400
Mwanzo wa kusoma Yaliyomo Maelekezo kwa mtumiaji Maelekezo kwa mtumiaji T N L M he ew ife ission J, U U KWELI M R ? E MEZALIWA PYA AJI NA KWA OHO KWA

Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

Mwanzo wa kusoma

Yaliyomo

Maelekezo kwa mtumiajiMaelekezo kwa mtumiaji

T N L Mhe ew ife ission

J ,U U

KWELI

M R ?

E

MEZALIWA PYA

AJI NA KWA OHO

KWA

Page 2: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

JE, UMEZALIWA UPYA

KWELI KWA

MAJI NA KWA ROHO?

JE, UMEZALIWA UPYA

KWELI KWA

MAJI NA KWA ROHO?

PAUL C. JONG

Hephzibah Publishing House A Division of THE NEW LIFE MISSION

SEOUL, KOREA

Page 3: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho? Hati nakili © 2006 na The New Life Mission Hairuhusiwi kuchapisha kuhifadhi kwa mfumo wa marejeo au kusambaza kwa njia za elektronikali au mekamikali, kunakili kwa kupiga picha na kwa sauti na njia nyinginezo pasipo ruhusa ya kimaandishi kwa mchapishaji na mmiliki wa hati: Vifungu vya maandiko katika kitabu hiki ni marejeo katika Biblia; Tafsiri ya ushirikiano wa Makanisa – Kenya (Nairobi) na Tanzania (Dodoma) ISBN 89-8314-473-4

SHUKRANI Tunapenda kutoa sala zetu za shukrani

kwa Bwana kwa kuweza kutupatia maneno ya wokovu na baraka katika Injili ya kuzaliwa upya tena katika maji na Roho.

Shukrani pia kwa Watumishi wa Mungu

akijumuishwa Mch. Samuel J. Kim na Mch. John K. Shin ambao walitoa huduma ya thamani katika uchapishaji wa kitabu hiki; kwa Bi. Jungpil Sul kwa tafsiri, kwa kaka na dada zetu katika Haphzibah Publishing House; na kwa Elaine Dawe wa chuo kikuu cha Kangwon na Ross Wallace wa THE KOREA TIMES. Kwa ujumla wote wamefanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kitabu hiki. Natoa shukrani tena kwenu wote.

Page 4: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

Tumaini langu na maombi yangu juu ya kitabu hiki na kanda zake za kaseti ziweze kusaidia nyoyo nyingi kuzaliwa upya, na napenda kutoa shukrani za dhati tena kwa wote waliofanya kazi nasi kwa bidii.

Kwa uaminifu natumai Bwana atatupa

kibali cha kueneza Injili ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho duniani kote kwa watakao mwamini Yesu.

Kwa imani ya milele, namshukuru Bwana.

PAUL C. JONG.

Page 5: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

5 UTANGULIZI

UTANGULIZI Inatulazimu kuzaliwa upya kwa Maji na Roho.

Mungu alipoumba mbingu na nchi hapo mwanzo, aliumba pia dunia ya nje, mbinguni na jehanamu. Alimuumba mwanadamu kwa mfano wake, lakini tangu mwanadamu huyo wa kwanza, Adamu, atende dhambi mbele za Mungu watu wote wanapaswa kufa. “Basi kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu” (Waebrania 9:27).

Kifo cha mwili wetu ni njia ya kupitia kuelekea uzima wa milele. Wale wote wasio na dhambi wataingia kwenye dunia ya umilele Mbinguni kwa furaha isiyo na

Page 6: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

6 UTANGULIZI

mwisho kwa kuwa wana wa Mungu ambapo wenye dhambi watatupwa kwenye “ziwa linalowaka moto wa kiberiti” (Ufunuo 20:10) na kuteswa mchana na usiku milele.

Hivyo, wanadamu wote wanapaswa kuzaliwa upya. Tunapaswa kuzaliwa upya kupitia imani zetu, kukombolewa kutoka dhambini mwetu na kufanywa wenye haki. Na ndivyo pekee tunaweza kuingia katika ufalme wa milele Mbinguni Biblia inasema, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). “Kuzaliwa upya kwa maji na Roho” ni njia pekee ya kuingia katika ufalme wa Mungu wa milele.

Nini basi maana ya “maji” na kwa “Roho” ambamo kunaruhusu kuzaliwa upya. “Maji” katika Biblia inamaanisha “ubatizo wa Yesu.”

Kwa nini Yesu aliye Mungu, alibatizwa na Yohana Mbatizaji? Je, ilikuwa ni kuonyesha

unyenyekevu wake? Je, ilikuwa ni kutangaza kwamba yeye ni Masiha? La, hasha! Haikuwa hivyo.

Wakati Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji kwa njia ya “kuwekewa mikono juu ya kichwa chake” (Walawi 16:21) ilikuwa ni “kitendo kiadilifu cha mtu mmoja” (Warumi 5:18) kinachotwalisha mbali dhambi za mwanadamu.

Katika Agano la Kale, Mungu aliwapa Waisraeli sheria ya wema ya ukombozi. Hivi ndivyo ilivyo kuwa ile siku ya Upatanisho ambapo dhambi zote za Israeli katika mwaka huo zingelipizwa kwa maungamo kupitia Kuhani Mkuu Haruni, kwa kuwekea mikono yake kwenye kichwa cha mnyama wa kafara.

Palikuwa na maneno ya ufunuo yaliyotabiriwa kuhusu sadaka ya ondoleo la dhambi milele. Ilionyesha ukweli kwamba

Page 7: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

7 UTANGULIZI

dhambi za wanadamu zingetwaliwa kwa mara moja na Yesu aliye kuja katika mwili wa mwanadamu kutokana na mapenzi ya Mungu Baba. Na alibatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye alikuwa ni wa uzawa wa Haruni na kuwa alikuwa mwakilishi wa wanadamu wote.

Wakati Yesu alipotaka kubatizwa alimwambia Yohana “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

Hapa neno “ndivyo itupasavyo” ina maana ya “kwa kuwekewa mikono” ni kwa nia ya kubebeshwa dhambi za ulimwengu kwa Yesu ili haki yote iweze kutimizwa kwetu sisi sote. Neno “haki” kwa Kigiriki “dikaiosune” lina maana ya “hali ya kustahiki” au “kuwa na stahili katika tabia au matendo katika kufanyizwa kuwa mwenye haki au kufaa.”

Yesu alihimiza haki zote kwa niaba ya watu wote kwa kupitia ubatizo katika namna ya haki na stahili zote. Hivyo kwa kuchukua dhambi za watu wote kupitia ubatizo wake, siku iliyofuata baada ya ubatizo huo, Yohana Mbatizaji alishuhudia kwa kusema “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29).

Kwa dhambi zote za wanadamu juu ya mabega yake, Yesu alitembea kuelekea msalabani. Kwa niaba alichukua hukumu ya dhambi alizo zibeba mwenyewe kupitia ubatizo wake. Alikufa msalabani hali akisema “Imekwisha” (Yohana 19:30). Kwake yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu sote na kupokea hukumu iliyo kamili kwa niaba yetu.

Page 8: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

8 UTANGULIZI

Maji, yakiwa na maana ya Ubatizo wa Yesu, ni Mfano wa mambo haya ya Wokovu.

Hivyo, pasipo “kuwa na imani juu ya

ubatizo wa Yesu” hatutookolewa. Na ndiyo maana Mtume Paulo alitamka kwamba “mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1 Petro 3:21).

Siku hizi watu wengi wenye kumwamini

Yesu hawauamini ubatizo wake wa “maji” bali huamini kifo chake tu, katika msalaba. Je, imani hii yaweza kweli kuokoa wenye dhambi? Je, itawezekana kweli kukombolewa kutoka kwenye dhambi zetu zote kwa kuamini Damu ya Yesu tu? Je, itaweza kutuletea wokovu wetu?

Hasha! Hatutaweza kupata ukombozi wa Mungu kwa imani juu ya kifo cha Yesu msalabani pekee.

Wakati wana wa Israeli walipotoa sadaka ya upatanisho katika nyakati za Agano la Kale, isingekuwa njia sahihi kumchinja mnyama wa sadaka pasipo kwanza kuwekewa mikono juu ya kichwa chake kwa kutwikwa dhambi juu yake kwa niaba yao. Hivyo inakuwa ni kosa na kuvunja sheria ya Mungu kuamini msalaba wa Yesu pekee bila kuamini pia ubatizo wake.

Hivyo, Mtume Paulo alisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo (1Petro 3:21).

Kama ilivyo kwa wale walio acha kuamini “maji” makuu (mafuriko) nyakati za Nuhu

Page 9: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

9 UTANGULIZI

waliangamizwa, ndivyo ilivyo kwa wale ambao hawata amini “maji” yaani “ubatizo wa Yesu” hakika wataangamia!

Imani iliyo kamili ituongozayo kuelekea wakovu ulio wa kweli ni ile iliyo juu ya “aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo” (1Yohana 5:6). Yatubidi kuamini yote mawili, ubatizo na msalaba wa Yesu Kristo.

Mtume Yohana alinena juu ya imani iliyo sahihi ni kuamini “ushuhuda wa Roho, maji na damu” (1Yohana 5:8).

Kinachojenga na kubainisha imani iliyo ya kweli ni kuamini kwamba, “Yesu ni Mungu Halisi na alikuja katika mwili wa mwanadamu kwa uweza wa Roho kwa njia ya Mwanamwali Mariam na kubeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa katika mto Yordan na Yohana Mbatizaji aliye kuhani mwakilishi wa wanadamu. Yesu alikwenda msalabani akiwa amezibeba dhambi zote za

ulimwengu, na kupata hukumu isiyostahili kwake kwa ajili yetu.” Hivyo basi, Injili haitoweza kukamilika pasipo “ubatizo wa Yesu” yaani “maji” Haijalishi ni kwa namna ipi iliyo sahihi una mwamini Yesu, pasipo kuamini jambo hili hautoweza kuingia katika wokovu wa milele.

Historia ya awali ya Kanisa katika kupotea kwa Injili iliyo ya kweli

Kwa nini katika nyakazi hizi “Injili iliyo ya

kweli ya maji na Roho” imekuwa adimu nafasi yake kuchukuliwa na Injili isiyo ya kweli ienezwayo duniani pote?

Baada ya Yesu kufufuka alipaa mbinguni, na Mitume walianza kuhubiri “Injili ya maji na damu.” Ikiwa tutasoma Agano Jipya kwa

Page 10: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

10 UTANGULIZI

makini, tutaweza kuona si pekee kwa waandishi wa Biblia akiwemo Mtume Paulo, Petro na Yohana bali hata Mitume wote na watenda kazi katika Kanisa la mwanzo walihubiri kwa uwazi juu ya “Injili ya maji na Roho”.

Kwa nyakati hizi shetani amekuwa akitumia namna ya ujanja kubadilisha kwa kuongeza Injili hii ili kuondoa nguvu ya Uhai wa Kanisa. Katika kipindi cha Mtaguso wa Milan 313AD; Kanisa la Kikristo lilikumbana na mtego uliowekwa na Shetani. Nguvu za kisiasa za Dola ya Kirumi ili kubadilika kwa kuukubali Ukristo kuwa ni dini ya Taifa, waliweza kujinyakulia umadhubuti wa kisiasa.

Kwa kusisitiza kwamba “ubatizo ni kwa yeyote anayejiunga na Kanisa.” Dola ya Kirumi iliweza kudhibiti umoja kwa makoloni yake yaliyo na utofauti.

Ilikuwa katika matokeo haya ya mazingira yaliyosababisha utamkwaji wa Kanuni ya Imani ya Mitume iliyokuwa mbadala wa msingi wa mafunzo ya dini, kwa sababu hiyo “Injili yenye msisitizo wa kibiblia.” Kwa maneno mengine “Injili ya maji na kwa Roho” yenye “nguvu na katika Roho Mtakatifu na uthibitifu mwingi” (1Wathesalonike 1:5) – ilikuja kubadilishwa na kuwa Injili isiyo ya kweli, ikiruhusu kutozaliwa upya kwa yeyote, na hivyo kufanikiwa kuenea ulimwenguni pote.

Kwa zaidi ya miaka elfu moja baada ya Tamko la Milan, Kipindi cha giza katika Ukristo kilitanda mahala pote katika ulimengu wa Bara la Ulaya. Ingawa matokeo ya mfululizo wa harakati za mageuzi mapya yalikuwepo pia katika nchi nyingi, yakiwaasa watu kurudi katika “Neno, Neema na Imani”,

Page 11: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

11 UTANGULIZI

bado hapakuwepo yeyote aliye pata injili ya kweli, “injili ya maji, Roho na damu”.

Injili hii ilikwisha wekwa bayana katika mikono ya wale walio wachache wenye kufuata maneno ya tangu nyakati za Mitume. Kama kijito kilichopotea juu ya ardhi kinapo tokeza tena katika tambarare, injili hii imetapakaa tena katika Nyakati za Mwisho ili kuhubiriwa pande zote za ulimwengu

Hiki ni Kitabu cha kwanza kabisa katika nyakati hizi kuhubiri Injili ya Ubatizo wa Yesu kama ilivyo andikwa katika Biblia.

Hiki ni kitabu cha kwanza katika nyakati hizi kuhubiri Injili ya ubatizo na damu ya

Yesu kama ilivyoandikwa katika maandiko Matakatifu kwa ufasaha Injili inatueleza kwamba Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake na kubeba hukumu yake Msalabani. Na hakika kwamba hapana kitabu kingine chenye kuhubiri “Injili ya maji na kwa roho” kwa ufasaha na kwa uaminifu kama ilivyo kwa kitabu hiki.

Katika ulimwengu wa sasa, mawasiliano kwa kompyuta ni ya umuhimu mkubwa kama chombo cha kutafiti na ugunduzi wa ujuzi, nimejaribu kutafuta kwa baadhi ya watendakazi wengine wenye ueleo juu ya siri ya ubatizo wa Yesu, wenye kuhubiri Injili iliyo ya kweli kama ilivyo andikwa kwenye Biblia na wenye kufahamu na kuhubiri siri ya ubatizo wa Yesu kwa imani. Hadi leo hii sijapata! Kwa maana hiyo, nimeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya

Page 12: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

12 UTANGULIZI

Kiingereza na kutafsiriwa kwa lugha nyinginezo.

Wakati mafuriko ya maji yanapo ifunika dunia yote, maji humiminika pote, lakini maji haya si salama kwa kunywewa. Na ndivyo ilivyo kwa njia kama hii. Wapo wanaoitwa “watumishi wa Mungu” wenye kuhubiri Injili isiyo ya kweli na wasio weza kutupatia uzima halisi.

Yule Mwanamke Msamaria aliye kunywa maji kutoka katika kisima cha Yakobo kila siku hakuweza kumaliza kiu ya kiroho lakini alipokunywa maji ya uzima kutoka kwa Yesu alisikia wokovu na hivyo, kuikata kiu yake kwa mara moja na kwa wakati wote.

Maji ya uzima katika Yesu yanabubujika katika kila sehemu ya faragha na ya uwazi wa chamichemi ya kitabu hiki. Kwa yeyote anywaye kutoka humo ataokolewa na dhambi milele. Hatofungwa na dhambi tena,

bali maji ya uzima yatamiminika kutoka ndani mwake na kumaliza kiu ya mioyo imzungukayo mahala popote.

Natuwe watendakazi wa Mungu kwa kutengeneza upya mahusiano yaliyovunjika.

Tunaishi katika kipindi cha karibu na

mwisho wa ulimwengu. Huu ni wakati ambamo dhambi za wanadamu zimefikia kipimo cha juu sana na hukumu ya haki ya Mungu imo mbioni. Baadhi ya wataalamu wa Sayansi wamefanikiwa kumzalisha kondoo kulingana na matakwa ya maumbile wanayoyahitaji kinyume na utaratibu wa asili. Kondoo huyo aliyezaliwa wamemwita “Dolly” na hivyo kupelekea kukubalika ifanyike hata kwa wanadamu.

Page 13: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

13 UTANGULIZI

Leo, tunajenga mnara mwingine wa Babeli. Mara ya mwisho mwanadamu alipojaribu kufanya mambo kama haya, Mungu aliwatawanya pande zote za dunia kwa kuzichanganya ndimi zao kwa lugha tofauti na mbalimbali. Sasa tena hiki ni kipindi cha Tabu Kuu, laana ya haki kwa Mungu itaachiwa punde, kwa kila roho isiyo zaliwa upya.

Hivyo, nakushauri ufuatilie kitabu hiki kwa makini. Nakuomba ili “uzaliwe upya katika maji na katika Roho.” Kitabu hiki kinahubiri Injili kama ilivyo sambamba na Biblia.

Hivyo kama ilivyonenwa: Nina uhakika kwa yeyote atakaye fuatilia

hiki kitabu hatoshindwa sambamba na kuzaliwa upya. Bwana wetu Yesu anasema “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli

itawaweka huru” (Yohana 8:31-32). Matumaini yangu nawe upate kujua kweli kupitia kitabu hiki ili uwe huru katika dhambi na kifo. Na ukombolewe na kupata uzima wa milele katika yeye.

Na tufanye kazi ya Baba pamoja katika kuhudumia roho zilizopotea kwa kuhubiri “Injili ya maji na damu” kwa uaminifu. Natumaini kwamba Injili iliyo ya kweli itang’ara mahali popote duniani tena. Na hakika Injili ya kweli itakarabati matawi ya Imani ya Ukristo wa nyakati hizi kwa maneno ya kweli.

“Na watu wako watapajenga mahali palipo kuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwaa, Mwenyewe kutengeneza mahali palipo bomoka; na Mwenye kurejeza njia za kukalia” (Isaya 58:12).

Page 14: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

14 UTANGULIZI

Wengi wenu mnauhakika wa kutoelewa Injili ya kuzaliwa upya katika maji na Roho. Hivyo nimejaribu kuweka msisitizo mkubwa kwenye Injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba katika kila mahubiri.

Kama kusinge kuwepo na ubatizo wa Yesu, kifo chake msalabani kingekuwa ni bure kisicho na thamani kwetu sote wenye kuamini. Zipo sababu kwa nini nimesisitiza zaidi ubatizo mara kwa mara.

Nia yangu ni kuweka kwako bayana. Hadi hapo wote mtakapo barikiwa kwa Injili ya maji (ubatizo wa Yesu) na kwa Roho. Ningependa kurudia tena kwa ajili yako.

Ni matamanio na matarajio yangu kwa wote muamini katika Injili ya maji ya ubatizo wake na damu ili kuokolewa kutoka dhambini. Na hakika kitabu hiki kitakuongoza katika kuzaliwa upya kwa maji na Roho.

Page 15: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ Ukurasa wa jalada ►

YALIYOMO UTANGULIZI -------------------------------------- 5

Sehemu ya Kwanza – Mahubiri, 1. Yatupasa kwanza kutambua dhambi

zetu ili tuweze kukombolewa (Marko 7:8-9, 20-23) -------------------------- 16

2. Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye

dhambi (Marko 7:20-23) ---------------------- 34 3. Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

(Luka 10:25-30) -------------------------------- 47 4. Ukombozi wa Milele (Yohana 8:1-12) ------ 70 5. Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa

Dhambi (Mathayo 3:13-17) ----------------- 105

6. Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na

kwa Roho (1Yohana 5:1-12) --------------- 161 7. Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa

wenye dhambi (1Petro 3:20-22) ------------ 201 8. Injili ya Upatasho ulio kamilifu

(Yohana 13:1-17)----------------------------- 221 Sehemu ya Pili – Mwisho 1. Shuhuda za Wokovu ------------------------- 297 2. Maelezo ya Ziada ----------------------------- 317 3. Maswali na Majibu --------------------------- 353

Page 16: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 1

Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu

ili tuweze kukombolewa

Page 17: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

17 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili

tuweze kukombolewa (Marko 7:8-9)

“Ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.”

(Marko 7:20-23) “Akasema, kimtokacho mtu ndicho

kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi,

kijicho, matukano, kiburi, upumbavu; Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”

Kwanza ningependa kufafanua nini maana ya dhambi. Kuna dhambi zilizoelezwa na Mungu na nyingine kuelezewa na mwanadamu. Neno dhambi kwa Kigiriki ‘hamartia’ maana yake ni ‘kukosea katika kulenga shabaha”. Kwa maneno mengine, ni kufanya jambo pasipo usahihi. Ni dhambi kutotii maelekezo ya Mungu. Hebu na tuangalie kwa awali maana ya dhambi kwa mtizamo wa mwanadamu.

Nini maana ya dhambi

Ni kutotii maelekezo ya Mungu.

Page 18: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

18 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Twagundua dhambi zetu kupita dhamira zetu. Ingawa kiwango cha ubinadamu hutofautiana kulingana na jamii anayotoka, hali ya kimawazo, katika mazingira na dhamira.

Hivyo, maana ya dhambi inatofautiana kati ya jamii na jamii. Kitendo cha aina moja chaweza au kisiweze kuchukuliwa kama dhambi endapo kila jamii itakuwa na aina yake ya vipimo. Ndiyo maana Mungu ametupa vipengele vya sheria 613 ili vitumike kama vipimo halisi vya dhambi.

Mchoro ufuatao unatuelekeza dhambi za mwanadamu.

Sheria ya Mungu

Dhamira ya Mwanadamu,

Uongofu na kanuni za kijamii

Sheria ya kitaifa, Sheria ya kiraia

Hatupaswi kamwe kuweka viwango vya

dhambi kwa kutumia dhamira iliyowekwa kwa kanuni zetu za kijamii.

Dhambi za dhamira siyo zitokanazo na jinsi ile Mungu anavyoelezea nini maana ya dhambi. Hivyo tusizisikilize dhamira zetu, bali tulinganishe viwango vya dhambi zetu na amri za Mungu.

Kila mmoja ana wazo lake juu ya nini maana ya dhambi. Wengine huchukulia ni udhaifu hali wengine hudhani kwamba ni

Page 19: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

19 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

kutokana na kilema cha tabia. Mathalani, katika nchi ya Korea, watu

hujengea makaburi ya wazazi wao kwa kupanda nyasi na kuyatunza hadi wenyewe wanapofariki. Lakini kwa kabila Fulani duni katika nchi ya Papua New Guinea, wanawatukuza wazazi wao waliofariki kwa kufanya sherehe ya kuila miili yao wakiwa na ndugu wa familia (sina uhakika sana endapo huipika kwanza kabla ya kula). Naimani hupenda kuizuia miili hiyo isiliwe na funza. Utamaduni huu ni kielelezo cha mtazamo wa kibinadamu kuhusiana na dhambi ulivyo na utofauti.

Matendo ya kistarabu katika jamii moja yanaweza kuchukuliwa kwa jamii nyingine kuwa yasiyo ya kistaarabu na kinyama. Ingawa Biblia inatueleza kwamba dhambi ni kutotii maelekezo ya Mungu. “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika

mapokeo yenu” (Marko 7:8-9). Muonekano wetu wa nje ni muhimu mbele za Mungu kwa kuwa yeye huangalia kina cha mioyo yetu.

Kanuni za mtu ni dhambi mbele za Mungu.

Dhambi ipi iliyo hatari zaidi?

Ni kupuuzia Neno la Mungu.

Kushindwa kuishi katika mapenzi ya Mungu ni dhambi. Ni sawa na kutoamini neno lake. Mungu alisema, ni dhambi kuishi kama Wafarisayo ambao walikataa sheria ya Mungu kwa kukazia zaidi msisitizo wa mafundisho ya desturi zao. Yesu

Page 20: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

20 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

aliwachukulia kuwa ni wanafiki. “Ni Mungu yupi unayemwamini? Je,

unaniheshimu na kunitukuza? Unajivunia juu yangu, lakini je unaniheshimu? Mara nyingi watu huangalia umbo la nje na kupuuzia neno la Mungu ndani ya nafsi zao. Je wajua hilo?

Matendo ya kuvunja sheria chanzo chake yametokana na udhaifu ambao ni maovu. Makosa tuyafanyayo na upotovu tuutendao kutokana na kutokuwa wakamilifu siyo dhambi kuu ndani yetu bali ni kuanguka katika usahihi. Mungu ametofautisha kati ya dhambi na uovu. Wale wote wenye kulidharau neno lake ni wenye dhambi, hata ikiwa hawana makosa. Ni wenye dhambi zaidi mbele ya Mungu. Na hii ndiyo maana Yesu aliwakemea Mafarisayo.

Katika nyakati za Agano la Kale, kitabu cha mwanzo hadi kumbukumbu la Torati

ziliwekwa sheria zilizotaja nini cha kutenda na nini cha kutotenda. Ni maneno ya Mungu Sheria yake. Haitowezekana kwetu kuzitekeleza katika asilimia mia moja, lakini yatubidi kuzikubali kama ni sheria za Mungu. Alitupatia hapo mwanzo na yatupasa kuzikubali kuwa ni Maneno ya Mungu.

“Hapo mwanzo palikuwepo na Neno, naye Neno alikuwepo kwa Mungu, naye Neno alikuwa ni Mungu” Naye alisema “Na uwepo mwanga na ukawepo” Aliumba vyote. Na baadaye, akaiweka Sheria.

Na baadaye “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu;” (Yohana 1:1, 14). Ni kwa namna gani basi Mungu alijidhihirisha kwetu? Alijidhihirisha kwetu kupitia sheria kwa maana Mungu ni Neno na Roho. Sasa je, Biblia inaitwa nini? Tunaita Neno la Mungu.

Imesemwa hapa “Ninyi mwaiacha amri ya

Page 21: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

21 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu” vipo vipengele 613 katika sheria ya Mungu. Fanya hivi na usifanye vile waheshimu wazazi wako… nakadhalika. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi imetajwa ni kwa namna gani mwanamume na mwanamke wanapaswa kuenenda na nini kifanyike endapo mifugo ikitumbukia shimoni… Hivi ni baadhi ya vipengele 613 katika sheria.

Kwa kuwa haya si maneno ya mwanadamu, tunapaswa kuyatafakari nyakazi zote. Ingawa tutashindwa kutekeleza sheria yote, tunapaswa kwa kiasi Fulani kuzitambua na kumtii Mungu.

Je, kuna kifungu hata kimoja cha maneno ya Mungu yasiyo sahihi? Mafarisayo waliziacha sheria za Mungu na kuzifuata taratibu za mafundisho ya wanadamu dhidi ya sheria ya Mungu. Maneno ya wakuu wao

yalichukua nafasi ya uzito wa juu dhidi ya yale ya Mungu. Yesu alipokuwa duniani, haya ndiyo aliyoshuhudia, na ndicho kilicho umiza moyo wake zaidi kwa kuona Neno la Mungu likipuuziwa na wanadamu.

Mungu ametupa vipengele 613 vya sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kutuonyesha kuwa yeye ni mkweli na mtakatifu kwetu. Kwa kuwa sisi sote ni wenye dhambi mbele yake, tunapaswa basi kuenenda kwa imani na kumwamini Yesu kuwa ndiye aliyeletwa na Mungu kwa upendo kwetu.

Wenye kuweka neno lake kando na kutoamini watakuwa ni wadhambi. Wenye kushindwa kuenenda katika neno lake pia ni wadhambi, ingawa kuweka kando neno lake ni hatari zaidi. Wenye kutenda dhambi hii wataishia motoni. Kutoamini Neno lake ni dhambi iliyo hatari zaidi mbele za Mungu.

Page 22: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

22 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Sababu ya Mungu kutupatia Sheria.

Kwa sababu zipi Mungu alitupa sheria?

Ni kutufanya tuzitambue dhambi zetu na

Hukumu juu yake. Sababu ipi Mungu alitupatia Sheria?

Ilikuwa ni kutufanya kuzitambua dhambi zetu na kumrudia kwake kwa toba. Alitupatia vipengele 613 vya sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kuweza kukombolewa kupitia Yesu Kristo. Na hii ndiyo maana ya Mungu kutupatia sheria.

Warumi 3:20 inasema “… kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya Sheria.” Hivyo twajua kwamba sababu ya Mungu

kutupatia sheria ilikuwa si kutulazimisha kuenenda nayo.

Kwa namna hii sasa, tunapata kujua nini juu ya Sheria? Ni hivi, sisi tu wadhaifu kwa kuitimiza sheria yote na ni wenye dhambi sana. Tunatambua nini juu ya vipengele hivyo 613 vya Sheria? Tunang’amua mapungufu yetu na kushindwa kwetu kuifuata Sheria yake. Tunatambua yakwamba sisi ni viumbe wa Mungu, tulio dhaifu, na wenye dhambi mbele zake. Ilitupasa sisi sote kutupwa motoni kwamujibu wa Sheria ya Mungu.

Tunapo tambua dhambi zetu na kushindwa kwetu kuishi kwa kuzifuata sheria, sasa, na tufanye nini? Je tunajaribu kuishi kwa ukamilifu wenyewe? Hasha! Yatulazimu kukubali kuwa sisi ni wadhambi, tumwamini Yesu ili tukombolewe kupitia wokovu wake katika Maji na Roho na

Page 23: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

23 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

kumshukuru yeye. Sababu ya Mungu kutupa sheria ilikuwa ni

kutufanya tuzitambue dhambi zetu na kujua adhabu yake juu ya dhambi hizo. Hivyo, itatufanya kuelewa kuwa hakuna njia ya kuokolewa toka motoni pasipo Yesu ikiwa tutamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi, tutakombolewa. Mungu alitupa sheria ili ituongoze kuelekea kwa Mwokozi Yesu.

Mungu alizifanya sheria ili kutufanya tuweze kutambua ni kwa namna gani tulivyo wenye dhambi na kuhitaji wokovu wa roho zetu kutoka kwenye dhambi hizo. Alitupa sheria na kumtuma mwana wake wa pekee, Yesu, kutuokoa kwa kuzibeba katika ubatizo wake. Kumwamini Yeye kutatufanya tuokolewe.

Sisi ni wadhambi tusio na tumaini lolote, yatulazimu kumwamini Yesu ili kuwa huru kutoka dhambini, kuwa watoto wa Mungu na

kuurudisha utukufu wake. Yatupasa tuelewe, kufikiri na kuamua

kupitia neno lake kwa kuwa yeye ni asili ya yote. Yatupasa tuikubali kweli ya wokovu kupitia Neno lake. Hii ni Imani ya Haki na kweli.

Nini kilichomo ndani ya Moyo Wa Mwanadamu

Natufanye Nini Mbele za Mungu?

Tunapaswa tuzikubali dhambi zetu na kumwomba Mungu

atuokoe. Ni lazima imani ianze kwa neno la Mungu,

Page 24: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

24 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

kwa kuliamini. Ikiwa sivyo, basi tutaanguka katika makosa. Itakuwa katika makosa na imani isiyo ya kweli.

Wakati Mafarisayo na Wanasheria walipomwona Yesu akila na wanafunzi wake mikate huku mikono ikiwa michafu, wasingeweza kusahihisha hilo ikiwa wangeliweka katika mtazamo wa neno la Mungu. Neno latuambia chochote kinachoingia ndani mwa mtu tokea nje, hakimtii najisi kwa kuwa huenda moja kwa moja kupitia tumboni na kutoka nje, na hakiuharibu moyo.

Kama isemavyo Marko 7:20-23 “Akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo

yamtia mtu unajisi.” Yesu alisema watu ni wadhaifu kwa kuwa wamezaliwa na dhambi ndani mwao.

Je, waelewa maana yake? Tumezaliwa wadhambi kwa kuwa sisi ni uzao wa Adamu lakini hatuwezi kuiona kweli kwa sababu hatujakubali na kuamini maneno ya Mungu. Hivyo, nini kilichomo ndani ya moyo wa mwanadamu?

Ujumbe uliopo hapo juu unasema “ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.” Aina zote za uovu hutoka ndani ya mioyo ya wanadamu na kuwatia unajisi.

Imeandikwa katika Zaburi “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha, mtu ni kitu gani hata umkumbuke. Na mwanadamu hata

Page 25: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

25 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

umwangalie” (Zab. 8:3-4). Kwa nini Mungu mwenyewe

ametutembelea? Anatutembelea kwa sababu anatupenda, alituumba na kutuonea huruma kwa kuwa tu wadhambi. Alizifuta dhambi zetu zote na kutufanya watu wake “Bwana, Bwana wetu Ni kwa namna gani jina lako ni lakuheshimiwa duniani pote, na Mbinguni!” Mfalme Daudi aliimba Zaburi hii katika kitabu cha Agano la Kale alipotambua kwamba Mungu atakuja kuwa Mwokozi wa wenye dhambi.

Katika Agano Jipya, Mtume Paulo alirudia maneno hayo. Ni jambo la kushangaza sana, viumbe wa Mungu kuweza kuwa watoto wa Mungu. Hili hufanyika kupitia huruma yake tu. Huu ni upendo wa Mungu.

Tunapaswa tuelewe kuwa, tunapo jaribu kuishi kwa sheria ya Mungu ni ujasiri ulio wa hatari kwake. Na pia ni ujeuri utokanao na

upumbavu. Si vyema kuishi nje ya upendo wake huku tukijitahidi kufuata sheria wenyewe na kusali pasipo na matumaini katika maisha yetu. Ni mapenzi ya Mungu tujitambue kwamba tu wadhambi katika sheria na kuamini ukombozi kupitia maji na damu ya Yesu.

Neno lake limeandikwa katika Marko 7:20-23 “Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani ya moyo nayo yamtia mtu unajisi.”

Yesu alisema kile kitokacho ndani ya mwanadamu, dhambi ya ndani, humtia najisi. Kamwe chakula kisicho safi toka kwa Mungu hakiwezi kututia najisi. Viumbe wote ni safi, isipokuwa kile kitokacho ndani ya

Page 26: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

26 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

mwanadamu nayo ni dhambi humtia najisi. Sote ni wazawa wa Adamu. Hivyo, tumezaliwa na nini? Tumezaliwa na dhambi kumi na mbili ndani yetu. Je hii si kweli?

Je, twaweza kuishi bila kutenda dhambi? Tutaendelea kutenda dhambi kwa kuwa tumezaliwa wenye dhambi. Twaweza kuacha kutenda dhambi kwa kuwa twaielewa sheria? Twaweza kuishi kwa kuifuata sheria? Hasha!

Kwa kiasi tunapo jaribu kuishi kwa kufuata sheria ndivyo itakavyo kuwa ngumu kuifuata. Tunapaswa kutambua mwisho wetu na kuachilia matendo yetu ya awali na kwa unyenyekevu wa ufahamu wetu, twaweza kukubali ubatizo na damu ya Yesu, ambao hutuokoa.

Vipengele vyote 613 vya sheria ni vyenye haki na vyema. Lakini watu ni wadhambi toka tumboni mwa mama zao. Tunapo

tambua ya kwamba Sheria ya Mungu ni njema lakini sisi wanadamu tumezaliwa wenye dhambi hatutoweza kuwa wenye haki kwa juhudi zetu binafsi, tutagundua kuwa tunahitaji rehema ya huruma ya Mungu na ukombozi wa Yesu katika Injili ya maji, damu na Roho. Tunapogundua vikomo vyetu – kwamba hatutoweza kupata haki kwa uwezo wetu na tutakwenda motoni kwa dhambi zetu – basi yatupasa kutegemea ukombozi wa Yesu.

Tunaweza kuponywa. Tunapaswa kuelewa kwamba, tumeshindwa kuwa wenye haki na wema mbele za Mungu kwa juhudi zetu wenyewe. Sasa basi tunapaswa kukubali mbele za Mungu kwamba sisi ni wenye dhambi ambao mwisho wetu ni jehanamu, na tuweze kuomba huruma yake, “Mungu uniokoe kutoka dhambini na unihurumie.” Ndipo Mungu hakika atakutana

Page 27: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

27 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

nawe kwa Neno lake. Katika njia hii tutaweza kuponywa.

Natuone basi sala ile ya Daudi. “Nimekutenda dhambi wewe peke yako, Na kufanya uovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo na kuwa safi utoapo hukumu” (Zaburi 51:4).

Daudi alitambua yeye ni mwenye wingi wa dhambi na muovu wa kutupwa motoni, lakini alikubali mbele za Mungu, “Bwana ukiniita kuwa mwenye dhambi hakika ni mwenye dhambi mimi. Ukiniita mwenye haki, hakika ni mwenye haki mimi. Ukiniokoa, nitaokoka na ukinitupa motoni, nitaishia motoni.”

Hii ni imani sahihi na njia ya kuokolewa. Hivi ndivyo tunavyopaswa tuwe, ikiwa tunatumaini la wokovu katika Yesu.

Tunapaswa tuelewe ni zipi dhambi zetu halisi.

Kwa kuwa sisi tu uzao wa Adamu, basi

sote tuna tamaa mbaya ndani ya mioyo yetu Hivyo, Mungu anasemaje katika hili? Anatueleza tusitende uzinzi ingawa mioyoni mwetu tuna dhambi ya uzinzi. Tuna uuaji ndani ya mioyo yetu, lakini Mungu anasemaje? Anatueleza tusiwe tunadharau wazazi wetu mioyoni mwetu lakini anatueleza tuwaheshimu. Tunapaswa kutambua kwamba neno lake ni kweli na jema, lakini ndani yetu mioyoni kuna dhambi.

Je hii si sawa? Hakika ni kweli. Hivyo yatupasa tufanye nini mbele za Mungu? Tunapaswa kukubali kwamba sisi ni wenye wingi wa dhambi tusio na matumaini.

Page 28: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

28 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Hatupaswi kudhani kuwa sisi ni wenye haki jana kwa kuwa hatukutenda dhambi siku hiyo ya jana. Tumezaliwa wenye dhambi chochote tufanyacho tutaendelea kuwa wenye dhambi. Na hii ndiyo maana tunahitaji ukombozi kupitia imani katika ubatizo wa Yesu.

Sisi si wenye dhambi kutokana na matendo yetu kama vile uzinifu, uuaji, wizi… bali tu wenye dhambi kwa kuwa tumezaliwa wenye dhambi ndani yetu. Tumezaliwa ndani yetu tukiwa na aina kumi na mbili za dhambi, hivyo kwa kuwa tu wadhambi mbele ya macho ya Mungu, kamwe hatutoweza kuwa wema kwa uwezo wetu binafsi. Twaweza kujifanya kuwa wema kwa muda tu.

Ikiwa tumezaliwa wenye nia zenye dhambi katika nafsi zetu, ni kwa namna gani basi twaweza kuwa wenye dhambi ikiwa

hatutotenda dhambi? Hatuwezi kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa kutegemea nafsi zetu. Ikiwa tutajifanyia haki yetu tutakuwa wanafiki. Yesu aliwaita mafarisayo na wanasheria kuwa “ni wanafiki.” Wanadamu wamezaliwa wakiwa wadhambi na hutenda dhambi katika kipindi chote cha maisha yao hapa duniani.

Anayedai kwamba hana dhambi ambaye hajapigana au kumpiga yeyote au kuiba hata sindano kwa yeyote kwa maisha yake yote anadanganya, kwa kuwa wanadamu wamezaliwa na dhambi ndani yao. Mtu huyo ni mwongo, mdhambi na mnafiki. Hivi ndivyo Mungu amuonavyo.

Kila mmoja ni mdhambi toka tumboni mwa mamae. Ingawa hata tusipotenda dhambi hata moja, bado tumepangiwa kwenda motoni. Haitajalisha ni kwa kiwango gani umefuata sheria na amri za Mungu,

Page 29: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

29 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

bado wewe ni mwenye dhambi ndani yako na hukumu ile ya motoni ina kusubiri.

Sasa, natufanye nini juu ya huu mwisho wa hukumu ya motoni? Tunapaswa kuomba huruma ya Mungu na kumtegemea yeye kwa wokovu wa dhambi hizo. Tusipokubali kuokolewa naye, basi ni wazi tutakwenda motoni huu ni mwisho wetu.

Ni kwa wale tu watakao likubali neno la Mungu kwamba wao ni wenye dhambi. Na wajue na kuelewa kuwa watafanywa kuwa wenye haki kwa imani tu. Hivyo fahamu kwamba, kudharau na kuweka kando neno la Mungu bila ya kulitambua ni dhambi iliyo hatari zaidi. Watakao likubali neno lake ni wenye haki, ingawa hapo nyuma walikuwa ni wenye dhambi. Wamezaliwa upya kwa Neno lake na kwa neema, na ndio pekee waliobarikiwa.

Wenye kujaribu kukombolewa kwa kupitia Matendo yao bado ni wenye dhambi.

Ni yupi mwenye dhambi hata baada ya kumwamini Yesu?

Ni yule mwenye kujaribu kukombolewa

kupitia matendo yake. Hebu na tusome Wagalatia 3:10 na 11

“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana: maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu

Page 30: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

30 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Mwenye haki ataishi kwa Imani.” Imesemwa “Amelaaniwa kila mtu

asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati ayafanye “Wale wenye kufikiri kuwa wana mwamini Yesu, hali wakitaka haki kupitia matendo yao, wamelaaniwa. Wapo wapi wenye kujaribu kuwa wenye haki? Wapo chini ya laana ya Mungu.

Kwa nini Mungu ametupa Sheria? Ametupa sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu (Warumi 3:20). Na pia alitaka tujue kwamba sisi ni wenye dhambi na mwisho wetu ni jehanamu.

Amini ubatizo wa Yesu, Mwana wa Mungu na uzaliwe upya kwa maji na kwa Roho. Ndipo utakapo okolewa dhambini, kuwa mwenye haki, kupata uzima wa milele na kwenda mbinguni. Uwe na Imani moyoni mwako.

Dhambi kuu ya Majivuno Duniani.

Ni ipi iliyo dhambi kuu ya Majivuno Duniani?

Ni kujaribu kuishi

Kwa matendo ya Sheria Tumebarikiwa kwa kuwa na Imani ya

baraka zake. Mungu huwaokoa wale wote wenye Imani kwa Neno lake.

Leo hii kati ya wale wenye kuamini, wamo Wakristo wenye kujaribu kuenenda katika matendo ya sheria. Imewapasa kuishi kwa matendo ya sheria, lakini je, yawezekana?

Tunapaswa tuelewe kwamba ni kwa namna gani itakuwa ni upumbavu kujaribu kuishi kwa matendo ya sheria.

Page 31: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

31 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Tutakapojaribu sana na ndivyo itakapo kuwa ngumu zaidi. “Imani huja kwa kusikia, na kusikia ni neno la Mungu” Yatupasa tutupilie mbali majivuno yetu ili tuweze okolewa.

Yatupasa tuache vipimo tujiwekeavyo ili tuweze kuokolewa.

Tunapaswa tufanye nini basi, ili tupate okolewa?

Yatupasa tuache kujiwekea vipimo vyetu.

Kwa namna gani mtu ataokolewa? Itawezekana pale tu mtu huyo atakapo tambua yeye binafsi kwamba ni mwenye dhambi. Wapo wengi ambao

awajakombolewa kwa sababu awataki kuacha Imani potofu na juhudi zao binafsi.

Mungu anasema kwa wale wenye kuzishika sheria wamelaaniwa. Wale wenye kuamini kuwa wataweza kuwa wenye haki kutoka hatua hadi hatua kwa kujaribu kuishi kwa matendo ya sheria baada ya kumwamini Yesu, wamelaaniwa wanamwamini Mungu lakini bado wanafikiri kwamba wanapaswa kuishi katika sheria ili kuendelea katika wokovu.

Ndugu zangu, twaweza vipi kuwa wenye haki kupitia matendo yetu? Tunakuwa wenye haki pale tu tunapo amini Neno la Yesu; na ndilo pekee lenye kuokoa. Imani katika ubatizo wa Yesu, damu yake, na Mungu Mkuu ndivyo pekee viokoavyo.

Na ndiyo maana Mungu alileta kanuni ya Imani kwetu ili iwe njia ya kuwa wenye haki mbele zake. Ukombozi katika maji na katika

Page 32: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

32 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

Roho hauhitaji matendo ya sheria ya mtu, bali ni Imani juu ya Neno la Mungu. Mungu ametukomboa kwa imani na huu ndiyo mpango ulio kamilika katika wokovu kwetu.

Kwa nini wale walio mwamini Yesu hawakukombolewa? Kwa sababu hawakukubali neno la wokovu kupitia maji na katika Roho lakini sisi wale tusiokamili ndani yetu kama walivyo wao, tumekombolewa kupitia Imani katika Neno la Mungu.

Ikiwa watu wawili watafanya kazi katika jiwe la kusagia nafaka, atakaye achwa upande mmoja akifanya kazi ataendelea hali yule mwingine atanyakuliwa. Aliyeachwa akiendelea anafananishwa na yule asiyekombolewa. Kwa nini basi mmoja anyakuliwe na mwingine kuachwa?

Sababu ni kwamba yule mmoja alisikiliza na kuamini Neno la Mungu, hali mwingine

alifanya kwa bidii kutenda matendo ya sheria na kutupwa jehanamu. Mtu huyu alikuwa akitambaa kuelekea mbele za Mungu lakini alitupwa pembeni kama mdudu mchafu amtambaaye mtu. Ikiwa mtu anajaribu kutambaa ili kumfikia Mungu kwa matendo ya sheria hakika atatupwa motoni.

Na ndiyo maana tunapaswa kukombolewa kwa Imani katika maji na katika Roho.

“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa. Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria, kwa sababu mwenye haki ataishi kwa Imani” (Wagalatia 3:10-11, Warumi 1:17).

Usipoamini Neno la Mungu ni dhambi mbele zake. Na kwa kuongezea, vilevile ni

Page 33: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

33 Yatupasa kwanza kutambua dhambi zetu ili tuweze kukombolewa

dhambi kulipuuzia kwa kujiwekea vipimo binafsi. Mwanadamu hawezi kuishi kwa kuifuata sheria ya Mungu kwa kuwa amezaliwa na asili ya dhambi ndani yake na ataendelea kutenda dhambi maishani mwake. Tunatenda dhambi hapa leo na kesho pale kidogo hadi kufikia mahala pote tunapokwenda. Yatupasa kuelewa kwamba sisi tu ndani ya mwili usioweza kuacha kutenda dhambi.

Mwanadamu amefananishwa na ndoo iliyofurika mbolea ambayo ikibebwa huvuja na kumwagika kila pahala ipitishwapo. Ndivyo tulivyo. Tunamwagika dhambi kila pahala tupitapo. Je, waona hiyo?

Je, unaweza kuendelea kusema kuwa wewe ni mtakatifu? Ikiwa utajigundua hivyo binafsi, hutojaribu tena pasipo na matumaini kujitafutia utakatifu ila kwa kuamini kwa maji na kwa damu ya Yesu.

Wale ambao hawajazaliwa upya yawapasa kutupilia mbali mioyo yao migumu na kukubali kwamba wao ni wadhambi mbele za Mungu. Na ndipo wanapopaswa kulirudia Neno la Mungu na kugundua kwamba aliwaokoa kwa maji na kwa Roho.

Page 34: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 2

Wanadamu Wamezaliwa wakiwa

Wenye dhambi

Page 35: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

35 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

(Marko 7:20-23) “Akasema kimtokacho mtu ndicho

kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”

Watu wamechanganyikiwa na kuishi kwa hisia potofu.

Ni yupi hasa anayeweza Kuokolewa?

Ni yule mwenye kujiona ni

Mwenye dhambi zaidi. Kabla ya yote, napenda kukuuliza swali.

Binafsi unajionaje? Je, unafikiri wewe ni mwema au mwovu? Unafikiri vipi?

Kila mtu anaishi kwa hisia zake potofu. Waweza kuwa si mwovu kama udhaniavyo au si mwema kama ujionavyo.

Au unafikiri wewe binafsi si mwema? Jibu la mwisho ndilo, kwamba wewe ni mwovu?

Hebu nikuulize swali jingine. Ni yupi aliye na nafasi zaidi ya kukombolewa – yule

Page 36: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

36 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

aliyetenda uovu zaidi au yule aliyetenda uovu kidogo tu? Yule aliye kubali kwamba ametenda dhambi zisizo na idadi ana nafasi zaidi ya kukombolewa kwa sababu mtu huyo amekubali kuwa yeye ni mwenye dhambi zaidi. Mtu huyu ni rahisi zaidi kuamini neno la ukombozi kwa ajili yake toka kwa Yesu.

Hakika tunapojichunguza nafsini mwetu tunashuhudia kwamba ni wenye dhambi nyingi. Mwanadamu ni nani? Ni mtu aliye “mbegu ya uovu” Isaya 59, inasema kwamba kuna aina za maovu ndani ya moyo wa mwanadamu. Kwa maana hiyo ni wazi kwamba wanadamu ni wenye wingi wa dhambi. Ikiwa tutasema wanadamu ni wenye wingi wa dhambi, wengi watakataa. Lakini ukielezea kwamba mtu ni “mbegu ya uovu” ni maelezo yaliyo sahihi. Tukijichunguza wenyewe kwa uaminifu, ni wazi na kweli kwamba tu viumbe waovu.

Wale wote walio wakweli katika nafsi zao watakubaliana na hili.

Ingawa inaonekana kwamba wengi wenu watakataa kukubaliana na jambo hili kwamba ni wenye wingi wa dhambi. Wengi huishi kwa amani kwa sababu hawajali kwamba wao ni wenye dhambi nyingi. Kwa kuwa sisi ni waovu tumeunda ustaarabu wa dhambi. Kama isinge kuwa hivyo, basi tungeona haya kutenda dhambi Ingawa wengi wetu hatuoni aibu tena tunapotenda dhambi.

Hata ikiwa dhamira zetu zinajua. Kila mmoja ana dhamira inayomshuhudia “ni aibu.” Adamu na Hawa walijificha baada ya kutenda dhambi. Na leo hii wenyedhambi hujificha nyuma ya pazia la utamaduni – utamaduni wetu wa uovu. Wanajificha kati ya watenda dhambi wenzao kuzuia hukumu ya Mungu.

Page 37: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

37 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

Watu wengi wamedanganywa na hisia zao potofu. Wamefikiri kwamba ni waadilifu zaidi ya wengine. Hivyo wanapopata taarifa mbaya za wengine, hupayuka na kusema “Ni kwa vipi huyu mtu ametenda haya? Inawezekanaje mtu kutenda hili? Ni kwa namna gani mwana kuwatendea wazazi wake?” Huku wakiamini kwamba wao hawawezi kuyafanya mambo haya.

Rafiki zangu, ni vigumu kwako kujitambua nafsi yako. Ili uweze kuitambua nafsi yako katika kweli, tunapaswa kwanza kupata ondoleo la dhambi. Inatuchukua muda mrefu kwetu kupata ufahamu wa kweli juu ya asili yetu ya uanadamu, na wapo wengi kati yetu kamwe hawatagundua hili hadi pale watakapofikwa na mauti.

Ijue Nafsi yako

Wasiotambua nafsi zao Huishi vipi?

Huishi katika unafiki kwa kujaribu

Kuficha uovu wao. Wakati mwingine tunakutana na watu wa

aina hii ambao kwa kweli hawazitambui nafsi zao. Ndugu mmoja alisema, “Itambue nafsi yako.” Ingawa, wengi wetu hatujui mioyoni mwetu kuna: uuaji, wizi, tamaa ya mali, madhaifu, hila, tamaa ya mwili,, jicho la husuda na mengine mengi.

Yule asiyejitambua ana sumu ya nyoka katika kinywa chake ingawa hunena mema. Sababu yake ni kwamba, mtu huyu hajaweza kujitambua ya kwamba amezaliwa

Page 38: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

38 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

kuwa mwenye dhambi asiye zuilika. Wapo wengi wa aina hii wasiojua asili yao

wamejipotosha wenyewe na kuishia katika maisha yaliyo vishwa uongo wa nafsi zao. Hawatambui kwamba wanajiingiza wenyewe kwenye jehanamu kwa kujidanganya nafsi zao.

Dhambi huendelea kuchafua watu Kwa maisha yao yote.

Kwa nini wanakwenda motoni?

Kwa sababu hawazitambui Nafsi zao.

Tuone katika Marko 7:21-23 “Kwa maana

ndani ya mioyo ya watu, hutoka mawazo

mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.” Mioyo ya watu imejawa na mawazo ya uovu tangu kutungwa mimba katika matumbo ya mama zao.

Hebu na tufikiri kwa mfano huu, ya kwamba moyo wa mwanadamu uwe umeundwa kwa vioo na kujazwa kwa wingi kwa maji machafu yanayoitwa dhambi. Je, itatokea nini ikiwa mtu atazunguka hapa na pale? Maji haya machafu yatamwagika na kuchafua kila pahala. Na kila mtu huyu atakapopita dhambi hizo ziturudi kumwagika mahali pote.

Kwa jinsi hii sisi ni wenye dhambi kupindukia, tunao ishi kwa namna hii maishani mwetu pote. Tunapaka madoa ya dhambi kilatuendapo. Tutaendelea kutenda

Page 39: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

39 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

dhambi sikuzote za maisha yetu kwa sababu sisi ni wenye dhambi kupindukia.

Taabu yetu ni kuwa, hatujatambua sisi ni wenye dhambi kupindukia, au kwa maneno mengine tu mbegu za dhambi. Ni wenye dhambi kupindukia na wenye dhambi mioyoni mwetu toka siku tulipozaliwa

Wingi wa dhambi umefikia kikomo na kumwagika nje. Ingawa watu hawaamini hili kwamba ni warithi wa dhambi, wanafikiri kwamba wao huongozwa na wengine kutenda dhambi na hivyo, wao binafsi si waovu.

Ingawa watu wanapotenda dhambi, hufikiri kwamba kinachohitajika katika kusafisha na kuwaweka wasafi tena ni kwa dhambi hizo kuzifuta katika kumbukumbu zao (kujisahihisha). Hujutia kwa kulia mara zote wanapotenda dhambi, na kujiona kwamba haikuwa kosa lao. Je tunapojitakasa

wenyewe, yatupasa basi kuendelea na uchafu mwingine? Basi ina maana tutaendelea kujuta na kulia siku zote.

Bilauri inapojaa dhambi itaendelea kumwagika na kuchafua. Hakuna sababu ya kulia na kujutia kwa nje. Haijalishi na kwa mara ngapi tutalia na kujutia kwa tabia zetu mbovu ni bure ikiwa bilauri itaendelea kujaa dhambi.

Tumezaliwa na wingi wa dhambi mioyoni mwetu hapatakuwa patupu ingawa ni kwa kiasi gani zitajaa na kumwagika pahala pote tuendapo. Hivyo tunatenda dhambi maishani mwetu hadi mwisho.

Yeyote asiyetambua hili, huendelea kificha asili yake. Dhambi hukaa ndani ya mioyo ya watu na haitaweza kutoka kwa kulia ili itakaswe. Tunapochafua kwa dhambi kidogo tunasafisha kwa tambaa safi na baadaye kwa tambaa chafu na kuendelea ingawa

Page 40: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

40 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

utakuwa safi bado utaendelea kuchafua tena na tena!

Itaendelea hivi mpaka lini? Hadi pale mtu atakapo kufa. Watu hutenda dhambi hadi mwisho wa siku za maisha yao. Na hii ndiyo maana yatupasa kumwamini Yesu ili tukombolewe. Ili tuweze kukombolewa yatupasa kwanza kuzitambua nafsi zetu.

Ni yupi kwa shukrani zaidi Hupokea upendo wa Yesu?

Ni yule mwenye kukubali Kwamba

ametenda wingi wa makosa maishani.

Na tuseme kwa mfano, kuna watu wawili

wenye kufananishwa na bilauri mbili zilizojaa maji machafu. Bilauri zote zimejaa dhambi mmoja wao akisema “Oh, mimi ni mwenye

dhambi” na hivyo kwenda kumtafuta mtu wa kuweza kumsaidia.

Lakini yule mwingine mwenye kufikiri kwamba yeye si mwenye dhambi, hatoweza kuona wingi wa uovu ndani yake na kufikiri kwamba yeye ni mwema. Maishani mwake huendelea kusafisha uchafu unaomwagika. Atasafisha upande moja hadi nyingine kwa haraka.

Wapo wengi wa aina hii wenye kuishi maisha ya kusafisha dhambi ili kujizuia kuchafua upya tena. Na kwa kuwa bado wanazo dhambi ndani ya mioyo yao, je itasaidia nini? Kuwa waangalifu kwa kutumia juhudi zao haitosaidia kuwa karibu na mbingu. Uangalifu wa aina hii huwaongoza katika njia ya kwenda motoni zaidi.

Rafiki wapendwa “kuwa waangalifu kwa juhudi zetu! Hutupeleka motoni. Na tuchukue fundisho hili kwa dhati mioyoni

Page 41: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

41 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

mwetu. Ingawa unapokuwa mwangalifu na kutochafua kwa dhambi bado wewe ni mwenye dhambi!

Nini kilicho ndani ya moyo wa mwanadamu? Dhambi? tamaa mbaya? Ndiyo! Mawazo potofu? Ndiyo! Wizi? Ndiyo! Majivuno? Ndiyo!

Hatuwezi kujizuia, bali tukubali kwamba sisi ni wadhambi hasa pale tunapojiona kwamba tunatenda dhambi na kuwa dhaifu bila hata kuambiwa.

Tunaweza tusitambue hili tunapokuwa bado ni vijana. Lakini tunapoendelea kuwa watu wazima inakuaje? Tunapo kuwa shule, hadi vyuoni na zaidi, tunakuja kugundua kwamba kila tulicho nacho ndani yetu ni dhambi tupu! Je hii si kweli? Kwa uwazi na uaminifu, ni vigumu kuficha asili zetu za dhambi, Sawa? Hatuwezi kuacha kuwa na dhambi ndani yetu kama si nje! Hujutia na

kusema “Oh, nilipaswa nifanye hivi” Kamwe tunaona ni vigumu kubadilika. Kwa nini ipo hivi? Kwa sababu kila mmoja wetu amezaliwa na wingi wa dhambi mioyoni mwake.

Hatuwezi kuwa safi kwa kuwa waangalifu tu. Tunachohitaji kujua ni kwamba tumezaliwa tukiwa na wingi wa dhambi ndani yetu ili tuweze kukombolewa kabisa. Ni wale tu wenye kukubali ukombozi ulioletwa na Yesu ndiyo watakao okolewa.

Wenye kufikiri kwamba hawajatenda dhambi nyingi, hawamwamini Yesu kwamba alizichukua dhambi zao zote. Na wataishia motoni. Tunapaswa kujua kila mmoja wetu anazo hizi dhambi nyingi ndani yake kwa kuwa tumezaliwa nazo.

Ikiwa mtu atafikiri kwamba “Sijatenda maovu mengi, hivyo sihitaji ukombozi wa dhambi hizi ambazo ni chache sana.” Je,

Page 42: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

42 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

atakuwa huru hapo baadaye? Hili si jambo la maana.

Anayekombolewa hutambua ni mwingi wa dhambi. Hutambua hakika Yesu alizichukua dhambi zote kwa ubatizo katika mto Yordan na pia alizilipia dhambi pale alipokufa msalabani.

Haijalishi tumekombolewa au la, bado tutaendelea kuishi na kusumbuliwa na fikra potofu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi. Na hivi ndivyo tulivyo. Tunaweza kukombolewa endapo tukimwamini Yesu kwamba, alizichukua dhambi zetu zote.

Mungu Hakuwakomboa wale wenye “dhambi chache”

Ni yupi amdanganyae Bwana?

Ni yule mwenye kuomba msamaha wa dhambi za kila siku.

Mungu hawakomboi wale wenye “dhambi

chache” Mungu hawezi kuwatazama wale wenye kusema “Mungu, tazama mimi ninadhambi chache sana” Anao waonea huruma ni wale tu wenye kusema “Mungu, nitaokolewa ikiwa utaniokoa. Siwezi kamwe kuomba toba tena kwa sababu nafahamu siwezi kujizuia kuacha kurudia kutenda dhambi. Naomba uniokoe”

Mungu huwaokoa wale tu wenye kumtegemea yeye pekee. Hata mimi

Page 43: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

43 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

nilijaribu kuomba sala za toba kila siku lakini hazikuniacha huru. Hivyo nilipiga magoti mbele za Mungu na kuomba “Mungu nakusihi unihurumie na uniokoe kwa dhambi zangu.” Nawaombao namna hii huokolewa na kuamini katika ukombozi wa Mungu na ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji. Wataokolewa.

Mungu huwaponya wale tu wenye kujitambua ndani ya nafsi yao kwamba ni wenye wingi wa dhambi, wasemao, “nina dhambi kidogo tu, hivyo naomba unisamehe” bado ni wenye dhambi na Mungu hawezi kuwaokoa. Mungu huwaokoa wale tu wenye kuzikubali dhambi zao kuwa ni nyingi.

Katika Isaya 59:1-2 imeandikwa, “Tazama mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia, lakini maovu yenu

yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimewaficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

Kwa kuwa tumezaliwa na wingi wa dhambi; Mungu hawezi kututazama kwa kuvutiwa nasi. Si kwa sababu mkono wake ni mfupi, macho yake ni mazito au hawezi kusikia tunapo omba msamaha.

Mungu anatuambia “maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu na dhambi zimewaficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Kwa kuwa tunadhambi nyingi ndani ya mioyo yetu hatuwezi kamwe kuingia mbimbuni, hata ikiwa milango itafunguliwa na kuwa wazi zaidi.

Ikiwa sisi tulio na wingii wa dhambi tukiomba msamaha kila tunapotenda dhambi, Ingempasa Mungu kurudia mara kwa mara kumsulubisha Mwana wake kwa ajili ya toba hizo za kurudiwa. Hakika Mungu

Page 44: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

44 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

hapendezwi kufanya njia hii. Anasema “Usije kwangu kila mara na kila siku kwa dhambi zako. Nilimtuma Mwanangu kuwakomboa na dhambi zenu zote. Inawapasa kuelewa ni kwa namna gani alizichukua dhambi zenu zote na kuamini hili ni la kweli. Hivyo amini Injili ya maji na kwa Roho ili muokolewe. Huu ni upendo mkuu niliowapa watu wangu.”

Hivi ndivyo atuambiavyo “Mwamini Mwana wangu na mpokee ondoleo la dhambi Mimi Mungu wako nilimtuma Mwana wangu wa pekee kuwapatanisha na maovu yenu yote kwangu. Mwamini Mwana wangu ili muokolewe.”

Wale wote wasiojitambua kuwa wenye wingi wa dhambi huenda mbele zake bila kuelewa hatari ya wingi wa dhambi zao na kuomba “tafadhali, Bwana nisamehe dhambi hizi tu ambazo ni chache.”

Wanaojaribu kumlaghai Mungu kwa maombi ya namna hii. Hatutendi dhambi mara moja tu, bali tunaendelea kutenda hadi kifo. Kwa hili tungepaswa basi kuendelea kuomba msamaha mara zote hadi mwisho wa maisha yetu, kwa sababu hatuwezi kuzuia kutenda dhambi, na miili yetu ipo chini ya sheria ya kutenda dhambi hadi kufa.

Kusamehewa dhambi chache si suluhisho la tatizo la dhambi kwa sababu tutaendelea kutenda dhambi nyingine tena pasipo idadi. Hivyo njia pekee ya kutuacha tuwe huru ni kuzitwika dhambi zetu zote kwa Yesu.

Nini asili ya Mwanadamu?

Mwingi wa dhambi.

Page 45: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

45 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

Biblia inatoa idadi ya dhambi za wanadamu; “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli, hutumaini ubatili, hunena uongo, hupata mimba ya madhara na kuzaa uovu. Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa na hilo livunjwalo hutoka nyoka nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao, kazi zao ni kazi za uovu na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao. Miguu yao hukimbilia mabaya nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. Njia ya amani hawajui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo

yao; wamejifanyizia njia zilizo potoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani” (Isaya 59:3-8).

Mikono ya watu ina najisi ya uovu na yote, wayatendayo maishani mwao ni dhambi tu! Kila watendalo ni dhambi. Na ndimi zetu zimenena uongo. Kila litokalo kinywani ni udanganyifu.

“Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo” (Yohana 8:44). Wale ambao hawajazaliwa upya husema “Ninakueleza kweli … hakika kweli. Ninachosema ni kweli…” Ingawa kila alichosema si kweli. Ni kama ilivyoandikwa Shetani “asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe.”

Watu huweka imani yao palipo na maneno matupu na kusema uongo. Watu hubeba dhambi na kuzaa uovu. Huatamia

Page 46: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

46 Wanadamu Wamezaliwa wakiwa wenye dhambi

mayai ya fira na kusuka wavu wa buibui. Mungu anasema “yeye alaye mayai yao hufa, la hilo livunjwalo hutoka nyoka.” Anasema kuna mayai ya fira moyoni mwako. Mayai ya nyoka! Kuna uovu ndani ya moyo wako. Na ndiyo maana tunapaswa kukombolewa kwa kuamini Injili ya maji na kwa damu.

Ninapoanza kuongea juu ya Mungu, wapo wenye kusema “Oh, mpendwa, usinizungumzie juu ya huyu Mungu, kwani kila ninapojaribu kutenda jambo, dhambi hutoka ndani mwangu. Inafurika nje. Siwezi kuchukua hatua bila ya kutenda dhambi mahala popote. Sina msaada! Nimejawa na dhambi. Sina matumaini. Hivyo usinizungumzie juu ya Mungu huyu Mtakatifu.”

Mtu wa aina hii ni mwenye hakika kwamba ni mwingi wa dhambi lakini

hajafahamu kwamba Mungu amekwisha mwokoa kwa ukamilifu wote wa Injili ya upendo wake. Ni wale tu wenye kuzitambua nafsi zao kuwa na wingi wa dhambi ndiyo wenye kuokolewa.

Kwa hakika kila mtu yupo namna hii. Kila mtu huendelea kutokwa dhambi mahala pote aendapo. Dhambi hufurika na kumwagika kwa kuwa watu ni wenye wingi wa dhambi. Njia pekee kwetu ya kuokolewa kutoka mazingira ya aina hii ni kwa kupitia uweza wa Mungu. Je huoni ni rahisi na ajabu? Wote wale wenye kujikuta wakitenda dhambi mara zote husononeka, kukosa furaha ingawa utulivu wao hupatikana kwa Bwana Yesu Kristo aliyekuja kutuokoa.

Kwa ukamilifu, alizifuta dhambi zetu zote. Kubali tu kwamba wewe ni mwingi wa dhambi ili uokolewe.

Page 47: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 3

Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Page 48: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

48 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

(Luka 10:25-30) “Na tazama, mwana-sheria mmoja

alisimama amjaribu akisema Mwalimu, nifanye nini ili nirithi uzima wa milele? Akamwambia, imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. Naye akitaka kujidai haki; alimwuliza Yesu, na jirani yangu nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka kwenda Yeriko,

akaangukia kati ya wanyang’anyi wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao wakimwacha karibu kufa.”

Je, tatizo kuu la Mwanadamu ni lipi?

Wanaishi kwa wingi wa fikra potofu.

Luka 10:28, “fanya hivi nawe utaishi.” Watu wengi huishi kwa fikra potofu.

Inaonekana kwamba jambo hili huwafadhaisha sana. Huonekana kwamba ni wenye uerevu lakini rahisi kudanganyika na mwisho kutokujua wapo kwenye upande wa maovu. Tumezaliwa bila ya kutambua nafsi zetu, lakini tunadhani tunazijua. Ikiwa basi watu hawazitambui nafsi zao, Biblia inarudia

Page 49: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

49 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kutueleza kwamba sisi sote ni wenye dhambi.

Kwa kawaida watu huongea habari za dhambi zao. Inaonekana kwamba watu hawana uwezo ndani yao wakutenda mema, ingawa wao wamejiundia tabia ya kujiona ni wema. Hujigamba kwa matendo mema ambayo wametenda ingawa hukubali kwa kushuhudia kwa vinywa vyao kuwa ni wenye dhambi.

Hawajui ya kwamba labda wanayo mazuri ndani mwao au hawana uwezo wa kutenda mema na hivyo kujaribu kudanganya wengine na kwa nyakati nyingine kijidanganya wenyewe. “Tazama hatuwezi kuwa si wema kabisa! Kuna mambo kiasi ambayo ni mazuri ndani yetu.”

Kwa yote haya watu wa aina hii huwaona wengine na kusema “Lo! Sikudhani kama angeweza kufanya hivi. Ingekuwa ni vema

kama asingefanya hili. Angeweza kufanya vizuri zaidi kama asingetenda jambo hili. Ingekuwa vizuri zaidi kama angesema hivi. Nafikiri ingekuwa vizuri kama angehubiri Injili namna hii. Ameokoka kabla yangu, hivyo nadhani alipaswa kutenda mambo kama aliyeokoka zaidi yangu. Nimeokoka hivi karibuni, lakini najua mengi na nitafanya vizuri zaidi yake.”

Hunoa makali ya visu mioyoni mwao wakisema, “subiri, utaniona mimi si kama wewe. Unaweza kudhani wewe ni zaidi yangu, lakini utaona. Imeandikwa kwenye biblia wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza. Najua itakuwa kwangu. Subiri nitakudhihirishia.” Watu hujidanganya nafsi zao.

Ingawa angeweza kujibu mashambulizi ya maneno haya kama angekuwa ni yeye mwenye kuambiwa haya, bado ataendelea

Page 50: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

50 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kutoa hukumu. Anaposimama madhabauni hujikuta akipata kigugumizi kwa kuwa dhamira yake inamhukumu. Swali linapokuja mbele za watu ikiwa wanao uwezo wa kutenda mema, wengi husema hawana uwezo wowote. Lakini ndani ya nafsi zao wanazo fikra kwamba wao wanao uwezo huo. Hivyo hujaribu kutenda mema hadi wanapo kufa.

Hufikiri wanayo mazuri ndani ya mioyo yao na wanao uwezo wa kutenda mema. Na huamini kuwa wao ni wema wa kutosha. Ukiachilia mbali ni kwa muda gani wamekuwa wenye kushika dini, hasa wale ambao waliopata mafanikio makubwa katika kazi za Mungu, hufikiri “Nimeweza kufanya hivi na vile kwa ajili ya Bwana.”

Je, ikiwa tutamweka Bwana kando ya maisha yetu, tutaweza kweli kutenda mema? Kuna mema kweli ndani ya utu wetu?

Tutaweza kweli kuishi kwa kutenda mema? Wanadamu hawana uwezo binafsi wa kutenda mema. Wanapojaribu kwa nafsi, hujikuta wakiishia kutenda dhambi. Wengine humweka Yesu kando baada ya kumwamini kwa kujaribu kutenda mema kwa kutegemea nafsi zao. Hakuna la zaidi bali ni uovu kwetu na hivyo kutenda dhambi tu. Kwa wote (hata waliookoka) tunaweza kutenda dhambi. Ni ukweli wa miili yetu.

Mara nyingi tunatenda yapi? Mabaya au mazuri?

Mabaya!

Katika kitabu chetu cha nyimbo za kusifu “Lisifuni jina la Yesu” kuna wimbo Fulani huimbwa “Bila Yesu tumekwama. Hatuna thamani kama vile merikebu ipitavyo bahari

Page 51: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

51 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kuu bila nahodha.” Bila Yesu, tutaweza kuanguka dhambini tu! Sisi ni viumbe waovu. Tutaweza kutenda mema pale tu tutakapookolewa.

Mtume Paulo alisema “Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo” (Warumi 7:19). Kama mtu akiwa ndani ya Yesu, haijalishi hili, ingawa atakapo jaribu kutenda mema bila Mungu wakati wote atajikuta akiishia kutenda dhambi.

Hata mfalme Daudi aliwahi kuwa mwenye asili hii. Wakati ufalme wake ulipostawi na kuwa wenye amani, siku moja aliamka na kwenda juu ya dari la nyumba yake kupunga hewa. Hapo aliona kishawishi na kuanguka kwenye tamaa ya mwili. Alikuwa vipi alipo msahau Bwana? Alikuwa mwovu! Alifanya tendo la zinaa na Basheba na kumuua Uria, mumewe na hakuuona uovu wake. Badala

yake alijitetea kwa matendo yake. Ndipo siku moja, nabii Nathari alipomjia

na kusema “Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wapili maskini, Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwanakondoo mmoja, mdogo ambaye amenunua na kumlea; naye akakuwa pamoja naye na pamoja na wanawe, hula sehemu ya posho lake, na kukinyanyua kikombe chake na kulala kifuani mwake akawa kwake kama binti. Hata msafiri mmoja akamfikia yule tajiri, naye akaacha kutwaa moja ya kondoo zake mwenyewe, au moja ya ng’ombe zake mwenyewe, ili kumuandalia yule msafiri aliyemfikia, bali alimnyang’anya yule maskini mwanakondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikia.” (2Samweli 12:1-4)

Daudi akasema “mtu aliyetenda jambo

Page 52: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

52 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

hili, hakika yake astahili kufa!” Hakika hasira yake ilimpanda na kusema “Alikuwa na mifugo yake mingi na yakutosha; ilimpasa kuchukua moja wapo. Badala yake alichukua kondoo wa masikini kwa matayarisho ya chakula cha mgeni wake. Yampasa kufa!” Ndipo Nathani alipomwambia “Wewe ndiwe mtu huyo” kama hatumfuati Yesu na kuwa naye, hata yule aliyeokoka aweza fanya kama haya.

Ndivyo ilivyo kwa watu wote, hata wale waaminifu mara nyingi huanguka kwa kutenda uovu bila Yesu. Hivyo yatupasa tushukuru sana nyakati hizi kwamba Yesu ametuokoa, ingawa ndani yetu hatuna lililo jema. “Naam tena mtulie chini ya kivuli cha Msalaba.” Miyoyo yetu imetulia chini ya kivuli cha ukombozi wa Kristo, lakini ikiwa tutakiacha na kutafuta wenyewe, hakika hatutapata pumziko.

Mungu ametupatia Haki kwa Imani katika sheria

Ni ipi inapaswa kuwa ya kwanza Imani au Sheria?

Imani.

Mtume Paulo alisema kwamba, Mungu ametupatia haki kwa imani toka mwanzo. Alimpatia Adamu na Hawa, Kaini na Abeli, Sethi na Enoki, Nuhu, Abrahamu, Isaka na mwisho Yakobo na watoto wake kumi na wawili. Hata pasipo sheria, walifanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu kupitia haki itokanayo na Imani ya Neno lake. Walibarikiwa na walipata pumziko kupitia imani ya Neno lake.

Muda uliopita wakati uzao wa Yakobo

Page 53: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

53 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

uliishi Misri kama watumwa kwa miaka 400 kwa sababu ya Yusufu. Ndipo Mungu alipowaongoza kutoka kupitia Musa kuelekea Kanaani, pamoja na kuwa watumwa kwa miaka 400, walisahau haki katika Imani.

Ndipo Mungu alipowaongoza kupita kati ya Bahari ya Shamu kwa muujiza na kuwaongoza jangwani. Walipofika jangwa la dhambi, akawapa sheria katika Mlima Sinai. Aliwapa sheria ambazo zilikuwamo Amri kumi na vipengele 613. Mungu aliahidi “Ndimi Bwana Mungu wako, Mungu wa Abraham, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Musa apande na kuja katika mlima Sinai na nitawapa sheria.” Ndipo alipowapa Waisraeli Sheria.

Aliwapa Sheria ili waweze “kutambua dhambi” (Warumi 3:20). Ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya anachotaka na asichotaka na kuweka wazi haki yake na

utakatifu. Watu wote wa Israeli waliokuwa

utumwani Misri kwa miaka 400 walipita kati ya Bahari ya Shamu. Hawakuwahi kukutana na Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Hawakumjua.

Walipokuwa wakiishi kama watumwa kwa kipindi hicho cha miaka 400, walisahau haki ya Mungu katika muda huo hawakuweza kuwa na kiongozi. Yakobo na Yusufu walikuwa viongozi hapo awali. Inaonekana Yusufu alishindwa kuirithisha Imani hiyo kwa watoto wake wa kiume, Manase na Efraimu.

Hivyo, walihitaji kumtafuta Mungu tena na kukutana naye kwa kuwa waliisahau haki yake. Tunapaswa kuweka akilini kwamba Mungu aliwapa haki kwa imani mwanzo na kuwapa sheria baada ya kuisahau Imani. Aliwapa Sheria ili waweze kumrudia.

Kuiokoa Israeli na kuwafanya kuwa wana

Page 54: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

54 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

wake, aliwaambia kwamba iliwalazimu kutahiriwa.

Nia ya kuwaita ilikuwa ni kuwafanya watambue kwamba alikuwa kati yao ili kuanzisha Sheria na pili, kufanya watambue walikuwa ni wenye dhambi mbele zake. Mungu alitaka waje mbele zake na kuwa watu wake kwa kukombolewa kwa mfumo wa sadaka ambayo aliyokuwa amewapa. Na aliwafanya kuwa watu wake.

Wana wa Israeli walikombolewa kupitia mfumo wa sadaka wa Sheria kwa kumwamini Masiya ajaye. Lakini mfumo huu ulipitwa na wakati. Na tuangalie hii, ilikuwa ni lini.

Katika Luka 10:25 mwanasheria mmoja alitajwa kumjaribu Yesu. Alikuwa ni Mfarisayo. Mafarisayo walikuwa ni wenye kuyashika mafundisho bila kukubali kubadilika kwa kufanya jitihada zao binafsi

kuishi kwa kufuata neno la Mungu; Walijaribu kuzilinda sheria za nchi kwanza kwa kuishi kadiri ya maandiko ya sheria. Walikuwa ni “wakereketwa” (kwa lugha ya kisasa) ambao walihamasisha na kufanya ghasia za kuvunja sheria ili kufanikisha malengo ya maono yao juu ya uhuru wa Waisraeli toka kwa Warumi.

Yesu alitaka kukutana Na watu gani?

Wenye dhambi wasio na Mchungaji.

Kuna baadhi yao hata nyakati hizi wamo kwenye dini tuzionazo. Huongoza harakati za kijamii kwa usemi kama vile “Okoa wanaogandamizwa duniani!” Huamini Yesu alikuja kuokoa maskini na

Page 55: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

55 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

wanaogandamizwa. Hivyo baada ya kujifunza theologia katika seminari, huchukua nafasi katika mambo ya kisiasa na kujaribu kuwakomboa wanaonyanyaswa katika kila sehemu ya jamii.

Ndiyo wenye kushinikiza kwa kusema “Hebu na tuishi kwa sheria na rehema ya sheria takatifu. Tuishi kwa sheria, kwa neno la Mungu.” Lakini hawatambui hakika ya ukweli wa Sheria. Hujaribu kuishi kwa sheria iliyoandikwa bila kufahamu na kupata ufunuo wa Mungu juu ya Sheria hiyo.

Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba hapakuwepo na manabii, watumishi wa Mungu katika Israeli kwa kipindi hicho cha miaka 400 kabla ya Kristo. Kwa sababu hii basi, walikuwa ni kundi la kondoo wasio na Mchungaji.

Hawakuwa na sheria wala Kiongozi wa kweli. Mungu hakujidhihirisha mwenyewe

kwa hao walio kuwa ni viongozi wa dini zao walio wanafiki. Nchi ilitawaliwa na Dola ya Warumi. Hivyo Yesu aliwaambia watu hawa wa Israeli walio mfuata jangwani kwamba hawatarudishwa kutoka kwake wakiwa na njaa. Alijawa na huruma juu yao waliokama kundi la wanakondoo wasio na Mchungaji kwani wengi wao walikuwa kwenye mateso makubwa.

Wanasheria na wale wengine walio na nafasi za uongozi walikuwa ndiyo wenyewe tu wenye kunufaika. Mafarisayo walikuwa ni kizazi cha “Judaism” na walikuwa ni wenye majivuno sana.

Mwanasheria huyu alimwuliza Yesu katika Luka 10:25 “nifanye nini niweze kurithi uzima wa milele?” Alionekana kufikiri kwamba yeye ni bora zaidi kati ya watu wa Israeli. Hivyo mwanasheria huyu (ambaye hajakombolewa) alimwuliza Yesu kwa

Page 56: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

56 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kusema “nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?”

Mwanasheria huyu anasimama badala yetu leo. Alimwuliza Yesu swali hili, naye akajibu “imeandikwa nini katika Torati? Wasomaje?”

Naye akajibu “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote na akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”

Naye akamjibu “umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.”

Alijaribu kumtia changamoto Yesu bila ya kufahamu yeye alikuwa ni mwenye dhambi, asiyeweza kutenda mema. Hivyo Yesu alivyomwuliza, “imeandikwa nini katika Torati, wasomaje?”

Unasoma nini juu ya sheria?

Sisi ni wenye dhambi

tusioweza kufuata sheria.

“Wasomaje” kwa kifungu hiki Yesu

anauliza, ni kwa namna gani mimi na wewe tunaijua na kuielewa sheria.

Kwa jinsi hii wengi wetu nyakati hizi ndivyo tulivyo. Mwanasheria huyu alifikiri kwamba Mungu alikusudia kuweka sheria ili zifuatwe. Hivyo alijibu kupitia maandiko “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote na jirani yako kama nafsi yako.”

Sheria haikuwa na kasoro. Alitupa sheria

Page 57: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

57 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

iliyo kamilifu. Alituambia tumpende Bwana kwa moyo na kwa roho na kwa nguvu na akili na kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu. Ni haki tumpende Mungu kwa moyo wetu wote na kwa nguvu zetu zote, lakini hii ni amri takatifu isiyoweza kutimizwa kwa nafsi zetu.

“Wasomaje?” Hii ina maana sheria ni kamilifu na sawa lakini je, wewe unaelewa nini juu yake? Mwanasheria alifikiri kwamba Mungu alileta sheria hii ili aweze kuitii. Ingawa Sheria ya Mungu imeletwa kwetu ili tuweze kuziona nafsi zetu na upungufu ndani yake kwa kuukubali udhaifu wetu uliowazi kabisa mbele za Mungu. “Umetenda dhambi, umeua hali nilikuambia usiue. Kwa nini hukunitii.” Ndivyo Mungu akuulizavyo.

Sheria huweka wazi dhambi ya watu ndani ya mioyo yao. Hebu na tufikiri kwa mfano nilipokuwa nikitembea, nikaona tunda

zuri na tamu lililoiva katika shamba la mtu. Mungu amenionya kwa sheria, “usichume tunda hilo katika shamba. Itaniaibisha mimi ukitenda hilo.” “Ndiyo Baba.” “Shamba hili ni la ndugu fulani, hivyo usichume.” “Ndiyo Baba.”

Tunaposikia hivyo tusichume, tunahisi msukumo ndani yetu wa kuchuma. Tunapochukua hatua ya kujizuia inashindikana. Na hii ndivyo ilivyo katika dhambi za watu.

Mungu ametuonya tusitende dhambi. Aweza kusema hivi kwa kuwa yeye ni mtakatifu, mkamilifu na mwenye uwezo wote. Kwa upande mwingine hatuwezi “kamwe” kutotenda dhambi na “kamwe” hatuna utakatifu. Hatuna mazuri ndani ya mioyo yetu. Sheria inatuhukumu na neno “kamwe.” Kwa nini? Kwa sababu watu husukumwa na tamaa ndani ya mioyo yao.

Page 58: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

58 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Hatuwezi kujizuia bila kufuata tamaa. Tunatenda dhambi ya uzinzi kwa kuwa tunayo dhambi ya uzinzi ndani ya mioyo yetu.

Tunapaswa kusoma biblia kwa makini. Niliposoma niligundua maneno haya. Nilisoma kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili yangu. Na nilishindwa kujizuia machozi yalinitoka. Hakika nilikuwa mwingi wa dhambi hata kumfanya afe kwa ajili yangu… Moyo wangu ulipondeka sana hata kumwamini. Na ndipo nilipowaza “ikiwa nitamwamini, basi nitaliamini neno lake.”

Niliposoma kitabu cha Kutoka 20, Biblia inasema “usiwe na miungu wengine zaidi yangu.” Niliomba toba kutokana na amri hii. Nilitafuta katika kumbukumbu za akili yangu ikiwa hapo awali niliwahi kuwa na miungu wengine zaidi yake, kulitaja jina lake bure, au kuabudu miungu wengine. Niligundua

kwamba niliabudu miungu wengine mara nyingi wakati nilipotoa kafara kwa heshima ya mababu zangu walio kufa. Nilitenda dhambi ya kuwa na miungu wengine.

Hivyo niliomba kwa kutubu, “Bwana, nimeabudu miungu wengine. Imenipasa kuhukumiwa kwa hilo. Nakusihi unisamehe dhambi zangu. Sinto tenda tena.” Na baadaye, dhambi moja itaonekana kuondolewa.

Hapo tena jaribu kukumbuka ikiwa niliitia jina la Mungu bure. Nagundua ya kwamba nilipo anza kumwamini Mungu, nilikuwa nikiendelea kuvuta sigara. Rafiki zangu walinieleza, “Huoni yakuwa unamwaibisha Mungu kwa kuvuta kwako sigara? Itawezekanaje kwa Mkristo kuvuta sigara?”

Hii ni sawa na kuliitia jina lake bure. Hivyo nikaomba tena “Bwana nimeliita jina lako bure, Naomba unisamehe. Nitaacha kuvuta.”

Page 59: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

59 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Hivyo nilijaribu kuacha kuvuta lakini nilishindwa na kuendelea na kuacha kwa muda tofauti katika kipindi cha mwaka mzima. Hakika ilikuwa ni vigumu kwangu na ilifikia kutowezekana kuacha kuvuta sigara. Lakini mwishowe niliweza kabisa nilidhani hii ilikuwa tayari dhambi niliyoweza kuidhibiti.

Nyingine ilikuwa, “Kuitakasa siku ya Sabato.” Hii ina maana kwamba nisifanye shughuli yeyote siku ya Jumapili, kazi au kutafuta fedha… Na niliweza kuacha hili pia.

Ndipo ilipokuja “Waheshimu baba na mama yako.” Niliwaheshimu nilipokuwa mbali nao, lakini nilipokuwa karibu nao nilikuwa na machungu juu yao. “Oh! Nimetenda tena dhambi mbele ya Mungu. Naomba unisamehe” niliomba toba.

Lakini sikuweza kuwaheshimu kwani wote walikwisha fariki kwa wakati huo. Nifanye nini sasa? “Bwana, naomba msamaha mimi

mwenye dhambi nisiye na thamani, ulikufa msalabani kwa ajili yangu” nilishukuru sana!

Njia hii ndiyo niliyo itumia kushughulikia dhambi zangu moja hadi nyingine. Palikuwa na sheria nyingine kama vile usiue, usizini, usitamani mpaka nilipokuja gundua sikuweza kufuata hata moja, niliomba usiku kucha! Je, wajua ya kwamba kuomba na toba haifurahishi kabisa. Hebu tuangalie hili.

Nilipowaza juu ya kusulubiwa kwa Yesu, niliona uchungu uliokuwepo. Alikufa kwa ajili yetu na ni nani asiye taka kuishi kwa neno lake. Nililia usiku mzima na kuwaza ni upendo wa namna gani juu yangu na nilimshukuru kwa kunipa faraja ya kweli.

Katika mwaka wangu wa kwanza kuhudhuria kanisani ulikua kwa ujumla ni rahisi, lakini miaka ilipozidi kuendelea ikawa ni vigumu kwangu kulia kwa kuomba toba kwani ilibidi nifikiri sana ili niweze kulia

Page 60: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

60 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kwani nilikwisha kuwa na mazoea. Machozi yalipoacha kunitoka, niliamua

kuomba milimani na kufunga siku hadi 3. Ndipo machozi yalipo toka. Yalinilenga tena nilipo kuja mbele ya kanisa nililia.

Walio nizunguka waliniambia “Oh! Umekuwa mtakatifu sana kwa sala zako za milimani.” Lakini baadaye yalikauka tena. Ikawa vigumu tena katika mwaka wa tatu. Nilijaribu hata kufikiri mabaya niliyotenda kwa rafiki zangu na ndugu katika Kristo ili niweze kutoka machozi Haikuwezekana kabisa!

Baada ya miaka 5, sikuweza kulia ingawa nilijitahidi kwa namna zote na hata kutokwa na makamasi. Baada ya miaka kadhaa katika hili, sikupata amani ndani yangu. Na ndipo Mungu alinifanya niirudie tena Biblia.

Sheria ni kwa ajili ya kuzifahamu dhambi

Tunagundua nini juu ya Sheria?

Kamwe hatuwezi kuzifuata Sheria.

Katika Warumi 3:20 tunasoma “Kwa

maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Mwanzo kabisa nilichukulia kifungu hiki kuwa ujumbe binafsi kwa Mtume Paulo na kuamini maneno niliyopendelea. Lakini baada ya machozi yangu kukauka hakika sikuweza kuendelea na maisha yangu ya imani ya kidini.

Hivyo niliendelea na dhambi na kufikia hatua ya kugundua nina dhambi ndani ya

Page 61: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

61 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

moyo wangu na kushindwa kuishi kwa sheria. Sikuweza kuvumilia ingawa sikuweza kuachana na sheria kwa kuwa niliamini ilikuwepo ili niweze kuitii. Hatima yake nikawa mwanasheria kama walionyeshwa katika maandiko hapo awali. Ikawa ni vigumu kwangu kuendelea na maisha ya imani.

Nilikua na dhambi nyingi hata kufikia kila ninapo soma sheria naanza kugundua dhambi hizo kila ninapozivunja amri 10 ndani ya moyo wangu. Ikumbukwe kuwa na dhambi moyoni ni sawa kutenda dhambi tu! Sikuweza kufahamu kwamba nilikuwa tayari muumini wa sheria.

Nilipofuata sheria nilifarijika. Lakini nilipoanguka nilikua mnyonge, mwenye hasira na huzuni. Na wakati huo nikawa mwenye kukosa matumini kwa yote. Ingeweza kuwa rahisi ikiwa hapo awali

ningefundishwa ukweli juu ya sheria kama vile “Hapana, siyo hivi! Ipo maana nyingine ya sheria nayo ni kama taa kuonyesha dhambi zako kama vile wewe unapenda fedha, kupenda jinsia tofauti na vitu vizuri vya kuonekana.Una vitu unavyovipenda kuliko umpendavyo Mungu. Unapenda sana kufuata mambo ya dunia. Sheria iliwekwa kwako si uifuate bali uweze kugundua nafsi yako kama mwenye dhambi aliye na uovu moyoni.”

Ikiwa mtu yoyote angeweza kunifundisha hivi basi nisingeweza kuteseka kwa miaka 10 namna ile. Hivi ndivyo nilivyo weza kuishi kwa sheria kwa miaka 10 kabla ya kuja kugundua hili.

Amri ya nne inasema “Ikumbuke siku ya Sabato na uitakase.” Hii ina maana kwamba tusifanye kazi siku ya jumapili.Tunafundishwa tusifanye kazi, sio

Page 62: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

62 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kutembea mwendo wa mbali katika safari kwa siku ya Jumapili. Nilidhani ilikuwa ni sahihi na niheshima kutembea sehemu nilizo hitaji kuhubiri. Hata hivyo nilitaka kuhubiri sheria. Na nilihisi ilinipasa kutenda yale nihubiriyo. Ikawa ni vigumu na kushindwa.

Kama ilivyo hapo mwanzo “wasomaje?” sikuelewa swali hili na kuteseka miaka 10. mwanasheria hakuelewa vema hili.Alifikiri ya kwamba ikiwa ataheshimu sheria na kuishi kwa uangalifu mkubwa atakuwa amebarikiwa na Mungu.

Lakini Yesu alimwambia “wasomaje?” Naye akajibu kwa imani itokanayo na sheria. Naye akamjibu “umejibu vema, unaichukua kama ilivyoandikwa. Jaribu kuifuata. Utaishi ikiwa utaweza na utakufa ukishindwa. Mshahara wa dhambi ni mauti. Hakika ukishindwa utakufa.” (kinyume cha kuishi ni kufa,sivyo?)

Lakini mwanasheria huyu hakugundua hili. Mwanasheria ni mfano wetu sisi leo, mimi na wewe. Nilijifunza theologia (elimu ya dini) kwa miaka 10. Nilijaribu kila namna, kusoma kila kitu na kutenda kila jambo; kufunga kula, kuwa na maono, kunena kwa lugha… Nilisoma Biblia kwa miaka 10 kwa kutegemea nitahitimisha jambo fulani mbeleni. Lakini kiroho nilikuwa bado kipofu!

Na ndiyo maana mwenye dhambi huitaji mtu fulani atakayefungua macho yake, na huyu ni Bwana wetu Yesu Kristo. Ndipo mtu hugundua “Ahaa! Hatuna uwezo wa kufuata sheria. Haijalishi ni kwa bidii gani tutaweza kujaribu kuifuata tutaishia kufa tukikosa matumaini. Lakini Yesu alikuja kutuokoa kwa maji na kwa Roho! Haleluya!” Kwa maji na kwa Roho tutaweza kukukombolewa. Ni neema, zawadi ya Mungu. Na tumsifu Bwana.

Page 63: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

63 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Nilikuwa mwenye bahati ya pekee kuhitimu toka kwenye njia ya kukosa matumaini katika sheria, naamini wengi huchukua muda mrefu zaidi katika maisha yao kusoma theologia katika njia panda na bila kugundua ukweli hadi umauti. Wengine huamini kwa mioyo mingi, kizazi hadi kizazi na hawazaliwi upya.

Tunahitimu kutokuwa wadhambi pale tu tunapogundua hatuna uwezo wa aina yeyote binafsi wa kufuata sheria na kusimama mbele ya Yesu kwa kukubali kuisikiliza Injili ya maji na kwa Roho. Tunapokutana na Yesu tunahitimu kutoka kwenye hukumu na jehanamu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi, lakini tunafanyizwa haki kwa sababu Yesu ametuokoa katika maji na damu yake.

Yesu amesema hatuwezi kuishi katika mapenzi yake. Alimwambia mwanasheria, lakini haelewa hili. Hivyo alimpa mfano huu.

Nini kimfanyacho Mwanadamu kuanguka tokakwenye

maisha ya imani?

Dhambi.

“Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang`anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha wakaenda zao,wakamwacha karibu kufa” (Luka 10:30 ). Yesu alimpa Mwanasheria mfano huu ili kuamsha dhamira yake kwakua huteseka kwa maisha yake yote kama jinsi Mtu yule aliyepigwa na wanyang`anyi karibu kufa.

Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko. Yeriko inawakilisha dunia hii ya sasa, hali Yerusalemu inawakilisha mji wa

Page 64: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

64 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kidini, mji wa imani uliojawa na majigambo ya sheria. Mfano huu hutuelezea ikiwa tutamwani Kristo kwa njia ya udini tutaangamia.

“Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akangukia kati ya wanyang`anyi, wakamvua nguo wakamtia jeraha wakenda zao wakimwacha karibu kufa.” Yerusalemu ulikuwa ni mji mkubwa ukiwa na wakazi wengi. Kulikuwa na Kuhani Mkuu, Jeshi la Makuhani Walawi na wengi wa Wakuu mashuhuri wa dini. Palikuwepo na wengi wenye kuelewa sheria vema. Na walijaribu kuishi kwa sheria, lakini walishindwa na kukimbilia Yeriko wakangukia duniani (Yeriko) na kushindwa kuzuia kukutana na wanyang`anyi.

Mtu huyu pia alikutana njiani na wanyang`anyi toka Yerusalemu kwenda Yeriko wakamvua nguo. “Kuvuliwa nguo”

maana yake kupoteza haki. Ni vigumu kwetu kuishi kwa kufuata sheria, kuishi kwa sheria Mtume Paulo amesema katika Warumi 7:19-20 “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilipendalo si mimi nafsi yangu nilitendalo, bali ni ile dhamiri ikaayo ndani yangu.”

Ningetamani kutenda mema na kuishi katika Neno lake Mungu. Lakini ndani ya moyo wa mwanadamu umefurika mawazo mabaya, uasherati,wivi, uuaji, unzizi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu (Marko 7: 21-23 ).

Kwa kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya mioyo yetu, basi tunafanya yale tusiyopaswa na hatufanyi yale yatupasayo kufanya. Tunaendelea kurudia maovu haya ndani ya mioyo yetu. Hivyo shetani huitaji

Page 65: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

65 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kukuhamasisha kwa kiasi kidogo tu ili uweze kutenda dhambi. Dhambi zilizo ndani ya moyo wa kila mwanadamu.

Je tutaweza kuishi Kwa sheria?

Hapana! Imeandikwa katika Marko 7:20

“kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.” Yesu anatueleza kwamba yapo mawazo

mabaya uasherati, wivi, uaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu katika moyo wa mwanadamu.

Wote tunauuaji ndani ya mioyo yetu. Hakuna asiyefanya mauaji. Akina mama hukemea watoto zao “Usifanye hivi. Nilikuambia usifanye, ole wako. Nilikueleza mara nyingi. Sasa nitakuua ukirudia tena.” Hii ni sawa na kuua! Unaweza kumuua mtoto wako katika mawazo yako kwa maneno yasiyo na fikara kama haya.

Imewapasa watoto wetu kuwa wepesi kutuepuka kwa kutukimbia; kwani pasipo hivyo tungeweza kuwashukia kwa vipigo vya hasira na hata kufikia hatua ya kuwaua. Wakati mwingine tunaingiwa hofu na kusema “Oh Mungu wangu! Kwanini nimefanya hivi?” Tunaanza kuona alama za uvimbe baada ya kuwapiga watoto wetu na kudhani yakuwa tulikuwa wendawazimu kwa kutenda hayo. Hatuwezi kujizuia kutenda haya kwa sababu ndani ya mioyo yetu kuna uuaji.

Page 66: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

66 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Hivyo “Ninatenda nisilo taka” maana yake tunatenda uovu kwa kuwa tuna uovu ndani yetu. Ni rahisi kwake shetani kutujaribu kutenda dhambi.

Na tuseme hivi kwa mfano, mtu ambaye hajakombolewa akae katika kibanda kwa miaka 10, akielekeza uso wake ukutani akiwazia kama Sungchol, kuhani wa dini ya Kijadi Korea. Ni vyema akiwa ameketi akielekeza uso wake ukutani, lakini itabidi mtu kumletea chakula na kufanya usafi mahala pale.

Itampasa awe na mawasiliano na mtu. Haitakuwa ni tatizo ikiwa atakuwa ni mwanaume kama yeye, lakini hebu tuseme akiwa ni mwanamke. Ikiwa atamwona kwa bahati, basi muda wote aliokaa utakuwa ni bure. Anaweza kuwaza moyoni “hainipasi kutenda uzinzi; lakini ninao moyoni; na inanibidi niuache. Niutoe. Hapana! Ondoka

kwenye akili yangu!” Lakini lengo lake litayeyuka pale tu

atakapomuona mwanamke huyo. Baada ya mwanamke huyo kutoka, ataangalia ndani ya moyo wake. Miaka 5 ya jitihada zake zitageuka kuwa ni bure na vyote kwa ukorofi.

Ni rahisi shetani kuteka haki ya mtu. Kile alichonacho shetani ni kuweka msukumo mdogo tu! Mtu anapohangaika kutotenda dhambi bila ya kukombolewa kwanza ni rahisi na haraka zaidi kuanguka kwenye dhambi. Mtu huyo anaweza kuwa ni mtoaji mzuri wa zaka kila Jumapili, mfungaji kwa siku 40, mwenye kujitoa kwa maombi ya siku 100, lakini shetani hufanikiwa kumshawishi na kumdanganya kwa mambo mazuri ya maisha.

“Nitakupa nafasi bora ya cheo katika shirika, lakini wewe ni Mkristo usiyefanya

Page 67: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

67 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kazi Jumapili, Vipi utaweza? Hii ni nafasi kubwa. Utaweza kufanya kwa muda wa wiki 3 za Jumapili na iliyobaki moja katika mwezi unaweza kwenda Kanisani. Na hakika utaifurahia nafasi hii nzuri yenye malipo manono. Unaonaje?” kwa hili mpendwa kati ya watu 100, watu 100 wangelikubali tu.

Kama halifanyi kazi hili, shetani atarudia mchezo mwingine kwa wale wenye tamaa ya ngono. Shetani atamleta mwanamke mbele yake na ataanguka kumtamani, na kumsahau Mungu mara moja! Na hivi ndivyo haki ya mtu inavyovuliwa.

Ikiwa tutajaribu kuishi kwa kuifuata sheria, mwisho wetu siku zote ni majeraha ya dhambi, maumivu na ufukara wa kiroho; tutapoteza haki zote. “Alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaanguka kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao,

wakimwacha karibu kufa.” Hii ina maana kwamba tunaweza kujaribu

kukaa Yerusalemu kwa kuishi katika mapenzi ya Mungu Matakatifu, tutajikwaa kila wakati kwa sababu ya udhaifu na mwisho kuangamia.

Yaweza kuwa unaomba toba kwa Mungu, “Bwana nimetenda dhambi. Naomba unirehemu; sitotenda tena. Naahidi kwako kwamba hili litakuwa ni mwisho. Nakusihi unisamehe hili tu!”

Lakini haichukui muda. Watu hawawezi kuishi katika ulimwengu huu bila kutenda dhambi. Wanaweza kujizuia kwa kiasi cha muda fulani, lakini haiwezekani kutotenda kabisa. Hivyo hatuwezi, ila tutaendelea kurudia kutenda dhambi tu! “Bwana, naomba unisamehe” ukiendelea hivi, utalihama Kanisa na kuacha dini kabisa. Utamwacha Mungu kwa kuwa na dhambi na

Page 68: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

68 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

kuishia jehanamu. Kushuka kwenda Jeriko ni sawa na

kuangukia katika ulimwengu wa sasa; kuwa karibu na dunia mbali na Yerusalemu. Hapo mwanzo, Yerusalemu ilikuwa karibu na kwa kadiri ya mzunguko wa dhambi na kuungama ulivyorudiwa tunajikuta tukisimama katikati ya mji wa Yeriko; kuanguka kabisa duniani.

Nani awezaye Kuokolewa?

Wale watakao acha Kujitafutia haki.

Alikutana na nani njiani alipokuwa akienda

Yeriko? Alikutana na wanyang’anyi. Yeyote yule asiyetambua, na kuishi kwa sheria maisha yake yanafananishwa na mbwa

aliyetelekezwa. Hula na kunywa na kwenda haja mahala popote. Mbwa wa aina hii huamka asubuhi nyingine na kwenda haja na kula tena. Huweza hata kula kinyesi chake. Ndiyo maana mtu huyu hufananishwa na mbwa. Hula na kwenda haja lakini huomba toba asubuhi inayofuata na kurudia yale yale kwa mara zote.

Ni sawa na mtu aliyekutana na wanyang’anyi akienda Yeriko. Akaachwa akiwa amejeruhiwa karibu ya kifo. Ina maana kwamba kuna dhambi ndani ya moyo. Na hii ndivyo ilivyo kwa mwanadamu.

Watu humwamini Yesu na kujaribu kuishi kwa sheria katika Yerusalemu, jamii ya dini, lakini wanaachwa na dhambi ndani ya mioyo yao. Kile wanachoweza kuonyesha katika maisha yao ya udini ni majeraha ya dhambi. Wale wenye dhambi mioyoni mwao hakika siku za mwisho watakwenda motoni.

Page 69: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

69 Ikiwa tutaenenda kwa Sheria, Je, itatuokoa?

Wanajua hili, lakini hawajui lakufanya. Je ni kweli hata wewe upo katika mji huo wa dini? Ndiyo. Hata sisi tulikuwepo.

Mwanasheria aliyeshindwa kuielewa sheria ya Mungu angehangaika maishani pote, lakini angeishia motoni kwa majeraha. Ni sisi kati yetu, mimi na wewe.

Yesu pekee aokoa. Wapo watu wengi wenye uerevu kati yetu na kila mara kupayuka wanayoyajua. Wote hawa hujifanya kwa kuishi katika sheria ya Mungu na hawapo kweli nafsini mwao. Hawawezi kuita beleshi kuwa ni beleshi, mara zote huzificha nafsi zao kwa nje ili kuonekana waaminifu.

Kati yao ni wenye dhambi kuelekea Yeriko, wale waliopigwa na waovu na kuachwa karibu kufa. Tunapaswa kuelewa vile tusivyo imara, wepesi wa kuumizwa mbele za Mungu.

Yatupasa tukiri mbele zake “Bwana, hakika nitaishia motoni ikiwa hutoniokoa. Naomba uniokoe. Nitakufuata popote, ikiwa ni penye kimbunga au dhoruba, ikiwa tu nitaweza kusikia Injili. Ukiniacha peke yangu, nitakwenda motoni. Nakusihi niokoe!”

Wale wenye kugundua kuwa wapo karibu na jehanamu na kujaribu kutenda matendo ya kujitafutia haki wakiwa wanaambatana na Bwana ndiyo pekee watakaookolewa. Hatuwezi kuokolewa kwa juhudi zetu binafsi.

Yatupasa kuelewa kwamba, tutafananishwa na mtu yule aliye angukia katika mikono ya wanyang’anyi.

Page 70: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 4

Ukombozi wa Milele

Page 71: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

71 Ukombozi wa Milele

Ukombozi wa Milele

(Yohana 8:1-12) “Walikwenda kila mtu nyumbani

kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlimani wa Mizeituni. Hata asubuhi kulipokucha akaingia hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha, Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati wakamwambia Mwalimu mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga, kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaji? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili

wapate sababu kumshitaki. Lakini Yesu akainama akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji alijiinua akawaambia. Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamira zao; wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata mwisho wao; akabaki Yesu peke yake na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akijiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende tena. Basi

Page 72: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

72 Ukombozi wa Milele

Yesu akawaambia tena, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu yeye anifuataye hatakwenda gizani, kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”

Ni dhambi ngapi Yesu alizifuta?

Dhambi zote za Ulimwengu.

Yesu ametupatia Ukombozi wa milele.

Hakuna awae yote duniani hapa atakaye achwa kukombolewa ikiwa atamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi. Alitukomboa sisi sote. Ikiwa yupo mwenye kuteseka na dhambi leo hii, ni kwa kuwa tu mtu huyo hajaelewa kwamba Yesu alimkomboa kutoka dhambini kupitia ubatizo na kusulubiwa kwake.

Sote yatupasa kuelewa na kuamini juu ya

siri ya wokovu. Yesu alizibeba dhambi zetu zote katika ule ubatizo wake na kubeba hukumu ya dhambi hizo kwa kufa msalabani.

Unapaswa kuamini wokovu utokanao na maji na kwa Roho; ukombozi wa milele kwa dhambi zote. Unapaswa kuamini upendo huu mkuu ulio kufanya kuwa mwenye haki. Amini Yesu alichokufanyia katika wokovu wako pale Mto Yordani na katika Msalaba.

Yesu alitambua juu ya dhambi zetu za sirini pia. Baadhi ya watu huelewa vibaya juu ya dhambi. Hufikiri kwamba baadhi ya dhambi wazitendazo hawatoweza kukombolewa nazo. Yesu alitukomboa na dhambi zote, kila moja ya dhambi.

Hakuna dhambi yeyote katika dunia hii aliyoiacha nyuma. Ikiwa basi alizifuta dhambi zote za dunia, ukweli ni huu kwamba hakuna wenye dhambi tena. Je,

Page 73: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

73 Ukombozi wa Milele

umegundua kuwa Injili imetukomboa kutoka dhambi zetu zote hata zile zijazo mbeleni? Amini juu ya hili na uokolewe na umpe Mungu utukufu wote.

Mwanamke aliyekamatwa katika tendo la uzinzi.

Ni wangapi wenye kuzini Duniani?

Ni watu wote.

Katika Yohana 8, ipo hadithi ya mwanamke aliyekamatwa akizini na tumeona vile Yesu alivyomwokoa. Tungependa kushiriki naye hii neema aliyoipokea. Siyo vibaya tukisema kwamba

kila mtu hufanya zinaa kwa kiwango fulani katika maisha. Kila mmoja hufanya zinaa.

Ikiwa hufikiri hivyo, ni kwa sababu tendo hili hulifanya mara kwa mara hivyo kujiona kwamba hufanyi. Kwa nini? Tunaishi na zinaa katika maisha yetu.

Hebu tizama mwanamke huyu katika Yohana 8, naweza kufananisha ikiwa hakuna au yupo kati yetu ambaye hajawahi kufanya uzinzi. Wote tumekwisha kutenda na kusingizia hatujafanya;

Je, unafikiri nimekosea? La! Sidhani. Tazama kwa uangalifu ndani yake. Kila mtu juu ya uso wa dunia hii ametenda hili. Wametenda hata kwa kuangalia kwa tamaa wanapokuwa wakitembea mitaani, katika mawazo yao na matendo kila wakati na mahala pote.

Hawajielewi wanapotenda hili. Wapo wengi wasiotambua hili hadi siku ya kufa

Page 74: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

74 Ukombozi wa Milele

wanapogundua wana idadi kubwa ya dhambi ya zinaa walizotenda maishani mwao. Si wale tu waliokamatwa. Hata wale walionayo katika mawazo yao na matendo yao sirini. Je, hii si sehemu ya maisha yetu?

Je, umechukizwa nalo? Huu ni ukweli. Tunaficha juu ya hili kwa kuwa ni fedheha kubwa. Ukweli ni kwamba, watu siku hizi hufanya zinaa wakati wote bila kugundua walifanyalo.

Watu hufanya zinaa katika mawazo yao pia. Sisi sote tulioumbwa na Mungu, tuishio hapa duniani bila kujitambua huwa tunatenda uzinzi wa kiroho. Kuabudu miungu wengine ni sawa na uzinzi kiroho kwani Bwana ndiye Mume wa wanadamu wote.

Mwanamke aliyekamatwa katika tendo hili ni mwanadamu, kama sisi sote, na alipokea neema ya Mungu, kama vile sisi tulivyo ipata

katika ukombozi wetu, lakini Mafarisayo walio wanafiki walimweka kati yao wakimzunguka kwa kumnyooshea vidole wakidhani ni wenye haki ya kuhukumu na hata kutaka kumpiga kwa mawe. Walitaka kumkemea na kumhukumu wakidhani wao walikuwa ni safi na hawakuwahi kuzini.

Wakristo walio washirika wenye kujitambua nafsi zao kuwa ni wenye wingi wa dhambi, mara zote hawawezi kuwahukumu wengine mbele za Mungu. Bali hutambua kwamba wao pia ni wenye kutenda uzinzi maishani mwao kote, na hupokea neema ya Mungu ambayo ilitukomboa sote. Ni kwa wale tu wenye kugundua hili ndiyo wenye haki ya kukombolewa mbele ya Mungu.

Page 75: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

75 Ukombozi wa Milele

Ni yupi apokeaye Neema ya Mungu?

Ni yupi apokeaye

Neema ya Mungu?

Wasio na thamani. Je, ni yupi kati ya hawa mwenye kupokea

Neema, anayeishi bila ya kutenda uzinzi kabisa au yule asiye na thamani mwenye kukubali ya kwamba ni mwenye wingi wa dhambi katika uzinzi? Atakayepokea neema ni huyu aliyepokea wingi wa neema ya ukombozi. Ni wale wasioweza, wadhaifu na wasio na msaada hupokea ukombozi. Ndiyo walio juu ya neema yake Mungu.

Wale wenye kufikiri kuwa hawana dhambi itakuwa vigumu kwao kukombolewa wataipokeaje neema ya ukombozi wa Mungu

ikiwa hawana cha kukombolewa ndani yao? Waandishi na Mafarisayo walimburuza

mwanamke aliyefumaniwa katika tendo cha uzinzi kwa Yesu na kumweka kati wakimuuliza, “mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini, nawe wasemaje?” kwa nini walimleta mbele zake kwa kumjaribu yeye? (Yesu)

Wao pia walitenda uzinzi mara nyingi, lakini walijaribu kutaka kuhukumu na kuua kupitia Yesu wakitaka lawama hizi ziwe juu yake.

Yesu alikwishaelewa nini kilichopo akilini mwao na kujua juu ya mwanamke yule. Hivyo akasema “yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe kwanza wa kumtupia jiwe.” Ndipo waandishi na Mafarisayo kwa kuanzia wazee hadi vijana, walipotoka na kumwacha Yesu na yule mwanamke.

Page 76: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

76 Ukombozi wa Milele

Waliondoka walikuwa waandishi na Mafarisayo, viongozi wa dini walikuwa wakitaka kumhukumu mwanamke aliyefumaniwa wakidhani wao siyo wenye dhambi.

Yesu aliutangaza upendo wake duniani. Alikuwa ni Bwana wa Upendo. Yesu aliwalisha watu chakula, alifufua wafu, alimpa uhai mtoto wa mjane, alimfufua Lazaro wa Bethani, aliponya viwete na kutenda miujiza kwa masikini. Alibeba uovu wa wenye dhambi wote na kuwarudishia wokovu.

Yesu anatupenda. Yeye ni mwenye enzi pekee awezaye yote, hali Mafarisayo na Wanasheria walidhani kwamba yeye ni adui kwao. Na ndiyo maana walimleta yule mwanamke mbele yake ili wamjaribu.

Walimuuliza “Mwalimu, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii,

nawe wasemaji?” Walifikiri kwamba angewaambia wampige kwa mawe. Kwa nini? Ikiwa tungetoa hukumu kulingana na kile kilichoandikwa kwenye sheria ya Mungu, kila mmoja wetu aliyefanya uzinzi angelipondwa kwa mawe hadi kufa bila huruma.

Wote walipaswa kupigwa kwa mawe hadi kufa na wote wamehukumiwa kwenda jehanamu. Malipo ya dhambi ni mauti. Ingawa Yesu hakuwaambia wampige mawe. Badala yake alisema “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Kwa nini Mungu alitupa Vipengele 613 vya Sheria?

Ili tuweze kujitambua kuwa ni wenye dhambi.

Page 77: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

77 Ukombozi wa Milele

Sheria huleta hasira ya Mungu. Mungu ni Mtakatifu na yeye mwenyewe ni Sheria. Sheria hii Takatifu ilikuja kwetu katika vipengele 613. Sababu Mungu kutupatia vipengele hivi 613 vya sheria yake ilikuwa ni kutufanya sisi wanadamu kwamba ni wenye wingi wa dhambi; si wakamilifu inatufundisha kwamba tunahitaji sana Neema ya Mungu kutukomboa. Kama tusinge jua hili na kufikiri tu juu ya sheria basi tungepaswa kupigwa kwa mawe hadi kufa kama ilivyo yule mwanamke aliye fumaniwa.

Waandishi na Mafarisayo ambao hawakujua ile kweli ya sheria ya Mungu wangefikiri ya kwamba wangeweza kumpiga kwa mawe mwanamke yule, labda hata sisi tungefanya hivyo. Lakini ni nani atathubutu kurusha jiwe kwa mwanamke huyu asiye na tumaini ikiwa sisi pia ni viumbe waovu mbele

ya Mungu?. Ikiwa yule mwanamke na wengi wetu sisi

tukihukumiwa kwa sheria tu, sisi na mwanamke huyu tungepokea adhabu ya kutisha na kali. Lakini Yesu alituokoa sisi sote wenye dhambi, kutoka kwenye dhambi zetu na kutoka katika ile hukumu ya haki. Sisi na dhambi zetu zote, ikiwa sheria ya Mungu itatumika kwa umakini kila neno, ni nani angesimama hai? Kila mmoja wetu angekwenda motoni.

Lakini waandishi na Mafarisayo walijua sheria tu kama ilivyo andikwa. Ikiwa sheria hii ingetumika kwa haki na kweli kama hukumu ya kweli, hakika wangestahili kifo. Kwa kweli sheria ya Mungu ililetwa ili watu waweze kuelewa dhambi zao ni zipi mbele ya Mungu, ingawa wanateseka kwa kutoelewa ipasavyo na kuitumia visivyo.

Mafarisayo wa leo, kama walivyo wale wa

Page 78: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

78 Ukombozi wa Milele

kwenye Biblia wanaijua sheria kama ilivyo andikwa tu!. Wanapaswa kuelewa neema, hukumu na kweli ya Mungu, kwa kufundishwa juu ya ile Injili ya ukombozi ili waokolewe.

Mafarisoyo walisema, “sheria imetuamuru kuwapiga mawe wanawake namna hii, nawe wasemaje?” Walimuuliza kwa hakika huku wakibeba mawe mikononi mwao. Walifikiri hakika Yesu hangekuwa na lakusema juu yake. Walimsubiri yeye ili wachukue hatua zao.

Ikiwa angetoa hukumu kulingana na sheria, hata yeye wangempiga mawe. Nia yao ilikuwa kuwapiga wote wawili. Ikiwa angesema wasimpige, wangesema kwamba Yesu ameidharau sheria ya Mungu, na wagempiga kwa kosa la kuasi. Ulkuwa ni mpango mbaya.

Lakini Yesu aliinama chini na kuandika

ardhini kwa vidole vyake, na wakaendelea kuhoji, “Wewe wasemaje?” Unaandika nini kwenye aridhi? Hebu tujibu swali letu. Unasamaje?” Walimsumbua kwa maswali.

Na ndipo Yesu aliposimama na kuwaambia kwamba yule asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe. Waliposikia hili walijiona kuhukumiwa nafsi zao na kuondoka mmoja baada mwingine kwa kuanzia yule mkubwa hadi mdogo. Yesu akibaki peke yake na mwanamke akisimama mbele zake.

Page 79: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

79 Ukombozi wa Milele

“Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Kumbukumbu ya dhambi Zetu huwekwa wapi?

Katika vibao vya mioyo yetu Na kwenye kitabu cha

Matendo.

Yesu aliwaambia “yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe,” na kuendelea kuinama akandika aridhini. Baadhi ya wakubwa walianza kuondoka. Mafarisayo walio wazee ambao ndiyo wenye dhambi zaidi na ndiyo wangekuwa wa kwanza. Wako wadogo nao walifuatwa. Na tuseme Yesu angekuwa

amesimama kati yetu na sisi tuwe tumemzunguka huyu mwanamke. Ikiwa Yesu atasema kwetu, yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe kwanza kumtupia jiwe, je,wewe ungefanya nini?

Yesu alikuwa akiandika nini pale chini? Mungu aliyetuumba sisi huandika dhambi zetu katika sehemu mbili tofauti.

Kwanza huandika dhambi katika vibao vya mioyo yetu. “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao na katika pembe za madhabahu zenu” (Yeremia 17:1).

Mungu amezungumza nasi kupitia Yuda, ambaye ni mwakilishi wetu. Dhambi za wanadamu zimechorwa kwa kalamu ya chuma, yenye ncha ya almasi. Zimewekwa kumbukumbu katika vibao vya mioyo yetu. Yesu aliinama na kuandika kwenye ardhi ya

Page 80: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

80 Ukombozi wa Milele

kwamba wanadamu wote ni wenye dhambi. Mungu anajua ya kwamba tunatenda

dhambi na ameziandika dhambi zetu katika vibao vya mioyo yetu. Kwanza kabisa, ameweka kumbukumbu za matendo yetu, dhambi tulizo tenda, kwa kuwa sisi tu wanyonge mbele ya sheria. Kwa jinsi dhambi zetu ziandikwavyo mioyoni mwetu, tunagundua kwamba tu wadhambi tunapolinganisha na sheria kwa kuwa zimehifadhiwa ndani ya mioyo yetu kwa hisia, basi tunaweza kuona kwamba tu wenye dhambi mbele ya Mungu.

Yesu aliinama kwa muda mara ya pili na kuendelea kuandika katika ardhi. Maandiko vile vile yanasema kwamba dhambi zetu zote zimewekwa kumbukumbu katika kitabu cha Matendo mbele ya Mungu (Ufunuo 20:12). Kila jina la mwenye dhambi limehifadhiwa kwa kumbukumbu ndani ya

Kitabu hicho. Na pia imeandikwa katika vibao vya moyo wake. Dhambi zetu zimeandikwa katika kitabu cha Matendo na katika vibao vya mioyo yetu.

Dhambi zimewekwa kumbukumbu katika vibao vya mioyo ya vijana na wazee. Na hii ndiyo maana wale waliomshitaki yule mwanamke hawakuwa na la kusema mbele za Yesu. Wale waliotaka kumpiga yule mwanamke hawakujizuia mbele ya maneno ya Yesu.

Ni lini dhambi zetu zilizowekwa kumbukumbu katika sehemu

hizo mbili hufutwa?

Tunapokubali ukombozi katika maji na katika damu ya Yesu

ndani ya mioyo yetu.

Page 81: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

81 Ukombozi wa Milele

Hivyo unapopokea wokovu wa Yesu, dhambi zako zote katika kitabu cha Matendo zinafutwa na jina lako kuorodheshwa katika kitabu cha Uzima. Wale wote walio na majina katika kitabu cha Uzima watakwenda Mbinguni. Matendo mema, mambo waliyofanya katika ulimwengu huu kwa niaba ya Ufalme wa Mungu na haki zake vimeandikwa pia katika kitabu cha Uzima. Wamekubalika Mbinguni. Wale wote waliokombolewa kutoka dhambini wataingia katika uzima wa milele.

Ikumbukwe kwamba kila dhambi za mtu zimeandikwa katika sehemu kuu mbili, hivyo si rahisi kwa yeyote kumdanganya Mungu. Hakuna ambaye hajatenda dhambi au kuzini katika moyo wake. Watu wote ni wenye dhambi na wapungufu.

Wale wote ambao hawajaukubali ukombozi wa Yesu katika mioyo yao hawana

namna zaidi ya kuteseka kwa dhambi zao. Hawana ushupavu ndani yao humwogopa Mungu na wanadamu wenzao kwa sababu ya dhambi zao. Lakini pindi wanapoikubali Injili ya ukombozi katika maji na kwa Roho ndani ya mioyo yao, dhambi zote zilizo andikwa vibao vya mioyo yao na katika kile kitabu cha matendo hufutwa na kusafishwa. Hukombolewa kutoka katika dhambi zao zote.

Kipo kitabu cha Uzima kule Mbinguni. Majina ya wale walio amini ukombozi katika maji na kwa Roho yamehifadhiwa kwa kumbukumbu ndani yake, hivyo watakwenda Mbinguni. Wataingia Mbinguni si kwa sababu hawakutenda dhambi hapa duniani bali kwa kuwa walikombolewa kutoka katika dhambi zao zote kwa imani juu ya ukombozi wa maji na kwa Roho. Hii ni “sheria ya imani” (Warumi 3:27).

Page 82: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

82 Ukombozi wa Milele

Walio Wakristo, Waandishi na Mafarisayo walikuwa wenye dhambi kama alivyo mwanamke yule aliyefumaniwa.

Ukweli ni kwamba, yawezekana walikuwa wamewahi kutenda dhambi zaidi ya moja na kujiaminisha mbele za watu kwamba wao si wadhambi. Viongozi wa dini walikuwa wezi kwenye vibao vya zamani, wezi wa roho, au kwa maneno mengine wezi wa uzima. Walithubutu kufundisha wengine kwa mamlaka, ingawa wao wenyewe hawakuwa wamekombolewa.

Hakuna awaye yote asiye na dhambi kutokana na maandiko ya sheria. Lakini mtu aweza kuwa mwenye haki si kwa sababu hajatenda dhambi, bali ikiwa amekombolewa na dhambi zake zote. Mtu wa aina hii huwekwa kumbukumbu katika kile kitabu cha Uzima. Jambo muhimu hapa ni ikiwa jina lake limehifadhiwa katika kitabu cha

Uzima au la! Ikiwa mtu hawezi kuishi bila kutenda dhambi katika maisha yake, basi yampasa kukombolewa ili jina lake liwekwe kumbukumbu katika kitabu hicho.

Ikiwa utakubalika kuingia Mbinguni itategemea kama utaamini Injili iliyo ya kweli au la! Kupokea au kutopokea neema ya Mungu hutegemea kukubali kwako wokovu wa Yesu. Nini kilimpata Mwanamke yule aliyefumaniwa? Angeliweza kuangukia magoti na kufunika macho yake kwa kuwa alijua angekufa kwa mawe tu! Labda alikuwa akilia kwa kuogopa na kujutia. Ukweli ni kwamba watu wanapokutana na mauti ndipo wanapo kuwa wenye uaminifu ndani ya nafsi zao.

“Ah, Mungu, ni sawa kwangu kufa! Nakusihi uipokee roho yangu mikononi mwako, na unionee huruma. Nakusihi unionee huruma, Yesu.” Mwanamke huyu

Page 83: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

83 Ukombozi wa Milele

alimsihi Yesu kwa upendo wa ukombozi. “Mungu ukinihukumu, nitahukumiwa, na ikiwa utasema sina dhambi tena basi dhambi zangu zitafutika. Ni hiyari yako.” Labda alinena haya yote. Alikiri kuwa yote aliyaweka mbele za Yesu.

Mwanamke huyu aliyeletwa mbele ya Yesu hakusema, “Nimetenda dhambi ya uzinzi, naomba unisamehe,” bali alisema “Nakusihi, uniokoe na dhambi zangu. Ikiwa utaniokoa, nitaokoka. Ikiwa sivyo nitakwenda motoni. Nahitaji ukombozi wako. Nahitaji upendo wa Mungu na nahitaji huruma yake,” alifunika macho yake na kutubu makosa yake.

Na yesu akumuuliza, “Wako wapi wale washitaki wako?” “Je, hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?” Akajibu “hakuna Bwana.”

Naye Yesu akamwambia “wala mimi

sikuhukumu.” Yesu hakumhukumu kwa sababu alikwisha zibeba dhambi zake zote kwa kupitia ubatizo wake katika ule mto Yordani na tayari alikwisha kombolewa. Hivyo sasa, ni Yesu na wala si yule mwanamke tena aliyepaswa kuhukumiwa kwa dhambi.

Akamwambia, “wala mimi sikuhukumu.”

Je, alihukumiwa Na Yesu?

Hapana.

Mwanamke huyu alibarikiwa na wokovu katika Yesu. Alikombolewa na dhambi zake zote maishani. Bwana wetu Yesu

Page 84: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

84 Ukombozi wa Milele

ametuambia kwamba amekwisha tukomboa na dhambi zetu zote na hivyo sote tu wenye haki.

Anatuambia hili katika Biblia. Alikufa msalabani ili kulipia madhambi yetu ambayo aliyabeba pale katika ubatizo wake mto Yordani. Kwa uwazi anatuambia kwamba ametukomboa sisi wale wenye kuamini ubatizo wake na hukumu ile ya msalaba. Sisi sote tunahitaji maandiko ya Neno la Yesu na kuyashikilia. Na ndipo tutakapo barikiwa na huu ukombozi.

“Mungu, sina urithi mbele zako, sina chochote kilicho chema ndani yangu. Sina la zaidi ya dhambi mbele yako. Lakini namwamini Yesu kuwa ni Bwana wa Ukombozi. Alizichukua dhambi zangu zote katika mto Yordani kwa upatanisho wake pale msalabani. Alizichukuwa dhambi zangu zote kwa ubatizo wa damu yake. Nakuamini

wewe Bwana.” Hivyo ndivyo unavyookoka. Yesu

hatuhukumu. Anatupa haki ya kuwa watoto wa Mungu. Kwa wale tu watakao amini ukombozi katika maji na kwa Roho, amezichukua dhambi zetu zote na kutufanya wenye haki.

Rafiki zangu! Mwanamke yule alikombolewa. Mwanamke aliyefumaniwa alipata baraka ya ukombozi wa Bwana wetu Yesu. Hata sisi leo hii tunaweza kupata baraka ya aina hii. Kwa yeyote mwenye kuzikiri dhambi zake na kumwomba Mungu huruma yake, na kwa yeyote mwenye kuamini ukombozi wa maji na kwa Roho katika Yesu hupokea baraka ya ukombozi kwa Mungu. Wale wenye kukiri uovu wao mbele za Mungu watakombolewa lakini wasiotambua juu ya dhambi zao hawawezi kubarikiwa na ukombozi huu.

Page 85: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

85 Ukombozi wa Milele

Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu (Yohana 1:29). Mwenye dhambi yeyote katika dunia hii aweza kukombolewa ikiwa atamwamini Yesu. Yesu alimwambia mwanamke “wala mimi sikuhukumu.” Alisema hivi kwa sababu, dhambi zake zote alikwisha zibeba katika ubatizo wake. Alichukua dhambi zote kwake, na alihukumiwa badala yetu.

Yatupasa tukombolewe mbele ya Yesu

Lipi ni kuu, Upendo wa Mungu au hukumu ya Mungu?

Upendo wa Mungu.

Mafarisayo wakiwa na mawe mikononi

mwao na wale viongozi wa kidini kwa nyakati hizi, hutafsiri sheria hizi kwa kila neno. Huamini kwamba, kwa kuwa sheria inasema usizini, na afanyaye hilo atapigwa kwa mawe hadi kufa. Hata wao walimkodolea macho kwa kumtamani huku wakiwa na unafiki wa nafsi zao kwamba hawatendi uzinzi kwa wakati huo. Hawawezi kukombolewa wala kuokolewa. Mafarisayo na Waandishi ni watu wa kimwili katika ulimwengu huu wa leo. Hawakuwa wameitwa na Yesu na wasingeweza kuelewa pale aliposema “wala mimi sikuhukumu.”

Ni yule mwanamke pekee aliye fumaniwa aliweza kusikia maneno haya ya kufurahisha na yenye matumaini kwake. Ikiwa nawe ni mkweli mbele zake, waweza pia kubarikiwa kama yeye “Mungu, nimeshindwa, maishani mwangu naendelea kufanya uzinzi. Nimekufa ganzi moyoni kwa kuwa

Page 86: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

86 Ukombozi wa Milele

nimekwisha zoea kufanya hili. Natenda kila siku.”

Tunapoikubali sheria na ukweli ya kuwa sisi tu wadhambi na lazima tufe kwa uaminifu tunapomwendea Mungu kwa kusema “Mungu hivi ndivyo nilivyo; Naomba uniokoe.” Hakika Mungu atakubariki na ukombozi wake.

Upendo wa Yesu, Injili ya maji na kwa Roho ilikwisha ishinda hukumu ya Mungu. “Wala mimi sikuhukumu” Hatuhukumu. Anasema “umekombolewa” Bwana wetu Yesu Kristo ni Mungu wa huruma. Alitukomboa kutoka katika dhambi zote za ulimwengu.

Mungu wetu ni Mungu wa Haki na Mungu wa Upendo! Upendo wa maji na kwa Roho ni mkuu zaidi ya Hukumu yake.

Upendo wake ni mkuu zaidi ya hukumu yake

Kwa nini alitukomboa sisi sote?

Kwa kuwa upendo wake ni Mkuu zaidi ya Hukumu yake.

Ikiwa Mungu angeshurutisha hukumu yake ili kukamilisha haki yake, angelihukumu wale wote wenye dhambi na kuwatupa motoni wote. Lakini kwa kuwa upendo wa Yesu ulituokoa kutoka hukumuni ni mkubwa mno! Mungu alimtuma kwetu mwanawe wa pekee, Yesu. Yesu alibeba dhambi zetu zote na kupokea hukumu ya dhambi hizo mwenyewe kwa niaba yetu. Hivyo, kila amwaminiye Yesu kama ni mwokozi

Page 87: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

87 Ukombozi wa Milele

hufanywa kuwa mwana wa Mungu mwenye haki. Kwa kuwa upendo wake ni mkuu kupita haki yake, ndiyo maana ametukomboa sisi sote.

Tumshukuru Mungu kwani yeye hatuhukumu kwa haki yake. Wakati Yesu alipowaambia Waandishi. Mafarisayo na wafuasi wao “Nenda na mjifunze hii maana yake nini: ‘Nataka rehema, wala si sadaka.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Mathayo 9:13). Wengine wanaweza kuendelea kutoa sadaka ya ng’ombe au mbuzi kwa kuchinja kila siku ili kumtolea Mungu na kuomba, “Mungu nisamehe dhambi zangu kila siku.” Mungu hazihitaji sadaka zetu, bali imani yetu katika ukombozi wa maji na kwa Roho. Anapenda tukombolewe na kuponywa. Anapenda kutupa upendo wake na kuikubali imani yetu. Je, wote mnaona hii? Yesu ametupatia

wokovu ulio kamili. Yesu huchukizwa na dhambi, lakini ana

Upendo mkuu juu ya wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu, alikwisha amua hata kabla ya uumbaji kutufanya kuwa wana kwake, na kuzifuta dhambi zetu kwa ubatizo na kwa damu. Mungu alituumba kwa wakati huo na kutukomboa, kutuvika katika Yesu na kutufanya kuwa watoto wake. Huu ni upendo alio nao juu yetu sisi tulio viumbe wake.

Ikiwa Mungu hutuhukumu kwa sheria yake tu, sisi tulio na dhambi tulipaswa kufa. Lakini alitukomboa kupitia ubatizo na hukumu ile ya Mwana wake Yesu pale msalabani. Je, unaamini hili? Hebu, na tulithibitishe hili katika Agano la Kale.

Page 88: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

88 Ukombozi wa Milele

Haruni aliweka mikono yake juu ya sadaka ya kuachiliwa (Azazeli)

Nani aliyeweka mikono juu ya kichwa cha Mbuzi ili

kuwakilisha dhambi Zote za wana wa Israel?

Kuhani Mkuu. Dhambi zote za ulimwengu zililipwa kwa

Imani kupitia Ibada ya Agano la Kale na kwa ubatizo wa Agano Jipya. Katika Agano la Kale dhambi zote za mwaka mzima za wana wa Israeli zililipiwa kwa kupitia Kuhani Mkuu, ambapo aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Mbuzi aliye hai asiye na doa.

“Ni Haruni ataweka mikono yake miwili

juu ya kichwa cha yule Mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao, naam dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule Mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari” (Walawi 16:21).

Hivi ndivyo walivyofanya upatanisho katika nyakati zile za Agano la Kale. Ili kukombolewa na dhambi za kila siku, ilipaswa kumleta kondoo au Mbuzi asiye na doa mbele ya Hema na kumchinja katika madhabahu. Aliweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka hiyo na ndipo dhambi zake zote ziliwekewa juu ya toleo hilo la dhambi. Mnyama huyu wa kafara alichinjwa na kuhani aliweka damu yake kwenye pembe za madhabahu ya kuteketeza.

Palikuwa na pembe katika kila kingo zikutanazo kuta za madhabahu. Pembe hizi

Page 89: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

89 Ukombozi wa Milele

huwakilisha kitabu cha Matendo ilivyoandikwa katika Ufunuo 20:12. Damu iliyobaki ya yule mnyama wa kafara ilinyunyizwa ardhini pia. Ardhi inawakilisha moyo wa mtu kwa kuwa aliumbwa kutokana na mavumbi. Hivi ndivyo watu walivyopatanishwa kwa dhambi za kila siku.

Ingawa haikuwa rahisi kwao kutoa sadaka hii ya dhambi kila siku, Mungu aliwaruhusu wapatanishwe mara moja kwa mwaka kwa dhambi zao zote za mwaka. Na hii ilifanyika katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, siku ya upatanisho katika siku hiyo, Kuhani Mkuu ambaye ndiye mwakilishi wa Waisraeli wote aliwaleta Mbuzi wawili na kuweka mikono yake juu ya vichwa vyao kuwekea dhambi zote za watu juu yake na kuwatolea kwa Mungu kwa upatanisho wa watu wote wa Israeli.

“Na Haruni ataweka mikono yake miwili

juu ya kichwa cha yule Mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao.”

Mungu alimteua Haruni, ili awe Kuhani Mkuu wa Israeli, mwakilishi. Badala ya kila mmoja kupaswa kuwekea mikono sadaka yake binafsi, kuhani mkuu akiwa mwakilishi wa wote, aliwekea mikono juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai kwa ondoleo la dhambi za watu wote kwa mwaka mzima.

Alizitaja dhambi zote moja hadi nyingine za wana wa Israeli mbele ya Mungu “Ee Mungu, watoto wako Israeli wamekutenda dhambi. Tumeabudu miungu wa sanamu tumevunja vipengele vyote vya sheria yako, tumetaja jina lako bure, tulijiundia sanamu na kuzipenda zaidi yako. Hatukuitukuza Sabato takatifu, hatukuwaheshimu wazazi wetu, tuliua, fanya uzinzi na kuiba… Tulijiingiza katika wivu na magombano.”

Page 90: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

90 Ukombozi wa Milele

Alizitaja dhambi zote “Mungu si mimi wala si wana wa Israeli tulio zishika Amri zako. Ili tukombolewe kutoka dhambi hizi, naweka mikono yangu juu ya kichwa cha mbuzi huyu ili kuzitwika dhambi hizi zote. Hapo Kuhani Mkuu huweka mikono yake yote juu ya kichwa cha sadaka hiyo. Ibada hii au kuwekea mikono maana yake ni kubebesha, kuwekeza au kutwika” (Walawi 1:1-4, 16:20-21).

Ni kwa namna gani upatanisho ulifanywa wakati wa Agano

la Kale? Kwa kuwekea mikono juu ya kichwa

cha sadaka ya dhambi.

Mungu ametoa mpangilio wa kutoa kafara kwa watu wa Israeli ili dhambi hizo

zibebeshwe na kuweza kukombolewa. Alitoa maelekezo ya kwamba sadaka hiyo ya upatanisho lazima iwe safi isiyo na dosari na ife kwa kuchinjwa kwa niaba ya mtoaji, Ukombozi wa kila mtu binafsi mwenye dhambi ulikuwa wa namna hii.

Kwa namna hii basi, katika ile siku ya upatanisho sadaka ya dhambi ilichinjwa na damu yake kuchukuliwa sehemu ya Patakatifu na kunyunyizwa kwenye kiti cha Rehema mara saba. Hivyo, watu wa Israeli walipatanishwa kwa dhambi zao za mwaka katika siku ya kumi ya mwezi wa saba.

Kuhani Mkuu aliingia Patakatifu peke yake kutoa sadaka, hali watu wengine waliobaki walikusanyika nje wakisikiliza sauti ya kengele za dhahabu katika mishipi izungukayo kifuko cha kifuani juu ya joho la Kuhani Mkuu. Kengele za dhahabu ziligonga mara saba damu iliponyunyizwa katika kiti

Page 91: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

91 Ukombozi wa Milele

cha rehema. Ndipo watu hufurahi kwa kuwa dhambi zao zimesamehewa. Sauti ya Kengele za dhahabu inafananishwa na suti ya Injili ya furaha.

Si kweli kwamba Yesu anaupendo na watu wa aina fulani na kuwakomboa wao pekee. Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu mara moja na kwa wakati wote. Dhambi zetu zisinge weza kombolewa kila siku, hivyo zilifutwa zote na kwa mara moja tu!

Katika Agano la Kale, upatanisho ulitolewa kupitia Ibada na damu ya sadaka ya dhambi. Haruni aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi mbele ya watu wote na kuzitaja dhambi zote watu walizotenda kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Alizitwisha dhambi zote kwa yule mbuzi mbele ya watu wote wa Israeli. Je, ni wapi basi dhambi hizo zilikwenda baada ya Kuhani Mkuu kuwekea

mikono sadaka ile ya mnyama? Alibeba yule mbuzi wa sadaka.

Ndipo mbuzi yule aliongozwa katika mikono ya “mtu aliye tayari.” Akiwa amezibeba dhambi zote za watu wa Israeli, alipelekwa jangwani ambako hakuna maji wala nyasi. Mbuzi huyo alitangatanga jangwani kwa jua kali na hatimaye kufa. Alikufa kwa dhambi za watu wa Israeli.

Huu ni upendo wa Mungu, upendo wa ukombozi.Hivi ndivyo ilivyokuwa namna ya upatanisho wenye thamani wa dhambi za siku zote. Lakini tunaishi katika nyakati za Agano Jipya. Imekwisha kuwa karibu miaka 2000 tangu Yesu aje katika dunia yetu. Alikuja na kutimiza ile ahadi aliyowekwa katika Agano la Kale. Alikuja na kutukomboa kwa dhambi zote.

Page 92: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

92 Ukombozi wa Milele

Kutukomboa sote.

Nini maana ya YESU?

Mwokozi, yeye ndiye Atakaye waokoa watu Wake na dhambi zao.

Na tusome Mathayo 1:20-21 “Basi

alipokuwa akifikiri hayo, tazama malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake YESU, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:20-21).

Baba yetu wa Mbinguni aliuazima mwili wa Bikira Mariamu kumtuma Mwana wake kuja duniani ili kusafisha dhambi za watu wa

ulimwengu. Alituma malaika kwake Mariamu na kumueleza “Tazama, na utachukua mimba nawe utamzaa mwana nawe utamwita jina lake YESU.” Hii ina maana mtoto atakaye kuja kupitia Mariamu atakuwa Mwokozi. Yesu Kristo maana yake yeye atakaye wakomboa watu wake, kwa maneno mengine, Mwokozi.

Sasa ni kwa namna gani atatuokoa sisi sote na dhambi zetu? Namna Yesu alivyochukua dhambi zetu ni katika ule ubatizo wake pale mto Yordani. Wakati Yohana Mbatizaji alipombatiza, dhambi zote za dunia alizibeba kwake. Hebu na tusome Mathayo 3:13-17.

“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali

Page 93: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

93 Ukombozi wa Milele

hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye.”

Yesu alikwenda kwa Yohana mbatizaji ili kutukomboa sisi sote kutoka dhambini. Alijitumbukiza kwenye maji na kuinamisha kichwa chake mbele ya Yohana “Yohana nibatize sasa. Ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Kama nilivyo ninataka kubeba dhambi zote za dunia kwa kuwakomboa wenye dhambi na hakika kuzichukua dhambi hizi kwa ubatizo huu. Nibatize sasa. Ruhusa iwe hivyo.”

Hivi ndivyo ilivyopaswa kutimiza haki zote.

Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto Jordan na katika wakati huo, haki zote za Mungu ziletazo ukombozi wetu zilitimizwa.

Na hivi ndivyo Mungu alivyozichukua dhambi zetu zote. Dhambi zote alitwikwa Yesu pia. Je unaelewa juu ya hilo?

Amini katika ukombozi wa ubatizo wa Yesu na kwa Roho na uokolewe.

Ni kwa namna gani Haki zote zilitimizwa?

Kupitia ubatizo wa

Yesu. Mwanzo Mungu aliwaahidi wana wa

Israeli kwamba dhambi zote za ulimwengu zitasafishwa kwa kuwekea mikono kafara ya

Page 94: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

94 Ukombozi wa Milele

sadaka ya dhambi. Hata hivyo kama isivyo rahisi kwa kila mmoja kuweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi kwa binafsi Mungu alimteua Haruni ili awe Kuhani Mkuu ili aweze kumtolea kafara kwa niaba ya watu wote. Na hii, aliweza kutwika juu ya kichwa dhambi zote za mwaka za watu wote kwa ile sadaka ya dhambi kwa mara moja. Hii ilikuwa ni Hekima ya Mungu na nguvu ya ukombozi. Mungu ni mwenye Hekima na wa ajabu.

Alimleta mwana wake Yesu kuukomboa ulimwengu wote. Hivyo sadaka ya dhambi ilikuwa tayari. Sasa, alihitajika mwakilishi wa wanadamu wote, yeye pekee atakayewekea mikono juu ya kichwa cha Yesu (sadaka ya upatanisho) na kutwika dhambi zote za ulimwengu kwake. Mwakilishi huyo alikuwa ni Yohana Mbatizaji. Imeandikwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuma mwakilishi

wa wanadamu kabla ya Yesu. Alikuwa Yohana Mbatizaji, kuhani wa

mwisho wa mwanadamu. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo 11:11 “Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.” Ni mwakilishi pekee wa wanadamu. Alimtuma Yohana kama mwakilishi wa wanadamu wote ili aweze kumbatiza Yesu kwa kumtwika dhambi za dunia.

Ikiwa watu bilioni sita ulimwenguni watakwenda mbele za Yesu na kumwekea mikono ili kumtwika dhambi zao, nini kingetokea katika kichwa chake? Ikiwa zaidi ya watu bilioni sita ulimwenguni wakimwekea mikono Yesu, ingekuwa ni mahala pa ajabu. Wale walio wakereketwa wangeweza kumkandamiza kwa nguvu zaidi

Page 95: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

95 Ukombozi wa Milele

kiasi cha kumng’oa nywele! Hivyo basi katika hili kwa Hekima ya Mungu alimteua Yohana ili awe mwakilishi na kumtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu, mara moja na kwa nyakati zote.

Imeandikwa katika Mathayo 3:13. “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.” Na hii ilikuwa wakati Yesu ana umri wa miaka 30. Alitahiriwa akiwa na umri wa siku 8 baada ya kuzaliwa na kuanzia hapo hapakuwahi kuwa na kumbukumbu za habari zake hadi umri wa miaka 30.

Sababu za Yesu kusubiri kuitimiza miaka hiyo 30 ilikuwa aweze kutimiza umri wa kisheria wa kuwa Kuhani mkuu Mbinguni kulingana na Agano la Kale. Katika Kumbukumbu la Torati, Mungu alimwambia Musa ya kwamba Kuhani Mkuu anapaswa awe kati ya miaka 30 kabla ya kupewa

huduma ya Ukuhani. Yesu alikuwa kuhani wa Mbinguni aliye Mkuu. Je, waamini hili?

Katika Agano Jipya, Injili ya Mathayo 3:13-14 inasema, “Wakati huu Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordan kwa Yohana ili abatizwe lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” Ni nani mwakilishi wa wanadamu? Yohana Mbatizaji. Na ni yupi aliye mwakilishi wa Mbinguni? Yesu Kristo ndiye. Wawakilishi hawa walikutana. Sasa ni yupi aliye juu zaidi? Hakika ni yule wa Mbinguni ndiye aliye Mkuu zaidi.

Hivyo Yohana Mbatizaji, aliyekuwa jasiri kupaza sauti kwa viongozi wa dini kwa wakati huo, “Enyi wazao wa nyoka!” ghafla alinyenyekea mbele za Yesu, “mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”

Katika hatua hii, Yesu alisema “kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza

Page 96: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

96 Ukombozi wa Milele

haki yote.” Yesu alikuja ulimwenguni kuitimiza haki ya Mungu. Na ilitimizwa pale Yohana Mbatizaji alipombatiza.

“Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini, na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka Mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye.”

Hivyo ndivyo ilivyo tokea wakati Yesu alipobatizwa. Milango ya Mbinguni ilifunguka alipobatizwa na Yohana Mbatizaji na kubeba dhambi zote za ulimwengu.

“Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka” (Mathayo 11:12).

Manabii wote na Sheria ya Mungu ulitoa unabii juu ya Yohana Mbatizaji. “Tangu siku

za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu na wenye nguvu wauteka.” Kila mmoja anayeamini ubatizo wa Yesu huingia katika ufalme wa Mbinguni bila pingamizi. “Wala mimi sikuhukumu”

Kwa nini Yesu Alihukumiwa Msalabani?

Kwa sababu alibeba dhambi zetu zote.

Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na

kubeba dhambi za ulimwengu. Na baadaye aliweza kumwambia yule mwanamke aliye fumaniwa “wala mimi sikuhukumu.” Hakumhukumu yule mwanamke kwa sababu

Page 97: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

97 Ukombozi wa Milele

alikwisha zibeba dhambi zote za ulimwengu katika mto Yordani yeye binafsi na si yule mwanamke tena aliye paswa kuhukumiwa kwa dhambi hizo.

Yesu alizifuta dhambi za dunia. Tunaweza kuona ni kwa namna gani ilivyo mtia hofu juu ya maumivu aliyo paswa kuvumilia pale Msalabani, kwa kuwa “mshahara wa dhambi ni mauti.” Alimwomba Mungu mara tatu katika mlima wa mizeituni kuipishia hukumu hiyo mbali kwake. Yesu alikuwa mwenye mwili na damu kama ilivyo sisi sote,na hivyo inaeleweka kwamba alitishika na maumivu. Ilimpasa Yesu atoe damu ili kutimiza hukumu.

Kama ilivyo sadaka ya dhambi katika Agano la kale ilvyo paswa kutoka damu kulipia dhambi pia yeye ilimpasa atolewe sadaka pale Msalabani. Alikwisha zibeba dhambi za ulimwengu tayari na sasa

ilimpasa kuyatoa maisha yake kwa ukombozi. Alifahamu hili kabla kwamba ilimpasa ahukumiwe na Mungu.

Yeye hakuwa na dhambi yoyote moyoni, lakini kama dhambi zote alizibeba katika ubatizo, basi ilimpasa Mungu kumhukumu kama Mwana wake. Hivyo mwanzoni katika hatua ya kwanza hukumu ya Mungu ilitimizwa, hatua ya pili alirejesha Upendo wake kwetu kwa wokovu wetu. Hivyo ilipasa Yesu ahukumiwe msalabani.

“Wala mimi sikulaumu au kukuhukumu.” Dhambi zetu zote, za kudhamiria au kutodhamiria, za kujua au kutojua zilihukumiwa na Mungu.

Hata hivyo Mungu hakutuhukumu sisi, bali Yesu ndiye aliye hukumiwa kwa kubeba dhambi zetu mwenyewe kwa ubatizo wake. Mungu hakutaka kuwahukumu wadhambi kwa sababu ya Upendo wake na huruma.

Page 98: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

98 Ukombozi wa Milele

Ubatizo na damu ya Msalabani ulikuwa ndiyo ukombozi wa upendo kwetu, “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Hivi ndivyo tunavyo uelewa Upendo wake. Yesu hakumhukumu yule mwanamke aliyefumaniwa.

Alijua kuwa yeye ni mwenye dhambi kwa kuwa alifumaniwa. Hakuwa tu na dhambi moyoni, pia alizibeba mwilini. Hakuwa na jinsi ya kuzikana kwa kuwa aliamini kwamba Yesu alikwishabeba dhambi zake zote, aliweza kuokolewa. Nasi, ikiwa tutaamini ukombozi wa Yesu tutaokolewa. Amini hili! Ni kwa faida yetu.

Ni yupi mwenye Baraka zaidi?

Ni yule asiye na dhambi. Watu wote hutenda dhambi. Wote huzini.

Lakini hakuna anayehukumiwa kwa dhambi. Wote tumetenda dhambi, lakini wale wote wenye kuamini ukombozi wa Yesu Kristo hawana dhambi mioyoni mwao. Yule mwenye kuamini wokovu wa Yesu ni mwenye furaha zaidi. Wale waliokombolewa toka dhambi zao zote wamebarikiwa zaidi. Kwa maneno mengine, wamefanywa kuwa haki kupitia Yesu.

Mungu anatuambia kuhusu furaha katika Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao na waliositiriwa dhambi zao.” Wote

Page 99: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

99 Ukombozi wa Milele

tunatenda dhambi hadi kifo. Hatuna sheria na ukamilifu mbele za Mungu. Tunaendelea kutenda dhambi hata pale tunapofahamu sheria sisi ni wadhaifu.

Lakini Mungu anatukomboa kwa ubatizo na kwa damu ya Mwana wake wa pekee na kutuambia, mimi na wewe, kwamba si wadhambi tena na sasa ni wenye haki mbele zake. Anatuambia kwamba sisi ni watoto kwake.

Injili ya maji na kwa Roho ni Injili ya Ukombozi wa milele. Je, unaamini hivyo? Kwa wale wenye kuamini, Mungu huwaita kuwa wenye haki, waliokombolewa ni watoto wake. Ni yupi mwenye furaha duniani? Ni yule mwenye kuamini na amekwisha kukombolewa kwa kuamini Injili ya kweli. Je, umwekwisha kukombolewa?

Je, Yesu alisahau kuzichukua dhambi zako? La, alizichukua dhambi zote kwa

ubatizo. Amini hili. Amini na uwe umekombolewa kwa dhambi zako zote. Na tusome Yohana 1:29.

Kama nisafishavyo na fagio.

Ni dhambi kiasi gani Yesu alizichukua?

Dhambi zote za

Ulmwengu. “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja

kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29).

“Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”

Page 100: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

100 Ukombozi wa Milele

Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi za Ulimwengu kwa Yesu katika Yordani. Siku iliyofuata alishuhudia kwamba Yesu ni Mwana kondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu. Alizibeba kwenye mabega yake dhambi zote za ulimwengu.

Dhambi zote za ulimwengu, hii ina maana dhambi zote walizotenda wanadamu hapa ulimwenguni tokea kuumbwa hadi mwisho wake. Karibu miaka 2000 iliyopita, Yesu alizibeba dhambi za ulimwengu na kutukomboa. Akiwa Mwana kondoo wa Mungu, alizichukua dhambi zetu na kuhukumiwa kwa ajili yetu.

Kila dhambi ya mwanadamu anayotenda ilitwikwa kwake YESU. Alikuwa Mwana Kondoo wa Mungu achukuae dhambi zote za Ulimwengu.

Yesu alikuja ulimwenguni akiwa mtu mnyenyekevu, kama mmoja atakaye okoa

wenye dhambi ulimwenguni. Tunatenda dhambi kwa kuwa sisi ni dhaifu, waovu wapumbavu, na kwa sababu tu wajinga na tusio wakamilifu. Kwa maneno mengine, tunatenda dhambi kwa sababu tumerithi dhambi toka kwa uzao wetu Adamu. Dhambi zote hizi zilisafishwa kwetu na kuwekwa juu ya kichwa cha Yesu kupitia ubatizo wake katika mto Yordani. Aliishia na yote haya katika kifo cha mwili wake Msalabani. Alizikwa lakini Mungu alimfufua toka kwa wafu katika siku ya tatu.

Alikuwa Mwokozi wa wenye dhambi kama mshindi, kama Hakimu ameketi mkono wa kuume kwa Mungu. Haitaji kutukomboa tena na tena. Yote yatupasa kumwamini yeye ili tuokolewe. Uzima wa milele unatusubiri sisi wote wenye kuamini, na uangamizi unawasubiri wale wasio amini. Hakuna chaguo lingine!

Page 101: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

101 Ukombozi wa Milele

Yesu amewakomboa ninyi nyote. Nanyi ni wenye furaha zaidi ya wote ulimwenguni. Hakika yawezekana ukatenda dhambi baadaye kwa sababu ya udhaifu wako,lakini pia hizi nazo alizibeba.

Je, una dhambi iliyo baki moyoni? -Hapana.-

Je, Yesu alizichukua zote? –Ndiyo- Alichukuwa.

Watu wote ni sawa. Hakuna aliye Mtakatifu zaidi ya jirani yake. Lakini wengi wenye unafiki, huamini kwamba wao hawana dhambi,hali ni wenye dhambi pia. Ulimwengu huu ni mahali penye rutuba ya dhambi, kijani kibichi.

Wakati wanawake wanapotaka kutoka matembezini, hujipaka rangi ya mdomo, poda, kutengeneza nywele zao, huvaa nguo maridadi na viatu virefu kisigino… Wanaume nao huenda kwa vinyozi kupunguza nywele

zao, kujisafisha kuvaa shati safi na tai maridadi na kung’arisha viatu vyao.

Lakini wanapo onekana wana wa mfalme kwa nje, ndani yao ni wenye uchafu.

Je, fedha yaweza kumfanya mtu awe mwenye furaha? Afya yaweza kumfanya mwenye furaha? La, Ukombozi wa milele pekee, msamaha wa dhambi zote, ndiyo umfanyao mtu awe mwenye furaha ya kweli. Haijalishi ni kwa kiasi gani mtu anaweza kuonekana kwa nje, mtu huyo ni hovyo kabisa mwenye dhambi moyoni, na huishi maisha ya kuogopa hukumu.

Aliyekombolewa ni mwenye ujasiri kama simba, hata akiwa matambara. Hapana dhambi moyoni mwake. “Nakushukuru Bwana, ulimwokoa mwenye dhambi kama mimi. Ulizifuta dhambi zangu. Najua sikustahili kupokea upendo wako, lakini nakusifu kwa kuniokoa. Nimekombolewa

Page 102: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

102 Ukombozi wa Milele

milele dhambi zangu zote. Utukufu kwako Mungu.”

Mtu aliye kombolewa hakika ni mwenye furaha. Aliyebarikiwa kwa Neema ya Mungu ya ukombozi ni mwenye furaha sana.

Kwa kuwa Yesu “Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi ya Ulimwengu,” alikwisha chukua dhambi zetu zote, hatuna tena dhambi. “Amemaliza” wokovu wetu katika Msalaba. Dhambi zetu zote, zangu na zako zimejumuishwa kwenye dhambi za ulimwengu na hivyo wote tumeokolewa.

Kwa Mapenzi ya Mungu

Je, tuna dhambi moyoni tunapokuwa ndani ya Yesu?

Hapana, hatuna.

Rafiki wapendwa, yule mwanamke

aliyefumaniwa aliamini maneno ya Yesu na aliokolewa. Habari hii imeandikwa kama kumbukumbu katika Biblia kwa kuwa mwanamke huyu alibarikiwa kwa ukombozi ule wa milele. Hata hivyo wale wanafiki, Waandishi na Mafarisayo walitoweka mbele za Yesu.

Ikiwa utamwamini Yesu ni mbingu ikusubiriayo, lakini ukimkimbia utaishia motoni (jehanamu) Ukiamini matendo yake ya haki, ni sawa na mbingu na usipoamini

Page 103: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

103 Ukombozi wa Milele

kazi zake, hii ni jehanamu. Ukombozi si jitahada ya mtu binafsi awaye yote, bali ni kwa wokovu wa Yesu.

Na tusome Waebrania 10:1-10, “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi kwa wakati wote kuwakamilisha wakaribiao, kama ndivyo, Je, Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo lipo kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni asema, dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari. Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hakupendezwa nazo, Ndipo

mliposema, Tazama nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi kuhuzitaka, wala hakupendezwa nazo, (zitolewazo kama ilivyoamuru torati) Ndipo niliposema, Tazama, mmekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo nimepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu!” (Waebrania 10:1-10).

“Kwa mapenzi ya Mungu” Yesu aliyatoa maisha yake kubeba dhambi zetu zote kwa mara moja, na alihukumiwa kwa zote na kufufuka.

Hivyo tumetakaswa. “Mmepata utakaso” (Waebrania 10:10) imeandikwa kama tendo la nyakati iliyopita linaloendelea kwa nyakati iliyopo sasa. Ni kitendo kilichofanyika hapo

Page 104: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

104 Ukombozi wa Milele

zamani na ambacho kinaendelea hadi leo hii. Hii ina maana kwamba ukombozi wetu ulikamilika wote, na hauhitaji kutafutwa tena mmepata utakaso.

“Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya Ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu, tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa” (Waebrania 10:11-14).

Nyinyi nyote mmetakaswa milele. Je, ukitenda dhambi kesho, utakuwa mwenye dhambi tena? Je, Yesu alizichukua dhambi hizo pia? Alizichukua. Alizichukua dhambi hata za nyakati zijazo pia.

“Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia kwa maana baada ya kusema, Hili ni agano nitakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao. Na katika nia zao, nitaziandika ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao, sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya Dhambi” (Waebrania 10:15-18).

Yesu ni Mwokozi kwetu sisi sote, mimi na wewe. Mwamini Yesu alituokoa. Huu ni ukombozi katika Yesu na neema kuu na zawadi toka kwa Mungu mimi na wewe, tuliokombolewa na dhambi zetu zote ndiyo tuliobarikiwa zaidi.

Page 105: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 5

Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Page 106: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

106 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

(Mathayo 3:13-17) “Wakati huo Yesu akaja kutoka

Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akamjibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi alikubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua. Akija juu yake, na tazama sauti kutoka mbinguni

ikisema, Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.”

Je, Kuna yeyote ambaye bado anasumbuka kwa dhambi?

Je, kifungo chetu cha dhambi kilikwisha?

Ndiyo.

Bwana Mungu wetu alizikata pingu za

dhambi kwa watu wote. Wale wote wenye wakati mgumu chini ya dhambi zao ni watumwa wa dhambi hizo; lakini kwa ukombozi wake, Bwana wetu alizikata hakika. Aliziondoa dhambi zetu zote Je, kuna yeyote ambaye bado anasumbuka kwa

Page 107: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

107 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

dhambi? Tunapaswa kuelewa vita yetu dhidi ya

dhambi ilikwisha hatutosumbuka kwa dhambi tena. Kifungo chetu cha dhambi kilikwisha pale Yesu alipotukomboa kwa ubatizo na damu yake. Dhambi zetu ndipo zilipoishia hapo. Mwana wa Mungu alijitoa kwa dhambi zetu. Mungu alizilipia zote kupitia Yesu aliyetuacha huru milele.

Je, unajua ni kwa kiasi gani watu huteseka kwa dhambi zao? Ilianzia kwa Adamu na Hawa Mwanadamu huteseka kwa dhambi ya urithi toka kwa Adamu.

Lakini Mungu wetu aliweka agano lililoandikwa katika kitabu cha Mwanzo 3:15, na agano hili lilikuwa kwamba Yeye atawakomboa wenye dhambi wote. Alisema kwamba watu watakombolewa na dhambi zao kupitia sadaka ya Yesu Kristo kwa maji na kwa Roho. Wakati ulipowadia, Mungu

alimtuma Mkombozi, Yesu, ili aishi kati yetu. Pia aliahidi kumtuma Yohana Mbatizaji

kabla ya Yesu, hakika alitimiza ahadi hii. Marko 1:1-8 Inasema “‘Mwanzo wa Injili

ya Yesu Kristo’ Mwana wa Mungu kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako, atakaye itengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana yaonyesheni mapato yake. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, Nao wa Yerusalemu wote wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kulikoni mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza

Page 108: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

108 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

gidamu ya viatu vyake. Mimi nilibatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”

Yohana Mbatizaji kama Shahidi na Mhamasishaji wa Injili.

Yohana Mbatizaji ni nani?

Kuhani Mkuu wa mwisho na Mwakilishi wa wanadamu wote.

Neno ubatizo kwa Kigiriki “baptizo” maana yake ni “zamisha”, lakini pia lina maana ya “kusafishwa. Wakati Yesu alipobatizwa, haki ya Mungu ilitimizwa “Haki” kwa Kigiriki ni “dikaiosune” na maana yake ni “kuwa

mustahiki wa jambo” na pia “kuendesha jambo kwa kufuata inavyostahiki, uadilifu, uangalifu wa sawa, sahihi, ndivyo, barabara sawasawa.”

Yesu alibatizwa ili aweze kuja kuwa Mwokozi katika hali iliyostahiki. Na hivyo, wale wote wenye kuamini ubatizo wake na msalaba kupokea zawadi ya ukombozi toka kwa Mungu.

Katika Agano Jipya, Yohana Mbatizaji ndiye Kuhani Mkuu wa mwisho wa Agano la Kale. Hebu na tuangalie Mathayo 11:10-11. Maandiko husema kwamba Yohana Mbatizaji ni mwakilishi wa wanadamu na kama Kuhani Mkuu katika kipindi cha Agano Jipya, alimwekea dhambi zote za ulimwengu Yesu. Hivyo kafanya huduma ya ukuhani mkuu kama ule wa kipindi cha Agano la Kale wa Haruni.

Binafsi Yesu alishuhudia juu ya Yohana

Page 109: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

109 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

mwenyewe. Alisema haya katika Mathayo 11:13-14 “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja,” kwa hiyo, Yohana Mbatizaji aliye mbatiza Yesu alikuwa ni wa uzao wa Kuhani Mkuu Haruni na ni kuhani Mkuu wa mwisho. Biblia pia inatushuhudia ya kuwa Yohana alikuwa ni wa uzao wa Haruni katika Agano la kale (Luka 1:5; Mambo ya Nyakati 24:10).

Sasa ni kwa sababu ipi Yohana aliishi nyikani akiwa peke yake, akivalia mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia? Ilikuwa ni kudhihirisha Ukuhani Mkuu. Akiwa mwakilishi wa wanadamu wote, Yohana Mbatizaji hakupaswa kuishi kati ya watu. Hivyo alipaza sauti kwa watu “Enyi wazao wa nyoka, tubuni” na aliwabatiza kwa tunda la toba ili kuwarejesha kwa Yesu

atakayeondoa dhambi zao zote. Juu ya yote, Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi za ulimwengu kwa Yesu kwa ajili ya wokovu alipomwekea mikono juu ya kichwa chake.

Aina mbili za Ubatizo

Kwa nini Yohana Mbatizaji Aliwabatiza watu?

Kuongoza watu katika toba ya Dhambi zao na kuamini ubatizo

wa Yesu kwa wokovu wao. Yohana Mbatizaji aliwabatiza watu na

baadaye Yesu. Huu wa kwanza ni “Ubatizo wa toba” unaowaita wenye dhambi kwa Mungu. Watu wengi waliosikia wito huu wa

Page 110: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

110 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Mungu kupitia Yohana waliziacha sanamu zao na kumrudia.

Ubatizo wa pili ulikuwa ni wa Yesu, ubatizo ulio mbebesha dhambi za Ulimwengu zote. Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kuitimiza haki ya Mungu. Kwa maneno mengine, Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili kuwaokoa watu kwa dhambi zao zote (Mathayo 3:15).

Kwa nini Yohana ambatize Yesu? Ili kufuta dhambi za Ulimwengu, Mungu aliruhusu Yohana kumbebesha Yesu dhambi ili kwa kila mtu atakayemwamini Yesu aweze kuokolewa.

Yohana Mbatizaji alikuwa ni Mtumishi wa Mungu ambaye mpango wake uliwekwa ili kumtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo na kushuhudia juu ya Yesu ili wanadamu wote watubu na kutakaswa dhambi zao kwa kuamini Injili ya Ukombozi.

Hivyo, Yohana ilimpasa kuishi mwenyewe nyikani. Katika kipindi cha Yohana Mbatizaji, watu wa Israeli wote walikuwa waovu na waliooza kinani.

Hivyo Mungu akasema katika Agano la Kale, Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya naye ataigeuza mioyo ya Baba iwalekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

Mbele ya macho ya Mungu, watu wote wa Israeli waliomwabudu Yehova walikuwa waovu. Hakuna aliyekuwa mwenye haki mbele zake. Viongozi wa dini hekaluni, kwa mfano, Makuhani, wanasheria, waandishi wao hasa ndiyo walioza kwa kina zaidi. Waisraeli pamoja na makuhani wao hawakuweza kumtolea Mungu dhabihu iliyo njema kulingana na sheria yake.

Page 111: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

111 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Makuhani waliacha kuwekea mikono na kafara za sadaka za damu ambazo Mungu aliamuru kwa upatanisho wa dhambi. Imeandikwa kwamba Makuhani katika kipindi cha Nabii Malaki waliacha mfumo wa sheria ya utoaji dhabihu, kuwekea mikono na kutoa sadaka ya damu ya mnyama wa kafara.

Kwa hivyo Yohana Mbatizaji hakuweza kukaa nao. Alikwenda nyikani na kupaza sauti huko. Alisema nini?

Imeandikwa katika Marko 1:2-3 ikinukuu maneno ya Nabii Isaya “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakayetengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani itengenezeni njia ya Bwana yanyosheni mapito yake.”

Sauti iliayo nyikani ikiwaambia watu juu ya ubatizo na toba. Nini maana ya “Ubatizo na toba” ambao Biblia inazungumzia? Ni

ubatizo ambao Yohana Mbatizaji aliupigia kelele; ubatizo uliowaita watu kumrudia Yesu ili wakimwamini yeye azichukuaye dhambi zao wataweza kuokolewa. Ubatizo wa Toba uliwaongoza kwenye wokovu.

“Tubuni na kubatizwa. Mwokozi wetu Yesu atabatizwa kwa njia hiyo ili kuzichukua dhambi zetu zote.” Wito wa Yohana Mbatizaji ulikuwa kwamba Yesu atazichukua dhambi za ulimwengu na kuhukumiwa msalabani ili kuokoa watu wote ili waweze kurudishwa kwa upatanisho mbele za Mungu.

“Mimi niliwabatiza kwa maji, bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” Maana yake “kuosha.” Ubatizo wa Yesu katika mto Yordani unatuelezea juu ya Mwana wa Mungu alibatizwa na kubeba dhambi zetu zote ili kutuokoa.

Hivyo yatupasa kuyageuzia mgongo

Page 112: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

112 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

maisha yetu ya dhambi na kumwamini Yesu. Ni Mwana kondoo, azichukuaye dhambi za ulimwengu. Hii ni Injili ya ukombozi ambao Yohana Mbatizaji alishuhudia.

Jukumu la Kuhani Mkuu katika Upatanisho wa Madhambi

Nani aliyetayarisha njia ya wokovu?

Yohana Mbatizaji. Nabii Isaya alitoa unabii “Semeni na Moyo

wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa umepokea kwa mkono wa Bwana adhabu mara dufu kwa dhambi zake zote” (Isaya 40:2).

Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote pasipo kuchagua dhambi za asili, dhambi za wakati huu na hata zile za wakati ujao, zilisafishwa kupitia ubatizo wake. Alitukomboa sisi sote. Yatupasa kuelewa vyema juu ya ukombozi wa Mungu.

Ili kuokolewa na dhambi zetu, yatupaswa kuamini injili isemayo kwamba, Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote kwa kupitia njia ya ubatizo.

Hatupaswi kuelewa vibaya ya kwamba “ikiwa Mungu ni upendo, tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni kwa kumwamini Yesu tu hata kama tunazo dhambi mioyoni mwetu.”

Ili kukombolewa na dhambi zako zote, yakupasa kuamini ubatizo wake, ambao kupitia Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi za ulimwengu na pia kuamini Msalaba. Ni kwa njia ya “Maji” Yohana

Page 113: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

113 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote za wanadamu.

Jambo la awali Mungu alilofanya katika kutuokoa lilikuwa ni kumtuma Yohana ulimwenguni. Akiwa mjumbe wa Mungu, Yohana Mbatizaji alitumwa kama balozi wa Mfalme, aliye mtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo. Alihudumu katika nafasi ya ukuhani mkuu zaidi ya wanadamu wote.

Mungu alisema yakwamba atamtuma mjumbe wake, Yohana Mbatizaji kwetu.

“Namtuma mjumbe mbele ya uso wako” Mbele ya uso maana yake ni kabla ya Yesu. Kwa nini Mungu alimtuma Yohana kabla ya Yesu? Ili kuzitwika dhambi zote za dunia juu ya Yesu mwana wa Mungu kwa ubatizo. “atakayeitengenezea njia yako” Na hii ndiyo maana halisi ya ujumbe huu.

Ni nani yule aliyetayarisha njia ili

tukombolewe na kwenda Mbinguni? Yohana Mbatizaji. “Mbele ya” huyu ni Yesu, na “namtuma” huyu ni Mungu mwenyewe. Hivyo mwenyewe. Hivyo anaposema “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako,” maana yake nini?

Ni nani anayepaswa kutayarisha njia yetu ya kwenda Mbinguni? Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zetu zote kwa Yesu ili tuweze kuamini kwamba alizisafisha zote kwa kazi ile ya ubatizo wa Yesu Kristo. Ni Yesu na Yohana ndiyo waliofanikisha yote haya kwetu ili tuweze kuamini ile kweli na kukombolewa.

Wokovu wetu hutegemea nini? Hutegemea ikiwa kwamba tunaamini matendo haki ya Yesu, Mwana wa Mungu na ukweli kwamba mjumbe wa Mungu Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zote za

Page 114: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

114 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

ulimwengu juu ya Yesu. Wote yatupasa kuielewa Injili ya msamaha wa dhambi. Mungu Baba alimtuma mjumbe wake awali, ambaye yeye angembatiza Mwana wake, na kumfanya kuwa mwakilishi wa wanadamu. Kwa maana hii alikamilisha ile kazi ya ukombozi wetu.

Mungu alimtuma mtumishi wake Yohana Mbatizaji ili ambatize mwana wake ili atayarishe njia ya wokovu kwa wale watakao mwamini Yesu. Na hii ndiyo sababu Yohana kumbatiza Yesu. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji ulikuwa ni kuitimiza kazi ya ukombozi wa Mungu, ambapo dhambi zote za wanadamu alitwikwa Yesu ili wote wamwaminio waweze kuingia mbinguni.

Hata zile dhambi tutakazotenda mbeleni zilitwikwa kwa Yesu kupitia ubatizo huu. Yesu na Yohana Mbatizaji kwa pamoja

walihusika kutayarisha njia ya kwenda Mbinguni kwetu. Kwa njia hii, Mungu alitufunulia siri ya ukombozi kupitia Yohana Mbatizaji.

Akiwa ni mwakilishi wa wanadamu, Yohana alimbatiza Yesu ili tuweze kuamini ukombozi wetu na kwenda Mbinguni. Alimtwika Yesu dhambi zote kupitia ubatizo. Hii ni habari njema ya kufurahisha juu ya ukombozi wetu.

Kwa nini Yohana Mbatizaji alizaliwa?

Kupitia nani tunaweza Kumwamini Yesu?

Yohana Mbatizaji.

Page 115: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

115 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Katika Malaki 3:1 imeandikwa “Angalieni namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu” Yakupasa usome Biblia kwa makini. Kwa nini Mungu alimtuma mjumbe mbele ya Yesu? Kwa nini Yohana alizaliwa miezi 6 kabla ya Yesu?

Yatupasa kuielewa Biblia ina maana gani? Agano la Kale inaelezea jukumu la Kuhani Mkuu Haruni. Haruni alikuwa ni kaka mkuu kwa Musa Mungu alimpaka mafuta (alimsimika) yeye na watoto wake kuwa makuhani. Walawi wengine walifanya kazi chini yake, kumletea vyombo vilivyoteuliwa, kuchanganya siagi ya mkate na mengineyo, wakati watoto wa Haruni wakitoa dhabihu ndani ya madhabahu takatifu.

Watoto wa Haruni walipakwa mafuta katika kufanya kazi kwa usawa kati yao, lakini katika siku ya Upatanisho, siku ya kumi ya mwezi wa saba; Kuhani Mkuu pekee

ndiye aliyeruhusiwa kutoa dhabihu ya upatanisho wa dhambi za mwaka mzima kwa niaba ya watu wake.

Katika Luka 1:5 ipo habari ya uzao wa Yohana Mbatizaji. Yatupasa kwa makini kuelewa ujumbe wa Mungu ili tumwelewe Yesu, sawa sawa. Huwa tunajaribu kufikiri mengi sana juu ya Yesu lakini tunapuuzia zaidi juu ya Yohana Mbatizaji, ambaye alikuja kabla ya Yesu. Ningependa kwa hili nijaribu kukuelewesha.

“Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakayeitengeneza njia yako.” (Marko 1:1-2) Injili ya Mbinguni nyakati zote huanza kwa Yohana Mbatizaji.

Tunapojifunza kwa ukamilifu juu ya Yohana Mbatizaji ndipo tunapoelewa kwa uwazi na kuamini Injili ya ukombozi wa

Page 116: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

116 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Yesu. Ni sawa na kuwasikiliza mabalozi tuliowatuma duniani pote ili tuweze kuelewa juu ya hali ya mataifa yote. Tunapofahamu juu ya Yohana Mbatizaji, tunaweza kuelewa vizuri zaidi juu ya ukombozi wa Mungu.

Ni kwa namna gani ni masikitiko makubwa kwa wakristo walio wengi katika nyakati hizi hawajaona umuhimu wa Yohana. Mungu hakumtuma Yohana Mbatizaji kwa sababu alikuwa amechoka na hakua na la kufanya zaidi ya kumtuma. Injili zote katika Agano Jipya zimezungumzia juu ya Yohana Mbatizaji kabla ya kuzungumzia ukombozi wa Yesu.

Yakushangaza, wainjilisti wengi nyakati hizi humpuuza kabisa na kuwaambia watu wamwamini Yesu tu inatosha na wataokoka. Ukweli ni kwamba, huwaongoza watu kuendelea kuwa wenye dhambi maishani mwao pote na kuishia motoni. Ikiwa

Wakristo wote watamwamini Yesu tu bila kuelewa jukumu la Yohana Mbatizaji, Ukristo utakuwa na kasoro na kuwa kama dini nyingine za duniani. Utakombolewa vipi kwa dhambi zako ikiwa hutaki kuelewa ukweli? Si rahisi!

Injili ya ukombozi sivyo ufikiriavyo wewe kwa wepesi na urahisi huo. Kwani watu wengi hudhani ukombozi huwa umewekwa kwa imani katika Msalaba kwa kuwa Yesu alikufa juu yake kwa ajili yetu. Ikiwa utaamini hilo tu katika kusulubiwa kwake bila ya kuelewa kweli yote juu ya kutwikwa kwa dhambi, hakika imani aina hii haitakupeleka katika ukombozi ulio kamili bila kujali imani yako ni imara vipi.

Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji ili kuufanya ulimwengu kutambua juu ya ukombozi utakaokwenda kubeba dhambi zote za dunia. Hii ni pale tu tutakapojua

Page 117: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

117 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

ukweli wote ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, aliyezichukua dhambi zetu zote.

Yohana Mbatizaji ndiye atuelezaye ukweli juu ya ukombozi. Anatuelezea ni kwa vipi alikuja kushuhudia juu ya Yesu kuwa ni Mungu na Nuru ya ukweli. Kwa uwazi yeye mwenyewe alikataa kuwa ndiye huo mwanga, bali ni mshuhudiaji wa mwanga. Alishuhudia katika Yohana 1 kuwa yeye amekuja kutayarisha Injili ya ukombozi kwa kumbatiza Yesu Kristo.

Kama tusingekuwa na ushuhuda juu ya ukombozi kupitia Yohana Mbatizaji tungeamini vipi juu ya Yesu? Hatukuwahi kumwona Yesu, na tumetoka katika tamaduni na dini mbalimbali, ingewezekanaje kuamini Yehova kuwa ndiye Mungu wetu.

Kuwa na dini mbalimbali duniani pote, ingewezekanaje kumjua Yesu Kristo?

Tungefahamu vipi kuwa Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu, aliyetukomboa kwa kuchukua dhambi za ulimwengu juu yake?

Yatupasa kuangalia ndani ya Agano la Kale na kutafuta maandiko juu ukombozi tokea mwanzo kujua kwamba Yesu ni Mwokozi. Yatubidi kupata ufafahamu sahihi ili kuwa na imani iliyo ya kweli. Hakika hutoweza chochote bila kuwa na ufahamu wa kweli. Ili uweze kumwamini Yesu na uokolewe, itakubidi kujua Injili ya ukombozi ambayo Yohana Mbatizaji aliishuhudia na nafasi yake katika hilo. Ili kuweza kuwa na imani iliyokamilika katika Kristo yatupasa kufahamu ukweli juu ya ukombozi.

Hivyo, kama Yesu alivyo sema “na utajua ile kweli na itakuacha huru” yatupasa kuelewa kweli ya ukombozi wa Yesu.

Page 118: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

118 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Uthibitisho wa Biblia.

Katika kipengele kipi Injili imeanzia?

Katika ujio wa

Yohana Mbatizaji.

Hebu na tuendelee na ugunduzi wa ukweli wa ukombozi katika Biblia. Na tuweke wazi ni juu ya hizi Injili nne zinazungumzia juu ya Yohana Mbatizaji, alikuwa ni nani, na ni kwa nini aliitwa “mwakilishi wa wanadamu” au “kuhani mkuu wa mwisho” kwa namna gani dhambi za ulimwengu alitwikwa Yesu kupitia yeye, na endapo kama Yesu alizichukua dhambi zetu zote au la.

Yatupasa kuwa makini ili hakika Injili zote nne zianzie na Yohana Mbatizaji. Yohana 1:6

inaongelea juu ya moja ya ukweli ulio muhimu katika Injili. Inatuelezea juu ya nani aliyefanya kazi ya kutwikwa dhambi zote za ulimwengu kwa Yesu “Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Hivyo alikuja kushuhudia ile nuru wote wapate kuamini kwa yeye” (Yohana 1:6-7).

Inasema “wote wapate kuamini kwa yeye” na ndiyo maana “alikuja kushuhudia ile nuru” Nuru ni Yesu Kristo. Ina maana kwamba Yohana alishuhudia juu ya Kristo ili wote waweze kumwamini kupitia yeye. Na hebu tuangalie kwa karibu katika Mathayo sura ya 3.

Katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe, lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu

Page 119: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

119 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

akamwambia, kubali hivi sasa kwani ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote. Basi akamkubali Naye Yesu alipokwisha kubatizwa akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama ua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, ‘Huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye” (Mathayo 3:13-17)

Kwa nini yatupasa kuelewa juu ya uzao wa Yohana?

Kwa sababu Biblia inatueleza

juu ya Yohana kuwa ni Kuhani Mkuu wa wanadamu.

Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili

kukamilisha msamaha wa dhambi zote za

Ulimwengu. Ubatizo Yesu alioupata kutoka kwa Yohana ulikuwa na umuhimu mkubwa katika tukio la wokovu wetu.

Na ili uweze kuelewa na kuamini ukweli wote kwa ujumla na kwa undani zaidi, yatupasa kwa karibu kujifunza juu ya Yohana Mbatizaji kwanza.

Katika Luka 1:1-14 “Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyohimizwa katikati yetu kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu upate kujua hakika ya mambo yale yaliyofundishwa. Zamani za Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na Kuhani mmoja jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya na mkewe

Page 120: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

120 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

alikuwa mmoja wapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Basi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia . Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule Malaika akamwambia, usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikia na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na

jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.”

Hapa, Luka mwanafunzi wa Yesu, anatueleza kwa undani juu ya uzao wa Yohana. Luka, mwanafunzi wa Yesu ameelezea uzao wa Yohana. Toka mwanzo Luka alimhubiria Injili mtu aitwaye Theofilo ambaye ni kutoka utamaduni tofauti naye ambaye hakufahamu juu ya Bwana.

Na ili kumfundisha juu ya Yesu mwokozi wa wenye dhambi, Luka aliona umuhimu wa kuelezea kizazi cha Yohana Mbatizaji kwa undani. Nasi kama watu wa Mataifa toka jamii tofauti, hatuwezi kuelewa wokovu wa Yesu ikiwa hatutaelezewa kwa umuhimu hatua kwa hatua. Hebu tuangalie undani huu ni upi.

Katika Luka 1:5-9 inafafanua “zamani za Herode, mfalme wa Wayahudi palikuwa na

Page 121: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

121 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Basi ikawa walipokuwa wakifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, kama ilivyo desturi ya ukuhani, kura ikamwangukia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.”

Hapa jambo la ghafla lilimtokea Zakaria wakati akimtumikia Mungu kulingana na desturi ya ukuhani. Luka anashuhudia wazi kwamba Zakaria alikuwa wa uzao wa Haruni. Na ni katika kundi lipi akitokea? Hii ndiyo muhimu zaidi.

Alieleza “Basi ikawa alipokuwa akifanya

kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu.” Tunaweza kuona kwamba Luka alimfahamu Zakaria vizuri zaidi kwa kuelezea Injili ya ukombozi kwa kumtaja yeye na mke wake Eliabeti.

Yohana Mbatizaji alizaliwa kwa Zakaria na mkewe Elizabethi aliyekuwa bintiye Haruni. Sasa, na tuangalie uzao wa Zakaria, baba yake Yohana.

Ukoo wa Yohana Mbatizaji.

Yohana Mbatizaji alikuwa wa uzao wa nani?

Haruni, Kuhani Mkuu.

Ili kuelewa ukoo wa Yohana Mbatizaji yatupasa kusoma katika kitabu cha Agano la

Page 122: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

122 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Kale 1 Nyakati 24:1-19. “Na zamu za wana wa Haruni ni hizi.

Wana wa Haruni; Nadabu na Abihu, na Eleazari na Ithamari. Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya Ukuhani. Akawagawanya Daudi na Sadoke wa wana wa Eleazari na Ahimeleki wa wana wa Ithamani katika utumishi wa kadiri ya usimamizi wao. Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari; kuliko wana wa Ithamari wakagawanyika hivi, wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wana wa Ithamari sawasawa na mbari za baba zao, wane. Ndivyo walivyogawanyika kwa kura wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu wana wa Eleazari na wana wa Ithamarii pia. Naye

Shemaya, wana wa Nethaneli, mwandishi aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme na mbele ya wakuu na Sadoki kuhani, na Ahimeleki mwana wa Abiathari na wakuu wa mbari za baba za Makuhani, na za Walawi ikatwaliwa ya Eliazari mbari moja ya baba na moja ikatwaliwa ya Ithamari. Kura ya kwanza, ikamtokea Yehoiaribu na ya pili Yedaya; ya tatu Harimu ya nne Seorimu ya tano Malkia ya sita Miyamini ya saba Hakosi ya nane Abia ya kenda Yeshua ya kumi Shekania ya kumi na moja Eliashibu ya kumi na mbili Yakimu ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu; ya kumi na tano Bilga ya kumi na sita Imeri ya kumi na saba Hezuri, ya kumi na nane Hapisesi, ya kumi na kenda Pethahia ya Ishirini Ezekieli, ya ishirini na moja Yakini ya Ishirini na mbili Gamuli, ya ishirini na tatu Delaya ya Ishirini na nne Maazi. Huu ndio usimamizi wao

Page 123: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

123 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

katika huduma yao, waingie nyumabini mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao kwa mkono wa Hruni kama Bwana Mungu wa Israeli alivyomwamuru.”

Na tusome mstari wa 10 tena “ya saba Hokoso ya nane Abia” Katika siku za Mfalme Daudi palikuwapo na idadi ya Makuhani, hivyo palikuwa na hitaji la kuweka taratibu ya mpango wa huduma. Hivyo Daudi alipiga kura kwa kila mtoto wa Haruni ili dhabihu ziweze kutolewa katika mpangilio (kama wote mjuavyo, Haruni alikuwa kaka yake mkubwa Musa. Mungu alimchagua Musa kama wakala, na Haruni kuwa Kuhani Mkuu wa Hema Takatifu mbele ya watu wa Israeli).

Walawi wote walikuwa chini ya Haruni na Makuhani, watoto wake wa kiume, ili kusimamia dhabihu zote mbele ya Mungu. Kabla Daudi hajapiga kura, Makuhani

waliokuwa uzao wa Haruni, iliwapasa kupiga kura kila wakati na ilileta kutoelewana.

Hivyo, Daudi aliandaa mpangilio kwa kuweka kila kundi katika mpangilio. Palikuwa na makundi 24 kwa mpangilio kuanzia wajukuu wa Haruni na wanane alikuwa Abiya. Ilisemekana “palikuwa na Kuhani mmoja, jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.” Hivyo Zakaria alikuwa ni Kuhani wa kundi la Abiya na wote wawili walikuwa uzao wa Haruni Kuhani Mkuu.

Alikuwa ni Zakaria, Kuhani wa kundi la Abiya ambaye alikuwa Baba yake Yohana Mbatizaji. Kutokana na Biblia tunaelewa ya kwamba walikuwa wakioana kati ya familia za kikuhani.

Hivyo Yakobo alichukua mke kwa mjomba wake kwa upande wa mama yake. Kwa ufafanuzi huu wa ukoo hii ndiyo misingi muhimu. Inasema “palikuwa na Kuhani

Page 124: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

124 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

mmoja, jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.”

Hivyo, alikuwa bila shaka uzao wa Haruni. Zakaria alikuwa ni nani? Baba yake Yohana Mbatizaji. Huu ni ukweli muhimu kuelezea ukombozi wa Yesu na huduma ya Yohana Mbatizaji na kumtwika Yesu dhambi za ulimwengu.

Ni watoto wa kiume wa Haruni pekee ndio Watahudumu kama Makuhani.

Ni nani aliyeruhusiwa kuhudumia kama kuhani katika

kipindi cha Agano la kale?

Haruni na katika aliowachagua kizazi chake.

Hivyo, ni wapi katika Biblia inasisitiza kwamba watoto wa kiume wa Haruni walipaswa kuhudumia wakiwa Makuhani? Hebu tupaangalie.

Katika Hesabu 20:22-29. “Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima wakafikilia mlima wa Hori. Bwana akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia Haruni alikusanywa awe pamoja na watu wake kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu niliasi kinyume cha neno la langu hapo penye maji ya Meriba. Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori umvue Haruni mavazi yake ukamvike Eleazari mwanawe mavazi yako; kasha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. Musa akafanya kama Bwana alivyomwagiza; wakakwea katika

Page 125: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

125 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote. Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake akamvika mwanawe Elezari mavazi yake, hayo. Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani. Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana nyumba yote ya Israeli ikamwombolea.”

Katika kitabu cha kutoka, sheria ya Mungu iliandikwa kwamba watoto wa kiume wa Haruni, Kuhani Mkuu ndio watakao shika wadhifa wa Ukuhani, na mmoja kati yao atakayechaguliwa ndiye atakaye chukua nafasi ya ukuhani mkuu kama ilivyokuwa kwa Baba yake kama wote wakifikia umri wa miaka 30.

Kutoka 28:1-5 “Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye miongoni mwa wana wa Israeli, ili

anitumikie katika kazi ya ukuhani, Haruni na Nadabu, na Abihu na Eleazari na Ithamani, wana wa Haruni Nawe utamtamfanyia Haruni ndugu yako mavazi matakatifu kwa utukufu na kwa uzuri. Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani. Na mavazi watakayoyafanya ni haya; Kifuo cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urimbo; na kilemba na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo na wanawe mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau na ya rangi nyekundu na nguo ya kitani nzuri.”

Mungu alimwelekeza Haruni kaka yake Musa kwa uwazi wote juu ya ukuhani.

Page 126: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

126 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Ukuhani haukuwa wazi kwa yeyote yule. Mungu alimwagiza Musa kumtakasa Haruni kama Kuhani Mkuu na kumtengenezea vazi rasmi kwa ajili yake kulingana na maagizo yake. Yatupasa kutosahau maagizo ya Mungu.

Pia katika kitabu cha Kutoka 29:1-9 “Nawe uwafanyie jambo hili ili kuwatakasa, wapate kunitumikia mimi katika kazi ya Ukuhani; twaa ng’ombe mmoja mume kijana na kondoo waume wawili walio wakamilifu na mkate usiotiwa chachu, yaliyokandwa kwa mafuta, na kaki zisizotiwa chachu zilizotiwa mafuta; utazifanya za unga mzuri mwembamba wa ngano. Nawe vitie vyote katika kikapu, na uvilete ndani ya kikapu, pamoja na hiyo ng’ombe na hao kondoo wa waume wawili. Kisha mlete Haruni na wanawe hata mlangoni pa hema ya kukutania ukawaoshe kwa maji. Kisha twaa

hayo mavazi ya kumtwika Haruni itie kanzu, na joho ya naivera, na kifuko cha kifuani na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba. Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kumiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.”

Nawe uwakaze mshipi, Haruni na wanawe na kuwavika kofia…. nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu…. Mungu alisisitiza kwamba Haruni na wanawe walipaswa kutakaswa kwa kuhudumia katika ukuhani milele.

Page 127: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

127 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Aliposisitiza kuhusu “umilele” ina maana ukuhani uliendelea kufanya kazi hata kipindi cha kuja kwa Yesu duniani.

Luka anaelezea kwa undani kwamba Zakaria alikuwa wakutoka katika kizazi cha Haruni Kuhani Mkuu. Zakaria alipokuwa akihudumu kama Kuhani wa zamu mbele za Mungu katika Hekalu la Bwana, Malaika alimtokea na kumwambia sala zake zilifika mbele za Mungu na Elisabeti mkewe atapata mtoto wa kiume.

Zakaria hakuweza kuamini, na alisema “Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi?” Kwa sababu ya shaka lake, Mungu alimfanya kuwa bubu kwa muda ili kumwonyesha ya kwamba maneno yale yalikuwa ni kweli.

Kwa wakati muafaka, mkewe alipata mimba na baadaye Bikira Mariamu naye akapata mimba. Matukio yote mawili

yalitayarishwa kwa kazi ya wokovu wa Mungu. Ili kuwaokoa wanadamu waliopotoka, ilimbidi amtume mtumishi wake Yohana Mbatizaji na Mwana wake wa pekee Yesu duniani.

Hivyo, Mungu aliruhusu Mwana wake abatizwe na Yohana ili kumtwika dhambi zote za ulimwengu ili wale wote watakaomwamini yeye wataokolewa.

Uweza Pekee wa Mungu.

Mungu alimtayarisha nani Kabla ya Yesu kwa ajili ya kazi ya Ukombozi?

Yohana Mbatizaji.

Page 128: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

128 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Yesu Kristo alikuwa ni Mwokozi wa wanadamu aliyezaliwa katika mwili na mwanamwali Mariamu. Mariamu alichumbiwa na Yusufu mzao wa Yuda ilimbidi Yesu azaliwe kupitia uzao wa Yuda ili kutimiza Agano la Mungu, kama ilivyo Yohana Mbatizaji ilivyompasa kuzaliwa kutoka nyumba ya Haruni, Kuhani Mkuu.

Mungu aliwatayarisha wote wawili kuzaliwa katika ulimwengu katika mpangilio huo, Yohana kabla ya Yesu. Yohana alizaliwa ili aweze kuja kumbatiza Yesu na kumtwika dhambi zote za dunia kwake. Mzawa wa Kuhani Mkuu alitoa sadaka ya upatanisho ili kutimiza Agano la Mungu alilofanya katika Agano la Kale; hii ni Injili ya ukombozi wa Yesu ambayo ilipaswa kuchukuliwa kwa usahihi ili watu wote waweze kukombolewa.

Katika kitabu cha Kutoka, Mungu aliwapa Israeli sheria yake na Maagano; sheria ya

Mungu na kanuni ya matoleo ya dhabihu katika madhabahu na pia kwa undani juu ya makuhani, maelezo juu ya dhabihu na jinsi ya kurithisha ukuhani kwa watoto wa kiume wa makuhani. Mungu alimweka Haruni pamoja na uzao wake kuwa makuhani wa kudumu milele.

Hivyo wale wote walio uzao wake waliweza, kutoa dhabihu na Makuhani wakuu walipatikana kutoka katika nyumba ya Haruni tu. Je, umeona kwa nini hii ilikuwa namna hii?

Kati ya walio wengi katika uzao wa Haruni, Mungu alimchagua kuhani fulani aitwaye Zakaria na mkewe Elisabeti. Alisema “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Wakati Mungu alipomwambia Zakaria kwamba atamwezesha Elisabeti kuwa na mtoto na angemwita jina lake Yohana, alipatwa na mshangao sana na

Page 129: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

129 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

kuwa bubu kwa amri ya Mungu hadi pale mtoto yule mume alipopewa jina.

Hii ndivyo ilivyo, mtoto mume alizaliwa katika nyumba yake. Na ilipowadia muda wa kumpa jina kulingana na desturi za Israeli, jina lake lilipaswa aitwe kama la baba yake au moja kati ya jamaa ya ukoo.

“Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye. Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu akasema la sivyo; bali ataitwa Yohana. Wakamwambia hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo. Wakamwashiria babaye wajue, akaandika ya kwamba jina lake ni Yohana wakastaajabu wote. Papo hapo kinywa chake

kikafunguliwa na ulimi wake pia akaanza kunena akimsifu Mungu. Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima ya Uyahudi. Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye” (Luka 1:57-66).

Zakaria alikuwa bado ni bubu kabla ya mtoto wake kuzaliwa. Ilipofikia wakati wa kumpa jina mtoto wake, jamaa zake walipendekeza mtoto huyo aitwe Zakaria. Lakini mama yake alimwita Yohana. Katika hili, ndugu walisema ya kwamba hapakuwa na yeyote katika ukoo wao mwenye jina hilo na hivyo ingekuwa vyema angeitwa jina la baba yake.

Wakati Elisabeti akisisitiza kumpa jina hilo, ndugu walimwendea Zakaria na kumuuliza

Page 130: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

130 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

aitwe jina gani mtoto yule. Kwa kuwa hakuweza kuongea, walimwomba kuandika kwa mkono wake katika kibao, na aliandika jina “Yohana.” Ndugu wote walishangaa kwa namna hii ya upatikanaji wa jina.

Lakini baada ya kutoa jina hili, mdomo wa Zakaria ulifunguka mara. Alimsifu Mungu na alijazwa na Roho Mtakatifu kwa kutoa unabii.

Hivi ndivyo Luka anatueleza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji katika nyumba ya Zakaria “palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.” Kwa uweza pekee wa Mungu, Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu alizaliwa kutoka kwa Zakaria mzao wa Haruni.

Kupitia Yohana Mbatizaji na Yesu Kristo, ilimlazimu Mungu kukamilisha ukombozi wa wanadamu. Tumekombolewa dhambi zetu zote kwa kuamini kazi ya ukombozi,

iliyofanywa kupitia Yohana na Yesu Kristo.

Ubatizo wa Yesu.

Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana?

Ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu.

Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba,

Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu na alichukua dhambi zetu zote Alikuwa ni Yohana Mbatizaji mtumishi wa Mungu aliyetumwa kubeba ushuhuda wa wokovu wa Mungu. Haina maana kuwa Mungu hatuelezi mwenyewe ya kuwa yeye ni Mwokozi. Mungu hufanya kazi kupitia

Page 131: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

131 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Watumishi wake Makanisani na pia katika midomo ya watu wake walio okolewa.

Mungu husema “Semeni na moyo wa Yerusalemu kauambie kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote… Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isaya 40:2, 8).

Mungu amekwisha toa ahadi zaidi ya miaka mia saba kabla ya kuzaliwa kwa Kristo “wewe si mwenye dhambi tena. Nimekwisha kupatanisha kwa dhambi zako zote na vita imekwisha.” Na hivyo, sauti ya Injili ya ukombozi inaendelea kutuita; Na hii ndiyo inayoitwa Injili iliyotayarishwa.

Tunapoelewa juu ya kazi za Yohana Mbatizaji na kuelewa kwa hakika ya kwamba dhambi zote za ulimwengu alitwikwa Yesu

kupitia Yohana Mbatizaji; tunaweza wote kuwa huru kutoka dhambini.

Injili zote nne hutuelezea juu ya Yohana Mbatizaji, na Malaki, nabii wa mwisho katika Agano la Kale pia alishuhudia ya kwamba Yohana Mbatizaji ni Mtumishi wa Mungu aliyetayarishwa. Agano Jipya limeanza na habari ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji na kutwika dhambi kupitia yeye.

Sasa ni kwa sababu gani anaitwa Yohana Mbatizaji? Ni kwa sababu alimbatiza Yesu. Nini maana ya Ubatizo? Una maana ya “kuwekea, kutwika, kuzika kusafisha” ni sawa na “kuwekea mikono” katika Agano la Kale.

Katika Agano la Kale mtu alipotenda dhambi, alimtwika dhambi zake zote mnyama wa kutolewa dhabihu, na alikufa kwa dhambi hizo. “Kuwekea mikono” maana yake ni “kubebesha.” Hivyo “kuwekea

Page 132: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

132 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

mikono” na “ubatizo” una maana sawa. Ingawa kuna onekana tofauti katika kitendo.

Hivyo, ubatizo wa Yesu ulikuwa una maana gani? Ubatizo wake ulikuwa ndiyo njia pekee kwetu kupokea ondoleo la dhambi. Mungu alianzisha sheria ili dhambi ziweze kuhamishiwa kwa dhabihu kupitia “ kuwekewa mikono.” Hivyo katika nyakati za Agano la Kale, wenye dhambi iliwapasa kuwekea mikono juu ya kichwa cha yule mnyama wa kafara ili kutwika dhambi zao zote kwake. Na baada ya hapo, walimchinja kondoo na kuhani kuchukua damu yake ili kuweka katika pembe za madhabahu ya sadaka za kuteketezwa. Hii ilikuwa ndiyo njia pekee ya msamaha wa dhambi za kila siku.

Hivyo, ni kwa namna ipi walipata ondoleo la madhambi ya mwaka mzima?

Kwa jambo hili, Haruni, Kuhani Mkuu alitolea dhabihu kwa niaba ya Israeli yote.

Kwa sababu Yohana Mbatizaji alizaliwa toka nyumba ya Haruni ilikuwa sawa kwake kuwa kuhani Mkuu na Mungu alimtambua kabla ya kuzaliwa kwake kwamba atakuwa Kuhani Mkuu kulingana na ahadi yake ya ukombozi.

Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu wa mwisho kwa sababu Agano la Kale limeishia wakati Yesu Kristo alipozaliwa. Ni nani zaidi ya Yohana Mbatizaji angeweza kutwika dhambi zote za Ulimwengu kwa Yesu katika Agano Jipya kama ilivyo Haruni alivyotolea dhambi za watu wake katika Agano la Kale? Kama alivyo Kuhani Mkuu katika Agano la Kale na mwakilishi wa wanadamu. Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zote za dunia kwa Yesu alipombatiza.

Kwa kuwa Yohana alimtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu, basi kuamini Injili ya maji na kwa Roho hakika itatukomboa. Yesu

Page 133: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

133 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

alikuwa mwanakondoo ili atuokoe wenye dhambi, hivyo alifanya kazi ya ukombozi ilivyopangwa na Mungu.

Yesu alituambia ya kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ni Nabii wa mwisho, Kuhani mkuu wa mwisho aliyetwika dhambi zote za ulimwengu kwake.

Kwa nini Yesu asingefanya mwenyewe? Kwa nini alimwitaji Yohana Mbatizaji? Palikuwa na sababu ya Yohana Mbatizaji kuzaliwa miezi sita kabla ya Yesu; Ilikuwa ni kuhimiza sheria ya Agano la Kale, kukamilisha ahadi.

Yesu alizaliwa toka kwa mwanamwali Mariamu na Yohana Mbatizaji alizaliwa toka kwa mwanamke mzee aliye tasa aitwae Elisabeti.

Hii ilikuwa kazi ya Mungu na aliipanga kwa hao ili, kuwaokoa wenye dhambi.

Kutuokoa toka katika vita isiyokwisha

dhidi ya dhambi pamoja na mateso yatokanayo na uovu uliopo kati yetu. Alimtuma Mtumishi wake Yohana, na baadae mwana wake Yesu. Yohana Mbatizaji alitumwa kama mwakilishi wa wanadamu, Kuhani mkuu wa mwisho.

Mtu katika uzao wa mwanamke aliye mkuu.

Ni mwanadamu gani aliyekuwa mkuu?

Yohana Mbatizaji

Na tuone Mathayo 11:7-14 “Na hao

walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, mlitoka kwenda

Page 134: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

134 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika jumba la Mfalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? naam nawaambia na aliye mkuu zaidi ya Nabii Tazama mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako,atakayeitengeneza njia yako,mbele yako. Amin nawaambieni hajaondokea mtu katika wazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu; nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.”

Watu walikwenda jangwani kumwangalia

Yohana Mbatizaji aliyekuwa akipaza sauti . ‘Tubuni enyi uzao wa nyoka’ naye Yesu alisema “Lakini mlitoka kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.”

Yesu mwenyewe alitoa ushuhuda juu ya ukuu wa Yohana. “Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu wa msituni aliyevaa singa za ngamia apazae sauti yake kwa juu sana? Atakuwa amevalia singa za ngamia. Mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevalia mavazi mororo? Wale waliovalia mavazi mororo wamo katika nyumba za Wafalme.Lakini yeye ni mkuu zaidi ya wafalme” Lakini yeye ni mkuu zaidi ya Wafalme.” Yesu alishuhudia “Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme, lakini mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam nawaambia aliye mkuu zaidi ya Nabii.”

Page 135: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

135 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Katika nyakati za zamani Nabii alichukuliwa kuwa ni mkuu zaidi ya mfalme. Yohana Mbatizaji alikuwa ni zaidi ya mfalme, na zaidi ya Nabii. Alikuwa ni zaidi ya Manabii wote wa Agano la Kale. Hakika Yohana, Kuhani Mkuu wa mwisho na mwakilishi wa wanaadamu alikuwa ni muhimu zaidi ya Haruni Kuhani Mkuu. Yesu mwenyewe alimshuhudia Yohana kwa hilo.

Ni nani aliye mwakilishi wa wanaadamu? Zaidi ya Kristo mwenyewe, ni nani mwanadamu aliye mkuu ulimwenguni? Yohana Mbatizaji. “Naam nawaambia na aliye mkuu zaidi ya Nabii. Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, tengeneza njia yako mbele yako.”

Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba vita dhidi ya dhambi vilikwisha. “Tazama, mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Alikuwa ni Yohana

Mbatizaji aliyemshuhudia Yesu ndiye azichukuaye dhambi za dunia.

Katika Mathayo 11:11 “Amin, nawaambia hajaondokea mtu katika wazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.” Je, hapakuwahi kuwa na mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji kati ya uzao wa mwanamke?

Ni nini maana ya “Kati ya uzao wa mwanamke?” Hii inawakilisha wanadamu wote, isipokuwa Adam na Hawa pekee. Wanadamu wote walizaliwa kupitia mwanamke. Ndio kati ya uzao wa mwanawake, hapakutokea mkuu kumshinda Yohana Mbatizaji. Hivyo alikuwa ni Kuhani Mkuu na mwakilishi wa wanadamu. Yohana Mbatizaji alikuwa mkuu, Nabii na mwakilishi wa wanadamu.

Katika Agano la Kale, Haruni na wanawe wa kiume walichaguliwa na Mungu

Page 136: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

136 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

kumtumikia milele. Dhambi zote zilisafishwa na Haruni na wanawe wa kiume. Ni Mungu aliyetoa agizo hilo.

Ikiwa Walawi wengine watajitokeza na hata kuthubutu kuacha Ukuhani, bila shaka wangekufa. Yote waliyoweza kufanya ni kukusanya kuni kwa ajili ya kuwasha moto katika altare, kuchuna ngozi wanyama, kutoa mafuta, kuosha utumbo na kutoa mabaki ya viungo vingine vya ndani nje ya makutano. Ikiwa wangedharau kwa kujaribu kwa kutumia nguvu zao kufanya kazi ya Ukuhani wangeweza kufa. Ni sheria ya Mungu wasingeweza kuvuka mstari.

Duniani hapajawahi kutokea Mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Alikuwa mkuu kati ya waliokuwa na mwili. “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”

Ukombozi wa mwanadamu ulikamilishwa pale Yohana Mbatizaji alipombatiza Yesu, na wale wote wamwaminio Yesu wataingia katika ufalme wa mbingu kwa kuwa wamefanywa haki kwa imani.

Sasa na tuangalie baba yake Yohana alivyoshuhudia juu ya mwanawe.

Ushuhuda wa Zakaria, baba yake Yohana.

Zakaria alitoa unabii gani juu ya mtoto wake?

Yohana angetayarisha njia ya Bwana kwa kufundisha njia ya

Wokovu kwa watu wake.

Page 137: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

137 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Na tuangalie Luk. 1: 67-80. “Na Zakaria, baba yake akajazwa Roho Mtakatifu akatabiri akisema, Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; tuokolewe na adui zetu, na mikononi mwao wote wanaotuchukia, ili kuwatendea rehema baba zetu na kulikumbuka Agano lake takatifu, uapo aliomwapia Ibrahim, baba yetu ya kwamba atatujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu; na kumwabudu pasipo hofu, kwa utakatifu na kwa haki mbele zake siku zote. Nawe mtoto utaitwa Nabii wake aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za Uso wa Bwana umtengenezee njia zake, uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi

zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti na kuongoza miguu yetu kwenye njia ya amani. Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni, akakaa, majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.”

Zakaria alitoa unabii wa vitu viwili. Alitoa unabii wa Mfalme wa watu wote ajaye, toka msitari wa 68 hadi 73 altoa unabii kwa furaha. Mungu hakusahau ahadi yake na kwamba Yesu, kama Mungu alivyoahidi kwa Musa atazaliwa kwa mwanamwali Mariamu ili kuokoa uzao wake toka mikononi mwa adui azo.

Mwanzo wa mstari wa 74 “atatujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu na kumwabudu pasipo hofu”. Huu ni ukumbusho wa ahadi ya Mungu kwa

Page 138: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

138 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Abrahamu na watu wa Israeli, na alitabiri “na kutujalia ili kumwabudu pasipo hofu.”

Mwanzo wa mstari wa 76 pia alitabiri juu ya mtoto wake “Nawe mtoto, utaitwa nabii wake aliye juu kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake. Uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti. Kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”

Alisema, “uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu.” Ni kwa nini aliyasema haya awajulishe kupatiwa wokovu? Yohana Mbatizaji je, nyote mnaweza kuona haya? Yohana Mbatizaji kupitia maneno ya Mungu, alipaswa

kutujulisha ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu.

Sasa na tuangalie Marko 1 “ Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayetengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake. Yohana alitokea akibatiza nyikani na kuhubiri Ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakaziungama dhambi zao” (Marko 1: 1-5).

Waisraeli walipomsikia Yohana Mbatizaji waliacha kuabudu sanamu zao za mataifa na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Lakini Yohana alishuhudia ya kwamba “Nawabatiza ninyi ili muweze kumrudia Mungu. lakini

Page 139: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

139 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Mwana wa Mungu atakuja na kuwabatiza ninyi ili dhambi zenu zote ziweze kutwikwa kwake kwa namna hii. Na ikiwa mtamwamini yeye Ubatizo wake kama mlivyobatizwa nami, dhambi zenu zote atabebeshwa yeye kama vile dhambi zilivyoweza kuwekwa juu kwa kuwekewa mikono katika Agano la Kale.” Hii ndio maana ya ushuhuda alioutoa Yohana Mbatizaji.

Ukweli kwamba Yesu alibatizwa katika mto Yordani una maana ya kuwa alibatizwa katika mto wa mauti. Tunaimba “katika misiba katika huzuni na uzuri, tutakutana Pwani njema, tutakutana Pwani hiyo njema.” Tutakapokufa tutavuka mto Yordan. Mto Yordani ni mto wa mauti. Yesu alibatizwa katika mto wa mauti kwa kuzibeba dhambi zetu za ulimwengu mahali hapo na “Mshahara wa dhambi ni mauti.”

Ubatizo ulichukuwa dhambi zetu.

Kuwekea mikono ni badala ya

nini katika Agano Jipya?

Ubatizo wa Yesu

Katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akjibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. Naye yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake,

Page 140: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

140 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema Huyu ni Mwanangu, Mpendwa Wangu, Ninayependezwa naye.”

Yesu alikwenda Yordani na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Aliamuru “Nibatize.” Yohana akajibu “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu.” Kuhani Mkuu wa mbinguni alikutana na Kuhani Mkuu wa duniani.

Kama ilivyoandikwa katika Waebrania, Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu wa milele, kutokana na maelekezo ya Melkizedeki. Hii ina maana kwamba Yesu hakutoka katika ukoo wa mwanadamu. Yeye si uzao wa Haruni, au wa mtu yeyote duniani.yeye ni Mwana wa Mungu, Muumba wetu. Yeye ndiye aliye, hana ukoo. Yesu aliuacha Utukufu wake mbinguni na kuja duniani kuokoa watu wake.

Sababu ya kuja kwake ulimwenguni

ilikuwa ni kuokoa watu wote wenye dhambi watesekao kwa ulaghai wa shetani. Kwa nyongeza alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji. “Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

“Kubali hivi sasa” Kubali hivi! Yesu aliamwamuru mwakilishi wa wanadamu kwa kuinamisha kichwa chake iliabatizwe. Katika Agano la Kale, wakati sadaka ya mnyama ilipokuwa ikitolewa kwa Mungu, kati ya mwenye dhambi au kuhani aliwekea mikono ili kuitwika dhambi. “Kuwekea mikono” maana yake ni “kutwika”.

Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu. Ilikuwa ni sawa na kuwekea mikono wakati wa Agano la Kale. “Kutwika” kuzikwa ”Kusafishwa” na “kutolewa kwa kafara” vyote ni sawa. Agano Jipya ni ukweli hali kwa Agono la Kale ni kivuli.

Page 141: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

141 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Wakati wa Agano la Kale mwenye dhambi alipomwekea mikono mwanakondoo wa sadaka, dhambi zake zilitwikwa kwa mwanakondoo huyo na ilimpasa amchinje. Mwanakondoo huyo alipouwawa ndipo alipo futiwa dhambi. Dhambi za aliye wekea mikono juu ya mwanakondoo zilitwikwa kwa mwankondoo aliye sadaka, hivyo ilimpaswa auwawe kwa sababu ya dhambi alizo beba juu yake! Je, ikiwa dhambi zilitwikwa kwa mwanakondoo huyo, basi ina maana mwenye dhambi hakuwa tena na dhambi? Ndiyo.

Hebu na tuseme kwa mfano kitamba hiki cha mikono ni dhambi na kipaza sauti ni mwankondoo. Ninapo weka mikono yangu juu ya hiki kipaza sauti, hii ni kutwika dhambi juu yake, mwanakondoo. Mungu ndiye aliye amuru iwe hivyo. “Kuwekea mikoo”. Ili kuweza kukombolewa toka

dhambini katika nyakati za Agano la Kale, ilimpasa mtu kuwekea mikono sadaka ya dhambi. Nabaada ya hapo hakuwa tena mwenye dhambi. Hali kadhalika, ubatizo wa Yesu ulikuwa ni kwaajili ya kusafisha, kuzika na kubebesha dhambi za ulimwengu juu yake. Na hii ndiyo maana halisi.

Nini maana ya kutimiza Haki zote?

Ni kutakaswa dhambi zote Kwa kumtwika Yesu.

Hivyo, Je, Yesu alipo batizwa, dhambi

zote ulimwenguni hazikuwekewa juu yake? Dhambi zote za ulimwenguni zilitwikwa kwake Yesu na watu wote walikombolewa hakika. Ni sawa na kutwika dhambi kwa mnyama wa sadaka ya dhambi katika Agano

Page 142: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

142 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

la Kale. Yesu alitoka Galilaya kuja Yordani na kumwambia Yohana “Kubali hivi sasa: kwakuwa ndivyo itupasavyokuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

Ndipo Yohana akambatiza Yesu. Alimwambia Yohana ilifaa kwao kutimiza haki yote kwa ubatizo wake. “Haki zote” Maana yake “namna pekee ya kufaa.” “Kwa kuwa ndivyo” kwa maneno mengine, kwa njia ya ubatizo, haki zote zilitimizwa. Hii maana yake ilikuwa sawa kwa Yohana kumbatiza Yesu na Yesu kubatizwa na Yohana ili kumbebesha dhambi za ulimwengu.

Mungu alitupa ukombozi kupitia msingi wa Ubatizo wa Yesu, sadaka yake Msalabani, na imani zetu. “Watu wote huteseka kwa dhambi na kunyanyaswa na shetani kwa sababu ya dhambi zao. Hivyo ili waokolewe na kwenda mbinguni, wewe, kama

mwakilishi wa wanadamu na uzao wa Haruni, yakupasa kunibatiza mimi kwa ajili ya watu wote. Nitabatizwa nawe, Yohana, ndipo kazi ya ukombozi itakapokamilika.”

“Nimeelewa” Yohana alijibu. Hivyo Yohana alimbatiza Yesu. Alimwekea

Yesu mikono yake kichwani na kumtwika dhambi zote za ulimwengu kwake. Hivyo Yesu alikuwa Mwokozi asafishaye dhambi zetu zote. Hivyo kuamini ukombozi wake kutatuokoa. Je, unaamini hivyo?

Baada ya Ubatizo wake katika Yordani, kupitia mikono ya mwakilishi wa wanadamu, Yesu alisafiri huku na kule na kuanza kuhubiri kwa miaka mitatu na nusu akiwa na dhambi zote za ulimwengu juu ya mwili wake akihudumia watu kwa mara ya kwanza.

Alimwambia yule mwanamke aliyefumaniwa “Nami pia sikuhukumu.”

Page 143: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

143 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Asingeweza kumhukumu mwanamke huyu kwa kuwa tayari alikwisha zichukuwa dhambi zake na alikuwa mbioni kufa Msalabani kwa ajili yake. Alipokuwa akiomba katika sehemu iitwayo Gethesemani aliomba mara tatu akimsihi Baba akiepushe kikombe chake kimpishie mbali, lakini punde aliachia na kusema “Si kwa mapenzi yangu bali kwa mapenzi yako.”

“Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”

Ni dhambi kiasi gani Yesu alizichukuwa?

Dhambi zote zaUlimwengu.

Yohana 1:29 Inasema “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu na siku iliyofuata Yesu alikuja kwake, hivyo awaambia watu, “tazama, Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Ilikuwa ushuhuda wake.

Mwana wa Mungu alikuja duniani, na kuchukuwa dhambi zote. Yohana Mbatizaji alishuhudia tena katika Yohana 1:35-36, “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu akitembea akasema, tazama Mwanakondoo wa Mungu!”

Mwanakondoo wa Mungu inaonyesha ukweli kwamba Yesu ndiye Kweli na Halisi, sadaka iliyotajwa katika Agano la kale,

Page 144: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

144 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

ambayo ilikufa kwa ajili ya dhambi za Israeli. Kwako mimi na wewe, Mwana wa Mungu na Mwuumbaji wetu, alikuja ulimwenguni ili kuzichukuwa dhambi zetu zote; dhambi zote toka ulimwengu kuumbwa hadi siku yake ya mwisho, kuanzia dhambi ya asili hadi uovu wetu, toka mapungufu yetu, toka udhaifu wetu hadi makosa. Alitukomboa sisi sote kwa Ubatizo na Damu yake katika Msalaba.

Yesu alizichukua dhambi zetu zote na kutupa sisi wenye kuamini ukombozi kamili. Je, unaelewa hii? “Mwana kondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu.”

Miaka 2000 imekwisha pita tangu azaliwe hapa duniani na katika miaka 30 (BAADA YA KRISTO) Yesu alizichukua dhambi zote. Mwaka wa 1 (BAADA YA KRISTO) ndio ulikuwa mwaka uliozaliwa. BK. ni mwaka Baada ya Kristo na ni miaka 2000 imepita tangu Yesu aje duniani.

Katika mwaka 30 BK, Yohana alipaza sauti kwa watu akisema “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu.” “Tazama!” aliwaambia watu kumwamini Yesu, aliyezichukua dhambi zao zote. Alishuhudia kwamba Yesu alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu; yeye atuokoae sisi sote na dhambi zetu zote.

Yesu alizichukua dhambi zetu na kumaliza kabisa vita ile isiyokwisha ya dhambi. Sasa hakuna tena dhambi tangu Mwana wa Mungu alipozichukua. Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote, zangu na zako “Huyu alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye” (Yohana 1:7).

Pasipo ushuhuda wa Yohana, ni kwa namna gani tungefahamu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote? Biblia

Page 145: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

145 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

inatueleza mara kwa mara kwamba alikufa kwa ajili yetu, lakini ni Yohana Mbatizaji pekee ashuhudiae kwa uwazi zaidi kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote.

Ni dhambi ngapi

za dunia?

dhambi zote za watu toka mwanzo hadi mwisho

wa dunia hii.

Wengi walishuhudia baada ya kifo cha Yesu, lakini ni Yohana pekee alishuhudia wakati yesu akiwa hai. Hata hivyo wanafunzi wa Yesu pia walishuhudia juu ya ukombozi wa Yesu. Walishuhudia kwamba Yesu alizichukuwa dhambi zetu zote, ni Mwokozi.

Yesu alizichukuwa dhambi zote za dunia, Sasa msomaji wangu wewe bado hujawa na

umri wa miaka 100? Yesu alichukua dhambi zote za duniani akiwa na umri wa miaka 30. Tazama mchoro huu.

Adam→ Abrahamu→Ubatizo wa Yesu→Wakati huu→Mwisho

4000 2000 30 Baada ya 2002 Baada Baada

Kabla ya Kristo Kabla ya Kristo Kristo ya Kristo ? Kristo

Dhambi zote za Ulimwengu

Kwa mfano ilikuwa miaka 4000 kabla ya Kristo kuja mwanadamu wa kwanza aliumbwa. Na imekuwa kidogo zaidi miaka 2000 tangu Yesu aje. Hatufahamu ni kwa miaka mingapi dunia itaendelea kuwepo, ingawa hakika upo mwisho utakuja. Yesu alisema “Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza” (ufunuo 22:13).

Hivyo, hakika kutakuwa na mwisho. Kwa sasa tupo kipindi kioneshacho mwaka 2002. Yesu alizichukua dhambi zetu zote miaka 30

Page 146: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

146 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

BK na ilikuwa miaka 3 kabla ya kifo chake msalabani.

“Tazama! Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu.” Alizichukua dhambi za dunia zangu na zako. Tupo miaka 2000 zaidi tangu kuzaliwa kwa Yesu na tunaishi miaka hii 2000 baada ya Yesu kuzichukua dhambi zetu zote. Tunaendelea kuishi kwa kuendelea kutenda dhambi siku hadi siku, ingawa Yesu ni mwana Kondoo wa Mungu aliyekwisha chukua tayari dhambi za ulimwengu huu.

Tunaanza na kuishi na kutenda dhambi tokea pale mwanzo tunapozaliwa. Je ni wote hutenda dhambi tangu tuzaliwapo au la? Ni wote! Hebu natuone mpango wote. Tangu siku tuliyozaliwa hadi kufikia umri miaka 10, je tunatenda dhambi au la? Tunatenda –Je dhambi hizo hakubebeshwa Yesu ?. Alizibeba.Ikiwa basi alizibeba ni Mwokozi

wetu. Ikiwa sivyo, atakuwa vipi Mwokozi wetu? Dhambi zote ziliwekewa Yesu.

Toka miaka 11 hadi 20 tunatenda dhambi au la? Tunatenda ndani ya mioyo yetu na kwa matendo… kwa ustadi mkuu. Tumefundishwa tusitende dhambi, lakini tumeumbwa kwa asili kutenda.

Mungu anatueleza ya kwamba, dhambi zote zilitwikwa kwake Yesu. Alifahamu jinsi ile tulivyo wenye dhambi na ndiyo maana aliziondoa kabla.

Na muda gani basi, tunaishi duniani? Hebu na tuseme miaka 70, ni kwa namna gani basi mzigo utakuwa mzito? Tukizipakiza katika lori la tani 8, hakika tutapakia zaidi ya malori 100.

Jaribu kufikiri ni dhambi kiasi gani tungetenda katika kipindi chetu chote cha maisha. Je, hisi sizo dhambi za ulimwengu ama sizo? Hizi ni sehemu za dhambi za

Page 147: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

147 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

ulimwengu. Tunatenda dhambi toka pale tunapozaliwa kufikia miaka 10, 10 hadi 20, 20 hadi 30 na kuendelea hadi siku tunapo kufa lakini yote haya yanajumuishwa katika dhambi za dunia ambazo tayari zilikwishabebwa na Yesu katika ubatizo wake.

Mwokozi wa watu, Yesu Kristo

Ni kiasi gani cha dhambi Yesu alibeba?

dhambi zote za mababu zetu na uzao wetu hadi mwisho

wa ulimwengu. Yesu anatuambia ya kwamba, alikuja

katika mwili kusafisha dhambi hizo. Lakini

hakuweza kujibatiza mwenyewe, hivyo Mungu alimtuma mtumishi wake Yohana kabla yake, mteule mwakilishi wa wanadamu. Kama ilivyoandikwa “Na jina lake ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenyezi. Kwake mwenyewe, kwa Hekima yake na kwa shauri lake, alimtuma mwakilishi wa wanadamu mbele yake, na Yesu mwenyewe Mwana wa Mungu alikuja katika mwili kubeba dhambi zote za ulimwengu Je, jambo hili si wokovu wa ajabu wenye msingi ulioletwa na Mungu?

Ni wa ajabu, je si kweli? Hivyo, kwa ubatizo wa Yohana Mbatizaji, alisafisha dhambi za ulimwengu wote na kuwakomboa wanadamu wote kila mmoja toka dhambini kwa kusulubiwa kwake, mara moja na kwa wakati wote. Alitukomboa sisi sote. Hebu fikiri jambo hili. Hebu tuangalie dhambi zetu zote kuanzia miaka ya 20 hadi 30, 30 hadi

Page 148: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

148 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

40, 40 hadi 60 hadi 70 na 100 na kuendelea na si hivyo tu hata za watoto wako. Je, alizifuta! Dhambi zote hizi au la? Ndiyo alizifuta. Ni Yesu Kristo, Mwokozi wa wanadamu.

Tangu Yohana Mbatizaji amtwikwe Yesu dhambi zetu, na kwa kuwa Mungu aliweka mpango huo hivyo, basi tutaweza kukombolewa na yeye tu ikiwa tutamwamini. Je, mimi na wewe si wenye dhambi? Je, dhambi zote alizichukua Yesu? Ndiyo, sisi si wadhambi tena, kwa kuwa dhambi zetu tayari zilikwisha bebwa na Yesu.

Ni nani athubutuye kusema kuna dhambi ulimwenguni? Yesu alikwisha zichukua zote. Alijua ya kwamba tutatenda dhambi tena na hivyo alizichukua hata zile zijazo. Wengi wetu hatujafikia umri wa miaka 50, na hata wengine hatujaishi hata nusu ya maisha

yetu bado lakini wachache wetu tunazungumza juu ya kuishi tukidhani tutaishi milele.

Wapo wengi wenye kuishi maisha yenye kuelekea katika mitafaruku ya aina mbalimbali. Hebu nifafanue namna hii. Yupo mdudu fulani apendaye kutembea juu ya maji ya vijito, huishi katika umri wa saa 12.

“Lo! Yupo mtu fulani alichota maji yenye wadudu hao katika mto na kunimwagia! Nilikimbia na kuanguka karibu kuzimia. Hakika hakuna mtu katili kama huyu katika maisha yangu.” Ajabu ni kwamba wadudu wale walikwisha karibia umri wao wa saa 12 lakini sikuacha kulalamika juu ya kitendo hiki. Nusu ya maisha yao ilikwisha isha.

Ikifikia saa 1 au 2 jioni, wanakumbana na kikomo cha maisha yao kwa muda huo mfupi, kifo. Wengine huishi saa 20 au 21, na wengine huvuna umri mzuri wa saa 24.

Page 149: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

149 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Wanaweza kuzungumzia juu ya maisha yao marefu na waliyo pitia je hii ina maana gani kwetu? Tunapo ishi miaka 70 au 80 kwa umri, tunaweza kusema “Usinichekeshe” umri wa wadudu hawa si kitu mbele yetu. Saa 24?

Hebu tufananishe mfano huu kati yetu na uhusiano tulio nao na Mungu. Mungu ni wa milele. Anaishi milele. Anaamua mwanzo na mwisho wa dunia. Aishivyo wakati wote, anaishi milele zaidi ya muda uliowekwa katika milele. Hutuangalia sisi maisha yetu na kuhusisha na umilele wake.

Hapo kale, Mungu alizichukua dhambi zetu zote za dunia, na kufa msalabani kwa kusema “IMEKWISHA.” Alifufuliwa baada ya siku 3 na kupaa mbinguni sasa amekaa mbinguni milele. Na hutuangalia sisi sote kila mmoja wetu.

Mtu mmoja aweza kusema “Oh, mpendwa

mimi ni mwingi wa dhambi. Ingawa nimeishi umri wa miaka 20, nimetenda dhambi nyingi.” “Nimeishi miaka 30 na nimetenda dhambi nyingi. Ni nyingi sana. Nitakuwa vipi bila dhambi?”

Lakini Bwana wetu wa milele atasema “Usinichekeshe. Sijakukomboa na dhambi zako tu sasa, bali hata zile za mababu zako kabla hujazaliwa na zile za kizazi chako ambacho kitakuja kuishi baada yako.” Huzungumzi hivi kutokana na mtazamo wa milele. Je, unaamini haya? Amini hili ili upokee wokovu wa bure wa milele. Ingia katika Ufalme wa Mbinguni.

Usifungwe na mawazo yako, bali amini neno la Mungu. “Hivi ndivyo itupasavyo kutimiza haki zote.” Mwana kondoo wa Mungu, azichukuae dhambi za ulimwengu alikwisha timiza haki zote. Yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu. Je ni kweli au si

Page 150: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

150 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

kweli? Ni kweli, alichukua!

Yesu alisema neno gani mwisho alipokata roho?

“IMEKWISHA”

Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote

ulimwenguni kupitia ubatizo wake, alihukumiwa kifo mbele ya Mahakama ya Pilato na kusulubiwa msalabani.

“Akatoka hali akijichukulia msalaba wake mpaka mahali paitwapo Fuvu la kichwa, au kwa kiebrania Golgotha. Wakamsulubisha huko, na wengine wawili pamoja naye mmoja huku na mmoja huku na Yesu katikati. Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa YESU MNAZARETI MFALME WA WAYAHUDI. Basi

anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi maana mahali pale aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania na Kirumi na Kiyunani” (Yohana 19:17-20).

Hebu na tuangalie nini kilitokea baada ya kusulubiwa msalabani “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe Alikwisha zibeba dhambi zote kulingana na maandiko akasema naona kiu, kulikuwa huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa kisopo wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” (Yohana 19:28-30).

Baada ya kuipokea sifongo iliyojaa siki, alipaza sauti na kusema “Imekwisha.” Aliinamisha kichwa na kufa. Hakika alikuwa amekufa. Yesu Kristo alifufuka baada ya siku

Page 151: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

151 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

3 na kupaa mbinguni. Hebu tuangalie Waebrania 10:1-9 “Basi

torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayotawala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni asema dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi kuhupendezwa nazo. Ndipo niliposema tazama nimekuja (katika gombo la chuo imeandikwa) niyafanye mapenzi yako Mungu. Hapo juu asemapo,

dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyo amuru torati) ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.”

Ukombozi wa Milele.

Je, tunaweza vipi kutatua tatizo la dhambi za kila siku tuzitendazo

baada ya kumwamini Yesu?

Kwa kuthibitisha ya kwamba Yesu alikwisha zifuta dhambi zetu zote kwa

kupitia ubatizo wake.

Page 152: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

152 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Kwa maneno mengine, Sheria ya mpango wa sadaka ya upatanisho ilikuwa ni kivuli cha mambo mema yajayo. Sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale, ya Kondoo na mbuzi, imetuonyesha ya kwamba Yesu Kristo angekuja na kuchukua dhambi zetu katika ufunuo huo ili kuzifuta kabisa.

Watu wote katika Agano la Kale, Daudi, Abrahamu, na wengine wote, walijua na kuamini juu ya mfumo wa sadaka ya upatanisho ulivyo wa maana kwao. Ulifunuliwa juu ya Masiya Kristo (Kristo maana yake “mfalme mpakwa Mafuta”) angekuja siku moja kusafisha dhambi zao zote. Waliamini katika ukombozi wao na waliokolewa kwa imani zao.

Sheria ilikuwa ni kivuli cha mambo mema yajayo. Sadaka ya ubatanisho wa dhambi zao za kila siku, mwaka hadi mwaka, isingeweza kuwakomboa kwa ukamilifu.

Hivyo ukamilifu na kuwepo milele, yule asiye na doa, Mwana wa Mungu ilipasa aje duniani kwa ajili hiyo.

Yesu alisema alikuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake kama ilivyo andikwa kitabuni juu yake. “Akasema Tazama, nimekuja ili niyatimize mapenzi yako.aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili.” Tumekombolewa kutoka dhambini kwa kuwa Yesu Kristo alichukua dhambi zetu zote kama ilivyoandikwa katika Agano la Kale, na kwa kuwa tunamwamini Yeye.

Hebu na tusome Waebrania 10:10 “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” Kwa hivi tungeweza kutakaswa kupitia sadaka ya mwili wa Yesu Kristo mara moja. Je, hatujatakaswa? -Tumetakaswa.-

Hii ina maana gani? Mungu Baba alimtuma Mwana wake na kumtwika dhambi

Page 153: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

153 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

zetu zote kwake kupitia ubatizo wake. Alipokea hukumu kwa yote katika msalaba. Hivyo, alitukomboa sisi sote tulioteseka kwa dhambi. Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu.

Ili kutukomboa, Yesu alijitoa mwenyewe kama sadaka ya milele mara moja na kwa wakati wote katika msalaba ili tutakaswe. Tumetakaswa kwa sababu Yesu alijitoa sadaka mwenyewe kwa dhambi zetu zote na kufa kwa ajili yetu ili tusihukumiwe tena.

Sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale ilitolewa kila siku na kila mwaka kwa sababu dhambi zote za siku zilihitaji upatanisho mwingine ili kusafisha.

Maana halisi ya kiroho kwa Yesu kusafisha miguu ya Petro.

Je, zipo dhambi nyingine tena tunazopaswa kuomba sala ya toba?

Hakuna.

Katika Injili ya Yohana 13 ipo habari ya

Yesu kusafisha miguu ya Petro. Alisafisha miguu ya Petro ili kuonyesha ya kwamba, Petro angetenda dhambi katika kipindi kijacho na kumweleza ya kuwa alikwisha mkomboa kwa dhambi hizo pia, Yesu alikuja Petro angetenda dhambi tena katika siku zijazo, hivyo alimimina maji katika karai na kuosha miguu yake.

Petro alijaribu kukataa, lakini Yesu alimwambia “Nifanyalo wewe hujui sasa;

Page 154: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

154 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

lakini utalifahamu baadaye.” Kifungu hiki kina maana kwamba “utatenda dhambi tena baadaye. Utanikana na kutenda dhambi tena baada ya kuosha dhambi zako zote. Utatenda dhambi hata wakati nitakapo paa kwenda mbinguni. Hivyo, nasafisha miguu yako ili kumtaadharisha shetani asikutie majaribuni kwa kuwa nimekwisha zichukuwa dhambi zako hata zile zijazo za nyakati.

Je, unafikiri alisafisha miguu ya Petro ili kutueleza kwamba yatupasa kutubu kila siku? Hapana! Ikiwa tulipaswa kutubu kila siku ili tukombolewe basi ina maana kwamba Yesu isingempasa kuchukua dhambi hizo mara moja na kwa wakati wote wa maisha yetu.

Lakini Yesu alisema alitutakasa mara moja na kwa wakati wote Ikiwa tungehitajika kutubu kila siku, basi ingekuwa kama vile tumerudi katika kile kipindi cha Agano la

Kale. Sasa, tungeweza kuwa wenye haki? Nani angeweza kukombolewa kwa ukamilifu? Hata kama tulimwamini Mungu, ni nani angeweza kuishi bila dhambi?

Nani atakayetakaswa kwa kutubu? Tunatenda dhambi pasipo kukoma kila siku hivyo ni vipi tunaweza kuomba msamaha kwa kila dhambi? Ni kwa namna gani tunaweza kuwa wavumilivu na kumuudhi Mungu kila siku kwa kuhitaji ukombozi? Tunajaribu kusahau dhambi zetu tulizotenda alfajiri hadi mwisho wa siku na zile za jioni hadi alfajiri nyingine. Ni vigumu kwetu kuomba toba kamili kwa dhambi zetu zote.

Hivyo, Yesu alibatizwa mara moja na kujitoa yeye mwenyewe msalabani mara moja ili tuweze kutakaswa mara moja na kwa wakati wote. Je, unaweza kuelewa hili? Tumekombolewa kwa dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote.

Page 155: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

155 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Hatukombolewi kila pale tunapo ungama. Tumeokolewa kutoka dhambini kwa

kumwamini Yesu aliyezichukua dhambi zetu zote, zangu na zako.

“Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya Ibada na kutoka dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao

sitaukumbuka tena kabisa Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:11-18).

Nini maana ya “basi ondoleo la hayo likiwapo” katika mstari wa 18 hapo juu? Hii ina maana ya kwamba, kila dhambi ilifutwa kabisa bila uchaguzi Mungu alizifuta dhambi zote na kutusamehe. Je, unaamini hili? “Hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”

Hebu na tufupishe kila kitu sasa. Ikiwa Yohana Mbatizaji ilimpasa kumwekea Yesu mikono, kwa maneno mengine, kama asingembatiza Yesu, Je, tungeweza kukombolewa? La! Bila shaka hapana! Tulifikiri nyuma tena. Ikiwa Yesu asingemteua Yohana Mbatizaji kuwa mwakilishi wa wanadamu na kuchukua dhambi za ulimwengu kupitia kwake, je, angewea kusafisha dhambi zetu? Asingeweza.

Page 156: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

156 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Sheria ya Mungu ni yenye haki. Ni ya usawa. Asingeweza kusema kwamba ni Mwokozi wetu na alichukua dhambi zetu. Ilimpasa Yesu azichukue dhambi zetu kimatendo. Kwa nini Yesu aliye Mungu alikuja duniani akiwa katika mwili? Alikuja ili azichukue dhambi zetu zote sisi wanadamu kwa kupitia ubatizo wake. Yesu alizijua dhambi zetu zote za moyoni na mwilini ambazo zisingeweza kufutwa ikiwa asingekuja katika mwili ili kujitoa sadaka ya milele.

Ikiwa Yesu asingebatizwa dhambi zetu bado zingebaki pale pale, kama asingesulubiwa kabla kwanza ya kuchukua dhambi zetu, Kifo chake kisingekuwa na maana kwetu. Ingekuwa haina maana kabisa.

Hivyo alipoanza huduma, yake ya wazi katika umri wa miaka 30, alikwenda kwa

Yohana Mbatizaji katika mto Yordani ili abatizwe. Huduma yake nje ilianza akiwa na umri wa miaka 30 na kuishi, akiwa na umri wa miaka 33. Alipokuwa na umri wa miaka 30 alikwenda kwa Yohana Mbatizaji ili abatizwe. “Kubali iwe hivyo, kutimiza haki zote ili watu wote waokolewe na kuwa wenye haki. Ni sahihi kwetu kutenda hili, sasa mbatizaji.” Ndiyo, Yesu Kristo alibatizwa ili aweze kuwakomboa watu wote.

Hivyo Yesu alibatizwa na kuchukua dhambi zetu zote, na kuwa dhambi zote alitwikwa kwake kupitia mikono ya Yohana Mbatizaji, Mungu mwenyewe aligeuza uso wake pembeni wakati Yesu alipokuwa akifa msalabani. Ingawa Yesu alikuwa ni mwana wake wa pekee, ilimpasa amtoe sadaka.

Mungu ni upendo lakini ilimbidi amwachie mwana wake afe. Hivyo kwa masaa 3 palikuwa na giza juu ya nchi yote. Yesu alilia

Page 157: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

157 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

kabla ya kufa kwake “Eloi, Eloi, lama sabathani!” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Yesu alijitwika dhambi zetu zote na kupokea hukumu katika msalaba kwa niaba yetu. Hivyo, alituokoa sisi sote. Bila ubatizo wa Yesu, kifo chake kingekuwa hakina maana yoyote.

Je, wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki?

Mwenye haki asiye na dhambi

zozote ndani ya moyo. Ikiwa Yesu angekufa malabani bila

kuchukua dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake, kifo chake kingekuwa hakijakamilisha ukombozi. Ili kukamilisha ukombozi wetu, Yesu alibatizwa na Yohana, mwakilishi wa

wanadamu, na kupokea hukumu katika msalaba ili wote wale wenye kumwamini waokolewe.

Hivyo, tangu kipindi cha Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu unachukuliwa kwa nguvu. Kwa sababu Yohana Mbatizaji alimtwika dhambi za ulimwengu Yesu, dhambi zetu zililipiwa Mimi na wewe leo tunaweza kumwita Mungu kuwa ni Baba na kwa uhakika tutaingia ufalme wa mbinguni.

Katika Waebrania 10:18 “Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo kwa ajili ya dhambi.” Je, bado una dhambi? Sasa Yesu umekwisha lipia madeni yote, Je, unahitaji kulipia tena madeni hayo?

Palikuwa na mtu mlevi ambaye alikuwa anadaiwa na watu wengi. Basi, siku moja, mtoto wake wa kiume kwa bahati alimlipia madeni yote aliyodaiwa. Baba huyu hakuwa tena na madeni ingawa alikuwa akidaiwa

Page 158: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

158 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

sana na kila mtu. Hivyo ndivyo Yesu alivyo tutendea. Alilipa

zaidi ya ziada ya dhambi zetu zote. Si dhambi zote maishani mwetu, bali zote za ulimwengu. Zote zilibebeshwa kwake Yesu alipobatizwa Je, wewe ni mwenye dhambi bado? Sasa wewe si mwenye dhambi tena.

Ikiwa tunataka kuelewa Injili ya Ukombozi toka mwanzo ni rahisi namna gani? itakuwa rahisi ikiwa tutamwamini Yesu. Lakini kama ilivyo inaonekana ni mpya kwa watu na inashangaza.

Lakini hili si jambo jipya hata kidogo. Ilikuwepo tangu hapo awali tangu historia ya mwanadamu. Hatukutambua hili kabla. Injili ya maji na kwa Roho imekuwa kwa wakati wote katika kumbukumbu ya maandiko na imekuwa ikitenda kazi. Imekuwepo hapo nyakati zote. Imekuwepo katika Biblia kabla yetu imekuwepo tangu uumbaji.

Injili ya Ukombozi wa Milele

Inatupasa tufanye nini mbele ya Mungu?

yatupasa tuamini Injili ya ukombozi wa milele.

Yesu Kristo, aliyechukua dhambi zetu

zote, aliyafanya haya yote kabla ya kuzaliwa kwetu, mimi na wewe. Alizichukua zote. Je, bado una dhambi? –Hapana- Sasa vipi juu ya dhambi utakazotenda kesho? Nazo pia zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu, sivyo? Je, hakubebeshwa Yesu, au la? Ndiyo alibebeshwa.

Sasa, zile za kesho alibeba? Ndiyo alibeba, alichukua zote bila uchaguzi. Hakuacha hata moja nyuma. Injili inatuambia kumwamini

Page 159: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

159 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

Yesu kwa moyo wetu wote, ambaye ndiye aliyezichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote na kuzilipia.

“Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, mwana wa Mungu” (Marko 1:1). Injili ya Mbinguni ni habari njema. Anatuambia “nimechukua dhambi zenu zote mimi ni Mwokozi wenu. Je, unaniamini?” Kati ya watu wengi ni wachache tu watajibu, “Ndiyo, naamini. Naamini kama uniambiavyo. Imekuwa ni rahisi kuweza kuelewa mapema.” Wale wenye kukiri imani zao kama hivi hufanywa wenye haki kama Abrahamu.

Lakini wengine watasema “siwezi kuamini, Inaonekana kitu kigeni kwangu.”

Ndipo atasema “Hebu niambie, Je, sikuchukua dhambi zako zote au la?”

“Nilifundishwa kwamba alizichukua zile za asili tu na wala si zile za kila siku.”

“Naona wewe unaelewa zaidi kama ulivyo

fundishwa sasa utakwenda kuzimu kwa kuwa sina cha kukueleza.”

Kuamini ukombozi ulio kamili umetuokoa wale wote wenyekutilia mkazo kwamba ni wenye dhambi na watakaokwenda motoni wamejichagulia.

Injili ya ukombozi huanzia kutoka katika ushuhuda wa Yohana Mbatizaji. Tangu Yesu asafishe dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake kwa Yohana Mbatizaji, tumetakaswa tunapoamini.

Mtume Paulo alizungumzia juu ya Yesu katika nyaraka zake. Katika Wagalatia 3:2-7 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” “Kubatizwa katika Kristo” maana yake tumeungana na Kristo kwa kuamini ubatizo wake. Wakati Yesu alipobatizwa, dhambi zetu zote alizibeba kupitia Yohana Mbatizaji na zilisafishwa zote.

Katika 1Petro 3:2, “Mfano wa mambo

Page 160: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

160 Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi

hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”

Ni wale tu wenye kuamini ushuhuda wa Yohana Mbatizaji, ubatizo wa Yesu na damu katika msalaba wanayo neema ya ukombozi toka juu.

Pokea ubatizo wa Yesu kama mfano wa wokovu ndani ya moyo wako na uokolewe.

Page 161: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 6

Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na

kwa Roho

Page 162: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

162 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

(1Yohana 5:1-12) “Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni

Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu, mwenye kuushinda

ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo, si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiyo kweli kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni) BABA na NENO na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni wamoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi Kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake.

Page 163: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

163 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima, asiye na mwana wa Mungu hana huo uzima.”

Kwa namna gani

Yesu alikuja?

Maji, damu na kwa Roho.

Je, Yesu alikuja kwa maji? Ndiyo. Alikuja

kwa ubatizo wake. Maji yanasimama badala

ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordani. Ulikuwa ubatizo wa ukombozi ambao ulimbebesha dhambi zetu zote ulimwenguni.

Je, Yesu alikuja kwa damu? Ndiyo alikuja katika mwili wa mwanadamu na alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kuzilipia mshahara wa dhambi kwa kutoa damu yake pale msalabani Yesu alikuja kwa damu.

Je, Yesu alikuja kwa Roho? Ndiyo. Yesu alikuwa ni Mungu lakini alikuja akiwa Roho ndani ya mwili. Ali kuwa mwokozi wa wenye dhambi.

Watu wengi hawaamini ya kwamba Yesu alikuja kwa maji, damu na kwa Roho. Ni wachache wenye kuamini kwamba hakika Yesu ni Mfalme wa Wafalme na Mungu wa miungu. Wengi bado wanatangatanga “hivi kweli Yesu ni Mwana wa Mungu au mwana

Page 164: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

164 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

wa mtu?” Na wengi, pamoja na wana theologia na Watumishi, huamini Yesu kama mtu zaidi ya kuwa ni Mungu, mwokozi na Ndiye.

Lakini Mungu alisema kwa yeyote atakaye amini kwamba Yesu ni Mfalme wa wafalme, Mungu wa kweli na Mwokozi wa kweli atakuwa amezaliwa naye. Wale wampendaye Mungu humpenda Yesu na wale wenye kumwamini kweli Mungu humwamini Yesu kwa njia hiyo pia.

Watu hawawezi kuishinda dunia ikiwa hatazaliwa upya. Ni hivi, Mtume Yohana ametueleza kwamba ni wale Wakristo wa kweli tu ndiyo watakao ishinda dunia. Sababu kwa nini waaminifu wataweza kuishinda dunia, ni kwamba wana imani katika maji, damu, na kwa Roho. Nguvu ya kuishinda dunia haiwezi kutoka kwa mapenzi ya mtu matamanio au hamu.

“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upata uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu, kiasi cha kuweza kuhamisha milima kama sina upendo si kitu mimi; Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitioa mwili wangu niungue moto kama sina upendo hainifai kitu” (1Wakorinto 13:1-3).

“Upendo” hapa una maana ya Yesu aliyekuja kwa maji, damu na kwa Roho. Katika Biblia neno “upendo” mara zote kumaanisha “ile kweli ya upendo” (1Wathesolanike 2:10). Ukweli ni kwamba upendo wa Mungu ulidhihirika kupitia Mwana wake wa pekee (1Yohana 4:9).

Page 165: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

165 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Ni Yule Tu Anayeamini Katika Maji Na Kwa Damu Ataweza Kuushinda Ulimwengu.

Ni nani anayeweza kushinda Ulimwengu?

Ni wale wenye kuamini katika ukombozi wa Ubatizo wa Yesu na Damu yake na kwa Roho.

1Yohana 5:5-6 inasema “Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu , Yesu Kristo; si katika maji tu bali katika maji na katika damu. Yesu Kristo.”

Wapendwa Wakristo, Aliyeweza

kumshinda Shetani na ulimwengu ni Yesu Kristo. Wale wenye kuamini neno la maji, damu na Roho la Yesu wanaweza pia kuushinda ulimwengu. Kwa namna gani Yesu aliushinda ulimwengu? Kupitia ukombozi wa maji, damu na kwa Roho.

Katika Biblia “maji” lina maana ya “Ubatizo wa Yesu” (1Petro 3:21). Yesu alikuja duniani katika mwili. Alikuja kuokoa wadhambi wa dunia hii; alibatizwa ili kuzichukua dhambi hizo zote na kufa katika msalaba kulipia dhambi hizo.

Damu katika msalaba ina maana ya ukweli kwamba alikuja ulimwenguni katika mwili alikuja kama mwili ulio na dhambi kuokoa wenye dhambi na alibatizwa kwa maji. Hivyo, Yesu alikuja kwa yote mawili, kwa maji na damu kwa maneno mengine, alichukua dhambi zetu zote za ulimwengu kwa yote, maji ya ubatizo na damu ya kifo

Page 166: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

166 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

chake. Ni kwa namna gani shetani anatawala

ulimwengu? Shetani anasababisha wanadamu kutia shaka juu ya Neno la Mungu na kupanda mbegu ya uasi mioyoni mwao. Shetani hujaribu kubadilisha watu kuwa watumishi wake kwa kuwalaghai ili wasitii neno la Mungu.

Ingawa, Yesu alikuja duniani na kufuta kabisa dhambi zote kwa maji ya ubatizo wake na kwa Damu yake katika Msalaba; Alimshinda shetani na kufuta dhambi zote za ulimwengu.

Hii hutokea kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa Mwokozi wa wenye dhambi. Amekuwa Mwokozi wetu aliyekuja kwa maji na kwa damu.

Yesu Alizichukua Dhambi zote za Dunia kwa Ubatizo wake wa Ukombozi.

Nini maana ya Yesu Kuushinda Ulimwengu?

Aliushinda Ulimwengu kwa

Kuzichukua dhambi zake zote.

Tangu abatizwe ili kuzichukua dhambi

zote za ulimwengu na kufa ili kuzilipia, anaweza kutukomboa kwa dhambi zetu zote. Sababu Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu katika mto Yordani ilikuwa ni kuzifanya dhambi zetu zote ziwe juu yake badala yetu. Yesu alitoa maisha yake msalabani kwa mshahara

Page 167: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

167 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

wa dhambi. Alimshinda Shetani kwa kifo na ufufuo. Alilipa mshahara wa dhambi zote kwa kifo chake.

Yesu alikuja kwa wenye dhambi katika maji ya Ubatizo wake na Damu katika Msalaba.

Kwa namna gani alishinda Nguvu za shetani?

Kwa ubatizo, damu na Roho.

Mtume Yohana alisema, ukombozi si kwa maji tu bali kwa yote mawili, maji na damu. Hivyo, kama ilivyo Yesu kuchukua dhambi zetu zote na kuzifuta milele, wenye dhambi

wote wataokolewa kwa kumwamini yeye, na kuwa waaminifu kwa maneno yake.

Yesu alipokuja ulimwenguni, hakuzichukua dhambi zetu tu, bali pia alizilipia kwa damu yake katika kifo cha msalaba. Alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake pale Mto Yordani na kuzilipia katika msalaba kwa kifo chake. Sheria ya haki ya Mungu inasema “mshahara wa dhambi ni mauti” (Waruni 6 : 23) ilitimizwa.

Sasa, nini maana ya Yesu kuushinda ulimwengu? Imani inayoushinda ulimwengu ni ile imani juu ya Injili ya ukombozi ambao Yesu alituletea kwa maji na damu. Alikuja akiwa na umbo la mwili na kushuhudia wokovu kwa ubatizo wa maji na kifo chake msalabani.

Yesu aliushinda ulimwengu, kwa jina shetani. Wafuasi wa Kanisa la kwanza walisimama kidete mbele ya kufia dini bila

Page 168: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

168 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

kujisalimisha kwa utawala wa Warumi au kwa aina zote za vishawishi vya ulimwengu.

Hii yote ni matokeo ya imani zao kwa Yesu aliyekuja kwa maji (alibatizwa kwa kuzichukua dhambi zote) na kwa damu yake Msalabani (alizilipia dhambi zote kwa kifo chake).

Yesu alikuja katika Roho (alikuja kwa mwili wa mwanadamu) na kuzichukua dhambi zote za wenye dhambi kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani ili sisi sote tuweze kukombolewa na tuweze kuushinda ulimwengu.

Upo mfano wa Mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoaa ninyi pia siku hizi; kwa kufufuka kwake Yesu Kristo (1Petro 3:21)

Ni upi mfano wa wokovu?

Ni ubatizo wa Yesu. 1Petro 3:21 inasema “Mfano wa mambo

hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.” Mtume Petro anadhihirisha kwamba Yesu alikuwa mwokozi na kwamba alikuja kwa maji ya ubatizo na damu.

Matokeo yake yatupasa kumwamini Yesu aliyekuja kwa maji na damu. Yatupasa pia

Page 169: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

169 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

kujua ya kwamba maji ya ubatizo wa Yesu ni mfano wa wokovu. Mtume Petro alitueleza kwamba “maji” ya ubatizo, damu na Roho “ni vyanzo hakika” vya ukombozi wetu.

Wanafunzi wa Yesu waliamini damu katika msalaba uliotokana na ubatizo wa Yesu. Kuamini damu pekee ni kushikilia nusu ya imani ya kweli. Imani iliyo upande mmoja au ukweli usio kamilika hufifia kwa muda. Kwa hakika wale wenye Imani katika Injili ya maji, damu na kwa Roho watakuwa, imara kwa muda wote.

Sauti ya Injili ya kwa damu tu, inaendelea kukua duniani nyakati hizi. Kwa nini hivi? Watu hawajui ukweli wa Neno la Mungu, ukombozi wa maji na kwa Roho, hivyo hawawezi kuzaliwa upya.

Wakati fulani, Kanisa katika Mashariki ya mbali liliangukia katika imani za kichawi. Walionekana kustawi kwa muda, lakini

watumishi wa shetani walisaidia kugeuza imani kuwa uchawi.

Uchawi ni kuamini kwamba shetani atakimbia ikiwa utachora msalaba katika kipande cha karatasi au kutengeneza msalaba wa mbao, na shetani atafukuzwa ikiwa mtu ataikiri imani yake juu ya damu ya Yesu. Shetani atadanganya kuwa ameogopa damu, kwa kusema Yesu alichoweza kukifanya kwa wenye dhambi ni kumwaga damu yake msalabani tu.

Ingawa Petro na wafuasi wengine walishuhudia Injili ya kweli ya Ubatizo wa Yesu na kwa damu katika msalaba. Lakini ni nini Wakristo wa nyakati hizi wanacho shuhudia? Hushuhudia damu ya Yesu tu.

Yatupasa kuamini maandiko katika Biblia na kuwa imani ya wokovu katika Roho, kwa ubatizo wa Yesu, na kwa Damu yake. Ikiwa tutapuuzia ubatizo wa Yesu na kushuhudia

Page 170: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

170 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

ukweli wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu msalabani pekee, wokovu wetu hautakamilika kamwe!

“Neno la ushuhuda” Wokovu wa Mungu katika Maji.

Upo ushahidi gani kwamba Mungu ametuokoa?

Maji, damu na kwa Roho. Katika 1Yohana 5:8, Bwana anasema

“Kwa maana wako watatu washuhudiao duniani” Kwanza ni Roho, pili ni Maji ya ubatizo wa Yesu, na tatu ni damu yake msalabani. Vyote hivi vitu vitatu ni kimoja Yesu alikuja duniani kutuokoa sisi sote toka

dhambini. Yeye akiwa mmoja alifanya yote haya matatu, ubatizo, damu na kwa Roho.

“Kwa maana wako watatu washuhudiao.” Yapo mambo matatu yatupayo uhakika kwamba Mungu ametuokoa nayo ni Maji ya ubatizo wa Yesu, damu yake na kwa Roho. Mambo haya matatu aliyatimiza Yesu kwa ajili yetu hapa duniani.

Ikiwa moja kati ya haya matatu itatolewa wokovu hautakamilika. Kwa maana wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na Damu.

Yesu Kristo aliyekuja kwetu katika mwili ni Mungu, Roho na Mwana wa Mungu. Alikuja duniani kama Roho ndani ya mwili wa mwanadamu na kubatizwa na maji ili kubeba dhambi zote za ulimwengu. Alichukua dhambi zote mwilini mwake na kutuokoa sisi wenye dhambi kwa damu yake msalabani. Alilipa madhambi yetu yote. Ni

Page 171: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

171 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Injili ya ukombozi kamili katika maji, damu na kwa Roho.

Ikiwa moja kati ya haya itatolewa, itakuwa sawa na kuuukataa wokovu wa Mungu, aliotuokoa sisi sote toka dhambini. Kama tungekubaliana na wingi wa wanaoamini katika nyakati hizi, tungeweza kusema “Wapo wawili washuhudiao duniani damu na Roho.”

Lakini mtume Yohana alisema wapo watatu washuhudiao duniani; maji ya ubatizo wa Yesu, damu katika msalaba na Roho. Mtume Yohana ameweka wazi juu ya ushuhuda huu.

Imani inayo mkomboa mwenye dhambi ni imani katika Roho, maji na damu. Ni imani gani inayomwezesha mtu kuushinda ulimwengu? Na ni wapi yaweza kupatikana? Ni katika Biblia. Ni kuamini Yesu aliyekuja kwa maji, damu na kwa Roho. Uwe na imani

hiyo ili upokee Wokovu na Uzima wa milele.

Je, wokovu wa Mungu unaweza Kukamilika bila ubatizo wa Yesu?

La! Hautoweza

Hapo mwanzo kabla sijaokoka, nami pia

nilikuwa Mkristo aliyeamini kwamba ni damu tu katika msalaba na Roho, ndivyo viletavyo wokovu. Niliamini kuwa Yesu alikuja kama Roho na kufa kwa ajili yangu msalabani ili kuniokoa toka dhambi zangu. Niliamini hayo mambo mawili tu na nikawa mpotofu kwa kufikia hatua ya kuhubiri kwa watu.

Nikuwa na mpango wa kusomea Theologia na kuja kuwa Mmisionari ili nifanye kazi hadi mwisho wa maisha yangu kwa ajili ya roho zipoteazo kama Yesu.

Page 172: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

172 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Niliweka malengo makubwa. Lakini, kwa kuwa niliamini mambo hayo

mawili tu, palikuwa na dhambi moyoni mwangu ikiendelea kuwepo. Matokeo yake, sikuweza kuushinda ulimwengu. Sikuweza kuwa huru toka dhambini. Nilipoamini mambo hayo mawil tu,damu na Roho, nilibaki na dhambi moyoni mwangu.

Sababu iliyonifanya kuwa na dhambi moyoni mwangu, ingawa nilimwamini Yesu, ilikuwa kwamba sifahamu juu ya maji, ubatizo wa Yesu. Uponyaji wangu haukukamilika hadi pale nilipokombolewa kwa imani iliyokamili katika maji ya ubatizo wa Yesu, damu na Roho.

Sikuweza kushinda dhambi za mwili kwa kuwa sikufahamu maana ya ubatizo wa Yesu. Hata wengi wenu mnamwamini Yesu, huku mkiendelea kutenda dhambi za mwilini. Watu bado wanaendelea na dhambi

ndani ya miyoyoni mwao na kujaribu bila mafanikio kwa kuhuisha upendo wao wa kwanza waliokuwa nao kwa Yesu.

Hawawezi kuhuisha matamanio yao ya kwanza ya shauku kwa sababu hawajatakaswa kikamilifu na dhambi zao kwa maji. Hawajagundua kwamba dhambi zao zote zilibebwa na Yesu pale alipobatizwa, na hawatoweza kupata imani yao tena baada ya kuanguka.

Napenda kuweka bayana kwenu nyote juu ya hili. Tunaweza kuishi kwa imani na kuushinda ulimwengu ikiwa tu tutamwamini Yesu. Ijapokuwa hatujitoshelezi, haijalishi ni mara ngapi mara kwa mara tunaanguka dhambini tuwapo duniani, ikiwa tutamwamini Yesu kama Mwokozi wetu, aliyetufanya wakamilifu kwa kuwa huru na dhambi kwa ubatizo wake na kwa damu yake, hakika tutasimama kuwa washindi

Page 173: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

173 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

daima. Kamwe haitojalisha ikiwa tutamwamini

Yesu pasipo maji ya ubatizo wake, hatutoweza kukombolewa kabisa. Mtume Yohana ametueleza kwamba imani yenye kuushinda ulimwengu ni imani ile yenye kumwamini Yesu Kristo, aliye kuja kwa maji ya ubatizo, damu na kwa Roho.

Mungu alimtuma mwana wake wa pekee kuokoa wale wote wenye kuamini ubatizo na damu yake. Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Yesu, mwana wa pekee wa Mungu, alikuja kwetu kwa Roho (katika mwili wa mwandamu). Na baadaye kuitoa damu yake msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zetu. Hivi ndivyo alivyo wakomboa wandamu wote kwa dhambi.

Imani ituongozayo kuushinda ulimwengu huja kwa kuamini ukweli kwamba Yesu alikuja kwa maji, damu na kwa Roho,

ambayo kwa hakika itatuweka huru na dhambi kikamilifu na daima.

Ikiwa hakuna maji ya ubatizo ya damu kwa msalaba, basi pasingekuwa na wokovu wa kweli. Ikikosekana moja kati ya hayo yaliyo matatu hakuna ukamilifu na wokovu wa kweli. Wokovu wa kweli ni kuamini maji, damu na kwa Roho. Ujue hili na utakuwa na imani ya kweli.

Page 174: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

174 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Nawaeleza ya kwamba hapatokuwa na wokovu wa kweli pasipo ushuhuda wa Maji, Damu na kwa Roho.

Ni mambo gani matatu yaliyo muhimu yabebayo ushuhuda

wa wokovu?

Maji, Damu na Roho. Mtu anaweza kufikiri juu ya swali hilo

hapo juu kwamba. “Yesu ni mwokozi wangu. Naamini damu yake msalabani na niko tayari kufa kama shahidi. Namwamini Yesu ingawa nina dhambi moyoni. Nimetubu kwa makini na kuwa mwangalifu kwa matendo mema haki na kujitoa kila siku. Nimetoa maisha yangu na tamaa zote za dunia hii kwako

Yesu. Nimekuchagua wewe na kuacha ndoa. Itawezekana vipi Mungu kutonitambua? Yesu alikufa kwa ajili yangu msalabani. Mungu wetu Mtakatifu alikuja kama mwanadamu na kufa msalabani. Nakuamini, najitoa kwa ajili yako, natenda mema kwa uaminifu kwa ajili yako. Ingawa sina thamani na bado mwenye dhambi moyoni, Je, Yesu utanihukumu kwenda motoni? Hapana, sidhani.”

Wapo wengi wenye kufikiri namna hii. Hawaamini yakwamba Yesu alibatizwa ilikuzichukuwa dhambi zote za ulimwengu. Je, Wakristo hawa wa jina, wanaoamwamini Yesu hali mioyoni mwao ni wenye dhambi, wanapo kufa, watakwenda wapi? Watakwenda motoni. Niwenye dhambi tu!

Wapo wengi wenye kufikiri namna hii na kudhani Mungu anafikiri hivyo pia, wataishia motoni. Zaidi ya hayo wengine baadhi yao

Page 175: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

175 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

husema ya kwamba kwa kuwa Yesu alizichukuwa dhambi zote alipokufa pale msalabani, basi hakuna dhambi tena duniani. Ingawa hii ni kuzungumza juu ya damu na Roho pekee. Hii si imani kwa kweli itakayo waongoza watu katika ukombozi ulio kamili.

Yatupasa kuamini kwamba Yesu alichukuwa dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, alihukumiwa na kufa msalabani kwa ajili yetu, na akafufuka siku ya tatu, baada ya kifo chake.

Bila imani hii, ukombozi usingewezekana. Yesu Kristo alikuja kwetu kwa ubatizo, damu na Roho. Alichukuwa dhambi zote za ulimwengu.

Yapo mambo muhimu matatu yenye kushuhudia juu ya wokovu wake hapa duniani, Roho, maji na damu.

Kwanza; “Roho” Mtakatifu hushuhudia

Yesu ni Mungu na alikuja katika mwili. Pili; “Maji” hushuhudia ubatizo wa Yesu

katika mto Yordani kwa Yohana Mbatizaji kupitia kwake dhambi zetu zote alimtwika Yesu. Dhambi zetu alizibeba Yesu alipobatizwa (Mathayo 3:15).

Tatu; “Damu” inasimama kama Yesu kukubali kujitoa kwa hukumu ya dhambi zetu. Alikubali ili afe kwa hukumu ya Mungu Baba na alifufuliwa siku ya tatu ili kutupa uhai mpya.

Mungu Baba alimtuma Roho ndani ya mioyo ya wale wote wenye kuamini ubatizo na damu ya mwana wake ili aweze kushuhudia ndani yao juu ya ukombozi.

Wale wote waliozaliwa upya wana neno ndani yao lenye kuushinda ulimwengu. Waliokombolewa watamshinda Shetani, uongo wa manabii, walaghai, vikwazo au misukosuko ya ulimwengu ambayo haiachi

Page 176: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

176 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

kushambulia. Sababu ya kuwa na nguvu hii ni kwamba, tuna ushuhuda wa yale mambo matatu ndani ya mioyo yetu; Maji ya Yesu, Damu yake na Roho.

Tunaweza kumshinda Vipi shetani?

Kwa kuamini ushuhuda Wa mambo matatu.

Tunaweza kumshinda shetani na

ulimwengu kwa kuwa tunaamini katika Roho, maji na Damu. Wale wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu wana uweza wote wa kuushinda ulimwengu na vishawishi vya manabii wa uongo kwa nguvu hizi zitokanazo na maji, damu na Roho. Je, unaamini hili?

Haiwezekani kuzaliwa upya au kuushinda

ulimwengu ikiwa huna imani katika ukombozi utakanao na ubatizo wa Yesu, Damu yake na kuamini Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi. Je, Imani hii imo ndani ya moyo wako?

Je, unayo Roho na maji ndani ya moyo wako? Unaamini kwamba dhambi zako zote alibeba Yesu? Je, unayo damu ya msalabani moyoni mwako?

Utaushinda ulimwengu ikiwa utakuwa na imani katika maji na katika damu ya Yesu ndani ya moyo wako. Ikiwa unaamini Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako na kubeba hukumu kwa ajili yako utaushinda ulimwengu.

Mtume Yohana aliushinda ulimwengu kwa sababu alikuwa na yote haya yaliyo muhimu ndani ya moyo wake. Pia alizungumzia juu ya ukombozi kwa ndugu zake kwa imani walistahimili vikwazo na vitisho katika

Page 177: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

177 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

huduma zao. Yesu alikuja kwa Roho, maji na damu. Kwa jinsi alivyoushinda ulimwengu hata sisi pia kwa wale walio waaminifu tutaushinda. Hii ndiyo njia pekee kwa waaminifu kuushinda ulimwengu.

Katika 1Yohana 5:8 inasema “Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Wengi bado huzungumzia juu ya damu na Roho tu wakiacha maji ya ubatizo wa Yesu. Ikiwa wataacha habari ya maji, bado watandelea kudanganywa na shetani. Wanapaswa kuacha upotovu wao na kutubu na kuamini maji ya ubatizo wa Yesu katika kuzaliwa upya.

Hakuna yeyote mwenye kuushinda ulimwengu bila kuamini maji na damu ya Yesu. Nasema tena, hakuna! Yatupasa kupigana kwa kutumia maji na damu ya Yesu kama silaha nzito na kali za kiroho.

Neno lake ni upanga wa Roho, Nuru. Wapo wengi wasioamini ubatizo wa Yesu

ulichukua dhambi zetu zote. Wapo wengi wenye kuamini mambo mawili tu. Hivyo, Yesu anapowaeleza “amka na uangaze”, hawawezi kuangaza kwa vyovyote vile. Bado wanazo dhambi mioyoni mwao. Ingawa wanamwamini Yesu, lakini bado watakwenda motoni.

Page 178: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

178 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Injili ya Ubatizo na Damu ya Yesu bila shaka ndiyo Inayoshuhudia ili watu wasikie, waamini na kuokolewa.

Je, Imani katika ubatizo wake ni aina ya mafundisho ya

kawaida katika kanuni?

Si mafundisho ya kanuni Ni ukweli.

Tunaposhuhudia juu ya Injili, inapasa iwe

hakika. Yesu alikuja kwa Roho, kwa ubatizo (uliozichukua dhambi zetu zote) na kwa damu (iliyolipia dhambi zetu zote) Yatupasa kuamini yote haya matatu.

Kinyume chake, basi hatujahubiri Injili bali ni dini ya kawaida tunahubiri. Wakristo

wengi nyakati hizi huchukulia Ukristo ni aina ya dini kama dini nyingine, lakini Ukristo hauwezi kuwekwa katika hadhi ya dini. Ni imani ya ukombozi uliojengeka katika msingi wa ukweli wa kumtumaini Mungu. Hauwezi kuwa dini.

Dini ni kitu kilichoanzishwa na mwanadamu, hali imani ni kumtumaini Mungu atupaye wokovu. Hii ni tofauti yake halisi. Ikiwa utapuuzia ukweli huu, utauona Ukristo kama dini nyingine tu na kuhubiri kwa njia ya ustaarabu na kanuni za wanadamu zilizo njema kwa wanadamu.

Yesu Kristo hakuja kuanzisha dini ulimwenguni. Hakuwahi anzisha dini inayoitwa Ukristo. Kwa nini unaamini kuwa ni dini? Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa nini basi usiamini dini ya Budha badala yake? Unadhani nimekosea kusema hili?

Baadhi ya watu humwamini Yesu kama

Page 179: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

179 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

njia ya dini maishani mwao, na wakiishi wakisema tofauti iko wapi? Mbinguni Nirvana, Paradiso… Yote sawa tu, tofauti ni majina. Tutaishia sehemu moja kwa vyovyote.

Wapendwa Wakristo, yatupasa kusimama imara katika kweli, Yatupasa “kuamka na kuangaza” ndipo tutaweza kuhubiri kweli bila kusita.

Wakati wengine wanaposema “Hiyo haiwezi kuwa ndiyo njia pekee kwenda mbinguni” yakupasa ujibu kwa sauti ya uhakika “Ndiyo! Hakika ni njia pekee. Unaweza kwenda mbinguni ikiwa tu utamwamini Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji, damu na Roho.” Yakupasa uangaze kwa nuru ili roho nyingine ziweze kusikia Neno la ukombozi kwa kuzaliwa upya na kwenda mbinguni.

Uwe na imani sahihi. Wapendwa wasiomrudia Yesu ambao hawafahamu ukombozi katika ubatizo wa Yesu na Damu yake wataangamia.

Ni nani wataangamia hata Ikiwa wanamwamini Yesu?

Wale wote wasioamini

Ubatizo wa Yesu. Kudai kwamba unamwamini Yesu pasipo

kuwa na sababu ya msingi na ya kweli ni sawa kutorudia upendo wa Yesu na kuwa na njia fupi ya kuwa mkristo wa dini.

Meli ilipita katikati ya Bahari ya Pasifiki na kuzama, waliokoka watu wachache huku wakielea juu ya mabaki ya vipande vyake

Page 180: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

180 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

vilivyo vunjika. Wakatuma taarifa kwa alama ya kuomba msaada kwa meli nyingine zilizo mbali na pale, lakini kwakuwa bahari ilichafuka kwa mawimbi haikuweza kufikia meli nyingine zilizo mbali na pale. Hatima yake ndege ya ilifika na kuwashushia kamba ya kukwea. Ikiwa mmoja kati yao angeishika kama ile kwa mikono yake badala ya kuifunga kiunoni itakuwa ni sawa na kuanguka mbali na Upendo wa Yesu; kumwamini Mungu kwa namna yake. Hajawa salama bado, lakini atasema “Naamini Niokoe Naamini, hivyo nafikiri nitaokoka.”

Asiyefahamu kweli ya ubatizo wa Yesu na Damu yake hudhani ataokoka kwa kushikilia kamba.

Lakini atakapo vutwa juu, mikono yake italegea kushika kamba baada ya muda. Ni mbali kwake kufika ufukweni akiwa

amening’inia kwa kushika kamba hiyo kwa nguvu zake. Nguvu zitakapomwishia ataachia na kutumbukia baharini tena.

Kutokurudisha Upendo kwa Yesu ni sawa na hili la kurushiwa kamba, badala ya kuifunga kiunoni unashikilia kwa mikono kwa kutumia nguvu zako ambazo baada ya muda zitachoka. Wengi mnaweza kusema mnamwamini Mungu na Yesu; na kuamini Yesu aliyekuja katika Roho, lakini hii ni sehemu tu ya mlingano wa yale mambo matatu. Wanaweza wasiamini kweli na wasiwe ndani ya Injili, hivyo kujilazimisha kusema wanamwamini Yesu.

Kuamini na kujaribu kuamini ni mambo tofauti. Wanasema watamfuata Yesu hadi mwisho, lakini katika siku ya mwisho watatupwa kando kwa kuwa na dhambi zilizobaki ndani ya mioyo yao. Wanampenda Yesu bila kuelewa kuwa alikuja kwa ubatizo,

Page 181: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

181 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

damu na kwa Roho. Ikiwa watampenda Yesu kwa damu yake tu, watakwenda motoni.

Funga moyo wako kwa kamba ya Injili ya kweli, Injili ya maji na damu. Yesu anapokushushia kamba ya wokovu wale watakao jifunga viunoni kwa maji, damu na kwa Roho wataokoka.

Yule mwokoaji katika ile ndege alipaza sauti kwa kuwaambia “tafadhali sikilizeni kwa makini, nitakapotupa kamba kwenu chukueni na mzifunge kuzunguka kati ya makwapa katika sehemu ya kifua. Na msubiri hapo mlipo. Usining’inie kwa kamba kwa kutumia mikono yako kuishika bali mfunge kuzunguka vifua vyenu na mtulie. Na hapo mtachoka.”

Mtu wa kwanza akafuata maelekezo vyema na kujifunga kamba ile na akaokolewa. Lakini yule mwingine akasema,

“Usitie shaka. Mimi ni mwenye nguvu. Nafanya mara kwa mara mazoezi ya viungo. Hebu angalia misuli yangu! Unaona? Naweza kuning’inia maili nyingi tu.” Hivyo alishikilia ile kamba kwa mikono yake na kamba ilianza kuvutwa.

Wote wawili walivutwa. Lakini tofauti ilikuwa kwamba yule aliyefuata maelekezo alijifunga kuzunguka mwili wake kifuani bila ya kutumia nguvu zake katika kuning’inia. Ilifika wakati hata kujisahau ingawa aliendelea kuning’inizwa na kamba.

Yule mwenye majigambo ya nguvu zake baada ya muda alishindwa kung’ang’ania kamba kwa sababu kungu za mikono zilimwishia. Alikufa kwa sababu hakupenda kusikiliza na kufuata maelekezo.

Ili kupata ukombozi ulio kamili, yakupasa kuamini ukombozi wa maji ya ubatizo wa Yesu, na damu inayo okoa roho zote toka

Page 182: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

182 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

dhambini. Wokovu unapatikana kwa wale tu wenye kuamini kwa moyo wao wote neno; “nimekuokoa kikamilifu kwa ubatizo wangu kwa Yohana Mbatizaji na damu yangu katika kifo kile cha msalaba.”

Wale wenye kuamini damu tu, husema “usiwe na wasiwasi, ninaamini. Nitaishukuru damu ya Yesu tu hadi mwisho. Nitamfuata Yesu hadi mwisho wa maisha katika damu yenye kutosha kuushinda ulimwengu na dhambi zote maishani mwangu.”

Ingawa hii haitoshi. Wale Mungu anaowakubali kuwa watu wake ni wale wenye kuamini ushuhuda wa yale matatu: Yesu aliyekuja katika Roho, na alibatizwa (kwa kuzichukua dhambi zote katika mto Yordani kwa ubatizo wake) na alikufa katika msalaba kulipia gharama ya dhambi zote, na alifufuka siku ya tatu toka kifoni.

Roho Mtakatifu huja kwa wale tu wenye

kuamini mambo hayo matatu yanayoshuhudiwa. “Ndiyo, mimi ni mwokozi wako. Nimekuokoa kwa maji na damu. Mimi ni Mungu wako.”

Kwa watu wasioamini yote matatu, Mungu haweze kuwapa wokovu. Hata ikiwa ni moja, Mungu anasema “Hapana, bado hujaokoka.” Wale wafuasi wa Yesu waliamini yote matatu. Yesu anasema kwamba ubatizo wake ni mfano wa wokovu na damu yake ni hukumu.

Page 183: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

183 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Mtume Paulo na Petro nao pia walishuhudia vyote, ubatizo na Damu ya Yesu.

Wanafunzi wa Yesu walishuhudia nini?

Ubatizo wa Yesu na

Damu yake.

Je, Mtume Paulo aliongelea juu ya ubatizo wa Yesu? Hebu na tuone alizungumzia hili mara ngapi juu ya ubatizo wa Yesu. Amesema katika Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Na katika 6:5 “Kwa maana kama mlivyo unganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa

kufufuka kwake.” Alisema pia katika Wagalatia 3:27 “Maana

ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” Mitume wa Yesu wote walishuhudia juu ya “maji” ubatizo wa Yesu. “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1Petro 3:21).

Wokovu wa ukombozi wa Bwana ulikuja kwa Maji na kwa Damu ya Yesu.

Ni nani anayeitwa mwenye haki na Mungu?

Wale wote wasio na dhambi mioyoni mwao.

Page 184: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

184 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Ukombozi ambao Yesu alimwekea mwanadamu ni wa maji ya ubatizo wake na damu yake katika msalaba. Kwa ukombozi huo twaweza kuamka na kuangaza. Kwa namna gani? Kwa kushuhudia haya matatu.

“Ondoka; uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa Bwana umekuzukia” (Isaya 60:1). Mungu ametuangazia na kutuambia tuangaze pia. Yatupasa kutii amri hii.

Tumekuwa tukihubiri Injili kwa nguvu zetu zote. Ijapokuwa watu wengi bado hawasikilizi. Amini Yesu na utakombolewa. Utakuwa mwenye haki. Ikiwa dhambi bado itaendelea kuwepo ndani ya moyo wako bado hujawa mwenye haki. Bado hujaishinda dhambi za Ulimwengu.

Huwezi kuachana na dhambi ndani ya moyo wako ikiwa huamini juu ya maji ya Yesu (ubatizo wake) Huwezi kamwe kuzuia

hukumu ikiwa huamini juu ya damu ya Yesu. Huwezi kuokolewa ikiwa huamini juu ya Yesu Kristo, aliyekuja kwa Roho. Huwezi kukamilika kuwa mwenye haki kama hutaamini mambo haya matatu yashuhudiayo.

Haki isiyojitosheleza ina pelekea kupatikana kwa aina fulani nyingine ya haki. Ikiwa mtu yeyote atasema bado ana dhambi, lakini bado anajichukulia ni mwenye haki, basi mtu huyu bado hajawa ndani ya Yesu. Watu wengine siku hizi hujaribu kusimamia kwa muda katika ukombozi kwa kupitia aina fulani ya haki. Wameandika makala nyingi zisizo na maana juu ya somo la haki.

Je, Mungu humwita mtu kuwa asiye na dhambi ikiwa bado mtu huyo ana dhambi? Hakika hafanyi hivyo. Humwita mtu jinsi alivyo. Ni Mwenyezi hawezi kudanganya.

Page 185: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

185 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Watu hawaelewi maana halisi ya haki. Tunaita kitu fulani “safi” ikiwa tu ni kisafi. Hatuwezi kusema “mwenye haki” ikiwa bado pana dhambi.

Unaweza kufikiri ya kwamba unaweza kuitwa mwenye haki na Yesu ingawa una dhambi moyoni, lakini bado si sahihi.

Yesu hutuita wenye haki ikiwa tu, tutamwamini yeye kama ndiye aliye kuja katika Roho, maji (kwa ubatizo wake alizibeba dhambi zetu zote) na kwa Damu (kwamba alikuja katika mwili na kufa kwa ajili yetu).

Wapendwa Wakristo, hizi aina fulani za haki hazina cha maana dhidi ya Injili ya maji na damu. Aina hizi za haki au kuitwa mwenye haki ikiwa bado unadhambi ndani ya moyo wako hakika haitowezekana. Haijalishi ni kwa kiasi gani mtu huyu aweza kumwamini Yesu, Yesu hawezi kudanganya.

Je, bado unaweza kufikiri Mungu anaweza kumwita mtu fulani mwenye haki ikiwa ana dhambi moyoni? Hivyo ndivyo watu wadhaniavyo, si Mungu. Mungu hapendi uongo. Je anaweza kukuita mwenye haki ikiwa utaamini “maji” na “damu” tu? Kamwe!

Yupo mtu wa aina moja Mungu anaweza kumwita mwenye haki. Ni yule tu asiye na dhambi moyoni mwake. Anawatambua wale wenye kuamini mambo matatu! Yesu aliye Mungu aliyekuja ulimwenguni katika mwili, akabatizwa mto Yordani na kutoa damu yake msalabani ili kufuta dhambi zetu zote.

Ni wale tu, wenye kuamini habari njema ya ukombozi ndiyo wenye kutambuliwa kuwa wenye haki na Mungu. Ni walio na imani sahihi, moja kwa moja wanaamini yote Yesu aliyotufanyia. Wanaamini kuwa Yesu alikuja, alibatizwa ili kuchukua dhambi zetu zote, alihukumiwa kwa ajili yetu na kufa

Page 186: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

186 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

msalabani na akafufuka kutoka mauti. Yote haya yalifanyika kwa upendo wa

Mungu. Yesu alikuja ulimwenguni akitokea mbinguni. “Njooni kwangu ninyi, nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Alifanya haya kwa kuyachukua madhambi yetu yote.

Mungu hawatambui wale wenye kuamini damu ya Yesu pekee. Wale wenye kuamini damu ya Yesu bado wana dhambi mioyoni mwao. Ni nani Yesu huwatambua kuwa wamekombolewa?

Amini ubatizo wa Yesu, damu yake na ukweli kwamba yeye ni Mungu yote haya ni muhimu kwa wokovu “Nimechukua dhambi zako zote nilipo kuja ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Nashuhudia kwamba dhambi zote za dunia zimetwikwa kwangu. Nimelipa dhambi hizo msalabani.

Kwa hayo nimekuokoa.” Kwa wale wenye kuamini mambo haya

matatu Yesu anasema “Ndiyo umeokoka. Ni mwenye haki na mtoto wa Mungu” wewe nawe waweza kuokoka ikiwa utaamini ubatizo wa Yesu damu yake na Roho kwa pamoja. Wenye kuamini damu na Roho pekee bado wanadhambi mioyoni.

Katika ufalme wa Mungu upo ukweli tu. Ipo haki, ukweli, upendo na rehema. Hakuna kusema uongo. Uongo na hila haupo Mbinguni.

Ni nani asiyetenda haki?

Yule asiye amini ubatizo wa Yesu.

“Wengi wataniambia siku ile Bwana,

Page 187: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

187 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?” (Mathayo 7:22)

Mungu hawatambui kazi hizo za watu kuwa ni halali kuingia katika ufalme wake “Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (7:23).

“Nimekutolea nyumba mbili. Nimekutolea maisha yangu. Sijakukana maishani mwangu hadi mwisho wa pumzi ya mwisho. Hukuniona?”

“Je, una dhambi moyoni?” “Ndiyo, Bwana. Nina ninazo kidogo.” “Basi, uondoke mbele zangu! Hapana

mwenye dhambi aliye ruhusiwa kuwa mbele zangu.”

“Lakini nilikufa kama shahidi mfia dini kwa kukuamini wewe Bwana!”

“Una maana gani kufia dini? Ulikufa kwa

huo moyo wako mgumu na ubishi Je, uliutambua ubatizo wangu na damu? Je, nilikukushuhudia moyoni mwako kuwa wewe ni mtoto wangu? Huamini ubatizo wangu na sikukushuhudia kuwa wewe ni mwanangu, na ndiyo maana uling’ang’ana kwa imani yako na kufa kwa hiyo. Je, nilikushuhudia? Uliyaleta kwa nafsi yako unayo amini. Ulijaribu kufanyiza ukombozi wa aina yako mwenyewe. Je, unaelewa? Sasa endelea na njia zako.”

Yesu alituambia tuamke na tuangaze. Waliokombolewa wanaweza kuogopa madhehebu mengi ya Ukristo wa majina na manabii wa uongo, hivyo kushindwa kuangaza vizuri. Lakini dini ya moto yaweza kuanzisha moto mkubwa. Ikiwa mtu atasimama kwa ujasiri na kushuhudia ukweli, dunia yote itaangaziwa.

Katika Isaya 60:1-2 inasema. “Ondoka,

Page 188: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

188 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia, maana, tazama, giza litafunika dunia na giza kuu litazifunika kabila za watu, bali Bwana atakuzukia wewe na utukufu wake utaonekana juu yako.”

Mungu anatuamrisha kuondoka na kuangaza na kuwa nuru. Kwa kuwa giza la uongo, yaani Injili isiyo ya kweli imefunika ulimwengu wote. Ni kwa wale wenye kumwamini Yesu wataweza kunipenda . Wasiokombolewa hawawezi kunipenda ikiwa hawataweza kuamini ukweli wote.

Yapo Mambo Matatu yenye kushuhudia juu ya Wokovu wa wenye dhambi.

Ni upi ushuhuda wa wokovu Ndani ya moyo wetu?

Ubatizo wa Yesu.

“Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Yesu alikuja ulimwenguni na alifanya kazi yake kwa maji na damu. Alifanya haya na kutuokoa.

“Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo

Page 189: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

189 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima asiye na Mwana wa Mungu hana huo uzima” (1Yohana 5:9-12).

Wale waliozaliwa upya hupokea ushuhuda wa wanadamu. Tunatambulika kama wenye haki. Waliozaliwa upya, walio kombolewa, wanaponena ukweli juu ya ukombozi, watu hawawezi kupinga. Hukubaliana nalo. Husema kuwa wameamini vema na wako sahihi kwa imani yao. Tunapowaeleza ni kwa namna gani wamezaliwa upya hakuna awezaye kusimama kinyume na Injili ya kweli tunayo shuhudia. Husema tupo sahihi. Tunapokea ushuhuda wa wanadamu.

Lakini kifungu hicho kusema “ushuhuda wa Mungu mkuu zaidi kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu.” Hapa inasema ushuhuda wa Mungu ni wa Mwana wake. Je, ni sawa? Ni upi ushuhuda wa Mwana wa Mungu? Ushuhuda wa Munngu alituokoa ni ule wa Yesu aliyekuja kwa Roho; kwa maji ya ukombozi na kwa damu yake msalabani. Ushuhuda wa Mungu kwamba hii ndiyo njia aliyotuokoa na ya kwamba sisi ni watu wake kwa kuwa tuna iamini njia hiyo.

“Yeye amwaminiye mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia mwanawe.”

Kifungu hiki kinatueleza zaidi ni yupi aliye kombolewa. Kinasema ni yule amwaminiye Mwana wa Mungu na kuwa na ushuhuda

Page 190: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

190 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

ndani yake. Je, unao ushuhuda ndani yako? Umo ndani yetu sote. Yesu alikuja duniani kwa ajili yetu sote (Alikuja katika mwili kupitia mwili wa Mariamu kwa Roho Mtakatifu) Alipokuwa miaka 30, alibatizwa ili kuchukua dhambi zetu zote na akiwa nazo zote, alihukumiwa msalabani alifufuliwa siku ya tatu ili kutupatia uzima wa milele. Hivi ndivyo Yesu alivyo tuokoa.

Ingekuwa vipi ikiwa asingefufuka? Angeshuhudia vipi kwangu akiwa kaburini? Na ndiyo maana ni mwokozi wangu. Hivi ndivyo tuaminivyo.

Kama alivyosema, alituokoa kwa ubatizo wake na kwa kuwa tunaamini, mimi na wewe tumeokoka ushuhuda umo ndani yangu na ndani yako. Waliokombolewa hawawezi kudharau “maji” ya ubatizo wa Yesu. Hatuwezi kamwe kuondoa mambo aliyofanya ili kutuokoa.

“Hivi ndivyo itupasavyo kutimiza haki zote” (Mathayo 3:15). Kamwe hatuwezi kukana yale yote Yesu aliyofanya ili kubeba dhambi zetu zote katika Mto Yordani alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Waliokombolewa hawawezi kuyakana “maji” ya ubatizo wa Yesu.

Wenye kuamini, lakini Bado hawajakombolewa, hukana ubatizo wa Yesu hadi mwisho

Ni nani amfanyaye Mungu kuwa mwongo?

Yule asiye amini juu Ya ubatizo wa Yesu.

Page 191: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

191 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Alisifu vipi Mtume Yohana aliposema “Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo.” Ikiwa Mtume Yohana angekuwepo leo, angetueleza nini Wakristo? Bila shaka angetueleza ikiwa kwa kupitia ubatizo wa Yesu dhambi zetu alitwaa au la.

Je, Yohana Mbatizaji naye pia hushuhudia juu ya Injili juu ya Yesu kutukomboa kwa ubatizo wake? “Je, dhambi zenu hakujitwika Yesu na hakuzibeba alipobatizwa nami? Hivi ndivyo ukweli ulivyo anapomshuhudia Yesu aliyebatizwa ili kutuokoa sisi sote (Yohana 1:29, 1Yohana 5:4-8).

Wale wasiomwamini Mungu kwa maneno mengine ni wale wasio amini yote aliyofanya kutuokoa na humfanya kuwa mwongo. Tunaposema Yesu alichukua dhambi zetu zote alipobatizwa, wao husema “Hapana! Asingeweza chukua zote! Bali alichukua ile dhambi ya asili tu, hivyo zile zote za kila siku

bado ninazo.” Hivyo huendelea kusisitiza kwamba

inawapasa kuomba sala ya toba ili kuomba msamaha wa dhambi za kila siku ili kuombolewa. Hivi ndivyo walivyo amini. Je, na wewe unaamini hivyo? Yeyote mwenyekuamini ya kwamba dhambi zetu zote hazikutakaswa katika ubatizo wa Yesu anamfanya Mungu ni mwongo.

Page 192: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

192 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Yesu ametukomboa kwa mara moja na kwa wakati wote alipobatizwa na kutoa damu yake Msalabani.

Ni nani aliye Mwongo?

Yule asiye amini Juu ya ubatizo wa Yesu.

Yesu alibatizwa na kuzichukua dhambi

zetu zote kwa mara moja na wakati wote. Mungu huwaokoa wale wote wenye kuamini ubatizo na damua ya Yesu bali huwa mbali na wale wasio amini. Hawa watakwenda motoni. Hivyo, ukiokoka na usipo okoka hutegemea ni lipi unaloamini. Yesu aliukomboa ulimwengu kutoka dhambini. Wenye kuamini wameokolewa wasioamini

bado hawajaikolewa na wanamfanya Mungu kuwa mwongo.

Watu hawaendi motoni kwa dhambi zao, bali kwa kutoamini. “Asiyeamini Mungu amemfanya kuwa mwongo” (1Yohana 5:10) wasioamini ya kuwa dhambi zao zote alibeba Yesu bado watabaki na dhambi mioyoni mwao. Hawawezi kusema hawana dhambi.

Siku moja nilikutana na Shemasi fulani, na kumuuliza “Shemasi, je, dhambi zako zote zilitoka moyoni mwako ulipomwamini Yesu?”

“Bila shaka, zilitoka” alijibu. “Hivyo tangu Yesu azichukue dhambi za

ulimwengu na kusema imekwisha umeokolewa je, hivi ndivyo?”

“Ndivyo.” “Hivyo huna tena dhambi?” “Ndiyo, sina.” “Sasa inatokea nini ukitenda dhambi

tena?”

Page 193: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

193 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

“Sisi ni wanadamu tu. Itawezekana vipi tusitende dhambi? Hivyo inatubidi tutubu kwa kuzisafisha kila siku dhambi hizo.”

Shemasi huyu bado anazo dhambi moyoni kwa kuwa, hajatambua juu ya ukombozi ulio wa kweli.

Watu wa aina hii humfanya Mungu mjinga na mwongo. Je, Yesu aliye Mungu alishindwa kuziondoa dhambi zote za dunia hii? Inasikitisha kwa kweli! Ikiwa Yesu hakuziondoa dhambi zote, basi ataweza vipi kuwa Mungu wa Wokovu? Angeweza vipi kutueleza tumwamini yeye? Je, utakwenda kumfanya yeye kuwa mwongo? Nakushauri usifanye hivyo!

Biblia inatuonya tusimdhihaki Mungu. Maana yake tusimfanye kuwa mwongo na kujaribu kumlaghai. Sivyo alivyo tulivyo sisi.

Mtume Yohana anatueleza kwa hakika juu ya Injili ya ukombozi. Wengi hawaamini

Mungu aliyoyafanya kwetu – ukweli wa Yesu Kristo kuja kwa maji, kwa damu na kwa Roho.

Yapo makundi mawili ya Wakristo; wale wasio amini Biblia isemavyo na kusema “mimi ni mwenye dhambi” na wale wenye kuamini yote Mungu aliyoyafanya kwao kwa kusema “Mimi ni mwenye haki.” Je, ni kundi lipi husema kweli?

Wale wasio amini yale Mungu aliyotafanya kwa usemi mwingine, wasio amini ushuhuda wa maji, damu na kwa Roho ni waongo. Wana imani isiyo ya kweli. Wasio amini humfanya Mungu mwongo.

Usimfanye Mungu kuwa mwongo. Yesu alikuja Mto Yordani na hivyo (kwa kubatizwa) alitimiza haki yote (kwa kuchukua dhambi zote za ulimwengu).

Page 194: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

194 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Wasioamini huukana ubatizo wa Yesu na Utukufu wake.

Ni kipi shetani Anacho kikana?

Ubatizo wa Yesu.

Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Wale waliozaliwa upya huamini kwamba dhambi zao zilitwikwa kwa Yesu alipobatizwa na walikombolewa kwa maji na damu ya Yesu. Huamini kwamba Yesu alizaliwa duniani kupitia Bikira Mariamu, na alibatizwa Yordani kabla ya kufa kwake msalabani na alifufuka.

Wenye haki wanao ushuhuda huu mioyoni mwao. Ukweli wa wokovu umo ndani ya imani juu ya Yesu, aliyekuja kwa maji, damu

na Roho ushuhuda umo ndani yako. Nakushauri uwe na ushuhuda ndani yako. Hakika nakueleza. Utakuwa si wokovu ikiwa hakuna ushuhuda, ukweli wa wokovu ndani yako.

Mtume Yohana alisema “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake” (1Yohana 5:10). Je, kuamini damu yake msalabani tu ndiyo kuwa na ushuhuda? Au maji bila damu? Yakupasa kuamini mambo yote matatu ili utambuliwe na Mungu.

Ni Yesu pekee aweza kukushuhudia kuwa umeokoka Je, unasema waweza kuwa na ushuhuda wa mambo mawili kati ya matatu? Hii ni kuamini Mungu kwa njia yako. Ni ushuhuda wa nafsi yako.

Wapo wengi wa aina hii. Wapo wengi duniani wenye kuamini mawili kati ya yale matatu. Hushuhudia ya kwamba wameokoka

Page 195: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

195 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

na hata kuandika vitabuni juu yake. Ni kwa namna gani walivyo na ulaghai. Ina leta mtafaruku. Hujiita Wainjilisti. Hudhani kuwa si hivyo tu bali pia ni wenye kushika dini” Hawaamini juu ya “maji” na bado hajigamba juu ya wokovu! Wanaweza kueleweka, lakini bado hawana ushuhuda wa Mungu moyoni mwao. Ni wanafiki.

Unaweza vipi kuuita ni wakovu? Wale tu wenye kumwamini Yesu, aliye kuja kwa Roho, maji na damu ndiyo wenye ushuhuda wa Mungu na wanadamu.

Mtume Paulo alisema “ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali katika nguvu na katika Roho Mtakatifu na uthibitifu mwingi (1Wathesalonike 1:5). Shetani hupendezwa na watu wanapo amini damu ya Yesu pekee. Lo! Nyie wajinga sana nimewalaghai!” Wapo wengi wenye kuamini kwamba wanapoisifu damu ya Yesu shetani

hukimbia. Hufikiri Shetani huogopa msalaba pekee. Yakupasa uelewe shetani hugeuka kivuli tu, na yakupasa usidanganyike na hilo.

Mtu aliyepagawa na mapepo hutoa povu mdomoni. Si jambo gumu kwa shetani kufanya atakalo juu ya mtu huyo kwa kuwa anayo nguvu juu yake. Atatumia ujanja kidogo tu. Mungu alimpa shetani nguvu aina zote, isipokuwa nguvu ya kuua. Shetani anaweza kumfanya mtu atetemeke kama unyasi, kupiga mayowe, kutoa povu mdomoni.

Sasa yote haya yanapotokea, waumini hukemea “Toka! Katika jina la Yesu!, Toka! Katika jina la Yesu!” Na mtu huyo anaporudia fahamu zake na kuwa kawaida, humwambia ilikuwa ni kwa nguvu ya damu ya Yesu pekee iliyokuwa na nguvu ya kumuokoa na kumponya. Lakini hii sivyo, si damua ya Yesu pekee. Ni shetani anafunika

Page 196: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

196 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

kwa kivuli tu. Shetani anawaogopa sana wale tu wenye

kumwamini Bwana Yesu, walio safishwa na kuwa safi kwa ubatizo wake, na kuchukua hukumu zao kwa damu yake na baada ya siku tatu alifufuka. Shetani hawezi kuwa karibu na ushuhuda wa ubatizo wa Yesu na wokovu wa damu.

Kama ninavyoelewa Mapadre wa Kikatoliki mara nyingine hufanya huduma ya kutoa pepo wachafu kwa namna hii. Tumeona katika sinema, kwa jina “THE OMEN”, Padre aliyebeba msalaba mdogo wa mbao na kuutikisa, hatimaye alikufa. Aliyezaliwa upya (aliye okoka katika damu na maji) hawezi kushindwa namna hii hata kidogo!

Aliyezaliwa upya ana uhakika anapotaja damu na maji katika Yesu. Shetani anapojaribu kumwogopesha, atamwambia “Je, unajua Yesu alizichukua dhambi zangu

zote?” Ndipo shetani atakapokimbia kwani hapendi hata siku moja kukaa karibu na walio okoka. Aliye okoka akiwa hapo, shetani atajaribu kwa njia zote kumkimbia. Inasemekana wale wasio mwamini Mungu wamemfanya kuwa mwongo. Hawaamini ushuhuda wa mwana wake, juu ya maji na damu yake.

Ushuhuda wa Mwana na Mungu ni upi?

Ubatizo wake, Damu yake

na kwa Roho.

Ni upi ushuhuda wa Mwana wa Mungu? Nao ni huu, alikuja kwa Roho, na kuchukua dhambi zetu zote kwa maji. Alichukua dhambi zote za ulimwengu na kutoa damu yako msalabani kwa dhambi zote. Je, huu

Page 197: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

197 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

siyo ukombozi wa damu, maji na kwa Roho? Watu husema uongo mbele za Mungu

kwa sababu hawaamini Injili iliyo ya kweli katika maji na damu, Injili ya ukombozi kamili. Injili nyingine zaidi ya hii ni ulaghai mtupu! Imani zao ni potofu, na hueneza Injili ya ulaghai bila malengo.

Hebu na turudi katika 1Yohana 5, mstari wa 11 unasema “Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.” Inasema Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu upo kwa yule mwenye kuupokea tu! Nao upo kwa mwanawe.

Wale wenye kupokea uzima wa milele ni wale walio kombolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Wamepokea uzima wa milele ni wale walio kombolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Wamepokea uzima wa milele na kuishi

milele pia. Je, wewe umeupokea? Katika mstari wa 12 “Yeye aliye naye

mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima” kwa namna nyingine, yule anaye amini mambo mwana wa Mungu hana huo uzima.” Kwa namna nyingine, yule anayeamini mambo mwana wa Mungu aliyotenda hapa duniani – Ubatizo wake, kifo chake msalabani na ufufuko wake – unao huo uzima wa milele. Lakini yule anayeondoa hata moja kati ya haya hakika hawezi kupata uzima wa milele na pia ukombozi.

Mtume Yohana aliwatofautisha watu wa Mungu kwa msingi wa Imani ya mambo Yesu aliyofanya, maji, damu na kwa Roho; Haya mambo hutuelezea ikiwa wanalo Neno ndani yao au la! Alibainisha ukombozi kwa imani zao juu ya maji ya ubatizo wa Yesu, damu yake na kwa Roho.

Page 198: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

198 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

Wasiozaliwa upya hawawezi kutambua kondoo kati ya Mbuzi.

Nani awezaye kutambua Waliokombolewa

na wasiokombolewa?

Aliyezaliwa upya.

Mtume Yohana kwa uwazi alionyesha wenye haki waliokombolewa. Mtume Paulo pia. Ni vipi Mtumishi wa Mungu kwa umakini anaweza kutofautisha kati ya watumishi wa Mungu na walaghai? Wale waliokombolewa kwa kuamini katika maji na damu ya Yesu hupokea nguvu ya utambuzi.

Hata ikiwa mtu ni Mchungaji, Mwinjilisti au Mzee wa Kanisa ikiwa anashindwa

kumgundua aliyekombolewa au kutofautisha kati ya kondoo na mbuzi, hakika yeye binafsi hajazaliwa upya bado na hana uzima ndani yake. Lakini wale waliozaliwa upya kweli wanaweza kwa hakika kutofautisha. Wasio na uzima hawawezi kuona tofauti na hata kutambua.

Ingawa hatuwezi kutofautisha rangi gizani, kijani, nyeupe itabaki nyeupe. Lakini pia unapofumba macho, huwezi kuona wala kutambua rangi.

Bali, wale wenye kuangaza macho yao wanaweza bila shaka kuona hata tofauti ndogo ya aina za rangi. Wataweza kutaja ipi kijani na ipi nyeupe. Vile vile upo wazi tofauti kati ya waliokombolewa na wale wasiokombolewa.

Yatupasa kuhubiri Injili ya ukombozi, Injili ya maji, damu na kwa Roho. Yatupasa kuamka na kuangaza. Tunapo kusanya watu

Page 199: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

199 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

na kueneza imani ya kweli, hatuneni maneno yetu. Katika Biblia 1Yohana 5 inatuelezea maana yake. Yatupasa kuelezea hatua kwa hatua ili kusiwepo na mkanganyiko.

Neno tunalo hubiri, yaani Neno la maji, damu na kwa Roho la Yesu ni nuru ya ukombozi. Kufanya “maji” ya Yesu kujulikana kwa watu wote yatupasa tuangaze. Kufanya “damu ya Yesu” ijulikane ni kuangaza. Yatupasa kuifanya ieleweke wazi ili pasiwepo na yeyote duniani asiyefahamu ukweli huu.

Ikiwa walio okoka hawajaamka na kuangaza, basi watu wengi watakufa bila ukombozi na haitamfurahisha Mungu. Atatuita kuwa ni watumishi wavivu. Ni lazima tueneze Injili ya maji na damu ya Yesu.

Unajua kwa nini narudia rudia haya mara

nyingi, ni kwa sababu ubatizo wa Yesu ni muhimu sana kwa wokovu wetu. Tunapoongea na watoto wetu yatupasa kuwaelezea mambo kwa kurudia rudia, kupitia kila jambo muhimu ili wawe na uhakika wa kuelewa.

Ikiwa tunamfundisha mtu asiyejua chochote, yaani mbumbumbu, asiyefika shule, yatupasa kuanza herufi moja baada ya nyingine. Na ndipo kwa hatua tutaweza kumfundisha jinsi ya kuandika maneno kwa herufi. Anapoweza kuweka maneno pamoja kama vile “HUKUMU,” basi tuanze kumueleza nini maana ya neno hilo. Na hii ndiyo sawa na jinsi ya kuwaelezea watu juu ya Yesu ili kuhakikisha wanaelewa kweli.

Yatupasa kwa uwazi kuelezea juu ya ubatizo wa Yesu. Alikuja duniani kwa maji, damu na kwa Roho. Nakuombea ili umwamini Yesu kama Mwokozi na

Page 200: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

200 Yesu Kristo Alikuja kwa Maji, Damu na kwa Roho

kukombolewa. Ukombozi wa maji na Roho hububujika

toka katika imani juu ya ubatizo wa Yesu, Damu yake katika msalaba, na kwa imani kwamba Yesu ni Mungu na Mwokozi wetu.

Page 201: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 7

Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa

wenye dhambi

Page 202: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

202 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa

wenye dhambi

(1Petro 3:20-22) “Watu wasiotii hapo zamani,

uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja siku za Nuhu, Safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache; yaani watu wanane, walio okoka kwa maji. Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu,

amekwenda zake mbinguni. Malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiisha chini yake.”

Kwa njia gani tutaweza Kuwa wenye haki?

Kwa Neema ya Mungu.

Mungu alitutambua kabla ya kuzaliwa kwetu hapa duniani. Alitambua ya kwamba tutazaliwa tukiwa wenye dhambi na kutuokoa wote wenye kuamini kupitia ubatizo wake uchukuao dhambi zote za ulimwengu. Aliokoa wote wenye kuamini na kuwafanya kuwa watu wake.

Haya yote ni matokeo ya Neema ya Mungu. Kama inavyosema Zaburi ya 8:4 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie?”

Page 203: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

203 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Waliokombolewa na kuokolewa toka dhambini ni wapokeaji wa upendo wake wa pekee. Ni watoto wa Mungu.

Tulikuwa vipi hapo awali sisi wenye kuamini damu tu na Roho kabla ya kuwa watoto wa Mungu kabla ya kufanywa wenye haki na kuokolewa kwa kupewa haki ya kumwita Baba? Tulikuwa wenye dhambi, wenye dhambi tu, tuliozaliwa ili tuishi duniani miaka 70 au 80 kama tutakuwa na afya.

Kabla ya kuoshwa dhambi zetu, na kabla ya kuwa na Imani juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake tulikuwa watu wasio haki na wenye uhakika wa kuangamia.

Mtume Paulo alisema ilikuwa ni neema ya Mungu kwake yeye kuwa alivyo sasa. Tunamshukuru Mungu kwa neema yake. Muumba alikuja duniani na kuokoa kutufanya watoto wake, watu wake.

Tunamshukuru kwa neema ya wokovu wa maji na Roho.

Nini sababu inayoruhusu sisi kuwa watoto wake, wenye haki? Je, ni kwa sababu ya uzuri wetu? Je, ni kwa kuwa ni wenye thamani? Au ni wema sana? Hebu na tufikiri jambo hili na kushukuru pale panapo hitajika.

Sababu ni kwamba Mungu alituumba ili tuwe watu wake na kuturuhusu tuishi katika Ufalme wa Mbinguni pamoja naye. Mungu ametufanya kuwa watu ili kuturuhusu tuishi naye milele. Na hii ndiyo sababu pekee Mungu kutubariki na uzima wa milele. Hakutufanywa kuwa watu wake kwa kuwa tu wazuri, wenye thamani au muhimu zaidi ya viumbe wake. Sababu pekee ni kwamba ametupenda.

“Mfano wa mabo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1Petro

Page 204: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

204 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

3:21). “Watu wanane waliokoka kwa maji” (1Petro 3:20).

Ni watu wachache, mmoja katika mjini na wawili katika familia moja ndiyo walio okoka. Je, walikuwa ni wenye thamani zaidi ya wengine? Hata kidogo! Sisi sote si wenye thamani, bali tumeokolewa kwa njia nyingine kupitia imani katika maji na Roho.

Huu ni muujiza kati ya miujiza kwa kuokolewa na ni zawadi isiyo na pingamizi, zawadi ya Mungu kuweza kumwita yeye ni Baba, Bwana wetu. Hatuwezi kukataa hili. Tunaweza vipi kumwita yeye kuwa ni Baba au Bwana ikiwa bado ni wadhambi?

Tunapofikiri ukweli huu kwamba tumeokolewa tunajua kwamba Mungu alitupenda pasipo kikwazo Je, hatuwezi kumshukuru kwa hilo? Tungeweza kuzaliwa na kufa bila tegemeo lolote maishani mwetu na kuishia motoni kama si upendo na baraka

yake. Tunamshukuru Mungu tena na tena kwa baraka na upendo uliotufanya wenye thamani kuwa watoto wake mbele ya macho yake.

Tuliupata Wokovu huu wenye thamani kupitia ubatizo wa Yesu.

Kwa nini watu wale wa Kipindi cha Nuhu waliangamia?

Kwa sababu hawakuamini maji

(ubatizo wa Yesu). “Mfano wa mambo haya ni ubatizo

unaowaokoa ninyi pia siku hizi.” Imeandikwa katika 1Petro na roho nane tu ndizo ziliokoka

Page 205: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

205 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

kwa maji. Ni watu wangapi walikuwepo kipindi hicho cha Nuhu? Hatuna njia ya kujua ni wangapi, lakini hebu tufikiri ikiwa walikuwa kiasi cha milioni. Watu 8 tu katika familia ya Nuhu kati ya mamilioni ndiyo walio okoka.

Kwa kuonyesha ni sawa na nyakati hizi. Wanasema leo kuna zaidi ya watu bilioni 6 ulimwenguni. Ni watu wangapi walio takaswa dhambi zao kati ya wale wenye kumwamini Yesu leo. Ikiwa tulipaswa kuangalia mji mmoja, basi wapo wachache kati yao.

Katika mji wangu wenye watu 250,000 ni wangapi waliokombolewa toka dhambini? Labda 200? Sasa uwiano utakuwa vipi? Itakuwa na maana kwamba pungufu ya mtu mmoja kati ya elfu moja ndiyo pekee walio pokea bara ya ukombozi.

Inakadiriwa kwamba, wapo watu milioni

12 walio Wakristo hapa Korea, pamoja na Wakatoliki. Kati ya hawa ni wangapi kati yao waliozaliwa upya katika maji na Roho? Tunapaswa kukumbuka kwamba wapo watu 8 tu walio okoka kati ya idadi ya watu wote duniani kwa kipindi kile cha Nuhu. Yatupasa kujua na kuamini kwamba Yesu alichukua dhambi zote za wale wenye kuamini ubatizo wake.

Ni watu wachache wenye kuamini kwamba Yesu ametukomboa sisi sote kwa ubatizo wake na damu yake msalabani. Hebu jaribu kuangalia picha maarufu ya ufufuko wa Yesu. Ni watu wangapi wali onyeshwa wamefufuka? Unaweza kuona wakishuka toka jumba la Yerusalemu kuelekea aliko Yesu aliyenyosha mikono kuwapokea. Jaribu kufikiri ni wanatheologia au watumishi.

Leo hii wapo wanatheologia wengi

Page 206: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

206 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

ulimwenguni, lakini tunapata wachache wenye kuelewa na kuamini juu ya ubatizo wa Yesu kama nyenzo muhimu ya ukweli wa ukombozi. Wengine husema alibatizwa ili kuweza kufanana nasi zaidi sisi wanadamu.

Lakini imeandikwa katika Biblia kwamba Mitume wote pamoja na Petro na Yohana, walishuhudia juu ya ubatizo wa Yesu kama kuhamisha dhambi zetu kwake na tunaamini hivyo pia.

Mitume wanashuhudia maandiko ya kwamba dhambi zetu zilihamishiwa kwame Yesu kwa ubatizo wake. Huu ni ushuhuda wa ajabu wa neema ya Mungu kwamba tunaweza kombolewa kwa kuamini hilo tu.

Hakuna neno “Labda” juu ya habari ya Ubatizo wa Ukombozi.

Ni nani apokeaye upendo

Usio na mipaka kwa Mungu?

Yule anaye amini ubatizo wa Yesu na Damu yake.

Watu huona ni sawa kumwamini Yesu ili tu waokoke. Madhehebu yote hukubali juu ya wokovu katika imani za aina yao, na wengi hudhani ubatizo wa Yesu ni sehemu tu ya mafundisho ya kanuni ya jamii ya Kikristo. Lakini hii sivyo. Kati ya maelfu ya vitabu, vichache nilivyobahatika kusoma sikuweza kupata kitabu chochote juu ya wokovu unaozingatia kwa kina uhusiano kati

Page 207: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

207 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

ya ukombozi katika ubatizo na damu ya Yesu na wokovu wa Mungu.

Ni watu 8 tu ndiyo walio okolewa kipindi cha Nuhu. Sijui ni wangapi katika nyakati hizi, lakini nafikiri si wengi. Wale walio okolewa ni wale walioamini ubatizo wa Yesu na Damu yake. Nilipo tembelea Makanisa mengi, niligundua tena kwamba wapo watu wachache wenye kuhubiri Injili ya ubatizo wa Yesu, ambayo ndiyo injili ya kweli.

Ikiwa hatutaamini ukombozi wa ubatizo na damu ya Yesu, bado sisi ni wadhambi na hatujaokoka, haijalishi uaminifu wetu kuhudhuria ibada Kanisani. Tunaweza kuwa waaminifu kwa kwenda Kanisani katika maisha yetu yote, bado tu wadhambi.

Ikiwa tumekwenda miaka 50, bado tu wadhambi mioyoni imani yetu ya miaka 50 si kitu bali unafiki. Ni vema zaidi kuwa na siku moja ya ukweli. Kati ya wale wenye

kumwamini Yesu, ni wale tu wenye kuamini ukweli juu ya ubatizo wake na Damu yake wataingia katika ufalme wa Mbinguni.

Imani ya kweli ni kuamini ukweli kwamba Mwana wa Mungu alishuka ulimwenguni na alibatizwa ili kuchukuwa dhambi zote za ulimwengu. Na hii ndiyo imani ituongozayo kwenda katika ufalme wa Mbinguni. Yatupasa pia kuamini Yesu alitoa damu yake msalabani kwa ajili yako na yangu. Yatupasa kuelewa mpangilio huu ili tuweze kumshukuru na kumtukuza Mungu.

Sisi ni nani? Ni watoto wa wanadamu ambao walio okolewa kwa ubatizo na damu ya Yesu. Kwa nini tusimshukuru yeye? Yesu alibatizwa mto Yordani alipo kuwa na umri wa miaka 30 ili kutuokoa. Kwa hili, alizichukuwa dhambi zetu zote na kupokea hukumu yetu pale msalabani.

Tunapowaza juu ya hili, hatuna la ziada

Page 208: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

208 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

bali ni kunyenyekea kwa kumshukuru. Yatupasa kuelewa yote Yesu aliyo yafanya ulimwenguni ni kwa ajili ya Wokovu wetu. Kwanza alikuja ulimwenguni. Alibatizwa akasulubiwa msalabani, alifufuka kutoka wafu baada ya siku tatu na amekaa mkono wa kuume wa Mungu Baba.

Ukombozi wa Mungu ni wa kila mtu bila upendeleo. Wokovu wa Yesu ni wa wote, mimi na wewe. Tunamsifu Mungu kwa upendo wake na baraka.

Upo wimbo usemao “Ipo habari njema, kati ya watu, ulimwenguni, mimi ni mmoja wao niliye na upendo na wokovu wa Mungu. Ni upendo wa ajabu. Upendo wake kwangu. Ipo habari njema ulimwenguni, mimi ni mmoja wao niliye okolewa, nimefanya kuwa wake, nimevishwa upendo wake. Oh! Upendo wa Mungu neema ya Mungu. Ni upendo wa ajabu. Upendo wake kwangu.”

Yesu alishuka kutuokoa, wewe na mimi na ukombozi wa ubatizo wake ni kwa ajili yetu sote. Injili hii si visa na ngano (hadithi, simulizi za kale) ni ukweli uliotuletea uhai toka magumu ya ulimwengu kuelekea ufalme mzuri wa Mungu. Yakupasa uelewe kwamba imani ni mahusiano kati yako na Mungu.

Yesu alishuka ulimwenguni ili kutuokoa. Alibatizwa na kupokea hukumu ya msalaba ili kututakasa dhambi zetu.

Ni baraka ya namna gani kwa aliye mwaminifu, kuliita jina la Mungu Baba. Tunaweza vipi kuamini katika Yesu kama Mwokozi kwa kuokolewa kutoka dhambini kwa imani? Ni rahisi kwa kuwa anao upendo usio na mpaka kwetu. Tumeokolewa naye aliye tupenda kabla ya kumpenda.

Page 209: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

209 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Yesu alizitakasa dhambi zetu zote kwa mara moja na kwa wakati wote.

“Kwa maana Krsito naye aliteswa mara

moja kwa ajili ya dhambi mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1Petro3:18). Yesu Kristo alibatizwa kwa ajili ya ukombozi wetu na kufa mara moja msalabani ili kutuokoa, tusio haki.

Je, tumeokolewa mara moja au kwa hatua?

Mara moja na kwa wakati

wote.

Alikufa mara moja hapa duniani ili kutukinga na hukumu ya Mungu. Ili tuweze

kuingia katika ufalme wa Mbinguni na kupata uzima wa milele, alishuka duniani katika umbo la mwanadamu na kutakasa kabisa dhambi zetu zote kwa mara moja kwa ubatizo wake, kifo na ufufuo.

Je, unaamini kuwa Yesu Kristo ametuokoa kwa ukamilifu wote katika ubatizo wake na damu yake? Ikiwa hujaamini Injili ya ubatizo na damu yake, hujaokolewa bado. Kwa kuwa sisi ni wenye udhaifu hatuwezi kuzaliwa upya ikiwa hatutoamini kwamba Yesu alizisafisha dhambi zetu zote kwa mara moja na wakati wote kwa ukamilifu wote. Kwa ubatizo wake na damu yake.

Alibatizwa ili kuzichukua dhambi zetu zote na kuhukumiwa msalabani kwa ajili yetu sote. Alitakasa dhambi zote mara moja na kwa wakati wote kwa ukombozi wetu sisi wanadamu katika ubatizo na damu yake.

Haiwezekani kwa wanadamu

Page 210: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

210 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

kukombolewa ikiwa tutaendelea kutubu kila wakati tunapotenda dhambi, kuwa wema na wenye fadhila nyakati zote kwa kutoa, sadaka na mali zetu Makanisani na penye huduma.

Hivyo, imani katika ubatizo wa Yesu ni lazima kwa ajili ya ukombozi wetu. Inatulazimu kuamini juu ya maji na damu. Kwakufanya matendo mema pekee hakuhusiani na ondoleo la dhambi zetu.

Haiwezi kuleta jambo jema katika wokovu wetu ikiwa tutagharamia kununua nguo nzuri kwa ajili ya maskini au kuandalia chakula kizuri wachungaji. Yesu ametuokoa kupitia ubatizo wake na damu yake. Ikiwa tutaamini kwamba Mungu ametuokoa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake kwa mara moja na kwa wakati wote, basi hakika tumeokolewa.

Wengi wataweza kudhani kwamba ingawa

Mungu alisema hivyo katika Biblia, itawabidi wafikiri zaidi. Hili ni shauri lao, lakini yatupasa kuamini Neno lake kama ilivyo andikwa.

Katika Waebrania 10:1-10 imeandikwa kwamba Yesu ametuokoa mara moja. Ni kweli kwamba Mungu ametuokoa mara moja. Ni kweli kwamba Mungu ametuokoa sisi tulioamini ubatizo wa Yesu na damu yake mara moja. Tuamini hili. “Alikufa mara moja, alituokoa sote mara moja, Ndugu amini na ukombolewe. Utue mzigo wako katika ubatizo wa Yesu.” Huu ni wimbo wetu siku zote. Yesu alituokoa kwenye uhasi na dhambi mara moja na kwa wakati wote kwa kubatizwa kwake mara moja na kwa damu yake msalabani.

“Mwenye haki kwa ajili yao wasio haki” (1Petro 3:18). Yesu ni Mungu asiye na dhambi, na hakutenda dhambi kamwe.

Page 211: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

211 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Alishuka kwetu katika mwili ili kuokoa watu wake na dhambi zao. Alibatizwa na kuchukua dhambi zote ilikutuokoa dhambini.

Dhambi za watu wote toka kuzaliwa kwao hadi mwisho wa kifo zilitwikwa kwake Yesu alipobatizwa na wote wameokolewa hukumuni alipo toa damu yake msalabani. Alibatizwa kwa ajili ya wenye dhambi na kufa kwa ajili yao kama kafara.

Upo ukombozi katika ubatizo wake. Yesu alituokoa sisi sote, wote tulio wadhambi, mara moja na kwa wakati wote. Ni kwa kiasi gani tulivyo dhaifu! Yesu alitukomboa sisi sote toka kuzaliwa kwetu hadi kifo kwa kujitoa yeye mwenyewe kwa hukumu ile ya msalaba. Sisi wenye kumwamini Yesu yatupasa kuamini kwamba ametuokoa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wake na damu yake.

Sisi ni dhaifu, lakini Yesu si dhaifu. Sisi si

waaminifu, lakini yeye ni mwaminifu. Mungu alituokoa mara moja na kwa wakati wote. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Mungu alitupa mwanae wa pekee. Alimbatiza ili azibebe dhambi zote za ulimwengu ili aweze kupokea hukumu za wanadamu wote.

Huu ni ukombozi wa ajabu. Ni upendo wa ajabu. Tunamshukuru Mungu kwa upendo wa wokovu wake. Yeye huokoa wale wote wenye kuamini maji na damu ya Yesu; Ubatizo na damu aliyotoa Yesu na ukweli ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Wenye kumwamini Yesu wataweza kuokolewa kwa kuwa wameamini ukweli wa ubatizo wake na damu yake na kuweza kuwa na uzima wa milele kama haki yao. Yatupasa sote tuone hili.

Page 212: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

212 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Ni nani aliye tuokoa? Je, ni Mungu, au ni moja kati ya alivyo viumba ndivyo huokoa? Ni Yesu, aliye Mungu, ndiye aliye tuokoa. Tumeokolewa kwa kuwa tumeamini ukombozi wa Mungu na huu ndio wokovu wake.

Yesu ni Bwana wa Wokovu.

Nini maana ya “Kristo”?

Kuhani, mfalme na

Nabii.

Yesu Kristo ni Mungu. Yesu maana yake ni Mwokozi na Kristo “Mpakwa mafuta”. Kama vile Samweli alivyo mpaka mafuta Sauli katika Agano la Kale, Wafalme walipakwa mafuta, makuhani na manabii ili

kuhudumia kazi, walipaswa kupakwa mafuta.

Yesu alikuja duniani na kupakwa mafuta kwa kazi tatu, ile ya ukuhani, ufalme na unabii. Ikiwa kuhani wa mbinguni, alibatizwa ili kubeba dhambi zote za wanadamu.

Kwa kutii mapenzi ya Baba yake, alijitoa kuwa sadaka ya upatanisho mbele ya Baba. “mimi ndimi njia, kweli na uzima, Mtu haji kwa Baba bila kwangu.” Yesu anaokoa sisi wale wenye kumwamini kwa kuzichukua dhambi zote kupitia ubatizo wake na kwa kusulubiwa kwake.

“Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu” (Walawi 17:11). Yesu alimwaga damu yake msalabani baada ya ubatizo wake, hivyo alitoa mwili wake mbele ya Mungu kama mshahara wa dhambi zetu ili wale tunao mwamini tuweze kuokolewa.

Alifufuka siku ya tatu baada ya kufa

Page 213: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

213 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

msalabani na alikwenda kuhubiri Injili kwa roho zilizo fungwa jela. Wale ambao bado hawajakombolewa wanafananishwa na wafungwa wa kiroho katika jela ya dhambi, na kwao Yesu anahubiri injili ya kweli injili ya maji na damu. Mungu ametupa Injili ya maji na roho ili kutuokoa. Kwa yeyote mwenye kuamini atazaliwa upya.

Ubatizo na Damu ya Yesu unaokoa wenye dhambi.

Kwa vipi unaweza kuwa na Dhamira njema Mbele za Mungu?

Kwa kuwa na imani katika ubatizo na Damu ya Yesu.

Yesu Kristo ni mwokozi wetu na imethibitishwa katika 1Petro 3:21 “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu).” Ubatizo wa Yesu kwa maji ni lazima uwe we wokovu kwa wenye dhambi.

Yesu amesafisha dhambi zetu kwa kuzibeba yeye mwenyewe kwa kupitia ubatizo wake. Je, unaamini ubatizo wa Yesu? Je unaamini ya kwamba mioyo yetu ilisafishwa na kuwa safi kwa dhambi zetu zote kupitia ubatizo wa Yesu? Mioyo yetu ni safi kwa kusafishwa dhambi zote, lakini bado miili yetu inatenda dhambi.

“Kuzaliwa upya” haina maana kwamba mtu hatotenda dhambi tena. Sisi tulizaliwa upya, pia hutenda dhambi lakini mioyo yetu ni safi kwa sababu imani yetu ipo katika ubatizo. Kwa kifungu hicho kisemacho “siyo

Page 214: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

214 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu” (1Petro 3:21).

Ikiwa Yesu alizisafisha dhambi zangu, na ikiwa Mungu ameikubali hukumu badala yangu, basi ni kwa vipi nisimwamini Yesu? Kwa kujua ya kwamba Yesu, aliye Mungu, aliniokoa kwa ubatizo wake na damu yake, ni kwa vipi nisimwamini? Tumeokolewa mbele ya Mungu na sasa dhamiri (mioyo) ni safi. Hatuwezi kamwe kusema mbele ya Mungu kwamba Yesu hakuzisafisha dhambi zetu zote kama vile pia hatuwezi kusema Mungu hatupendi.

Dhamira zetu zimekuwa mbali zaidi na hisia ya dhambi baada ya kuzaliwa upya na hutuambia kila tunapo tenda dhambi. Ikiwa dhamira zetu zitatusuta hata kwa jambo dogo, hatuwezi basi kuwa huru kikamilifu kwa dhambi hadi pale tutakapo jikumbusha

juu ya nguvu ya ubatizo wa Yesu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa na dhamira njema.

Dhamira yetu inapotusuta, maana yake lipo jambo baya. Maji ya ubatizo wa Yesu hutakasa uchafu wote wa dhambi. Yesu alizichukuwa dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kututakasa hata dhamira zetu. Hakika tunapo amini hili, dhamira zetu zaweza kweli kutakaswa. Ni vipi dhamira zetu zaweza takaswa? Kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Kila mtu ana uovu na dhamira chafu toka kuzaliwa kwake, lakini tunapo amini hili, dhambi zetu zote hutwikwa kwake Yesu na kuondoa doa hili.

Hii ndiyo imani ya waliozaliwa upya. Siyo jambo ambalo huongozwa kwa fikra ndani yako kwa kitu fulani ili udhamirie kwa kukubali. Je, dhamira yako ni safi? Ni safi kwa kuwa umeishi kwa matendo mema au ni safi kwa kuwa dhambi zako zote alizibeba

Page 215: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

215 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Yesu na unamwamini yeye? Ni kwa imani pekee ndipo unapo pata dhamira safi.

Yapo maneno yenye uhai na yasiyo na uhai. Ni kwa namna gani dhamira zetu zaweza kutakaswa? Njia pekee ambayo tunaweza kuwa wenye haki na kuwa na dhamira safi ni kwa kuamini ukombozi wa Yesu kikamilifu.

Tunapo amini ubatizo wake unaotutakasa, haina maana kwamba uchafu wa miili yetu umeondokana nasi bali dhamira zetu ndizo safi mbele ya Mungu! Kwa hilo Yesu alikuja kubatizwa, kufa msalabani na alifufuka toka kifoni na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu.

Siku itakapo wadia atarudi ulimwenguni tena “atatokea mara ya pili, pasipo dhambi kwa hao wamtazamiao kwa wokovu” (Waebrania 9:28). Tunaamini atakuja kutuchukuwa, sisi wale tumtazamiao, na

tusio na dhambi kwa kuamini Ubatizo wa Yesu na damu yake.

Jaribio la Uchunguzi wa Imani.

Je, tunaweza kuokolewa bila ya

Ubatizo wa Yesu?

Kamwe hatuwezi.

Tulifanya uchunguzi na jaribio la ghafla katika Kanisa letu hapa Daejeon.

Mchungaji Park wa Kanisa hilo aliwaeleza waumini ya kwamba hakuna dhambi ulimwenguni bila ya kuelezea maana ya ubatizo wa Yesu. Mwanaume mmoja alizoea kusinzia wakati wa mahubiri anapokuwa

Page 216: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

216 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

anahudhuria katika makanisa mengine kwa sababu wachungaji waliokua wakihubiri walizungumzia Injili isiyo na ukombozi utokanao na ubatizo wa Yesu, hivyo ilimlazimu kutubu kila siku.

Lakini alipokuja hapa Kanisani petu Taejon, alisikiliza mahubiri macho yake yote yakiwa maangavu, kwa sababu ameelezwa ya kwamba dhambi zake zote alizibeba Yesu. Ikawa ni rahisi sana kwa mke wake kumshawishi kuendelea kuja Kanisani naye.

Siku moja alipokuwa amekaa Kanisani na kusikia maandiko katika Warumi 8:1, “Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Ghafla aliwaza “Ahaa! Ikiwa mtu atamwamini Yesu hawezi kuwa na dhambi tena. Hivyo hata mimi sina dhambi.”

Hivyo alimpigia simu shemeji yake na marafiki wengine moja baada ya mwingine

na kuwaeleza “Je, unayo dhambi moyoni mwako? Basi imani yako si sahihi.” Kwa hili, Mchungaji Park hakueleweka. Mwanaume huyo hakujua juu ya ubatizo wa Yesu ila alisisitiza ya kwamba yeye hakua na dhambi tena kwasababu ya maandiko hayo.

Hivyo akaanza kuwa na mtafaruku na mkewe. Mkewe huyo alikuwa ni mshika dini, lakini ndani ya moyo wake alikuwa na dhambi. Mumewe aliendelea kusisistiza yakuwa hakuwa na dhambi. Mwanaume huyo walihudhuria ibada mara chache lakini tayari hakuwa na dhambi moyoni mwake.

Mkewe aliamini ya kwamba wao wote, na mume wake walikuwa bado ni wenye dhambi mioyoni mwao. Walianza kubishana juu ya hili. Mwamaume waliendelea kusisitiza kuwa hawakuwa na dhambi kwa sababu “hakuna hukumu ya dhambi juu yao walio katika Kristo.” Na mkewe alibisha, na

Page 217: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

217 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

kusema bado ni wenye dhambi mioyoni mwao.

Siku moja mmoja wa mkewe alikerwa na jambo hili na kuamua kwenda kumuulizia Mchungaji Park, alikuwa na maana gani aliposema dhambi zote alitwikwa Yesu.

Hivyo siku moja, baada ya ibada, alimwacha mumewe arudi nyumbani na yeye kubaki ili amuuliza Mchungaji Park swali lake. Alisema “Najua unajaribu kutueleza jambo fulani, lakini naamini lipo jambo muhimu lililofichika. Tafadhali nieleze.” Basi Mchungaji Park alimwambia juu ya kuzaliwa upya katika maji na Roho.

Na aligundua mara moja, kwa nini imeandikwa katika Warumi 8:1 “hakuna ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Aliamini mara moja na aliokolewa hatimaye aligundua kwamba dhambi zake zote alitwikwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake na

kwa wale wote walio katika Kristo hawatahukumiwi tena.

Alianza kuelewa juu ya andiko hili. Hatimaye aligundua ufunguo wa ukombozi wake ulikuwa ni ubatizo wa Yesu na kwa hiyo tunaweza kuwa wenye haki kupitia ukombozi wa ubatizo wa Yesu.

Huku nyuma kumbe mume wake hakuwa amekwenda nyumbani bali alikuwa akimsubiri nje. Alipotoka akamuuliza juu ya ushuhuda wake ya kwamba dhambi zake zote zimetakaswa na kwa furaha alimuuliza “sasa umekombolewa?”

Lakini aliposikia juu ya Mchungaji alichomwelezea mkewe, alichanganyikiwa. Hakuwa amesikia bado juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu. Alikuwa na uhakika kwamba hakuwa na dhambi moyoni hata kama haamini ubatizo wa Yesu. Kwa mara nyingine tena wakaanza kubishana.

Page 218: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

218 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Mara hii mambo yalikuwa kinyume. Mke alimwuliza ikiwa mumewe alikuwa na dhambi moyoni au la! Alimuuliza ni kwa vipi hawezi kuwa na dhambi ikiwa bado hajaamini ubatizo wa Yesu. Alimsihi achunguze dhamira yake kwa makini ndipo alipogundua. Na katika ugunduzi wake aliona dhahiri ya kwamba bado anayo dhambi moyoni mwake.

Hivyo, mume huyo alikwenda kwa Mchungaji Park na kukiri anayo dhambi moyoni. Alimuuliza, “Walipokuwa wakiweka mikono juu ya kichwa cha yule mnyama wa kafara, ilikuwa ni kabla ya kuchinjwa, au baada ya kuchinjwa?” Hakuwa amesikia juu ya Injili ya maji na Roho, hivyo alijawa na hofu.

Na hii ndiyo maana halisi ya uchunguzi huu wa kiroho. Ilimbidi Yesu abatizwe ili azibebe dhambi za ulimwengu. Hivyo ilibidi

pia afe msalabani kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.

“Je, waliwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kabla au baada ya kuuwawa? Aliuliza hili kwa kuwa hakuelewa juu ya kuwekea mikono na juu ya ubatizo wa Yesu. Hivyo Mchungaji Park alimwelezea juu ya Ukombozi katika ubatizo wa Yesu kwa undani zaidi.

Kwa siku hiyo, Mume huyo alisikia kwa mara ya kwanza Injili ya maji na Roho na alikombolewa. Alisikia mara moja na kukombolewa mara moja.

Hili ndilo jaribio litokanalo na kuondoa ubatizo wa Yesu. Tunaweza kusema hatuna dhambi, lakini hakika tuna dhambi ndani ya dhamira zetu bila ya ubatizo wa Yesu. Watu mara nyingi husema kwamba, Yesu alisafisha dhambi zote kwa kufa kwake msalabani, lakini ni kwa wale tu wenye

Page 219: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

219 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

kuamini ubatizo na damu ya Yesu ndiyo wanao weza kusema kweli kwamba hawana dhambi mbele za Mungu.

Mchungaji Park alithibitsha kwa wanandoa hawa katika Kanisa hili kwamba hawawezi kupata ukombozi wa kweli katika dhambi zao bila kuwa na Imani juu ya ubatizo wa Yesu.

Mfano wa Wokovu: Ubatizo wa Yesu.

Ni upi mfano wa Wokovu?

Ubatizo wa Yesu. “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo,

unaowaokoa ninyi pia siku hizi.” Yesu

alishuka duniani ili kusafisha dhambi zote na kufanya dhamira zetu kuwa nyeupe kama theluji. Tumetakaswa na dhambi zetu zote kwa kuwa Yesu alizichukua yeye mwenyewe kupitia ubatizo wake na damu yake. Hivyo, viumbe wote yawapasa kupiga magoti mbele yake.

Tukimwamini Yesu tutaokoka. Tunakuwa watoto wa Mungu na kwenda mbinguni kwa kumwamini Yesu. Tunafanywa kuwa haki kwa kumwamini Yesu. Sisi ni uzao wa kuhani. Tuna haki ya kumwita Mungu kuwa Baba yetu. Tunaishi duniani tukiwa wafalme.

Je, hakika unaamini kwamba Mungu amewaokoa wale kati yetu wenye kuamini katika ukombozi wa maji na Roho? Ukombozi wetu hautoweza kamwe kukamilika bila ya ubatizo wa Yesu. Imani ambayo Mungu Baba anaikubali kuwa ya kweli ni ile imani ya Injili ya ubatizo wa Yesu

Page 220: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

220 Ubatizo wa Yesu ni mfano wa Wokovu kwa wenye dhambi

Kristo, msalaba wake na Roho ambayo imetuokoa kwa ukamili wote. Hii ndiyo imani ya kweli.

Dhambi zetu zimetakaswa kabisa pale Yesu alipozibeba kwa ubatizo wake, na zililipiwa pale alipo toa damu yake msalabani. Yesu Kristo alituokoa kwa maji na Roho. Ndiyo! Tunaamini!

Page 221: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MAHUBIRI 8

Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Page 222: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

222 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

(YOHANA 13:1-17) “Basi kabla ya sikukuu ya Pasaka,

Yesu hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeda upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda mwana wa Simoni Iskariote moyo wa kumsaliti Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu aliondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake

akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuufuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni, Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia kama nisipo kutawadha huna shirika nami Simoni Petro akamwambia Bwana, si miguu yangu tu hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote, nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. Kwa maana alimjua yeye

Page 223: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

223 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

atakaye msaliti; ndiyo maana alisema, si nyote mlio safi. Basi alipokwisha kuwatawadha miguu na kuyatwaa mavazi yake na kuketi tena akawaambia Je, mmeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mwaniita, Mwalimu na Bwana, nanyi mwanena vema; maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu nimewatawadha miguu imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo ili kama mimi nilivyo watendea; nanyi mtende vivyo Amin, amin, nawaambia ninyi, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliye mpeleka; mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda. Sisemi habari za ninyi nyote, nawajua wale niliowachagua, lakini andiko lipate

kutimizwa aliyekula chakula changu ameniiunulia kisigino chake.”

Kwa nini Yesu alimwosha miguu Petro

siku moja kabla ya sikuu ya Pasaka? Punde kabla ya kumsafisha miguu Yesu alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa lakini utalifahamu baadaye.” Petro alikuwa wa pekee zaidi kwa Yesu kati ya wanafunzi wote. Aliamini kwamba Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu na alishuhudia kwamba ndiye Kristo. Wakati Yesu alipokuwa akisafisha miguu yake, palikuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo. Petro alipo kiri imani yake kwamba Yesu alikuwa Kristo, maana yake alimwamini Yesu kuwa ni Mwokozi aliye mwokoa na dhambi zake zote.

Page 224: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

224 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Kwa nini Yesu aliwaosha

Miguu wanafunzi wake kabla Ya kusulubiwa kwake?

Kwa sababu alitaka wajue kwamba

Yeye ndiye wokovu hakika. Kwa nini aliosha miguu ya Petro? Yesu

alijua kwamba Petro angelimkana punde mara tatu na angeliendelea kutenda dhambi.

Ikiwa baada ya Yesu kupaa mbinguni, Petro angeliendelea kuwa na dhambi moyoni asingeweza kuungana na Yesu. Lakini Yesu alikua akijua juu ya udhaifu wa wanafunzi wake wote kila mmoja, na hakupenda dhambi ikae kati yake na wanafunzi wake. Hivyo, alihitaji kuwafundisha ya kwamba uovu wao wote alikwisha usafisha. Hii ndiyo sababu aliwaosha miguu wanafunzi hao.

Kabla ya kufa kwake, alitaka kuhakikisha ya kwamba wamesimama imara katika Injili ya ubatizo na pia msamaha kamili wa dhambi za maisha yao yote.

Yohana 13 inazungumzia juu ya wokovu kamili aliotimiza Yesu kwa wanafunzi wake alipokuwa akiwaosha miguu, Yesu aliwaambia juu ya hekima ya Injili ya Ubatizo wake kupitia hivyo watu wote walitakaswa kwa makosa yao yote.

“Usidanganyike na shetani wakati mwingine. Nimekwisha zichukua dhambi zenu zote kwa ubatizo wangu katika mto Yordani na nitabeba hukumu badala yenu msalabani. Na baadaye nitafufuka katika wafu na kutimiza wokovu wa kuzaliwa upya kwenu nyote. Ili kuwafundisha juu ya haya kwamba nimekwisha safisha vile vile hata zile dhambi zenu zijazo, sasa nawaosha miguu kabla ya kusulubiwa. Hii ni siri ya

Page 225: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

225 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Injili ya kuzaliwa upya. Yawapasa nyote kuamini hili.”

Yatupasa wote kuelewa ni sababu ipi iliyo mfanya Yesu aoshe miguu ya wanafunzi wake na kujua ni kwa nini alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Hii pekee itatuwezesha kuamini juu ya Injili ya kuzaliwa upya na kutufanya sasa kuzaliwa upya maishani mwetu.

Yesu alisema katika Yohana 13:12

Ni yapi makosa yetu?

Ni dhambi tutendazo kila siku Kutokana na udhaifu wetu.

Kabla ya kufa msalabani, Yesu aliandaa karamu ya Pasaka kwa wanafunzi wake na kuwathibitishia juu ya Injili ya ondoleo la dhambi kwa kuwaosha miguu kwa mikono yake.

“Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu aliondoka chakulani akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa, lakini utalifahamu baadaye” (Yohana 13:3-7).

Aliwafundisha wanafunzi wake Injili ya ubatizo na msamaha wa dhambi kupitia

Page 226: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

226 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ubatizo wake. Kwa muda Petro alipokuwa mwaminifu

kwa Yesu hakuweza kuelewa sababu ya Yesu aliye Bwana kumwosha miguu. Na baadaye alipoelewa sababu halisi Yesu kumfanyia haya ghafla alibadilika kwa namna anayomfahamu kuwa yeye ni nani. Yesu alitaka kuwafundisha juu ya ondoleo la dhambi juu ya maji ya ubatizo wake.

Alitia shaka juu ya Petro asingeweza kuja kwake kutokana na dhambi atakazotenda hapo baadaye, kwa maneno mengine dhambi za mwilini zijazo; Yesu aliwaosha miguu ili shetani asipate kuchukua imani ya wanafunzi wake. Baadaye, Petro alikuja kuelewa sababu yake.

Yesu alikuja kutayarisha njia ili kila amwaminiye katika maji ya ubatizo wake na damu yake aweze kukombolewa kwa dhambi zake zote daima.

Katika Yohana 13, maneno aliyokuwa akisema wakati akiwasafisha miguu wanafunzi wake yamewekwa kama kumbukumbu. Ni maneno muhimu ambayo waliozaliwa upya tu wataweza kuyaelewa kiundani.

Sababu ya Yesu kuosha miguu ya wanafunzi wake kabla ya Pasaka ilikuwa ni kusaidia kuelewesha ya kwamba alikwisha safisha dhambi zao zote katika maisha yao. Yesu alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa, lakini utalifahamu baadaye.” Maneno haya kwa Petro yaliondokea kuwa kweli ya ukombozi wa milele kwake.

Yatupasa kuelewa na kuamini juu ya ubatizo wa Yesu ambao ulitakasa dhambi zetu zote na uovu wake. Ubatizo wa Yesu katika Yordani ilikuwa ni Injili ya kutwisha dhambi kwa kuwekea mikono. Yatupasa pia kuamini maneno ya Yesu alibeba dhambi

Page 227: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

227 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

zote za ulimwengu kwa ubatizo wake na kukamilisha ondoleo la dhambi kwa kuhukumiwa kifo msalabani. Yesu alibatizwa ili kuwaachanisha watu wote na dhambi zao.

Ondoleo la makosa yetu yote ya maishani lilitimizwa kwa ubatizo na kwa damu ya Yesu.

Ni upi “mtego” wa shetani Dhidi ya wenye haki?

Shetani hujaribu kulaghai wenye Haki ili kuwafanya wawe

wadhambi tena.

Yesu alikwisha elewa vyema, baada ya kusulubiwa kwake, kufufuka na kupaa

mbinguni, shetani na wale wahamasishaji wa imani ya uongo watajitokeza na kujaribu kuwalaghai wanafunzi wake. Tunaweza kuona katika ushuhuda wa Petro “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” ya kwamba anamwamini Yesu. Lakini bado Yesu alipenda kumkumbusha Petro kwa mara nyingine kuishika Injili ya ondoleo la dhambi moyoni mwake. Injili hiyo ilikuwa ni ya ubatizo wa Yesu kupitia hiyo alichukua dhambi zetu zote ulimwenguni. Alipenda kumkumbusha tena Petro, wanafunzi wengine na hata sisi leo hii. “Nifanyalo wewe hujui sasa lakiniutalifahamu baadaye.”

Kila wanafunzi wa Yesu wanapotenda dhambi shetani hujaribu kuwahukumu kwa kuseama “Tazama ikiwa bado unaendelea na dhambi utasema vipi kuwa huna dhambi? Bado hujaokoka; Bado wewe ni mwenye dhambi tu.” Ili kuzuia aina hiyo ya

Page 228: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

228 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

maambukizo, Yesu aliwaambia kuwa imani yao katika ubatizo wake ilikwisha safisha dhambi zao zote za maishani za kale, wakati uliopo na ujao.

“Nyote mwafahamu nilibatizwa! Sababu ya kubatizwa Yordani ilikuwa ni kusafisha dhambi zenu zote maishani pamoja na ile dhambi ya asili ya mwanadamu. Je, unaweza kuelewa sasa kwa nini nilibatizwa na kwa nini nilisulubiwa na kufa msalabani?” Yesu aliwaosha wanafunzi wake miguu kuwaonyesha yeye alikwisha zichukua dhambi zao zote za kila siku kupitia ubatizo wake na ataichukua hukumu msalabani.

Sasa wewe na mimi tumekombolewa toka dhambi zetuzote kwa imani zetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo imetuwezesha kupokea ondoleo la dhambi zetu zote. Yesu alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yetu. Ametakasa dhambi zetu zote

kwa ubatizo na damu na kwa wote wenye kuelewa na kuamini katika Injili ya ondoleo la dhambi na wenye kuamini ukombozi wa kweli toka dhambini huokolewa.

Sasa wale waliozaliwa upya yawapasa kufanya nini baada ya kuokolewa? Yawapasa kukiri dhambi zao za kila siku na kuamini katika wokovu wa ubatizo na damu ya Yesu injili ya upatanisho kwa dhambi zote. Injili ya ondoleo la dhambi ndiyo itupasayo sisi wote tuliozaliwa upya kukiri ndani ya mioyo yetu kwa undani sana.

Ikiwa utatenda dhambi tena, ina maana wewe ni mwenye dhambi? La! Sivyo kwa kujua kwamba Yesu alichukua dhambi zako zote, utaweza vipi tena kuwa mwenye dhambi? Ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ilikuwa injili ya ondoleo la dhambi zote. Kwa yeyote anayeamini katika Injili hii halisi ya ondoleo la dhambi ataweza

Page 229: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

229 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kuzaliwa upya, bila kikwazo, “kama mwenye haki.”

Wenye haki hawawezi kuwa wenye dhambi tena.

Kwa nini wenye haki hawawezi Kamwe kuwa

wenye dhambi tena?

Kwa sababu Yesu alikwisha jitoa kwa

Dhambi zao zote maishani mwao.

Ikiwa utaamini Injili ya ondoleo la dhambi

kwa maji na kwa Roho lakini bado unahisi wewe ni mwenye dhambi kwa sababu ya

makosa ya kila siku, basi yakupasa uende Yordani alipobatizwa Yesu ili kuondoa dhambi zako zote. Ikiwa utakuwa ni mwenye dhambi tena baada ya kupokea ondoleo la dhambi ina maana Yesu anapaswa kubatizwa tena. Yakupasa uwe na imani katika ondoleo la dhambi litokanalo na Injili ya ubatizo wa Yesu. Yakupasa uzingatie moyoni kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa mara mmoja na kwa wakati waote wa maisha yetu kwa ubatizo wake. Yakupasa uwe na imani isiyo yumba na kukengeuka kuwa Yesu Kristo, ndiye Mwokozi.

Kumwamini Yesu kama Mwokozi maana yake ni kuamini ubatizo wa Yesu; ambao ulizichukua dhambi zetu zote maishani. Ikiwa kweli utaamini ubatizo wa Yesu msalabani, kifo na ufufuko wake, hakika kamwe huwezi kuwa mwenye dhambi tena,

Page 230: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

230 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

bila kujali aina gani ya dhambi ulitenda. Umekwisha kombolewa kwa dhambi zako zote kwa maisha yako yote kwa Imani.

Yesu Kristo alisafisha hata dhambi zijazo tutakazo tenda kutokana na udhaifu wetu. Kwa kuwa alisisitiza umuhimu wa ubatizo wake, aliwaosha wanafunzi wake miguu kwa maji kuonyesha juu ijili ya msamaha wa dhambi ambao ni ubatizo wake. Yesu Kristo alibatizwa akasulubiwa akafufuka na kupaa mbinguni ili kutimiza ahadi ya Mungu ya upatanisho kamili wa dhambi za ulimwengu na wokovu wa wanadamu kwa matokeo haya wanafunzi wa Yesu waliweza kuhubiri Injili ya upatanisho wa dhambi ubatizo wa Yesu, msalaba na ufufuko mwanzoni kabisa hadi mwisho wa maisha yao.

Udhaifu wa kimwili wa Petro

Kwa nini Petro alimkana Yesu?

Kwa sababu alikuwa

dhaifu.

Biblia inatueleza kwamba Petro alikumbana na Mtumishi wa Kayafa Kuhani Mkuu akimtuhumu kuwa naye pia alikuwa mfuasi ya Yesu, alikana mara mbili kwa kusema “si mimi.” Na ndipo kwa mara ya tatu aliapa kwa hasira kutomtambua Yesu.

Hebu tusoma kifungu toka Mathayo 26:69. “Na Petro alikuwa ameketi nje behewani, kijakazi mmoja akamwendea, akasema wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana mbele ya wote akisema sijui usemalo, Naye alipotoka nje

Page 231: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

231 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona akawaambia watu walikuwako huko, huyu alikuwapo pamoja Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, simjui mtu huyu. Punde kidogo wale waliohudhuria wakamwendea wakamwambia Petro hakika wewe nawe ni mmoja wao; kwa sababu usemi wako wakutambulisha . Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo. Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilosema kabla ya kuwika jogoo utanikama mara tatu. Akatoka nje; akalia kwa majonzi” (Mathayo 26:69-75).

Ukweli ni kwamba, Petro alikuwa akimwamini Yesu na kuwa mfuasi mwaminifu. Aliamini ya kwamba, Bwana Yesu alikuwa Mwokozi na “nabii ajaye”. Lakini Yesu alipofikishwa mbele ya Mahakama ya Pilato na ikawa hatari kwake

kuonyesha uhusiano wake na Yesu kwa mamlaka, alimkana na kumlaani mbele yao.

Petro hakujua kwamba angeweza kumkana Yesu lakini Yesu alifahamu hilo kabla. Alifahamu udhaifu wake kwa undani zaidi. Hivyo, Yesu alisafisha miguu ya Petro kusimika Injili ya wokovu katika ushuhuda wake kama ilivyoandikwa katika Yohana 13, “utatenda dhambi baadaye kwa nyakati zijazo, lakini nimekwisha kutakasa dhambi zako zote za nyakati zijazo.”

Hakika Petro alimkana Yesu alipoona maisha yake yamo hatarini, lakini ilitokana na udhaifu wa kimwili uliomfanya kutenda hayo. Hivyo kwa Yesu kuweza kuwaokoa wanafunzi wake kwa dhambi zao za nyakati zijazo ilimbidi awasafishe miguu yao kabla.

“Nitaziondoa dhambi zenu zote zijazo pia. Nipo karibu kusulubiwa kwa kuwa nilibatizwa na kuchukua dhambi zenu zote nitalipia zote

Page 232: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

232 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ili niwe mwokozi wenu wa kweli kwa wote. Mimi ni Mungu wenu, Mwokozi wenu, nitazilipia zote na nitakuwa Mchungaji kwenu kwa ubatizo wangu na damu yangu. Mimi ndiye Mchungaji wa wokovu wenu.”

Ili kupandikiza imani hii mioyoni, Yesu aliwaosha miguu baada ya karamu ya Pasaka. Hii ndiyo Injili iliyo kweli na hakika.

Kwa kuwa kimwili tu dhaifu hata baada ya kuzaliwa upya tutaendelea kutenda dhambi. Hata hivyo hatupaswi kutenda dhambi, lakini tunapokutana na matukio ya kutisha kama Petro, tunajikuta bila kutarajia tukianguka. Tunaishi katika mwili, hivyo nyakati nyingine tunapelekwa kati kwa kuangamizwa na dhambi zetu. Mwili utaendelea kutenda dhambi ikiwa tutaendelea kuishi katika mazingira ya ulimwengu huu, lakini Yesu amekwisha ondoa dhambi zote kwa ubatizo na damu yake msalabani.

Hatuwezi kumkana Yesu kuwa ni Mwokozi wetu, lakini tunapo ishi katika mwili, bado tutaendelea kutenda dhambi kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni kwa sababu tumezaliwa na mwili.

Yesu alijua yote haya, alipoishi katika mwili, hivyo akawa Mwokozi wetu kwa kulipia dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu yake. Amezifuta dhambi za wale wote wenye kuamini wokovu na ufufuo wake.

Na ndiyo maana Injili zote nne huanzia na ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji. Lengo la maisha ya ubinadamu wake lilikuwa ni kutimiza Injili ya kuzaliwa upya, Injili ya wokovu.

Page 233: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

233 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Ni mpaka lini tutaendelea

Kutenda dhambi katika mwili?

Tutaendelea hivyo mpaka Mwisho wa maisha yetu.

Petro alipomkana si mara moja wala mbili,

bali mara tatu kabla ya kuwika jogoo, ni kwa maana gani iliumiza moyo wake! Alijisikia aibu namna gani? Alikwisha apa mbele za Yesu ya kwamba hatomkana. Alitenda dhambi kwa sababu ya udhaifu wa mwili lakini ni kwa kiasi gani alifedheheka moyoni alipodhoofika katika udhaifu na kumkana Yesu si tu mara moja bali mara tatu? Ni fedheha ya namna gani aliyo isikia Yesu alipomwangalia kwa huruma tena?

Lakini Yesu alikwisha yajua yote hayo na zaidi hivyo alisema “Najua utaendelea

kutenda tena na tena. Lakini nimekwisha kuzichukua dhambi zako zote katika ubatizo wangu, usikubali dhambi zako zikukwaze na kuwa tena mwenye dhambi, usije shindwa kurudi kwangu. Nimekuwa mwokozi wako kikamilifu kwa kubatizwa kwangu na kuhukumiwa kwa dhambi zako zote. Nimekuwa Mungu wako, Mchungaji wako. Amini Injili ya ondoleo la dhambi zako. Nitaendelea kukupenda ingawa utaendelea kutenda dhambi katika mwili, nilikwisha kutakasa kwa makosa yako yote. Injili ya ondoleo la dhambi linatenda kazi milele. Upendo wangu kwako ni wa milele.”

Yesu alimwambia Petro na wanafunzi “kama nisipo kutawadha huna shirika nami.” Sababu ya kuongea Injili hii katika Yohana 13 ilikuwa ni muhimu kwa watu kuzaliwa upya katika maji na kwa Roho. Je, unaamini hili?

Page 234: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

234 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Katika mstari 9 “Simon Petro akamwambia Bwana si miguu yangu tu hata na mikono yangu na kichwa changu pia, Yesu akamwambia yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote.”

Ndugu wapendwa je, utaweza kuja tenda “dhambi za mwili” tena au hapana? Hakika utaendelea kutenda. Lakini Yesu alisema kwamba alikwisha kutakasa hata zile dhambi za nyakati zijazo katika maisha yako duniani makosa yote ya mwili kwa ubatizo wake na kwa damu yake na kukufanya kuwa safi kupitia maneno aliyowaeleza mitume wake yaliyo ya kweli, Injili ya upatanisho kabla ya kusulubiwa.

Kwa kuwa tunaishi katika mwili ulio na udhaifu wa aina zote, hatuwezi kujizuia kutenda dhambi. Yesu alitakasa dhambi za ulimwengu wote kwa ubatizo wake.

Hakusafisha vichwa vyetu tu na miili yetu, bali pia miguu yetu yaani dhambi zetu zijazo maishani. Hii ni Injili ya kuzaliwa upya, ubatizo wa Yesu.

Baada ya Yesu kubatizwa, Yohana Mbatizaji alishuhudia “Tazama, huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu!” (Yohana 1:29) Inatubidi kuamini kwamba dhambi zote za ulimwengu zilitakaswa kwa kutwikwa Yesu wakati wa ubatizo wake.

Tunapoishi katika ulimwengu huu wenye uovu, hatuwezi kujizuia kutenda dhambi. Huu ni ukweli usiofichika. Inapotokea udhaifu wa miili yetu, yatupasa kujikumbusha kwamba Yesu alikwisha tutakasa kwa dhambi zetu zote ulimwenguni kupitia Injili ya ondoleo na malipo kwa damu yake. Yatupasa kutoa shukrani kwake toka moyoni mwetu. Hebu na tukiri kwa imani

Page 235: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

235 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kwamba Yesu ni Mwokozi na Mungu wetu. Bwana asifiwe!

Kila mmoja ulimwenguni hawezi kujizuia kutotenda dhambi mwilini. Watu wataendelea kutenda dhambi katika miili yao na kufa kwa dhambi hizo. Mawazo ya Uovu ndani ya mioyo ya Watu.

Nini kimtiacho najisi mtu?

Dhambi za aina mbalimbali Na mawazo ya uovu.

Yesu anasema katika Mathayo 15:19-20. “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wivu,

ushuhuda wa uongo na matukano hayo ndiyo yamtia ya mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.” Kwa sababu ya aina za dhambi mbaya mioyo ya watu huwatia najisi na kuwafanya wasiwe safi. Yampasa mtu kugundua asili ya uovu wake.

Nini kulichomo ndani Ya moyo wa kila mtu?

Aina kumi na mbili za Dhambi

(Marko 7:21-23).

Yatupasa kuwa na uwezo wa kusema “Hizo aina kumi na mbili za dhambi zimo ndani ya moyo wa kila mwanadamu. Mimi

Page 236: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

236 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ninazo zote ndani ya moyo wangu. Ninazo aina kumi na mbili za dhambi ndani yangu zilizo ainishwa katika biblia.” Kabla ya kuzaliwa upya katika maji na Roho, yatupasa kukiri kwamba dhambi asili yake ni mioyoni. Yatupasa kukubali sisi ni wenye dhambi kabisa mbeli ya Mungu, lakini mara nyingi hatufanyi hilo. Wengi wetu hujikosha kwa kusema “sikuwa na mawazo haya moyoni, nilijikuta tu nikitumbukizwa bila kupenda.”

Lakini Yesu alisema nini juu ya wanadamu? Kwa ufasaha alisema kile kinachotoka moyoni mwa mwanadamu ndicho “kimtiacho najisi” yeye. Alitueleza kwamba watu wamejawa na mawazo maovu ndani yao. Unafikiri nini? Wewe ni muovu au mwema? Je, unajua kwamba kila mtu anayo mawazo ya uovu? Ndiyo kila mtu anayo!

Miaka michache iliyopita hapa Seoul, palikuwa na ajali ya kuanguka kwa jengo la

maduka. Familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao ziliingia katika kipindi kigumu cha majonzi na machungu, lakini watu wengi walikimbilia kwenda kushuhudia jambo hili likiwa kama ni tukio la kupendeza machoni pao.

Wengine walisema mioyoni mwao “wangapi wamekufa? 200? Ah! Kumbe wachache tu! 300? Labda? Ingekuwa jambo la ajabu na la kushangaza kama wangekufa kama elfu moja hivi…” Hii ndiyo mioyo ya watu inavyo ongea kwa ndani uovu wake. Inatubidi tukubali haya ni heshima mbaya kwa walio athirika na jambo hili. Ni kwa namna gani jambo hili limekuwa la kukatisha tamaa kwa ndugu wafiwa! Wengine walipoteza fedha na mali.

Wapita njia wengi hawakusikitika “ingekuwa labda watu wengi wamekufa ingekuwa jambo la kushangaza, lakini hawa

Page 237: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

237 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

tu. Ah! Wachache. Inashangaza! Ni vipi kama ingekuwa uwanja wa mpira? Maelfu wengelifunikwa na vifusi? Ah, ndiyo, labda ingekuwa tukio la kwanza kutokea!” Inawezekana wengi waliwaza namna hii mioyoni. Mawazo kama haya yanaweza kusikika katika ajali ya gari. Mashabiki wenye kupenda mambo ya ajali husikika wakisikitika kwamba ilikuwa ni ajali ndogo tu.

Wote tunafahamu ni kwa namna gani tulivyo waovu wakati mwingine. Tunaweza kutoa kauli zetu na kuelezea masikitiko yetu tunapo ona ajali, lakini kwa siri mioyoni mwetu tunapenda kuona kama ni jambo la kuburudisha. Tunapenda kuona majanga makubwa ya ajali ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha yao, ili mradi haiendani kinyume na mapenzi yetu. Hii ndiyo namna ya mioyo yetu inavyofanya kazi. Wengi wetu

tulikuwa namna hii hapo mwanzo.

Mauaji ndani ya kila moyo wa Mwanadamu.

Kwa nini tunatenda Dhambi?

Ni kwa sababu tunayo mawazo Ya uovu ndani ya mioyo yetu.

Mungu ametuambia ya kwamba ipo dhambi ya mauaji ndani ya kila moyo wa mwanadamu. Lakini wengi watakataa hili mbele ya Mungu “utasema vipi hivyo! Unawezaje kunifananisha na mtu wa aina hiyo!” Iliwapasa kukubali juu ya hili mioyoni mwao. Wao hufikiri anayefanya mauaji ni wa

Page 238: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

238 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kizazi kingine tufauti yao. “Yule muuaji katika habari siku zile,

aliyewaua watu wengi kwa kuwachoma katika chumba cha chini ni yule mtu aliye na dhambi ya mauaji moyoni mwake! Yule ni kizazi kingine! Siwezi kuwa kama yeye! Sithubutu kama yeye! Muuaji!” Wanakuwa wageni katika uhalifu na kupiga kelele “wale waliozaliwa na mbegu ya uovu walipaswa kufutwa kabisa juu ya uso wa dunia! Walipaswa kuhukumiwa kifo!”

Lakini kwa bahati mbaya mawazo ya kuua yamo ndani ya mioyo ya wale wenye hasira, navile vile katika mioyo ya wale wanye matukio ya mauaji ya mfululizo na wenye kuua katika tukio moja. Mungu anatuambia yakwamba ndani ya mioyo ya watu, yapo mawazo ya uuaji. Yatupasa kukubaliana na Neno la Mungu ambaye yeye aweza kuyaona mambo yaliyo fichika ndani ya

fikara zetu. Kwahilo, yatubidi tukubali kwa kusema “Mimi ni mwenye dhambi niliye na mawazo ya uuaji ndani ya moyo”.

Ndiyo, Mungu ametueleza ya kwamba yapo mawazo ya uovu ndani mioyoni mwetu, ikiwa ni pamoja na uuaji ndani ya kila mwanadamu. Hebu basi na tulikubali neno la Mungu. Kwajinsi kizazi hiki cha wanadamu kinavyo zidi kuwa kiovu, kila aina ya vifaa vya kujilinda vinazidi kuwa ni nyenzo za kuua. Hii ni matokeo ya uuaji nadani ya mioyo yetu. Waweza kuua katika kiwango cha hasira au woga. Sisemi ya kwamba kila mmoja wetu ataweza kuua katika maana halisi ya tendo la kuua, bali tunafikra hizi hata ndani ya mioyo yetu.

Tumezaliwa tukiwa na mioyo yenye uovu mioyoni mwetu. Wengine hutenda kabisa na kuua, si kwa sababu wamezaliwa mahususi kuwa wauaji, bali kwa sababu sisi sote tuna

Page 239: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

239 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

uwezo wa kuwa wauaji mioyoni mwetu. Hii ni kweli. Hakuna awezaye kukwepa ukweli huu.

Hivyo, njia sahihi yetu ya kuchukulia jambo hili ni kulikubali neno la Mungu na kulitii. Tunatenda dhambi hapa ulimwenguni kwa sababu tuna mawazo yaliyo maovu ndani ya mioyo yetu.

Uzinzi ndani ya mioyo yetu Mungu anasema kwamba upo uzinzi ndani

ya kila moyo wa mtu. Je, unaamini hilo? Je, unakubali kwamba wewe una uzinzi moyoni mwako? Ndiyo, upo uzinzi katika kila moyo wa mwanadamu.

Na hii ndiyo maana ukahaba na uhalifu unao andamana na matendo ya ngono umestawi katika jamii zetu. Ni njia

mojawapo ya hakika katika kujitengenezea kipato kirahisi katika kila vipindi vya historia ya mwanadamu. Biashara nyingine mathalani zaweza kutetereka kiuchumi, lakini aina hii za biashara kamwe hazianguki kirahisi kwa sababu uzinzi bado unadumu na kuweka makazi ndani ya mioyo ya kila mtu.

Tunda la Mwenye kutenda dhambi ni Dhambi.

Mwanadamu anaweza Kufananishwa na nini?

Mwanadamu ni mfano wa mti Utoao matunda ya dhambi.

Kama ulivyo mti wa mtufaha utoao

Page 240: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

240 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

matunda ya tufaha, mti wa mtende utoao tende, mti wa mzabibu utoao zabibu, sisi tuliozaliwa na aina 12 za dhambi mioyoni mwetu, hatuwezi kujizuia bila kutoa matunda ya dhambi hizi.

Yesu alisema kile kinacho toka moyoni mwa mtu ndicho kimtiacho najisi. Unaamini? Tunaweza kukubali kwa maneno tu haya “Ndiyo, sisi ni kizazi cha dhambi waovu. Hakika ni kweli Bwana.” Ndiyo, yatupasa kukubali uovu wetu. Yatupasa kukubali ukweli mbele za Mungu.

Kama ilivyo kwake Yesu Kristo alipotii mapenzi ya Mungu; yatupasa pia nasi kulikubali neno la Mungu na kulitii. Hii ndiyo njia pekee tutaweza kuokolewa toka dhambini kwa kupitia maji na Roho. Hii ndiyo zawadi toka kwa Mungu.

Nchini mwangu tumebarikiwa kwa aina nne za misimu. Misimu hii inapo kuwepo,

aina mbalimbali za miti huzaa matunda. Kwa mfano huu dhambi 12 ndani ya mioyo yetu zimeshikana ndani yetu hivyo kendelea kutuongoza kutenda dhambi. Hii leo yaweza kuwa tumetingwa na dhambi ya uuaji mioyoni mwetu na kesho yaweza kuwa uzinzi.

Baadaye, siku inayofuata, mawazo ya uovu, baadaye tamaa mbaya, wizi, ushuhuda wa uongo…na kadhalika. Tunaendelea kutenda dhambi mwaka hadi mwaka, kila mwezi, kila siku, kila saa. Hakuna siku isiyopita bila kutenda dhambi ya aina fulani. Tunaendelea kujilaumu na kuahidi kutorudia lakini hatuwezi kwa sababu tumezaliwa hivyo.

Je, umewahi kuona mti wa tufaha kukataa kubeba tunda la tufaha kwa sababu tu haupendi? “sipendi kubeba tunda la tufaha!” Hata ikiwa mti umeghairi na kukubali bado

Page 241: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

241 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

utabeba tunda lake bila pingamizi kipindi cha masika, na tunda litakuwa tayari kuliwa wakati wa kiangazi.

Hii ni matokeo ya asili, na maisha ya mwenye dhambi vile vile huwa kama hivi. Wenyedhambi hawawezi kujizuia kubeba matunda ya dhambi maishani mwao.

“Ubatizo na msalaba wa Yesu” ulikuwa ni kwa ajili ya upatanisho wa wenye dhambi

Nini maana ya upatanisho wa Yesu?

Ni malipo ya mshahara wa dhambi kwa ubatizo wake (kuwekewa mikono)

na kumwaga damu yake msalabani.

Hebu na tusome kifungu hiki katika Biblia ili tuone ni kwa namna gani wenye dhambi, kizazi cha uovu wameweza kupatanishwa kwa dhambi zao mbele ya Mungu na kupata maisha ya furaha. Hii ni Injili ya upatanisho wa dhambi.

Katika Walawi 4, inasema “Na mtu awaye yote katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kusudia kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe naye akapata hatia akijulishwa hiyo dhambi yake aliyofanya, ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu, awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyofanya naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi na kumchinja sadaka ya dhambi, mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake na kuitia katika pembe za madhabahu

Page 242: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

242 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu. Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake naye atasamehewa” (mambo ya Walawi 4:27-31).

Katika kipindi cha Agano la kale, watu walipatanishwa vipi kwa dhambi zao? Waliwekea mikono yao juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi ambayo ni mbuzi, na kumtwisha mbuzi huyo dhambi zao zote.

Imeandikwa katika Walawi pia “Nena na Wana wa Israeli, uwaambie, mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo. Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya

ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu, ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake” (Walawi 1:2-4).

Mtu wa kipindi hicho anapogundua dhambi ndani ya moyo wake, ilimpasa kutayarisha sadaka ya dhambi ambayo itatumika katika kumpatanisha kwa dhambi. Ilimpasa “kumwekea mikono” juu ya kichwa cha yule mnyama wa sadaka ili kumtwisha dhambi alizotenda ndani ya ukumbi wa hema takatifu, palikuwa na madhabahu ya kuteketezea dhabihu. Lilikuwa ni sanduku la muundo wake, kubwa kiasi zaidi ya meza ya madhabahu, na katika kila kingo zake palisimikwa pembe. Watu wa Israeli walipatanishwa kwa dhambi zao kwa

Page 243: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

243 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na nyama yake kuchomwa juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka.

Mungu aliwaambia watu katika kitabu cha Walawi “ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana.” Dhambi zao zilitwikwa kwa yule mnyama wa sadaka walipo mwekea mikono kichwani na wenye dhambi walichinja koo lake na kumtoa damu yake kwa kuimimina katika zile pembe nne katika kingo za madhabahu ya kuteketeza kwa moto.

Baada ya hapo, mwili wa sadaka hiyo ulitolewa kwa kusafisha viungo vya ndani na nyama yake ilikatwa vipande na kuchomwa hadi majivu juu ya altare hiyo. Na ndipo harufu ya kupendeza ya nyama ile itatolewa kwa Mungu kwa ajili ya upatanisho wao naye. Hivi ndivyo walivyopatanishwa kwa dhambi za kila siku.

Mungu aliruhusu pia sadaka ya upatanisho kwa dhambi za mwaka. Hii ilikuwa hai na tofauti na ile ya dhambi za kisiku. Kwa hili, Kuhani Mkuu ndiye pekee aliyeruhusiwa kuwekea mikono sadaka ya dhambi kwa niaba ya watu wa Israeli na kunyunyizia damu upande ule wa Mashariki wa kiti cha Rehema mara saba. Pia kuwekea mikono juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai kulifanyika mbele ya watu wote wa Israeli katika siku ya kumi ya mwezi wa saba kila mwaka (Walawi 16:5-27).

Nani ni mfano wa Sadaka ya dhambi

Katika Agano la Kale?

Yesu Kristo

Hebu sasa na tuangalie mfumo wa matoleo au kafara ulivyobadilika katika

Page 244: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

244 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Agano Jipya na kwa vipi hadhi ya umilele wa Mungu ilivyobaki kwa miaka yote hii bila kubadilika.

Kwa nini Yesu ilimbidi afe msalabani? Alikosa nini ulimwenguni hapa hadi Mungu kuruhusu afe msalabani? Ni nani aliye mshurutisha afe kifo hicho? Wakati walimwenguni, yaani sisi wote, tulipoanguka dhambini Yesu alikuja duniani kutuokoa.

Alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani na kubeba hukumu msalabani kwa dhambi zetu zote na kwa niaba yetu wote sisi wanadamu. Kwa njia aliyobatizwa na kwa njia ile pia iliyotoa damu yake msalabani inafanana na sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale, kuwekea mikono sadaka ya dhambi na kutoa damu yake.

Hii ndiyo njia iliyofanyika katika Agano la Kale. Mwenye dhambi aliweka mikono juu ya

sadaka ya dhambi na kukiriu dhambi zake, kwa kusema “Bwana, nimetenda dhambi. Nimeua na kuzini.” Na ndipo dhambi hizo zinapotwikwa sadaka hiyo ya dhambi.

Kama ilivyo mwenye dhambi hiyo anapo mchinja koo sadaka yule wa dhambi na kumtolea kwa Mungu, Yesu alitolewa kwa namna hii ili kutupatanisha sisi sote kwa dhambi zetu. Yesu alibatizwa na kutoa damu yake pale msalabani ili kutuokoa na kutupatanisha kwa dhambi zetu zote kwa kujitoa kwake.

Ukweli ni kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu. Tunapofikiri hili, ilikuwa na maana gani juu ya matoleo ya wanyama hawa, wasio na doa kama kafara za dhambi zetu zote za watu? Je, wanyama hawa wote walikuwa wanaelewa nini maana ya dhambi? Hawajui juu ya dhambi. Walitolewa pasipo kuwa na doa.

Page 245: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

245 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Kama ilivyo kwa wanyama hao wasivyo na doa, ndivyo ilivyo pia kwa Yesu asiye na dhambi. Ni Mungu Mtakatifu, Mwana wa Mungu na hakutenda dhambi. Hivyo, alibeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani katika umri wa miaka 30.

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi alizo beba kwa niaba yetu. Ilikuwa ni huduma yake ya wokovu katika kutakasa dhambi za wanadamu.

Mwanzo wa Injili ya Upatanisho wa dhambi.

Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji Mto Yordani?

Kutimiza haki zote.

Imeandikwa katika Mathayo 3, “Wakati huyo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali” (Mathayo 3:13-15).

Yatupasa kujua na kuelewa sababu ya ubatizo wa Yesu katika umri wa miaka 30. Alibatizwa ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote na kutimiza haki zote za Mungu. Kuokoa watu wote kwa dhambi zao, Yesu Kristo, Yeye yule asiye na doa alibatizwa na Yohana Mbatizaji.

Hivi ndivyo Yesu alivyochukua dhambi za ulimwengu na kujitoa nafsi yake ili kupatanisha wanadamu wote ili uweze kuokolewa toka dhambini, yatupasa kujua

Page 246: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

246 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kweli yote na kuiamini. Ni hiyari yetu kuamini wokovu wa Yesu na kuokolewa.

Ubatizo wa Yesu una maana gani? Ni sawa na kuwekea mikono katika Agano la Kale. Katika kipindi hicho, dhambi za watu wote zilibebeshwa kichwani pa yule mnyama wa sadaka ya dhambi na Kuhani Mkuu ndiye aliyewekea mikono. Kwa mfano huo, katika Agano Jipya, Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu kwa kujiweka yeye kuwa sadaka ya dhambi kwa kubatizwa na Yohana.

Yohana Mbatizaji alikuwa ni mkuu kati ya wanadamu wote kwa kuwa mwakilishi aliyeteuliwa na Mungu. Akiwa mwakilishi wa wanadamu, Kuhani Mkuu wa wanadamu aliweka mikono juu ya kichwa cha Yesu na kumtwisha dhambi zote za ulimwengu kwake. “Ubatizo” humaanisha “kutwika, kuzikwa na kutakaswa.”

Je, unajua ni kwa nini Yesu alikuja

ulimwenguni na alibatizwa na Yohana Mbatizaji? Je unaamini katika Yesu kwa kuelewa maana ya ubatizo wake? Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni wa kuzichukua dhambi zetu zote; sisi uzao wa uovu, tulizo tenda kwa miili yetu kwa maisha yetu yote. Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kuitimiza ile Injili halisi ya ondoleo la dhambi zetu zote.

Katika Mathayo 3:13-17 inaanza na maneno “Wakati huo,” na kuonyesha muda Yesu alipobatizwa, ndiyo wakati dhambi za ulimwengu zilipotwikwa juu yake.

“Wakati huo” Yesu alizibeba dhambi zote za wanadamu kufa msalabani baada ya miaka mitatu na alifufuka siku ya tatu. Ili kutakasa ulimwengu kwa ajili ya wote, alikufa mara moja na kwa wote. Alikufa mara moja kwa wote na alifufuka kutoka kifoni mara moja kwa wote. Kwa wale

Page 247: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

247 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

wenye kuhitaji kukombolewa kwa dhambi zao mbele ya Mungu, Yesu alikwisha chukua dhambi za ulimwengu na kutuokoa mara moja na kwa wote.

Kwa nini Yesu ilipaswa kubatizwa? Kwa nini ilimpasa kuvaa taji la miiba na kuhukumiwa mbele ya mahakama ya Pilato kama mhalifu wa kawaida? Kwa nini alihukumiwa msalabani kwa kutoka damu hadi kufa? Sababu ya hayo yote hapo juu ni kwamba, alizibeba dhambi zote za ulimwengu, zangu na zako, katika ubatizo wake. Kwa dhambi zetu ilimpasa afe msalabani.

Yatupasa kuamini neno la msalaba ambalo Mungu ametuokoa na kushukuru yeye. Bila ya Ubatizo wa Yesu, Msalaba wake, na ufufuo wake hakika pasingekuwepo na wokovu wetu.

Yesu alipobatizwa na Yohana ili kubeba

dhambi za ulimwengu, alizibeba dhambi hizo na hivyo kutuokoa sisi wale tu wenye kuamini Injili ya wokovu. Wapo watu wenye kufikiri kwamba “Yesu alizichukua dhambi zile za asili tu.” Hakika watu wa aina hii wamepotoka kwa aina hii ya imani katika mafundisho ya aina hii.

Imeandikwa kwa uwazi kabisa ndani ya Biblia kwamba Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu mara moja na zote pale alipobatizwa dhambi zetu zote, ikiwa zile za asili nazo, zimetakaswa kabisa. Yesu anasema katika Mathayo 3:15 “kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki zote.” Kutimiza haki zote maana yake, dhambi zote pasipo kuchagua ziliondolewa kwetu sisi sote.

Je, Yesu ametakasa dhambi zote katika maisha yetu, pia? Ndiyo ametakasa. Hebu na tuone uthibitisho wa maandiko katika

Page 248: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

248 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kitabu cha Walawi kwanza. Inatueleza juu ya Kuhani Mkuu na sadaka ya Siku ya Upatanisho.

Sadaka ya Upatanisho wa dhambi za mwaka mzima za Waisraeli wote.

Je, Waisraeli waliweza kutakaswa Mara moja na kwa wakati

wote Kwa sadaka ya dhambi itolewayo Duniani?

Kamwe.

“Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa

sadaka ya dhambi aliye kwa ajili ya nafsi yake na kufanya upatanisho kwa ajili ya

nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake kisha atatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajili ya Bwana, na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kunganyia upatanisho, ili kumpelekea jangwani kwa ajili ya Azazeli” (Walawi 16:6–10). Hapo Haruni alichukuwa mbuzi wawili mbele ya lango la hema la kukutania kwa matoleo ya dhambi za mwaka za Israeli.

“Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.”

Page 249: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

249 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Mnyama wa Sadaka alihitajiwa kwa sheria ya ondoleo la dhambi za kila siku ili kumtwika dhambi za wenye dhambi kwa kuwekewa mikono juu ya kichwa chake. Lakini kwa dhambi za mwaka za Waisraeli, Kuhani Mkuu kwa niaba ya watu wote, alitwika dhambi za mwaka juu ya sadaka ya dhambi katika siku ya kumi ya mwezi wa saba kwa kila mwaka.

Katika Walawi 16:29-31 imeandikwa “Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu msifanye kazi ya namna yoyote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu, kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa, nanyi mtatakaswa na dhambi zetu zote mbele za Bwana Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele” (Walawi 16:29-31).

Katika Agano la Kale, watu wa Israeli walileta sadaka ya dhambi ili kupatanishwa na dhambi za kila siku na kumtwisha dhambi hizo juu ya kichwa chake kwa kuungama “Bwana nimetenda dhambi kadhaa….kadhaa…. Nakusihi unisamehe.” Baadaye atamchinja koo mnyama yule na kumpa Kuhani damu yake, na kwenda nyumbani akiwa na imani kwamba alikuwa huru kwa dhambi katika yote haya, sadaka ile ya dhambi hufa kwa niaba ya mwenye dhambi aliye itoa ikiwa na dhambi zake juu yake. Mnyama huyu wa kafara alitolewa kufa kwa niaba ya mwenye dhambi. Katika Agano la Kale sadaka ya dhambi aliweza kuwa mbuzi dume, ndama dume au ng’ombe dume, na hao walikuwa ni wanyama wa kafara ambao Mungu aliwatofautisha.

Mungu kwa rehema yake isiyo na mwisho,

Page 250: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

250 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

aliruhusu maisha ya wanyama hawa kutolewa kafara kwa niaba ya wenye dhambi ili wafe kwa niaba yao.

Kwa jinsi hii katika Agano la Kale, wale wenye dhambi waliweza kupatanishwa kwa dhambi zao kupitia sadaka ya upatanisho. Makosa ya wenye dhambi waliweza kupatanishwa kwa dhambi zao kupitia sadaka ile ya dhambi kwa kuwekewa mikono, na damu yake alipelekewa Kuhani ili kuzifuta dhambi zao.

Ingawa hivyo; ilikuwa si rahisi kupatanishwa kwa dhambi za kila siku. Na matokeo yake, Mungu aliruhusu Kuhani Mkuu kufuta dhambi za mwaka mzima katika kila siku ya kumi ya kila mwezi wa saba katika mwaka kwa niaba ya watu wa Israeli.

Hivyo nini ilikuwa nafasi ya Kuhani Mkuu katika siku ya upatanisho? Kwanza, Haruni,

Kuhani Mkuu aliweka mikono juu ya kichwa cha yule sadaka wa dhambi, kutubu dhambi za watu wote, “Bwana, watu wa Israeli wametenda dhambi kadhaa wa kadhaa, waliua, walizini, walifanya uasherati, wizi, walishuhudia uongo, walikufuru…”

Na ndipo humchinja koo mnyama yule, kuchukua damu yeke na kunyunyizia mara saba katika kiti cha rehema ndani ya Madhabahu takatifu (Kibiblia namba 7 huchukuliwa kama namba kamili.)

Ilikuwa ni kazi yake kila mwaka kufanya yote haya katika kutoa sadaka ya upatanisho ya dhambi za mwaka.

Kwa sababu Mungu ni mwenye haki, katika kuwaokoa watu wote kwa dhambi zao, aliruhusu sadaka hii ya dhambi kufa kwa niaba ya watu kwa kuwa yeye ni mwingi wa rehema, aliruhusu watu kuyatoa maisha ya wanyama hawa wa sadaka kwa

Page 251: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

251 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

niaba yao. Kuhani Mkuu alinyunyizia damu yake mnyama huyo upande wa mashariki ya kiti cha rehema na kwa haya yote msamaha ulitolewa kwa watu wote katika siku ya upatanisho kwa siku ile ya kumi katika mwezi wa saba.

Ni nani mwanakondoo wa Sadaka kulingana na Agano

la kale?

Yesu asiye na doa. Kuhani Mkuu alitoa mbuzi wawili katika

siku ile ya upatanisho kwa ajili ya watu wa Israel. Mmoja wao aliitwa Azazeli; maana yake “kutoa” Na kwa njia hiyo, Azazeli wa Agano la Jipya ni Yesu. “Kwa maana hii jinsi Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila yule

amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Mungu ametupa Mwana wake kama mwana kondoo wa sadaka. Akiwa kama mwanakondoo wa sadaka kwa wanadamu wote, alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kuwa Mwokozi, Masia wa dunia. Yesu maana yake “Mwokozi” na Kristo “Mfalme aliyepakwa mafuta.” Hivyo Yesu Kristo maana yake “Mwana wa Mungu alikuja kutuokoa sisi sote.”

Kama ilivyo dhambi zote za watu wote katika mwaka mzima zilivyo futwa katika siku ile ya Upatanisho katika Agano la Kale, Yesu Kristo katika miaka 2000 iliyopita, alikuja duniani ili kubatizwa na kutoa damu yake kwa kifo cha msalabani ili kikamilishe Injili ya ondoleo la dhambi zetu.

Katika jambo hili, hebu na tusoma kifungu katika Walawi. “Na Haruni ataweka mikono

Page 252: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

252 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote mpaka nchi isiyo watu naye atamwacha mbuzi jangwani” (Walawi 16:21-22).

Imeandikwa ya kwamba dhambi za Waisraeli wote zili twikwa juu ya kichwa cha mbuzi kama ilivyo katika Walawi 1. “uovu wao wote” inamaana dhambi zote zilizo tendwa ndani ya mioyo yao na kwa miili yao. Na “uovu wao wote” ulitwikwa juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu

Kwa sheria ya Mungu, yatupasa kuwa na ufahamu wa kweli wa Dhambi zetu zote.

Kwa nini Mungu Alitupatia sheria?

Ili tuweze kuzifahamu

Dhambi zetu.

Sheria ya Mungu imeundwa kwa vipengele 613 vya amri. Ukweli na kwamba, tunapo waza juu yake, tunafanya vile anavyosema juu ya sheria za kufanya na kutofanya anachohitaji tufanye.

Hivyo, sisi ni wenye dhambi. Imeandikwa katika Biblia kwamba Mungu alitupa sheria hizo ili tuweze kuzitambua dhambi zetu (Warumi 3:20). Hii ina maana kwamba

Page 253: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

253 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

alitupa sheria zake na amri ili kutufundisha sisi wenye dhambi. Hakutupa kwa sababu tungeweza kuzifuata bali ili tuweze kutambua dhambi zetu.

Hakutupa ili tuzifuate. Huwezi kutegemea mbwa kuishi kama mwanadamu. Kwa njia hiyo pia hatuwezi kuishi kwa kufuata sheria ya Mungu, bali tutaweza kupitia sheria hizo kugundua dhambi zetu kupitia amri zake.

Mungu alitupa kwa kuwa tuna wingi wa dhambi ingawa mara nyingi hatugundui hili. “Wewe ni muuaji, mzinzi, mtenda maovu.” Mungu hutuambia kwa namna hii kupitia kwa kuzingatia amri za sheria yake. Anatuambia tusiue, lakini bila kizuizi tunaua ndani ya mioyo yetu na wakati mwingine kwa matendo kimwili.

Hata hivyo, kwa kuwa imeandikwa katika Sheria ya kwamba tusiue, tunajua ya kwamba ni wauaji kwa kusema “Ah,

nilikosea tu! Mimi ni mwenyedhambi kwa kuwa nimefanya nisicho takiwa kufanya. Nimetenda dhambi.”

Ili kuokoa watu wa Israeli kwa dhambi zao Mungu aliruhusu Haruni kutoa sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale na ilikuwa ni yeye pekee aliye patanisha watu kwa dhambi za kila mwaka mara moja.

Katika Agano la Kale, sadaka za dhambi zilihitajika kutolewa kwa Mungu katika siku ya upatanisho. Moja ilitolewa mbele za Mungu wakati ile nyingine ilitumwa jangwani baada ya kuwekwa mikono kwa kubeba dhambi zote za mwaka mzima za watu wote. Kabla ya mbuzi huyo kupelekwa jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari, Kuhani Mkuu aliweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi huyo akiwa hai na kutaja dhambi kwa kutubu.

Nchi ya Palestina ni jangwa. “Azazeli”

Page 254: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

254 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ndiko walipo pelekwa huko, jangwa lisilo na mwisho na kutangatanga hadi kufa. Wakati azazeli akipelekwa jangwani, watu wa Israeli husimama na kushuhudia hadi kutokomea mbali, na hivyo kuamini kwamba dhambi zao zimetokomea na azazeli huyo. Na ndipo watu wanapopata amani juu ya yote haya, na azazeli huyo baada wa kutangatanga jangwani akiwa na dhambi hufikia kikomo na kufa.

Kwa namna hii, Mungu hupatanisha watu wake wote kwa dhambi zao kwa kupitia mwana kondoo wake, Yesu Kristo. Dhambi zetu zote zilitakaswa kabisa kupitia ubatizo wa Yesu na kwa damu yake Msalabani.

Yesu ni Mungu na Mwokozi. Ni mwana wa Mungu aliye kuja kuokoa wanadamu wote na dhambi zao zote. Ni muumba aliyetufanya kwa mfano wake na alikuja ulimwenguni kutuokoa toka dhambini.

Si dhambi za kila siku tu tuzitendazo kwa miili yetu ndizo alitwikwa Yesu, bali hata pia zile zijazo katika maisha yetu, zile katika mioyo yetu na kwa miili yetu pia. Kwa hiyo, ilimpasa abatizwe na Yohana Mbatizaji ili kutimiza haki ya Mungu, upatanisho kamili kwa dhambi zote za ulimwengu.

Miaka mitatu kabla ya Yesu hajasulubiwa, alipoanza huduma yake ya uwazi, alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake mto Yordani. Ubatizo huu ndio mwanzo wa upatanisho kwa mwanadamu.

Katika mto Yordani, ambapo ni sehemu ya kina cha maji yafurikayo kiunoni, aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Yesu na kumzamisha kwenye maji. Ubatizo huu ni sawa na kuwekea mikono kwa Kuhani Mkuu juu ya sadaka ya dhambi.

Kuzamishwa maana yake ni kufa na kuibuka maana yake kufufuka. Yote haya,

Page 255: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

255 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kwa kubatizwa na Yohana, Yesu alitimiza na kubainisha viungo vile vitatu katika mpango wake; kubeba dhambi zote, kusulubiwa na kufufuka.

Tutaweza kuokolewa ikiwa tu tutatii maneno yale ya Yesu yaliyo tuokoa toka dhambini. Mungu amekwisha amua kutuokoa kupitia Yesu, na agano aliloweka katika Agano la Kale limekwishatimia kwa kupitia tendo hili, Yesu alikwenda msalabani akiwa na dhambi zetu zote juu ya kichwa amezibeba.

Amekwisha futa dhambi

zetu zote? Nini kilichobaki kwa Upande wetu ikiwa Yesu

Amekwisha futa dhambi zetu zote?

Kile kitupasacho ni kuwa na Imani katika Maneno ya Mungu.

Katika Yohana 1:29 imeandikwa “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana Mbatizaji alishuhudia hili. Dhambi za wanadamu wote alibeba Yesu alipobatizwa mto Yordani. Amini hili! Ndipo utakapo barikiwa kwa ondoleo la dhambi zako zote.

Yatupasa kuwa na Imani ya neno la Mungu tuweke kando mawazo yetu na ugumu wa mioyo na tutii Neno la Mungu lililoandikwa. Inatulazimu kuamini katika kweli hii kwamba Yesu alichukua dhambi za ulimwengu huu.

Kusema kwamba Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu huu na kuseama pia alitimiza haki zote za Mungu kwa kutupatanisha kwa dhambi ni jambo sawa na moja katika maana. “Kuweka mikono” na “ubatizo” pia ni kitu kimoja katika tafsiri.

Page 256: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

256 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Haijalishi ikiwa tutasema “yote” “kila kitu” au “kwa jumla” tafsiri inabaki kuwa ni ile ile maana ya “kuwekea mikono” katika Agano la kale inabaki ile ile katika Agano Jipya, isipokuwa neno “ubatizo” ndilo hutumika badala yake.

Huja katika maana rahisi iliyo ya kweli kwamba Yesu alibatizwa na kuhukumiwa msalabani ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote. Tutaweza kuokolewa pale tutakapo amini Injili hii halisi.

Biblia inaposema Yesu “alichukua dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29) nini maana ya “dhambi za ulimwengu”? Maana yake ni dhambi zile zote tulizozaliwa nazo mioyoni, mawazo machafu, wizi, uasherati, ulafi, udhaifu, uhasi, majivuno na upumbavu yote haya hukaa akilini mwetu. Pia inahusu makosa na maovu tutendayo kwa miili na ndani ya mioyo yetu.

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana” (Warumi 6:23). “Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). Kama ilivyo katika mistari hii, dhambi zote hulipiwa gharama. Yesu Kristo, ili kuokoa wanadamu kutoka dhambini, aliyatoa maisha yake na kulipia gharama ya dhambi mara moja kwa wakati wote.

Hivyo, ilikuwa huru toka dhambini, yatupasa kuamini Injili ile halisi – ubatizo wa Yesu, Damu yake na Umungu wake (akiwa ni Roho).

Page 257: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

257 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Upatanisho wa Dhambi za Kesho.

Je, ipo haja ya kutoa sadaka Kwa ajili ya dhambi zetu tena?

Kamwe hatupaswi.

Dhambi za kesho, siku baada ya kesho,

na zile tutakazo tenda hadi siku tutakapo kufa; pia nazo zimejumuishwa katika “dhambi za ulimwengu” kama zile za leo, jana na keshokutwa pia zimo katika “dhambi za ulimwengu.” Dhambi ya asili na za maishani zote zimejumuishwa katika “dhambi za ulimwengu” na kila moja alitwikwa Yesu katika ubatizo wake. Hivyo majumuisho yote haya yamechukuliwa toka kwetu, hatuna tena dhambi.

Jambo pekee ni kuamini Injili hii (habari njema) iliyo halisi, maandiko ya Mungu, na kutii ukweli ili tuokolewe. Yatupasa kuweka kando hisia zetu ili tukombolewe toka dhambini. Unaweza kuuliza “itawezekana vipi achukue dhambi ambazo sijatenda?” Nami nitakuuliza “Ina maana Yesu inambidi arudi tena ulimwenguni kila tunapotenda dhambi na kutoa damu yake tena na tena?”

Ndani ya Injili ya kuzaliwa upya, ipo sheria ya upatanisho wa dhambi na “pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). Ikiwa yeyote atataka kukombolewa toka dhambini kwa siku hizo za Agano la Kale, ilimbidi azitwike dhambi kwa kuwekea mikono sadaka ya dhambi (mnyama), nayo sadaka hiyo itakufa kwa kuchunjwa koo kwa niaba yake na dhambi zake.

Kwa kiasi hiki ni sawa na Mwana wa

Page 258: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

258 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Mungu ialiyeshuka ulimwenguni kuokoa wanadamu. Alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu, alitoa damu yake msalabani kwa kusema “yamekwisha”. Alifufuka toka kuzimu baada ya siku 3 na ameketi kuume kwa Mungu kwa haya yote, amekuwa Mwokozi wetu daima.

Ili kuondolewa kabisa dhambi zetu, yatupasa kuondokana na fikra zilizonasa akilini mwetu na kuachana na mafundisho ya udini yanayotueleza kwamba tujikomboe kwa sala za toba kila siku. Ili dhambi za wanadamu ziweze kufutwa, sadaka halali inapaswa kutolewa mara moja na kwa wakati wote. Mungu wa Mbinguni alimtwika mwana wake dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na kuruhusu asulubiwe kwa ajili yetu. Kwa ufufuo wake toka kifoni wokovu wetu ulikamilika.

“Bali aliyejeruhiwa kwa makosa yetu.

Alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona … Na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.” Katika Isaya 53 imesema kwamba makosa na maovu yetu yote ulimwenguni ya wanadamu wote alibebeshwa Yesu Kristo.

Katika Agano Jipya, Waefeso 1:4 umeandikwa “kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Hii inatuambia kwamba Mungu alituchagua tuwe wake kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Kabla hata ya ulimwengu haujaumbwa. Mungu alikwisha amua kutufanya kuwa watu wake, wenye haki bila doa; katika Kristo chochote tungeliweza kuwaza kabla, yatupasa sasa kuamini na kutii Neno la Mungu, neno la maji, damu na Roho.

Mungu ametueleza Mwanakondoo wake,

Page 259: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

259 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Yesu Kristo, alichukua dhambi za ulimwengu na kutupatanisha wanadamu wote. Katika Waebrania 10:1 “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayo kuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakimbiao.”

Hapa inasema kwamba, kwa jinsi ile iliyokuwa ikitolewa mara kwa mara katika mwaka hadi mwaka, kamwe haitoweza kuwafanya kuwa wakamilifu. Sheria ni kivuli cha mema yatakayokuwa na si sura yenyewe ya mambo. Yesu Kristo, Masia aliyekuja, ametufanya kuwa kamili kwa mara moja na wakati wote (kama ilivyo dhambi za mwaka za Israeli walivyopatanishwa mara moja na wakati wote wa mwaka mzima) kwa ubatizo na kusulubiwa ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote.

Hivyo, Yesu ametuelezea katika

Waebrania 10, “ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi, ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu, tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa na Roho Mtakatifu naye amshuhudie kwa maana, baada ya kusema hili ni agano nitakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika

Page 260: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

260 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa, Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:9-18).

Tunaamini kwamba Yesu ametuokoa kutoka dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na damu yake msalabani.

Wokovu katika kuzaliwa upya kwa Maji na kwa Roho umeandikwa katika mioyo yetu na katika nia zetu

Je, sisi ni wenye haki kwa kutotenda tena dhambi?

Hapana sisi ni wenye haki kwa sababu

Yesu alizichukua dhambi zetu zote na tunamwamini yeye.

Je, wote mpo katika imani kamilifu ya wokovu? – Amen – Je, mnatii kwa imani maneno ya Mungu kwamba Yesu Kristo alibatizwa na kutoa damu yake pale msalabani ili kutuokoa? Yatupasa kuwa na imani na Neno lake ili tuweze kuzaliwa upya. Tutaweza kuokolewa ikiwa tu, tutaamini kwamba Yesu Kristo, kupitia Injili ya ondoleo la dhambi, alitutakasa dhambi zetu zote pamoja na dhambi za ulimwengu.

Hakika hatuwezi kuwa watakatifu kwa kutii sheria ya Mungu bali tutaweza kuwa wakamilifu kupitia imani yetu juu ya kazi ile aliyo ifanya Yesu (Kazi ya ukombozi kamili) Yesu Kristo alichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake mto Yordani, na akateswa kwa hukumu na kuadhibiwa kwa dhambi zetu zote msalabani kwa kuamini Injili hii kwa moyo wetu wote tutaweza kwa hakika kukombolewa na dhambi zetu zote na kuwa

Page 261: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

261 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

wenye haki daima. Je unaamini hili? Ubatizo wa Yesu, kusulubiwa kwake na

ufufuko wake ni ondoleo la dhambi zote za wanadamu na sheria ya Wokovu inayohusu upendo wa Mungu usio na mwisho wala masharti. Mungu anatupenda kama tulivyo na ni mwenye haki, hivyo alitufanya kuwa haki kwanza. Alitufanya kuwa haki kwa kumtwika dhambi zetu zote Yesu kwa ubatizo wake.

Ili kututakasa kwa dhambi zetu zote, Mungu alimtuma mwana wake, Yesu kuja ulimwenguni kwa ajili yetu. Aliruhusu Yesu azichukue dhambi za ulimwengu kupitia ubatizo wake na kumuhukumu. Alitufanya kuwa wana wenye haki kwa kupitia wokovu kwa maji na kwa damu, upendo wa Kimungu wa agape

Imeandikwa katika Waebrania 10:16 “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na

katika nia zao nitaziandika.” Ndani ya mioyo yetu na nia zetu je, ni

wenye dhambi mbele ya Mungu au wenye haki? Ikiwa tunaimani na Neno la Mungu, basi ni wenye haki Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote na alihukumiwa kwa ajili yake. Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Unaweza kudhani “Kwa sababu tunatenda dhambi kila siku itakuwa vipi ni wenye haki? Hakika sisi ni wenye dhambi.” Lakini tunapo amini neno la Mungu, kama vile Kristo Yesu alivyomtii Baba, tunakuwa wenye haki pia.

Bila shaka, kama nilivyokwisha sema hapa mwanzo, tuna dhambi mioyoni mwetu kabla ya kuzaliwa upya. Baada ya kuikubali Injili ya ondoleo la dhambi mioyoni mwetu, tumeokolewa na dhambi zetu zote. Kabla hatujafahamu hili tulikuwa wenye dhambi. Sasa tumekuwa wenye haki tunapo anza kuamini wokovu wa Yesu na kuwa wenye

Page 262: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

262 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

haki ndiyo Mtume Paulo aliyo kuwa akiiongelea sana. Imani ya Injili ya ondoleo la dhambi imetufanya tuwe “wenye haki.”

Si Mtume Paulo, wala Abrahamu na hata mababu zetu wa imani hawakuwa wenye haki kwa matendo ya sheria, bali kwa kuwa na imani ya Neno la Mungu, maneno ya baraka zake katika ondoleo la madhambi.

Katika Waebrania 10:18 “Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.” Kama ilivyoandikwa, Mungu ametuokoa ili tusiweze kufa kwa dhambi zetu. Je, unaamini hilo? – Amina –

Katika Wafilipi 2 “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yu namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa,

akawa ana mfano wa wanadamu, tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya duniani na vya chini ya nchi na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Wafilipi 2:5-11).

Yesu Kristo, aliyejawa na utukufu wa Mungu na ni Mungu halisi (Wafilipi 2:6) hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho. Bali alijifanya kuwa mtumwa, na kuja kwa mfano wa mwanadamu. Alijishusha na kuwa mtiifu hadi kufa ili kutuokoa.

Hivyo tumsifu Yesu “ndiye Mungu wetu, Mwokozi wetu na Mfalme kwetu.” Sababu ya kumtukuza na kumsifu Yesu ni kwamba yeye

Page 263: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

263 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

alitii mapenzi ya Baba yake hadi mwisho. Kama asinge yatii, tusinge mtukuza mwana wa Mungu leo hii. Lakini kwa sababu Mwana wa Mungu alimtii Baba yake hata kufa, viumbe na watu wote hapa duniani watamtukuza, na watafanya hivi milele.

Yesu Kristo alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu aliyechukua dhambi za ulimwengu, na imeandikwa kwamba alizichukua kwa ubatizo wake. Sasa ni miaka zaidi ya 2000 imepita tangu alipozichukua dhambi za ulimwengu. Mimi na wewe tumeishi duniani hapa tangu kuzaliwa kwetu, na dhambi zetu zote pia zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu.

Je, tutaweza kuwa wenye Dhambi Ikiwa tutatenda

dhambi kesho?

Hapana, kwa sababu Yesu alikwisha Chukua dhambi zetu zote zile za siku

Za nyuma, sasa na wakati ujao.

Bila kutenga dhambi ya sili toka makosa ya maishani petu, Je, hatukuwa wa dhambi toka kuzaliwa kwetu? – Ndiyo – sisi ni wadhambi.

Yesu alikwisha jua kwamba tutatenda dhambi kuanzia siku ile tuliyozaliwa hadi siku ya kufa. Hivyo alichukua dhambi hizo kabla. Je, waweza kuona sasa? Ikiwa tulipaswa kuishi umri wa miaka 70, dhambi zetu zingekuwa nyingi kiasi cha lori 100 za taka! Lakini Yesu alizichukua zote hizi mara moja

Page 264: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

264 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kwa ubatizo wake na kuzipeleka msalabani kwa malipo.

Ikiwa Yesu angelichukua dhambi ya asili tu, hakika sisi wote tungelikufa na kwenda motoni. Hata ikiwa hatuhisi kwamba Yesu hakuchukua dhambi zetu zote, kamwe haiweze kubadilisha ukweli wa Yesu kufuta dhambi zetu zote.

Ni kiasi gani cha dhambi tunachotenda hapa ulimwenguni? Dhambi zote tutendazo zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu.

Wakati Yesu alipomwambia Yohana ambatize alikuwa akimaanisha juu ya kubeba dhambi za ulimwengu. Yesu alishuhudia ya kwamba yeye alikwisha chukua dhambi zote za ulimwengu. Mungu alimtuma mtumishi huyu Yohana mbele ya Yesu ili ambatize Yesu. Kwa kubatizwa, na Yohana ambaye ni mwakilishi wa

wanadamu, Yesu aliinamisha kichwa chake mbele yake ili abatizwe ili azichukue dhambi zote za ulimwengu.

Dhambi zetu zote tokea umri wa miaka 20 hadi 30 na 40 na zaidi hata zile za watoto wetu zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu ambazo Yesu alibeba kwa ubatizo wake.

Ni nani awezaye kusema zipo dhambi zilizobaki Ulimwenguni? Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu huu na tunaweza wote kuokolewa kwa kuamini kwa moyo wetu wote, bila kivuli cha shaka juu ya nini Yesu aliyofanya katika kuleta upatanisho wa dhambi zetu yaani ubatizo na kutoa damu yake ya thamani.

Wengi huishi maisha ya kuchanganyikiwa yaliyo funikwa kwa fikra binafsi, wakizungumzia juu ya maisha yao tu, wakidhani kwamba yalikuwa ni muhimu

Page 265: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

265 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

sana. Lakini wapo wengine wanaishi maisha magumu. Wengine wameishi maisha ya kuchanganyikiwa. Hata mimi niliwahi kuishi namana hii kabla ya kuzaliwa upya, yaani kuokoka. Utawezaje kukataa kuelewa na kutokukubali juu ya Injili ya ondoleo la dhambi katika ubatizo wa Yesu na damu yake?

Wokovu wa wenye dhambi ulikwisha kamilishwa.

Sababu gani Yesu aliosha Miguu ya Petro?

Alitaka Petro awe na Imani madhubuti,

Ukweli Yesu alikwisha takasa tayari Dhambi zake zote zijazo

kwa ubatizo wake.

Hebu tusome Yohana 19 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania Golgotha. Wakamsulubisha huko na wengine wawili pamoja naye, moja huku na mmoja huku, na Yesu kati kati. Naye Pilato akaandika anwani akaiweka juu ya msalaba imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji, nayo iliandikwa kwa kiebrania, na Kirumi na Kiyunani” (Yohana 19:17-20).

Ndugu wapendwa, Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu akahukumiwa na kusulubiwa mbele ya Pilato. Hebu sasa tufikirie juu ya tukio hili pamoja.

Kwa kuanzia mstari wa 28. “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe

Page 266: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

266 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

akasema, Naona kiu. Kulikuako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo Wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki alisema imekwisha. Akainama kichwa akisalimu roho yake” (Yohana 19:28-30).

Yesu alisema “imekwisha” na baadaye alikufa pale msalabani. Baada ya siku tatu, alifufuka toka kifoni na kupaa mbinguni.

Ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji na kifo chake msalabani ni mambo mawili yasiyoweza kuachanishwa, moja halina sababu ya kuwepo pasipo jingine. Hivyo, tumsifu Bwana wetu Yesu kwa kutuokoa kupitia Injili yake ya ondoleo la dhambi.

Mwili wa mwanadamu mara nyingi hufuata matakwa yake ya kimwili, hivyo hatuwezi kujizuia kutotenda dhambi kwa miili yetu. Yesu Kristo ametupa ubatizo wake

na damu yake ili kutuokoa na dhambi za mwili. Alituokoa na dhambi za mwili kwa Injili yake. Wale walio na ondoleo kamili la dhambi ndiyo watakaoweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni wakati wowote kwa kumwamini Yesu, aliyezaliwa Bethlehemu, alibatizwa Yordani na kufa Msalabani na alifufuliwa baada ya siku tatu. Tuna msifu Bwana na kulitukuza Jina lake milele.

Sura ya mwisho katika Injili ya Yohana, Yesu alikwenda kwa Petro na kumwambia “Je, Simon wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?” naye Petro akamjibu “Ndiyo Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.” Ndipo Yesu akamwambia “lisha kondoo zangu.”

Petro alielewa kila kitu juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, ondoleo la dhambi. Hivyo, kuamini Injili ya maji na damu ambayo ilimpatia ondoleo la dhambi

Page 267: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

267 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

zake zote na pia kwa nini Yesu alimwosha miguu, ndiko kulikofanya Imani yake katika Yesu iwe madhubuti.

Hebu tusome Yohana 21:15 tena “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simon Petro, Je! Simon wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda Akamwambia, lisha wana kondoo wangu.” Aliweza kumkabidhi wana-kondoo wake Petro kwa kuwa alikuwa ni mwanafunzi wake aliye okoka kikamilifu na kwa kuwa Petro alikuwa mwenye haki na mtumishi kamilifu wa Mungu.

Ikiwa Petro angerudia tena kuwa mdhambi kwa makosa ya kila siku, Yesu asingeweza kumwambia ahubiri Injili ya upatanisho wa dhambi tena, kwa kuwa yeye na wenzake wasingeweza kujizuia bila kutenda dhambi kila siku katika mwili. Hivyo

Yesu aliwaambia wahubiri Injili ambayo iliyofuta kabisa dhambi zao zote kwa sababu ndiyo waliyo iamini kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, Injili ya upatanisho wa dhambi.

Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.

Utakuwa mwenye

dhambi tena ikiwa utatenda dhambi?

Hapana Yesu alikwisha zichukua dhambi zako zote zijazo mbeleni pale Yordani.

Hebu natufikiri juu ya maneno ya Yesu

kwa Petro “Je, Simon wa Yohana wewe

Page 268: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

268 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

wanipenda kuliko hawa?” “Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.” Kukiri kwake kwa upendo kulikuwa ni kwa ukweli ulio chipuka kwa imani itokanayo na Injili ya upatanisho wa dhambi.

Ikiwa Yesu asingemfundisha Petro na Mitume wake juu ya Injili ya ondoleo la dhambi kwa kuwaosha miguu asingeweza kukiri upendo wao kwa namna hiyo.

Badala yake Yesu alipokuja na kumuuliza “wanipenda kuliko hawa?” Petro angeweza kujibu “Bwana mimi ni mtu asiye mkamilifu. Mwenye dhambi asiyeweza kukupenda kuliko vingine. Nakusihi uniache tu.” Naye angetoweka, kwa kujificha mbele ya Yesu.

Lakini hebu tufikiri, juu ya jibu hili la Petro. Hakika alikuwa amebarikiwa kwa Injili ile ya ondoleo la dhambi, ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo ni wokovu wa wanadamu wote.

Hivyo Petro alikuwa na uhakika kwa kusema “Naam, Bwana wewe wajua kuwa nakupenda,” kukiri upendo kulikuja kwa imani katika Injili ya ondoleo la dhambi, ambayo Yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu. Hii ni pamoja na zile zijazo, ambazo watu wamefungwa kuzitenda kwa sababu ya udhaifu na upungufu wa miili yao.

Petro aliamini kwa dhati katika Injili ya ondoleo la dhambi na kwa kuwa pia aliamini kwamba Yesu alikuwa ni Mwana kondoo wa Mungu hivyo kuweza kumjibu Bwana bila kughairi. Wokovu wa Yesu ulikuja kutoka Injili (habari njema) ya ondoleo la dhambi, na hivyo Petro aliokolewa toka dhambi za kila siku pia. Petro aliamini wokovu kupitia Injili ya ondoleo la dhambi zote za ulimwengu.

Je, na wewe u kama Petro? Je, waweza kumpenda na kumtumaini Yesu

Page 269: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

269 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

aliyezichukua dhambi zako zote kwa Injili ya ondoleo la dhambi, kwa njia ya ubatizo na damu yake? Waweza vipi kutoamini au kutompenda? Hakuna njia nyingine.

Ikiwa Yesu alichukua dhambi zako za siku za nyuma na zile za wakati uliopo tu, hakika tusingeweza kumsifu kama tufanyavyo sasa. Kwa nyongeza ya hili, na hakika tungeishia motoni tu. Hivyo yatupasa tukiri kwamba Injili hii ya ondoleo la dhambi imetuokoa.

Siku zote mwili umelazimika kutenda dhambi, hivyo tutaendelea kutenda dhambi bila hiyari. Hivyo yatupasa kukiri kwa kuamini Injili ya upatanisho kamili wa dhambi zetu ambao ametupatia Yesu, Injili ya ubatizo na damu ya Yesu, umetuokoa.

Ikiwa hatutaamini Injili hii hakuna atakaye okolewa kutoka katika dhambi maishani mwake kwa nyongeza, ikiwa tutakombolewa na dhambi zetu zote maishani kwa kukiri na

kutubu kila mara, bila shaka tungekuwa wazembe kuendelea kuwa wenye haki na kuendelea kuwa dhambi mioyoni mwetu siku zote.

Kama ingekuwa namna hii, tungerudi kuwa wenye dhambi na tusinge mpenda Yesu au hata kuwa karibu naye. Pia tusingeweza kuamini wokovu wa Yesu na kumfuata hadi mwisho wa maisha yetu.

Yesu ametupatia Injili ya ondoleo la dhambi na kutuokoa sisi sote wenye kuiamini. Amefanyizwa kuwa Mwokozi kamili na kututakasa makosa yetu ya kila siku ili tuweze kuwa huru kumpenda.

Sisi wenye kuamini hatuwezi kujizuia kupenda Injili ile ya ubatizo na damu ya Yesu, ondoleo la dhambi zetu zote. Wenye kuamini wote watampenda Yesu milele na kushikwa kwa pendo la wokovu kupitia Injili ya ondoleo la dhambi ambalo Yesu

Page 270: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

270 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

mwenyewe ametuachia. Wapendwa! Ikiwa Yesu amebakiza hata

dhambi ndogo, hakika tusingeweza kumwamini, au hata kuwa mshuhudiaji wa Injili hii. Usingeweza pia kutembea kama Mtumishi wa Mungu.

Lakini ikiwa utaamini Injili hii ya ondoleo la dhambi kwa kweli utaokolewa na dhambi zako zote. Ameachilia uokolewe toka dhambi zako zote pale utakapo fahamu ukweli wa Injili ya ondoleo la dhambi, iliyomo katika Neno la Yesu.

“Wanipenda kuliko hawa?”

Jambo gani litufanyalo kumpenda Yesu zaidi ya chochote?

Upendo wake kwetu kupitia ubatizo wake uliotutakasa dhambi zetu zote hata zile

za nyakati zaijazo.

Mungu alimwaminisha mwana kondoo wake kwa wale watumishi walio ikubali Injili ya ondoleo la dhambi kwa uaminifu. Yesu aliuliza mara tatu “Je! Simon wa Yohana wewe wanipenda kuliko hawa?” naye Petro akamjibu kwa mara zote “Naam Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda,” sasa hebu tufikiri juu ya jibu la Petro. Tunaweza kuona huu ulikuwa si utashi wake binafsi bali imani iliyokuwa ndani yake juu ya ondoleo la dhambi.

Page 271: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

271 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Tunapo mpenda mtu, na ikiwa upendo huo unatokana na hiyari yetu, utaweza kushindwa tutakapo kuwa dhaifu. Lakini upendo utokanao na nguvu ya upendo wa Mungu huo utakuwa usio na mwisho wala mipaka. Upendo wa Mungu, uliosheheni upatanisho wa dhambi zetu zote, wokovu kwa maji ya ubatizo wa Yesu na Roho ndivyo ulivyo.

Imani yetu katika Injili ya ondoleo la dhambi ni lazima uwe ndiyo msingi na upendo wetu na matendo yetu kwa Bwana. Ikiwa tunampenda Yesu kwa hiyari yetu tutakwazika baadaye na kuishia kujeruhiwa kwa maovu yetu. Ijapokuwa Yesu ametutakasa kabisa na madhambi yetu yote; yale ya asili, yale ya kila siku, kwa wakati uliopita, uliopo na ujao katika maisha yetu yote hapa ulimwenguni. Hukumwacha yeyote katika wokovu huu.

Yote haya ni ukweli mtupu. Ikiwa upendo wetu na imani zetu itategemeana na hiyari na maamuzi binafsi, tutapotoka kiimani. Lakini ikiwa upendo wetu na imani zetu itategemeana na Injili ya ondoleo la dhambi Yesu alilotupa, tutakuwa tayari ni watoto wa Mungu, wenye haki. Hivyo tukiamini wokovu katika maji na Roho, tutakuwa hatuna dhambi.

Kutokana na ukweli kwamba wokovu ulikuja si katika namna ya kimungu ndani yetu, bali kwa upendo wa Mungu na sheria yake ya wokovu wa kweli katika ondoleo la dhambi, sisi ni wenye haki ingawa ni kwa namna gani hatujakamilika na kwa kuwa dhaifu kimwili maishani mwetu. Tutaingia ufalme wa Mbinguni na kumsifu Mungu milele. Je, unaamini hili?

1Yohana 4:10 inasema “Hili ndilo pendo la Mungu, si kwamba sisi tulimpenda Mungu,

Page 272: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

272 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

bale kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.” Yesu alituokoa kwa maji na Roho, hivyo yatupasa kuamini Injili ya ondoleo la dhambi ubatizo wa Yesu na damu yake.

Ikiwa Mungu hajatuokoa kwa Injili hii, tusinge okoka, bila kujali ni kwa kiasi gani tunamwamini. Lakini Yesu alitutakasa na dhambi zetu zote tulizotenda moyoni na katika mwili.

Ili tuweze kuwa wenye haki, yatupasa kuwa na uhakika na wokovu wetu kupitia imani katika maneno ya maji na Roho, Injili ya upatanisho, Injili ya ondoleo la dhambi za ulimwengu imeundwa kwa ubatizo wa Yesu na Damu yeke. Injili ya ondoleo la dhambi ni mjumuiko wa Imani ya kweli, msingi wa wokovu wa kweli na ni ufunguo wa kuingia Ufalme wa Mungu.

Yatupasa kuachana na Imani ya utashi wetu.

Imani iliyo ya kweli

huja toka wapi?

Huja toka juu kwa Bwana aliye kwisha takasa dhambi zetu

za nyakati zijazo.

Imani na upendo wa mtu utokanao na utashi wake si imani na upendo wa kweli. Wapo wengi katika dunia hii waliomwamini Yesu kwa mara ya kwanza kwa utashi mzuri, na baadaye waliacha imani zao kwa sababu ya uchungu wa dhambi zao moyoni.

Lakini yatupasa kuelewa kwamba Yesu alikwisha takasa dhambi zote za ulimwengu; si zile tuzionazo ndogo tu bali hata zile kuu tuzifanyazo kwa kutoelewa.

Page 273: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

273 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Katika Yohana 13, ili kuwafundisha wanafunzi wake namna gani wokovu wake ulivyo wa kutumainiwa na wakuendelea kuwepo milele, Yesu aliwakusanya wanafunzi wake pamoja kabla kusulubiwa kwake. Alipokuwa nao kwa chakula cha jioni, alinyanyuka na kuanza kuwakosha miguu ili kusisitiza juu ya ukweli wa wokovu uliokamilifu ndani ya mioyo yao. Nasi sote yatupasa kufahamu na kuamini juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ambayo Yesu alitufundisha wanafunzi wake kwa kukosha miguu yao.

Mwanzo Petro alikataa kumruhusu Yesu kuosha miguu yake “Wewe hutanitawadha miguu kamwe.” Na huu ndiyo uhalisi wa imani itokanayo na utashi binafsi. Lakini Yesu alimwambia “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utafahamu baadaye.”

Hivyo sasa kwa Injili ya maji na Roho

tutaweza kuelewa maneno ya Biblia ambayo yalikuwa kinyume na ufahamu wetu. Ni neno la kweli; injili ya maji na Roho, ondoleo la dhambi limfanyalo mwenye dhambi kuwa mwenye haki kwa kuamini kwa moyo wako wote.

Petro alikwenda kuvua samaki na wanafunzi wengine, kama ilivyo kawaida yao kabla ya kukutana na Yesu. Ndipo Yesu alipowatokea na kuwaita kwake. Yesu alikuwa ametayarisha kifungua kinywa kwa ajili yao, na walipokuwa wakishiriki, Petro aligundua maana ya maneno Yesu aliyokuwa akiwaelezea hapo awali. “nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utafahamu baadaye.” Hatimaye aligundua kile Yesu alichokuwa akimaanisha kwa kuosha miguu yao hapa awali.

“Bwana aliosha dhambi zangu zote. Dhambi zote nilizo tenda kwa udhaifu

Page 274: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

274 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

wangu, zikiwa pamoja na zile zote nitakazo tenda hapo awali pia.” Petro aliacha ile imani yake itokanayo na utashi wake na fikra zake na kuanza kusimama imara katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.

Baada ya kifungua kinywa Yesu alimuuliza Petro, “Je, wanipenda zaidi ya hawa?” Kwa kuimarisha imani katika upendo wa Yesu Petro alikiri “Ndiyo Bwana; wewe wajua kwamba nakupenda.” Yamkini Petro angeweza kujibu kwa kusema “utajua baadaye” alikuwa na nafasi ya kukiri imani yake ya kweli, imani katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.

@

Na baadaye, alikuwa Mtumishi wa kweli wa Mungu

Baada ya uzoefu, Petro na wanafunzi

wengine walihubiri Injili hadi mwisho wa pumzi yao. Hata Paulo aliyewatesa na kuwaua bila huruma Wakristo, alishuhudia Injili katika vipindi hivyo vya utawala wa Dola ya Warumi.

Je, waweza kuwa vipi mtumishi wa Mungu?

Kwa kuamini upatanisho

wa milele wa dhambi zangu zote.

Kati ya wanafunzi wale kumi na wawili wa

Yesu, Yuda ndiye aliye muuza Yesu na

Page 275: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

275 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

baadaye kujinyonga. Alikuwa Paulo ndiye mtume aliyechukua nafasi yake. Wanafunzi wa Yesu walimchagua Mathiasi kati yao, lakini Mungu alimteua Paulo, hivyo akawa Mtume wa Yesu na kuhubiri Injili ya ondoleo la dhambi pamoja na wanafunzi wengine.

Wengi wa wanafunzi hawa walikufa wakiwa mashahidi wa Mungu. Hata pale walipotishiwa kuuawa hawakuikana imani na kuendelea kuhubiri Injili ile halisi.

Yamkini wangehubiri kwa namna hii “Yesu Kristo alizitakasa dhambi zetu zote za mwili kwa ubatizo na damu yake na kwa hivyo, kwa injili ya ondoleo la dhambi yeye alizibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa kwake mto Yordani na kubeba hukumu yetu msalabani. Amini Injili ya Yesu katika ubatizo na damu yake msalabani ili muokolewe.”

Kwa kusikia Injili hii halisi na kuiamini hakika kila mtu ataokolewa. Ni nguvu ya imani katika Injili ya ubatizo wa Yesu, damu yake na Roho.

Mitume walihubiri Injili ya maji na Roho kwa kusema “Yesu ni Mungu na Mwokozi.” Ni kwa sababu walikwisha shuhudia juu ya Injili hii ya Yesu kwamba ni Mwokozi na kuokolewa dhambini. Kwa sababu ya upendo wa Mungu usio na mwisho na wokovu kamili toka kwa Yesu sote tumekuwa wanafunzi wa Yesu.

Je, wote mnaamini hivyo? Yesu alitupenda sote kwa upendo mkuu hata kutupa Injili ya maji na Roho, ondoleo la dhambi na kuwa wenye haki wanafunzi wa Yesu. Ili kutufundisha Injili ya kweli ya ondoleo la dhambi, Yesu aliosha miguu ya wanafunzi wake.

Yesu alisafisha miguu ya wanafunzi wake

Page 276: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

276 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ili kuwafundisha wao na hata sisi leo hii kwamba dhambi zote za ulimwengu, zikiwa zile tuzifanyazo maishani mwetu pote na hata zile zijazo za nyakati, yeye alikwisha zitakasa kwa ubatizo wake na damu yake msalabani. Tunamshukuru Yesu kwa upendo wake na kwa Injili ya ondoleo la dhambi.

Yesu alitufundisha mambo mawili kwa kuosha miguu ya wanafunzi wake.Kwanza ilikuwa ni kama alivyo alisema “Nifanyalo huwezi kufahamu sasa utalifamu baadaye,” ya kwamba dhambi zetu zote alizitakasa kwa injili ya ondoleo la dahmbi, ubatizo wa Yesu wa damu yake.

Pili,somo lingine litakuwa ni kujishusha yeye mwenyewe ili kuokoa wenye dhambi na kuwafanya wenye haki, sisi tulio zaliwa upya yatupasa kuwatumikia wengine kwa kuhubiri injili ya undoleo la dhambi. Ni haki yetu sisi tulio amini awali kutumikia wanao

kuja. Sababu mbili hizi ndizo zilizomfanya Yesu

kuosha miguu ya wanafunzi wake katika siku ile ya pasaka na ndiyo sababu zilizo wazi hadi hivi leo katika kanisa lake.

Mwanafunzi hawezi kuwa zaidi ya mwalimu, hivyo tuna hubiri injili duniani na dunia iokolewe kama tupasavyo kumtumikia Yesu sisi tulio okolewa hapo awali yatupasa tuwatumikie wale wajao nyuma yetu. Kwa kufundisha haya Yesu aliosha miguuu ya wanafunzi wake.Kwa nyongeza kwa kuosha miguu ile ya Petro alituonyesha kwamba yeye ndiye Mwokozi wa kweli hivyo tusiweze kudanganywa na shetani tena.

Wote mtaweza kuokolewa kwa kuamini injili ile ya indoleo la dhambi maji na Roho. Yesu alitutakasa na dhambi zetu zote kwa ubatizo wake kusulubiwa kwake na kwa ufufuo wake. Ni wale tu watakao amini injili

Page 277: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

277 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

yake ndiyo watako okolewa kwa dhambi zote za ulimwengu huu milele.

Uwe na imani katika injili ile itakasayodhambi zetu zote za kila siku.

Tunaondolea mbali ulaghai wa shetani

kwa kuamini injili ya ondoleo la dhambi, maneno ya maji na Roho. Nirahisi kwa watu kudanganywa na shetani na shetani huyo kuendelea kuwanong’oneza katika masikio yao. Je, kwa kujua yakwamba miili ya wanadamu wakati wote itaendelea kutenda dhambi duniani, ni kwa vipi basi wanadamu hao hawatoweza kuwa na dhambi? Watu wote ni wenye dhambi.

Hivyo basi tunafahamu jibu lake “kwa

kutambua yakwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Je, nikwanamna gani basi mwenye kuamini aweza kuwa si mwenye dhambi tena? Je, Yesu amelipa mshahara wote kwa dhambi zote, na hivyo hakuna kilicho baki kwetu kukilipia?

Ikiwa hatuta amini injili ya maji na damu maneno ya ibilisi yanaweza kuwa yenye sababu, lakini ikiwa tutakuwa na injili kwa upendo wetu tutaweza kuwa na imani isiyo tikisika katika neno la Mungu lililo la kweli.

Yatupasa kuwa imani katika inji ya kuzaliwa upya kwa maji na damu.imani ya kweli ni katika injili ya ubatizo wa Yesu damu yake pale msalabani, kifo chake na ufufuo wake.

Je umeshakwisha ona picha ya umbile la madhabahu takatifu? Ni nyumba ndogo ya turubai, ilivyo gawanyika katika sehemu kuu

Page 278: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

278 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

mbili, eneo la inje ni eneo takatifu na sehemu ya ndani ni patakatifu madhabahuni, ambapo kile kiti cha rehema kilimo.

Zipo jumla ya nguzo 60 zilizo zunguka wima sehemu ya nje ya madhabahu takatifu pa patakatifu zikizungukwa na kuta 48. Yatupasa tuweke ndani ya mawazo yetu mtazamo wa madhabahu takatifu ndani yafkra zetu ili tuweze kuelewa maana ya maneno ya Mungu.

Je malango ya ukumbi wa madhabahu yalitengenezwa kwa namna gani?

Malango ya ukumbi wa madhabahu hayo yaliundwa

kwa nini?

Chandarua ya kufumwa rangi ya Samawati Zambarau na

nyekundu na kitani ya kusokotwa.

Lengo la ukumbi wa Madhabahu

umeelezewa katika kitabu cha cha Kutoka 27:16 “Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa na ya rangi ya zambarau na nyekundu na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na matako

Page 279: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

279 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

yake manne.” Vitu hivi vilivyo tumika kutengenezea lango hili la ukumbi wa madhabahu vilikuwa samawati, zambarau, nyekundu na kitani ya kufumwa, ilifumwa na kuwa na rangi ya kuvutia.

Mungu alimwamuru Musa kupamba lango kwa rangi za kuvutia za samawati, zambarau na nyekundu na kitani ya kusokotwa ili iwe ni rahisi kwa kila mmoja kuweza kuuona mlango kwa urahisi. Lango hili lililo fumwa kwa rangi hizo katika kitani cha kufumwa lilining’inizwa kati ya pembe nne za minara.

Vitu hivi vinne vina simama badala ya mpango wa wokovu wa Mungu, ambao atawaokoa wale wote wenye kumwamini mwana wake, kwa kupitia ubatizo na kwa damu ya Yesu, na kwa kupitia hali yake ya kuwa yeye ndiye Mungu.

Kila kifaa kilicho tumika kujengea hema hii kilikuwa na maana yake ya pekee na vyote

viliwakilisha Neno la Mungu na mipango yake katika kuwaokoa wanadamu kupitia Yesu.

Kila kimoja ya vitu hivi vilivyo tumika kujenga madhabahu takatifu? Aina nne tofauti zilitumika! Samawati, zambarau, nyekungu na kitani ya kufumwa; vitu hivi vinene vilikuwa na umuhimu katika kuimarisha imani zetu katika Injili ya kuzaliwa upya. Kama havikuwa muhimu habari hii isingewekwa kwa kumbukumbu katika Biblia kwa maelezo ya kina kama haya.

Vitu vyote vilivyotumika katika lango la ua wa madhabahu takatifu vina maanisha umuhimu wa tafsiri katika wokovu wetu. Hivyo Mungu alimfunulia Musa na kumwambia jinsi ile ya kufanya kama aelezwavyo.

Page 280: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

280 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Nini maana ya kitambaa cha samawati, zambarau, nyekundu na kitani ya kufumwa katika Injili ya Mungu?

Vitu vyote hivi vilivyo tumika viliashiria nini?

Wokovu wa Yesu kupitia ubatizo

wake na damu yake.

Ndani ya madhabahu takatifu kitambaa cha samawati, zambarau na nyekunda na kitani ya kufumwa vilitumika kwa ajili ya pazia lililo tundikwa kati ya pahala patakatifu na patakatifu pa patakatifu. Vitu vya namna hiyo pia vilitumika kumvika Kuhani mkuu ambaye alipaswa kuingia patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka.

Kitambaa cha samawati kinaashiria ubatizo wa Yesu katika 1Petro 3:21 inasema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unao waokoa ninyi siku hizi.” Petro anahakikisha juu ya ubatizo wa Yesu kupitia kwake dhambi zote za ulimwengu alizibeba kwa mstari huu kama mfano ya wokovu katika ondoleo la dhambi. Dhambi zetu zote alibebeshwa Yesu kupitia ubatizo wake. Hivyo kitambaa cha samawati, ubatizo wa Yesu ni moja kati ya sehemu muhimu ya Neno la wokovu.

Kitambaa chekundu kinamaanisha damu ya Yesu na kitambaa cha zambarau nacho ni Uungu wake – hadhi ya Yesu kama Mfalme na Mungu. Rangi hizo tatu zilikuwa muhimu kwa ajili ya imani yetu katika Yesu na wokovu wake.

Vazi lile la nje, maridadi avaalo Kuhani Mkuu liliitwa kifuko cha kifuani, na kamba ya

Page 281: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

281 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kusokotwa iliyo samawati. Kuhani mkuu alivaa kilemba kilicho bandikwa kwa bamba la dhahabu safi na kuandikwa juu yake, mfano wa kuchorwa kwa mhuri “MTAKATIFU KWA BWANA.” Ulitiwa mkanda wa rangi ya samawati ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu.

Ukweli utokanao na maana ya kitambaa cha rangi ya Samawati.

Nini kinachowakilishwa na kitambaa cha rangi

ya samawati?

Ubatizo wa Yesu.

Nilitafuta maana ya rangi ya kitambaa cha Samawati katika Biblia. Biblia inasema juu ya rangi ya samawati? Yatupasa kuelewa maana ya rangi ya samawati, zambarau, na nyekundu katika kitambaa.

Kitambaa cha samawati kinawakilisha “maji” nao ni ubatizo wa Yesu. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu (Mathayo 3:15).

Ikiwa Yesu hakuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake, leo hii tusingeweza kutakaswa mbele za Mungu. Hivyo Yesu Kristo ilipasa aje ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto Yordani ili aweze kuchukua dhambi za ulimwengu.

Sababu na maana ya kuwepo kwa rangi ya samawati katika kitambaa kilichopo malangoni mwa ukumbi wa madhabahu

Page 282: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

282 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

takatifu ilikuwa ni kwamba tusingeweza kutakaswa pasipo ubatizo wa Yesu.

Kitambaa chakundu kinawakilisha damu ya Yesu, kifo chake msalabani. Zambarau inawakilisha Uungu wa Yesu, hadhi ya Yesu kama “yeye alihimidiwa, mwenye uweza peke yake mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana” (1Timotheo 6:15).

Ukweli ni kwamba kitambaa cha rangi nyekundu kinawakilisha damu ya Kristo, iliyotoka pale msalabani kulipia mshahara wa dhambi zote za wanadamu. Yesu Kristo alikuja ulimwenguni katika mwili ili kubeba dhambi zote za wanadamu juu yake kwa ubatizo wake na kulipia mshahara wa dhambi kwa kujitoa kwake msalabani. Ubatizo na damu ya Yesu ndiyo Injili ya kweli kwa ondoleo la dhambi lenye unabii kupitia rangi za kitambaa cha pazia lililotumika katika lango la madhabahu

takatifu kipindi cha Agano la Kale. Nguzo za madhabahu zilitokana na mbao

za mti wa mshita, viunganishi vyake vilitokana na shaba iliyo pakwa utepe wa fedha juu yake wenye dhambi wote walihukumiwa kwa makosa yao kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Kabla ya mtu yeyote hajabarikiwa na Mungu ili kupata maisha mapya, yampasa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake za siku kwa nyakati hizo za Agano la Kale.

Kwa jinsi hiyo basi, ubatizo wa Yesu kipindi cha Agano Jipya unawakilishwa na rangi ya Samawati katika madhabahu takatifu iliyo beba dhambi zetu zote msalabani, alitokwa na damu na kuhukumiwa kwa ajili yake ili kwa hayo ametuokoa sisi sote wenye kuamini Injili ya ondoleo la dhambi. Yeye ni mfalme wa falme na Mungu mtakatifu.

Page 283: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

283 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Wapendwa Wakristo, ubatizo wa Yesu ulikuwa ni wokovu toka kwake, ulio tuokoa sisi sote kwa kuzibeba dhambi zetu zote. Yesu yeye aliye Mungu alishuka ulimwenguni katika mwili (kitambaa cha rangi ya zambarau); Alibatizwa ili kubeba dhambi zetu zote ulimwenguni (kitambaa cha rangi ya samawati); Alisulubiwa na kutokwa damu pale msalabani ili kuikubali hukumu kwa niaba yetu (kitambaa cha rangi nyekundu). Ubatizo wa Yesu bila shaka unatufundisha kwamba yeye amekuwa Mwokozi wa kweli kwa wanadamu.

Tunaweza kuona pia katika rangi zilizopakwa katika malango ya madhabahu takatifu.

Kufumwa kwa kitambaa cha malango ya madhabahu takatifu kwa rangi ya samawati zambarau na nyekundu kwa nyuzi nzuri za hariri ni ishara tosha inayotueleza bayana

ukweli wa wokovu wa Mungu. Nyuzi nzuri za hariri hapa zinatuonyesha kwamba ameniokoa pasipo kizuizi cha dhambi zetu. Ilikuwa hakika ni muhimu katika wokovu wa upatanisho wa dhambi zetu zote.

Tunaweza kuona toka katika vitu vingine vilivyotumika kwa malango ya madhabahu takatifu jinsi ile Yesu Kristo asivyo chagua kuokoa sisi wenye dhambi bila kuweka mpangilio. Alitii mpango makini wa Mungu alibatizwa akasulubiwa na kufufuka toka kifoni ili kukamilisha wokovu wa wanadamu kwa rangi ya samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa, hii ndiyo malighafi iliyo tengeneza Injili ya ondoleo la dhambi ambayo Yesu alituokoa, sisi sote wenye kuamini wokovu wake.

Page 284: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

284 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Birika la Shaba katika Agano la Kale ni mfano wa ubatizo katika Agano jipya.

Sababu gani makuhani waliosha mikono na miguu kabla ya

kuingia sehemu takatifu?

Iliwapasa kusimama mbele ya Mungu pasipo na dhambi

Yeyote.

Birika lilitengenezwa kwa shaba. Shaba inawakilisha hukumu aliyopata Yesu kwa ajili yetu. Maji katika birika hilo yanawakilisha neno la Injili, linalo tueleza juu ya kutakasa kwa uovu wetu wote.

Hutuonyesha jinsi ile dhambi za kila siku zilivyoweza kutakaswa. Dhambi za kila siku za wanadamu ziliweza kutakaswa kwa

kupitia imani katika maneno ya ubatizo wa Yesu.

Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa inawakilisha hukumu. Maji ya Yesu, ambayo ni Samawati ni Injili ya ondoleo la dhambi kwa wenye dhambi wote, kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji (Mathayo 3:15, 1Yohana 5:5-10). ni neno la ushuhuda la Injili ya wokovu kupitia ondoleo la dhambi.

Katika 1Yohana 5 imeandikwa “Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu – hiyo imani yetu. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Inatueleza pia kuwa Yeye amwaminie Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake katika maji, damu na Roho.

Mungu alituruhusu sisi tuweze kutakaswa kwa kupitia imani katika Injili ya upatanisho

Page 285: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

285 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

na kuingia madhabau takatifu. Hivyo tunaweza sasa kuishi katika imani, kulishwa neno la Mungu, kubarikiwa naye na kuishi maisha ya haki. Ilikuwa watu wa Mungu maana yake ni kuokolewa kwa imani katika Injili ya upatanisho na kuishi ndani ya hekalu takatifu.

Watu wengi hivi leo husema inatosha tu bila hata ya kufikiri na kujua juu ya maana ya rangi ya samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa kilicho, malangoni pa madhabau takatifu. Ikiwa mtu atamwamini Yesu bila kujua juu ya vitu hivi imani yake haitoweza kuwa ya kweli kwa sababu ataendelea kuwa na dhamira ya dhambi moyoni mwake. Hii itatokana na kutoamini ukweli wa kuzaliwa upya kupitia injili ya ondoleo la dhambi katika maji, damu na Roho.

Ikiwa mtu alipaswa kumtathimini mtu

fulani ambaye asiye mfahamu na ikiwa atataka kumfurahisha msikilizaji atasema “Ndiyo namwamini mtu huyu. Bila shaka sijakutana naye kabla lakini namwamini hata hivyo.” Je, unadhani msikilizaji ataridhika kusikia hilo? Labda baadhi yenu mtaweza kuwa na tabia hii ya kibinadamu lakini hii si tabia ya Mungu anayo hitaji toka kwetu.

Mungu anatutaka kuamini Injili ya ondoleo la dhambi Wokovu wa Yesu kupitia samawati (ubatizo wa Yesu), zambarau (Uungu wa Yesu) nyekundu (damu ya Yesu) katika kitambaa. Yatupasa kujua kabla ya kuwa na imani katika Yesu jinsi alivyotuokoa kwa dhambi zetu zote.

Tunapo mwamini Yesu yatupasa kuelewa jinsi alivyo tuokoa toka dhambini kupitia maji (ubatizo wake) damu (kifo chake) na Roho (Yesu aliye Mungu).

Tunapoelewa kwa uhakika, tutaweza

Page 286: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

286 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kuona ukweli wa imani iliyo kamili. Imani yetu haitokamilika bila kuelewa ukweli huu. Imani ya kweli huja tu kwa kuelewa ushuhuda wa wokovu wa Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi na Yesu kuwa Mwokozi wa kweli kwa wanadamu.

Nini basi imani ya anayemdhihaki Yesu ilivyo? Hebu na tuone.

Imani ya dhihaka kwa Yesu

Nini tunachohitaji katika Imani?

Kujua kwa uhakika juu ya Ubatizo wa Yesu.

Unapasa kuelewa kwamba kumwamini

Yesu pasipo kwa undani ni sawa na

kumdhihaki. Ukidhani ya kwamba “naona ni vigumu kuamini, na kwa kuwa yeye ni Mungu na ni Mwana wa Mungu inanilazimu kuamini hata hivyo” hapo ndipo unapo mdhihaki Yesu. Ikiwa unahitaji kuokoka kwa uhakika, huna uchaguzi zaidi ya kuamini ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.

Kumwamini Yesu pasipo kujua juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ni hatari zaidi kuliko kutomwamini kabisa. Kuhubiri Injili ya damu ni kufanya kazi ya bure pasipo kuelewa ukweli.

Yesu haitaji mtu yeyote azunguke na kuhubiri juu ya kumwamini yeye kijuu juu, au kuwa na imani pasipo na sababu. Anatutaka tumwamini kupitia kujua Injili ya ondoleo la dhambi.

Tunapomwamini Yesu yatupasa kukubali ya kwamba Injili ya ondoleo la dhambi ndiyo

Page 287: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

287 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

ubatizo na damu ya Yesu tunapomwamini Yesu. Yatupasa kuelewa vyema Injili hii kupitia Neno lake na kujua kwa makini namna alivyo zisafisha dhambi zetu zote.

Yatupasa pia kujua nini maana ya rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa kilicho malangoni mwa madhabau takatifu inasimama badala ya nini. Hapo ndipo tutakapo weza kuwa na imani ya kweli ambayo itadumu milele maishani.

Hatutoweza kuzaliwa upya bila ya kumwamini Yesu, Ukweli wa Samawati, Zambarau na nyekundu katika kitambaa

Makuhani walifanya nini kabla Ya kuingia pahala patakatifu?

Walisafisha mikono na miguu kwa

Maji yaliyomo katika Birika la shaba.

Bwana wetu Yesu alituokoa. Hatuna budi

zaidi ya kumsifu Bwana pale tunapo ona namna aliyo tuokoa kwa ukamilifu. Yatupasa kuangalia katika madhabau takatifu. Ametupatia maneno ya Injili ya ondoleo la dhambi kupitia Samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa cha madhabau

Page 288: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

288 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

takatifu na kutuokoa kwa hayo. Tumshukuru na kumsifu Bwana.

Wenye dhambi wasingeweza kuingia mahala patakatifu bila ya kupitia hukumu ya kutisha. Ni vipi mtu angeingia mahala patakatifu bila ya kuhukumiwa dhambi zake? Hii isingewezekana. Ikiwa mtu huyo angeingia sehemu iliyo katazwa angepatwa na kifo papo hapo. Ingekuwa angamizo kubwa. Mwenye dhambi asingeweza kuingia mahala patakatifu na kuweza kuishi tena.

Bwana wetu ametuokoa kwa kupitia uficho wa siri katika malango ya madhabau takatifu. Kwa rangi za kitambaa cha samawati, zambarau na nyekundu na nyuzi za hariri zilizo fumwa, hakika alituokoa sisi sote. Alitueleza siri ya wokovu kupitia vitu hivi.

Je, mimi na wewe hatukuokolewa kupitia hivyo? Ikiwa hatutoamini maneno

yatokanayo na samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa, hapatakuwa na wokovu mwingine tena kupitia Injili ya ondoleo la dhambi. Rangi ya samawati haiwakilishi Mungu; inasimama badala ya ubatizo wa Yesu pekee. Ni ubatizo wa Yesu ambao ulio zichukuwa dhambi zetu zote.

Mtu ataweza kuingia katika madhabau ya sadaka za kutekelezwa bila ya kuamini kitambaa cha samawati. Isipokuwa hawezi kuingia pahala patakatifu alipo kaa Mungu.

Hivyo kabla ya kuingia malangoni pa mahala patakatifu pa madhabau yatupasa kuamini katika rangi ya samawati katika kitambaa (ubatizo wa Yesu) kitambaa chekundu (Damu yake msalabani) na zambarau (Uungu wa Yesu na mwana wa Mungu). Ikiwa tu, tutaamini tutakubalika naye na kukubalika kuingia kupitia pazia la mahala patakatifu pa patakatifu.

Page 289: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

289 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Wengine huingilia ukumbi wa nje na kufikiri kwamba wamo ndani. Lakini huu si wokovu. Namna gani inatupasa tuokolewe? Yatupasa kuwa na uwezo wa kuingia patakatifu pa patakatifu.

Ili kuweza kuingia pahala pa patakatifu pa patakatifu yatupasa kupitia katika birika la shaba. Birika la shaba linawakilisha ubatizo wa Yesu na yatupasa kusafisha dhambi zetu za kila siku kwa ubatizo wa Yesu na kutakaswa ili tuingie pahala patakatifu.

Katika Agano la Kale, kuhani ilimpasa kujisafisha kabla ya kuingia patakatifu na katika Agano Jipya, Yesu alisafisha miguu ya wanafunzi ili kuonesha kuwa alikwisha safisha makosa yao yote katika maisha yao.

Sheria ya Mungu inanena “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23). Mungu

humhukumu mtu kwa dhambi pasipo msamaha, lakini alipitisha dhambi hizo kwa Mwana wake na kumhukumu yeye badala yetu. Huu ndiyo upendo wa Mungu, wokovu wake. Wokovu wa kweli hupatikana tu pale tunapoamini Injili ya ondoleo la dhambi linalo jumuisha ubatizo, damu, kifo na ufufuo wa Yesu.

Ili uweze kuzaliwa Upya, yakupasa kutodhihaki ukweli wa kibiblia, Injili ya ondoleo la dhambi

Nini kilicho baki kwetu kufanya?

Ni kuamini Injili, neno la maandiko ya Mungu.

Page 290: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

290 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Sikuwahi kumdhihaki mtu. Ikiwa mtu fulani atazungumza juu ya jambo fulani ambalo silielewi, nitauliza kwa unyenyekevu ili amuelezee kwa undani. Lakini niulizapo juu ya matumizi ya madhabau takatifu, hakuna aliyewahi kunipa jibu.

Hivyo nifanye nini? Ndipo ilinibidi kuirudia biblia. Katika biblia ni wapi imeelezewa juu ya jambo hili? Imeelezewa kwa undani katika kitabu cha Kutoka. Ikiwa mtu atasoma kitabu hiki kwa makini, ataweza kuelewa maana yake kupitia neno la maandiko ya Mungu.

Rafiki wapendwa, hauwezi kamwe kuokoka kwa kuamini pasipo uangalifu juu ya Yesu. Huwezi kuokoka kwa kuhudhuria mara kwa mara ibada za kanisa. Tunaelewa kwamba Yesu alimwambia Nikodemo “Amin, amin nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu, Je!

wewe u mwalimu wa Israeli na mambo haya huyafahamu” (Yohana 3:5, 10).

Wote wamwaminio Yesu yawapasa kuamini juu ya kitambaa cha samawati (dhambi zote za ulimwengu alitwikwa Yesu alipobatizwa). Kitambaa rangi nyekundu (kifo cha Yesu kwa dhambi zetu zote) na zambarau (Yesu ni mwokozi, Mungu na mwana wa Mungu).

Yatupasa kuamini kwamba Yesu ni mwokozi wa wote wenye dhambi ulimwenguni. Bila imani hii, mtu hawezi kuzaliwa upya hata kuingia mahala patakatifu katika ufalme wa Mungu mtu vile vile hawezi kuishi kwa uaminifu hapa ulimwenguni bila haya.

Je, ingekuwa ni rahisi vipi ikiwa mtu atazaliwa upya kwa kuwa na imani na Yesu? – Ndiyo upo wimbo usemao “Umeokolewa, nimeokolewa sote tumeokolewa.” Ni vyema!

Page 291: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

291 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Lakini wapo walio na imani kwa Yesu bila ya kuokolewa kwa kuzaliwa upya.

Yatupasa kujua ukweli katika Biblia pamoja na kuwa na imani na Yesu. Yatupasa kuelewa juu ya Injili ya ondoleo la dhambi katika biblia na maana ya rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa ili tuweze kuingia madhabau takatifu na kuwa na Mungu katika ulimwengu wa imani. Ndani ya madhabau ya imani, tutaweza kuishi kwa furaha hadi muda ambao Yesu atakapo kuja tena kutupeleka katika ufalme wake. Ni muhimu kwetu kumwamini Yesu katika njia sahihi.

Injili halisi ilianza kwa utakaso wa kitambaa cha rangi ya samawati

Nini sharti lisilo kwepeka katika wokovu wetu zaidi

ya msalaba wa Yesu?

Ubatizo wa Yesu. Watu hufikiri kwamba wataweza kuishi

kwa ukamilifu pasipo kutenda kosa. Ingawa kwa kujibidisha huko kutenda mema, ndipo kwa kiasi hicho hugundua udhaifu wao zaidi. Wanadamu hawana ukamilifu na hivyo si rahisi kwao kutotenda dhambi. Kwa namna hiyo basi Yesu alituokoa kwa rangi ya samawati, zambaru na nyekundu katika kitambaa, Injili ya upatanisho ili tuweze

Page 292: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

292 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

kutakaswa na kuingia patakatifu pa Mungu. Ikiwa Mungu asingetuokoa kwa rangi hizo

tusingeweza kamwe kuingia pahala patakatifu kwa uwezo wetu. Nini sababu ya hili? Ikiwa kwa wale pekee wenye kuishi kimakini katika mwili wangeweza kuingia patakatifu, basi pasingekuwepo hata mmoja angeweza kuhitimu. Ikiwa mtu atamwamini Yesu bila kufahamu ukweli wa Injili, basi ataongeza dhambi juu ya moyo wake.

Yesu alituokoa kwa ubatizo wake ulio makini katika mpango wa wokovu, wokovu wa Samawati zambarau na nyekundu katika kitambaa na nyuzi nzuri za hariri zilizofumwa. Alisafisha dhambi zetu zote. Je, unaamini hilo? – Ndiyo – Je, unao ukweli juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ndani ya moyo wako na kuwa na ushuhuda juu ya hilo? – Ndiyo –

Ikiwa utakuwa na ushuhuda wa injili

utaweza kuwa katika paji la uso vibao vya dhahabu visemavyo “MTAKATIFU KWA BWANA” na kujiunga na “Makuhani wakuu” (1Petro 2:9). Na ikiwa tu, utaweza kusimama mbele ya watu na kuwalezea kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, ufanyaye kazi kama kuhani mkuu.

Kilemba cha Kuhani Mkuu kilikuwa na vibao vya dhahabu na vilifungwa kwa kamba za samawati. Kwa nini samawati? Kwa sababu Yesu alituokoa kwa Injili ya ondoleo la dhambi lililochukua dhambi zetu zote na kutufanya tusio na dhambi kwa ubatizo wake. Ubatizo katika Agano Jipya ni sawa na kuwekea mikono katika Agano la Kale.

Haijalishi ni kwa namna gani ya uangalifu na uaminifu tuaminivyo katika Yesu tusingeweza kupata tuzo ile iliyo andikwa kwa kugongwa muhuri “MTAKATIFU KWA BWANA” bila ya kugundua siri ya maneno

Page 293: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

293 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

katika rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa.

Ni kwa namna gani tunakuwa wenye haki? Imeandikwa katika Mathayo 3:15 “Yatupasa kuitimiza haki yote.” Yesu alibatizwa na kutuokoa sisi sote toka dhambini. Kwa ubatizo wake, alibeba dhambi zetu zote, nasi wenye kuamini tumefanywa wenye haki.

Ni vipi basi tutaweza kusema hatuna dhambi ikiwa hapajakuwepo ubatizo wa Yesu? Hata ikiwa tunamwamini Yesu na kupiga kelele tukidhani kwa kufikiri juu ya kifo chake pale msalabani, machozi yote ya ulimwengu yasingeweza safisha dhambi zetu zote. Kamwe haijalishi ni kwa kiasi gani tutaweza kulia na kutubu, dhambi zetu zitabaki nasi.

“MTAKATIFU KWA BWANA.” Ikiwa Yesu amebeba dhambi zetu zote kwa ubatizo

wake na damu Bwana ameturuhusu dhambi zetu zote sisi kuweza kutwikwa juu yake na kuwa neno la wokovu liliwekwa kumbukumbu katika Biblia, tumekuwa wenye haki kwa imani, bila kujali makosa yetu na udhaifu.

Hivyo, tunaweza kusimama mbele za Mungu. Tutaweza sasa kuishi kama wenye haki na kuhubiri Injili ulimwenguni. Upo wimbo usemao “Nimeokolewa, umeokolewa, sote tumeokolewa.” Tumeokolewa kutokana na rehema za Mungu katika mpango wake.

Bila neno la Injili ya ondoleo la dhambi ndani ya moyo, hakuna wokovu, haijalishi bidii utakayo jaribu. Ni sawa na wimbo fulani wa Korea mashuhuri usemao “Oh moyo wangu unadunda haraka bila ya sababu kila nimwonapo, kila wakati nipo karibu naye. Bila shaka mtakuwa mwenye upendo usio tulia.” Moyo wangu unadunda haraka, bali si

Page 294: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

294 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

wake. Upendo haurudishwi. Kwa bahati mbaya, wapo wakristo wengi bado wanao upendo usiotulia mbele ya Mungu.

Watu hudhani wokovu huja katika njia mbali mbali toka kwa watu mbalimbali. Huuliza “Kwanini ujue kwa Injili ya ubatizo pekee?” Lakini usingeweza kuwa wokovu ulio kamilika ikiwa usingekuwepo Injili ya ubatizo wa Yesu. Ni njia pekee tuwezayo kupata haki mbele za Mungu kwa sababu ni njia pekee ituwezeshayo kutakaswa na dhambi zetu zote.

Ni wokovu gani wa Samawati ambao Yesu ametupatia?

Nini kilicho tufanya Kuwa wenye haki?

Injili ya Samawati, zambarau

na nyekundu katika kitambaa.

Wokovu kupitia Injili ya Samawati,

zambarau na nyekundu katika kitambaa ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu wote. Zawadi hii imetufanya sisi tuweze kuingia madhabau takatifu na kuishi maisha ya amani. Imetufanya kuwa wenye haki na kutuwezesha kuishi ndani ya Kanisa na kuwa chini ya mafundisho ya maandiko matakatifu kupitia Kanisa.

Page 295: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

295 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Tunapo kwenda mbele za Mungu kila mara, katika sala, Injili hii hutubariki katika upendo wa Mungu. Na hii ndiyo maana wokovu ni wenye thamani kwetu. Yesu anatueleza tujenge nyumba ya imani “juu ya mwamba.” Mwamba huo ni Injili ya ubatizo wa Yesu. Yatupasa sote tuokolewe kuishi na wokovu, kwenda mbinguni, kupata maisha ya milele na kuwa wana wa Mungu.

Rafiki wapendwa kwa sababu ya Injili hii ya upatanisho tumeweza kuwa na uwezo wa kuingia madhabau takatifu kwa imani. Kwa kuwa tumesafishwa dhambi zetu zote (ubatizo wa Yesu) na hukumu ile msalabani, basi tumeokolewa kwa Imani katika Injili ya ubatizo wa Yesu.

Utele wa upatanisho wa dhambi zetu zote, ubatizo wa damu ya Yesu, ni Injili iliyosafisha dhambi zetu zote. Je, unaamini hili? Injili ya kweli ni Injili itokayo mbinguni

kwa upatanisho uliosafisha kwa ukamilifu dhambi zetu zote.

Tumezaliwa upya kwa kuamini Injili ya upatanisho, Yesu ametupa Injili hii iliyosafisha dhambi zetu zote za kila siku na hata zile zijazo. Bwana asifiwe. Haleluya!

Injili ya maji na Roho (Injili ya maji na damu) ni Injili ya kweli iliyokamilika na kuhubiriwa na Yesu Kristo. Kitabu hiki kiliandikwa kubainisha siri ya Injili ya Yesu, Injili ya maji na Roho.

Kwa kuwa watu wengi humwamini Yesu bila kujua kikamilifu ukweli, sasa leo hii hujigamba kwa nafsi zao kuwa ni wenye ukereketwa au wenye udini katika ulimwengu wa thiologia za Kikristo (wenye kuitwa wanafilosofia wa kitheologia) kwa ufupi, huishi kwa taabu na kuchanganyikiwa. Hivyo yatupasa kurudi hatua nyuma na kuamini Injili ya kweli. Bado hujachelewa!

Page 296: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

296 Injili ya Upatanisho ulio kamilifu

Nitakwenda kwa undani zaidi katika kitabu cha pili kwa wale wenye maswali juu ya Injili ya kuzaliwa upya katika maji na Roho.

Page 297: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MENGINEYO 1

Shuhuda za Wokovu

Page 298: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

298 Shuhuda za Wokovu

Shuhuda za Wokovu

Nilitaabika kwa dhambi zangu

Kaka Jae-dong Park, Korea

“Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

Yule aliyewekewa mwisho wa kwenda, motoni amekwisha okolewa. Utukufu kwa Mungu!

“Simama sasa na uganga wako na wingi wa uchawi wako” (Isaya 47:12). Ndivyo nilivyofanya.

Nalizaliwa katika familia isiyopenda mabadiliko, mama yangu alikuwa mwaminifu

katika dini ile ya Budha. Kadiri nilivyokuwa, nilishiriki mafunzo ya dini ya Ki-Budha na kukariri maandiko ya dini hiyo na kuhudhuria hekaluni kwa hamu kubwa. Nilifikiri kuyaachilia mbali mambo ya uchawi wa Budha ambayo wanawake wengi waliyafuata hivyo nilijaribu kutafuta kitu kingine zaidi ili kuleta uhalisi wa maisha yangu. Lakini bado nilihisi mzigo wa dhambi ndani ya moyo wangu, na nilijaribu kusahihisha mwenendo wangu, ili niweze kusifiwa na wale wote wanizungukao!

Nilipokuwa nikihudhuria mafunzo katika chuo cha Sokcho-City nilikutana na rafiki mmoja Mkristo, na huo ndio uliokuwa mwanzo wangu wa mageuzi. Mungu alikwisha panga kukutana huku. Baadaye niligundua kwamba rafiki huyu kama nilivyokuwa mimi, yeye naye pia aliyatupilia mbali mambo ya kafara za kidini na hamasa

Page 299: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

299 Shuhuda za Wokovu

zake lakini bado hakupata faraja katika maisha yake; nilisikitika sana juu yake. Ndani ya Kanisa niligundua ya kwamba jitihada za kushinikiza kuwa na nia njema zenyewe pia ni dhambi.

“Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho matukano, kiburi upumbavu” (Marko 7:21-22).

Niligundua ya kwamba nisingeweza kuwa na uzuri wa kweli kwa kuwa nafsi yangu ilijaa mambo ya uovu, na tabu ya dhambi haijatafutiwa suluhisho. Niligundua karibu kuelekea motoni. Kuanzia hapo nilipata taabu juu ya dhambi zangu na kuamua kumuuliza Mchungaji Samuel Kim kwa msaada. Nilijifunza toka kwake kwamba Yesu ndiye pekee “aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29) na kwa hilo yeye

alikwisha zibeba dhambi zangu na kulipa yote pia. Ilinipa faraja kubwa na moyo wangu uliojeruhiwa ulionekana kuingia tena katika tulizo litokalo Mbinguni.

Baadaye nilikutana tena na Mchungaji Paul Jong na kujifunza ni kwa namna gani Yesu alisafisha dhambi zangu na namna gani watu wa Israel kwa nyakati za mwanzo walitoa dhabihu katika Agano la Kale. Kwa nyongeza pia niligundua sababu gani Yesu aliye tungwa mimbani kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 1:20) ilivyo mpasa kulaaniwa na kutundikwa mtini (Wagalatia 3:13). “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Yohana Mbatizaji, aliye kuhani mkuu wa mwisho alimbatiza Yesu na kumtwika dhambi zote za Ulimwengu, Mwanakondoo asiye na doa ndipo Yesu alipolipia mshahara wa dhambi zetu zote pale msalabani.

Page 300: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

300 Shuhuda za Wokovu

Hii ilikuwa ni Injili ya kweli iliyoamsha hamasa ndani yangu na kunifanya mwenye haki. Mimi ndiye hapo mwanzo niliyekuwa na dhambi, sasa ni mwenye haki.

“Ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya” (2Korintho 5:17). Ndiyo ilivyo kwangu. Nilitubu juu ya maisha yangu (Matendo 11:18). na nilibatizwa katika Kristo, na hapo hapakuwepo tena na hukumu (Warumi 8:1). Nimetulia juu ya Neema ya Kristo, namshukuru Mungu kwa kuniokoa. Nawatakia wote wale wenye kuteseka juu ya dhambi zao na kumtafuta Yesu waweze kupata Injili yake ya Ukombozi kamili! Haleluya.

Toka uchawi hadi Imani ya kweli Ndani ya Mungu.

Dada Sung-neo Kim, Korea

Niliolewa katika umri wa miaka 19, na

ndugu wa mume wangu walikuwa ni fukara. Tokea hapo sikuwahi kuwa na utajiri wala kamwe sikupendwa na mume wangu. Niliwaonea wivu wanawake wale walio na upendo kwa waume zao na kufurahia utajiri. Ndugu wa mume wangu waliamini miungu wa mlimani, na Baba mkwe wangu alikuwa ni mpiga ramli. Mume wangu aliandikishwa kwenda jeshini siku 3 baada ya ndoa yetu, na shemeji yangu alipata wazimu katika umri wa miaka 22 zaidi ya hayo Mama mkwe alipata upofu wa macho kati ya umri wa miaka 50. Nyakati hizo zilikuwa ni balaa

Page 301: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

301 Shuhuda za Wokovu

kwangu. Kwa kuwa sikuwa na kisomo wala uzuri

wa sura hata akili ya maendeleo au uhodari nilifikiri huo ulikuwa mwisho wangu kuishi namna hiyo maishani mwangu. Mama mkwe alihitaji upasuaji, lakini sikuweza kumpeleka hospitalini na sikuhangaika kumtafutia dawa. Nilitumaini kwamba angeendelea kuugua na punde angefariki.

Sasa ni umri wa miaka 54 na mama mkwe wangu alikwisha fariki miaka 2 iliyopita. Upo usemi usemao, ni nuksi kumzika mtu aliyekufa na mto wake ndani ya jeneza lake, na sikuelewa juu ya hilo, hivyo nilimzika mama mkwe wangu na mto wake wa kulalia ndani ya jeneza alimozikiwa.

Tokea hapo alinitokea ndotoni na nasikitika kuweka mto wake ndani ya jeneza na nilikuwa mkali sana kwake wakati wa uhai wake. Watu wengine huwa ni kwa

wakwe zao, lakini mimi sikujizuia kumnyanyasa. Niliteseka kwa ndoto na dhamira ilinichoma.

Nina mtoto mmoja wa kiume na wanne wa kike nilihofu juu ya jambo baya lingeweza kumpata mwanangu wa kiume. Nilipowaeleza juu ya ndoto yangu, majirani zangu walinishauri kwamba pepo wachafu walipaswa kuaguliwa, nilikwenda kwa waaguaji na kwenye mahekalu kusujudu bila kikomo na kusihi niweze kupata ahueni lakini haikuwa suluhisho. Nilihisi kuchukua hatua ya kukatisha maisha yangu ili kukwepa dhamira yangu.

Kama nisinge mpata Yesu wala kukombolewa leo hii nisinge kuwa hai. Siku moja nilikimbia nyumba yangu na kwenda kuishi na mtoto wangu wa kike na ndipo niweze kumpumzika na kunywa dawa za mitishamba. Na hii ndiyo njia Mungu

Page 302: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

302 Shuhuda za Wokovu

aliyonionyesha katika maisha. Moja kati ya watoto wangu wa kike ameokoka, na alimwalika mke wa Mchungaji wake kwa ajili yangu. Alikuja na baadhi ya wanawake wengine na kuzungumza nami.

Sikujua chochote juu ya Mungu. Lakini waliponieleza kwamba Yesu alikwisha zibeba dhambi zangu zote, niliamua kuamini maneno ya Yesu. Nilikuwa nikiwaeleza binti zangu wasiende Kanisani kwa sababu wangeweza kuleta nuksi kwa kuleta miungu wawili chini ya dari moja. Lakini nilifikiri sana mambo yangeweza kuwa mabaya zaidi na sikupenda kufa nikiwa mwenye dhambi.

Mke wa Mchungaji aliniambia kwamba watu wote huzaliwa wakiwa wenye dhambi lakini Mungu alikwisha zichukua dhambi hizo zote kwa kupitia Yesu na hatutoweza kuwa wenye dhambi kamwe ikiwa tutamwamini Yesu. Hivyo nilianza kuhudhuria Kanisani

mara kwa mara na kujaribu kusikiliza neno la Mungu, lakini sikuweza kuelewa mengi yaliyosemwa. Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda, maneno ya Mungu yalianza kuleta maana kwangu. Niligundua kwamba nilizaliwa mwenye dhambi na sina msaada wa kutokuwa mwenye dhambi kwa sababu ya dhambi ya asili. Pia niligundua kwamba mawazo ya uovu akilini mwangu yalikuwa ni dhambi mbele ya Mungu.

Kutoa dhabihu katika Agano la Kale ilikuwa ndiyo njia ya Mungu kuonyesha mambo mema yajayo. Na Yesu, kama ilivyokuwa katika kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka katika Agano la Kale, ndivyo alivyo batizwa na Yohana na dhambi zote alitwikwa yeye katika Yordani. Alibeba dhambi zetu zote na kutoa damu yake msalabani ili kuzilipia.

Hatimaye nilikubali ya kwamba sina

Page 303: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

303 Shuhuda za Wokovu

dhambi na hakuna awezaye kunihukumu. Na ndipo nilipolala kwa amani kuanzia hapo.

“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1). Niliteseka sana kwa dhambi ndani ya moyo wangu na sasa dhambi zimetoweka. Sina tena ndoto mbaya.

Siwezi kuandika vyema juu ya hisia zangu kwani sijui kusoma vyema lakini naweza kuelezea kwa mtu yoyote namna vile Yesu alivyobeba dhambi zote za moyoni mwangu. Naomba kwamba Yesu aweze kumwokoa mume wangu na ndugu wa familia yangu kama alivyo niokoa. Natumaini ushuhuda huu utawasaidia wengine kutafuta ukombozi katika Yesu.

Namshukuru Mungu kwa kuniokoa na nina furaha kuweza kusambaza Injili kwa watu wengi. Sasa sina wivu juu ya wenye utajiri wala walio nadhifu tena.

Moscow yahubiriwa kwa Injili ya kweli

Dada Belova Lyssa

Moscow – Russia

Napenda kuwasalimu watumishi wote katika Korea katika jina la Yesu na kushiriki nao katika tukio la furaha lililo badilisha kabisa maisha yangu.

Katika semina iliyofanyika Moscow miaka ya nyuma kidogo, nilipata kusikia maneno ya Mungu yaliyo nishangaza. Nilipo shiriki katika mafunzo ya semina pale Korea mwaka uliofuata, nilisikia mafunzo mengi yahusuyo Neno la Mungu hasa juu ya kuzaliwa upya katika maji na Roho. Furaha ilioje kuona kwa ufasaha zaidi jinsi nilivyoachiwa huru toka dhambi zangu zote!

Page 304: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

304 Shuhuda za Wokovu

Yapata miaka 6 tangu nilipo mwamini Yesu. Kabla ya kuzaliwa upya nilifundishwa kwamba mimi nilikuwa mdhambi mkubwa na hivyo kutubu kila siku mara zote. Nilipata ubatizo wa maji mengi, lakini bado nilikuwa sijazaliwa upya. Niligundua kwamba mimi ni mwenye dhambi moyoni. Ilinibidi kuendelea kuomba msamaha mara kwa mara mbele za Mungu. Nilikuwa mara zote kwenye mateso ya dhambi. Lakini ukweli ni kwamba nilimwamini Mungu na asingeweza kuniacha katika simanzi hilo na hivyo angeweza kwa kiasi fulani kuniokoa hapo mwishoni.

Hapa ndipo Mungu alipo nipeleka kwa mtumishi wake aliyezaliwa upya. Kwa kupitia yeye niliweza kusikia ile Injili yenye thamani katika ulimwengu huu, iliyo ya kweli kwa wokovu. Nilijifunza kuwa Yesu alizitakasa dhambi zangu zote kwa ubatizo wake na kwa msalaba hivyo sikuwa na dhambi tena!

Sasa mimi si mwenye dhambi tena, na moyo wangu umejawa na furaha. Hivyo kwa sasa badala ya sala za toba, ninatoa shukrani zangu kila siku mbele za Mungu na maisha yangu yamekuwa ya amani na furaha najua sasa hakuna Injili nyingine tena, hakuna imani nyingine tena kama ilivyo hii sasa. Ninachoomba ni imani yangu iweze kuwa imara na madhubuti. Natoa sifa kwa Mungu kila siku na kuamini kwamba hakuna imani iliyo na thamani kama hii.

Niko na amani huku nikijua nitaingia katika ufalme wa Mbinguni maisha yangu yatakapo fika mwisho. Sasa namtumikia Mungu na kuhubiri kwa wengine wanizungukao. Naishi katika furaha isiyokwisha, huku nikishiriki upendo wa Mungu kwa wengine katika ulimwengu huu.

Page 305: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

305 Shuhuda za Wokovu

Sasa nina imani madhubuti katika Kristo

Peter Chris, kijana wa Kristo, Nigeria.

Ninachoelewa kutoka na kitabu hiki,

ambacho ni ueleo sahihi wa haki ya Mungu, ni juu ya ubatizo wa Yesu na Msalaba. Vyote hivi viwili vinapaswa kwenda pamoja ili kuleta hitimisho la kweli katika wokovu wetu. Ubatizo wa Yesu (maji) alioupata, toka kwa Yohana Mbatizaji aliye mwakilishi wa wanadamu wote, ulichukua dhambi za wanadamu wote juu ya kichwa chake kwa kupitia ubatizo (ulio katika kuwekewa mikono) na hivyo kuzibeba hadi msalabani kwa hukumu yake badala yetu. Hivyo ikiwa nisinge ukubali ubatizo wake, ambao ndio ulio mpeleka msalabani, wokovu wangu

usingeweza kukamilika bila kujali ni kwa namna gani ushindi wa Kristo pale msalabani ulivyo.

Bado natenda dhambi ingawa ukweli kwamba nimempokea Kristo lakini mimi si mwenye dhambi kwa ajili ya Kristo asiye na dhambi na kufanya mwenye dhambi kwa ajili yetu ili tuweze kuhesabiwa haki mbele za Mungu kutokana naa kitabu chako, sasa nina imani madhubuti katika kazi ya wokovu kupitia Kristo kwa ubatizo wake na msalaba (maji na damu) uliolipa dhambi zote za nyuma, sasa na hata zijazo. Mungu amenitakasa kwa dhambi zangu zote na kumhukumu Kristo badala yangu.

Nikiwa Mkristo niliyezaliwa upya napenda kufanya niwezalo kuzuia jambo lolote litakalo tupeleka dhambini. Yakupasa kuelewa Kristo alikwisha lipa dhambi zetu zote kwa niaba yetu lakini tusipende dhambi

Page 306: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

306 Shuhuda za Wokovu

tena na tukienenda tunadhihaki neema yake ya wokovu.

Yesu alizibeba dhambi zangu

Mchungaji Timothy kutoka, Kenya.

Mungu akubari Mchungaji Paul C. Jong kwa kuleta Injili iliyo ya kweli kwa ufasaha zaidi kwa wasomaji wa kitabu hiki “Je umezaliwa kweli upya katika Maji na Roho?” Niliposoma kitabu hiki baadaye katika majuma machache yaliyopita, ujumbe wa ukombozi kupitia kifo cha Mwokozi wetu Yesu Kristo ukawa wa dhahiri zaidi maishani mwangu. Ukweli wa ubatizo wake ambao ulimtwika dhambi zote Yesu na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani, ulio mpatia kila

mwanadamu uhakika kwamba mzigo wote wa dhambi uliondolewa katika maisha mara moja tunapo amini Injili hii.

Yohana Mbatizaji alifananishwa na Haruni Kuhani Mkuu katika Agano la Kale, aliye toa dhabihu kwa ajili ya dhambi ya wana wa Israeli. Haruni alitoa dhabihu ili kumsihi Mungu aweze kusamehe dhambi zilizo tendwa na Waisraeli. Alimtwika dhambi zote yule mnyama wa kafara kwa kumwekea mikono juu ya kichwa chake. Ndivyo ilivyo pia, Yesu katika ubatizo wake alichukua dhambi zetu alipowekewa mikono juu yake na Yohana Mbatizaji. Kuhani mkuu ilimpasa kutoa mnyama wa kafara kila mwaka. “Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka, maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi” (Waebrania 10:3-4). Hivyo basi, Yesu Kristo alifanya hili mara moja na

Page 307: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

307 Shuhuda za Wokovu

kwa wakati wote kwa wanadamu wote. Tunapomwamini Bwana Yesu Kristo, tunapokea msamaha wa dhambi mara moja kwa wakati wote.

Paul C. Jong anatuonyesha kwa ufasaha namna vile dhambi zetu zilivyo bebwa na Yesu na hivyo hazitoweza kamwe kuwa ni tatizo ndani ya maisha yetu. Mimi sasa si mwenye dhambi kamwe kwa kuwa nimesamehewa baada ya YESU KUBEBA DHAMBI ZANGU KWA NIABA YANGU kwa kupitia ubatizo na alikufa badala yangu.

Kila mtu tatizo lililo kubwa zaidi leo hii ni uhuru toka asili ya dhambi. Kitabu hiki kinaonyesha bayana namna ile tutakayoweza kuishi maisha yasiyo na dhambi pia hukumu ikiwa tutaamini Injili ya kweli ya Kristo. Namshukuru Mungu sana kwa ufunuo huu kupitia mtumishi wake Paul C. Jong.

LO! Ni ajabu!

Mmisionari Brualla Johnson, USA.

Nawaletea salamu na habari njema katika jina lile lenye Thamani la Bwana na Mwokozi Yesu Kristo. Hili ni jibu la swali ulilonitumia kwa barua pepe (e-mail) siku chache zilizopta. “Kwa nini Yohana Mbatizaji alimwekea mikono Yesu katika mto Yordani?”

Ilikuwa ni Sheria ya Upatanisho katika Agano la Kale. Ilikuwa ni amri ya Mungu kwa Musa kuwasimika ndugu zake, Haruni Kuhani Mkuu wa kwanza, kwa kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka (mbuzi) na kukiri dhambi kuu za wana wa Israeli na makosa yao (Isaya 53:3-5). Na baada ya hapo, mbuzi huyo angetwikwa na kubeba uovu na makosa

Page 308: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

308 Shuhuda za Wokovu

hayo ya Israeli juu yake na kupelekwa katika mikono ya mtu anayefaa aliyemwachilia mbuzi huyo jangwani (Walawi 16:21-22).

Yohana Mbatizaji aliweka mikono juu ya kichwa cha Yesu kwa namna hiyo punde kabla ya huduma ya Yesu kuanza. Ili Yesu aweze kuzibeba dhambi na uovu wote wa ulimwengu huu, alikubali kwa hiyari na kunyenyekea ili abatizwe na Yohana kwa namna hiyo.

Alibeba dhambi na uovu wetu wote juu ya kichwa na mabega yake (Kuhani mkuu na mbuzi; Isaya 53:3-5, Mathayo 3:13-17).

Ubatizo (kuzama kwenye maji), ni huu Yesu alichukua au kubeba dhambi zote za ulimwengu juu yake. Ulikuwa sasa liwe ondoleo, usafi, utakaso na utakatifu kwa sakramenti ya ubatizo (Yohana 1:29).

Biblia inasema hivi “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia

yake ajapo jikwaa hataanguka chini, Bwana hushika mkono na kumtengeneza” (Zaburi 37:23-24). “Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Kama ilivyo andikwa, ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja, Hakuna afahamuye hakuna amtafutaye Mungu (Warumi 3:10 –12).

Lo! Lakini Mungu asifiwe, Haleluya! Utukufu ni kwa Mungu! “kwa neema tumeokolewa kupitia imani” (Waefeso 2:8, 1Yohana 1:9). Mwanakondoo wa Mungu aliyezichukua dhambi za ulimwengu juu yake kupitia ubatizo na kifo chake msalabani (Yohana 1:29).

Sina dhambi kwa kuwa nimeokolewa kwa neema ya Yesu Kristo kupitia imani ya kuoshwa na kutakaswa na Yesu Kristo kwa ubatizo wake na damu ya Mwana Kondoo wa Mungu.

Page 309: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

309 Shuhuda za Wokovu

Sasa yatupasa “kuirudia Injili ya Maji na Roho.” Kuirudia Injili hii maana yake ni kuja na moyo wa unyenyekevu na moyo wa kujitolea na kukiri kwa kinywa. Na Bwana Yesu atatusamehe dhambi zetu zote na kutuponya maumivu na magonjwa hata udhalimu wote (1Yohana 1:9, 2Nyakati 7:14, 3Yohana 2) kwa kupitia Injili ya kweli katika maji na Roho na pia kufanya “tamko la kweli juu ya dhambi” na kuhuishwa kwa kugeuzwa nia ya dhamira na Roho wa Mungu hivyo na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu (Matendo 1:5).

Nina shauku na furaha kwa kusoma kitabu hiki iliyo nifanya nielewe na kunipa ueleo wa wa ndani juu ya neno la Mungu. Nyenzo hii ya ajabu na nguvu imenipa pia elimu na neno nilitegemealo ambalo sikulijua hapa awali LO! Ni ajabu!

Nilikuwa mwenye dhambi asiye na tumaini

Bi Alderman, USA

Kwanza ya yote, Mungu alimtuma

mtumishi wake Yohana Mbatizaji ili ambatize mwana wake ili Yohana aweze kusaidia kutayarisha njia ya wokovu. Yohana Mbatizaji aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Yesu katika mto Yordani. Ilikuwa ni tendo la haki ya mwanadamu lililochukua dhambi zote za wanadamu, Yesu alibeba dhambi za ulimwengu kwa ubatizo wake. Yesu alitoa maisha yake katika msalaba kwa mshahara wa dhambi. Alilipa mshahara wa dhambi kwa kifo chake msalabani.

Dhambi zote alibebeshwa Yesu na alihukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo kwa

Page 310: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

310 Shuhuda za Wokovu

ajili yetu ili aweze kuwaokoa wanadamu. Ilimbidi Yesu azibebe dhambi zetu na kufa kwa dhambi hizo. Mtu atakuwa mwenye dhambi ikiwa hatoamini ubatizo wa Yesu Kristo na Msalaba. Hivyo ni dhambi kukataa Neno la Mungu na kukwepa ukweli na kuelekea kanuni potofu. Ni dhambi ikiwa mtu hatoamini Maandiko ya neno la Mungu kwamba Yesu alibatizwa na kufa msalabani na alifufuliwa ili kutuweka huru kwa dhambi zetu.

Kwa kutubu na kukiri kwetu kwamba sisi ni wenye dhambi na kwa kumwamini Yesu Mwana wa Mungu, kuwa ni Mwokozi aliye tuokoa toka dhambini, tutaweza kuwa huru kabisa. Hivyo yatubidi kuamini ubatizo na damu ya Yesu kwa utakaso wa dhambi zetu zote.

Nalikuwa mwenye dhambi asiye na tumaini kabla ya kumwamini Yesu na

ubatizo wake! Ikiwa Yesu Kristo asingebatizwa na Yohana Mbatizaji, nisingeweza chochote bali kuwa mwenye dhambi na kuangamia.

Leo naweza kusimama mbele za Mungu

Mchungaji Steven Icke, England

Katika agano la Kale, Kuhani Mkuu

aliweka mikono yake juu ya sadaka ile ya mnyama wa kuteketezwa ili kumtwika dhambi zote (Walawi 16:3-4) kuwekea mikono ilikuwa ni sehemu muhimu ya tendo la siku ya upatanisho. Kama isingefanyika sadaka hii itolewayo isingeweza kutolewa

Page 311: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

311 Shuhuda za Wokovu

kwani upatanisho wa dhambi usingekamilika bila ya tendo hilo, kumtwika mnyama wa sadaka dhambi zote za mwaka za wana wa Israeli.

Walawi 16:21 “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende Jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.”

Alitwaa mbuzi wawili kwa sadaka ya dhambi na ndama kwa sadaka kuteketezwa toka kwa watu. Aliwaleta mbele ya Mungu malangoni pa madhabau na kupiga kura kwa uchaguzi wa mmoja kati yao “awe wa Bwana” na aliyebaki kuwa wa “Azazeli.” Yule wa “Bwana” alitolewa mbele za Bwana kama sadaka ya dhambi na yule wa “Azazeli”

alitolewa akiwa hai mbele za Bwana kwa upatanisho wa dhambi za wana wa Israeli katika mwaka mzima na aliachiliwa atange tange jangwani hadi kufa (Walawi 16:7-10).

Dhambi za wana wa Israeli zilipaswa kutwikwa “Azazeli” kwa kuwekewa mikono. Hapo Azazeli aliyebeba dhambi zote za wana Israeli aliachiwa jangwani kwa ajili ya amani kati ya watu na Mungu. Hivyo dhambi za mwaka za wana wa Israeli zilitakaswa. Na kwa njia hiyo pia katika Agano jipya Yesu Kristo alibatizwa (kwa kuwekewa mikono katika Agano la Kale) na Yohana Mbatizaji ambaye aliyekuwa uzao wa Kuhani Mkuu Haruni, na kubeba dhambi zote za ulimwengu akiwa Mwana Kondoo wa sadaka ili kukamilisha wokovu wa Mungu (Walawi 20:22, Mathayo 3:15 Yohana 1:29, 36).

Katika Agano la Kale, kabla ya kupiga kura, Haruni alimchinja ndama kama sadaka

Page 312: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

312 Shuhuda za Wokovu

ya dhambi zake na nyumba yake (Walawi 16:11). Na baadaye alibeba chetezo iliyojaa makaa ya moto toka altare mbele za Bwana na akiwa amebeba mikononi uvumba wenye harufu nzuri uliosagwa vyema na kupeleka nyuma ya pazia. Ndipo alipoweka uvumba huo katika makaa yale ya moto yaliyo katika chetezo mbele ya Bwana ili wingu la moshi wa uvumba huo uweze kusambaa juu ya kiti cha rehema. Pia alichukua kiasi cha damu ya ndama na kunyunyizia kwa vidole vyake juu ya kiti cha rehema mara saba (Walawi 16:12-19).

Katika siku ile ya upatanisho kuwekea mikono ya Haruni juu ya sadaka ile ya mnyama kusingeweza kuachwa. Haruni aliweka mikono juu ya mbuzi na kumtwika dhambi zote na uovu wote wa wana wa Israeli juu ya kichwa chake. Na ndipo alipokabidhiwa katika mikono ya mtu aliye

tayari kwa kumpeleka jangwani na kuachiwa kutangatanga hadi kufa. Azazeli huyo alitangatanga jangwani hadi kufa. Alitangatanga jangwani na dhambi za wana wa Israeli na mwishowe kufa. Hii ilikuwa sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale.

Hii inafanana na Agano Jipya ambapo Yesu Kristo, KAMA Azazeli, aliyezichukua dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa kupita ubatizo na kutokwa damu na kufa juu ya msalaba kwa ajili yetu.

Hivyo sasa, wokovu utokanao na dhambi zetu zote hauwezi kuletwa bila ubatizo na kusulubiwa kwa Kuhani Mkuu wa Mbinguni, Yesu Kristo. Hii ni kuhitimisha wokovu wa kuzaliwa upya katika maji na Roho.

Yesu ndiye “aondoaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29) na yeye ndiye aliyezichukuwa dhambi zangu na kuzilipia gharama pia. Yesu alitakasa dhambi zetu

Page 313: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

313 Shuhuda za Wokovu

zote kwa jinsi ile wana wa Israeli walivyotoa sadaka katika Agano la Kale. Na hii ndiyo sababu Yesu aliye tungwa katika mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 1:20) ilimbidi alaaniwe na kutundikwa mtini (Wagalatia 3:13). “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

Yohana Mbatizaji kama Kuhana Mkuu alimbatiza na kuweka dhambi zetu zote pale msalabani hii ni kweli ya Injili iliyo nihamasisha na kunifanya kuwa mwenye haki. Mimi ambaye hapo awali nilikuwa mwenye dhambi, imenipasa kuwa mwenye haki.

“Ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2Korintho 5:17). Niliungama maisha yangu (Matendo 11:18) na kubatizwa katika Kristo, na hakuna hukumu juu yangu tena (Warumi 8:1). Nimo ndani ya

neema za Mungu na namshukuru Mungu kwa kuniokoa. Ingawa nikiwa na dhambi nitaugeukia ubatizo wa Yesu kwa kufahamu kuwa Yesu alikwisha zilipia gharama na kwa kupitia neema yake napokea moja kwa moja msamaha BWANA ASIFIWE!

Sasa sina dhambi tena ingawa sitoacha kutenda dhambi katika maisha yangu ya kila siku. Imeandikwa “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Nimegundua kwamba nisingeweza simama mbele ya Mungu nikiwa na dhambi zote hizi na moyo wangu ukiwa mzito, ingawa Mungu ANANIPENDA. Alimtuma mwana wake ili anikomboe “Tazama, huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29). Nimegundua kwamba dhambi za ulimwengu maana yake ni dhambi zote, pamoja na zangu. Si zile za jana na leo, bali hata zile za kesho na

Page 314: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

314 Shuhuda za Wokovu

nyakati zijazo. Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu alipobatizwa.

“Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasvyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali” (Mathayo 3:15)

Ndipo mwishoni nimekuja kuamini kwamba dhambi zangu zote alizibeba Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji na hivyo dhambi zangu zote zilipo lipiwa alipokufa msalabani “kwa kuwa uhai wa mwili katika hiyo damu nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu kwani hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi!” (Walawi 17:11). Yesu hakufa bali alisema “yamekwisha” (Yohana 19:30) ubavu wake ulichomwa kwa mkuki na papo hapo maji na damu vilitoka (Yohana 19:34) na kuangusha ukuta wa utengano wa dhambi kati ya Mungu na wanadamu. Naweza sasa

kusimama mbele ya Mungu nikiwa nimekombolewa hakika!

Sasa naamini hakika Injili ya maji na Roho

Kaka Godson, India.

Katika biblia takatifu tunaweza kuona

maelezo juu ya ubatizo wa Yesu. Yohana 3:5 alisema “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu “Maji yaliyo tajwa hapa ni ubatizo wa Yesu hatutoweza kuokolewa bila ubatizo. Na mtume Petro alitaja hii kuwa ni “mfano wa mambo yale yaokoayo” (1Petro 3:21).

Hatuwezi kukombolewa na Mungu kwa kuamini kifo cha Yesu tu pale msalabani.

Page 315: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

315 Shuhuda za Wokovu

Katika Agano la Kale, ikiwa Waisraeli walitoa sadaka bila ya kuwekea mikono juu yake, isingekuwa sahihi. Na kwa namna hiyo basi Yohana Mbatizaji kama mwakilishi wa wanadamu, aliweka mikono yake juu ya Yesu alipombatiza, ambayo inafanya maana ya kutwikwa kwa Yesu dhambi zetu zote.

Sasa ni wazi kwetu Yesu alitimiza haki ya Mungu kwa watu wote kwa ubatizo wake kwa haki na ukamilifu. Hivyo Yohana Mbatizaji alishuhudia siku iliyo fuata baada ya kumbatiza Yesu “Tazama huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29). Akiwa na dhambi zote za walimwengu juu ya mabega yake Yesu alikwenda nazo pale msalabani na kupokea hukumu kwa dhambi hizo alizo beba mwenyewe kwa ubatizo wake. Ndipo alikufa msalabani kwa kusema “yamekwisha” (Yohana 19:30).

Yesu Kristo alizitakasa dhambi zetu zote hata kabla ya kuzaliwa kwetu. Alibeba zote. Dhambi tutakazo tenda kesho nazo pia zilijumuishwa katika dhambi za ulimwengu. Dhambi hizi alitwishwa Yesu miaka 2000 iliyopita. Hakuacha hata moja nyuma. Injili yatuambia tuamini kwa moyo wetu wote kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote za zamani na zijazo kwa mara moja na kuzilipia zote.

“Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27). Kwa kubatizwa katika Kristo maana yake tumeungana na Kristo kwa imani katika ubatizo wake Yesu alipobatizwa, dhambi zetu zote alitwikwa yeye na Yohana Mbatizaji na tulitakaswa kwa usemi mwingine, hatuna dhambi tena sasa. Tumekuwa wenye haki tangu pale wakati ule tulipo upokea ubatizo wa Yesu mioyoni

Page 316: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

316 Shuhuda za Wokovu

mwetu kwa kuamini. Nyakati hizi wengi hawana uhakika ikiwa

wamekwisha samehewa dhambi zao zote au la. Wengi hutumia muda wao wote katika maisha yao wakiwa njia panda. Ingawa kwa jinsi hii, ikiwa tutajisalimisha kwa injili ya kweli, tutaweza kuwa na uhakika kwa kusema hatuna dhambi kamwe sasa.

Yesu alisema yakwamba, ametutakasa sisi sote mara moja na kwa wakati wote. Ikiwa tutaendelea kutubu kila siku, bila shaka tutakuwa tunarudi katika nyakati za Agano la Kale. Hapo ndipo hatutoweza kamwe kuwa wenye haki. Hata kama tuna mwamini Mungu, hatuwezi kuishi bila kutenda dhambi. Na kwa jinsi hiyo hatutoweza kutakaswa kwa kufanya toba za mara kwa mara. Tutaendelea kutenda dhambi kila leo bila kikomo. Hivyo si rahisi kutubu kwa ukamilifu kwa dhambi zetu zote.

Katika Kitabu cha Waebrania, tunaweza kuona kwamba madeni yetu yalilipwa kwa wakati mmoja. Hivyo Yesu alibatizwa mara moja na kujitoa nafsi yake msalabani mara moja ili tuweze kutakaswa sisi sote kwa wakati mmoja. Hatukukombolewa pale tunapo tubu, bali tumekombolewa toka dhambini mara moja na kwa wakati wote. “Katika mapenzi hayo tumepata kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10). Na mwisho jambo litupasalo kufanya ni kuamini ubatizo na kusulubiwa.

Sasa hakika naamini Injili ya maji na Roho ambayo bila shaka ni Injili ya kweli. Naahidi kufanya mambo yote kwa uaminifu unipayo kwa kuwa nampenda Yesu zaidi ya chochote na hiki ndicho kitu pekee ninachoweza kufanya kwake.

Page 317: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MENGINEYO 2

Maelezo ya Ziada

Page 318: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

318 Maelezo ya Ziada

Maelezo ya Ziada

Dia Kutolewa kwa mali au mtu kwa kulipia

thamani inayodaiwa. Thamani au malipo ya fedha yanayodaiwa kutolewa. Mara nyingi hutumika kama uwakilishi wa moja kwa moja katika ukombozi (mfano Kutoka 21:30; kiasi cha fedha; Hesabu 35:31-32, Isaya 43:3 “dia’’). Katika Agano Jipya, Mathayo 20:28 na Marko 10:45 yaeleza kafara kama “malipo ya fedha.”

Patana / Upatanisho Tendo la ibada katika kutwika dhambi za

wanadamu wote kwa Yesu. Katika Agano la Kale upatanisho ulikuwa ni kutwika dhambi zote kwa sadaka ya mnyama kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama huyo. Katika Agano Jipya, maana yake ni ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji. Kwa Kiebarania na Kigiriki neno hili humaanisha kutwika dhambi juu ya Yesu Kristo ili wenye dhambi waweze kuingia kwenye haki ya mahusiano na Mungu. Agano Jipya linaeleza juu ya kutolewa sadaka kwa upatanisho kwa uwazi; ubatizo wa Yesu na Kifo chake Msalabani.

Katika Agano la Kale: Neno “upatanisho” limetumika zaidi ya mara 100 na mara zote limeelezea kama (Walawi 23:27, 25:9, Hesabu 5:8) ‘kaphar’ Kiebrania (kila mara huandikwe kama “kufanya upatanisho”) Upatanisho ni tafsiri ya neno la Kiebrania lenye maana kamili ya kutwika dhambi kwa

Page 319: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

319 Maelezo ya Ziada

kuwekewa mikono juu ya kichwa cha mbuzi na kuzitamka juu yake maovu yote ya waisraeli (Walawi 16:20).

Katika Agano Jipya: Upatanisho unahusishwa katika Karamani ‘Kpr’ ikiwa na maana ‘kufunika’. Maana yake upatizo wa ukombozi wa Yesu katika Agano Jipya. Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa akiwa na umri wa miaka 30 ili kutimiza ukombozi wa wanadamu wote.

Upatanisho wa Kibiblia. A. Katika Agano la Kale, upatanisho kwa

kawaida ulipatikana kwa kupitia mnyama wa sadaka (Mf. Kutoka 30:10, Walawi 1:3-5, 4:20-21, 16:6-22).

B. Katika Agano Jipya maana ya sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale ilikuwa ni

msingi uliwekwa, lakini ukombozi wa wanadamu ungeweza kukamilishwa tu endapo mwili wa Kristo Yesu ungetolewa kwa kufa kwa ajili ya dhambi zetu (1Wakorintho 15:3).

Neno upatanisho halikutumika tu katika kumaanisha kifo cha Kristo kulipia dhambi ya asili, bali ilikuwa pia kubeba dhambi zote za wanadamu. Baada ya ubatizo ambao dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa kwake Yesu (Mathayo 3:15), aliokoa wanadamu wote kwa kuitoa damu yake msalabani. Walawi 1:1-5, Yahana 19:30).

Mtume Paulo ameelezea katika 2Wakorintho 5:14 kwamba “mmoja alikufa kwa ajili ya wote” ndipo basi katika mstari ufuatao wa 21 inaelezea kwamba ilikuwa “ni kwa ajili yetu”. Ni mistari michache katika Agano Jipya hufananisha na Yesu kama Sadaka (mf. Waefeso 5:2); Yohana 1:29, 36

Page 320: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

320 Maelezo ya Ziada

(Mwanakondoo – Yohana Mbatizaji) na 1Wakorintho 5:7 (pasaka wetu – Mtume Paulo).

Hata hivyo, Paulo ameweka bayana kwamba ubatizo wa Yesu katika mto Yordani ulikuwa ni upatanisho wa dhambi zote za ulimwengu. Ameelezea katika Warumi 6 kwamba dhambi zote za ulimwenguni alitwikwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake na Yohana Mbatizaji.

Ameendelea kuelezea juu yake kusulubiwa kwa Yesu kuwa ni hukumu na fidia kwa dhambi zetu na ya upatanisho ilitolewa kwa roho za watu wote.

Kifo cha Yesu kilikuwa ni utambulizi wa mpango wa Mungu unao onyeshwa katika sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale. Kuwekea mikono katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ni kulingana na sheria ya Mungu. (Isaya 53:10,

Mathayo 3:13 –17, Waebrania 7:1-10, 18 1Petro 3:21).

Agano Jipya haliishii hapo tu na ubatizo na kifo cha Yesu, bali linakwenda zaidi kwa kutuelezea juu ya kutimizwa kwa wokovu kwa kubatizwa kwetu katika Kristo, ambapo kunatuwezesha sisi binafsi kufa na Yesu (Warumi 6:3-7, Wagalatia 2:19-20).

Inatuelezea kuwa Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu Kristo ili kubeba dhambi zetu zote za ulimwengu na kwa matokeo hayo alisulubiwa. Yesu Kristo kwa kupitia ubatizo wake na damu yake si pia alitakasa dhambi za ulimwengu, bali pia aliokoa kila mmoja wetu toka nguvu za shetani na kuturudisha katika nguvu za Mungu kwa kukubali adhabu na kuvumilia maumivu kwa niaba ya wanadamu wote.

Hivyo ukombozi wa Yesu umesuluhisha tatizo la dhambi lililoweka kizuizi kwa

Page 321: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

321 Maelezo ya Ziada

wanadamu kutoweza kuwa karibu na Mungu. Tendo hili la kihistoria la muda limerudisha amani na utulivu kati ya wanadamu na Mungu kwa kuleta wokovu, furaha (Warumi 5:11), uzima (Warumi 5:17-18) na ukombozi (Mathayo 3:15, Yohana 1:29, Waebrania 10:1-20, Waefeso 1:7, Wakolosai 1:14) katika wakati mmoja.

Siku ya Upatanisho. Kiebrania ni umaanisho wa siku ya

“kufunika au “kusuluhisha”. Sehemu muhimu ya siku ya Wayahudi ilikuwa ni siku ya Upatanisho katika siku ya kumi ya mwezi wa saba (Walawi 23:27, 25:9). Tunaweza kuona katika walawi 16 kwamba hata Kuhani Mkuu hakuruhusiwa kuingia Patakatifu pa Patakatifu isipokuwa katika

ibada iliyo tengwa katika siku hiyo. Upatanisho pia ulihitajika kabla ya kuingia

patakatifu pa patakatifu, na pia ulihitajika kwa Wana wa Israeli; kwa njia hii, ndipo Kuhani mkuu aliweza kutoa sadaka ili aweze kutwisha dhambi kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka. Waisraeli walifikiri juu ya utakatifu wa Mungu na juu ya dhambi zao katika Siku hiyo ya Upatanisho.

Katika muda huo, kwa kiasi cha sadaka 15 (ikijumuishwa na Azazeli) 12 sadaka ya kuteketezwa na 3 sadaka ya upatanisho walitolewa kwa Mungu (Walawi 16:5-29, Hesabu 29:7-11). Ikiwa tutahesabu “mwana kondoo mwingine” aliyetajwa katika Hesabu 28:8 zipo sadaka 13 za kuteketezwa na 4 za upatanisho.

Siku Waisraeli walipokuwa wakitoa sadaka ya upatanisho kwa dhambi za mwaka ilikuwa

Page 322: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

322 Maelezo ya Ziada

ni siku ya kumi katika mwezi wa saba. Kwa jinsi hiyo hiyo siku ya upatanisho wa dunia ilikuwa ni siku ile Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Hakika ilikuwa ni siku ya upatanisho wa wanadamu. Ilikuwa ni siku ya Mungu kutakasa dhambi zote za wanadamu ulimwenguni (Mathayo 3:13-17). Ilikuwa ni siku ya Upatanisho ambayo Mungu “alitimiza haki zote.”

Sadaka ya Upatanisho. Katika Agano la Kale, kama ilivyo sadaka

nyenginezo, sadaka ya utakaso wa Waisraeli wote ilitolewa katika madhabahu Kuhani Mkuu alijitakasa yeye binafsi kwanza na kuvaa vazi lile takatifu badala ya vazi lile la kawaida la ibada, alichagua ndama dume kwa sadaka ya dhambi na kondoo dume

kama sadaka ya kuteketezwa kwa matoleo yake binafsi na nyumba yake (Walawi 16:3-4). Kuhani Mkuu aliweka mikono yake juu ya kichwa cha kila mmoja wa sadaka hizi ili kutwika dhambi za mwaka za watu wake.

Kuwekea mikono kulikuwa ni jambo muhimu katika siku ya upatanisho. Kama isingefanyika matoleo ya sadaka hizo yasingeweza kufanyika kwa kuwa upatanisho wa dhambi usingekamilika bila kuwekewa mikono, hivyo ndivyo kutwika dhambi za mwaka za Waisraeli juu ya sadaka ya dhambi.

Katika Walawi 16:21 “Na haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa

Page 323: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

323 Maelezo ya Ziada

mtu aliye tayari.” Alichukuwa mbuzi wawili na kondoo dume

kama sadaka ya kuteketezwa kwa watu (Walawi 16:5). Na ndipo aliwatoa mbele za Bwana katika malango ya madhabahu na kupiga kura ili kuchagua moja wa Bwana na mwingine kuwa Azazeli.

Yule mmoja wa Bwana alitolewa akiwa hai mbele za Bwana kupatanisha kwa dhambi za mwaka za Waisraeli na kupelekwa jangwani (Walawi 16:7-10).

Dhambi za Israeli zilipaswa kutwikwa kwa azazeli kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu ndipo azazeli aliyebeba juu yake dhambi zote za Israeli alipopelekwa jangwani kwa kusulihisha watu na Mungu. Hivi ndivyo dhambi za mwaka zilivyotakaswa.

Katika Agano Jipya kwa namna hiyo, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji (kwa

kuwekewa mikono katika Agano la Kale) na kubeba dhambi zote za ulimwengu akiwa kama mwanakondoo wa sadaka ili kutimiza wokovu wa Mungu (Walawi 20:22, Mathayo 3:15, Yohana 1:29, 36).

Katika Agano la Kale kabla ya kupiga kura Haruni alimchinja ndama dume kama sadaka ya dhambi kwa ajili yake na nyumba (walawi 16:11). Na baadaye kuchukua chetezo kilichojaa makaa ya moto toka altare mbele ya Bwana huku mikononi akiwa amebeba uvumba wa kunukia, uliosagwa na kuwa laini, na kuchukua nyuma ya pazia. Baadaye aliweka uvumba huo juu ya chetezo yenye makaa ya moto mbele ya Bwana ili wingu la moshi wa uvumba liweze kutanda juu ya kiti cha rehema. Pia alichukua kiasi cha damu ya ndama dume na kunyunyizia kwa vidole vyake juu na mbele ya kiti cha rehema mara saba (Walawi 16:12-19).

Page 324: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

324 Maelezo ya Ziada

Katika siku ya upatanisho, kuwekea mikono kwa Haruni juu ya kichwa cha sadaka kusingeweza kuachwa. Haruni aliweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi na kumtwika dhambi zote na uovu wote wa Israeli juu ya kichwa chake. Na ndipo mtu aliye tayari atamchukua mbuzi huyo jangwani na kumwachia huko. Mbuzi huyo wa Azazeli atatangatanga huko jangwani na dhambi za Israeli mwishowe kufa. Huu ndiyo mpango halisi wa sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale.

Ni sawa sawa kama ilivyo katika Agano Jipya isipokuwa mbuzi huyo alikuwa badala ya Yesu Kristo alibeba dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa ubatizo wake, na kutokwa damu na kufa msalabani kwa ajili yetu sote.

Hivyo leo, wokovu toka dhambini hauwezi kuletwa bila ya ubatizo na kusulubiwa kwa

Yesu Kristo, Kuhani wa mbinguni aliye mkuu. Hitimisho hili ni la wokovu wa kuzaliwa upya katika maji na Roho.

Ibada ya kuwekea mikono. Huu ulikuwa ni mpango ulioletwa na

Mungu kwa ajili ya kutwika dhambi juu ya sadaka ya dhambi katika nyakati za Agano la Kale (Walawi 4:29, 16:21). Katika siku hizo za Agano la Kale, Mungu aliruhusu watu kupatanishwa kwa dhambi zao kwa kuwekea mikono sadaka za dhambi mbele ya malango ya Hema Takatifu. Ilikuwa ni kuonyesha jinsi ya ubatizo wa Yesu utakao kuja katika Agano Jipya.

Page 325: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

325 Maelezo ya Ziada

Ubatizo Ubatizo maana yake (1) kusafishwa (2)

kuzikwa (kuzamishwa) na maana ya kiroho (3) kutwika dhambi kwa kuwekea mikono, kama ilivyofanywa katika Agano la Kale.

Katika Agano jipya, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatiizaji ulikuwa ni kusafisha dhambi za ulimwengu. “Ubatizo wa Yesu” una maana ya kuchukua dhambi za wanadamu zote, kutakaswa kwa dhambi zote za ulimwengu.

Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu katika uzao wa Haruni, na kubebeshwa dhambi zote za ulimwengu juu yake. Hii ni dhumuni halisi la ubatizo.

Maana ya kiroho neno “ubatizo” ni “kutwika, kuzikwa”. Hivyo “ubatizo wa Yesu” maana yake dhambi zote alitwikwa Yesu na

kuhukumiwa badala yetu. Ili kuokoa wanadamu Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kufa kwa dhambi hizo.

Yote haya, kifo chake na pia kifo chako na changu wenye dhambi wote ulimwenguni na ufufuko wake ni ufufuo wa watu wote. Kujitoa kwake sadaka ni wokovu wa wenye dhambi na ubatizo ni ushuhuda halisi katika kutusafisha dhambi zetu zote sisi walimwengu.

Biblia inatueleza “upo mfano wa mambo haya, ambao sasa ni ule ubatizo” (1Petro 3:21). Ubatizo wa Yesu ni njia ya haki ya kuokoa wanadamu kwa kutakaswa dhambi zetu.

Dhambi. Kila jambo liendalo kinyume na Mungu ni

Page 326: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

326 Maelezo ya Ziada

dhambi. Hii inamaanisha dhambi zote, ikijumuishwa dhambi ya asili na makosa ambayo tutendayo siku zote za maisha yetu kwa jumla.

Dhambi ni “hamartia” kwa Kigiriki. Na kwa maana ya msemo ni “hamartano” yaani “kukosea kulenga” Hivyo moja ya hatari ya dhambi ni kukosa kumwamini Yesu na hivyo kukosa kuwa na uwezo wa kuokoka. Kutojua au kutoamini ukweli ni kutenda dhambi ya uasi na kumkufuru Mungu.

Ikiwa kweli hatupendi kutenda dhambi aina hii mbele ya Mungu yatupasa kuelewa Neno lake na kutambua ukweli kuwa Yesu ni Mwokozi.

Yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake kupitia maneno ya Mungu. Ni dhambi kutokubali Neno la Mungu, kupindisha ukweli, na kuamini kanuni potofu.

Biblia inatuelezea kwamba dhambi iliyo hatari zaidi, “dhambi iletayo kifo” (1Yohana 5:16) ni kutoamini kwamba Mungu alitakasa ulimwengu wote kwa dhambi. Yatupasa kuamini kuzaliwa kwa Yesu, katika kutusafisha dhambi zetu kupitia ubatizo wake, na katika kutoa maisha yake kwa damu yake pale msalabani. Ni dhambi ikiwa mtu hatoamini maandiko ya neno la Mungu kwamba Yesu alibatizwa, alikufa msalabani na alifufuliwa ili kutuweka huru kwa dhambi zetu zote.

Toba Ikiwa mtu aliyetengwa mbali na Mungu

amegundua hilo juu ya dhambi zake na kumshukuru Yesu kwa kusafishwa na dhambi hizo na kurudi kwa Mungu, hii ni

Page 327: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

327 Maelezo ya Ziada

toba. Sote sisi tumejawa na dhambi. Toba ya

kweli ni kukubali kufuata kweli; kwamba sisi ni wenye dhambi mbele ya Mungu, na hivyo hatuwezi kujizuia kutenda dhambi maishani mwetu na kwenda jehanamu tutakapo kufa, hivyo yatupasa kumkubali Yesu kama mwokozi wetu kwa kuamini kwamba alikuja ulimwenguni kutuokoa sisi wenye dhambi na hivyo alibeba dhambi zetu (kupitia ubatizo), akafa na alifufuliwa kutuokoa. Toba ya kweli ni kuacha fikra zetu na kumrudia Mungu (Matendo 2:38).

Toba ni kukiri dhambi zetu na kulirudia neno la Mungu kukubali wokovu katika maji na kwa damu kwa moyo wetu wote (1Yohana 5:6).

Toba ya kweli ni kukubali wenyewe kwamba sisi ni wenye dhambi kabisa na kumwamini Yesu, Mwana wa Mungu kama

Mwokozi wetu aliye tuokoa na dhambi zetu zote. Ili tuweze kuokolewa na kusafishwa dhambi zetu zote, yatupasa kuacha kujaribu kujitakasa kwa kupitia matendo ya sheria, na kukiri kwamba sisi ni wenye dhambi mbele ya Mungu na sheria yake, sisi basi yatupasa kukubali kweli ya wokovu wa Yesu, Injili ya maji na Roho, ambayo Yesu alituachia kwa ubatizo na damu yake.

Mwenye dhambi yampasa kuacha mawazo yake na kumrudia Yesu kikamilifu. Tutaokolewa pale tutakapo amini ubatizo wa Yesu uliozichukua dhambi zetu zote kwake.

Kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu, kusulubiwa kwake, na ufufuko wake umetimiza haki ya Mungu wokovu wa wenye dhambi. Yesu alikuja katika mwili, alibatizwa na kusulubiwa ili kutusafisha kwa dhambi zetu zote. Kwa kuwa na imani iliyo kamili katika yote haya na kuamini kwamba Yesu

Page 328: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

328 Maelezo ya Ziada

alifufuka ili awe Mwokozi wa wote wenye kumwamini katika toba ya kweli na imani ya halisi.

Wokovu. Wokovu katika Ukristo maana yake ni

“ukombozi toka kwenye nguvu au adhabu ya dhambi.” Tunapokea wokovu pale tunapokiri kwamba hatuna uwezo kujizuia kwenda motoni na kumwamini Yesu ametuokoa sisi sote toka dhambi zetu zote kwa kupitia kuzaliwa kwake, ubatizo na damu yake msalabani.

Wale wasio na dhambi kwa kuamini wokovu wa Yesu, ubatizo na damu ya Yesu huitwa “walio okoka, waliozaliwa upya, wenye haki.”

Tunaweza kutumia neno “wokovu” kwa

wale wote walio okolewa tokana na dhambi zao, pamoja na hata zile za asili na zile za kila siku, kwa kumwamini Yesu. Kama alivyo mtu aliyejongea kwa Mungu, yule ajongeaye dhambi za ulimwengu atakuwa ameokolewa kwa kumwamini Yesu kama mwokozi, kwa kuamini ubatizo na damu, maneno ya kweli ya kiroho.

Kuzaliwa upya Maana yake “kuzaliwa mara ya pili”

Mwenye dhambi atazaliwa upya na kuwa mwenye haki ikiwa ataokoka kiroho kwa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake.

Tutaweza kuzaliwa upya kiroho kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu. Waliozaliwa upya ni wale wote aliosafishwa kwa dhambi zao zote na “atatokea mara ya

Page 329: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

329 Maelezo ya Ziada

pili pasipo dhambi kwa hao wamtazamiao kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

Ondoleo la dhambi Hili ni jambo muhimu na pia kumaanisha

kusamehewa dhambi. Dhambi husamehewa pale tunapotakaswa kwa dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote kupitia Injili ya maji na kwa Roho. Imani katika Injili ya maji na kwa Roho ni kuamini mlolongo wa kweli. Uungu wa Yesu Kristo, kufanywa Mwana wa Mungu, ubatizo wake na kusulubiwa kwa ajili ya wokovu wetu wote na kufufuliwa kwake.

Ukombozi wa Yesu aliotupa waweza kuwa wetu kupitia imani katika ubatizo na damu kama ulivyo unabii uliotolewa katika Agano la kale, Yesu mwenyewe aliokoa watu wote

toka dhambini. Ukombozi katika Biblia unalenga sehemu ya kusafishwa dhambi kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na Damu yake. Dhambi zote alitwikwa, Yesu, hivyo kamwe hakuna dhambi mioyoni kwa wanadamu.

Twaweza kujiita tuliokombolewa na wenye haki pale tu dhambi zetu zote zinapotwikwa kwa Yesu kupitia imani kwa ubatizo wake.

Yesu Kristo YESU: “Mwokozi aliye okoa watu wote

kwa dhambi zao zote na kuadhibiwa nazo” Yesu humaanisha Mwokozi aliye wa pekee mwenye kuokoa watu wote toka dhambini.

KRISTO: “Mpakwa mafuta.” Palikuwapo na watu watatu walioruhusiwa kupakwa

Page 330: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

330 Maelezo ya Ziada

mafuta mbele ya Mungu kwa kuteuliwa (1) Wafalme (2) Manabii (3) Na Makuhani. Yesu alikamilika kwa haya yote.

Yesu Kristo alikuwa yote haya. Alifanya kazi katika yote haya. Yatupasa kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mfalme, Nabii na kuhani aliyeleta ukombozi na wokovu. Kwa yote haya tutamwita “Yesu Kristo.” Alikuwa ni Kuhani wa mbinguni aliyetuokoa toka dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na damu.

Hivyo, yeye ni Mfalme wa wote wenye kumwamini. Hutufanya kuelewa dhambi zetu pale tunapo kuja mbele zake. Alitufundisha kwamba sisi ni wenye dhambi toka kizazi cha mababu zetu na kwa matokeo haya, tupo chini ya hukumu ya Mungu.

Yeye pia ametufundisha ya kwamba tumesafishwa dhambi zetu kupitia ubatizo wake na damu. Aliyafanya yote haya kwa

ajili yetu sisi wenye dhambi.

Sababu gani Mwana wa Mungu kuwa mwanadamu? Alikuwa mwanadamu ili aweze kuwa

Mwokozi na kutuokoa sisi sote wenye dhambi toka dhambini na hukumuni katika jehanamu.

Yesu ni Nani? Kama ilivyo andikwa katika Mwanzo 1:3

na Yohana 1:1-3, Yeye ni Muumba, Mungu wa kweli, Mungu wa ulimwengu wote aliye okoa wenye dhambi toka dhambi za ulimwengu (Wafilipi 2:6, “ambaye yeye

Page 331: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

331 Maelezo ya Ziada

mwanzo alikuwa yu namna ya Mungu naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho,” John 1:2-3 “Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”) Yesu ni Mungu Muumba, Bwana wa ulimwengu.

Kwanamna hii, watu wengi hushuhudiwa kuokolewa kwa kutoamini juu ya upendo na wokovu wa Yesu aliyeshuka ulimwenguni katika mwili. Lakini wengi wamepokea wokovu, na kuwa watu wa Mungu na kupata uzima wa milele kwa Yesu. Wamekuwa wenye haki.

Sheria zipi zilizoletwa na Mungu? Mungu ni wa mipango, ndiye Mungu wa

kweli na hakika ndiye aliye hai. Hivyo,

aliweka sheria ulimwenguni kwa sababu zifuatazo:

1. Aliwapa wenye dhambi Sheria na Amri ili waokolewe kwa dhambi zao “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20).

2. Sheria ya pili ni Sheria ya Imani iokoayo wenye dhambi. “Sheria ya Roho wa uzima” (Warumi 8:2) inayotoa njia ya wokovu kupitia imani katika Yesu Kristo mwokozi wetu (Warumi 5:1-2). Yesu alishuka ulimwenguni kuitimiza hii sheria. Alibatizwa akatoa damu yake Msalabani na akafufuka. Yesu aliweka sheria ya wokovu ili kuokoa wale wote wenye dhambi ulimwenguni.

Mungu aliweka Sheria ya Imani kwa wale tu wenye kuamini wokovu utokanao kwa maji na Roho. Yeyote atakaye okolewa na kuwa mwana wa Mungu yampasa kwanza

Page 332: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

332 Maelezo ya Ziada

kuamini Sheria hii ya Imani ambayo Mungu ameitoa. Ndiyo pekee njia ya kuokoka. Kwa haya, ameruhusu njia ya kwenda mbinguni kwa wale wenye kuamini kuzaliwa kiroho katika kweli tokana na sheria hii.

Sheria ya Mungu. Amri kumi Vipo vipengele 613 vya sheria ya Mungu

vinavyohusu maisha yetu ya kila siku. Lakini iliyo kuu kati ya hii ni Amri kumi ambazo yatupasa kuzifuata mbele ya Mungu. Yapo maelekezo na maonyo kama vile “Ufanye hivi” na “Usifanye hivi.” Na huu ndiyo mwongozo wa maisha, na amri za Mungu tulizopewa ili tuweze kutambua dhambi zetu. Kupitia Amri zilizo andikwa na Mungu tutaweza kutambua ni kwa kiasi gani tumeacha utii kwake (Warumi 3:19-20).

Sababu Mungu kutupatia amri zake ilikuwa ni kutufanya tugundue na kuziona dhambi zetu kamwe hatutoweza kuzishika Amri zote, hivyo yatupasa kunyenyekea kwa kukubali ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi mbele yake kabla ya kumwamini Yesu. Sisi sote ni wenye dhambi na Mungu anajua kwamba kamwe hatutoweza kuishi kwa kufuata sheria yake. Hivyo, alishuka ulimwenguni kama mwanadamu, alibatizwa na kuhukumiwa msalabani. Kujaribu kuishi kwa sheria ya Mungu ni dhambi ya kiburi. Hatupaswi kufanya hivyo.

Sheria yatuonyesha ni kwa vipi Mungu alivyo mkamilifu na Mtakatifu na kwa upande mwingine ni kwa jinsi gani mwanadamu alivyo dhaifu. Kwa msemo mwingine, utakatifu na ukamilifu wa Mungu umefunuliwa katika sheria ya Mungu.

Page 333: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

333 Maelezo ya Ziada

Je, yatupasa kumwamini Yesu? Ndiyo, yatupasa kwa sababu ni Bwana

wetu, aliye pekee wa haki, na kwa sababu ni mapenzi yake “kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Hakuna Mwokozi mwingine Yesu ndiye Mwokozi wetu wa pekee. Tutaweza kukombolewa na kuzaliwa upya pale tu tutakapo mwamini yeye. Kwa kuwa na imani kwake na ndipo tutaweza kwenda mbinguni na kupata uzima wa milele.

Je, sisi Wakristo tutaweza kuwa wenye dhambi? Hapana. Mtume Paulo anasema katika

1Timotheo 1:15 kwamba yeye alikuwa “wa kwanza wao” wenye dhambi akikumbuka nyakati zile kabla ya kukutana na Yesu. Katika jumuiya za Kikristo leo hii wapo wengi wanaodhani ni wenye dhambi hata baada ya kumwamini Yesu. Lakini hivyo sivyo.

Sisi sote ni wenye dhambi kabla ya kumwamini Yesu. Ingawa tunapomwamini Yesu tu, katika njia iliyo sahihi tokana na Neno lake, tunakuwa wenye haki mara moja. Mtume Paulo anakumbuka nyakati zile kabla ya kumjua Yesu na kumkiri kwamba alikuwa Mkuu wa wenye dhambi wote.

Paulo aliyeitwa Sauli alikutana na Yesu akiwa njiani kuelekea Dameski na aligundua kwamba Yesu ndiye Mwokozi, hivyo aliamini na kumshukuru. Na kwa maisha yake yote alishuhudia kwamba haki ya Mungu, ubatizo wa Yesu uliweza kufuta dhambi zote za ulimwengu na ilimpasa afe ili kufuta dhambi

Page 334: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

334 Maelezo ya Ziada

zote za ulimwengu. Kwa maneno mengine, alikuja kuwa

mtumishi wa Mungu aliyehubiri Injili ya maji na Roho. Kwa jinsi hiyo, Wakristo wengi bado hudhani kwamba Mtume Paulo alikuwa mwenye dhambi hata baada ya kukuutana na Yesu. Wanaelewa visivyo juu ya maelezo yahusuyo Mkristo mwenye dhambi, ambaye hajazaliwa upya.

Ukweli ni huu, hakuwa tena mwenye dhambi baada ya kukutana na Yesu, bali alikuwa na uwezo wa kukutana naye popote atakapo. Alijitolea maisha yake yote kuhubiri Injili ya wokovu, ule ukombozi wa ubatizo na damu ya Yesu. Hata baada ya kufariki kwake, bado nyaraka zake zipo kwa ajili yetu kwenye Biblia, kushuhudia Injili ya maji na Roho ndiyo Injili iliyo ya kweli toka Kanisa la mwanzo. Hivyo kukiri kwake katika 1Timotheo 1:15 kulikuwa ni marudio ya

nyakati zake za nyuma na kumshukuru Bwana pia.

Je alikuwa mwenye dhambi tena baada ya kumwamini Yesu? Hapana. Alikuwa ni mwenye dhambi kabla ya kuzaliwa upya. Kwa nyakati ile alipomwamini Yesu kama Mwokozi wake, ndipo pia alipogundua kwamba dhambi za ulimwengu zilitwikwa kwa Yesu, kupitia ubatizo wake, na wakati huo kuamini upatanisho wa damu yake msalabani na akawa mwenye haki.

Sababu ya kujiita mkuu wa wenye dhambi, ilikuwa kwa sababu alikumbuka nyakati zile alizowatesa wafuasi wa Yesu na kumshukuru Mungu kwa kumuokoa, yeye aliye kosa tumaini.

Ni nani awezaye kumwita mwenye dhambi? Ni nani awezaye kumuita mtu fulani mwenye dhambi ikiwa atakuwa mwenye haki kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu

Page 335: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

335 Maelezo ya Ziada

kuwa ndipo wokovu? Ni wale wasio elewa ukweli wa wokovu wa Yesu ndiyo wenye kuweza kufanya hivyo.

Mtume Paulo alikuja kuwa mwenye haki kwa kuamini wokovu kupitia Yesu na kuanzia muda huo, kama mtumishi wa Mungu, alihubiri Injili ya kuwa mwenye haki kwa kumwamini Yesu Kristo kwa kila mmoja Mwana wa Mungu kama Mwokozi. Tokea hapo, Mtume Paulo hakuwa mwenye dhambi tena bali mwenye haki Mtumishi wa Mungu, Mtumishi wa kweli aliyehubiri Injili kwa wenye dhambi ulimwenguni pote.

Je mwenyedhambi aweza kuhubiri kwa wenye dhambi? Haitofanikiwa. Ni vipi mwenye dhambi ataweza kumhubiria mwenye dhambi mwenzake kila ambacho yeye hana! Mtu asiye okoka ataweza vipi kuokoa wengine!

Ikiwa mtu amesukumwa ataweza vipi

kumvuta mtu kwake asiye okoka, wote wataishia kuanguka. Mwenye dhambi ataweza vipi kuokoa wengine? Ataweza kwenda nao motoni. Mgonjwa ataweza vipi kumtunza mwenye ugonjwa mwingine? Anayedanganywa na Shetani ataweza vipi kuokoa wengine?

Mtume Paulo alikuwa ni mwenye dhambi, lakini akawa mwenye haki alipoamini ubatizo na damu ya Yesu na kuokolewa toka dhambini. Hivyo, aliweza kuwa mtumishi wa Mungu na kuhubiri Injili kwa wenye dhambi ulimwenguni. Aliokoa wenye dhambi wengi kwa haki ya Mungu yeye binafsi hakuwa tena mwenye dhambi tokea hapo.

Alizaliwa upya na kuishi si kwa haki ya sheria bali kwa haki ya Mungu. Akawa mtumishi wa Mungu na Mhubiri wa haki ya Mungu, na aliweza kuvua roho za wengi wasio idadi kwa Mungu. Hakuwa Mhubiri

Page 336: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

336 Maelezo ya Ziada

kwa msisimko wake au kwa haki ya sheria, bali kwa haki ya Mungu.

Je aliendelea kuwa mwenye dhambi hadi mwisho? Hapana. Alikuwa mwenye haki. Akiwa hivyo, alikuwa Mtume wa kweli kwa Mungu. Usimwite mwenye dhambi kwa sababu itakuwa ni kejeli kwa Mungu na pia dhahiri kutoelewa ukweli. Alikuwa mwenye haki. Tusimkejeli yeye wala Yesu kwa kufikiri namna hii.

Ikiwa tutaendelea kusema ni mwenye dhambi baada ya kukutana na Yesu ni sawa na kumwita Yesu ni mwongo. Yesu alimfanya kuwa mwenye haki, na ndiye aliyemfanya kuwa mtumishi wa haki yake.

Je sala ya toba itaweza kutakasa dhambi zetu? Hakika Sala ya toba haitoweza kamwe

kutakasa dhambi zetu kwa sababu ukombozi hauwezi kuja kwa kupitia matendo yetu. Bali, ili tuweze kuwa wenye haki kamili na kwa wakati wote tukiwa tumeoshwa dhambi zetu zote, yatupasa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu, na kuamini kuwa Yesu ni Mungu. Ukombozi kamili hupatikana kwa wale tu wenye kuamini kuwa Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kutoa damu yake msalabani kutupa uhai mpya.

Sasa basi, je tutaweza kutakasa dhambi zetu za kila siku kwa kufanya sala za toba kila mara? Hapana. Dhambi zote tuzitendazo maishani mwetu kila siku zilikwisha takaswa takribani miaka 2000 iliyopita pale Yesu

Page 337: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

337 Maelezo ya Ziada

alipozibeba kwa ubatizo wake. Hakika tumepata utakaso wa kudumu kwa dhambi zetu zote kwa ule ubatizo wa Yesu na kutoka kwa damu yake pale msalabani. Amekuwa mwanakondoo wa sadaka kwa ajili yetu wenye kumwamini, kusafishwa dhambi zetu zote, na kulipia yote kwa ubatizo na kwa damu yake msalabani.

Hata zile dhambi tuzitendazo baada ya kumwamini Yesu zilikwisha safishwa kwa imani katika kijito kimiminikacho cha wokovu wa ubatizo, ukombozi wa kweli; Yesu tayari alikwisha kuwa Mwokozi na kubeba dhambi zetu zote tutakazo tenda hadi pale mwisho wa kifo chetu. Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa “hivi ndivyo” (Mathayo 3:15) impasavyo kuitimiza haki yote kwa kubeba dhambi zetu zote. Mwana wa Mungu alichukua hukumu ya dhambi zetu kwa kubatizwa.

Ubatizo wa Yesu una maana ya “kutakaswa” kwa sababu dhambi zetu zote alibeba yeye pale alipobatizwa, na hakika tukasafishwa kabisa na kutuacha huru toka dhambi zote.

Ubatizo pia una maana “kuzamishwa, kuzikwa.” Ikiwa dhambi zetu zote alibeba Yesu ilimbidi afe kwa niaba yetu sisi wenye dhambi hizo. Wale wote wenye kuamini kwamba dhambi zote alibeba Yesu kwa kupitia ubatizo hakika hawatakuwa na dhambi tena!

Imani ya kweli ni kuamini kwa moyo wote kwamba dhambi zetu zote, hata zile tutakazo tenda mbeleni maishani, zilikwisha bebwa na Yesu miaka 2000 iliyopita, alipo pata ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji na “hivi ndivyo” kutimiza haki yote ya Mungu.

Ikiwa hajasafisha dhambi zetu bado katika muda wote uliopita kwa ubatizo wake, basi

Page 338: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

338 Maelezo ya Ziada

pasingekuwepo na njia kwetu kuweza kutakaswa dhambi zetu. Kumbuka kwamba Yesu alitakasa dhambi zetu zote miaka mingi iliyopita.

Imani ya kweli na wokovu wa kiroho katika nyakati hizi maana yake ni kuleta mbele za Yesu dhambi zetu ili tuwe na uhakika kwamba zimekwisha takaswa kabisa kwa kusema “Yesu ulikwisha takasa dhambi hizi zote pia je, hivi ndivyo?” Ina maana pia kumwamini yeye na kumshukuru. Na ndiyo maana alikuja ulimwenguni, alibatizwa, akafa msalabani na alifufuliwa baada ya siku 3; kwa hayo yote yeye ni Mwokozi wetu.

Heri wale waliotakaswa dhambi zao kwa kuamini ubatizo wa Yesu uliosafisha dhambi zetu zote. Huu ni ukweli wa kutakaswa dhambi zetu za kila siku. Imani ya kweli ni kumwamini Yesu, aliyebeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake.

Warumi 8:30 inasema “Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; hao akawatukuza.” Je, maandiko haya yanaunga mkono juu ya mafundisho ya utakaso wa hatua kwa hatua? Kifungu cha maandiko haya, hakifundishi

juu ya utakaso tunaoweza kuupata hatua kwa hatua. Wana theologia wengi na wale wahubiri walio waongo hufikiri hivyo kwa kufundisha “Wale wenye kuamini katika Kristo Yesu watabadilika hatua kwa hatua na kuweza kutakaswa kabisa katika mwili na Roho,” na wengi huamini hivyo!

Lakini kwa jambo la kweli Wakristo ambao

Page 339: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

339 Maelezo ya Ziada

bado hawajazaliwa upya hujikuta wakiwa wagumu siku hadi siku katika imani na kuelewa kwao. Dhambi iliyo mioyoni mwao hukua kadiri wanavyo kuwa. Itawezekanaje utakaso wetu kwenda na muda? Neno “Utakaso wa hatua kwa hatua” ndiyo maneno ambayo hakika Mungu huyachukia sana, na ndiyo shetani huyapenda na kuyatumia katika kuwapotosha watu wa Mungu.

Tutaweza tu kuwa wenye haki pale tunaposhindwa kwa dhambi zetu wenyewe. Kwa sababu Yesu alitakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na kujitoa kwake sadaka ili kulipia gharama zake yeye mwenyewe, tunadai haki yetu kupitia ubatizo na damu ya Yesu. Tunakuwa wenye haki kupitia imani kwamba Yesu alibeba dhambi zetu kwake yeye binafsi.

Neno “utakaso” maana yake “kuwa

mtakatifu” Kwa kujaribu kutakaswa kwa juhudi zetu hii si kuamini katika kweli bali ni kuhamasishwa na miili yetu iliyo dhaifu.

Tumaini la hatua kwa hatua katika utakaso pia huja tokana na matamanio yetu ya koroho. Kila dini inalo neno lake la utakaso, lakini sisi sote tuaminiio katika Yesu hatupaswi kubadilisha umuhimu wa neno hili lenyewe.

Hatuwezi kutakaswa hatua kwa hatua kwa kuamini katika Yesu; tunakuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya kutahiriwa kiroho. Wenye haki wa kweli ni wale tu walio zaliwa upya kwa imani ya Injili ya ubatizo na damu ya Yesu.

Page 340: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

340 Maelezo ya Ziada

Je kwa kutubu dhambi kutafanya dhambi hizo kufutika? Hapana. Dhambi haziwezi kufutika kwa

toba, bali kwa imani katika Injili ya maji na Roho. Dhambi zetu zaweza kufutika ikiwa tu tutaamini ubatizo na damu ya Yesu, ambayo imetutakasa sisi sote kwa dhambi zote. Hii ni Injili ya wokovu wa roho utokao kwa Yesu aliye takasa dhambi zetu zote kwa ubatizo katika mto Yordani.

Kutubu dhambi ni njia pekee ya kuonyesha kwamba mtu Fulani bado ana fuata sheria ya Mungu, lakini ukombozi umetolewa kwetu wale wenye kuamini ubatizo na msalaba wa Yesu.

Maji ya ubatizo na damu ya Kristo ndiyo kweli ya mbinguni ambayo ndiyo iokoayo watu wote na dhambi, na wokovu wetu hautegemei jinsi tufanyavyo toba, bali katika

kumwamini Yesu kwamba alikwisha beba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Kusulubiwa kwa Yesu ilikuwa ni adhabu kwa zile dhambi zote alizo beba kwetu sisi wenye dhambi.

Hivyo, ukweli wa wokovu wetu upo katika ubatizo katika mto Yordan na damu ya msalabani sababu ya kutakaswa kwetu na dhambi zetu zote ni kwa kuwa tunamwamini Yesu yeye aliye takasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu yake.

Wale wote wenye kuhubiri kwamba, tutaweza kukombolewa kwa toba ya dhambi wanadharau ukweli wa wokovu wa Mungu.

Hivyo yatupasa kuamini ubatizo na damu ya Yesu, wokovu wa Mungu. Usithubutu kusema tena kwamba dhambi zote za wanadamu zitaweza kusamehewa kwa kutubu mbele ya Mungu kila mara.

Ujue ya kwamba dhambi zetu zitatuweka

Page 341: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

341 Maelezo ya Ziada

motoni lakini tukimwamini Yesu ubatizo na damu yake ambao ndio ukombozi na njia ya haki mbele ya Mungu, na ndipo dhambi zetu zote kwa mara moja kwa kuamini maneno ya kweli, maji na damu ya Yesu tutaokolewa (1Yohana 5:4-8).

Dhambi haziwezi kufutwa kila tunapotubu. Ikiwa utaendelea kusisitiza kutegemea toba utaishia motoni! Hebu na tuamini Injili ya kweli ili dhambi zetu mioyoni mwetu ziweze kutakaswa. Amini kwa moyo wako wote, na si kwa akili zako tu na uwe huru kwa dhambi hizo daima.

Ni ipi Injili ya kweli? Injili ya kweli ni ile pekee yenye

kutuwezesha kuwa huru kwa dhambi zetu kikamilifuu, mara moja na kwa wakati wote

pale tunapoiamini Nguvu ya Injili ya Mungu ni ile iendeleayo daima bila kupungua.

Injili ya Mungu ni ile “Yesu Kristo alilipa deni la wadaiwa (wenye dhambi) wasio weza bila shaka kulilipia wenyewe.” Sababu ya kuita ni Injili ya “nguvu iendeleayo” ni pale inapotupasa kufa kwa dhambi na kwenda motoni kwa hukumu mwana wa Mungu akaja kuwa sadaka ya kujitoa kwa ajili yetu ili kufuta dhambi zetu zote.

Alikuja hapa ulimwenguni na kubeba dhambi zote kwa ubatizo wake katika mto Yordani na kututakasa daima.

Amelipia mshahara wa dhambi kwa kuchukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake Yordani na kwa kufa msalabani Kalvari. Yesu alizifuta dhambi zote za ulimwengu kwa mithili ya nguvu kwa ubatizo na damu yake. Hii ndiyo habari njema (Injili) ya kweli.

Page 342: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

342 Maelezo ya Ziada

Injili ya kweli ni ile Yesu kuja ulimwenguni na kwa ubatizo wake na damu yake msalabani umetuokoa sisi sote wenye kuiamini.

Kama iandikwavyo katika 1Yohana 5:6 “Huyu ndiye aliye kuja katika maji na katika damu – Yesu Kristo si kwa maji tu, bali katika maji na katika damu.”

Sababu gani Yesu alijitoa sadaka katika msalaba? Kujitoa kwa Yesu kama sadaka kwa ajili

ya dhambi zetu kulifanyika kutokana na kujitoa kwake kupitia ubatizo wake. Alitupa mwili wake ili kulipia dhambi zetu zote ili tuweze kuachwa huru toka hukumu ya dhambi zetu zote.

Tunachopaswa kuelewa ni kwamba, Yesu

alibatizwa katika mto Yordani ili kubeba dhambi zetu zote. Yatupasa kuamini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa sababu hii.

Ikiwa Yesu asingebatizwa kabla ya kusulubiwa na ikiwa asinge kufa pale msalabani, dhambi zetu zingebaki pale pale. Hivyo, yatupasa kuamini yote haya mawili, ubatizo na damu ya Yesu. Kwa sababu Yesu ni mwana wa Mungu, Mwana kondoo wa sadaka, alitolewa sadaka ili kufuta dhambi zetu zote.

Yatupasa sisi sote kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwamba alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu, na alisulubiwa kwa dhambi hizo. Yesu alibatizwa na kusulubiwa ili wenye dhambi waweze kuokolewa na kuachwa huru toka katika adhabu ya dhambi – mauti.

Page 343: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

343 Maelezo ya Ziada

Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu ni nani hasa? Mungu aliwapa Waisraeli sheria kupitia

Musa na pia mpango wa kutoa sadaka ili waweze kupatanishwa kwa dhambi na uovu watakao utenda mbele yake. Alimchagua Haruni, kaka yake Musa, kuwa Kuhani Mkuu na akamwamuru kutoa sadaka ya upatanisho katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, siku ya upatanisho, ili dhambi zote za mwaka za Israeli ziweze kusafishwa (Walawi 16).

Mungu alitaja namna moja ya sadaka katika siku ya upatanisho iwe tu ikitolewa na Haruni na Makuhani warithi kati ya uzao wake. Mungu alifungua njia kwa Israeli kupatanishwa kwa dhambi zao zote kupitia kuwekea mikono ya Haruni juu ya sadaka ya mnyama wa Kafara. Hii ni sheria ya

upatanisho iliyowekwa na kuanzishwa na Mungu kwa ajili yao.

Kwa kivuli hiki, amefanya ieleweke wazi kwamba Yesu alikuwa mwokozi wa wanadamu. Katika nyakati za Agano Jipya. Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji, mrithi wa Haruni (1Nyakati 24:10, Luka 1:5) na Kuhani Mkuu wa Mwisho wa Agano la Kale (Mathayo 11:11-13). Yohana Mbatizaji mtume aliyeletwa na Mungu, mwakilishi na Kuhani Mkuu wa wanadamu, alimbatiza Yesu ili kumtwika dhambi zote za wanadamu juu yake, Mwana wa Mungu aliyekuja kwa ajili ya wenye dhambi.

Watu wote wamebarikiwa hakika kuweza kutwika dhambi zao kwa Yesu kupitia Yohana Mbatizaji. Nafasi ya Yohana ilikuwa ni Kuhani Mkuu aliyewakilisha wanadamu na ni Mtumishi wa Mungu aliyemtwika dhambi zote Yesu.

Page 344: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

344 Maelezo ya Ziada

Yohana Mbatizaji alikuwa mwakilishi na Kuhani Mkuu wa wanadamu aliyetumwa na Mungu, na ni mjumbe aliyetumwa miezi 6 kabla ya Yesu. Kwa upande mwingine, Yesu alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi zote za ulimwengu hali Yohana Mbatizaji alikuwa Kuhani Mkuu wa mwisho aliyemtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo. Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtumishi wa Mungu.

Mto Yordani, ndipo Yesu alipobatizwa. Mto Yordani humwagika kuelekea bahari

ya chumvi (Dead sea) kina cha Bahari ya chumvi ni takribani mita 400 pungufu usawa wa bahari. Hivyo, maji ya Bahari ya chumvi hayawezi kumwagika sehemu nyingine;

yamesimama hapo katika Bahari ya chumvi. Chumvi chumvi ya bahari hiyo ni mara 10

zaidi ya ladha ipatikanayo bahari nyingine za kawaida na hivyo hakuna kiumbe chochote chenye kuishi ndani yake. Hivyo ndivyo ilivyoitwa Bahari ya Chumvi (Dead sea). Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto wa kifo (Yordani). Hii inawakilisha wanadamu wote, isipokuwa tu wale wasio na dhambi mioyoni mwao, watapatwa na laana ya milele kwa dhambi zao mwishoni.

Hivyo basi Mto Yordani ni mto wa kusafisha dhambi, mto ambao wenye dhambi hufa. Kwa kifupi, ni mto wa ukombozi ambao dhambi zote za ulimwengu zilisafishwa hapo kwa ubatizo wa Yesu, kubebeshwa kwa dhambi Yesu.

Page 345: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

345 Maelezo ya Ziada

Ni ipi ilikuwa sadaka ya upatanisho wa dhambi za kila siku katika Agano la Kale? Palikuwa na sadaka ya upatanisho wa

dhambi za kila siku. Ili kuweza kupatanishwa kwa dhambi za kila siku, ilipasa mtu alete kati ya kondoo dume, kondoo jike, ng’ombe dume au njiwa mbele ya hema na kumwekea mikono juu yake ili kumtwika dhambi. Hii ilikuwa sadaka ya upatanisho iliyo amriwa kwa Sheria ya Mungu (Walawi 3:1-11)

Ni ipi ilikuwa sadaka ya upatanisho wa dhambi za mwaka katika Agano la Kale?

Ilikuwa ni sadaka ya upatanisho kwa

mwaka iliyo yenye thamani kwa Israeli yote kwa pamoja Kuhani Mkuu aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na kumtwika dhambi zote za mwaka za watu wote wa Israeli kwa mara moja (Walawi 16:1-34).

Yesu Kristo alikamilisha sadaka ya siku na ile ya mwaka mzima alipokuwa mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi zote juu ya kichwa chake kwa ubatizo wake.

Page 346: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

346 Maelezo ya Ziada

Sadaka ipi ilikuwa ni ya upatanisho wa milele? Ilikuwa ni upatanisho wa dhambi za

ulimwengu ni wa mara moja kwa kumwamini Yesu. Kwa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na Bwana aishiye milele, ataweza kubeba dhambi zote za ulimwengu milele. Ni kwa vipi alibeba dhambi zetu milele?

Ni kwa namna hii: 1. kwa kuzaliwa katika mwili wa

kibinadamu. 2. kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji –

Yordani. 3. kwa kusulubiwa msalabani kubeba

hukumu yote kwa niaba yetu. Mwana wa Mungu alikuja ulimwenguni

katika mwili wa mwanadamu na kubatizwa ili kubeba dhambi zote za dunia kupitia Yohana Mbatizaji. Na pia alitoa damu yake

msalabani kuokoa wanadamu kwa dhambi zao milele (Walawi 16:6-22, Mathayo 3:13-17, Yohana 1:29, Waebrania 9:12, 10:1-18).

Je, ondoleo la dhambi limetolewa mara moja au hatua kwa hatua? Limetolewa mara moja kwa sababu Yesu

alibeba dhambi zetu mara moja na kwa wakati wote kwa kubatizwa mara moja na kupokea hukumu kwa wote mara moja. Amesema kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3:15 “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”

Katika Yohana 1:29 Yohana Mbatizaji alisema “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” na katika Yohana 19:30 Yesu alisema “Imekwisha.”

Page 347: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

347 Maelezo ya Ziada

Katika Waebrania 10:9-18 “Ndipo aliposema Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatiifu naye atashuhudia kwa maana baada ya kusema, hili ni agano mtakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika

ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”

Ubatizo na damu ya Yesu umefuta dhambi zote za ulimwengu mara moja.

Upi ni mshahara wa dhambi? Mshahara wa dhambi ni mauti. Haijalishi

ni dhambi ipi au ya namna gani, kila dhambi itahukumiwa mbele ya Mungu, na hukumu ya kila dhambi ni kifo. Ili tuweze kupata upatanisho wa dhambi, watu wa Israeli iliwapasa kutoa kondoo asiye na doa mbele ya Mungu. Lakini aina hii ya sadaka haikuweza kwa namna fulani kutakasa dhambi zote kwa wakati wote, “maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi

Page 348: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

348 Maelezo ya Ziada

kuondoa dhambi” (Waebrania 10:4). Kwa hiyo, Mungu alitayarisha sadaka ya

Kondoo kukomboa watu toka dhambini. Kila mnyama wa sadaka alipaswa kuwekewa mikono kuweza kubeba dhambi zote na kufa badala yao.

Katika Agano Jipya, Yesu alichukua dhambi zote kwa kupitia ubatizo wake katika mto Yordani akiwa ni Mwanakondoo wa Mungu na kufa kwa ajili yetu. “Mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Mshahara wa dhambi ni mauti, lakini Yesu alionyesha upendo wake kwa kufa badala yetu na kutuletea zawadi ya uzima wa milele kwa sisi wale tulio wenye dhambi ulimwenguni.

Kwa nini Yesu ilimpasa afe msalabani? Kifo cha Yesu ilikuw ni malipo ya dhambi

zote za ulimwengu alizobeba kwa kupitia ubatizo wake. Wanadamu walikuwa na adhabu ya kifo cha motoni kwa dhambi zao, lakini kwa kuwa Yesu alitupenda alikubali ubatizo, ambao ulimbebesha dhambi zote juu yake na kufa msalabani ili kutuokoa.

Alijitoa mhanga ili kutuokoa toka dhambini na laana ile ya jehanamu. Kifo chake kilikuwa ni malipo ya dhambi za wanadamu. Alibatizwa ili azichukue dhambi zote za dunia na kujitoa ahukumiwe msalabani ili kutuokoa toka dhambini, hukumuni na kwenye laana.

Kifo cha Yesu ni kwa ajili ya dhambi za ulimwengu alizobeba pale Yordani ili aweze kupokea hukumu ya dhambi za wanadamu. Alikufa msalabani na kufufuka ili

Page 349: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

349 Maelezo ya Ziada

kutuwezesha kuishi tena kama wenye haki.

Tunapata nini pale tunapomwamini Yesu? 1. Tunapokea msamaha wa dhambi zetu

zote na kuwa wenye haki (Warumi 8:1-2). 2. Tunapokea Roho wake na kuishi milele

(Matendo 2:38, 1Yohana 5:11-12). 3. Tunapokea haki ya kuwa wana wa

Mungu (Yohana 1:12). 4. Tunapokea upendeleo wa kuingia

Ufalme wa Mungu, Ufalme wa Mbinguni (Ufunuo 21 – 22).

5. Tunapokea baraka zote za Mungu (Waefeso 1:3-23).

Kwa nini yatupasa kumwamini Yesu? Yatupasa kumwamini Yesu: 1. Kutimiza mapenzi ya Mungu. 2. kuokolewa na dhambi zetu zote. 3. kuingia ufalme wa Mbinguni ili tuishi

milele na Bwana. Sisi sote ni wenye dhambi ambao

tutaangukia motoni pasipo imani katika Kristo, mwokozi wetu. Ni Yesu pekee ndiye mwokozi wetu ambaye ataweza kutuokoa toka motoni. Yatupasa kumwamini kwa kuwa ndiye pekee wa kweli.

Page 350: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

350 Maelezo ya Ziada

Ni wapi watu wenye kumwamini Yesu na kuokolewa mwishoni huenda?

- Mbinguni -

Ni wapi watu wasio mwamini Yesu wala kukombolewa mwishoni huenda?

- Motoni kwa dhambi zao zote; ziwa la moto liwakalo na kiberiti - (Ufunuo 21:8).

Ni nani Kondoo wa Mungu?

Wale wote wapokeao msamaha wa dhambi kwa kuamini ubatizo wa damu ya Yesu.

Na “Kondoo wale wasio wa zizi hili” (Yohana 10:16) ni wale mbuzi kwa sababu kuamini kwa ufinyu kwa kile wanachoelewa

kwa kuchagua, kwa sababu bado ni wenye dhambi wakati wale wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu wameokolewa wote kwa wakati mmoja na kuwa kondoo wa Mungu.

Lipi ni Kanisa la kweli la Mungu? Kanisa la kweli la Mungu ni pale wenye

haki, wale walio kombolewa na kutakaswa katika Kristo kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu, wanapo kusanyika na kumwabudu Mungu (1Wakorintho 1:2). Kanisa la kweli la Mungu, kama ilivyoandikwa katika Waefeso 4:5 ni mahala ambapo washirika huamini katika “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; Mungu mmoja na Bwana wa wote.”

Page 351: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

351 Maelezo ya Ziada

Ni nani mzushi katika Biblia? Mzushi ni yule mwenye dhambi moyoni

huku akimwamini Yesu. Katika Tito 3:11 inasema “akijua yakuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hata yeye mwenyewe.”

Yesu alizichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake, lakini mzushi haamini juu ya baraka ya Injili ya maji (ubatizo wa Yesu, ubatizo wa ukombozi) ambao ni zawadi ya thamani kwa Mungu, bali yeye hujihukumu mwenyewe kama mwenye dhambi huku akikataa wokovu kamili.

Biblia inaeleza aina hii ya watu kama “wazushi” wenye kumwamini Yesu lakini wakiendelea kujihukumu kuwa wenye dhambi (Tito 3:11) utaweza kushangaa ikiwa wewe nawe ni “mzushi” au la. Ikiwa una mwamini Yesu, huku bado ukijiita

mwenye dhambi, basi hujaelewa ukweli wa kiroho wa Injili ya maji na Roho.

Ikiwa utaamini katika Yesu, lakini bado unajichukulia kuwa ni mwenye dhambi asiye na tumaini, hivyo wewe ni mzushi. Maana yake ni kwamba, unadhani Injili ya kweli katika maji na Roho ni dhaifu mno katika kufuta dhambi zetu zote na kutufanya watoto wa Mungu. Ikiwa wewe ni mmoja kati ya hawa waitwao wazushi wenye kukiri imani kila siku mbele ya Mungu ili wasamehewe na kukubali kwamba ni wenye dhambi, basi wewe ni hatari kwa kufikiria upya imani yako.

Utaweza vipi kuwa mwenye dhambi ikiwa Yesu alikwisha beba dhambi zako zote? Kwa nini unaendelea kujaribu kulipia deni ambalo tayari lilikwishalipwa na Yesu kama zawadi kwako? Ikiwa utaendelea kusisitiza kulipia deni hilo binafsi wewe ni mzushi! Kwa

Page 352: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

352 Maelezo ya Ziada

sababu imani yako ni tofauti na ile aliyo kupa Mungu. Kila Mkristo aaminiye katika Yesu, lakini hajazaliwa upya ni mzushi. Yakupasa ujue kweli hii. Mungu alizichukua dhambi zote za ulimwengu, na ikiwa utadharau wokovu wake wewe ni mzushi.

Mzushi ni yule ajiitaye yeye ni mwenye dhambi, kwa maneno mengine, mwenye kujihukumu nafsi yake mwenyewe. Je, unadhani ni rahisi kwa Mungu aliye Mtakatifu atakubali mwenye dhambi awe mtoto wake? Ikiwa unajiita wewe ni mwenye dhambi hali una mwamini Mungu Mtakatifu, wewe ni mzushi. Ili usiwe mzushi, yakupasa uamini ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani kama mambo ya kweli.

Utaweza kuokoka ikiwa utaamini yote haya kwa wakati mmoja: ubatizo wa Yesu na damu yake.

Page 353: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

MENGINEYO 3

Maswali na Majibu

Page 354: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

354 Maswali na Majibu

Maswali na Majibu SWALI 1: Nimekuwa nikijisomea

vitabu ulivyonitumia kwa wema wa kutosha na kukuta baadhi ya maswala yahusuyo ubatizo wa Yesu kuwa ni ya ajabu. Je, unaweza kunielezea juu ya mafundisho yako yahusuyo mahusiano kati ya ubatizo wetu na ubatizo, kifo na ufufuo wa Yesu Kristo?

JIBU: Kwanza ya yote yatupasa kuwa

makini juu ya “mafundisho ya ubatizo” kama ilivyo Waebrania 6:2. Kutokana na Biblia, ipo aina tatu za ubatizo; ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji na ubatizo wa maji kwetu kama ibada.

Ubatizo tunaoupokea ni kukiri kwa imani

yetu katika ubatizo wa Yesu. Hii ni kusema kwamba tunabatizwa ili tukiri imani yetu kwamba tunamwamini Yesu aliyebaitizwa ili kubeba dhambi zetu zote na kufa msalabani kutupatanisha. Sasa waweza kuelewa Mathayo 3:15 pale anaposema “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Hapa neno “kwa kuwa ndivyo” lina maana kwamba Yesu mwenyewe alibeba dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu wote.

Ulikuwa mpango mahususi wa Mungu kutuokoa toka mtego usioweza kuzuilika wa dhambi. Bwana Mungu “ameweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6) na kutupatia sisi haki. “Haki” hapa maana yake kwa Kigiriki “dikaisune” ambayo humaanisha “usawa na sheria.” Inatueleza kuwa Yesu alibeba uovu wa wanadamu katika namna

Page 355: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

355 Maswali na Majibu

ya usawa na sheria kwa kubatizwa katika kuwekewa mikono.

Tumeokolewa kwa umadhubuti wa imani ya ubatizo, kifo na msalaba na ufufuo wa Yesu. Nguvu ya tohara ya koroho (Warumi 2:29) katika ubatizo, ambayo ilikatia mbali dhambi zetu moyoni, imetutakasa mioyoni mwetu. Hivyo, Mtume Petro alisema mbele za watu “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38) katika siku ya Pentekoste.

Wenye dhambi wote hupata msamaha katika mioyo yao kwa kumwamini Yesu. Nini maana ya jina la YESU? “Nawe utamwita jina lake YESU, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). Jina la Yesu maana yake “Mwokozi” aokoaye watu wake kwa dhambi

zao. Kwa namna gani aliokoa? Yesu alituokoa na dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo na kifo chake msalabani.

Mitume wa Yesu Kristo walipohubiri Injili walikuwa na uhakika wa kuelewa juu ya ubatizo wa Yesu na msalaba, hivyo walifundisha ile Injili ya kweli na kuwabatiza wale wote walio amini ubatizo huo. Kwa jinsi hiyo walibatizwa ili wakiri kwa nje kwamba wanaamini ubatizo na kifo cha Yesu kwa ndani ya mioyo yao. Tunapobatizwa, tunakiri “Na kushukuru Bwana ulibeba dhambi zangu zote kwa ubatizo wako, ukafa kwa ajili yangu na ukafufuka ili uniokoe mimi. Naamini Injili yako.” Tunabatizwa kwa maji na watumishi wa Mungu kama ishara ya imani katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani, kama alivyobatizwa na Yohana Mbatizaji. Kwa haya, watakatifu wa nyakati za Kanisa la kwanza walibatizwa ili

Page 356: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

356 Maswali na Majibu

kuthibitisha imani yao, baada ya kuikiri katika Injili na walikombolewa na kupata msamaha wa dhambi.

Ibada ya ubatizo si sharti muhimu la wokovu Ingawa ni jambo la maana katika kubainisha imani zetu. Maji ya ubatizo hayana cha kufanya katika wokovu wetu. Tutaweza kuokolewa pale tu tutakapo amini Injili ya maji na damu Biblia yatueleza kwamba tunabatizwa katika Yesu Kristo (Warumi 6:3, Wagalatia 3:27) pale tunapoamini ubatizo wake.

Sasa ni vipi tutaweza “kubatizwa naye.” Hii ni rahisi pale tu, tutakapo amini ubatizo ikiwa mwili, utu wetu wa kale utaweza kuungana na Yesu na kusulubiwa naye kwa imani yetu kwa ubatizo wake. Kwa matokeo haya ikiwa Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, kifo chake kilikuwa ni hukumu ya udhalimu wetu. Hivyo basi, nasi

pia tunakufa msalabani naye. Kwa maneno mengine, utu wetu au nafsi yetu, ambayo haina jinsi zaidi ya kuendelea kutenda dhambi hadi kufa, yenyewe hufa na tumeokolewa toka udhalimu wetu na kuungana na Yesu kwa ubatizo wake.

Wale walio ungana na Yesu kwa ubatizo na kifo wataweza pia kuungana naye katika ufufuo wake. Ufufuo huu si pekee kwake bali hata kwetu ambao hutuwezesha kuzaliwa upya kama wana wa Mungu na kututenga kuwa wake, walio safi na wasio na dhambi mbele yake.

Ikiwa hatuja mtwika dhambi Yesu kwa kutoamini ubatizo wake, kifo chake na ufufuko utaweza kuwa usio na maana, usio na la kufanya kwa wokovu wetu. Wale wote walio mtwika dhambi zao Yesu kwa imani wameungana na kifo chake, msalabani, kunako ruhusu kuzaliwa upya wakiwa wenye

Page 357: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

357 Maswali na Majibu

haki. Kwa jinsi hiyo, wale wasio mtwika dhambi zao yeye kwa kutoamini ubatizo, hawana usharika naye katika kifo na ufufuo wa jinsi hii.

Ubatizo wa wenye kuamini ni wakutegemewa kama tuwezavyo kukubaliana juu ya mke na mume kuwa washirika kisheria kwa kupitia maagano ya ndoa. Ubatizo wa watakatifu ni tamko la mwonekano wa nje au hadharani tokana na imani ya ndani mioyoni. Tunapo tamka imani yetu huwa yenye uimara isiyo futika kamwe.

Tusipoelewa vyema juu ya ukweli halisi wa maana ya ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, yatupasa kutoamini ya kuwa tungeweza kuokolewa ikiwa hatutoamini juu ubatizo huo na umuhimu wake. Una maana ya mtego wa hadaa toka kwa shetani. Tutaweza kupokea ondoleo la dhambi na kukaribishwa

Mbinguni kwa kuamini kwa dhati ubatizo wa Yesu moyoni badala kuamini ubatizo wa jinsi yetu.

SWALI 2: Nitawezaje kusema “mimi

ni mwenye haki” hali kila siku Ninaanguka dhambini?

JIBU: Sisi kama wanadamu tutaendelea

kutenda dhambi siku hadi siku mpaka kifo chetu. Kama ilivyo ukweli huu, hii ni kutokana na asili ya msingi wa maisha yetu; ya kwamba tulitenda dhambi tokea mwanzo Biblia inasema “Hakuna mwenye haki hata mmoja” (Warumi 3:10). Na ndiyo maana Mtume Paulo alikiri mbele ya Mungu kwamba “Ni neno la kuamini, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi

Page 358: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

358 Maswali na Majibu

ambao wa kwanza wao ni mimi” (1Timotheo 1:15).

“Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana kuna tofauti kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (Warumi 3:21-24).

“Haki” hii ya Mungu maana yake ni Yohana Mbatizaji kumbatiza Yesu Yordani. Alipo taka kubatizwa alimwambia Yohana “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Alibeba dhambi za ulimwengu katika namna ya haki na ifaayo alipobatizwa na Mwakilishi wa wanadamu wote, Yohana Mbatizaji. Na kwa jinsi hiyo Yohana akaja

kushuhudia baada ya ubatizo huo ya kwamba “Tazama! Huyo ndiye Mwanakondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29).

Sasa basi, nini maana ya “dhambi za ulimwengu.” Hii inawakilisha dhambi zote za wanadamu tokea Adamu na Eva, wanadamu wa kwanza duniani hadi yule mwanadamu wa mwisho kuishi hapa ulimwenguni. Watu wa kale ni wa ulimwengu huu, watu wa nyakati hizi ni wa ulimwengu huu pia na hata wale wajao majaliwani ni wa ulimwengu huu. Yesu, Alpha na Omega, alitoa sadaka moja kwa dhambi za wakati wote, kwa kubeba dhambi za ulimwengu mara moja za wote kwa ubatizo wake Yordani na kufa msalabani. Na “hivi ndivyo” tumetakaswa.

Kwa uwazi Biblia inatamka “katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa

Page 359: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

359 Maswali na Majibu

kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10). Angali kwamba hii sentensi ni ya wakati uliopo. Tumetakaswa kwa hakika na hatuna dhambi, toka pale tulipo mwamini Mungu hadi sasa na siku zote itakuwa hivyo. Kwa kuwa Mungu ni mwenye Enzi, anauweza wa kuona mbali toka mwanzo hadi mwisho wa dunia. Ingawa yapata miaka 2000 sasa iliyopita alipobatizwa Yesu, alibeba dhambi zetu zote wanadamu tutendazo toka mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Hivyo, kabla ya kufa kwake Yesu pale msalabani alisema “Imekwisha!” (Yohana 19:30). Alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni miaka 2000 iliyopita na kufa msalabani ili kututakasa.

Bado tunaendelea kutenda dhambi hata baada ya kuokoka kwa sababu miili yetu ni dhaifu. Kwa namna hiyo Yesu ametukomboa sisi sote tokana na dhambi zote za zamani,

sasa na za nyakati ijayo kwa kubeba dhambi zote juu ya mwili wake kwa ubatizo na kuhukumiwa nazo msalabani. Hii ni haki timilifu ya wokovu wa Mungu.

Ikiwa Yesu asingebeba dhambi zetu zote hata zile tutakazo tenda mbeleni, basi pasinge kuwepo mwanadamu yeyote aliyekombolewa kwa dhambi za kila siku, “kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) wakati Yokobo na Esau walipokuwa bado tumboni mwa Mama yao, Mungu aliwatenganisha kuwa mataifa mawili hata kabla hawajatenda mema au mabaya mbele zake, na alimpenda Yakobo na kumchukia Esau na alisema “Na mkubwa atamtumikia mdogo” (Mwanzo 25:23). Ujumbe huu una maana kwamba wokovu wa Mungu hauna lakufanya juu ya matendo yetu ya sheria, bali hutolewa kwa wale wenye kumwamini Mungu kwa usahihi

Page 360: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

360 Maswali na Majibu

katika wokovu wake ulio kwenye ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake.

Sisi wanadamu tumewekewa mwisho wetu kuwa motoni kama viumbe waovu toka mwanzo tulipozaliwa hadi tutakapo kufa lakini Mungu alitangulia kuona dhambi zetu kabla ya yote, na kuzisafisha zote mara moja kwa wote kwa ubatizo wa Yesu na msalaba wake kwa sababu anatupenda tunaishi kipindi cha baraka. Nabii Isaya alisema “Semeni na moyo wa Yerusalemu, kawaambieni kwa sauti kuu ya kwamba, vita vyake vimekwisha uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote” (Isaya 40:2). Kipindi cha utumwa wa dhambi kimekwisha kwa kupitia ubatizo wa Yesu na msalaba wake, hivyo, yeyote aaminiye Injili ataokolewa na dhambi zake zote. “Hili ni agano mtakaloagana nao baada ya siku zile,

anena Bwana, nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo, dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:16-18).

Mungu hatuhukumu kwa dhambi za kila siku tena kwa sababu alikwisha tutakasa sisi wanadamu na kuhukumiwa nazo kupitia Yesu.

Na kwa matokeo hayo tutaweza kumsubiri yule ajaye, Bwana na kufuata Neno lake, kama aliye mwenye haki asiye na dhambi, ingawa bado tunaendelea kutenda dhambi maishani.

Page 361: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

361 Maswali na Majibu

SWALI 3: Nini maana ya ubatizo wa toba alio leta Yohana?

JIBU: Yohana Mbatizaji alikuwa ni

mtumishi wa Mungu, aliye zaliwa miezi sita kabla ya Yesu, na alitabiriwa kuja kwake katika Malaki, awe nabii wa mwisho katika Agano la Kale.

“Ikumbuke torati ya Mungu, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu, Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana” (Malaki 4:4-6).

Wakati Yesu alipozaliwa, watu wa Israeli waliyaacha maneno ya magano ya Mungu na kuabudu miungu ya kigeni. Walitolea

wanyama walio vipofu na wasio safi kama sadaka, na kufanya hekalu ya Mungu kuwa sehemu ya biashara, Yesu Kristo, pia alitabiriwa kuja kwake katika Sheria ya Musa na Manabii. Sheria humpa mwanadamu ufahamu wa dhambi, kwa kumuonyesha jinsi ile alivyo mwovu (Warumi 3:20). Ni dhambi kutofuata hata amri mojawapo iliyoandikwa katika kitabu cha Sheria.

Katika Agano la kale, mwenye dhambi asiye heshimu vipengele vya sheria alileta sadaka ya dhambi mbele ya madhabau, kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha yule mnyama ili kumtwika dhambi juu yake, na kumchinja mnyama huyo kama sadaka ya dhambi ili aweze kusamehewa dhambi zake na kuunganishwa tena na Mungu Ndipo pia kuhani huchukua kiasi cha damu na kuweka katika pembe zilizo katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kumwaga

Page 362: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

362 Maswali na Majibu

ilibayoki chini ya madhabahu. Hivyo, watu wa Israeli hawakuweza

kukombolewa toka dhambini, ukiachilia zile sadaka zisizo na idadi zilizotolewa kila siku. Hivyo, Mungu akafanya azimio la kudumu kwao, siku ya upatanisho. Ilikuwa katika kipindi hicho Mungu angeweza kusamehe dhambi za mwaka katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika siku hiyo Haruni, Kuhani Mkuu, aliwachukua mbuzi wawili na kupiga kura juu yao; mmoja wa Bwana na mwingine wa Azazeli ndipo alipowekea mikono yake juu ya kichwa cha yule wa Bwana ili kumtwika dhambi za mwaka za wana wa Israeli juu yake. Haruni alimchinja na kuichukua damu kwa kunyunyizia mara saba juu ya uso wa kiti cha rehema.

Alipo maliza kupatanisha kwa ajili ya Hekalu takatifu, alimtoa mnyama mwingine. Alimwekea mikono yake juu ya kichwa cha

yule mbuzi aliye hai na kutubu juu yake dhambi zote za mwaka za wana waisraeli. Kwa njia hii, dhambi zote za mwaka zili wekewa juu yake, na kupelekwa kwa kutelekezwa jangwani katika mikono ya mtua liye tayari. Waisraeli walikombolewa kwa dhambi zao kwa namna hii.

Ingawa sadaka ilitolewa kulingana na sheria ya Agano la Kale haikuweza kuwafanya wale wote waliotolea sadaka ya mwaka kwa mwaka kuwa safi. Ilikuwa ni jinsi ya kivuli au mfano wa mambo mema yatarajiwayo (tendo la haki kwa Masia) mbeleni (Waebrania 10:1). Watu wa Israeli hawakumngojea Yesu Kristo, Mwokozi badala yake waliabudu miungu ya ugenini katika ulimwengu wa uovu waliacha maneno ya unabii wa Agano la kale.

Kwa haya yote Mungu alisema kabla kwamba atamtuma Yohana Mbatizaji ili

Page 363: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

363 Maswali na Majibu

kurudisha mioyo ya Waisraeli, kurudia kwa Mungu na kutayarisha mioyo hiyo pia kumpokea Yesu Kristo. Kabla Yohana Mbatizaji kumbatiza YESU, alitoa ubatizo wa toba kwa waisraeli jangwani Yedea.

Dhumuni lake kubatiza kwa maji lilikuwa kuwaongoza katika kusubiri na kumwamini Yesu aliwafundisha kwamba Mwokozi atabatizwa naye kwa njia ya kuwekewa mikono ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kusulubiwa ili kuwaokoa toka dhambini. Alisema kwamba Yesu atakuja na kuiondolea mbali sadaka ile isiyo kamilika ya kale na kutoa sadaka ya milele kwa mwili wake; yeye atabeba dhambi zote kwa ubatizo wake, kama ilivyo wana wa Israeli walipo kombolewa kwa kuleta sadaka ya dhambi isiyo na doa, kwa kuwekea mikono juu yake, na kuchinjwa kulingana na utaratibu wa kutoa sadaka katika Agano la kale.

Waisraeli wengi walikiri dhambi, kutubu na kubatizwa naye. “Tubuni” maana yake “kumrudia kwa moyo Bwana.” Kwa kukumbuka sheria ya Agano la kale, walimjia Yohana na kukiri kwamba walikuwa hawana tumaini wenye dhambi, ambao wasingeweza kujizuia kutenda dhambi hadi kifoni. Walikiri pia kwamba hawatoweza kuingia katika ufalme wa Mbinguni kwa matendo yao mema ya sheria na kumrudia kwa moyo Yesu Kristo ambaye angefuta dhambi zao zote mara moja na kwa wote, na kuwafungulia malango ya ufalme wa Mbinguni.

Ubatizo ambao Yohana Mbatizaji alio utoa kwa Waisraeli ulikuwa ni katika mfululizo wa matukio. Aliwaongoza kukiri juu ya dhambi zao maishani, kutubu na kumgeukia Yesu Christo, ambaye naye atakuja kubatizwa kwake, yeye (Yohana) akiwa Kuhani Mkuu

Page 364: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

364 Maswali na Majibu

na mwakilishi wa wanadamu, na hatimaye kusulubiwa ili kuwaokoa kwa dhambi zao zote, punde atakapo wabatizwa. Hii ndiyo toba ya kweli kibiblia.

Hivyo, Yohana aliwaambia makutano waliokusanyika “kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Mathayo 3:11).

Yohana Mbatizaji aligeuza nia za watu kwa Yesu, kwa kuwashuhudia kwamba Yesu atakuja kubeba dhambi zote za ulimwengu (Yohana 1:29) na kufa kwa ajili yao kwa kujitolea. Kwa haya, Yesu binafsi alibeba ushuhuda ya Yohana aliyekuja kutuonyesha njia ya haki (Mathayo 21:32).

SWALI 4: Je unafikiri kwamba kuelewa juu ubatizo wa Yesu ndiyo lazima kwa wokovu ambao umeondoa sheria ya kifo cha msalaba katika Injili?

JIBU: Ubatizo wa Yesu na kifo chake

msalabani ni mambo yaliyo na umuhimu sawa kwa wokovu wetu. Hatuwezi kamwe kusema kati ya moja ya haya ni muhimu zaidi ya jingine. Kwa njia hii, tabu ni hii kwamba Wakristo wa nyakati hizi hujua na kuitambua damu ya Yesu msalabani tu! Huamini walisamehewa kwa sababu Yesu aliwafia msalabani tu, lakini ukweli ni kwamba si kwa msalaba tu ambao Yesu alibeba dhambi za ulimwengu. Kwa kuwa alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kubeba dhambi za ulimwengu juu yake, kifo chake msalabani kingekuwa kwa kimatendo kuwa

Page 365: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

365 Maswali na Majibu

ni hukumu ya dhambi zetu zote. Kuamini msalaba pekee bila kuamini au

kuelewa juu ya ubatizo wa Yesu ni sawa na kutoa sadaka mnyama mbele ya Bwana bila kuwekea mikono juu yake. Wale watoa sadaka kwa namna hii hawatoweza kamwe kukombolewa kwa dhambi zao kwa sababu namna hii ya sadaka ilikuwa ni kinyume cha sheria ya sadaka, ambayo Bwana Mungu asingekubali. Bwana alimwita Musa na kunena naye mbele ya hema ya kukutania, akasema, “Matokeo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana. Kisha atawawekea mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa ajili yake” (Walawi 1:3-4).

Mungu ni mwenye haki na afuataye sheria

kwa mpango wa matoleo ya sadaka ili kutakasa dhambi zetu. Tunapotoa sadaka ya haki, sadaka hiyo hukubaliwa na Bwana kwa upatanisho wetu. Pasipo kuwekea mikono, sadaka hiyo haitoweza kamwe kukubaliwa na Mungu. Kwa jinsi hiyo pia, ikiwa tutaondoa ubatizo wa Yesu katika Imani yetu kwake, hatutoweza kupata msamaha wa dhambi kwa imani ya aina hiyo.

Moja ya mafundisho potofu katika nyakati hizi za Imani ya Kikristo ni kwamba, utaweza kuokolewa unapo mkiri Yesu huwa Mwokozi kwa kuwa Bwana ni upendo. Biblia hata hivyo inasema “Yeyote aliitiaye jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21, Warumi 10:13) ambapo pia inasema “Si kila aniitaye ‘Bwana Bwana’ ataingia ufalme wa mbinguni, bali wale wote watendao mapenzi ya Baba yangu wa Mbinguni” (Mathayo 7:21).

Ili kumkiri Kristo Yesu kuwa ni Mwokozi,

Page 366: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

366 Maswali na Majibu

yatupasa kujua sheria ya wokovu wa Mungu aliouweka. Ikiwa tutaweza kuokolewa kwa kuamini kirahisi Jina la Yesu pasingekuwa na sababu basi kwa maandiko yeyote kuandikwa juu ya mpangilio wa utoaji wa sadaka katika Agano la Kale na kuhusiana na walo wote waendao kinyume na sheria katika Mathayo 7:21 kwa namna hii njia ya kweli na sahihi ya wokovu wa Bwana ipo ndani ya biblia kwa wazi na kwa kueleweka. Hakika tutaweza kwa uwazi kuona katika kitabu cha Walawi sura ya 3 na 4 kwamba wenye dhambi iliwapasa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka ili kumbebesha juu yake dhambi zao zote na kumchinja ndipo kunyunyizia damu anapotoa sadaka ya dhambi na ya amani. Kutoa sadaka bila kuwekea mikono au kutoa sadaka aliye na doa pia hii ilikuwa kinyume cha sheria ya upatanisho.

Yote haya, maneno ya Agano Jipya na lile la Kale yalikuwa na pande zifananazo kwa kila moja (Isaya 34:16) ubatizo wa Yesu Yordani ni sawa na mwenye dhambi kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka katika Agano la Kale. Yesu alipotaka kubatizwa katika Yordani na Yohana Mbatizaji, alisema “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15).

Hapa “haki yote” maana yake “sheria na usawa.” Hii maana yake ina mpasa Yesu kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu kwa kupitia njia hii. Ilimpasa pia yeye kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika namna ya kuwekewa mikono ili kubeba dhambi zote za ulimwenguni kwa njia ya usawa kulingana na mpango wa matoleo ya sadaka, uliojumuisha kuwekea mikono na damu ambao Mungu aliuweka katika Agano la

Page 367: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

367 Maswali na Majibu

Kale. Kuamini msalaba pekee maana yake

matokeo ya kifo cha Yesu hayana maana kwa dhambi zetu kwa sababu dhambi zetu zingeweza kuwekewa juu yake bila ya ubatizo wake. Hii huleta matokeo ya kuichukulia damu yake kuwa si takatifu na haina uwezo wa kutakasa dhambi (Waebrania 10:29).

Hivyo, damu ya Yesu itakuwa hakika yenye kuleta matokeo katika kutakasa dhambi mioyoni mwa wenye kuamini ikiwa tu wanaamini kwamba dhambi zao zote zilibebwa naye pale Yohana Mbatizaji alishuhudia kwamba kwa yeyote amwaminie Yesu kuwa ni mwana wa Mungu aliye kuja katika maji na damu, ataushinda ulimwengu. Yesu alikuja kwa maji na damu si kwa maji tu, au damu tu (1Yohana 5:4-6).

Yesu Kristo alielezea kwa wafuasi wake

juu ya mambo yamhusuyo yeye katika maandiko yote. Kuanzia Musa na manabii wote, aliwaonyesha kwamba sadaka ya dhambi katika Agano la Kale alikuwa ndiye mwenyewe. Daudi alisema katika Zaburi juu yake “Tazama nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikwa) – kuyafanya mapenzi yako Ee Mungu wangu” (Zaburi 40:7, Waebrania 10:7).

Na kwa matokeo haya, ubatizo wa Yesu hauondoi maana ya msalaba, bali kwa hakika ni sehemu ya Injili ya Bwana ambayo yenye kuhitimisha na kutimiliza maana ya msalaba. Pia hutufunza kwamba hatutoweza kuwa na ukombozi hadi pale patakapokuwepo na ubatizo na ile damu ya thamani ya Yesu Kristo. Kumaanisha kuokoka ni pale tu unapopata ondoleo la dhambi kwa kuamini juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani na kupokea

Page 368: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

368 Maswali na Majibu

kipawa cha Roho Mtakatifu (1Yohana 5:8, Matendo 2:38).

SWALI 5: Je unaweza kunipa

maelezo juu ya Injili ya maji na Roho? JIBU: Ikiwa tumepoteza sindano mahala

fulani nje tungetafuta mahala pale ilipopotelea bila shaka. Kwa jinsi hii, haitoleta maana hata kidogo ikiwa tutajaribu kuitafutia ndani ya nyumba si kwa sababu nje ni penye mwanga zaidi. Nimekutana na watu wasio na maana kwa namna hii nyakati hizi Makanisani. Wanapo jihusisha na mambo ya utata katika biblia juu ubatizo wa waumini, hawajiulizi wenyewe nafsini umuhimu wa swali “sababu gani Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji?” Kutokana na tabia za aina hii, kumekuwepo na

madhehebu na vitengo vingi leo hii katikati ya jamii ya Wakristo wa leo.

Ili kuweka mwisho wa utata huo uendeleao siku hadi siku, yatupasa kujitoa katika kijiji hiki chenye ghasia na kurudi nyuma pale tulipo potezea sindano yetu. Ikiwa tutakuwa waaminifu kutafuta kweli yatupasa kuachana kabisa mawazo potofu juu ya kile tushindwacho kukipata katika kijiji cha udini. Kwa nini Mitume waliweka mkazo juu ya ubatizo wa Yesu Kristo? Siri ya ukweli wa Injili ya maji na Roho waliyo ipokea toka kwa Yesu ilihubiriwa ulimwenguni pote kwa uwazi.

Yesu alisema “Amin, amin nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Biblia yatuambia kwamba Yesu alikuja kwa maji na damu ili atuokoe toka dhambini mwetu (1Yohana 5:6). Maana ya damu ni

Page 369: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

369 Maswali na Majibu

kifo chake msalabani. Hivyo una maana gani juu ya “maji”? Kwa nini Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu? Kwa nini alitangaza “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15) punde kabla ya kubatizwa?

Tumaini langu nafikiri unaelewa na kuamini juu ya Injili ya maji na Roho, hasa katika ubatizo wa Yesu. Huo hapo juu ni muhtasari wa maelezo juu ya Injili ya maji na Roho ambao Yesu aliwapa wafuasi wake. Mitume walitilia mkazo mkubwa juu ya ubatizo wa Yesu pindi walipohubiri Injili. Mtume Paulo alisema “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama yanenavyo maandiko na ya kuwa alizikwa; na yakuwa alifufuka siku ya tatu kama yanenavyo maandiko” (1Wakorintho 15:3-

4). Nini maana ya “Kristo alikufa kwa ajili ya

dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko” Maana yake ni kwamba, kifo cha Yesu kimetupatanisha kwa dhambi zetu zote kulingana na mpango uliowekwa na Mungu katika Agano la Kale. Alikufa kwa ajili yetu kulingana na ufunuo na agano katika Agano la Kale. Waebrania 10:1 inasema, “Basi torati, kwakuwa ni kivuli cha mema yatakayo kuja” Hebu tuone namna ile halisi ya utoaji wa sadaka katika Walawi 1:3-5. Mwenye dhambi ilimpasa kutimiza mambo matatu kama sharti la sadaka ya kuteketezwa kwa upatanisho wa dhambi zake.

1. Kumleta mnyama wa sadaka asiye na doa (Walawi 1:3).

2. Ilimpasa kumwekea mikono juu ya kichwa chake yule mnyama wa sadaka (Walawi 1:4). Hapa, yatupasa kuweka wazi

Page 370: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

370 Maswali na Majibu

sheria ya Mungu; kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ilikuwa ni sheria ya Mungu kuwezesha kutwika dhambi juu yake.

3. Ilimpasa kumchinja kwa upatanisho wa dhambi (Walawi 1:5).

Katika siku ya upatanisho, Haruni aliweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai, kutubu juu yake udhalimu na makosa ya wana wa Israeli, juu ya dhambi zao zote na kumwekea juu yake, kichwani, mbuzi huyo (Walawi 16:21). Katika muda huo, Haruni alikuwa ni mwakilishi wa Israeli. Binafsi aliweka mikono yake juu ya mbuzi, lakini madhambi yote ya mwaka ya watu wa Israeli (kati ya milioni 2-3) yalitwikwa juu yake. Matoleo ya sadaka katika Agano la Kale ni kivuli cha mambo mema yajayo. Yesu alikijitoa nafsi yake kwa mapenzi ya Mungu ili atutakase kulingana na maandiko.

Kwanza ya yote, alikuja katika mwili wa

mwanadamu na kuwa mwana kondoo asiye na doa yeye pia ni mwana wa pekee wa Mungu asiye na doa ”ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Waebrania 1:3). Kwa yote haya imempasa kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu.

Pili, Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu katika Yordani. Ubatizo uliotolewa kwa namna ya “kuwekea mikono” na Yohana Mbatizaji ni mzao wa Haruni na mwakilishi wa wanadamu. Wakati Yohana alipoweka mikono yake juu ya kichwa, cha Yesu Kristo, dhambi zote za dunia zilibebeshwa juu ya Yesu kulingana na sheria ya Mungu aliyoweka. Yesu alimwambia Yohana kabla “kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote,” na akambatiza. Dhambi zetu zote mwishowe alibeba yeye. Siku iliyofuatia, Yohana akasema “Tazama! Mwana Kondoo wa

Page 371: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

371 Maswali na Majibu

Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu“ (Yohana 1:29).

Tatu, Yesu alipokaribia kufa pale msalabani kwa ondoleo la dhambi zetu zote alisema “Imekwisha” (Yohana 19:30). Alifufuka tena toka kifoni ili kutufanya kuwa wenye haki mbele ya Mungu. Kumbuka kwamba sadaka ya dhambi ilitolewa kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Mwenye dhambi ilimpasa kuweka mikono juu ya sadaka yake kabla ya kuchinjwa. Kama angesahau hatua mojawapo, kwa maneno mengine, ikiwa ataondoa kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka asingeweza kukombolewa tokana na kutenda kinyume cha sheria. Ikiwa Mkristo hana ufahamu nini maana ya ubatizo, mtu huyo lazima ataendelea kuwa na dhambi moyoni mwake na hatoweza kuokolewa kwa sababu tu ya imani yake.

Wakristo wengi hujua nusu ya haki ya Yesu tu! Mtume Yohana ameweka wazi katika waraka wake “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo si katika maji tu bali katika maji na katika damu, naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli” (1Yohana 5:6) Vipo vifungu vingi ndani ya Biblia vinavyo unga mkono juu ya umuhimu wa ubatizo wa Yesu katika kukamilisha haki zote za wokovu wetu. Wakristo wote yatupasa kurudi katika Injili ya maji na Roho.

SWALI 6: Ni maandiko yapi

huthibitisha kwamba “Mitume waliwekea mkazo mkubwa wa ubatizo wa Yesu?”

JIBU: Kati ya yote, yatupasa kung’amua

Page 372: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

372 Maswali na Majibu

maana ya ubatizo wetu toka ule ubatizo wa Yesu. Hatutoweza kuzaliwa upya kwa kupokea ubatizo wa maji tu. Tutaweza kuzaliwa upya pale tu tutakapo mwamini Yesu Kristo. Ibada kama ubatizo au tohara ni vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa wa kuwepo katika wokovu wa Mungu. Biblia haijaelezea ubatizo wa washirika kama jambo la lazima kwa wokovu. Bali inawekea mkazo juu ya ubatizo wa Yesu alioupokea toka Yordani na Yohana Mbatizaji.

Kwa kweli, sehemu nyingi katika Biblia huunga mkono kwamba ubatizo wa Yesu ni kitu cha lazima na muhimu kwa wokovu wetu. Kwanza ya yote, ubatizo wa Yesu umetamkwa kama utangulizi kwa tendo lake la haki kwa kila Injili zote nne. Kwa mfano, Injili ya Marko huanza na Injili juu ya Yesu Kristo, mwanzo toka ubatizo wa Yesu, na Yohana na aliandika Injili katika mfumo wa

tarehe, kwa kutumia maneno kama “siku ya pili yake” (1:29) “na siku ya tatu” (2:1) akianzia siku ile Yesu alipobatizwa.

Yohana Mbatizaji alitamka Neno la Mungu katika siku ile Yesu alipobatizwa, kwa kusema, “Tazama! Huyu ndiye mwana kondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29) ujumbe huu maana yake ni kwamba dhambi zetu zote ulimwenguni zilibebeshwa kwake Yesu pale Yohana Mbatizaji kumbatiza. Na ndipo, alikufa msalabani kwa upatanisho wa dhambi zetu kwa kusema “Imekwisha” (Yohana 19:30) na kufufuka tena toka kifoni siku ya tatu.

Mtume Paulo alisema “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko” (1Wakorintho 15:3) maandiko hapa humaanisha katika Agano la Kale. Ni kwa namna gani mwenye dhambi ataweza kutoa

Page 373: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

373 Maswali na Majibu

sadaka ili aweze kusamehewa katika Agano la Kale? Ilimpasa kuweka mikono juu ya kichwa cha sadaka ya mnyama wa kuchinjwa kabla. Ikiwa ataondoa mpangilio wa “kuwekea mikono” juu ya kichwa cha sadaka ya mnyama hangeweza kupata msamaha kwa kutoa sadaka iliyo kinyume cha sheria.

Mtume Paulo alisema “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:3). Hivyo, ni kwa vipi itawezekana kubatizwa katika Yesu? Kubatizwa katika Kristo Yesu ni kuuamini ubatizo wake Yordani, na si ubatizo wetu. Tunapo amini ukweli wa Yohana Mbatizaji kumtwika Yesu dhambi zetu kwa kumwekea mikono juu ya kichwa chake, ndipo tutaweza kubatiza naye.

“Maana ninyi nyote mliobatizwa katika

Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27) wale wote waliomtwika Yesu dhambi zao kupitia ubatizo wa Yohana kwa imani wamekuwa watoto wa Mungu wasio na dhambi tena!

“Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo” (Wakolosai 2:11). Njia ya kukombolewa toka dhambini kwa kuvua mwili wa dhambi ni kutahiriwa kiroho bila ya kutumia mikono (Warumi 2:29 inasema “na tohara ni ya moyo, katika roho”) maana yake, kuamini ubatizo wa Yesu ulio ondoa dhambi za moyoni, Paulo alisema.

“Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo” (1Petro 3:21). Ubatizo ni

Page 374: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

374 Maswali na Majibu

mfano tu uletao wokovu kwetu. Kama tulivyokwisha jua, watu walipotoka nyakati zile za Nuhu kwa kutoamini maji na hivyo ndivyo ilivyo hata leo, wapo ambao bado hawatii na watapotea ingawa wanaweza kuwa wanamwamini Yesu, kwa sababu hawajauamini ubatizo wa Yesu ambao ni maji.

Mtume Yohana aliweka bayana kila kitu juu ya Injili hii katika waraka wake wa kwanza kwa kuandika “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo si katika maji tu, bali katika maji na katika damu” (1Yohana 5:6). Yesu alikuja katika yote mawili kwa ubatizo wa msalaba kutuokoa sisi sote kwa dhambi zetu zote Yohana pia alisema kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni, Baba na Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja) (1Yohana 5:8). Hii inatueleza kwamba

ubatizo wa Yesu, msalaba na Roho vyote kwa pamoja vimeunda wokovu mmoja ulio sahihi.

Yesu alimwambia Nikodemasi “Amin, amin na kwambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Tunazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Imani katika ubatizo wa maji na msalaba wa Kristo ndicho unachohitaji ili ukombolewe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Na hii ndiyo maana Biblia inasema “kuzaliwa upya.”

Kwa hayo, Mtume Petro alisema “tubuni na kila mmoja abatizwe katika jina la Yesu Kristo ili mpate kusamehewa dhambi na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38). Ili tuweze kupokea msamaha wa dhambi zetu, zote na kipawa cha Roho Mtakatifu, yakupasa uwe na imani

Page 375: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

375 Maswali na Majibu

isiyo badilika juu ya ubatizo wa Yesu kwa moyo wako wote. Nini tena tunachoweza kusema? Usikane ukweli ambao ujumbe mwingi huunga mkono ubatizo wa Yesu kuwa ni jambo lisiloweka kando tendo la haki yake kwa wokovu wetu. Ukristo unalazimika sasa kuirudia Injili ya maji na Roho.

“Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na Imani kwa Mungu na wa mafundisho ya uabatizo na kuwekea mikono na kufufuliwa wafu na hukumu ya milele” (Waebrania 6:1-2). Hapa tunaweza kupata chanzo cha kuweza kutafuta juu ya Injili halisi ya Kanisa la Kale. Walifundisha juu ya kanuni za ubatizo, kuwekea mikono, ufufuko wa wafu na hukumu ya milele kwa wale

waliokuwa wapya katika Ukristo. Yatupasa sisi sote tuamini kwa moyo wetu kwamba Yesu Kristo alibeba dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake na kufa msalabani ili kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo kulingana na sheria ya haki ya Mungu.

SWALI 7: Hili ni jambo ambalo tayari

nilikwisha amini na kufundishwa labda yawezekana unajaribu kulitilia mkazo mara kwa mara kwa kuwa ubatizo wa Yesu huwekwa kando mara nyingi katika mafundisho ya msingi. Nini zaidi kilicho cha tofauti kuhusiana na hii Injili ya maji na Roho?

JIBU: “Kuokolewa” maana yake ni

kupokea msamaha wa dhambi zetu zote. Na pia ni kuzaliwa upya. Wakati mwenye

Page 376: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

376 Maswali na Majibu

dhambi anapokuwa mtu mwenye haki kwa kuamini Injili ya uzima, tunasema “amezaliwa upya kwa maji na kwa Roho katika Wokovu wa Yesu.” Roho Mtakatifu huja juu ya wale waliokombolewa na kuzaliwa upya na kushuhudia ndani yao kuwa ni watoto wa Mungu. Hivyo kwa haya yote ni sawa; kupokea msamaha wa dhambi, kupokea Roho Mtakatifu, kukombolewa, kuzaliwa upya, kuwa watoto wa Mungu na kuwa watu wenye haki.

Yesu alisema “mimi ndimi njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa baba ila kupitia kwangu” (Yohana 14:6), hii ina maana Yesu ndiye pekee, mwana pekee wa Mungu kwa kupitia kwake tutaweza kuingia ufalme wa Mungu. Hivyo basi, yatupasa kuelewa jinsi ile Yesu alivyotakasa dhambi zetu zote na kutuhesabu kuwa watu wake, wenye haki ya kuingia ufalme wa Mbinguni.

Baadhi ya Wakristo bado hudhani kwamba kwa kuliitia jina la Yesu tu wataweza kuokolewa. Huamini katika Yesu bila hata ya kuifungua Biblia, bila hata ya kujua nini alichotufanyia ili kutuokoa sisi sote toka dhambini. Mungu ni Roho na Mtakatifu ambaye ndani yake habadiliki, lakini bado tunaendelea kuishi maisha ya dhambi mbele yake. Kuingia ufalme wa Mungu yawezekeana ikiwa tu kwa kupitia Yesu na tutaweza kumwamini yeye kwa imani katika “sheria ya Roho wa uzima” (Warumi 8:1-2).

Watu wengi hawajui hata kile Yesu alichofanya kwa wokovu wao, bali huamini kwa upofu juu yake katika njia panda husema “Bwana, Bwana!” Hudhani pia wameokoka lakini bado wanadhamira za dhambi mioyoni mwao. Ikiwa bado unadhambi au dhamira ya dhambi moyoni

Page 377: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

377 Maswali na Majibu

ingawa imani yako ipo kwa Yesu, sasa umeokolewa na kipi? Akija mtu na akakuuliza “kwa namna gani Yesu alizitakasa dhambi zako zote?” wengi hujibu kirahisi “Labda alizitakasa pale msalabani.” Ndipo kwa swali jingine “sasa je, bado unadhambi au dhamira ya dhambi moyoni mwako?” husema, “Bila shaka! Kwani ni nani asiye na dhambi duniani?”

Jina la Yesu maana yake “Mwokozi aokoaye watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). Tunaamini katika Yesu ili tuokolewe kwa dhambi zetu.

Ingawa, ikiwa bado tunadhambi ndani ya mioyo yetu, huku tukimwamini bado sisi ni wenye dhambi tuliouzwa katika nira ya dhambi na tutahukumiwa kwa hilo. Mtume Paulo alisema “Sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1). Hivi ndivyo baadhi ya watu

ambao bado wanadhambi mioyoni mwao huku bado hawajawa na Kristo Yesu. Kwa nini bado wanabaki kuwa wenye dhambi wasio kombolewa na kupungukiwa wokovu ingawa bado humwamini Yesu? Hii ni kwa sababu wao huamini damu ya Yesu tu, bila ya kuweka dhambi zao juu yake kwa ubatizo. Hivyo bado watakuwa na dhamira za dhambi mioyoni mwao ingawa Yesu alikufa msalabani kwa dhambi zao.

Upo umuhimu wa tofauti wa Wakristo wenye kuamini ubatizo wa Yesu na wale wasio amini, baadhi yao wana ukombozi na kuwa wenye haki kwa kuwa na imani katika ubatizo wa Yesu, hali wale wengine bado hubaki wenye dhambi. Yesu alikuja kwa wenye hati tu, wale waliozaliwa upya kwa maji na kwa Roho.

Kwa haya Mtume Paulo alisema “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa

Page 378: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

378 Maswali na Majibu

katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:3) Watu wengi huamini kuwa Yesu alibeba dhambi zetu pale msalabani, lakini hatutoweza kukiri kwamba hatuna dhambi mioyoni mwetu ikiwa hatutoamini ubatizo wa Yesu. Ikiwa tutafanya hivyo tunatenda kosa la kumdanganya Mungu, ambalo huenda kinyume na dhamira zetu.

Hakika bado tunadhambi au dhamira ya dhambi mioyoni mwetu kwa kuwa hatujamtwika Yesu dhambi zetu zote kwa njia ya imani katika ubatizo wake. Wale wote basi ambao bado hawajaamini Injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba, wako hatarini kuangukia katika kaburi la wapendwa usawa wenye dhambi. Hivyo, haijalishi nini wanachofanya kwa usawa, kama vile kusali sana milimani au kusali kwa dhati kwa kuomba msamaha wakati wa mikutano ya

sala, bado watajikuta wamebaki na dhambi mioyoni mwao.

Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana Bwana, atakaye ingia katika ufalme wa mbinguni bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi watamwambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu!” (Mathayo 7:21-23)

Nani “ninyi mtendao maovu”? Ni wale ambao bado hawajapokea ukombozi wa kweli ndani ya mioyo yao kwa kuamini msalaba pekee. Hii ni imani ya kufikirika, siyo itokayo kwa Mungu. Tunavunja sheria ikiwa hatutoamini ukweli wa wokovu wa Yesu kupitia ubatizo na msalaba. Hatuwezi

Page 379: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

379 Maswali na Majibu

kamwe tukasema tunayo imani ya kweli kabla ya kuamini yote haya mawili ubatizo wa Yesu na msalaba.

Yesu alisema kwamba ikiwa watu watataka kuzaliwa upya ni rahisi ikiwa tu ni katika maji na Roho. Ikiwa pia kwa jinsi ile wangeweza kukombolewa toka mafuriko ya maji kama wangekuwa katika safina ya Nuhu ndivyo hivyo tutaweza kupokea ondoleo la dhambi zetu zote na kuishi maisha ya uaminifu ikiwa tu tutaamini Injili ya maji na Roho. Bila Injili ya maji na Roho hautoweza kupokea msamaha wa dhambi au kufanywa mtoto wa Mungu.

SWALI 8: Na uhakika kwamba

kuamini katika Yesu kumeniokoa. Nina amani na moyoni. Lakini bado sijaelewa juu ya ujumbe wako. Je

yanipasa kuamini ubatizo wa Yesu pamoja na msalaba wake ili niokolewe?

JIBU: Ikiwa huamini ubatizo wa Yesu, hii

ni hakika kwamba bado una dhambi moyoni. Mtume Yohana alisema “Tukisema kwamba hatuna dhambi twajidanganya wenyewe wala kweli haimo mwetu” (1Yohana 1:8) Ukisema ya kwamba huna dhambi, ingawa ukweli ni kwamba unadhambi kwa sababu hukuamini ubatizo wa Yesu ni tendo la kujidanganya katika dhamira yako na ni ushahidi tosha ya kwamba kweli haimo ndani yako. Ushuhuda wa wokovu huingia moyoni mwetu pale tunapopokea ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu kuwa kipawa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na msalaba wake.

Mtume Paulo alisema “…Injili ya namna nyingine wala si nyingine…” (Wagalatia 1:6-

Page 380: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

380 Maswali na Majibu

7). Hakuna Injili nyingine zaidi ya Injili ya maji na Roho, ambayo Mitume walipokea toka kwa Yesu na kuhubiri kwa watu, ndiyo itakayo tuokoa na dhambi zetu zote. Ikiwa hatutoamini Injili ya maji na Roho ambayo mitume walihubiri, hakika bado dhambi imo kati yetu.

Ni kwa namna gani tunaweza kuwa na dhamira ya wokovu ikiwa bado tuna dhambi? Pale Wakristo, ambao hawajazaliwa upya wanapokuwa na tabia njema mbele ya Mungu wanakuwa na uhakika juu ya wokovu wao wakiwa na furaha na uhakika kwa jinsi hii wanakosa uhakika na wana woga wa mzigo wa dhambi ulio moyoni mwao pale inapojitokeza kwamba wametenda dhambi mbaya. Huu ni wokovu wa kwenda pasipo mwelekeo wa kutumainiwa ulio na msingi wa hisia na mawazo yetu ambamo Mungu hausiki. Watu wa aina hii wamo hatarini

zaidi katika ule mpango wa kufanya sala za toba kila siku ili waweze kuwa watakatifu hatua kwa hatua na kuendelea na wokovu uyumbao.

Wale wote wenye kuamini wokovu usio wa kweli hufikiri kwamba wataendelea kuwa na wokovu ulio sahihi katika nyakati zijazo za maisha yao ikiwa wataweza kuendelea kuishi maisha matakatifu kwa kumuomba Mungu msamaha kila siku na kufuata sheria yake kwa matendo. Hata hivyo bado ni wenye dhambi ikiwa bado hawajamtwika Yesu dhambi zao kwa kupitia imani katika ubatizo wake.

Wokovu Mungu alioufanya ni wokovu ulio sahihi unatueleza juu ya Yesu kubeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wa Yohana kule Yordani na alifuta kabisa dhambi hizo msalabani.

Kwa haya yote Mtume Yohana alisema

Page 381: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

381 Maswali na Majibu

“Tukizi ungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:9). Ikiwa dhambi zetu zote hazijasamehewa kupitia Injili ya maji na Roho kwa kutoijua, yatupasa kukiri mbele ya Bwana kuwa ni wadhambi, ingawa tunamwamini Yesu na kujua kuwa ni wenye dhambi bado ambao mwisho wetu ni jehanamu kwa dhambi hizo. Huku ndiko kukiri kwa ukweli dhambi. Dhambi hazitoweza kutakaswa bila Injili ya maji na Roho, haijalishi udogo wa dhambi. Tunapokiri kwa namna hii basi, Injili ya maji na Roho hututakasa dhambi zetu mara moja na kutufanya wenye haki.

Sasa ndio wakati uliokubalika (2Wakorintho 6:2). Kwa yeyote asikiaye na kuiamini Injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba wake ataokolewa na dhambi zake

zote, kuwa mwenye haki, na anayo imani madhubuti ya kuweza kuingia ufalme wa Mbinguni wakati Bwana atakapo rudi. Imani yeyote katika mafundisho, kanuni na thiologia zaidi ya Injili ya kweli, hakuna wokovu wa dhambi zetu ile ni mitego tu ambayo ibilisi ameiweka ndani ya mawazo ya wanadamu. Yatupasa kurudia Injili ya maji na Roho na kupokea wokovu wa kweli toka dhambi zilizomo mioyoni mwetu. Huku ndiko kumpenda Yesu na alichotufanyia.

SWALI 9: Ikiwa ufahamu wako juu

ya maji na Roho ulikuwa sahihi, hivyo wokovu ingekuwa rahisi kwa yule mwovu aliyesulubiwa na Yesu. Ikiwa mwovu huyo angelichukuliwa kuwa na msamaha kulingana na sheria, basi Mungu asingekuwa mwenye haki, kwa

Page 382: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

382 Maswali na Majibu

sababu angevunja sheria yake mwenyewe ya kuingia ufalme wa Mbinguni. Je, waweza vipi kulielezea hili juu ya wokovu wa huyu mwovu pale msalabani?

JIBU: Katika wakati huo, Wayahudi wote

walikuwa wakisubiri kuja kwa Masia. Hivyo, walijua fika juu ya “sheria na mpangilio wa kutoa zabihu ambao Mungu alikwisha wapa kwa kupitia Musa, kuliko watu wengine wowote. Waliamini kwamba Masia angekuja kulingana na sheria ya Mungu katika upatanisho, na angewaweka huru tokana na dhambi zao zote.

Ingawa hawakuamini ubatizo wa Yesu uliotoka kwa Mungu kupitia Yohana Mbatizaji ambao ungemtwika dhambi zote za ulimwengu Yesu (Marko 11:27-33) lakini walimchukulia Yesu kama aliye wapotosha

watu hivyo wakimsulubisha. Kwa kuwa Warumi walilindwa na sheria ya

kuteswa au kusulibiwa kulingana na sheria ya Kirumi (Matendo 22:25-29, 23:27) twajua basi wale waovu pale msalabani hawakuwa Warumi bali ni Wayahudi. Na pia tunajua kuwa waovu hawa walikuwa ni Wayahudi waliomwogopa Mungu kutokana na maneno yake aliyasema “Bwana unikumbuke utakapofika katika Ufalme wako” (Luka 23:42). Yule muovu wa Kiyahudi tayari alikuwa akielewa sheria na mpangilio wa utoaji wa dhabihu ambao Mungu alimpa Musa. Hivyo aliamini kwamba Masi angelikuja kulingana na sheria ya Mungu ya Mungu katika msamaha.

Wale wajao kwa Mungu yawapasa kukiri kwamba ni wenye dhambi,walio wekewa mwisho wa jehanamu kwa dhambi zao. Mwovu yule alikiri dhambi zake kwa kusema

Page 383: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

383 Maswali na Majibu

“nayo ni haki kwetu sisi kwa kuwa tunapokea malipo tiliyostahili kwa matendo yetu” (Luka 23:41). Twawezaia kujua kwamba mwovu huyu alikuwa na hofu ya Mungu na tumaini lake lilikuwa ni kuingia katika Ufalme wa Mbinguni kutokana na maneno yake aliyosema “Bwana unikumbuke utakapofika katika Ufalme wako” (Luka 23:42).

Alisema “lakini huyu mtu hakutenda lolote baya” (Luka 23:41). Alijua vipi juu ya matendo ya Yesu? Aliamini kwamba Yesu alitungwa katika mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu alizaliwa na Bikira Mariam,alibatizwa na Yohana Mbatizaji mwakilishi wa wanadamu wote. Alibeba dhambi za ulimwengu na kusulubiwa. Alikuwa ni Myahudi aliyeamini kile Yesu alichofanya kwa watu wote, pamoja na yeye ingawa alikuwa akisulibiwa kwa sababu ya

kupokea ujira wa matendo hapa duniani. Wale wote wenye kutubu dhambi zao kwa

kupitia ubatizo wa Yohana huitambua haki ya Mungu pale wanaposikia kwamba dhambi zao zote zilikwisha bebwa na Yesu kwa ubatizo wake.Ili haki kwa wale wasio upokea ubatizo huo wa toba kukataa mapenzi ya Mingu kwa sababu hawakuamini ubatizo wa Yesu (Luka 7:28-30).

Kinyume chake yule mwovu aliyeokoka alikiri kila kitu Yesu alichofanya kilikuwa ni sahihi hali kwa yule Myahudi mwingine hakufanya hivyo. Yawezakana akawa ni mojawapo ya wayahudi ambao waliosikia habari hizo zote ambazo zilikwisha timia kati yao (Luka 1:1). Angeweza hata kusema kwamba Yesu alikuwa ni mwenye haki na Masia aliyetabiriwa kuja kwa sababu mwishowe alikuja kuamini pale msalabani kwamba Yesu alizibeba dhambi zake zote

Page 384: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

384 Maswali na Majibu

kwa kupitia ubatizo wake.Kwa hilo aliweza kuokolewa. Alikuwa pia ameokolewa kwa kuamini Injili ya ubatizo wa maji na Roho kwa sababu Mungu ni haki hutoa haki kwa wale waaminio ubatizo wa Yesu na msalaba wake kutokana na sheria yake ya Roho wa Uzima.

SWALI 10: Kwa kuwa Mungu ni wa

rehema na mwenye huruma je! asingeweza kutuchukulia kuwa wenye haki, ingawa tumetenda dhambi mioyoyoni mwetu ikiwa tumeamini katika Yesu tu?

JIBU: Mungu ni Upendo na pia ni wa haki

kwa hinyo, hutoa hukumu ya dhambi kwa haki hata iwe vipi. “Mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) maana yake wenye

dhambi mwisho wao ni motoni baada ya hukumu. Hutenga wenye haki toka kwa wenye dhambi kama alivyofanya mwanga toka kwenye giza. Mungu huwaita wale wasio na dhambi walio mwaamini Yesu kwa kutakaswa dhambi zao zote kupitia ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kweke kuwa ndiyo wenye haki.

Kwa hivyo wale wote ambao bado wana dhambi ndani yao kwa kutoamini batizo wa Yesu, ni wenye dhambi mbele ya Mungu. Ndio wasio na imani katika maji kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu kama wakati ule wa watu wa Nuhu.Ikiwa Mungu atawachukulia wale wenye dhambi ambao bado dhambi zimo ndani yao kuwa wenye haki na watakatifu, basi ni lazima kwake atakuwa ni mwongo na hivyo hatoweza kutoa hukumu ya haki au kutawala viumbe wake.

Page 385: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

385 Maswali na Majibu

Mungu amesema “sinto wapa haki waovu” (Kutoka 23:7) waovu ni wale wafuatao na kutegemea zaidi taratibu za kibinadamu na kuacha injili ya maji na Roho ambayo Mungu alileta ukombozi wetu katika dhambi zetu zote katika haki na usawa kwa njia iliyo sahihi.Yesu alisema “kwa habari ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi” (Yohana 16:9). Dhambi iliyobaki duniani pekee sasa nikutoamini ukweli kwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo na msalaba na kuwa Mwokozi wetu. Hii ni dhambi ya kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu ambayo haitoweza samehewa. Hakuna njia nyingine tena kwa wale waliokufuru dhidi ya Roho Mtakatifu kuweza kuokolewa kwa sababu hawaamini kuwa Yesu alitakasa dhambi zao zote.

Mtume yohana alisema “Kila atendaye dhambi afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni

uasi. Nanyi mnajua ya kuwa alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi na dhmbi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila aatendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua” (1Yohana 3: 4-6). Ni kutenda uasi kwa kutoamini ukweli kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo na msalaba. Yeye atawakana wale wote waliotenda dhambi hii katika siku ya mwisho.

Wale wote wenye kumwamini hawana dhambi na wanaungana na Yesu kwa ubatizo wake. Wale ambao walio mwachia dhambi zao zote katika maisha yao juu yake kwa imani katika ubatizo hawana tena dhambi ingawa bado watendelea kutenda dhambi kutokana na udhaifu wa miili yao.

Mungu huwaita wale walioziweka dhambi zao juu ya Yesu na kutakaswa kwa sheria ya Roho ya Uzima kwa kuwa ndiyo wenye haki.

Page 386: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

386 Maswali na Majibu

Amewapa Roho Mtakatifu kama kipawa. Roho Mtakatifu kamwe haji juu ya wale walio na dhambi mioyoni mwao. Daudi alisema katika Zaburi “Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya. Mtu mwovu hatakaa kwako” (zaburi 5:4). Roho mtakatifu wa mungu kamwe hawezi kukaa mioyoni mwa wale wenye dhambi ndani yao. Hata mwenye dhambi asiye na Roho Mtakatifu ndani yake aweza kusema ameokoka toka dhambini kulingana na mafundisho na kanuni za mawazo yake. Hata hivyo mtu hawezi kusema hana dhambi moyoni na ni mwenye haki mbele ya Mungu. Lakini Mungu hawezi kumwita mwenye dhambi kuwa ni mwenye haki. Mwenye dhambi ana wajibu kuhukumiwa na hivyo yampasa kuamini injili ya maji na Roho ili aweze kuokolewa.

SWALI 11 Ikiwa twasema kwamba Yesu alishaondoa dhambi zetu zote za zamani sasa, na zile zijazo mbeleni maishani mwetu, nikwa namna gani basi matarajio ya mtu mbeleni yatageuka ikiwa ataendelea kuwa na dhambi kwa kufikiri juu ya ukweli kwamba alikwisha samehewa dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake? Hata ikiwa ataua, yeye hutambua ya kwamba alikwisha patanishwa hata kwa kosa la aina hii kwa kupitia Yesu msalabani. Hivyo, ataendelea kutenda dhambi bila ya kusita kwa kuwa tunaamini Yesu alikwisha samehe hata dhambi zijazo maishani. Hebu tafadhali naombauelezee juu ya mambo haya

JIBU: Kwanza ya yote nakushukuru kwa

Page 387: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

387 Maswali na Majibu

kuleta maswali juu ya injili hii ya maji na kwa Roho. Swali uliloleta ndiyo moja ya maswali ambayo Wakristo waliyojiuliza hapo mwanzo kabla ya kuzaliwa upya. Najua kwamba una wasiwasi kwamba watu waliozaliwa upya wataendelea kutenda dhambi kwa kuwa wamefunuliwa juu ya injili iliyo sahihi ingawa napenda kukwambia kwamba watu hawa wanaoamini injili ya maji na kwa Roho kamwe hawapo hatarini kuishi katika maisha ya aina hii unayotia wasiwasi juu yake, bali kwao wataishi maisha yale ya haki badala yake.

Yakupasa kwanza ufikiri juu ya hili. Ikiwa Roho Mtakatifu ni mkweli ndani yako,basi siku zote utazaa matunda matakatifu hata kama si kwa hiyari yako. Kwa upande mwingine, ikiwa Roho Mtakatifu hakai ndani yako, hutoweza kuzaa matunda ya aina yoyote ya Roho, haijalishi ni kwa namna

gani utajaribu kwa bidii. Ni vipi mtu labda ataweza kuzaa matunda ya Roho ikiwa hana Roho Mtakatifu ndani yake hata kama anamwamini Yesu kwa namna gani? Hii haiwezekani! Bwana alisema kwamba mti mbaya hautoweza kuzaa matunda mema (Mathayo 7:17-18).

Napenda sasa nikuulize swali na unipe jibu lake Unaamini katika Yesu? Lakini je! kweli unaishi maisha yako huku ukishinda dhambi za ulimwengu? Je, unaishi maisha ya haki kama Mtumishi wa Mungu huku ukishinda dhambi za dunia,kumtumikia zaidi na kuwaongoza wengine kuokoka toka dhambini kwa kupeleka Injili ya maji na kwa Roho kwao? Je umekuwa kweli mwenyehaki asiye na dhambi hata kidogo baada ya kuwa na imani juu ya Yesu? Imani pekee na Injili ambayo itaweza kukuruhusu kujibu ndiyo kwa maswali haya ni Injili ya maji na kwa

Page 388: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

388 Maswali na Majibu

Roho, ambayo Bwana iliyomshindia katika Agano la Kale na Jipya.

Tunaendelea kutenda dhambi hapa ulimwenguni hata baada kumwamini Yesu.

Ijapokuwa Bwana wetu alibatizwa na Yohana na kumwaga damu yake msalabani kutuokoa na dhambi zetu zote ulimwenguni. Hivyo, Bwana ametenda jambo la haki kwetu na tumeokolewa toka dhambini kwa kupitia imani ya haki ya Mungu, ubatizo wa Bwana na damu ambayo iliondolea mbali dhambi zetu.

Napenda nikuulize maswali kadhaa tena. Je, upo huru kwa dhamira za dhambi? Je, wewe ni mwenye dhambi tena kama hapo awali hata baada ya kumwamini Yesu? Ikiwa hivi ndivyo kweli, bila shaka kwakuwa hukuifahamu injili ya maji na Roho. Hivyo basi umeangukia katika tatizo na uharibifu wa kurithiwa na mwili kwa sababu huna

Roho moyoni mwako. Haijalishi ni kwanamna gani ulivyo muumini aliye mwaminifu, njia pekee ya kuepuka mawazo ya kimwili ni kuufungulia moyo wako kwa kuingiza injili ya maji na Roho. Yakupasa kuachana na mawazo yako ya kimwili na kurudia maandiko ya Neno la Mungu ili uelewe ukweli wa Injili ya maji na Roho iliyo ya kweli.

Wapo watu ulimwenguni humu wenye kubadili sheria ya wokovu ambao Bwana aliweka kwa namna wapendavyo ingawa humkiri Bwana kwa vinywa vyao. Ikiwa nawe mmoja wao kati ya watu wa aina hii, Bwana atakukana siku ile ya mwisho. Natumaini kwamba hili halitatokea kwa yoyote yule ulimwenguni. Nachukua nafasi hii kukuombea wewe mwenye kuamini juu ya damu ya Yesu msalabani ndiyo pekee iwezayo kuokoa, na hivyo uliuliza maswali

Page 389: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

389 Maswali na Majibu

kutokana na hamu ya kuishi maisha yaliyobaki katika muda wa uhai wako mbali ya dhambi.

Yamkini mawazo yako ni ya kimwili mbayo “hayatii sheria ya Mungu,wala hawezi kutii” (Warumi 8:7). Paulo husema “Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:8). Ikiwa kwa ukweli unatamani kuwa na imani yenye kumpendeza Mungu yakupasa uamini kazi ile njema ya Bwana ambayo iliyomfanya aje ulimwenguni kupitia Bikira Mariam, kuchukua dhambi za wanadamu kwa ubatizo alioupokea kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordan, na ndipo kuitiza haki ile ya Mungu.

Unafikiri ni nani awezaye kubeba kazi ile ya haki ya Mungu, aliye haki au mwenye dhambi? Mwenye dhambi yumo katikati ya dhambi kwa sababu hajapokea msamaha wa dhambi mbele za Mungu. Hivyo, jambo la

pekee asubirilo ni hukumu ya Mungu kwa dhambi zake. Mungu hatoweza kamwe kumwacha mwenye dhambi aingie katika Ufalme wake kwa sababu “Maana hawi Mungu apendezwaye na ubaya, mtu mwovu hatakaa kwake” (Zaburi 5:4). Mungu alisema kwamba ikiwa mwenye dhambi angalikuja kwake na kumuomba kitu toka kwake, kamwe hatomsikiliza sala zake mwenye dhambi kwa kuwa “dhambi zake zimeuficha uso asiune” (Isaya 59:1-2). Mwenye dhambi bila shaka atakwenda motoni kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.

Wenye haki ndiyo pekee watakuwa Watakatifu na hivyo hawana dhambi mioyoni mwao kwa kutenda matendo ya haki. Kwa nyongeza. Roho Mtakatifu hukaa ndani ya wote wenye haki, wasio na dhambi baada ya kuamini ubatizo wa Yesu na msalaba wake. Mtume Petro alisema katika siku ile ya

Page 390: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

390 Maswali na Majibu

Pentekoste “tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu (Matendo 2:38).

Kinachosemwa katika kifungu hiki ni kwamba, ikiwa unataka imani ya kweli na kupokea msamaha wa dhambi zako zote kwa imani, yakupasa basi kuamini yote mawili, Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Imani hii itaweza kukuruhusu “kupokea ubatizo katika Jina la Yesu” maana yake tunaweza kusema,utaweza kupokea msamaha wa dhambi zako kwa imani katika matendo ya haki ya Yesu. Bila shaka wafuasi wa Yesu walihudumia kwa ibada hii ya ubatizo kwa wale wenye kuzaliwa upya, wenye kuamini, walio na imani katika ubatizo wa Yesu na msalaba wake. Yesu aliamuru wafuasi kumbatiza yeyote katika Jina Baba na Mwana na Roho na Mtakatifu

(Mathayo 28:19). Zaidi pia Mtume Paulo alisema “lakini mtu

awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyu si wake” (Warumi 8:9). Mungu kamtoa Roho Mtakatifu kwa wenye haki ili kuweka muhuri kuwa watoto wake. Roho Mtakatifu hatoweza kamwe kuwa ndani ya wenye dhambi, badala yake hupendelea Utakatifu(kwa kuwa mbali na dhambi). Roho pia huongoza wenye haki katika njia za haki kufuata mapenzi ya Baba. Sasa basi ni yapi mapenzi haya ya Baba? Ni kueneza Injili ya maji na Roho kwa watu wa mataifa yote na kuwabatiza kulingana na Amri Kuu. Miili ya wenye haki na wenye dhambi hutenda dhambi hadi siku ya mwisho kifoni. Ijapokuwa Bwana amekwisha tenda tendo la haki la kufuta dhambi zote za watu wazitendazo katika mwili na mioyoni kwa ubatizo wake na damu yake. Hii ni haki ya

Page 391: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

391 Maswali na Majibu

Mungu ambayo Yesu aliitimiza. Hivyo imeandikwa katika Biblia “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani” Neno “ndani yake” ndiyo hii Injili iliyo ya kweli. Mtu aliyekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kuamini haki ya Mungu ataishinda ile “sheria ya kifo na dhambi” na badala yake kuifuata haki ya Kristo Yesu. Hii ndiyo pekee kwa kupitia Roho aliyekuja na kuishi ndani ya wale waaminio Injili ya maji na kwa Roho.

Dhambi zote za kale sasa na zijazo mbeleni za mwenye haki zilikwisha twikwa kwa Yesu siku ile alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Mwili wa mwenye haki pia na umekufa pamoja na Yesu. Mtu anapoamini, huungana na Yesu na kufanana pia na kifo chake. Hii huwa ni hukumu ya wote wenye dhambi (Warumi 6).

Hivyo basi, ingawa mwili wa mwenye haki

unatenda dhambi mara kwa mara maishani mwake, Roho Mtakatifu akaaye ndani yake humwongoza katika kumfuata. Mwenye haki humfuata Roho Mtakatifu na hufanya kazi ya Mungu kwakuwa Roho huyo Mtakatifu hukaa nadni yake siku zote.

Hata katika nyakati za Mitume, watu wengi walikuwa waki washutumu bila sababu wale waliozaliwa upya kwa sababu walikuwa na chuki ya kutoamini juu ya maisha ya watu wenye kuzaliwa upya ambao walikuwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Ijapokuwa watu wa aina hii walipotoka juu ya injili ya Kweli katika maji na kwa Roho ambayo Mitume walihubiri ikiwa walidhani ni mawazo ya kimwili. “Tuseme nini basi tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi 6:1-2) akaongeza. “Namshukuru

Page 392: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

392 Maswali na Majibu

Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, basi kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi” (Warumi 7:25).

Kwa hitimisho, mwili wa mwenye dhambi bado haujitoshelezi na hauna uchaguzi bali kuendelea kutenda dhambi isipokuwa utaendelea kumfuata Roho Mtakatifu, kwa kuhubiri Injili ulimwenguni pote. Mwenye haki hutembea katika Roho kwa kuwa moyo wake umetulia chini ya neema “Ni nini basi? tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! Hatujui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa Watumwa wake katika kumtii, mmekuwa Watumwa wake yeye mnayemtii kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki?” (Warumi 6:15-16).

Kama ilivyo maua bandi yalivyo tofauti na kweli yenye uhai, Bwana aliye ndani ya moyo wa mwenye haki na mwenye dhambi ni tofauti kwa kila mmoja. Ikiwa Bwana wa mwenye haki ni Roho Mtakatifu huyu ataenenda katika Roho na kufuata njia za kweli na za haki zinazompendeza Mungu. Kwa upande mwingine mwenye dhambi hana uchaguzi bali kufuata dhambi kwani bwana aliye ndani yake ndivyo alivyo. Mwenye dhambi kamwe hataishi maisha Matakatifu kwa sababu hana Roho wa Mungu, kwa kuwa ana uovu mwingi ndani yake.

Fikra za kwamba wenye kuamini Injili ya maji na Roho hatoweza kwa kiasi fulani kuishi maisha Matakatifu ni aina za fikra na kanuni potofu zitokazo kwa kusema “Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyo yajua, na mambo wayatambuyo kwa asili

Page 393: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ YALIYOMO ►

393 Maswali na Majibu

wajiharibu kwa hayo kama wanyama wasio na akili” (Yuda 1:10). Walio wengi nyakati hizi hawaelewi ndani yao juu ya maisha ya haki hata ikiwa wanaikiri Injili ya maji na Roho kuwa ni Injili ya kweli kwa sababu hawaamini kikamilifu na hawajapokea hilo ndani ya mioyo yao.

Unafikiri nini juu matendo ya haki kwa aliyezaliwa upya? Wameachilia mambo yao yote yenye thamani hata nafsi zao kama sadaka iliyo hai, kwa mambo mema katika kueneza Injili ulimwenguni pote.Kutokana na mawazo yako, kwa nini unafikiri kwamba wenye kuamini Injili ya maji na Roho wataweza kutenda dhambi kwa makusudi katika kificho cha sababu ya Injili waaminio?

Wenye haki hutenda mema kwa imani mbele ya uwazi wa kweli na haki ya Mungu. Wale wote watendao haki ya Mungu wamezaliwa upya. Tunatumaini wenye

dhambi wote watarudia Injili ile ambayo Yesu aliyohuisha dhambi zao zote kwa ubatizo na damu yake.

Ndiyo hamu yetu ni kuona unapokea msamaha wa dhambi zako zote kwa kuamini Injili hii kwa moyo wako wote na kusubiri hadi Bwana atakapo kuja siku ile ya mwisho bila ya dhambi.

Page 394: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

e-Bookse-BooksTheNewLifeMission

?

MAELEKEZO KWA MTUMIAJI

Namna ya kujisomea

Namna rahisi ya kujisomea

Ukurasa wa jalada

Page 395: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ MAELEKEZO KWA MTUMIAJI ►

395 MAELEKEZO KWA MTUMIAJI

NAMNA YA KUJISOMEA

KUPITIA KURASA ZA KITABU

Kurasa hadi kurasa

Kufungua ukurasa unaofuata

Page 396: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ MAELEKEZO KWA MTUMIAJI ►

396 MAELEKEZO KWA MTUMIAJI

KURASA HADI KURASA

• Baobonye

1) Gombo kwenda juu / kibonye cha gombo kwenda chini Gombo kwenda juu = Gombo la nyuma, Kibonye cha gombo kwenda chini = Gombo la mbele

2) Kibonye cha mshale

← au ↑ = Gombo la nyuma, → au ↓ = Gombo la mbele

• Kitufe cha menyu ya programu ya Acrobat Reader

◄ = Gombo la nyuma, ► = Gombo la mbele • Kiungo

◄ = Gombo la nyuma, ► = Gombo la mbele

Yaliyomo = Nenda katika Yaliyomo

Page 397: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ MAELEKEZO KWA MTUMIAJI ►

397 MAELEKEZO KWA MTUMIAJI

KUFUNGUA UKURASA UNAOFUATA

1) Baobonye

Ctrl + N Key : Idadi ya kurasa unazo taka kupitia

2) mwambaa biringizo wa programu ya Acrobati Reader

Bofya na kokota katika mwambaa birigizo hadi pale tarakili au namba katika uga itakapo fanana na kurasa unayo ihitaji.

Page 398: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

◄ MAELEKEZO KWA MTUMIAJI ►

398 MAELEKEZO KWA MTUMIAJI

NAMNA ILIYO RAHISI KATIKA KUJISOMEA

Kutumia alamisho

Waweza kusogeza kwa urahisi pale utakapo kwa kutumia alamisho

- Kuonyesha alamisho: Bonyeza Kibonye chenye alama F5 katika baobonye yako

- Kuficha alamisho: Bonyeza tena Kibonye chenye alama F5

Page 399: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

www.nlmafghanistan.comwww.nlmafrikaans.comwww.nlmalbania.comwww.nlmamharic.comwww.nlmangola.comwww.nlmarabemirates.comwww.nlmarabic.comwww.nlmargentina.comwww.nlmarmenia.comwww.nlmaruba.comwww.nlmaustralia.comwww.nlmaustria.comwww.nlmbahamas.comwww.nlmbahrain.comwww.nlmbangladesh.comwww.nlmbelarus.comwww.nlmbelgium.comwww.nlmbengali.comwww.nlmbenin.comwww.nlmbhutan.comwww.nlmbolivia.com

www.nlmbotswana.comwww.nlmbrasil.comwww.nlmbriton.comwww.nlmbrunei.comwww.nlmbulgalia.comwww.nlmburkinafaso.comwww.nlmburundi.comwww.nlmcameroon.comwww.nlmcanada.comwww.nlmcebuano.comwww.nlmchichewa.comwww.nlmchile.comwww.nlmchin.comwww.nlmchina.comwww.nlmcolombia.comwww.nlmcongo.comwww.nlmcostarica.comwww.nlmcotedivoire.comwww.nlmcroatia.comwww.nlmczech.comwww.nlmdenmark.com

www.nlmdioula.comwww.nlmdominica.comwww.nlmdutch.comwww.nlmecuador.comwww.nlmegypt.comwww.nlmelsalvador.comwww.nlmequatorialguinea.comwww.nlmethiopia.comwww.nlmfinland.comwww.nlmfrance.comwww.nlmfrench.comwww.nlmgabon.comwww.nlmgeorgian.comwww.nlmgerman.comwww.nlmgermany.comwww.nlmghana.comwww.nlmgreek.comwww.nlmgrenada.comwww.nlmguatemala.com

A

B

C

D

E

F

G

Please find your vernacular websites below.

You can download Christian e-books and request Christian books for free.

Feel free to visit our websites below right now!

Please find your vernacular websites below.

You can download Christian e-books and request Christian books for free.

Feel free to visit our websites below right now!

Please find your vernacular websites below.

You can download Christian e-books and request Christian books for free.

Feel free to visit our websites below right now!

The Official Website of The New Life Mission

www.nlmission.comwww.nlmission.comor

www.bjnewlife.orgwww.bjnewlife.orgW

The New Life Mission

orldwide websites of

� Some of these websites may not work because they are still under construction.

◄ YALIYOMO ►

Page 400: Je, umezaliwa upya kweli kwa maji na kwa roho?

www.nlmgujarati.comwww.nlmhaiti.comwww.nlmhindi.comwww.nlmholland.comwww.nlmhonduras.comwww.nlmhungary.comwww.nlm-india.comwww.nlmindonesia.comwww.nlmiran.comwww.nlmiraq.comwww.nlmisrael.comwww.nlmitaly.comwww.nlmjamaica.comwww.nlmjapan.comwww.nlmjavanese.comwww.nlmkannada.comwww.nlmkazakhstan.comwww.nlmkenya.comwww.nlmkhmer.comwww.nlmkirghiz.comwww.nlmkirundi.comwww.nlmkorea.comwww.nlmlatvia.comwww.nlmluganda.comwww.nlmluo.comwww.nlmmadi.comwww.nlmmalagasy.comwww.nlmmalayalam.comwww.nlmmalaysia.comwww.nlmmarathi.com

www.nlmmauritius.comwww.nlmmexico.comwww.nlmmindat.comwww.nlmmizo.comwww.nlmmoldova.comwww.nlmmongolia.comwww.nlmmyanmar.comwww.nlmnepal.comwww.nlmnewzealand.comwww.nlmnigeria.comwww.nlmnorthkorea.comwww.nlmnorway.comwww.nlmpakistan.comwww.nlmpanama.comwww.nlmperu.comwww.nlmphilippines.comwww.nlmpoland.comwww.nlmportugal.comwww.nlmportuguese.comwww.nlmprcongo.comwww.nlmqatar.comwww.nlmromania.comwww.nlmrussia.comwww.nlmsaudiarabia.comwww.nlmserbian.comwww.nlmshona.comwww.nlmsingapore.comwww.nlmslovakia.comwww.nlmslovene.comwww.nlmsolomon.com

www.nlmsouthafrica.comwww.nlmspain.comwww.nlmspanish.comwww.nlmsrilanka.comwww.nlmsuriname.comwww.nlmswahili.comwww.nlmswaziland.comwww.nlmsweden.comwww.nlmswiss.comwww.nlmtagalog.comwww.nlmtaiwan.comwww.nlmtamil.comwww.nlmtelugu.comwww.nlmthailand.comwww.nlmtogo.comwww.nlmtonga.comwww.nlmturkey.comwww.nlmuganda.comwww.nlmukraine.comwww.nlmurdu.comwww.nlmusa.comwww.nlmvenezuela.comwww.nlmvietnam.comwww.nlmzambia.comwww.nlmzimbabwe.comwww.nlmzou.com

H

J

K

L

M

N

P

Q

R

S

T

U

V

Z

I

W The New Life Missionorldwide websites of

◄ YALIYOMO ►