kinachofuata cha 4(c) cha Sheria ya Elimu ambayo huainisha kwamba kuingia katika ndoa ni kigezo cha kufukuzwa shule). Kusema kweli, ―makosa dhidi ya maadili‖ ni kosa au kundi la makosa yanayoainishwa katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu Tanzania. Hakuna suala la mimba au kupata mimba kwa namna yoyote ile kuainishwa kama mojawapo ya kosa dhidi ya maadili. Vilevile, kama watunzi wa sera ya Tanzania ya kufukuza wanafunzi shuleni walimaanisha kwamba mimba ni sababu ya kufukuzwa shule, inaonekana tu kwamba wangeongeza tu neno ―mimba‖ katika orodha ya makosa kama yanavyoainishwa na sera ya kufukuzwa shule hapo juu; hata hivyo hawakufanya. Wengine wanaelezea zaidi katika nyanja ya kufukuza inavyotajwa na Sheria ya Elimu:

(URT, 2002b) Mazoea na utaratibu wa kuwafukuza shule wasichana wajawazito ni kinyume na haki ya kupata elimu ambayo mikataba mingi inaelezea bayana. Kuhusu Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, Tume ya Afrika kimsingi inaeleza:

4. Kufukuzwa kwa mwanafunzi kutoka shuleni kwaweza kufanywa – … (b) Ambapo mwanafunzi ametenda kosa la jinai kama vile wizi, kuharibu mali kwa nia, umalaya, matumizi ya dawa za kulevya, makosa dhidi ya maadili bila kujali kama mwanafunzi husika ameshtakiwa au hakushtakiwa kwa kosa hilo;

7. Kufukuzwa kwa mwanafunzi kutoka shule kwaweza kuamriwa ambapo – … (b) Hali ya afya ya mwanafunzi kimwili au kiakili imeathirika kiasi cha kumfanya mwanafunzi asiweze kuendelea shule.

Page 42: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

35

(Tume ya ACHPR, 2009) Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto unaainisha:

(OAU, 1990) Nchi ya Tanzania inaonekana kufanya kinyume na yale yaliyokubaliwa katika umoja wa Afrika. Katika mtazamo mpana, suala hili ni haki mojawapo ya haki za kupata elimu, na kama itashindaniwa mahakamani, yaweze kufanyika vizuri sana kama kesi inayopinga ubaguzi, kitu ambacho mahakama zinafahamu zaidi. Inahitaji watu wawili ili mimba kubebwa, wakati wasichana wanabeba asilimia mia moja uthibitisho wa kitendo na wanaadhibiwa kitaaluma vijana na wanaume hawapatikani kirahisi (Nkwame, 2010). Matumizi ya fungu la 7(b) hapo juu ya kuwaondoa wasichana wajawazito kwa sababu ya afya ―mbaya‖ ya mwili yanaathari za kibaguzi kwa kuwa lipo kimya hasa kwa upande ambao wabia wanaume ambao ukweli (au zaidi kwa masuala ya ubakaji/ngono ya lazima) wanawajibika. Mfano mmoja ni kwamba msichana mjamzito kufukuzwa lakini mwenzake wa kiume hachukuliwi hatua ni ubaguzi wa aina yake, lakini ubaguzi hutiliwa mkazo au unakuwa mbaya zaidi wakati matukio yanajirudia na kuwa kama kawaida kwa wasichana kwa kuwaondoa katika haki yao ya msingi ya kupata elimu wakati wale wenye jinsi tofauti wanaendelea. Hii inaonesha pia eneo jingine lenye tatizo katika kutafsiri kifungu cha 4(b) hapo juu: hata kama itatumika bila ubaguzi, itasababisha kufukuza watoto wote wavulana kwa wasichana, na ni hatari sana kwa maisha ya watoto na taifa kwa ujumla katika siku za usoni. Uvunjifu huu wa kibaguzi kwa haki ya kupata elimu kwa wasichana Tanzania inaoneshwa katika muktadha wa A-4 (angalia katika sehemu ya ―Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii‖) katika Kampeni ya Kidunia ya Elimu, Mradi wa Haki ya Elimu na Campaña Latinoamericana katika utafiti unaoitwa ―Ubaguzi, Ubaguzi wa Rangi, Ubaguzi wa Wageni na Ukosefu wa Stahamala katika Elimu: Suala la Vijana Wasichana Tanzania‖:

Kwa kuwafukuza wasichana wajawazito shule, Serikali ya Tanzania, katika kile ambacho kinapaswa kuwa jukumu lake la msingi kuhakikisha haki ya kupata elimu kwa raia wote, inawajibika moja kwa moja kwa ubaguzi wa kijinsia na kwa kukiuka haki ya kupata elimu. Inafanya hivyo kwa kutohakikisha upatikanaji wake katika misingi ya usawa, wakati inapowabagua wanafunzi wajawazito; kwa kuifanya isipatikane, wakati wanawakatalia wasichana na wenye mimba wasiipate, na kuwaadhibu wahanga badala ya wanaosababisha; kwa kuifanya isikubalike, wakati

57. Haki katika kifungu cha 17 zinaweka, miongoni mwa mengineyo, majukumu yafuatayo kwa nchi wanachama: … xiv. Kuhakikisha kwamba wasichana wanaopata ujauzito kabla ya

kumaliza elimu yao wana fursa ya kuendelea.

Kifungu cha 11: Elimu 6. Nchi wanachama katika Mkataba huu watachukua hatua zote muafaka

kuhakikisha kwamba watoto wanaopata mimba kabla ya kuhitimu elimu yao watapata fursa ya kuendelea na masomo yao kwa kuangalia vigezo vya uwezo wao.

Page 43: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

36 Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

inashindwa kuweka mazingira rafiki kwa msichana katika shule yaliyo huru kutokana na ngono za lazima; kwa kutofanya isirekebishike, wakati inashindwa kuheshimu, kulinda na kutimiza haki ya kupata elimu ya msichana, na bila kujali sauti yao na hali yao ya maisha, na kuendeleza vitendo vya kibaguzi kwa kukiuka maslahi na haki ya mtoto.

Ubaguzi wa kijinsia unazuiwa na Katiba ya Tanzania, Sheria ya Elimu, Sheria ya Haki za Mtoto na sehemu nyingine zozote. Nje ya sheria za ndani, Tanzania inawajibika kuondoa ubaguzi wa kijinsia kwa kuridhia ICESCR, CADE, CEDAW, CRC, ACHPR na ACRWC. Maoni juu ya ripoti kutoka Lesotho, Kamati juu ya Haki za Mtoto moja kwa moja inaunganisha vyote viwili ubaguzi na haki ya kupata elimu wakati inajadili jambo hili:

(Kamati ya UNCRC, 2001a) Japokuwa kisheria suala hili laweza kushughulikiwa vizuri zaidi ndani ya nchi kama suala la ubaguzi, inaweza isifikie huko kwa vile maendeleo ya Siasa yapo. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameshatoa matamko mara kadhaa kuhusu kubadili sera ya kufukuza kwani haikukusudiwa kutumika dhidi ya wasichana wajawazito. Japokuwa UNICEF imeonesha dalili ya ushindi juu ya hili, hata hivyo (MediaGlobal, 2010, Machi 19, Sheria mpya zinaruhusu mama watoto kupata elimu nchini Tanzania; Mama watoto sasa wanaweza kurudi darasani, 2010, Machi 21, Citizen), mabadiliko ya sera kuruhusu mama watoto kurudi shuleni yanasubiriwa (‗Hakuna mpango wowote kuhakikisha wanafunzi wenye mimba wanarudi shule,‘ 2010, Aprili 19). Kimsingi kubadilika kwa sera ambako Wizara inajadili si kuzuia ufukuzaji wa wasichana wenye mimba lakini ni kuwapatia fursa mama watoto kurudi shule. Hata hivyo hii ni hatua nzuri kuelekea kutimiza makubaliano ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambayo Serikali ya Tanzania imeridhia. Kwa kuangalia ile hali tete ya kijamii katika suala la wanafunzi wajawazito katika mashule, huu si mwanzo mbaya katika jitihada za kutafuta na kuipata haki ya kupata elimu kwa watoto wote. Ni kwa sababu ya mitazamo hii ya kijamii kwamba kila mmoja ajue uhalali wa uwezekano wa kupigania haki hii kwa njia ya Mahakama, hata kama sheria imebadilika, kwa sababu mwisho wa siku ni mazingira ya kijamii yanayoweka tishio kubwa kwa mama watoto kupata elimu, katika maeneo kadhaa nchini Tanzania. Elimu kwa wasichana inaonekana kuwa ni anasa na kama msichana akipata mimba akiwa shuleni, ni kwamba kuna makubaliano katika jamii kwamba sasa msichana huyu anapata fursa ya kufanya majukumu yake kama mama na sasa jukumu la kuwa mwanafunzi basi. Kwa maneno mengine japo kuwa elimu ya msichana inaendelea, mahali pa mwanamke bado panaonekana kuwa ni nyumbani. Kwa mantiki hiyo, hata kama kuna mabadiliko katika sheria, vikwazo vya kijamii bila shaka vitaendelea kukwamisha mama watoto wasihitimu elimu yao ya msingi. Japo sheria ya kuhakikisha kwamba mama watoto wanaendelea na elimu inaweza kubadili mtazamo wa kijamii na mambo mengine ya msingi katika hili, mchakato huu hauwezi kuanza endapo tunu za

53. Kamati kwa hisia za ndani kabisa imeona kwamba wasichana wanapata mimba wakati wakiendelea na masomo mara nyingi wanaondolewa shuleni na kwamba tendo hili si tu kwamba ni ubaguzi dhidi ya wasichana bali ni ukiukaji wa haki ya kupata elimu. 54. Kamati inasema na kuomba kwamba nchi wanachama kuhakikisha kwamba wasichana na wenye mimba wanaruhusiwa kuendelea na shule wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.

Page 44: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kufukuzwa kwa Wanafunzi Wajawazito

37

jamii zina nguvu kiasi cha kuathiri utekelezaji wa sheria mpya, mathalani katika mashule, kuwabagua mama watoto kwa mtazamo wa kihistoria zaidi kuliko kisheria ni ushahidi tosha kwamba tunu hizi za kijamii zina nguvu, na ipo hatari kwamba hata kama sera itabadilika walimu wanaweza kuendelea kutotilia mkazo kuhakikisha kwamba mama watoto wanakaa shuleni. Nchini Tanzania kwa sasa kuna maoni toka kwa waelimishaji wengi kwamba wasichana wenye mimba na mama watoto si watu wa kuwa shuleni. Wanaamini kwamba uwepo wa wasichana hawa ni tishio kwa nidhamu shuleni na machafuko ya kijamii yaweza tokea. Endapo wasichana wajawazito na mama watoto wataruhusiwa kuendelea na shule, wasichana wengine watakuwa na mtazamo kwamba tabia hii inakubalika na wao pia watajihusisha na ngono na pia mimba za utotoni (Policy Forum, 2007; MediaGlobal, 2010). Japokuwa kuna hatari ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, hatari wakati wa kijifungua na wakati mwingine na hatari za kimaono zinazosababishwa na kubakwa na mimba za utotoni, waelimishaji wengi nchini Tanzania wanaamini kwamba ujumbe kwamba mimba za utotoni zina madhara makubwa, unaweza tu kuoneshwa au kutolewa kwa njia ya kuwafukuza kabisa wasichana wajawazito kutoka shule na wasirudi tena. Mtazamo huu ambao upo miongozi mwa walimu wa Tanzania—ambao hasa walipaswa kuisimamia elimu—wanaendeleza mtazamo kwamba wasichana hawa kuendelea kupata elimu ni anasa kwao na wala si kuwanyima haki. Kwa hiyo hata kwa kuwa na sera mpya yenye kulinda tunu za jamii zinazopelekea walimu wenyewe kushikilia msimamo na mtazamo kinzani kwa haki ya elimu, waweza hatimaye kuleta hatari kubwa katika kuendelea kielimu kwa mama watoto. Ukizingatia kudai haki hii kwa njia ya mahakama kwa mama watoto, ni hali hii inapaswa kuangaliwa—kukataliwa kurudi shule kwa mama licha ya kulindwa kisheria. Kwa kupata Sera mpya ndani ya nchi itakayoanza karibuni, kesi ya kimkakati ya suala hili ingelenga kuhakikisha utekelezaji wake kwa kushinda kesi ya aina hii katika mahakama za ndani ili kuonesha taifa kwamba sera mpya ni lazima ifuatwe. Kwa kuangalia umuhimu wa hali ya juu wa suala hili, serikali bila tashwishwi itaweka bayana nia ya kubadilika, na mahakama zitafuata mabadiliko katika sheria ili kuendana na nia hiyo uamuzi ulio wazi wenye mtazamo chanya utasaidia sana katika kutekeleza sera mpya. Kwa sheria mpya na maamuzi tarajiwa ya mahakama kuhakikisha kwamba mama watoto wanapata haki sawa ya kupata elimu, suala la msingi la kufukuza wasichana wenye mimba litapata fursa zaidi ya kuangaliwa kwani masuala haya hujadiliwa kwa pamoja. Wakati jamii, walimu, na maafisa wa serikali wanaendelea kuelimishwa ili kufikia uelewa wa juu wa kutokuwa na ubaguzi na haki ya kupata elimu, yaweza kuja siku moja watu wengine zaidi wakiwa na mtizamo wenye kufanana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Colombia ambayo iliona kwamba ―kupata mimba—kupitia kanuni za shule—kama kigezo cha adhabu hukiuka haki za msingi za usawa, usiri, uhuru wa kukua kwa haiba na elimu‖ (UNCHR, 2000, §60).

Page 45: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

38 Adhabu ya Viboko

Adhabu ya Viboko

Kwa maoni ya Kamati, adhabu ya viboko inakinzana na haki ya msingi ya kanuni mwongozo ya haki za binadamu kimataifa kama inavyoainishwa katika utangulizi wa Tamko la Dunia la Haki za Binadamu na Mikataba yote miwili: utu wa mtu.

(UNCESCR, 1999b, §41) Kamati kwa kurudia tena na tena imeweka wazi katika kuhitimisha kwamba matumizi ya adhabu ya viboko hayaheshimu haki ya utu wa mtoto ambayo anaipata kwa kuzaliwa na hata mipaka ya kinidhamu katika shule.

(Kamati ya UNCRC, 2001b, §8) Kuhakikisha usalama wa watoto wa shule kwa…kuchukua na kutekeleza upigaji marufuku juu ya matumizi ya adhabu ya viboko.

(Tume ya ACHPR, 2009, §57(xv)) Nchi wanachama wa Mkataba huu watachukua hatua muafaka kuhakikisha kwamba mtoto ambaye amepitia kuadabishwa shuleni au nyumbani atatendewa kwa utu na heshima yake na kwa kufuata Mkataba huu.

(OAU, 1990, §5) Adhabu ya viboko yaweza kutolewa kwa makosa makubwa ya kinidhamu au uvunjifu mkubwa ….

(URT, 2002b) Kuchapa viboko wanafunzi watukutu katika shule za msingi na sekondari ni lazima….

(Margaret Sitta, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Mwandishi wa Daily News, 2006)

Kimsingi kuna tatizo hapa, ambalo ni kwamba japokuwa nchi zimeridhia makubaliano na mikataba kadhaa ya kikanda na kimataifa kuhakikisha kwamba adhabu ya viboko haitumiki mashuleni, Tanzania, kupitia sheria zake na viongozi wake, kiukweli kabisa hutekeleza adhabu hii. Kama inavyoonekana hapo juu, wakati upigaji marufuku wa adhabu ya viboko unapata chanzo chake kutoka ICESCR, CRC, ACHPR na ACRWC, Sheria ya Elimu ya Tanzania na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi vimerasimisha adhabu hii na kusimamia matumizi yake. Adhabu ya viboko haifanyiki kwa bahati mbaya katika shule za Tanzania, bali ni mfumo ulioendelezwa. Kanuni za adhabu ya viboko zinapatikana katika Tangazo la Serikali Na. 294 la mwaka 2002 likirekebisha Sheria ya Elimu. Miongoni mwa vitu kadhaa, linaeleza:

―Adhabu ya viboko‖ humaanisha adhabu ya kumchapa kwenye mikono yake au kwenye matako yake ambayo kwa kawaida hufunikwa kwa kutumia fimbo nyepesi lakini huondoa kumchapa mtoto kwa kutumia aina nyingine au kitu chochote au katika sehemu nyingine ya mwili;

Page 46: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Adhabu ya Viboko

39

(URT, 2002b) Kwa ufupi, mambo ya msingi ya kuangalia yanaonekana kuwa ni adhabu ya viboko kwa kuwadhibu wanafunzi ―kwenye mikono yake au kwenye matako yake ambayo kwa kawaida hufunikwa kwa kutumia fimbo nyepesi.‖ Inatakiwa kutolewa pale ambapo ―makosa makubwa‖ au ―makosa ya hatari‖ yametendeka kwa kuzingatia kiwango na ―isizidi viboko vine.‖ Ni wakuu wa shule tu, au walimu wengine kwa ruhusa ya maandishi ya mkuu wa shule, wanaweza kutoa adhabu hii, na wanafunzi wa kike wanaweza tu kupata adhabu hii ya viboko kutoka kwa walimu wa kike, isipokuwa pale ambapo hakuna mwalimu wa kike. Hatimaye, matukio yote ya adhabu ya viboko ni lazima kuandikwa katika kitabu kwa kumbukumbu. Ni wazi kwamba, sheria hizi mara kwa mara zinavunjwa, wanafunzi wanachapwa viboko kwa sababu ya kufanya karibu kila kosa au utovu wa nidhamu, bila hata ya kutunza kumbukumbu. Ni wazi kabisa inakubalika kama ada, hata hivyo kuna nyakati ambapo kukubalika kwake hufikia ukomo, mnamo mwaka 2004, wanafunzi wa shule ya sekondari Kahororo kule Bukoba waligoma kwa masaa matano, wakipiga walimu wao, na viranja na kuvunja madirisha, baada ya mwanafunzi wa kidato cha pili kupigwa hadi kuzimia na kiranja ―katili‖ (Mwandishi wa Guardian, 2004). Hali hii haikupingwa na uongozi wa shule, ambao unasemekana kwamba ulishampatia ruhusa kiranja huyu kuchapa wenzake hadi viboko vitano. Tukio hili linaonesha ni jinsi gani uzembe katika kusimamia adhabu hii kunavyoweza kujenga utamaduni wa kuvunja haki za binadamu. Katika tukio hili, kiranja alipewa mamlaka kinyume na taratibu kutoa adhabu ya viboko katika kiwango kinachozidi idadi ya viboko vinne na akazidisha kiwango cha kuchapa kwa kuchapa zaidi na kufanya mwanafunzi azimie. Na wakati huo huo, kesi nchini kote zinazohusu wanafunzi wanaopewa adhabu kupita kiasi hazitangazwi kwa sababu mambo haya yamekuwa ni ya kawaida tu. Inaonekana kwamba kuruhusu adhabu ya viboko kwenye eneo la elimu kunasababisha uharibifu wa mifumo mingine ya nidhamu ya sekta nyingine—pale taifa ―linapofundishwa‖ kwamba hii ndio njia sahihi ya kutoa nidhamu ni lazima kwamba njia hiyo itatumika kwengine pia. Mnamo mwaka 2009

3. (1) Adhabu ya vikobo yaweza kutolewa pale ambapo kuna makosa makubwa ya kinidhamu shuleni au makosa ya hatari, makubwa yaliyotendwa ndani au nje ya shule, ambayo pia uongozi wa shule unaona yanaweza kuleta vurugu shuleni . (2) Adhabu ya viboko itakuwa ya maana endapo itakuwa imezingatia ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi vikobo vinne kwa kila tukio au kosa. 4. (1) Mkuu wa shule kwa uamuzi wake anaweza kutoa adhabu ya viboko au anaweza kumruhusu mwalimu mwingine kwa njia ya maandishi, mwalimu anayechaguliwa kwa makini miongoni mwa walimu ilimradi tu mwalimu huyu anapotoa adhabu husika awe ameidhinishwa kwa maandishi na mkuu wa shule, kila anapotoa adhabu ya viboko. (2) Kwa mujibu wa kanuni hii utoaji wa adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa kike umeruhusiwa kwa walimu wa kike tu isipokuwa pale ambapo shule haina mwalimu wa kike, mwalimu wa kiume aweza kutoa adhabu ya viboko. 5. (1) Katika kila tukio ambapo adhabu ya viboko inatolewa, kumbukumbu itatunzwa kwa njia ya maandishi; kumbukumbu hiyo itataja jina la mwanafunzi, kosa lake au uvunjifu wa nidhamu, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo. (2) Kila kumbukumbu ya adhabu itaandikwa na kutolewa na mkuu wa shule.

Page 47: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

40 Adhabu ya Viboko

kulitokea zogo baada ya walimu 19 wa shule tatu tofauti huko Bukoba kutandikwa viboko mbele ya wanafunzi wao kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya kwa sababu ya tabia za uzembe na uvivu za walimu zilizosababisha matokeo mabovu kwenye mitihani. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kiliwasilisha mashitaka ya kudai kwamba walimu hawa ―waliaibishwa,‖ na kusababisha Mkuu wa Wilaya kufukuzwa kazi (BBC, 2009). Ya kufanana na hayo, huko Shinyanga kwenye miezi ya kwanza ya mwaka 2010, walimu wanne walichapwa viboko hadharani na walinzi wa jadi wa Sungusungu kwa kushindwa kuhudhuria mkutano ulioitishwa. Hapo tena, CWT kililalamika kwamba kwa kupitia adhabu hiyo walimu hawa walikuwa ―wamevuliwa utu wao.‖ Simulizi za aina hii zinaibua maswali mengi, la kwanza likiwa kwa nini watu wanashangaa matukuo kama haya? Shule ni asasi za kijamii zinazoandaa kizazi cha vijana wadogo ili waweze kujumuika katika jamii kwa mafanikio, na pia kuwafundisha kwa ujumla namna ya kuenenda katika jamii. Kama wanafunzi wanafundishwa kwamba adhabu ya viboko ni njia sahihi ya kuleta nidhamu, kuna uwezekano mkubwa kwamba wataiga na kutumia njia hiyo wenyewe, kama wanafunzi na kama watu wazima kwenye sekta yoyote ya jamii watakayoingia katika siku za mbeleni. Kwa walimu wenyewe kushangaa wanapopewa adhabu hiyo, wakati wao ndio watekelezaji wa mfumo huu, ni kuonesha kuwa na upeo mdogo wa kutazama mbele. Vile vile, sababu zinazotolewa na walimu hawa za kuwafanya walalamikie adhabu hiyo ni zilezile zinazotolewa na taasisi za kimataifa zinazopinga adhabu ya viboko. Walimu wamelalamika (hapo wao wanapokuwa wahanga) kwamba adhabu hii ―imewadhalilisha‖ na ―kuwavua utu wao.‖ Ukweli ni kwamba lugha hii ndiyo hiyohiyo inayotumika kwenye mikataba ya haki ya Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika wakati wa kupinga adhabu ya viboko na kuelezewa kwamba haiendani na kanuni za msingi za ―ubinadamu‖ pamoja na za ―heshima ya binadamu.‖ (OAU, 1990, §5; UNCESCR, 1999b, §41; Kamati ya UNCRC, 2001b, §8). Je, walimu hawa, ambao wao wenyewe wamewahi kutoa adhabu za viboko zisizoweza kuhesabika, wanaweza kutambua kwamba watoto nao ni sehemu ya ―binadamu‖ kwa tafsiri ya chini kabisa? Je, ni kweli kwamba elimu bora inaweza kutolewa kwa watoto kutoka kwa wakufunzi wasiotambua kwamba watoto nao wanastahili kuwa na haki za binadamu? Kwa kutathmini, mfumo wa kisheria wa ndani ya nchi, ijapokuwa umehalalisha adhabu ya viboko, unaweza kutoa mlango mzuri wa kuingilia—kwa kuweka kanuni zinazoeleweka vizuri zinazohusu adhabu ya viboko, pia inatoa mianya mikubwa ya kukiuka kanuni hizo, hali ambayo kwa sasa inajitokeza sana katika mifumo ya shule zetu. Kisiasa, tunu za kijamii zina nafasi kubwa ya kuweza kuleta suluhu kwenye maendeleo ya kisheria kama wanasiasa, watunga sera na watekelezaji wa sera wataweza kufumbia macho sheria yoyote inayopiga marufuku adhabu ya viboko. Kizuizi kikubwa cha kukomesha adhabu ya viboko mashuleni ni mtazamo huu wa kijamii. Inaonekana kwamba asilimia kubwa ya Wantanzania—kuanzia viongozi wa jamii kwenda kwa wazazi na kuelekea kwa walimu—wanaamini sana kwamba adhabu ya viboko ni lazima wakati wa kufundisha watoto, wawe nyumbani au shuleni. Mara nyingi, maongezi yanayohusu uharibifu katika jamii yanaambatana na malalamiko kwamba watoto hawapigwi sana au kwa mara nyingi kama ilivyokuwa zamani. Watu huongelea kwamba adhabu ya viboko ni lazima katika malezi ya mtoto kwa Kiafrika, na kwamba kupiga watoto ni sehemu ya utamaduni wa Kiafrika ili kuwafanya wawe na tabia njema. Mara nyingi, walimu wenyewe wanashindwa kupata picha jinsi wanavyoweza kutunza amani kwenye vyuo ikiwa watanyang'anywa uwezo wa kupiga wanafunzi. Ingawa walitoa tahadhari kwa sauti kubwa, kitendo hapo juu cha kupiga watu wazima kilionesha jinsi adhabu ya viboko inavyokubalika katika jamii. Katika kesi moja, kuna wazazi waliolalamika kwamba Mkuu wa Wilaya asifukuzwe kazi kwa sababu alikuwa sahihi kwa kuchapa viboko walimu wale.

Page 48: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Adhabu ya Viboko

41

Pamoja na hayo, upigaji marufuku wa adhabu ya viboko kwenye shule na kwingineko, umeweza kupenya kwenye Rasimu ya Sheria ya Watoto ya Zanzibar 2010, na ingawa wapo raia wanaotoka sekta za kila aina—ukijumlisha elimu, siasa, na dini—wanaopendekeza mabadiliko (Yussuf, 2010a), wapo wengine wanaoendelea kutoa sababu zile zile za kuendeleza adhabu ya viboko. Mbunge mmoja alitoa hoja kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Juni na kusema: ―Adhabu ya viboko inabaki kuwa muhimu kwenye malezi ya watoto pamoja na kujenga tabia njema shuleni. Tusipige marufuku adhabu ya viboko.‖ Mbunge mwingine aliunga mkono kuendeleza matumizi ya adhabu ya viboko, akisisitiza kwamba imeruhusiwa na mafundisho ya Kurhani, na kwa namna fulani akaongezea kwamba ―kuwe na upigaji marufuku tu wa wanafunzi kuumizwa na kunyanyaswa shuleni‖ (Yusuf, 2010b). Ingawa kesi ya kupinga mapigo ya kupita kiasi, kwa kutumia sheria za ndani ya nchi, inaweza kuleta majibu ya sehemu moja ya muda mfupi, mabadiliko ya kweli ya sera (na zaidi ya hayo, utekelezaji wake) kwa kuibana serikali ya Tanzania kwenye Mahakama ya Afrika ndiyo yatakayoleta mafanikio makubwa kushughulikia muktadha huu kijamii. Kanuni na sheria ya adhabu ya viboko inavunjwa kila siku na wakosaji hawa ni lazima wawajibishwe. Wakati kanuni iliyopo inapaswa kutekelezwa, haipaswi kuimarishwa—yaani, wakati wakosaji wanapaswa kuwajibishwa, wanaharakati wawe makini ili kwamba wasichochee sheria iliyopo kuonekana kwamba inafaa kama nia ni kuhakikisha kwamba adhabu ya viboko inapigwa marufuku. Wakati huohuo, kampeni ya kijamii inatakiwa. Jamii inahitaji kuelimishwa kwamba japo kuna maoni mbalimbali, tafiti zinaonyesha kwamba adhabu ya viboko haileti mabadiliko yanayotarajiwa katika maisha au tabia ya mtoto (Kelly na Wesangula, 2010) na kwamba kuchapa si sehemu ya asili ya utamaduni wa Kiafrika bali ni utamaduni wa kitumwa na ukoloni ulioletwa Afrika na watu wa Magharibi (Mkakati wa Dunia Nzima wa Kukomesha Adhabu Zote za Viboko kwa Watoto, 2010). Katika kuhakikisha mabadiliko katika tabia ya watoto, walimu wanahitaji kufunzwa na kuoneshwa aina zingine za njia zinazoweza kuchochea mabadiliko ya tabia kwa mtoto na mbinu zingine ambazo si korofi, kwa hiyo kunapokuwa na mjadala katika adhabu ya viboko, hawatajisikia kwamba mbinu yao pekee imeondolewa. Wanapoona wenzao wanawajibishwa kwa sababu ya kukiuka kanuni au sheria ya viboko, walimu wanaweza kujielekeza katika mbinu mbadala za kuadabisha watoto. Endapo masuala haya hayatazungumziwa ili kupata suluhisho adhabu ya viboko bila shaka itaendelea katika sehemu nyingi kwa matakwa ya jamii, wazazi, na walimu hata kama kuna mabadiliko katika sera yanayozuia adhabu hii. Sura hii ya mwisho ni sawa kabisa na kile kinachotokea Uganda ambapo adhabu ya viboko inaendelea shuleni ilhali kuna waraka wa mwaka 2006 ulitolewa na Wizara ya Elimu na Michezo ukipiga marufuku adhabu hii. Matokeo yaleyale pia nchini Kenya ambako adhabu ya viboko inaendelea japokuwa vifungu vya sheria vilivyokuwa vinairuhusu vilifutwa rasmi mwaka 2001 na katiba mpya inapiga marufuku adhabu ya viboko katika nyanja zote. Lengo la kesi yoyote kuhusu suala hili ni kuondoa adhabu ya viboko, si tu kupata mabadiliko ya kisera. Hata kama adhabu ya viboko itafutwa ukiukaji huu wa haki ya kupata elimu hautakoma katika jamii inayoamini kwamba ―ukiacha kiboko unamharibu mtoto.‖ Nchi jirani kwa Tanzania zinajaribu kuondoa adhabu ya kiboko baada ya miaka mingi ya kushuhudia watoto wakichwapwa hadi kulemaa, kuharibiwa viungo vyao, kulazwa hospitali na hata kifo. Matukiko kama haya pia nchini Tanzania si kwamba hayasikiki. Je Tanzania itasubiri kwa muda gani ili kukomesha hali hi?

Page 49: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

42 Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II Mnamo mwaka 2009, matokeo ya mtihani wa shule ya msingi yalishuka kwa kiwango cha 50% kwa maneno mengine wanafunzi waliopata elimu ya msingi nusu yao hawakupata elimu kwa kiwango kilichotarajiwa:

(URT 2008a, 2010b) Kupanda na kushuka huku kunaendana na mpango wa elimu wa hivi karibuni ambao ulikuwa unatolewa na mkakati wa kitaifa wa serikali unaoitwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). MMEM ni mpango mkakati muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sekta elimu ya msingi Tanzania. Unajadili na kuonesha shabaha, kwa namna mbili ya kimatokeo na kibajeti, kwa ajili ya kuandikisha, kuajiri walimu, kujenga madarasa, nyumba za walimu, na vyoo, ununuzi wa madawati, na mengineyo. Kwa sasa mpango huu upo katika awamu ya pili. MMEM I ulianza mwaka 2002 hadi mwaka 2006, na MMEM II unaendelea toka mwaka 2007 hadi mwaka 2011. Japokuwa zinabeba majina sawa na malengo sawa, awamu hizi mbili za MMEM zinaonekana kuwa tofauti kabisa kiutendaji. Wakati utekelezaji wa MMEM I ulishuhudia kukidhi na nyakati zingine kuzidi malengo, MMEM II haifikii malengo na utekelezaji wake ni wa viwango vya chini sana kwa kuwa na asilimia zenye tarakimu moja tu. Mathalani, mwaka 2003 MMEM I ulijenga madarasa mapya 10,771 (asilimia 80) kati ya malengo ya madarasa 13,396, wakati mwaka 2008, MMEM II ulijenga madarasa 1,263 (asilimia 12) ya madarasa 10,753 yaliyotarajiwa. Katika hali hiyo, mwaka 2005 MMEM I ulijenga nyumba za walimu 3,528 (asilimia 111) kati ya nyumba 3,169 zilizokusudiwa, lakini mwaka 2008 MMEM II ulijenga nyumba 277 (asilimia 1) wakati mpango ulitarajia kujenga nyumba 21,936 (HakiElimu, 2007; URT, 2008b; URT, 2006b). Mahitaji haya yanaathiri matokeo ya elimu. Wakati uandikishaji wa wanafunzi unaongezeka lakini madarasa mapya hayajengwi, madarasa yanafurika, na uwiano wa darasa kwa wanafunzi unaongezeka. Wakati ujenzi wa madarasa kipindi cha MMEM I ulisaidia uwiano wa darasa kwa wanafunzi kuwa 1:72, ukosefu wa ujenzi umeuruhusu tena kuongezeka kuwa 1:78, uwiano ambao ni

70.5%

49.4%

0

10

20

30

40

50

60

70

80

2002

2003

2004

2005

2006

2007

2008

2009

2010

Asi

lim

ia W

ali

ofa

ulu

Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi

Page 50: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

43

wa juu zaidi hata kabla ya MMEM kuanza. HakiElimu, katika chapisho lake la ―Elimu Inaenda Kinyume: Je, MMEM II Inabatilisha Maendeleo ya MMEM I?‖ ililinganisha mwenendo huu:

(HakiElimu, 2010) Vile vile, nyumba za walimu ni tatizo kubwa kwa walimu wanaopelekwa maeneo ya vijijini. Mara nyingi nyumba hizi ni chini ya viwango ambavyo walimu wamezoea kuishi, endapo nyumba zipo. Ukijumlisha na mishahara duni, suala hili la tatizo la nyumba linasababisha waelimishaji kuacha kazi ya ualimu au kutoingia kazi hii kabisa. Hali hii inaathiri sana upatikanaji wa walimu na pia huathiri sana uwiano kati ya walimu na wanafunzi kwa mantiki hiyo, wakati MMEM I ilishuhudia kuajiriwa kwa walimu kwa kiwango cha juu kwa idadi ya 14,423 mwaka 2004, MMEM II iliajiri nusu ya hao tu yaani 7,800 mnamo mwaka 2008, na sasa tena uwiano katika ya walimu na wanafunzi umeongezeka:

(HakiElimu, 2010) Maelezo ya tofauti kubwa katika awamu hizi mbili za MMEM ni bajeti: MMEM I ulipata fedha nyingi za maendeleo kuliko MMEM II. Kwa wastani, MMEM I ulipokea shilingi bilioni 109.1 kama fedha za maendeleo kwa mwaka, wakati MMEM II umekuwa ukipokea shilingi bilioni 14.5 kwa mwaka, asilimia 13 tu ya fedha za maendeleo za MMEM I. Kwa hiyo, wakati madarasa 8,817 yalijengwa mnamo mwaka 2002 kwa shilingi bilioni 43.4, madarasa 1,263 yalijengwa mwaka 2008 kwa shilingi bilioni 1.8 (URT, 2002a, uk. 20, 40; URT, 2008b, uk. 11). Mwenendo mzima katika fedha za MMEM unaainishwa katika ukurasa ufuatao. Kwa sababu ya upatikanaji wa taarifa za

Page 51: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

44 Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

bajeti, fedha nyingine zinaainishwa kama fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo wakati nyingine ni kama matumizi halisi.

(URT, 2003b, 2004, 2006d, 2007, 2009e) Chati hapo juu haioneshi tu tofauti ya kibajeti kati ya awamu mbili za MMEM, bali inaonesha suala jingine la kibajeti, ambayo ni tofauti ya fedha zinazotolewa mwanzoni mwa mwaka, na matumizi halisi mwishoni mwa mwaka. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha wa 2005/2006, bilioni 76.8 ziliidhinishwa na Bunge kama fedha za MMEM lakini shilingi bilioni 31.9 tu zilitumika. Je, ilikuwa ni kwa sababu wafadhili walishindwa kutoa asilimia 40 ya ahadi yao katika elimu hadi robo ya mwisho wa mwaka, na kuifanya serikali ya Tanzania ishindwe kuzitumia ndani ya mwaka husika (URT, 2006a, c)? Au hii inahusiana na kubadilika kwa vipaumbele vya elimu kutoka maendeleo ya elimu ya msingi kwenda katika mkazo wa elimu ya sekondari ambayo ndiyo ilikuwa sehemu ya agenda ya kampeni za ushindi mnamo mwaka 2005 katika majukuwaa ya kisiasa? Vyovyote vile, mwenendo kati ya MMEM I na MMEM II yaweza kwa usahihi na usalama zaidi kuhitimishwa kama suala zaidi la kibajeti na vipaumbele vyake. Wakati MMEM unaendelea kupokea fedha za maendeleo kila mwaka, bajeti yake hata hivyo imekuwa ikipungua kila mwaka. Chati katika ukurasa unaofuata unaweka bajeti ya maendeleo ya mpango wa MMEM ndani ya bajeti yote. Tafiti zaidi na upatikanaji wa taarifa unatakiwa kuziba pengo katika miaka ambayo jumla ya bajeti ya MMEM haijulikani, lakini inadhaniwa kwamba jumla yote ya bajeti ya MMEM imefikia kukua kwa ujumla kama inavyooneshwa mnamo mwaka 2008 unaofahamika:

Shilingi bilioni 7.3

Shilingi bilioni 149.4

0

20

40

60

80

100

120

140

160

2002

2003

2004

2005

2006

2007

2008

2009

2010

PEDP I PEDP II

Mab

ilio

ni

ya S

hil

ing

i

Fedha za Maendeleo ya MMEM

PEDP Development Budget PEDP Development Expenditure

MMEM I MMEM II

Bajeti ya Maendeleo ya MMEM Matumizi ya Maendeleo ya MMEM

Page 52: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

45

(URT, 2003b, 2004, 2005, 2006d, 2007, 2009e)

Wakati mihimili hapo juu inawakilisha bajeti ya jumla ya MMEM na sehemu ya kiitwacho fedha ya maendeleo ya MMEM, sehemu ya ziada ya bajeti ya MMEM inajumuisha mishahara na marupurupu, ruzuku, mitihani ya taifa, na gharama zingine. Kwa juu juu, kutokuongezeka kwa fedha za MMEM hakuoneshi uhalisia wa ongezeko la kutokuwepo jitihada za maendeleo katika mpango huu. Walimu na uandikishaji umeongezeka kukaribia asilimia 40 tangu mwaka 2002, na ruzuku zimepungua hasa kuanzia MMEM II kuliko wakati wa MMEM I. Hata hivyo, bajeti isiyo ya maendeleo ya mwaka 2008 katika MMEM II, ni mara nne zaidi kuliko ile ya MMEMI. Tafiti zaidi zinatakiwa ili kujua kwa hakika pesa hizi zinakwenda wapi, kwa yakini kabisa zile zinazotolewa katika eneo la jumla la matumizi mengine. Kupanuka kwa MMEM II katika mgao wa fedha kwa matumizi yasiyo ya maendelo kunaibua bendera nyekundu. Serikali ina vyanzo viwili vya msingi vya matumizi—matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Fedha ya matumizi ya kimsingi ni fedha zinazotumika ili kuhakikisha serikali inafanya kazi, ambapo fedha za matumizi ya kawaida ya serikali husaidia shughuli mbalimbali za serikali na kuboresha miundombinu na utoaji huduma. Fedha za matumizi ya kawaida ni lazima kwa serikali ili iweze kufanya kazi, lakini pia inapigiwa kelele kama chanzo cha matumizi mabaya ya fedha ya umma kwa sababu ina vitu kama vile posho, semina, kusafiri nje ya nchi na usafiri au mafuta (Sikika, 2010). Matumizi kama haya yanaongezeka wakati miradi ya maendeleo inapunguziwa fedha. Mwaka 2008/09, wakati matumizi yote ya maendeleo ya serikali yalipunguzwa kwa asilimia 34, ukilinganisha na bajeti yote ya taifa na matumizi halisi (URT, 2010a), posho kwa maafisa wa Serikali kusema kweli ziliongezeka kwa asilimia 20 na kufikia shilingi bilioni 506 (Policy Forum, 2009), mara hamsini zaidi ya bajeti ya maendeleo ya MMEM. Katika mwaka huo, Serikali ilitumia shilingi bilioni 31 kwa safari za nje (Sikika, 2010), mara tatu zaidi ya bajeti ya maendeleo ya MMEM. Hili ni suala la msingi la kuangalia nini vipaumbele vya serikali. Wakati MMEM I ilikuwa chini ya mfumo wa ufadhili wa miradi, ikimaanisha kwamba wafadhili walitoa fedha mahsusi kwa ajili ya MMEM I, MMEM II hufadhiliwa na Msaada wa Kiujumla wa Bajeti (GBS), ikimaanisha kwamba Serikali hupokea fedha toka kwa wafadhili na yenyewe kuamua ni jinsi gani itumike. Je, kushuka kwa ghafla kwa bajeti ya maendeleo ya MMEM na matumizi yake katika muktadha wa kuongezeka kwa bajeti ya MMEM kunaashiria au kuonesha kwamba maendeleo ya elimu ya msingi yamekuwa ni kipaumbele cha wafadhili na si kipaumbele cha Serikali? Au haya ni matokeo ya kukataa mkopo mwingine mkubwa kutoka Benki ya Dunia ambao ndio ulitoa sehemu kubwa ya ufadhili toka nje wa

0

100

200

300

400

500

2002

2003

2004

2005

2006

2007

2008

2009

2010

PEDP I PEDP II

Mab

ilio

ni

ya S

hil

ing

iFedha za maendeleo ya MMEM ikiwa sehemu ya bajeti ya jumla

ya MMEM

Total PEDP Budget PEDP Development Budget PEDP Development Expenditure

MMEM I MMEM II

Bajeti ya Maendeleo ya MMEM Matumizi ya Maendeleo ya MMEMJumla ya bajeti ya MMEM

Page 53: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

46 Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

MMEM I? Au kama wengine wanavyoamini katika sekta, kwamba fedha za MMEM II zilipelekwa katika kusaidia mpango wa Serikali wa kujenga majengo ya shule za sekondari ulioanza mwaka 2005? Zaidi ya suala hili, inaibua mjadala ni nini vipaumbele vya serikali katika matumizi ya fedha za wafadhili, yaweza kuonesha au kuwakilisha ukiukaji wa haki ya kupata elimu. Katika mifumo yote miwili ya haki za binadamu katika Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, ni wajibu wa kila mwanachama kuhakikisha upatikanaji wa haki ya kupata elimu, kwa kutumia ―kwa kiwango cha juu cha rasilimali zilizopo,‖ kwamba, nchi wanachama zinawajibika kutumia rasilimali zilizopo, ndani na nje ya nchi, katika kupata na kutekeleza haki za binadamu (Tume ya ACHPR, 2009, §14; UNCESCR, 1999b, §45). Ukianzia hapa ni ukiukwaji wa hatua za kukabiliana na kupungua huku—kwamba nchi wanachama hawawezi kurudi nyuma katika kuhakikisha haki hizi zinapatikana (Tume ya ACHPR, 2009, §21; UNCESCR, 1999b, §45). Kimsingi hii inazungumzwa katika maana ya kushindwa kwa Serikali kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo kuelekea katika kutekeleza haki za binadamu. Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu inaeleza:

(Tume ya ACHPR, 2009, §21) Tume ya Afrika inaelezea tabia zaidi za hatua kupunguza rasilimali inasema, ―Hatua zitakuwa na matukio ya kudumu katika kuhakikisha upatikanaji wa haki zinazolindwa‖ au ―hatua zina matokeo ambayo hayana mantiki kwa mtu binafsi au kundi linalonyimwa kiwango cha chini kabisa cha haki inayolindwa‖ (Tume ya ACHPR, 2009, §21). Je, kupunguzwa kwa fedha za maendeleo za MMEM II kunaleta ―madhara ya kudumu katika kuhakikisha upatikanaji‖ wa haki ya kupata elimu? Ikiwa ukosefu wa ujenzi wa nyumba za walimu unaleta kukatishwa tamaa kwa walimu na kupelekea upungufu wa walimu unaosababisha kukosekana kwa uwiano wa mwalimu-mwanafunzi katika huduma na hivyo matokeo duni ya masomo, basi jibu ni ndiyo. Je, kupunguzwa kwa fedha za maendelo za mpango wa MMEM II kumeondoa haki ya msingi ya kupata elimu? Tunapoangalia mambo ya msingi katika mfumo wa A-4 katika haki ya kupata elimu—uwepo, upatikanaji, kukubalika na kurekebishika (angalia sehemu ya ―Mazingatio ya Kisheria, Kisiasa na Kijamii‖)—uwepo kimsingi tunaufikiria tunapoangalia na kujadili maendeleo ya miundombinu katika sekta ya elimu. Je, ni kwa jinsi gani uwepo unaonekana kuwa ni mdogo kabla haujafikia ―kiwango cha chini kabisa‖? Kupuuzia ujenzi wa madarasa, unaosababisha uwiano wa wanafunzi katika darasa kuwa mara mbili zaidi ya lengo la taifa? Shule zenye wanafunzi 200 na mwalimu 1? Hali hii kimsingi inaonekana kuwa chini ya kile kinachoweza kuitwa ―kiwango cha chini kabisa‖ na kwa wazi kabisa mambo haya yametajwa katika UNCESCR wakati wa kujadili majukumu ya nchi wanachama katika kutimiza upatikanaji wa elimu ―kwa kuendeleza mifumo ya shule, kama

Hatua zinazopunguza kufurahia haki za uchumi, jamii na kiutamaduni kwa watu binafsi au watu kwa ujumla, ni ushahidi wa wazi wa ukiukaji wa Mkataba wa Afrika. Hatua yoyote inayopunguza kiwango cha kufurahia haki za kiuchumi, kiraia, kijamii na kiutamaduni au uwepo wake; ni lazima kuhalalishwa kwa muktadha wa haki zinazoainishwa katika mkataba wa Afrika na katika muktadha wa matumizi ya rasilimali zote zilizopo, katika muktadha huu rasilimali zilizopo una maana ya rasilimali zilizopo ndani ya nchi na kutoka katika misaada ya ushirikiano wa kimataifa.

Page 54: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

47

vile kujenga madarasa, kuendesha programu na kuleta zana za kufundishia…‖ (UNCESCR, 1999b, §50). Hali hizi zimedunishwa kwa sababu ya kupunguzwa kwa fedha za maendeleo za mpango MMEM II na unaonekana kuchukua hatua za kurudi nyuma, hasa kupunguza huku kwa fedha kunapotokea katika sura ya kuongezwa kwa fedha ya mpango wa MMEM II kutoka katika bajeti ya jumla. Swali la msingi katika Mahakama ya Afrika ingekuwa ni kwa kiwango kipi hatua za kurudisha nyuma zinatumika. Bajeti yote ya MMEM II inaongezeka, na si hatua ya kurudisha nyuma. Kipengele chake muhimu ni makato ya mara kwa mara, je ni sehemu ya hatua za kurudisha nyuma? Lakini kama kupunguzwa huku kumefanywa ili kuchukua fedha kwenda sekta nyingine katika kusimamia haki ya kupata elimu, mpango ule wa elimu ya sekondari, je, ndizo hatua za kurudisha nyuma rasilimali za elimu? Kufanya jambo hili lisilete mkanganyiko na liwe halisi, linaweza kuleta aina fulani ya ukiukaji wa haki ya kupata elimu ambayo ni matokeo ya bajeti hii iliyopunguzwa. Kwa mfano, fedha hizi za maendeleo moja kwa moja zinaathiri mazingira ya kazi na mazingira ya kuishi ya walimu. Kwa pamoja AU na UN wanazungumzia jukumu la nchi wanachama kuendelea kuboresha mazingira ya kufundisha:

(UNGA, 1966)

(ACHPR Commission, 2009) Kwa hiyo kunapokuwa na mjadala katika muktadha wa kisiasa juu ya kesi ya haki ya kupata elimu, kimsingi kuna mambo mawili ya kuzingatia. Kwanza, kama hapo juu, matumizi ya kila siku ya serikali, yanapigiwa kelele kwa sababu ya asili yake ya faida binafsi kwa hiyo kama katika MMEM II matumizi ya maendeleo yanapunguzwa wakati matumizi ya kila siku ya serikali yanaongezwa. Kuna uwezekano mkubwa kwamba katika serikali wapo watu wanaofaidika isivyo halali na mipangilio hii. Kwa tishio kwamba faida hizi zaweza kuondolewa, kundi hili laweza kuingizwa katika Mahakama ili kuzuia hali hii, lakini wapo watu wenye mtazamo wa haki na kundi la watu ndani ya serikali ambao wana nia ya dhati ya kuondoa tabia hii, ni wazi wataunga mkono kesi ya aina hii. Pili, serikali na vyama vya siasa wana maslahi katika kutoa huduma kwa raia, lakini pia wana maslahi katika kulinda sifa ya mwonekano wao katika jamii. Wakati fulani HakiElimu ilirusha kipindi katika runinga/redio ikionesha taarifa bayana kuhusu kutokuwepo kwa ujenzi wa nyumba za walimu katika mpango wa MMEM II, ilipokea mwitikio wa kisiasa kwa haraka sana (Siyame, 2010) na pia ikaonekana kana kwamba inaingia katika siasa za vyama. Wanaharakati wa kesi yoyote ya aina hii inayojadili kushindwa kwa Serikali wajiandae kupambana na upinzani mkubwa toka kwa serikali.

57. Haki katika kifungu cha 17 inaweka miongoni mwa mengine, majukumu na wajibu ufuatao kwa nchi wanachama: … ii. …kuendeleza na kuboresha mazingira ya kufundishia walimu.

Kifungu cha 13 2. Nchi wanachama wa mkataba huu zinatambua kwamba, wakiwa na mwono

wa kuhakikisha upatikanaji wa haki hii: … (e) … mazingira ya kazi ya walimu yanaendelea kuboreshwa.

Page 55: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

48 Kupungua kwa Rasilimali za MMEM II

Tukizungumza kijamii, jamii ipo tayari kutatua tatizo hili kama ilivyojadiliwa katika sehemu ya ―Elimu ya Msingi ‗Bure,‘‖ kushindwa kwa serikali kujenga madarasa, nyumba za walimu, na vyoo vya mashimo kunaonekana kwa jamii katika kusukumwa kulipa michango mingi ili jamii zifanye zenyewe. Kesi ya namna hii mahakamani itaungwa mkono na jamii kwani karibu kila mmoja ameshuhudia upungufu huu katika elimu na angependa kuona ukiondolewa. Swali kubwa katika kesi ya aina hii linabaki kuwa ni uhalali wa kiwango cha kutokuwepo kwa uwiano katika hatua zinazotumika. Wakati watu wengi wanawekeza katika kuboresha elimu msisitizo wa rasilimali za MMEM II zisizokuwa za maendeleo kwa MMEM haziwezi kukanushwa kwamba zinazuia haki ya kupata elimu. Hata hivyo, kwa sababu ya ugumu mwingine katika sekta ya elimu, muundo wa bajeti ya elimu yenye kujirudia, mchanganuo kamili wa matumizi yote ya mpango wa MMEM unatakiwa ili kubaini kama ni lazima kweli kuwepo kupunguzwa kwa fedha za maendeleo katika mpango huu. Baada ya hapo itakuwa rahisi kutambua endapo serikali ya Tanzania imekuwa ikitumia ‗rasilimali zilizopo kwa kiwango cha juu‖ bila ya kujali utekelezaji wa bajeti ndogo ya maendeleo ya MMEM II.

Page 56: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Marejeo

49

Marejeo African Commission on Human and Peoples‘ Rights (2009). Draft principles and guidelines on

economic, social and cultural rights in the African Charter on Human and Peoples‘ Rights. Nairobi. Ilipatikana Novemba 8, 2010, kutoka http://www.achpr.org/english/other/ Draft_guideline_ESCR/Draft_Pcpl%20&%20Guidelines.pdf

Agola, E. (2010, Julai 29). Dar schools seriously short of desks. The Gaurdian. Dar es Salaam: IPP

Media. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.ippmedia.com/frontend/?l=19283 Antonowicz, L., Lesné, F., Stassen S., & Wood, J. (2010). Africa education watch: Good governance

lessons for primary education. Transparency International. Ilipatikana Julai 29, 2010, kutoka http://www.transparency.org/content/download/50164/802844/Africa_ Education_Watch_eng.pdf

Baker, T. (2009a). Lessons for Tanzania on achieving the right to information: The 2003 campaign

of Anti Corruption Coalition Uganda. HakiElimu. Dar es Salaam. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.hakielimu.org/hakielimu/documents/document155wp_09_1e_ lessons_for_tanzania.pdf

Baker, T. (2009b). Anti-corruption and access to information: The Right to Information Bill, 2007.

HakiElimu. Dar es Salaam. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.hakielimu.org/ hakielimu/documents/document156wp_09_2e_anti_corruption_access_info.pdf

BBC (2009, Februari 14). Tanzanian teacher whipping move. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka

http://news.bbc.co.uk/2/hi/7890177.stm BBC (2010, Aprili 23). Tanzania union sues after teachers caned. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/8640959.stm Bébien, A. (2010, Machi 10). Pregnant teens forced out of school. Inter Press Service. Ilipatikana

Agosto 3, 2010, kutoka http://ipsnews.net/news.asp?idnews=50623 Child Rights Information Network (CRIN) (2009). Children‘s rights: A guide to strategic litigation.

London: CRIN. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://www.crin.org/docs/ Childrens_Rights_Guide_to_Strategic_Litigation.pdf

Global Campaign for Education, Right to Education Project, & Campaña Latinoamericana (n.d.).

Racism, racial discrimination, xenophobia and related intolerance in education: The case of adolescent girls in Tanzania. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://www.right-to-education.org/sites/r2e.gn.apc.org/files/Case_Study_Tanzania[1].pdf

Claussen, J. & Assad, A. S. (2010, Februari, 8). Public expenditure tracking survey for primary and

secondary education in mainland Tanzania. United Republic of Tanzania. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://www.ansa-africa.net/uploads/documents/publications/ PETS_Education_Tanzania_Final_Report_March2010.pdf

Citizen Reporter (2010, Mei 11). Official orders schools to build latrines. The Citizen. Dar es Salaam:

Mwananchi Communications.

Page 57: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

50 Marejeo

Citizen Reporters (2010, Juni 19). Appeal court ruling denounced. The Citizen. Dar es Salaam:

Mwananchi Communications. Ilipatikana Agosto 9, 2010, kutoka http://www.thecitizen. co.tz/news/4-national-news/2509-appeal-court-ruling-denounced.html

Community Court of Justice, ECOWAS (2009). Registered Trustees of the Socio-Economic Rights

and Accountability Project (SERAP) v. Federal Republic of Nigeria and Universal Basic Education Commission. ECW/CCJ/APP/08/08. Abuja, Nigeria.

Consesa, J. (2010, Juni 17). No private candidate in Novemba. Daily News. Dar es Salaam: Daily

News Media Group. Ilipatikana Agosto 9, 2010, kutoka http://dailynews.co.tz/home/?n= 10905

Coomans, F., Ph.D. (2007, Juni). Identifying the key elements of the right to education: A focus on

its core content. CRC Day of General Discussion. Geneva, Switzerland. Daily News Reporter (2006, Mei 1). Minister defends caning in schools. Daily News. Dar es Salaam:

Daily News Media Group. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.corpun.com/ tzs00605.htm#17647

Department for International Development (2005, Oktoba 6). Tanzanian success in education and

health brings further UK support. Press release. Ilipatikana Novemba 10, 2010, kutoka http://www.dfid.gov.uk/news/files/pressreleases/tanzania-education.asp

East African Community (2007). Treaty for the Establishment of the East African Community.

Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.eac.int/index.php?option=com_docman& task=doc_download&gid=158&Itemid=163

Global Initiative to End All Corporal Punishment of Children (2010). Prohibiting all corporal

punishment of children: Frequently asked questions. Ilipatikana Agosto 10, 2010, kutoka http://www.endcorporalpunishment.org/pages/intro/faqs.html

Guardian Correspondent (2004, Septemba 9). Kahororo students go on the rampage. The Guardian.

Dar es Salaam. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.corpun.com/tzs00409.htm #14005

Hahn, K. (2005, Machi). Towards a SADC area of higher education. NEPRU research report no.

30. Namibian Economic Policy Research Unit. Windhoek. Ilipatikana Agosto 5, 2010, kutoka http://www.nepru.org.na/index.php?id=126&no_cache=1&file=112&uid=183

HakiElimu (2004). Elimu Tanzania: Majibu ya maswali yanayoulizwa na Marafiki wa Elimu

(Education in Tanzania: Answers of questions asked by Friends of Education). Dar es Salaam: HakiElimu. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://hakielimu.org/hakielimu/ documents/document75foe_maswali_majibu_INSIDE_sw.pdf

HakiElimu (2007, Oktoba). What has been achieved in primary education? Key findings from

government reviews. Dar es Salaam: HakiElimu. Ilipatikana Agosto 9, 2010, kutoka http:// www.hakielimu.org/hakielimu/documents/document94what_has_been_achieved_pri_edu_en.pdf

Page 58: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Marejeo

51

HakiElimu (2010). Education in reverse: Is PEDP II undoing the progress of PEDP I? 10.1E. Dar

es Salaam: HakiElimu. Human Rights Commission (2010). Chapter 15: The right to education. Human rights in New Zealand

today. Ilipatikana Julai 30, 2010, kutoka http://www.hrc.co.nz/report/chapters/chapter15/ education01.html

Ibadi, M. (2011, Februari 18). Don‘t expel pupils who can‘t pay fees – call. The Citizen. Dar es

Salaam: Mwananchi Communications. James, B. (2010, Aprili 9). Independent candidacy: High Court has no mandate, says AG. The

Citizen. Dar es Salaam: Mwananchi Communications. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.thecitizen.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/1263-independent-candidacyhigh-court-has-no-mandate-says-ag.html

Kapama, F. (2010, Februari 14). Dar lawyer cautions AG over statement on private candidates.

Daily News. Dar es Salaam: Daily News Media Group. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.dailynews.co.tz/home/?n=7505

Kelly, K. & Wesangula, D. (2010, Aprili 3) Spanking does more harm than good. Daily Nation.

Nairobi. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.nation.co.ke/News/Spanking% 20does%20more%20harm%20than%20good%20to%20children%20/-/1056/892392/-/view/printVersion/-/tug9wdz/-/index.html

MDG Awards Committee (2010, Septemba 21). MDG Awards Committee showcases United

Nations progress on Millennium Development Goals (MDGs) at awards ceremony and concert in New York City. New York: MDG Awards Committee. Ilipatikana Novemba 10, 2010, kutoka http://mdgawards.org/files/FileUpload/files/MDG_Awards_Post_Event_ PR.pdf

MediaGlobal (2010, Machi 19). New laws allow teen mothers better access to education in

Tanzania. New York: MediaGlobal. Ilipatikana Novemba 10, 2010, kutoka http://www.mediaglobal.org/article/2010-03-19/new-laws-allow-teen-mothers-better-access-to-education-in-tanzania

Mlacky, H. (2011, Januari 11). Serikali yapiga marufuku wanafunzi kudaiwa michango (Government

prohibits students from being demanded contributions). HabariLeo. Dar es Salaam: Daily News Media Group. Ilipatikana Februari 22, 2011, kutoka http://www.habarileo.co.tz/ kitaifa/?n=13403&cat=kitaifa

Mukajanga, K. D. (2010, Aprili 22). Tanzania: Political will required to achieve freedom of

information. Pambazuka News. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://pambazuka.org/en/ category/advocacy/63861

Mwera, M. J. (2010, Juni 16). Tanzania: Lack of latrines hampers education. Voices of Africa.

Ilipatikana Julai 29, 2010, kutoka http://www.africanews.com/site/Tanzania_Lack_of_ latrines_hampers_education/list_messages/32768

Page 59: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

52 Marejeo

National Bureau of Statistics (2008, Novemba). Household budget survey 2007. Dar es Salaam. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://www.nbs.go.tz/index.php?option=com_ phocadownload&view=category&id=75:hbs-2007&download=169:hbs-2007&Itemid=106

Nkwame, M. (2010, Mei 18). School pregnancy cases reportedly drops in Arusha. Daily News. Dar es

Salaam: Daily News Media Group. Ilipatikana Novemba 10, 2010, kutoka http://www. dailynews.co.tz/home/?n=10025

‗Nothing yet on pregnant pupils back to sch plan‘ (2010, Aprili 19). The Citizen. Dar es Salaam:

Mwananchi Communications. Ilipatikana Julai 29, 2010, kutoka http://www.thecitizen. co.tz/news/4-national-news/1474-nothing-yet-on-pregnant-pupils-back-to-sch-plan.html

Nyerere, J. K. (1974). Freedom and development. In Man and Development. Dar es Salaam: Oxford

University Press. Organization of African Unity (1981). African Charter on Human and Peoples‘ Rights. Ilipatikana

Mei 1, 2010, kutoka http://www.achpr.org/english/_info/charter_en.html Organization of African Unity (1990). African Charter on the Rights and Welfare of the Child.

Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.achpr.org/english/_info/child_en.html Organization of African Unity (1998). Protocol to the African Charter on Human and Peoples‘

Rights on the establishment of an African Court on Human and Peoples‘ Rights. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.achpr.org/english/_info/court_en.html

Policy Forum (2007, Agosto). Should pregnant girls be expelled from school? Jukwa. 5. Dar es

Salaam: Policy Forum. Ilipatikana Februari 24, 2011, kutoka http://www.policyforum-tz.org/files/jukwaa_issue5.pdf

Policy Forum (2009). Reforming allowances: A win-win approach to improved service delivery,

higher salaries for civil servants and saving money. 9.09. Dar es Salaam: Policy Forum. Ilipatikana Agosto 9, 2010, kutoka http://www.policyforum-tz.org/files/ ReformingAllowances.pdf

Sikika (2010). Allowances, seminars, vehicles and travel: A brief on the government‘s initiative to

refocus expenditure. 02.10. Dar es Salaam: Sikika. Ilipatikana Agosto 9, 2010, kutoka http://www.sikika.or.tz/yavworks/Analytical%20works/Allowances%20Seminars% 20Vehicle%20and%20Travel%20april%202010.pdf

Siyame, P. (2010, Juni 19). JK aponda NGO zinazobeza maendeleo yaliyopatikana (JK crushes

NGOs disregarding progress made). HabariLeo. Dar es Salaam: Daily News Media Group. Southern African Development Community (1997, Septemba 8). Protocol on Education and

Training. Blantyre. Ilipatikana Agosto 5, 2010, kutoka http://www.ub.bw/ip/documents/ 1997_SADC_protocol.pdf

Southern African Development Community (2001, Agosto). Consolidated text of the Treaty of the

Southern African Development Community, as amended. Blantyre. Ilipatikana Agosto 5, 2010, kutoka http://www.sadc.int/index/browse/page/120

Page 60: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Marejeo

53

Southern African Development Community Tribunal (2010). The SADC Tribunal in 20 questions:

A guide to SADCT. Ilipatikana Agosto 5, 2010, kutoka http://www.sadc-tribunal.org/ docs/A_Guide_to_SADC_T.pdf

Teen mothers may now go back to class (2010, Machi 21). The Citizen. Dar es Salaam: Mwananchi

Communications. Ilipatikana Novemba 10, 2010, kutoka http://www.thecitizen.co.tz/ news/2-international-news/810-teen-mothers-may-now-go-back-to-class.html

Tomasevski, K. (2006, Agosto). The State of the right to education worldwide: Free or fee: 2006

global report. Copenhagen. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www. katarinatomasevski.com/images/Global_Report.pdf

Tomasevski, K. (2010). The State of the right to education worldwide: Free or fee: 2006 global

report. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.katarinatomasevski.com United Nations Commission on Human Rights, 56th Session (2000, Februari 1). Progress report of

the Special Rapporteur on the right to education, submitted in accordance with Commission on Human Rights resolution 1999/25. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.unhcr.org/refworld/docid/3b00f4290.html

United Nations Committee on the Elimination of Discrimination Against Women, 6th Session

(1987, Aprili 11). General recommendations nos. 2, 3 and 4. A/42/38. Ilipatikana Julai 30, 2010, kutoka http://www.unhcr.org/refworld/docid/453882a822.html

United Nations Committee on Economic, Social and Cultural Rights, 20th Session (1999a, Mei 10).

General comment no. 11: Plans of action for primary education (Art. 14 of the Covenant). E/C.12/1999/4. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.ub.fu-berlin.de/service_neu/ ubpubl/mitarbeiter/dbe/UDHR60/general_comment_CESCR-11.pdf

United Nations Committee on Economic, Social and Cultural Rights, 21st Session (1999b, Desemba

8). General comment no. 13: The right to education (Art. 13 of the Covenant). E/C.12/1999/10. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.unhcr.org/cgi-bin/texis/vtx/refworld/rwmain?docid=4538838c22&page=search

United Nations Committee on the Rights of the Child, 26th Session (2001a, Februari 21).

Concluding observations of the Committee on the Rights of the Child: Lesotho. CRC/C/15/Add.147. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www.unhchr.ch/ tbs/doc.nsf/(Symbol)/CRC.C.15.Add.147.En?Opendocument

United Nations Committee on the Rights of the Child, 26th Session (2001b, Aprili 17). General

comment no. 1: The aims of education. CRC/GC/2001/1. Ilipatikana Julai 30, 2010, kutoka http://daccess-dds-ny.un.org/doc/UNDOC/GEN/G01/412/53/PDF/ G0141253.pdf?OpenElement

United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (2010). Education for all global

monitoring report 2010: Reaching the marginalized. Oxford: UNESCO & Oxford University Press. Ilipatikana Agosto 6, 2010, kutoka http://unesdoc.unesco.org/images/ 0018/001866/186606E.pdf

Page 61: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

54 Marejeo

United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization, 11th Session (1960, Desemba 14).

Convention Against Discrimination in Education. Paris. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/english/law/education.htm

United Nations General Assembly, 3rd Session (1948, Desemba 10). Universal Declaration of

Human Rights. A/RES/217. New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.un. org/en/documents/udhr/

United Nations General Assembly, 21st Session (1966, Desemba 16). International Covenant on

Economic, Social and Cultural Rights. A/RES/2200 (XXI). New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/english/law/cescr.htm

United Nations General Assembly, 34th Session (1979, Desemba 18). Convention on the

Elimination of All Forms of Discrimination against Women. A/RES/34/180. New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/english/law/cedaw.htm

United Nations General Assembly, 44th Session (1989, Novemba 20). Convention on Rights of the

Child. A/RES/44/25. New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/ english/law/crc.htm

United Nations General Assembly, 45th Session (1990, Desemba 18). International Convention on

the Protection of the Rights of All Migrant Workers and Members of Their Families. A/RES/45/158. New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/ english/law/cmw.htm

United Nations General Assembly, 61st Session (2006, Desemba 13). Convention on the Rights of Persons with Disabilities. A/RES/61/106. New York. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www2.ohchr.org/english/law/disabilities-convention.htm

United Republic of Tanzania (1978). The National Education Act. Dar es Salaam: Government

Printer. United Republic of Tanzania (1998). The Constitution of the United Republic of Tanzania. Dar es

Salaam: Government Printer. Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://www.tanzania.go.tz/ images/theconstitutionoftheunitedrepublicoftanzania1.pdf

United Republic of Tanzania (2002a, Septemba). Primary Education Development Plan 2002-2006:

Annual PEDP performance national monitoring report 2001-2002. President‘s Office – Regional Administration and Local Government. Dar es Salaam: Government Printer.

United Republic of Tanzania (2002b). Principal and Subsidiary Legislation Revised Edition 2002.

Dar es Salaam: Government Printer. United Republic of Tanzania (2003a, Aprili). Education Sector Development Programme: Primary

Education Development Programme (2002-2006). Ministry of Education and Culture: Basic Education Development Committee. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://moe.go.tz/pdf/PEDP.pdf

Page 62: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Marejeo

55

United Republic of Tanzania (2003b, Desemba). Joint review of the Primary Education Development Plan (PEDP). Ministry of Education and Culture. Dar es Salaam.

United Republic of Tanzania (2004, Oktoba). Joint review of the Primary Education Development

Plan (PEDP). Ministry of Education and Culture. Dar es Salaam. United Republic of Tanzania (2005, Mei). Education Sector Development Programme: Primary

Education Development Plan (2002-2006): Progress report July-December FY 2004. Ministry of Education and Culture & President‘s Office – Regional Administration and Local Government. Dar es Salaam.

United Republic of Tanzania (2006a, Mei). Budget for fiscal year 2005/06: Quarterly budget

execution report fiscal quarter III January-March 2006. Ministry of Finance. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://www.mof.go.tz/mofdocs/ budget/BerQrtIII2006.pdf

United Republic of Tanzania (2006b, Novemba). Education Sector Development Programme

(ESDP): Primary Education Development Programme II (2007-2011). Ministry of Education and Vocational Training: Basic Education Development Committee. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://moe.go.tz/PDF/ PEDP%20II%20Final%20Doc.pdf

United Republic of Tanzania (2006c, Oktoba). Quarterly budget execution report fiscal quarter 4

and full year 2005/06. Ministry of Finance. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://www.mof.go.tz/mofdocs/budget/ber4200506final.pdf

United Republic of Tanzania (2006d). Volume IV: Public expenditure estimates development votes:

Ministerial and regional development programmes: For the year from 1st July, 2006 to 30th June, 2007. Dar es Salaam: Government Printer.

United Republic of Tanzania (2007). Volume IV: Public expenditure estimates development votes:

Ministerial and regional development programmes: For the year from 1st July, 2007 to 30th June, 2008. Dar es Salaam: Government Printer.

United Republic of Tanzania (2008a, Juni). Basic education statistics in Tanzania (BEST) 2004-

2008: National data. Ministry of Education and Vocational Training. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://educationstatistics. moe.go.tz/Files/2008/National%20Best%202008.zip

United Republic of Tanzania (2008b, Agosto). Education Sector Development Programme: Primary

Education Development Programme II (2007-2011): Annual performance report FY 2007/2008. Ministry of Education and Vocational Training & Prime Minister‘s Office – Regional Administration and Local Government. Dar es Salaam: Government Printer.

United Republic of Tanzania (2009a, Julai). Basic education statistics in Tanzania (BEST) 2005-

2009: National data. Ministry of Education and Vocational Training. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://educationstatistics. moe.go.tz/Files/2009/National%20Best%202009.zip

Page 63: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

56 Marejeo

United Republic of Tanzania (2009b, Desemba). Basic education statistics in Tanzania (BEST) 2009: Regional data. Ministry of Education and Vocational Training. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://educationstatistics. moe.go.tz/Files/2009/Regional%20Best%202009.zip

United Republic of Tanzania (2009c). The Law of the Child Act. Dar es Salaam. Ilipatikana Mei 1,

2010, kutoka http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/21-2009.pdf United Republic of Tanzania (2009d). Millennium development goals report: mid-way evaluation:

2000-2008. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http:// www.tz.undp.org/docs/MDGprogressreport.pdf

United Republic of Tanzania (2009e). Volume IV: Public expenditure estimates development votes:

Ministerial and regional development programmes: For the year from 1st July, 2009 to 30th June, 2010. Dar es Salaam: Government Printer.

United Republic of Tanzania (2010a, Machi). Annual general report of the Controller and Auditor

General: On the audit of the financial statements of central government for the year ended 30th June, 2009. National Audit Office of Tanzania. Dar es Salaam. Ilipatikana Agosto 1, 2010, kutoka http://www.nao.go.tz/files/CENTRAL%20GOVERNMENT% 20GENERAL%20REPORT%202008-2009.pdf

United Republic of Tanzania (2010b, Juni). Basic education statistics in Tanzania (BEST) 2006-

2010: Revised national data. Ministry of Education and Vocational Training. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://educationstatistics. moe.go.tz/Files/2010/National%20Best%202010.zip

United Republic of Tanzania (2010c, Oktoba). Basic education statistics in Tanzania (BEST) 2010:

Regional data. Ministry of Education and Vocational Training. Dar es Salaam: Government Printer. Ilipatikana Februari 21, 2011, kutoka http://educationstatistics.moe.go.tz/Files/ 2010/Regional%20Best%202010.zip

Uwugiaren, I. (2009, Novemba 22). Nigerians have legal right to education, ECOWAS Court rules.

Ilipatikana Mei 1, 2010, kutoka http://allafrica.com/stories/200911230024.html Vavrus, F. & Moshi, G. (2009). The cost of a ‗free‘ primary education in Tanzania. International

Critical Childhood Policy Studies Journal (2009), 2(1), 31-42. Ilipatikana Agosto 3, 2010, kutoka http://journals.sfu.ca/iccps/index.php/childhoods/article/viewFile/8/12

Yussuf, I (2010a, Januari 25). Campaign against corporal punishment picks up. Daily News. Dar es

Salaam: Daily News Media Group. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://www. dailynews.co.tz/home/?n=6982&cat=home

Yussuf, I (2010b, Juni 28). Reps want corporal punishment returned in schools. Daily News. Dar es

Salaam: Daily News Media Group. Ilipatikana Agosto 4, 2010, kutoka http://dailynews. co.tz/home/?n=11254

Page 64: Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya Mahakama nchini ...hakielimu.org/files/publications/Kudai Haki ya Kupata Elimu kwa Njia ya... · 1.4.3 Sheria ya Haki za Mtoto ... kupitishwa

Marejeo

57

HakiElimu inawezesha wananchi kuleta mabadaliko katika elimu na demokrasia.

SLP 79401 ● Dar es Salaam ● Tanzania Simu (255 22) 2151852/3 ● Faksi (255 22) 2152449

[email protected] ● www.hakielimu.org