16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1108 RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA , JANUARI 17 - 23, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz CHADEMA wavuruga Maulidi Morogoro Wavamia gari la matangazo Wafanya fujo Msikitini Boma Jaji ataka sababu Masheikh Uamsho kunyimwa dhamana Mapinduzi yawakuta ndani mara 2 Danadana zinaendelea hadi Jan. 31 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Nyamagana jijini Mwanza imeridhia maombi ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu, kwenda kutibiwa nchini India. Aidha Mahakama imeridhia Sheikh Ilunga kurejeshewa hati yake ya kusafiria, ambayo ilikuwa Mahakama yaridhia Ilunga kwenda India Umati wafurika mahakamani Watoka Musoma, Bukoba, Geita 'Passport’ yake kurejeshwa Na Mwandishi Wetu Inaendelea Uk.16 Tupo Mwananyamala Islamic Club Kona ya Makumbusho Dar es salaam. Tunaendelea Kusajili wanafunzi wa Q.T, Reseaters O-Level, waliofeli Kidato cha Pili na Kidato cha nne. Kwa mawasiliano zaidi tutembelee Shuleni au piga simu 0767 307 607, 0783- 723 312 au 0652 010 136. Pata elimu Bora kwa Gharama Nafuu. SEKONDARI YA JIONI ( MESS) Inatangaza nafasi za masomo 2014 SHEIKH Farid Hadd kabla ya kuwekwa ndani. Na Bakari Mwakangwale WAISLAMU Mjini Mrogoro, wamelaani kitendo Cha Chama Cha CHADEMA, kuvamia na kulifanyia fujo gari lililokuwa likitangaza sherehe za Maulidi na kusababisha kusitishwa kwa matangazo hayo. Inaendelea Uk. 3 Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Philman Mbowe. SHEIKH Ilunga Kapungu.

ANNUUR 1108

Embed Size (px)

Citation preview

ISSN 0856 - 3861 Na. 1108 RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA , JANUARI 17 - 23, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

CHADEMA wavurugaMaulidi Morogoro

Wavamia gari la matangazo Wafanya fujo Msikitini Boma

Jaji ataka sababu MasheikhUamsho kunyimwa dhamana

Mapinduzi yawakuta ndani mara 2Danadana zinaendelea hadi Jan. 31

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Nyamagana jijini M w a n z a i m e r i d h i a maombi ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu, kwenda kutibiwa nchini India.

A i d h a M a h a k a m a imeridhia Sheikh Ilunga kurejeshewa hati yake ya kusafiria, ambayo ilikuwa

Mahakama yaridhia Ilunga kwenda India

Umati wafurika mahakamaniWatoka Musoma, Bukoba, Geita'Passport’ yake kurejeshwa

Na Mwandishi Wetu

Inaendelea Uk.16

Tupo Mwananyamala Islamic Club Kona ya Makumbusho Dar es salaam. Tunaendelea Kusajili wanafunzi wa Q.T, Reseaters O-Level, waliofeli Kidato cha Pili na Kidato cha nne. Kwa mawasiliano zaidi tutembelee Shuleni au piga simu 0767 307 607, 0783- 723 312 au 0652 010 136.

Pata elimu Bora kwa Gharama Nafuu.

SEKONDARI YA JIONI ( MESS)Inatangaza nafasi za masomo 2014

SHEIKH Farid Hadd kabla ya kuwekwa ndani.

Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU Mjini Mrogoro, wamelaani kitendo Cha Chama C h a C H A D E M A , k u v a m i a n a kulifanyia fujo gari lililokuwa likitangaza sherehe za Maulidi n a k u s a b a b i s h a k u s i t i s h w a k w a matangazo hayo.

Inaendelea Uk. 3

Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Philman

Mbowe.

SHEIKH Ilunga Kapungu.

2 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari

Jaji ataka sababu MasheikhUamsho kunyimwa dhamanaM A H A K A M A K u u ya Mjini Zanzibar i m e u t a k a u p a n d e w a m a s h i t a k a kuwasilisha vielelezo na maelezo ya ushahidi vitakavyotumika katika kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Vi e l e l e z o h i v y o ni kuwasil isha kwa m a a n d i s h i s a b a b u za kuzuiya dhamana ya viongozi hao 10 waliowekwa rumande kwa zaidi ya mwaka m m o j a s a s a t o k e a kufunguliwa mashitaka ya kutaka kuhatarisha hali ya amani nchini.

Jaji wa Mahkama hiyo, Fatma Hamid Mahmoud aliyasema hayo mahakamani hapo alipokuwa akiendesha kesi katika Mahakam k u u V u g a M j i n i Zanzibar.

“Kwa kuwa muda umeshakuwa mwingi, viongozi wa Uamsho w a m e k u w e p o k i z u w i z i n i , h i v y o n a o m b a n i p a t i w e sababu za maandishi za kuzuwia dhamana zao”. Alisema Jaji Fatma.

Hatua hiyo imefuatia baada ya mwendesha m a s h i t a k a w a Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Rashid Abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushaidi wa kesi hiyo tayari vimemeshakamil ika hivyo ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vielezo vya mashahidi.

Kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa wa kesi hiyo Abdal la Juma ameiomba mahakama hiyo kuzingatia madai ya upande wa utetezi kwa vile ushahidi wa kesi hiyo umekamilika hivyo ipangwe tarehe ya kusikilizwa na siku hiyo vielelezo viwasilishwe mahakamani hapo.

Hata hivyo upande

Na Alghaithiyyah Zanzibar

wa mashitaka haukuwa na pingamizi na ombi hilo na umedai kuwa unaiachia mahakama k u a m u a b a a d a y a kusikiliza pande zote mbili.

Watuhumiwa hao ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa Makadara n a A z z a n K h a l i d Hamdan (48) mkaazi wa Mfenesini. Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara.

Wengine ni Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, G h a l i b A h m a d a Juma (39) mkaazi wa M w a n a k w e r e k w e , Abdal lah Sa id (48 ) mkaazi wa Misufini na Fikirini Majaliwa Fikirini.

Wote kwa pamoja walisomewa mashitaka ya kuharibu mali za serikali na wananchi, Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo na kula njama ya kufanya kosa.

K o s a j e n g i n e

likimkabili mshitakiwa n a m b a n n e A z z a n K h a l i d H a m d a n ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa Kamishna wa Polisi vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Makosa hayo yanadaiwa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti katika manispaa ya mji wa Zanzibar na kusababisha taharuki kubwa nchini.

Jaji Fatma ameikhirisha kesi hiyo na kutaka upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo kabla ya Januar 31 mwaka huu.

Masheikh hao wapo ndani toka mwaka 2012, hii ikiwa na maana kuwa wamekula sherehe za ‘Mapinduzi Matukufu’ ya Zanzibar mara mbili wakiwa ndani.

Haya ni mapinduzi a mb a y o yamel e n g a k u w a w e k a h u r u Wazanzibari , kuleta utawala bora, utawala wa haki na sheria kwa wananchi wote ambapo mtu hataadhibiwa kwa tuhuma tu, ila mpaka sheria imtie hatiani.

SHEIKH Farid Hadd.

H I V I s a s a Masheikh kadhaa wanakabiliwa na kesi katika mahakama mbalimbali nchini.

Pamoja mashitaka m e n g i n e , l a k i n i sehemu kubwa ya watuhumiwa hawa w a m e f i k i s h w a mbele ya mahakama w a k i k a b i l i w a n a m a s h i t a k a ya uchochezi.

B a a d h i ya k e s i a m b a z o t a y a r i zipo mahakamani zinawahusu viongozi wa UAMSHO kule Zanz ibar , She ikh Ponda Issa Ponda, Iman Hamza kule mwanza na Sheikh Ilunga Hasan.

Hatuna tatizo kwa M a s h e i k h h a w a kufikishwa katika vyombo vya kisheria k a m a m a h a k a m a k w a t u h u m a zinazowakabili, ila ni matara j io yetu kwamba mahakama z e t u z i t a a c h w a huru na kuongozwa na uadilifu katika kushughulikia kesi za Masheikh hawa ili haki iweze kutendeka.

Wasiwasi wetu ni juu ya watu wengine ambao kwa namna moja au ny ingine wanaweza kuhusika n a m a k o s a y a uchochezi, hususan katika masuala ya kiimani, lakini hatuna taarifa za wahusika kuchukuliwa hatua, japo kukamatwa.

K w a m f a n o , wa k o wa p i wa l e w a n a o t u h u m i w a wa uchochezi wa kuchinja. Redio Kwa Neema, walikuwa

Tuwe makini katikakutekeleza sheria

m s t a r i wa m b e l e kueneza farka hii, labda tufahamishwe, wahusika wa Redio hii ambayo kwa kiasi kikubwa ilihusika na uchochezi huu wa kuchinja hadi maafa yakatokea wameishia wapi.

Tuhoji tu kwamba ni wangapi walikamatwa n a k u f i k i s h w a mahakamani kwa k u c h o m a m s i k i t i kule Tunduma katika kadhia hiyo hiyo ya kuchinja?

Kukosekana kwa taarifa za kukamatwa a u k u f i k i s h w a mahakamani kwa watu wa aina hii, ndiko kunakozua mashaka katika upande mmoja wa jamii, hususan katika mizozo hii ya kiimani.

Ni ushauri wetu kwamba, ili kujenga imani na kuondoa dhana mbaya juu ya vyombo vyetu v y a d o l a k a t i k a kuiendea haki, basi tunahitaji kusikia sasa kwamba, si Masheikh t u wa l i o f i k i s h wa m a h a k a n i k w a u c h o c h e z i , b a l i wapo hata Makasisi w a l i o f i k i s h w a mahakamani kwa kueneza uchochezi hususan katika sakata la kuchinja.

Tunafahamu fika kwamba faraka hii haikuanzishwa wala kupig iwa chapuo na Waislamu wala v i o n g o z i w a o . H a t a h i v y o , wa o n d i o w a m e k u w a waathirika wakubwa mbele ya vyombo vya dola. Hii si ishara nzuri huko mbeleni.

3 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Habari

CHADEMA wavuruga Maulidi MorogoroWA I S L A M U M j i n i Mrogoro , wamelaani kitendo Cha Chama Cha CHADEMA, kuvamia na kulifanyia fujo gari lililokuwa likitangaza sherehe za Maulidi na kusababisha kusitishwa kwa matangazo hayo.

Tukio hilo, limetokea, Jumapili ya wiki iliyopita, katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Boma Road, na kusababisha tafrani baina ya Waislamu na wafuasi hao wa CHADEMA, ambao walinusurika kipigo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, mmiliki wa gari hilo lenye namba za usaji l i T 677 AFG, Suzuki (Escudo), Bw. Isihaq Ramadhan Kambi, alisema ni kweli alivamiwa na wafuasi wa chama hicho kisha kumfanyia fujo na kusababisha upotevu wa kipaza sauti (microphone) chenye thamani ya zaidi ya Shilingi laki moja.

B w . K a m b i a l i d a i anawushukuru Waislamu ambao walifika katika eneo la tukio hilo kwa haraka na kumnusuru kabla wafuasi h a o wa C H A D E M A , hawajamdhuru .

“Wakati mimi natangaza sherehe za Maulidi ya Mfungo si ta , nikiwa katika gari langu wafuasi wa CHADEMA wakaja kunizuia kwa mbele na gari lao la M4C, likiwa limewasha taa kubwa, kisha walishuka na kuvamia gari yangu na kufungua mlango kwa nguvu huku wakilazimisha kuchomoa funguo za gari”. Alisema Bw. Kambi.

Alisema, akiwa katika mshangao, ghafla wengine walimpoka kipaza sauti kisha wal ikata nyaya z a s p i k a n a k u z u i a matangazo kwenda hewani akiwa maeneo ya hapo Msikitini, kitendo ambacho kimesababisha uharibifu katika vifaa vyake vya kurushia matangazo.

“Bahati nzuri tukio hilo la kuvamiwa na watu wa CHADEMA, lilifanyika jirani na Waislamu ambao k wa m u d a h u o n d i o walikuwa wateja wangu niliokuwa nawafanyia kazi yao baada ya kukodi gari langu kwa ajili ya shughuli yao ya Maulidi.

“Nashukuru walinihami kwa kiwango kikubwa l a k i n i l a u i n g e k u wa ni tofauti na pale hali kwangu na gar i kwa ujumla ingekuwa mbaya kwani jamaa walikusudia kunidhuru kabisa, jambo ambalo mpaka sasa nafsi

Na Bakari Mwakangwale yangu inaumia juu ya tukio hilo”. Alisema Bw. Kambi.

A l i s e m a , b a a d a ya tafrani hiyo, aliongozana na Waislamu chini ya Imamu wa Msikiti huo kuelekea kituo cha Polisi kutoa taarifa ili sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wafuasi hao wa CHADEMA.

Bw. Kambi alisema, walipofika katika geti la Polisi, waliwakuta wafuasi wale wa CHADEMA, nje na walipoona zile sura za Waislamu na lile gari walilolifanyia fujo pale Msikitini, waliwafuata na kuomba mazungumzo na kuahidi kulipa hicho kipaza sauti.

Bw. Kambi, alisema toka siku ya Jumapili walipotoa a h a d i h i y o m p a k a Jumatano (wiki hii) hakuna dalili zozote za jamaa hao kulipa kipaza sauti hicho kama walivyoahidi, ambapo yeye amedai kuwa ni sehemu ya kitendea kazi katika shughuli zake za matangazo.

“ L e o ( J u m a t a n o ) nimejaribu kuwatafuta ili niweze kuwauliza juu ya ahadi yao kwa maana kifaa hicho ni sehemu ya kazi zangu na kwa sasa zimesimama, nimeambiwa wameenda Tungi kurejesha fomu ya mgombea wao”. Alifafanua Bw. Kambi.

Alisema, kwa ujumla kitendo walichokifanya wafuasi hao wa Chadema, k i m e w a k a s i r i s h a Waislamu wengi Mjini hapo na wapenda amani kwa ujumla kwani alidai kitendo hicho kimeelezwa kuwa si cha Kidemokrasia.

Akielezea kilichopelekea wafuasi wa CHADEMA, kuvamia gari yake alisema, ni kutokana na gari hiyo kukodiwa na Chama cha Wananchi CUF, siku ya Jumapili i l iyopita, kuhamasisha urejeshaji wa fomu ya mgombea wao wa Udiwani Kata ya Tungi.

Bw. Kambi, alisema gari yake ikiwa mbele, nyuma yao kulikuwa na gari (Kosta) iliyobeba wafuasi wa CUF, ambapo walipofika maeneo ya N a n e n a n e i k a t o k e a kukwaruzana baina ya vipando vya wafuasi wa CUF na CHADEMA.

Al isema, gar i yake ililazimika kurudi nyuma katika eneo la tukio na kukuta fujo baina ya pande hizo mbili lakini alidai gari yake halikuhusika na fujo hizo zaidi ya kukodiwa kwa ajili ya hamasa.

“Waliponivamia pale Msikitini walidai kuwa wanalihitaji gari liende kituo cha Polisi, ambapo

Waislamu waliwahoji amri hiyo wanaitoa wao kama nani, wakaelezwa kama wanatuhuma yoyote na gari hilo, wanaofanya kazi za ukamataji ni Polisi, sio wao.

“Walihojiwa hatua ya kuzuia gari linalotangaza sherehe za Maulidi na kufanya fujo matokeo yake ni nini, wakawaeleza kama walifanyiwa vurugu na CUF, wao wanaofisi zao zinajulikana, lakini sio kuja hapa Msikitini na kufanya fujo”. Alisema akifafanua maelezo ya Waislamu kwa wafuasi wa CHADEMA.

Bw. Kambi, alisema kama wao walikuwa na nia ya kulikamata gari lake kutokana na ghasia baina yao na wenzao wa CUF, walitakiwa wafuate taratibu za kisheria kwani gari hiyo si ya chama (CUF), kuliko hatua waliyochukua ambayo inaweza kuleta maafa makubwa katika jamii wakati mwingine.

Alisema, gari yake ipo katika mfumo wa biashara wa matangazo na hana mtu mmoja anaye mtangazia, ni gari ambalo hukodishwa na watu, taasisi na makundi mbalimbali kwa ajili ya kurusha matangazo yao.

“Gari langu ni maarufu kwa kukodishwa kwa ajili ya matangazo mbalimbali, sibagui mteja wakiwemo watu wa mpira, siasa na hata mihadhara, lakini i n a c h o o n e k a n a w a o wa l i t e n g e n e z a c h u k i fulani ndio wakafikia kufanya hivyo.” Alisema Bw. Kambi, na kufafanua kuwa mpaka anavamiwa, hakuwa na taarifa zozote za Kipolisi, kama gari

yake inatakiwa Polisi au inatuhumiwa kwa makosa yoyote.

Akielezea tukio hilo, mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Dotto (AB) alisema, siku ya Jumapili ya wiki iliyopita, wafuasi wa CUF, walikuwa katika msafara wakielekea kwa Afisa Mtendaji kuchukua fomu ya mgombea wa Udiwani katika Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro, kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Diwani mteule.

Dotto, alisema wafuasi wa CUF, walipokuwa wanarudi na mgombea wao katika Ofisi zao za Kata, walikuta na watu wa CHADEMA, wakiwa katika gari moja na Pikipiki mbili.

“ K a t i k a h a l i i s i y o ya kawaida jamaa wa CHADEMA, waliigonga moja ya Pikipiki ya CUF zilizokuwa zimewabeba baadhi ya viongozi wao, akiwemo Mwenyekit i wa Jumuiya ya vijana ambaye ni mwanadada, katika maeneo ya Nane nane, majira ya saa nane mchana”. Alisema Dotto, na kuongeza

“Baada ya kutokea ajali hiyo, msafara ulisimama na palitokea tafrani baina ya pande hizo mbili yaani CUF na CHADEMA, kisha mzozo huo ulikwisha na kila upande ulitawanyika.”

A l i s e m a , w a f u a s i w a C U F , b a a d a y a kurudi katika ofisi zao, walitawanyika na kuachana na gari ambalo walikuwa wamelikodi katika msafara wao na kuingia katika

shughulizake zingine za kawaida.

Alisema, baada ya hapo, inasemekana BAKWATA , Mkoa waliikodi gari hiyo siku hiyo hiyo ya Jumapili (iliyopita) kwa ajili ya kuwatangazia Waislamu wa Manispaa ya Morogoro shughuli za Sherehe za Maulidi.

Imeelezwa kuwa wafuasi h a o wa C H A D E M A , wakiwa katika mitaa ya mjini, waliliona gari hilo na kuamua kulidhibiti likiwa jirani na Msikiti wa Boma road, likitangaza sherehe za Waislamu Maulidi.

Shuhuda huyo alisema, kwa kuwa muda u le Wa i s l a m u wa l i k u wa wakitoka Msikitini, baada ya swala ya Al-asir, walifika pale haraka wakitaharuki v ip i gar i ina tangaza sherehe za Maulidi watu wa Siasa (CHADEMA) wanaivamia na kufanyia fujo dereva na mtangazi.

Baada ya Waislamu kuhoji kulikoni na kupata maelezo, huku wafuasi wa CHADEMA, wakiitaka g a r i h i y o wa i p e l e k e Pol is i , Waislamu hao w a l i w a g o m e a k w a k u w a e l e z a k w a m b a hawawezi kuondoka na gari hilo kwa kuwa wao (Waislamu) wameikodi na kuwataka waondoke mara moja waende ofisi za CUF na si hapo Msikitini.

“ K u t o k a n a n a Waislamu kuwa wengi na kuwagomea wafuasi hao wa CHADEMA, waliamua kuingia katika gari yao na kuliacha gari hi lo huku Waislamu wakipiga Takbir”. Alifafanua Dotto.

RAIS mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kutoka kulia) akiwa na Masheikh wengine kwenye hafla ya Maulid Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Bw. Reginald Mengi.

4 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

A N T I - B A L A K A n i j ina la kikundi cha wapiganaji cha Kikristo k i l i c h o u n d wa h u k o J a m h u r i y a A f r i k a ya Kati baada ya Bw. Michel Djotodia kutwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi kutoka kwa Rais Francois Bozize.

J i n a A n t i - b a l a k a l inatokana na neno la jadi katika lugha za jamii ya watu wa Sango na Mandja, lenye maana ya mapambano dhidi ya upanga (anti-machete).

M i c h e l D j o t o d i a , amekuwa kiongozi wa muungano wa wapiganaji ambao wengi wao ni Waislamu waliofahamika kama Seleka, ambao ndio waliuondoa madarakani utawala wa Bw. Francois Bozize , baada ya mzozo mwezi Mach 2013.

Baada ya mapinduzi, D j o t o d i a a n a k u w a Kiongozi wa kwanza Muislamu kuiongoza nchi hiyo. Kwa miaka yote ya nyuma,Taifa hilo limekuwa ni milki ya utawala wa jamii ya Wakristo.

Septemba 2013 Michel Djotodia , a l i tangaza k u v u n j wa k u n d i l a Seleka li l i lomuingiza madarakani. Pamoja na kutoa tangazo hilo, wapiganaji zaidi wa Seleka wal igoma kuvun jwa kundi lao.

Kwa kiasi kikubwa ongezeko la machafuko Jamhuri ya Afrika ya Kati limetokana na vitendo vya kulipizana visasi kati ya waliokuwa wapiganaji wa k u n d i l a S e l e k a l i l i lovun jwa , amb ao kwa kiasi kikubwa ni Waislamu na wapiganaji wa Anti Balaka, ambao linaundwa na wapiganaji Wakristo.

M a p i g a n o h a y o yamesababisha mauaji ya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo mgogoro huo umechagizwa pia na mizozo ya ardhi, hasa ikizingatiwa kwamba jamii kubwa ya Waislamu n c h i n i h u m o , n i ya wafugaji na wahamaji huku jamii za Wakristo

Mafunzo kutoka anti bakala, SelekaYanayotokea ni zao la dhambi ya ubaguzi

Na Shaaban Rajab wakihodhi sehemu kubwa za ardhi.

Novemba 2013, Umoja wa Mataifa ulitoa tahadhari juu ya kuwepo hatari ya nchi hiyo kukumbwa na mauaji ya halaiki kufuatia kuwepo kila dalili ya kuibuka mzozo mkubwa nchini humo.

Ufaransa nayo ilielezea wasiwasi wake kwa nchi hiyo kuingia kwenye mauaji hayo ya halaiki.

Decemba 2 mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa ya serikali, wapiganaji wa anti-balaka walituhumiwa kuua watu 12 wakiwemo watoto, huku wengine wapatao 30 wakijeruhiwa katika shambulio kwenye eneo l inalokaliwa na Waislamu wengi wa jamii ya Peuhl katika mji wa Boali.

Mauaji haya yamekuja baada ya utawala wa Bw. Djotodia huko CAR kuingiza madarakani.

Kar ibu watu 1 ,000 waliuliwa katika siku mbili za mapigano nchini humo, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty.

Mauaji zaidi yalitokea Bangui Desemba 5 baada ya wapiganaji wa anti-balaka kusaka Waislamu mlango kwa mlango katika baadhi ya maeneo ya mji wa Bangui na kuua Waislamu wanaokadiriwa kufikia 60, imedhibitisha taarifa ya Amnesty.

Awali UN ilikadiria kuwa watu wapatao 450 wameuliwa mjini Bangui na wengine 150 katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

J a m h u r i ya A f r i k a ya Kati imeingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya Michel Djotodia, kupitia kundi la wapiganaji lenye Waislamu wengi la Seleka kuuangusha utawala wa Rais François Bozizé mwezi Machi mwaka jana.

Umoja wa Mata i fa u m e k a d i r i a k u w a kiasi cha watu 210,000 wamelazimika kukimbia makazi yao, hiyo ikiwa ni idadi katika Mji Mkuu Bangui pekee.

Moja ya miji mingine iliyoadhirika zaidi ni ule wa Bossangoa, uliopo

Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambao umebaki magofu, huku wakazi wake wakiishi katika hali ya wasiwasi kwenye makambi.

M a k a m b i h a y o yametengwa ya Wakristo n a Wa i s l a m u , h u k u kambi hizo zikipakana na uwanda wa eneo lisilomilikiwa na yeyote, ambalo wafanyakazi wa kutoa misaada pekee ndio wanaokatiza katika maeneo hayo ya mipaka ya kutenganisha makambi ya jamii hizo mbili.

Kwa jinsi hali ilivyo, kuna uwezekano mkubwa wa kufunguliwa kesi za jinai za kivita. Amnesty International wameandaa ripoti kufuatia uchunguzi wao wa wiki mbili wa kusaka ukweli huko CAR. Ripoti hiyo imeeleza kuwa makosa ya kivita yamefanywa na pande zote mbili za mzozo, kwa maana na Anti Balaka na Seleka.

" T h e i n f o r m a t i o n gathered has lef t no room for doubt that war crimes and crimes against h u m a n i t y a r e b e i n g committed by all parties to the conflict," alinukuliwa akisema Christian Mukosa, mtaalamu wa Amnesty International Afrika ya Kati.

U f a r a n s a t a y a r i imepeleka askari 1,600 katika nchi hiyo ambayo ilikuwa ni koloni lake zamani, ili kuungana na walinzi wa amani wa AU kujaribu kutuliza hali.

Hata hivyo Amnesty imesema kwamba pamoja na uingiliaji kati huo wa kigeni, raia wamezidi kuuliwa kila siku, ambapo inasadikiwa kuwa zaidi ya watu 90 waliuliwa tangu Desemba 8 mwaka jana.

Kutokana na ugumu w a l i o k a b i l i a n a n a o Ufaransa katika ulinzi wa amani katika nchi hiyo, imezitaka serikal i za nchi nyingine za Ulaya kuchangia jitihada zao kat ika operesheni za kijeshi ndani ya Afrika ya Kati.

Pamoja na wito huo, wakati Ujerumani na Uingereza zikitoa msaada w a v i f a a , U f a r a n s a imeendelea kubaki kuwa

nchi pekee ya Ulaya mpaka sasa, ambayo imepeleka vikosi vyake Afrika ya Kati.

Ripoti hiyo imeonya kwamba bila kuongezwa vikosi zaidi vya kigeni ku ing i l i a ka t i , kuna uwezekano wa kuibuka machafuko zaidi Jamhuri ya Kati.

Kutokana na kuendelea kuwepo viashiria vya hatari zaidi nchini humo, ripoti hiyo imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kutuliza hali nchini humo.

Wakati Ufaransa ikijitosa na kutaka washirika zaidi kuingia Afrika ya Kati kusaidia kutuliza hali, t u h u m a m b a l i m b a l i zimetolewa kwao kutoka kwa wenyeji.

Isa Hassan, Imam wa Masjid Al Noor uliopo katika eneo linaloitwa Kilometa 5 mjini Bangui, amesema kuwa askari wa Ufaransa wamewaua Waislamu watatu kwa kuwapiga risasi vichwani.

Kwa mujibu wa taarifa i l i y o p a t i k a n a W o r l d Bul let in , Imam huyo alisema Waislamu hao waliuliwa siku ya Jumapili ya Desemba 22, 20013.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Msikiti huo Yahiya Abu Bakr, naye alithibitisha mauaji hayo.

“ N i l i w a f u n i k a vichwani kwa mifuko ya plastiki baada ya wote kupigwa risasi vichwani” alinukuliwa Imam huyo.

Hata hivyo hakuna kamanda wala kiongozi ye y o t e wa U f a r a n s a aliyethibitisha au kutoa maelezo juu madai ya

mauaji hayo.Kufuatia hali hiyo,

waandamanaji walifunga barabara katika maeneo yenye Waislamu wengi mjini Bangui, wakipaza sauti za "Hollande is a criminal," wakimlenga Rais wa Ufaransa Francois Hollande.

Kufuatia hali hiyo askari wa Ufaransa walirusha mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji hao.

I m a n H a s s a n , amesema kuwa matatizo zaidi yal ianza baada ya askari wa Ufaransa kuingia nchini humo, ambapo walidai kuwa askari hao wamekuiwa wakiukandamiza zaidi umma wa Kiislamu.

"Tatizo lilianza muda mfupi baada ya wafaransa kuingiza nchini.

W a i s l a m u h a t u j a m s h a m b u l i a yeyote na kila mmoja ametulia, lakini Wafaransa wanawaandama Waislamu na kuruhusu wauliwe na makundi ya wahuni. Tatizo ni kwamba mara baada ya kuingia nchini wamekuwa wakipendelea” Alisema.

Nalo Shirika la Msalaba Mwekundu l imesema kuwa limegundua maiti zipatazo 40 katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika kati Bangui.

Kugunduliwa kwa maiti hizo, kumekuja baada ya mapigano, ambapo tayari imeripotiwa kuwa zaidi ya watu elfu moja w a m e u w a w a k a t i k a mapigano ya wiki tatu baina ya Wakristo na Waislamu.

Inaendelea Uk. 12

RAIS wa muda wa Afrika ya Kati aliyejiuzulu, Michel Djotodia.

5 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Habari za Kimataifa

Muislamu aliwa nyama CARRais Michel awakimbia ‘Seleka’

R A I S wa m u d a wa Afrika ya Kati, Michel Djotodia, amejiuzulu na kukimbilia Benin.

Djotodia alitangaza kujiuzulu kwake katika k i k a o c h a v i o n g o z i wa kanda (10-nation Economic Community of Central African States (Eccas)), kilichofanyika Chad Ijumaa iliyopita.

P a m o j a n a y e amejiuzulu pia aliyekuwa Waziri Mkuu, Nicolas Tiengaye.

B w a n a D j o t o d i a , a m b a ye n i R a i s wa k wa n z a M u i s l a m u , alitwaa madaraka mwaka jana Machi, 2013 baada ya kikundi chake cha waasi Seleka kutwaa mji mkuu Bangui na aliyekuwa Rais, Francois Bozize, kukimbia.

W a c h u n g u z i w a mambo wanasema kuwa hali ya Waislamu ni mbaya huenda kukawa na umwagikaji damu mkubwa zaidi kwa jinsi Wakristo walivyokuwa wakishangilia kung’oka k w a M i c h e l h u k u wakijiapiza kulipa kisasi.

Inaelezwa kuwa mamia kwa maelfu wa Wakristo wakazi wa mji mkuu Bangui walimwagika mitaani kushangilia mara baada ya kusikika habari za kuj iuzulu Bwana Djotodia na Waziri Mkuu Nicolas Tiengaye.

“ Wa n a o s h a n g i l i a kuondoka Mr Djotodia n i Wa k r i s t o p e k e e , w a k a t i W a i s l a m u wengi wamej i fungia majumbani”, aliripoti mpasha habari wa BBC, Pa u l W o o d k u t o k a Bangui.

Japo kunatolewa miito ya kuweka silaha chini na kurejesha hali ya amani baina ya Waislamu na Wa k r i s t o k a b l a y a kuibuka Seleka na anti-balaka, lakini bado wapo watu waliopania kulipiza kisasi.

" T o d a y , w e a r e g o i n g t o k i l l s o m e Musl ims" , anar ipot i Paul Wood akimnukuu mwandamanaji mmoja.

A n a s e m a , m a r a alipita mtu akiendesha gari akionekana kuwa Muislamu kwa kofia a l i y o k u wa a m e va a , akaponea chupuchupu baada ya kushambuliwa.

Wakiwa na mapanga, v i s u , m a r u n g u n a mikuki, anti-balaka wanaona hii ni fursa pekee ya kulipiza kisasi

Na Mwandishi Wetu

baada ya Rais kujiuzulu ambaye wanamtuhumu k u w a a l i k u w a a k i wa u n g a m k o n o S e l e k a wa l i o d a i wa kuuwa Wakristo.

Wakiwa wamevaa marundo ya hirizi, anti-balaka wanaamini kuwa hirizi hizo zinawakinga risasi zisiwapate.

Japo uvaaji wa hirizi na imani za namna h i y o h a z i k u b a l i k i katika Ukristo, lakini vijana na wapiganaji wa Kikristo, anti-balaka huvaa lundo la hirizi shingoni na moja ya vitu vinavyowekwa ndani ya hirizi hizo ni nyama za watu waliowauwa.

Inaelezwa kuwa japo nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa madini pamoja na miti ya mbao, lakini watu wamebaki wajinga kwa kuwa idadi

kubwa haqwasomi.N i k u t o k a n a n a

hali hiyo, imekuwa rahisi kutumbukizwa katika vurugu bila ya kutafakari wanapata nini na nini athari ya mambo wanayofanya.

Ni kutokana na ujinga huo pia, baadhi ya watu wamefikia hatua ya kula nyama ya binadamu mwenzao wakidai kuwa ni hasira ya kulipiza kisasi.

Katika tukio moja, kijana kutoka kundi la anti-balaka, alimuuwa M u i s l a m u n a k u l a mguu wake wote huku akitamba na kushangilia.

Shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Ghislein Nzoto, anasema kuwa mtu mmoja aliyekuwa ndani ya basi, alitolewa nje baada ya kutambulika

kuwa ni Muislamu.Vijana wapatao 20

wakaanza kumpiga mpaka akafa k isha wakamchoma moto.

A n a s e m a , k a n a kwamba hiyo haikutosha kutuliza chuki na hasira z a o , wa l i i k a t a k a t a maiti ndio mmoja wao akachukua mguu na kuanza kuula.

“I ate his leg, the whole thing right down to the bone - with bread. That's why people call me Mad Dog.”

Anasimulia kijana O u a n d j a M a g l o i r e aliyekula nyama ya Muislamu huku akijisifu mbele za kamera za waandishi wa habari kwa kujiita "Mad Dog", mbwa kichaa.

Tukio hilo lilifanyika mbele ya wanaoitwa walinzi wa amani, askari

kutoka Burundi ambapo mmoja wao alitapika kuona mtu akila nyama ya binadamu.

"This was right in front of the Burundian peacekeepers. One of the soldiers vomited. Then he chased people away with his gun." Anasimulia mpasha habari, Ghislein Nzoto.

A l i p o u l i z w a n a waandhsi wa habari ni kwa nini alifanya kitendo cha kishenzi kama kile cha kula nyama ya mtu, Ouand ja Maglo i re , alisema kuwa alikuwa ameapa kulipa kisasi kwa sababu Waislamu walikuwa wamemuuwa mke wake mjamzito, shemeji yake (sister-in-law) pamoja na mtoto wake mchanga.

Rekodi zinaonyesha kuwa, japo kulikuwa n a m a l a l a m i k o ya W a i s l a m u w a l i o wachache, kubaguliwa na maeneo yao kuachwa bi la ya maendeleo, lakini bado Waislamu na Wakristo waliishi pamoja kwa amani.

Lakini pia nchi hiyo imekuwa ya machafuko toka imepata uhuru kutoka kwa Ufaransa a m b a p o m a r a k a d h a a k u m e k u wa n a m a c h a f u k o n a kupinduliwa serikali.

Katika machafuko y a h i v i k a r i b u n i yaliyoongozwa na waasi wa Seleka, wanasiasa wa ndani na mataifa ya kibeberu kupitia vyombo vya habari na wapiganaji wa nje, wametumbukiza sumu ya chuki za kidini.

Wakristo na Waislamu wanauwana, lak in i hakuna hata mmoja wao mwenye agenda ya kidini.

WAKRISTO nchini Afrika ya Kati wakishangilia baada ya Rais Djotodia kuachia madaraka.

Ouandja Maglo i re aliyekula nyama ya Muislamu.

6 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

“Lau kama angalitoa Swadat (sadaka) ya vyote vilivyomo ardhini, asingefikia fadhila za wenziye waliokwenda (Jihad).”

Hadithi hii inatufunza kwamba kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni kule kumtii mara moja bila ya hiyari yale yote a l i y o t u a m r i s h a n a kuyatekeleza na sio kujidai kupenda na kufuata ili hali tumuhasi katikaAmri zake.

N a i m e p o k e w a na Anas ( Mwenyezi Mungu amuwiye radhi) kwamba Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“ H a w i m w e n y e kuamini mmoja wenu, mpaka niwe kipenzi zaidi kwake kuliko mwanae, mzazi wake, na watu wote.” (Bukhari na Muslim)

Imepokewa kwamba Omar b in khatwab (Mwenyez i Mungu a m u w i y e r a d h i ) amesema:

“ E we M t u m e wa M w e n y e z i M u n g u hakika wewe ni kipenzi kwangu kuliko chochote isipokuwa nafsi yangu.”

A k a s e m a M t u m e Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi kwake, mpaka niwe kipenzi zaidi kwako kuliko hata nafsi yako.”

Akasema Omar bin khatwab (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi): “Hakika kuanzia sasa hivi wewe ni kipenzi kwangu zaidi kuliko nafsi yangu.” Akasema Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Hivi sasa ewe Omar.” (Bukhari)

Aya pamoja na hadithi hizi zina tutufahamisha umuhimu na maana ya kupenda Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kwani upendo wa kweli wa kupenda ni kutii ujumbe aliokuja nao na kufuata kwa ukamilifu.

Kumuamini Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakuishii k w e n y e k u f u a t a mafundisho yake tu bali na kuiga tabia yake kwa kadiri ya kiwango

Namna ya kumpenda MtumeMFANO mzuri wa maana sahihi kupenda na kufuata Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) tunapata katika kisa mashuhuri cha Swahaba Abdullah bin Rawaaha (Mwenzi Mungu amuwiye Radhi) aliyetakiwa kwenda Jihad, lakini yeye akabaki nyuma, yaani hakutaka kwenda Vitani ili kusudi abakiye Maddina, apate kuswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipopata habari kuwa Swahaba wake huyo hakwenda vitani kusudi abaki na yeye kwa kule kumpenda kwake, basi Mtume akamwambia maneno haya;

cha ubinadamu na imani zetu tulizokuwa nazo. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakufanya jambo lake lolote katika maisha yake lilokuwa kinyume na ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na akawa amemridhia. Kwahivyo kila mwenye kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kitabia na mwenendo kwa “Ikhlis” atakuwa na uhakika wa kupata upendo na radhi ya Mwenyezi Mungu.

A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Ta’ala):

“ H a k i k a n y i n y i mnayo ruwaza njema k w a M t u m e w a M w e n y e z i M u n g u kwa anaye mtara j i M w e n y e z i M u n g u na Siku ya Mwisho, n a a k a m k u m b u k a M w e n y e z i M u n g u sana.” (Al ah’zab 33:21)

“Enyi mlio amini!

M t ' i i n i M w e n y e z i M u n g u , n a m t ' i i n i M t u m e , w a l a msiviharibu vitendo vyenu.” (Muh’ammad 47:33)

“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni m i m i , M w e n y e z i Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. (Al I’mran 3:31)

Imani ya kweli juu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni pamoja na kuridhia kwa moyo mkunjufu na hukumu yake katika kuwaamua waliogobana na kuridhika kwa moyo mkunjufu na uamuzi wake juu ya jambo lolote lile. Lakini ni masikitiko makubwa sana kati yetu Waislamu tunaodai k u m p e n d a M t u m e (Swalla Allaahu ‘alayhi

wa sallam) tunapo teta (kugombana) hatuwezi kukaa meza moja na kutafuta sulhu baina yetu, bali tunarejea k wa m a t wa a g h u u t ili kutuhukumu kwa wakati mwengine lipo kabisa ndani ya uwezo wetu kuweza kulipatia sulhu. Hali hii ni kwa watu wa mapote yote iwe ni wa Man-Haj ya Salafi au Masufi.

A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Ta’ala):

“ L a ! N a a p a k wa M o l a wa k o M l e z i ! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.’ (An Nisaai 4:65)

“Haiwi kwa Muumini m wa n a m u m e wa l a Muumini mwanamke kuwa na khiari katika j a m b o , M w e n y e z i

M u n g u n a M t u m e wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” (Al Ah’zab 33:36)

“ N a w a n a s e m a : T u m e m u a m i n i Mwenyezi Mungu na Mtume, na tumet'ii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini”.(An Nur 24:47)

“ N a wa n a p o i t wa kumuendea Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, kipo kikundi katika wao kinakataa.” (An Nur 24:48)

Hitimisho: Matatizo yote tunayoyapa kwenye mujitamaa wetu kisiasa, kiuchumi, kitamduni n . k . y a m e t o k a n a kutokuwa na mapenzi ya kweli ya kumpenda kwa kufuata Mtume Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika amri zake.

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi M u n g u n a M t u m e anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa M w e n y e z i M u n g u huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. (An Anfaal 8:24)

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. (An Anfaal 8:24)

Hivyo ili utukufu wa Uislamu na Waislamu uweze kurejea mahali pake, hakuna njia ya mkato , ba l i kupi ta pale walipopita wema waliotutangulia kwa kukandamiza nafsi zetu na kuwa tayari kugeuza nyendo zetu na kuwa na mapenzi ya kweli ya kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

WANAWAKE wa Kiislamu wakiwa katika sherehe za Maulid yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

7 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

Jiji la Colombo lilikuwa na ulinzi mkali ambao si jawahi kushuhudia katika maisha yangu. Kila baada ya hatua kumi kulikuwa na askari wenye silaha, mbwa, farasi na magari ya deraya. Askari w e n g i n e w a l i k u w a wamejificha kwenye viota maalumu kama ndege. Barabara nyingi za kuingia katikati ya jiji la Colombo zilikuwa zimefungwa.

Tulikuwa tukitumia m a b a s i m a a l u m u ( Y u t o n g ) , a m b a y o yalikuwa mapya kabisa, kwenda 'Media Centre' na kurudi hotelini, na msafara wetu ulikuwa ukiongozwa na afisa wa jeshi.

Baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola - CHOGM 2013, Novemba 15 mwaka 2013, ambayo nakumbuka ilikuwa Ijumaa, kulikuwa hakuna shughuli nyingi sana kwetu. Wakuu hao walikuwa na vikao vya ndani zaidi, ambavyo waandishi wa habari hawakuruhusiwa. Baada ya kutuma stori yangu ya ufunguzi, nikaamua kwenda kuswali Ijumaa kwenye msikiti mmoja ulio mbali kidogo.

Nilipoingia tu msikitini, w a u m i n i w a l i a n z a kunishangaa. Nilikuwa Mwafrika peke yangu. Nikaswali rakaa mbili za sunna na kisha kusubiri hotuba ya Ijumaa. Bado walikuwa wananishangaa m p a k a n i k a p a t a wasiwasi. Nikajiuliza moyoni wananionaje? Au wanadhani miye Gendaheka?

Baada ya Swala ya Ijumaa, kijana mmoja alinifuata, akanipa mkono na kunitolea salamu ya Kiis lamu. Nikai t ik ia kwa unyenyekevu sana. Akaniuliza: "Are you a Muslim?" Nikajibu "Yes". Akanikumbatia huku akisema "MashaAllah!"

Akaendelea kuuliza: "From Nigeria?" Nikajibu "No, Tanzania". Waumini w e n g i n e w a k a a n z a kusogea na kusikiliza. A k a w a a m b i a k i t u kwa lugha yao, miye nikaambulia maneno matatu tu "Muslima", "Afrika" na "Tanzania", mengine yote yakanipita.

B a a d a y a k u o n a

Safari yangu Sri Lanka-2HII ni sehemu ya pili ya makala ya mwandishi Said Rajabu juu ya safari yake Sri Lanka. Fuatana naye. Alhamisi, Novemba 14, mwaka 2013 ilikuwa ndiyo siku ambayo Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na mkewe, Mama Salma Kikwete, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali waliwasili jijini Colombo kwa ajili ya mkutano huo, ulioanza siku ya Ijumaa, Novemba 15 mwaka 2013. Prince Charles na mkewe, Camilla Perker Bowels pia waliwasili siku hiyo ya Alhamisi.

kitambulisho changu k i f u a n i , a k a n i u l i z a : "Have you come for the CHOGM Meeting?" Nikajibu "Yes". Akaniuliza maswali yale yale ambayo nimeulizwa na kila Msri Lanka niliyekutana naye tangu nifike. Alitaka kujua maoni yangu kuhusu nchi yao na ukarimu wa watu wake. Nikahisi alikuwa n i mtu wa ' sys tem' . N i k a m wa m b i a k a m a nilivyowaambia wengine wote. Naye akawaambia kwa lugha yao wale waumini waliotuzunguka pale msikitini.

N i l i p o g u n d u a yule ki jana, Fayrooz, anazungumza v izur i sana lugha ya Kiingereza, n a m i n i k a m u u l i z a maswali mbali kuhusu hali ya Waislamu nchini Sri Lanka na changamoto z i n a z o w a k a b i l i . A k a n i s i m u l i a k w a k i n a j i n s i Wa i s l a m u w a n a v y o b a g u l i w a , wanavyonyanyaswa na

changamoto nyingine nyingi zinazowakabili.

Nami nikamwambia ya kwangu. Tukajadili hal i ya Waislamu na Uislamu duniani. Fayrooz ana ufahamu mkubwa sana wa masuala hayo na amehifadhi Aya nyingi za Qur'an. Anazifahamu vizur i sana s iasa za ulimwengu na Waislamu.

Anaifafanua vyema vita dhidi ya "ugaidi" i l i y o a n z i s h w a n a Rais George Bush wa Marekani mwaka 2001. K a d r i t u l i v y o k u w a tukizungumza, Fayrooz a l i s h a n g a z w a s a n a na uwezo wangu wa kuchambua masuala hayo. Akaniambia:

" N d u g u y a n g u , sikutarajia kabisa kukutana na Muislamu anayetoka upande wenu wa Afrika, l a k i n i a n a z u n g u m z a Uislamu wa dunia nzima". Nikamwambia mimi ni mwandishi wa habari, na siku hizi dunia ni kama

kijiji. Siye tunajua madhila yanayowapata Waislamu duniani na yanatuuma sana.

Baada ya kuzungumza kwa muda mrefu, Fayrooz akanialika chakula cha m c h a n a n y u m b a n i k w a k e . N i k a m t a k a radhi na kumwambia i s ingewezekana kwa wakati ule, kwa sababu lazima nirudi 'Media Centre' ili kuona mambo y a n a v y o k w e n d a . A k a n i e l e w a , l a k i n i akaniomba sana tuwe pamoja kwenye chakula cha jioni nyumbani kwake. Alitaka kunikutanisha na familia yake. Nikashindwa kabisa kukataa. Nilijisikia vibaya sana kukataa kwa jinsi alivyoniomba.

Akaniambia yeye ni mfanyabiashara na ana duka kubwa la vito vya thamani (sonara) kati kati ya jiji la Colombo. Ameoa na ana watoto watatu na anaishi na mama yake nyumbani kwake.

Aliniuliza kama nina usafiri wa kwenda 'Media Centre' au anipeleke kwa gari yake, nikwambia ninao na nikamshukuru sana. Baada ya kuomba dua na kupeana mikono na waumini waliokuwa wakitusikiliza, tukaagana na nikamwambia anifuate hoteli ya Colombo City baada ya magharibi.

Fayrooz alikuja kama ilivyokuwa miadi yetu, na baada ya kuswali maghar ib i , tukaanza kuelekea nyumbani kwake. Ni mwendo kidogo kutoka pale Colombo City Hotel na inaonekana ni eneo la watu wenye uwezo. Nyumba yake ni kubwa sana na ina mandhari nzuri. Nikakaribishwa sebuleni kwa bashasha. Mke wake, Shahnaz, na watoto wake wakaja kunisalimia. Shahnaz pia anazungumza vizuri Kiingereza.

Tumezungumza mambo m e n g i s a n a k u h u s u utandawazi, malezi ya watoto, siasa, uchumi, vita dhidi ya Uislamu na hata michezo.Watu wa kule wanapenda sana Kriketi. Tukapata chakula cha jioni kizito kwelikweli - ila pilipili siwezi kusahau. Mpaka machozi yalinitoka! Tumezungumza mpaka saa tano usiku. Fayrooz akanipa zawadi ya jiwe la thamani , l ina i twa 'moonstone' kwa ajili ya kutengeneza pete ya mke wangu.

Aliniuliza jina lake na tarehe yake ya kuzaliwa, n i k a m t a j i a , k i s h a akanichagulia jiwe liwe kutoka kwenye mawe m e n g i . A m e n i a m b i a lile ni j iwe la bahati. Nikashukuru sana kwa niaba ya mke wangu, na nikampigia simu pale pale kupitia Et-salat, lakini kwa bahati mbaya simu yake ilikuwa inaita bila ya kupokelewa.

Baada ya usiku mwingi k u f i k a , n i k a wa o m b a ruhusa, nikawashukuru kwa ukarimu wao na nikawaambia, Fayrooz na mkewe Shahnaz, kwamba sitakuja kuwasahau katika maisha yangu yote. Nao wakaniambia maneno hayohayo. Tukaomba dua na kuagana. Shahnaz aliniomba sana nirudi tena Colombo nikiwa na mke wangu, nikamwambia InshaAllah siku moja nitakuja naye.

WAISLAMU wakiwa kwenye Zaffa ya Maulid jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

8 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

KATIKA ulimwengu wa sasa wa vita kati ya Uislamu

na ‘utwaghuti’, kuna m i s a m i a t i a m b a y o hapana budi Waislamu waifahamu vizuri. Lakini pia inabidi ufahamu wao wa mambo uwe wa hali ya juu sana kwani kuna hatari ya kujikuta wanatumiwa kujiangamiza wenyewe w a k i p i g a n a v i t a isiyokuwa ya kwao.

Kuna kitu kinaitwa proxy war. Wiki iliyopita iliripotiwa kuwa wale wapiganaji wa Kiislamu walioingia katika vita ya kumng’oa Muammar Gadhaf i kwa j ina la U i s l a m u / J i h a d , k wa maana kuwa walidhani na kuamini kuwa wanashiriki vita kuondoa utawala usio wa Kiislamu ili wasimike m f u m o w a m a i s h a ya Kiislamu; hivi sasa wanajikusanya kuingia kupigana Syria. Msukumo ni ule ule. Wanaamini kwamba wanakwenda kufanya Jihad.

Mmoja wa makamanda hao ambao kikosi chake kilikuwa cha kwanza kuingia Tripol wakati wa vita Libya, anayetambulika kwa jina la Al-Mahdi al-Harati, anasema kuwa wao wamekuwa ni jeshi la kimataifa la Kiislamu. Kila panapotokea haja ya kwenda kupigana, wanakwenda. Kwa hiyo kwa kutumia uzoefu wa L i b ya , h i v i s a s a w a n a k w e n d a k u t o a mchango wake Syria.

Mpiganaji mwingine ambaye ka j i ta ja kwa jina moja la Mohammed anasema kuwa baada ya kumaliza kazi Libya, sasa anakwenda Syria k u u n g a n a n a wa a s i wanaotaka kumng’oa Rais Bashar.

Mohammed, mwenye u m r i wa m i a k a 2 3 , anasema asingependa kutaja jina lake la pili kwa sababu hataki watu wa familia yake wajue yupo wapi na kwamba anakwenda kupigana Syria. Hata hivyo anasema kuwa anahisi ana wajibu wa kwenda kuwakomboa watu wa Syria.

"What Bashar al-Assad is doing is unacceptable in Islam ... He is killing children and wiping out entire cities ... The Syrians need people to fight with them, this is Jihad, it does not have to be my (personal) cause ... As a Muslim I have to go and help them".

Tumekuwa wakala mzuri wa 'Proxy War' !

Hatufikiri, hatuzingatii, hatufahamu!

Na Omar Msangi

MAJESHI ya kigeni yakiwa nchini Libya.

H i v i n d i v y o anavyosema Mohammed kama alivyonukuliwa na

vyombo vya habari. Yeye ameridhika kuwa Syria kuna Jihad, na msingi

wenyewe ni kuwa Rais Bashar al-Assad anauwa watoto na kuangamiza

m i j i . N a ye ye k a m a Muislamu ni lazima aende Jihad.

Mgogoro hapa haupo katika kutizama ubaya au uzuri wa Bashar. Lakini nadhani, ingekuwa jambo la busara kama wapiganaji h a w a w a n g e t i z a m a k w a n z a k a m a k i l e walichokipigania Libya, k imepat ikana? Kama hakijapatikana, kwa nini? Kwa kufanya tathmini hii itasaidia hata wanapoingia S y r i a , wa j u e v i z u r i wanachopigania, kama watakipata au la.

Kwa Libya, hakuna walichopata waasi na ‘mujahidina’ na hakuna walichopata wananchi wa Libya. Wal iopata n i m a t w a g h u t i . Waliopata ni mabeberu. Wameiparaganya nchi w a n a v u n a m a f u t a w a t a k a v y o , h a k u n a s e r i k a l i m a d h u b u t i , makachero wa mabeberu wamejaa katika nchi na wanaingia na kutoka bila kutafuta kibali kwa yoyote katika serikali . Rejea walivyoingia na kumteka mmoja wa makamanda wa ‘mujahidina’ waliopigana k u m n g ’ o a G a d h a f i , wakatokomea naye bila kutaka ridhaa ya serikali ya Libya.

Makundi ya waas i yamebaki na silaha huku wakiwa wamenyimwa serikali. Tafsiri yake ni kuwa hakuna amani tena iliyokuwepo hapo a wa l i . K u u wa n a n a uasi , utakuwa jambo la kawaida Libya. Wiki iliyopita Waziri mdogo wa Viwanda Hassan al-Droui amemimin iwa risasi na kuuliwa. Kisa nini? Haijulikani. Lakini zipo taarifa kuwa wale Mujahidina waliopigana kumuondoa Gadhafi wana hasira. Wanasema, serikali imefuja na haithamini k a z i i l i y o f a n y wa n a ‘Mashaheed’ waliokufa katika vita. Kwa hiyo wanaigeuzi silaha serikali.

Lakin i wakat i huo huo, Waziri Mkuu Ali Zidan anasema, kamwe serikali haitayumbishwa na wanaharakati hao, aliowaita ‘Salafist Islamist militias’.

Yale mapato kutoka pato la mafuta ambapo wa n a n c h i wa l i k u wa wakipewa nyumba, elimu na huduma mbalimbali za kijamii bure, sasa itakuwa historia.

Sasa ukifanya tathmini ya kutosha utaona kuwa wa a s i n a wa l i o j i i t a ‘Mujahidina’, kwa Libya

Hakuna wa kuishinda Al Shabaab kwa sasa

Watasingiziwa hata wasipohusika

Inaendelea Uk. 9

IPO taarifa na uchambuzi wa matukio ya kigaidi y a l i y o t o k e a K e n y a ambayo unaweza kusema ni muhimu kwa Waislamu kuisoma na kuielewa. Taarifa hiyo inasema:

“Kenya for the third time becomes the scene of yet another “False Flag.”” (TRUTHERSEPTEMBER 24, 2013).

Kama sehemu utangulizi wake inasema, ”…the US Navy Seal Team Six were knocked off in a Chinook accident in Afghanistan….why?….because they never killed Bin Laden in North Pakistan last year as he had already died on the 14th of

Na Omar Msangi December 2001 from kidney failure!!!”

U f u p i wa m a n e n o anachosisitiza ni kuwa u l i m w e n g u w a l e o u m e k u wa wa h a d a a nyingi na hasa katika hii inayoitwa vita dhidi y a u g a i d i . N a k w a hiyo watu wanatakiwa kuwa makini . Akitoa mfano anahoji lile tukio lililodaiwa kuwa kikosi maalum cha Marekani kilivamia nyumba moja na kumuuwa Osama Bin Laden mwaka juzi 2012. Kwa maelezo yake, tukio lile lilikuwa mchezo wa kuigiza kwa vile Osama alishafariki toka miaka 10 iliyopita kutokana na

maradhi ya figo.A n a s e m a , k w a

bahati mbaya hata wale waliodaiwa kuhusika kat ika uvamiz i huo , walikufa wote kutokana na kilichoitwa ‘ajali ya helkopta’.

A k i z u n g u m z i a kulipuliwa kwa hoteli ya kitalii, Hotel Paradise M o m b a s s a , m w a k a 2002 inayomilikiwa na Muisrael, anasema hapo napo panahitaji watu kutafakari ili waone siri iliyojificha.

P a m o j a n a kushambuliwa hoteli hiyo, ilidaiwa kuwa kwa

Inaendelea Uk. 9

9 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

Tumekuwa wakala mzuri wa 'Proxy War' !Inatoka Uk. 8

walitumiwa kupigana ‘Proxy War’ ya mabeberu. Walipigana kama wakala wa mabeberu ambao walitaka kumwondoa G a d h a f i . M a z i n g i r a yalitengenezwa kwa waasi wakaona wanapigania haki zao kumwondoa dikiteta. Kwa ‘Mujahidina’ nao wakatengenezewa m a z i n g i r a , wa k a o n a kupambana na Gadhafi ni Jihad. Wakapewa misaada ya kila aina. Wakipigana ardhini, ndege za NATO zinamshambulia Gadhafi kutoka angani. Kazi ikawa nyepesi kabisa.

K u m b e m a h e s a b u hayakuwa rahisi kiasi hicho. Wametumiwa, wameuwa mamia kwa maelfu ya wananchi na Wais lamu wa Libya , wamehar ibu mi j i na miundo mbinu; na hakuna walichovuna zaidi ya kuwatumbukiza Walibya katika machafuko na dhiki ya muda mrefu. Hiyo ndiyo proxy war.

S a s a k a m a ninavyojitahidi kuweka wazi mara kwa mara, hoja hapa sio kuhoji Jihad wala kumuunga mkono Gadhafi au Bashar, hoja ni kuchukua tahadhari tusiingizwe katika hizi proxy war za mabeberu. Kama tunaingia, tujue wanachopanga huko m b e l e n i n a k u p i g a hesabu vizuri namna ya kukabiliana nacho.

K w a m a a n a h i y o , nadhani ingekuwa vyema kwa Mujahidina kufanya k wa n z a t a t h m i n i ya yaliyojiri Libya na kisha kusoma vizuri siasa za Syria, Mashariki ya Kati na inachotaka Marekani na Israel katika eneo hilo. Suala hapa ni kuwa ‘ M u j a h i d i n a ’ wa s i j e wakajitosa, wakaangamiza watu, kumbe mwisho wa yote wanapigana proxy war ya Marekani na Israel.

Z i p o t a a r i f a ( G u l f Today) kuwa makamanda wa wapiganaji kutoka Islamic Front, ambao kwa siku za hivi karibuni walipambana na kuteka baadhi ya miji iliyokuwa ikishikiliwa na waasi wengine wa Syria, Free Syrian Army, watakutana na maofisa wa Marekani nchini Uturuki.

M k u t a n o h u u k a t i y a Wa s h i n g t o n n a Islamic Front alliance, unadhihirisha jambo moja: Kwamba wanaotafuta watu wa kupigana proxy war katika Syria, wameona kuwa Free Syrian Army

b r i g a d e s , h a wa we z i k u f a n i k i s h a k a z i ya kupambana na jeshi la Bashar. Mchezo sasa ni

kuwatumia Mujahidina.K w a m u j i b u w a

tafiti mbalimbali, vita inayoendelea Syria hivi

sasa , i l ipangwa toka mwaka 2007 ambapo Tony Cartalucci anasema kuwa huo ndio mwaka

ilifichuliwa kuwa:“US, Israel, and Saudi

Arabia were planning on building up extremists w i t h i n a n d a r o u n d Syria for the purpose of eventually overthrowing the government.”

Akielezea jambo hili m wa n d i s h i S e y m o u r Hersh anasema kuwa moja ya malengo ya mradi huo ni kuidhoofisha Iran, ambayo inaongozwa na itikadi ya Kishia. Syria inaonekana i k i b a k i m a d h u b u t i n a i k i s h i k a m a n a n a Iran, zitafanya nguvu inayotishia Israel, lakini pia wakiungana na Hizbulla kule Lebanon, watajenga nguvu zaidi itakayotishia ‘uhai’ wa nchi nyingine za Kiarabu zinazotumiwa k a m a v i b a r a k a w a Marekani. Mwisho wa yote ni udhibiti wa mafuta na nafasi ya Israel katika Mashariki ya Kati.

Katika kutimiza lengo hili, mabeberu wameona watu wa kuwatumia ni ‘Sunni’ hata kama watakuwa Mujahidina au magaidi kwa lugha yao. Kwa Waarabu, hasa Saudi Arabi na Qatar, wao wamefanywa waamini kuwa ni vita dhidi ya Shia Iran na vita dhidi ya Shia wa Alawites kwa Bashar.

Kwa namna hii, Saudi Arabi inafanya kazi kubwa kutoa kila aina ya msaada kuhakikisha kuwa Bashar anaondoka.

Kwa wapiganaji wa kigeni kama yule kijana wetu Mohammed wa Libya, yeye anaona kuwa ni Jihad. Lakini ukweli ni kuwa wote hawa, Saudi Arabia na makundi haya ya Jihad ikiwemo al-Nusrah Front, wanapigana proxy war ya mabeberu na Israel.

Yupo msomaji mmoja alituma ujumbe kwa njia ya simu akisema kuwa kinachoendelea Syria, ni Jihad ya kuondoa Mashia na kusimamisha Khilafah. Hii ni kuoneshan kuwa wa l i o p a n g a v i t a h i i (regional "sub-imperialist" project), wanajua vizuri namna ya kucheza na akili za Waislamu.

T u n a c h o t a k i w a kufahamu hapa ni kuwa hii ni vita ya wenyewe kwa wenyewe-wa-Syria kwa wa-Syria, hii ni vita ya wenyewe kwa wenyewe Waislamu kwa Waislamu, hii vi vita ya wenyewe kwa wenyewe-Waarabu kwa Waarabu. Mwisho wa yote, watadhoofishana, itabakia vurugu.

Hakuna wa kuishinda Al Shabaab kwa sasaInatoka Uk. 8IPO taarifa na uchambuzi wa matukio ya kigaidi y a l i y o t o k e a K e n y a ambayo unaweza kusema ni muhimu kwa Waislamu kuisoma na kuielewa. Taarifa hiyo inasema:

“Kenya for the third time becomes the scene of yet another “False Flag.”” (TRUTHERSEPTEMBER 24, 2013).

Kama sehemu utangulizi wake inasema, ”…the US Navy Seal Team Six were knocked off in a Chinook accident in Afghanistan….why?….because they never killed Bin Laden in North Pakistan last year as he had already died on the 14th of December 2001 from kidney failure!!!”

U f u p i wa m a n e n o anachosisitiza ni kuwa u l i m w e n g u w a l e o u m e k u wa wa h a d a a nyingi na hasa katika hii inayoitwa vita dhidi y a u g a i d i . N a k w a hiyo watu wanatakiwa kuwa makini . Akitoa mfano anahoji lile tukio lililodaiwa kuwa kikosi

maalum cha Marekani kilivamia nyumba moja na kumuuwa Osama Bin Laden mwaka juzi 2012. Kwa maelezo yake, tukio lile lilikuwa mchezo wa kuigiza kwa vile Osama alishafariki toka miaka 10 iliyopita kutokana na maradhi ya figo.

A n a s e m a , k w a bahati mbaya hata wale waliodaiwa kuhusika ka t ika uvamiz i huo , walikufa wote kutokana na kilichoitwa ‘ajali ya helkopta’.

A k i z u n g u m z i a kulipuliwa kwa hoteli ya kitalii, Hotel Paradise M o m b a s s a , m w a k a 2002 inayomilikiwa na Muisrael, anasema hapo napo panahitaji watu kutafakari ili waone siri iliyojificha.

P a m o j a n a kushambuliwa hotel i hiyo, ilidaiwa kuwa kwa wakati huo huo mmoja, ndege ya abiria ya Israel, Arkia Airlines Boeing 757, nayo ilikoswakoswa kwa kombora wakati ikiruka katika uwanja wa Ndege

Mombasa kuelekea Tel Aviv.

Kama ilivyo kawaida, haraka haraka ikadaiwa kuwa wahusika ni magaidi wa Al Qaida. Waislamu!!!

Lakini katika uchambuzi wake makala hiyo inasema kuwa zipo ishara na ushahidi mwingi kuwa jambo hilo lilikuwa la kupangwa.

“The first proof that the Kikambala Beach operation was a covert Israeli sting, came less than an hour after the massive bomb blast, with a tame television anchorman in New York repeatedly asking a reporter at the Paradise hotel about “the other attack on the Israeli airliner taking off from Mombasa.” The timing of these questions was impossible, because the pilots aboard the Arkia Airlines Boeing 757 had not reported any incident. Serving as proof of this critical omission, there is no record of any “Mayday” or “Pan” call on the Kenyan air traffic control tapes at any time on 28 November 2002. So

Inaendelea Uk. 11Inaendelea Uk. 11

HALI ya maangamizi Syria kutokana na vita.

10 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

KWA maana hii, Uislamu ni dini ya ulimwengu, a m b a y o k w a n z a inayaangalia masuala ya kilimwengu ya binadamu. Maisha baada ya kifo, ni mwendelezo tu wa maisha ya ulimwengu. Ni vigumu kufikiria kwamba mtu anaweza kupata mafanikio ya Akhira, bila ya kunusuriwa kwanza hapa duniani.

Njia bora ya kufuata ni ile tuliyoonyeshwa na Mtume Muhammad (saw). Mke wake, Aisha alipoulizwa na sahaba kuhusu tabia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, alijibu tabia yake ni Qur'an. Sasa Qur'an ni muongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ndiye aliyepewa mamlaka na Mwenyezi Mungu kuitafsiri.

Hiyo ndiyo sababu tabia yake ni ya kupigiwa mfano kwa binadamu wote . Uis lamu kama u l i v y o f u n d i s h wa n a Mtume Muhammad (saw), umeeleweka vibaya sana kwa baadhi ya Waislamu, ambao hudhani dini hii ni ya vitendo vya ibada tu kama swala, funga, kutoa zaka, kwenda hija, ndoa na talaka.

Angalau katika miaka ya hivi karibuni, kufuatia maendeleo ya kiteknolojia duniani, Uislamu umeanza kuangaliwa kwa mtazamo mpana za id i , ku l iko ilivyokuwa awali. Hamasa ya kuusoma Uislamu, kwa Waislamu na wasio Waislamu, imeongezeka sana na kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukuaji wa teknolojia za uchapaji, habari na mawasiliano.

M a e n d e l e o h a y a ya m e a n z a k u f u n g u a macho ya watu wengi ulimwenguni kuhusu mafundisho sahihi ya Uislamu na misingi yake ya ndani, katika nyanja mbalimbali. Tukielekea maadhimisho ya kuzaliwa M t u m e M u h a m m a d ( s a w ) , n i v y e m a t u k a a n g a z i a m a e n e o machache ya ki jamii , kama yalivyofafanuliwa n a U i s l a m u , k u p i t i a mafundisho ya Mtume. Yeye ndiye mwalimu mkuu wa Uislamu wote tunaoufahamu leo.

Uchumi - katika nyanja ya maendeleo ya kiuchumi, lengo siyo kupata mali, bali ustawi wa maisha ya binadamu kwa ujumla. Uislamu unasisitiza haja ya kuweka mizania sawa kati ya mahitaji ya mali na mwili, mahitaji ya mtu binafsi na ya jamii, ili kupunguza pengo la pande hizo mbili za ulimwengu wa binadamu.

Imeelezwa ndani ya Qur'an: Sema. "Ni nani

M u h a m m a d n d i y o muongozo wa kufuata

Na Said Rajab

MUHAMMAD kama binadamu, tayari ameshakufa siku nyingi, lakini kama Mtume ametuachia urithi wa Qur'an na Sunna. Mtume alisisitiza sana haja ya Waislamu kushikamana na viwili hivi katika hotuba yake ya kuaga pale vilima vya Arafat. Iwapo Waislamu duniani, watashikamana na viwili hivi, kamwe hawatapotea. Mafundisho aliyotuachia Mtume, iwapo yatawekwa katika vitendo, kwa uhalisia na usahihi wake, yatatuletea furaha katika maisha yetu ya dunia na malipo mema baada ya kifo.

aliyeharimisha mapambo ya Mwenyezi Mungu a m b a y o a m e wa t o l e a waja wake . Na nani a l i y e h a r i m i s h a v i t u vizuri katika vyakula?" S e m a : ? " Vi t u h i v y o vimewahalalikia Waislamu (hapa) katika maisha ya dunia; na vitakuwa vyao peke yao siku ya Kiyama ...Sema, "Mola wangu ameharimisha mambo machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika, Qur(7:33).

Kwa hiyo kila mmoja y u k o h u r u k u f a n ya biashara yoyote halali anayoipenda, ili mradi tu azingat ie maonyo ya Mwenyezi Mungu. Iwapo atapuuza onyo la Mwenyezi Mungu, atapata matatizo. Biashara yoyote bora isiyo na madhara na inayofanywa kwa uadilifu inakubaliwa na Uislamu.

M t u m e m we n ye we alikuwa mfanyabiashara kabla hajateuliwa kuwa Mtume. Uwezo wake wa kuendesha biashara kwa umahiri wa hali ya juu, ukweli na uaminifu wake katika shughuli za kibiashara, vilimvutia sana mwajiri wake, bibi Khadija, ambaye baadaye alimuomba Mtume amuoe.

M t u m e a l i w a t a k a W a i s l a m u k u f u a t a

nyayo za Nabii Daudi za kufanyakazi kwa bidii, na kuishi kutokana na jasho lake mwenyewe. Pia alisema imani ya Muislamu haikamiliki iwapo atazembea katika taaluma yake.

A l i s e m a : " U k i a c h a mambo kwa wasio na ujuzi, basi usubiri maafa".

Iwapo unafanyakazi k w e n y e s e k t a y a uzalishaji, basi bidhaa zako lazima zilingane na zile zinazotoka kwenye viwanda au makampuni mengine.

I l i kupata masoko, lazima bidhaa zikidhi vionjo vya wanunuzi na viwango vyao vya k u i s h i . K a t i k a h i l i , Uislamu unakataza kabisa kudanganya wakati wa kuingiza bidhaa sokoni. Lazima bidhaa ionyeshwe k a m a i l i v y o b i l a ya kupewa sifa isizostahili kupitia matangazo au promosheni.

Wakat i wa k ipindi cha Mtume, alikutana n a m a m b o m e n g i sokoni ambapo baadhi ya wa f a n ya b i a s h a r a walijaribu kuwadanganya wateja. Mtume aliwaambia:

"Yeyote anayedanganya s i m i o n g o n i m w e t u Waislamu".

U i s l a m u u m e we k a kanuni na taratibu nyingi katika nyanja ya uchumi, kwa mfano biashara, ukodishaji, mihamala, mikataba na nyinginezo, ili kuepuka udanganyifu.

Uislamu pia umekataza ukiritimba na unyonyaji wa mtu mmoja au kundi moja la watu kwa gharama ya wengine.

Usafi - Kitu cha kwanza kabisa kwenye mafundisho ya dini i l iyoletwa na M t u m e M u h a m m a d (saw) ni kujali usafi . Dhana ya usafi katika Uislamu inakusanya usafi wa kimwili na kiroho, usafi kwenye masuala ya kidunia na kidini pia. Kabla ya kufanya ibada y o y o t e i l i y o a n i s h wa k w e n y e U i s l a m u , muumini lazima asafishe mwili wake, nguo zake, mahali pake pa kufanyia ibada na mazingira yake pia lazima yawe safi.

K a b l a y a k u a n z a Swala au Ibada ya Hija, Muislamu lazima achukue udhu kwanza. Au kama atakuwa kwenye dharura ya janaba au kumaliza hedhi, au damu ya uzazi, lazima aoge mwili mzima kwa kutumia maji safi. Kwa swala za kila siku, kila Muislamu lazima asafishe

viungo vyake mara tano. Hii pia inamkumbusha kuifanya roho yake kuwa safi kutokana na vitendo vyote vinavyomchukiza Mwenyezi Mungu.

Usafi hauna maana ya kimwili na kimaumbile peke yake. Mwili pia lazima utoharishwe na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuharibu uhusiano mzuri na binadamu wengine au Mwenyezi Mungu. Lazima Muislamu asafishe mawazo yake kutokana na dhamira chafu ya kufanya maovu. Lazima asafishe moyo wake kutokana na gere, husuda, unafiki, chuki na mambo mengine kama hayo. Aingize moyoni mwake, matumaini, ukweli, msamaha, huruma, udugu na upendo.

Muislamu pia anatakiwa kuwa makini na mlo wake dhidi ya vyakula vyote hatari kiafya na kidini. Lazima macho yake, masikio yake na ulimi wake vijiepushe na maovu. Hizi ni miongoni mwa tabia njema zilizofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w), tunayemuadhimisha leo.

Katika kusafisha mali, Uislamu umeweka mfumo wa zaka. Muislamu ambaye mali yake imefikia kiwango fulani, anawajibika kutoa zaka. Ni wajibu ambao umewekwa na Mwenyezi Mungu na kutekelezwa na Waislamu kwa manufaa ya jamii kwa ujumla.

Na wale wenye uwezo mdogo, ambao mali yao haijafikia kiwango cha kutoa zaka, anaweza kutoa tu kama sadaka kwa wale wenye kuhitaji. Hii haina maana kwamba wale wenye kuhitaji ndiyo wawe wapokeaji tu wa misaada.

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Mkono unaotoa ni bora zaidi kuliko mkono unaopokea".

Iwapo mpokeaji wa zaka atazingatia kauli hii ya Mtume, basi atajitahidi kwa kadri ya uwezo wake, ili naye awe mtoaji wa zaka, badala ya kuwa mpokeaji kila siku. Atarekebisha maisha yake kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu.

Katika Uislamu, kumiliki mali nyingi hakuongezi heshima ya mtu, wala umasikini haudhalilishi utu wake. Kweli mali ni muhimu kwa maisha ya binadamu, lakini mali ni njia tu ya kupitia, siyo lengo kuu la maisha ya hapa duniani.

Moja ya mafundisho mazuri ya Uislamu ni amri ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Mema yadumishwe na mabaya yatupwe. Kwa ufupi, U i s l a m u u m e j e n g wa k a t i k a m l o l o n g o wa maamrisho na makatazo. Maamrisho na makatazo hayo yamewekwa kwa manufaa ya binadamu hapa duniani.

Itaendelea toleo lijalo

RAIS mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiwa na Masheikh wengine kwenye hafla ya Maulid Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto kwake ni Bw. Reginald Mengi akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Bw. Said Meck Sadick.

11 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014Makala

Kiasi wiki mbili zilizopita nilihudhuria semina moja juu ya elimu. Mtaalamu mmoja kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akaarifu kuwa katika kukabiliana na changamoto za “Big Result Now (BRN)”, Wakristo kwa ujumla wao, bila kujali Sabato, Katoliki, KKKT, Anglikana n.k, wameomba wataalamu kutoka Wizara ya Elimu wapewe wataalamu wa kuwafunda walimu na wasimamizi wa taasisi zao za elimu kwa pamoja ili kwenda na changamoto za BRN.

Israel si Wakristo na hawaukubali uungu wa Yesu Kristo. Marekani na NATO unaweza kusema ni nchi za Wakris to . H a w a f u a t i d i n i y a Kiyahudi. Lakini wote wanaona Uislamu ni tatizo. Wanawaona Waislamu, ni maadui.

Kwa ajili ya kupambana na Uislamu, Mayahudi na Wakristo wameunganisha nguvu zao.

Marekani na Israel, zinawaona wapiganaji wa Hezbol lah , kama m a a d u i w a k u b w a . Na tunaambiwa kuwa Hezbullah, wanaingia Syria kumsaidia Bashar al-Assad.

Kwa upande mwingine, wapiganaji wa Kiislamu, Islamic Front na wengine,

Waislamu wanauwanawenyewe kwa wenyewe

Inatoka Uk. 9

nao pia ni maadui wa Marekani na Israel. Kwa M a r e k a n i n a I s r a e l , Hizbullah, al-Nusrah Front na Islamic Front, wote ni magaidi. Lakini katika vita hii ya Syria, Hizbullah wapo upande wa Bashar, wanapigana na al-Nusrah Front! Imekuwa vita ya panzi. Na ndio maana inaelezwa kuwa hawa wapigana j i wa Kiislamu wanapewa silaha kupitia mlango wa nyuma. Kupitia Saudi Arabia/Qatar. Ili nini? Mwisho wa yote wanaouwana ni Hizbullah na Islamic Front! Waislamu kwa Waislamu!

Kama alivyosema ‘neo-con extremist’ Daniel Pipes, kuendelea kwa vita Syria (na Somalia) kuna faida kubwa kwa Marekani na washirika wake Ulaya, kuliko kumalizika kwa vita hiyo.

K wa m a a n a k u wa wangetaka wangeweza kuwasaidia wapinzani vita ikamalizika haraka. Lakini manufaa yanayopatikana

k wa v i t a k u e n d e l e a n i m a k u b w a z a i d i : Wanadhoofika Hizbullah n a w a n a d h o o f i k a ‘Mujahidina’ wa Kisuni.

“Sunni jihadis killing Shia jihadis, and vice versa...This keeps them focused locally, and it prevents either one from emerging victorious and thereby posing a greater danger. Western powers should guide enemies to a stalemate by helping whichever side is losing, so as to prolong their conflict."

Hivi ndivyo anavyosema siasa kali ‘neo-con’ Daniel Pipes. Na ukichunguza hii ndiyo hali inayoendelea Syria na Somali.

Anayepewa msaada a n a p e w a k i a s i c h a kumwezesha kuendelea kupigana, sio kushinda.

Katika mapambano ya namna hii ni kwamba, bada la ya Wais lamu k u f i k i r i a n a m n a ya k u p a m b a n a n a a d u i mkubwa, mnamalizana wenyewe kwa wenyewe. H a m n a h a b a r i n a ‘ t w a g h u t i ’ . K i n c h i , Waarabu, hawana habari na Israel. Wanachinjana wenyewe kwa wenyewe.

Je, mkishadhoofishana, ndio mtaweza kupambana na ‘twaghuti’?

Hakuna wa kuishinda Al Shabaab kwa sasanow we know the New York media was deliberately telling us about a mid-air incident which never occurred in much the same way that during 9/11 Building seven was still standing after CNN and the BBC had announced its collapse……get the story?”

Anachosema hapa ni kuwa dalili moja wapo kuwa yalikuwa mambo ya kupangwa ni kitendo c h a m w a n d i s h i w a habari aliyekuwa New York kuulizia shambulio la ndege wakati rada za uwanja na harakati zote za usalama na upashaji habari katika uwanja, hakuna hata moja i l iyokuwa imeripoti tukio hilo. Kwa maana kuwa hakukuwa na shambulio kama hilo ila lilikuwa limetayarishwa u k a c h e z w a u s a n i i , waandishi wakapewa t a a r i f a n a n a m n a y a k u r i p o t i , s a s a

Inatoka Uk. 9 wanazungumzia jambo a m b a l o h a l i k u t o k e a kabisa.

Mengi yalisemwa na vyombo vya habari katika lile shambulio la ‘kigaidi’ katika jumba la kibiashara, Westgate Shopping Mall, Nairobi Kenya. Lakini katika jumla ya yote yaliyosemwa, makubwa ni haya:

Kwanza ni kuwaambia wasomaji na wasikilizaji kuwa waliohusika ni Al Shabab kutoka Somalia. P i l i , Al Shabab hao , ni magaidi hatari na wenye ujuzi mkubwa. Ndio maana waliweza kuingia wakashambulia na kuondoka bi la ya k u k a m a t w a . H a t a kamera za usalama (cctv), hazikuweza kuwapiga picha wakati zilinasa picha za wanajeshi walioingia ndani katika harakati za uokozi wakipora mali!, Tatu, ni Waislamu. Nne,

Waislamu hao ni watu katili sana. Bila shaka mtakuwa na kumbukizi ya zile taarifa za magazeti kuwa Al Shabab hao walikuwa wakiwakamata watoto wachanga na kuchonga mikono yao na kufanya kalamu za kuandikia huku damu ikiwa wino. Tano, Al Shabab hao ni wauwaji waliodhamiria kuwaangamiza Wakristo. R e j e a z i l e t a a r i f a z a m a g a z e t i k u w a magaidi hao walikuwa wakiwafolenisha watu na kuwahoji, ukithibitisha k u wa n i M u i s l a m u , unaachiwa, ukionekana Mkristo, unapigwa risasi.

Haya ndiyo kwa ufupi tuliyoambiwa.

Kiasi wiki tatu baada ya shambulio lile, kulitokea mzozo baina ya vyombo vya habari na serikali ya Kenya. Hii ni kwa sababu baadhi ya vyombo vya habari vilitoa picha

zilizonaswa na kamera za usalama zikionyesha askari wakipora mali. Na kwa kweli zipo taarifa nyingi kwamba wengi waliokuwa na maduka katika eneo hilo wamekuta mali zao zimeporwa, hasa zile rahisi kubebeka.

Lakini pamoja na ukweli huo kwamba kamera zilinasa askari wakifanya uporaj i , hakuna hata kamera moja iliyonasa sura ya ‘gaidi’ wa Al Shabab akipiga watu risasi.

Aidha tukumbuke kuwa zilisambazwa picha nyingi zikionyesha kizaazaa kilichokuwa ndani. Watu wakikimbia ovyo na pia ikionyeshwa askari na makachero walioingia kuokoa watu. Lakini hakuna hata picha moja iliyoonyesha watu wa Al Shabab. Kwa nini? Kwa sababu hawakuwepo. Kama ipo sababu nyingine, sema.

Binafsi s iamini , na huo ndio ukweli, kuwa Al Shabab, wanaweza wakatoka Mogadishu wakapakia silaha katika magari wakaingia Kenya na kufanya shambulio kama lile la Westigate. Hawana uwezo huo. Na kwa upande mwingine, hakuna serikali yoyote duniani iliyo ya hovyo, nyoronyoro na isiyo na ulinzi kiasi hicho.

Pengine kwa kuhemkwa na kwa jazba , wapo baadhi watakaoona ni ushujaa kwa Al Shabab kufanya vile, na hoja ikiwa kwamba wanalipa kisasi kwa sababu Kenya imevamia nchi yao. Ukija na ‘jazba’ hiyo, kwanza utakuwa unajitukanisha wewe mwenyewe na kuwatukanisha Waislamu kuwa hawana uwezo wa kuona kiini macho k a m a h i c h o k i l i c h o

Inaendelea Uk. 12

ASKARI wa Burundi wa kulinda amani nchini Somalia.

12 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

Hakuna wa kuishinda Al Shabaab kwa sasaInatoka Uk. 11

dhahir i kabisa . P i l i , utakuwa unaimba wimbo wa l i o t a k a m a k a f i r i . Maana ukishashabikia k u wa n i A l S h a b a b waliofanya shambulio lile, unachosema ni kuwa Uislamu unafundisha ukatili na mauwaji kama yale ya kuuwa watoto wadogo wasio na hatia. Tatu, utakuwa unasaidia k u p a n d i k i z a c h u k i baina ya Waislamu na Wakristo (kwa sababu ilielezwa kuwa walikuwa wakiuliwa Wakristo tu). Kwa maana hii utakuwa u n a i m b a w i m b o wa mabeberu wa kupandikiza mbegu ya chuki, fitna na machafuko ya kidini. Nne, utakuwa unaipa nguvu propaganda ya kuwapachika ugaidi Waislamu na kuhalalisha m a u wa j i n a m a t e s o wanayofanyiwa.

Ambalo ningependa lionekane hapa ni kuwa Al Shabab, kutokana na historia yao na malengo yao, wameibuka kama a m b a v y o i n g e k u wa k w a w a t u w a n c h i yoyote: kupambana na maadui waliovamia nchi yao. Na baada ya hapo

wanapambana na serikali wanayoamini kuwa ni kibaraka wa maadui wa Uislamu.

Lakini maadui hao hao wa Uislamu, kwa matukio kama lile la Kampala na hili la juzi Westigate

Shopping Mall, Nairobi, wameigeuza Al Shabab kuwa mtaji wa kuupiga vita Uislamu. Ukisha waaminisha watu kuwa Al Shabab (Waislamu) ndio waliofanya shambulio na mauwaji kama yale

ya Westigate, maana yake ni kuwafanya hata hao Waislamu wenyewe kujisikia vibaya. Kuhoji dini yao. Kwa upande mwingine, unawakimbiza hata wale waliokuwa wakifikiria kusilimu,

k u o n a k u wa k u m b e dini yenyewe/Waislamu wenyewe hawana maana. Lakini pia, unajipa uhalali wa kukusanya nguvu za kilimwengu kupambana na Waislamu. Na ndio kinachofanyika hivi sasa.

K a t i k a h a l i k a m a h i i , wa n a c h o t a k i wa Wa i s l a m u , k w a n z a ni kutambua mchezo kama huu kwamba upo. Na hivyo, linapotokea shambulio linalodaiwa k u w a l a k i g a i d i , wasikimbilie tu kulaani. Bal i watumie vyema bongo zao kuchambua na kuhoji. Isije ikawa ni mambo ya kupanga ili kupata sababu. Majukwaa kama hotuba za Ijumaa zitumike kuwaelimisha Waislamu.

Lakini Waswahili wana msemo wao, ukipunjwa nyama buchani, lalamikia pale pale buchani. Ukienda kulalamikia nyumbani kwa mkeo haisaidii. Na ugomvi wa ‘kilabuni’, umalizikie ‘kilabuni’.

Sasa kama wengine wa n a t u m i a v y o m b o vya habari, kuulaghai u l i m w e n g u m z i m a , hapana shaka kungekuwa na vyombo vya habari vya Kiislamu/vya Waislamu,

Mafunzo kutoka anti bakala, SelekaInatoka Uk. 4

Taarifa kutoka Shirika la habari la AFP zinasema kuwa miongoni mwa waliouawa, ni walinzi w a t a n o w a a m a n i kutoka Chad, ambao wa l i s h a m b u l i wa n a wanamgambo wa Kikristo wa 'anti-balaka mjini Bangui, siku ya Jumatano.

Kufuatia kuzuka kwa mapigano, kumezusha hali ya wasiwasi zaidi kwa maelfu ya wakazi w a B a n g u i , a m b a o wamelazimika kukimbilia Uwanja wa Ndege kupata hifadhi na vyakula, eneo ambalo walinda amani kutoka Ufaransa na Afrika wamepiga kambi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Shrika la Msalaba Mwekundu Bw. David Pierre Marquet, mbali ya mauaji hayo, lakini

pia takriban watu 30 wamejeruhiwa vibaya na kwamba, idadi ya v i f o h i v y o i n a we z a kuongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano.

Ukiacha athari za vifo vya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenyewe, Nigeria nao sasa wanalia. Kiasi cha raia 83 wa Nigeria wa l i o k u wa wa k i i s h i humo wameuliwa mjini Bangui katika mapigano yanayoendela nchini humo limeripoti Daily Trust.

Kiongozi wa Jumuia ya wa-Nigeria mjini Bangui, Muhammad Kalanbai, ambaye alizungumza n a g a z e t i l a D a i l y Trust, alisema wengi wa-Nigeria waliouawa katika machafuko hayo ni Wais lamu kutoka Kaskazini mwa Nigeria.

“ H i v i ninavyozungumza na

wewe kuna miili 16 ya Waislamu wa Nigeria katika Msikiti wa Ali Baglo mj in i Bangui , a m b a o h a wa j a z i k wa kwasababu ya vurugu zinazoendelea,” alisema Kalanbai , ambaye ni kiongozi wa watu wa N i g e r i a K a s k a z i n i wanaoishi nchini Jamhuri ya Kati.

“Wiki iliyopita tu zaidi ya wanigeria 67 ambao ni Waislamu waliuliwa na watu wanaomuunga m k o n o B o z i z e . Tunashambuliwa hasa”. Alisema Bw. Kalanbai.

Kufuatia mashambulizi hayo, Wanigeria ambao ni Waislamu wanaoishi nchini humo, wamekuwa wakik imbi l i a ka t ika u b a l o z i wa o n c h i n i humo mjini Bangui ili kusalimisha maisha yao na wamemtaka Rais G o o d l u c k J o n a t h a n ,

k u w a n u s u r u k w a kuwasaidia ndege ya kuwarejesha nyumbani Nigeria .

Kalanbai al ie leza kuwa tayari baadhi ya nchi za African zikiwemo Cameroon, C h a d n a M a l i , zimeshatuma ndege kuwaokoa raia wake.

Wanigeria wengi, hasa kutoka Kaskazini wapo nchini Jamhuri ya A f r i k a ya K a t i wakijishughulisha na uchimbaji madini ya dhahabu na biashara.

Wanamgambo kutoka makundi ya Wakristo na Waislamu wamekuwa wakipambana tangu kuangushwa kwa Rais Francois Bozize mwezi Machi mwaka huu.

T a k r i b a n w a t u 700,000 katika Jamhuri h iyo ya Afr ika ya Kati wamelazimika

kuyakimbia makazi yao, ambapo idadi ya wakimbizi inazidi kuongezeka kwa mjibu wa Adrian Edwards wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR.

Watanzania wana la kujifunza kutokana na yanayoendela huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bila shaka mauaji yanayoendelea huko, watu kukimbia makazi yao, uharibifu wa mali na madhara mengine yanayopatikana sasa, ni matokeo ya dola kukumbatia ubaguzi k a t i k a j a m i i , h a s a ubaguzi wa kiimani katika mamlaka za dola.

Fikra za kibaguzi ndizo hasa zimekuwa chimbuko la kuzaliwa anti balaka na Seleka na kuleta maafa kwa raia wasio na hatia.

WAPIGANAJI wa Al Shabaab.

13 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

LIKITANGAZA kifo cha Ariel Sharon, komandoo, jenerali, waziri wa ulinzi na waziri mkuu wa zamani wa Israeli aliyepata hitilafu kubwa ya moyo mapema mwaka 2006, mwaka mmoja na miezi miwili baada ya kifo cha Rais Yasser Arafat wa Palestina aliyekuwa ni takriban mfungwa wa Waziri Mkuu Sharon, gazeti la New York Times lilisema alikuwa m we we a l i ye t a k a a m a n i kwa masharti yake. Gazeti la Washington Post lilisema ni mtu asiye wa kawaida katika historia ya hivi karibuni ya Israeli ambaye "alitaka kuwa mbunifu wa kufikia hatma ya amani," likiweka picha ya mzee mpole, babu wa watu. USA Today lilisema alikuwa akizua hisia tofauti na kuwa mtu adimu na muhimu kwa watu wengi. Ndivyo magazeti na vyombo vingine vya habari vikubwa vilivyosema kuhusu kifo cha Ariel Sharon.

Siyo watu wengi duniani waliodanganywa na kilichokuwa kinasemwa na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu S h a r o n , n a z a i d i , w a t u wa Palest ina na Lebanon wanamfahamu Sharon vyema, maelfu wakiwa wameuawa katika kampeni za huyu mhalifu wa kivita mwenye mlolongo wa mauaji ya halaiki aliyosimamia. Sifa za Sharon kama kamanda wa kivita zilijengwa katika mauaji ya watu wengi - kuanzia Qibya mwaka 1953 hadi Sabra na Shatila mwaka 1982, hadi Jenin mwaka 2002.

M b a g u z i m k e r e k e t w a a l i ye wa c h u k i a Wa a r a b u , Sharon alikuwa na historia ndefu iliyotapakaa damu katika kuwaua na kuwakandamiza watu wa Palestina. Katika miaka ya 1950 alikuwa mkuu wa kikundi cha wauaji kiitwacho Unit 101, ikiwa ni kombania maalum ya kutekeleza mauaji dhidi ya wa-Palestina walioko uhamishoni ukanda wa Gaza na nchini Jordan.

Licha ya kuwa walikuwa wameiteka asilimia 78 ya ardhi ya Palestina katika vita vya mwaka 1948, viongozi wa Israeli walikuwa hawajaridhika kabisa. Kama ambavyo imeainishwa na wanahistoria wa Israeli na Palestina, Israeli ilitaka kuchokoza 'mzunguko wa pili' wa vita katika miaka ya 1950, ili kuteka Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, ambao wakati huo unatawaliwa na Jordan, Gaza na kwingineko.

Moja ya mbinu muhimu za Israeli ilikuwa ni 'kujibu m a s h a m b u l i o ' d h i d i y a wa - Pa l e s t i n a wa l i o k u wa wamefukuzwa katika miaka ya karibuni wakirudi kutoka mipakani kuja nchini kwao kutoka Gaza na eneo la Ukingo wa Magharibi wa Jordan. Jeshi la Israel lingefanya mashambulio makubwa na mauaji ya watu wengi.

Kwa dhamira za kidiplomasia na mahusiano, i l ikuwa ni muhimu sana kwa Israel i kuonekana kama mwathiriwa na siyo mshambuliaji. Hali hiyo bado inaendelea.

‘Kujibu shambulio' kulikuwa hasa ni kushambulia, kuchokoza; nia ilikuwa ni kuisukuma Jordan au Misri ijibu kijeshi mauaji hayo ya watu wengi, ambayo ingeweza kutumiwa na Israeli

Ariel Sharon: Mhalifu wa kivita muuwaji wa halaikikama kisingizio cha kuanza vita mpya ya kuteka maeneo.

Hapo Oktoba 14, 1953, U n i t 1 0 1 i k i o n g o z wa n a Sharon ilishambulia Qibya, kijiji kidogo kisicho na ulinzi ndani ya Ukingo wa Magharibi, na kuua watu 69, wengi wao wakiteketea kwa moto wakiwa hai ndani ya makazi yao. Unit 101 haikupoteza mtu hata mmoja. Ilikuwa ni uharamia ulioamuliwa katika ngazi za juu na kufanywa kwa malengo ya kisiasa.

Mauaji ya Qibya yalizusha kulaani kitendo hicho kote duniani, na Jordan, ikiwa dhaifu zaidi kuliko Israeli, haikujibu kama viongozi wa Israel i walivyotumaini. Utekaji wa Ukingo wa Magharibi na Gaza ikabidi ungoje hadi 1967.

Mauaji ya Sabra na ShatilaKufuatia vita ya utekaji

maeneo ya mwaka 1967, Sharon alikuwa gavana wa kijeshi wa Gaza, akiwa na sifa ya ukatili wa kushangaza katika kutekeleza sera ya utesaji na uuaji wa Wapalestina wanaopambana na kukaliwa nchi yao.

U h a r a m i a w a S h a r o n ulijionyesha kwa nguvu zaidi katika uvamizi wa mwaka 1982 nchini Lebanon katika kambi za wakimbizi za Sabra na Shatila eneo la Beirut. Akiwa waziri wa ulinzi, Sharon aliandaa na kuongoza, kwa kukingiwa kifua na Marekani, mashambulizi makubwa dhidi ya Lebanon. Kwa miezi mitatu katika kipindi cha kiangazi cha 1982, ndege za kubeba mabomu za Israeli, zil izotolewa na Marekani, z i l iangusha mabomu bi la kikomo juu ya Beirut na miji mingine, wakauawa watu zaidi ya 20,000 wakiwa raia wa Lebanon na Palestina. Lebanon haikuwa na mfumo wa ulinzi wa anga.

Lengo rasmi la uvamizi huo lilikuwa ni kukiondoa chama cha ukombozi wa Palestina (PLO) kutoka Lebanon. Kuna zaidi ya wakimbizi 400,000 wa ki-Palestina - wale walioondolewa katika makazi yao ya jadi kupisha kuundwa kwa nchi ya Israeli mwaka 1948 na wazaliwa wao wanaoishi Lebanon. Kwa jumla zaidi ya Wapalestina milioni saba hivi leo wanaishi uhamishoni.

Baada ya miezi mitatu ya mabomu, uongozi wote wa PLO ulikubali kuondoa wapiganaji wake kutoka Lebanon, Kama s e h e m u ya m a k u b a l i a n o ya kuwahi ta j i kuondoka , raia waliobaki wa Palestina wangewekwa chini ya ulinzi wa kimataifa. Sharon hata hivyo alisema hadharani kuwa kuna 'magaidi' 2,000 wamebakia katika makambi ya wakimbizi ya Sabra na Shatila magharibi ya Beirut. Katika hali halisi, waliobaki katika makambi walikuwa karibu wote ni watoto, wanawake na wazee. Wanaume vijana na wale wa umri wa kati walikuwa takriban wote wameondolewa.

Vifaru vya Israeli vilizunguka makambi hayo kinyume cha kile kilichokubaliwa katika m a k u b a l i a n o ya k u a c h a mapigano. Halafu, mnamo Septemba 16, 1982 kwa ufahamu wa kina na rukhsa ya Sharon na wavamizi wa Israeli waliokuwa wameshika eneo hilo wakati huo, ma-Falanga wa Lebanon

ARIEL Sharon.

waliruhusiwa kuingia Sabra na Shatila magharibi ya Beirut.

Ma-Falanga hao wa kifashisti walikuwa wanamhusudu Adolf Hitler na walichukua jina lao kutoka chama cha Jenerali Francisco Franco wa Hispania, fashisti wa mwelekeo sawa na Hitler, na walikuwa washiriki wa karibu wa Israeli nchini Lebanon. Ma-Falanga walivaa sare zilizotolewa na Israel na kubeba silaha zilizotolewa pia na Israeli.

Kwa siku tatu walivinjari na kuteketeza katika makambi ya wa-Palestina, wakitesa, kubaka na kuua. Wengi kati ya waliouawa walitolewa matumbo au kukatwa vichwa. Hakuna aliyeachwa, siyo vikongwe wala vichanga. Kufikia mwisho, zaidi ya watoto, wanawake na wanaume zaidi ya 1,900 walikuwa wamekufa.

Licha ya kuwa ushahidi ulionyesha kwa wazi kuwa Sharon na makamanda wengine wa Israeli walikuwa wamepeleka mafashisti hao katika makambi yasiyo na ulinzi, mahakama il iyoamuru uchunguzi wa mauaji hayo ulimwona Sharon kuhusika kwa mbali na mauaji hayo. Mtu anaweza kudhania kuwa hata kuhusika kwa mbali kwa mauaji ya watu karibu 2000 ingekuwa angalau ndiyo mwisho wa maisha ya kisiasa ya mhusika. Lakini siyo katika nchi ya kibaguzi ya Israeli.

Wakati Sharon alilazimika kujiuzulu kutoka baraza la mawaziri la Israel kutokana na hukumu hiyo ya uchunguzi, al iendelea kuwa mshir iki muhimu wa siasa na akarudi tena katika baraza la mawaziri

miaka ya 1990.Intifada ya Al Aqsa na

kuchaguliwa Sharon kuwa waziri mkuu

Mnamo Septemba 28, 2000 Sharon al i fanya uchokozi m w i n g i n e u l i o m p a s i f a , 'kutembelea' msikiti wa Al Aqsa mjini Yerusalemu, eneo muhimu takatifu la Kiislamu. Akiwa anaitangaza 'haki' yake ya kwenda kokote Yerusalemu, muuaji huyo bayo maaluni, hakufanya utembeleaji huo peke yake. Tofauti na hapo, alifuatana na polisi 1,500 wenye silaha. Hata hivyo, mamia ya Wapalestina walipigana nao, ikaanza Intifada ya Al Aqsa, uamsho au mapambano, ambayo yalidumu kwa miaka mingi.

Miez i miwi l i baadaye , F e b r u a r i 2 0 0 1 , S h a r o n alichaguliwa waziri mkuu, ,na mwezi Machi 2002, jeshi la Israeli lilifanya operesheni kubwa Ukingo wa Magharibi na Gaza, likitaka kuisambaratisha Intifada.

Kati ya mashambulio ya kikatili zaidi lilikuwa ni dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Jenin kaskazini ya Ukingo wa Magharibi. Kwa siku kadhaa, wa k i t u m i a m a t i n g a t i n g a yaliyoundwa kivita na silaha nzito, jeshi la Israeli liliteketeza sehemu kubwa ya kambi hiyo, likifukia watu wengi huku wako hai. Mwaka huo huo, Sharon alianza kujenga ukuta wa kibaguzi kuukata Ukingo wa Magharibi, akatwaa ardhi zaidi ya wa-Palestina.

Sharon: Mtafutaji bandia wa amaniDai lisilo la kweli kuwa

Sharon alibadilika na kuwa

'mtu wa amani' inajikita katika uamuzi wake wa kuondoa makambi ya kijeshi na makazi madogo na yasiyokuwa na hatma nzuri mbeleni, ya wakazi wa Israeli kutoka eneo la Gaza. Wakati ambapo wa-Palestina katika eneo la Gaza walifurahia kuondolewa kwa makazi hayo, Israeli iliendelea kuiweka Gaza imezingirwa na haina njia ya kutokea.

Kuondoka Israeli kutoka Gaza, licha ya kupingwa na baadhi ya wakazi mafashisti, ilikuwa na msingi wake katika dhamira ya kuchukua sehemu kubwa zaidi ya Ukingo wa Magharibi. Katika mahojiano ya Julai 21, 2000 na gazeti la Jerusalem Post, miezi kadhaa kabla hajawa waziri mkuu, Sharon alitoa mwito kwa Israeli "kushikilia upana wote wa Yerusalemu, ikiwa imeungana na bila kugawanywa chini ya milki kamili ya Israeli." Hii inazungumzia Mji Mkongwe wa Palestina na maeneo yote yanayozunguka ambayo Israeli iliyapora baada ya vita ya mwaka 1967.

"Israeli itashikilia chini ya udhibiti kamili maeneo mapana kiasi cha kutosha magharibi na mashariki. Bonde la Jordan, kat ika upana wake kama lilivyoainishwa katika Mpango wa Allon (waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Israeli, Yilgal Allon) litakuwa ndiyo ukanda wa usalama wa mashariki wa Israeli.

Sharon alitoa mwito kuwa maeneo makubwa ya Ukingo wa Magharibi unaoshikiliwa na Israeli yachukuliwe. "Miji ya Kiyahudi, vijiji na jumuia za Judea, Samaria na Gaza, pamoja na njia za kufikia maeneo hayo ....zitabaki chini ya udhibiti kamili wa Israeli," Sharon aliainisha. "Judea na Samaria" ndiyo jina la Israeli kwa Ukingo wa Magharibi.

Sharon alikuwa muwazi katika kiburi chake cha kikoloni, akisema "Israeli haikubali katika hali yoyote ile dai la Wapalestina la haki ya kurudi. Israeli haiwajibiki kihisia kuhusu hali ya wakimbizi."

Pia alisema "kama sehemu mahususi ya kuishi, Israeli lazima iendelee kushika vianzio vya chini ya ardhi vya maji magharibi ya Samaria (Ukingo wa Magharibi) ...Wapalestina wanawajibika kuzuia uchafuzi wa vianzio vya maji vya Israeli."

'Dola' ya Palestina ambayo Sharon alipendekeza ilikuwa ni ya aina ambayo haipo kokote pa le duniani . Hai tashika raslimali zake yakiwemo maji. au njia zake za anga, au hata mipaka yake, na itakuwa ni dola-eneo lisilo na ulinzi kando ya moja ya dola zenye kiwango kikubwa cha urasimishaji jeshi duniani.

Bila kujali vichwa potofu vya habari, Sharon ataingia katika historia siyo kama mtaka amani wa aina yoyote, ila kama mkono wa damu, mbaguzi na muuaji wa watu wengi kama alivyokuwa.

(Imefasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija. Kutoka makala Ariel Sharon: Serial war criminal, mass murderer *The true legacy of a virulent anti-Arab racist)

14 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

K i l a s i f a n j e m a zinamstahiki Mwenyezi Mungu Swala na Amani z i m f i k i y e M t u m e Muhammad (s .a .w) (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na jamaa zake.

S u a l a l a k u we p o Mahakama ya Kadhi ni nyeti na kubwa mno ambayo inagusa uhai wa Uislamu na Waislamu. N i s u a l a a m b a l o halina majadala juu ya umuhimu wake.

Na kwa hakika itakuwa ni jambo la kujidhalilisha i k i w a b a d a l a y a kuweka tarat ibu za kuwa na Kadhi wao na kuhakikisha kuwa ofisi hiyo inafanya kazi, Waislamu watakuwa w a k i p i g a m a g o t i kuomba ruhsa ya kuwa na Kadhi.

A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Ta’ala):

Wa l a h a wa t o a c h a kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao a'mali zao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu.” (Al Baqara 2:217)

“Mayahudi hawawi r a d h i n a w e , w a l a Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. N a k a m a u k i f u a t a matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kukujia, hutapata mlinzi wala msa id iz i kwa Mwenyezi Mungu.” ( Al Baqara 2;120)

Kama ilivyo lazima kwa Muislamu kwenye kutekeleza ibada ya Swala, Saumu, Zakat, Hija n.k. hangojei kupata idhini ya mtu au watu ili kutelekeleza ibada hizo na ndio hivyo ilivyo faradhi ya kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi.

Kuna mihimili mitatu ya dola: Bunge (Shuurah), Urasimu (Mamlaka ya Utendaji) na Mahakama. Vitu hivi ndio ambavyo v i n a u n d a d o l a . Kukosekana kuwepo

Haja ya kuwa na KadhiNa Abu Saumu, Kombo Hassani Kidumbu

k w a k i m o j a w a p o , n i k u a n g a m i a a u k u t a s a b a b i s h a kusiwepo na Utawala wa Sheria. Wajibu wa Mahakama ya Kadhi ni kufafanua, kusimamia na kuhakikisha Sheria na Hukumu za Allah zinatekelezwa katika ki la k ipenge le cha maisha ya Waislamu na ili kulinda Haki, Kuzuia Maovu, Uf isadi na Dhuluma katika jamii.

“Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha ya l iyo kuwa kab la yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi, hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake.” (5:48)

W a i s l a m u w a s i p o k u w a n a Mahakama ya Kadhi watakuwa na dhima m b e l e y a A l l a h (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kutoitekeleza ibada hiyo hadhimu (tukufu). Hivyo jamii hiyo itakuwa ama ni ya Madhalimu, Mafaski (waovu) na au Washirikina kama alivyotufahamisha Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwenye Qur’an Tukufu.

A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Ta’ala):

“ H a k i k a S i s i tuliteremsha Taurati y e n y e u w o n g o f u n a n u r u , a m b a y o kwayo Manabii walio nyenyekea Kiislamu, n a w a c h a m n g u , n a w a n a z u o n i , w a l i w a h u k u m u M a y a h u d i ; k w a n i w a l i k a b i d h i w a kukihi fadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. N a o w a k a w a n i mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri”. (5:44)

“Na wasio hukumu k w a y a l e a l i y o yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” (5:45)

“Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” (4:47).

Ilivyo, Ukafiri ni Giza na Uislamu ni Nuru. Katika hali ya kawaida ya maumbile nuru na giza haviwezi kuishi

pamoja bali giza likizidi nuru, nuru itatoweka na kinyume chake ni sahihi. Kwa mantiki hii, ukafiri ukiwa na nguvu ya kutawala jamii, Uislamu u t a t o w e k a k a t i k a jamii hiyo hata kama Waislamu watakuwepo. Kwa maana nyingine, pa le ambapo jami i huongozwa kwa sheria na sera zinazopingana na sheria na utaratibu a l i o u w e k a A l l a h (Subhaanahu wa Ta’ala) katika kuendea Uchumi, Siasa, Utamaduni na vipengele vingine vya maisha ya jamii hiyo, watakuwa wanaishi k ikaf i r i hata kama w a t a b a k i a k u j i i t a Waislamu na kufanya matendo binafsi ya Kiislamu kama vile k u s wa l i , k u f u n g a , k u h i j i , n k . K w a mantiki hii vilevile, ili Waislamu waweze kuufuata Uislamu wao katika ila kipengele cha maisha, hawana budi kuutawalisha Uislamu katika jamii, yaani , hawanabudi k u u s i m a m i s h a Uislamu katika jamii k w a k u h a k i k i s h a k u w a S h a r i a h n a mwongozo wa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndio unaotawala kila kipengele cha maisha

ya jamii.Kihalisia sio jambo

jepesi kusimamisha Uislamu na kuwa na Mahakama ya kadhi yenye kufanya kazi kwa lengo lilokusudiwa kwenye Uislamu katika jamii , kwani daima makafiri (Matwaaghuut) wanapenda kubakia k a t i k a g i z a i l i waendeleze dhuluma na maovu katika jamii. Hivyo makafiri hawako tayari kumulikwa na nuru ya Uislamu. Nia ya makafiri ya kuzima n u r u y a U i s l a m u inabainishwa na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia” (61:8)

Kama ilivyo Sunnah (kawaida) yake, Allah ( S u b h a a n a h u w a Ta’ala) hatausimamisha Uislamu katika jamii kwa kuwahi l ik i sha makafiri wote katika jamii au kuwalazimisha w a t u w o t e w a w e waumini, bali ana ahidi kutimiza Nuru yake kwa kuwasaidia waumini dhidi ya makafiri pale watakapokuwa tayari kujitoa muhanga kwa mali zao na nafsi zao kupigania uhuru wao wa kufuata Uislamu katika kla kipengele cha maisha ya jamii.

K a t i k a h a l i y a kawaida ya utaratibu wa maumbile aliouweka Al lah (Subhaanahu wa Ta’ala), hatotokea Waislamu kujikuta tu wapo katika mazingira mazuri ya kumtii Mola wao na kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya binafsi na ya jamii kwa wepesi tu bila ya kipingamizi chochote kama viumbe wengine wal io mbinguni na ardhini wanavyomtii M o l a w a o k a m a inavyobainika katika aya ifuatayo.

A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Ta’ala):

Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu

WAISLAMU wakiwa kwenye Zaffa ya Maulid jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

15 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

LICHA ya makatazo makali ambayo yamo ndani ya mafundisho ya Kiislamu juu ya talaka, lakini bado utoaji wa talaka umekuwa n i t a t i z o k u b wa k wa Zanzibar ambayo wananchi wake kwa asilimia kubwa ni Waislamu.

Migogoro inayosababisha kuachana ni mingi ikiwemo wanaume kuongeza wake zaidi ya mmoja, wanawake kupigwa na waume zao, ulevi, kutotenda haki kwa mwanandoa mmoja dhidi ya mwengine, wazazi kuingilia famil ia za wana ndoa, kutoaminiana kati ya wana ndoa ni miongoni tu mwa mambo ambayo huchochea wanaume kuamua kutoa talaka kwa wake zao jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa utelekezaji wa watoto.

Kadhi wa Mahkama ya Kadhi Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar, Ali Khamis Mussa amesema kesi za ndoa kat ika mahkama hiyo zinazidi kuongezeka kutokana na ndoa hizo kukosa mashiko na hivyo wa n a n d o a we n g i wa o wanapokwenda kushitaki huamua kutaka kuachana.

Alisema laiti kungetolewa elimu ya ndoa kabla ya kufungwa kwa ndoa, basi ingeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wana ndoa hao kuishi kwa uvumilivu na kustahamiliana na hata kama kutatokea migogoro, basi wazazi ndio wangekuwa waamuzi wa kesi hizo na sio kukimbilia mahakamani kutaka kuvunja ndoa.

“Ni muhimu sana elimu ya ndoa kwa sababu sasa hivi kesi nyingi za mke na mume zinazokuja hapa mwisho wake inaishia mwanamke kudai apewe talaka yake, na wazazi nao wana nafasi kubwa katika suala zima la wana ndoa kuweza kuishi kwa kustahamiliana” alisema Kadhi huyo.

Al isema kukosekana kwa elimu kumechangia kwa kiasi kikubwa wana ndoa kuwa na mifarakano isiyoweza kusuluhishika na kusababisha ta laka kuongezeka kwa kias i ambacho kinasikitisha katika jamii ya Wazanzibari.

Alisema mdai au mdaiwa m a r a n i n g i n d o a z a o zinakuwa zile zisizofuata mafunzo na sheria ya dini ya Kiislamu tokea awali na hivyo ndoa hizo huwa ni zile za mkeka au kukamatiwa na kulazimishana, hivyo utulivu unakosekana kwa wana ndoa hao na mwisho wake huishia kukosana na kupeana talaka muda mchache baada ya kufunga ndoa.

Jambo jengine ni ndoa za umri mdogo ingawa wengine tayari wameshafika umri wa miaka 18 lakini utulivu bado unakuwa haujapatikana kulingana na umri wa wastani wa miaka 20-25 ambapo mwanamke anakuwa na mawazo na fikra za kuaminika katika ndoa yake

Kadhi huyo a l i sema mara nyingi ndoa za watoto

Talaka zimekithiri ZanzibarNa Alghaithiyyah Zanzibar

kuwa watoto wa mitaani.Jumla ya kesi mia 799

z i m e f u n g u l i wa k a t i k a mahkama hiyo ya kadhi Mwanakwerekwe kuanzia Januar 2013 hadi Desemba 2013 kati ya hizo kesi 521 zimetolewa maamuzi na kesi 278 zinazoendelea zikiwemo kesi za ndoa na matelekezo ya watoto.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika wilaya mbali mbali uliosimamiwa na Chama Cha Waandishi wa H a b a r i Wa n a wa k e Tanzania (TAMWA) kwa u p a n d e w a Z a n z i b a r kimegundua kuwepo kwa ongezeko kubwa la talaka jambo ambalo linatishia mustakabali wa jamii ya Wa z a n z i b a r a m b a o n i Waislamu na wanatakiwa kufuata sheria na mafunzo yaliyopo ndani ya Quraan Tukufu.

“ W a i s l a m u w a n a p o k h i t i l a f i a n a wanapaswa kurudi katika kitabu kitukufu na wana ndoa wanapokosana kuna taratibu zake nyingi hatua baada ya hatua kabla hata ya kwenda kutoa talaka kwani talaka ni suluhisho ya mwisho kabisa lakini tatizo siku hizi ukitokea ugomvi mdogo tu hata mwanamke kakosea kut ia chumvi chakula basi anaandikiwa talaka”, alisema Sheikh Ali Bin Issa.

A l i s e m a h a t u a zilizowekwa na Mwenyeenzi Mungu za talaka moja na mbili zote zinapaswa kuzingatiwa kwa sababu unapomuacha mwanamke talaka ya kwanza anatakiwa abaki ndani ya nyumba ili kuweza kujirekebisha

makosa yake na lakini kubwa alisema wazazi sana wanachangia kuwashawishi watoto wao katika utoaji wa talaka na kuwaoza wake wengine hivyo kasi ya utoaji talaka imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na wazazi kushindwa kufuata mafunzo ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w).

A k i z u n g u m z a n a ANNUUR wiki hi i S i t i Abass kutoka Chama Cha Wanasher ia Wanawake Zanzibar (ZAFELA) amesema wanawake wengi wamekuwa wakidhalilishwa na waume zao amma kwa kupigwa au kukosa kuhudumiwa jambo ambalo linachangia kuhatarisha ustawi wa ndoa zao.

“Wanawake wanapokosa huduma bora majumbani mwao au kukosa matunzo wao au watoto wao na waume wengine hudiriki kuwapiga wake zao vipigo vya kuwaumiza khasa, basi wanawake wale huwa hawataki ushauri mwengine wowote zaidi ya talaka”, a l i s e m a n a k u o n g e z a kwamba.

“Sisi tunakuwa wagumu kuwashauri wadai talaka lakini pia tunatizama wale wanawake wanaporudi kwa waume zao wakati wanapata vipigo vya kuwaumiza na manyanyaso makubwa, jee wataweza kustahamili na jee haitakuwa madhara kwao? Ikiwa ni madhara basi shauri lake tunalipeleka mbele yaani mahakamani lakini sio kama tunawaambia wadai tu talaka”, alisema Siti.

Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Bi Maryam Hamdan amesema kwamba tofauti ya malezi ya watoto wa siku hizi na yale ya

zamani inachangia katika kuwaharibu wanandoa kutokana na mafunzo kutofautiana.

“ S i s i t u l i p o k u w a tunaposwa kwanza ilikuwa tunafundishwa namna ya kuishi na mume, kuwa na subra, kutomjibu mume ujeuri kuwa mpole na kadhalika lakini watoto wa sasa wanashindana na waume zao, wanajibu wanavyotaka wanafanya wanavyotaka wakipewa ruhusa au kama hawakupewa wao wanatoka t u s a s a m u m e h a t a k i kufanyiwa hivyo na ndio maana utakaona na mume naye akiwa mshindani basi mara hutoa talaka”, alisema Bi Maryam.

Wa k i t o a m a o n i ya o wananchi mbal i mbal i kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa wametoa maoni tofauti ambapo baadhi yao wametaka sheria za ndoa zipit iwe upya i l i kunusuru talaka za ovyo na zisizozingatia sheria.

Hata hivyo baadhi yao w a m e s e m a Wa i s l a m u wanapaswa kurudi katika mafunzo ya dini yao na wachukulie kwa uzito wa pekee suala la talaka kama ambavyo l i l ivyoelezwa katika Quran lakini pia katika mafunzo ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w).

“ K w a t a k w i m u z i n a z o o n e s h a k u h u s u talaka kwa hakika inatisha na ni bora serikali iweke sheria kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakioa na kuacha kwani Quran imekemea na arshi ya Rahman huwa inatikishika mtu anapokamata kalamu na kuandika talaka sasa iweje watu wasiogope suala hilo lazima elimu itolewe kwa vijana ili wajiepushe na kuandika andika talaka ovyo”, a l isema Sheikh Ahmed Said ambaye ni mwalimu wa chuoni.

wenye umri wa miaka 18 au chini ya hapo huwa zina matatizo kwa kuwa bado ni umri mdogo na wana ndoa hao wote wawili wanakuwa na joto ambalo kawaida umri huo huwa hawakubali suluhu na kila mmoja huwa anataka aonekane yeye ndiye mshindi wa tukio husika.

“ K a t i k a m a h k a m a hii hatutoi talaka moja kwa moja lakini hutoa ushauri kwanza na kama haikuwezekana suluhu hushauri wahusika kufungua kesi na talaka haitolewi ila wahusika waweze kufika na kuthibitisha wote wawili lakini pamoja na hivyo wapo ambao wanashikilia talaka talaka tu”alisema Sheikh Ali.

A l i s e m a wa n a wa k e wanapofika Mahakamani hapo kwa ajili ya kudai talaka wamekuwa wakitakiwa kufuata taratibu na sio kupewa ta laka tu ba l i hutizamwa kwanza vigezo maalum vitakavyo thibitisha kuwa anastahiki kuwa ndoa hiyo itenguliwe na mahkama au laa.

“ Y o t e h a y o h u w a tunayafanya ili kupunguza idadi ya ta laka kwani tunafahamu suala la kutoa talaka ni baya katika jamii lakini jamii nayo huwa ikishikilia jambo haitaki kukubali kama talaka ina madhara”, alisema Kadhi huyo.

Akivitaja Vigezo ambayo huzingatiwa na mahakama hiyo ni pale wanawake wanapopeleka malalamiko ya kuwa wanadhalilishwa na kunyanyasika kutoka kwa wanaume kwa kipigo, ulevi, kunyimwa haki zake na mambo mengine ambayo mume huwa mkaidi hataki kutenda haki na kukataa kutoa talaka.

“Wapo wanaokuja hapa na tukawasikiliza pande zote mbili lakini mwanamme akashikilia kwamba yeye anajua kuoa tu hajui kutoa talaka na hivyo husababisha matatizo katika ndoa hiyo kwa sababu mwanamke anakuwa hawezi kuendelea kuvumilia manyanyasho anayoyapata na wengine hudhurika sana maana wanapigwa na waume zao”, alisema.

S h e i k h K a d h i h u y o ameishauri jamii na wazee kutizama na kuchunguza kwa kina pale watoto wao wanapokuja kuposwa ili kujua tabia za waposaji ili wasije kuwaingiza watoto wao katika mtego ambao mwisho wake ni mbaya kwa kuwa huishia talaka muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa hizo.

A l i s e m a n i w a k a t i mzuri sasa jamii kuanza kufundishana maadili na taratibu za ndoa kabla ili kufungwa kwa ndoa hizo ili kuinusuru jamii na wimbi hilo la talaka ambalo linaonekana kama ni utamaduni mpya ambapo wajane wamejazana na wengi wao wakiwa na umri mdogo na wengine wakiwacha watoto wadogo m b a o b a a d a e h u k o s a matunzo mazuri na kuishia

16 AN-NUURRABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

AN-NUUR16 RABIUL AWWAL 1435, IJUMAA JANUARI 17-23, 2014

Soma Gazeti la AN-NNUR

kila Ijumaa

Z I P O t a a r i f a k u wa h u e n d a k u k a w a n a m c h u a n o m k a l i katika Bunge la katiba baina ya kambi mbili zilizosheheni vigogo wa serikali waliomo madarakani na wastaafu.

Wachambuzi wa duru za kisiasa wanabaini kuwa kambi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad inaona kuwa Zanzibar haitakuwa imetendewa h a k i k u t o k a n a n a kuondolewa pendekezo la kuwa na muungano wa mkataba.

Wa n a - k a m b i h a o ambayo wapo pia wazee mashuhuri wastaafu na makada wa CCM, kama Mzee Moyo, wanadaiwa kusimama katika hoja k u wa n i m u u n g a n o tu wa mkataba pekee utakaowapa Wazanzibar m a m l a k a k a m i l i ya kupanga mambo yao kama nchi yakiwemo ya kisiasa na uchumi.

A i d h a w a n a s e m a kuwa, kama ni suala la kidemokrasia, wanaamini kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibari walitoa maoni kutaka muungano wa mkataba.

Hata hivyo, baadhi ya watu katika kambi hiyo wamechukua msimamo wa wastani wakisema kuwa heri nusu shari kuliko shari kamili, kwa maana kuwa kuja serikali tatu ni hatua muhimu kuendelea madaraka kamili.

K a t i k a h a l i h i y o wanasema, heri kushika tisa, kuliko kumi neda rudi mikono mitupu.

Duru za kisiasa zinaarifu kuwa kama hakutakuwa na makubaliano baina ya makundi hayo mawili yaliyotofautiana katika lile kundi la Zanzibar yenye

Mahakama yaridhia Ilunga kwenda India

Mchuano mkali:Mamlaka kamili Vs Serikali tatu

Na Mwandishi Wetu mamlaka kamili, huenda mvutano ukahamia ndani ya Bunge la Katiba.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanaarifu kuwa kwa kuwa kipengele cha mamlaka kamili , kwa maana ya kuwa na muungano wa mkataba hakikupendekezwa katika Rasimu ya Katiba, basi lile kundi la msimao wastani

itakuwa wepesi kushinda.Kwa hiyo mchuano

utakabaki ni dhidi ya lile kundi linalokuja kwa nguvu likiwa na hoja ya kukataa serikali tatu.

Pa m o j a n a m a m b o m e n g i n e , h o j a inayopepewa hivi sasa ni kuwa gharama za kuendesha serikali tatu zitakuwa kubwa sana.

Inatoka Uk. 1ikishikiliwa kama moja ya masharti ya dhamana na kutotakiwa kutoka nje ya nchi.

Sheikh Ilunga alifika m a h a k a m a n i h a p o j a n a a s u b u h i , h u k u ukishuhudiwa umati m k u b w a Wa i s l a m u kutoka jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya Geita, Mara, Singida, Shinyanga n a K a g e r a , u l i o f i k a mahakani hapo kwa ajili

ya kusikiliza kesi yake.Kesi hiyo imeahirishwa

hadi Februari 25, 2014 i takapotajwa tena na dhamana ya Sheikh Ilunga bado inaendelea.

S h e i k h I l u n g a alikamatwa na Polisi mjini Tabora Desemba mwaka jana na kufikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza Jumanne ya Desemba 17 mwaka jana, ambapo al isomewa mashitaka matatu.

M a s h i t a k a h a y o y a l i d a i w a k u w a yalitokana na hotuba zake zi l izorekodiwa katika CD mbalimba zilizodaiwa kuwa ni za uchochezi.

Sheikh Ilunga alikana m a s h i t a k a h a y o n a kupewa dhamana na kesi kuahirishwa hadi jana.

Wakati hayo yakijiri, Naye Imam Hamza anapandishwa kizimbani leo katika mahakama hiyo hiyo kwa ajili ya kesi

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa na uchambuzi wa wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba, hakuna n a m n a n y i n g i n e ya kuunusuru muungano zaidi ya kuwa na serikali tatu: Ya Tanganyika, ya Zanzibar na ile ya muungano.

Hii ni kutokana na sababu kwamba, kwanza

mpaka sasa Zanzibar washakuwa na katiba y a o m p y a a m b a y o inaitambulisha kama nchi.

K u j a n a m f u m o ambao utapingana na Katiba hiyo, ni kutafuta mgogoro wa kisiasa an kikatiba ambao hatma yake itakuwa kuhatarisha muungano wenyewe.

inayomkabili.K a m a i l i v y o k wa

Sheikh Ilunga, Imam Hamza, ambaye naye anakabiliwa na kesi ya uchochezi mahakani hapo, naye anafikishwa katika mahakama hiyo ya Nyamagana leo.

Moja ya mashitaka yanayomkabil i Imam H a m z a n i k u d a i wa kumuunga mkono Sheikh Ilunga katika hotuba zake hizo zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.

WAISLAMU wakiwa kwenye Zaffa ya Maulid jijini Dar es Salaam hivi karibuni.